Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

SBL YACHEZESHA DROO YA NNE YA PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI YAENDELEA .

$
0
0
Pichani kati ni Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo jijini dar  kuhusiana na mshidi aliyejishindia tiketi ya kwanza ya kwenda nchini Brazili 
Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo akizungumza na mshidi huyo kwa njia ya simu ya kiganjani.

SBL YACHEZESHA DROO YA NNE YA PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI YAENDELEA   .

Hatimaye mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazili kupitia bia ya Serengeti apatikana.

  Baada ya kusubiri kwa kipindi cha wiki 3 hatimaye mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazili kupitia promosheni ya 3 Winda Safari ya Brazili na Serengeti amepatikana katika droo ya nne ya promosheni hiyo. Katika droo hiyo pia wamepatikana washindi wawili wa simu aina ya Samsung galaxy tab, pamoja na washindi hao wa droo pia kuna washindi waliojipatia zawadi za papo hapo kama bia za bure, fedha taslimu pamoja na ving’amuzi. 

Droo hiyo imechezeshwa leo asubuhi katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti huku ikishuhudiwa na waandishi wa habari, maofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, PWC na push mobile media. Promosheni hiyo bado ina wiki 8 mbele hadi kumalizika na ndani yake bado droo kubwa 2 za kujishindia tiketi za kwenda Brazili.

Akiongea kwa furaha iliyopita kifani kwa njia ya simu mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazil Deusdedit Kahwa kutoka Mbezi, Dares Salaam alisema alipata mshangao mkubwa sana kwa kuwa hakutarajia kupata bahati hii ya kuwa mshindi wa tiketi na alishiriki promosheni hii baada ya kuona matangazo yake kwenye televisheni. Aliishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa  kumpa fursa hiyo kubwa katika maisha yake na kuipongeza kwa kuwajali wateja wake kwa kuwapa zawadi mbalimali zinogusa maisha yao.

“nimefurahi sana na ninajiona mwenye bahati sana kwa kushinda zawadi hii kubwa, hii ni mara ya kwanza kushinda zawadi katika promosheni hii na nimepata zawadi kubwa sana na itakuwa ni mara yangu ya kwanza kutoka nje ya nchi, nawashukuru sana Serengeti kwa kutujali wateja wao” alimalizia Deusdedit.

Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo alisema kuwa promosheni hiyo ipo wazi kwa wanywaji wote wa bia ya Serengeti, na mpaka sasa kumekuwa na washindi Zaidi ya 50000 waliojishindia bia za bure na pia zaidi ya washindi 2000 wa fedha taslimu kiasi cha shilingi 5000 na 10,000. Washindi waliojishindia simu za Samsung tab katika droo ya leo ni Deo Msofe kutoka Kiboroloni, Moshi na Jeremiah Ndelekwa kutoka Arusha. Pia wamepatikana washindi watano (5) wa ving’amuzi ambao wote kwa pamoja watakabidhwa zawadi zao katika sherehe maalum.

Nae Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw Allan Chonjo alisema “promosheni ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti bado inaendelea na tunapenda kuwakumbusha wateja wetu kuwa hii ndio tiketi ya kwanza bado kuna tiketi nyingine na zawadi nyingine nyingi zaidi, unaweza kufuatilia kupitia ukurasa wetu wa     facebook www.facebook.com/serengetipremiumlager kwa taarifa zaidi. Napenda kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia bidhaa zetu na sisi tunawaahidi kuendelea kuwapa bidhaa zilizo bora na zenye viwango na ubora wa hali ya juu”

Kunywa kistaarabu. Washiriki wanatakiwa kuwa na umri unaozidi miaka 18. Vigezo na masharti kuzingatiwa.

Wanafunzi wa Sekondari Tanzania Sasa Wanaweza Kujadiliana Mtandaoni Popote Walipo

$
0
0

Kwa siku za hivi karibuni matokeo ya mitihani yamekuwa sio mazuri sana na kuna baadhi ya watu wengi wanalaumu mitandao ya kijamii na internet kwa hili, kwamba inawafanya wanafunzi wawe busy kufanya mambo yasiyo ya msingi na kusahau kusoma. 

Kwa kiasi Fulani ni kweli kwani kumekuwa na ongezeko la idadi ya vijana nchini Tanzania wanaojiunga na mitandao ya kijamii na internet kwa ujumla. Hata hivyo, ongezeko hili sio jambo la kuliangalia kwa jicho baya bali kulikumbatia kwani linaweza kusaidia wanafunzi wa sekondari, hasa sasa hivi ambapo kuna website kwa ajili ya wanafunzi wote Tanzania kukutana na kujadiliana masomo na topic mbali mbali wanazofundishwa darasani, na masuala yote ya kielimu kwa ujumla. Website hiyo inaitwa myElimu.com.

 Given Edward, mwanzilishi wa myElimu Project, amesema website hiyo itawasaidia wanafunzi kujadiliana na wanafunzi wenzao mambo mbali mbali ya darasani, popote pale walipo. MyElimu.com itamuwezesha mwanafunzi wa shule yoyote ile, mfano ya Dar-es-Salaam, kujadiliana na wanafunzi wengine wa mkoa wowote wa Tanzania mfano mwanza, Arusha au Mbeya kuhusu masomo yao ya darasani. 

Hii ina maana kwamba mwanafunzi aliyeko shule ya sekondari Kibasila, anaweza kuanzisha mjadala na wanafunzi wenzake wa Azania, Shaaban Robert, Nyakato au St. Francis wakaweza kujadiliana naye ndani ya mtandao huo wa myElimu.com. Safi!

MyElimu.com inapatikana kwa lugha 32 duniani nah ii itawezesha hata watembeleaji wa mtandao huo kutoka nje ambao hawajui Kiswahili na kiingereza waweze kutoa michango yao ambayo inaweza kutafsiriwa kuja kwa tena kuwa kwa Kiswahili au kiingereza kutegemea na chaguo la mtu.
Kitu kizuri kuhusu myElimu.com ni kwamba kuna sehemu ya games ambapo members wake wanaweza kwenda na kucheza pale ambacho watakuwa wameboreka au kuchoka kwenye discussions au wakiwa wanasubiri kitu kwenye mijadala yao..
 
Given aliitangaza rasmi myElimu siku 3 zilizopita katika post iliyosomeka:-
 
"I've been working on an initiative. Creating a platform where students all over Tanzania can meet and discuss school topics and every academic related issue. Currently it's difficult for students to share information mainly due to geographical distances. Nevertheless, with the increase in books with no single authorized source, it has been hard for students to know what materials are correct and good for use, hence they're stuck with wrong things. 

So I created My Elimu. My Elimu is a project which will make it possible for students in Dar es Salaam to exchange ideas and learn together with students in Arusha, Mwanza, Iringa and all other parts of Tanzania through www.MyELimu.com. It will be a meeting point for all students from Form 1 to Form 6 to meet and help each other out.

When you visit the website, you will be met with an interactive user interface that displays forums of various subjects of which you will select any that interests you and start or join a topic discussion. You need to register to the website in order to participate or start a discussion. Guests can only read the discussions but not participate."

Kwa wanafunzi wote wa sekondari Tanzania kuanzia form 1 mpaka form 6 mnashauriwa mjisajli kwani ni sehemu nzuri ya kuweza kujikuza kielimu na kutumia internet kwa manufaa yako. Unaweza kujisajili moja kwa moja hapa http://goo.gl/2NvPbO au kwa kutembelea http://goo.gl/j1kMzh na kisha kubonyeza “Register”. Ukijisajili ndio utaweza kuanzisha mijadala na kushiriki katika mijadla iliyoanzishwa tayari.

KAMPENI ZA CCM KALENGA ZATINGA KIJIJI ALICHOZALIWA MGOMBEA WA CHADEMA, MWENYEKITI WA CHADEMA NA WANACHAMA 50 WATIMKIA CCM

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kijiji cha Wangama, Fred Mgata (kulia) akikabidhi kadi za chyama hicho kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga baada ya yeye na wanachama wengine 50 wa Chadema kuamua kukihama na kujiunga CCM katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika  katika Kijiji hicho kilichopo Kata ya Luhota, Iringa Vijijini leo. Mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chadema ambaye ni mzaliwa wa kijiji hicho,  Grace Tendega alikuwa chini ya uongozi wa Mgata.
 Mgata akisalimiana na mgombea wa CCM Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa
 Mgata akipongezwa na wafuasi wa CCM kwa kitendo chake cha kuamua kuihama Chadema na kujiunga na CCM
 Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akihutubia katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Wangama.
 Ofisa wa Umoja wa Vijana wa CCM Makao Makuu, Mariana Shonzaakimuombea kura  mgombea ubunge wa CCM, Mgimwa.

 Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa 9kulia) akilakiwa kwa shangwe na vigeregere na wananchi wa Kijiji cha Ikuvilo, Kata ya Luhota alipowasili kwa ajili ya mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo leo Iringa Vijijini.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

GARI INAUZWA

$
0
0
GARI INAUZWA TOYOTA LEXUS IPO KATIKA HALI NZURI IMETUMIKA MWAKA MMOJA TU HAPA TANZANIA KWA MAELEZO ZAIDI PIGA 0715590859 AU 0714667175 
ASANTE

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AOMBOLEZA KIFO CHA MTOTO WA WAZIRI SOPHIA SIMBA, DAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Lefoord Simba, mtoto wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwa Waziri Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Lefoord Simba. Mazishi yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Kinondoni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwa Waziri Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Lefoord Simba. Mazishi yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Kinondoni.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa, Waziri mstaafu (wa pili kulia) Mjumbe wa Nec Wilaya ya Busega, Chegeni (kulia) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, wakizungumza jambo wakati wakijumuika kwa pamoja katika maombolezo ya msiba wa Lefoord Simba, mtoto wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, Masaki jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya waombolezaji.Picha na OMR

maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi jijini dar es salaam

TANGAZO ARUSHA

MNUSO WA SEND OFF YA MDAU TUKAE MOHAMED

$
0
0
 MC Luvanda akiwapanga wajumbe  wa kamati ya maandalizi kwa picha ya pamoja katika mnuso wa Send Off ya mdau Tukae Mohamed usiku huu katika ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam. Chini ni marafiki wa Tukae kwenye mnuso huo wa nguvu. Tukae atameremeta rasmi wiki ijayo jijini Mwanza


taswira toka bunge maalum la katiba mjini dodoma leo

$
0
0
 Mwenyekiti wa kamati ya maadili Mhe. Profesa Costa Mahalu akiteta jambo na katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dkt. Thomas Kashilila kulia na Mhe.John Magufuli.
 Spika wa Bunge la Jahmuri ya Muungano Mhe. Anna Makinda akijadiliana jambo na Mhe. Dkt Mohamed Seif Khatib
 Wajumbe Mhe Machali  na Mhe.Mchungaji Kadiva wakijadiliana
 Waziri mkuu mstaafu Mhe Edward Lowassa kulia aliyekaa akijadiliana jambo na Mhe.Philemon Ndesamburo
Mhe.Andrew Chenge akijadiliana  jambo na Mhe. Sadifa Juma Khamis 
 Picha na Deusdedit Moshi wa Globu  ya Jamii, Kanda ya Kati

introducing 'Ndoto za kitaa' by Amini, Barnaba, Mwasiti, Linah na Ditto

libeneke la anko john kitime lakata mbuga

$
0
0
HAHAHAHAHAHAAAA.... MPAKA SASA WALIOINGIA <www.chekanakitime.blogspot.com
NA KUCHEKA WAMEKWISHA FIKA MILIONI MOJA!!!! 
JE WEWE ULIKUWA MMOJA WAO??? 
KAMA BADO UNAKOSA UHONDO.
tangazo hili kwa hisani ya mjomba
 wangu (Kitime) wa Tosamaganga

WANTED: WEB DEVELOPERS & DESIGNERS

$
0
0

We are looking for  talented web developers and designers to join our Dudumizi Team, full-time in Dar es salaam, Tanzania. 
A highly skilled team with flat hierarchies, a creative environment and a lot of fun makes Dudumizi a great place to work at. If you love developing cutting-edge software for the web, and are passionate about the latest web technologies, join our team!

Web Developers

Responsibilities 

Develop cutting-edge web applications
Integrate and customize Joomla and wordpress extensions
Working with an international community
 
Requirements:
 
Knowledge of Object-Oriented programming, patterns and frameworks
Experience with PHP and other web programming languages
Experience with JavaScript and jQuery
Knowledge of databases (Mysql) and SQL
Experience with Joomla and Wordpress is an added advantage
Salary:
Depending on your capabilities.
Office Location:
2nd floor, Gates of Paradise Hotel, Beside Shamo Tower, Mbezi Beach, Dar es Salaam, Tanzania.

How to Apply
 
If you are interested email your resume and a portfolio to info@dudumizi.com and we'll be in touch shortly. 

Dudumizi Technologies Limited

ujumbe maridhawa

ngoma azipendazo ankal

REMEMBRANCE OF 2ND YEAR SINCE PROMOTION TO GLORY

$
0
0
JUDICA STEPHANO TERI
22.06.1946 to 08.03.2012

Passed away peacefully after a short illness.

Deeply missing you daily! You were a very loving husband to Jane (Mwl Teri); a loving, caring dad to Joan, Linda, Davis & Hillary and a dedicated brother to Monyiaichi. All of us including your other brothers Eliona, Tumaini and sister Elingienengasia, the in-laws (Aliko, Leonard & Tina), grand-children (Tumpe-Janice, Lusako-Luke, Evan-Tumaini Alex & Jeannete-Elsa), the entire TERI family, relatives and friends deeply miss you!

It is just like it happened yesterday, yet days have turned into months and it is two years today (08.03.2014) since you departed from this life and promoted to glory.

Each day we are filled with fresh memories of your love, wisdom and care.

However, WE THANK GOD FOR HIS PROTECTION AND BLESSINGS TO ALL OF US.

"John 11:25.. whoever believes in me (Jesus), though he die,

yet shall he live!"

TANZIA

$
0
0
Caroline Mbilinyi Enzi ya uhai wake 

polite reminder: MISA YA KUMUOMBEA MAJOR SAMUEL ISAAC CHEKINGO - ARUSHA (TANZANIA) & CHICAGO (USA)

$
0
0
Samson Chekingo wa CHICAGO – IL na Brenda Chekingo-Masha wa Kijenge – Arusha wanapenda kuwataarifu Misa ya kumuombea Mpendwa Marehemu Baba yao Major Samuel Isaac Chekingo (pichani),  zitafanyika sehemu mbili tofauti Tanzania na USA) leo na kesho.
1-       (Kwa wa USA)-Jumamosi March 8, th 2014 Kuanzia Saa 9 Jioni (3PM) hadi 1 Usiku (7 PM) katika kanisa la Augustana Lutheran of Hyde Park
Anuwani ya Kanisani:

AUGUSTANA LUTHERAN CHURCH OF HYDE PARK
AND LUTHERAN CAMPUS MINISTRY
5500 SOUTH WOODLAWN AVE
CHICAGO - IL 60637
 2-       (Kwa TANZANIA)- Misa Itafanyika siku ya Jumapili  March 9th, 2014  saa Tatu na nusu Asubuhi Kijenge – ARUSHA, Katika kanisa la Kilutheri la KIJENGE,

Kwa wale tuliopo Marekani - Tafadhali tunaomba kuzingatia muda wa Ibada. 

 Major Samuel Isaac Chekingo alifariki Tarehe January 28, 2014 Katika Hospitali ya Lugalo huko Dar es Salaam, Tanzania.
 Kwa taarifa zaidi unaweza kuwasiliana na:

Samson Chekingo (USA)Phone #: 847-987-9637 Email address: samchecks@hotmail.com
Brenda Chekingo – Masha (ARUSHA -TANZANIA)

Mama yangu hakuwa amesoma lakini alihakikisha naingia sekondari: Hajjat Amina Mrisho Saidi

$
0
0

Hajjat Amina Mrisho Saidi, 
Kamishna wa Sensa Tanzania 
Kuwapatia wanawake fursa katika nyanja zote ni muhimu kwa maendeleo ya kaya zao na hata taifa kwa ujumla. Kauli hiyo imejidhihirisha kwa Hajjat Amina Mrisho Saidi, Kamishna wa Sensa Tanzania mwaka 2012 ambaye baada ya kumaliza elimu ya msingi alijikita katika kuchunga mbuzi huko kwao mkoani Arusha akidhani ndoto ya elimu ya sekondari imetuwama! 
Hata hivyo jitihada za mama yake mzazi na zake yeye binafsi pamoja na serikali zilimwezesha kufika alipo sasa. Hajjat Amina alifunguka bayana katika mahojiano maalum na Assumpta Massoi wa Idhaa hii kuhusu siku ya wanawake duniani ambapo anaanza kwa kuelezea familia yao..
(KUSIKILIZA BOFYA HAPO CHINI)

Mwenyekiti wa CCM shina la Essex Uingereza Bibi Maryam Seif agawa misaada kwa yatima kurasini

$
0
0
 Mwenyekiti wa CCM shina la Essex Uingereza, Bibi Maryam Seif akigawa misaada hiyo kwa  watoto hao yatima wa  kituo cha Kurasin jijini 
Dar es salaam
 Bibi Maryam Seif, akiendelea kugawa misaada kwa watoto hao yatima wa Kurasini.
  Mwenyekiti wa CCM shina la Essex Uingereza, Bibi Maryam Seif,  akimkabidhi misaada hiyo mlezi wa  watoto hao yatima wa  kituo cha Kurasin jijini Dar es salaam
Bibi Maryam Seif, akiwa na baadhi ya watoto hao yatima wa Kurasini.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 08.03.2014.

Viewing all 109984 articles
Browse latest View live




Latest Images