Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

STAMICO yaipongeza SUMA JKT

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Uzalishaji Mali  la Jeshi la Kujenga Taifa,  SUMA JKT, limepongezwa kwa juhudi zake katika kuhakikisha ulinzi unaimarika katika maeneo ya mgodi wa STAMIGOLD uliopo Biharamulo Kagera.

Mgodi huo kwa sasa umekabidhiwa kwa serikali ambapo unaendeshwa chini ya shirika la madini la STAMICO.

Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  wa STAMICO,  Rumisha Kimambo katika kikao kilichojumuisha Bodi yake na uongozi wa mgodi wa huo kilichofanyika mgodini hapo  hivi karibuni.

Mwenyekiti huyo ambae pia alipata fursa ya kutembelea eneo la westzone na mojamoja uliopo Mgodi huo alionesha kuridhishwa na mfumo wa mbinu shirikishi zinazotumiwa na mgodi huo katika kulinda mgodi bila ya kuharibu uhusiano kati ya mgodi huo na wananchi.

“Tumefurahishwa sana na kazi inayofanywa na SUMA JKT hapa STAMIGOLD kwani wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana  kuondoa tatizo la wachimbaji haramu na wavamizi ndani ya  mgodi.” 

Alisema kuwa wachimbaji haramu wengi katika migodi ni tatizo na kunakuwa na njia mbadala katika kuwakabili kitu ambacho SUMA JKT imefanikiwa.

Shughuli za uchimbaji katika mgodi huo zinatarajiwa kuanza  mwezi April mwaka huu baada ya kukamilika kwa barabara ya urefu wa takribani Kilometa 3.9 kutoka eneo la ofisi za Mgodi kuelekea kwenye maeneo ya uchimbaji.

Mapema mwezi huu kampuni ya African Barrick Gold  iliyokuwa ikimiliki mgodi wa TULAWAKA ilifanikiwa kuhamisha  kibali  na baadhi ya leseni  za uchimbaji  katika eneo la westzone na mojamoja kwa shirika la madini STAMICO hivyo kuwezesha shirika hilo kuwa katika nafasi nzuri ya kuendeleza sekta ya madini hapa nchini.


The Ministry of Water to observe 26th Maji week Event from 16th to 22nd march,2014

TASWIRA YA MVUA JIJINI DAR LEO KUTOKEA KWENYE KIOO CHA GARI

Article 15

$
0
0

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD
WAZEE WA KAZI
MIZIGO KWA NDEGE SASA MARA MBILI KWA WIKI
MONDAY NA WEDNESDAY
MZIGO SASA UNACHUKUA SIKU TANO TU
UKIONDOKA JUMATATU UNACHUKUA IJUMAA DAR
AIR CARGO TO DAR £3.80 INCLUSIVE CLEARANCE
FREE STORAGE IN OUR OFFICE
FREE COLLECTION FROM EAST LONDON 
£50 COLLECTION FROM ANYWHERE IN UK
COLLECTION POINT IS
ILALA MTAA WA BUKOBA
CONTACT; TORNADO+255713607116

SAVE OVER £600 ON CONTAINERS!
20' CONTAINER TO DAR /MOMBASA NOW £1,200 
40' CONTAINER TO DAR MOMBASA NOW £1,700

CRDB yazindua huduma ya malipo ya gharama za matibabu kwa njia ya Kadi KCMC

$
0
0
Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheli dayosisi ya kaskazini Dk Martini Shao akiwa na mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB pamoja na kaimu mkurugenzi wa hosptali ya KCMC .Prof Raimosi Ollomi wakati akizindua tawi dogo la Benki ya CRDB.
Mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB,Dk Charles Kimei akimuelekeza jambo Askofu Dk Martin Shao kabla ya uzinduzi wa huduma ya malipo ya gharama za matibabu kwa njia ya Kadi.
Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheli dayosisi ya kaskazini,Dk Martin Shao akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi dogo la CRDB pamoja na uzinduzi wa utolewaji wa huduma ya malipo ya gharama za matibabu kwa njia ya Kadi katika hosptali ya rufaa ya KCMC.
Wachungaji wakishirikisha neno la Mungu wakati wa hafla ya katika hosptali ya rufaa ya KCMC ya uzinduzi wa tawi dogo la CRDB pamoja na uzinduzi wa utolewaji wa huduma ya malipo ya gharama za matibabu kwa njia ya Kadi katika hosptali ya rufaa ya KCMC.
Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheli dayosisi ya kaskazini Dk Martini Shao akiwa na mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB Dk Charles Kimei pamoja na wageni wengine mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja wakionesha kadi ya mfano ya kulipia gharama za matibabu katika hospitali ya rufaa ya KCMC.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MZUNGU TAPELI ANASWA NA MAHERA KIBAO FEKI HAPA BONGO

$
0
0
  Kamanda Suleiman Kova
 JAN ELOFF AKITOLEWA  NJE YA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM
JAN ELOFF AKIHOJIWA NDANI YA CHUMBA MAALUM KILICHOPO NDANI YA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY

Yule mzungu aliyekuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kutuhuma za kuwatapeli wananchi kwa Euro Feki hatimae amekamtwa akijaribu kununua gari kwa pesa hizo feki.
Habari za uhakika zilizotua mezani zilisema mzungu huyo ambae ni Raia wa South Africa aliyefahamika kwa jina la  JAN ELOFF ambae anaishi maeneo ya Msasani Jijini Dar. 
Taarifa zilisema mzungu huyo ambae alikuwa anatuhumiwa kumpiga zaidi ya Euro hizo feki 700 mwandishi (jina kapuni) na DTV Bw. Livingstone Mkoi mwanzoni mwa januari mwaka huu kisha kufungua kituo cha polisi Oysterbay nakupatia kumbukumbu hii OB/RB/ 2972/14 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU, pamoja na Kutoa Euro Feki.
Baada ya tukio hilo la kutapeliwa mwanahabari huyo Jeshi la Polisi lilitangaza msako mkali wa kumtafuta mzungu huyo ambae alikuwa akishirikiana na wadada wawili ambao ni raia wa Cameroon na Nigeria pamoja na mwanaume wa kitanzania ambao baada ya tukio la kukamatwa mwenzao wanaendelea kutafutwa usiku na mchana na tayari ameshawataja wenzake anaoshirikiana nao.Kufuatia kukamtwa kwa mzungu huyo wananchi wengi wamempongeza Kamanda Kova kwa kufanikisha kukamatwa mzungu huyo. 
Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni limetoa rai kwa mtu yeyote ambae amewahi 'kupigwa' na mzungu huyo basi wafike haraka kituo cha polisi Oysterbay kwa ajili ya kumtambua mzungu huyo.
Habari na Kili Nyepesi

PROIN PROMOTIONS LIMITED KUANZA KUSAKA VIPAJI VYA UIGIZAJI NCHINI TAREHE 1 APRIL 2014

$
0
0
Meneja wa Mradi wa Kusaka Vipaji Vya Uigizaji Tanzania (Tanzania Movie Talents) Bw Joshua Moshi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakutambulisha kampeni mpya ya kusaka Vipaji vya uigizaji kutoka kampuni ya Proin Promotions Limited mapema leo katika Ofisi za Proin Promotions Limited, Mikocheni, Mtaa wa Ursino, Pembeni ni Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited Bw Evance Stephen.

Muigizaji wa Filamu za Kitanzania Single Mtambalike almaarufu Richie Richie ambae pia ni mmoja wa majaji katika Shindano la kusaka vipaji vya uigizaji lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents lililopo chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited akiongelea jinsi washindi watakavyopatikana katika shindano hilo linalotarajia kuanza tarehe 1 Aprili 2014
 Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Runinga Cha Channel Ten, Bw Fredy Mwanjala akiuliza swali kwa Meneja Mradi wa Tanzania Movie Talents, Bw Joshua Moshi (hayupo pichani) kuhusiana na Shindano la kusaka vipaji vya uigizaji nchini
 Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited, Bw Evance Stephen (wa kwanza kushoto) akionyesha stika za TRA ambazo zinaonyesha Uhalali wa filamu za Proin Promotions lakini Pia Wateja watakaonunua Filamu kutoka Proin Promotions wanatakiwa kutuma namba zilizopo kwenye stika hizo za TRA kwaajili ya kuweza kujishindia zawadi mbalimbali kutoka Proin Promotions kama Vile TV za Samsung na deki zake

taswira zaidi toka bunge la katiba mjini dodoma leo

$
0
0
 Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakitoka Bungeni Mjini Dodoma leo baada ya Bunge hilo kusitishwa  kwa muda kufuatia Sintofahamu iliyotokea.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba Mhe Halima  Mdee   akitafakari baada ya wenzake kuondoka bungeni wakati Bunge hilo lilipositishwa  kwa muda mjini Dodoma leo  kufuatia sintofahamu iliyokea.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba Mhe Halima  Mdee   akitafakari baada ya wenzake kuondoka bungeni wakati Bunge hilo lilipositishwa  kwa muda mjini Dodoma leo  kufuatia sintofahamu iliyokea.
 
7  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd  (wapili kushoto) wakijadili jambo na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba baada ya Bunge hilo kusitishwa kwa  muda leo kufuatia sintofahamu ilitokea. Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge Thomas Kashilillah, Waziri  wa Nchi,Ofisi ya  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira,  Waziri wa Katiba na Sheria  wa Zanzibar,  Abubakar  Khamis Bakari  na Mwanasheria  Mkuu wa Tanzania, Frederick Werema. 
 Katibu wa Bunge Thomas Kashilillah akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda  pamoja na Waziri  wa Nchi,Ofisi ya  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira,  Waziri wa Katiba na Sheria  wa Zanzibar,  Abubakar  Khamis Bakari  na Mwanasheria  Mkuu wa Tanzania, Frederick Werema. 

TAIFA STARS KUREJEA NCHINI KESHO MCHANA KUTOKA NAMIBIA

$
0
0
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kurejea nchini kesho (Machi 7 mwaka huu) saa 12.45 jioni kutoka Windhoek, Namibia kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA.

Taifa Stars ambayo katika mechi hiyo dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ilitoka sare ya bao 1-1 itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.15 mchana kwa ndege ya South Africa Airways.

Timu inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager baada ya kuwasili itakwenda hoteli ya Accomondia kwa ajili ya chakula cha mchana na baadaye kuvunja rasmi kambi yake.

Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer

Tanzania Football Federation (TFF)

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA TAARIFA YA 'THE CONNECTED WOMEN INITIATIVE' YA VODAFONE FOUNDATION

$
0
0
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwahutubia waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Taarifa ya 'THE CONNECTED WOMEN INITIATIVE' ya Vodafone Foundation. Uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Golden Tulip hapa Dar es Salaam tarehe 5.3.2014.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa Taarifa ya THE CONNECTED WOMEN INITIATIVE wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi huo.

shehe mkuu wa mkoa wa iringa marehemu Ally Tagalile azikwa leo

$
0
0
Jeneza lenye mwili wa  Shehe Mkuu wa Mkoa wa Iringa Marehemu Sheikh Ally Tagalile  likipelekwa makaburini kwa mazishi mjini Iringa jioni hii.

JEHI LA POLISI DODOMA LAWASHIKILIA WANAWAKE 15 WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA UKAHABA

$
0
0
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeendelea kufanya msako katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata wanawake wapatao 15 wanaojihusisha na biashara haramu ya kuuza miili yao kutoka mikoa mbalimbali nchini. Msako huo ulifanyika tarehe 05/02/2014 majira ya 21:00hrs katika mitaa ya uhindini na Air Port.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi DAVID MISIME - SACP amewataja watu hao kuwa ni:

1.   VERONICA D/O JOEL mwenye miaka 23, Mnyakyusa mkazi wa Sai Mbeya.

2.   ROSE D/O MICHAEL mwenye miaka 30, Mgogo, Mkazi wa Kikuyu Dodoma.

3.   MARIAM D/O JORDAN mwenye miaka 26, Mhehe mkazi wa Tukuyu Mbeya.

4.   REHEMA D/O RAMANDANI mwenye miaka 38, Mlugulu makazi wa Airport Morogoro.

5.   JOYCE D/O MARTINE mwenye miaka 22, Mnyamwezi mkazi wa Chinangali West Dodoma.

6.   FATIA D/O SARATIELI mwenye miaka 20, Mgogo mkazi wa Makanda Bahi Dodoma.

7.   BOKE D/O CHACHA mwenye miaka 27, Mkurya mkazi wa Tarime Mara.

8.   SWAUMU D/O BAKARI mwenye miaka 23, Mnyamwezi mkazi Chinangali Dodoma.

9.   ROSS D/O MASAKI mwenye miaka 28, Mchaga mkazi wa Sanya juu Moshi.

10.               SCOLASTIA D/O COSTANTINO mwenye miaka 22, Mnyakyusa mkazi wa Gongolamboto Dar es salaam.

11.               HAPPY D/O JULIUS mwenye miaka 31, Mnyamwezi mkazi wa  Urambo Tabora.

12.               AISHA D/O HASSAN mwenye miaka 38, Mbulu mkazi wa Babati Manyara.

13.               JULIANA D/O DOMINICK Mwenye miaka 31, Mnyakyusa, mkazi wa Airport Dodoma.

14.               DATIVA D/O LUKWEMBE mwenye miaka 29, Mhaya mkazi wa Kiziba Bukoba Kagera.

15.               DORIN D/O MASSAWE mwenye miaka 23, Mchaga mkazi wa Kiboshomaro Moshi.


Aidha Kamanda MISIME amesema katika msako huo watu wawili wanaume walikamatwa wakiwa na mirungi robo kilo katika mtaa wa barabara ya nane (8) Manispaa ya Dodoma ambao ni NASSOR S/O ALLY mwenye miaka 45, Mwarabu mkazi wa barabara ya kumi na AYUBU S/O TEPO mwenye miaka 40, Muarusha, Fundi cherehani mkazi wa Chamwino.

Pia huko katika Wilaya ya Kongwa kijiji cha Mlanje kata ya Matongoro Tarafa ya Zoisa alikamatwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la SHEDRACK S/O MACHILE mwenye miaka 46, Mgogo, Mkulima akiwa na Lita 30 za pombe ya moshi akiziuza.

Kamanda MISIME amesema msako unaendelea na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.

Serikali, UNDP, PATH wakubaliana njia bora ya kukabiliana na TB, Malaria na magonjwa kwenye nchi za joto

$
0
0
DSC_0773
Kaimu Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Neema Rusibayila, akifungua rasmi warsha ya mradi wa upatikanaji na utekelezaji wa pamoja kati ya Shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP) na Shirika la Kimataifa lisilokuwa la Kiserikali (NGO) PATH kwenye sekta ya Afya katika utumiaji na uanzishwaji wa Teknolojia mpya katika kupamba na magonjwa ya TB, Malaria na magonjwa yaliyoachwa katika nchi za joto. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkazi, Oparesheni wa UNDP, Bw. Titus Osundina.
DSC_0730
Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika warsha hiyo ya siku moja ambayo ilikuwa inazungumzia mradi wa pamoja wa upatikanaji na utekelezaji kati ya UNDP na PATH jinsi ya uanzishwaji wa Teknolojia mpya katika kupamba na magonjwa ambayo yanapatikana katika nchi za joto.
DSC_0789
DSC_0732
DSC_0804
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Neema Rusibayila akiteta jambo na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Bw. Titus Osundina wakati wa warsha ya Upatikanaji na Utekelezaji wa pamoja katika miradi ya utathimini na mipango inayowashirikisha UNDP na PATH.
DSC_0723
Picha juu na chini ni Kaimu Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Neema Rusibayila, akibadilishana mawazo na kusalimiana na baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
DSC_0708

TASAF NA MKAKATI WA KUKABILIANA NA TATIZO LA LISHE DUNI NCHINI.

$
0
0
 Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent Assey akizungumza na wataalam walioshiriki katika mkutano uliojadili namna ya kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi unaoratibiwa na TASAF
 Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent Assey akizungumza na wataalam walioshiriki katika mkutano uliojadili namna ya kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi unaoratibiwa na TASAF
 Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent Assey akizungumza na wataalam walioshiriki katika mkutano uliojadili namna ya kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi unaoratibiwa na TASAF
 Baadhi ya washiriki wa mkutano uliondaliwa na TASAF kujadili namna bora ya kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini sana nchini wakimsikiliza mkurugenzi Mtendaji wa TASAF , Ladislaus Mwamanga ( hayupo pichani) wakati alipofungua mkutano huo kwenye ukumbi wa CEEM ,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent Assey akizungumza na wataalam walioshiriki katika mkutano uliojadili namna ya kuhusisha masuala ya lishe katika mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi unaoratibiwa na TASAF
===========  ===========   ============
TASAF NA MKAKATI WA KUKABILIANA NA TATIZO LA LISHE DUNI NCHINI.


Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF kupitia Mpango wa kunusuru kaya masikini sana na zilizo katika mazingira hatarishi ,PSSN umekutana na wadau wa sekta mbalimbali za kiserikali kujadili namna ya kushirikiana katika kuhakikisha kuwa suala la lishe bora linapewa umuhimu mkubwa ili kupambana na tatizo la utapiamlo hususani kwa watoto nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wadau wa sekta za afya na lishe kwenye ukumbi wa CEEMI jijini DSM,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga amesema jitihada zaidi zinapaswa kuelekezwa katika kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuboresha afya kwa kutumia lishe bora hususani kwa watoto ili kujenga makuzi sahihi ya ubongo wao.

Mwamanga amesema TASAF kwa upande wake imeweka mfumo imara wa kuwahusisha watalaamu wake ambao wamesambazwa katika maeneo mbalimbali nchini kote na kutoa rai ya kuwahusisha katika kampeni mbalimbali za kuwaelimisha wananchi juu  ya matumizi sahihi ya vyakula kwenye maeneo husika.

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesisitza kuwa pamoja na TASAF kuanza utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi ambapo suala la lishe ni moja ya vipengele muhimu, ni vema sekta nyingine pia zikashirikiana na taasisi yake katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata elimu sahihi juu ya namna bora ya kuboresha lishe hususani kwa watoto na akinamama wajawazito.

Mwamanga pia ametoa rai kwa wataalam kutumia mbinu mbalimbali za kuwasilisha ujumbe sahihi wa masuala ya lishe na kuzisambaza kwa walengwa jambo litakalosaidia kupambana na tatizo la kudumaa kwa makuzi na ubongo kwa watoto ambapo kwa sasa inakadiriwa kuwa asilimia 42 ya watoto nchini wamedumaa kimakuzi.

Mapema akizungumza katika mkutano huo ulioshirikisha wadau kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wizara ya mifugo na Uvuvi ,Wizara ya Kilimo,Taasisi ya Lishe na Chakula na wataalamu kutoka TASAF,Mkurugenzi wa uratibu wa Shughuli za Serikali katika Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Obeyi Assery amesema suala la kudumaa katika makuzi ya mtoto ni tatizo kubwa nchini ambalo linapaswa kutatuliwa kwa nguvu za wadau mbalimbali .

Naye mkurugenzi msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Vicent Assey amepongeza jitihada za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF kwa kubuni mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi kwenye mazingira hatarishi ambapo suala la lishe litawekewa msukumu mkubwa kama moja ya vigezo vya kuzisaidia kaya zitakazoingizwa kwenye mpango huo mkubwa wa aina yake.

IZAAS office invaded by goiter patients

$
0
0
With salams and jambo from IZAAS IZAAS 
We now appeal our generous donors to help the suffering humanity at the cost of $350 per patient, we accept any amount of donation of donation,you can give your sadaka, garib,bewa,Yatim,Nazer manta and hazrat Abbas funds.   Kindly read below:
. Mubaarak Abdullah.

hoja ya haja: Stendi ya Mabasi ya Mikoani Mbezi Luis au Luguruni?

$
0
0
Moja ya kero kubwa hapa Dar ni msongamano unaotokana na kutopangilia miundombinu na huduma vizuri. Kwenye magazeti ya siku za karibuni, imeripotiwa kuwa mpango wa kujenga stendi ya mabasi yaendayo mikoani eneo la Mbezi Luis umekwama kwa sababu eneo lile halifai kutokana na kuwepo mkondo wa maji. 
 Nimekuwa najiuliza kwa nini kujengwa stendi pale mahali hajapapimwa (hivyo ni vigumu kujengwa huduma za mahoteli, nk na kumwaga maji taka)... wakati mbele kidogo tu pale Luguruni kuna eneo kubwa limetengwa kuwa satellite city na mpaka sasa limebaki pori?
Kujenga hapo stendi kuu ya mabasi ya mikoani pamoja na soko kubwa la jumla kungetosha kuhamasisha uwekezaji ambao ndio ungesaidia patumike kama kituo cha huduma kama ilivyokusudiwa na kupunguza msongamano mji mkongwe wa Dar. 
Dar City Council bado wanatafuta maeneo kuweka hiyo stendi wakati Luguruni iko pori kubwa pale. Hata waliwahi kutaka kujenga stendi ya muda pale Chuo Kikuu Dar.
   Hivi humu hakuna anayehusika na haya mambo atuelimishe?
Mdau wa Mbezi

NANI KUIBUKA MSHINDI WA SAFARI YA BRAZILI WIKI HII?

$
0
0
Tiketi ya kwanza ya kwenda Brazili na Serengeti kutolewa wiki hii:

Machi 4, 2014; Kampuni ya Bia ya Serengeti inatarajia kuchezesha droo ya nne ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti ambapo mshindi wa kwanza wa kwenda Brazili atapatikana. Licha ya zawadi kibao kutoka kampuni hiyo kama ving’amuzi, ipad, bia za bure, na fedha taslimu kufaidisha wateja wengi wa bia ya Serengeti kwa wiki tatu za mwanzo na zinazoendelea, wiki hii kutakua na zawadi kubwa zaidi ya promosheni hiyo ya safari ya kwenda Brazili ambapo mshindi atalipiwa gharama zote kwenda kutembea nchini humo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti washindi wa wiki ya tatu ya promosheni hiyo wameonesha furaha zao kwa kupata zawadi hizo huku wakiishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwajali wateja wake huku wengi wao wakiwa na shauku ya kupata zawadi kubwa zaidi ya promosheni hiyo ya kwenda nchini Brazil ambayo droo yake itachezeshwa wiki hii huku gharama zote zikilipwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika mapema wiki hii mmoja wa washindi wa Samsung tablet Vedastus Kalinga kutoka Mbeya alisema amefarijika sana kupata zawadi ya simu hiyo ya mkononi kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti kwani itamsaidia kufanya vitu vyake kwa urahisi zaidi katika ulimwengu huu wa dijitali ingawa ndoto yake ni kupata safari ya kwenda Brazili.

Naye Meneja wa Bia ya Serengeti Rodney Rugambo alisema mpaka sasa washindi watano wameshakabidhiwa simu aina ya ‘Samsung Galaxy tab 3’ na kumi na nne wameshapata ving’amuzi kupitia promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti. Promosheni hiyo  zaidi ya zawadi za washindi wa droo za kila wiki pia kuna washindi wa bia za bure za papo hapo na fedha taslimu ambapo zaidi  ya wateja 716 wameshajipatia fedha taslimu Tsh 5000 na washindi 400 wameweza kujipatia Tsh 10,000 .

“Tunapenda kuwataarifu wateja wetu kuwa wiki hii kutakuwa na droo kubwa yakupata mshindi wa kwanza wa safari ya Brazili ambaye atalipiwa gharama zote na Kampuni ya Bia ya Serengeti. Zawadi hii kubwa ni kwaajili ya wateja wetu chakufanya ni kufungua bia yako ya Serengeti kokote nchini na fuatilia maelezo ya promosheni na uweza kuwa mshindi wetu wa wiki inayokuja. 

Pia unaweza kufuatilia kupitia ukurasa wetu wa facebook www.facebook.com/serengetipremiumlager. Hivyo hatuna budi kuwashukuru wateja wetu kwa ushirikiano wanaotupa”, aliongeza Rugambo.
Kunywa kwa tahadhari. Inauzwa kwa wenye miaka 18+.

SHULE BINAFSI NA MCHANGO WAKE WA PEKEE KATIKA SEKTA YA ELIMU HAPA NCHINI

$
0
0
 SHULE binasi zina mchango wa pekee katika sekta ya elimu hapanchini,  kwa kutambua wingi wa watoto na ufinyu wa nafasi za shule za serikali
zilizopo.

Hiyo imefanya serikali kuchagua wale wenye uelewa wa juu pekee
kujiunga na shuleza elimu ya juu, huku wale ambao pengine kwa bahati
mbaya wamekwama kufikia alama zilizowekwa na serikali, wakiokolewa na
shule binafsi.

Hii imesaidia idadi kubwa ya watoto nchini kupata elimu ya sekondari
tofauti na miaka ya nyuma ambapo watoto wengi waliokuwa wakifeli na
kukosa shule basi huishia nyumba.Shule za Filbert Bayi, nazo ni miongoni mwa shule binafsi zilizokuwa na mchango wa pekee, hususani katika elimu ya sekondari.

Miaka  tangu kuanzishwa kwa shule ya Sekondari Filbert Bayi, na miaka
sita ya mahafali ya kidato cha nne, imeweza kuonyesha maajabu ya aina
yake kwa kufuta kabisa daraja sifuri.

Shule ilianza ikiwa na wanafunzi 28 na hadi sasa wamefikia 380, na
Mkurugenzi wa shule hizo Anna Bayi anasema wamefikia idadi hiyo kwa
sababu  ya kuchagua watoto wanaokidhi viwangovilivyowekwa na shule.

"Tungekuwa tunachukua watoto wa kila aina, basi nadhani idadi ingekuwa
kubwa zaid, lakini kwanza hatupokei watoto we na wenye utovu wa
nidhamu na wenye uelewa  wa hali ya chini.

Anasema ingawa wanachangamoto  ya kuachiwa watoto wasio na uelewa
sana, kwa kuzingatia wote wanaofanya vizuri kuchukuliwa shule za
serikali, lakini bado wameweza kutoa watoto bora kielimu.

Hata  hivyo, nao huwachuja na kupata wenye uelewa wastani, na tangu
wameanza kufanyamitihani yakidatocha nne hawajawahi kupata daraja
sifuri.

"Tulianza kwa kupata dara la nne, ambapo walikuwa wachache sana,na
tulishuka hadi akabaki mmoja, na mwaka jana hatukupata daraja la nne,
na badala yake daraja moja na mbili ndio walikuwa wengi huku daraja la
tatu wakiwa wachachekabisa,"anabainisha.

Kutokana na matokeo hayo, shule ya sekondari Filbert Bayi iliyoko
Kibaha mkoani Pwani, imefanikiwa kushika nafasi ya sita kimkoa, kati
ya shule 105,na nafasi ya 71 kitaifa kati ya shule zaidi ya 3000 na
nafasi ya nne kiwilaya.

Pamoja na mafanikio hayo, lakini shule hiyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo kubwa ya kunyoosha maadili ya watotona hatimaye
kuwa wamoja.

HALI YA HEWA YACHAFUKA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Semina ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba leo imelazimika kuahairishwa baada ya kuibuka vurugu ndani ya ukumbi wa Bunge. 
Zogo hilo liliumuka baada ya kuibuka kwa mvutano baina ya wajumbe uliosababishwa na kutuhumiana kwamba zipo dalili za upendeleo wanazofanyiwa baadhi ya wajumbe kutokana na sababu za kiitikadi za vyama. 
Hali hiyo ya hewa ilichafuka  baada ya kuibuka kwa mvutano baina ya Mjumbe Mhe. Christopher Ole Sendeka ambaye aliingia katika mvutano na Mjumbe wa Kamati ya Kanuni Mhe Abubakar Hamis Bakari kuhusiana na uwasilishwaji wa majedwali ya marekebisho ya kanuni. 
 Awali Mjumbe Sendeka alipewa ruksa na Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo Mhe Pandu Ameir Kificho,  awasilishe mapendekezo ya mabadiriko katika kifungu cha 58 cha kanuni hizo kilichokuwa kikijadiliwa muda huo. 
 Lakini baada ya Mhe Sendeka kuwasilisha mabadiriko yake, alisimama Mjumbe Bakari ambaye kiutaratibu alipaswa kujibu hoja hiyo hasa kwa kuwa ni mjumbe wa kamati ya kanuni. 
Mhe. Bakari alikataa kupokea hoja ya mabadiriko ya Mhe. Sendeka kwa kusema kuwa hayakuwa yamewasilishwa kwa kufuata taratibu za uwasilishwaji wa mabadiriko ya majedwali, na kwamba Kamati haina mapendekezo hayo hivyo haiwezi kujibu jambo lisilo jadiliwa. 
Katika kukataa huko Bakari alikitupia lawama kiti cha Mwenyekiti huyo kwa madai kuwa kimekuwa kikitaja majina ya wajumbe na kuwapa nafasi ya kuongea wakati hawapo kwenye utaratibu wala hawakuwa wameomba toka awali. 
 Aliongeza kuwa si kwa Mhe. Ole Sendeka pekee, bali pia Mwenyekiti huyo amekuwa akiataja wajumbe wengine wakiwamo Peter Serukamba pamoja na Umy Mwaimu ambao wote hawakuwa wamewasilisha majedwali ya mapendekezo ya marekebisho toka awali. 
 "Mheshimiwa Mwenyekiti, Ole Sendeka hayupo katika orodha ya walioleta mapendekezo, lakini nashangaa wewe unampa nafasi ya kuzungumza wakati hakuwapo kwenye orodha yetu, kamati hatuwezi kumpa nafasi ya kujibu hoja yake hatuitambui. 
"Hata hao wakina Ummy Mwalimu hawapo katika orodha. Mwenyekiti ukiendeleza huu mtindo wa kuruhusu kila anayetaka kuzungumza hapa azungumze hatutofika. tutatumia miezi 6 hapa kutengeza kanuni tu. Lazima uwe na maamuzi kuwa wanaoleta mapendekezo hivi sasa hatupokei"alisema Mhe Bakari 
 Baada ya Mhe Bakari kumaliza kuzungumza, Mhe Kificho aliingilia kati na kusema kuwa jambo hio linaweza kuwa limechanganywa na sekretarieti inayoandaa na kwamba yeye binafsi amepewa majina ya waliopeleka marekebisho hivyo anashangaa kuona kama hayapo kwa wajumbe hao. 
Mhe Kificho alitoa ruksa kwa Ole Sendeka kuongea tena, ambapo katika mazungumzo yake alitoa kaulia akisema kuwa mapendekezo yake aliyawasilisha mapema na kwamba kama Mhe Bakari ana itikadi zake za vyama asimuhusishe humo. 
 Mhe. Ole Sendeka alisema kuwa yeye ana uzoefu wa kanuni na kwamba alifuata taratibu akiwa na wenzakeMhe Serukamba pamoja na Mhe Mwalimu na kwama kama mapigo yao yanawaumiza wajumbe wengine wavumilie tu. 
 "Mheshimiwa mwenyekiti tuliopo hapa ni wajumbe. Nilijua na mimi sio dhaifu kwenye kanuni. Nnajua haki yangu kwa kuwasilisha kwa wakati, nilitimiza wajibu wangu, kama mapigo yetu yanawaumiza. 
 "Kazi yetu si kupeleka majina yetu kwa Abubakari, kama yeye ana chama chake na hoja zetu zinamuuma, asimame na kutuweka wazi kuwa yupo katika msimamo gani. Lakini mimi nimewasiisha kama taratibu zinavyonitaka"alisema Ole Sendeka 
 Kauli ya Mhe Sendeka ilianzisha sintofahamu ndani ya Bunge hilo baada ya baadhi ya wajumbe kuanza kuzomea na wengine wakisiama na kutaka kupewa ruksa ya kuzungumza huku wakiwasha vipaza sauti.
 Hali hiyo ilimuinua Mhe Kificho ambaye aliwasihi wajumbe kuacha kuingiza masuala ya vyama hasa kwakuwa wajumbe walioingia hapo ndani wamewakilisha makundi. 
"Niwaombe wajumbe tujitahidi sana, tusionyeshe misimamo ya vyama, tumepata heshima kubwa ya kuwapo humu ndani hivyo si vyema kuanza kuonesha vidole kwasababu huyu katika CCM, sijui CUF ama Chadema au kokote itaibua hisia ambazo si vyema.
 "Mheshimiwa Ole Sendeka naona ulimi umekwenda mbali kidogo ukamgusa mheshimiwa Bakari. Mimi naona hili jambo limekwenda nje. Kwa hiyo naomba tuwe makini"alisema Kificho Baada ya kauli ya Kificho, wajumbe walianza kupiga kelele wakitaka Mhe Ole Sendeka kumwomba radhi Mjumbe Bakari huku wengine wakimtaka asifanye hivyo. 
Mhe Kificho alitoa nafasi nyingine kwa Mhe Bakari kuzungumza, ambapo katika mazungumzo yake ndipo fujo hizo zilipoibuka. Katika Mazungumo yake, Mhe Bakari alisema kuwa alichosema yeye ni kwa faida ya Bunge na nchi, na kwamba taratibu ni kuwasilisha mapema mapendekezo na kwamba majina ya kina Sendeka hayakuwapo. 
 "Mimi nilizungumza vizuri hili kuweka utaratibu mzuri wa kupokea majedwali haya. Mheshimiwa mwenyeiti kwa bahati mbaya mdogo wangu Ole Sendeka anadai kanuni anazijua vizuri, lakini ninachosema sifikirii..sifikirii kama ana uzoefu wa kujua kanuni kunishinda mimi.
"Mheshimiwa mwenyekiti toka mwaka 1980 nipo katika mabunge haya, kwa hivyo sifikirii kama mtu katoka Simanjiro miaka kumi iliyopita anaweza akaja hapa na kusema anajua kanuni kunizidi. "Mimi sitaki aniombe radhi, ila ninachotaka kumfahamisha ni kwamba kuna watu wana ujuzi zaidi kuliko yeye hivyo awe makini katika mazungumzo yake"alisema Bakari 
Kauli hiyo ilizidisha mgawanyiko katika Bunge hilo, ambapo wajumbe walisimama na kuanza kupiga meza wengine wakizomea.  
Baadhi ya wajumbe walionekana wakirushiana maneno na hata kupeleka kutaka kurushiana makonde. 
 Hali hiyo ilipeleka askari ambao ni wapambe wa Bunge kusogea karibu ikiwa ni njia ya kutuliza vurugu hizo, huku wajumbe hao wakiendelea kurushiana maneno. 
 Vurugu hizo zilionekana kusambaa katika ukumbi mzima ambapo wajumbe wengine walionekana kurushiana maneno, hali iliyopelekea Mhe Kificho kuahirisha Semina hiyo.

Sehemu ya Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba wakitawanyika mara baada ya mwenyekiti kuahirisha kikao kutokana na baadhi ya wajumbe kutoelewana katika hoja.Semina imeahirishwa hadi saa 11.00 jioni.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Ole Sendeka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tuhuma za baadhi ya wajumbe kuwa Mwenyekiti anampendelea kwa kumpa nafasi nyingi za kuchangia hoja katika semina ya kanuni za bunge maalum.
Mjumbe wa Bunge la Katiba na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,Mhe. Freeman Mbowe akiongea na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo,mara baada ya kuahirishwa kwa kikao.
Mjumbe wa Bunge la Katiba,Mhe. Kajubi Mkajanga kutoka taasisi ya vyombo vya Habari akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mwemyekiti kulazimika kiuahirisha semina ya kujadili kanuni hadi saa kumi na moja (11:00) jioni.

Airtel Yatoa Msaada wa Samani kwa Ofisi ya Usalama Barabarani Kinindoni

$
0
0
Ofisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki (kulia)akiteta na Afisa Mnadhimu wa Polisi Kinondoni, Bibie Juma Athumani (wa kwanza kushoto)baada ya Airtel kukabidhi viti na meza kwa ajili ya polisi wa kituo cha oysterbay hivi karibuni.Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa wa Polisi wa kituo hicho.
Ofisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki (kulia) akisalimiana na Afisa Mnadhimu wa Polisi Kinondoni, Bibie Juma Athumani baada ya Airtel kukabidhi viti na meza kwa ajili ya polisi wa kituo cha oysterbay hivi karibuni.Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa wa kituo hicho.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendelea kuunga mkono serikali kupitia jeshi la polisi usalama barabarani kwa kuwapatia vifaa vya ofisi kwa ajili ya kituo cha Usalama Barabarani cha Oysterbay kilichopo wilaya ya Kinondoni.
  
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Afisa uhusiano na matukio wa Airtel  Dangio Kaniki alisema “Airtel inatambua umuhimu wa kazi inayofanywa na Kitengo cha Usalama Barabarani katika kusimamia na kuhakikisha usalama wa watanzania na kuamua kushirikina nao katika kuboresha mazingira ya kufanyia kazi. Leo tunatoa meza pamoja viti vya ofisi kwa kitu hiki cha polisi oystebay tukiamini   kwamba tutaongeza ari na moyo wa kujituma kwa maofisa hawa  na kuleta ufanisi wa kazi ,”

kwa miaka mitano mfululizo sasa Airtel imekuwa ikishirikiana na jeshi la polisi katika kufanikisha zoezi la usalama barabarani hivyo tumeonelea ni vyema kuendelea kushirikiana nao  ili kuleta mafanikio makubwa katika kutekeleza kazi zao  nchini.

Airtel itaendelea na dhamira yake  yakushirikiana na jeshi la polisi katika juhudi za kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa na kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua kwa kiasi kikubwa nchini

Kwa upande wake, Afisa Mnadhimu wa Polisi  Kinondoni, SSP. Bibie Juma Athuman alisema “Naishukuru sana Airtel kwa kutoa mchango wa vifaa vya ofisi kwenye kituo changu kwani tulikuwa na uhaba mkubwa wa viti na meza za kukalia wafanyakazi pindi wakiwapo ofisini. Msaada huu utasaidia kutatua matatizo tuliyokuwa nayo na kuboresha mazingira ya wafanyakazi wa kituo hiki kuwa mazuri zaidi.  Tunawaomba makampuni mengine pia yashiriki katika kuwawezesha jeshi la polisi na kuchangia katika kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa kama wanavyofanya wenzetu wa Airtel.”

 Msaada huo ni muendelezo wa mpango wa Airtel kusaidia Polisi  Usalama Barabarani hapa nchini ambapo mwezi Septemba mwaka jana kampuni hiyo imetoa T-shirt zenye ujumbe Maalum wa Usalama Barabarani, stika zenye ujumbe wa kuelimisha na mafunzo kwa ajili ya kuelimisha Usalama Barabarani kwa waendesha bodaboda mkoani Mwanza.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>