Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

JOB OPPORTUNITIES AT EAC SECRETARIAT

0
0
The Ministry of East African Cooperation (MEAC) would like to encourage qualified and eligible Tanzanians to apply for various job vacancies available at The East African Community (EAC) Secretariat in Arusha. The following vacancies are available:

1.       Director of Trade

2.       Director of Finance

3.       Principal Economist (Fiscal and Monetary Affairs)

4.        Principal Trade Officer (International Trade)

5.       Senior Trade Officer (Competition)

6.       Principal Customs Officer (Tariffs & Valuation)

7.       Principal Labour & Employment Officer

8.       Principal Administrative Officer

9.       Principal Civil Aviation Officer

10.Senior Public Relations Officer

11.Senior Conference Officer

12.EALA: Principal Clerk Assistant

13.EALA: Senior Clerk Assistant

14.EALA: Clerk Assistant

15.EALA: Sergeant -at- ARMs

16.EACJ: Court Administrator

17.EACJ: Personal Assistant

18.EACJ: Network Administrator

19.EACJ: Court Recorder /Transcriber

Interested candidates should submit their applications by registered mail, courier service, e-mail or dispatch together with Curriculum Vitae, copies of both academic and professional certificates and testimonials, names and addresses of three referees, and day time telephone contact to:


The Secretary General

East African Community

P. O. Box 1096

Arusha - Tanzania.


Fax No: +255 27 2504255/ +255 27 2050281

E-mail: vacancies@eachq.org


To be received not later than Thursday 06th March 2014, 1700Hrs local time. For more information on how to apply visit www.eac.int


MAHAFALI YA TATU YA SHULE YA SEKONDARI YA KAJUMULO GIRLS HIGH SCHOOL BUKOBA YAFANA, BW. JAMES RUGEMALIRA ATOA MILLIONI 200/-

0
0

wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya Kajumulo Girls High School wakati wa kusherekea mahafali ya tatu
Wanafunzi wa Kajumulo Girls High School wanaohitimu kidato cha 6 wakati wa kusherekea mahafali ya tatu katika shule yao.
Prof. Anna Tibaijuka kwa furaha akitoa neno.
Kwa niaba ya Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea na Mwana hisa wa “VIP Engineering and Marketing Ltd” Mzee James Rugemalira aliyependa kuwa nasi leo lakini akashindwa kutokana na majukumu mengine, tunayo furaha kuwatangazia, kuwa VIP ataanzisha mfuko maalum wa kusaidia katika kuboresha utoaji Elimu katika nchi yetu, utakaoitwa “Auleria Kobulungo Muganda Memorial Education Foundation Trust”. Mfuko huu unaanzishwa kwa heshima na kumbukumbu ya mzazi wetu mpendwa marehemu Ma Auleria Kobulungo Muganda.

Mheshimiwa mgeni rasmi, Tunayo furaha kutangaza kwamba shule yetu ya Kajumulo Girls High school ndio itakuwa shule ya kwanza kufaidika na mfuko huu, na leo, VIP kwa niaba ya “Auleria Kobulungo Muganda Memorial Education Foundation Trust” imetoa jumla ya TZS 200 million (TZS 200,000,000) kwa ajili ya kuwasadia baadhi ya watoto wasio na uwezo wa kujilipia lakini wana sifa za kujiunga na kusoma katika shule hii.Baba Methodius Askofu Kilaini nae alitoa neno
Mkuu wa Shule ya Kajumulo Girls High School Jospina Leonidace(kushoto) na kulia ni Fr. Vitus Mrosso (Nyuma) katikati ni Mr. Adrew Kagya akiwa na Rahim Kabyemela.

KAMPENI ZA UCHAGUZI JIMBO LA KALENGA:CCM YAZIDI KUJIHAKIKISHIA USHINDI

0
0
 Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (32), akiwapungia wananchi huku akiwa amebebwa alipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Mangalali,  Kata ya Ulanda, Iringa Vijijini leo mchana.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akiongoza msafara wa mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa aliyebebwa walipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Mangalali.
 Mgimwa akiungana na wanakijiji kucheza ngoma ya asili ya kabila la Wahehe alipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kibebe, Kata ya Ulanda mchana leo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Mwigulu Nchemba (kulia), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Joyce Msamba tavangu (katikati) na mgombea ubunge kupitia CCM,Godfrey Mgimwa wakicheza walipofika kwenye kampeni katika Kijiji cha Kibebe.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA WASHIRIKI TAMASHA LA MICHEZO DAR LIVE

0
0
Mpango wa Taifa wa damu salama kanda ya mashariki jana ulishiriki Tamasha la michezo katika ukumbi wa Dar Live kwa kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuchangia damu na kuendesha zoezi la kuchangia damu kwa hiari.

Tamasha hilo liliandaliwa na kuratibiwa na klabu ya Magenge ishirini na mianzini kwa kushirikisha klabu mbalimbali kama last jogging, Temeke family, kingugi, Respect na nyingine nyingi. Tamasha hilo lilidhaminiwa na Global publisher, PSPF, Akiba Commercila Bank na Damu salama ambapo mgeni rasmi alikuwa Mheshimiwa Angela Kizigha Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki ambaye aliongozana na Mbunge wa Kigamboni Mheshimiwa Dr Faustine Ndugulile pamoja na Diwani wa keko Bwana Noeli.

Tamasha hilo lilikuwa na malengo yafuatayo:

Kuchangia damu kuisaidia kuondokana na changamoto ya upungufu wa Damu katika hospitali za serikali na binafsi.

kujadili kwa pamoja changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana kama ukosefu wa ajira na madawa ya kulevya, kuleta umoja, mshikamano na undugu baina ya vijana kupitia michezo na kuburudika na kufurahi kwa pamoja kwani ni sehemu ya maisha.

Akijibu risala ya klabu ya magenge ishirini, Mgeni rasmi aliwashukuru kwa moyo waliouonyesha wa kuandaa tamasha ambalo lina lengo la kukutanisha klabu mbalimbali na kuchangia damu kwa hiari na pia aliahidi kuwazawadia shilingi milioni moja na nusu ambazo zitatumika katika shughuli mbalimbali za klabu, pia mbunge wa kigamboni mheshimiwa Dr Faustine ndugulile aliwazawadia shilingi milioni moja na diwani wa keko Bwana Noel alitoa zawadi ya shilingi laki tano.

Katika Tamasha hilo Jumla ya chupa za damu 90 zilikusanywa ambazo zitapimwa na kusambazwa katika hospitali mbalimbali jijini Dar-es-salaam.

Mbunge wa kigamboni mheshimiwa Dr Faustine ndugulile pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika mashariki Mheshimiwa Angela Kizigha wakichangia damu.
Mmoja wa washiriki wa Tamasha la michezo akipimwa wingi wa damu kabla ya kuchangia.

SHORT TRAINING CERTIFICATE COURSES AT GTI

EdExpo Tanzania, Spring 2014 Information, Partnerships and Collaboration Seminar at - Dar es Salaam Serena Hotel, 12th March, 3.00pm to 6.00pm

0
0
Dear Seminar Participant,
 
We hope this finds you well.

Catalyst International Ltd once again invites you to the EdExpo Tanzania,  Spring 2014 Information, Partnerships and Collaboration Seminar to be held at the Dar es Salaam Serena Hotel on 12th March 2014 starting at 3.00pm.

The seminar will be presented by representatives of the universities and institutions taking part in EdExpo Tanzania 2014 from 11th to 12th March 2014 at Dar es Salaam Serena Hotel.  They will discuss their available undergraduate/postgraduate study  programs and possible collaboration in higher, tertiary and vocational education,  the setting up of long-term collaborative staff development programs and tailor made courses, available scholarships and form international strategic alliances that will enhance joint learning, teaching and research.

IE Business School (Spain) and Toulouse Business School (France), two out of the worlds accredited and top ranked business schools will be available both at the exhibition (11th and 12th March) and at the seminar (12th March) to meet qualified MBA and Executive MBA professional candidates who are serious about their business and career prospects, with information about online, distance and on site courses.

Other universities at the exhibition and seminar offering undergraduate and postgraduate/research programs include University of Wolverhampton (England), University of Newcastle (Australia), North-West University (South Africa),   University of South Australia (Australia), Bahcesehir University (Turkey), Symbiosis International University (India), Istanbul Aydin University (Turkey), University of Johannesburg (South Africa), Swiss Education Group - SEG (Switzerland), St. George's University (Grenada), Riga Technical University (Latvia), SRM University (India), European University of Lefke (Cyprus).  

Attendance to the seminar is free, but by invitation only
 (Attendance to the exhibition is free - no invite required)

To get an invitation to the seminar, please email your full names, institution/business name, job title and full contact details to register@catalystexpo.com  and we will send you an official invitation to the seminar.

More details are available at www.edexpo.fall.catalystexpo.com

Lupita Nyong'o kutoka kenya ashinda tuzo ya oscar ya muigizaji msaidizi bora wa kike

0
0
Muigizaji Lupita Nyong'o kutoka Kenya amenyakuwa tuzo ya Oscar ya mwigizaji msaidizi wa kike (Best Supporting actress) kwa uigizaji wake katika  filamu ya utumwa ya ''12 Years A Slave.'' leo  alfajiri mjini Los Angeles, Marekani. 
Muigizaji  Will Smith ndiye aliyetangaza matokeo hayo, na baada ya kupokea tuzo hiyo kwa shangwe Lupita alifunguka na kusema: " Haikwepi mawazo yangu kwamba hata dakika moja ya furaha katika maisha yangu ni shukrani na maumivu makubwa kwa mtu mwingine.'' pia aliongezea na kusema " Na iwe ukumbusho kwangu na kila mtoto kwamba kokote unakotoka, ndoto zako ni halisi.''

New City Pub ndio Mabingwa wa Safari Nyama Choma 2014 jijini Mbeya

0
0
Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Dk.Samweli Lazaro (katikati) na jaji Mkuu wa mashindano ya Safari Nyama Choma, Lawrence Salvi (kulia) wakimkabidhi zawadi ya Kombe na fedha taslimu Shilingi milioni moja(1,000 000) mpishi Mkuu wa New City Pub, Geofrey Mwashilindi mara bada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma 2014 yaliyojanyika katika Viwanja vya CCM Ilomba Mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki .Wapili kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo na Meneja wa Tawi la TBL Kanda ya Kusini, Vivianus Rwezahula.
Mpishi Mkuu wa New City Pub, Geofrey Mwashilindi akishangilia na kitita cha Shilingi milioni moja(1,000 000) mara baada kibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma 2014 kwa Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika CCM Ilomba mwishoni mwa wiki .Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa mashndano hayo, Lawrence Salvi,Meneja wa bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mbeya, Sameli Lazaro, Meneja wa Tawi la Tbl Kanda ya Kusini, Vivianus Rwezahula na Meneja mauzo na matukio Tbl Mbeya, Clauds Chawene.
Mashabiki wa New City Pub wakiwa wamembeba juu mpishi mkuu wa pub hiyo, Geofrey Mwashilindi mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma 2014 kwa Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Ilomba mwishoni mwa wiki.
Mashabiki na wapishi wa New City Pub wakishangila ndano ya gali lao aina ya Pic up yenye namba za usajili T952 BFB wakielekea kwenye Pub yao mara baada ya kuibuka mabingwa wa Safari Nyama Choma 2014 yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Ilomba mwishoni mwa wiki.

MISA YA KUMUOMBE MZEE WETU MAJOR SAMUEL ISAAC SHEKINGO -JUMAMOSI MARCH 8, 2014 CHICAGO-ILLINOIS

0
0
Mdau Samson Chekingo anapenda kuwataarifu wote Misa ya kumuombea Mpendwa Baba Yake Major Samuel Isaac Chekingo.Itakayofanyika siku ya Jumamosi 3-8-2014 kuanzia saa  9 jioni (3 PM) had 1 usiku (7 PM) Katika Kanisa la kiluteri lililopo HYDE PARK-South Side of Chicago.

Anuwani ya Kanisani:

AUGUSTANA LUTHERAN CHURCH OF HYDE PARK
AND LUTHERAN CAMPUS MINISTRY
5500 SOUTH WOODLAWN AVE
CHICAGO - IL 60637
Tafadhali tunaomba kuzingatia muda wa Ibada ambayo itaanza saa 9 kamili (3pm).

Major Samuel Isaac Shekingo alifariki Tarehe 01-28-2014 Katika Hospitali ya Lugalo.
Kwa taarifa zaidi unaweza kuwasiliana na:

RSVP to:
Samson Chekingo
Phone #: 847-987-9637
Email address: samchecks@hotmail.com

MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANZANIA NA USHIRIKIANO KATIKA UTUMISHI WA UMMA.

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) katikati akiongea katika kipindi cha Jambo Tanzania kuhusu Mashirikiano katika Utumishi wa Umma katika miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, kulia ni Mh. James Mbatia, kushoto ni Mtangazaji wa TBC Shaban Kissu.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 03.03 .2014

MECHI YA YANGA, AHLY YAINGIZA MIL 488

0
0
 Mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly kutoka Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki imeingiza sh. 448,414,000.

Mapato hayo yametokana na watazamaji 50,202 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 7,000, sh. 13,000, sh. 25,000 na sh. 35,000. Yanga ilishinda mechi hiyo kwa bao 1-0.

Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 68,402,135.59, gharama za kuchapa tiketi ni sh. 10,343,219, waamuzi na kamishna sh. 14,665,930 na matangazo sh. 15,679,000.
Uwanja sh. 50,898,557.31, gharama za mchezo sh. 33,932,371.54, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)/Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 33,932,371.54 wakati Yanga ilipata mgawo wa sh. 220,560,415.01.

Nayo mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa jana (Machi 2 mwaka huu) imeingiza sh. 20,610,000 ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh. 4,402,492 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 3,143,898.31.

KIKOSI CHA TAIFA STARS CHATUA WINDHOEK

0
0
Kikosi cha Taifa Stars kimeondoka leo alfajiri kwenda Windhoek, Namibia kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya wenyeji itakayochezwa Machi 5 mwaka huu.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ina msafara wa watu 25 unaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Timu imefikia hoteli ya Safari jijini humo.

Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Sam Nujoma, na kikosi cha Taifa Stars kipo chini ya Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi ambaye ana leseni A ya ukocha inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).


Namibia (Brave Warriors) inayofundishwa na kocha Ricardo Mannetti imeingia kambini jana (Machi 2 mwaka huu) kwa ajili ya mechi hiyo ambayo tiketi zake zilianza kuuzwa Februari 28 mwaka huu.

HESLB YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MSAADA ORCI

0
0
WAFANYAKAZI Wanawake wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa misaada kwa wagonjwa takriban 200 waliolazwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) ya jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya wafanyakazi wa wanawake wa HESLB ndani ya Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Utafiti na kazi nyinginezo (RAAWU), Bi Octavia Selemani amesema kuwa wameafikiana kufanya hivyo kama taasisi ili kutoa mchango wao kwa wanajamii ambao wanahitaji zaidi msaada na faraja kutokana na kuwa katika hali ya maradhi sugu ya saratani.

Katika kutekeleza tukio hilo ambalo limefanyika wiki moja kabla ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, Wafanyakazi hao kutoka idara na vitengo mbalimbali vya taasisi hiyo ya serikali, wametoa msaada wa bidhaa za mahitaji ya kila siku ikiwa ni pamoja na mchele, unga wa sembe, maharage, sukari, mafuta ya kupikia, sabuni za mche, sabuni za unga na dawa za meno.

Msaada huo wa thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2 ulikabidhiwa Jumamosi ya Machi mosi, 2014 kwa Muuguzi Mkuu wa zamu Bi Ofarasia Muhoha (Registered Nurse) kwa niaba ya uongozi wa taasisi hiyo.

Kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, 2014, Bi Octavia amesema kuwa siku hiyo wafanyakazi wanawake watashiriki shughuli za maadhimisho ikiwa ni pamoja na kuandamana na kusikiliza hotuba ya mgeni rasmi kupata ujumbe wa siku hiyo.

Baada ya maandamano, watakaa pamoja, kuzungumza na kutathmini mchango wao wa utendaji kazi katika kujenga taifa kwa kupima mafanikio dhidi ya changamoto wanazokabiliana nazo na kutafuta mbinu za kupata mafanikio zaidi.

Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa Machi 8 kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya jitihada za wanawake katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa miaka iliyopita na kupanga mikakati ya mafanikio zaidi kwa miaka ijayo.

Katika baadhi ya nchi kama China, Russia, Vietnam na Bulgaria, siku hii ni ya mapumziko na inaadhimishwa kwa wananchi kuonyesha jinsi wanavyothamini na kutambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya nchi zao.

Mwaka huu maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kitaifa yanafanyika kwa ngazi ya mkoa yakiongozwa na kauli mbiu isemayo, “Chochea Mabadiliko kuleta Usawa wa Kijinsia”, ikisisitiza na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia masuala ya jinsia katika kuandaa mipango, bajeti na programu za maendeleo katika jamii.
Jengo jipya la mawadi ya wagonjwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Mtaa wa Luthuli, Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakishusha mahitaji kutoka kwenye gari tayari kuikabidhi wa uongozi wa ORCI.
Baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakijiandaa kuingia katika wodi la kwanza la wanaume ambako kuna wagonjwa 60.

TASAF YAFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA MAAFISA WAKE JIJINI DAR LEO

0
0
 Maafisa ufuatiliaji wa TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (aliyeketi katikati) baada ya kufungua semina elekezi jijini DSM
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga akisisitiza jambo wakati alipofungua semina elekezi kwa maafisa ufuatiliaji (TA) iliyofanyika kwenye ukumbi wa CEEMI jijini DSM.
 Baadhi ya Maafisa ufuatiliaji ambao wanatarajiwa kuanza kazi katika halmashauri kadhaa za wilaya nchini wakimsikiliza mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani)alipofungua semina elelekezi .
Mkurugenzi wa Uratibu wa TASAF Alphonce Kyariga akitoa neno la utangulizi kwa maafisa Ufuatiliaji wa TASAF ambao wameanza semina  elekezi ya siku TATU kwenye ukumbi wa CEEM jijini DSM.

WADAU WA AFYA WAKUTANA MOSHI KUJADILI SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

0
0
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas gama akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa Afya kujadili juu ya saratani ya mlango wa kizazi.
Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Rufaro Chatora akizungungumza kwa niaba ya wadau wa Maendeleo.
Mkurugenzi huduma za Afya toka wizara ya Afya,Dk Neema Rusibamayile akizungumza kwa niaba ya mganga mkuu wa serikali katika mkutano huo unaofanyika Uhuru Hotel.

Balozi Seif Ali Idd awapongeza Viongozi na Wanachama wa CCM wa Tawi la Mafufuni,Bumbini kwa uamuzi wao wa kujenga Tawi jipya la CCM

0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi amewapongeza Viongozi na Wanachama wa CCM wa Tawi la Mafufuni Jimbo la Bumbwini kwa uamuzi wao wa kujenga Tawi jipya la CCM lenya hadhi ya Chama chenyewe.

Balozi Seif alisema hayo wakati akikabidhi mchango wa Shilingi Milioni moja kwa ajili ya uwezekaji wa Tawi hilo kufuatia ahadi aliyoitoa ya kusaidia harakati za ujenzi wa Jengo hilo mchango alioukabidhi kwa uongozi wa Tawi hilo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Alisema lengo la Chama cha Mapinduzi katika Maboresho yake ya uimarishaji wa Chama hicho imewaagiza Viongozi na Wanachama wa Chama hicho ngazi za Matawi, Wilaya na Mkoa kujikita katika ujenzi wa Ofisi zitakazofanana na Chama chao.

Alifahamisha kwamba wakati umefika kwa Wana CCM kuhakikisha kwamba wanaondokana na tabia iliyozoeleka katika baadhi ya Matawi Nchini kukutana katika vikao vyao chini ya Miti.

Alisema kwamba Uongozi wa Juu ya Chama cha Mapinduzi ngazi ya Taifa utaendelea kutoa muongozo sambamba na kushajiisha wanachama wake kuendeleza mpango huo hasa katika yale maeneo ambayo hadi sasa hayajaamua kujenga majengo ya kudumu na ya Kisasa ya chama chao.

Alielelezea matumaini yake kwamba juhudi zinazochukuliwa na wanachama walio wengi katika maeneo mengi Nchini za ujenzi wa majengo yao utawawezesha wanachama hao kuingia katika chaguzi za chama hicho katika mazingira mazuri ya makazi.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi mchango wa Shilingi 1,000,000/- kwa Katibu wa CCM Tawi la Mafufuni Jimbo la Bumbwini Nd. Muslih Maulid Fidia kwa ajili ya uwezekaji wa Tawi lao la CCM. Kati kati yao aliyevaa suti ni Diwani wa Wadi ya Makoba Bwana Juma Zahor.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa CCM Tawi la Mafufuni mara baada ya kuukabidhi mchango wa Fedha kwa ajili ya uwezekaji wa Tawi lao. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

KITAMBI NOMA ILIPOONYESHANA KAZI NA USHIRIKA VETERANI

MATUKIO MBALI MBALI KUELEKEA US-AFRICA LEADERS SUMMIT AGOSTI 5-6 WASHINGTON DC

0
0
Pichani Mhe. John Haule akisalimiana na Balozi Teitelbaum katika Wizara ya Nje ya Marekani. Kulia ni Mhe.Liberata Mulamula,Balozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mhe. John Haule(katikati) katika picha ya pamoja na Mhe.Balozi Donald Teitelbaum(kushoto) na Mhe.Balozi Mulamula (kulia)
Mhe. Balozi Liberata Mulamula baada ya kumaliza mazungumzo yake na Bw. Michael Morrow, Mkurugezi wa Idara ya Afrika Mashariki baada ya mazungumzo yao katika Wizara ya nje Marekani.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Balozi S.Beattle, Mshauri wa Rais Obama kuhusu US-African Leaders Summit baada ya mazungumzo yao Ubalozini Tanzania House Washington DC.
Mhe.. Balozi Liberata Mulamula (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Beattle(Kushoto) na Bw. Sam Watson (kulia) Msaidizi Maalum wa Balozi Beattle

Kufuatia mwaliko wa viongozi 45 wa bara la Afrika kuhudhuria mkutano wa kihistoria uliopewa jina la US-Africa Leaders Summit utakaofanyika Washington DC,Marekani tarehe 5-6 Agosti 2014, mchakato na mikutano mbalimbali imeendelea kufanyika kuelekea k mkutano huo wa kihistoria ambao Rais Barack Obama atachanganyika na viongozi kuzungumza nao na kuwasikia hoja zao mbali zitakazolenga kuimarisha uhusiano wa nchi hizo na Marekani.

Kwa upande wa Serikali ya Tanzania Mhe. John Haule,Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alipata fursa ya kukutana na Balozi Donald Teitelbaum, Naibu wa Naibu wa Waziri wa Nje wa Marekani katika Wizara ya Nje ya Marekani hivi karibuni na kuzungumza nae masuala mbali yanayohusu mkutano wa US-Africa Leaders Summit pamoja na masuala mengine ya mashirikiano baina ya Tanzania na Marekani.

MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAKUTANA NA WAANDISHI NA WADAU WA HABARI JIJINI DAR LEO KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio akizungumza wakati wa mkutano na waandishi na wadau wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam leo. 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absolom Kibanda, akizungumza wakati wa  mkutano na waandishi na wadau wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano ambao pia ni waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano uliondaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati wa  mkutano na waandishi na wadau wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam leo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images