Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 363 | 364 | (Page 365) | 366 | 367 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kukagua gari aina ya Ashok Leyland iliyotolewa na Wizara yake kwa ajili kuimarisha viteule vya kijeshi vya Kasanga na Kirando Mkoani Rukwa. Katika kukabiliana na changamoto zilizokuwa zinavikabili vitua hivyo Wizara ya ulinzi kupitia kwa Katibu Mkuu huyo imetoa gari mbili, boti mbili na fedha Tsh. Milioni 150 kwa ajili ya kuboresha makazi na miundombinu katika viteule hivyo. Kwa upande mwingine amesema kuwa baadhi ya vifaa vingine vitatoka makao makuu ya jeshi katika kuboresha viteule hivyo. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akimkabidhi funguo ya gari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kama ishara ya makabidhiano ya gari mbili pamoja na michango mingine itakayotumika katika viteule vya jeshi vya Kasanga na Kirando Mkoani Rukwa.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwasha gari hilo kama ishara ya kupokea misaada hiyo kwa viteule viwili vya Kirando na Kasanga vilivyopo Mkoani Rukwa.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima wa pili kushoto akitoa majumuisho ya ziara yake kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa leo. Katika majumuisho yake pamoja na mambo mengine aliongeza kuwa mchakato wa kupanua kiteule cha Kasanga utawekwa kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha ili kukiongezea ufanisi zaidi. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ambae ndiye chachu kubwa ya mafanikio haya kwa kumualika Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi kuja kujionea changamoto zilizopo amemshukuru kwa kuitikia wito wake na mchango wa ujumla uliotolewa na Wizara yake katika kuimarisha ulinzi katika ukanda wa ziwa Tanganyika unaopakana na nchi za Burundi, Zambia na DRC. 
  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu  Symthies Pangisa kushoto  akizungumza katika kikao hicho cha majumuisho ambapo amemshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na msafara wake kwa kazi nzuri waliyoifanya Mkoani Rukwa katika kipindi chote cha ziara yake ya siku tatu.
  Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao hicho cha majumuisho wakifuatilia kwa makini.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  TWIGA STARS, ZAMBIA SASA KUCHEZA FEB 28

  Mechi ya pili ya raundi ya kwanza kuwania Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Zambia (Shepolopolo) sasa itachezwa Februari 28 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.


  Twiga Stars tayari ipo kambini kujiandaa kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni. Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage inafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Karume ambao ni wa nyasi za bandia kama ulivyo ule wa Azam Complex.


  Shepolopolo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Februari 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.


  Iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuiondoa Shepolopolo itacheza na mshindi wa mechi kati ya Botswana na Zimbabwe. Zimbabwe ilishinda mechi ya kwanza ugenini.


  Wachezaji wa Twiga Stars waliopo kambini ni Amina Ali, Anastazia Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Everine Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma Mustafa, Fatuma Mwisendi, Fatuma Omari, Flora Kayanda, Happiness Mwaipaja, Maimuna Mkane, Mwajuma Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Pulkeria Charaji, Sherida Boniface, Sophia Mwasikili, Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.


  MECHI TANO VPL KUCHEZWA JUMAMOSI

  Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 19 kesho (Februari 22 mwaka huu) kwa mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Bukoba, Morogoro, Tanga na Arusha.


  Yanga itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting ya mkoani Pwani katika mechi itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Nayo Kagera Sugar inaikaribisha Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.


  Uwanja wa Manungu uliopo Turiani mkoani Morogoro ndiyo utakaotumika kwa mechi kati ya Mtibwa Sugar na Ashanti United, wakati Coastal Union itaumana na Mbeya City katika mechi itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kutoka Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.


  Maafande wa Oljoro JKT watakuwa nyumbani kupambana na Mgambo Shooting katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.


  Jumapili (Februari 23 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa ni Simba dhidi ya JKT Ruvu, mechi ambayo pia itaoneshwa moja kwa moja na Azam Tv. Mechi kati ya Azam na Tanzania Prisons iliyokuwa ichezwe kesho (Februari 22 mwaka huu) Uwanja wa Chamazi sasa itachezwa Jumapili (Februari 23 mwaka huu) ambapo na itakuwa ‘live’.


  Ligi hiyo itaendelea Jumatano (Februari 26 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Ashanti United na Azam itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex (Chamazi).


  MICHUANO YA MIKOA KUSAKA VIPAJI YATIMUA VUMBI

  Michuano ya mikoa katika mpango maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuboresha Taifa Stars inaanza kutimua vumbi kesho (Februari 22 mwaka huu) kwa mechi nne.


  Mechi rasmi ya ufunguzi wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa kati ya Ilala na Temeke. Mechi hiyo ya kundi G itachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kuanzia saa 9.30 alasiri.


  Kundi A kutakuwa na mechi kati ya Pwani na Morogoro kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi wakati Kusini Unguja na Kaskazini Unguja zitacheza kwenye Uwanja wa Mao Tse Tung mjini Unguja katika kundi H.


  Kusini Pemba na Kaskazini Pemba zitacheza mechi ya Kundi I katika Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.


  Mechi za keshokutwa (Februari 23 mwaka huu) ni Simiyu itacheza na Shinyanga mjini Bariadi katika kundi E. Nayo Ruvuma itacheza na Njombe kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea katika kundi D.


  Kundi C ni Tanga na Kilimanjaro kwenye Uwanja wa Mkwakwani wakati Kagera itacheza na Geita kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika kundi B. Mtwara itacheza na Lindi kwenye Uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara katika kundi F.


  Wang’amuzi 40 wa vipaji tayari wamesharipoti kwenye vituo vya mechi hizo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.


  RAIS MALINZI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika Jumatatu (Februari 24 mwaka huu).


  Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ofisi mpya za TFF zilizopo ghorafa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Garden na Ohio jijini Dar es Salaam.


  Boniface Wambura Mgoyo

  Ofisa Habari na Mawasiliano


  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akifafanua jambo kwa mmoja wa washindi wa Bodaboda Amanzi Mohamed kutoka Bagamoyo wakati wa zeozi la washindi hao kuchukua bodaboda hizo Makao Makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es salaam.Washindi hao ni wa Promosheni ya Timka na Bodaboda iliyomalizika hivi karibuni.
  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akifurahi na Mama Domotila Charles akikwaa bodaboda yake tayari kuiwasha na kuondoka nayo kutoka Makao Makuu ya kampuni hiyo akiwa ni mmoja wa washindi wa Promosheni ya Timka na Bodaboda iliyomalizika hivi karibuni.
  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim (wa pili kushoto) akiwaruhusu washindi wa iliyokuwa promosheni ya Timka na Bodaboda kuondoka na bodaboda zao mara baada ya kuzipokea rasmi makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam.
  Ofisa Masoko wa Vodacom Prestin Lyatonga na Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni hiyo Salum Mwalim wakiwaanga washindi wa bodaboda wa iliyokuwa promosheni ya Timka na Bodaboda. Iliyomalizika. Washindi mbalimbali wanaendelea kuchukua zawadi zao hizo kutoka Makao Makuu ya Vodacom jijini Dar es salaam.

  0 0

  Uchaguzi wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utafanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam.

  Fomu kwa ajili ya waombaji uongozi zinaanza kutolewa Jumatatu (Februari 24 mwaka huu) kwenye ofisi za Idara ya Habari. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri.

  Ada kwa wagombea wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhazini na Mhazini Msaidizi ni sh. 50,000 kwa fomu. Nafasi za wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu zinapatikana kwa sh. 20,000.

  Kamati ya Uchaguzi inawahimiza wanachama wa TASWA kujitokeza kwa wingi kugombea, lakini vilevile waisome vizuri Katiba ya chama chao.

  Boniface Wambura
  MWENYEKITI KAMATI YA UCHAGUZI

  0 0

  Na woinde shizza,Arusha

  Raisi wa Chama cha Wanasheria Tanzania ,Tanganyika Law Society (TLS),Francis Stola amesema kuwa kazi ya Bunge la Katiba itapimwa na wananchi kupitia kura ya maoni ya Katiba inayowapa mamlaka ya kuikataa katiba hiyo ama kuikubali endapo wanaona kuwa maoni yao hayakuzingatiwa.

  Licha ya kifungu cha 25 cha sheria ya mabadiliko kutokufafanua madaraka halisi ya tume hiyo lakini pia wametakiwa kutengeneza katiba inayotakiwa na Watanzania walio wengi.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano wa chama hicho ,Stola amesema kuwa kiwango cha madaraka ya Bunge la Katiba hakijaainishwa wazi na sheria hiyo na hata hivyo katiba watakayoipendekeza itarudishwa kwa wananchi ambao ndio wana mamlaka kamili katika kuipigia kura ipitishwe ama isipitishwe.

  “Wananchi wakiona maoni yao hayamo wanaruhusiwa kuikataa ,tunaamini madaraka ya Bunge la Katiba hayataathiri maoni ya wananchi kwasababu Rasimu ya pili ya Katiba imejengwa na Sauti za watanzania na maoni yao pia ” Alisema Stola.

  Kwa upande Jaji Mstaafu Agustino Ramadhani amesema kuwa Bunge la Katiba lina mipaka haliwezi kubadilisha kila kitu ni kuinoa tu. “Msimamo wa tume umeshatolewa na na Mwenyekiti Jaji Warioba ,maoni yangu ni kwamba Wajumbe Waangalie maslahi ya Tanzania tunayoitaka wasiangalie misimamo ya vyama” Alisema Warioba.

  Pia amezungumzia suala la posho ya Wajumbe wa Bunge la Katiba na kueleza kuwa malipo hayo ya kiasi cha laki tatu 300,000 ni kiasi ambacho ni kikubwa kwa Watanzani walioajiriwa na waliojiajiri hawaingizi hiyo hela kwa siku hivyo amewataka waone ni heshima kubwa wamepewa kwa kufanya jambo k wa mustakabali wa taifa na hakuna anyeweza kuwalipa kwa kazi hiyo.

  Naye Raisi wa Shirikisho la Wanamuziki Tanzania ,Ado Novemba Masongo akizungumzia suala la posho ya wajumbe wa bunge hilo amesema kuwa suala hilo ni fedheha na wamesikitishwa sana na jambo hilo kwani walipaswa kugharamiwa na taasisi walizotoka ili kulifanya jambo hilo kwa uhuru zaidi.

  “Inasikitisha sana kuna walimu mishahara yao haifiki laki 3 kwa mwezi,polisi na wanajeshi lakini wao wanaitaka kwa siku moja,wameonyesha makucha yao mapema tuko tayari kuandaa maandamano tukishirikiana na wananchi kupinga suala hili” Alisema Ado

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Mahindra&Mahindra Ltd,kutoka India ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.ujumbe huo unaoongozwa Bw.Sanjay Jadhar, ulifanya mazungumzo na Rais.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Bw.Sanjay Jadhar, Kiongozi wa Ujumbe wa Kampuni ya Mahindra&Mahindra Ltd,kutoka India walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi na kufanya mazungumzo na Rais.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0

  Greetings, a group of more than 1000 humble good Samaritans have joined and opened a group on face book for blood donations for free in Dar.


  0 0

  Zaidi ya wajasiriamaili wanawake 1000 kutoka katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wamepata mafunzo ya kuwajengea uwezo wakati wa tamasha la Mwanamke na Akiba, 2014 lililofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala.

  Akizungumzia Tamasha hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, Naima Malima alisema kuwa lengo la semina hiyo ni kuchochea utamaduni wa kuweka akiba kwa wanawake wajasiriamali na kuwaelimisha aina tofauti ya kuweka akiba.

  Aidha Naima aliongeza kuwa pia itachoche kuwakomboa wanawake toka kwenye lindi la umaskini kupitia uwekaji wa akiba, uwekezaji wa kuongeza kipato, pia kuongeza wanawake katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

  "Kupitia semina hii wanawake wataweza kupata njia bora za kuwawezesha kuweka akiba kwa muda mfupi, mudac wa kati na muda mrefu"

  Tamasha hilo lilidhaminiwa taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo, Benki ya CRDB, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). PSPF,  SS Bakhresa, GEPF, Stanbic Bank, Convenant Bank, K-Finace, UTT, Montage, HSC, Minjingu Mazao, Dar Live, Afrcan Real Estate na ETG Group.

  Kupitia tamasha hilo wadhamini walipata fursa ya kujitangaza na kutangaza bidhaa na huduma zao, kwa lengo la kuongeza ufahamu wa bidhaa zao kwa wanawake wa Kitanzania.
   Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB tawi la Mbagala, Mohamed Madengelo akitoa mada wakati wa Tamasha la Wanawake na Akiba 2014 lililoandaliwa na Kampuni ya Angels Moment  kwa ajili ya kuwajenga uwezo wanawake wajasiriamali na kufanyika jijini Dar es Salaam. Benki ya CRDB ilikuwa moja ya wadhamini wa tamasha hilo. 

   Baadhi ya akinamama wakifuatilia mada wakati wa Tamasha la Wanawake na Akiba 2014 lililowashirikisha wanawake wajasiriamali kutoka maeneo ya Mbagala na vitongoji vyake. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 02/21/14--04:45: Job Opportunity
 • Job Opportunity

  Sales
  We are looking for highly motivated sales people to market auto repair & maintenance services.

  Responsibilities:

  • Develop new business opportunities through cold calls and lead generation.

  • Develop and execute a comprehensive monthly sales plan and expand our business with our existing as well as our new customers.

  • The sales person will coordinate closely with our inside sales support team the promotion of products and services to our customers.

  • The development and execution of a detailed annual sales plan will be a critical requirement for this position.

  • Organize sales activities so that face to face selling time to the customer is maximized.

  • Utilize selling and professional traits needed to make a positive impact on all prospects and customers.

  • Display enthusiasm and treat all prospects and customers with respect.

  • Display professionalism in appearance and mannerisms at all times.

  • Samples, sales aids and personal grooming are neat, clean and fresh looking.

  • Constantly work on self-improvement and learning.

  • Analyze personal performance and learn from mistakes.

  • React positively to evaluations, appraisals, and feedback and work to improve development objectives.

  • Observe and benchmark off of other outstanding Sales Representatives in all aspects of the sales process to utilize skills necessary in your sales territory.

  • Consistently make the kind of effort necessary to accomplish sales goals.

  Requirements:

  • Fluency in both English and Swahili

  • Sales experience will be considered an advantage

  • Fast Learner & self-starter

  • Excellent communication skills

  • At least high school education with good grades

  How to Apply:

  ·          Send your CV, a brief cover letter and expected monthly income to careers@staralliancelogistics.com

  ·           Deadline to apply is 28th February 2014

  All shortlisted candidates will be contacted to interview

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSPF, Adam Mayingu akizungumza na Waandishi wa habari pamoja na wadau wa mfuko huo katika semina ya siku moja kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo na fursa mbalimbali pamoja na mafao yanayotolewa na mfuko. 

  Miongoni mwa huduma wanazotoa na ikiwa ni huduma ya fao jipya ni Mpango wa Uchangiaji kwa Hiyari  (PSS) ambapo mwanachama anatakiwa kujiunga kwa kiwango cha chini cha shilingi 10,000/= na kuchangia kadri awezavyo kila siku, wiki, Mwezi na kwa msimu kadri uwerzavyo. Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jengo la Golden Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.
   2 
  Neema Muro Mkurugenzi wa Uwekezaji katika mfuko huo akitoa mada juu ya uwekezaji katika mfuko wa PSPF.
  Mkurugenzi wa Fedha Masha Mushomba akizungumzia masuala ya fedha na ukusanyaji pamoja na ulipaji mafao kwa wanachama wa mfuko huo.
  Andrew Nkangaa Mkurugenzi wa Tehama katika mfuko huo akizungumzia jinsi wanachama wanavyoweza kuchangia mfuko huo kwa kutumia mitandao ya simu na  kurahisisha shughuli zao za kila siku badala ya kufuata ofisi za PSPF zilipo kwa ajili ya kwasilisha michango yao.
   Wanahabari ambao ni washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakifuatilia mada kwa umakini.HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Faustine Ruta, Bukoba
  Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 19 kesho (Februari 22 mwaka huu) kwa mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Bukoba, Morogoro, Tanga na Arusha.
  Kocha wa Rhino Rangers
  Wachezaji wa Timu ya Rhino Rangers kutoka Tabora wakifanya mazoezi yao ya mwisho kwenye Uwanja wa Kaitaba jioni hii, Kesho Kuwakabili Wenyeji Kagera Sugar. Rhino Rangers ambao wanashika nafasi ya mkiani mwa ligi hiyo pendwa ya Vodacom wanapointi 23.
  Kesho tunataka tuondoke na Pointi zote tatu!!

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Mhe. Nabil Fahmy  wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu  ziara ya siku tatu ya Mhe. Fahmy hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 23 Februari, 2014. Mhe. Fahmy yupo nchini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan katika nyanja za afya, elimu, uwekezaji na siasa. 
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwasikiza Mhe. Membe na Mhe. Fahmy (hawapo pichani) walipozungumza nao
  Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Vincent Kibwana (kushoto waliokaa)  na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga wakinukuu mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Fahmy (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wao na Waandishi wa Habari. 
  Mhe. Fahmy nae akizungumza wakati wa mkutano huo.
  Waandishi na Maafisa kazini.

  0 0

  HAYAWI hayawi, sasa yamekuwa! Ule uzinduzi wa albamu ya ‘Mtendwa Akitendewa’ kutoka bendi ya Extra Bongo kesho utafikia kilele ambapo watadondosha bonge la shoo katika ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem. 
  Akizungumzia maandalizi ya mwisho kuelekea shoo ya albamu hiyo katika hoteli maarufu ya Atriums iliyoko Afrika Sana, Sinza, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choky, alisema kila kitu kinaenda sawa na hivi sasa kilichobaki ni kudondosha mashambulizi siku ya kesho usiku. 
  Burudani hiyo itanoga zaidi kutokana na kusindikizwa na wakali wa Bongo Fleva kina Amin na Linah, Makhirikhiri wa Bongo, Bendi ya Mashujaa, TOT Band chini ya ‘Malkia wa Mipasho’ Khadija Kopa. Kiingilio kitakuwa ni sh. 6,000 tu. 
  HABARI/PICHA: ANDREW CARLOS, GPL
  Kiongozi wa Extra Bongo, Ally Choky, akizungumzia uzinduzi huo ndani ya hoteli ya Atriums iliyopo Afrika Sana, Sinza.
  Mratibu wa Burudani Dar Live, Luqman Maloto, akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Choky na Muumin Mwinjuma.
  Extra Bongo wakiwa katika picha ya pamoja na Maloto katika hoteli ya Atriums.

  ...Titi, Super Nyamwela na Sharapova wakionyesha mbwembwe zao kwa wanahabari (hawapo pichani).
  Mnenguaji wa Extra Bongo, Sharapova akiwa katika pozi.
   
  Titi Mwinyi katika pozi.

  Banza Stone mmoja wa vivutio katika uzinduzi huo wa kesho.
  Titi, Nyamwela na Sharapova wakiwa katika pozi.
  Wanamuziki wa Extra Bongo wakipozi pamoja na Muumin Mwinjuma kwenye ukumbi wa hoteli ya Atriums iliyopo Afrika Sana, Sinza.


  0 0

  Sophia Kindamba akiwa na mwanae Junior Richard Rutta
  .....................................
  MTOTO Junior Richard Rutta ambaye jinsia yake haieleweki anatafuta msaada utakaomuwezesha kufanyiwa uchunguzi katika hospitali ya CCBRT, jijini Dar es Salaam.
  Mtoto huyo mwenye miaka miwili na miezi saba anaishi na mama yake mzazi, Sophia Kindamba, mtaa wa Mtwivilla, mjini Iringa.
  Akiomba msaada huo, mama yake alisema jitihada za madaktari wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuchunguza na hatimaye kujua mtoto huyo ana jinsi gani zinaelekea kukwama.
  “Kwa mara ya kwanza nilimpeleka katika hospitali hiyo mwanzoni mwa mwaka 2012, lakini hadi hii leo hakuna majibu yoyote; kwahiyo haieleweki kama ni msichana au ni mvulana” alisema huku machozi yakimtoka.
  Alisema mapema mwaka huu alikwenda Muhimbili lakini kwa majibu aliyopewa amepoteza imani ya tatizo la mwanae kushughulikiwa hospitalini hapo.
  Kindamba alisema “nimeambiwa kipimo kile kinatakiwa kupelekwa nje ya nchi baada ya uchunguzi wake hospitalini hapo kushindikana.”
  Alisema wakati akipewa majibu hayo ameshauriwa akajaribu pia kupata vipimo hivyo katika hospitali ya CCBRT.
  “Nimerudi Iringa kutafuta hela ili nikienda CCRBT nisipate shida ya gharama za uchunguzi na matibabu,” alisema.
  Kindamba alisema Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa leo amempa barua itakayomuwezesha kupita kwa watu, taasisi na mashirika mbalimbali kuomba mchango.
  “Naomba mnichangie; baba wa mtoto alinikimbi baada ya kubaini mtoto ana tatizo hili na sijui aliko; mimi mwenyewe nashindwa kufanya biashara yangu ya kutembeza mitumba  kwasababu hali ya mtoto huyu sio nzuri,” alisema.
  Alisema mtoto huyo huanguka na kupoteza fahamu kwasababu ana tatizo lingine la mtindio wa ubungo lililogundulika katika hospitali ya Muhimbili.
  Iwapo  umeguswa na upo tayari  kumsaidia  waweza  kupiga  namba0754026299 ili kuunganisha  nguvu zetu. 

  0 0

  Bondia Kalama Nyilawila katikati akitia saini ya kucheza pambano siku ya mei mosi atacheza na Thomasi Mashali au Japhert Kaseba inategemea na mshindi wa mechi hiyo ya March 29 itakayofanyika PTA Sabasaba kulia ni Alli Mwazoa na Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ustaadhi' 

  Promota wa ngumi nchini Ali Mwazoa akipeana mkono na Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ustaadhi baada ya kumsainisha bondia Kalama Nyilawila katikati anaetarajia kuzipiga Mei Mosi.

  Bondia Kalama Nyilawila ameingia mkataba wa makubaliano na promota Ali Mwazoa wa Tanga kwa ajili ya mpambano wa Mei Mosi mwaka huu ambapo  anasubiri mshindi wa mpambano kati ya Thomasi Mashali na Japhert Kaseba ambao watazichapa March 29 katika ukumbi wa PTA Sabasaba.
  Bondia Kalama Nyilawila alijitapa kwa kusema iwe Mashali awe Kaseba yoyote atakae kutana nae hatokuwa na masihara nae na kuwa  atampiga kipigo cha mbwa mwizi kwani nafasi hiyo alikuwa anaitafuta siku nyingi baada ya kupoteza uwezo wake katika masumbwi hivyo sasa wakae mbali na mimi kwani nakuja kwa nguvu mpya kabisa akisema atakuwa hatari kama 'Mbeya City' timu ambayo inatoka mkoani kwao kwa  kufanya maajabu kwa kuitawala ligi kuu ya Tanzania bara ndivyo na mimi nitakavyofanya
  Kalama katika harakati zake za kuhakikisha anarudi katika chati kama zamani mechi yake ya mwisho katika kuukaribisha mwaka 2014 alimsambaratisha bondia Ibrahimu Maokola bila huruma kwa kumpiga KO ya raundi ya pili mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Msasani Club jijini Dar.
  Nae promota wa mpambano huo Mwazoa amesema kila kitu kinaendelea vizuri ikiwemo mapambano ya utangulizi yenye mabondia bora wanaotamba kwa sasa ambao wapo kwenye kiwango cha ali ya juu kwa kuwa mwaka huu ni wa masumbwi nchini Tanzania nimeanza na nitaendelea kusapoti na kupromot mchezo wa ngumi popote nchini.
  Akizungumza kwa niaba ya chama kilichopewa dhamana ya kusimamia mchezo huo wa mei mosi Rais wa TPBO Yassini Abdallah 'Ustaadhi' amesema Watanzania wana bahati sana kwa kujitokeza promota mwenye uchu wa maendeleo kwa mabondia kwani mabondia wote wamesaini mkataba na kupewa posho ya kufanyia mazoezi isipokuwa bondia mmoja tu kati ya watakaocheza march 29 ni Kaseba au Mashali jibu ndio tunasubili siku hiyo nani zaidi na atakaepata nafasi ya kuchapana na Kalama

  0 0


  .Kutolewa vyeti maalum
  ..wadau kukata keki ya pamoja
  ..Slim kutumbuiza

  Na Andrew Chale
  KILELE cha Miaka 10  na ‘After Party’ ya onesho la mavazi la ‘Lady in Red Super Brand’ kinatarajia kufikia tamati usiku wa Jumamosi, Februari 22, ndani ya Ukumbi ulio na mgahawa wa kisasa wa hadhi jijini  Dar es Salaam, wa Nyumbani Lounge, huku kukitarajiwa kuwa na surprise mbali mbali kwa wadau watakaojitokeza.
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions,  Asia Idarous Khamsin, wandaaji wa Lady in red, kila mwaka hapa nchini, alisema, ‘after party’  hiyo ni maalum kwa ajili ya kutoa  shukrani na  vyeti maalum kwa wadau wanaoliunga  mkono jukwaa la Lady in red kwa kipindi chote hadi kufikia hapo ambapo pia watapata wasaha wa kukata keki  ya ukumbusho.
  “After party ya miaka 10 ya Lady in red, kwa mwaka huu itakuwa ya aina yake sambamba na surprise, hivyo nyote munakaribishwa na hakuna kiingilio na kwa watakaokuwa tayari kujiunga siku maalum pale  Nyumbani Lounge, wafike  katika duka la Fabak Fashion, lililopo  jirani na kituo cha Msasani, Kwa Mwalimu Nyerere au kwa kupiga simu namba 0713263363  ama0784263363” alisema Asia Idarous.
  Na kuongeza kuwa, pia tiketi maalum za bure zitatolewa mlangoni Nyumbani Lounge, kwa wadau watakaofika. Aidha, alisema msanii wa muziki wa kizazi kipya, Slim Guapo Sosa anayetamba na kibao cha ‘ LOVE YOU ’ na vingine vingi anatarajiwa kuwakonga nyoyo watakaojitokeza kwenye ‘after party’ hiyo.
   Party hiyo imedhaminiwa na  wadhamini mbali mbali wakiwemo Times fm, Michuzi media group, mo blog, Nyumbani Lounge, Darling air, G one Media na wengine wengi.

  0 0

   Mwakilishi wa Kudumu wa Sweden Jumuiya ya Ulaya Balozi Anders Ahnlid (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika. Balozi Ahnlid amekutana na Mabalozi hao leo Brussels.

  0 0

  Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani  la Tanzania,  Dk. Charles Msonde, akitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mtendaji wa  baraza hilo, Edward Haule. (PICHA NA KHAMIS MUSSA)
  Kupata matokeo ingia kwenye tovuti ya NECTA ya: 
  Kisha bofya sehemu ilioandikwa MATOKEO YA CSEE 2013 & MATOKEO YA QT 2013 Upande wa juu  kulia pembeni mwa tovuti
  0 0

  MHE. Murtaza Mangungu(MB)Kilwa Kaskazini akiwa na Bwana Phanuel Ligate (Mwakilishi wa Diaspora) Kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma November 2012

  Habari za Wakati huu ! Nimekuwa nikifuatilia mijadala na maoni mbalimbali kupitia mitandao na wengine walionitumia e-mail au kunipigia simu. 
  Kwa Kuwa mawasiliano yetu hayakuwa bayana nilidhani nitoe ufanunuzi kuhusu suala la uraia pacha (Dual citizenship ) . Awali ya yote Naomba radhi sana ikiwa maelezo ninayotoa nitamkwaza yeyote ila naomba iaminike si kusudio langu, pengine ni uelewa na nitakuwa tayari kukosolewa.
  Nawapongeza sana kwa jitihada kubwa mnazozifanya ili kufikia lengo , nawahakikishia Kuwa nitakua wa mwisho kukubaliana na suala hili kutoingizwa kwenye katiba mpya. 
  Binafsi naelewa kila neno mnalomaanisha na faida ya kuwapo kwa 'dual citizenship " kwa faida ya nchi yetu na ustawi maridhawa wa jamii zetu kwa ujumla.
  Ukisoma katiba yetu ya sasa na rasimu ya katiba mpya hakuna kipengele ambacho kinazungumza Aina ya uraia na pia hakuna tafsiri ya Raia ni ipi . Ibara ya ya katiba ya Mwaka 1977 kifungu 13(1)(3) ,17(1), 22(2), 28(1), 29(1)(2)(3) zimetamka Raia bila kutafsiri 'Raia" ni nani.
   Aidha kwenye vifungu au kwenye jedwali la tafsirihttp://www.katiba.go.tz/. Rasimu ya katiba ya 2013 Ibara ya 38 imetamka ya uraia bila ya kutoa kwa ufafanuzi 'Raia " ni nani au aina za uraia. 
  Ukisoma sheria ya uraia ya Mwaka 1995( The Tanzania Citizenship Act, 6 of 1995 )http://polis.parliament.go.tz/PAMS/docs/6-1995.pdf ndipo unapata tafsiri zote kuwa raia wa Tanzania ni nani na aina zipi za uraia kwa mujibu wa sheria. Kimsingi aina za uraia ama 'Dual Citizenship " si suala la kikatiba bali ni sheria ya Uraia . 
  Zipo jitihada kubwa za kiushawishi kutoka kwa Mh. Rais Dr. Jakaya Kikwete , Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe pamoja na viongozi wa Sekretarieti ya CCM (Mh. Madelu Mwigulu Mchemba na Ndugu Nape Nnauye) Kuwa lazima suala hili lipewe kipaumbele na msimamo wa chama 'CCM" ni Kuwa lazima pawepo na haki hii ya uraia pacha.

  Zipo namna mbili za kuwasilisha hili kwenye Bunge la katiba

  I. Kupeleka jedwali la mabadiliko ( schedule of amendment )
  II. Kupeleka mabadiliko ya kifungu kwenye Kamati ili iwasilishwe bungeni kwa mjadala.
  Binafsi nimeamua kutumia njia zote ili kuhakikisha hakuna mkwamo. Nawashukuru sana wale wote walioniagiza nihakikishe suala hili nalisimamia ipasavyo , Ndugu Iddy Sandaly, Alhaj Kalala , Ndugu Phanuel Ligate , Richard Mwandemani ,Khalfani Lyimo na wengineo wengi. Ninawahakikishia Kuwa nitalisimamia jambo hili kwa kadiri ambavyo Mungu ataniwezesha. 
  Siwezi kusahau hata kidogo maisha ya wema niliyoishi na wenzangu huko ughaibuni , pia hakuna namna itakayonifanya nisahau umuhimu wa jambo hili ikiwa binafsi ni miongoni mwa ' wahanga'' wa janga hili

  Ahsanteni
  Murtaza Mangungu(MB)
  Kilwa Kaskazini

  0 0

   Newdeal  Africa   in  collaboration  with  Kass  Grill  and  Didas  Entertainment  brings  to  you the  Mboni  show  who  are  filming  in  London  starting  from  the 24th /2/2014.

  Je  we ni  mjasiliamali au  unamafanikio  unayotaka  tuyajuwe  kama  wa Tanzania au  una  hadith  ambayo una  nadhani  ni  mfano  wa  kuigwa?

  Basi  wasiliana  nasii  kwenye  simu :

  Ayoub: 07960811614

  Kassongo: 07404062209

  Didas:07556171941

  EMAIL: swahilidiaries@yahoo.co.uk

  Thank you

  Ayoub  Mzee

  Chief Coordinator 

  New deal Africa

   


   Dada Mboni  inspecting  the clothes  designed  by  Tanzanians  that  are  displayed  at  the  Tanzani  High  commission in  London during  the  London  Fashion  week
   Dada Mboni pays a courtesy call on Tanzania's High Commissioner to the UK Ambassador Peter Kallaghe in London
  Dada Mboni  inspecting  the clothes  designed  by  Tanzanians  that  are  displayed  at  the  Tanzani  High  commission  London during  the  London  Fashion  week

older | 1 | .... | 363 | 364 | (Page 365) | 366 | 367 | .... | 3272 | newer