Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 362 | 363 | (Page 364) | 365 | 366 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Mwenyekiti wa Muda wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Pandu Ameir Kificho akiwashukuru wajumbe wa Bunge hilo baada ya kuchaguliwa.
   Muonekano wa Ukumbi wa Bunge Maalum la Katiba wakati wajumbe wakisubiri kupiga kura ya kumchagua Mwenyekiti wa muda
   Mchakato wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba
    Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe akifafanua jambo  kabla ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba.
    Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mchungaji Christopher Mtikila akitoa maoni yake baada ya uchagizi wa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba.
   Kamati ndogo ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba chini ya uongozi wa Mhe. Pandu Ameir Kificho (kushoto). Kamati hii itakayoongozwa na Mhe. Costa Mahalu na Mhe. Magdalena Rwebangula itafanya kazi ya kuichambua rasimu ya Kanuni zitakazoongoza Bunge Maalum la Katib
   Katibu wa Bunge la Muungano Dk Thomas Kashilillah (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Muda Mhe. Pandu Kifico wakati Kamati maalum ya Kanuni ilipokutana. Kamati hiyo inaundwa na wajumbe ishirini.Picha na Prosper Minja - Bunge Maalum la Katiba

  0 0

  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt Pindi Chana leo ametembelea Dawati la Jinsia na Watoto la Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Dodoma Mjini kwa lengo la kukagua utendaji kazi wa madawati haya yaliyoanzishwa kwa lengo kushughulikia kesi zote zinazohusiana na unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto nchini, kama njia moja wapo ya kuboresha utoaji wa huduma bora za ulinzi na usalama kwa watoto na watu wa jinsi zote.
   Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt Pindi Chana ( mwenye suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Dawati la jinsia na watoto la Polisi wilaya ya Dodoma, Kulia kwake ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma, Thadeus Malingumu na Kushoto kwake ni Mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa Dodoma, ASP Hamida Hiki.
  Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime akitoa Maelezo mafupi kwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt.Pindi Chana (Mb.) (mwenye suti nyeusi) Wakati alipotembelea Dawati la Jinsia na Watoto katika Mkoa wa Dodoma.
  Katika taarifa yake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma alieleza kuwa Mkoa wa Dodoma una jumla ya Madawati 9 yaliyopo katika Wilaya saba za mkoa huo. aliainisha moja ya changamoto za uendeshaji wa Madawati hayo kuwa ni baadhi ya wananchi kutokuwa tayari kutoa ushahidi wakati kesi hizo zinapofikishwa Mahakamani. Hivyo, Mkoa umejipanga kuendelea kuimarisha utoaji huduma kupitia madawati haya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Jinsia na Watoto.
  Wakati wa Ziara hiyo, Mheshimiwa Naibu Waziri Dkt. Pindi Chana alilisisitiza Wananchi kutumia madawati ya Polisi ya jinsia na watoto kutoa ripoti za matukio yeyote ya unyanyasaji  wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto yanayotokea katika jamii zetu. Aidha, alisisitiza kuwa huduma katika vituo hivi hupatikana pasipo malipo yeyote, na hutolewa kwa usiri stahiki.

  0 0


  Maoni ya baadhi ya wadau kuhusu lawama kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuwa posho ya Shilingi 300,000/= wanayolipwa kwa siku, haikidhi haja.

  Maria Sarungi-Tsehai, Mjumbe wa Bunge la Katiba kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook ameandika:
  Kimsingi tuliteuliwa kwenda kuwakilisha wananchi wa vikundi mbalimbali katika Bunge maalum la katiba kufanya kazi moja tu kwa siku 70 - kuandaa pendekezo la katiba kisha tutawanyike turudi makwetu. Hatujaenda huko kutajirika wala kupata ajira. Tunashukuru kwamba pamoja na hayo tumepatiwa hela ya kujikimu ya laki 3 kwa siku ambayo mtu akitumia vyema inatosha kabisa. Kuomba kuongezewa posho si haki kwa 80% ya watanzania wanaoishi kwa shilingi 1,000 kwa siku. Tutambue kuwa ni kweli gharama za maisha mjini ziko juu lakini tusitake kuleta ulafi. Mwenye mamlaka ya kuongeza posho za wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ni rais Jakaya Kikwete, tumtumie ujumbe kwamba asiongeze posho hizo - iliyopo inatosha!

  Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook ameandika:
  Naomba niseme wazi kabisa kwamba, sitapokea nyongeza yeyote ya posho hata ikiongezwa. Inaweza isisaidie kuzuia walafi wengine kupata posho kubwa lakini ni bora kuhesabika kwamba nimesema hapana. Ifikie wakati tuseme hapana kwa excesses zisizo na maana. Ninamwomba Rais asikubali kuongeza posho kama baadhi ya wajumbe wa BM wanavyotaka. Wanachopata kinawatosha sana. Nawasihi wananchi mumwombe na ikibidi kumshinikiza Rais kukataa.

  Mwenyekiti Msaidizi CUF, Julius Mtatiro kwenye ukurasa wake wa Facebook, Mtatiro kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook ameandika:
  NCHI HII ITAMALIZWA;
  Tunafahamu kuwa kuna njama zinapangwa ili wajumbe wa bunge la katiba ati waongezewe fedha zaidi.
  Hoja hii imetolewa leo hii na mmoja wa wajumbe huku ikionekana kuwa maarufu na inayoungwa mkono na baadhi ya wajumbe, hasa wabunge wa CCM.
  Binafsi na wenzangu wengi tumepanga kutumia kila uwezo kuzuia nia hiyo OVU, ifikie wakati tuambiane ukweli vinginevyo nchi hii watu watakufa masikini.
  Shilingi laki tatu tunazopewa kwa siku zinatosha kabisa, ambaye hazimtoshi aongeze za kwake, na ambaye anaona hawezi kuongeza zake aondoke Dodoma ili kupisha wanaoweza kutunga katiba kwa posho ya shs 300,000 waendelee.
  Laki tatu tunazopata zinatosha kila kitu na CHENJI inabaki, zinatosha kula, kulala, kumpa dereva na kuishi Dodoma.
  Lazima sisi tunaotunga katiba tufahamu kuwa maisha ya wananchi ni muhimu na kwamba wana mahitaji yasiyokwisha hata baada ya bunge hili.
  Baadhi yetu tulioko humu bungeni tutakataa jambo hili kwa maneno na vitendo. Wakipitisha kwa wingi wao tuta-boycott kuzipokea.
  Kenya pale mnakumbuka hoja ya wabunge kujiongezea mapesa ilipingwa vikali na wananchi waliandamana hadi nje ya ukumbi wa bunge. Hapa Tanzania hata zikiongezwa milioni kila siku hutaona mwananchi anachukua hatua kwa vitendo, kuoneshwa kutoridhishwa kwake.
  Tuna tatizo kubwa sana, sisi viongozi na wananchi wetu. Kuna mtu anasema, viongozi ni zao la jamii hiyohiyo.
  Tuungane pamoja kusimamia jambo hili, ninyi mlioko nje na sisi tulioko ndani.

  Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Wilbrod Slaa akizungumza na gazeti la MWANANCHI amesema posho wanayopewa wajumbe ya Sh 300,000 kwa siku inatosha kabisa:
  “kwa kuwa hata wafanyakazi wengine wa serikali wanapokea mshahara wa laki tatu mwisho wa mwezi.”
  Joshua Nassari, Mbunge wa Arumeru Mashariki katika tovuti ya JamiiForums ameandika:
  MSIMAMO WANGU, SAKATA LA POSHO BUNGENI.
  Nimeona nukuu kwenye gazeti la nipashe la leo. Kimsingi ike nukuu si ya kwangu ni nineshazungumza na Mhariri wa jipashe Bw. Kwayu.
  Sijui kama nukuu ile imewekwa kwa kukosea au kwa makusudi, wameahidi kurekebisha makosa lakini ni vyema nikaweka msimamo wangu hapa.
  Kwa hali halisi ya maisha ya kawaida ya Mtanzania wa shilingi laki 3 ni fedha nyingi. Na taasisi ya Bunge ndiyo inayopaswa kuwapigania hawa watanzania ili vipato vyao vipande lakini taasisi hii siku zote imekubali kuwa upande wa serikali badala ya kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi.
  Fedha hiyo bado ni nyingi mno kama kipato cha mtanzania kinabaki kuwa hapo kilipo.
  Kabla ya kupigania ongezeko ambalo linaweza wakati mwingine likawa na mantiki, ni vyema wabunge wakaifanya kwanza kazi yao ya kupigania maisha bora na maslahi bora kwa wananchi hiki hiyo mantiki yao kama ya kufanya mabadiliko ya posho ya shilingi elfu arobaini 40,000/= atakayolipwa mbunge iwapo ataugua akiwa Dodoma iweze kuonekana. Otherwise na sisi wabunge tutakuwa ni sehemu ya dhambi ya mateso na hali ngumu ya maisha ya watanzania ambao bado wanajifungulia sakafuni na hawana maji safi ya kunywa.
  Joshua Nassari (MB) na mjumbe wa bunge maalum la katiba.

  0 0

  Mwenyekiti wa muda wa Bunge Maalum la Katiba, Ameir Pandu Kificho, ametangaza majina ya watu sita watakaounda timu kwa ajili ya kuyafanya bora malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wajumbe wa Bugne hilo kuwa ya posho ya Shilingi 300,000/= kwa siku haitoshi kuwawezesha kuifanya kazi hiyo kwa makini.


  Akitangaza majina hayo kabla ya kuanza kwa semina kwa wajumbe hao, Kificho alirejea Sheria ya Mabadiliko ya Bunge la Katiba Sura ya 83 toleo la mwaka 2014 na kusema:
  “Kuhusu suala la kumudu kuishi vizuri na hii kazi nzito tuliyonayo bado halina majibu kwa sasa” 
  Kificho aliyataja majina ya wanaounda tume hiyo kuwa ni:-
  1. William Lukuvi
  2. Mohammed Aboud Mohammed
  3. Freeman Mbowe 
  4. Paul Kimiti 
  5. Asha Bakari Makame
  6. Jenista Mhagama.
  Alisema timu hiyo itakutana mara baada ya semina hiyo leo na ikiongozwa na Mwenyekiti huyo wa muda ili kuweza kukaa pamoja na kupanga ya kuweza kuiomba Serikali kuangalia jambo hilo na kuweza kupata majibu.

  Timu hiyo imeundwa baada ya baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kulalamikia posho hizo ndani na nje ya ukumbi wa Bunge jana.

  0 0

  Usharika wa St Anne’s Lutheran church unapenda kuwakaribisha wote kwenye ibada na sherehe ya kusimikwa (ordination) kuwa Mchungaji ndugu yetu Moses Shonga (pichani). 

  Sherehe itaanza saa nane mchana (2.00pm) na kufuatia na sherehe pamoja na vyakula na vinywaji baada ya ibada. Nyote mnakaribishwa.


  Anuani ni:

  St Anne’s Lutheran church
  St Mary at Hill church


  Lovat lane
  Eastcheap
  London
  EC3R 8EE


  Kituo cha karibu ni monument tube station.


  Mnakaribishwa.


  0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Lizzy Lloyd akizungumza wakati wa hafla hiyo.
   Balozi wa  Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mhe. Lv Youqing akitoa neno la shukrani kwa Benki ya Standard Chartered kwa kuandaa hafla hiyo.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza kwenye halfa ya kuadhimisha mwaka mpya wa China, iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered na kufanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro, Dar es Salaam. Wakati wa hafla hiyo Balozi Gamaha aliupongeza Ubalozi wa China katika kusaidia na kuchangia maendeleo ya Tanzania. Pia Balozi Gamaha aliipongeza Benki ya Standard Chartered kwa kushirikiana na Ubalozi wa China nchini katika kurahisisha  biashara kati ya Tanzania na China. 
    Wageni waalikwa walioshiriki hafla hiyo.
   Balozi Gamaha akizungumza na Waandishi wa Habari.
  Balozi Gamaha (kulia) akimsikiliza Bw. Nathaniel Kaaya,  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa hafla hiyo. Wengine wanaosikiliza  kutoka kushoto ni Bw. Iman Njalikai na Bw. Emmanuel Luangisa, Maafisa Mambo ya Nje.Picha na Reginald Kisaka

  0 0

  Wapendwa tunahitaji misaada yenu ya hali na mali.Hali halisi ndiyo kama mtakavyoisoma katika hii taarifa kwa ufafanuzi wowote waweza kuwasiliana nami kwa njia hii ama simu yangu +255 713682268
  Regards
  Novatus Makunga
  Mkuu wa Wilaya ya Hai, 
  Kilimanjaro

  0 0
 • 02/20/14--12:58: Article 11


 • 0 0


  cid:image001.png@01CF2C0E.5B7A9C00

  The 11th EAC Technical Working Group (TWG) meeting on HIV and AIDS, Tuberculosis (TB) and Sexually Transmitted Infections (STIs) commenced 17 February 2014 in Entebbe, Uganda. The 5 day meeting will among other issues, review progress of implementation of the EAC Regional HIV and AIDS programme and map a way forward for the programme for FY 2014/15.

  The meeting will also review and validate the 1st EAC HIV and AIDS Epidemic Report whose development was commissioned by the EAC Secretariat in collaboration with UNAIDS RST and also review and validate the study report on Comprehensive Analysis of the HIV and AIDS Legislation, Bills, Policies and Strategies in the East African Community.

  The TWG is expected to endorse a work plan for the HIV and AIDS project for the period 1stJuly 2014 to 30th June 2015; as well as receive updates from Lake Victoria Basin Commission on  a Sero-behavioural study in the Republic of Rwanda; review and input into concept note to Global Fund on HIV, TB and Malaria; revise Terms of Reference for conducting a midterm review of the EAC HIV and AIDS project and for conducting a size estimation study for MAPS in the EAC; and finally develop the EAC HIV and AIDS Multisectoral Strategic plan 2015 - 2020.

  The outputs of this meeting will feed into the 18th Ordinary Meeting of the Sectoral Committee on Health scheduled to be held in March 2014 and subsequently, the 9th Sectoral Council on Regional cooperation on Health to be held in April 2014.

  Participants of the meeting include members of the TWG on HIV and AIDS, TB and STIs, EAC Partner States, technical officers from National AIDS Councils/Commissions, National AIDS Control Programmes, East Africa National Networks of AIDS Services Organization (EANASSO) as well as representatives from LVBC, IUCEA, LVFO and development partners.

  0 0

    
   Makamu mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TASAF Taifa Abbas Kandoro akizungumza na Wazee wa Mtaa wa Mbulani katika kata ya Ruvuma Mjini Songea mara baada ya kukagua mradi wa Mashine ya kusaga na kukoboa nafasi wa wazee hao
   Wazee wa Kata ya Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF
   Wajumbe wa kamati Tendaji ya TASAF Kitaifa wakikagua mradi wa ufugaji wa Ngombe wa Vijana wa Mtaa wa Muungano Mjini Songea. Katika mradi huu TASAF imewawezesha vijana kupata shilingi milioni 5 za kununulia mitamba kwa ajili ya mradi huo. 
   Makamu Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TASAF Taifa Abbas Kandoro akisoma nembo ya TASAF katika jengo la vyumba viwili vya madarasa lililojengwa katika shule ya Sekondari Ndongosi Songea Vijijini. vyumba hivyo pia vimekewa meza na viti kwa ajili ya wanafunzi 70 pamoja na meza na makabati
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu anayeshughulikia TAMISEMI Zuberi Tamasaba akizungumza na wanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Ndongosi Songea Vijijini. Picha na Estom Sanga
  1.  

  0 0

   : Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko (kushoto) akikabidhi funguo za gari jipya kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Naftali Saioloyi (kulia).Gari hilo aina ya Landcruiser Station Wagon lenye namba DFPA 160 limetolewa kwa msaada wa shirika la Waltereed Program kusaidia utoaji wa huduma za UKIMWI .Tukio la makabidhiano imefanyika leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
  Gari hili ndilo lililokabidhiwa leo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea likiwa ni msaada kutoka shirika la Waltereed Program kuhudumia shughuli za UKIMWI katika Manispaa hiyo. Picha na Revocatus Kassimba
  Afisa Habari  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma.

  0 0

  Taasisi ya RAFIKIELIMU FOUNDATION kupitia mradi wa ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINI, inatangaza nafasi za MAFUNZO YA UALIMU WA UJASIRIAMALI . Wahitimu wa mafunzo haya watapata nafasi ya kufanya kazi kwa kujitolea kama waalimu wa ujasiriamali katika MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI & VIJIJINI. 
   IDADI YA NAFASI : 
   Nafasi 5 katika kila kata ya jiji la Dar Es salaam. 
   SIFA ZA MWOMBAJI : 
   1. Awe raia wa Tanzania mwenye elimu ya kuanzia kidato cha nne na kuendelea.
   2. Awe mkaazi wa Dar Es salaam.
  3. Awe na wito wa kufanya kazi ya ufundishaji.
  4. Awe tayari kufanya kazi kwa kujitolea kama mwalimu wa ujasiriamali katika kata yoyote ya jiji la Dar Es salaam. 
   MAFUNZO yatatolewa kwa mwezi mmoja kuanzia tarehe 02 MACHI 2014 katika Chuo Chetu kilichopo katika eneo la CHANGANYIKENI. 
   ADA YA MAFUNZO : MAFUNZO HAYA YANATOLEWA BURE.

  0 0

  Miaka minne iliyopita, tarehe kama ya leo, ni siku ambayo hatuwezi kuisahau kamwe. Ni siku ambayo ulituacha ndugu zako katika majonzi makubwa sana. Ingawa hatukuoni, hatuongei na wewe, hatubadilishani mawazo kama ilivyokuwa wakati wa uhai wako, hatujaacha kukukumbuka na kukuombea kwa Mwenye ezi Mungu kila siku.
  Unakumbukwa sana Mama yako, ndugu na jamaa zako wote. Mwenye ezi Mungu Ailaze roho yako Mahala Pema Peponi, Amina.

  Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un!  0 0


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0
 • 02/20/14--14:06: bei ya madafu leo


 • 0 0

  KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager jana imetoa mafunzo kwa wachoma nyama kutoka Baa mbali mbali za Mkoa wa Mwanza ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2014 yatakayo fanyika katika viwanja vya Furahisha.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Ziwa, Erick Mwayela, alisema lengo la kutoa mafunzo ni kutoa elimu kwa wachoma nyama ukizingatia uchomaji nyama ni moja sehemu ya kujiingizia kipato katika Bar.

  Kwa upande wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Laurence Salvi ambaye pia ni Jaji Mkuu wa mashindano hayo amesema huwezi kuandaa mashindano bila ya kutoa Elimu, hivyo TBL wamefikiria jambo la msingi sana lenye manufaa kwa waandaaji yaani wachoma nyama mpaka kwa watumiani yaani mlaji.

  Bwana Lawrence binfsi aliishukuru TBL kupitia bia ya Safari Lager kufikiria jambo zuri la kufadhili elimu kwa kwa wachoma nyama jambo ambalo si faida kwa wachoma nyama tu bali hata watumiaji sasa watakula nyama inayostahili.
  Jaji Mkuu wa Safari Lager Nyama Choma, Lawrence Salvi, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Semina ya Wachoma Nyama Mkoa wa Mwanza ikiwa ni maandalizi ya Mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2014.
  Baadhi ya wachoma Nyama Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Mkufunzina Jaji Mkuu wa Mashindano ya Safari Nyama Choma Mkoa wa Mwanza, Lawrence Salvi (hayupo pichani) ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Safari Nyama Choma.
  Mmoja ya washiriki wa Semina ya Wachoma nyama Mkoa wa Mwanza akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)

  0 0


older | 1 | .... | 362 | 363 | (Page 364) | 365 | 366 | .... | 3285 | newer