Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 361 | 362 | (Page 363) | 364 | 365 | .... | 3348 | newer

    0 0
  • 02/19/14--12:30: Article 16


  • 0 0     Wanainchi wakiangalia Lori baada ya kuungua
     Mabaki ya Lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii
     Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii

     Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa
     Hii ni njia ya mlima sekenke
    Lori la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani singida na kuua watu wanne hapohapo.
    Chanzo cha ajali hiyo ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo.
    Shuhuda wa ajali hiyo bwana Julius chacha alipoongea na mtandao wetu wa Dj sek blog amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.
    Akiendelea kuongea shuhuda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kwa moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.
    Watu wanne wamekuufa papo hapo kutokana na ajali hiyo. Polisi walikuwa bado hawajafika eneo la tukio mpaka tunaondoka eneo hilo.

    0 0
  • 02/19/14--12:35: bongo tambarareeeee....


  • 0 0
  • 02/19/14--12:36: uzee mwisho chalinze...  • 0 0    0 0

     Hapa Marikiti mjini Zanzibar ndipo kilipokuwepo kituo cha daladala mjini Unguja, Hivi sasa kimeshahamishwa na kuachwa kweupe na raha mustarehe kwa wakazi wa visiwani
     Raha mustarehe kwa wana Unguja
     Zogo sasa limehamia Michenzani karibu na afisi kuu za CCM za Kisiwandui ambako daladala zote husimama kwa sasa. Hakika kuna haja kubwa ya kuliangalia swala hili..Maana hapa pahala pafinyu mno!


    0 0


    Wsanii 12 wakiwemo viongozi toka Shirikisho la muziki, Shirikisho la Filamu, Shirikisho la Sanaa za ufundi, Mtandao wa Wanamuziki Tanzania walifunga safari na kuvamia Dododma na kuwa na mfululizo wa mikutano na wabunge mbalimbali ili kuwashawishi waunge mkono vipengele viwili ambavyo wasanii wanavitaka katika Katiba 
    1. Kundi la wasanii kutambuliwa katika Katiba kama vile walivyotambuliwa Wakulima, wafugaji, wavuvi na wafugaji walivyotajwa 
    2. Milliki Bunifu kwa kiingereza Intellectual Property ambamo ndani yake kuna Hakimiliki itajwe rasmi katika Katiba hili litawezesha sheria mwafaka zitungwe katika kuendeleza sanaa na kulinda kazi za sanaa na kazi za ubunifu. Kundi hili limepokelewa vizuri sana na wabunge wote lililokutana nao
    Mjumbe wa Bunge Maalumu la katiba Mhe Maria Sarungi akiwa na wawakilishi wa wasanii hao mjini Dodoma
    Kikao kimoja kati ya vingi vya wasanii na wajumbe wa Bunge maalumu la Katiba
    Kikao kikiendelea..

    0 0


    MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya usambazaji wa filamu za kiswahili Lufingo Exaud amesema kuwa wameingiza mtaani filamu yao mpya ijulikanayo kwa jina la xdent ambayo imeshilikisha wasanii mbalimbali wenye majina katika tasnia  hiyo

    utakutana na King Majuto, Muhogo Mchungu, Lufingo, Mzee Pembe na wasanii mbalimbali walio bobea katika sanaa hii ya filamu nchini

    filamu hiyo iliyorekodiwa kwa ubora wa hali ya juu na umakini mkubwa yenye mafundisho ndani yake itakuwa chachu kwa jamii kujirekerbisha katika maisha yao ya kila siku

    kwa sasa filamu hiyo inapatikana maduka yote yanayouza kanda za kiswahili nchini tanzania na mikoa yote kiujumla.

    hivyo wapenzi wa filamu waende kununua dvd halali ili waendelee kukuza kipato cha wasanii nchini filamu hiyo ambayo imewashilikisha wasanii wengi wakubwa imekuwa ikigombaniwa sokoni kutokana na ubora wake pamoja na wasanii wenyewe jinsi walivyo onesha uwezo mkubwa wa kuitendea haki filamu hiyo

    0 0

    Balozi Mero alipokutana na Dkt. Chan mjini Geneva, Uswisi

    Wakati zikiwa zimesalia siku zisizozidi elfu moja kufikia kikomo cha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia mwaka 2015 mwakilishi wa kudumu wa Tanzania  katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva balozi Modest Jonathan Mero amesema sekta ya afya inahitaji msukumo zaidi katika kutekeleza malengo hayo.
    Katika mahojiano maalum na idhaa hii Balozi Mero ambaye hivi karibuni alikutana na Mkuu wa shirika la afya duniani Magreth Chan, amesema anatarajia kukutana pia na mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mapambano dhidi ya ukimwi UNAIDS katika juhudi za kujadili mbinu za kutekeleza lengo hilo la sita. Na hapa anaanza kwa kufafanua lengo la mkutano wake na mkuu wa WHO
    (SAUTI MAHOJIANO)
    Kusikiliza bofya hapa

    0 0

    Tanzanian nationality law is the law which deals with citizenship and other forms of nationality. A Tanzanian citizen is anyone who is in possession of citizenship to the United Republic of Tanzania. Nationality law is mentioned in the Constitution of Tanzania. 
    The citizenship law was first implemented after independence in 1961, and amended in 1964 when Tanganyika and Zanzibar united to form Tanzania. 
    For more CLICK HERE

    0 0    0 0

    Misaada ya hali na mali imeanza kumiminika kwa ajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya. 
     Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ametuma maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto, ambavyo vimewasili salama katika ofisi za Michuzi Media Group (MMG) inayoendesha Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure na Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza. 
     Hivi sasa MMG ikishirikiana na waratibu wa misaada kwa mama huyo, Mbeya Yetu Blog, wanaandaa utaratibu wa kumfikishia Mama Aida mizigo yake haraka iwezekanavyo. 
     Kwa niaba ya mzazi wa mapacha hao, Michuzi Blog na Mbeya Blog zinatoa shukrani za dhati kwa msamaria mwema Gladness Sariah kwa wema na upendo aliouelekeza kwa mzazi huyo. Huo ni mfano wa kuigwa, na tunatarajia misaada zaidi itatolewa na wasamaria wema ambao tunajua mko wengi kila kona ya dunia. 
     Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com 
    nasi tutafikisha ubani wako. 
    Serengeti Freight wametoa ofa ya 
    kusafirisha bure misaada ya aina hii 
    ASANTENI SANA
    Michuzi Blog/Mbeya Yetu Blog

    Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.

    Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.     Misaada kwaajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya mara baada ya kufikishwa katika makao makuu ya Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure toka Uingereza na Wazee wa Kazi Serengeti Freight.


    0 0


    0 0

    Kwa muda wa wiki sasa Watanzania tunaoishi ughaibuni tumekuwa tukiendesha kampeni yakuelimisha umma kuhusu maombi yetu ya kupatiwa haki ya kikatiba ya kuwa na uraia pacha. “Mimi ni Mtanzania” ni ukweli uliopo kwa mtu yeyote mwenye asili ya Tanzania bila ya kujali anaishi Tanzania au ughaibuni. 
    Leo tunapenda kutoa wito kwa serikali, kwa Bunge Maalumu la Katiba na kwa vyama vyote vya kisiasa katika jitihada zetu za kuwasilisha maombi yetu ya uraia pacha kwenye Bunge Maalumu la Katiba ili yafanyiwe kazi na ni matumaini yetu baada ya Bunge Maalumu la Katiba kumalizika kila Mtanzania atapewa haki ya kupata uraia wa nchi nyingine kwa kuzingatia sheria za nchi. Tukianza na serikali, kwanza kabisa kama Watanzania wanaoishi kwenye diaspora, tunatambua jitihada za dhati za Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Serikali ya Awamu ya Nne kutambua mchango wa wana-diaspora katika maendeleo ya nchi. 
    Hii imedhiirishwa kwa kuanzishwa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kuteuliwa Mkurugenzi kuiongoza ili kurahisisha mahusiano na utengenezaji wa Sera na mikakati inayowahusu wana-Diaspora katika kuwashirikisha kusaidiana na Watanzania waishio Tanzania kuleta maendeleo ya nchi yao. 
    Pili, tunatambua mchango wa Serikali katika kuhamasisha uundwaji wa Jumuiya za Watanzania nje ya nchi kama njia bora ya kuwaunganisha Watanzania kujadili mambo muhimu kwa nchi yao na maslahi yao. Jumuiya hizi zinaundwa na Watanzania na Watu wenye asili ya Tanzania na marafiki wa Tanzania. 
    Watanzania wanaounda jumuiya hizi wamekuwa ni mabalozi wazuri katika kuitangaza Tanzania nje ya nchi na vile vile wana mchango mkubwa wa kuendeleza utamaduni wa Mtanzania nchi za nje, lakini vile vile kudumisha huduma za biashara na kubadilishana utaalamu kati ya Tanzania na nchi nyingine kupitia programu mbalimbali kama za mawasiliano ya kijamii, michezo na mambo mengine mengi. 
    Kihistoria Watanzania wengi wanaoishi nje ya nchi wamekuwa wakishiriki katika mambo ya kimaendeleo na wamekuwa na sifa nzuri katika mahusiano yao na nchi nyingine na katika kudumisha lugha ya Kiswahili, utalii, mahusiano ya kibiashara na viwanda kati ya Tanzania na nchi nyingine na bila kusahau elimu katika fani mbalimbali. 
    Tatu, tunatambua mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika kuwasilisha maoni ya wana-diaspora kwa Tume ya Katiba ili yafikiriwe na kuwekwa ndani ya Katiba Mpya. 
    Na ni matumaini yetu kuwa wizara hii na taasisi nyingine husika zitashirikiana nasi katika kuhakikisha kuwa suala la uraia pacha linawekwa kwenye Katiba mpya ya Tanzania. Tunazidi kuiomba serikali ma wizara zake kuhakikisha kuwa changamoto zetu na suluhisho zake zinaingizwa kwenye katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likiwemo vile vile suala la uraia pacha. Nne, mchango wetu kama Watanzania wanaoishi kwenye diaspora ni mkubwa sana katika kuendeleza uchumi wa Tanzania. 
    Kwa mfano, mwaka wa 2012 Watanzania waishio nje ya nchi walituma pesa kiasi cha dola milioni 250 kwenda Tanzania. Idadi ya Watanzania waishio nje ya nchi wanakisiwa kuwa asilimia 5 ya Watanzania wote, yaani karibia watu milioni 2.25 (Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje). Na kiasi cha fedha zinazotumwa Tanzania kutoka kwenye diaspora kinazidi kuongezeka siku hadi siku. Hivyo sisi wanadiaspora bado tunachangia sana katika shughuli za maendeleo ya nchi yetu. Tukija kwenye vyama vya siasa, sisi Watanzania tunaoishi ughaibuni tunaviomba vyama vya siasa vyote vya Tanzania kwa pamoja bila kujali itikadi zao kulipigia kura suala la uraia pacha ili liingizwe kwenye katiba mpya. 
    Sisi kama Watanzania wa ughaibuni lengo letu ni kujenga umoja baina ya Watanzania na kuitangaza nchi yetu nchi za nje na hasa tunapoishi ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano mazuri kati yetu na nchi zilizotukaribisha uhusiano ambao unavuka mipaka yetu na kuifanya Tanzania kuwa na mahusiano mazuri na nchi nyingine. 
    Tunaomba vyama vyote vya siasa vikubali maombi yetu ya kuwa na uraia pacha, kupewa haki ya kupiga kura “voting right” na kepewa haki ya kurudi Tanzania “right of return” ikiwa ni pamoja na sisi tupate wawakilishi wetu kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano na Serikalini ili tuweze kwakilisha changamoto zetu na tuweze kuijenga Tanzania pamoja na watanzania wengine. Tukija kwenye Bunge Maalumu la Katiba, kwanza kabisa tunawapongeza wawakilishi wote wa Bunge Maalumu la Katiba kwa kuteuliwa kwao na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kushiriki katika Bunge hilo muhimu litakalotuletea katiba mpya.
    Pili tunapenda kumpongeza aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Bunge hilo. Tunawaomba wawakilishi wote wa Bunge Maalumu la Katiba kumpa ushirikiano Mwakilishi wetu kutoka Diaspora Mheshimiwa Kadari Sanga ili pale atakapoziwakilisha changamoto zetu zipatiwe suluhisho zuri na la kudumu. 
    Tunawaomba wabunge wote walipigie kura ya ndio suala la uraia pacha ili liingizwe kwenye katiba maana lugha ya sasa iliyotumika kwenye rasimu ya katiba bado haisema wazi kama uraia pacha unaruhusiwa. Tunaomba katiba iseme wazi ni ruksa kwa Mtanzania kupewa uraia pacha. Mwisho tunawashukuru Watanzania wote kwa kuielewa hoja hii. 
    Tunawaomba wasaini petition yetu tuliyoiweka kwenye blogi mbalimbali ili watusaidie katika kutimiza lengo letu la kupeleka sahihi za Watanzania kwa wahusika wa suala hili. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika. 
    Imeandaliwa na Deogratius Mhella, 
    Katibu wa vikao vya Jumuiya za Watanzania Marekani na DICOTA, 
    katika jitihada za Watanzania kuelimisha umma juu ya maombi yao ya uraia pacha.

    0 0

    Ujumbe wa Ankal kwa wadau ni kwamba, pamoja na kazi nyingi ikiwemo kubeba boxi lakini hakuna raha kama ya kutumia muda wako wa ziada (kila upatapo nafasi) kuutumia ukiwa na familia yako. Familia ndiyo muhimili muhimu katika maisha yako. 
    Ni raha ilioje uonapo mng'ao wa furaha katika jicho la mwanao unapomtoa out kila upatapo nafasi. Kwa umri wake tendo hilo atalikumbuka milele. Na yeye atawafunza wanae na wajukuu faida ya kuwa pamoja kifamilia. 
    Fikiria; hizo pesa na muda unavyotupa pembeni (ambavyo ni mara mia ya gharama ya kuitoa familia out) zina faida gani katika maisha yako. Ankal anasema; JALI FAMILIA YAKO hata kama ni kwa mara moja kwa mwezi. Utafurahi nao watafurahi na Mola atakuafu.     0 0
  • 02/21/14--12:30: wosia wa baba wa taifa
  • Hotuba ya Mwalimu Nyerere hoteli ya 
    Kilimanjaro jijini Dar es salaam June 14, 1994

    0 0

    Kama ulikuwa haufahamu, habari kuu katika ulimwengu wa Teknohama kwa siku ya leo ni Facebook kuinunua Whatsapp kwa bei ya dola bilioni 19.  
    Nunuzi hilo ni la programu pekee na siyo kampuni ingawa wafanyakazi wa whatsapp watajiunga na timu ya Facebook moja kwa moja, mission za whatsapp zitaendelea kubaki kama zilivyo, alieleza Jan Koum ambaye ni muanzilishi wa whatsapp.

    Kwa wasio fahamu, whatsapp ni moja ya programu ya simu za mkononi inayokuwezesha kutuma ujumbe wa simu kupitia kwenye intaneti badala ya ujumbe mfupi (sms). Kwa kutumia whatsapp, inamaana utaepuka gharama za sms huku ikiwa imesheheni matumizi mengine mengi zaidi kama kutuma picha, sauti uliyojirekodi nk.

    Hadi sasa, whatsapp ina watumiaji hai milioni 450 kila mwezi kutoka nchi nyingi duniani, huku kukiwa na watumiaji wapya zaidi ya milioni moja kila siku. Hivyo, ni dhahiri kuwa whatsapp ni programu pendwa na yenye kutumika.

    Whatsapp inaweza kutumika kama njia rahisi zaidi ya mawasiliano kwa watu binafsi na hata makampuni, kwa mfano, sisi Dudumizi tunatumia whatsapp kama njia ya kuwasiliana na mamia ya wateja wetu walio nje ya nchi na kutuwezesha kupunguza gharama za mwasiliano.

    Ingawa makampuni mengi ikiwemo Facebook yamekuwa yakitegemea huduma za matangazo kama njia ya kuingeza kipato, whatsapp ni programu ambayo, huwezi kuonana na matanagazo na wamejizatiti kuwa ni wataendelea hivyohivyo bila ya matangazo. Na pia whatsapp ni bure kwa kwa mwaka wa kwanza na huchaji $1 kwa mwaka kama gharama ya kujiunga kwa miaka inayofuata. Hivyo kabla ya Facbook kuinunua whatsapp ni dhahiri walishajipanga kwenye hili, kwani, hili ndilo linaloifanya whatsapp iwe tofauti.

    Akielezea sababu ya kuinunua whatsapp, mwanzilishi wa Facebook alisema, wameinunua whatsapp kwa sababu whatsapp ina thamani. Na wao wakiwa kama wafanya biashara lengo lao kubwa ni kuongeza thamani ya biashara yao illi waendelee kuwa salama. 
    Hivyo, wanaamini nunuzi la whatsapp litakuwa na tija na manufaa kwa wote, wanunuzi na walionunuliwa. Hivyo ubora na misingi ya huduma ya whatsapp utaendelea kuwa juu kama ilivyo sasa.

    0 0

    Godfrey Mgimwa

    Lile pingamizi lililokuwa limewekwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) dhidi ya mgombea ubunge katika jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) limetupwa.

    Katika pingamizi lao lilowasilishwa juzi, Chadema walikuwa wanapinga Godfrey Mgimwa kugombea ubunge kupitia CCM kama alivyoomba kwa kuwa sio raia wa Tanzania.

    Tetesi za tatizo la uraia wa Godfrey Mgimwa zilisambaa mjini Iringa baada ya Chadema kuweka pingamizi hilo.

    Katika Pingamizi lao hilo, Chadema ambao katika uchaguzi huo mdogo wamemsimamisha Grace Tendega kupeperusha bendera yao walisema Godfrey Mgimwa anakosa sifa ya kuwamgombea wa chama chochote cha siasa nchini kwa kuwa aliukana uraia wake.

    Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Iringa, Pudenciana Kisika hakuweza kupatikana jana, lakini Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga alithibitisha pingamizi hilo kutupiliwa mbali.

    "Ulikuwa ni uzushi dhidi ya mgombea wetu, hatukuwa na hofu yoyote kwa kuwa mgombea wetu anakidhi sifa zote," alisema.

    Alisema Chadema wameshindwa kuwasilisha ushahidi unaonesha Godfrey Mgimwa aliukana uraia wa Tanzania alipokuwa masomoni nchini Uingereza. 

    Baada ya kushindwa kuwasilishwa ushahidi wowote, madai hayo yamedhihirika kwamba ni ya uongo na msimamizi wa uchaguzi ametupilia mbali pingamizi hilo hivyo Mgimwa ni mgombea halali wa CCM katika uchaguzi huo.


    Katibu wa Chadema Iringa Vijijini Felix Nyondo hakupatikana kuzungumzia pingamizi lao kutupwa na hata alipokuwa akitafutwa kwa simu yake ya mkononi ilikuwa haipokelewi.

    Mtenga alisema kesho atakutana na wanahabari ili kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu maandalizi ya kampeni za uchaguzi huo.

    Kampeni za uchaguzi huo zilianza februari 19 na zinatarajia kukoma Machi 15 ambayo ni siku moja kabla ya Uchaguzi huo wa Machi 16.

    0 0

    Mkurugenzi wa ANSAF, Audax Rukonge alipokuwa akieleza maudhui ya siku ya Mwaka wa Kilimo wa Afrika

    Ukaguzi wa shamba la mfano katika kijiji cha Kaning'ombe ulifanywa
    Wasanii, Mrisho Mpoto na Profesa J ambao ni mabalozi wa kampeni ya "Kilimo Kinalipa, Jikite" walikuwepo

    Naye Mwakilishi wa shirika la Afrika One kutoka Afrika Kusini alikuwepo kuelezea kilimo kinavyoweza kuwatoa watanzania

    Msanii Dokii naye alisema mambo na jinsi kilimo kinavyomtoa

    Wazee wa kampeni, Mrisho Mpoto, Profesa J na Masoud Kipanya walisema maneno yao kwa kupokezana wakieleza jinsi kilimo kinavyoweza kuwa mkombozi kama dhamira itakuwepo

     
    Mkulima wa mfano, Bw. Eusebio Mbagile, alizungumzia changamoto wanazopata wakulima wadogo katika shughuli hiyo ya kilimo

    Baada ya kueleza changamoto zinazowakabili, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma aliishia kwa kupata ka KUKU ka zawadi ili akale yeye na familia yake

    JUKWAA la Wadau wa Kilimo (ANSAF) limekumbushia ahadi  ya kutenga asilimia 10 ya bajeti ya nchi kwa ajili ya Kilimo, iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2012.

    Mkurugenzi wa ANSAF, Audax Rukonge aliyasema hayo leo wakati Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal aliyewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma akizindua Mwaka wa Kilimo wa Afrika.

    Uzinduzi wa mwaka huo unaokwenda na kampeni iliyopewa jina la ‘Kilimo Kinalipa, Jikite’ ilifanyika katika kijiji cha Kaning;ombe, wilayani Iringa mkoani Iringa.

    Mbali na ANSAF, wengine wanaoratibu kampeni hiyo ni mashirika ya Cloud Media na Afrika ONE inayowataka viongozi wa Afrika kutimiza Azimio la Maputo linalohimiza uwekezaji katika kilimo

    Mabalozi wa kampeni hiyo, wasanii maarufu, Mrisho Mpoto, Profesa J na Masoud Kipanya walizungumzia namna kilimo kinavyoweza kuwakwamua vijana na lindi la umasikini huku msanii wa filamu nchini Dokii akieleza mafanikio yake ya kilimo katika shamba lake lililoko wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

    Mkurugenzi wa ANSAF, alisema kwa kupitia azimio hilo la Maputo wakuu wa nchi walikubalina watenge bajeti ya asilimia 10 ya bajeti zao kwa ajili ya kilimo.

    Alisema kiwango hicho kilitarajiwa kutosha kuchangia kuongeza uzalishaji na tija, kukuza sekta ya kilimo kwa asilimia 6 kwa mwaka na kuondoa tatizo la njaa na umasikini.

    “Leo hii ni miaka 10 tangu makubaliano ya Maputo. Ni nchi nane tu za Afrika zimetimiza ahadi hiyo; Tanzania haimo katika nchi hizo,” alisema bila kuzitaja.

    Alisema tafiti zinathibitisha kuwa kilimo huchangia mara 11 zaidi katika kuondoa umasikini ikilinganishwa na uwekezaji mwingine.

    Alisema kama taifa limedhamiria kuondoa umasikini ni lazima kukipatia kilimo mtazamo mpya wa kiuchumi, usiokuwa na chembe za kisiasa huku uwekezaji ukifanywa kwenye maeneo ya kimkakati.

    Katika hotuba yake kwa wadau wa Kilimo, Makamu wa Rais alisema kilimo ni lazima kiendelezwe kwa usalama wa chakula na maisha.

    Alisema program ya kuendeleza kilimo ilizinduliwa mwaka 2005/2006 ikilenga kilimo kikue kwa asilimia sita kutoka asilimia nne ya hivisasa.

    Alisema kwa kushirikisha sekta binafsi program hiyo inalenga pia kuwatoa wakulima katika kilimo cha kujikimu ili kiwe cha kibiashara.

    “Tunatakiwa kuwa na muda maalumu wa kushughulikia ahadi ya Maputo ya kutenga asilimia 10 ya bajeti ya serikali, kufanya mabiliko ya sera na kuongeza uwajibikaji katika sekta hiyo,” alisema.

    Mmoja wa wakulima wa mfano katika kijiji hicho, Eusebio Mbangile alisema shughuli ya kilimo ni kero kubwa kwa wakulima wadogo kutokana na ukubwa wa bei za pembejeo, upatikanaji wake na masoko.

    Alisema “ninazo heka 45; ninazolima ni 19, wakati wa masika 15 na wakati wa kiangazi heka nne, kwa wastani natumia karibu Sh Milioni 4 kwa shughuli nzima ya kilimo kila mwaka;” alisema huku akionesha mashamba yake hayo ya mahindi.

    Alisema kwa wastani hupata gunia 25 za mahindi kwa kila heka ambayo hata hivyo huwa hauzi kwa vipimo vinavyokubalika kisheria.


    Alisema walanguzi wamekuwa wakinunua gunia la mahindi lenye ujazo wa kilo 150 hadi 160 kwa Sh 38,000 tu hali inayowapa hasara kubwa na kuwafanya waendelee kuwa masikini.

    0 0

     Waziri Mkuu  ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Maalum wa Bunge la Katiba Mizengo Peter Pinda (kushoto) akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzake Said Mtanda (kulia) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko.
     Waziri Mkuu  ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Maalum wa Bunge la Katiba Mizengo Peter Pinda (kushoto) akibadilishana mawazo na mjumbe Said Mtanda na wenzake  jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko.
      Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum  la Katiba  Joshua Nasari(kushoto) akibadilishana mawazo na Mjumbe mwenzie ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Mhagama(kulia) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko.
     Mjumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum  la Katiba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha Mwingulu Nchemba (kushoto) akibadilishana mawazo na wajumbe mwenzie  Zitto Kabwe(kulia) na Albert  jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko.
    Wajumbe wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba wakibadilishana mawazo na jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko. Picha na MAELEZO-DODOMA

older | 1 | .... | 361 | 362 | (Page 363) | 364 | 365 | .... | 3348 | newer