Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 357 | 358 | (Page 359) | 360 | 361 | .... | 3353 | newer

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akimuonesha Waziri wa Maji, Profesa Maghembe samaki waliokufa katika bwawa linalosadikiwa kutiwa sumu na mtu asiyejulikana.

   Mto Wame ambao ndiyo chanzo kikuu cha maji cha mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Chalinze jinsi ulivyochafuka.
  Mkurugenzi wa majisafi na usafi wa mazingira Chalinze Christa Mchomba akimuonesha Waziri wa Maji Profesa Jumanne maghembe na aliyoongozana nao jinsi mto Wame ulivyochafuka, aliyeinama ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza.
  Waziri wa maji Profesa Jumanne Maghembe, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kibindu wilayani Bagamoyo. Waziri aliwahakikishia kisima cha maji katika kijiji chao.


  Atoa maagizo kwa kwakurugenzi na wahandisi wa maji
          *Ajionea Maji yalivyochafuko mto Wame


  Na Athumani Shariff

  Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, amefanya ziara Mkoani Pwani ili kukagua na kutoa maelekezo katika miradi ya maji ya Mkoani humo.
  Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, ilikagua miradi mbalimbali ya maji katika maeneo ya Chalinze, Visiga, Vigwaza, Kibinda na mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Chalinze.

  Profesa Maghembe pia alitembelea bwawa la maji la Pigo shule ilikagua na kujionea hali ya bwawa hilo lililotiwa sumu na watu wasiojulikana.

  Bwawa la Pigo linasadiwa kuwa limetiwa sumu na watu wasiojulikana kutoka na maji yake kuwa na mapovu huku samaki na vyura kufa na kuonekana wakielea katika bwawa hilo.

  Akiueleza msafara huo, Waziri Maghembe alisema, tayari ameshawaagiza wataalamu wa maabara ya maji kutoka Wizara ya Maji ili wakayakague maji hayo, lakini wananchi wasiyatumie maji haya.

  Profesa Maghembe pia alimuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira chalinze Christa Mchomba, ahakikishe watu waishio maeneo hayo hawapati mgao wa maji ili wasiende kuchota maji hayo yenye sumu.

  “Mkurugenzi hakikisha wananchi hawa hawapati mgao wa maji ili wasijekuchota maji haya” alisisitiza Waziri Maghembe.

  Pamoja na miradi hiyo, Waziri pia alitembelea na kujionea jinsi mto Wame ulivyochafuka. Mto Wame ambao ndiyo chanzo kikuu cha maji cha Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Chalinze umechafuka kutoka na shughuli za kibinaadamu zinazofanywa kwenye vyanzo vyake vya Mkoani Morogoro.

  Akieleza katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Chalinze, Christa Mchomba alisema “Mto Wame umechafuka sana hali ambayo haijawahi kutokea tangu kuanza kwa mamlaka hii ya maji ya Chalinze. Maji yamekuwa tope kutokana na shughuli za kibinaadamu zinazofanywa hasa katika vyanzo vya Morogoro.

  Kutokana na uchafuzi huo uliopelekea maji kuwa tope uzalishaji wa maji umepungua hadi kufikia asilimia 8 kitu ambacho kimepelekea mgao wa maji katika maeneo mengi yaliyokuwa yakipata huduma ya maji kupitia mamlaka hiyo.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, alimshukuru Waziri wa Maji kwa kutenga muda wake ili kutembelea miradi ya maji katika wilaya ya Bagamoyo.

  “Kwa niaba ya wananchi wa Bagamoyo, nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kwakutenga muda wako kuja kututembelea na kujionea miradi ya maji katika Halmashauri yetu.   0 0  0 0

  A validation workshop on modalities for digitization of EAC information resources is set to be convened from 13th-14th February 2014 in Nairobi; Kenya. The workshop aims to undertake a study on the digitization of information as a resource for the Community.


  The study is a continuity of Library initiatives to streamline the EAC information resources in a structured manner in all its Organs and Institutions. This initiative is in line with Article 71 of the Treaty which states the responsibility of the Secretariat to promote and disseminate information on the Community to the stakeholders, the general public and the international Community as an effort to preserve EAC information and harmonize it for effective dissemination.

  Currently, information is scattered around EAC’s Organs and Institutions such as the legal, information and public relations, libraries, registries, archives and in offices as opposed to a well-organized data storage system. It is also not effectively shared internally neither is it effectively disseminated to the public.

  Drawing from the integration process, a lot of information has continued to be generated that is of great educational, economic as well as historic value. Such information material include EAC reports; published or non-published, maps, books, recordings, films, prints, photographs, architectural drawings, databases and other types of primary sources of data, depicting various integration processes from negotiations to protocols to information from EALA and EACJ including the hansards, court cases and judgments.

  In a bid to strengthen and streamline such information resources, a number of initiatives have been undertaken such as the Information Communications Project funded by DFID and the establishment of the library and documentation centre. 
  Among the expected outputs of the study is an inception report, a draft on modalities for digitizing EAC information resources, a report of the stakeholders’ validation workshop and a final draft report planned for submission. 
  EAC Organs and Institutions namely the Secretariat, EALA and EACJ  LVBC, LVFO, IUCEA and CASSOA; will be meeting tomorrow to validate the draft report on modalities for digitizing EAC information resources and consequently outline a report

  0 0

  Na Andrew Chale MKALI wa R&B na Afro Pop, ambaye aliwahi pia kushiriki shindando la BSS, Nemo (pichani), anayetamba na wimbo wa ‘My Number One’ aliyomshirikisha Ommy Dimpoz anatarajia kupafomu kwenye shoo ya miaka 10 ya onyesho la mavazi lijulikanalo kama ‘Lady in red Super brand, 10th Anniversary’ linalotarajiwa kufanyika Februari 14, kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
   Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions inayoandaa onyesho hilo , Asia Idarous Khamsin, alisema tayari msanii huyo ameingizwa kwenye listi ya wasanii watakaotoa burudani kali nay a aina yake siku hiyo ya Februari 14. Asia Idarous alisema msanii Nemo anatarajia kuimba vibao vyake mbali mbali vikiwemo vya “Vumilia”, “Wife” na wimbo ulio kwenye chati ndani na nje ya Tanzania unaotamba kwa sasa wa “My Number 0ne”. 
  “Hii ni ‘Surprise’ kwa wapendanao katika onyesho letu la Miaka 10 ya jukwaa la Lady in red’ hivyo mbali na kushuhudia mavazi ya ubunifu yaliyobuniwa na wabunifu magwiji na wale wanaochipukia kwenye fani hii, pia watakonga nyoyo zao kwa kupata burudani ya aina yake kutoka kwa Msanii Nemo” alisema Asia Idarous. 
  Aidha, katika onyesho hilo, mbali na Nemo, pia kunatarajia kuwa na burudani kutoka mwanamuziki wa nyimbo za asili, Wanne Star na bendi ya Babloom Trio. Kwa upande wa wabunifu magwiji watakaopamba steji hiyo siku hiyo ni pamoja na Mustapha Hassanalli , Ally Rhemtulla, Lucky Creation, Martin Kadinda, Ghymkana Hilali, Paka wear, Gabriel Molel, Fransiska Frankoo Shirima, Salim Ally, Ameed Abdul, Mgese Makory, Kiki Collection, Rose fashion, Diana Magesa, Rio Paul na wengine. 
   Kwa upande wa wabunifu chipukizi: Faustin Simon, Water Edward, Brian Hango, Benedict Mnzava,Crissiwelly Uissoson,Willex Willibard, Jackson, Gumbala, Jabir Jumanne, Alabama King, Agusta Masaki, Nelson Tomas, Bebi Juliet Mtandu, Ummi fashion/Ummi Investiment Comapany, Asmahan Eva, Hassan Nasor, Juniper Mafuru, Ante Ngongi, Adam Hassan, Jaquline, Kijangwa na Waiz Shelukindo. 
  Katika onyesho hilo ambalo litafanyika siku hiyo ya Februari 14, ambayo pia itakuwa ni siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ , kiingilio kitakuwa sh 30,000 kwa viti vya kawaida huku viti maalum ikiwa sh 50,000. 
  Tayari tiketi za onyesho hilo zimeanza kuuzwa ikiwemo vituo vya duka la Fabak fashion, lililopo mikocheni mkabala na kituo cha Mwalimu Nyerere huku kwenye hoteli ya Serena, zikipatikana mapokezi. Kwa mwaka huu onyesho hilo limedhaminiwa na adhamini mbalimbali wakiwemowadhamini wakuu ambao ni kinywaji cha Zanzi pamoja na kampuni ya nywele ya Darling. Wengine ni CXC, Times fm, Clouds media, Vijimambo blog, michuzi media group, channel ten, Elite Computer, Eventlites, One touch-solution, Raysa Style, Paka Wear, Dj Bula, Magic fm, DTV, Jambo Leo, I View media, Vayle Spring, Voice of American na wengine wengi.

  0 0


  0 0

   Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ilala, Jesca Njau (kushoto) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi wodi ya watoto wachanga Katika Hospitali ya Rufaa ya Amana Ilala iliyokarabatiwa kwa msaada kampuni hiyo, Dar es Salaam jana.  Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Daktari Bingwa wa Watoto wa Hospitali hiyo, Dk. Mtagi Kibatala, Mhandisi wa TBL, John Malisa na Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Meshack Shimwela. TBL ilitumia sh. mil. 68 kukarabati wodi hiyo na miundombinu yake. 
   Jesca Njau akipongezwa na Daktari Bingwa wa Watoto wa Hospitali hiyo, Dk. Mtagi Kibatala,
   Dk. Kibatala akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo ambao alidai umepunguza kwa asilimia kubwa kupunguza adha kwa wazazi waliozaa watoto njiti. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la Tafakuri na Maridhiano kuelekea Katiba mpya, lililofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia. Picha na OMR

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, baada ya kufunguliwa rasmi rasmi Kongamano la Tafakuri na Maridhiano kuelekea Katiba mpya, lililofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia. Picha na OMR

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiagana na wajumbe walioshiriki Kongamano hilo baada ya ufunguzi uliofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia. Picha na OMR


  Picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo. Picha na OMR

  0 0
 • 02/12/14--09:57: TASAF YANUFAISHA WANA-MTWARA
 •  Na Hassan Simba, Mtwara 
  IMEELEZWA kuwa kufikishwa kwa elimu juu ya mpango wa kunusuru kaya masikini unaoendeshwa na mfuko wa maendeleo ya jamii nchini tasaf awamu ya tatu, ndio chachu ya mafanikio ya mpango huo yaliyokwishaanza kuonekana kwa jamii ya wakazi wa Mtwara. 
  Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa mfuko huo Bw. Ladislaus Mwamanga, alipokuwa anaongea na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara Idd Mshili, ofini kwake alikokwenda kumtembelea kabla ya kwenda vijijini kujionea namna mpango huo unavyotekelezwa wilayani humo. 
  Bw. Mwamanga alisema kuwa chini ya mpango huo wawezeshaji wamelimishwa vizuri na wao wanaweza kufikisha ujumbe kwa jamii na baada ya kuanza kuelewa ndio maana kumekuwa na mwitikio chanya katika maeneo yote ambako mradi huo umeanza kutekelezwa. 
  "Ndugu mkurugenzi hayo mafanikio unayoanza kuyaona hata kabla ya kuanza kutolewa kwa ruzuku kwa kaya masikini ni matokeo ya elimu ambayo tumewapatia jamii...kwa hakika tumepata mwitikio mzuri kila tulikoenda na hii inatutia faraja na kutuongezea hali ya kufanyakazi kwa bidii", alisema Mwamanga. 
  Mkurugenzi huyo aliyasema hayo baada ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri kuueleza ujumbe wa tasaf makao makuu uliomuhusisha mwakilishi kutoka benki ya dunia.Idda Manjolo. kwamba tayari mafanikio ya mpango huo yameshaanza kuonekana katika wilaya yake hata kabla ya ruzuku kuanza kutolewa kwa kaya masikini. 
  "Nataka niwaambie tu kwamba wakati nyinyi mnasema mpango huu upo katika hatua ya pili ambayo ni kutambua kaya masikini na hatua ya tatu ndio itakuwa ya kuanza kutoa ruzuku lakini hapa kwetu tumeanza kuona mafanikio...uandikishaji wa watoto wa darasa la kwanza umevuka lengo na wakinamama wanaohudhuria kliniki imeongezeka mara dufu", alisema Mshili. 
  Mshili alisema kuwa kwakua mpango huo unalenga pia kutoa ruzuku kwa kaya masikini ambazo watoto wao wanahudhuria shuleni kaya nyingi zimehamasika kuandikisha watoto wao na kufuatilia mahudhurio yao ili kuweza kupata sifa ya kupata ruzuku hiyo na hjivyo kufanya maeneo mengi kuvuka malengo ya uandikishaji waliyojiwekea.
   Mkurugenzi huyo alisema kuwa hiyo ni hatua kubwa ya mafanikio kwani katika kipindi cha nyuma wataalamu wake wamekuwa wakiwahimiza wananchi kuwapeleka watoto wao shuleni na wakinamama kuhudhuria kliniki lakini mwitikio ulikua mdogo kulinganisha na baada ya kuanza kwa mpango huo wa tasaf. 
  Akiwa katika kijiji cha Chawi alikukonda kuona namna ambavyo wanakijijikupitia mkutano wao mkuu wa kijiji wanachaguana kuongoza kamati ufuatiliaji na kuthibitisha majina ya kaya masikini, mkurugenzi huyo alisifu uwazi katika uendeshaji wa zoezi na uelewa mkubwa wa wawezeshaji juu yanmpango huo. 
  Mwamanga alisema chini ya mpango huo uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete 2012 na kuanza kwa majaribio katika wilaya za Bagamoyo, Kibaha na Chamwino, kaya masikini zinapatiwa ruzuku katika elimu, afya na kujikimu kimaisha kila mwezi kwa miaka mitatu ambapo hadi sasa halmashauri 22 zimekwishafikiwa. 
  Mwamanga alisema kwa namna walivyojipanga hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu halimashauri zote kwa upande wa Tanzania bara na visiwani zitakuwa zimefikiwa na mpango huo ambao unalenga kupunguza umasikini miongoni mwa jamii nchini.
   Mwezeshaji  wa jamii wilaya ya Mtwara, Yusufu namoto, akisoma majini ya kaya masikini zitakazoingia katika mpango wa kunusuru kaya masikini katika mkutano wa kijiji cha Chawi wilayani humo ambapo ujumbe wa tasaf makao makuu ukiongozwa na mkurugenzi mtendaji. Ladislaus Mwamanga, mwakilishi wa benki ya dunia Ida manjolo.

  Wananchi katika mkutano wa kijiji cha Chawi 

   Mkurugenzi  Mtendaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii nchini (TASAF) Bw. Ladislaus Mwamanga, (mwenye suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji cha Chawi wilaya ya Mtwara mkoani hapa mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kijiji uliothibitisha majina ya kaya masikini zitakazoingia katika mpango wa kunusuru kaya masikini, kushoto kwake ni mwakilishi wa benki ya dunia Ida Manjolo

  Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii nchini. Ladislaus Mwamanga, (mwenye suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji cha Chawi wilaya ya Mtwara mkoani hapa mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kijiji uliothibitisha majina ya kaya masikini zitakazoingia katika mpango wa kunusuru kaya masikini, kushoto kwake ni mwakilishi wa benki ya dunia Ida Manjolo 

  0 0


  0 0


   KAMPUNI ya Bia (T.B.L) kupitia Brand ya KILIMANJARO imeamua kuliboresha Bonanza la Twanga Pepeta la kila Jumapili linalofanyika katika viwanja vya Leaders Club.

  Maboresho hayo ni kutoa Bia moja ya Kilimanjaro kwa kila atakayelipa kiingilio. Licha ya kupewa Bia moja ya Kilimanjaro, kiingilio cha mlangoni kimepunguzwa sana mpaka kufikia Tshs 2,500. 
  Kwa kawaida kiingilio cha Leaders huwa ni Tshs 5,000/= lakini TBL imeamua kukipunguza mpaka Tsh 2,500 kwa kuwa italipia mapungufu. 
  TBL imeamua kuliboresha Bonanza ili kuwawezesha wapenzi wa Twanga Pepeta na wa muziki wa dansi, kupata fursa ya kukutana kwa pamoja mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kupata burudani ya michezo mbalimbali na hatimaye kuburudika na muziki. 
  TBL kwa muda mrefu imekuwa ikiisapoti Twanga Pepeta na kwa wakati wote itaendelea kuisapoti kwa kuwa ni Bendi kubwa Tanzania. 
  Ikumbukwe pia TBL ndio muanzilishi wa Mabonanza mengi Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla na kwa kushirikiana na Twanga Pepeta ndio walioanzisha Bonanza la Leaders Club. 
  Imetolewa na JESCA NJAU 
  T.B.L RETAIL SALES MANAGER.

  0 0

   Moja ya mabango yaliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Faru nchini. Hafla hii ilifanyika muda mfupi kabla Rais Kikwete hajapanda ndege kuelekea London, Uingereza, kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa kupanga mikakati ya kupambana na ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo na faru.
   Rais Jakaya Kikwete (kulia) akibofya kwenye kompyuta kuzindua rasmi  mabango hayo ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Faru  kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Mahamoud  Mgimwa. 
   Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabango ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Far baada ya kuyazindua rasmi kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam 
   Moja ya mabango hayo likiwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
   Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabango ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Farubaada ya kuyazindua rasmi kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma Pinto. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk. Mahamoud  Mgimwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Said  Meck Sadick.

  0 0

  Wajumbe  wa mkutano  mkuu wa kura za maoni jimbo la Kalenga  wa CHADEMA jioni hii wametegua kitendawili  cha nani kati ya  makada 13 atakayevaana na mgombea wa CCM katika uchaguzi huo baada ya kumchagua  mwanasheria Sinkala Mwenda kwa kura 132 dhidi ya kura 122 alizopata mpinzani  wake wa karibu Grace Tendega huku  Zuberi Mwachura  akiambulia   0 katika uchaguzi huo uliofanyika mjini Iringa.
  0 0

  JD's Entertainment inakwambia kama una mume au mke na unampenda sana, kama una girlfriend au boyfriend na mnapendana kweli na kama uko na rafiki na uko tayari kwa chochote juu yake na atakama uko single lakini moyo wako umejaa mapenzi lakini ujuwi wapi paku yapeleka:basi karibu sana isumba lounge (jollies club). Wapendanao watazungumza,  hadithi na safari za maisha yetu ya kimapenzi zitasikika,ni  valentine hii ya tarehe 14/02/2014 pale pale isumba lounge zamani jollies. Kiingilio ni 10000, karibu tusherehekee mapenzi kwanii LOVE IS GONNA BE IN THE AIR

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji amewapongeza Wakuu wa Mikoa wa Kanda ya Ziwa katika juhudi zao za kuhakikisha Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa linafanyika.

  Mikoa ambayo itashiriki katika Kongamano la Uwekezaji la Kanda ya Ziwa ni Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kagera na Shinyanga Kongamano ambalo kwa pamoja litawakutanisha Wawekezaji pamoja na Serikali katika kujadili vivutio vya Uwekezaji vinavyopatikana katika mikoa hiyo ya kanda ya Ziwa.

  Kituo cha Uwekezaji Kimejizatiti kushirikiana na Mikoa katika kuhakikisha kuwa wawekezaji wanapatiwa huduma zinazohitajika katika Mikoa.

  Kituo cha Uwekezaji na Mikoa wamekubaliana kushirikiana na kuhakikisha kupatikana kwa Ardhi katika Mikoa ili iweze kuwekwa kwenye Benki ya Ardhi kwa ajili ya kupatia Wawekezaji na pia kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu sheria na taratibu zinazomtaka muwekezaji kuzifuata kabla ya kupata ardhi kwa ajili ya uwekezaji.

  Kituo cha Uwekezaji pia kitafanya kazi na Makatibu Tawala wa Mikoa ili kujenga uwezo ili nao waweze kusimamia utoaji wa huduma vizuri kwa wawekezaji katika mikoa yao.

  Kwa maelezo zaidi kuhusu Kongamano la Uwekezaji Tanga na Vivutio vya Uwekezaji vinavyopatikana Kanda ya Ziwa tembelea tovuti ya www.lakezoneinvestmentforum.go.tz
  Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji TIC,Bi Juliet R. Kairuki (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa mikoa ya kanda ya ziwa,toka kushoto ni Mhe. Chief Kishosha Pascal Mabiti (Mkuu wa Mkoa Simiyu); Eng. Evarist Ndikilo (Mkuu wa Mkoa Mwanza) Mhe. Magalula Said Magalula (Mkuu wa Mkoa, Geita); Mhe. John Gabriel Tuppa (Mkuu wa Mkoa Mara); Col Phabian Massawe (Mkuu wa Mkoa Kagera); Mhe. Ali Nassor Rufunga (Mkuu wa Mkoa Shinyanga)

  0 0  0 0

   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets British Foreign Secretary William Hague in his London office this evening. The two leaders then held talks on bilateral issues concerning their two countries.
   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, British Foreign Secretary William Hague and Tanzania’s Minister for Foreign Relations and International Cooperation Bernard Membe pose for a photograph shortly after they met Mr.Hague in his London office this evening.President Kikwete is in London to attend the London Conference on Illegal Wildlife Trade
   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete with British Foreign Secretary William Hague in London  this evening after the  two leaders  held talks on bilateral issues concerning their two countries. Photos by Fred Maro

  0 0


  Watanzania  tujumuike na dada yetu Loveness Mamuya, na kuhudhuria msiba wa  kifo cha  dada yake mpendwa MERCY MAMUYA MTUI kilichotokea leo alfajiri Tanzania.

  Kwa wakazi wa DMV na vitongoji vyake msiba upo nyumbani kwa Bi Loveness Mamuya.

   kama ilivyo mila na desturi yetu tunaomba tumfariji katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

  ADDRESS:  1005 Meandaring way Odeton MD 21113

  NAMBA YA SIMU: LOVENESS MAMUYA:240-4230437

         AZIZI: 301-768-9195  


  Mwenyezi mungu amlaze marehemu mahala pema peponi, 
  Amina. 


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akishuka kwenye ndege wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza jioni ya leo,tayari kwa ufunguzi Kongamano la uwekezaji kwa Kanda ya Ziwa,linaotarajiwa kuanza kesho kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza jioni ya leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Naibu Waziri wa Madini,Mh. Charles Kitwanga.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ambao ndio waratibu wa Kongamano hilo,Bi. Julieth Kairuki,wakati wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza jioni ya leo.Makamu wa Rais yupo jijini Mwanza kwa ajili ya Ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji kwa Kanda ya Ziwa,linalotarajiwa kuanza kesho kwenye Hoteli ya Malaika,jijini humo. 
   Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo (kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Kanali Mstaafu Fabian Massawe wakati walipotembelea hoteli ya Malaika kukagua maendeleo ya Maandalizi ya Kongamano hilo litakalofunguliwa na Makamu wa Rais,Dkt. Mohammed Ghalib Bilal.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ambao ndio waratibu wa Kongamano hilo,Bi. Julieth Kairuki 


  0 0


  Designer LINDA BEZUIDENOUT (LB) dressed in LB at the Legendary Awards in Atlanta, GA, USA.
  Designer Linda Bezuidenhout featured on the cover of ZHe Magazine, February 2014 issue .ZHe magazines goes to 130+ countries such as Nigeria, Cote D'Ivoire, UK, St. Lucia, Kingston JAMAICA, Germany, India, South Africa, Malaysia, US, Mexico, Afghanistan, Antigua, Barbados, Haiti. and in the US they are also placed in many locations from colleges, hotels, airports, business offices lobbies and more. LB DESIGNS ARE FEATURED ON PAGE 11 to 13 pls get your copy http://www.zhemagazine.com/Subscriptions.html

  0 0

  New Jersey - Feb 13, 2014 – Kwanza Press announced today the launch of a new print community journal, Tanzanian Mirror.

  The journal will make its debut with an April edition and will publish every month thereafter. Subscribers receive the publication for free.  Our journal will depend extensively upon loyal readership to beeffective at advertising. The journal will also be available on demand at MagCloud.com. The on-demand journal will allow us to repackage stories and offer it for those in international who want to have the print journal or for those who want the back issues of a digital version.

  Tanzanian Mirror will promote the positive image of Tanzania and enterprises in the USA, will celebrate the intellectual and cultural "renaissance" of Tanzanians living in the USA also willencourage them to give of their time, talents, ideas and expertise whilst inspiring the next generation of Tanzanian leaders.

  Kwanza Press has identified a void in East African communities’ media market in the USA. "We know through our market research that there is a real need for a publication like this," said Kwanza Press’s Vice President Pauline Emmanuel, who will serve as the journal’s chief-in- editor.    

  The initial press run of Tanzanian Mirror will be 20,000 copies monthly, of which 18,500 copies will be direct-mailed to households with an average household income of $70,000 or more in the USA. The remaining 1,500 copies will be targeted through higher institutions and venue distribution (churches, high end retail stores, high end restaurants, businesses, etc.).  


  Florah Mruga will serve as editor assistant of Tanzanian Mirror previous editorial endeavors include freelance ghost writer and book editor. "This publication will also aim to embody the cultivated and innovative the awareness of Tanzania in the USA through impassioned and independent coverage of the Tanzanian’s arts, entertainment and businesses," she said. 

  Kwanza Press is a fast-growing integrated media company that aims to publish multicultural literature and literacy eBooks and paperback books, journals and magazines In addition to its physical magazines, Kwanza Press also produces 4 publication-related websites.

  For more details and submissions, please contact us through the information below

  CONTACT:
  Kwanza Press  
  Pauline Emmanuel (908) 376 6750 

  Vice President/Chief-in Editor
  Email: pemm(at) kwanzapress.com

older | 1 | .... | 357 | 358 | (Page 359) | 360 | 361 | .... | 3353 | newer