Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 344 | 345 | (Page 346) | 347 | 348 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

  Askari polisi watano mkoani dodoma wafariki dunia papohapo katika ajali ya gari iliyotokea 31/01/2014 majira ya 23.45 hrs katika barabara kuu ya Dodoma – Morogoro eneo la Mtumba Center, Kata ya Mtumba Tarafa ya Kikombo Manispaa ya Dodoma, ambapo gari namba T.770 ABT Toyota Corolla lililokuwa likiendeshwa na Askari namba H. 3783 PC DEOGRATIUS wa Polisi Wilaya ya Kongwa likitokea Dodoma mjini likielekea Wilayani Kongwa liligongana uso kwa uso na gari namba T.997AVW Scania Bus mali ya Kampuni ya Mohamed Trans lililokuwa likiendeshwa na JUMA s/o MOHAMED, miaka 38, Mkazi wa Mwanza, likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma na kusababisha vifo kwa askari watano papohapo. 

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amewataja Askari hao waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni:-
  1.          D.9084 D/CPL. ADOLF S/O MESHACK SILLA mwenye miaka 51, Mgogo.
  2.          F.6459 D/C. EVARIST s/o MOSES BUKOMBE mwenye miaka 34, Muha.
  3.          H.3783 PC. DEOGRATIUS s/o PATRICK MAHINYILA mwenyw miaka 29, Mgogo.
  4.          WP.10337 PC. JACKLINE d/o AUGUSTINE TESHA mwenye miaka 22, Mchaga.
  5.          WP.10382 PC. JEMA d/o JIMMY LUVINGA mwenye miaka 20, Mhehe. 
  Wote ni askari Polisi Wilaya ya Kongwa na hakuna abiria aliyeumia katika basi.

  Kamanda MISIME amesema chanzo cha ajali hiyo kulingana na uchunguzi wa awali ni mwendo kasi kutokana na uharibifu uliotokea kwa gari dogo walilokuwa wamepanda askari na jinsi lilivyoburuzwa na basi kwa umbali wa mita 56 kisha kwenda kusimama umbali wa mita 97, kwa hali hiyo umbali kutoka eneo walipogongana hadi basi liliipoenda kusimama ni mita 152. Dereva wa Bus alitoroka mara baada ya ajali hiyo kutokea, juhudi za kumtafuta zinaendelea. Miili ya maerehemu imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya mkoa Dodoma.

  Aidha Kamanda MISIME ametoawito kwa madereva kila mara wawe na udereva wa tahadhari na na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa wa Mambo ya Nje wa Japan, Norio Mitsuya (kulia kwake) aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 01, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR

  0 0

   Kikosi cha timu ya Simba kilichoanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Oljoro JKT uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa. Simba imeshinda 4-0.
    Kikosi cha timu ya Oljoro JKT kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao dhidi ya Simba.
   Waamuzi wa mchezo huo wakiwa katika picha ya pamoja na waamuzi.
   Haruna Chanongo (shoto), akiwania mpira na beki wa Oljoro JKT, Aziz Yusuf.
   Chanongo akimtoka beki wa Oljoro JKT.
   Kiungo wa Simba, Jonas Mkude akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza.
   Wachezaji wa Oljoro JKT wakitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Simba.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amewaonya wanachama na mashabiki wa timu hiyo wanaotishia maisha Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya imataifa wa klabu hiyo, Seif “Magari” Ahmed kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.

  Katika taarifa yake aliyoitoa leo, Manji amesema kuwa si suala jema kwa wanachama kumuhusisha Seif na matokeo ya timu hiyo ambayo kwa sasa imeshinda mechi moja na kutoka sare mechi moja katika mzunguko wa pili wa Ligi kuu ya Tanzania Bara.

  Manji amesema kuwa madai kuwa Seif siyo mwanachama halali  wa Yanga hayana msingi wowote na kuyaita madai hayo kuwa ni ya uzushi na yanaenezwa na maadui zao ambao hawaitakii Yanga mema.

  Alisema kuwa hivi karibuni kumekuwa na madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu, taarifa za hujuma ndani ya timu ambazo zimewahusisha uongozi na baadhi ya wanachama jambo ambalo si la kweli.

  Alifafanua kuwa ni haki kwa kwa nia njema kwa wanachama kuhoji mwenendo wa timu yao pale wanapoona-hairidhishi na ni wajibu wa wanachama kuchanganua mawazo merna na mabaya na siyo kumuhisha mtu kwa moja kwa moja kutokana na mtazamo hasi walionao.

  “Ushindi au mwenendo mzuri  wa timu unatokana na viwango vizuri, nidhamu na ushirikiano wa wahusika wote, wachezaji, walimu, viongozi, wanachama na wapenzi kwa ujumla. Uongozi ulikutana na wachezaji, walimu, baadhi ya wanachama na wapenzi na kuyazungumzia na kukubaliana kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa wahusika wote na kuchukua hatua ya kubadilisha benchi la ufundi,” alisema Manji.

  Aliongeza kwa kusema kuwa uongozi ulifika mbali zaid kwa kutoa adhabu na onyo kali kwa baadhi ya wachezaji walionyesha utovu wa nidhamu kwa kipindi kilichopita na kusikitishwa kuona kuwa baadhi ya wadau kwa kutumia vyombo vya habari wanachochea na kutengeneza uhasama ambao kwa kweli haupo ama kwa faida zao binafsi, au kwa kutumiwa na watu ambao hawana nia njema kwa klabu.

  Manji pia aliwaomba wadau wote wanamichezo na hasa wahariri wa michezo kudhibiti matumizi mabaya ya watu au vyombo vya habari yanayochangia sana kuzorotesha michezo nchini.

  0 0

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri Mwandamizi wa Mambo ya Nje wa Japan Norio Mitsuya alipomtembelea ofisini kwake jana .
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akibadilishana mawazo na Naibu Waziri Mwandamizi wa Mambo ya Nje wa Japan Norio Mitsuya alipomtembelea ofisini kwake jana. Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika mahafali ya tano ya chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar, katika Viwanja vya Wizara ya Habari, Mnazi mmoja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhi zawadi kwa mmoja kati ya wanafunzi waliofanya vizuri katika chuo hicho.
  Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Cha Uandishi wa Habari Zanzibar nd. Chande Omar akitoa ushauri wake kwenye mahafali ya tano ya chuo hicho.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika mahafali ya tano ya chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar, katika Viwanja vya Wizara ya Habari, Mnazi mmoja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar, katika Viwanja vya Wizara ya Habari, Mnazi mmoja. (picha na Salmin Said, OMKR)

  0 0

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Sokoine ,ambapo alisema maandalizi yote yamekamilika ,majukwaa yamekamilika, uwanja umerekebishwa vizuri na vijana wa Halaiki wamejiandaa vya kutosha tayari kwa sherehe ya kuzaliwa kwa CCM tarehe 2 Februari.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki hatua za mwisho za maandalizi ya mahala ambapo maandamano yatahitimishwa.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na vijana wa Halaiki ambao watashiriki kuonyesha Halaiki kwenye kilele cha miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Mbeya tarehe 2 Februari.
  Jukwaa litakalotumika kwa burudani likiwa kwenye hatua za mwisho kufungwa kwenye uwanja wa Sokoine ambapo Band ya TOT na wasanii wa vizazi vipya wanategemewa kutumbuiza.

  0 0
 • 02/01/14--08:58: Article 7
 • SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD 
  WAZEE WA KAZI
  NEW YEAR OFFERS!
  SAVE OVER £600 ON CONTAINERS!
  20' CONTAINER TO DAR /MOMBASA NOW £1,250 
  40' CONTAINER TO DAR MOMBASA NOW £1,750 

  SALOON CARS TO DAR/MOMBASA NOW £700
  4 X 4 CARS TO DAR MOMBASA NOW £780
  AIR CARGO TO DAR £3.80 INCLUSIVE CLEARANCE
  FREE COLLECTION FROM EAST LONDON 

  0 0

  Hey guys. At Miss World, contestants usually need as much support as they can get. I would therefore like to ask for your help in spreading the word to your fellow fans, friends, family, acquaintances etc. about the representative for Tanzania this year;
  Happiness Watimanywa.

  People around the world can help me make an even bigger impact through social media and I would like you to be informed of my journey from as early as now.

  Please follow:
  @misstanzania2013 on Instagram
  @misstz2013 on twitter
  And Like Miss World-Tanzania on Facebook
  Thanks for the support.
  Happy

  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaosoma katika Vyuo Vikuu vya Ubelgiji. Balozi Kamala kakutana na Watanzania hao leo hii Ubelgiji- Brussels kushauriana nao masuala mbalimbali ya kitaifa.

  0 0

  Balozi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa,Geneva,Mhe. Balozi Modest J.Mero amekutana na Dr. Margert Chan, Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani, katika ofisi za Shirika la Afya Dunia jana tarehe 31 Januari 2014. 

  Huu mkutano ni moja ya mikutano ambayo Mhe Balozi anafanya na wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yenye makao makuu hapa Gevena, Uswisi Katika kajenga mahisiano ya karibu kikazi. Katika mkukutano huu msimamo wa Tanzania kuhusu masuala mbalimbali ya Afya yalijadiliwa.

   Maeneo ya kipaumbele ya ushirikiano na shirika hili ni pamoja na kutimiza maelengo ya millenia (MDGs), kuuipa kipaumbele maendelo na ustawi wa jamii na kuhakikisha Afya ina pewa kipaumbele baada ya mwaka 2015. Moja ya maeneo muhimu ya kuendeleza ushirikiano kati Tanzania na Shirika hili, ni eneo la kuboresha upatikanaji wa dawa na chanjo bora, kwa kuangalia jinsi Tanzania itakavyo weza kuwa na viwanda vyenye uwezo huo, na kupunguza utegemizi kutoka nje ya nchi.

  0 0

   Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwapungia Viongozi mbalimbali wa chama,Serikali,na viongozi wa dini na watu mbalimbali (hawapo pichani) waliofika kumpokea mara baada kuwasili jioni ya leo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe  tayari kwa kuongoza maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya chama hicho yatakayofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine mjini humo. 
   Pichani Kati ni Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa chama hicho,Ndugu Kinana (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh Godfrey Zambi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe jioni ya leo. 
  Pichani kati Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete pamoja na Viongozi wa ngaji za juu wa chama hicho,kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho,Ndugu Kinana,Makamu Mwenyekiti Taifa,Mh.Phillip Mangulla na shoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh Godfrey Zambi wakiwa kwenye kikao cha wanachana mbalimbali wa chama hicho (hawapo pichani) ndani ya ofisi ya makao makuu jijini Mbeya jioni ya leo mara baada ya kuwasili.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akilakiwa na waendesha boda boda kutoka sehemu mbali mbali,alipowasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa Songwe,jijini Mbeya mapema leo wakati alipokwenda kumpokea Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete aliyewasili jioni ya leo kwa ajili ya kuhserehekea maadhimisho ya miaka 37 ya chama cha CCM yatakayofanyika katika uwanja wa Sokoini mkoani humo.
   Katibu wa Uchumi na Fedha Bi.Zakia Meghji akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum na Mbunge wa jimbo la Rungwe Mashariki,Mh.Prof.Mark Mwandosya walipokutana jioni ya leo kwenye uwanja wa Ndege wa songwe walipokuwa wakimsubiri Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete aliyewasili leo jioni tayari kwa kuongoza maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya chama hicho yatakayofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine mjini humo. 
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kushoto akizungumza jambo kwa msisitizo na Waziri wa uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe,ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kyela walipokutana jioni ya leo kwenye uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Songwe walipokuwa wakimsubiri Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete aliyewasili leo jioni tayari kwa kuongoza maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya chama hicho yatakayofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine mjini humo.

  0 0

  Wakati wa mahojiano kati ya Ndaba Mandela na Joseph Msami wa Idhaa hii

  Nelson Mandela, ametutoka lakini uwepo wake utaendelea kuwa dhahiri . Hilo limedhihirika baada ya mjukuu wake Ndaba Mandela kuzindua kampeni ya Linda Lango iliyoko chini ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Ukimwi UNAIDS ambapo Ndaba ni msemji wa kampeni hiyo inayotumia michezo kuhamasisha jamii hususani vijana.

  Katika mahojiano maaluma na Joseph Msami wa idhaa hii Ndaba anaanza kwa kujibu swali kwanini aliamua kujihusisha na masuala ya michezo katika kuhamasisha amani na maendeleo?

  Kusikiliza mahojiano haya bonyeza hapa


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wake wakiongozana na Balozi wa Tanzania Nchini India John W.H.Kijazi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Indra Gandhi,Rais atakua nchini India kwa ziara rasmi ya siku tisa.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na akizungumza na Balozi wa India nchini Tanzania Debnath Shaw katika ukumbi wa VIP wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Indra Gandhi Nchini India Rais akiwa huko atatembelea sehemu mbali mbali ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe aliofuatana nao wakipata maelezo kutoka kwa Kiongozi Panraj Dharendra,katika Sehemu ya Historia inayoitwa Amber,wakati alipotembelea sehemu hiyo maarufu katikan jimbo la Rajastan Nchini India,akiwa huko Rais atatembelea Taasisi mbali mbali ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.


  0 0


  0 0

  Mshindi wa promosheni ya WEKA UPEWE ya NBC Limited Bw. Abib Gervas Ndendya (kushoto) akipokea funguo ya bodaboda kutoka kwa Meneja wa tawi la NBC Njombe bi Dorah Godfrey Lewis (kulia) baada ya kuibuka mshindi katika promosheni hiyo hivi karibuni na baadhi ya wafanyakazi wa tawi hilo wakishuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Njombe. Droo kubwa ya promosheni hiyo itafanyika wiki ijayo.
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kagera Mheshimiwa Elizabeth Batenga akiwa na wafanyakazi wa NBC tawi la Bukoba Bw. Emmanuel Minja (wa pili kulia) na Bw. Jackson Kajuna (kulia) alipokabidhiwa zawadi yake ya bodaboda baada ya kuibuka mshindi katika promosheni ya WEKA UPEWE ambayo droo yake kubwa inatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

  0 0

  Mkurugenzi mkuu wa shirika la hifadhi za jamii Tanzania,TANAPA,Alan Kijazi akizungumza jambo wakati kamati ya Bunge ya ardhi,maliasili na mazingira ilipotembelea hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.
  Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ardhi,maliasili na mazingira wakifuatilia maelezo ya mkurugenzi mkuu wa TANAPA(hayupo picani).
  Naibu waziri wa maliasili na Utalii,Mahamud Mgimwa akizungumza mbele ya kamati ya Ardhi ,maliasili na mazingira ilipotembelea hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro.
  Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro ,Erasimus Lufunguro akitoa maelezo kuhusu nusu maili katika mlima Kilimanjaro kwa kamati ya Ardhi ,maliasili na mazingira ilipotembelea hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro.


  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia anayemaliza muda wake, Evaristus Shikongo(katikati) akipokea Salaamu ya heshima toka kwa Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa na Askari wa Magereza wa Namibia(hawapo pichani) wakati wa sherehe za kukabidhi rasmi Uongozi(kulia) ni Waziri wa Ulinzi na Usalama Nchini Namibia, Mhe. Immanuel Ngatjizeko na kushoto kwake ni Kamishna Jenerali Mpya wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela. Sherehe hizo zimefanyika Februari 01, 2014 katika Chuo cha Maafisa Magereza Mahoto kilichopo nje kidogo ya Mji Mkuu wa Windhoek, Namibia.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia(hivi sasa Mstaafu) wa kwanza kulia mstari wa pili akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa Magereza wa Nchini Namibia katika sherehe za kukabidhi Madaraka ya Uongozi wa Jeshi la Magereza Nchini Namibia kufuatia kustaafu kwake kwa mujibu wa Sheria. Sherehe hizo zimefanyika Februari 01, 2014 katika Chuo cha Maafisa Magereza Mahoto kilichopo nje kidogo ya Mji Mkuu wa Windhoek, Namibia.
  Baadhi ya Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa wamesimama kabla ya Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Evaristus Shikongo kupita akiwa kwenye gari Maalum la Wazi wakati akiwapungia mikono Maafisa, Askari pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Namibia ikiwa ishara ya kuwaaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma akiwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia tangu mwaka1995. Wa kwanza kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa pili kulia) ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Namibia, Luteni Jenerali John Mutwa(wa tatu kulia) ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Namibia, Inspekta Jenerali wa Polisi Denga Ndaitunga(wa tatu kulia) ni Mkuu wa Majeshi Mstaafu Nchini Namibia, Lueni Jenerali Mstaafu Martin Chalinde( wa pili kulia).

  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Evaristus Shikongo akiwa kwenye gari Maalum la Wazi huku akiwapungia mikono baadhi ya Maafisa na Askari wa Magereza Nchini Namibia katika sherehe za kukabidhi Madaraka ya Uongozi wa Magereza Nchini Namibia Februari 01, 2014 ambapo sherehe hizo zimefanyikia katika Chuo cha Maafisa Magereza wa Namibia kilichopo nje kidogo ya Mji Mkuu wa Windhoek, Namibia.
  Gadi iliyounda Gwaride Maalum ya Wanawake, Maafisa wa Jeshi la Magereza Nchini Namibia wakipita mbele ya Mgeni rasmi huku wakiwa katika Mwendo wa haraka kama wanavyoonekana wakiwa kikakamavu Februari 01, 2014 katika Sherehe za Makabidhiano ya Uongozi wa Jeshi la Magereza kufuatia kustaafu rasmi Utumishi wa Umma kwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Evaristus Shikongo( hayupo pichani).
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(kushoto) akimpongeza Kamishna Jenerali Mstaafu wa Magereza Nchini Namibia, Evaristus Shikongo(kulia) mara baada ya kukabidhi rasmi Madaraka ya Uongozi wa Jeshi la Magereza Nchini Namibia Februari 01, 2014 katika Sherehe zilizofana sana nje kidogo ya Mji Mkuu wa Windhoek, Namibia( Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Mkuu wa kituo cha Kulelea watoto yatima cha Msimbazi Centre Sister. Ehienne(kushoto),akipokea moja ya msaada wa katoni ya pambazi kwaajili ya matumizi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho toka kwa Mkurugenzi Mtendeji wa Benki ya Biashara ya NBC Tanzania,Bi.Mizinga Melu(katikati) Mkurugenzi huyo alikabidhi vitu mbalimbali kama vile mchele ,mafuta na mashine ya kusagia juisi baada ya kuguswa kama mzazi na maisha ya watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho,kulia ni Katibu Mhitasi wa benki hiyo Jolanda Songoro.
  Mkuu wa kituo cha Kulelea watoto yatima cha Msimbazi Centre Sister. Ehienne(kushoto),akipokea kifaa cha kusagia bidhaa za chakula kwaajili ya matumizi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho toka kwa Mkurugenzi Mtendeji wa Benki ya Biashara ya NBC Tanzania,Bi.Mizinga Melu(katikati) Mkurugenzi huyo alikabidhi vitu mbalimbali kama vile mchele ,mafuta na mashine ya kusagia juisi baada ya kuguswa kama mzazi na maisha ya watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho,kulia ni Katibu Mhitasi wa benki hiyo Jolanda Songoro.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya biashara ya NBC Tanzania,Bi.Mizinga Melu akiongea na watoto wanaolelewa katika kituo cha Yatima cha Msimbazi Centre jijiini Dar es Salaam, wakati alipofika kituoni hapo kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na mashine ya kusagia juisi, alipoguswa kama mzazi na maisha ya watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho.
  Mkurugenzi Mtendeji wa benki ya Biashara ya NBC Tanzania,Bi. Mizinga Melu(kulia)akimuongelesha jambo mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Yatima cha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam,alipotembelea kituo hicho kama mzazi aliyeguswa na maisha ya watoto hao na kutoa msaada wa vitu mbalimbali,Kushoto ni Katibu Mhitasi wa benki hiyo Jolanda Songoro.

older | 1 | .... | 344 | 345 | (Page 346) | 347 | 348 | .... | 3272 | newer