Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 343 | 344 | (Page 345) | 346 | 347 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mwanafunzi wa Shuke hiyo ya Kabale iliyopo Bukoba Vijijini akimkabidhi Bw.  Joe Ricketts maua ikiwa ni ishara ya kumkaribisha mgeni huyo kutoka USA ambaye ni Mwenyekiti wa Mradi wa (Opportunity Education Foundation) kwenye shule hiyo leo hii.

  Bw. Joe Ricketts  kutoka USA kupitia Mradi wa (Opportunity Education Foundation)  akiingia kwenye eneo la Shule hiyo kwenye shule hiyo ya Kabale, Baada ya kupokelewa na Walimu wa Shule hiyo. Kutoka kushoto wa Pili ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Kalafaelia Madiloba na kulia ni Dada Sandra aliyeambatana nae Mgeni huyo Bw. Joe Ricketts kutoka USA.
  Wanafunzi wa Shule Kabale wakimkaribisha Mgeni huyo kwenye Shule yao leo.
  Bw. Joe Ricketts  kutoka USA kupitia Mradi wa (Opportunity Education Foundation)  akiingia kwenye eneo la Shule hiyo na hapa alikuwa akiteta jambo na  Dada Sadra.

  0 0

   Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Bw. Norio Mitsuya, mara baada ya kuwasili katika stesheni ya  Shirika la Reli Tanzania(TRL) kuangalia namna usafiri wa Treni ya Dar es Salaam Unavyofanya kazi, leo mchana

   Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, akimuonyesha mchoro wa njia ya treni ya Bara na ile ya inayofanya Safari zake kutoka stesheni mpaka Ubungo Maziwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Norio Mitsuya huku wakiwa ndani ya treni hiyo, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Shirika la Reli Tanzania (TRL) kujionea namna ya treni ya kutoka stesheni hadi Ubungo Maziwa inavyofanya kazi. Naibu Waziri huyo ameahidi kuwa Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) wataendelea kuisadia miradi mbalimbali ya Reli.

   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan, Norio Mitsuya (mwenye tai ya mistari ya Manjano) akishuka katika kituo cha Ubungo Maziwa, baada ya kumaliza ziara yake ya kuangalia namna treni ya Dar es Salaam, maarufu kama ‘treni ya Mwakyembe’ inavyofanya kazi leo mchana.

  Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Charles Tizeba (wa pili kutoka kushoto), akitoa ufafanuzi wa namna  treni ya Shirika la Reli Tanzania(TRL), inayofanya safari zake kutoka Stesheni mpaka Ubungo Maziwa inavyofanya kazi pamoja na Matarajio ya Serikali katika kuimarisha usafiri huo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Norio Mitsuya leo mchana baada ya Naibu Waziri wa Japan kutembelea usafiri huo na kuona namna ambavyo Serikali yake inaweza kusaidia kuimarisha Usafiri huo. Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi

  0 0

  Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youping akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Leteni Jenerali Sylivester Rioba. msaada huo ambao unathamani ya Shilingi milioni 32 umetolewa kwa ajili ya watu walioathirika na mafuriko mkoani Morogoro.
  Balozi wa China (katikati) akishikana mikono na Luteni Generali Rioba na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Athony Mtaka wakati wa hafla ya kukabidhi msaada iliyofanyika katika Ubalozi wa China. nyuma yao lori aina ya fuso likiwa limejazwa baadhi ya bidhaa za msaada huo.
  Balozi wa China akikabidhi stakabadhi za vifaa vya msaada kwa Leteni Jenerali Rioba huku Mkuu wa Wilaya ya Mvomero akishuhudia.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Na Miza Othman Maelezo Zanzibar
  Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu amesema ucheleweshwaji wa kesi katika Mahakama za Zanzibar unasababishwa na mambo mengi ikiwemo kukosekana mashahidi na kutokamilika kwa upelelezi na ukosefu wa vitendea kazi. 
  Hayo ameyaeleza leo huko Ofisini kwake Vuga wakati alipokuwa akizungumza na waaandishi wa Habari juu ya sherehe ya siku ya sheria Zanzibar ambayo itaadhimishwa tarehe 10 Februari 2014. Amesema kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni “Saidia mahaka kutenda haki “ ikiwa na lengo wadau wote wa mahakama kutoa mchango wao kuiwezesha mahakama kutenda haki. 
  “Kesi sio mahakama pekee wadau wengi wanahusika na kila mmoja anapaswa kutekeleza wajibu wake katika utolewaji wa haki lakini inayolaumiwa zaidi ni Mahakama kwa sababu utoaji wa haki unamalizia hapa” alisema Jaji Mkuu. 
  Amesema kesi za jinai mara nyingi huanzia Polisi na baadae kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mshtaka na hatimae kuwasilishwa mahakamani kwa mashtaka lakini mahakama hushindwa kumaliza kesi kwa haraka kutokana na kukosekana mashahidi na kutokamilika upelelezi. Kwa upande wa kesi za madai Jaji Mkuu amesema zimekuwa na changamoto nyingi baadhi ya wakati mdaiwa hajulikani alipo na mdai anashindwa kuwa na mawasiliano naye. 
  Jaji mkuu wa Zanzibar ameongeza kuwa baadhi ya wakati bajeti nayo inakuwa ni kikwazo kwani imekuwa haitoshi na haipatikani kwa wakati. 
  Amesema siku ya sheria Zanzibar itatoa nafasi kwa wadau wa mahakama ikiwemo Polisi Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na serikali kukaa pamoja kutafakari njia zilizobora za kuendesha kesi kwa haraka. 
  Akizungumzia malalamiko ya rushwa katika mahakama, amesema suala hilo linachangamoto nyingi kwani rushwa hutolewa kwa njia ya siri lakini amewashauri wananchi wanaoombwa rushwa kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa kwa hatua zaidi. 
  Hata hivyo amekumbusha kuwa suala la rushwa ni kosa linalowahusu mtoaji na mpokeaji hivyo amewataka wananchi kutokuwa tayari wanapoombwa rushwa ili kuepuka kuingia kwenye makosa. Jaji Makungu amesema kabla ya kilele cha sherehe hiyo kutakuwa na harakati mbali mbali ikiwemo mdahalo wa wanafunzi utakaozungumzia umuhimu wa heria na vipindi vya Televisheni na Radio ambavyo vitahusu juu ya siku hiyo.
  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akizungumza na waandishi wa habari juu ya sherehe ya siku ya sheria Zanzibar ambayo itaadhimishwa tarehe 10 Februari 2014.  Mkutano huo ulifanyika  Ofisini kwake Vuga, Mjini Zanzibar.
   Mwandishi wa habari wa Idara ya Habari Maelezo Ramadhani Ali akimuuliza swali Jaji Mkuu wa Zanzibar (hayupo pichani)  wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.
   Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akitoa ufafunuzi wa jambo wakati wa mazungumzo yake na waandishi wa habari yaliyofanyika ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.
  Baadhi ya watendaji wa Mahakama ya Vuga mjini Zanzibar na waandishi wa habari wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake Vuga, Mjini Zanzibar leo.
  (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).


  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt Kamugisha Kazaura(aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Mkongo wa Taifa wa TEHEMA kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu. Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mama Edwina Lupembe; kushoto ni katibu wa TTCL Bi. Lugano Rwetaka.
  Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea ofisi za mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
  Mhandisi Adam Mwaipungu akifafanua jambo kuhusu mtambo wa RCIP ambao unawezesha uunganishaji wa Intanet za Kimataifa kwa ofisi za Serikali, Wizara, Idara na vyuo mbalimbali vya elimu ya juu hapa nchini. 

  mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Prof. Juma kapuya.
  Mkuu wa Uendeshaji na matengenezo ya Mtandao wa TTCL Mhandisi Enocent Msasi akitoa maelezo kuhusu mtambo wa DWDM ambao unasafirisha mawasiliano kwa njia ya mwanga kutoka eneo moja kwenda jingine.
  Picha ya pamoja.

  0 0

  Pichani ni mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kawe,Halima  Mdee wakiwa wameachiwa na jeshi la polisi akisindikizwa kwenda kupanda chopa katika viwanja vya mwembetogwa mara baada ya kudaiwa kuzidisha muda kwenye mkutano wao wa hadhara mkoani Iringa. (picha zote na denis mlowe)
  Na Denis Mlowe,Iringa
  MWENYEKITI wa Chadema Mhe. Freeman Mbowe na Mbunge wa jimbo la Hai na Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe. Halima Mdee walishikiliwa kwa muda na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu Iringa, kwa kosa linalosemekana  kuzidisha muda wa mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mgama wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.
  Kwa majibu wa  Mhe. Mbowe alisema jeshi la polisi walimshikilia kwa masaa mawili kwa mahojiano na mkuu wa kituo cha polisi na kisha kumwachia huru.
  Akizungumza na wafuasi wa Chadema kabla ya kupanda Helikopta na kuelekea mkoa wa Pwani akiambatana na Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee aliwataka wananchama wa Chadema kuungana katika kukijenga chama bila hofu na kuwashukuru kwa kuwaunga mkono katika harakati za kuikomboa nchi.
  Alisema wakati wanajiandaa kuondoka alipata malalamiko kutoka kwa kamanda wa Polisi wa Wilaya kuwa wamezidisha muda wa kufanya mkutano katika kijiji hicho.
  Mhe. Mbowe alisema kuwa chanzo kingine ni baadhi ya viongozi wa kijiji kuwadanganya wananchi katika mkutano uliotakiwa kufanyika katika vijiji vya kata ya Ukumbi kuwa watakuwepo  wabunge na mwenyekiti wa chama katika mkutano  kitu kilichosababisha kuwepo na dalili za ugomvi.

  “Jeshi la polisi limetuhoji kuhusu mambo hayo na baada ya kuwaeleza walituachia huru... ila wamesema wakituhitaji watatuita lakini makamanda naomba sana mjenge chama na nawashukuru sana kwa kutuunga mkono katika harakati za kuikomboa nchi” Alisema Mhe. Mbowe.


  0 0

  Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia kipeperushi cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kinachoelezea fao la wastaafu wakati alipotembelea banda la Mfuko huo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Maendeleo Tengeru.
   Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa Sabi akiteta jambo na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Kagenzi Trasias baada ya kupata ufafanuzi kutoka kwa Maofisa wa NHIF kuhusiana na namna ya kujiunga na Mfuko huo kwa wanafunzi wa Vyuo vikuu.
   Ofisa wa NHIF, Paul Minzi akiendelea na zoezi la kupima uzito na urefu kwa wananchi waliojitokeza kupima katika banda la Mfuko huo.
   Upimaji wa afya za wananchi sambamba na ushauri wa namna ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza ukiendelea.


  0 0

   Katibu Mkuu wa Chama cha CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia waendesha Bodaboda ambap wameonekana kufurahia sana mkutano huo uliofanyika leo ukumbi wa Mtenda,Soweto jijini Mbeya.
   Waendesha Bodaboda kutoka sehemu mbalimbali jijini Mbeya,wakiwa wamembeba Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kuzungumza nao mapema leo jioni ndani ya ukumbi wa Mtenda,Soweto mkoani Mbeya.
   Waendesha Bodaboda kutoka sehemu mbalimbali jijini Mbeya,wakiwa wamembeba Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kuzungumza nao mapema leo jioni ndani ya ukumbi wa Mtenda,Soweto mkoani Mbeya.
   Baadhi ya Waendesha boda boda wafurahia jambo kwenye mkutano huo
  Waendesha Bodaboda wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Katibu wa Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye wakati wa mkutano huo.
  Katibu wa Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akizungumza wakati wa mkutano na Waendesha Bodoboda kutoka sehemu mbalimbali jijini Mbeya leo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Inspekta Isack Lema ambaye ni Mlezi wa Bodaboda Mkoani Mbeya,kwa upande wa jeshi la Polisi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Mtenda uliopo Soweto mjini Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na Waendesha Bodaboda wa mjini humo,ambapo Wamemweleza matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo na jinsi wanavyoshirikiana na jeshi la Polisi na Polisi Jamii katika kulinda Usalama wa Wananchi,wao wenyewe na mali kwa ujumla ,Changamoto mbalimbali za kimaendeleo zimetatuliwa na zitaendelea kutatuliwa ili waendesha bodaboda wafanye kazi zao kwa ufanisi na Utulivu.

  0 0  0 0  0 0
 • 01/31/14--12:30: ngoma azipendazo ankal
 • ODYSSEY WANAKUPA 'GOING BACK TO MY ROOTS' MWAKA 1981
  -Makala hii ni kwa udhamini wa The Legend is Back @ Isumba Lounge, Dar es salaam ambao wameingia mkataba na Globu ya Jamii leo hii kurudisha enzi za enzi za disco katika miondoko ya Old School. Usikose kuchungulia hapa kila siku kuanzia saa 12 asubuhi usikie na kuona mambo ya Isumba Lounge kwa mwezi huu mzima wa Februari 2014.

  0 0

  My bad, nimesahau kuweka anwani ya mtandaoni ya RADIO MBAO. Ni www.radiombao.com na itakuwa hewani kuanzia Februari Mosi 2014. Sie tunaamini katika #SharingIsCaring , na RADIOMBAO inakuhamasisha nawe ku-share nasi habari yoyote ile . Usihofie kwamba “ah mie sio mwandishi” tutahariri habari yako na itasomwa/kusikika katika nchi 138 duniani. Na wala usikwazwe na “ah mie sijawahi kuandika” kwani kama unaweza kuandika SMS basi kwa hakika unaweza pia kuandika habari. Pia kila jambo lina mwanzo, mtoto hazaliwi akitembea. Kwahiyo yawezekana RADIOMBAO ikaibua kipaji chako…lakini ili hilo liwezekane basi usihofie ku-share nasi habari. Ni Jumamosi Februari 1, 2014, mahali pa kukutana ni www.radiombao.com #SharingIsCaring (at Glasgow)

  RADIO MBAO: Ninaomba kuwafahamisha kuwa mie na mwenzangu @djkvelli mkongwe wa masuala ya entertainment kama dj nchini Marekani na mmiliki wa kituo maarufu cha radio mtandaoni, RADIOMBAO, tumeunganisha nguvu, na kwa pamoja tunawaletea uzinduzi RADIOMBAO katika sura mpya. Licha ya matangazo ya radio, RADIOMBAO sasa inakuletea habari mbalimbali katika namna tofauti (bringing you news not in your traditional way). Uzinduzi rasmi utakuwa LEO  Jumamosi ya Februari 1 mwaka huu 2014.

   Tunataka nawe uwe mshiriki kwa kututumia habari kwa email radiombao@gmail.com nasi tutataja jina lako kama utapenda tufanye hivyo. Hii pia ni fursa adimu kwa wasanii kutangaza kazi zenu DUNIANI kwani RADIOMBAO inasikika katika NCHI 138 DUNIANI. Tutatangaza kazi yako ya sanaa BURE. Kwa kuunganisha uzoefu na ujuzi wa muda mrefu wa @djkvelli katika masuala ya entertainment nchini Marekani, na uzoefu wangu wa takriban miaka 10 katika fani ya habari, tunawaahidi kuwaletea kitu kipya,tofauti na kitakachokidhi mahitaji yako ya habari,mahojiano,burudani na soka, maisha najamii, teknolojia na mengineyo mengi. Ombi letu kwako ni kuwa sehemu ya familia ya RADIOMBAO: Mfahamishe ndugu, jamaa na rafiki yako kuhudu ujio mpya wa RADIOMBAO. Karibuni sana kutembelea tovuti yetu inayopatikana katika anwani hii

  Wasiliana nasi kwa email radiombao@gmail.com

  0 0

  Ilikuwa patashika nguo chanika katika sherehe ya Harusi ya Alex Mwalwiba na Flora Japher  iliyofungwa katika kanisa la KKKT Mjini Lindi na baadaye mnuso wa nguvu  katika ukumbi wa Lindi Beach hotel.
    Bwana Harusi ni Fundi mkuu wa kampuni ya Uniglobex ya mjini lindi huku Bi Harusi akiwa mwajiriwa wa Jeshi la polisi Mkoani Lindi kitengo cha Usalama barabarani Sote kwa pamoja Tunawaombea Dua katika maisha yao Mapya ya Ndoa 
  Picha na Abdulaziz Video Rec Ya Mjini Lindi
  Wadau  Alex Mwalwiba na Flora Japher wakiwa na nyuso za furaha baada ya kumeremeta
   Alex Mwalwiba na Flora Japher katika taswira ya kumbukumbu Lindi Beach
  Alex akiwa na wapambe
   Alex Mwalwiba na Flora Japher na wapambe wao
   Alex Mwalwiba na Flora Japher wakikata keki kwenye mnuso wao wa nguvu Lindi Beach hotel. Globu ya Jamii inawapongeza na kuwatakia maisha ya heri na ya furaha na yenye watoto kibao.


  0 0

   Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Ardhi maliasili na mazingira Mh James Lembeli akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Mahamud Mgimwa wakisalimiana na wafanyakazi wa hifadhi ya Taifa ya
  Mkomazi.

   Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, maliasili na mazingira wakitembelea eneo la mradi wa kufuga faru pamoja na Mbwa Mwitu.
  Naibu waziri wa maliasili na mazingira ,Mahamud Mgimwa akiwa amemshika 
  mtoto wa Tembo katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi,wengine ni
  mwenyekiti wa kamati ya Ardhi,maliasili na Mazingira James Lembeli na
  mkurugenzi wa shirika la WTPF, Tony Fitzjohn. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  BABA PAROKO CHRISTIAN LIKOKO AKITOA MAWAIDHA WAKATI WA MAZISHI YA MWALIMU FELIX SHAABAN HONERO KATIKA KIJIJI CHA MBOGA, CHALINZE, MKOA WA PWANI JANUARI 30, 2014

  0 0

  TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

  “PRESS RELEASE” TAREHE 01.02. 2014.  MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI.


  gari ambalo halikuweza kufahamika namba zake za usajili wala jina la dereva wake lilimgonga mtembea kwa miguu mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi mbuyuni aliyetambulika kwa jina la daima faida (08) mkazi wa mbuyuni na kusababisha kifo chake papo hapo. ajali hiyo ilitokea majira ya saa 06:55hrs asubuhi wilayani mbarali mkoa wa mbeya. chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi, dereva alikimbia mara baada ya tukio. mwili wa marehemu umekabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi. juhudi za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea. kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed z. msangi anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa wa tukio hili azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na sheria ichukue mkondo wake.  Signed by:

  [AHMED Z. MSANGI – SACP]


  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mashada ya mauwa wakati wa mapokezi nyake alipowasili katika uwanja wa ndege wa Jaipur Nchini India katika Jimbo la Rajastan,akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo mkewe Mama Mwanamwema Shein katika ziara rasmi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kiongozi wa Ulinzi wakati wa mapokezi yake alipowasili katika uwanja wa ndege wa Jaipur Nchini India katika Jimbo la Rajastan,akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo mkewe Mama Mwanamwema Shein.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Viongozi wakati wa mapokezi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Jaipur Nchini India katika Jimbo la Rajastan,pamoja na ujumbe waliofuatana katika ziara rasmi nchini India.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Uhusiano wa Mambo ya Nje Mam Raj Behamni, mara baada ya mapokezi na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakilipowasili katika Uwanja wa dege wa Jaipur Nchini India katika Jimbo la Rajastan,pamoja na ujumbe katika ziara rasmi nchini India[Picha na Ramadhan Othman, India.]

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia katika shamba la Magreth Kalimwa (wapili kulia), katika Kijiji cha Mlimanyoka, Kata ya Nsalanga, wilala ya Mbeya mjini. Kinana alifika kumsaidia mkulima huyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, inayofanyika Kitaifa Jumapili hii mjini Mbeya.

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Bi.Magreth Kalimwa mara baada ya kuwasili kwenye shamba lake kwa ajili ya kushiriki kupalilia shamba hilo lenye ekari moja na nusu
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi na Wanachama wa CCM,(hawapo pichani) katika kijiji cha Itesi Mashariki,Kata ya Nshalanga,alipokwenda kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya kata ya chama cha CCM,Wilaya ya Mbeya Mjini mkoani Mbeya mapema leo.
  Ujenzi wa jengo la Ofisi ya kata ya chama cha CCM,Wilaya ya Mbeya Mjini mkoani Mbeya mapema leo kama ionekanavyo mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokwenda kufanya ukaguzi
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisaidiana na vijana kuandaa jukwaa litakalotumika wakati wa mapokezi ya matembezi ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, kwenye Uwanja wa Sokine mjini Mbeya. Matembezi hayo yanaongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
  Vijana wakiwa kwenye mazoezi ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM yatakayofanyika Jumapili hii mjini Mbeya.

  0 0

  f4702a40d1bf22563232e0028aa968db-e1391201911777
  Mohammed Dewji, Tanzania, Group Chief Executive Officer of Mohammed Enterprises Tanzania Limited

  Dewji is the Group Chief Executive Officer of Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) and at 39 is the youngest member of the Forbes’ Africa’s 50 Richest list with an estimated net worth of USD $500 million.
  The MeTL Group began as a family business, a small trading company which Mohammed transformed into one of the largest industrial conglomerates in East Africa, with interests ranging from real estate, agriculture, finance, distribution and manufacturing.

  The company employs more than 24,000 people across Tanzania and according to Dewji, generates annual revenues of USD$1.3 billion.
  Dewji has been a Member of Parliament in the National Assembly of Tanzania since 2005. Dewji graduated from Georgetown University with a degree in International Business and Finance with a minor in Theology.
  January-Makamba1
  January Makamba Tanzania, Deputy Minister of Communication, Science & Technology and Member of Parliament
  Makamba is one of Tanzania‘s rising stars in government. He is currently the Deputy Minister of Communication, Science and Technology and is rumored to run for President in 2015.

  Makamba is a Member of Parliament for Bumbuli constituency in the National Assembly of Tanzania. Before running for the Bumbuli parliamentary seat, Makamba was aide to Tanzanian President Jakaya Kikwete for 5 years.

  Named Young Global Leader class of 2012 by the World Economic Forum, Makamba comes from a political family; his father, Yusuf Makamba was Secretary General of the ruling CCM party under Julius Nyerere.
  More story click here

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akuhutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Jumuiya ya Istiqaama, uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Feb 01, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Istiqaama, leo Feb 01, 2014.
  Baadhi ya Wanachama wa Jumuiya ya Istiqaama, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akihutubia kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo leo katika Ukumbi wa Karimjee.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, baada ya kufungua rasmi Mkuu wa Jumuiya hiyo leo katika Ukumbi wa Karimjee.
  Picha ya pamoja baada ya kufunguliwa mkutano huo.Picha na OMR.

older | 1 | .... | 343 | 344 | (Page 345) | 346 | 347 | .... | 3272 | newer