Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110017 articles
Browse latest View live

WAJUMBE WA KAMATI YA MAENDELEO YA JAMII, WATEMBELEA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII, RUNGEMBA IRINGA

$
0
0
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii leo wametembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kilichopo Wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa. Lengo la ziara hii ni kukagua utekelezaji wa shughuli za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto katika utoaji wa Mafunzo ya Maendeleo ya Jamii kupitia chuo hiki. Katika ziara hii, wajumbe wa kamati walipata fursa ya kupokea taarifa ya chuo na kutembelea maeneo / miradi mbalimbali ya chuo.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (mb.) akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kilichopo Wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe.Saidi Mtanda (Mb.) wakikagua maeneo / miradi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba na kutoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, katika baadhi ya maeneo yenye kuhitaji maboresho.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Kati) pamoja na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba, (Kulia, mwenye nguo ya kahawia) Bibi Santina Mbata wakiwapitisha Waheshimiwa Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Majengo / miradi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba.

MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA AU WAFUNGULIWA LEO ADDIS ABABA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Mkutano wa  Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) ambao  umefunguliwa  rasmi  leo tarehe 30 Januari, 2014 mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mwenyekiti wa Kamisheni  ya Umoja wa Afrika (AU), Mhe. Dkt. Nkosazana Dlamini-Zuma akisoma hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja huo mjini Addis Ababa, tarehe 30 Januari, 2014. Katika hotuba yake Dkt. Dlamini-Zuma alisisitiza umuhimu wa matumizi ya Lugha ya Kiswahili kwani ni moja ya lugha kubwa Barani Afrika.
Jopo la Marais Wastaafu wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mhe. Olusegun Obasanjo, Rais Mstaafu wa Nigeria, Mhe. Thabo Mbeki, Rais  Mstaafu wa Afrika Kusini na Mhe. Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana.
Rais Mpya wa Madagascar, Mhe. Henry Rajaonarimampianina akitoa hotuba yake ya shukrani kwa nchi za Afrika kwa michango yao iliyopelekea uchaguzi wa amani na demokrasia nchini Madagascar na pia kwa  Madagascar kurejea AU.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MCHANGO WA MASJID COVENTRY UK

$
0
0
URGENT APPEAL
MADRASATUL AQSAA COVENTRY (Reg Charity No 1148412)
We humbly appeal to All Islamic Organisation and Muslims for kind and argent financial support to purchase building for Masjid and Madrasah.

The purchase price of the building is £300,000. We have only six months to pay this sum You can donate by:

1- Making a Standing Order will ensure you donate a regular amount to this noble cause.
2- Sending us a cheque made payable to Madrasatul Aqsaa
3- Making a refundable goodly LOAN (Qardhan Hassanah) to the Madrasah
Bank detail
Hsbc , A/c #14062833, Sort Code 40-18-17, IBAN: GB75MIDL40181714062833
Post your Cheque(Payable to Madrasatul Aqsaa) or postal order to Madrasatul Aqsaa, 188 Eagle Street, Coventry, CV1 4GQ.
If you would like to speak to someone about the project, please telephone us (Sheikh Dawood: 07882442699/ ust Ali: 07767241499 / Ust Yakoub: 07800526992 and we will be please to discuss further over the phone. Jazaka Allahu Khayran for your Support.

Bendi ya 'Sikinde' kutoa burudani ya nguvu kesho Sinza, Meeda

$
0
0
Bendi ya Mlimani Park Orchestra almaarufu kama Sikinde inategemea kuburudisha wapenzi wa muziki wa dansi kutoka Dar es Salaam kesho Ijumaa (31 Januari 2014) katika ukumbi wa Meeda Sinza wilayani Kinondoni.

Akizungumza kwa niaba ya bendi ya Sikinde, Katibu wa bendi hiyo Hamis Mirambo amesema “baada ya kukaa muda mrefu bila kufanya shoo yeyote katika wilaya ya Kinondoni ,bendi ya Sikinde sasa ipo tayari kuwakosha moyo za wapenzi wa muziki wa dansi katika wilaya hiyo pamoja na watu wa wilaya za jirani.”

“Tunapenda kuwaalika wapenzi wote wa muziki wa dansi wasikose kuhudhuria shoo yetu ambayo itaanza ukumbini Meeda kuanzia saa mbili usiku,” alisema Mirambo.

Aliongeza, “Karibuni mpate kuburudika na nyimbo za zamani na mpya kutoka bendi hii kongwe hapa nchini. Mpate kusikia kutoka kwa msanii Bichuka na wengine wengi…karibuni sana!”

Kwa hivi sasa bendi hiyo ya Mlimani Park Orchestra inamalizia kukamilisha albamu yao mpya iitawayo “Jinamizi la talaka” ambayo inabeba nyimbo kama Kibogoyo, Deni ntalipa, Ng’ombe haelemewi nunduwe, Kukatika kwa dole gumba, Tabasamu na Mkwezi.

WAZIR MKUU FINLAND AOKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri Mkuu wa Finland Bw.Jyrki Katainen alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ziara ya siku moja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Waziri Mkuu wa Finland Bw.Jyrki Katainen alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ziara ya siku moja,mazungumzo yao yaligusia zaidi katika uhusiano na ushirikiano katika njanja mbali mbali za kijamii,(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.)

Ujenzi wa miundombinu ya umeme Kanda ya ziwa waanza kushika kasi

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mh. Evarist Ndikilo (aliesimama) akitoa ripoti fupi mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Wizara ya Nishati na Madini juu ya miradi inayotekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini walipomtembelea ofisini kwake ili kuelezea nia yao ya kufanya ziara katika mkoa huo.

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Wizara ya Nishati na Madini wameanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na wizara hiyo kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Victor Mwambalaswa, kamati hiyo ilipata nafasi ya kupokea taarifa fupi kuhusu utekelezwaji wa miradi hiyo iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo ambaye aliwaeleza namna sekta hiyo inavyochangia katika kuinua vipato vya wananchi na taifa kwa ujumla.

Akitoa taarifa kuhusu mahitaji ya umeme Mkoani humo alieleza kuwa kiasi cha juu kinachotumiwa na mkoa huo ni megawati 46 na kuongeza kuwa , kiasi hicho kinaonesha mahitaji halisi na umuhimu wa nishati hiyo na namna umeme unavyochangia ukuaji wa uchumi mkoani humo.

Akizungumza kuhusu ujenzi wa miundombinu ya umeme, alieleza kuwa ujenzi huo umeshika kasi na kuongeza kuwa tayari tayari mradi uliotekelezwa na Millenium Challenge Corporation (MCC) umekamilika wakati miradi mingine inayotekelezwa na REA na Electricity Five inaendelea ambapo takribani wilaya 9 za mkoa wa mwanza zimeguswa na miradi hiyo.

Aidha alisema mradi wa REA phase 1 unajegwa na mkandarasi toka Symbion umegusa wilaya ya Sengerema, Magu na Ukerewe, REA awamu ya pili utaigusa wilaya za Magu, Misugwi, Ukerewe, Sengerema na kwimba na kumalizia kwa mradi wa electricity five unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika kuwa unagusa wilaya za Magu, Misubwi, Kwimba, na Sengerema ambapo alisema katika mradi huo ulipwaji wa fidia kwa wananchi watakaoathirika umeshaanza.

‘‘Kazi ya usambazaji wa umeme Mkoani Mwanza inakwenda vizuri, kukamilika kwa miradi hii kutasaidia vijiji vingi kuwasha umeme hivyo kukuza pato la taifa’’ alisema Ndikilo.

Alimalizia kwa kuwataka wajumbe hao kuwafahamisha wananchi kutumia vipato na akiba zao katika kujenga nyumba zenye ubora ili waweze kuunganishwa na huduma ya umeme.

Vilevile Mhe Ndikilo aliwaomba wajumbe kuwaeleza wananchi wanaowahudumia kujenga mazoea ya kuwa na mwamko wa kupokea na kupenda maendeleo yanayopelekwa kwao na serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati jhiyo Mhe. Victor Mwambalaswa akipokea taarifa hiyo alieleza kuwa nia ya serikali ni kuhakikisha kuwa idadi ya watu waliounganishiwa umeme inapanda toka asilimia 14 hadi kufikia asilimia 30 ifikapo 2015.

WAZIRI MKUU WA FINLAND ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA) KEMPASI YA VUGA

$
0
0
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Rashid Seif Suleiman akimkaribisha Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen alipkutana na uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Kempasi ya Vuga alipofanya ziara ya siku moja Zanzibar.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Professa Idrss Ahmad Raia akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen alipotembelea chuo hicho Kempasi ya Vuga alipokuwa na ziara ya siku Zanzibar.
Waziri mkuu wa Finland Jyrki Katainen akizungumza na uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) alipotembelea chuo hicho katika ziara yake ya siku moja Zanzibar (wa kwanza kulia) ni Waziri wa Miundombinu na Mwasiliano Rashid Seif Suleiman na (kati kati) ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Professa Idriss Ahmad Rai.
Baadhi ya wahadhiri na viongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen wakati akiwahutubia katika Kempasi ya Vuga wakati wa ziara yake ya siku moja Zanzibar.
Picha ya pamoja ya Waziri Mkuu wa Finland na baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar na viongozi aliofutana nao kutoka Tanzania Bara. (wa kwanza kushoto) ni Balozi wa Finland nchini Tanzania Sinikka Antila.(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

Ziara ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala bora yatinga Makao makuu ya TASAF

$
0
0
Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala bora Mh. Abdallah Sallehe Ahmed akifuatilia kwa makini taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF BW. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani).

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala bora imefanya ziara ya kikazi katika Makao makuu ya TASAF jijini Dar es Salaam ili kupata taarifa za utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini na zilizo katika Mazingira hatarishi unaotekelezwa chini ya TASAF awamu ya tatu kote nchini.
 Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala bora Mh. Deogratius Ntukamazina akichukua dondoo muhimu za TASAF awamu ya tatu kama zilivyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF BW. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani)
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF BW. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama pichani) akitoa kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala bora taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini na zilizo katika Mazingira hatarishi unaotekelezwa chini ya TASAF awamu ya tatu.

 Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala bora Mh. Abdallah Sallehe Ahmed akifuatilia kwa makini taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF BW. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani)
 Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala bora Mh. Abdallah Sallehe Ahmed akifuatilia kwa makini taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF BW. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani).


BALOZI KAMALA AKABIDHIWA UENYEKITI WA KAMATI YA MABALOZI WA AFRIKA, KARIBIANI NA PACIFIC (ACP)

$
0
0
  Balozi wa Tanzania  Ubelgiji, Luxembourg na Jumuiya  ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Samoa Ubelgiji na Jumuiya ya Ulaya Mhe. Balozi Dr. Luteru  aliyemaliza kipindi chake cha uenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa ACP. Balozi Luteru amemkabidhi Balozi Kamala uenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa ACP leo, Brussels.

TANGAZO KWA WAOMBAJI WA LESENI ZA UTAFUTAJI WA MADINI

$
0
0
Kamishna wa Madini anawataarifu wenye maombi ya leseni za utafutaji wa madini yaliyoainishwa kwenye jedwali hapa chini kufanya marekebisho ya maombi yao ndani ya siku thelathini (30) tangu tangazo hili kutolewa. Maombi ambayo yatakuwa hayajarekebishwa ndani ya kipindi kilichotajwa yatakataliwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2010.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA WAZIRI MKUU WA FINLAND BAADA YA KUMALIZA ZIARA YAKE NCHINI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiagana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Waziri huyo ameondoka jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiagana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Waziri huyo ameondoka jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akimsindikiza na kuagana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Waziri huyo ameondoka jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. Picha na OMR.

Dkt. Fenella Mukangara akabidhi vifaa vya Michezo kwa Shule za Sekondari jijini Dar leo

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akimkabidhi vifaa vya Michezo mmoja wa wanafunzi waliowakilisha shule zao katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom Salum Mwalimu.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Salum Mwalimu(kushoto) akimkabidhi hundi ya mfano yenye thamani ya shilingi Milioni moja Katibu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT) Henry Lihaya leo jijini Dar es Salaam, katikati yao ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel. Msaada huo ni kwa ajili ya kugharamia mahitaji madogomadogo wakati wa mshindano yanayotarajiwa kuanza mapema hivi karibuni.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akizungumza na wadau wa michezo (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa shule 12 za Sekondari kutoka manispaa zote za jijini la Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano yanayotaraji kufanyika mapema hivi karibuni, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom Salum Mwalimu.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom Salum Mwalimu akizungumza na wadau wa michezo (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa shule 12 za Sekondari kutoka manispaa zote za jijini la Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano katikati ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangarawa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel. Vodacom ndiyo waliodhamini upatikanaji wa Vifaa hivyo.
Baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule zilizokabidhiwa vifaa vya michezo wakifuatilia zoezi la makabidhiano hayo leo jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Frank Shija - Wizara ya Habari

MH. PINDA AZINDUA RASMI MAPITIO YA MFUMO WA UWEKEZAJI TANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (kulia) akikata utepe kuzindua ripoti ya hali ya Uwekezaji nchini Tanzania leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine ripoti hiyo imegusia sera na na maendeleo ya uwekezaji nchini pamoja na changamoto zinazokwamisha ustawi wa uwekezaji Tanzania.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akionyesha vitabu vya ripoti ya Uwekezaji Tanzania kwa wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa ripoti kuhusu hali ya Uwekezaji nchini Tanzania leo jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi kitabu cha Ripoti ya hali Uwekezaji nchini Tanzania Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi (kulia) leo jijini Dar es salaam.

Tanzania na Colombia zajadili namna ya kuboresha ushirikiano wa kiuchumi

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Balozi Rajabu Gamaha (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Asia, Afrika na Oceania kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Colombia, Bibi Sandra Salamanca. katika kikao hicho, viongozi hao walijadili namna Tanzania na Colombia zitakavyoweza kushirikiana ili kutumia fursa zinazopatikana katika nchi hizo kwa madhumuni ya kuinua kipato cha wananchi wao.
Bibi Salamanca (kulia) akisisitiza jambo huku Balozi wa Colombia nchini Tanzania mwenye makao yake Nairobi, Kenya Mhe. Maria Lugenia Correa akisikiliza kwa makini.
Mkurugenzi wa Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu akifafanua jambo katika kikao hicho huku Bw. Graison Ishengoma, Afisa Mambo ya Nje akinukuu masuala muhimu ya mazungumzo. 
Picha ya pamoja, wa tatu kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu ambapo kulia kwake ni Mratibu wa Masuala ya Afrika, Mashariki ya Kati na Asia ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Colombia, Balozi Betty Escorcia.
Picha na Reginald Philip Kisaka.

MANGULA NA KINANA WAWASILI MKOANI MBEYA KWA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM

$
0
0
 Makamu Mwenyekiti wa CCM,Phillip Mangula akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Mary Mwanjelwa baada ya kuwasili leo asubuhi kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya , tayari akwa maadhimisho ya miaka 37 ya CCM yatakayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya Jumapili Februari 2. Kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
 Mangula (katikati) akiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati) akizungumza na Nape (kulia) pamoja na Zambi kwenye chumba cha watu mashuhuri (VIP) alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Mbeya leo mchana, tayari kwa maadhimisho hayo.
 Nape (kulia) akizungumza na Kinana pamoja na Zambi kwenye Uwanja wa Ndege wa Songwe
Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) akijadiliana jambo na Makmu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Dogo Idd Mabrouk wakati wa mapokezi hayo.

CISA REVIEW CLASSES

$
0
0
                                             

Registration is NOW open for CISA Review Class for the forthcoming CISA exam on 14th June, 2014. Our Reviews are due to begin on Monday 24Th February, 2014. Get discount of $75 if you register for the Exam before 12 February, 2014

This CISA Review Class focuses exclusively on the essential areas covered in the CISA exam. This review class covers the core sections and a series of sample exam questions that provide participants with a "feel" of the format and the types of questions encountered on the CISA exam.


Our trainers are qualified Professionals with technical experience, skills and knowledge of specific domain(s). Participants will gain an overall understanding of the relevant CISA Examination DOMAINS.


At the end of the course the MOCK EXAM will be set which will provide the participants with a general idea of the examination questions format. 


Course Contents

Domain 1

Domain 2

Governance and Management of IT

Domain 3

Info Systems Acquisition, Dev & Implementation

Domain 4

Info Systems Operations, Maint & Support

Domain 5

Protection of Information Assets


Two Separate  Mock Exams with 200 Questions Each

                                                           

Study Materials

Our Courses utilize official ISACA presentations and study materials provided by our head office in USA. We will inform you about recommended materials upon your enrolment authorized by us.

Fees- 1,200,000 Tshs.  per Participant (Ask for available discounts in various groups and  possibility of instalment payments)

WARNING:
Any training institution offering review has to be approved by ISACA Tanzania Chapter   before it begins to offer review classes.



For more details about the course and online registration visit our website www.isaca.or.tz www.isaca.org or contact - info@isaca.or.tz. Mobile No 0754 274491/0715274491 

WAZIRI MEMBE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UTURUKI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mhe. Ahmed Davutoglu walipokutana Mjini Addis Ababa kwa mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki. Mhe. Membe yupo Addis Ababa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika kuanzia tarehe 30 hadi 31 Januari, 2014.
Mhe. Membe (katikati) akiwa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Mhe. Balozi Tuvako Manongi (kushoto) pamoja na Bw. Togolani Mavura, Msaidizi wa Waziri wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki (hayupo pichani)
Mhe. Membe (kushoto) akimsikiliza Mhe. Davutoglu (wa pili kulia) wakati wa mazungumzo yao.
Mhe. Membe akifurahia jambo na Mhe. Davotoglu huku akiondoka baada ya mazungumzo yao.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS SASA!

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata Breaking News za wasanii, watu maarufu na zingine kutoka Magazeti Pendwa ya IJUMAA WIKIENDA, UWAZI, RISASI, AMANI, IJUMAA na CHAMPIONI moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa shilingi 100 tu kwa SIKU!

Kujiunga tuma GLOBAL kwenda 15778
Huduma hii ni kwa watumiaji wa Vodacom pekee. 
Kwa maelezo zaidi LIKE Ukurasa wetu wa Facebook hapa: http://on.fb.me/L0OSPD

HIVI NDIVYO HALI ILIVYOKUWA KATIKA TUKIO LA AJALI ILIYOTOKEA MCHANA WA LEO JIJINI DAR

MBUNGE WA SONGEA MJINI, DK EMMANUEL NCHIMBI APATA MAPOKEZI MAKUBWA JIMBONI KWAKE.

$
0
0
 Juu wananchi waliojitokeza kwa wingi kumpokea mbunge wao Mhe Dkt Emmanuel Nchimbi leo mjini Songea. Chini Dkt Nchimbi akiongea na wapiga kura wake na amewashukuru sana kwa mapenzi waliyoonesha kwake baada ya kurejea kutoka Dar es salaam alikopata ajali ya kisiasa iliyomplekea kuwajibika kwa kujiuzuru nafasi yake ya waziri wa mambo ya ndani.

Viewing all 110017 articles
Browse latest View live


Latest Images