Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 341 | 342 | (Page 343) | 344 | 345 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Marehemu Felician B. Lutazengelera
  25 Novemba 1949 – Desemba, 2013

  Kwa masikitiko makubwa, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italia anasikitika kutangaza kifo cha raia wa Tanzania, MAREHEU FELICIAN B. LUTAZENGELERA, ambaye picha yake imeonyeshwa hapo juu.
  Taarifa za kifo hicho zimepokelewa Ubalozini tarehe 14/01/2014 kutoka kwa Mamlaka ya Jiji la Milani, Italia, ambako mwili wa marehemu uliokotwa mtaani hapo tarehe 21/12/2013. 
  Kwa wiki mbili sasa Ubalozi haujafanikiwa kuwapata ndugu wa marehemu, na sasa Ubalozi unatoa tangazo hili leo 29/01/2014 ukiomba msaada ili kuwapata ndugu wa marehemu.

  Ubalozi utashukuru kupokea taarifa kuhusu anuani, na simu, za ndugu wa marehemu kupitia anuani ya baruapepe: info@embassyoftanzaniarome.info  

  Asanteni kwa ushirikiano


  Tangazo limetolewa na Balozi James Alex Msekela, 
  Roma, Italia.
  Simu: +39 0633 4858 20 


  0 0
 • 01/30/14--01:00: DJ JD AFUNGUKA
 • DJ John Dillinga aongelea dicko la Old School na Isumba Lounge

  0 0


  0 0

  Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mhandisi Dkt. Crispin Kinabo akiwasilisha mada juu ya utunzaji wa mazingira kwenye migodi wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika mapema leo katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. Mafunzo hayo yalishirikisha viongozi na watendaji wa wilaya, madiwani, wakuu wa vitongoji na wachimbaji wadogo lengo lake likiwa ni kuwapa uelewa wa kanuni za uchimbaji bora wa madini.
  Mmoja wa wakilishi wa wachimbaji wadogo ambaye ni mmiliki wa mgodi katika eneo la Mhesi Mapinduzi lililopo wilayani Tunduru Bi Sofia Hamdan akichangia mada wakati wa mafunzo hayo.
  Mpepo Ismail ambaye ni mmoja wa wachimbaji wadogo na mmiliki wa machimbo ya shaba Mbesa akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho. Ameitaka Serikali kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa kuwakopesha vifaa vya kuchimba madini.
  Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na watoa mada kwa nyakati tofauti (hawapo pichani).

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  By Hassan Abbas

  Former Rwandan Ambassador to Tanzania, Fatma Ndagiza has been appointed new chair of the Panel of Eminent Persons of the African Peer Review Mechanism (APRM). The Panel is the main advisory body to the APRM Heads of State and Government.

  The appointment was announced at the end of the 20th Summit of APRM Heads of State and Government held on 29th January 2014 in Addis Ababa, Ethiopia.

  A press release from the APRM headquarters said Ambassador Ndangiza succeeds the outgoing Chairperson of the APR Panel, Barrister Akere Tabeng Muna, who served as a Panel Member from inception of the Mechanism in 2003 to January 2014. Barrister Muna was also the team leader of the Tanzanian review process. 

  “She was first appointed as member of the APR Panel of Eminent Persons at the 16th Summit of the APR Forum in 2012. She is currently the Deputy CEO of the Rwanda Governance Board…. Prior to her assumption of these positions, she served as Rwandan Ambassador to Tanzania and was also accredited to Malawi, Zambia, Seychelles and Madagascar,” said the statement.

  Speaking after the appointment, Ambassador Ndagiza expressed her commitment to strengthen the Mechanism to greater heights. She said her tenure as the Chairperson of APRM starts at a time when the APRM celebrated its 10th Anniversary and when there is great interest in the replication of the successes of the Mechanism from other Continents.
    
  Speaking in Addis Ababa, the APRM Tanzania Executive Secretary, Rehema Twalib who attended the meeting, said apart from the appointment of Ambassador Ndagiza, some more countries joined the APRM and South Africa and Mozambique presented their progress reports.


  Tanzania is among the 34 members out of 54 African Union member states who have voluntarily joined the Mechanism which seeks to foster accelerated development, adoption of democratic principles and cherishing principles of good governance among member states.

  0 0

  Na Abdulaziz Video,Lindi

  SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco)mkoani Lindi,limeanza kupokea vifaa mbalimbali,zikiwemo nguzo,Mita na waya,vitakavyotumika kuwaunganishia wateja wapya wapatao 1,413 waliokwishaomba kupatiwa huduma hiyo na kulipia kati ya June na Disemba 2013.

  Meneja wa Shirika hilo mkoani Lindi,Eng John Bandiye ameyaeleza hayo jana alipokuwa akizungumza na timu ya waandishi wa Habari kuhusiana na jitihada za shirika kutoa huduma kwa wateja.

  Vifaa hivyo vimeanza kuwasili mkoani hapa,kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu, na tayari vimeanza kugaiwa Katika wilaya zote tano zilizopo katika mkoa huo.

  Amevitaja vifaa vilivyowasili kuwa ni pamoja na Mita za LUKU 1,413, Nguzo 450 kwa ajili ya Service Line katika njia kubwa za umeme na kwenye mita majumbani.

  Meneja Bandiye amefafanua kuwa kufuatia kupatikana kwa vifaa hivyo,tayari wateja wapatao 1,413 waliotuma maombi ya kupatiwa umeme na kulipia kwa muda mrefu uliopita ,wataunganishiwa huduma hiyo katika kipindi kifupi kijacho kuanzia sasa,ili waondokane na tatizo hilo lililodumu kwao kwa muda mrefu.

  Aidha ameeleza pia katika maombi 1,413 waliyoyapokea kutoka kwa wateja wapya mwaka 2013,wapo 1,132 hawahitaji nguzo na 281 ndio wanaohitaji kupelekewa nguzo na kubainisha kwa kusema wilaya ya Lindi waliotuma maombi yao ni (509) kati ya hao (73) wanaohitaji kupelekewa nguzo,Nachingwea 322 wasiohitaji nguzo ni 263,Kilwa 275 wakiwemo (81) wanaohitaji nguzo,Liwale 154 kati yao 128 hawahitaji nguzo na Ruangwa wapo 153 wanaohitaji huduma ya nguzo ni 42.

  "Tatizo kubwa lililochelewesha wateja wetu wakae muda mrefu ilikuwa ni vifaa,kwa vile vimewasili tatizo hilo,naweza kusema limeisha na kazi ya kuwaunganishia wateja wetu limeanza,hivyo hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Februari 2014,zoezi la kuwaunganishia umeme liwe limekamilika" Alisema Bandiye.

  Kutokana na kufika kwa vifaa hivyo amewashauri wale wateja wapya ambao walikuwa wakisita kulipia kwa hofu ya kuchelewa kuunganishiwa,wafanye hivyo bila ya kukosa ili na wao waweze kufungiwa Mita kwa lengo la kupatiwa huduma waliyoiomba ambayo pia kwa sasa imepunguzwa bei hadi kufikia 27000 kwa wateja walio vijijini kulikopita bomba la Gesi
  Meneja wa Tanesco mkoa wa Lindi Eng John Bandiye
  Ofisi ya Tanesco Mkoa wa Lindi.
  baadhi ya Vifaa vilivyowasili kwa ajili ya kuondoa kero za umeme ikiwa ni pamoja na kuondoa ukatikaji wa umeme mara kwa mara kwa sababu ya Nguzo kuchakaa na kuanguka mara kwa mara hususan katika njia kuu ya Mtwara.

  0 0

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Saseni Media, Bw. Issa Mbura akizungumza katika warsha hiyo kwa wasanii mbali mbali wa filamu hapa nchini.

  Kampuni ya Saseni Media, kwa kupitia mpango wake wa kukuza vipaji vipya vya uigizaji na kuvisimamia, iliendesha kwa mafanikio makubwa zoezi la usaili kwa waigizaji wazoefu na wanaochipukia siku ya jumamosi, tar 25 Januari 2014.

  Idadi kubwa ya watu ilijitokeza kujisajili na kufanyiwa usaili na kila mwigizaji alionekana kuwa ni mwenye shauku ya kutaka kupata fursa hiyo na hivyo kuonyesha umahiri wake katika uigizaji. Akizungumzia usaili huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Saseni Media, Bw. Issa Mbura amesema

  “Zoezi lilienda vizuri na pamoja na kupata vipaji kama lilivyokuwa kusudio letu, pia tumeshuhudia mambo kadhaa yakijitokeza kama changamoto kwa tasnia ya filamu inayotegemea sana waigizaji ili kufanya vizuri,” “Moja, ni kwamba Tanzania kuna waigizaji wengi wanaochipukia na kutafuta fursa za kuigiza kuliko wale wachache tuliozoea kuwaona kwenye luninga zetu,”anasema Mwl. Issa.


  0 0


  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma kamishna msaidizi mwandamizi DAVID MISIME (SACP) anawashukuru wananchi wa kondoa kwa jinsi walivyotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kufanikisha kumkamata mwanamke aliyeiba mtoto mchanga wa siku moja tarehe 20.01.2014 huko katika maeneo ya Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.

  Mtoto huyo wa jinsia ya kiume alizaliwa tarehe 19.01.2014 huko katika zahanati ya Thawi. Mama yake mzazi SALMA S/O ZUBERI, mpare, mkazi wa kijiji cha Mwembeni, Kata ya Changaa - Kondoa, alipatwa na matatizo ambayo yalimlazimu kuhamishiwa katika hospitali ya Wilaya ya Kondoa. Wakati mama huyo akiwa anapatiwa matibabu na daktari alibidi mkwe wake aitwaye HADIJA D/O SAID awe anambeba mtoto huyo mchanga. Alitoka naye nje na ndipo akakutana na AMINA D/O JUMANNE MWASI, 22 Yrs, mkazi wa Mningani, Kondoa mjini, alianza akuongea na nyanya wa kichanga hicho cha siku moja baada ya kuzoeana na mwanamke ambaye alijieleza kuwa amelazwa hapo hospitali kutokana na ujauzito aliomba kumshika au kumpakata mtoto huyo.

  Mama mkwe huyo alitoka kwenda kutafuta chakula ili mgonjwa atakapomaliza matibabu aweze kula. Baada ya muda alirudi akashangaa kutokumwona mama ambaye naye alikuwa amejifanya ni mjamzito haonekani, alijaribu kumtafuta maeneo mbalimbali na kuuliza watu mbalimbali bila mafanikio ndipo akaamua kutoa taarifa Polisi.

  Kwa vile taarifa zilikuwa zimetolewa maenoe mbalimbali wananchi wema walimtilia mashaka mwanamke aliyeiba mtoto na andipo kwa ushiriano mkubwa baada ya kumfuatilia kwa karibu sana Polisi wakafanikiwa kumtia mbaroni tarehe 29.01.2014 wakati alipompeleka motto huyo hospitali ya Wilaya kwani mtoto alianza kuugua.

  Baada ya mahaojiano alikubali kuwa alimuiba mtoto huyo na hata uchunguzi wa kitaalamu umebaini mwanamke huyo hajajifungua siku za karibuni.

  Ninatoa wito kwa wananchi kutokuamini watu wasiwafahamu kwa asilimia mia, hata kama wanalugha nzuri kiasi gani pia nawatahadharisha wanawake waliokosa watoto kwa muda mrefu utatuzi wake sio kuiba watoto wa watu wengine.

  DAVID MISIME – SACP
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA

  0 0

  Leo tarehe 30 January, 2014 Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeiondolea Vikwazo Madagascar na kuiruhusu kuendelea na Uanachama katika Jumuiya hiyo, kufuatia uchaguzi uliozingatia misingi ya Demokrasia. Pichani ni Rais mpya wa Madagascar Mhe. Herry Rajaonarimampianina akizungumza kwenye mkutano unaoendelea leo jijini Addis Ababa,Ethiopia.

  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Mwigulu Nchemba hii leo amekutana na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Njombe kuzungumza nao Kuhusu Wajibu wao wa Kulipa Kodi,Matatizo wanayokumbana naYo kwenye Biashara na namna ya Kuinua Uchumi wao kama Wafanyabiashara wadogo na wakubwa ndani ya Mkoa wa Njombe na Taifa kwa Ujumla.Sehemu ya Wafanyabiashara waliofika kwenye Ukumbi wa Turbo hapa Njombe mjini kwaajili ya Kuzungumza na Naibu waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba.Kubwa zaidi linaloendelea hapa ni Mkutano wa Kubadilishana mawazo kati ya Naibu waziri,Viongozi wa Uchumi Mkoa,TRA na Taasisi mbalimbali za Uchumi pamja na Wafanyabiashara wa Mkoa huu.

  0 0  0 0

  Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe(kushoto), akimtabulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka(aliyevaa tai nyekundu) kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen, wakati Waziri Mkuu huyo alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), leo asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
  Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadh Massawe akitoa ufafanuzi wa namna Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen(wa tatu kutoka kushoto) , wakati alipotembelea Mamlaka hiyo leo asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka. Kulia kwa Waziri Mkuu wa Finland ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe na kushoto kwa Waziri Mkuu huyo ni Waziri wa Niashati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Madeni Kipande, akitoa maelezo ya awali ya namna ambavyo Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen wakati alipotembelea Mamlaka hiyo leo asubuhi kuangalia namna Mamlaka hiyo inavyofanya kazi. Aidha, Waziri Mkuu huyo alitembelea Gati namba 1-7.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akichangia mada wakati wa Mkutano na Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) leo asubuhi kuangalia utendaji wa Mamlaka hiyo.
  Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen wakati alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), kuangalia utendaji wa Mamlaka hiyo. Nyuma ya Waziri Mwakyembe ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi.

  0 0

  Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Ummy Mwalimu, kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014.
  Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha George Boniface Tuguluvala Simbachawene, kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014.
  Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Kaika Saning’o Telele, kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014.
  Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014.
  Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakia katika picha ya pamoja na Waziri na Manaibu Waziri walioapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wapya na wa zamani wa Ofisi yake, baada ya kuapishwa wapya katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kutoka (kulia) ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Muhangwa Kitwanga, ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu na aliyekuwa Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Terezya Huvisa, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR.

  0 0

  Na Miza Kona  -Maelezo Zanzibar 

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeombwa kuipatia fedha Wizara ya Kilimo na Maliasili kwa ajili ya kulipa deni wanalodaiwa na wakulima wa mbegu za mpunga nchi

  Akiwasilisha Ripoti ya Kamati ya Fedha Biashara na Kilimo katika Ukumbi wa Baraza La Wawakilishi Chukwani,  Mwenyikiti wa Kamati hiyo Salmin Awadh Salmin amesema Wizara hiyo inadaiwa jumla ya sh milioni 240 na wakulima wanaozalisha mbegu za mpunga katika mabonde mbalimbali ya kilimo hicho.

  Alifahamisha kuwa wakulima hao wanadai fedha  hizo zaidi ya miezi minne hali inayopelea kurudisha nyuma maendeleo ya kilimo hicho na kukosa kujikimu kimaisha.

  “Kamati ilielezwa kuwa wakulima wa mikataba wanaozalisha mbegu za mpunga katika mabonde mbali mbali wanaidai Wizara jumla ya Tsh milioni 240 baada ya Wizara kuchukua mpunga huo bila ya kuwalipa kwa zaidi ya miezi minne ambapo wakulima wa bonde la Mtwango pekee wanadai Tsh milioni 60,” aleleza Mwenyekiti huyo.

  Ameeleza kuwa tatizo hilo linaweza  kuathiri uzalishaji wa mbegu hizo za mpunga kitendo ambacho kinawavunja moyo wakulima na kuathiri kilimo hicho.

  Aidha Mhe Salmin ameitaka Wizara hiyo ya Kilimo na Maliasili kukipatia mtaalam wa maabara ya Mifugo na ulinzi wa uhakika  Chuo cha Kilimo kiliopo Kizimbani ili kiweze kufanya kazi zake kwa ufanisi.

  Akichangia Ripoti ya Kamati hiyo Mwakilishi wa Viti maalum Asha Bakari Makame ameiomba Serikali kuweka Benki ya mikopo kwa wakulima kutokana na asilimia kubwa ya wazanzibari ni wakulima ili waweze kujikimu wakati wanapopata shida.  


  0 0

  DSC_0014

  Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond juu ya umuhimu wa kujifunza mauaji ya kimbari ya wayahudi ya mwaka 1933.

  Na Mwandishi Wetu

  Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimeendelea kutoa mafunzo na elimu juu ya umuhimu wa kukumbuka maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya ukombozi wa kambi za mateso ya Auschwitz kwa wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.

  Akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond ya jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Afisa habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama amesema kwamba ni muhimu kwa kizazi na kizazi kujifunza madhara ya mauaji na maangamizi ya moto dhidi ya wayahudi yaliofanywa na askari wa kinazi wa Ujerumani.

  “Ni muhimu kutoa mafunzo kwa vijana wakitanzania wa shule za msingi na sekondari ili wajue kwamba tofauti za rangi na za kidini hazina nafasi ya kutugawa kama binadamu,” amesema Nkhoma.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro, wakati alipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 kwa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwakaribisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa (katikati) wakati walipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 kwa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa (katikati) wakati walipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR

  0 0

  Kuna mdada wa miaka 18 Ambae amejifungua binti anaeitwa Maryam kwa bahati mbaya sana mtoto Huyo alipozaliwa hakua na sehemu ya kutoa choo kikubwa hali ya Kua kwamba sehemu hiyo imefunga. Kwa ujuzi wa ma daktari wa muhimbili wamemtoboa hapo ubavuni ili atoe choo kikubwa kwa njia hii. 

  Madaktari walimshauri mama mzazi kuwa mtoto huyo atafanyiwa operation wa kufungua njia ya choo kikubwa akifika mwaka na nusu. Sasa amefika umri na mama mzazi yupo kwenye hali Duni sana na Hana hela ya kumfanyia mtoto operation huo. 

  Nawaomba ndugu zanguni tumsaidie huyu mtoto, kwani hali hii Inaweza kumkuta mtu yoyote. Haya ni Maisha Yake nawaomba mjitokeze kwa Moyo mkunjufu tumsaidie huyu mtoto. 

  Kama Una msaada Wowote ule tafadhali nipigie mimi apa kwa kutumia number: +255719009004 au Kama upo nje ya Tanzania na umeguswa na hili na unataka kutoa sadaka yako tafadhali Tuma kwenye account yangu ya Barclays: Miss S.Yussuf sort code: 207103 acc: 73049328 pia unaweza kutuma njia ya wastern union. 

  Kwa mlikuwepo Tanzania hiyo number yangu ya TIGO PESA. Ahsante sanaa

  KUTOA NI MOYO SI UTAJIRI. MUNGU AWABARIKI SANA.

  0 0

  MS Training Centre for Development Cooperation (MS TCDC), in Usa Rive, Arusha, Tanzania is hosting five day training in peace building and conflict resolution for religious leaders in East Africa. 

  The training brings together 32 religious leaders including traditionalists to share experiences, gain new insights and competencies on peace building and conflict resolution to champion peace and religious tolerance in their communities/countries.

  The training is part of a series of Governance and Accountability courses offered by MS-TCDC through funding from DANIDA. More training opportunities for training on Peace Building and Conflict Resolution will be offered for religious leaders from Africa. Religious leaders have surmountable influence in their communities and hence a force to reckon with in peace building and conflict resolution initiatives.

  Amid emerging and in some places growing religious tensions in East Africa, MS-TCDC a training centre with a mission to train for promotion and protection of human rights saw it fit to contribute to the regional peace building initiatives by organizing trainings on peace building and conflict resolution for religious leaders in East Africa.

  MS TCDC is formerly known as the Danish Volunteer Training Centre, and is a regional Training Centre of ActionAid Denmark. The centre was established in 1967 under a bilateral agreement between the Government of the United Republic of Tanzania and the Royal Danish Government. 

  Today the center trains Civil Society Organizations; public and private organizations from all walks of life with a special focus on governance, human rights based approaches and development studies. The centre also offers academic programs including certificates, diplomas, and bachelor and master degrees.

  MS-TCDC feels privileged to have been accorded the opportunity to host and train religious leaders from East Africa.

  “The choice of MS-TCDC as a destination for training is recognition of our 47 years experience in development management training and contribution to human rights promotion and protection in the region says Principal Suma Kaare” .

  For further information please contact: Dr. Suma Kaare on 0753087713 or MS-TCDC marketing on +255 27 2541044 or visit our website at www.mstcdc.or.tz

  0 0

  Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na niwapongeze kwa kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania.

  Ndugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia -na kumuona kijana wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana Paul Makonda akiwa na ujasiri wa kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhio ya viongozi bila uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.

  Nadiriki kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za kijasiri kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee kupendwa na kuchaguliwa na watanzania.


older | 1 | .... | 341 | 342 | (Page 343) | 344 | 345 | .... | 3270 | newer