Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 340 | 341 | (Page 342) | 343 | 344 | .... | 3284 | newer

  0 0

   Waziri Mkuu wa Finland,Jyrki Katainen akizungumza wakati wa Mkutano uliokuwa ukijadili maendeleo endelevu ya Taasisi za uongozi wa Afrika ulioandaliwa na Uongozi Institute,uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri Mkuu wa Finland,Mh. Jyrki Katainen akisisitiza jambo wakati wa Mkutano uliokuwa ukijadili maendeleo endelevu ya Taasisi za Uongozi Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi,uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,Prof. Joseph Semboja.
  Waziri Mkuu wa Finland,Mh. Jyrki Katainen (kushoto) akiendeleo kutoa hotuba yake mbele ya wageni mbali mbali waliohudhulia Mkutano huo uliokuwa ukijadili maendeleo endelevu ya Taasisi za Uongozi Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi,uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,asie na Wizara Maalum,Mh. Prof. Mark Mwandosya akitoa hotuba yake mbele ya wageni mbali mbali waliohudhulia Mkutano huo (hawapo pichani) uliokuwa ukijadili maendeleo endelevu ya Taasisi za Uongozi Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi,uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Waziri Mkuu wa Finland,Mh. Jyrki Katainen na Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,Prof. Joseph Semboja.
  Muanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mandela na Maendeleo ya Masomo nchini Afrika Kusini,Dkt. Nkosana Moyo akizungumza wakati akiwasilisha mada yake kwenye Mkutano uliokuwa ukijadili maendeleo endelevu ya Taasisi za Uongozi Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi,uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam leo.
  Wageni mbali mbali wakimsikiliza Muanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mandela na Maendeleo ya Masomo nchini Afrika Kusini,Dkt. Nkosana Moyo.


  0 0

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizidua kisima cha maji kilichojegwa na taasisi ya REHEMA Friendship And Solidarity Trust Kwa kushirikiana na Umoja wa Majirani Dunda (UMADU- PUGU) Kisima hicho kimegarimu kiasi cha Shilingi milioni 20.Kulia ni Mwenyekiti wa UMADU-PUGU Jackob Ayo.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimpongeza Mchungaji Secilia Mkude wa EAGT mara baada ya kumtuisha ndoo ya maji baada ya kuzindua Kisima cha maji kilichojegwa na na taasisi ya REHEMA Friendship And Solidarity Trust. Kwa kushirikiana na Umoja wa Majirani Dunda (UMADU- PUGU) Kisima hicho kimegarimu kiasi cha Shilingi milioni 20.kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meki Sadiki na Mwenyekiti wa REHEMA Asir Karabacaar.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia wananchi wa Pugu – Dunda mara baadaya kuwazindulia mradi wa kisima cha maji uliojegwa na taasisi ya REHEMA kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo kupitia umoja wao UMADU-PUGU kwa gharama ya shilingi milioni 20 kulia ni mwenyekiti wa REHEMA Asir Karabacaar na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki.
  Wananchi wa eneo la Pugu – Dunda Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam wakimsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda hayupo picha mara baada ya kuwazindulia mradi wa Kisima cha maji kilichojegwa na taasisi ya REHEMA Friendship And Solidarity Trust. Kwa kushirikiana na Umoja wa Majirani Dunda (UMADU- PUGU) Kisima hicho kimegarimu kiasi cha Shilingi milioni 20.
  Meneja wa Usanifu na Mipango wa TANESCO Mhandisi Theodary Bayona akifafanua jambo mbele ya Waziri Mkuuu wakati mkutano wa hadhara mara baada ya kuzinduliwa mradi wao wa maji uliojengwa na taasisi ya REHEMA Friendship And Solidarity Trust. Kwa kushirikiana na Umoja wa Majirani Dunda (UMADU- PUGU) Kisima hicho kimegarimu kiasi cha Shilingi milioni 20.
  Mhandisi Charles Makoye wa DAWASA akifafanua jambo mbele ya Waziri Mkuuu wakati mkutano wa hadhara mara baada ya kuzinduliwa mradi wao wa maji uliojengwa na taasisi ya REHEMA Friendship And Solidarity Trust. Kwa kushirikiana na Umoja wa Majirani Dunda (UMADU- PUGU) Kisima hicho kimegarimu kiasi cha Shilingi milioni 20
  Kisima cha maji ambacho Waziri Mkuu alikizindua katika eneo la Pugu ambacho kimejegwa na taasisi ya REHEMA Friendship And Solidarity Trust. Kwa kushirikiana na Umoja wa Majirani Dunda (UMADU- PUGU) Kisima hicho kimegarimu kiasi cha Shilingi milioni 20.Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  0 0

  Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ulanga Magharib,Mh. Juma Ngasongwa amenusurika kifo katika ajali iliyo tokea jana jioni maeneo ya Kibaha Picha ya ndege Mkoani Pwani.

  Ajali hiyo iliyohusisha gari aina ya Rav 4 mali ya Mh. Ngasongwa ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe kutoka jijini Dar es salaam wakati akielekea Mkoani Morogoro,ambapo kwa mujibu wa Ngasongwa alichomekewa na lori la Shirika la Umeme (Tanesco) lenye Nambari za Usajili SU 37199 na kupelekea kutokea kwa ajali hiyo.

  Mh. Ngasongwa alikimbizwa Hospitali ya Tumbi,Kibaha na kuanza kupatiwa matibabu mara moja na baadae alihashiwa Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili katika taasisi ya Mifupa (MOI) kwa ajili ya matibabu zaidi.
  Pichani anaonekana Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mh. Mwantumu Mahiza akimjulia hali Mh. Ngasongwa alipokuwa kwenye Hospitali ya Tumbi Kibaha alipo fikishwa kwa ajili ya huduma ya kwanza.katikati ni Dkt. Loti Kiwelu wa Hospitali hiyo.
   Mh. Ngasongwa akisaidiwa na muuguzi wa Hospitali ya Tumbi.
  Hii ndio gari iliyosababisha ajali hiyo.
  Hivi ndivyo ionekanavyo Gari aliyokuwa akiendesha Mh. Ngasongwa.Picha na Chriss Mfinanga.

  0 0

  Kampala, Uganda: The House has passed a Resolution according special thanks to Hon Shem Bageine, Minister of State for the EAC in the Republic of Uganda, for his exemplary performance as Chairperson of the Council of Ministers.

  The Resolution moved by Hon Valerie Nyirahabineza, noted that Hon Bageine represented his people and the citizens of the EAC in the last one year with maximum dedication and commitment. During the period of service as Chair of the Council of Ministers (Nov 30th, 2012 – Nov 30th, 2013), the Minister made invaluable contribution to the advancement of the integration process and spent time in Arusha thus undertaking supervision and co-ordination.

  The Resolution recognizes Hon Shem Bageine’s commitment to enhance regional integration and his leadership style that has helped to hasten the process of regional integration.The Resolution avers that Hon Bageine competently steered Council business within the Assembly, answering questions put before Council, introducing Council Bills and debating important Bills and assisting in the passage of Bills before the House.

  It further appreciates Hon Bageine’s role in the EAC Monetary Union negotiations by inspiring Members of the High Level Task Force to fast-track the negotiations on the Protocol and his personal commitment.

  “EALA appreciates his outstanding contribution as the Chairperson of EAC Council of Ministers as the Chairperson of the EAC Council of Ministers on the EAC major projects including the fight against Non Tariff Barriers and assignment of specific tasks to Ministers” the Resolution reads in part.

  During debate, Members hailed the Minister for his energetic approach, selflessness and sincerity. “You could take his word which many times was equivalent to a ‘One Million dollar cheque’ to the bank”, Hon Kimbisa said.
  “Hon Bageine managed the challenging task of taking the integration process very well,” Hon Nancy Abisai added.

  The Resolution was further supported by Hon Shy-Rose Bhanji, Hon Joseph Kiangoi, Hon Mumbi Ngaru, Hon Emmanuel Nengo, Hon Dora Byamukama, Hon Adam Kimbisa and Hon Susan Nakawuki. Others were Hon Chris Opoka, Hon AbuBakr Ogle, Hon Twaha Taslima, Hon Peter Mathuki, Hon Nusura Tiperu, Hon Hafsa Mossi and Hon Abubakar Zein

  The Members further welcomed on board the new Chair of Council of Ministers, Hon Phyllis J. Kandie.  “You have the support of the whole House and we shall continue to collaborate closely with the Council”, they added.
  The Assembly also asked questions to the Council of Ministers.

  Three papers were also laid on the table in the busy day of activities. The papers are a Report of the East African Inter-Parliamentary Forum on Health, population and Development (EAIPFHPD), Report of the delegation to the Pan African Parliament Annual 2013 Women’s Conference and the Financial Statement and Estimates of Expenditure of the EAC Supplementary Budget for the Financial Year 2013/14.
  The Minister for State in charge of EAC Affairs: EALA moved a Resolution hailing his exemplary performance.
  Hon Valerie Nyirahabineza, the mover of the Resolution.

  0 0

  Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akisisitiza jambo wakati akichezesha droo ya kumi ya promosheni ya Mimi ni Bingwa liyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam. Kushoto ni Muwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Bw. Emmanuel Ndaki.

  WAKATI washindi wa tiketi wa awamu ya kwanza ya promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’ wakitarajiwa kuwasili nchini Alhamis, kampuni hiyo ya simu imechezesha droo nyingine na kumchagua mkazi wa jijini Dar es Salaam, Msemwa George Makuzi kuwa mshindi wa tiketi mbili za kwenda Old Trafford katika wiki ya kumi ya droo hiyo.

  Akizungumza mara baada ya droo hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde alisema kilele cha promosheni hiyo kinakaribia, ambacho tutashuhudia mshiriki wa ‘Mimi ni Bingwa’akiondoka na kitita cha shilingi milioni 50 katika droo kubwa itakayohusisha kila aliyejisajili katika promosheni hiyo.

  “Tukiwa tunafikia kilele cha promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’, nataka niwahakikishie wateja wote wa Airtel kuwa washiriki wapya bado wanakaribishwa kutokana na kuwa mshindi wa pesa taslim ya milioni 50 atapatikana kupitia droo ya bahati nasibu.

  “Kupitia droo hii kubwa, ndiyo tutajua ni nani ataondoka na zawadi kubwa ya ‘Mimi ni Bingwa’. Kutokana na vigezo na masharti ya promotion hii, kila namba iliyosajiliwa kwa ajili ya promosheni, hata kama mshiriki alijibu swali moja tu, ataingia katika droo kubwa.

  “Hii sasa ni nafasi kwa wateja wa Airtel ambao hajajisajili kwenye promosheni kujisajili kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo, na unaweza kuwa mshindi wa zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 au zawadi nyingine za milioni 1 kila siku na milioni 5 kila wiki kwa wiki zilizobaki,” alisema Jane.

  Alisema kuwa ‘Mimi ni Bingwa’ imeonyesha mafanikio makubwa kwa kuwa imepokelewa vizuri na wateja waliojisajili kwa wingi na kujikusanyia pointi kwa kujibu maswali mengi yaliyorahisi yanayoulizwa.

  Jane aliongeza kuwa Airtel itaendelea kuanzisha promosheni na kampeni mbali mbali zinazolenga kuwazawadia wateja wake pamoja na kuyabadilisha maisha yao na kuwa washiriki mahiri wa kuubadilisha uchumi wa Tanzania.

  Alibainisha kuwa washindi wote wa tiketi za safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford watasafiri kabla ya mwisho wa mwezi wa Februari, huku akiongeza kuwa mkakati ni kuwawezesha washindi kwenda Uingereza katika awamu tatu tofauti.

  Katika droo hiyo ya wiki ya kumi, Bi Hawa Mohammed Hussein kutoka Tanga na Godlove William Kayonga kutoka Mara walijishindia shilingi milioni 5 kila mmoja na washindi wengine 12 kujinyakulia shilingi milioni 1 kila mmoja.

  Washindi wengine wa tiketi za ‘Mimi ni Bingwa’ ni pamoja na Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa, Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bw. Shaibu Rashid Dege, Mtendaji wa kijiji cha Nang’olo wilayani Kilwa – mkoani Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro in Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini Dar es Salaam na Salma Farid Mughery kutoka Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Marcel Escure (kulia kwa Waziri) pamoja na Waziri Mstaafu wa Viwanda na Nishati wa Ufaransa Bw. Eric Besson (kulia kwa Balozi), pamoja na watendaji kutoka Ubalozi wa Ufaransa na Wizara ya Nishati na Madini, wakati walipomtembelea wizarani ili kufahamu fursa za uwekezaji katika sekta hizo.
  Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) , Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Marcel Escure (kulia kwa Waziri), Waziri mstaafu wa Viwanda na Nishati kutoka nchini Ufaransa Bw. Eric Besson (kulia kwa Balozi), pamoja na mtendaji kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini, wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyolenga katika kuendeleza sekta za Nishati na Madini nchini.

  Na Teresia Mhagama

  Balozi wa Ufaransa nchini Bw. Marcel Escure akiongozana na Waziri mstaafu wa Viwanda na Nishati kutoka nchini Ufaransa, Bw. Erick Besson wamemtembelea wizarani Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ili kufahamu fursa za uwekezaji katika sekta za Nishati na Madini.

  Waziri huyo mstaafu wa Ufaransa, Bw.Erick Besson alikuwa akiiwakilisha kampuni ya GDF Suez ya Ufaransa.

  Katika suala la usimamizi wa bomba la gesi asilia, Profesa Muhongo alimweleza Bw. Besson kuwa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) litahitaji kupata uzoefu na pengine mbia aliyebobea katika usimamizi wa bomba hilo atakayeshirikiana na TPDC katika usimamizi wa bomba la gesi nchini.

  Kuhusu umeme, Waziri Muhongo alimweleza Waziri mstaafu huyo wa Ufaransa kwamba serikali inajikita katika miradi ya usambazaji umeme kwa utaratibu wa ubia au mikopo ya bei nafuu na ina mpango wa kujenga njia ya umeme ya msongo wa 400kv kuelekea ziwa Tanganyika hivyo aliikaribisha kampuni ya GDF Suez kuwekeza katika miradi hiyo ya usambazaji umeme.

  Aidha Profesa Muhongo alimweleza Bw. Besson kuwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) linatafuta mbia watakayeshirikiana naye katika kuendesha mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe, Kiwira mkoani Mbeya hivyo kama wana nia ya kuwekeza katika eneo hilo pia wanakaribishwa kuingia katika ushindani wa kupata nafasi hiyo.

  Naye Waziri mstaafu wa Viwanda na Nishati kutoka nchini Ufaransa, Bw. Besson alimshukuru Profesa Muhongo kwa taarifa nzuri kuhusu fursa za uwekezaji nchini na ameahidi kupata taarifa zaidi za uwekezaji katika mashirika ya TPDC, STAMICO na TANESCO ili kuona jinsi kampuni ya Suez itakavyoshirikiana na mashirika hayo katika kuendeleza sekta za Nishati na Madini.

  0 0


  0 0

  Mhe. Abdulkarim Shah, Mbunge wa Mafia, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamishna wa Tume ya Utumishi ya Bunge, anasikitika kutangaza kifo cha mama yake mzazi, Bi. Fatma Abdulkarim Mussa (pichani) kilichotokea Chennai, India tarehe 28 Januari, Mwili wa marehemu utawasili nchini tarehe 30 Januari, 2014 kwa ndege ya Shirika la Emirates, saa tisa alasiri na kuzikwa siku ya Ijumaa saa saba mchana katika makaburi ya Kisutu.

  Msiba upo Magomeni, Mtaa wa Matombo, Mwembechai karibu na kwa Sheikh Yahya Hussein.

  Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:

  1. Mhe. Abdulkarim Shah - +918 015 026 119 (India)
  2. Ndg Khalid Shah - 0715 567865
  3. Ndg. Athumani Kwikima - 0759 683 421 - 0787 965 965/0759 305 739

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala bora) Kapteni mstaafu George Mkuchika, akizungumza juzi mjini Babati, kwenye mkutano wa 20 wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Manyara RCC, katikati ni Mkuu wa Mkoa huo Elaston Mbwilo na Kaimu Katibu Tawala Missaile Musa.
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo akizungumza juzi Mjini Babati wakati wa mkutano wa 20 wa Kamati ya ushauri ya mkoa huo RCC (kulia) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala bora) Kapteni mstaafu George Mkuchika na Kaimu Katibu Tawala Missaile Musa.
  Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Mkoani Manyara, Kisiery Werema Chambiri (CCM) akizungumza juzi mjini Babati kwenye mkutano wa 20 wa Kamati ya Ushauri ya mkoa huo (RCC).

  0 0
 • 01/29/14--05:52: JOB OPPORTUNITIES

 • 0 0

   Kipre Tchetche akimtoka beki wa Rhino Rangers, Laban Kambole katika mchezo wa Ligi nKuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo mkwenye Uwanja wa Chamazi. Azam imeshinda 1-0.
  Kipre Tchetche  akipiga mpira uliozaa bao pekee la timu hiyo.
   Mshambuliaji wa Azam FC, Kone Mohamed (katikati), akiwania mpira huku akizongwa na beki wa Rhino Rangers.
   Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre TcheTche akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa timu ya Rhino Rangers, Julius Masunga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam jana. Azama ilishinda 1-0. 
   Kipre Tchetche akimshukuru Mungu baada ya kuifungia timu yake bao.
  Wachezaji wa Azam Fc wakipongezana baada ya Kipre Tchetche kuipatia timu yake bao pekee.
  Wachezaji wa Rhino Rangers wakitoka mapumziko.

  0 0  0 0

  Mgeni rasmi katika kipute hicho alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi na hapa akisalimiana na wachezaji kabla ya mtanange kuanza katika uwanja wa Kaitaba.Mkuu wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Mstaafu Issa Njiku (kulia) akisalimiana na mchezaji wa Mtibwa Sugar ambaye pia ndie aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye mtanange huo ambao timu zote zimamaliza dakika 90 kwa sare ya kutofungana na kugawana pointi moja moja.
  Timu zote mbili zikimsikiliza Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Mstaafu Issa Njiku, kabla ya mtanange kuanza.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, 
  Mhe. Bernard K. Membe 

  Na Mwandishi wetu, Addis Ababa

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaotarajiwa kuanza kesho Alhamisi tarehe 30 Januari, 2014 mjini Addis Ababa, Ethiopia.

  Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa AU uliofanyika tarehe 27 na 28 Januari, 2014 ambao Mhe. Membe aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo.

  Kaulimbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni “Kilimo na Usalama wa Chakula” unalenga kuweka mikakati madhubuti katika kuhakikisha kilimo kinakuwa mkombozi wa watu Barani Afrika kwa kuwainua kiuchumi na kuondokana na wasiwasi wa njaa unaolikabili Bara hili mara kwa mara.

  Mkutano wa Wakuu wa nchi pia utapokea Ripoti mbalimbali ikiwemo ile ya Kamati ya Kimataifa ya Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (CAHOSCC) iliyokuwa chini ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali unatarajiwa kumalizika tarehe 31 Januari, 2013.
  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye akicheza draft na vijana wafanyabiashara wa soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya.
  Nape yupo mjini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambazo kitaifa zitasheherekewa mkoani hapo.
  Katibu huyo wa NEC alikutana na vijana mbali mbali ambao walifurahi sana kumuona kiongozi wao akiwa pamoja nao kiasi soko zima lilipuka kwa nyimbo za hamasa za CCM zilizoimbwa na Kapteni John Komba,Nape pia alipata fursa ya kusalimiana na baadhi ya madereva wa Taxi wa kituo maarufu cha Mafiati.

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na mpiga picha na blogger wa CCM Adam Mzee akila chakula cha mchana kwenye kibanda cha Mama Lishe anayefahamika kama Bi. Tandiwa Tewete kwenye soko la Sido Mwanjelwa mjini Mbeya.
   
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikatiza katikati ya soko la Sido Mwanjelwa kwenda kwenye viwanja vya mpira vya soko hilo kushuhudia mechi ya mpira ya wafanyabiashara wa sokoni hapo.

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiangalia mechi ya mpira kati ya timu ya soka ya sokoni Sido wauza Mitumba na wafungua Mabelo kwenye uwanja wa mpira wa sokoni Sido.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa timu za mpira sokoni Sido Mwanjelwa mjini Mbeya mara baada ya mpira kumalizika.  0 0

   Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kushoto ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Rished Bade.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.
  --
  Na Frank Mvungi
  Serikali imesema pato la Taifa limeendelea kukua kwa asiliamia 7 kwa mwaka katika kipindi cha mwaka 2012 hadi 2013 kutokana na mikakati mizuri ya maendeleo iliyotekelezwa kwa kuzingatia dira ya Taifa ya maendeleo.Hayo yamesemwa na Waziri wa fedha Mh.Saada Mkuya Salum wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
   
  Saada alibainisha kuwa katika robo ya tatu ya mwaka 2013 kiwango halisi cha ukuaji wa uchumi kilikuwa asilimia 6.5 ikilinganishwa na asilimia 7.2 katika kipindi kama hicho cha mwaka 2012.
   
  Katika hatua nyingine Saada alisema kuwa Serikali imejipanga kuongeza pato kwa ufanisi zaidi ili kuongeza pato la Taifa na kupunguza ukwepaji wa kodi kwa kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi na kuwa ya kisasa zaidi.Aliongeza kuwa Serikali kupitia mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) itaendelea kutoa elimu ya matumizi ya mashine za kielektroniki ili kusaidia wananchi kuelewa umuhimu wake kwa maendeleo ya Taifa.
   
  Hata hivyo alibainisha kuwa Serikali imekubaliana na wafanyabiashara kuwa mwisho wa kuanza kutumia mashine za kielektroniki umesogezwa hadi tarehe 30 januari, 2014 ili kuwapa wananchi muda wa kujiandaa na kuanza matumizi ya mashine hizo.
   
  Pia alitoa rai kwa wadau wote kutoa ushirikiano wa dhati katika utekelezaji wa azma ya kuboresha mapato ya Serikali ili kuwaletea wananchi maendeleo endeleo.
   

  Wizara ya Fedha imekuwa ikitimiza majukumu  yake kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025,Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUKUTA) malengo ya maendeleo ya Milenia (MDGs) Ilani ya Uchaguzi mkuu ya CCM  ya mwaka 2010.

  0 0

  The car carrying Finland's Prime Minister Jyrki Katainen arrives at the East Gate of the State House in Dar es salaam this morning for his official reception, ahead of his three-day visit of Tanzania.

  The purpose of their visit is to strengthen bilateral relations and trade and development links, as well as promoting export and internationalisation opportunities for Finnish companies in Ethiopia and Tanzania. In Tanzania, The ministers will also conduct negotiations on bilateral development cooperation. The trip to Tanzania will include a short visit to Zanzibar.

  During this Team Finland trip for the promotion of exports and internationalization, the Prime Minister and the Minister for International Development will be accompanied by a business delegation, assembled by Finpro, with representatives from 27 Finnish companies. The companies involved operate internationally in the fields of energy, infrastructure construction, logistics, the information society, extractive industry, education, health, and agriculture and forestry.


    Finland's Prime Minister Jyrki Katainen stands at attention for the national anthems with his host President Jakaya Kikwete
   Gun-salute for  Finland's Prime Minister Jyrki Katainen
    A member of  TPDF Brass band play as Finland's Prime Minister Jyrki Katainen arrives at the State House
   Finland's Prime Minister Jyrki Katainen receives red carpet reception 

  0 0
 • 01/29/14--12:39: GADO LEO


 • 0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, (CHADEMA), Zitto Kabwe, akiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam Jumatano Januari 29, 2014, akikagua vitabu vya ziada. Kamati ya bunge ya PAC, ilifanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo ili kubaini kama vitabu vilivyonunuliwa kutokana na chenji ya rada vimekwishagawiwa kwenye shule mbalimbali kama ilivyoahidi serikali. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, kamati yake ilikuta vitabu hivyo vikitumiwa na wanafunzi.
  Zitto akizungumza na wanafunzi
  Wanafunzi wakipiga makofi, wakati mwenyekiti huyo akizungumza nao
  Wanafunzi wakisikiliza maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC), ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, kwenye shule ya msingi Bunge katikati ya jiji la Dar es Salaam Jumatano Januari 29, 2014.Picha na K-Vis Blog.

older | 1 | .... | 340 | 341 | (Page 342) | 343 | 344 | .... | 3284 | newer