More Channels
Showcase
Articles on this Page
(showing articles 6721 to 6740 of 65691)
- 01/24/14--22:58: _friji inauzwa
- 01/24/14--23:09: _TUME YA TAIFA YA SA...
- 01/24/14--23:13: _WAZIRI NAGU AMMWAGI...
- 01/25/14--01:00: _Rais Kikwete aongoz...
- 01/25/14--01:09: _Mh. Mhagama afungua...
- 01/25/14--01:18: _BENKI YA CRDB TAWI ...
- 01/25/14--01:53: _BG Tanzania and Bri...
- 01/25/14--02:00: _Dk. Shein kumnadi m...
- 01/25/14--02:05: _SITASITA KUWAONDOA ...
- 01/25/14--02:16: _Kusainiwa kwa Mkata...
- 01/25/14--03:53: _TAARIFA YA JESHI LA...
- 01/25/14--04:17: _Mabalozi wa Nchi za...
- 01/25/14--05:32: _RAIS KIKWETE ALIPOK...
- 01/25/14--06:51: _MOHAMED CHIMSALA (D...
- 01/25/14--07:20: _TAARIFATOKA POLISI ...
- 01/25/14--07:23: _MABONDIA WAPIMA UZI...
- 01/25/14--08:35: _Loyola Sekondari Ya...
- 01/25/14--08:58: _JUMUIYA YA MAENDELE...
- 01/25/14--10:18: _hapo vipi?
- 01/25/14--11:30: _YANGA YAANZA LIGI K...
(showing articles 6721 to 6740 of 65691)
Channel Description:
Most read Swahili blog on earth
Habari za leo,
Nauza fridge kubwa la kisasa, aina a HITACHI, mpya kabisa
Serious Buyer only, Wasiliana nami kwa number 0754360817
0 |
|
0 |
|
Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Mhandisi Omar Bakar ambaye pia alikuwa mfanyakazi wa COSTECH akikata keki maalum iliyoandaliwa na Wafanyakazi wa COSTECH kwa ajili ya kumuaga rasmi tarehe 24 January 2014 katika ukumbi wa Eskape One Hotel Mikocheni jiji Dar es salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa COSTECH Bw Hussein Shaaban akifurahia tukio hilo.COSTECH ni Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia iliyo chini ya Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia ikiwa na jukumu la kuratibu na kuendeleza shughuli zote za Utafiti,Sayansi,Teknolojia na Ubunifu nchini Tanzania kwa Mujibu wa Sheria no 7 ya Bunge ya mwaka 1986
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa COSTECH Bw Shaaban Hussein(Kushoto) akimpongeza Mhandisi Omar Bakari kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mkurugenzi Mkuu wa SIDO mwishoni mwa mwaka jana.
Afisa Utawala Mwandamizi wa COSTECH Bw Audax Mutagwa(Kulia)akimtakia heri na fanaka Mhandisi Omar Bakar kwa kuteuliwa kwake kuwa Mkurugenzi Mkuu wa SIDO
Kaimu Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa ya COSTECH Bw Faith Shimba(wa kwanza kulia) akimsikiliza kwa makini Mhandisi Omar Bakar wakati akiwashukuru wafanyakazi wa COSTECH kwa kumuandalia sherehe hiyo.
0 |
|
0 |
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji). Dk. Mary Nagu (katikati) akikabidhi pikipiki kwa moja ya vikundi 130 vya Vicoba vilivyo chini ya Taasisi ya PFT katika hafla ya kuviongezea uwezo kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es Salaam . Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo. Abbas Mtemvu. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Mwenyekiti wa PFT, Abbas Mtemvu akihutubia wakati wa hafla hiyo
Waziri, Dk Mary Nagu akihutubia katika hafla hiyo, ambapo alimsifia Mtemvu kwa kuanzisha taasisi hiyo ambayo imewasaidia kupunguza umasikini wa wananchi jimboni humo.
0 |
|
0 |
|
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa mbunge wa Chalinze,Mh. Said Bwanamdogo wakati wa mazishi yaliyofanyika kijijini kwake Miono Wilayani Bagamoyo,Mkoani Pwani leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe (CHADEMA) wakati wa mazishi ya mbunge wa Chalinze Marehemu Said Bwanamdogo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika huko Miono Wilayani Bagamoyo,Mkoani Pwani leo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
0 |
|
0 |
|
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mh. Jenista Mhagama (kushoto) akigawa zana za kazi kwa mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk. Primus Mkwela baada ya kulifungua baraza hilo jijini Dar es Salaam jana Ijumaa Januari 24, 2014. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa TET, Dk Leonard Akwilapo.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mh. Jenista Mhagama (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Profesa Idris Kikula ( katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk Leonard Akwilapo, wakati naibu waziri huyo alipofungua Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) jijini Dar es Salaam jana Ijumaa Januari 24, 2014.
Vicheko na nderemo vilitawala wakati Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mh. Jenista Mhagama (katikati) alipokwenda kufungua Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na kukutana na wenzake waliosoma naye na kufanyakazi ya kufundisha miaka mingi iliyopita. Naibu Waziri huyo alikuwa mgeni kwenye uzinduzi wa baraza hilo la TET jijini Dar es Salaam jana Ijumaa Januari 24, 2014.
Keki iliyoandaliwa na uongozi wa Benki ya CRDB tawi la Ubungo kwa ajili ya sherehe za kutimiza miaka 2 tangu kuanzishwa kwa tawi hilo, ambapo wateja wa benki hiyo walijumuika na wafanyakazi wa tawi hilo kusherehekea kwa pamoja.
Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB anayeshughulika na wateja wadogo na wa Kati, Eribariki Masuke, akikata keki wakati wa hafla ya kutimiza miaka 2 kwa tawi la Benki ya CRDB Ubungo. Kulia ni Meneja wa CRDB tawi la Ubungo, Oswald Kweka na wa pili kulia ni Ofisa wa benki hiyo, Angelitha Msaki.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Ubungo, Oswald Kweka akizungumza na wateja wa tawi hilo wakati wa hafla ya kutimiza miaka 2 tangu kuanzishwa kwa tawi hilo. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Wateja Wadogo na wa Kati, Eribariki Masuke.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
0 |
|
0 |
|
BG Tanzania and the British Council today officially launched an international programme offering scholarships to Tanzanian graduates to study for Masters of Science degrees in UK universities. The scholarships will provide opportunities for 10 Tanzanians each year to study in the UK and to become part of the future work force in Tanzania’s oil and gas sector.
A range of courses relevant to the sector are available under the programme at three UK universities; Imperial College London, Aberdeen University and Robert Gordon University.
The scholarships, funded by BG Tanzania and administered in partnership with the British Council, cover the cost of academic fees, travel, living expenses and pastoral support while the graduates are in the UK. Successful candidates will be provided support when applying for a visa.
Derek Hudson, BG Group President and Asset General Manager – East Africa, said: “One of the many ways the oil and gas industry can have a positive impact on the people of Tanzania is through employment. BG Group’s preference, wherever we operate in the world, is to employ skilled people from the communities in which we operate. Initiatives like the international scholarship programme are crucial to maximising local employment, not only with BG Group but across Tanzania’s growing oil and gas sector”.
Mr Hudson said the international scholarship programme is one of several investments by BG Tanzania to improve the livelihoods of Tanzanians, complementing initiatives in secondary education and vocational education training.
Richard Sunderland, the British Council’s Country Director, added: “By building expertise in the oil and gas sector, we will help Tanzania to secure the maximum benefits from an industry that has the potential to bring positive change to the country. Our work with partners such as BG Tanzania is core to our capacity and skills development remit to build trust and understanding between Tanzania and the UK. The scheme will help young Tanzanians to contribute to building a successful future for their country.”
Na Andrew Chale, Zanzibar
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein kesho Jumamosi Januari 26, anatrajiwa kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki, Mahmoud Thabit Kombo, katika uchaguzi mdogo unaoendelea kwenye jimbo hilo.
Katika tarifa yake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kuwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Shein atakuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo wa nne wa hadhara kwenye kampeni hizo zinazoendelea hivi sasa kwenye jimbo hilo.
Na kuongeza kuwa, Dk. Shein atawahutubia wananchi sambamba na kumnadi, Mgombea huyo wa nafasi ya uwakilishi, Mahmoud Thabit Kombo, anayewania nafasi hiyo kwenye jimbo hilo la Kiembesamaki.
Vuai aliwataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi ilikusikiliza sera na ilani za chama hicho katika utekelezaji wake iliwakichague chama cha Mapinduzi kwa misingi imara ya kuwaletea maendeleo.
Aidha, kwa upande wake, Mahmoud Thabit Kombo aliwaomba wananchi wa jimbo hilo, kumpigia kura hiyo Februari mbili, ili akawawakilishe kwenye Baraza la Wawakilishi.
“Nawaomba Wanakiembesamaki, kutumia fursa ya kipekee ya kunichagua ilikuweza kuwawakilisha kwenye BAraza, hakika chama chetu ni sikivu na daima kipo na wananchi katika kuwatetea na kuwaletea maendeleo” alisema, Mahmoud.
Kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembesamaki, zilianza Januari 21, ambapo zinatarajia kumalizika Februari Mosi, mwaka huu huku wananchi wakitarajia kupiga kura ya chaguzi huo, Februari mbili.
0 |
|
0 |
|
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kilichofanyika jana tarehe 25 Januari 2014 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo Sumbawanga Mjini.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akizungumza katika kikao hicho ambapo alitilia mkazo juu kuboresha elimu na ufaulu katika halmashauri hiyo ambayo haijafanya vizuri katika siku za karibuni. Alisisitiza pia umuhimu wa upandaji miti hususani katika msimu huu wa masika.
Mbunge wa Jimbo la Kwela (CCM) Ignas Malocha akishukuru ujio wa Mkuu huyo wa Mkoa katika kikao hicho na maelekezo aliyoyatoa ambayo alisema ni muongozo mzuri na wa kuzingatiwa katika maendeleo ya halmshauri hiyo.
BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI
BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI
0 |
|
0 |
|
Kufuatia kusainiwa kwa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kampuni ya kimataifa ya utafiti na Uzalishaji wa gesi (Shell) tarehe 28 Agosti 2013, wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Shell walikutana huko The Hague, Uholanzi kwa ajili ya uzinduzi wa kamati ya utekelezaji (JIC) tarehe 19 na 20 Januari 2014.Wakati wa mkutano huo, majadiliano muhimu yalifanyika katika maeneo ya kujenga uwezo, uwekezaji wa jamii na maendeleo katika mafuta na sekta ya gesi.
JIC ilianzishwa kwa lengo la utekelezaji wa makubaliano. Makubaliano yameainisha ushirikiano kati ya Shell na Zanzibar katika mafuta na sekta ya gesi na inaelezea shughuli za awali.
"Tunategemea ushirikiano wa muda mrefu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya maendeleo ya sekta za mafuta na gesi Zanzibar," alisema Axel Knospe, mwakilishi Shell visiwani Zanzibar. "
Wawakilishi kutoka Kampuni ya Shell International Exploration na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wao uliofanyika huko Hague, Uholanzi
Mabalozi kutoka nchi za SADC wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Zimbabwe Ubelgiji Mhe. Mary Margaret Muchada (wa tatu kulia). Mabalozi hao walikutana Brussels kumuaga Balozi wa Zimbabwe ambaye anarejea Zimbabwe kuendelea na majukumu mengine.
Balozi Mary Margaret Muchada wa Zimbabwe nchini Ubelgiji Akifurahia Zawadi Aliyopewa na Mabalozi wa Nchi za SADC Ubelgiji. Balozi Hanno Rumpf wa Namibia nchini Ubelgji (mwenye miwani) Ndiye Alimkabidhi Balozi Muchada zawadi kwa niaba ya Mabalozi wa SADC.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Profesa Jeffrey Sachs usiku wa juzi, Jumatano, Januari 22, 2014, wakati wa mjadala kuhusu jinsi ya kuongeza kasi ya mafanikio katika kilimo cha Afrika kwenye Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na Taasisi ya Kilimo ya Grow Africa mjini Davos, Uswisi, ikiwa ni moja ya shughuli za Mkutano wa Mwaka 2014 wa Taasisi ya Uchumi Duniani (WEF). Katikati ni Waziri wa Kilimo wa Nigeria Mhe Dr. Akinwumi Adesina. Picha na IKULU
Marehemu Mohamed Chimsala (Danny) enzi za uhai wake
Familia ya Kanali Chimsala wa Jeshi la wananchi Tanzania anaeishi Masaki Dar es salaam anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake Mohamed Chimsala (Danny) ambaye alikuwa ni askari Polisi kitengo cha Trafiki Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kilichotokea leo asubuhi katika hospitali ya Jeshi la polisi Kurasini. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam
Kwa sasa msiba upo nyumbani kwa kaka yake huko Masaki Dar es salaam.
Taarifa zaidi za taratibu za mazishi mtazipata baadae, baada ya familia kukaa kikao.
Kwa mawasiliano zaidi piga namba:-
"in lillahi wa inna ilaihi rajioon"
"Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe"
Amen.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME ametoa tahadhari kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma kuwa na tahadhari katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha maeneno mbalimbali.
Ametoa thahadhari hiyo baada ya kutokea tukio la PHILIPO SUNGURA, Miaka 55, Mgogo Mkazi wa Kijiji cha Mpinga Kata ya Kigwe WilayaniBahi kufa maji wakati akijaribu kuvuka mto Mpinga ambao ni wa msimu. Tukio hilo lilitokea tarehe 24.01.2014 majira ya saa 18:45 jioni wakati akijaribu kuvuka mto huo huku maji yakiwa ni mengi.
Kamanda Misime ameeleza imembidi kutoa tahadhari hiyo kwani kumbukumbu zinaonyesha watu wengi hupoteza maisha inapofika msimu wa mvua wakiwemo watoto wanaokwenda kuoga na kuchota maji katika mabwawa, mito ya msimu na madimbwi yaliyotuama maji kwa kunasa kwenye tope na kupoteza maisha.
Mfano anaeleza tangu mvua za msimu zilipoanza mwaka huu 2014 watu wanne (4) wameshapoteza maisha.
Amewaomba Viongozi wa Mitaa, Vitongoji, Vijiji, Kata, Tarafa na waalimu mashuleni kuwaeleimisha wananchi na wanafunzi ili kuepukana na matukio hayo.
[DAVID A. MISIME - SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA
Bondia Muss Chitepete kushotoakipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Ramadhani Shauli kulia |
SHULE ya Sekondari ya Loyola ya Jijini Dar es Salaam leo imeadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike shuleni hapo kwa kutoa semina mbalimbali kwa wanafunzi wa kike juu ya changamoto zinazowakabili watoto wa kike na namna ya kukabiliana nazo hasa kwa wanafunzi shuleni.
Mada anuai zimetolewa kwa wanafunzi juu ya changamoto zinazowakabili hasa katika kipindi hiki ambacho nchi zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto ya utandawazi.
Miongoni mwa watoa mada waalikwa katika maadhimisho ya siku hiyo ni Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambao walitoa mada anuai kwa wanafunzi juu ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili hasa kipindi hiki ambacho wanahudhuria masomo yao.
Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.


Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akikata keki maalumu ya kuchangisha fedha zinazowasaidia baadhi ya wanafunzi wanaokubwa na matatizo ambayo familia zao hushindwa kuwasaidia. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
0 |
|
0 |
|
Afisa Mipango Wilaya Kusini Unguja Bw. Faida Khamis Ali akifungua mafunzo ya siku tatu juu ya uelimishaji wa sheria ya uvuvi kwa wakuu wa madiko na wavuvi,katika skuli ya kitogani Kusini Unguja (kulia) Mratibu wa mradi Bw. Omar Muh'd na (kushoto) ni Makamo M/kiti wa Jumuiya maendeleo ya Wavuvi wa Kojani (KOFDO) Ussi Suleiman.
Mkufunzi Muhammed Kassim (alie simama kulia) akitoa elimu yuu sheria ya uvuvi ya Zanzibar katika mafunzo yaliyo fadhiliwa na the Foundation for Civil Society huko Kitogani Kusini Unguja.
Baadhi ya washiri wa mafunzo ya uelimishaji wa sheria ya uvuvi wakimsikiliza kwa makini Mkufunzi Muhammed Kassim (hayupo pichani) katika mafunzo juu ya sheria ya uvuvi.
Mshika Fedha wa Jumuiya maendeleo ya Wavuvi wa Kojani (KOFDO) Faki Othman akichangia katika mafunzo ya sheria ya uvuvi huko Kitogani Kusini Unguja.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Raha ya ushindi.....Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao pili la timu hiyo dhidi ya Ashanti United.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao pili la timu hiyo dhidi ya Ashanti United, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 2-1. Kutoka kushoto ni Frank Domayo, Simon Msuva na David Luhende. Yanga imeshinda 2-1.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la ushindi wa timu yao dhidi ya Ashanti United.
Idd Seleman wa Ashanti United akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa Yanga, Simon Msuva.
Davidi Luhende wa Yanga akiipangua ngome ya Ashanti wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo.
David Luhende akimtoka Hussein Mkongo wa Ashanti wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
David Luhende wa Yanga, akipiga mpira uliozaa bao la pili la timu yake. Huku Hussein Mkongo (kulia), akiwa hana la kufanya.
Benchi la ufundi la Yanga likiongozwa na Kocha Mkuu, Hans Van Der Pluijm (kulia), Kocha Msaidizi, Charles Boniface na Kocha wa Makipa Juma Pondamali.
Moja ya heka heka zilizotokea katika lango la Yanga.
Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Kocha wa Ashanti, Abdallah Kibaden akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm akibadilishana mawazo na David Luhende wakati wa mapumziko.
Moja ya heka heka zilizotokea katika lango la Yanga.
Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Kocha wa Ashanti, Abdallah Kibaden akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm akibadilishana mawazo na David Luhende wakati wa mapumziko.