Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MATUKIO YA STARTIMES 2019

$
0
0
Tangu kuingia katika soko la Afrika Mwaka 2018,StarTimes  inajitahidi kufikia Malengo yake, ili Kuhakikisha kwamba  kila Familia ya Kiafrika inapata ,nafasi na uwezo wa kuangalia/Kutazama Televisheni ya Kidigitali.
Na hivi sasa StarTimes inatoa huduma kwa  watu takribani Milioni 30 katika Nchi 37. Ukuaji Huu mkubwa  umeifanya  StarTimes kua Muendeshaji mkubwa wa Runinga  Barani Afrika na pia katika kuhakikisha inaleta maudhui mazuri kwa wateja wake.
StarTimes imetoa kipaumbele kwa jamii katika  kuhakikisha inarudisha kile inachopata hasa katika kuwaunga mkono Taasisi zidizo  za kiserikali,Sekta ya Filamu Afrika.
Mwaka 2019 StarTimes ilitoa mchango wake  kwa Jamii:

UCHANGIAJI
 Kampuni ya StarTimes Ilichangia Polisi  vifaa vya Michezo ikiwemo Tshirt,hii ilikua  katika kuchangia jamii na kusaidia mahitaji mbalimbali.
Vile vile StarTimes ilichangia Elimu katika kampeni ya TOKOMEZA ZERO Kisarawe kiasi cha Shilingi Milioni 10 katika kusaidia Serikali kwenye jitihada za kuhakikisha inatokomeza Zero.
Pia iliweza  kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni 4 kwenye Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Cardiac Institute at Muhimbili National Hospital,Pesa hizo zilitolewa kusaidia Matibabu pamoja na huduma nyingine kwa watoto wenye matatizo ya Moyo.

HUDUMA KWA JAMII
StarTimes iliweza kutembelea kituo cha watoto yatima kitwacho (CHAWAMA ) kilichopo Sinza ,na kuwapatia msaada  kiasi cha Shilingi Milioni 3.
Kwa Upande wa Tamthilia mwaka 2019 StarTimes iliweza kuleta Tamthilia ya Waaris yenye maudhui yaliyopendwa  na watazamaji Wengi na imejichukulia umaarufu sana ikifuatiwa na Wild Flower,Blood Sister na The queen of Flow.
UDHAMINI
Mwaka 2019,StarTimes waliweza kudhamini tamasha la wasafi lililofanyika katika mikoa mitano na kumalizikia jijini Dar es salaam,na ilifanikiwa kudhamini mashindanoo ya kusaka vipaji ya Bongo Star Search ambayo yalikwenda vizuri na kuhitimishwa vizuri.

MATUKIO
Startimes iliweza kufanya matamasha  ya kuleta wasanii wa tamthilia ya Ode to Joy  iliyofayika  katika Hotel ya  Hyatty iliyopo Posta jijini Dar es Salaam.
ni wasanii maaurfu sana nchini China,Tamthilia hii iliweza kufanyiwa tafsiri kwa lugha ya kiswahili

TUZO
Startimes imekabidhiwa TUZO  kutoka shirika la TACAIDS  Tanzania kwa kutambua mchango wao StarTimes nao wakatoa mchango wa shilingi Million 5 ilikusaidia  Serikali katika mapambano dhidi ya  kutokomeza virusi vya Ukimwi.

MEJA JENERALI KINGU AKABIDHI RASMI OFISI KWA KAIMU KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI, JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (kulia) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (kushoto) akimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia), pamoja na Watendaji wa Wizara, mara baada ya makabidhiano yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (kushoto) akizungumza na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia), pamoja na Watendaji wa Wizara, mara baada ya makabidhiano yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (wapili kulia-mstari wa mbele), aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (wapili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji mbalimbali wa Wizara hiyo, mara baada ya kumaliza makabidhiano yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI ZUNGU AWASILI MTUMBA NA KUSISITIZA UADILIFU

$
0
0
Na Lulu Mussa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amemtaka kila mtumishi katika Ofisi ya Makamu wa Rais atimize wajibu wake katika kuleta maendeleo ya Taifa letu.
Hayo ameyasema hii leo mara baada ya kuwasili rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma na kupokewa na Menejimenti na watumishi na Ofisi hiyo. 

Akizungumza na watumishi wa Ofisi yake Waziri Zungu amewataka wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kuahidi kuendelea kusimamia Sheria, Taratibu na Kanuni zilizopo.
Ametoa rai kwa watanzania kuwa chachu ya mabadiliko katika kuhifadhi na kusimamia Mazingira. “Simamieni Sheria bila kumuonea mtu, pale ambapo Sheria imekataza jambo simamieni Sheria na kuchukua hatua kwa wote wanaokiuka” Zungu alisisitiza.

Awali aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ambae sasa ni wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene amekabidhi Ofisi rasmi kwa Waziri Zungu na kumtakia kila la heri katika kutekeleza majukumu yake mapya.
“Tumefanikiwa katika katazo la mifuko ya plastiki, tumeridhia Mikataba na Itifaki mbalimbali na pia tuna program maalumu ya Upandaji mti nchi nzima ambayo ni endelevu” Simbachawene alisisitiza.

Pia Mhe. Waziri Simbachawene alisema kuwa mbali ya kufanikiwa katika kampeni ya katazo la mifuko ya plastiki lakini zaidi na elimu inapaswa kutolewa kwa wananchi kuhusu tofauti ya vifungushio na vibebeo ambavyo bado wananchi wanachanganya.

Amempongeza na kumshukuru Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mhandisi Joseph Malongo kwa muda aliofanya nae kazi kwa ukaribu ambapo wameweza kutekeleza majukumu mbalimbali yakiwemo kuridhia mikataba, itifaki na kanuni zinazohusu mazingira.

Waziri Zungu ameteuliwa hivi karibuni na Rais Dkt. John Magufuli kushika nafasi hiyo baada ya kufanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri ambapo Mhe. Simbachawene aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akikaribishwa rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na Balozi Joseph Sokoine Naibu Katibu Mkuu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongea na Menejimenti ya Ofisi yake mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba mapema leo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongea na sehemu ya watumishi wa Ofisi yake mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba mapema leo. Pamoja na mambo mengine amewasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo.
 Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ambae sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene akimkabidhi rasmi Ofisi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu. Makabidhiano hayo yamefanyika hii leo katika Mji wa Serikali Mtumba – Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene mara baada ya kukabidhiana Ofisi hii leo Mtumba Dodoma. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo, Naibu Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC) Dkt. Samwel Mafwenga.

MWAKILISHI MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA AJITAMBULISHA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kulia) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bi. Christine Musisi alipomtembelea ofisini kwake, Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma kwa ajili ya kujitambulisha. Mwingine pichani ni  Bw. Godfrey Mulisa Mtaalam wa masuala ya utawala wa Umoja wa Mataiafa. 

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) akiongea na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bi. Christine Musisi (kulia) alipomtembelea ofisini kwake, Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma kwa ajili ya kujitambulisha. Wengine pichani ni Wakurugenzi kutoka Wizarani hapo

KAMATI ZA USIMAMIZI WA MAAFA MIKOA YA MRADI BOMBA LA MAFUTA ZASHAURIWA KUUWEKA MRADI MPANGO WA KUJIANDAA KUKABILIANA NA MAAFA

$
0
0
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, imezishauri Kamati za Usimamizi wa Maafa katika  mikoa 8 na vijiji 184  vinavyopatikana   katika wilaya 24 zilizopo katika mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga, ambapo Mradi wa Bomba la Mafuta utatekelezwa kuuweka Mradi huo katika Mipango yao ya kujiandaa na kukabiliana na Maafa ili kuhakikisha mradi huo hauthiriwi na majanga yanayoweza kutokea.

Kwa mujibu wa sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha majukumu ya  kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutoa taarifa za tahadhari ndani ya eneo husika, Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji  wilaya au mkoa, pamoja na kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika ngazi husika.

Akiongea mara baada ya kutembelea eneo la kwenye peninsula ya Chongoleani karibu na bandari ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa, Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amefafanua kuwa Kamati za maafa zinalo jukumu la kuchukua tahadhari ya namna ya kuhakikisha majanga yanayoweza kuuathiri mradi huo yanakuwa katika mipango yao ya menejimenti ya maafa ili faida zitakazotokana na utelelezaji wa mradi huo zinakuwa endelevu.

Kwa upande wake,  Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Noel Kazimoto ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo utafungua fursa za kiuchumi kwa watanzania hivyo ni dhahiri kuwa eneo la Chongoleani litakuwa na mwingiliano mkubwa wa watu na shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii zitakuwa zikiendeshwa, kwa kuwa wananchi ni wadau wa menejimeti ya maafa kupitia kamati za menejimenti  za maafa kuanzia ngazi ya vijiji, wataendelea kuelimishwa juu ya majanga  yanayoweza kuuathiri mradi huo ili waweze kuhakikisha mradi unakuwa endelevu.

Kwa mujibu wa Tovuti rasmi ya Kampuni inayojenga mradi huo, East African Crude Oil Pipeline www.eacop.com. Kampuni hiyo inabainisha kuwa wanao mpango unaohakikisha utelezaji wa mradi huo unazingatia majanga na maafa wakati wa kupanga, kujenga na kuendesha Bomba, ambapo Mpango huo unahakikisha kwamba, katika tukio la dharura linaloweza kutokea, hatua za haraka, zinachukuliwa.

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi unatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikisha kampuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikali za Tanzania na Uganda. Mafuta ghafi yatasafirshwa kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. Mradi wa Bomba hilo una umbali wa kilometa 1,445 ambapo kilometa 298 zitakuwa nchini Uganda, na kilometa 1,147 zitakuwa nchini Tanzania.
 Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akisisitiza umuhimu wa Mipango ya kujiandaa na kukabiliana na maafa ya Mikoa linakopita Bomba la Mafuta, kuzingatia athari zinazoweza kujitokeza na kuathiri Mradi huo, wakati alipotembelea eneo la kwenye peninsula ya Chongoleani karibu na bandari ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa .
 Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akisisitiza umuhimu wa Mipango ya kujiandaa na kukabiliana na maafa ya Mikoa linakopita Bomba la Mafuta, kuzingatia athari zinazoweza kujitokeza na kuathiri Mradi huo, wakati alipotembelea eneo la kwenye peninsula ya Chongoleani karibu na bandari ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa.
 Kaimu Katibu Tawala, Mkoa wa Tanga, Noel Kazimoto, akimueleza Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe umuhimu wa Mpango wa kujiandaa na kukabiliana na maafa wa Mkoa huo linakopita kuzingatia athari zinazoweza kujitokeza na kuathiri Bomba la Mafuta ,  wakati walipotembelea eneo la kwenye peninsula ya Chongoleani karibu na bandari ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa.
 Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe na  Kaimu Katibu Tawala, Mkoa wa Tanga, Noel Kazimoto, wakisoma Jiwe la uzinduzi wa utekelezaji wa Mradi wa Bomba la mafuta, wakati walipotembelea eneo la kwenye peninsula ya Chongoleani karibu na bandari ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa na kushauri mipango ya menejimenti ya maafa ya mikoa linakopita bomba hilo  izingatia athari zinazoweza kujitokeza na kuathiri mradi huo.
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiangalia sehemu ya peninsula ya Chongoleani karibu na bandari ya Tanga wakati alipotembelea eneo la utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta, ambapo ameshauri mikoa linakopita Bomba hilo kuzingatia Mradi  huo katika mipango ya menejimenti ya maafa kwa athari zinazoweza kujitokeza na kuathiri mradi huo.


MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf  Masauni (kushoto) na Mbunge wa Manonga, Seif Khamis Gulamali Bungeni jijini Dodoma, Januari 28, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Manonga, Seif Khamis Gulamali, Bungeni jijini Dodoma Januari 28, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wananchi watakiwa kufika katika Vituo vya Afya kwa ajili ya uchunguzi na kupatiwa matibabu

$
0
0
Na Rahma Khamis Maelezo  
Wananchi wametakiwa kufika katika Vituo vya Afya kwa ajili ya uchunguzi na kupatiwa matibabu mara watapobaini kuwa na mafua na homa kali ili kujikinga na maradhi ya Corona yaliyojitokeza nchini China hivi karibuni.

 Hayo yameeleza Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt Fadhil Mohamed Abdallah huko Ofisini kwake Wizara ya Afya Mnazimmoja wakati aliopokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maradhi hayo.

Amesema dalili ya maradhi hayo ni kuhisi mafua na homa ambayo baadae huzidi hatimae kupata homa kali, vidonda vya mdomo na kwenye mishipa ya koo pamoja na homa ya mapafu.

Mkurugenzi huyo amewasisitiza wananchi kufuatia taarifa zinazotolewa katika vyombo vya habari kuhusiana na maradhi hayo ili kuepuka uzushi katika jamii na kuishi kwa amani kutokana na hali ya maradhi ilivyo nchini.

Dkt Fadhil amefahamisha kuwa kirusi cha maradhi hayo kipo toka zamani lakini kwa sasa kimezuka kirusi chengine kipya kinachoitwa Novel Corona Virus ambacho kinatokana na jamii hiyo na kinaenea kwa kutumia njia ya hewa.

 Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wameongeza nguvu za ziada katika maeneo ya Uwanja wa Ndege na Bandarini kwa kuwapa mafunzo maafisa wa vitengo hivyo pamoja na kuweka vifaa maalum vya kutumia katika Hospitali ya Mnazi mmoja pindi yakigundulika maradhi hayo ili kuweza kudhibiti yasienee nchini.

“Lakini pia tumeandaa eneo maalum huko Fuoni Kibondeni  kwa ajili kuwaweka wagonjwa pindi tu tukigundua kuwa mgonjwa  amejitokeza na maradhi hayo, na pia tunatoa mafunzo katika  vituo vya afya jinsi ya kuhudumia wagonjwa na kutoa fomu maalum kwa wageni wote wanaotoka nchi ambazo zimegundulika kuwa na maradhi hayo na tutawafatilia kwa muda wa siku 14 ili kupata taarifa zake”, alisema Dkt Fadhil.

Amefahamisha kuwa Serikali imejipanga kwa ajili ya kujikinga na maradhi hayo tayari imeshaunda timu sita ili kufuatilia wagonjwa wanaopata maradhi hayo na kuwapatia mafunzo pamoja na kutoa taarifa mbalimbali kupitia vyombo vya habari kuhusu ugonjwa huo.

Akizungumzia kuhusu maradhi ya Malaria Dkt Fadhil amesema kuwa katika jamii kuna mbu wanaosababisha maradhi hayo  hivyo amewataka wananchi kuchua tahadhari kwa kuweka mazingira safi pamoja kutumia vyandarua vyenye dawa ili kujikinga na maradhi hayo.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dk,Fadhill Mohamed Abdalla akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Tahadhari zilizochukuliwa kujikinga na Maradhi ya Corona yaliozuka katika Nchi ya China hafla iliofanyika Ofisini kwake Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar.

MGALU AWATUMIA SALAMU KALI VISHOKA NA BAADHI YA WATUMISHI REA,TANESCO WATAKAOUZA NGUZO

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE
NAIBU Waziri Wa Nishati ,Subira Mgalu ametoa tahadhali kwa vishoka baadhi ya watumishi REA ,ama shirika la umeme Tanesco kujiepusha na uuzaji wa miundombinu ya umeme na vifaa mbalimbali ikiwemo nguzo .

Ameeleza ,endapo atabainika yeyote kujihusisha na vitendo hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria kwakuwa anarudisha nyuma juhudi za serikali na ni uhujumu uchumi.

Akihitimisha ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa Peri -Urban wilayani Kisarawe, Subira alisema, msimamo wa serikali nguzo haziuzwi ,hata kama mtumishi upo REA ama TANESCO .

Aidha Subira ,alitoa rai kwa wananchi wasithubutu kulipia nguzo au kufanya makubaliano yoyote nje ya utaratibu wa serikali .

Akizungumzia suala la vishoka wanaofoji vitambulisho, alisema serikali pia imeweka msimamo, endapo kuna mazingira hayo wananchi watoe ushirikiano ili kuwabaini wahusika.

Aliomba vyombo vya usalama vya ngazi husika kuliona hilo ni moja ya majukumu yao kubaini vishoka wanaouza miundombinu mbalimbali na vifaa na kubaini mtumishi yeyote atakaehusika.

Pamoja na hayo,Naibu Waziri huyo alitaka maeneo ya taasisi za umma ikiwemo shule na viwanda kupewa kipaombele kufikishiwa umeme na kumtaka mkandarasi aendane na kasi inayoendana na muda aliopangiwa ili jamii iondokane na adha ya kukosa huduma ya nishati ya umeme.

Nae diwani wa kata ya Msimbu ,Mama Lilomo alifafanua, kata yake imeguswa na  umeme eneo la Homboza lakini bado kuna changamoto ya ukosefu wa umeme katika vitongoji saba.

Kwa upande wake ,Mkuu wa shule ya sekondari Christon ,August Minja alieleza kwamba, mradi huo utakapokamilika na kufika shuleni hapo, itakuwa ni chachu ya kuinua taaluma,pia aliipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais John Magufuli kwa kuhakikisha umeme unafika pembezoni na miji na vijijini.

MAKALA: MFAHAMU MSICHANA MDOGO WA KITANZANIA ALIEJIWEKEA MALENGO YA KUPANDA MILIMA MIREFU YOTE ILIOPO KATIKA MABARA SABA DUNIANI

$
0
0
Rawan Dakik akizungumza na wanahabari nje ya jengo la TANAPA.
 Mama mzazi wa Rawan, Hala akiongea na waandishi wa habari.

Na Woinde Shizza, Arusha
MFAHAMU msichana mdogo wa kitanzania aliezaliwa mkoani Arusha alieweza kupanda milima sita mirefu duniani na mwezi march anaenda kutimiza ndoto zake kwa kupanda mlima mkubwa kuliko yote Mlima Everest ni mlima mkubwa kabisa duniani, wenye kimo cha m 8,848 juu ya usawa wa bahari, Ni sehemu ya safu ya milima ya Himalaya Kilele chake kipo katika mpaka wa Nepal na China (Tibet).

Msichana Rawan Dakik ni msichana wa kitanzania mwenye umri wa miaka 18 msichana huyu ni mtoto wa tatu kutoka kwa mama yake aliyejulikana kwa jina la Hala Dakik ,msichana huyu alianza kupanda mlima ndani ya nchin ya Tanzania akiwa anaumri wa miaka 12 baada ya kujiunga na timu ya shule ya upandaji milima ambapo alipata elimu ,ujuzi na taarifa mbalimbali za milima duniani.

Baada ya kupata mafunzo haya msichana huyu alivutiwa sana na mchezo ya kupanda na kujua kuhusu milima hivyo akaamu kuweka rekodi ya kupanda milima yote saba mirefu kutoka katika mabara saba duniani na aliaanza akiwa na umri mdogo sana.

Msichana Rawan  akizungumza na mwandishi wa MICHUZI BLOG  kuwa ni uamuzi wake mwenyewe uliomfanya kuanza michezo hiii yakupanda milima na uhamuzi wake huu ulizingatia kutoharibu masomo yake na ufaulu wake katika masomo.

Amebainisha kuwa ndoto yake imekuwa kweli mpaka sasa ameweza kupanda milima sita katika mabara manne na kupeperusha bendera katika kila kilelel, aliweza kupandisha bendera mbili moja ikiwa ya nchi yake ya Tanzania huku bandera ya pili ikiwqa Amani ya dunia .

Amesema kuwa lengo lake haswa ni kufikisha ujumbe wa kutaka amani duniani, kuhamasisha maendeleo kwa wanawake na vijana wa rika lake na kuwataka wajitahidi kutimiza ndoto zao na kufahamu kuwa ukiwa na nia chochote kinawezekana.

Ametaja baadhi ya milima aliyoipanda kuwa ni pamoja na Kilimanjaro uliopo hapa Nchini Tanzania katika bara la Afrika na una urefu wa mita 5,895 mlima mungine ni Elbras uliopo nchini Urusi barani Ulaya wenye urefu wa mita 5,648, mwingine ni Aconcagua uliopo nchni Argentina barani Amerika ya kusini wenye urefu wamita 6,961 pamoja na Carstenz Pyramid uliopo nchini Indonesia ndani ya bara la Asia wenye urefu wa
mita 4884, pia amepanda mlima uliomrefu zaidi katika bara la Antartica karibu kabisa na nchin ya Chile wenye urefu wa mita 4,892.

Ili aweze kupanda milima hii ametakiwa kufanya mazoezi masaa ishirini kwa wiki na mazoezi haya yatampa uwezo wa kubeba mzigo wake mwenyewe wenye kilo thelathini na tano (35 kg) na kuvuta mwingine wenye vifaa vya kupandia mlima wenye uzito wa kilo 30 kufanya mazoezi ya
kuhimili kupanda mlima katika hali ya hewa ya chini ua kiwango cha baridi cha nyuzi 30c ,na hivi sasa anaendelea na mazoezi hayo ambapo amesema mwezi machi mwaka huu anampango wa kupanda mlima mrefu kuliko yote duniani ujuliokanao kwa jina la Everest”.

Ametaja milima mingine ambayo ameipanda ni pamoja na mlima wenye baridi kali wa Kazbek wenye urefu wa mita 5,o33  ulioko Georgia nchini Urusi kama sehemu ya mazoezi, Aidha ameweza kupanda katika vilelel vya milima miwili iliyopo mkoani Arusha Tanzania na kilele cha
mlima mmoja uliopo nchini Uganda hii yote ni sehemu ya mazoezi ya kupanda mlima Everest.

Rawan (17) kufikia kiwango cha kupanda mlima Vinson Massifna mlima Dinal atakuwa amaevunja rekodi mara baada ya kupanda mlima Everest na ataliwa mwanamke wa kwanza kupanda mlima huo akiwa mdogo, pia ndio mtanzania wa kwanza kupanda mlima huo na kuvunja rekodi ya kupanda
milima yote mirefu iliopo katika mabara saba.

"Nafanya mazoezi ya ndani kwa masaa 20 kwa wiki mazoezi yanayonipa uwezo a kubeba mzigo ene kilio hadi kumi na tano kuvuta mwingine wenye uzioto wa hadi kilo 25 ,mazoezi mengine nayoyafanya ni kupanda mlima katika hali ya baridi inayoweza kufikia chini ya kiango cha nyuzi 50, mazoezi haya yamenilazimu kupanda mlima kilimanjaro uliopo Tanzania wenye mita 5,895, mlima wenye baridi kali wa Kazbek wenye urefu wa mita 5,033 uliopo Georgia nchini Urusi ,mlima Rwanzari wenye mita 5,109 uliopo uganda , Mlima Meru wenye mita 4,562 uliopo Arusha Tanzania pmoja na milima midogo eye mita 3,820 katika kuendelea na mazoezi milima mingine niliopanda ni mlima Ararat wene mita 5,137 uliopo Turkey, Mlima kenya enye mita 4,985 uliopo kenya, mlima Qurnat al sada enye mita 3,088 uliopo Lebanon milima yote hii nimepanda ni kwaajili ya mazoezi yakupanda mlima mrefu kuliko yote duniani "amesema Rawan

Rawan amesema kuwa Mlima Everest ni mlima mkubwa kabisa duniani, wenye kimo cha m 8,848 juu ya usawa wa bahari. Ni sehemu ya safu ya milima ya Himalaya Kilele chake kipo katika mpaka wa Nepal na China (Tibet) historia inaonyesha kuwa Watu wa kwanza wa kufika kwenye kilele
walikuwa Edmund Hillary wa New Zealand na sherpa Tenzing Norgay wa
Nepal tarehe 29 Mei 1953 hivyo na yeye anaamini kabisa atafika
kileleni kama hao wa awali walivyofika na kuandika historia ya kwake
na ya nchi yetu kwa ujumla kwani atawekwa kwenye historia za mtanzania
wa kwanza mwanamke na mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kuweza
kupanda mlima huo hadi kileleni amebainisha kuwa ataanza safari yake
mwezi ya kupanda mlima mwezi machi mwaka huu na atatumia muda ya
miezi miwili kupanda mlima huo.

Ombi kwa Watanzania
Amesema safari hiyo ni ngumu ila anaamini ataimaliza vyema huku
akiwaomba watanzania wote bila kujali madhehebu yao kumuombea safari
yake ikamilike na aweze kutimiza ndoto zake za kupanda milima yote
mirefu iliopo katika mabara saba duniani, ambapo hadi sasa ameshapanda
milima sita na anaenda kumalizia mmoja.

MAMA WA RAWAN ALONGA
Hala ni mama mzazi wa Rawan amesema kuwa baada ya kugundua ndoto ya
mtoto wao waliamua kumuunga mkono kwa kumpa ushirikiano wa kila hatua ambayo alikuwa akiifanya ili tu mtoto wake atimize ndoto yake.

Amebainisha kuwa wazazi wengi wamekuwa hawataki kufata ndogo za watoto wao waliojiwekea badala yake wamekuwa wakifata vitu ambavyo wao ndio wanavipenda kitu ambacho kinawarudisha nyuma watoto wengi kwani baadhi yao unakuta ana ndoto zake na hafurahi kupangiwa na mzazi wake kitu cha kufanya.

Amesema kuwa mtoto wake alikuwa na malengo (ndoto) za kupanda milima
yote mikubwa duniani na hadi kufikia sasa ameshapanda milima mitano
mikubwa na aliaanza kupanda milima hiyo akiwa na umri wa miaka 12 na
sasa hivi anajiandaa kwenda kupanda mlima mrefu kuliko yote duniani
akiwa kama mtanzania wa kwanza kupanda mlima huo na mwanamke mdogo kuliko wote aliyewahi kupanda mlima huo .

“Tuliona mtoto wetu anandoto na tukaamua kumsapoti na ndio maana hadi
sasa amepanda milima mitano mikubwa Afrika lengo lake ni kupanda
milima yote mikubwa Afrika na sisi lazima tuakikishe amefanikisha
ndoto zake wazazi wenzangu napenda kuwaambia mtoto akiwa na ndoto yake tusiipuuze bali tumsaidie kufikia anapotaka “amesema Hala


Kamishna wa Hifadhi za Tanapa Dk Allan Kijazi anena
Kwa upande wake Kamishna wa Hifadhi za Tanapa Dk Allan Kijazi (TANAPA) Allan Kijazi amempongeza msichana huyo kwa kuweza kupanda milima hiyo ikiwemo Kilimanjaro akiwa na umri mdogo na kumuandi kuwa wao kama TANAPA watampa ushirikiano wa kutosha katika swala zima la
kutimiza ndoto yake.

Amebainisha kuwa pindi msichana huyo akirudi kutoka katika safari yake
ya kupanda mlima huo atakuwa balozi mzuri wa kuutangaza mlima
Kilimanjaro kwa watu mbalimbali, huku akibainisha kuwa msichana huyo
akirudi wataanzisha program ambayo ataifanya kwa kupita mashuleni
kuwahamasisha vijana wenzake kupanda mlima Kilimanjaro.

WANACHUO KIKUU HURIA MKOANI SINGIDA WAJIPANGA KWA UFUGAJI NYUKI

$
0
0




Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Huria Tawi la Singida, imepokea msaada wa mizinga kumi ya kisasa ya kufugia nyuki, yenye thamani ya shilingi milioni mbili, ikiwa ni mwendelezo wa mkakati uliopo wa wanachuo hao nchini kote kuhakikisha wanaanza kubuni na kuibua miradi yenye tija, itakayosaidia kuinua kipato cha mtu mmoja-mmoja na taifa kuelekea uchumi wa kati.


Akizungumza kabla ya kupokea mizinga hiyo, kutoka Taasisi ya ‘Youth Enterpreneurs and Consultants Cooperative Society (Syeccos), kupitia kijiji cha Nyuki Kisaki, Waziri wa Mipango na Fedha wa Tawi la chuo hicho mkoani hapa, Frederick  Ndahani, alisema mradi huo unakwenda kuinua kipato cha wanachuo katika kuwawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo upatikanaji wa ada.


Ndahani ambaye pia ni Kaimu Afisa Vijana wa Mkoa, alisema kwa sasa serikali tayari imewakabidhi eneo la Mwankonko lenye ekari zipatazo 1663, ambalo anaamini kila mwanachuo atatumia fursa hiyo kuwekeza kwenye mradi wowote wa kiuchumi atakaoubuni, lakini pia hata mizinga hiyo waliyopokea kama msaada wanatarajia kuipeleka kwenye eneo hilo.


“Niwasihi wanachuo wenzangu na serikali za wanafunzi kwenye vyuo vingine nchini badala ya kukaa na kufikiria kuanzisha migomo sasa tuanze kubuni namna ya kuanzisha miradi yenye tija kwa manufaa yetu na taifa kwa ujumla, ni fursa kwa mwanachuo yeyote mwenye mzinga wake alete kwenye eneo letu,” alisema Ndahani.


Alisema mbali ya mkakati huo wa kufuga nyuki, pia serikali ya wanafunzi hao kwa kushirikiana na Kampasi ya Makao Makuu ya chuo hicho wanakusudia kuwa na kiwanda cha kuchakata asali ndani ya mda mfupi ujao, azma hasa ni kuwafanya kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa asali nchini.


Kwa upande wake, Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Tawi hilo, Nassoro Matulanga, alisema kwa sasa kama sehemu ya jumuiya ya chuo hicho wapo katika kipindi cha kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Chuo Kikuu Huria, ikiwemo kutekeleza miradi mbalimbali kama sehemu ya mageuzi ya kiuchumi.


“ Tukio la leo ni tukio kubwa linaloingia kwenye historia ya chuo, msaada huu tutautumia kikamililifu kwa tija na manufaa ya wanachuo… kwa kuzingatia kwa sasa tumekusudia kuwa na miradi mingi itakayoinua uchumi kama sehemu ya kuchangia juhudi ya nchi katika kuelekea uchumi wa kati,” alisema Matulanga.


Naye, Rais wa Umoja wa Wafugaji Nyuki nchini, Philemon Kiemi, aliwataka wanachuo hao kuwa chachu ya mabadiliko ya kifikra katika muktadha chanya wa maendeleo endelevu ya kiuchumi kupitia elimu na maarifa wanayoyapata.


“Andikeni papers (maandiko ya miradi) mbalimbali za namna ya kutafuta changamoto na fursa zilizopo kwenye sekta ya nyuki nchini, sisi wasomi tunafahamu eneo hili kuna resources za aina nyingi, una ardhi unataka hela njoo tukuonyeshe, una mizinga unataka hela njoo tukuonyeshe…usikae bure  fanya kitu,” alisema Kiemi, na kuongeza:


“Tunaamini elimu hii ya ufugaji itasaidia watanzania wengi kupitia chuo hiki, mizinga hii tunayowakabidhi ni ishara ya mwanzo wa ushirikiano, msisite kutuita au kutushirikisha kwa lolote, mkituhitaji wakati mnataka kutoa elimu tutakuja kushirikiana, na wakati mnataka kuipeleka shamba tutakuwepo kushauriana,” alisema.
 Rais wa Umoja wa Wafugaji Nyuki Nchini, Philemon Kiemi, akizungumza na viongozi wa serikali ya wanafunzi na Jumuiya ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania  tawi la Singida jana.
 Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria, tawi la Singida, Nassoro Matulanga, akizungumza muda mfupi kabla ya hafla ya kupokea msaada wa mizinga 10 ya kisasa ya kufugia nyuki kwa niaba ya serikali ya wanafunzi wa chuo hicho.
 Waziri wa Mipango na Fedha, Frederick  Ndahani akizungumza kwenye tukio hilo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Kituo, Chuo Kikuu Huria, Tawi la Singida, Bernard Komba, akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Mwonekano wa mizinga ya kisasa iliyotolewa na Syeccos kama msaada kwa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria, tawi la Singida.
 Washiriki wakifuatilia tukio hilo.
 Hafla ikiendelea.
Baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi wakifuatilia hotuba mbalimbali.
 

DC Nyasa agawa miche bora ya kahawa kwa wakulima

$
0
0
 Ofisa kilimo wa kata ya Kingerikiti Wilayani hapa Richard Katale (Mwenye kanzu) ambaye pia ni mkaguzi wa zao la kahawa wilayani Nyasa, akitoa mafunzo kwa wakulima wa zao la kahawa juu ya upandaji miche mipya, ya kahawa aina ya Compact kabla ya kuwagawia wakulima waweze kupanda miche hiyo hivi karibuni katika Kata ya Kingerikiti Wilayani Nyasa.
Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na ushirika Menance Ndomba, (mwenye shati jeupe) aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela chilumba akipanda mti kuashiria uzinduzi kulia kwake ni mmiliki wa shamba Bi Desderia Komba ambaye amehamasika kulima zao hilo kutokana na maboresho ya serilali ya awamu ya tano.

Na Netho Sichali
Wakulima wa zao la kahawa Wilayani Nyasa, kwa kushirikiana na Vyama vya Msingi vya mazao na watu binafsi, wamezalisha miche ya kahawa 262,500 kwa msimu wa kilimo 2019/2020 ili kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa na kukuza uchumi  wa wananchi.
Hayo yamesemwa na wakulima wa zao la kahawa katika Risala yao, kwa mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela O.Chilumba, wakati akizindua ugawaji wa miche mipya  ya kahawa aina ya “Compact” Uzinduzi uliofanyika hivi karibuni, katika Kijiji cha Kingerikiti Kata ya Kingerikiti Wilayani hapa.
Wakulima hao wamefafanua kuwa, wamelazimika kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa ikiwa ni pamoja, na utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Cassim Majaliwa aliyezitaka kili Halmashauri Nchini kuzalisha miche ya kahawa zaidi ya laki mbili.

Waliongeza kuwa Vyama saba vya Ushirika wa mazao vimezalisha miche hiyo na tayari kwa kugawa kwa wananchi kwa mchanganganuo ufuatao Nambawala AMCOS (10250), Kingerikiti AMCOS miche( 37,705), Tingi AMCOS (4,300) LIPO AMCOS MICHE (40,000), Mapendo AMCOS Miche (36,000) na Luhangarasi AMCOS 9890.
Pia wakulima hao walikipongeza kituo cha utafiti cha Ugano (TACRI) kwa kuwagawia bure miche kahawa 18,200 aina ya  compact, ambayo wameigawa kwa wakulima  ambao wanauhitaji wa miche hiyo.

Akitoa maelekezo ya upandaji wa miche hiyo kwa wakulima wa zao la kahawa, Ofisa kilimo wa Kata ya Kingerikiti ambaye pia ni Mkaguzi wa zao la Kahawa Bw.Richard Katale, aliwataka wakulima, kulihudumia vizuri, kwa kupanda kwa nafasi ya Meta mbili na kwa Hekari moja watapanda meche mia sita.
Aliongeza kuwa sifa za mche wa compact unazaa mapema na unavumilia ukame. Alikawataka wananchi  kupanda kwa maelekezo aliyoyatoa, ili kufikia uzalishaji wenye tija kwa kuwa Serikali imedhamiria kuboresha maisha ya wakulima wa zao la Kahawa.

Aidha wakulima hao, waliipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya maboresho mbalimbali ya zao la kahawa, na kuwaletea mnada wa kahawa katika Wilaya ya Mbinga na kuwapunguzia usumbufu kwa kuwa awali walikuwa wakienda moshi kufanyia mnada.

“kwa kweli awamu hii tunaona jinsi gani Serikali inatujali wakulima, kwa kuwa tunapewa mafunzo ya kulima kahawa, lakini pia kitendo cha kutupa miche ya ya kahawa bure , Serikali imetusaidia sana. Nimejaribu kupanda na nimeona ni mbegu nzuri inayotoa mavuno mengi kwa muda mfupi ukilinganisha na kahawa tuliyozoea kupanda awali”. Alisema Bonus mapunda mkulima wa zao la kahawa kutoka katika kijijii cha kingerikiti.

Akizungumza na wakulima wa zao la Kahawa Wilayani hapa, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Bw.Menance Ndomba aliyemwakilisha mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi,Isabela Chilumba,Aliwapongeza wakulima wa Zao la kahawa Wilayani Nyasa, kwa juhudi wanazozifanya za kulima na kutunza zao hilo na kuinua mapato ya Halmashauri na kuwa na kipato bora cha Familia na kuchangia maendeleo mbalimbali katika maeneo yao.

Aidha aliwataka kuendelea kuongeza uzalishaji wa zao la Kahawa kwa kuwa , Wilaya ya Nyasa ina Fursa ya  mashamba makubwa, kwa mujibu wa Utafiti uliofanyika hivi karibuni na “CAFE Afrika” katika Wilaya ya Mbinga na Nyasa Wilaya ya Nyasa ina fursa kubwa ya kupanua mashamba ya kahawa ukilinganisha na  Wilaya ya Mbinga.

“nachukua fursa hii kuwapongeza sana wakulima wa zao la kahawa Wilayani Nyasa, kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kujituma kulima na kuzalisha zao hili la kahawa ambalo linatupa faida kubwa sana katika Halmashauri yetu kama vile ,mapato ya ndani na mnachangia maendeleo mbalimbali katika maeneo yenu.Serikali ipo pamoja nanyi na itatatua changamoto mbalimbali mtakazokutana nazo katika shughuli zenu na kuhakikisha Miundombinu inajengwa. Alisema ndomba.
Wilaya ya Nyasa ipo katika Mkakati wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara ya Kahawa,kakao, na korosho ili kukuza uchumi wa kipato cha mwananchi mmoja mmoja na Wilaya kwa ujumla.

SPIKA WA BUNGE KUZINDUA PROGRAMU YA KULIOMBEA TAIFA

$
0
0
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Programu ya Kitaifa ya Kuliombea Taifa inayoratibiwa na Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania.

Programu hiyo ya kitaifa ambayo itaratibiwa nchini kote kupitia kusanyiko kubwa la ibada itakuwa inalenga kuombea Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli na wasaidizi wake ili Mungu azidi kuwapa hekima, maarifa na bidii ya kuendelea kuwahudumia Watanzania.

Hayo yalisemwa jana na Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania na Mratibu wa Programu hiyo kitaifa, Nabii Joshua Aram Mwantyala wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.

Alisema kuwa, uzinduzi huo utafanyika Februari 15 na 16, mwaka huu katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.

"Tunatarajia hii itakuwa ni programu ya kipekee sana, maana Mungu anaenda kuonekana katika Taifa letu, tumekuwa katika maombi mfululizo kwa ajili ya kuombea uzinduzi huo ambao itakuwa ni ibada ya miujiza na uponyaji.

"Hivyo, nichukue nafasi hii kuwakaribisha Watanzania wote katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Februari 15 hadi 16, mwaka huu, tuamke Watanzania, tuliombee Taifa,"alifafanua Nabii Joshua.

Alisema, baada ya uzinduzi huo programu hiyo itazunguka mikoa yote nchini kwa ajili ya kufanya maombi, hatua ambayo itasaidia miradi na mipango inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano ikafanikiwe kwa haraka, kwa kuwa wataikabidhi mbele za Mungu.

Nabii Joshua alifafanua kuwa, wito huo wa kuliombea Taifa ni kwa Watanzania wote, hivyo bila kujali imani, kabila au rangi kila mmoja atashiriki kwa ajili ya kumlilia Mungu ili azidi kulitendea mema Taifa letu.

"Kwa sababu tulimlilia akatupatia kiongozi na Rais Dkt.Magufuli ambaye anatutetea wanyonge na kuzipigania rasilimali zetu ili ziweze kutumika katika uwiano sahihi kwa maslahi ya Watanzania wote, vivyo hivyo tunapaswa kumuombea Rais wetu ili kwa kushirikiana na wasaidizi wake wazidi kuliletea Taifa letu heshima kubwa, hakika Mungu ameweka kusudi ndani yao kwa maslahi ya Taifa, tunaamini yote yanawezekana,"alifafanua Nabii Joshua.

Kiongozi huyo alisema, katika maombi hayo watamuomba Mungu azidi kuibariki miradi yote iliyopo nchini ikiwemo ya kimkakati kuanzia barabara, reli, viwanja vya ndege, elimu, afya, nishati, mipango ya kudumisha amani na upendo, uchaguzi ujao na mingine mingi.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha afungua Mafunzo ya Wakurugenzi na Wenyeviti wa Bodi wa Taasisi, Wakala na Mashirika ya Umma

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akizungumza katika mafunzo ya Wakurungezi na Wenyeviti wa Bodi mbalimbali za Taasisi, Wakala na Mashirika ya Umma alipowasili kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, mafunzo hayo yanalenga kuimarisha utendaji kazi wa bodi hizo.
  Msajili wa Hazina, Athumani Mbutuka akizungumza katika mafunzo ya Wakurungezi na Wenyeviti wa Bodi mbalimbali za Taasisi, Wakala na Mashirika ya Umma yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, mafunzo hayo yanalenga kuimarisha utendaji kazi wa bodi hizo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James, akiwa katika  picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), mara baada ya kufungua mafunzo ya Wakurungezi na Wenyeviti wa Bodi mbalimbali za Taasisi, Wakala na Mashirika ya Umma yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, mafunzo hayo yanalenga kuimarisha utendaji kazi wa bodi hizo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James, akiwa katika  picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) mara baada ya kufungua mafunzo ya Wakurungezi na Wenyeviti wa Bodi mbalimbali za Taasisi, Wakala na Mashirika ya Umma yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, mafunzo hayo yanalenga kuimarisha utendaji kazi wa bodi hizo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James, akiwa katika  picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) mara baada ya kufungua mafunzo ya Wakurungezi na Wenyeviti wa Bodi mbalimbali za Taasisi, Wakala na Mashirika ya Umma yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, mafunzo hayo yanalenga kuimarisha utendaji kazi wa bodi hizo.

WAFANYABIASHARA WANNE WA MAZAO YA MISITU WAFIKISHWA KORTI WAKIKABILIWA NA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
Na Karama Kenyunko globu ya jamii.

WAFANYABIASHARA wanne wa mazao ya Misitu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi ikiwemo kukwepa kodi na kutakatisha fedha wa zaidi ya Sh. Mil 155.

Wafanyabiashara hao ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Allvay Product Farm, Ebenezer Mmanyi (38),Jumanne Brashi (37), Manish Khattar (38) na Rajesh Velram (52) ambapo wamesomewa makosa yao mbele ya Mahakimu watatu tofauti na kurudishwa rumande kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Washtakiwa wote wanakabiliwa na shtaka la kuongoza genge la uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za uongo, kukwepa kodi na kutakatisha fedha.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mwandamizi Ladislaus Komanya amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Vicky Mwaikambo  kuwa, kati ya Januari Mosi, na Oktoba 31,2015 katika maeneo tofauti tofauti ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, mshtakiwa Ebenezer akiwa na wenzake ambao hawapo mahakamani walitengeneza kundi la uhalifu kwa lengo la kupanga mipango ya uhalifu.

Pia anadaiwa kusafirishia mazao ya misitu yenye thamani ya sh. 6,526000 bila ya kupata kibali cha kusafirishia mazao hayo kutoka kwa Afisa aliyeidhinishwa huku pia anadaiwa kughushi leseni na cheti na kutengeneza nyaraka ya uongo kujaribu kuonesha kwamba nyaraka hizo ni halali na zimetolewa na Afisa aliyeidhinshwa na Zambia huku akijua kuwa siyo kweli.

Mshtakiwa Ebenezer  anadaiwa kughushi leseni ya uzalishaji ( Production license), leseni ya ushirika(Convience license) na pia alitoa nyaraka mbali mbali ikiwemo nyaraka ya uongo ya idhini ya usafirishaji (export permit).


Kosa jingine ni utakatishaji fedha ambapo anadaiwa amelitenda Oktoba 31, 2015 akidaiwa kutakatisha Sh.Mil 6, 526,000 wakati akijua fedha hizo ni zao la makosa tangulizi.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Mfanyabiashara Brashi amesomewa Mashtaka  yake na Wakili wa Serikali, Tuli Helela na kudaiwa kuwa kati ya Januari mosi, 2015 na Oktoba 31, 2015 katika sehemu mbalimbali, mshitakiwa huyo akiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani hapo waliongoza genge la uharifu.

Mstakiwa Brashi anadaiwa kusafirisha mazao ya misitu ambayo ni kontena tano za magogo yenye thamani ya Sh. Milioni 32.6 bila kuwa na kibali kutoka kwa mamlaka husika. Pia anashtakiwa kwaa shtaka la kukwepa kodi. Helela alidai kuwa tarehe hiyo hiyo katika Jiji na mkoa wa Dar es Salaam mshitakiwa huyo aliwasilisha nyaraka za uongo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa nia ya kukwepa kodi kiasi cha Sh. Milioni 32.6.

Katika shitaka la mwisho la utakatishaji fedha,  inadaiwa kati ya Januari, 2015 na Oktoba 31, 2015 katika jiji na mkoa wa Dar es Salaam mshitakiwa huyo alijipatia kiasi cha Sh. 32,630,000 wakati akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa tangulizi la ukwepaji kodi.

Baada ya kusoma hati ya mashitaka, Helela alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado  haujakamilika hivyo aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Hata hivyo Hakimu Chaungu alisema kutokana na kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi,  mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpatia mshitakiwa huyo dhamana hivyo Brashi amerudishwa rumande.

Wakati huo huo, washitakiwa Khattar na Velram wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde na Silivia Mitanto mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega ambapo wanakabiliwa na makosa saba ikiwemo kughushi kusafirisha mazao ya Misituz kushindwa kulipa kodi na utakatishaji fedha.

Katika kosa la utakatishaji fedha, inadaiwa walilitenda kati ya Januari 1 na Oktoba 2015 kati ya Tanzania na Zambia kwa pamoja walitakatisha Sh.Milioni 117.48 ikiwa ni mali ya Serikali ya Tanzania huku wakijua zimepatika kwa makosa tangulizi.

Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na washitakiwa hawakutakiwa kujibu kitu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za Uhujumu Uchumi, hivyo wamerudishwa rumande.

Kesi zote zimeahirishwa hadi Februari 12, 202
0 zitakapokuja kwa ajili ya kutajwa





MABAKI YA MWILI YA ALIYEKUWA MCHEZA KIKAPU MAARUFU NCHINI MAREKANI KOBE BRAYANT NA MWANAE,WENGINE SABA YAPATIKANA

$
0
0
Na Al-Hassan Muhidin,Globu ya Jamii

Mabaki ya  ya miili yote tisa imepatikana katika eneo la tukio ambalo helikopta iliyokuwa imembeba gwiji wa mpira  wa kikapu Kobe Brayant,mwanae Gianna na wengine saba ilianguka.

Mamlaka katika jiji la Los Angeles nchini Marekani zimesema mabaki ya mwili wa rubani pamoja na mabaki ya miili ya abiria wote nane imepatikana baada ya operesheni  ya kuisaka  miili hiyo kukamilika, hii ikiwa ni baada ya kuwa na Ugumu wa kuifikia eneo ambalo helikopta hiyo iliangukia kutokana na ripoti kudai kuwa chombo hicho kiliangukia eneo la ardhi lenye mteremko mrefu sana.

Hapo awali siku ya jumanne, Alex Villanueva, mmoja wa maafisa wa operesheni hiyo alisema kuwa zoezi hilo lingechukua siku kadhaa kutokana na changamoto ya eneo ambalo helikopta  hio iliangukia, na leo afisa huyo amethibitisha kwamba tayari miili yote imepatikana.

Miili mitatu ilipatikana siku ya jumatatu na baada ya msako zaidi kufanyika mingine sita ikapatikana ambapo mwili wa Brayant ulitambulika kwa njia ya alama za vidole.

Wengine waliofariki katika ajali hiyo ni John Altobelli Kocha wa timu ya Baseball ya Orange Coast College, mke wake pamoja na mwanao wa kike Alyssa ambaye alikuwa akicheza timu moja ya mpira wa kikapu na mtoto wa Kobe,Gianna.
 

fifa yaipiga marufuku klabu ya Al Masry kutosajili madirisha matatu yajayo

$
0
0
Na Yassir Simba,  Globu ya Jamii

Shirikisho la kabumbu duniani FIFA, limeipiga marufuku klabu ya Al Masry yenye maskani yake Port Said nchini Misri kutosajili katika madirisha matatu yajayo kwa kosa la kumsajili Cheick Moukoroo raia wa Ivory Coast kinyume na sheria za usajili.

Taarifa kutoka shirikisho la kandanda Misri Egyptian Football Association (EFA) limethibitisha kupokea barua hiyo ya FIFA siku ya jumanne kusema " Masry imepigwa marufuku kuingia sokoni katika  madirisha matatu yajayo kutosajili mchezaji yeye." Aidha shirikisho hilo ( FIFA) limesema kuwa klabu hiyo ya Al Masry inayo nafasi ya kukata ruhusa kuhusu adhabu hiyo.

Moukoroo mwenye umri wa miaka 28, tayari alikuwa akitumikia adhabu yake ya kutojihusisha na kandanda kwa kosa la kukatisha mkataba pasipo kuwa na makubaliano na klabu yake aliyekuwepo Al Hilal Oubeid ya  nchini Sudan katika dirisha kubwa la usajili 2017.
 

SBL yazindua mpango wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kilimo

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto) akibadishana mkataba na Mkuu wa Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture muda mfupi baada ya kusaini mkataba huo utakaiwezesha SBL kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kilimo wa chuo hicho kila mwaka
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto) akifurahia jambo na Mkuu wa Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture muda mfupi kabla ya kusaini utakayoiwezesha SBL kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa klimo wa chuo hicho.
 

Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture watakaonufaika na mpango wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kilimo unaotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeri, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto) na mkuu wa chuo hicho Sinani Simba muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa ufadhili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kulia) akimpongeza mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture ambaye ni mnufaika wa programu ya ufadhili wa elimu kwa wanafunzi wa kilimo Emmanuel Ntandu muda mfupi
baada ya SBL kusaini mkata wa ufadhili na chuo hicho mjini Bagamoyo jana. 

****************************** 

Bagamoyo, January 29, 2020: Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), leo imezindua mpango wa ufadhili wa masomo utakaowanufaisha wanafunzi 30 kutoka katika jamii za wakulima hapa nchini kupata elimu ya ngazi ya chuo katika vyuo vya ndani vinavyofundisha masomo ya kilimo. 

Ukijulikana kama Kilimo-Viwanda scholarship program, mpango huu unalenga kuongeza wataalamu wa kilimo watakaowasaidia wakulima nchini kuongeza uzalishaji, alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti wakati wa uzinduzi wa program hiyo katika chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani. 

“Ni muhimu kwetu sisi kama SBL kuiunga mkono Serikali katika kuwajengea uwezo wakulimawetu kupitia kuwaongezea wataalamu wa kilimo watakaosadia kuwashauri na hivyo kuongezatija katika kilimo,” alisema Ocitti. 

Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture ni moja kati ya vyuo vitatu ambavyo kampuni ya SBL inashirikiana navyo katika kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kilimo hapa nchini. 

Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa, programu hiyo inawalenga siyo tu wanafunzi wanaotokakatika familia zenye vipato duni lakini pia wanafunzi wanaotoka katika jamii za wakulima katikasehemu mbali mbali hapa nchini. Kila chuo kitapata nafasi ya kutoa wanafunzi 10 kila mwaka na
watakaolipiwa ada na SBL mpaka watakapomaliza masomo yao. 

Kwa mujibu wa Ocitti, programu hiyo ni sehemu ya mkakati wa SBL wa kuongeza kiasi cha nafaka ambacho kampuni hiyo inanunua kwa ajili ya uzalishaji wa bia ambazo ni pamoja na mahindi, shayiri na mtama. Alisema, mwaka jana SBL ilinunua zaidi ya tani za ujazo 17,000 zanafaka kutoka kwa wakulima wa ndani sawa na asilimia 70 ya mahitaji yake yote ya malighafi kwa mwaka. 

“Kampuni ya SBL inalengo la kuongeza kiasi cha malighafi inayonunua kutoka kwa wakulima wa ndani hadi asilimia 85 kufikia mwaka 2020 na ndiyo maana tumeona umuhimu wa kusaidia kusomesha wataalamu wa kilimo ili wakafanye kazi ya kuboresha kilimo chetu. Kwa sasa
kampuni inanunua malighafi kutoka kwenye mtandao wenye wakulima 400 hapa nchini,”.alisema. 

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture Sinani Simba aliishukuru kampuni ya SBL kwa kuja na wazo la kutoa ufadhili wa masomo ya kilimo na kuongeza kuwa ili kilimo kiwe cha tija wataalamu wengi wanahitajika. 

“Tunayo Furaha kwa kuwa ufadhili huu unawalenga wanafunzi wanaotokea katika familia zenyevipato duni ambao kama siyo msaada wa SBL, wasingeweza kupata fursa ya kuendelea namasomo,” alisema

Pizza Hut na KFC Yafungua mgahawa wa 14 nchini

$
0
0
Pizza Hut Tanzania, imemaliza mwaka 2019 kwa kishindo,kwa kufungua mgahawa wa 8 nchini uliopo katika jengo la Mikocheni Plaza, ambao ulifunguliwa rasmi katika mkesha wa mwaka mpya ikiwa ni wa pili kufunguliwa katika mwezi huo ambapo pia imefungua mgawaha mpya wenye viwago vya kimataifa katika uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere International Airport (JNIA), Desemba 16, 2019.

Mtandao wa migahawa mingine ya Pizza Hut ipo katika maeneo ya Mlimani City, Oysterbay Mall, Mkuki House, Shoppers Plaza, Peugot House na  mjini Arusha katika eneo la maduka ya TFA .

Kampuni ya Dough Works Ltd, ambayo  inamiliki mtandao wa migahawa hiyo inafurahi kufungua mgahawa wa 8 nchini Tanzania na pia inajivunia kupitia uwekezaji huo kuweza kuzalisha ajira zaidi ya 400 “Tunayo furaha kuona biashara yetu inazidi kukua na kuwafikia wananchi wengi na bidhaa zetu za Pizza, zenye viwango vya kimataifa kuzidi kufurahiwa na wateja wetu”. alisema Vikram Desai, Mkurugenzi Mkuu katika hafla ya uzinduzi wa mgahawa mpya wa Pizza Hut wa Mikocheni Plaza iliohudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Mbali na kusherekea kufungua migahawa mipya ya Pizza Hut, Kampuni ya Dough Works Ltd, kwa sasa inaendesha  mtandao wa migahawa 4 ya KFC kuanzia Oktoba 3,mwaka jana.Katika kipindi cha miezi 3 mtandao wa migahawa ya KFC umezidi kukua na kuwa na migahawa 6 baada ya kufunguliwa migahawa mipya miwili mwezi Desemba mwaka jana.Kwa sasa migahawa ya KFC iko katika maeneo ya Kariakoo,Jengo la Diamond Plaza,Mlimani City,Uwanja wa ndege mpya wa JNIA na Mikocheni Plaza, Kampuni inao mpango wa kupanua huduma zake Zaidi kufikia maeneo mengine il ziwafikia wananchi wengi kwa karibu.

Mtandao wa migahawa ipatayo 14 ya KFC na Pizza Hut, inahudumia zaidi ya watu 1,000 ambao hufika kupata chakula pia inatoa huduma za kusambaza chakula chake maarufu cha Pizza na kuku maofisini mpaka majumbani na kampuni imejipanga kupanua huduma zake katika mikoa mbalimbali ikiwemo katika  mikoa ya Dodoma, Arusha na Mwanza. 

Kampuni pia inayo sera ya kusaidia huduma za kijamii kupitia sera yake ya kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii ambapo mwaka huu imepanga kutekeleza miradi mbalimbali ya kusaidia jamii nchini.

Mkurugenzi wa Dough Works Ltd,Vikram Desai alisema “Tunayo furaha kubwa kuona mtandao wetu  umefungua migahawa 4 katika kipindi kifupi na kuwawezesha wateja wetu kupata huduma zetu kwa urahisi,tutaendelea kupanua huduma zetu katika mikoa mingine na matarajio yetu hadi kufikia mwisho wa mwaka huu tuwe tumefungua mtandao wa migahawa yetu katika miji ya Dodoma na Mwanza ambayo itawezesha watanzania wapatao 250 kupata ajira”,alisema.

Kufunguliwa kwa migahawa ya kisasa ya Pizza Hut&KFC katika eneo moja katika jengo la Mikocheni Plaza, kunatoa fursa kwa wateja kupata huduma bora za chakula hususani Pizza na nyama ya kuku zinazotolewa na migahawa hiyo,inao ukubwa wa eneo la kutosha kuhudumia wateja 90 kwa wakati mmoja,menu za chakula za kidigitali,sehemu nzuri na salama za watoto kuchezea, na mazingira rafiki ya kukutana kwa chakula cha kifamilia na mijumuiko ya sherehe ndogondogo.

Pia migahawa hiyo inauza vyakula mbalimbali vya kuku waliotengenezwa kwa viwango vya kimataifa kwa gharama nafuu ambayo wananchi wengi wanaweza kumudu kuanzia  kati ya shilingi 7500/ -shilingi 10,000 kiwemo vinywaji vya soda.
 Meneja Mkuu wa Migahawa ya kuuza Pizza Hut Afrika ya KFC,  Ewan Davenport (katikati)  akikata utepe  wakati wa uzinduzi wa mgahawa wa kuuza Pizza  Hut ulioipo katika jengo la Mikocheni Plazza jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Dough Works LimIted ,Vikram Desai ( kulia)  na Meneja  wa Mgahawa wa Pizza Hut  Mikocheni Emmanuel Sizya.
 Meneja Mkuu wa Migahawa ya kuuza Pizza Hut Afrika ya KFC,  Ewan Davenport (katikati)  akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Dough Works Limeted ,Vikram Desai ( Kushoto) na Meneja  wa Mgahawa wa Pizza Hut  Mikocheni Emmanuel Sizya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dough Works Limited ,Vikram Desai (kulia) akiongea  kwa wandishi wa Habari hawapo pichani wakati wa hafla ya uzinduzi wa  Mgahawa w Pizza Hut  na KFC uliopo katika jengo la Mikocheni  Plaza jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kulia ni   Meneja Mkuu wa Migahawa ya  Pizza Hut Afrika , Ewan Davenport

MKURUGENZI KAMPUNI YA JALUMA NA WENZAKE NANE WAFIKISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA MASHTAKA 28 IKIWEMO YA KUKWEPA KODI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

MKURUGENZI,  wa Kampuni ya Jaluma General Supplies Limited,  Lucas Mallya (42) na wenzake nane wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka 28 ikiwemo ya kukwepa kodi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 31.57.

Mbali na Mallya washitakiwa wengine ni Emmanuel Peter  (25), Mkurugenzi wa Happy Imports Assosiates, Happy Mwamugunda, Prochesi Shayo, Prokolini  Shayo (49), Godfrey Urio, Nyasulu Nkyapi, Tunsubilege Mateni na Nelson Kahangwa

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa leo Januari 28, 2020 na  wakili wa Serikali,  Faraja Nguka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, mfawidhi, Godfrey Isaya, imedaiwa  kati ya Januari Mosi, 2015 na Januari 7, 2020 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam washtakiwa walitenda makosa ya kuongoza genge la uhalifu.

Imedaiwa kuwa, Juni 3 mwaka jana, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Mallya akiwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jeluma General Supplies Limited, alitengeneza nyaraka za kodi za kielektroniki ikionesha imetengenezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) huku akijua kuwa siyo kweli.

Pia Juni 3,2019, Mallya aliwasilisha hati ya kughushi kuonesha kuwa stempu za ushuru za  kielektroniki  ni halisi wakati wakijua si kweli.

Kayika shtaka jingine imedaiwa Januari 7, mwaka huu  huko Chang'ombe wilayani Temeke,  Mallya alipatikana na rola 93 za stempu za ushuru za kielektroniki zenye thamani ya Sh 80,516,000 zilizochapishwa bila mamlaka ya Kamishna wa kodi.

Aidha imedaiwa Januari Mosi 2016 na Desemba Mosi 2019, kwa makusudi mshitakiwa huyo alitengeneza stempu za ushuru za kughushi na kuisababishia serikali hasara ya Sh 15,241,075,169 huku ikidaiwa kuwa kati ya Januari Mosi 2016 na Desemba 31, mwaka jana , Mallya alitengeneza stempu za kodi rola 93 na kukwepa kodi ya  Sh 15,241,075,169.

Pia inadaiwa Mallya alijipatia  Sh 15,241,075,169 huku akijua kuwa fedha hizo ni mazalia ya makosa ya kukwepa kodi.

Pia wakili wa Serikali, Zacharia Ndaskoi, alidai Januari 3, mwaka huu maeneo ya Mbezi Makabe, Peter alikutwa ha rola nne za stempu za ushuru zenye thamani ya Sh 1,104,000 zilizochapishwa bila kibali cha Kamishna wa kodi huku mshtakiwa Mwamugunda akidaiwa Januari 3, mwaka huu akiwa Mkurugenzi wa kampuni  ya Happy Imports Associates bila kusajiliwa na Kamishna, aliingiza katoni 413 za bidhaa inayoitwa Drostay Hof Wine  zenye thamani ya Sh 24,780,000.

Mwamugunda anadaiwa pia kukwepa kodi ya Sh 9,584,401,393  baada ya kuingiza katoni hizo za bidhaa za vilevi na kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha baada ya kushindwa kulipa kodi pamoja na kutakatisha fedha hizo.

Aidha, mshtakiwa Proches na Prokolini wanadaiwa Desemba 19, mwaka jana hukoTabata, walisambaza bidhaa zilizowekwa  stempu za kughushi ambazo ni katoni 749 za Robertson Wine 75CL zenye thamani ya Sh 98,670,000, Drostdy Hof 37.5CL katoni 594 zenye thamani ya Sh 12,002,000, Four Cousins 75 CL katoni 14 zenye thamani ya 16,240,000 na Amarula 75 CL katoni 58 zenye thamani ya Sh 12,120,000 zote zikiwa na thamani ya 139,032,000 bila kufuata kanuni za uwekaji stempu.

Pia washitakiwa hao wanadaiwa kushindwa kulipa kodi ya Sh 38,827,267, na ya Sh 2,359,342,542.07 pamoja na kuisababishia serikali hasara ya fedha hizo kwa kusambaza bidhaa zilizowekwa stempu za kughushi.

Mshtakiwa Urio anadaiwa kuwa akiwa Mkurugenzi wa Kampuni ya GMU  Group  Limited kati ya Januari Mosi 2015 na Desemba 31,2018 kwa nia ya kukwepa kodi aliwasilisha taarifa za uongo TRA na kukwepa kulipa kodi ya Sh 4,265,882,773 na kwamba aliisababishia serikali hasara hiyo na kutakatisha fedha hizo ikiwa ni zao la kukwepa kodi.

Aidha, washtakiwa Mateni na Kahangwa wanadaiwa Januari Mosi 2015 na Desemba 31, 2018 huko Mbezi Africana wakiwa Mhasibu na Mkaguzi wa Hesabu walitengeneza taarifa za uongo za mapato za Kampuni ya GMU Group Limited kwa mwaka 2015, 2016 na 2017 kwa nia ya kupata faida.

Pia wanadaiwa walimsaidia Urio kuandaa taarifa za fedha za Kampuni hiyo kwa mwaka 2015,2016 na 2017 kwa lengo la kujipatia faida na kwamba walimsaidia Urio kujipatia Sh 4,265,882,773 wakati wakijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kukwepa kodi.

Mshtakiwa Nkyapi anadaiwa alishindwa kulipa kodi ya Sh 89,673,373 na kushindwa kutoa risiti za kielektroniki baada ya kupokea malipo ya Sh 98,670,000 ya Prochesi na Prokolini kwa mauzo ya katoni 759 ya Robertson Wine 75 CL.

Pia anadaiwa aliingiza bidhaa za vinywaji vikali zenye thamani ya Sh 95,100,297 bila kusajiliwa na kuisababishia hasara ya Sh 89,673,373  kwa kuingiza bidhaa ambazo hazijasajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) pamoja na kutakatisha fedha.

Hata hivyo, washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi na kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Fabruari 12, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wote wamerudishwa rumande.




TMDA YAKAGUA SHEHENA 3160 ZA DAWA ,VIFAA TIBA NA VITENDANISHI

$
0
0


Kaimu Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Proches Patrick akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Timu ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walipotembelea Mamlaka hiyo kuangalia mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya tano ikiwa Kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya iliyoratibiwa na Maafisa habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara.


Mkuu wa Msafara na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Gerald Chami akitoa maelezo kuhusiana na kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya kwa kuangalia mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya tano.
Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Gaudensia Simwanza akitoa akizungumza kuhusiana na mamlaka hiyo namna inavyofanya kazi za udhibiti wa dawa nchini
Mkaguzi wa Dawa wa Kanda ya Kaskazini wa (TMDA) Titus Malulu akitoa maelezo kuhusiana na wanavyofatilia dawa zikiwa sokoni kwa kutumia maabara hamishika.
Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Gaudensia Simwanza akionesha maabara hamishika ambayo wanaweza kukagua dawa sehemu yeyote.
Picha ya pamoja ya Kaimu Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Proches Patrick na waandishi wa habari pamoja na Timu ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walipotembelea Mamlaka hiyo kuangalia mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya tano ikiwa Kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya iliyoratibiwa na Maafisa habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara.
 
Na Chalila Kibuda,Michuzi Blog, Arusha

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Kaskazini imesema katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dk.John Magufuli imefanikiwa kukagua shehena 3,160 za dawa, vifaa tiba, vitendanishi kupitia vituo vya forodha vya Namanga, ,Holili ,Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro pamoja na Tarakea.

Hayo yalielezwa jana na Kaimu Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka hiyo Proches Patrick amesema kuwa katika ukaguzi huo ni mafanikio kwao kwani kunafanya dawa,vifaa tiba na vitandanishi kuwa salama na bora kwa kulinda afya za watumiaji

Patrick amesema katika utendaji wao wa kazi wamechunguza ubora,Usalama na ufanisi wa sampuli 243 za dawa, vifaa tiba na vitendanishi huku maeneo 5,531 yanayojihusisha na biashara za dawa ,vifaa tiba na vitendanishi vimekaguliwa pamoja na watendaji wa vituo vya afya 152 wamepatiwa mafanzo ya utoaji wa taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya dawa na vifaa tiba.

Amesema kwa kazi zote zilizofanyika ni mafanikio kwa kanda ya Kaskazini TMDA imefanikiwa kufanya kazi kwa kwa kutumia mfumo wa Kieletroniki unaowezesha utoaji wa huduma huduma ndani ya siku moja.

Patrick kuwa wakati walipokuwa hawana mifumu huo walikuwa wanatumia siku tatu kwa wanaohitaji kibali kusafiri na kufika katika ofisi za TMDA.

Patrick amesema kuwa licha ya kutoa vibali vya waingizaji dawa lakini wanafatilia dawa hizo katika soko ili kujiridhisha dawa zinazotumika ni zile zilizopewa kibali na mamlaka hiyo.

“TMDA ipo kulinda afya za wananchi kuhakikisha dawa wanzotumia zina ubora na ikitokea kuleta madha kwa wananchi dawa hiyo inaondoka katika soko mara moja”amesema Patrick

Patrick amesema kuwa TMDA baada ya kutoa vibali vya uingizaji dawa huwa wanafanya utafiti wa dawa hizo katika kuhakikisha wananchi wanapata dawa zenye ubora.

Hata hivyo amesema katika mikakati hiyo kwa kanda ya kaslazini wameweza kusajili kiwanda cha dawa za mifugo ambacho kitaanza hivi karibuni.
 
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images