Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

Balozi wa Tanzania nchi Afrika Kusini Meja Generali Gaudences Milanzi akabidhi hati ya Utambulisho kwa Rais wa Afrika Kusini

0
0
 Balozi mpya wa Tanzania nchini Afrika kusini Meja General Gaudence S Milanzi leo amekabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Afrika Kusini Ciril Ramaphosa Ikulu leo. Pamoja na Balozi wa tanzania, mabalozi wengine 11 toka nchi za mbali mbali duniani nao walikabidhi hati za utambulisho.
  Rais wa Afrika Kusini Ciril Ramaphosa pichani kati akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Afrika kusini Meja General Gaudence S Milanzi  (kushoto) mara baada ya kukabidhi hati ya utambulisho Ikulu leo.
Balozi mpya wa Tanzania nchini afrika kusini Meja General Gaudence S Milanzi leo amekabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Afrika Kusini Ciril Ramaphosa Ikulu leo. Pamoja na Balozi wa tanzania, mabalozi wengine 11 toka nchi za mbali mbali duniani nao walikabidhi hati za utambulisho

NAMUNGO FC WARAMBA UDHAMINI MNONO SPORTPESA

0
0
Na Khadija seif, Michuzi Tv
TIMU ya Namungo fc waahidi kuonyesha maajabu kesho katika mchezo wao dhidi ya wekundu wa msimbazi Simba fc.

Akizungumza hayo mara baada ya kutia saini makubaliano ya udhamini wa Kampuni ya ubashiri ya sportpesa baina ya timu ya Namungo Mwenyekiti wa timu hiyo Hassan Zidadu amewashukuru sportpesa kwa udhamini huo na kuhaidi kufanya vizuri kutimiza malengo ya udhamini huo.

"Kupewa kwetu udhamini huu ni furaha na itakua chachu kwetu kufanya vizuri zaidi na kuhakikisha timu ya namungo inafika mbali zaidi ili Kampuni ya sportpesa wahamasike na kushawishika kuongeza donge nono zaidi ya hili".

Hata hivyo Zidadu ameeleza kuwa kuelekea mchezo wao dhidi ya klabu ya simba na kuwahakikishia wapenzi wa namungo kuwa wamejipanga vizuri kuwakabili Simba.

"Kesho maajabu sio Simba kuifunga namungo bali maajabu yatakua namungo kuifunga Simba hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia mtanange huo ".

Pia Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya ubashiri ya sportpesa nchini Abbas Tarimba akiweka bayana udhamini huo uliogharimu shilingi za Kitanzania milioni 120.

"Tumeamua kudhamini timu ya namungo kutokana na weledi wake pamoja na bidii na wapo nafasi nzuri kwa sasa kwenye ligi kuu ambapo wapo nafasi ya tano na tumetoa udhamini wa milioni 120 na sio Mwisho tu tukiona wanafanya vizuri tutegemee dau litapanda zaidi,"
Mwenyekiti wa timu ya Namungo akitoa neno la shukrani kwa Kampuni ya ubashiri sportpesa jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini mkataba wa udhamini kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya ubashiri sportpesa na kushoto ni katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu (TFF) Wilfred kidao jijini Dar es salaam.

WAGONJWA 300,836 WAPATIWA HUDUMA JKCI KATIKA MIAKA MINNE YA JPM

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohammed Janabi akizungumza na waandishi wa habari wakati alieleza mafanikio ya taasisi hiyo ndani ya miaka minne ya utawala wa Rais Dkt. John Joseph Magufuli na kueleza kuwa Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha taasisi hiyo inaendelea kutoa huduma bora zaidi, leo jijini Dar es Salaam.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
TAASISI ya moyo ya JKCI ndani ya miaka minne ya utawala wa Rais Dkt. John Joseph Magufuli imefanikiwa kutoa huduma kwa wagonjwa 300,836 katika kliniki (outpatients) ambao walitibiwa na kuruhusiwa huku wagonjwa 14,960 walilazwa kwa ajili ya kupata matibabu zaidi kutoka katika taasisi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa kueleza mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha mwaka 2015/2019 Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete Profesa. Mohammed Janabi amesema kuwa Serikali na wadau mbalimbali wamekuwa sehemu ya mafanikio ya taasisi hiyo.

"Taasisi imefanikiwa kufanya pasuaji kubwa kwa kusimamisha moyo kwa wagonjwa 1,537 kwa mafanikio makubwa huku vifo vikiwa ni asilimia 6 sawa na wagonjwa 92, na kwa upande wa upasuaji wa moyo kwa njia ya tundu dogo linalotobolewa mtambo wa cathlab wagonjwa 4,207 walipata huduma hii huku vifo vikiwa ni asilimia 1.3 tuu sawa na wagonjwa 42" Ameeleza Janabi.

Amesema kuwa huduma zitolewazo na taasisi hiyo zimeweza kuokoa shilingi bilioni 86 kwa kufanya upasuaji kwa wagonjwa 5,744 na kueleza kuwa wagonjwa hao wangetibiwa nje ya nchi Serikali ingetumia zaidi ya shilingi bilioni 172 katika kulipia gharama za upasuaji.

Aidha amesema kuwa ndani ya miaka mitano watakuwa wamefanikisha programu ya kupandikiza moyo na hadi sasa Serikali tayari imetoa shilingi bilioni 4.6 kwa ajili ya kununua vifaa ili kuweza kutoa huduma bora zaidi.

Vilevile amesema kuwa ujuzi kwa wataalamu umeongezeka kwa kiasi kikubwa na pasuaji zikizofanyika zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kuhusiana na wingi wa wagonjwa wanaotibiwa katika taasisi hiyo Prof. Janabi amesema;

" Kwa siku wagonjwa wanaotibiwa katika taasisi hiyo ni kati ya 300 hadi 500 kwa siku na Serikali yetu kwa kushirikiana na Serikali ya China itajenga hospitali kubwa ya moyo katika eneo la mloganzila na hatua za awali zimeshakamilika" amesema.

Janabi amesema kuwa pia taasisi hiyo imefanikiwa kununua mashine mpya za matibabu ya moyo zikiwemo za kuchunguza jinsi moyo unavyofanya kazi, mashine ya kuchunguza mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi, mashine ya X-RAY  pamoja na vifaa vya upasuaji.

Kwa niaba ya taasisi hiyo Profesa Janabi amehaidi kuendelea kutoa huduma bora na za utaalamu wa hali ya juu na hiyo ni pamoja na kutoa elimu ya magonjwa ya moyo kupitia vyombo vya habari  pamoja na kutembelea hospitali za Mikoa na Wilaya na kuendelea kutoa huduma kupitia taasisi hiyo.

SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA BENKI RUFIJI

0
0
Na Josephine Majula na Saidina Msangi

Serikali imeahidi kuongeza jitihada za kuanzisha matawi ya benki ya uhakika katika Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za kifedha kwa urahisi.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa aliyetaka kujua ni lini Serikali itapeleka huduma za benki katika Wilaya hiyo.

Mhe. Mchengerwa alisema kuwa wananchi wa Jimbo kongwe nchini wamekuwa wakipata tabu ya kupata huduma za kifedha hali inayowalazimu kusafiri umbali wa Kilometa 100 kufuata huduma hizo.

Akijibu swali hilo, Dkt. Kijaji alisema kuwa wananchi wa Rufiji waendelee kutumia huduma za fedha zilizopo wakati Serikali ikiendelea kuboresha miundombinu muhimu pamoja na kufanya majadiliano na kuzishawishi benki kuanzisha matawi yao katika Wilaya hiyo.

“Kufuatia mabadiliko ya Sekta ya Fedha nchini ya mwaka 1991, Serikali ilitoa uhuru kwa benki kufanya tafiti za kuamua kuhusu maeneo ya kupeleka huduma za kibenki kulingana na taarifa za utafiti uliofanywa pamoja na vigezo vya benki husika. Kwa kuwa benki zinajiendesha kibiashara maamuzi ya kufungua tawi sehemu yoyote hapa nchini huzingatia vigezo hivyo”,alisisitiza Dkt. Kijaji.

Alisema Serikali inatambua umuhimu wa upatikanaji wa huduma za kifedha hasa zile zinazotolewa maeneo ya karibu na wananchi, itaongea na benki kuona namna ya kupunguza baadhi ya vikwazo vinavyoweza kusababisha gharama za uendeshaji wa shughuli za benki wilayani hapo kuwa juu ili wananchi waweze kupata huduma hizo kwa urahisi.

Alisema kwa sasa wananchi wa Wilaya hiyo wanapata huduma za kifedha kupitia Kituo cha Makusanyo ya Fedha cha NMB (Cash Collection Point - CCP) kilichopo katika Kata ya Utete pamoja na Mawakala wa Benki, hususan Benki ya NMB na CRDB waliopo katika Wilaya ya Rufiji. 
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akijibu swali bungeni Jijini Dodoma katika mkutano wa 18 wa Bunge la 11 ulioanza leo.
 

MAFUNDI SIMU JIUNGENI KWENYE UMOJA TCRA

0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha .

Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA Kanda ya kaskazini imewataka mafundi wa vifaa vya kieletroniki ikiwemo simu za mkononi kuwa kwenye mfumo wa umoja kwa kuanzisha vikundi vyao kwa Kanda au mkoa.
Kwa muktadha huo kuanzia mwezi julai mwaka huu hakuna fundu ambaye atafanyakazi kama hajasomo wala kusajiliwa hivyo ni muhimu kwenu kujiunga kwenye kikundi ili kupatiwa elimu. 

Kauli hiyo imetolewa na Mwanasheria wa mamlaka hiyo Kant Mosha wakati wa mkutano wa mafundi wa vifaa vya kieletroniki uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo aliwataka kuacha kutokuwa na usajili wa kikundi ndio suluhisho. 

Alisema kuwa mafundi simu ni kada ambayo ilikuwa imesahauliwa hapo awali lakini kupitia serikali ya awamu ya tano chini ya Rais dkt.John Magufuli imeamua kuwatambua hivyo kuungana ni sehemu ya kufanikiwa kwa malengo yenu. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mafundi simu Kanda ya ziwa Maguwa Manyanda amewataka kutambua kwamba mafundi simu ni wathamani kwani jamii inwategemea na wanachangia mapato ya serikali hivyo busara ni kuona umoja ndio suluhisho la changamoto zao.
Alisema kuwa mafunzo hayo yataondoa changamoto na kuwafanya kuwa huru katika shughuli zao za kila siku hivyo umoja ni nguzo ya kuwafikisha kuweza kushirikiana na serikali katika masuala mbalimbali ikiwemo vyombo vya Dola. 

Alieleza kuwa kufanikiwa ili kila moja aweze kutenda kazi zake ni muhimu Sana wakajiunga na umoja ili kuondoa changamoto zao ambazo zimekuwa zikiwafanya kujikuta wakikumbana na jeshi la polisi.
Nae Mwenyekiti wa umoja wa mafundi simu Kanda ya kaskazini Nasri Mshana Mtengeti alisema kuwa wamefirahi Sana kupata elimu hiyo ya umoja ambayo itawasaidia kuondokana na changamoto hivyo tuhamasishane kujiunga na umoja huu. 

Awali akitoa mafunzo kwenye mkutano huo mratibu wa vikundi hivyo kutoka mamlaka ya mawasiliano mhandisi Kadaya Buluhye aliwataka mafundi hao kufanyakazi kwenye umoja kwa lengo la kupata elimu na usajili. 

Alisema kuwa jeshi la polisi linafanyakazi ya kulinda usalama na Mali za raia Ila umoja wenu utasaidia kufanya kazi kwa karibu na jeshi hilo na kuondoa changamoto zenu ambazo mmekuwa mkikumbana nazo kama mafundi.

RAIS MAGUFULI APOKEA HATI ZA MABALOZI 9 WANAOWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI KATIKA HAFLA FUPI ILIYOFANYIKA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati yaUtambulisho kutoka kwa Balozi wa Djibouti hapa nchinimwenye makazi yake nchini Kenya Yacin Elmi Bouh marabaada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika
mazungumzo na Balozi wa Djibouti hapa nchini mwenyemakazi yake Kenya Yacin Elmi Bouh mara baada yakuwasilisha Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar esSalaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika
mazungumzo na Balozi wa Venezuela hapa nchini Jesus AgustinManzanilla PUPPO Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati yaUtambulisho kutoka kwa Balozi wa Israel mwenye makazi yakeKenya Oded Joseph Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati yaUtambulisho kutoka kwa Balozi wa Ufilipino hapa nchinimwenye makazi yake nchini Kenya Alex Chua katika hafla fupiiliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati yaUtambulisho kutoka kwa Balozi wa Ghana mwenye makaziyake nchini Kenya Fransisca Ashiete-ODUNTON Ikulu jijiniDar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati yaUtambulisho kutoka kwa Balozi wa Jamaica hapa nchinimwenye makazi yake Afrika Kusini Angela Veronica Comfortkatika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati yaUtambulisho kutoka kwa Balozi wa Austria mwenye makaziyake nchini Kenya Dkt. Christian Fellner Ikulu jijini Dar esSalaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati yaUtambulisho kutoka kwa Balozi wa Ureno hapa nchini mwenyemakazi yake nchini Msumbiji Maria Amelia Maio De PAIVAkatika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Singapore hapa nchini mwenyemakazi yake Singapore Douglas Foo Peow Yong mara baada yakuwasilishha Hati zake za utambulisho

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ghana mwenye makazi yake nchini Kenya Fransisca Ashiete-ODUNTON Ikulu jijini Dar es Salaam.

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA

0
0

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na wananchi kutoka Urambo walioambatana na mbunge wao, Margaret Sitta katika hafla ya kukabidhi majoho kwa Maspika wastaafu iliyofanyika Bugeni jijini Dodoma, Januari 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa bunge Job Ndugai  (aliyekaa wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maspika na Mawaziri Wakuu wastaafu katika hafla ya kukabidhi majoho kwa Maspika wastaafu iliyofanyika Bungeni jijini Dodoma, Januari 18, 2019.  Waliokaa kutoka kushoto ni Mbunge wa Urambo, Magaret Sitta ambaye pia ni Mke wa Spika Mstaafu, Marehemu Samuel Sitta, Spika wa Bunge Mstaafu, Pius Msekwa na kulia ni Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda. Waliosimama ni Maziri Wakuu Wataafu, kutoka kushoto ni Frederick Sumaye, Edward Lowassa na John Malecela. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Spika wa Bunge, Job Ndugai  (wa pili kulia) akimvalisha Joho, Spika  wa bunge Mstaafu, Pius Msekwa katika hafla ya kukabidhi majoho kwa Maspika Wastaafu iliyofanyika Bungeni jijini Dodoma, Januari 18, 2019. Kulia ni Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Bungeni jijini Dodoma, Januari 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wanakwaya wa Bunge  wakiimba Wimbo wa Taifa wakati Spika wa bunge, Job Ndugai  alipoafungua Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge jijini Dodoma, Januari 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Bungeni jijini Dodoma, Januari 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA YATOA MIEZI MIWILI KWA PANDE MBILI ZA FAMILIA YA MAREHEMU NILIONEA ERASTO MSUYA KUONDOA TOFAUTI ZAO

0
0
Na woinde shizz, Arusha

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imetoa miezi miwili kwa pande mbili za familia ya marehemu bilionea Erasto Msuya zenye mgogoro wa kugombea mali za marehemu kukaa meza moja ili kuondoa tofauti zao na kuleta mrejesho mahakamani hapo baada ya muda huo kupita.

Akitoa uamuzi huo leo Januari 28,2020 ,Jaji wa Mahakama hiyo anayesikiliza shauri hilo,Johannes Masara amesema kuwa mahakama hiyo imeridhia ombi la upande wa mleta maombi Ndeshukulwa Msuya la kuiomba mahakama hiyo kuondoa shauri lake la mirathi kwa muda ili familia hizo ziweze kukaa meza ya mazungumzo.

Amesema kuwa Mahakama baada ya kupokea ombi la mleta maombi imekubali pande hizo kuweza kukaa meza moja kupitia Mkuu wa wilaya ya Arumeru na imetoa miezi miwili kupata mrejesho.

Kesi hiyo ya Mirathi namba 66/2018 iliyopo ngazi ya rufaa mahakama kuu kanda ya Arusha ilifunguliwa na Ndeshukurwa Msuya mama wa marehemu bilionea Msuya akiiomba mahakama kumtengua Miriam Mrita mke wa marehemu kuwa msimamizi wa mirathi kutokana na kukabiluwa na kesi ya mauji ya WiFi yake iliyopelekea awe gerezani kwa muda mrefu na kushindwa kusimamia Mali za marehemu.

Akizungumza nje ya Mahakama Ndeshukurwa amesema kuwa uamuzi wa mahakama umetenda haki na umezingatia maslahi mapana ya pande zote mbili kwani anaamini jambo hilo linaenda kumalizika na watoto wa marehemu wataweza kupata haki yao ya msingi.

Amesema suala la maridhiano liliibuliwa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro na kuwataka ndugu hao waondoe kesi iliyopo mahakamani ili wakae mezamoja na kwamba angesaidia kusimamia meza ya mazungumzo ya famili hizo.

Hata hivyo upande wa wajibu maombi (Wajomba)hawakuwepo mahakamani hapo kwa madai kwamba wamefiwa na Dada yao mkubwa na kuwakilishwa na Mwanasheria wao Shilinde Ngalula.

Awali wakili wa upande wa wajibu maombi,Shilinde Ngalula,alipinga hatua ya mahakama hiyo kukubali ombi la kuondoa kesi hiyo kwa muda akiitaka mahakama iifute kabisa kesi hiyo na kusiwepo shauri hilo mahakamani wakati wa maridhiano nje ya mahakama.

Hata hivyo jaji Masara alikataa ombi hilo na kukubali ombi la upande wa waleta maombi la kuondoa kesi hiyo kwa muda bila kuifuta na kurejea meza ya mazungumzo na kwamba iwapo familia hizo hazitakubaliana watarejea mahakamani kuendelea na shauri hilo kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Ndeshukurwa anampinga Miriamu Mrita ambaye ni mke wa marehemu mwanaye kuwa msimamizi wa mirathi akidai kuwa ameshindwa kugawanya Mali za marehemu kwa wanufaika kwa kipindi cha miaka saba tangu kifo cha marehemu bilionea Msuya kilichotokea kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 mwaka 2013 wilayani Hai ,mkoani Kilimanjaro.

Ndeshukurwa anadai kwamba Miriamu ambaye kimsingi ndiye msimamizi wa mirathi ,yupo gerezani mahabusu kwa muda mrefu akikabiliwa na kesi ya mauaji ya WiFi yake,hivyo hatua hiyo imepelekea baadhi ya Mali za marehemu kupotea huku watoto wa marehemu wakishindwa kupatiwa mgawanyo wa Mali hizo za marehemu baba yao.

SERA YA USHIRIKA MSINGI WA MABADILIKO CHANYA YA SEKTA YA USHIRIKA

0
0


 Mkurugenzi wa Mipango Ufuatiliaji na Tathmini wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bw. Buji Bampebuye akifafanua jambo katika kikao cha Warsha ya kujadili maboresho ya Sera ya Ushirika (2002) kilichokuwa kikifanyika Mkoani Morogoro hivi karibuni
Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT) Bi. Anna Lupiano akieleza matarajio ya Vyama katika maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika.


 Mkurugenzi mstaafu wa Rabo Foundation Netherlands Bw. Pierre Van Hedel akielezea namna Vyama vya Ushirika vinavyofanya kazi katika nchi ya Netherlands kwa lengo la kujifunza na kuongeza ujuzi katika maboresho ya Sera ya Ushirika ya Tanzania


 Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika wa Kifedha Bw. Josephat Kisamalala akieleza jambo wakati wa Warsha ya maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika
 
 Mshauri wa Kibiashara wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali AGRITERRA Bw. Raymond Lyimo akitoa mada kwa wajumbe wa Warsha ya maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika
 Mshauri wa Kibiashara wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali AGRITERRA Bw. Mikidadi Waziri akitoa mada wakati wa Warsha ya maboresho ya Sera ya Ushirika



Mkurugenzi wa Mipango Ufuatiliaji na Tathmini wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Bw. Buji Bampembuye amesema wadau wote wa Ushirika wakitekeleza majukumu yao ya Kiushirika kupitia dira na mwelekeo wa Sera ya Ushirika, ni dhahiri kwamba Sekta ya Ushirika itakuwa na mabadiliko chanya na yenye tija kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya kujadili maboresho ya Sera ya Ushirika (2002) iliyoanza Jumanne 28 Januari, 2020 hadi 29 Januari 2020, Mkoani Morogoro.

“Ushirika ni moja ya nyenzo muhimu inayoweza kutumika nchini katika kuondoa umaskini na kuondokana na uchumi tegemezi. Hivyo, kwa kuimarisha Sera ya Ushirika tunajiwekea misingi imara ya kuendeleza Ushirika nchini,” alisema Bw. Bampebuye

Bw. Bambebuye amesema Tanzania tunaweza kujifunza mambo mengi mazuri kutoka kwenye nchi zilizofanikiwa katika Sekta ya Ushirika pia tunaweza kutumia tafiti zetu zilizowahi kufanyika na kuingiza yatakayoongeza chachu ya ukuaji wa Sekta ya Ushirika na kupata Sera itakayokuwa ikijibu Changamoto za wakulima na Wanaushirika kwa ujumla.

Mshauri wa Kibiashara wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Ushirika nchini liitwalo AGRITERRA Bw. Mikidadi Waziri akitoa mada katika Warsha hiyo ameeleza kuwa Shirika hilo kama mdau wa Ushirika limekuwa likifanya kazi katika kuongeza msukumo wa Maendeleo katika Sekta ya Ushirika kupitia mafunzo kwa Vyama vya Ushirika ya Utawala Bora, Usimamizi wa Fedha na uhamasishaji.

Bw. Mikidadi alisema kuwa baadhi ya Changamoto zilizopo katika Sekta ya Ushirika ni pamoja na ushiriki mdogo wa vijana na wanawake hususan katika ngazi za uongozi za Vyama vya Ushirika. Hivyo, akashauri haya ni mambo ya msingi ya kuzingatiwa katika maboresho ya Sera ili kuhakikisha kuwa Sekta inakuwa endelevu na inatoa fursa za kiuchumi kwa makundi yote ya jamii zetu.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT) Bi. Anna Lupiano amesema uboreshaji wa Sera ya Ushirika unatoa matazamio ya kupata utendaji na utekelezaji wa majukumu utakaoenda kujibu changamoto mbalimbali za Sekta ya Ushirika.

Bi. Lupiano ametoa wito kwa Viongozi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika kufuata na kutekeleza matakwa ya Sera mpya itakapokuwa tayari katika hatua za utekelezaji ili kuboresha na kuhakikisha uendelevu wa Vyama vya Ushirika.

SPIKA NDUGAI AWAKABIDHI MASPIKA WASTAAFU MAJOHO YAO BUNGENI JIJINI DODOMA

0
0



 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akimvalisha na kumkabidhi joho Mhe. Pius Msekwa alilokuwa akitumia wakati akiwa Spika wa Bunge la Nane Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai.
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge nje ya ukumbi wa Bunge baada ya wa Sherehe fupi za kukabidhiana majoho kwa Maspika wastaafu zilizofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kulia waliokaa ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Spika Mstaafu, Mhe. Anne Makinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Spika Mstaafu, Mhe. Pius Msekwa, Mbunge wa Urambo Mhe. Margaret Sitta na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Maspika wastaafu ambao ni Mhe. Anne Makinda (wa pili kushoto) na Mhe. Pius Msekwa (wa pili kulia) baada ya Sherehe fupi za kukabidhiana majoho kwa Maspika hao zilizofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Mbunge wa Urambo, Mhe. Margaret Sitta.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimkabidhi joho Mhe. Margaret Sitta kwa niaba ya mume wake aliyekuwa Spika wa Bunge la 9 Mhe. Samuel Sitta wakati wa Sherehe fupi za kukabidhiana majoho kwa Maspika wastaafu zilizofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimpa mkono wa pongezi Spika wa Bunge la Kumi Mhe. Anne Makinda baada ya kumkabidhi joho alilokuwa akitumia wakati akiwa Spika wa Bunge la Kumi.PICHA NA BUNGE

DAR ES SALAAM KUADHIMISHA WIKI YA MAHAKAMA KWA KUTOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI BURE.

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda anawaalika wananchi wote wa Mkoa huo wenye Kero za kisheria kujitokeza kwa Wingi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Mahakama yanayotaraji kuanza February 01 hadi 05 kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja.

RC Makonda kwa kushirikiana na Mahakama kuu ya Kanda ya Dar es salaam wameandaa wataalamu wakiwemo Mawakili, Wanasheria, Jeshi la polisi Dawati la Jinsia, Jeshi la Magereza, Chama cha Wanasheria Tanganyika pamoja na wadau wa kisheria wa kutosha kuhakikisha kila mwananchi anaefika kwenye viwanja hivyo anapata huduma stahiki ya kisheria pasipo usumbufu wowote.

Maadhimisho ya Wiki ya Mahakama yatatanguliwa na Maandamano yatakayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kuanzia Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam hadi viwanja vya Mmoja mapema Asubuhi.

Walengwa wa Zoezi hilo ni Wananchi wenye kero za migogoro iliyopo Mahakamani, Mienendo ya kesi, Wale ambao hukumu zao zimetoka na wanataka kukata rufaa lakini hawapewi nakala za hukumu kwa maandishi, Wananchi wasiojua wapeleke wapi kesi zao, Malalamiko ya maabusu, Polisi pamoja na kesi za ukatili wa kijinsia.

WAZIRI JAFO AZINDUA JENGO LA OFISI ZA ALAT, AWAPONGEZA KUHAMIA MAKAO MAKUU

0
0
Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo ameipongeza Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT) kwa kufanikiwa kujenga jengo la Ofisi zao jijini Dodoma.

Mhe Jafo ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa ofisi za Jumuiya hiyo na kusema wametii kwa vitendo agizo la Rais Dk John Magufuli la kuifanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi.

Jengo hilo ambalo lilianza kujengwa Septemba 2018 limekamilika tayari kwa kuanza kutumika ambapo limegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 121.3 ambazo ni fedha za ndani.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Jafo ameupongeza uongozi wa ALAT kwa ujenzi huo ambao umeacha historia kwani kabla ya hapo Jumuiya hiyo haikuwahi kumiliki ofisi zao wenyewe na badala yake walikua wamepanga.

" Nimeridhika na ujenzi wa jengo hili, hakika ni mzuri na thamani ya fedha imeonekana, Viongozi mliopo mtakumbukwa kwa hili ambalo mmelifanya. Mmefanya jambo la kihistoria na hii ndio maana ya uongozi ni alama.

Kwa muda mrefu ALAT ilikua ni kichaka cha watu kunufaisha matumbo yao lakini chini ya Mwenyekiti Gullamal Mukadam hata zile Halmashauri zilizokua haziipendi ALAT zitaanza kutoa michango bila kunung'unika," Amesema Mhe Jafo.

Ameipongeza Jumuiya hiyo kwa namna ambavyo imekua ikisimamia miradi ya serikali za mitaa na kuahidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao katika miradi mbalimbali ambayo imekua ikitekelezwa.

" Serikali za mitaa ndio utu wa mgongo wa Nchi yetu, tutaendelea kupeleka miradi mbalimbali ya kimaendeleo haswa kwenye afya na elimu na tunaamini hatua kubwa za kimaendeleo ya kiuchumi itapigwa kwa ushirikiano uliopo baina ya serikali na ALAT," Amesema Mhe Jafo.

Pia Waziri Jafo amezitaka Halmashauri zote nchini zinazodaiwa na Mabenki mikopo iliyokopwa na madiwani ziyalipe madeni hayo mara moja ili kuepusha Mabenki hayo kuzuia viinua mgongo vya madiwani pindi watakapomaliza muda wao.

" Nafahamu kuna halmashauri hazijalipa madeni ya madiwani wanayodaiwa benki baada ya madiwani wetu kukopa wakitegemea watakuwa wanakatwa kwenye posho zao za kila mwezi.

Ninawaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote zinazodaiwa zikiongozwa na halmashauri ya Gairo kulipa madeni hayo mara moja ili kuondoa usumbufu wa kuzuiliwa viinua mgongo vyao madiwani wetu hawa," Amesema Mhe Jafo.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo hilo, Katibu Mkuu wa ALAT, Elirehema Kaaya amesema kukamilika kwa ujenzi wa jengo lao hilo kutaokoa kiasi cha Sh Milioni Tano kila mwezi walichokua wakitumia kama pango kwenye ofisi zao zilizopo jijini Dar es Salaam.

" Mhe Waziri ujenzi umetumia takribani miaka miwili na tulijenga kwa fedha zetu wenyewe ambapo kiwanja pia kilikua ni chetu na mhandisi ni kutoka Jiji la Dodoma," Amesema Kaaya.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mhe Gulamal Mukadam amesema malengo yao ni kujenga jengo refu la kitega uchumi ambalo litaongezea kipato kikubwa kitakachowawezesha kuzidi kujiendesha wenyewe.

" Tunaipongeza serikali ya awamu ya tano kwa miradi makubwa ya kimaendeleo inayotekelezwa kwenye serikali za mitaa hasa kwenye sekta ya Elimu, afya na miundombinu.

Lengo letu baada ya kukamilika kwa ujenzi huu ni kujenga jengo kubwa la kitega uchumi ili kuendana na Sera ya Rais Magufuli ya kukuza uchumi ambapo tunaamini licha ya kutupatia fedha nyingi litakua msaada pia kwa halmashauri zetu," Amesema Mukadam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo (katikati) akizindua jengo la ofisi za Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) leo jijini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Gullam Mukadam.
Mwenyekiti wa ALAT, Gullam Mukadam akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la ofisi ya Jumuiya hiyo jijini Dodoma.

Wadau mbalimbali wa ALAT wakifuatilia uzinduzi wa jengo la ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Dodoma leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Ofisi za ALAT jijini Dodoma Leo.
Katibu Mkuu wa ALAT, Elirehema Kaaya akisoma taarifa ya jengo hilo mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa jengo la Ofisi za ALAT jijini Dodoma.
Muonekano wa Jengo la Ofisi za Jumuiya ya Tawala za Mitaa lililozinduliwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akiwa na viongozi wa serikali na ALAT wakati wa uzinduzi wa jengo la Ofisi za Jumuiya hiyo.

WAZAZI WASIOWAPELEKA WATOTO SHULE KUSHTAKIWA

0
0
Na Mwandishi wetu Mihambwe .

Mkuu wa Mkoa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa amewaagiza Watendaji Kata na Vijiji kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani Wazazi na Walezi wote ambao hawajawapeleka Watoto shule mpaka sasa ambao wanaostahili kuanza darasa la kwanza na wale waliofaulu kidato cha kwanza. 

Mhe. Byakanwa ameyasema hayo kwenye ziara ya siku aliyoifanya kwenye Tarafa ya Mihambwe ambapo alikuwa akikagua hali ya kuripoti Wanafunzi kidato cha kwanza pamoja na kukagua ujenzi wa miradi ya kimaendeleo kama vile Madarasa, Maabara pamoja na vyoo. 

“Nawaagiza Watendaji Kata na Vijiji kuwakamata na kuwapeleka Mahakamani Wazazi na Walezi wote ambao wamekaidi utekelezaji wa kuwapeleka shule Watoto wao. Watakaokaidi kukamatwa Watendaji nijulisheni haraka, nitawashughulikia mwenyewe.” Alisisitiza Mhe. Byakanwa. 

Kwenye upande wa ujenzi wa miradi ya maendeleo, Mhe. Byakanwa ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo na kuvutiwa zaidi na utekelezaji wa kampeni aliyoianzisha ya ujenzi wa vyoo kwenye shule. 

“Nilikuwa naona mitandaoni leo nimejionea mwenyewe, nakupongeza sana Afisa Tarafa Mihambwe Shilatu kwa kazi nzuri unayoifanya ya kusimamia miradi ya kimaendeleo. Nimevutiwa zaidi na namna ulivyosimamia kampeni ya shule ni choo, kote nilipopita nimeona kazi kubwa iliyofanyika. Hongera sana Shilatu.”* Alisema Mhe. Byakanwa alipokuwa akizungumza na Wazazi na Wananchi waliojitokeza Shule ya msingi Chikongo kilichopo Kijiji cha Chikongo kata ya Mkoreha wakati akihitimisha ziara yake ya siku moja alipotembelea Tarafa ya Mihambwe.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO JANUARI 29,2020

0
0
               
 

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA KWENYE BLACK HISTORY MONTH HAMBURG,UJERUMANI

0
0

Bendi ya maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya  “The Ngoma Africa Band”
aka FFU-Ughaibuni alimaarufu pia kwa majina ya utani kama viumbe wa ajabu
“Anunnaki Aliens” bendi inayoongozwa na mwanamuziki nguli kamanda Ras Makunja yenye maskani nchi Ujerumani, bendi hiyo inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho kubwa la kufungua mwezi wa Black History Month yatakayofanyika jijini Hamburg siku ya jumamosi tarehe 1 February 2020 katika ukumbi wa Grunspan. Ngoma Africa Band imeweka rekodi ya kuwa bendi ya muziki ya kigeni inayodumu kwa miaka 27 barani ulaya na katika mmajukwaa ya kimataifa ,ilianzishwa mwaka 1993 ka kiongozi wake kamanda Ras Makunja.

DEATH ANNIVERSARY

0
0


 MOSES TITO KACHIMA

27.01.1945 – 29.01.2013



It has been seven years now since you’ve left us, gone but not forgotten. We’re grateful for the life you’ve lived, lessons you’ve taught us and today we remember you, celebrate you and the life you lived. We still hold the memories we had shared throughout the years close to our hearts.
May your soul continue to rest in eternal peace.

Eternal rest grant to him O Lord and let perpetual light shine upon him.
May he rest in peace, Amen.

MRADI WA KUJENGEA UWEZO WATAALAM NA WAKULIMA KATIKA KILIMO CHA AUMWAGILIAJI WAFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA. DODOMA

0
0

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Marco Ndonde akifungua mkutano wa majadiliano ya wadau kuhusu mradi wa mafunzo na matunzo wa skimu za kilimo cha Umwagiliaji. Uliyofanyika Jijini Dodoma.
Bw. Ukombeso Emmanuel Afisa Kilimo kutoka Manyara akiongea na waandishi wa Habari hawapo katika Picha kuhusu faida iliyopatikana kutokana na mradi wa mafunzo na matunzo wa skimu za kilimo cha Umwagiliaji, katika Mkutano wa wadau uliofanyika Jijini Dodoma leo.
Katika Picha ni sehemu ya Washiriki katika majadiliano ya kubadilishana mawazo kuhusu mradi wa mafunzo na matunzo wa skimu za kilimo cha Umwagiliaji. Iliyofanyika Jijini Dodoma.


Imeelezwa kuwa , Mradi wa kujengea uwezo kwa wakulima na wataalamu katika Kilimo cha Umwagiliaji nchini umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia matumizi ya muongozo yakinifu wa umwagiliaji na Mafunzo ya uendeshaji na matunzo ya skimu za umwagiliaji katika maeneo ya mfano yaliyo chaguliwa na mradi huo.

Hayo yamelezwa Leo Jijini Dodoma na kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Marco Ndonde alipofungua warsha ya wadau na wataalam ya kubadilishana malengo na mbinu zitakazotumiwa kufanya mafanikio ya mradi kuwa endelevu ili kuwezesha ukuzaji wa sekta ya umwagiliaji kote nchini. .

Bw. Ndonde amesema kuwa, mradi huo umekuwa wa mafanikio kwa kiasi kikubwa kutokana na wadau wa kilimo hicho kutumia mwongozo wa umwagiliaji kwa umakini katika kutekeleza shughuli zote za kilimo cha Umwagiliaji.

Akiongea katika Warsha hiyo, Afisa Kilimo kutoka Ofisi za Kilimo cha umwagiliaji Manyara Bw. Lukombeso Emmanuel, amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika eneo la umwagiliaji kupitia Mradi huo jambo ambalo limewawezesha wakulima wenyewe kuweza kupata uelewa hususan katika eneo la matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji jambo ambalo awali muamko ulikuwa mdogo.

“Kwa upande wetu sisi kama wataalam katika ngazi zote tumejengewa uwezo juu ya uibuaji, , utekekelezaji, uendeshaji na mafunzo pamoja na ufuatiliaji na tathmin kwa kufuata mwongozoyakinifu wa Umwagiliaji na namna ya kuwawezesha wakulima kufanya shughuli zao kufuata Mwongozo huo.” Alisisitiza Bwana Lukumbeso

Pamoja na mafanikio hayo mradi umekuwa na changamoto mbalimbali kwa wakulima kama vile uelewa mdogo kuhusu Sheria, kanuni na Miongozo ya Kilimo cha Umwagiliaji jambo ambalo linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu kupitia kuitambulisha rasmi Sheria ya Umwagiliaji kwa wadau mbalimbali na kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari.

Awamu hiyo ya pili ya mradi wa kujengea uwezo wakulima katika Kilimo cha Umwagiliaji unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Balozi mpya wa Tanzania nchini afrika kusini Meja Jenerali Gaudence S Milanzi akabidhi hadi ya utambulisho kwa Rais Cyril Ramaphosa jijini Pretoria

0
0
Balozi mpya wa Tanzania nchini afrika kusini Meja Jenerali Gaudence S Milanzi Jumanne Januari 28, 2020  amekabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Pretoria. Pamoja na Balozi wa Tanzania, mabalozi wengine 11 toka nchi za mbali mbali duniani nao walikabidhi hati zao za  utambulisho tayari kuanza kufanya kazi katika nchi hiyo.




Balozi mpya wa Tanzania nchini afrika kusini Meja Jenerali Gaudence S Milanzi akiwa na Afisa Ubalozi mwandamizi Bw. Richard Lupembe wakisimama tayari kuwasilisha hati

 Balozi mpya wa Tanzania nchini afrika kusini Meja Jenerali Gaudence S Milanzi  akijitambulisha kabla ya kukabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Pretoria. 
  Balozi mpya wa Tanzania nchini afrika kusini Meja Jenerali Gaudence S Milanzi  akikakabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Pretoria. 
  Balozi mpya wa Tanzania nchini afrika kusini Meja Jenerali Gaudence S Milanzi  akikaribishwa kuanza kazi rasmi baada ya kukabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Pretoria. 
  Balozi mpya wa Tanzania nchini afrika kusini Meja Jenerali Gaudence S Milanzi  akipata picha ya kumbukumbu baada ya kukabidhi hati ya utambulisho kwa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Pretoria. 
 Balozi mpya wa Tanzania nchini afrika kusini Meja Jenerali Gaudence S Milanzi  na Afisa Ubalozi Mwandamizi Bw. Richard Lupembe wakipata picha ya pamoja na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Pretoria. Picha na Ikulu ya Pretoria

UZINDUZI WA KAMPENI MPYA YA KIFUA KIKUU WILAYANI TUNDURU

0
0
 Mratibu wa kifua kikuu na Ukoma Hospitali ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma Dkt Mkasange Kihongole akitoa elimu juu ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa wananchi wa kijiji cha Naikula wilayani humo kabla ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya Uelimishaji,uchunguzi na Upimaji wa ugonjwa huo  ambayo itafanyika Nyumba kwa nyumba inayolenga kutokomeza kabisa kifua kikuu kabla ya mwaka 2030 katika wilaya hiyo.

WAZIRI BITEKO AWATAKA STAMICO KUSHIRIKIANA NA WANACHAMA WAO WOTE NCHINI

0
0
WAZIRI wa madini Dotto Biteko amewataka wafanyakazi wa shirika la madini nchini (STAMI O) kuendelea kushirikiana na wanachama nchi nzima hasa kwa kuwasikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili.

Akizungumza katika mkutano huo wa baraza la wafanyakazi Waziri Biteko amesema kuwa shirika hilo limepiga hatua kubwa sana hasa kwa kutoka kwenye hatua ya kuzalisha madeni ya shilingi bilioni 63 bila faida na hadi kufikia sasa hakuna hakuna deni lolote linalozalishwa.

Amesema kuwa waendeleze miradi itakayowaletea faida ikiwemo mradi wa uchorongaji ulitoa faida ya Shilingi milioni 600 na kumwelekeza Mkurugenzi mkuu kuwachukulia hatua wale wote walioonesha ubadhilifu katika mradi huo.

Vilevile amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja na kutambua mchango wa kila mmoja.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa shirika la madini CPA Dkt. Venance Mwese  amesema kuwa wamepiga hatua kubwa hasa katika masoko ya madini na shughuli za u uchorongaji kwa kandarasi nne kwa shilingi bilioni 2.2 na faida ya shilingi milioni 600.

Ameeleza kuwa wamejipanga  kuboresha shirika hilo ili kuweza kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kuongeza mapato kwa serikali na kuinua maisha ya wafanyakazi na mazingira ya ufanyaji kazi.

Aidha amesema kuwa shirika hilo limekuwa na mlengo wa kuacha utegemezi kutoka kwa Serikali ambapo katika bajeti ya mwaka huu asilimia 77 ya bajeti hiyo ya shilingi bilioni 24.5 yametokana na vyanzo vya ndani.
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza akizungumza na uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakati wa kufunga mkutano wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo uliofanyika katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Madini, Profesa Simon Msanjila akisisitiza jambo wakati wa kufunga  mkutano wa baraza la wafanyakazi cwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kilichofanyika katika ofisi za Shirika hilo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse akitoa ufafanuzi kuhusu mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika hilo kwa Waziri wa Madini Doto Biteko alipofika kufunga mkutano uliofanyika katika ofisi zao zilizopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakimsikiliza Waziri wa Madini Doto Biteko wakati wa kufunga mkutano wa baraza uliofanyika katika ukumbi wa Shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Madini Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja  na wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) 


Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images