Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 333 | 334 | (Page 335) | 336 | 337 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais wa kampuni ya Intergen Consulting Group Bw. Heejeong Choi akitia saini mkataba wa Mfumo wa Ununuzi wa Kielektroniki baina ya Kampuni yake na Bohari Kuu ya Madawa ya Serikali (MSD). Kulia kwake ni Katibu Mkuu Utumishi Bw. George D. Yambesi (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Madawa ya Serikali Bw. Cosmas Mwaifwani. 
  Katibu Mkuu Utumishi Bw. George D. Yambesi (kushoto) akimkabidhi mkataba kwa Makamu wa Rais wa kampuni ya Intergen Consulting Group Bw. Heejeong Choi wa Mfumo wa Ununuzi wa Kielektroniki utakaotumiwa na Bohari Kuu ya Madawa (MSD) mara baada ya kusaini mkataba huo.

  0 0

  Maandalizi ya mbio za 12 za Kilimanjaro Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi 2, 2014 huko Moshi yanaendelea kushika kasi baada ya waandaaji wa mbio hizo kutangaza ada za ushiriki pamoja na ratiba ya mbio hizo.

  John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kwamba mbio ndefu za 42km Kilimanjaro Premium Lager Marathon zitaanza saa 12:30 asubuhi huku mbio za 10km Gapco Disabled Marathon zikianza saa 12:45 asubuhi, Nusu Marathon km 21 saa 1 kamili asubuhi na mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run zitaanza saa moja na robo asubuhi.

   Alisema ratiba hii imepangwa kwa mtiririko huu ili kuwapa fursa washiriki wa kila mbio kuona mandhari ya mji wa Moshi na Mlima Kilimanjaro.

  Alisema kuwa viingilio vya mbio ndefu za Full Marathon km 42 viingilio itakuwa ni dola 60 kwa washiriki wa kimataifa, Tsh 6,000 kwa raia wa Afrika Mashariki na dola 30 kwa raia wa kigeni wanaoishi au kufanya kazi Afrika Mashariki wakati huku Nusu Marathon viingilio ikiwa ni dola 60 kwa washiriki wa kimataifa, shilingi 4,000 kwa raia wa Afrika Mashariki na dola 30 raia wa kigeni wanaoishi Afrika Mashariki

  Aidha, washiriki wa kimataifa kwenye mbio za walemavu za GAPCO watalipia dola 10, shilingi 3,000 kwa raia wa Afrika Mashariki na dola tano kwa raia wa kigeni wanaoishi Afrika Mashariki. Mbio hizo za walemavu zitahusisha shindano la mbio za kutumia baiskeli za mikono (Handcycle) na viti vyenye magurudumu (Wheelchair) tu. Washiriki wa kimataifa na raia wa kigeni waishio Afrika Mashariki watalipa dola mbili na raia wa Afrika Mashariki watalipa shilingi 3,000 mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run.

  Kwa mujibu wa Addison, umri wa kushiriki mbio za kilomita 42 ni miaka 21, miaka 18 kwa nusu marathon na mbio za walemavu huku kwenye mbio za kujifurahisha ikiwa ni miaka kumi. “Tutasajili washiriki kwa muda wa siku mbili kabla ya mbio ambapo kwenye hoteli ya Keys Hotel mjini Moshi tarehe 28 Februari na tarehe 1 Machi kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 11 jioni kila siku na pia uandikishwaji utafanyika Arusha tarehe 27 Februari katika eneo ambalo litatangazwa badae,” alisema.

  Mbio hizo zinadhaniwa kuwa kati ya mbio kubwa zaidi duniani za kitalii na ndio tukio kubwa zaidi la kimichezo Tanzania. Kilimanjaro Marathon ya mwaka huu inatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 6,000 wakiwemo takribani wageni 600 kutoka nchi zaidi ya 40.

  Kilimanjaro Marathon 2014 inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager (wadhamini wakuu), Vodacom Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (10km Disabled Run), FNB Tanzania, TPC Sugar, Simba Cement, KK Security, Kilimanjaro Water, Keys Hotel, TanzaniteOne na UNFPA.

  0 0

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja, Borafya Silima alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo tarehe 22-2014 kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar utakaofanyika leo.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja, Alhajj Rajab Kundiya alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo tarehe 22-2014 kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar utakaofanyika leo. 
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mgombea Uwakilishi Jimbo la KiembeSamaki CCM Mahmoud Thabit Kombo, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo tarehe 22-2014 kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo utakaofanyika leo.(Picha na OMR)

  0 0


  0 0

   Mdau Fatima Adadi Rajab akiwa katika pozi mara baada ya kulamba nondozz yake ya maswala ya Usimamizi wa Biashara (Masters in Business Administration) katika mahafali yalitofanyika hivi karibuni katika Chuo Kikuu cha Derby (University of Derby) nchini Uingereza.
  Mdau Fatima Adadi Rajab akiwa (kati) akiwa katika picha ya pamoja na Baba yake,Balozi Adadi Rajab (pili kushoto),Balozi Peter Kallaghe (Kulia),Mdogo wake Mwanaidi Adadi Rajabu (kushoto) pamoja na Mama yake Mdogo kutoka nchini Belgium,Mama Hilda wakati wa kumpongeza kwa kulamba nondozzz yake hiyo ya maswala ya Usimamizi wa Biashara (Masters in Business Administration) katika mahafali yalitofanyika hivi karibuni katika Chuo Kikuu cha Derby (University of Derby) nchini Uingereza.
  Mdau Fatima akipozi na wazee.
  Dada na Mdogo wake.

  0 0

  Marehemu Said Bwanamdogo

  0 0

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne S. Makinda (Mb), anasikitika kutoa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Saidi Ramadhani Bwanamdogo Kilichotokea leo Jumatano asubuhi tarehe 22.1.2014 Katika hospitali ya MOI DSM alipokuwa amelazwa kwa Matibabu. 
  Ofisi inaendelea na taratibu za mazishi 
  kwa kushirikiana na familia ya Marehemu.
  Inna llilah Waina Illaih Rajiun!

  SPIKA WA BUNGE,
  22.01.2014.

  0 0

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akipokea ua kama isharaya kukaribishwa tena kwenye wizara hiyo, awali dkt. Seif alikuwa Naibu Waziri kwenye wizara hiyo.
  Waziri wa afya na Ustawi wa Jamii akisalimiana na baadhi ya wakurugenzi wa wizara hiyo.
  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Kebwe S. Kebwe akisalimiana na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Donan Mmbando,pembeni ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Charles Pallangyo mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya wizara hiyo.
  Baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo wakisubiri kuwapokea Mawaziri wao wapya nje ya viwanja vya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.( Picha zote na Catherine Sungura –MOHSW).

  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akizungumza wakati wa kikao chake na Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda wa Afrika Kusini, Mhe. Elizabeth Thabethe (wa pili kushoto). Mhe. Thabete anaongoza ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Afrika Kusini utakaoshiriki Semina kuhusu Biashara na Uwekezaji itakayofanyika hapa nchini tarehe 23 Januari, 2014. Wengine katika picha ni Mhe. Radhia Msuya (kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini na Mhe. Thanduyise Chiliza, Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini.
  Mama Hellen Rwegasira (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa kikao kati ya Mhe. Maalim na Mhe. Thabethe (hawapo pichani)
  Wajumbe wengine kutoka Afrika Kusini na Tanzania wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Maalim na Mhe. Thabete (hawapo pichani). Kulia ni Bw. Adam Isara, Msaidizi wa Mhe. Maalim.
  Mhe. Maalim akiagana na Mhe. Thabete mara baada ya mazungumzo yao.
  Picha ya pamoja.

  0 0


  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, (PMTCT OPTION B+) kwa Mkoa wa Dar es Salaam katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014.
  Washiriki waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakisikiliza na kushangilia hotuba ya uzinduzi iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014.


  0 0

  Kampala, Uganda: The Chair of the Council of Ministers, Hon Phyllis C. Kandie, has reiterated the need to collectively pool strengths together if the Community is to remain relevant in the fiercely globalized world.  The Chair maintained that such a move may necessitate occasions where Partner States cede part of their sovereignty and place the same on trusted regional institutions.

  In her maiden speech to the August House this afternoon, Hon Kandie, the Cabinet Secretary for East African Affairs, Commerce and Tourism in the Republic of Kenya, undertook to address as a priority, existing challenges and sensitivities involved in the implementation of the pillars of integration. 

  She remarked that as the region enters the Monetary Union and proceeds towards the Political Federation, moments of anxiety may occasionally be realized, leading to slower pace of implementation. 


  0 0

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtambulisha mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki CCM Mahamoud Thabit Kombo kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika leo 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Ilani Katiba na Sera ya CCM mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki CCM Mahamoud Thabit Kombo kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika leo 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki. (Picha na OMR)

  0 0

  kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii imefanya ziara ya Tathmini ya siku tatu katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Tanga na kuridhishwa na utekelezaji wa Mfuko wa maendeleo ya wanawake kwani umesaidia wanawake wengi kujiendeleza na kupambana na umasikini unaomkabili mwanamke, kamati hii ilipita katika vikundi vya wanawake wajasiriamali na kushuhudia shughuli wanazo zifanya kutokana na mkopo walioupata kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF).
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe Sofia Simba (kulia) akieleza mbele ya kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii mafanikio yaliyopatikana.
  Mjasiliamali akijieleza mbele ya kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii mafanikio aliyoyapata kutokana na mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF).

  0 0

  Since launching their Foundation in 2000, Bill and Melinda Gates have granted nearly $30 billion to organization and individuals working to eradicate poverty. In an Interview on Tuesday with The Takeaway Host John Hockenberry ( National Public Radio )the couple talked about why poor countries aren't doomed to stay poor.Pictured Above: Bill and Melinda Gates with Mr. Ban Ki Moon , Secretary General of the United Nations

  0 0
 • 01/22/14--23:52: CAR FOR SALE
 • RANGE ROVER VOGUE SPORTS , MODEL 2002 , DIESEL AUTOMATIC, DUTY HAS BEEN PAYED,IMPORTED FROM LONDON , THE CAR IS ONE MONTH OLD IN DAR ES SALAAM, LEATHER SEATS,AIR CONDITION. 

   PRICE NEGOTIABLE T.SH 35,000,000 

  CONTACT: +255713333312 OR +255772333723  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano kuhusu masuala ya Uhamiaji na Watanzania waishio nje (Diaspora). Ufunguzi huo ulifanyika katika Hoteli ya JB Belmont Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Januari, 2014. Mwingine katika picha ni Bw. Jo Rispoli, Mtaalam wa masuala ya Uhamiaji katika Shirika la Kimataifa la Uhamiaji.
  Baadhi ya wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa kongamano hilo wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe (hayupo pichani)

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba (wa pili kushoto) wakati alipokuwa akimtambulisha dada zake,wakati Mh Lowassa alipokwenda kumpa pole Mzee Makamba aliepatwa na msiba wa kufiwa na mama yake mzazi huko kijijini kwake Maezangula wilaya ya Korogwe,Mkoani Tanga jana.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba wakimsikiliza Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia,Mh. January Makamba wakati wa mazungumzo yao.Mh Lowassa aliitembelea Familia ya Mzee Makamba kwa  kumpa pole kwa kupatwa na msiba wa kufiwa na mama yake mzazi huko kijijini kwake Maezangula wilaya ya Korogwe,Mkoani Tanga jana.

  0 0

  Meneja wa benki ya Azania tawi la Moshi Hajira Mmbande(mwenye suti nyeusi) akimkabidhi cheti mmoja wa wafanyakazi katika benki hiyo Tumsifu Invocarith ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya tawi hilo.
  Meneja wa benki ya Azania tawi la Moshi Hajira Mmbande(mwenye suti nyeusi) akimkabidhi cheti mmoja wa wafanyakazi katika benki hiyo happness msengi ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya tawi hilo.
  Wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la Moshi wakiwa katika picha ya pamoja na vyeti vyao walivyokabidhiwa kama sehemu ya mafanikio ya tawi hilo.
  Wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la Moshi wakiwa katika picha ya pamoja na zawadi mbalimbali walizokabidhiwa baada ya kufanikisha tawi hilo kuwa miongoni mwa matawi yaliyopata mafanikio katika kipindi cha muda mfupi.
  Wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la Moshi wakigonga Cheers kufurahia mafanikio katika tawi hilo.

  Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

  MENEJA wa benki ya Azania tawi la Moshi,Hajira Mmbande amepongeza uongozi wa benki hiyo ambao pia ni wakurugenzi kwa kuwezesha tawi hilo kuwa miongoni mwa matawi yaliyopata mafanikio ndani ya kipindi kifupi.

  Akizungumza katika hafla fupi ya kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 iliyoenda sanjari na pongezi kwa wafanyakazi wa tawi hilo Bi Mmbande aliwapongeza wakurugenzi hao ambao ni mifuko ya hifadhi ya jamii, NSSF,PPF,PSPF,LAPF na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki(EADB) pamoja na wanahisa wengine.

  Aliipongeza pia Kurugenzi ya Azania bank chini ya uongozi wa Bw Charles Singili ,watumishi wote wa banki ya Azania hususani wale wa tawi la Moshi pamoja na wateja wote wa banki ya Azania kwa ushirikiano wao wa pamoja ulioowezesha kupatikana kwa mafanikio hayo ndani ya kipindi kifupi toka kufunguliwa kwa tawi hilo mjini Moshi .

  Bi Mmbande alitoa rai kwa kila mdau wa benki ya Azania kuongeza ari ,kasi na ushirikiano katika mwaka huu mpya wa 2014 ili kuifanya benki ya Azania iwe bora zaidi na kufikisha huduma kwa kila mtanzania kama ambavyo inavyojitangaza kwa watanzania.

older | 1 | .... | 333 | 334 | (Page 335) | 336 | 337 | .... | 3272 | newer