Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110034 articles
Browse latest View live

MTENDAJI MKUU MFUKO WA UWEKEZAJI WA NORWAY KWA NCHI ZILIZOENDELEA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI


WAZIRI KAIRUKI APONGEZA JUHUDI ZA BRELA

$
0
0
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki amepongeza juhudi zinazofanywa na Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) katika kuhamasisha urasimishaji wa Biashara.

Hayo yamebainiswa leo alipohudhuria kama Mgeni rasmi kwa niaba ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika Warsha ya kwanza ya Wanawake wa Kiislamu katika ujasiriamali na Tanzania ya viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Warsha hiyo Mhe. Kairuki amesema ni muhimu sana kwa Wajasiriamali kurasimisha Biashara kwa kuwa itafungua fursa nyingi sana.

“Kurasimisha Biashara ni muhimu sana, na ninafurahi sana kuwaona BRELA hapa, kwa sababu, urasimishaji wa biashara unakuja na fursa mbalimbali ambazo zinazaidia ukuaji na kuongeza kipato”.Alisema Mhe. Kairuki.

Naye Msaidizi wa Usajili Mkuu kutoka BRELA, Bw. George Chuwa ametoa wito kwa wanawake wote wajasiriamali kusajili majina ya Biashara zao, Alama za Biashara au huduma, Usajili wa Kampuni na pia huduma zingine za BRELA.

“Natoa rai kwa wanawake wajasiriamali wote kutumia huduma za BRELA ambazo zote zinapatikana kwa njia ya mtandao. 

Huduma hizo ni pamoj na Usajili waa Majina ya Biashara, Usajili wa Alama za Biashara au Huduma, Usajili wa Kampuni, Kutoa Hataza, Kutoa Leseni za Biashara Kundi A pamoja na kutoa Leseni za Viwanda”.

Aidha Bw. Chuwa ameeleza kuwa ili kuweza kufungua huduma katika mfumo wa ORS hitaji la kwanza ni kuwa na namba ya utambulisho wa Taifa kisha kutembelea www.brela.go.tz ili kupata huduma zote. 
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki akisikiliza kwa makini jambo katika Warsha ya kwanza ya Wanawake wa Kiislamu katika ujasiriamali na Tanzania ya viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
 Msaidizi wa Usajili Mkuu kutoka BRELA, Bw. George Chuwa akiwasilisha mada kuhusu nafasi ya BRELA kufanikisha Tanzania ya Viwanda katika Warsha ya kwanza ya Wanawake wa Kiislamu katika ujasiriamali na Tanzania ya viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam

Ally Rehmtullah Azindua Duka la Kisasa la Mavazi Yaliyobuniwa na Wabunifu wa Tanzania

$
0
0
 
Naibu Waziri Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiwa ameshika moja kati ya bidhaa zilizobuniwa na Mbinufu wa mitindo ya mavazi wa Tanzania, Ally Rehmtullah mara baada ya kuzindua duka la mavazi ya aina mbalimbali yaliyobuniwa na Rehmtullah. Hafla iliyofanyika leo Chole Road Masaki jijini Dar Es Salaam  
Naibu Waziri Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akizungumza  jambo na Mbinufu wa mitindo ya mavazi wa Tanzania, Ally Rehmtullah kwenye hafla ya uzinduzi wa duka la mavazi na mitindo yaliyobuniwa na wabunifu wa Tanzania
 
Naibu Waziri Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiwa kwenye picha ya pamoja na wabunifu mbalimbali

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Yatembelea Kiwanda cha ALAF.

$
0
0

Wajumbne wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mitaji ya Umma, wakiangalia jinsi uzalishaji unavyofanyika katika Kiwanda cha ALAF jijini Dar es Salaam walipotembelea ijumaa
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa Kiwanda cha ALAF, Wilberforce Msokwa akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Bune ya Kudumu ya Mitaji ya Umma walipotembelea kiwanda hicho.
Meneja wa Usalama pakazi wa Kiwanda cha ALAF, Fredrick Nowi (katikati) akimuongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kuduma, Dk Raphael Chegeni (kushoto) wakati wajumbne wa kamati hiyo walipotembelea kiwanda hicho



Fundi Mitambo na Uzalishaji wa Kiwanda cha ALAF, Paul Luambano (kulia) akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mitaji ya Umma jinsi mitambo inavyofanya kazi wakati kamati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea kiwandani hapo kuangalia jinsi uzalishaji unavyofanyika

 
 
==========  ========  =========
 
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Raphael Chegeni, leo imefanya ziara katika kiwanda cha ALAF jijini Dar es salaam. 

Madhumuni ya ziara hii ni kuipa Kamati hiyo uelewa zaidi kuhusu shughuli mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa zinazofanywa na kiwanda hicho.

Tarehe 14 Januari mwaka huu, Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Dipti Mohanty alipata mwaliko wa kuhudhuria kikao cha Kamati hiyo ya Bunge ya Uwekezaji, ambapo alipata fursa ya kuelezea mafanikio ya kampuni hiyo na changamoto mbalimbali za kibiashara.

Kamati hiyo iliipongeza ALAF kwa mafanikio makubwa iliyopata hivi karibuni, na kuahidi kuitembelea kampuni hiyo, ahadi ambayo imetimizwa leo na Mwenyekiti wa Kamati pamoja na Wajumbe wote.

Katika ziara ya leo, Kamati imepata fursa ya kutembelea kiwanda cha ALAF na kujionea hatua za uzalishaji, bidhaa na huduma mbalimbali. Pamoja na kukutana na baadhi ya wafanyakazi wa ALAF, pia walitembelea kituo cha afya kinachotoa huduma za matibabu kwa wafanyakazi na familia zao,.

Mtendaji Mkuu, Dipti Mohanty ameishukuru Kamati ya Bunge ya Uwekezaji kwa kupata muda wa kutembelea ALAF. Mtendaji Mkuu huyo ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika juhudi zake za kujenga Tanzania ya viwanda, na kuikaribisha Kamati hiyo kutembelea ALAF tena.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji, Mhe. Raphael Chegeni, alisema wamekuja kuangalia jinsi gani wanaweza kusaidia ukuwaji wa sekta ya viwanda pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo upatikanaji wa nishati ya umeme wa hakika pamoja na malipo ya VAT zinazodaiwa kutoka kwa mamalaka ya mapato TRA.

SERIKALI YAANDAA MKAKATI WA MIAKA MITANO WA KUKUZA ZAO LA PAMBA

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imesema imetengeneza mkakati wa miaka mitano kuhusu sekta ndogo ya pamba ili kukidhi mahitaji ya soko na upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima nchini.

Kauli hiyo Imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe wakati akifungua mkutano wa kamati ndogo ya wadau wa kilimo iliyokutana jijini Dodoma.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Wakuu wa mikoa inayolima zao la pamba nchini ambao wamepokea na kujadili taarifa ya kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza changamoto zinazoikabili tasnia na kutoa mapendekezo ya utatuzi wake.

Kamati ndogo ya wadau iliundwa Octoba mwaka jana jijini Mwanza kwa lengo la kuja na mapendekezo ya utatuzi wa changamoto za zao hilo nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mh Bashe amesema kikao hicho ni uhimu ili kutengeneza mustakabali mzuri wa tasnia ya pamba kwenye mikoa 17 inayolima zao hilo.

Bashe amesema msimu ujao wa kilimo cha pamba unapaswa uwe mzuri na usiwe na matatizo licha ya mikao michache bado kuwa na takribani asilimia 20 ya pamba isiyonunuliwa hadi sasa.

“Pamba na kilimo ni biashara tusipeleke siasa.Msimu huu ulikuwa mgumu. Tumekubaliana serikalini kuwa biashara hii ifanywe kwa uwazi zaidi ili mkulima apate manufaa ya jasho lake” amesema Bashe.

Bashe amesema tayari wizara ya Kilimo imefanya majadiliano na wizara za Viwanda na Biashara na ile ya Fedha na Mipango  juu ya mustakabali wa zao hilo msimu ujao.

“ Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya  2015-2020 imeelekeza ushirika kusimamia sekta ya pamba kwa manufaa ya wakulima nchini,hivyo lazima tutafute suluhu ya changamoto za masoko “ Amesema Bashe.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya wadau wa pamba  Adamu Malima  amesema ni wakati wa wizara ya kilimo kuweka mikakati mahsusi ya upatikanaji wa bei nzuri ya pamba ya wakulima kupitia mfumo wa ushirika.

“Ushirika nchini lazima uwe na takwimu sahihi za wakulima,kiasi cha pembejeo kinachotakiwa na eneo linalolimwa ili kuepusha hasara kwa wakulima kubebeshwa madeni yasiyo wahusu” Amesema Malima.

RC Malima amebainisha kuwa suala la utafiti  na ugani kwenye zao la pamba ni muhimu lipewe kipaumbele lakini   wizara ya kilimo haioneshi jitihada.

Amesema Wizara ya Kilimo inatakiwa pia kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo za pamba kwa wakati na zenye ubora  kuhakikisha zinawafikia kwa wakati na bei nafuu.

Kikao hiko maalum cha wadau wa Pamba kimehudhuriwa na Wakuu wa Mikoa ya Mara, Simiyu, Morogoro, Kagera,Kigoma, Singida, Mwanza, Geita, Shinyanga, Kilimanjaro na  Katavi.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe akizungumza na Wakuu wa Mikoa inayolima Pamba Katika mkutano wa kujadili zao hilo uliofanyika jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza na Wakuu wa Mikoa inayolima Pamba sambamba na wadau wa zao hilo wakati akifungua mkutano wa pamoja wa kujadili maendeleo ya zao hilo linalolimwa takribani Mikoa 17 nchini. Mkutano huo umefanyika jijini Dodoma.
 Baadhi ya Wakuu wa Mikoa inayolima Pamba wakifuatilia mkutano wa pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe na wadau wa zao hilo jijini Dodoma.
 Wadau mbalimbali wa zao la Pamba wakifuatilia mkutano wao wa pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe na Wakuu wa Mikoa inayolima zao hilo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe Rehema Nchimbi akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa wenzake wanaolima Pamba Katika mkutano wa kujadili maendeleo ya zao hilo uliofanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe.

Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri waagizwa kubadilika kiutendaji

$
0
0

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na wadau wa michezo wa Jiji la Arusha alipokua katika ziara ya kujadili maendeleo ya sekta hiyo pamoja na kutatua changamoto wanazokutana nazo wadau hao iliyofanyika Januari 25,2020.Kulia ni Katibu tawala Wilaya ya Arusha mjini Bw.Davis Mwaiposa.
Katibu tawala Wilaya ya Arusha mjini Bw.Davis Mwaiposa akizungumza na wadau wa michezo wa Jiji la Arusha  katika ziara ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe na wadau hao kujadili maendeleo ya sekta hiyo pamoja na kutatua changamoto wanazokutana nazo iliyofanyika Januari 25,2020.
Afisa Michezo wa Mkoa wa Arusha Bibi.Mwamvita Okeng”o akizungumza na wadau wa michezo wa mkoa huo katika ziara ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe na wadau hao   kujadili maendeleo ya sekta hiyo pamoja na kutatua changamoto wanazokutana nazo iliyofanyika Januari 25,2020.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bw.Maulid Mgeni akizungumza na wadau wa michezo wa mkoa huo katika ziara ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe na wadau hao   kujadili maendeleo ya sekta hiyo pamoja na kutatua changamoto wanazokutana nazo iliyofanyika Januari 25,2020.
Baadhi ya wadau wa Michezo  wa mkoa wa Arusha wakitoa maoni yao wakati wa kikao cha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe na wadau hao   kujadili maendeleo ya sekta hiyo pamoja na kutatua changamoto wanazokutana nazo iliyofanyika Januari 25,2020.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Arusha pamoja na wadau wa michezo mkoa huo mara baada ya kumaliza mkutano wa  kujadili maendeleo ya sekta hiyo pamoja na kutatua changamoto wanazokutana nazo wadau hao uliofanyika Januari 25,2020.
…………….

Na Shamimu Nyaki – WHUSM Arusha

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe amewaagiza maafisa michezo wote chini kubadilika katika utendaji wao kutokana na kulalamikiwa na wadau wengi wa michezo namna ambavyo wanashughulikia sekta hiyo

Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo jana Jijini Arusha alipokutana na wadau wa michezo kujadili maendeleo ya sekta hiyo ambapo amewataka maafisa michezo kuhakikisha masuala ya michezo katika maeneo yao hayakwami kutokana na wao kutowajibika.

“Nyinyi ni watumishi wa Serikali mnaposhindwa kutatua kero za wanamichezo na kusimamia sekta hii basi nyie hamtoshi na mimi sitawavumilia kuona mnakwamisha maendeleo ya michezo nchini”alisema Dkt.Mwakyembe.

Aidha Mhe.Waziri ameliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ifikapo Februari mosi 2020,liwe limewasilisha mapendekezo ya mabadilio ya Katiba ya Chama cha Riadha nchini ili kupata muongozo wa mchezo huo.
Mhe.Waziri ameongeza kuwa Serikali imerudisha michezo ya UMITASHUMTA na UMISETA ili kuhakikisha sekta hii inaendelea kukua na kuletea heshima taifa, huku akieleza kuwa Serikali inadhamiria kutofautisha viwanja vya sanaa na vya michezo kwasabu sekta hizi zina wadau wengi ambao wamekuwa na matukio yanayofanana na  yanayofanyika kwa wakati unaofanana hivyo ni vyema kila sekta ikajitegema katika maonyesho yake.
Vile vile Dkt.Mwakyembe amevitaka vilabu vya michezo na mashirikisho kuona umuhimu wa kutumia wanamichezo wa ndani ili kuinua vipaji walivyonavyo lakini pia kuwapatia ajira kuliko kusajili wachezaji wa nje wengi na kuwaacha wazalendo.

Kwa upande wake Afisa Michezo wa Mkoa Bibi  Mwamvita Okeng’o amesema kuwa Mkoa wa Arusha unaendelea kufanya vizuri katika michezo na unaendelea kukuza sekta hiyo kwa kuongeza idadi ya viwanja na tayari mipango imeanza ya kujenga uwanja kila Wilaya ya mkoa huo.

Katika hatua nyingine Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha Bw.Wiliam Kalaghe amesema kuwa maandalizi ya wanamichezo Alphonce Simbu na Failuna Abdu ambao wataliwakilisha Taifa mwaka huu katika mashindano ya Olympiki  huko Japan yanaendelea vizuri na tayari shirikisho hilo limetoa kiasi cha Sh. Milioni 03 kama chagizo la maandalizi hivyo watanzania wanapaswa kuwaunga mkono.

Naye Bw.Hamis mdau wa mchezo wa mpira wa miguu ameshauri wanamichezo kujifunza lugha na namna bora ya kufanya mahojiano ili wanapokuwa wamepata nafasi ya kucheza soka nje wasikwame kwa kigezo cha kushindwa kujibu maswali au kutumia lugha Fulani.

SERIKALI KUPELEKA MAWASILIANO YA SIMU SINGIDA MASHARIKI

$
0
0

NAIBU Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye,akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe.Miraji Mtaturu mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Msule kilichopo Kata ya Misugha ambacho kinatarajiwa kupata mawasiliano ya simu mwaka huu.
Wananchi wa kijiji cha Msule kilichopo Kata ya Misugha ambacho kinatarajiwa kupata mawasiliano ya simu mwaka huu wakifatilia hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe.Miraji Mtaturu alipokuwa akiongea nao.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe.Miraji Mtaturu akisalimiana na mmoja wa wazee wa kijiji ambaye pia ni mwenyekiti wa Amcos Misughaa(katikati) Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye mara baada ya kuongea na wananchi wa kijiji cha Msule kilichopo Kata ya Misugha ambacho kinatarajiwa kupata mawasiliano ya simu mwaka huu.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe.Miraji Mtaturu akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Edward Mpogolo (katikati) ni Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye mara baada ya kuongea na wananchi wa kijiji cha Msule kilichopo Kata ya Misugha ambacho kinatarajiwa kupata mawasiliano ya simu mwaka huu.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msule kilichopo Kata ya Misugha Jimbo la Singida Mashariki ambacho kinatarajiwa kupata mawasiliano ya simu mwaka huu.
,akiwasili katika kijiji cha Msule kilichopo Kata ya Misugha jimbo la Singida Mashariki akiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe.Miraji Mtaturu.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe.Miraji Mtaturu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msule kilichopo Kata ya Misugha ambacho kinatarajiwa kupata mawasiliano ya simu mwaka huu.



………….

NAIBU Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amelielekeza shirika la mawasiliano Tanzania(TTCL)kujenga mnara wa simu katika kijiji cha Msule kilichopo Kata ya Misugha jimbo la Singida Mashariki na kuhakikisha hadi Agosti mwaka huu wawe wamewasha mawasiliano rasmi.

Agizo hilo linafuatia ombi la mbunge wa jimbo hilo Miraji Mtaturu aliyeiomba serikali kupeleka mawasiliano ya simu kwa wananchi.

Akizungumza katika ziara yake ya kikazi jimboni humo ,mhandisi Nditiye amesema serikali imesikia kilio cha wananchi kupitia ombi la mbunge hivyo ni ahadi yao kwao kuwa watajibu ombi hilo kwa wakati.

“Ilani yetu ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)imeelekeza serikali kuhakikisha inafikisha mawasiliano kwa wananchi,na serikali yetu chini ya Rais Dokta John Magufuli ni sikivu,hivyo niahidi kwenu kuwa changamoto hii itapatiwa ufumbuzi,”alisema Mhandisi Nditiye.

Awali akitoa ombi hilo Mtaturu amesema wananchi wa Kata za Misughaa,Kikio na Ntuntu wana changamoto kubwa ya mawasiliano ya simu hivyo ni matarajio yao kuwa ombi hilo litasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi.

“Mheshimiwa naibu waziri juzi nilikuomba uje ujionee hali ya wananchi wangu ilivyo katika sekta ya mawasiliano,na nashukuru umekubali wito wangu umefika na umeshuhudia simu ulizokuwa nazo mwenyewe hazisomi mtandao wowote,kwa niaba ya wananchi hawa naomba tujengewe mnara ili kurahisisha mawasiliano ya kibiashara na kijamii kwani mawasiliano ndio kichocheo kikubwa cha maendeleo,”alisema Mtaturu.

Aidha upande wa barabara ameiomba serikali kutenga fedha ili kujenga barabara ya njia panda ya Singida kwa Mtoro kupitia Kiblashi hadi Tanga yenye urefu wa kilomita 461 kwa kiwango cha lami.

“Tangu mwaka 2017 serikali imemaliza kufanya upembuzi yakinifu kwenye barabara hiyo,tunachoomba sasa ni kutengwa kwa fedha ili barabara hiyo ijengwe kwa kuwa ni muhimu katika ukuaji wa uchumi kutokana na kugusa mikoa mitatu ya Dodoma,Singida na Tanga,”aliongeza Mtaturu.

Mbali na maombi hayo amemshukuru Rais Magufuli kwa kupeleka fedha nyingi katika miradi mbalimbali kwenye sekta ya elimu,afya na miundombinu ya mawasiliano katika maeneo mengine ya jimbo hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo ameeleza umuhimu wa mawasiliano kiusalama na katika kuchochea maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Kwanza nikushukuru Mbunge kwa kumualika kiongozi wetu aje ajionee kwa macho changamoto iliyopo kwenye wilaya yetu,ila tu nikuombe mbali na maeneo uliyoyataja,utusaidie pia kwenye maeneo mengine kama ya Ighombwe,Mgungira na Iyumbu ambako nako pia mawasiliano ni shida,”alitoa ombi Mpogolo.

Katika ziara hiyo mhandisi Nditiye ametoa Printer moja kwa shule ya sekondari ya Dokta Ally Mohamed Shein na kuahidi kutoa computer 25 zitakazogawanywa kwenye shule tano za sekondari zilizopo wilayani humo ambazo zitaunganishwa na internet ili zitumike kufundisha kwa njia ya masafa,msaada ambao umeahidiwa pia na mbunge Mtaturu.

Rais wa China atoa angalizo dhidi ya virusi vya corona

$
0
0
 Mlipuko wa virusi vipya vinavyouwa vinasambaa kwa kasi, Rais Xi Jinping ametoa tahadhari baada ya kufanya kikao maalum katika siku ya mwaka mpya wa Lunar.

Rais aliwaambia maofisa wa ngazi za juu kuwa nchi iko kwenye hali ya hatari kubwa , kwa mujibu wa televisheni ya taifa.Virusi vya corona tayari vimeuwa watu wapatao 41 na wengine 1,400 wameambukizwa tangu virusi hivyo vigundulike huko Wuhan.

Tayari miji mingi imeweka katazo la kusafiri kwa watu wake.
Na siku ya jumapili hata magari binafsi hayataruhusiwa kutoka Wuhan, eneo ambalo virusi hivyo viibainika kwa kwa mara ya kwanza.

Hospitali nyingine ya dharura inajengwa na inategemewa kuwa ndani ya wiki , itaweza kuwahudumia wagonjwa wapya 1,300, na itamalizika kujengwa ndani ya nusu mwezi, gazeti la serikali la la People's Daily limeripoti.


Wananchi Waipongeza NBS kwa Kufanya Tafiti Zinazochochea Maendeleo Endelevu

$
0
0

Gari lililowabeba wadadisi kutoka Ofisi ya Takwimu (NBS) likiwa limenasa katika Kitongoji cha Bacho A, Kata ya Dareda Wilayani Babati mkoani Manyara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo wakati wa Utafiti wa Feed the Future unaendelea kufanyika.
 Wadadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS wakimpima urefu mkazi wa Kitongoji cha Bacho A, Kata ya Dareda Wilayani Babati, mkoani Manyara Bi. Pascalina Martin wakati wa Utafiti wa Feed the Future unaoendelea kufanyika.Kushoto ni mdadisi kutoka NBS Bw. Hamis Sozigwa na kulia ni Bi. Albina Gabriel.
Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi.Getrude Rwehumbiza akifanaya mahojiano na moja ya familia katika Kitongoji cha Bacho A, Kata ya Dareda Wilayani Babati mkoani Manyara wakati wa utafiti wa Utafiti wa Feed the Future unaendelea kufanyika. (Picha zote na NBS)
Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Albina Gabriel akimpima uzito mtoto Fabiano Christopher wa Kitongoji Bacho A, Kata ya Dareda Wilayani Babati mkoani Manyara wakati wa Utafiti wa Feed the Future unaendelea kufanyika.








Kiongozi wa timu ya Wadadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Respicius Gaspar (katikati) akisisitiza jambo kwa mkazi wa Mangoya Kitongoji cha Bacho A, Kata ya Dareda Wilayani Babati, mkoani Manyara Bw. Patrice Martin Ami walipomtembelea nyumbani kwake kwa mahojiano wakati wa utafiti kuhusu hali ya Kaya, upatikanaji wa chakula, huduma za afya, ushirikishwaji wa wanawake katika kufanya maamuzi na masuala mengine yanayolenga kuleta ustawi wa wananchi. Kushoto ni mdadisi kutoka NBS Bw. Hamis Sozigwa, Utafiti huo unajulikana kama utafiti wa Feed the Future unaoendelea kufanyika.
Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Albina Gabriel akifanya mahojiano na mkazi wa Kitongoji cha Bacho A, Kata ya Dareda Wilayani Babati Mzee Lohay Luhiyo Magara wakati wa utafiti kuhusu hali ya Kaya, upatikanaji wa chakula, huduma za afya, ushirikishwaji wa wanawake katika kufanya maamuzi na masuala mengine yanayolenga kuleta ustawi wa wananchi, Utafiti huo unajulikana kama utafiti wa Feed the Future unaendelea kufanyika.
Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Amina Jumanne akisisitiza jambo kwa mkazi wa Kitongoji cha Bacho A, Kata ya Dareda Wilayani Babati Bi. Sophia Petro wakati wa Utafiti wa Feed the Future unaendelea kufanyika.


Na Mwandishi Wetu- Manyara

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imepongezwa na wananchi mkoani Manyara kwa kufanya tafiti zinazolenga kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Pongezi hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki katika mahojiano maalum na wananchi wa Dareda mkoani Manyara ambako Utafiti wa Feed the Future unaendelea kufanyika.

Bw. Patrice Martin Ami mkaazi wa Dareda mkoani humo amesema utafiti huo utaiwezesha Serikali kubaini hali halisi ya maisha ya wananchi wake na hivyo kuchukua hatua stahiki kulingana na matokeo ya utafiti huo yatakapotolewa.

“Tunaamini kuwa utafiti huu unafanyika kwa maslahi ya wananchi na utawezesha wananchi kupiga hatua baada ya kukamilika kwake kwa kuonesha hali halisi katika masuala yote yanayofanyiwa utafiti” alisisitiza Ami.

Utafiti wa Feed the Future ambao unaangalia hali ya ustawi katika kaya ikiwemo upatikanaji wa chakula, aina ya milo katika kaya kwa wanawake, huduma za afya, udumavu kwa watoto na nafasi ya mwanamke katika kufanya maamuzi unafanyika katika mikoa Dodoma, Iringa, Manyara, Mbeya, Morogoro pamoja na mikoa ya Zanzibar.

Bwana Ami alimueleza mwandishi wetu kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejikita katika kuhakikisha kuwa inawaletea wananchi maendeleo katika nyanza zote hivyo utafiti huo ni sehemu ya nyenzo muhimu kwa Taifa lolote kufikia maendeleo.

Kwa upande wake, Mkazi wa mwingine wa Dareda, Bw. James Sebastian amesema kuwa utafiti huo utasaidia kuongeza kasi ya maendeleo katika maeneo yao baada ya ripoti ya mwisho kutolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Aidha, utafiti huo utakapokamilika unatarajiwa kuwa kichocheo cha maendeleo katika maeneo yote yatakayohusika.

Utafiti huo unafadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la nchi hiyo (USAID) na kutekelezwa kwa pamoja na Benki ya Dunia na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

RAS TABORA AWATAKA MAOFISA TARAFA KUHAKIKISHA KERO ZA WANANCHI ZINATATULIWA KATIKA MAENEO WANAYOSIHI

$
0
0
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akifungua kikao kazi cha siku moja cha Maofisa Tarafa wanaotoka Wilaya zote za Mkoa huyo kwa ajili ya kuwajengea uwezo..Maofisa Tarafa za Mkoa wa Tabora wakiwa katika kikao kazi cha siku moja kilichoitishwa na katibu Tawala Mkoa wa Tabora

………………………………………………………….

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imewataka Maofisa Tarafa kutatua kero na migogoro inayowakabili wananchi katika maeneo yao badala ya kuwaacha bila usaidizi na kuwafanya kukimbilia kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kutafuta haki zao.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alipokuwa na Kikao kazi cha siku moja na Maofisa Tarafa wa Tarafa zote za wilaya zote za Mkoa huo.

Alisema ni jukumu la Maofisa hao kuhakikisha wanashughulikia migogoro ya ardhi, kuondoa madai ya wananchi kuombwa rushwa, mauaji na matumizi mabaya ya madaraka inayofanywa na Watendaji walioko chini yao ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri na wanayotarajia.

Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora alisema ni vema wakasimama vema katika nafasi zao za uongozi ili kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kutoka wanapoishi hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutafuta haki zao.

“Sifurahishwi kuona wananchi wengine ni wazee sana wameshindwa kusaidia kule wanapoishi na kuamua kuja katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kumuona Mkuu wa Mkoa au mimi ili niwasikilize kero zao ambazo kimsingi zilitakiwa kutatuliwa na viongozi walio karibu nao ambao wengine wao ni ninyi Maofisa Tarafa ” alisema.

Makungu alisema kuwa Maofisa Tarafa ndio kiungo kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa ni vema wakahakikisha kuwa shughuli zote zinazofanyika katika maeneo yao ya utawala yanazingatia Sheria za Nchi na zinatolewa kwa haki kwa wananchi wote.

Aidha Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora amewataka Maofisa Tarafa kuhakikisha mapato ya Serikali yanakusanywa na kudhibiti Wafanyabiashara wanaokwepa kodi za Serikali.

Alisema kuna baadhi ya wafanyabiashara bado wanaendesha shughuli bila kulipa kodi zinazotakiwa kwa mujibu wa Sheria.

MNUSO WA SHEREHE YA MIAKA 50 YA SIKU YA KUZALIWA YA PETER KIRIGITI, COLUMBUS, OHIO

$
0
0
Keki ya kusherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Peter Kirigiti miaka 50 iliyopita siku ya January 18, 2020 jijini Columbus, Ohio.
Birthday boy akikata keki tayari kumlisha mkewe na watoto waliozunguka meza,
Watoto wakiwa tayari kula keki.
Birthday boy akijiandaa kukata keki.
Birthday boy akijuandaa kumlisha keki mke wake.
Peter akimlisha keki mkewe.
Peter akitoa neno la shukurani. Bofya soma zaidi kwa picha zaidi

 

NAIBU WAZIRI MABULA AZITAKA HALMASHAURI KUTENGA BAJETI ZA MABARAZA YA ARDHI YA KATA NA VIJIJI

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na vibarua wa mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Obadia Kita na Yusufu Kijalo wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya mradi huo unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwenye Shamba la Misitu la Iyondo Msimwa Ileje mkoani Songwe mwishoni mwa wiki. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude (kulia kwake) kwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Meneja Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kwenye Shamba la Miti la Iyondo Msimwa wilayani ileje mkoa wa Songwe mwishoni mwa wiki alipokwenda kukagua mradi huo unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Kulia), Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Muungano Saguya, Mkuu wa wilaya ya Ileje Joseph Mkude na Kaimu Meneja wa NHC mkoa wa Mbeya Pauline Kamaghe wakitazama maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Meneja Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwenye Shamba la Miti la Iyondo Msimwa wilayani ileje mkoa wa Songwe mwishoni mwa wiki alipokwenda kukagua maendeleo ya mradi huo unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Mkuu wa wilaya ya Ileje Joseph Mkude akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati Naibu Waziri alipotembelea wilaya ya Ileje kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi pamoja na ujenzi wa miradi inayofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mwishoni mwa wiki. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisisitiza jambo alipozungumza na viongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Songwe.Anayemuangalia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemus Mwangela.

(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

…………………………………………………………

Na Munir Shemweta, WANMM ILEJE

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutenga bajeti kwa ajili ya Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji sambamba na kufuatilia tozo zinazotozwa na Mabaraza hayo ili yafanye kazi kwa ufanisi.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wilayani Ileje na Mbozi wakati akizungumza na viongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na ujenzi wa miradi inayofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani Songwe.

Naibu Waziri Mabula alisema, Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wamekuwa hawatengi bajeti kwa ajili ya Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji jambo linalosababisha Wajumbe wake kujifanyia mambo wanavyotaka ikiwemo kuweka viwango tofauti vya tozo za kwenda uwandani.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji yanapaswa kusimamiwa na Wakurugenzi wa Halmashauri kwa kuyapatia kwa kuyatengea bajeti za kuendesha ofisi kama vile Shajala sambamba na kujua yanayofanyika ikiwemo tozo zake ili kuepuka uonevu unaoweza kujitokeza kwa wananchi wanaoshitakiana.

‘’Katika Mabarza ya Ardhi ya Kata na Vijiji watu wanalipa tozo kulingana na sura kama mtu kavaa tai basi anapigwa shilingi elfu hamsini jambo linalowaumiza wananchi’’ alisema Mabula

Alizitaka ofisi za Wakurugenzi wa halmashauri nchini kuyasimamia Mabaraza hayo na kutoa semina kwa wajumbe wake na kuyapangia viwango vya tozo na kusisitiza kuwa hayo yasipofanyika kuna hatari wajumbe wake kufanya maamuzi kwa matakwa ya wenye uwezo.

Amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kubadilika katika kuyasimamia mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji na kubainisha kuwa Mabaraza hayo yakifanya vizuri yatapunguza mlundikano wa kesi za ardhi zinazokwenda Mabaraza ya ardhi ya nyumba ya Wilaya.

Awali Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe Dismas Ndinda alimueleza Naibu Waziri Mabula kuwa halmashauri hiyo pamoja na kuwa Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji sabini na moja lakini haina Baraza la ardhi la wilaya jambo linalowafanya wananchi wanaoshindwa kupata suluhu kusafiri hadi Mbeya kupata huduma za Baraza la Ardhi la Wilaya.

Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi na nyumba ya Meneja ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika shamba la Miti la Iyondo Msimwa wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe.

Akikagua maendeleo ya ujenzi huo, Dkt Mabula mbali na kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo alisema mradi wa ujenzi wa ofisi na nyumba ya Meneja wa TFS utasaidia ufuatiliaji wa msitu huo kwa kuwa Meneja wake atakuwa akiishi karibu na msitu huo. Aidha, ameuelezea mradi huo kuwa umesaidia pia kutengeneza ajira ya muda kwa wakazi wa eneo hilo na kuwawezesha kupata kipato cha mahitaji madogomadogo.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa NHC mkoa wa Mbeya Pauline Kamaghe alisema mradi huo unaojengwa na Shirika lake unatarajiwa kugharimu kiasi cha milioni 426.8 na kukamilika mwezi April mwaka huu wa 2020 na kubainisha kuwa kwa sasa mradi umefikia asilimia 38 ya ujenzi.

VULLU AHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA UBIRESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

$
0
0







****************************
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu, amewaasa viongozi wa kisiasa na wa Serikali kuwahimiza wananchi kujitokeza katika zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura.
Lengo kubwa ni kwa wananchi hao kuweza kishiriki zoezi la kupiga kura katika chaguzi zinazotarajia kufanyika mwaka huu 2020, kuanzia Udiwani, Ubunge na Rais.
Vullu alitoa rai hiyo katika Kijiji cha Kisangile, Kata ya Marui wilaya ya Kisarawe akiwa kwenye ziara iliyoratibiwa na Jumuiya ya Wanawake ya (UWT) ya chama hicho.
Alisema ,zoezi la uboreshaji wa daftari la wapigakura linalotaraji kuanza Feb 2 litalodumu kwa siku saba, limeandaliwa na serikali kwa lengo la kuwapatia nafasi wa-Tanzania kuhakiki majina yao kwenye daftari hilo.
“Serikali imeandaa daftari hilo kwa lengo la kuwapatia fursa wananchi kuhakiki majina yao, hatua itayomwezesha mlengwa kupara nafasi ya kushiriki zoezi la kupiga kura kwa kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi,” alisema Vullu.
Aidha alitolea ufafanuzi wa tofauti wa kadi ya kupigia kura na kitambulisho cha taifa, baada ya mkazi aliyejitambulisha kwa jina la Khalfan Mussa kuhoji utofauti wa kadi hiyo ya kupigiakura na kitambulisho cha taifa.
Nae Sophia ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya hiyo alielezea, zoezi hilo litakalodumu kwa wiki moja halitakuwa na muda wa nyongeza, hivyo amewaasa wana-Kisarawe kuchangamkia fufsa hiyo ili waweze kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
Diwani wa Kata hiyo Salehe Mfaume alieleza,wamejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa mafanikio makubwa.

TANZANIA, INDIA ZAAHIDI KUENDELEZA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA, KUKUZA MAENDELEO

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiwasilisha hotuba yake wakati wa maadhimisho ya miaka 71 ya Jamhuri ya India yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Ubalozi wa India jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Balozi wa India nchini Tanzania, Dan Kohli
Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Balozi Shri Sanjiv Kohli akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 71 ya Jamhuri ya India yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Ubalozi wa India jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro. Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia/kusikiliza hotuba ya mgeni rasmi (Dkt. Ndumbaro) hayupo pichani wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 71 ya Jamhuri ya India yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Ubalozi wa India …………………………………………………………..

Tanzania na India zimeahidi kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia pamoja na kushirikiana katika kuhakikisha kuwa na maendeleo endelevu baina ya nchi hizo mbili.

Akihutubia sherehe za maadhimisho ya 71 ya Jamhuri ya India, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesema kuwa Tanzania na India ni ndugu na nchi hizo zitaendelea kushikiana katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya diplomasia ya uchumi baina ya nchi hizo yanakuwa kila wakati.

“Nchi ya Tanzania na India zina uhusiano mzuri, imara na wa muda mrefu ulianzishwa na baba wa Taifa Mwl. Julias Nyerere pamoja na Mahatma Gandhi. Na uhusiano huu umekuwa ukisaidia kuimarisha maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa” alisema Dkt. Ndumbaro

Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa “sisi Tanzania na India ni ndugu, kwa hiyo basi tunawatakia sana kila la kheri katika kuiletea India maendeleo…lakini pia tukumbuke kuwa maendeleo ya India ni maendeleo ya Tanzania pia,”

Kwa sasa uchumi wa India na Tanzania umezidi kukuwa na kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya mataifa hayo. India imekuwa msharika mzuri wa maendeleo nchini Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo utalii, maji, afya, teknolojia na elimu. Msaada wa India katika sekta ya maji hadi sasa, imeweza kusaidia kusambaza maji safi na salama katika kwa jiji la Dar es Salaam pamoja na upanuzi na uboreshaji wa mitambo ya maji Zanzibar.

Aidha, kwa upande wa sekta ya elimu, Tanzania na India zimeshasaini makubaliano ya kushirikiana kujenga kituo cha ufundi na pia msaada wa kuendeleza vyuo vikuu vya Zanzibar ambavyo vinatoa ujuzi unaolengwa kuwaendeleza wanawake walio na elimu ndogo au isiyo rasmi.

Kwa upande wake, Balozi wa India chini Tanzania, Mhe. Balozi Shri Sanjiv Kohli ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa umoja na mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa India na kusema kuwa umoja huo umekuwa ni chachu ya maendeleo kwa Tanzania na Taifa la India.

“Napenda kuwafahamisha kuwa umoja na mshikamano wetu umekuwa chachu ya maendeleo baina ya mataifa haya mawili…..tukumbuke kuwa umoja ni nguvu na dhamira yetu ni kushirikiana na mataifa yote duniani. Na dhamira yetu ni kuishi kwa amani umoja na mshikamano ili kukuza uchumi wetu,” Alisema Balozi Kohli

Aidha, Balozi Kohli amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuwa ya kipekee kwa taifa la India kutokana na mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa nchi ya India kijamii, kisiasa na kiuchumi.

“India inajivunia kuwa na uhusiano na mzuri na Tanzania ambao umewezesha mataifa haya kufanya biashara, uwekezaji, kujenga uwezo, ujenzi wa miundiombinu pamoja na maendeleo ya kiuchumi,” ameongeza Balozi Kohli.

WIZARA YAHAMASISHA VIJANA WA BODA BODA PAMOJA NA WANAFUNZI KUHUSU TISHIO JIPYA LA UKIMWI

$
0
0

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Matias Haule akitoa elimu ya maambukizi ya UKIMWI kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Viganga na Shule ya Sekondari Mnyakongo zilizoko nje kidogo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa jana Wilayani humo.
Mtaalam Mhamasishaji wa Masuala ya Ukimwi kutoka TACAIDS Bw. Simon Ngaweye akitoa elimu ya maambukizi ya UKIMWI kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Viganga na Shule ya Sekondari Mnyakongo zilizoko nje kidogo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.

********************************

Na Mwandishi wetu Dodoma

Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii mefanya kampeini ya kujilinda na maambukizi ya UKIMWI kwa vijana wa bodaboda na wanafunzi wa Sekondari na shule za Msingi Wilayani Kongwa na kuwataka vijana hao kujilinda dhidi ya maambukizi hayo kwani takawimu zilizopo sasa zinaonesha maambukizi yanaongezeka kwa vijana walio katika umri wa miaka kati ya 18-24.

Akiongea na wazee pamoja na viongozi wa dini Wilayani Kongwa Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Matias Haule aliutaja ugonjwa wa UKIMWI kuwa ni tishio kwa vijana wa rika hiyo kwani maambukizi hayo kwa Siku yanawapata watu 200 kwa siku na katika idadi hiyo vijana ni 79 ambapo idadi ya wasichana peke yake wanaoambukizwa kwa siku ni 63 ukilinganisha na wavulana 14.

Bwana Haule aliwaambia viongozi hao wa dini pamoja na wazee kuwa ni kutokana na hali hiyo ya maambukizi Nchini Wizara imekuja na kampeini iitwayo Timiza Malengo ili kuwafanya vijana na wote Nchini kujilinda dhidi ya ugonjwa huo ili waweze kutimiza malengo ya kimaisha waliyojiwekea.

Mara baada ya kupokea taarifa hiyo Kiongozi wa Kanisa la Anglikani Wilayani Kongwa Mchungaji Luzineth Kingamkono alisema katika Kitabu cha Kutoka ambacho ni cha pili katika Biblia Sura ya Ishirini haya ya Saba mstari wa kumi nanne inasema usidhini kwa lengo la kukataza binadamu kutojihusisha zinaa kabla ya wakati.

Aidha kiongozi huyo wa kanisa hilo uku akiendelea kutumia kitabu hicho kitakatifu alisema katika Kitabu cha Wakolinto Sura ya saba inasema kwasababu ya zinaa kila mtu na awe na mke wake wake na kwa maana hiyo Mungu alipotoa amri hiyo katika zile amri kumi za Mungu alilenga kuwakataza wale walio tayari katika ndoa lakini pia kuwataka wale mbao hawajaoa wala kuolewa kusubiri wakati wao.

Aidha ni kwa mkutadha huo basi Kiongozi wa Baraza la Waislam Wilaya ya Kongwa Bw. Yahaya Said ameiomba Serikali kuacha kutoa vibari vya muziki kwa watoto yaani disko toto kwa kuwa haoni kama watoto wadogo wana kitu cha maana wanachojifunza kwa kuwepo disko toto katika jamii zaidi ya kuwaanda kupenda starehe katika maisha yao.

Pamoja na Wizara kukutana na wazee hao wa Wilaya ya Kongwa Wizara pia ilikutana na vijana wa Bodaboda wanaofanya kazi zao maeneo ya Kibaigwa kando ya barabara kuu iendayo Dodoma toka Dar es Salaam na kuwataka kujilinda na UKIMWI kufuatia magari kubwa ya biashara kutumia eneo hilo kutokana na uwepo wa Soko la Kimataifa la mahindi.

Mtoa mada za UKIMWI kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS Bw. Simon Ngaweye aliwataka vijana wa Boda boda kutokubali kushawishiwa kufanya ngono ili waweze kutimiza malengo yao ya kukua kibiashara na kuwataka kuamini inawezekana kuishi bila ukimwi endapo wataweza kujilinda.

Aidha Bw. Salim Ally Manyumba mfanyabiashara wa Kibaigwa Wilayani Kongwa ameiomba serikali kutoa elimu ya maambukizi ya UKIMWI kwa vijana wa boda boda kutokana na changamoto wanayaokutana nayo ya kurubuniwa na baadhi ya wanawake wanaotaka kujiridhisha kimapenzi kwa kuwa bodaboda ni rahisi kuingia katika mitego yao kutokana na wao kufanya biashara kwa karibu na vijana hao.

Wizara ya Afya Maendealeo ya Jamii kwa Kushirikiana na TACAIDS pamoja na Shirika la TASAF wako Mkoani Dodoma kutembelea wasichana barehe na wanawake vijana pamoja na Shule mbalimbali Mkoani humo kwa lengo la kuhamasisha vijana juu yatishio jipya la maambukizi ya UKIMWI kwa vijana na zoezi hili litaendelea kwa Mkoa wa Morogoro na baadae Nchi Nzima.

Vodacom Tanzania plc yaionesha PAPU namna inavyoweza kuhusika kwenye ujumuishwaji kifedha( financial inclusion)

$
0
0
Mkuu wa mauzo wa Vodacom kanda ya kaskazini, Brigita Stephen (kulia) akizungumza jinsi ambavyo kampuni ya Vodacom inaweza kuwa mshirika na PAPU katika ujumuishwaji wa kifedha (financial inclusion) kwenye mkutano wa Pan African Postal Union (PAPU) uliofanyika jijini Arusha. Pembeni ni Naibu katibu mkuu wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Dkt. Jim Yonaz.
  
Mkuu wa mauzo wa Vodacom kanda ya kaskazini, Brigita Stephen (kulia) akizungumza jinsi ambavyo kampuni ya Vodacom inaweza kuwa mshirika na PAPU katika ujumuishwaji wa kifedha (financial inclusion) kwenye mkutano wa Pan African Postal Union (PAPU) uliofanyika jijini Arusha. Pembeni ni Naibu katibu mkuu wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Dkt. Jim Yonaz.

Uhalifu umepungua Zanzibar-Masauni

$
0
0


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amezungumza hali ya usalama visiwani Zanzibar akisema imeimarika huku akisisitiza kuwa msimamo wa kuzuia mikutano yote ya siasa isiyofuata utaratibu upo pale pale.

Katika maelezo yake Masauni alisema muda wa siasa ukifika watu wataruhusiwa kuendesha mikutano mbalimbali yenye lengo la kueleza kwa wananchi walichokifanya kwa muda waliopewa nafasi baada ya kuchaguliwa na kuteuliwa katika nafasi mbalimbali.

Ameeleza hayo akitoa taarifa ya usalama na uhalifu visiwani hapa Zanzibar katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana katika mahojiano na kituo kimoja cha redio.

Katika mazungumzo hayo Masauni alianza kuzungumzia mauaji ambapo alisema mwaka 2018 jumla ya matukio 40 ya mauaji yalitokea tofauti na mwaka jana ambapo matukio hayo yalipungua na kufikia 35 huku akisema kazi imefanyika kuyadhibiti hadi kufikia idadi hiyo.

Alisema Serikali kupitia jeshi la polisi na pande zote zinazohusika zimeanza harakati kuweza kudhibiti matukio hayo yanayosababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo imani za kishirikina.


Matukio ya Udhalilishaji

katika kipindi cha mwaka 2019 Januari hadi Disemba matukio ya udhalilishaji yalionekana kuongezeka baada ya matukio 35 kuripotiwa tofauti na mwaka 2018 ambapo matukio 15 yaliripotiwa na jitihada mbalimbali zinafanyika ikiwepo utolewaji elimu kupitia askari wa Shehia na Ofisi ya Polisi Jamii na wadau huku sababu mbalimbali ikiwemo imani za kishirikina, jamii kukosa elimu ya kutosha kuhusu madhara ya makosa hayo, watu kushindwa kuzuia matamanio,ukuaji wa matumizi ya mitandao,kutotolewa adhabu stahiki na kwa muda muafaka kwa wakosaji na kuwepo mmomonyoko wa maadili.

“Matukio haya ya udhalilishaji ikiwepo kubaka, kulawiti na kunajisi serikali tumeyaundia mkakati maalumu ikiwemo kamati maalumu iliyoundwa ikisheheni wataalamu wa udhibiti uhalifu kutoka jeshi la polisi wakiwemo wapelelezi, wataalamu wa madawati ya jinsia, tunataka kuona kadhia hiyo ya udhalilishaji inaisha Zanzibar na kumekuwepo na tabia ya familia za mtendaji na mtendewa wa matukio ya udhalilishaji kuficha mtuhumiwa huku wakiyamaliza mambo hayo katika ngazi ya familia ambapo sio sahihi lazima watuhumiwa wakamatwe na wafikishwe mahakamani na wakithibitika basi sheria ichukue nafasi yake, hatuwezi ona watoto wakiaribiwa sasa tutakua na taifa gani ambalo watu wake wamearibika” alisema Masauni


Wizi wa watoto wachanga

Akizungumzia matukio ya kuibiwa watoto wachanga, Naibu Waziri Masauni alisema mwaka 2018 jumla ya watoto wachanga 2 waliibiwa na baada ya juhudi za jeshi la polisi kudhibiti vyanzo mbalimbali vya matukio hayo ikiwemo wapiga ramli mwaka 2019 hakuna mtoto mchanga aliyeibiwa

“Nilishawaagiza viongozi wa jeshi la polisi kushirikiana na masheha wa shehia mbalimbali kuhakikisha wanagundua maeneo yenye waganga wanaowadanganya wananchi kupata utajiri kwa njia haramu ikiwemo viungo vya watoto wachanga, nalipongeza jeshi lilifanya msako na kusambaratisha hao wanaojiita wataalamu wanaowadanganya wananchi wetu” alisema Masauni


Madawa ya Kulevya

Kutokana na kuwepo kwa tatizo la biashara haramu ya dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za Ulinzi na Usalama liko mbioni katika kudhibiti biashara hiyo

“Jeshi liko makini katika kudhibiti mtandao wa biashara hiyo ambayo tumeona siku za nyuma vijana wengi ambao ni nguvu kazi ya taifa wakiaribika kwa dawa za kulevya, na kuna mpango maalumu uko katika utekelezaji na tayari umeanza kutoa matokeo chanya ambapo mwaka 2019 watuhumiwa 496 wametiwa mikononi, tumekamata pia Cocaine gramu 960.65, Heroine Kilogramu 10.2 na gramu 806.102 imekamatwa, Bangi Kilogramu 659.6 na gramu 649.775 ilikamatwa,vijana wetu wamezamia kwenye utafunaji mirungi lakini nayo tushakamata kilogramu10.6 na gramu 096.648 pamoja na vidonge vya Valium gramu 10.30” alisema Masauni


Usalama Barabarani

Kumekuwepo kwa upungufu wa makosa yanayohusiana na suala la usalama barabarani ambapo mwaka 2018 makosa 31,524 yaliripotiwa tofauti na mwaka 2019 ambapo makosa 23,166 yaliripotiwa

“Serikali kupitia Baraza la Usalama Barabarani kupitia Wakuu wa Trafiki nchi nzima hapa nazungumzia Zanzibar lakini hata kule Bara wamekua na programu mbalimbali zenye lengo la kuhakikisha watumiaji wa barabara wanakua salama ili kuweza kuondoa vifo vya uzembe vinavyosababishwa na waendesha vyombo vya moto,baraza pia limekua likitoa elimu mashuleni na tumeona sasa kuna upungufu wa matukio takribani asilimia 26 japo tunapambana ndani ya mwaka huu kuondosha kabisa na mwaka huu Wiki ya Usalama Barabarani itafanyika hapa Zanzibar ili kuweka msisitizo kwenye hili la kupunguza ikiwezekana kuondosha ajali” alisema Masauni


Makosa mengine

Naibu Waziri Masauni aliyataja makosa mengine ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha, wizi wa magari, wizi wa mali za serikali kuu, wizi wa mifugo, ajali za moto, rushwa na wizi katika vyama vya ushirika kudhibitiwa huku makosa yake yakiendelea kushuka siku hadi siku kwa jitihada za jeshi la polisi na wadau wengine ikiwemo wananchi wema ambao hutoa taarifa mapema kwa jeshi la polisi.

“makosa kama rushwa ndani ya mwaka 2018 tukio moja tu liliripotiwa huku mwaka 2019 hakukua na tukio likihusisha utoaji na upokeaji rushwa.Wizi wa magari pia mwaka 2018 magari 5 yaliripotiwa kuibiwa huku kuonekana kushuka kwa makosa hayo mwaka 2019 baada ya matukio 2 kuripotiwa, kupatikana na nyara kwa miaka miwili 2018 na 2019 hakuna tukio lililotokea” alisema Masauni.

ZIARA YA KATIBU MKUU, OFISI YA WAZIRI MKUU ANDREW MASSAWE AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI KIWANDA KIPYA CHA BIDHAA ZA NGOZI CHA KARANGA MKOANI KILIMANJARO

$
0
0


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (katikati wenye koti la bluu) akizungumza na baadhi ya Viongozi kutoka Jeshi la Magereza wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho kilichopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe (wa tatu kutoka kushoto) akiwa ameambatana na Viongozi kutoka Jeshi la Magereza na wasimamizi wa mradi huo alipotembelea mradi huo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho.
Mkurungenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Hosea Kashimba (wenye koti la bluu) akijadili jambo na baadhi Viongozi kutoka Jeshi la Magereza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika Januari 25, 2020 Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
****************************
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe ametembelea eneo ambapo mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi cha Karanga kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Katika ziara hiyo iliyofanyika Januari 25, 2020 Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe alikuwa ameambatana na Mkurungezi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Hosea Kashimba, PSSSF wana ubia na Jeshi la Magereza katika utekelezaji wa kiwanda hicho kilichopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

SERIKALI YABORESHA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MAWENZI

$
0
0

#Yafanya upasuaji wa kuondoa ukungu wa jicho kwa wagonjwa 640

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

HOSPITALI ya Rufaa Mawezi ya Mkoa wa Kilimanjaro imesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli imefanikiwa kuboresha huduma za afya kutokana serikali kuwekeza wataalam pamoja na vifaa tiba.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Timu ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt.Jumanne Karia amesema kuwa utoaji wa huduma uimarishwa kwa kuwepo kwa vifaa tiba pamoja na wataalam katika maeneo mbalimbali.

Amesema kuwa katika uboreshaji wameongeza vitanda hadi kufikia 300 hali ambayo imefanya wagonjwa wote kulazwa kwenye vitanda pamoja na kupunguza vifo vya wajawazito kwa asiliamia 100.

Dk.Karia amesema katika kipindi cha miaka minne ya Dk.Magufuli hospitali hiyo imefanikiwa kufanya upasuaji wa kuondoa ukungu wa jicho kwa wagonjwa 640 pamoja na kupandikiza kioo cha jicho kwa wagonjwa watatu.

“Hospitali imepunguza rufaa mbalimbali kwa wagonjwa ikiwa ni serikali kuwekeza kwa vifaa na mashine za kisasa hii kwetu imetufanya kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na maeneo mengine”amesema Kiria.

Dkt. Karia amesema kuwa serikali katika uwekezaji imejenga jengo la kisasa lililogharimu sh.milioni 800 kwa ajili ya magonjwa ya mlipuko ambapo liko katika hatua za mwisho ya kuanza kutumika hali ambayo itasaidia kuboresha huduma za afya kwa magonjwa mbalimbali ya mlipuko.

Amesema tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya Tano upatikanaji wa dawa katika hospitali hiyo ni asilimia 90 lakini tutafikia asilimia 100 kutokana na mikakati ya serikali ya uwekezaji kwenye sekta ya afya.
Aidha amesema serikali imejenga jengo la mama na mtoto pamoja na huduma zote zitakuwa katika jengo hilo hali ambayo kwani hakuna mgonjwa anaweza kukosa dawa .
 Kaimu Mganga  Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt.Jumanne Karia akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Timu ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  walipotembelea  Hospitali hiyo kuangalia mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya tano ikiwa Kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya iliyoratibiwa na Maafisa habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara.
  Mkuu wa Msafara na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Gerald Chami akitoa maelezo kuhusiana na kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya kwa kuangalia mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya tano.

 Jengo la Mama na Mtoto  lililojengwa  kwa shi.bilioni Nane ambalo litakuwa na vifaa na mashine mbalimbali za kutolea huduma katika jengo hilo.
 Jengo la  magonjwa ya Mlipuko lililojengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mawezi Mkoa wa Kilimanjaro.
 Jengo la  magonjwa ya Mlipuko lililojengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mawezi Mkoa wa Kilimanjaro.

Kibong’oto kuwa taasisi ya kutibu magonjwa ambukizi

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Michuzi Globu,SIHA-Kilimajaro

HOSPITALI ya Taifa ya Kifuu Kibong’oto mkoani Kilimanjaro iko katika mchakato wa kuwa Taasisi kuwa Taasisi ya Magonjwa ambukizi na afya ya Jamii ilikupanua huduma zake pamoja na tafiti pamoja na kuweza kujiendesha.

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea na mchakato huo wa kufanya Hospitali ya Kibong’oto kuwa Taasisi na wakati wowote utakamilika.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Dkt. Donatus Tsere wakati akizungumza na pamoja na Maafisa Habari na Uhusiano wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee ,Watoto amesema na amesema kwa sasa taratibu zinaendelea na itakapokamilika itatanua wigo mpana upande wa huduma na tafiti.

Amesema katika utoaji wa majibu yanayotolewa katika Hospitali hiyo yamepata Ithibati na Shirika la Afya Duniani (WHO),majibu yanayotoka hapo ni uhakika hata ikitokea mtu aende hospitali yeyote majibu hayo hayawezi kubadilika.

Dkt.Tsere amesema uwekezaji wa vifaa vya maabara vya uchunguzi wa vumelea vya Kifua Kikuu Sugu kumefanya kutoa majibu ndani ya masaa mawili tofauti na awali majibu yalikuwa yanatoka kwa masaa 24 hali ambayo ilikuwa inafanya kukaa kwa sampuli kwa muda mrefu.

“Serikali imerahisha utoaji wa huduma zetu kwa kuleta vifaa vya kisasa huku maboresho mengine yakiendelea kufanyika ikiwa ni kuhakikisha jamii inapata huduma bora za afya na kuongeza watalaam wakiwemo Madaktari, Wauguzi na wataalam wa maabara.”amesema Kaimu Mkurugenzi Tsere.

Amesema kati ya wagonjwa 300 waliopima kifua kikuu Sugu (TB) asilimia 20 walipatikana kuwa Kifua Kikuu Sugu pamoja na virusi vya Ukimwi .

Amesema kuwa serikali imejenga maabara kubwa ya kisasa itakayogharimu kiasi cha sh. Bilioni Nane ambapo ujenzi wake wa hatua ya kwanza umkwiisha na wanakwenda hatua ya pili kukamilisha ujenzi huo na kuanza kutumika ifikapo 2021.

Dkt.Tsere kutokana na serikali kuwekeza katika Hospitali na Vituo vya Afya 145 Kibong’oto inapokea wagonjwa ambao wana kifua kikuu sugu kwani wengine wanagundulika katika Hospitali na Vituo vya Afya kwa ajili ya kuchunguza na kutibu kifua kikuu.

Baadhi ya mashine za kisasa zilizopo katika Hospitali ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Timu ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walipotembelea Hospitali hiyo kuangalia mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya tano ikiwa Kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya iliyoratibiwa na Maafisa habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara.
Mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro Thadeus Bwire akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma alizopata katika Hospitali ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto hadi kufikia hali ya kuruhusiwa akiwa na afya njema
Msimamizi wa Huduma Ubora wa Maabara wa Hospitali ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto Juma Elisha akizungumza namna serikali ilivyokeza vifaa na mashine katika hospitali hiyo hali ambayo imefanya kupima sampuli kwa masaa mawili.
Jengo la Maabara ya Kisasa Level Three” ambalo limejengwa na serikali ilikuboresha huduma




Baadhi ya mashine za kisasa zilizopo katika Hospitali ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto.
Viewing all 110034 articles
Browse latest View live




Latest Images