Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Serikali yaipa kipaumbele sekta ya michezo nchini kutoa ajira kwa vijana

$
0
0

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akifunguamashindano ya pili ya mchezo wa Taekwondo yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akisalimiana naBalozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini Cho Tae-ick ambaye ofisi yake ni mdhamini wamchezo wa Taekwondo kabla ya kufungua mashindano ya pili ya mchezo huo yanayofanyikakwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja waSheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini Cho Tae-ick ambaye ofisi yake ni mdhamini wamchezo wa Taekwondo akiongea wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mchezo wa Taekwondo yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Aliyeketi katikati ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza na Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Taekwondo Tanzania (TTF) Ramoudh Ally (kulia).
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea Taekwondo Cho Tae-ick (kushoto) akiteta jambo naNaibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza (kulia) wakati waufunguzi wa mashindano ya mchezo wa Taekwondo yanayofanyika kwa siku mbili kuanziatarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijiniArusha.
Rais wa Shirikisho la mchezo wa Taekwondo nchini (TTF) Ramoudh Ally akitoa historia ya mchezo wa Taekwondo nchini wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mchezo wa Taekwondo yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katikauwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Aliyeketi katikati ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza na kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini Cho Tae-ickWanamichezo wa mchezo wa Taekwondo wakiendelea na mashindano ya mchezo huo wakati wa ufunguzi wa mashindano yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria ufunguzi wa mashindano ya mchezo wa Taekwondo yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15 Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Arusha)
******************************
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Arusha
Serikali ya Awamu ya Tano imeipa kipaumbele sekta ya michezo nchini kwa kuweka mikakati inayohakikisha michezo yote ikiwemo Taekwondo inafanya vizuri ili kuwa chanzo cha kutoa ajira kwa vijana pamoja na kukuza uchumi wa taifa.

Akifungua mashindano ya Taekwondo ya pili ya mchezo wa yanayofadhiliwa na Ubalozi wa Korea nchini kwa mwaka 2019 kwa nchi za Afrika ya Mashariki yanayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha mwishoni mw wiki, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa michezo yote nchini ikiwemo mchezo wa Taekwondo.

Akijibu moja ya maombi yaliyotolewa na Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Taekwondo nchini (TTF) Ramoudh Ally la kupatiwa eneo la kujenga uwanja mkubwa wa ndani wa kisasa kwa ajili ya mchezo wa Taekwondo wakati akitoa historia ya mchezo huo nchini, Naibu Waziri alisemakuwa kwa mujibu wa Sera ya Maendeleo ya michezo nchini ya mwaka 1995 jukumu la kusimamia na kuendeleza sekta ya michezo ni la Serikali, jamii nzima pamoja na wadaumbalimbali ukiwemo Ubalozi wa Korea nchini.

“Natoa wito kwa wadau wa michezo kuendelea kushirikiana na Serikali kukuza, kuendeleza na kuwekeza katika sekta ya michezo nchini ikiwemo mchezo wa Taekwondo, kwani Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali kuendeleza michezo ikiwemo Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini ili kuhakikisha sekta hii inakuwa na tija kwa jamii na taifa zima” alisemaNaibu Waziri Shonza.

Aidha, ameataka maafisa michezo nchini kuanzia ngazi ya mikoa na wilaya kushirikiana na viongozi wa Mashirikisho na Vyama vya Michezo ili kuhakikisha vyama na vilabu ambavyo havijapata usajili kupitia Baraza la Michezo nchini (BMT) ambalo limepewa dhamana ya kusajilimashirikisho, vyama na vilabu hapa nchini.

Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini Cho Tae-ick ambaye ofisi yake ni mdhamini wa mchezo huo amesema kuwa mchezo wa Taekwondo unafaida nyingi na unachezwa na watu wa rika zote kuanzia watoto wadogo hadi watu wazima kwa kuimarisha na kujenga mwili ambapo husaidia kuimarisha umakini katika kutimiza majukumu yao ya kila siku.

Balozi huyo ameendelea kuzitaja faida nyingine za mchezo huo kwa ni kuwajengea uwezo wachezaji wa kujilinda kiusalama, kuwafundisha saikolojia ya namna bora ya maisha pamoja na kuwajengea urafiki miongoni mwa wachezaji.

“Taekwondo ni mchezo mzuri sana, kila kitu katika mwili wa binadamu ni silaha ya kujikinga, cha msingi ni kujua namna ya kuitumia kwa faida kwa jamii nzima, elimu hiyo inapatikana katika mchezo wa Taekwondo” alisema Balozi Cho.

Awali akitoa historia ya mchezo wa Taekwondo nchini Rais wa Shirikisho la mchezo huo nchini (TTF) Ramoudh Ally alisema kuwa Taekwondo ni mmoja kati ya michezo inayotambuliwa na Baraza la Michezo Tanzania pamoja na Kamati ya Olympic duniani.

Mchezo Taekwondo nchini ulianza kutambuliwa rasmi mwaka 2003 na Shirikisho la Taekwondo duniani ambalo makao yake makuu yapo nchini Korea ya Kusini ambapo hadi sasa Tanzania ni mwanachama hai na inashughulika na masuala yote ya mchezo huo duniani.

Mashindano Taekwondo ya mwaka 2019 yanayojulikana kama “Korean Ambassador’s Cup” ni ya pili kufanyika nchini ambapo hufanyika kila baada ya miaka miwili kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka 2017.

Mashindano ya mwaka huu yanafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14 hadi 15 Disemba 2019 jijini Arusha ambayo yanajumuisha jumla ya washiriki 172 kutokakatika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Rwanda, Uganda na mwenyeji Tanzania pamoja na washiriki kutoka nchini Malawi.

SERIKALI YABAINISHA FURSA YA UFUGAJI SAMAKI, KAA, KAMBAKOCHI NA MAJONGOO BAHARI UKANDA WA PWANI.

$
0
0

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akifungua eneo lililowekwa jiwe la msingi kuashiria ufunguzi rasmi wa FETA Kampasi ya Mikindani, Mkoani Mtwara.
Baadhi ya wahitimu wa kozi fupi za ufugaji samaki wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati wa ufunguzi wa FETA Kampasi ya Mikindani, Mkoani Mtwara.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (wa tatu kutoka kulia) akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa FETA Kampasi ya Mikindani, Mkoani Mtwara
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na wahitimu wa kazo fupi za ufugaji samaki (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa FETA Kampasi ya Mikiandani, Mkoani Mtwara.
*********************************

Na. Edward Kondela

Serikali imesema inahakikisha sera yake ya kuhamasisha wananchi kufuga samaki inatekelezwa kote nchini ili kutosheleza mahitaji ya soko la samaki nchini pamoja na kukuza pato la taifa na mtu mmoja mmoja.
Akizungumza Mjini Mtwara, wakati akifungua tawi la Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Kampasi ya Mikindani Mkoani Mtwara, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ameiagiza FETA kwa kushirikiana na Idara ya Ukuzaji Viumbe kwenye Maji kutoka katika wizara hiyo, kuandaa mitaala ya ufugaji viumbe kwenye maji wakiwemo samaki, kaa, majongoo bahari na Kambakochi kwa ajili ya wananchi wa Ukanda wa Pwani ili waweze kuongeza vipato vyao kupitia fursa ya ufugaji.

Mhe. Abdallah Ulega – Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi
Aidha Mhe. Ulega ameagiza uundwaji wa vikundi vya uzalishaji kaa, Kambakochi, majongoo bahari pamoja na wazalishaji wa zao la mwani ili iwe rahisi kwa vikundi hivyo kutambulika rasmi pindi mazao yao yanapohitajika sokoni, na watu waweze kufika katika mashamba yao ya ufugaji kwa ajili ya kuvua samaki na viumbe vingine wakiwemo kaa, kambakochi na majongoo bahari ambao wamekuwa na soko kubwa sana na mahitaji yake kuongezeka katika baadhi ya maeneo zikiwemo hoteli za kitalii.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka FETA Bw. Ambakisye Simtoe amesema chuo hicho kimepanga kuzalisha wagani kwa ajili ya kuendeleza na kukuza tasnia ya uvuvi nchini pamoja na kununua mashine ya kuzalisha vifaranga bora ili iwe rahisi kwa wananchi wa Ukanda wa Pwani kupata vifaranga hivyo kwa bei nafuu huku katika risala ya wanafunzi hao wakisema mafunzo waliyoyapata yakiwemo ya ufugaji wa samaki yatawawezesha kujiajiri. 


Bw. Ambakisye Simtoe – Mkurugenzi wa Mafunzo FETA
Bi. Monica Mfaume – Msoma risala kwa niaba ya wanafunzi
Jumla ya wanafunzi 62 wamehitimu kozi fupi ya ufugaji samaki katika chuo cha FETA Kampasi ya Mikindani Mkoani Mtwara na kukabidhiwa vyeti na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ambaye amekifungua rasmi chuo hicho chenye uwezo wa kudahili wanafunzi 240 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi mahitaji ya soko la samaki nchini ni Tani 700,000 hadi 800,000 kwa mwaka huku uzalishaji ukiwa wastani wa Tani 400,000 hadi 450,000 hali ambayo Naibu Waziri Ulega amesisitiza kwa chuo cha FETA Kampasi ya Mikindani Mkoani Mtwara kuwa kampasi ya mfano katika kutoa mafunzo ya ufugaji samaki, kaa, kambakochi na majongoo bahari ili wananchi waweze kutosheleza soko la ndani na kukuza vipato vyao na taifa kwa ujumla.

MISS JAMAICA ATWAA TAJI LA MISS WORLD 2019

$
0
0
Shindano la Urembo Dunia Miss World 2019, limefanyika usiku wa kuamkia Desemba 15, na Mrembo kutoka nchi ya Jamaica Toni-Ann Singh ametwaa taji hilo.

Toni-Ann ameitoa kimasomaso nchi yake mara baada ya kutwaa taji la Urembo wa Dunia katika mashindano ya kumsaka mlimbwende wa Dunia (Miss World), yaliyofanyika Jijini London, nchini Uingereza.

Shindano hilo ambalo jana ilikuwa ni mara yake ya 69 kufanyika, lilikutanisha warembo kutoka Mataifa mbalimbali duniani, ambapo nchi ya Tanzania iliwakilishwa na Mrembo Sylvia Sebastian Bebwa, ambaye yeye kwa juma lililopita aliingia katika 20 bora ya warembo wenye vipaji, baada ya yeye kuonesha kipaji cha kucheza 'Robot Dance'.

Mbali na Urembo, Mlimbwende huyo wa Dunia anapenda kutoa Elimu ya afya ya akili na matarajio yake ni kuwa Daktari na taji lake amelipokea kutoka kwa Venessa Ponce De Leon, Mrembo kutoka nchini Mexico alitwaa taji hilo mwaka 2018.

Katika mashindano hayo mshindi wa pili alikuwa mrembo kutoka Ufaransa, Ophely Mezino, wa tatu ni Suman Rao kutokea nchini India


Warembo waliofanikiwa kuingia 12 bora ya  Miss World 2019 Top
Kenya, Nigeria , Brazil ,Mexico ,India ,Nepal ,Philippines , Vietnam ,Jamaica, France ,Russia  na Cook Islands
 Miss World 2019 Toni-Ann Singh akiwa na wazazi wake baada ya kutwaa taji la urembo
Miss World 2019 Toni-Ann Singh akiwa katikati ya mshindi wa Pili Kutoka Ufaransa Ophley Mezino (Kushoto) na Sumao Rao kutoka India
 Kumi 10 ya Miss World 2019


SHILINGI BILIONI 1.8 ZA CHENCHI YA VIFAATIBA, DAWA,NA VITENDEA KAZI KUTUMIKA KWA MAENDELEO NA KUBORESHA HUDUMA BMC

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya BMC ya jijini Mwanza, Profesa Abel Makubi, kulia akifungua moja ya makufuli yaliyofungwa kwenye moja ya  kontena la vifaa tiba ,dawa na vitendea kazi kati ya makontena sita, baada ya kuwasili nchini na kupokewa jana na uongozi wa hospitali hiyo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki  cha Sayansi za Tiba za Afya (CUHAS) Profesa Paschalis Rugarabamu (kushoto) akikata utepe kuashirikia kupokea makotena ya vifaa tiba, dawa na vitendea kazi vya Hospitali ya Rufaa ya Kanda,  Bugando (BMC) vilivyonunuliwa kwa sh. bilioni 1.2 baada ya kuwasili nchini kutoka China.Kulia ni Mkurugenzi wa   hosptali hiyo Profesa Abel Makubi.

Askari wa Usalama barabarani akiwaongoza maandamano ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda , Bugando pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu Katoliki cha Sayansi za Tiba na  Afya (CUHAS)  wakiadhimisha Siku ya Bugando Day jana.

Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda , Bugando (BMC) Dk. Fabian Massaga (mwenye kofia wa tatu kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi wa kotena moja kati ya sita ya vifaa tiba na madawa baada ya kuwasili na kupokelewa na Vvongozi na watumsihi wa hospitali hiyo jana,  na watumishi.Wa tatu kutoka kulia mwenye suti ya michezo ni Mkurugenzi wa hospitali hiyo Profesa Abel Makubi.
****************************
 NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda,Bugando Medical Centre (BMC) imesema fedha zaidi ya sh. bilioni 1 zilizobaki kwenye manunuzi ya vifaa tiba,madawa  na vitendeakazi zitatumika kwa shughuli za maendeleo na kuboresha huduma mbalimbali za hospitali.
Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Abel Makubi alisema jana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Bugando (Bugando Day) muda mfupi baada ya kupokea moja ya makontena kati ya sita ya vifaa hivyo vilivyogharimush. bilioni 1.2 kati y ash. bilioni 3 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili hiyo.
Alisema hospitali  ya BMC ilikuwa na changamoto ya vifaa tiba na dawa na hivyo kuzua malalamiko kutoka kwa wagonjwa jambo lililousukuma uongozi na menejimenti kutafuta suluhu ya changamoto hiyo ambapo walishindanisha kampuni mbalimbali ili kujua bei ya vifaa tiba na madawa kulingana  mahitaji kabla ya kuagiza.
 “Ili kupunguza chagamoto hiyo uongozi na menejimenti ya hospitali  tulikubaliana kutumia fedha za ndani kuagiza vifaa tiba, madawa, vitendea kazi na sare za watumishi kwa gharama ya sh. bilioni 1.2  kutoka nchini China na kuokoa kiasi kikubwa cha fedha, endapo tungenunua hapa nyumbani ingetugharimu sh. bilioni 3,”alisema Profesa Makubi.
Alisema  kununua madawa na vifaa tiba nje kwa gharama nafuu wameokoa fedha nyingi wanazokusanya na kutumia kidogo lengo likiwa ni kuboresha huduma za tiba kwa wananchi na vitasaidia pia changomoto ya hospitali nyingi za umma kwa sababu zina matatizo ya vifaa tiba.
Alishauri taasisi za umma kulinda na kutumia kidogo wanachopata ili wananchi wapate huduma bora kwa kununua vitendea kazi katika kuboresha huduma  na kuzifanya kuwa bora.
“Ili kukabiliana na changamoto ya vifaa ni kuboresha huduma wananchi watibiwe kwa vifaa bora na katika mazingira bora, si vifaa tu hata mahali wagonjwa wapolala, hilo ndilo BMC tumefanya,”alisema Profesa Makubi.
Mkurugenzi huyo wa BMC alisema baada ya kupata vifaa tiba vya kisasa vya vipimo na upasuaji wa kibingwa kutaharakisha utoaji wa huduma na kwa ufanisi zaidi, kutaokoa muda na majibu kupatikana haraka badala ya mgonjwa kusubiri kwa saa mbili.
Dk. Makubi alitaja miongoni mwa vifaa tiba walivyopata kuwa ni mashine 6 za Utra Sound na vifaa vya upasuaji ambavyo vitawezesha wagonjwa kuchunguzwa na kufanyiwa upasuaji kwa haraka zaidi na kupunguza malalamiko ya kuchelewa kuhudumiwa.
Aliwataka watumishi wa hospitali hiyo wakiwemo wanaohudumu kwenye hospitali za serikali kujituma zaidi kuwahudumia wananchi haraka na kwa ubora kwani hiyo ndiyo rai ya menejimenti ya BMC na watumie lugha safi kwa wagonjwa.
“BMC tunawathamani watumishi kwa kuwapa faraja waone utendaji wao unathaminiwa, hii itawatia moyo na hamasa, hivyo kuwafanya wajitume zaidi kwa wananchi na kuhakikisha wanapata huduma bora za kiwango,”alisema Profesa Makubi.
Awali Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk.  Fabian Massaga, alisema shilingi bilioni 1.8 kati ya bilioni 3 zilizookolewa kwenye ununuzi wa vifaa tiba na madawa zitatumika kwa maendeleo na kuboresha huduma mbalimbali za hospitali.
Alivitaja baadhi ya vifaa tiba ni vitanda, mashine sita za Utra Sound,vifaa vya upasuaji (operating set), madawa mbalimbali, kompyuta zitakazounganishwa na mfumo na kuondokana na madaktari kutumia majadala kwa ajili ya kumbukumbu za wagonjwa na sare za watumishi vyote vikigharimu sh. bilioni 1.2 fedha za ndani.
Aidha, katika hatua nyingine Profesa Makubi, alisema wanapoadhimisha  Siku ya Bugando Day mwaka huu lengo ni kuwakumbusha watumishi wa  Hospitali ya BMC  majukumu yao, kuonyesha umoja na mshikamano kati yao na watumishi wa Chuo Kikuu Katoliki cha Sayansi za Tiba za Afya (CUHAS).   
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha CUHAS, Profesa Paschalis Rugarabamu,alisema wanashirikiana chuo na hospitali kujenga maadili na kuhimiza vijana kutimiza majukumu yao ya utoaji wa huduma za tiba kwa kuzingatia maadili ya kitaaluma ingawa ni kazi ngumu.
Pia wamepanua wigo wa taaluma nje ya BMC kwa kuwapeleka wanafunzi wa chuo hicho kujifunza kwenye maeneo tofauti licha ya matakwa ya mtaala wanafanya mazoezi katika mazingira halisi kwa kuzijengea uwezo wa elimu na huduma katika hospitali za Sekou Toure na Sengerema DDH.
Hospitali ya Bugando iliyojengwa mwaka 1967 kwa msaada wa Serikali ya Ujerumani Magharibi kwa ushirikiano na Uholanzi kupitia shirika moja la kikatoliki ambapo mwaka huu imeadhimisha miaka 52 na  ilifunguliwa, Desemb 3, 1971 na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere

WATU 37 WALAZWA HOSPITALI YA DODOMA KWA KUHISIWA KULA CHAKULA CHENYE SUMU

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

Watu 37 wamefikisha na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital)  kwa ugonjwa wa kuhara na kutapika baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.

Tukio hilo limetokea jioni ya leo katika eneo la Mtumba nje kidogo ya Manispaa ya Jiji la Dodoma ambapo walikula chakula hicho wakiwa kwenye msiba wa jirani yao.

Akizungumza hospitalini hapo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi amekiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza tayari ameshaagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi kwenye mabaki ya chakula hicho ili kugundua chanzo chake.

" Mara baada ya kupata taarifa hizi tumefika hapa na Timu ya viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa kwa hatua ya awali tumesimamia kuhakikisha watu wetu wanapata huduma ya kwanza na kiukweli wagonjwa wote wanaendelea vizuri.

Kati ya hao 37 waliolazwa, wanaume ni 10, wanawake wapo 23 na watoto wakiwa ni wanne, tayari nishatoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kujua chanzo, lakini pia tunafanya uchunguzi wa kitabibu kujua ni sumu ya mtu kuweka au ni sumu ya chakula," Amesema Mhe Katambi.

Amewataka wananchi kuwa watulivu kwa sasa na kusubiria kupata majibu kutoka kwa Timu inayofanya uchunguzi na kuwataka wale wote ambao wanaona dalili za kuhara na kutapika kufika katika vituo vya afya vilivyopo karibu ili kupatiwa matibabu.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Best Magoma amesema hali ya wagonjwa waliofikishwa hospitalini hapo inazidi kuimarika baada ya kuwapatia matibabu na pindi watakaporidhishwa na maendeleo ya afya zao wataruhusiwa kurudi majumbani mwao.

" Tunawashukuru viongozi wetu wa ngazi ya Wilaya wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya kwa kufika hapa na kutuongezea nguvu, na timu yetu kwa kushirikiana na wenzetu wa Polisi na TBS tumeshaanza uchunguzi wa kubaini nini chanzo cha tatizo hili, nitoe wito kwa wananchi ambao wanaona dalili kama hizi kujitokeza haraka kwenye vituo vya afya na sisi tupo tayari kuwahudumia," Amesema Dk Magoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa kile kinachodaiwa kula chakula chenye sumu.
 Mkuu wa Wilaya Dodoma (kushoto) Mhe Patrobas Katambi akiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Devis Mwamfupe baada ya kufika hospitalini hapo kujionea hali za wagonjwa 37 waliofikishwa na kulazwa baada ya kudaiwa kula chakula chenye sumu.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi (mwenye koti la suti) akiwa na wauguzi na madaktari wa Hospitali ya Rufaa Dodoma alipofika kuwajulia hali wagonjwa waliofikishwa hospitalini hapo ambao wamepata mgonjwa wa kuhara na kutapika wakihisiwa kula chakula chenye sumu
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Best Magoma akizungumza na wandishi habari juu ya tukio la kulazwa kwa watu 37 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa kile kinachoelezwa kula chakula chenye sumu.

 Watu mbalimbali walioleta wagonjwa wao katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakisubiri kupata huduma kwenye kitengo cha dharura.

BOOK TO MAKE AFRICA WORLD’S ECONOMIC POWERHOUSE LAUNCHED IN JANUARY

$
0
0
By Staff Reporter, Dar es Salaam

Dar es Salaam, 15 December, 2019: A Book that inspires Africa to think of implementing generational reforms to becoming world’s largest economy is expected to hit African book stores from January 2020.

Speaking during the interview with Tanzania’s ITV Channel over the weekend, Derek Murusuri, author of the much awaited book, said his 21-year researched book, is a game changer for Africa’s future.

“This book is for Africa. It brings back to African minds, the forgotten concept of liberation.

It breaths a fresh air in the struggle for Africa’s economic liberation in the World’s richest continent yet poor, a paradox indeed” the author said.

“The young men and women of Africa must now rise to the new helm, as the roads rise to meet them, to rejuvenate the possibilities embalmed in their dreams which will raise new values, norms and beliefs to lead the continent to economic triumphs,” he said.

The author who once lived and worked in the UK, said his book assures black people on earth to know and believe that they were never created to be followers, neither were they predestined underdogs.

He told ITV’s Kumekucha host, Abdallah Mwaipaya, that the book hits the African book stores on 15 January, 2020 after a grand launch in Tanzania’s business capital of Dar es Salaam.

Mr. Murusuri said he shares the ideas on solutions to end Africa’s centuries of economic bondage and hopelessness in his much awaited book. He did not reveal much contents neither did he reveal the presider.

The post-independence African leaders who came to power in recent years, exhibit the zeal to transform and change the continent, making it increasingly competitive.

What the book says and whether the continent will truly gamble to skip the hurdles and navigate through becoming the World’s leading economy, is a matter of weeks, when political scientists, academicians, politicians and other analysts will scan the book, review and implement the author’s ideas. 

In November, Tanzania’s third President, Dr. Benjamin Mkapa, had his memoirs titled “My Life, my Purpose,” inaugurated by Tanzania’s President Dr. John Pombe Magufuli.

Book readership in this East African country, is slowly rising as the country prides the largest University in East and Central Africa.



NHIF Yawapiga Msasa Wanahabari Mkoa wa Mbeya Kuhusu Vifurushi vya Bima ya Afya

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF) Bw. Bernard Konga akiongea na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya, ambapo aliwasisitiza kuhusu umuhimu wa kutumia vyombo vyao vya habari kuwaeleza wananchi faida za kujiunga na vifurushi vipya kwani vimezingatia makundi yote katika jamii kwa lengo la kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na uhakika wa huduma ya matibabu. Tarehe 15.12.2019 Mkoani Mbeya
Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF)Bw. Christopher Mapunda akiongea na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya, ambapo alisema kuwa viwango katikavifurushi vya bima ya afya sio gharama za matibabu bali ni uchangiaji ndio maana hata ukiumwa na kutumia zaidi ya kiwango cha laki moja na tisini na mbili, mfuko utagharamikia matitabu hayo. Tarehe 15.12.2019 Mkoani Mbeya
Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF) Bw. Hipoliti Lello na akitoa mada kwa wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya, ambapo aliwaeleza kuwa mpango wavifurushi sio mpya na NHIF imeanzisha mpango huo kwa lengo la kuwafikia watanzania wengi zaidi kulingana na mahitaji yao. Tarehe 15.12.2019 Mkoani Mbeya.
wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya wakifuatilia uwasilishaji wa mada kutoka kwa wataalam wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF), Tarehe 15.12.2019 Mkoani Mbeya
PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO

**************************
NA MWANDISHI WETU, MBEYA

Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) Umewapiga Msasa wanahabari Mkoa wa Mbeya kuhusu Vifurushi vya Bima ya Afya na kuwasisitiza kutumia kalamu zao kuwaeleza wananchi umuhimu wa kujiunga ili kuwa na uhakika wa matibabu. 

Akiongea wakati wa Kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Bw. Bernard Konga amewaeleza wanahabari hao kuwa kwa namna ambavyo mfuko umetengeneza vifurushi umezingatia gharama za matibabu ya kawaida ambayo ukienda hospitalini lazima uyapate. 

“Leo hii wapo wanaopotosha kuhusu gharama hizi, hatuwezi kuwaacha watanzania ambao wapo tayari kutumia bima ya afya ili kupata matibabu na kusema tusubiri, niwahakikishie tumefanya tafiti, kiasi cha Shilingi laki moja na tisini na mbili kimezingatia gharama za matibabu ya kawaida ambayo ukienda hospitalini lazima uyapate na utaratibu huu ni niwa hiari”-Alisema Bw. Konga. 

Aidha, Bw. Konga alisema kuwa umefika wakati kwa wananchi kujikatia bima ya afya kabla ya kuugua hasa katika kipindi hiki ambacho mfuko umeanzisha mpango wa vifurushi ili kuwa na uhakika wa matibabu na kupuuza maneno ya baadhi ya watu wanaoendesha mijadala isiyo na tija. 

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa Mfuko huo Bw Christopher Mapunda alisema kuwa viwango katika vifurushi vya bima ya afya sio gharama za matibabu bali ni uchangiaji tu na ndio maana hata ukiumwa na kutumia zaidi ya kiwango cha laki moja na tisini na mbili, mfuko utagharamikia matitabu hayo bila kujali kuwa umetibiwa kwa kiasi gani. 

Awali akiongea wakati akiwasilisha mada kwa wanahabari hao Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya( NHIF) Bw. Hipoliti Lello alisema kuwa mpango wa vifurushi sio mpya na NHIF imeanzisha mpango huo kwa lengo la kuwafikia watanzania wengi zaidi kulingana na mahitaji yao

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO DESEMBA 16,2019


K-Finance yaandaa maonyesho kwa wanawake wajasiriamali maarufu kama Women in Balance Business

$
0
0
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya K-Finance, Judith Minzi ametaja sababu za biashara nyingi zinazoanzishwa nchini zimeshindwa kuendelea kuwa ni pamoja na kutokujua namna ya kutafuta masoko, kunakili biashara ambayo anafanya mtu bila kujua wazo lake namna lilivyoanzishwa.

Hivi karibuni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji aliiagiza Benki Kuu ya Tanzania(BOT) kushirikiana na Mfuko wa Udhamini wa Sekta ya Fedha(FSDT) kufanya utafiti kujua sababu ya biashara nyingi hasa zinazoanzishwa na wanawake zinashindwa kufikisha miaka mitatu.

Ashatu alitoa maagizo hayo katika mdahalo wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuhusu sekta ya fedha, akiwataka watafute sababu zinazosababisha asilimia 51 ya biashara zinazoanzishwa na wanawake nchini hufa kabla ya kufikisha miaka mitatu.

Akizungumza katika maonesho ya Biashara ya Wanawake yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Judith alisema elimu ya biashara kwa wafanyabiashara wengi ni tatizo hivyo kushindwa kujiendesha.

Alisema changamoto nyingine ni uelewa mdogo wa wafanyakazi wanaomsaidia mfanyabiashara kuuza bidhaa hiyo kama wanaijua na wanajua maono ya mwanzilishi.

“Ni muhimu kwa wafanyabiashara kutafuta elimu ya biashara kupitia njia mbalimbali ikiwamo mafunzo yanayotolewa na taasisi nyingi hapa nchini,” alisema Judith.

Aliishauri serikali kuanzisha somo la ujasiriamali kwa shule za msingi ili kuwajengea uwezo wanafunzi waweze kukua wakijua namna ya kufanyabiashara.

“Tuendelee kushawishi wanafunzi wapende kusoma somo la hesabu kwani linasaidia katika uanzishaji na usimamizi wa biashara,” alisema Judith.

Alisema kwa kuliona hilo taasisi ya K-Finance imeandaa mafunzo kwa wajasiriamali yatakayofanyika Januari 18, 2020 pale Hekima Garden, Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa kufundisha jinsi ya kutumia vipaji vyako kufikia uhuru wa kiuchumi.

Judith alisema katika uchunguzi walioufanya wamebaini kuwa watu wengi wanaoanzisha biashara wanashindwa kufikia malengo kutokana na kutokuwa na elimu hiyo.

Alisema mafunzo hayo yatasaidia kuwapa uelewa wa biashara wanazofanya na watakazoanzisha ili kuziwezesha kuwa imara na kudumu kwa muda mrefu.“Tutawakutanisha wafanyabiashara waliofanikiwa na ambao ndio wanaanza ili kubadilishana uzoefu na changamoto zinazopatikana katika ufanyaji biashara,” alisema Judith.

Alisema wafanyabiashara wengi waliofanikiwa wamepitia changamoto mbalimbali ambazo wakibadilishana na wanaoanzisha biashara zitawasaidia kujua namna ya kuzitatua watakapokumbana nazo.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yaitwayo ‘Ignite Business Clinic’ yataongozwa na Mchumi Mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania(BOT) kwa Zaidi ya miaka 20, na ndiye Mkurugenzi Mwanzilishi wa K-Finance, Bi. Devotha Minzi pamoja na uwepo wa mgeni rasmi aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo na sasa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb)
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya K-FINANCE inayotoa Mikopo na Ushauri wa Kibiashara kwa wafanyabiashara na watu binafsi Judith Minzi (aliyesimama), akipewa maelezo na moja ya washiriki wa maonyesho ya wanawake wajasiriamali maarufu kama Women in Business Balance ambayo yalifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni. K-Finance ilidhamini maonyesho hayo kuongea na washiriki juu ya uhuru wa kiuchumi na vile vile kuhamasisha semina maarufu kama Ignite Business Clinic (IBC) Msimu wa pili ambao utafanyika Januari 18 2020 kwenye ukumbi wa Hekima jijini Dar es Salaam. (Picha na mpigapicha wetu).

VIJANA WATAKIWA KUWA NA MAONO ILI WAINUKE KIUCHUMI

$
0
0

 Mtume Paul Toritseju (kushoto)  kutoka Nigeria akizungumza wakati akitoa mada katika Kongamano la Kwanza la vijana 2019 kuhusu jinsi ya kupata mafanikio na utajiri kwa kijana katika mazingira ya kiafrika iliyoandaliwa na Succes Chapel, Mnazimmoja,  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkalimani wake,Mwenyeji wa Kongamano hilo, Mchungaji Dkt.Sako Mayrick.
Mwenyeji wa Kongamano hilo, Mchungaji Dkt.Sako Mayrick, akisisitiza jambo.
 Kongamano likiendelea.
 Kongamano likiendelea.
 Kongamano likiendelea.
 Kongamano likiendelea.
Mafundisho kwa vitendo katika  Kongamano hilo. 
 Mtume Paul Toritseju (kushoto)  kutoka Nigeria, akimkabidhi kitabu, Mwezeshaji katika semina hiyo, Mchungaji Dkt. Robert Mbelwa.
 Mwezeshaji katika semina hiyo, Mchungaji Dkt. Robert Mbelwa, akionesha kitabu hicho.
 Mwamasishaji wa vijana kufikia mafanikio, Mhandisi Nicholaus Moses akizungumza katika kongamano hilo.
Mmoja wa wachungaji akitoa neno la shukurani katika kongamano hilo.

Na Dotto Mwaibale
VIJANA wametakiwa kuwa na maono makubwa ili wainuke kiuchumi na kuwa na fedha badala ya kulalamikia kuwa maisha ni magumu.
Wito huo umetolewa na Mtume Paul Toritseju kutoka Nigeria wakati akitoa mada katika Kongamano la Kwanza la vijana 2019 kuhusu jinsi ya kupata mafanikio na utajiri kwa kijana katika mazingira ya kiafrika iliyoandaliwa na Succes Chapel, Mnazimmoja,  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
" Ukitaka ufanikiwe kwanza kabisa ni lazima uwe na maono na kuyafanyia kazi na si vinginevyo" alisema Toritseju. Aidha alisema mafanikio yanaanzia kichwani, ndani ya mtu na si kwa nje au kinachoonekana
Alisema haiwezekani mtu akawa tajiri lakini hafanyi kazi hapo ni lazima watu watalazimika kuuhoji utajiri alionao.
Alisema vijana wanapaswa kubadilisha mtazamo wa akili zao ili kuyaendea mafanikio na kuwa tatizo la umaskini linaanzia rohoni kwani mtu anatakiwa kuwa na nguvu na roho mpya.
Alisema mpango wa mungu ni vijana kuimarika kiuchumi na  kuongeza idadi ya vijana wengi zaidi kimafanikio. Hakuna kijana aliyemtegemea Mungu na akawa maskini.
Alisema Afrika tunafikiria zaidi watoto badala ya kuwa na mipango madhubuti ya kuanzisha biashara katika nyanja mbalimbali kama mawasiliano, utamaduni, ujenzi wa viwanja, elimu, kuanzisha blog na kuwa na mawazo mapya. 

Alisema changamoto nyingine kubwa iliyopo katika nchi za kiafrika ni matumizi ya mitaala ya elimu ya kizamani ambayo walitumia wazazi wetu iliyopitwa na wakati na sasa kuna mabadiliko makubwa na mambo mengi ni mapya.
Mwezeshaji mwingine katika semina hiyo, Mchungaji Dkt. Robert Mbelwa akilitoa mada kuhusu kijana kama kiongozi kwa ajili ya mafanikio ni lazima asimamie misingi iliyopo ili aweze kumiliki uchumi ambayo ni maono, malengo, kutumikia wengine, kusali, kutomdharau mtu wala kudharauliwa, kanuni za utunzaji wa fedha, kwenda na muda na kuwa na mauhusiano na watu mbalinbali.
Alitaja mambo mengine ya kuweza kumfikisha kijana katika mafanikio kuwa ni kuthubutu, jitihada na kufanya kazi kwa nguvu.
Dkt.Mbelwa alisema mafanikio hayo yatapatikana kwa kuwepo maono, kujua unapoelekea na kuwepo kwa taarifa na kama hakuna taarifa huwezi kufanya chochote.
Akizungumzia suala la viongozi alisema hawachaguliwi bali wanaandaliwa na kuwa pasipo taarifa huwezi kuwa na kiongozi hivyo alihimiza watu wasome sana vitabu ili kupata maarifa na si kupoteza muda katika mitandao ya kijamii kama facebook, twitter na mingine.
Mwenyeji wa Kongamano la Kwanza la  vijana, 2019,  Mchungaji Dkt.  Sako Mayrick alizungumzia umuhimu wa vijana wa kuwa na maono kwa ajili ya kumiliki uchumi kwa kusisitiza kuwa hapa duniani hakuna bosi bali tumeumbwa kutumikia wenginena watu waache uvivu na uzembe. 
Aidha,  vijana wametakiwa kuwa na nidhamu katika maisha hususan katika matumizi ya fedha na muda. Kongamano  la pili la  Vijana litafanyika Desemba, 2020. Success Chapel ni Huduma ya kumsaidia mwanadamu afikie uwezo wa ufanisi na kupata mafanikio katika nyanja zote na fedha

WAWILI WARUHUSIWA KATI YA 55 WALIOKULA CHAKULA CHENYE 'SUMU'

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

WAGONJWA waliofikishwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ilifikia 55 ambapo wawili kati yao wameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya hali zao kutengamaa.

Idadi hiyo ya watu walifikishwa hospitalini hapo baada ya kupata ugonjwa wa kuhara na kutapika kwa kile kinachosadikiwa kula chakula chenye sumu kwenye msiba wa jirani yao eneo la Mtumba jijini Dodoma.

Akizungumza hospitalini hapo alipoenda kuwajulia hali wagonjwa hao, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe DkBinilith Mahenge amewapongeza madaktari na wauguzi wa Hospitali hiyo kwa namna walivyowahudumia wananchi hao kwa haraka na kujitahidi kumaliza tatizo hilo.

Amesema idadi ya waliyofika hospitalini hapo walikua ni 45 lakini baadaye Serikali iliamua kupeleka gari mbili za wagonjwa ambapo wengine 10 walijitokeza na kuchukuliwa baada ya kufanyiwa vipimo.

" Tunawashukuru sana matabibu wetu hakika wamefanya kazi nzuri sana, nimepita wodi zote kukagua hali za wagonjwa ambao wote wamehudumiwa bure wanaendelea vizuri.

Niwaombe wananchi wetu wawe wasafi hasa katika mikusanyiko ya watu, lakini pia niwatake wawe watulivu wakati huu ambao Serikali inafanya uchunguzi wake kubaini nini chanzo cha tatizo hilo, " Amesema Dk Mahenge.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Best Magoma amesema utafiti unaendelea kujua chanzo cha ugonjwa huo huku akisema mpaka kufikia jioni idadi kubwa ya wagonjwa watakua wameruhusiwa kurudi majumbani mwao.

" Hali za wagonjwa ni nzuri na wengi wao tutawaruhusu leo kurejea majumbani mwao, jana tulifika kwenye eneo la tukio tukachukua sampo ya  Chakula, Maji na Damu kwa ajili ya kufanyia uchunguzi, " Amesema Dk Magoma.
 Wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma ambao walipata ugonjwa wa kuhara na kutapika baada ya kula kinachodaiwa kuwa na sumu.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge akizungumza na wandishi wa habari alipofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kudaiwa kula Chakula chenye sumu
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Best Magoma Akitolea ufafanuzi kuhusiana na hali ya wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kula Chakula kinachodaiwa kuwa na sumu.

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UAMUZI WA KUTOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA ZAIDI YA 5000.

$
0
0








Itakumbukwa kuwa Desemba, 9, 2019 katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru, Mheshimiwa Rais John Magufuli alitangaza msamaha na kuwaachia huru wafungwa 5,533.

Uamuzi huo wa Rais wa kuwasamehe wafungwa alioutoa wakati akihutubia wananchi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza umekuwa ukitekelezwa na wakuu wa nchi tangu tupate uhuru mwaka 1961. Hata hivyo, uamuzi wa Rais kuwasamehe wafungwa 5533 ni wa kipekee tangu Tanzania ipate uhuru kutokana na idadi kubwa ya wafungwa aliowasehe.

Kufuatia uamuzi huo, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa uamuzi wake huo uliojaa upendo kwa wananchi anaowaongoza.

Tume inachukulia uamuzi huo wa Rais kama jambo ambalo linaweka nguvu na mkazo katika sehemu ya majukumu yake ya kuhakikisha haki za binadamu zinafurahiwa na watu wote ikiwemo wale walio magerezani.

Aidha, Tume imefurahishwa na kauli aliyoitoa Mhe. Rais katika maadhimisho hayo kuhusu kusikitishwa kwake na hali ya magereza, kwani kauli hiyo inaonesha dhamira ya dhati aliyonayo yeye binafsi na serikali yake katika kulinda na kuhifadhi haki za Wafungwa na Mahabusu katika magereza hapa nchini.

Moja ya Jukumu la Tume kwa mujibu wa ibara 130 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kifungu cha 6 (1) cha sheria ya Tume ni kutembelea magereza ili kuangalia uhifadhi wa haki za binadamu katika sehemu hizo na kutoa mapendekezo yanayofaa katika kuimarisha na kuboresha mazingira ya magereza yetu.

Tume imekuwa ikifanya ziara za mara kwa mara katika Magereza mbali mbali kwa lengo la kutekeleza jukumu hilo. Katika ziara zake Tume imekuwa ikigundua changamoto kadhaa zinazowakabili wafungwa na mahabusu zikiwemo mlundikano wa wafungwa na mahabusu, na kesi zao kuchukua muda mrefu kumalizika. Tume imekuwa ikitoa mapendekezo kwa taasisi husika kurekebisha hali hiyo.

Kwa kauli hiyo ya Mhe. Rais, Tume inaamini kuwa taasisi zenye dhamana ya kuhifadhi wafungwa na mahabusu wataongeza kasi katika kulinda na kuhifadhi haki za makundi hayo.

Tume inaamini pia, kauli hiyo itazifanya taasisi zenye dhamana ya upelelezi kufanya kazi hiyo kwa haraka ili kupunguza muda wa mahabusu kukaa magerezani kwa muda mrefu.

Kwa upande mwingine Mahakama na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka hazina budi kuongeza juhudi katika kusikiliza na kumaliza kesi za jinai kwa haraka ili kupunguza muda wa mahabusu kukaa magerezani .

Tume inaziomba taasisi zote zenye dhamana ya usimamizi wa jinai kuichukulia kauli hiyo kama ni chachu katika utekelezaji wa majukumu yao hasa ya kulinda na kuhifadhi haki za wafungwa na mahabusu magerezani.

Mwisho, Tume inatoa ushauri kwa jamii na wanufaika wa msamaha wa Mhe. Rais kama ifuatavyo; 

1. Wafungwa wote walionufaika na msamaha huo, watumie mafunzo waliyoyapata wakiwa gerezani kushirikiana na Watanzania wenzao kuisaidia Tanzania kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda.

2. Wanufaika wa msamaha huo wakayatumie vyema mafunzo na maarifa waliyoyapata kufanya kazi za uzalishaji mali na kujipatia kipato; kwani tume inaamini wakifanya hivyo ndio njia pekee ya kumpa faraja Mhe. Rais kwa uamuzi wake.

3. Tume inawasihi Watanzania wote kuwapokea ndugu zao hawa kwa mtazamo chanya na kushirikiana nao katika kazi za ujenzi wa taifa, kwani kinyume na hapo, wakiwatenga itawajengea picha ya kuona wananyanyapaliwa na hivyo kupelekea uwezekano wa
kurudia makosa yatakayowarudisha tena gerezani.

WAZIRI BASHUNGWA AWAAGIZA WATUMISHI WA WIZARA YAKE NA TAASISI ZAKE KUSOMA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Ninamuagiza kila mtumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zake kuhakikisha anasoma hotuba aliyotoa Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ya tarehe 12, Disemba 2019 kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya taifa (HKT) ya CCM uliofanyika mjini Mwanza.

Hotuba imesheheni dira, fikra na maono ambayo utekelezaji wake utaleta mageuzi makubwa ya uchumi na maendeleo ya nchi yetu na wanachi wake kufikia mwaka 2030.

Kwa muktadha huo, Wizara inafanya zoezi la kuhakikisha sera na mipango mikakati yake yote inafanyiwa mapitio ili kuongeza weledi na wigo wa Wizara kuendelea kuratibu suala zima la ujenzi wa uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda.

Tanzania ya viwanda inazidi kuonekana. Watanzania Tumemuelewa Rais wetu Magufuli, vision na political leadership yake ya kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini. Watanzania tumeamua kutokurudi nyuma. Mashambani, viwandani, wafanyakazi, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara, wajasiriamali tuchape kazi. Tushike neno tutende neno ili mageuzi haya yalete heri kwenye kila kaya nchini.

By. Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Viwanda na Biashara.
Dec 16, 2019

WAHITIMU WA VYUO MBALIMBALI WAASWA KUTOJIHUSISHA NA UHALIFU

$
0
0
Na Pamela Mollel, Arusha

Wahitimu waliohitimu katika vyuo mbalimbali hapa nchini wametakiwa kutojihusisha na aina yeyote ya uhalifu Jambo ambalo litapelekea kuharibu malengo yao ya baadae

Akizungumza katika mahafali ya 21 katika chuo cha uhasibu Njiro Arusha hivi karibuni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Adv.Fancy  Nkuhi aliwasihi wahitimu kutojiingiza katika uhalifu wowote

Alisema kuwa wapo baadhi ya wahitimu hujiingiza hata katika mitandao ya kijamii na kuanza kutukana serikali au hata watu mbalimbali

"Jamanii ukiangalia vizuri hawa wanaotukana watu hovyo pamoja na serikali hiyo ni hasira na walishindwa kuchukua hatua baada ya kuhitimu na nini kinafata na nini afanye ili kutimiza ndoto zake au malengo"Alisema Adv.Nkuhi

Pia aliwajulisha wahitimu hao kuwa safari ya mafanikio siyo rahisi Kama ambavyo wanachukulia, tena kwa kijana ni safari iliyo na mabonde mengi

"Maisha yanahitaji kujituma na kujitoa,vijana wengi sasahv hawataki kujitoa wanataka kulipwa fahamu kuwa unapojitoa ndipo unajijengea uzoefu mkubwa utakaokuwezesha wewe kuwa na mtandao,yaani kujulikana na watu hii itasaidia wewe kupiga hatua Kila siku"Alisema Adv.Nkuhi

Hata hivyo aliwataka wanafunzi kujua kuwa hapo hapo walipofika ni juhudu za wazazi wao hivyo wasiwaangushe bali kuchangamkia fursa zilizopo

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Prof.Eliamani Sedoyeka aliwataka wahitimu hao kuendelea kujifunza mambo mapya kwa kujiwekea utaratibu wa kusoma vitabu hali itakayosaidia kujiongezea maarifa mapya

Alisema kuwa ni vizuri wakajiwekea desturi ya kujiandaa kabla ya kufanya jambo lolote hiyo itasaidia kufanya vizuri zaidi

"Sisi Kama wasimamizi wenu tunatarajia maarifa na ujuzi mlioupata hapa mtumie katika kuwatumikia watanzania wote kumuunga mkono Mh Rais John Pombe Magufuli"alisema Prof.Sedoyeka

Naye mtangazaji maarufu wa redio cloud's Meena Ally ambaye alikuwa mhamasishaji kwa wahitimu,Alisema kukata tamaa ndio dhambi kubwa inayowaangusha vijana wengi

"Mimi nilianza Kazi ya utangazaji nikiwa na umri mdogo wapo walioniona siwezi kutokana na umri lakini kwa vile nilikuwa napenda kazi ya utangazaji nilijituma kutimiza ndoto zangu bila kujali mazingira niliyokuwa nayo kwa wakati huo"Alisema Meena Ally
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Adv.Fancy Nkuhi akiongea katika wahitu wa chuo cha Uhasibu Njiro katika mahafali ya 21 ya idara ya usimamizi wa Biashara,ambapo na mambo mengine aliwataka wahitimu kujiepusha na uhalifu wowote utakaopelekea kuharibu maisha yao.
 Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka akizungumza na wahitimu ambapo amewataka kutumia maarifa na ujuzi waliyoupata katika kuwatumikia watanzania wote katika kumuunga mkono Mh Rais John Pombe Magufuli
 Mtangazaji maarufu wa redio cloud's Meena Ally ambaye alikuwa kama mhamasishaji kwa wahitimu akizungumza kwenye mahafali hayo huku akijitolea mfano kwa namna alivyopambana kutimiza ndoto zake bila kujali mazingira aliyokuwa nayo kwa wakati huo

 Rejina Charles ni mhitimu ambaye alishika nafasi ya kuwa mwanafunzi bora ambaye alijishindia zawadi mbalimbali pamoja na fedha shilingi Milioni moja kutoka benki ya Posta
 Mhitimu Boniface Nkaina  ni mwanafunzi bora ambaye alijishindia zawadi mbalimbali pamoja na fedha shilingi Milioni moja kutoka benki ya posta
 Samira Mohamed katika picha ambaye alijishindia zawadi mbalimbali pamoja na fedha shilingi Milioni moja kutoka benki ya posta
 Sehemu ya wahitimu wakiwa na nyuso za furaha.
Sehemu ya wahitimu

UBALOZ WA KENYA NCHINI WAADHIMISHA MIAKA 56 YA JAMHURI YAO

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Paramagamba Kabudi akiwa pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Dan Kazungu wakikata keki katika hafla ya Maadhimisho ya Miaka 56 ya Jamhuri ya Kenya, iliyoadhimisha Desemba 12, 2019 kwenye hoteli ya Seacliff, jijini Dar es salaam.
 Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Dan Kazungu akizungumza wakati akitoa hotuba yake katika hafla ya Maadhimisho ya Miaka 56 ya Jamhuri ya Kenya, iliyoadhimisha Desemba 12, 2019 kwenye hoteli ya Seacliff, jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Paramagamba Kabudi akiwa pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Dan Kazungu wakifatilia hafla hiyo.
 Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Dan Kazungu akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo sehemu ya picha za wapigania Uhuru wa Kenya, katika hafla ya Maadhimisho ya Miaka 56 ya Jamhuri ya Kenya, iliyoadhimisha Desemba 12, 2019 kwenye hoteli ya Seacliff, jijini Dar es salaam.
 Sehemu ya wageni waalikwa katika hafla ya Maadhimisho ya Miaka 56 ya Jamhuri ya Kenya, iliyoadhimisha Desemba 12, 2019 kwenye hoteli ya Seacliff, jijini Dar es salaam.





MFK AUTOMOBILE YAZINDUA MAGARI YA KISASA AINA YA HONGYAN

$
0
0
 Wafanyabiashara wa sekta ya usafirishaji waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa magari ya kisasa ya mizigo aina ya Hongyan wakishuhudia moja kati ya magari hayo, kampuni ya MFK Automobile Tanzania kushirikiana na Hongyan kutoka China walizindua magari hayo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa MFK Automobile Tanzania, Mehboob Karmali (kushoto) akikabidhiwa funguo na Mkurugenzi wa SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China, Winnie Xiong kuashiria uzinduzi wa magari ya mizigo ya kisasa aina ya Hongyan yenye uwezo wa hali ya juu na ya kwanza kutumia katika nchi za Afrika Mashariki kwenye  hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa MFK Automobile Tanzania, Ali Jawad Karmali akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kisasa ya mizigo kutoka china aina ya Hongyan
 Mkurugenzi wa SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China, Winnie Xiong akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kisasa ya mizigo kutoka china aina ya Hongyan
 Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), pia mfanyabiashara maarufu MS. Angelina Ngalula akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kisasa ya mizigo kutoka china aina ya Hongyan
 Picha ya pamoja kati ya  Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), pia mfanyabiashara maarufu MS. Angelina Ngalula (wa nne kulia) na viongozi wa MFK Automobile Tanzania na SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China kwenye hafla ya uzinduzi wa Hongyan.


 Kampuni ya MFK Automobile ambayo inajihusisha na uingizaji, usambazaji na uuzaji wa magari ya mizigo nchini, imezindua magari ya kisasa yenye uwezo wa hali ya juu na ya kwanza kutumia katika nchi za Afrika Mashariki. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa MFK Automobile Tanzania, Ali Jawad Karmali alisema shukrani za pekee kwenu kwa kuitikia wito wetu wa mualiko wa uzinduzi wa vifaa vipya vya kampuni ya MFK, Gari ambazo kwa mara ya kwanza kuingia Afrika Mashariki aina ya HONGYAN. 

MFK ni kampuni mpya ambayo inajishughulisha na uingizaji, usambazaji na uuzaji wa magari mbalimbali aina ya Tiper na Tracto head, tumekuja kuunga jitihada za serikali za kuelekea uchumi wa viwanda ambapo utawezesha fursa mbalimbali katika kukuza uchumi, tutatengeneza fursa kwa wasafiri na wasafirishaji na ndio sababu kuu iliyotufanya kuleta magari yenye teknolojia ya ulaya na umadhubuti wa China alisema Karmali 

Katika magari haya ya Hongyan, MFK Automobile inawapa Watanzania bidhaa yenye ubora kwa mtumiaji na mmiliki,bila usumbufu wowote na kiufundi wa gari hizi za HONGYAN, zina manufaa mengi kwa mmiliki kwa kumuwezesha kuhimili barabara zozote nchini, matumizi madogo ya mafuta na zina chumba cha kupumzika kwa dereva aliendelea kusema Karmali. 

Pia tumeona fursa katika sekta ya usafiri na usafirishaji, hivyo tumejipanga katika kuleta vifaa vyenye ubora ambavyo vitahakikisha Tanzania inakuwa kituo kikuu katika sekta hii kwenye ukanda huu wa Afrika ya mashariki na kati. 

“Lengo kuu la kampuni yetu ni kufanya Tanzania ipate bidhaa zenye ubora na za bei nafuu zinazoendana na kasi ya uchumi wa viwanda ambayo ni moja ya sera ya serikali ya awamu ya tano ili kufikia uchumi huo wa kati ifikapo mwaka 2025, MFK tunasimamia hilo”, alimalizia kusema Karmali. 

Tunajisikia fahari kufanya kazi na kampuni hii ya utengenezaji wa magari,katika ushirikiano huu wa IVECO GROUP NA WASHIRIKA WAO WA CHINA HONGYAN. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), pia mfanyabiashara maarufu MS. Angelina Ngalula alisema “sekta ya usafirishaji imetoka mbali sana nakumbuka tulianza tukiwa na malori aina ya Scania 682 hadi kufikia sasa tunatumia magari ya kisasa zaidi, tunawashukuru MFK kwa mpango huu wa kuleta magari haya ya kisasa, pia yatatufanya sisi wafanya biashara kuyanunua kwa umoja wetu tuuweze kufanya sekta hii ya usafirisahji kuwa pana zaidi ukanda huu,. Pia nawaomba mabenki yaweze kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa sekta hii kwani haina ubabaishaji kurudisha mikopo hiyo. alisema Ngalula. 

Aliongezea kusema Ngalula “tuna bidhaa nyingi sana zinahitaji usafirishaji kama vile mazao, shaba, madini mbalimbali, hii itasaidia kuweka vituo vya kufanyia huduma(service) za magari na kuuza vipuri mikoani ili kuepusha wizi unaotokana na madereva wasio waaminifu”. 

Hata standard gauge SGR itahitaji zaidi kushirikiana na sekta hii ya usafirishaji ili kuwafikishia mizigo kwa urahisi zaidi, huwezi kuwa na Treni bila kuwa na magari ya mizigo, ukizingatia usafirishaji wa kutumia barabara unahitajika kwa asilimia 75 . alimalizia kusema Ngalula. 

Nae Mkurugenzi wa SAIV IVECO-HONGYAN kutoka China, -MS Winnie Xiong alisema hii ni fursa ya kipekee kwa kampuni yetu kuleta magari haya nchini Tanzania, hasa ukizingatia Tanzania na china zimeweka mahusiano ya kidiplomasia miaka 55 hadi sasa tokea mwezi Aprili 26, 1964, nchi hizi mbili zimejenga uhusiano imara na kushirikiana bega kwa bega. Leo nawaahidi kuwa Hongyan itazalisha magari bora ya mizigo kwa soko la Tanzania kwa kupitia washirika wetu MFK na kuwawezesha wateja wetu kugharamia huduma na vipuri vya magari haya kwa bei nafuu. alimaliza kusema Xiong.



MAOFISA AFYA WATAKIWA KUWAKINGA WANANCHI DHIDI YA MAGONJWA-DKT. SUBI

$
0
0

Na. Catherine Sungura,Dodoma

Maofisa afya wa mikoa na halmashauri wametakiwa kusimamia afya ya jamii kwenye maeneo yao ili wananchi wajikinge dhidi ya magonjwa yakuambukiza na yele yasiyoambukiza.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa kinga Dkt. Leonard Subi wakati akiongea na maofisa hao ambao wanakutana jijini hapa  kwa  kikao kazi cha siku tatu wakijadili utekelezaji wa maazimio yaliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa kwanza mwaka jana  na  Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

“Mkutano huu ni wa pili mwaka huu,ni mkutano muhimu kwa maofisa afya kwani ndio wasimamizi wa shughuli za afya katika ngazi za jamii kwa kuhakikisha wananchi wanajikinga na maradhi, kula chakula bora kuishi makazi bora,usafi wa mazingira pamoja na kuwa vyoo bora”.Amesema Dkt. Subi

Aidha, amesema katika mkutano huu mambo mbali mbali yatajadiliwa ikiwemo  afya mazingira,usafi na uchafuzi wa mazingira na kila kinachotumiwa na kumzunguka  mwananchi ,pia wataangalia mabadiliko ya tabia nchi na kupata taarifa kutoka ngazi za mikoa ni jinsi gani walivyotekeleza majukumu yao.

“Maafisa afya muendelee kuishauri wizara kwa kutumia takwimu kwani tunatarajia mkutano huu mtabadilishana uzoefu  kutoka sehemu zenu za kazi,kama wizara tumekua tukitengeneza sera na miongozo mbali mbali ya kudhibiti maradhi yote yanayoweza kuathiri afya za binadamu hivyo kazi ya wizara ni kukusanya taarifa,kuchakata na kuzitolea miongozo na maelekezo”. Aliongeza Dkt. Subi.

Hata hivyo amesema maofisa hao wana majukumu ya kusimamia na  kulinda afya mipakani ili kusiingie magonjwa ya milipuko kutoka nje hususan  nchi za jirani pamoja na utoaji wa chanjo ambapo Tanzania ipo vizuri.

Mkutano huo ambao utafunguliwa kesho na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu umebeba Kauli mbiu isemayo “Huduma bora za afya mazingira na usafi ni kichocheo muhimu cha uchumi endelevu.
 Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akieleza jambo mbele ya Maafisa Afya wa Mikoa na Halmashauri, wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya usafi wa mazingira.
 Afisa kutoka Idara ya Mazingira Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto Bw. Anyitike Mwakitalima akieleza mafanikio mbali mbali yaliyopatikana kutokana na afua mbali mbali za usafi wa mazingira zinazotekelezwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau.

 Maafisa Afya kutoka Mikoa, Halmashauri na Wadau wakifuatilia kwa makini neno kutoka kwa Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi.


Maji ya JIBU yawapa fursa wajasiriamali

$
0
0

 "Tunaamini kila mji nchini Tanzania unapaswa kuwa na mjasiriamali wa ndani anayemiliki kiwanda cha kutengeneza maji safi ya kunywa. Wanapaswa kuwa wakizalisha na kuuza maji safi, yenye bei nafuu na yenye maji ya chupa. Tuko hapa kugharamia na kuandaa mapinduzi haya kwa wajasiriamali wa hapa nchini." - Jibu Tanzania. 

Kampuni ya Maji nchini, Tanzania Maji Jibu, kampuni iliyozaliwa katika mkoa wa Kaskazini mwa Tanzania, Arusha, inafanya mabadiliko kupitia mfano wa tofauti kulinganisha na kampuni zingine za maji zilizopo chini. 
 Kwa hiyo wanafanya nini? Katika taarifa kwa wanahabari jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Tayeb Noorbhai, alisema 'tuko hapa kukuza na kuwapa wajasiriamali fursa za biashara.' 

Imetengeneza dhana mbili ambayo inaamini wajasiriamali wanaofaa watapata fursa ambazo zitawawezesha sio tu kutoa maji yao ya kunywa katika kiwanda cha biashara lakini pia hutumia maeneo yale kama sehemu zilizo wazi za kuuza maji kwa rejareja na pia viwe 'vituo vya usambazaji' kwa bidhaa zao kufikia maeneo majirani popote nchini Tanzania.
Kulingana na taarifa hiyo, dhana hizo mbili zilizopewa jina la 'Franchise Opportunity' na 'Jibu Re-fill' zilibuniwa kutokana ya maono ya kampuni hiyo ya kukuza ujasirimali nchini na pia kuhakikisha kuwa watanzania wote wanapata maji safi na salama ya kunywa kwa bei nafuu kabisa.

Akielezea wazo hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Tayeb Noorbhai, alisema Dhana ya 'Franchise Opportunity' inamaanisha kutoa fursa kwa watanzania wamiliki kiwanda vyao vya maji - "Ni nafasi nzuri kwa wajasiriamali kupata kipato kikubwa lakini pia kujenge nafasi za ajira kwa jamii zao na kuunda upatikanaji wa bei bora za maji yenye ladha nzuri. Tunafadhili, kuanzisha kwa viwanda vyao chini kutumia mfano wetu wa kipekee wa udadisi na kutoa mafunzo kamili ya biashara na uzalishaji kusaidia kila mjasiriamali.

 Ni viwanda vyenye viwango vya hali juu zaidi ili waweze kuendesha viwanda vyao wenyewe. Tunafadhili kila mjasiliamali wa eneo husika na mfumo wa utakaso wa maji wa osmosis na uzalishaji wa hali ya juu, kwa kufuata udhibiti kamili wa alama ya viwango vya Kitanzania. Haijawahi kuwa na njia rahisi ya kuanzisha kiwanda chako cha maji nchini Tanzania” Mkurugenzi Mtendaji alisema.

Jibu Group inkuwa katika nchi mbali mbali za Kiafrika. Mfumo huo ulianzia katika maeneo madogo ya miji wa Rwanda kabla ya kufikia Uganda, Kenya, Zambia, Burundi na Barani Afrika. Tayari zaidi ya lita milioni mia za maji zimehudumiwa chini ya chapa ya Jibu ambayo inakuwa jina la kaya lenye zaidi ya vibalo 100 Barani Afrika.

Jacqueline, mkazi wa Arusha alisema, "Jibu amefumbua macho yangu kwa vitu vingi ambavyo sikuzingatia. Nilikuwa nanunua chupa 7 hadi 8 za lita 1 kwa wiki. Wakati huo, sikuelewa ni jinsi gani nilikuwa 'nikichoma shimo' kwenye mkoba wangu lakini pia nilikuwa nachangia kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira kupitia plastiki zinazotumika mara moja. Siku moja, jirani yangu aliniambia juu ya kuweza kujaza aina mpya ya chupa ya lita 20 na bomba lake kwa TSh 5,000 tu. Nilidhani, HAIWEZEKANI. 

Alisema hata sitahitaji mashine ya kutolea maji na ninaweza kujaza tena. Kwahiyo nilifikiria, kutembelea duka lao la biashara huko Sanawari, Arusha ninakoishi. Kwa mshangao wangu, ilikuwa kweli. Walikuwa na aina mbali mbali za chupa zingine. Bidhaa zao zote zilikuwa za kujaza na za bei nafuu sana.

 Hapo kwa papo sikupoteza mda na kuwa sehemu ya mabadiliko na hivi sasa, familia yangu na mimi tunatumia Jibu kama suluhisho la maji nyumbani kwa zaidi ya mwaka mmoja. Chupa iliyo na bomba ni rahisi kutumia kwa familia yangu yote. Ni tofauti sana na inatutosha." Maono ya Jibu ni kuwa na chupa ya ujazo wa lita 20 kwa kila kaya (familia) Tanzania ili matumizi ya plastiki moja moja yapunguzwe na familia zichague kutumia chupa za maji za kujaza kila maji yakiisha. 

Taarifa kutoka kwa Meneja Masoko, Cuthbert Mbowe, iliongeza kuwa kampuni hiyo inashukuru kwa kuongezeka kwa mahitaji ya wateja - "Tumefurahi kuwa na idadi kubwa ya wafuasi waaminifu ambao wanaamini kazi yetu na kuendelea kutupatia maoni ya mahali tunapohitaji kuboresha na jinsi tunaweza kuwatumikia vyema. Kwetu hii inamaana kubwa kwani tunayo timu yenye nguvu inayofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kila familia inatumia maji safi na salama.

 Tayari tumekua kwa haraka kufungua maeneo 15 kwa mkoa wa Arusha, Usa-River, Babati, Singida, Same, Dodoma, Iringa, na sasa Dar es Salaam. Nusu ya wamiliki na waongozaji wetu wa viwanda hivi ni wanawake. Lengo letu ni kuwa na Jibu Franchise katika kila kitongoji kikubwa kinachoendeshwa na mjasiriamali aliyejitolea kwa wa Tanzania, ni fursa kubwa kwa watanzania na wafanyabiashara. "Alisema Cuthbert.

Kuhusu Jibu Tanzania Jibu ni kampuni ambayo inaweka kipaumbele mapinduzi katika kijamii. Jibu imeanzisha suluhisho lenye nguvu ili kuhakikisha kila mtu anapata mahitaji ya msingi ya wanadamu, kama vile maji ya kunywa. Ni tofauti na inafanya kazi.

 Njia yetu ya mseto huchochea ukuaji wa uchumi na uhuru wa kujiboresha, wakati tunapowapa wanaohitaji maji salama ya kunywa. Kwa habari zaidi juu ya jinsi unaweza kuwa mmiliki wa biashara ya Franchise au kuwa sehemu ya uvumbuzi, piga simu kwa 0764-806682 au Jibu hotline 0757-121212. Barua pepe: tanzania@jibuco.com. Tovuti: www.jibuco.com/tz.

Wachuuzi wa maziwa eneo la ubungo wapewa wiki mbili kutafuta eneo rasmi la biashara ya maziwa .

$
0
0
Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Dkt.Sophia Mlote  ametoa wiki mbili kwa wachuuzi wa maziwa eneo la ubungo kutafuta eneo rasmi la kuendesha biashara ya maziwa kwani eneo linalotumika kwa sasa linahatarisha usalama wa maziwa kwa afya ya mlaji.

Hayo alisema leo (16.12.2019) wakati wa zoezi la ukaguzi wa ubora wa maziwa liloambatana na utoaji wa elimu kwa wadau katika eneo maarufu la uuzaji wa maziwa la ubungo jijini Dar es Salaam.

Dkt.Mlote amesema eneo hilo halijasajiliwa na Bodi na si salama kwa uendeshaji wa biashara maziwa kwa mujibu wa kanuni na sheria ya maziwa ya mwaka (2004).

Dkt.Mlote amesema ujenzi unaoendelea katika eneo la ubungo sambamba na uchafu wa mazingira katika eneo hilo unahatarisha usalama wa maziwa kwa mlaji na hivyo kuwataka wachuuzi hao kutafuta mbadala wa eneo lingine kwa ajili ya uendeshaji wa biashara ya maziwa.

"Natoa wiki mbili mtafute mahali tupasajili"  alisema

Aidha, Dkt Mlote ametoa katazo la matumizi ya vyombo vya plastic katika kuhifadhi maziwa kwani vyombo hivyo hufanya uchafuzi wa maziwa na kuhatarisha afya ya mlaji.

Dkt Mlote amewataka wachuuzi hao kutumia vyombo vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria katika kutunzia maziwa ambavyo ni metaliki na aluminiamu.

Katika zoezi hilo bodi ya maziwa iliweza kubaini uuzwaji holela wa maziwa usiofuata sheria na kanuni na hivyo kutoa elimu kwa wadau kuhusu sheria ya maziwa ikiwemo usajili wa wadau.
Afisa Usindikaji wa Bodi ya Maziwa  Emmanuel Mushi akitoa elimu ya upimaji wa ubora wa maziwa kwa wachuuzi wa maziwa leo maeneo ya ubungo.


Baadhi ya wachuuzi wa Maziwa eneo la Ubungo
Wachuuzi wa Maziwa eneo la Ubungo


KIPCHONGE MWANAMICHEZO BORA WA BBC 2019.

$
0
0
Mwanariadha Eliud Kipchoge amejishindia taji la BBC la kuwa ''Mwanamichezo Bora wa mwaka Duniani''.

Kipchoge alikuwa mtu wa kwanza katika historia ya mbio za Marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini ya saa mbili Oktoba, 2019.

Raia huyo wa Kenya, 35, alikamilisha muda wa kilomita 42.2 katika saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindano la Ineos Challenge mjini Vienna nchini Austria.

Miezi sita kaba ya ushindi wake, Kipchoge alikuwa ameshinda ubingwa wa London Marathon mara nne mfululizo.

Kipchoge, alipata medali ya dhahabu katika mbio za Marathon, Rio 2016, na kuvunja rekodi yake mwenyewe ya London aliyoiweka 2016, kwa sekunde 28.

Kupitia kura zilizopigwa kwa njia ya mtandao, Kipchoge amewashinda mwanariadha wa mazoezi ya viungo Simone Biles, nahodha wa timu ya taifa ya Raga ya Afrika Kusini Siya Kolisi, mchezaji Kriketi wa Australia Steve Smith, mchezaji gofu duniani Tiger Woods na mshambuliaji wa Marekani Megan Rapinoe, ambaye aliongoza tena timu yake katika mashindano ya Kombe la Dunia msimu wa joto uliopita.

Mshindi wa mwaka jana alikuwa mchezaji gofu Francesco Molinari, aliyeshinda mashindano ya Dunia 2018, pamoja na mashindano yote matano ya mechi za kombe la Ryder mjini Paris.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images