Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

KITUO CHA AFYA KOME CHAFANYA UPASUAJI WA KWANZA

$
0
0
Wataalam wa chumba cha upasuaji  kituo cha afya Kome wakiwa kwenye chumba hicho.
*************************
Na.Catherine Sungura
Kituo cha afya Kome kilichopo halmashauri ya buchosa wilayani Sengerema kimefanikiwa kufanya upasuaji wa kwanza  wa dharura wa kumtoa mtoto tumboni na hivyo kumuokoa mama na mtoto wake.
 
Akiandika kwenye mtandao wa kijamii Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa kwa mara ya kwanza kituo hicho kimeweza kufanya upasuaji huo baada ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  kujenga “theatre” na kuweka vifaa tiba kwenye kituo hicho.
 
Waziri Ummy ameendelea kuandika kuwa chumba hicho cha upasuaji ambacho kipo kituoni hapo kitawasaidia akina mama wajawazito wa kisiwa cha kome watakaopata uzazi pingamizi na hivyo kutokufuata huduma hizo wilayani sengerema na hivyo kutokuvuka tena maji.
 
“Hakika tumedhamiria kuokoa maisha  ya akina mama wajawazito na watoto wachanga,tutaendelea kuchukua hatua ili kuhakikisha huduma za uzazi  za dharura ikiwemo ya upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni(CEmONC) zinapatikana katika vituo vyote vya afya vya umma ,mama na mtoto huyo mwenye uzito wa kilo 3 na nusu wanaendelea vizuri”Amesema waziri Ummy
 
Naye Mganga Mkuu wa halmashauri ya buchosha Dkt. Ernest Chacha amesema walimpokea mama huyo kituoni hapo siku ya ijumaa ambaye alikua akihudhuria kliniki kwenye zahanati moja huko kisiwani hakuweza kujifungua kawaida kwani alikua akikabiliwa na uchungu pingamizi kwani nyonga zake  hazikuwa zinapanuka hivyo ili kumuokoa ilibidi afanyiwe upasuaji kuweza kumuokoa mama pamoja na mtoto .
 
Dkt. Chacha ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa uboreshaji wa vituo vya afya nchini ikiwemo kituo cha afya cha kome ambacho kipo kisiwani kwa kuboresha miundombinu kwa kujengewa chumba cha upasuaji pamoja na kuwekewa vifaa tiba hivyo kusaidia kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na watoto wachanga hususan visiwani humo.
 
“Wananchi walikua wanapata adha kubwa sana ya kuvuka maji kutoka kisiwani na kufuata huduma kwenye hospitali ya wilaya iliyopo sengerema,tunamshukuru Waziri Ummy Mwalimu kwa kuiagiza MSD kutufungia taa kwenye chumba cha upasuaji wakati wa ziara yake hivi karibuni visiwani hapa kwani tumeweza kuokoa maisha ya huyu mama muda mfupi baada ya taa hizo kufungwa”Amesema Dkt. chacha 
 
Hivi karibu waziri wa afya alitembelea kisiwa hicho na kuwaahidi  kuwapatia xray mashine ya kidigitali  kwenye kituo hicho cha afya na kuwataka MSD kufunga taa kwenye chumba hicho cha upasuaji mara moja.
Kisiwa cha kome kimeongeza  idadi ya akina mama wanaojifungulia  kwenye vituo vya afya  kwa  asilimia 80  kwa mwaka ambapo wastani akina mama  50 wanajifungulia kwa mwezi

MEYA SITA AVIPONGEZA VYAMA VYA USHIRIKA KINONDONI KWA KUTOA VIFAA VYA HOSPITAL KATIKA KITUO CHA AFYA KIGOGO

$
0
0


Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sita  akipokea mashuka na foronya zilizotolewa na vikundi vya ushirika vya Halmashauri hiyo, wanaoshuhudia ni wanakikundi hao pamoja na Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri hiyo  Ndugu Salehe Hija .
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sita  akikata utepe kwa ajili ya kuzindua mfumo wa usomaji data leo wakati alikuwa akikabidhiwa vifaa vya Hospital na vyama vya ushirika kutoka katika Halmashauri hiyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni  Mhe. Benjamini Sita , akizungumza na vikundi vya ushirika wakati akikabidhiwa vifaa vya Hospital vilivyotolewa na vikundi hivyo. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri hiyo  Ndugu Salehe Hija .
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sita  akisamiliana na Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri hiyo Salehe Hija.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sita  akimkabidhi mashuka Mganga mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Kigogo mara baada ya vyama hivyo kumkabidhi vifaa hivyo.
Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri hiyo  Ndugu Salehe Hija, mwenye miwani akimueleza jambo  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sita  wakati alipokuwa akipokea magodoro kutoka vikundi vya ushirika.
***************************
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sita amevipongeza vyama vya ushirika vilivyopo katika Halmashauri hiyo kwa kujitolea vifaa vya Hospitali katika Kituo Cha Afya cha Kigogo.
Aidha vyama hivyo vimemkabidhi Mhe. Sita  Magodoro 30, mashuka na foronya  150 ambapo wamesema kuwa vitasaidia wagonjwa watakaokuwa wanapatiwa matibabu katika kituo hicho.

 Akizungumza na vyama hivyo kabla ya kukabidhiwa vifaa hivyo, Meya Sita amesema kuwa  vitasaidia kuwahudumia wananchi mbalimbali watakao kuwa wanapatiwa huduma katika Kituo hicho cha Afya na kuwasihi  wengine kujitokeze kuchangia.

Amefafanua kuwa suala la Afya ni pana na kwamba Halmashauri iliamua kujenga Kituo hicho cha Afya ili kuwezesha wananchi kupata huduma kwa haraka na urahisi kutoka maeneo mbalimbali.

Ameeleza kuwa, Halmashauri ya Kinondoni inahudumia watu kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo Bagamoyo, na kwamba  kulingana na wingi huo, imeweza kununua eneo hilo na  kujenga Kituo hicho cha Afya na kwamba watu kutoka shemu mbalimbali watapata huduma safi na bora inayokidhi viwango.

 Ameongeza kuwa” Tumepambana usiku na mchana, na mpongeza sana Mkurugenzi wetu , Ndugu Aron Kagurumjuli na watendaji wote kwa kufanikisha ujenzi wa Kituo hichi cha Afya, ambacho kitahudumia watu sio Kigogo tu , bali kitatoa huduma Ilala, Ubungo, na maeneo mengine kama ilivyo kwa Kituo cha Afya cha Magomeni.” amesema Meya Sita.

Hata hivyo Mhe. Sita emesema “ ninawapongeza sana, ninaimani wadau wengine watakapo ona hivi, itawakumbusha kuona kwamba wanawajibu kufanya hivi kama walivyofanya hawa vyama vya ushirika kutambua umuhimu wa afya katika Halmashauri yetu” ameongeza.

Kwa upande wake  Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji, na Ushirika , Ndugu. Salehe Hija amekipongeza kitengo cha ushirika kwa kuandaa vifaa hivyo na kukabidhi katika Kituo hicho cha Afya na kusema kuwa kitendo hicho kitaonyesha njia  kwa watu wengine kujitolea.

Aidha Hija amesema kuwa vifaa hivyo vilivyotolewa vinathamani ya shilingi milioni 6.7 huku  kituo hicho kikiwa na uhitaji wa vitanda 150 ambapo  kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa Kituo hicho , magodoro hayo  yaliyotolewa ni ni sawa na asilimia 20 ya mahitaji hayo.

RAIS MAGUFULI AONGOZA WATANZANIA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA YA BOMBARDIER ILIYOWASILI JIJINI MWANZA

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameketi na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ndani ya ndege mpya iliyonunuliwa na Serikali aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege hiyo mara baada ya kuwasili.
Picha mbalimbali zikionesha Ndege hiyo ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza wakati ikitokea nchini Canada. PICHA NA IKULU

WIZARA YA MAJIYAENDELEA KUWABANA WAKANDARASI

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (katikati) akikagua ujenzi wa mradi wa maji wa Orukesment Wilayani Simanjiro wakati wa ziara yake kwenye mradi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (wa pili kushoto) akikagua ujenzi wa mradi wa maji wa Orukesment Wilayani Simanjiro wakati wa ziara yake kwenye mradi. Kushoto ni mwakilishi wa Kampuni ya Jandu Plumbers, Mhandisi Kotturu Ramnadh.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkandarasi Jandu Plumbers kuhusiana na uekelezaji wa mradi wa maji wa Orukesment Wilayani Simanjiro. Katikati ni mwakilishi wa Mkandarasi, Kotturu Ramnadh.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (katikati) akikagua ujenzi wa mradi wa maji wa Orukesment Wilayani Simanjiro wakati wa ziara yake ya kukagua hatua ya ujenzi wa mradi.

**************************
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony  Sanga amemtaka Mkandarasi Jandu Plumbers wa Arusha anayejenga mradi wa Maji wa Orukesment Wilayani Simanjiro kuukamilisha kwa muda uliyopangwa.
Ametoa maelekezo hayo Desemba 14, 2019 alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Wilayani Simanjiro sambamba na kuzungumza na mkandarasi.

Akiwa katika ukaguzi wa utekezaji wa mradi, Mhandisi Sanga alibaini shughuli zinazoendelea kutekelezwa na Mkandarasi kuegemea zaidi maeneo ambayo hayapelekei wananchi kupata huduma ya maji mapema iwezekanavyo kama ilivyo dhamira ya Serikali. 

Alibainisha kwamba Mkandarasi anajenga maeneo ambayo siyo kipaumbele cha mradi na hivyo alimtaka kuhakikisha anaelekeza nguvu zaidi kwenye ujenzi wa maeneo yatakayowapatia wananchi maji ikiwemo ujenzi wa chanzo, kituo cha tiba ya maji na bomba kuu la kusafirishia maji. 

”Nilichokiona hapa kwenye mradi ni kwamba Mkandarasi amejikita zaidi katika kujenga majengo ya ofisi na nyumba za wafanyakazi ambayo hayapelekei wananchi waanze kupata maji badala ya kujielekeza kwenye maeneo yenye tija ya kuleta huduma ya maji kwa haraka ili wananchi waanze kunufaika,” alisema Mhandisi Sanga. 

Mhandisi Sanga alifafanua kwamba mradi wa maji katika Mji wa Orukesment unao umuhimu mkubwa kwa wananchi wa maeneo hayo hasa ikizingatiwa kuwa umekuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu. 
“Wananchi wameusubiri sana huu mradi, wamekuwa na shauku kubwa ya kuanza kupata huduma kutoka hapa, sijaridhishwa na huu utaratibu anaoendelea nao Mkandarasi, ningependa kuona matokeo ya haraka kutoka hapa,” alisisitiza Mhandisi Sanga. 

Awali akiwasilisha taarifa ya maendeleo  ya ujenzi wa  mradi  huo kwa Mhandisi Sanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Babati (BAWASA), Mhandisi Iddi  Msuya ambao ndio wasimamizi wa mradi  huo alieleza tayari wamemuagiza Mkandarasi kuhakikisha anaongeza nguvu kazi ili kutekeleza maeneo nyeti kwa haraka zaidi.
Alibainisha kuwa kukamilika kwa mradi kutanufaisha zaidi ya wakazi 52,000 na mifugo katika mji wa Orkesumet pamoja na vijiji vinavyozunguka mji huo.

Mhandisi Msuya alimuahidi Naibu Katibu Mkuu Sanga kuhakikisha anasimamia vyema maelekezo aliyotoa ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma mapema iwezekanavyo. Kwa upande wake mwakilishi wa Kampuni ya Jandu Plumbers, Mhandisi Kotturu Ramnadh aliahidi kukamilisha ujenzi wa mradi huo katika kipindi kilichowekwa cha mwezi Aprili, 2020. 

Aidha aliahidi kuongeza nguvu katika ujenzi wa chanzo na kituo cha tiba ya maji sambama na bomba kuu la kusafirisha maji kama ilivyoelekezwa na Naibu Katibu Mkuu Sanga. 

Mradi wa maji Orukesment unatekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Nchi za Kiarabu kwa nchi za Afrika (BADEA) na Mfuko wa Maendeleo wa nchi zinazozalisha mafuta (OFID) kupitia mkopo wa masharti nafuu ambao umetengewa jumla ya Dola za Marekani Milioni 18.42

WAZIRI HASUNGA APIGA MARUFUKU VISIMA KUCHIMBWA KWA GAHARAMA YA ZAIDI YA MIL 20 WILAYANI MTWARA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua skimu ya umwagiliaji ya Kitere iliyopo katika kata ya Kitere Halmashauri ya wilaya ya Mtwara wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoa Mtwara kukagua miradi ya umwagiliaji, tarehe 14 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua skimu ya umwagiliaji ya Kitere iliyopo katika kata ya Kitere Halmashauri ya wilaya ya Mtwara wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoa Mtwara kukagua miradi ya umwagiliaji, tarehe 14 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wakulima mara baada ya kukagua skimu ya umwagiliaji ya Kitere iliyopo katika kata ya Kitere Halmashauri ya wilaya ya Mtwara wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoa Mtwara kukagua miradi ya umwagiliaji, tarehe 14 Disemba 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameiagiza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kubadili matumizi ya gharama za uchimbaji wa visima kutoka Tsh Milioni 160 mpaka kuchimba kwa Tsh Milioni 20.


Waziri Hasunga ametoa agizo hilo tarehe 14 Disemba 2019 wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kutembelea skimu ya umwagiliaji ya Kitere iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.


Amesema kuwa gharama za uchimbaji wa kisima kimoja kwa ajili ya umwagiliaji haipaswi kuzidi shilingi Milioni 20 kwani kufanya hivyo ni kinyume na utaratibu na kushindwa kuakisi kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.


Katika ziara hiyo Waziri Hasunga ameiagiza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuchimba visima vitatu katika eneo hilo kwa kiasi cha shilingi milioni 60 ikiwa ni shilingi milioni 20 kwa kila kisima kimoja.


Amesema kuwa umefika wakati wa wakulima kuachana na kilimo cha kutegemea mvua za msimu badala yake kuhakikisha kuwa wanalima kilimo bora cha umwagiliaji.


Kadhalika amekumbushia agizo lake alilolitoa hivi karibuni la kila mkoa kuwa na Afisa umwagiliaji wa mkoa huku wilaya zote zenye skimu za umwagiliaji kuwa na afisa umwagiliaji wa wilaya.


Waziri Hasunga amesema kuwa mkakati huo madhubuti wa serikali kuhakikisha kunakuwa na skimu nyingi za umwagiliaji utaimarisha sekta ya kilimo jambo litakaloongeza kipato cha mtu mmoja mmoja sambamba na Taifa kwa ujumla wake.


Kuhusu mkakati wa serikali kuwa na kiasi kikubwa cha umwagiliaji, ameiagiza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ndani ya kipindi cha miaka miwili kuongeza eneo la umwagiliaji ili kufikia hekta milioni moja huku kakiongeza kuwa hadi kufikia mwaka 2025 eneo la umwagiliaji liwe limefikia Hekta milioni tano.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda amewapongeza wakulima wa skimu hiyo kwa kuimarisha sekta ya kilimo huku akisisitiza kuwa serikali inapaswa kuongeza mkakati madhubuti wa kuimarisha masoko ya mazao ya wakulima.


Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Halmashauri Wilaya ya Mtwara Ndg Joseph Tesha akitoa taarifa fupi mbele ya Waziri wa Kilimo amesema kuwa skimu hiyo ya Kitere iliyopo katika kata ya Kitere inayohudumia vijiji vya Lilido na Chemchem ina jumla ya eneo la Hekta 920 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji huku eneo lililoendelezwa likiwa ni jumla ya Hekta 310 pekee.


Waziri Hasunga yupo mkoani Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo awali alitembelea mkoa wa Pwani na Lindi kwa ajili ya kukagua hali ya uuzaji wa korosho msimu wa 2019/2020, kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho zilizonunuliwa na serikali msimu wa mwaka 2018/2019 na kukagua skimu za umwagiliaji.

MAKAMU WA RAIS SAMIA AFUNGUA KITUO CHA AFYA UKARA

$
0
0



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Mnara wa kumbukumbu  Eneo waklipoozikwa Wahanga wa Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere Kisiwani  Ukara Wilayani Ukerewe leo Disemba 14,2019 wakati malipotembekea Eneo hilo.
Picha ya Wananchi wa Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akikata utepe kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe leo Disemba 14,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akimpa pole Mtoto Femia Sabato (3)mkazi wa Bwisya Ukara aliyelazwa katika  Kituo cha Afya  Bwisya Ukara kwa matibabu mara baada  kuzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Wilayani Ukerewe leo Disemba 14,2019. kushoto ni Bibi wa Mtoto huyo Silimagi Manyeji.
Picha ya Wananchi wa Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza.
Msanii wa Kikundi cha Sanaa cha Ngoma ya Matoigaa Charoo cha Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza Goabth Bwere akionesha Umahiri  wake katika uwanja wa Bwisye Ukara wakati wa Hafla ya  kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe leo Disemba 14,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akihutubia Wananchi wa wa Bwisye Ukara Wilayani Ukerewe baada ya kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe leo Disemba 14,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela alipowasili Uwanja wa ndege wa Mwanza  akitokea Kisiwani ukara wilayani Ukerewe  Baada ya kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe leo Disemba 14,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa Kikundi cha Sanaa cha Ngoma ya Matoigaa Charoo cha Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza Goabth Bwere katika uwanja wa Bwisye Baada ya Makamu wa Rais  kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe leo Disemba 14,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa Kikundi cha Sanaa cha Ngoma ya Matoigaa Charoo cha Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza Goabth Bwere katika uwanja wa Bwisye Baada ya Makamu wa Rais  kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe leo Disemba 14,2019.
Picha ya Wananchi wa Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza.
(Picha Na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Benki ya NBC yakutana na wateja wake kuwashukuru kwa mahusiano bora kwa mwaka 2019

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Fedha wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Abdallah Mwaduga katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni Ofisa katika kitengo cha wateja binafsi wa NBC, Rehema Chonde.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia), akifurahi pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Kampuni  G4S Cash Solutions Tanzania, Hassan Nuru na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya G4S Secure Solutions Tanzania, Barry Hogg.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akisalimia na Mkurugenzi wa Kampuni ya Enterprises Business Department, Tony Wu huku Ofisa Fedha Mkuu wa Kampuni ya Huawei Technologies Tanzania, Mao Jinbao akiangalia katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.

 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NBC, Dk. Kassim Hussein (kulia), akisalimiana na baadhi ya wateja waliohudhuria  hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.

 Mkurugenzi wa Wateja wa Makampuni wa Benki ya NBC, Linley Kapya (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Fedha wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Abdallah Mwaduga katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni Ofisa katika kitengo cha wateja binafsi wa NBC, Rehema Chonde.

 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NBC, Dk. Kassim Hussein (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Anga Tanzania, Hamza Johari, huku Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe (katikati), akiangalia,  katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.            
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis ndunguru (katikati), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi (kushoto), huku Mwenyekiti wa Kampuni ya Chelsea Starway Group, Martin Mbwana akisikiliza, katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC afanya ziara ya kikazi Kanda ya Ziwa.*akutana na kufanya mazungumzo na mkuu wa mkoa wa Kagera

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Marco Saguti (wa tatu kushoto), akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, wakati yeye na ujumbe wake walipomtembelea ofisini kwake katika ziara yao mkoani Kagera hivi karibuni.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (katikati), akipozi kwa picha na wafanyakazi wa benki hiyo wa tawi la Mwanza  wakati mkurugenzi huyo pamoja na ujumbe wake wakiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo hivi karibuni. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia), akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo wa Tawi la Mwanza, wakati wa ziara yake mkoani humo hivi karibuni.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (katikati), akipozi kwa picha na wafanyakazi wa benki hiyo wa tawi la Musoma wakati mkurugenzi huyo pamoja na ujumbe wake wakiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mara hivi karibuni. 
Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Ziwa, Japhet Mazumira (kulia), akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo wa Tawi la Mwanza wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi mkoani humo hivi karibuni. 

BENKI YA NMB YAKABIDHI VITANDA 15 VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 45 HOSPITALI YA MUHIMBILI NA MLOGANZILA.

$
0
0
Katika kutambua afya ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya jamii, Benki ya NMB imekabidhi vitanda 15 vyenye jumla ya thamani ya milioni 45 kwa ajili ya chumba cha watoto wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum (ICU) katika hospitali za Muhimbili na Mloganzila za jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi msaada huo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Afisa Mkuu wa Mahesabu wa Benki ya NMB, Juma Kimori, alibainisha kwamba thamani ya vitanda vyote ni Sh. Milioni 45 huku  akifafanua kuwa kitanda kimoja cha ICU ya watoto kimegharimu Sh. Milioni 7.5 na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali kuboresha sekta ya afya.

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Zuhura Mawona, aliishukuru na kuipongeza NMB kwa msaada huo na kuiomba iendelee kutoa msaada zaidi kwa ajili ya chumba hicho maalum kwa watoto.

“Tulipeleka maombi NMB na wametujibu hatuchoki, tunaendelea kuwaomba mtushike tena mkono, maana mahitaji ya vitanda katika chumba hicho muhimu cha kuokoa maisha ya watoto ni mkubwa, bado tunahitaji vingine saba mkiguswa tena mtukumbuke.

“Kabla ya wodi hii kuanza watoto walikuwa wanachanganywa kwenye ICU za wakubwa na kule vitanda sio sawa na hivi tulivyopokea vya NMB hata sisi  wahudumu hatupati tabu sana kuvinyanyua wala mgonjwa haumii kila kitu kinasetiwa kwenye umeme asanteni sana NMB,” alisema Mawona aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.#NMBKaribuYako
Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani wa Benki ya NMB, Peter Kimori akimkabidhi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto; Mh. Ummy Mwalimu masada wa vitanda 15 kwa ajili ya chumba cha watoto wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum(ICU) katika hospitali za Muhimbili na Mloganzila za jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto; Mh. Ummy Mwalimu na Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani wa Benki ya NMB, Juma Komori  wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao kutoka hospitali za Muhimbili na Mloganzila.

MAKMAR HOTELI YA MSATA WILAYANI BAGAMOYO MKOA WA PWANI INAKUKARIBISHA

DIAMOND PLATNUMZ NA WASAFI KAMPUNI, WAVUTIWA KUSAFIRI NA TRENI YA DELUXE KUTOKA DAR-KIGOMA

DKT. SHEIN KUFUNGUA RASMI KONGAMANO LA SITA LA DIASPORA TANZANIA LEO

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kesho tarehe 15 Desemba 2019, anatarajiwa kufungua rasmi Kongamano la sita la Diaspora Tanzania mjini Zanzibar.

Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi -Zanzibar wamekuwa wakiandaa makongamano ya Disapora kwa kuwakutanisha kila mwaka Watanzania waishio ughaibuni kujadili mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya uwekezaji, Utalii, Kilimo na mengine ya maendeleo.

Kongamano hili ni muendelezo wa makongamano mengine matano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Unguja na Pemba katika miaka ya kuanzia 2014 hadi 2018.
Lengo la kongamano hili la sita ni kuhamasisha na kushirikisha Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini. Dhamira ya kongamano hili kuendeleza ushirikiano uliopangwa na Diaspora na wawekezaji kama wadau wa maendeleo nchinichini ya kauli mbiu ya "mtu kwao ndio ngao".

Kongamano hili linatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 350 wakiwemo Diaspora, Viongozi wa Kitaifa, Wadau mbalimbali kutoka Serikalini na Sekta Binafsi ambapo pamoja na mambo mengine, watajadili mazingira ya uwekezaji na fursa za uwekezaji na utalii ziliopo nchini.

Leo tarehe 14 Desemba 2019 Diaspora na wadau wengine waliowasili wanafanya ziara ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwa ni pamoja na Zanzibar Village Icon na mashamba ya viungo mbalimbali vya chakula.

Mwezi Augusti, 2018 watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) walikutana Chake Chake, kisiwani Pemba katika kongamano la tano la Diaspora kufuatia  utaratibu uliowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar  kuwakutanisha kila mwaka Watanzania waishio ughaibuni.

Waandishi waaswa kuzingatia weledi na maadili ya uandishi

$
0
0
Waandishi na watangazaji wa Redio za Kijamii nchini wameaswa kuzingatia miiko,maadili na sheria zinazoongoza  taaluma ya habari nchini ili kulinda heshima ya taaluma yao.

Wito huo umetolewa na mjini Morogoro na Mratibu wa mafunzo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi Getrude John wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya waandishi wa habari kutoka redio za kijamii nchini.

Bi Getrude alisema ni vyema waandishi na watangazaji wa redio za kijamii wakatambua wajibu wao ndani ya jamii na hivyo kijibidiisha katika kuielewa taaluma ya habari, misingi, weledi, sheria, mahitaji na matakwa ya wasikilizaji wao pamoja na kuwajua wasikilizaji wao kiasili.

“Ukiwa mwandishi wa habari za kijamii una wajibu mkubwa katika jamii yako na hasa kuhakikisha unaijua jamii yako, hitaji lake pamoja na sheria na maadili ya utangazaji na uandishi wa habari” alisisitiza Bi Getrude.

Alisisitiza kuwa katika siku za hivi karibuni kumekuwa na changamoto nyingi za kiweledi kwenye maudhui ya habari hususani redio za kijamii makosa ambayo waandishi na watangazaji wa redio hizo wana nafasi kubwa ya kuyarekebisha ili kuepuka makosa ya kisheria,kimaadili na kushindwa kutengeneza maudhui yanayotengeneza jamiiyenye mtazamo chanya,yenye ubunifu na inayozingatia maadili ya jamii husika.

“Kazi ya uandishi wa habari ina maadili na sheria zake, ina miiko inayoiongoza,bila kuijua unaweza kujikuta unaingia kwenye mgogoro na jamii unayoihudumia”

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wameomba UNESCO kuyaendeleza mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo kutokana na walio wengi kukosa nafasi ya kupata mafunzo ya uandishi wa habari kabla ya kuanza kufanya kazi na redio za kijamii.

“Sisi wengi tunaofanya kazi na Redio za kijamii,hatukubahatika kupitia katika mfumo rasmi wa elimu ya habari, tunaomba tupatiwe mafunzo zaidi ya haya ili tuwe na utaalamu na maarifa yatakayotufanya tuandae maudhui yanayojibu changamoto ya jamii tunazozihudumia huku tukizingatia maadili na sheria” alisema Tumain Obel kutoka Redio Chai FM.

Jumla ya waandishi 24 kutoka redio 6 za kijamii kutoka Tanzania Bara wanahudhuria mafunzo ya siku tano yanayoratibiwa na kuendeshwa na UNESCO chini ya mradi wa SDC yenye lengo la kuwajengea uwezo waandishi na watangazaji wa redio za kijamii kwenye eneo la maadili, sheria, ujuzi na weledi katika taaluma ya habari.

Mafunzo kama haya yalifanyika wiki iliyopita visiwani Zanziar kwa kuhusisha waandishi na watangazaji wa redio za kijamii 16 kutoka vituo 4 vya redio za kijamii kutoka Unguja na Pemba.
Waandishi wa habari wanaoripotia redio Jamii (Mtwara), Ruangwa (Lindi), Pambazuko (Ifakara), Chai (Rungwe), Ileje ( Songwe), na Kitulo (Makete-Njombe) wakiwa kwenye kazi za makundi wakijadili namna ya kuandaa habari na kuiwasilisha kwa kutumia miundo mbalimbali ya maudhui.


KIFAA CHA KUDHIBITI WIZI WA PIKI PIKI NA VYOMBO VYA MOTO HIKI HAPA

$
0
0
Na Grace Gurisha

MENEJA Mauzo na Masoko wa Kampuni inayojihusisha na uundaji wa mifumo mbalimbali ya kiteknolojia ya MD Technology, Mohamed Kaddy amesema wameleta  kifaa maalumu chenye uwezo wa kudhibiti wizi wa pikipiki na vyombo vya moto.

Kaddy aliyasema hayo leo Desemba 14, mwaka huu, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kifaa hicho, ambapo alisema kwa kutumia teknolojia hiyo,pikipiki ikiibiwa, itapatikana na mmiliki atapata taarifa kupitia simu yake ya mkononi.

Meneja huyo alisema teknolojia hiyo ni rahisi, "Ukifunga kifaa cha kudhibiti wizi katika pikipiki yako,hata kama ikiibiwa usiwe na wasiwasi,itapatikana tu, lakini pia kama kuna mtu amesimama katika pikipiki yako utajulishwa”,.

"Kifaa hichi maalumu kitafungwa katika pikipiki na kuunganishwa na simu ya mkononi ambapo mteja atapata taarifa zote za uendeshaji wa pikipiki katika simu yake ya mkononi na pia hata akipoteza simu yake anaweza kutumia simu ya mtu mwingine na kupata taarifa kifaa chake kilipo," alisema 

Alisema mfumo huo husaidia kudhibiti udanganyifu wa madereva au marafiki katika matumizi ya umbali aliotumia kwa siku katika uendeshaji wa pikipiki,jambo litakalowawezesha wamiliki wa pikipiki kuwa na uhakika wa mapato, kwa zile zinazofanya usafiri wa abiria.

“Mfumo huu utawasaidia wamiliki wa pikipiki kupata taarifa kwa haraka pale chombo chake kikitaka kuibiwa au kushikwa na mtu, pia mfumo huo utamsaidia mtu kuzima au kuwasha chombo mahali popote atakapokuwa, kama umeibiwa unauwezo wa kuizima pikipiki yako kabla haijafika mbali," alisema

Alisema kifaa hicho tayari kimeshaanza kuuzwa kwa bei nafuu, hivyo madereva wajitokeze kwa wingi kununua ili kudhibiti wezi kutokana na wimbi la wizi wa Bodaboda linaloendelea hivi sasa.

Pia, alisema wanafunga vifaa kwenye nyumba kwa mfumo wa kisasa ambapo hata mwizi atakapokwenda kuiba hata gundua kama kuna kifaa cha usalama kimefungwa kwa hiyo itakuwa ni rahisi yeye kukamatwa kwa sababu kifaa kitaonesha kuna mtu ameingia.
 Meneja Mauzo na Msoko wa Kampuni inayojihusisha na uundaji wa mifumo mbalimbali yabkiteknolojia ya MD Technology, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kifaa cha kisasa cha kuzuia wizi wa vyombo vya moto.
 Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya MD Technology, Brian Kessy akiwaeleza madereva wa Bodaboda faida ya kifaa hicho ambacho kitawasaidia katika suala nzima la ulinzi wa pikipiki zao
 Mtaalamu wa Mifumo kutoka MD Technology, Salum Mntitiwa akionesha jinsi ambavyo kifaa hicho kilivyofungwa na kuunganishwa na simu ya mkononi kinavyoweza kufanya kazi kwa kuliweka gari katika hali ya usalama,

POLISI NA RSA WAFANYA OPERESHENI YA KUSHTUKIZA

$
0
0

Alanus Mbigi kutoka ofisi ya DTO Mombo akikagua Tairi kwenye moja ya bus la Abiria katika Eneo la Bwiko.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Solomon Mwangamilo akizungumza na Baadhi ya madereva katika eneo la Bwiko mpakani mwa Mkoa wa Tanga na Kilimanjaro.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Fortunatus Muslimu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Elimu kwa Umma RSA Ally Nurdin (aliyevaa miwani)Mwenyekiti wa RSA mkoa wa Tanga Eddo Mwakimwagile (wa kwanza kushoto)
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Fortunatus Muslimu,akizungumza na baadhi ya madereva wa Mabasi yanayotoka na kyingia Kanda ya Kaskazini ,mpakani mwa Mkoa wa Tanga na Kilimanjaro katika eneo la Bwiko.

Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Elimu kwa Umma RSA Ally Nurdin akizungumza katika kampeni abiria paza sauti eneo la Bwiko mpakani mwa mkoa wa Kilimanjaro na Tanga.
Mmoja wa Askari ofisi ya Taffic Korogwe Anna Mushi pamoja na Alanus Mbigi kutoka ofisi ya DTO Mombo akikagua Tairi kwenye moja ya bus la Abiria katika Eneo la Bwiko.
PC Hamis Mbilikila traffic kutoka ofisi ya Ofisi ya Rto Tanga akikagua tairi kwenye moja ya bus katika Eneo la Bwiko.
Mwenyekiti wa RSA mkia wa Tanga Eddo Mwakimwagile akitoa elimu kwa madereva wa mabus pamoja na wadau wa usafiri katika eneo la Bwiko
Mmoja wa Askari wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji akitoa elimu kwa dereva namna ya kukagua kidhibiti moto mara unapotokea ndani bus na namna ya kuhakikisha mara zote wanakagua muda wa matumizi sahihi kwaajili ya usalama zaidi.
Mmoja wa Askari kutoka ofisi ya Traffic Korogwe Anna Mushi akiwa ndani ya bus akitoa elimu kwa Abiria juu ya usalama wao wawapo ndani ya chombo cha usafiri,aliyepo nae ni Mwenyekiti wa RSA mkoa wa Tanga.





Na.Vero Ignatus Tanga.

Jeshi la polisi nchini kikosi cha usalama barabarani nchini kwa kushirikiana na mabalozi wa usalama barabarani limefanya opereshani ya kushtukiza ya kufanya ukaguzi wa kwenye mabasi makubwa ya mikoani yanayotoka na kuingia kanda ya kaskazini mpakani mwa Mkoa wa Tanga na Kilimanjaro katika eneo la Bwiko

Operesheni hiyo iliyopewa jila la abiria paza sauti imeongozwa na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Fortunatus Muslimu kwa kushirikiana RSA, pamoja Jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Tanga pamoja na wadau wengine wa usalama barabarani mkoani hapa

Akizungumza katika operesheni hiyo Kamanda Muslimu amesema kuwa kumekuwa na matukio mengi sana ya ajali za barabarani ,hivyo wamelazimika kuendesha operesheni hiyo ili kudhibiti wimbi la ajali hususani zinazotokea mwishoni na mwanzoni mwa mwaka

Amesema kwa kupitia kampeni hiyo ya abiria paza sauti amesema kutokana na kwamba jeshi la polisi barabrani ni wachache hivyo wameamua kushirikiana na RSA ili kuwafichua madereva wanaokiuka na kutofuata sheria na kanuni za usalama barabarani.

Amesema kuwa kampemni hiyo ni endelevu nchi nzima na imelenga kuhakikisha kwamba ajali za barabarani zinapungua na kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kwa madereva na makundi mengine amabao wanatumia barabara ili wanafuata sheria za usalama barabarani

''Maisha ya abiria hawa mnaowaona kwenye magari yanawategemea ninyi madereva na kipindi hilki cha mwishoni mwa mwaka na mwanzoni mwa mwaka matumizi yavyombo yanakuwa mengi barabarani watu wanatoka sehemu mioja kwenda nyingine kufanya biashara,likizo kusalimua ndugu na marafiki wengine wanakwenda kwenye starehe,kwenye sikukuu za Christmass na mwaka mpya.Alisema Kamanda Muslimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Elimu kwa Umma RSA Ally Nurdin amewataka baadhi ya madereva kutokutem bea kwa mwendo kasi na kusingizia kwamba watu wamekuwa wakitoa kafara badala yake waweze kufuata sharia za usalama barabarani ili waweze kwa salama wao pamoja na Abiria

''Tukiwa huku barabarani tunatoa elimu msije mkawaona askari ni maadui yote haya tunakumbushana ili sharia za usalama barabrani zifuatwe

Amewaoma Madereva wote kufuata sharia za usalama barabarani na kuzingatia yale yote yanayopaswa kufuatwa ili kuepusha ajali za barabarabarani zinazopelekea vifo na ulemavu wa kudumu"


Amesema kuwa madereva wasipokuwa makini na kuzingatia sheria ,kanuni na taratibu za usalama barabarani kama inavyohitajika wanaweza kusababisha ajali, vifo,ulemavu wa kudumu na nguvu kazi ya Taifa.

Kwa upande wake kamanda wa kikosi cha usalama baraarani mkoa wa tanga Solomon amewataka madereva kuzingatia yale yote ambayo wamepewa elimu hiyo ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika kwa kuzingatia moja kwa moja kanuni na sharia za usalama barabarani ili kuwafikisha abiria salama katika safari zao

''Natumaini kuwa mtayazingatia haya mwanzo mwisho wa safari nanyi mtakuwa mabalozi wazuri kwa wenzenu na kuwaambia nini cha kufanya barabarani mbiyo hazikupi Maisha wala chochote unachokitafuta maishani Zaidi mbio zitakupa ulemavu ama kifo

Amewataka madereva kutokuwa chanzo cha matatizo bali waungane na wengine ili kuhakikisha kuwa barabara zote zinakuwa salama bila kusababisha ajali na kupoteza maisha ya Watanzania wasiokuwa na hatia.

Kwa upande wao Wensley Olomi madereva wa Hai Express na amesema kuwa mpango huu wa kutokomeza ajali umesaidia kwa kiasi kikubwa kwani tangia mpango huo umeanza ajali zimepungua kwa kiasi kikubwa sana

‘’Tulikuwa tumezowea kila mwaka mwezi wa kumi na mbili tunasikia bus Fulani limeyua watu kadhaalakini siku hizi hakuna kitu kama hicho’’

TAHADHARI YA UTAPELI KUHUSU MSAMAHA WA MHESHIMIWA RAIS

Vodacom Tanzania Plc yawafikia wateja wake wa kanda ya ziwa, msimu huu wa sikukuu yazindua simu mpya ya Smart Kitochi jijini Mwanza

$
0
0


 
Wafanyakazi wa Kampuni ya mawasiliano ya  Vodacom wakiwa wamebeba bango lenye picha ya simu ya Smart Kitochi  wakati wa uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika jijini Mwanza.
Kaimu  mkuu wa mauzo wa Kampuni ya mawasiliano ya  Vodacom kanda ya Ziwa, Ayubu Kalufya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa simu ya Smart Kitochi, uliofanyika jijini Mwanza.
Wateja wa simu mpya za Smart Kitochi zenye uwezo wa 4G kutoka Vodacom wakipatiwa maelezo ya kuhusu simu hizo zitakazopatikana kwenye maduka ya Vodacom  nchini kote kwa bei ya shilingi 45,000/=  katika msimu huu wa sikukuu wakati wa uzinduzi wa simu hizo jijini Mwanza.
Wateja wa simu mpya za Smart Kitochi zenye uwezo wa 4G kutoka Vodacom, wakijipiga selfie kwa kutumia simu hiyo baada ya kuinunua jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa simu hiyo inayopatikana kwenye maduka ya Vodacom nchini kote kwa bei ya shilingi 45,000/= katika msimu huu wa sikukuu.

NEWS ALERT : WATU ZAIDI YA 37 WALAZWA HOSPITALI YA RUFAA DODOMA WAKIDAIWA KULA CHAKULA CHENYE SUMU MSIBANI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma ambao wamelazwa kwa kile kinachoelezwa kula chakula chenye sumu.


 Watu zaidi ya 37 wamelazwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital)  kwa ugonjwa wa kuhara na kutapika baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu kwenye msiba eneo la Mtumba nje kidogo ya Jiji la Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi tayari kashafika hospitalini hapo na amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


TUTAWALETEA TAARIFA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI KADIRI YA ZITAKAVYOPATIKANA.

SMZ yaahidi kukamilisha sheria ya Diaspora kabla ya Mei 2020

$
0
0

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia hadhara ya Diaspora Tanzania (haipo pichani) katika kongamano la sita la diaspora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Issa Haji Ussi Gavu, akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein kuhutubia kongamano la sita la Diaspora Mwenyekiti wa wanadiaspora, Bwn. Norman Jasson akitoa salamu za wanadiaspora wakati wa kongamano
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipokea moja ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wadogo Zanzibar wakati alipotembelea banda la wajasiriamali, kabla ya kufungua rasmi kongamano la sita la Diaspora Tanzania. Kulia kwake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akifuatiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, George Simbachawene.
Baadhi ya ujumbe wa Diaspora ukiwa umesimama wakati wa kuimba wimbo wa taifa katika kongamano la sita la Diaspora lililofanyika Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein katikati (mwenye tai ya rangi ya blu bahari) akiwa katika picha ya pamoja na vinongozi waandamizi wa serikali pamoja na baadhi ya ujumbe wa Diaspora mara baada ya kufungua rasmi kongamano la sita la Diaspora Tanzania
Baadhi ya ujumbe wa Diaspora ukifuatilia hutuba ya mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein kuhutubia kongamano la sita la Diaspora.
*******************************
Na Nelson Kessy, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, amewahakikishia wanadiaspora kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itasimamia na kuhakikisha kuwa sheria ya Diaspora inakamilika kabla ya mwezi Mei, 2020.

Rais Dkt. Shein ametoa kauli hiyo leo mjini Zanzibar wakati alipokuwa akifungua rasmi kongamano la sita la Diaspora ambalo limeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikianana Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi-Zanzibar.

Dhamira ya kongamano hili kuendeleza ushirikiano uliopangwa na Diaspora na wawekezaji kama wadau wa maendeleo nchini chini ya kaulimbiu ya”mtu kwao ndio ngao”.

Ndugu wanadiaspora mwaka jana nilieleza jitihada za kuanziasha ofisi za Diaspora hapa Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati ule kwa kuanziasha Diaspora.

"Kutokana na kutambua umuhimu wa watanzania waishio nje ya nchi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliunda idara maalumu ya kushughulikia masuala ya Diaspora katika wizara ya Mambo ya nje mwaka2010 ili kuvitekeleza kwa vitendo azma yetu ya kuwashirikisha wanadiaspora Tanzania katika kuendeleza nchi yetu”.

Ameongeza kuwa kwa umuhimu huohuo, na kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka 2010 na kuyapa nguvu masuala ya Diaspora tulianzisha kitengo cha Diapora na baadae idara ya Diaspora ilinzishwa hapaZanzibar. Tulitengeneza sera maalumu ya wanadiaspora, na sasa tupo mbioni kuanzisha sheria ya Diaspora, nimefurahi kuwa rasimu ya sheria hiyo imefikia katika hatua nzuri.

”Kwa matiki hiyo basi, namuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Issa Haji Ussi Gavu kuhakikisha anasimamia kwa karibu sana utayarishaji na kukamilika kwa rasimu ya sheria hiyo na iwasilishwe kwenye Baraza la wawakilishikabla ya mwezi mei 2020,”. Amesema Dkt. Shein na kuongeza kuwa atahakikisha kuwa kabla ya kumaliza muda wangu wa Urais hapa Zanzibar sheria hiyo itakuwa imekaa vizuri kimkakati, kisera pamoja na kisheria kwaupande wa Zanzibar.

Aidha, Rais Shein, aliwapongeza wanadiaspora kwa michango yao ambayo wamekuwa wakiitoa kwa kusaidia Serikali, pamoja na mambo mengine michango hiyo imekuwa ikisaidia kijamiii na kiuchumi.

Awali akitoa salamu za wanadiaspora, Mwenyekiti wa wanadiaspora, Norman Jasson alisema kuwa mchakato wa sera ya Diaspora umekuwa ni wa muda mrefu na kumekuwepo na ukimya takribani miaka mitatu na kumuomba Rais Dkt. Shein kuwasaidia kusimamia zoezi hilo.

”Sera ya Diaspora ina umuhimu wa kipekee kwani tunaamini kuwa sera hiyo itakapokamilika itatoa majibu ya maswali mengi ambayo yamekuwa yakitunyima usingizi. Tunaamini sera hii itasaidia sio tu masuala ya uraiawan chi mbili au hadhi maalum, bali pia masuala mengine kama umiliki wa ardhi, mirathi, ndoa kwa wenyeji na wageni, ruhusa ya makazi nchini kupitia vibali au visa na mengine mengi” Amesema Bwn. Jasson.

Aliongeza kuwa, pia wanadiaspora wanaamini kuwa sera hiyo itarahisisha utungaji wa sheria itakayowatambua watanzania wote walio ughaibuni bila kujali kama tayari wameshachukua uraia wa nchi nyingine au kama tayariwana vibali vya makazi katika nchi wanazoishi na pia bila kujaliwaliingiaje ughaibuni katika kusaka maisha.

Bwana Jasson aliongeza kuwa, msingi wa wanadiaspora ni utanzania wao na utayari wa kushiriki katika jitihada za kusuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii kama vile kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini ambapokwa sasa TDC-Global tayari imewaleta Tanzania watu wenye nia ya kuwekeza.

”Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa kushirikiana na Diaspora itafanikisha mambo mengi kwa kuanzisha mkakati wa wa kuhakikisha kuwa watanzania waishio nje ya nchi wanatayarishiwa mfumo ambao utasaidia kukusanya michango ya kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo”. Amesema Bwn. Jasson.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, George Simbachawene akitoa shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Shein amesema kuwa sera yaDiaspora kwa upande wa Tanzania rasimu ya kwanza tayari imekamilika na hatua inayofuata ni kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wanadiaspora wenyewe kupitia balozi zetu ili na wao waweze kutoa mawazoyao.

”Mhe. Rais, kwa sasa sera ipo katika hatua nzuri, jitihada kubwa zinaendelea na jambo hili linahitaji kushughulikiwa kwa uangalifu mkubwa kwa sababu ya historia ya nchi yetu," Amesema Simbachawene.

Aidha, Waziri Simbachawene aliongeza kuwa ni muhimu kutumia wanadiaspora kama fursa, sekta muhimu katika ujenzi wa uchumi wa taifa letu na mataifa mengi dunini yanafanya hivyo.

Pamoja na mambo mengine, kongamano hili la sita la Diaspora limejadili mada saba ambazo ni urejeshaji wa taka za plastiki, Tanzania na uwekezaji, Diaspora na uwekezaji, Mradi wa nyumba za bei nafuu, kilimo cha kisasa, kubadili mfumo wa utalii wa Zanzibar pamoja na Mradi wa daraja la Zanzibar – Tanzania bara.

Mwezi Augusti, 2018 watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) walikutana Chake Chake, kisiwani Pemba katika kongamano la tano la Diaspora kufuatia utaratibu uliowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwakutanisha kila mwaka Watanzania waishio ughaibuni.

TAHADHARI YA UTAPELI KUHUSU MSAMAHA WA MHESHIMIWA RAIS

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images