Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 3284 | 3285 | (Page 3286) | 3287 | 3288 | .... | 3352 | newer

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), (hawapo pichani), wakati wa ufunguzi wa baraza hilo la 13 lililofanyika mkoani Kagera.
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), (hawapo pichani), wakati wa ufunguzi wa baraza hilo la 13 lililofanyika mkoani Kagera.
  Mwenyekiti wa Baraza ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, akizungumza na wajumbe wa baraza hilo ambao limewakutanisha wajumbe kutoka mikoa yote nchini, mkoani Kagera.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), wakifuatilia maelekezo ya mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa kikao cha baraza hilo la 13 kilichofanyika mkoani Kagera.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe na Mwenyekiti wa Baraza ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale, pamoja na viongozi wengine wakishiriki kuimba nyimbo ya ‘Solidarity forever’ kuonyesha mshikamano katika utendaji kazi wakati wa Kikao cha 13 cha Baraza hilo, mkoani Kagera.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Baraza ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale, wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi la 13 lililofanyika mkoani Kagera.
  Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, mara baada ya kufungua kikao cha Baraza hilo la 13 lililofanyika mkoani Kagera.

  ………………….

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, ameutaka Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kusimamia kwa uadilifu pasipo kuyumbishwa taratibu za manunuzi ya umma na wala kutoruhusu kuingiliwa na watu wenye maslahi binafsi.

  Aidha, ameutaka Wakala huo kutafuta mbinu na mkakati mpya wa kukabiliana na vitendo vya utovu wa nidhamu na rushwa unaofanywa na baadhi ya watumishi wa mizani kwani unaharibu taswira na uaminifu wa Wakala huo.

  Waziri Kamwelwe ametoa kauli hiyo jana mkoani Kagera wakati akifungua mkutano wa kumi na tatu (13) wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS nchi nzima ambapo pamoja na mambo mengine amefurahishwa sana na utekelezaji wa maagizo yake katika kikao kilichopita ambayo ni kielelezo cha usikivu, ukomavu na utii wa hali ya juu kwa Serikali.

  “TANROADS msiyumbishwe katika taratibu za manunuzi na mtafute mbinu mpya ya kukabiliana na rushwa kwenye masuala ya ujenzi na mizani ili isiwaaharibie sifa yenu mliyonayo”, amesema Waziri Kamwelwe.

  Mhandisi Kamwelwe ameusisitiza Wakala kuendelea kuwajengea uwezo watumishi kwa kuwaongezea weledi na kuwapa vitendea kazi na vifaa hasa Kitengo cha Usimamizi wa Miradi (TECU) ili kiweze kusimamia miradi mikubwa zaidi nchini.

  “Naendelea kuwasihi na kuwatia moyo kuendelea kuchapa kazi kwa kutanguliza mbele maslahi mapana na Taifa na tunajua uwepo wa upungufu wa watumishi, vitendea kazi pamoja na ofisi kwa baadhi ya mikoa, jambo hilo lisiwavunje moyo na liwe chachu na hamasa ya kuwajibika, nasi tutaendelea kutafuta na kuweka mikakati mbalimbali ya kutatua changamoto hizo kwa kuzingatia vipaumbele ili tuweze kuhakikisha kuwa hakuna jambo lolote linaloweza kukwamisha utekelezaji wa majukumu yenu”, amesisitiza Mhandisi Kamwelwe.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale, amesema kuwa Wakala unaendelea kutekeleza na kuhakikisha kuwa miradi mbalimbali ya kimkakati na ile ya maendeleo inakamilika kwa wakati na viwango ili iweze kuchochea kasi ya maendeleo ya nchi yetu.

  Ameongeza kuwa kasi ya usimamizi na ukamilishaji wa miradi mikubwa kwa wakati itaenda sambamba na thamani ya fedha (Value for money katika miradi yote nchini na hivyo kuifanya TANROADS kuendelea kuwa injini ya uchumi wa Taifa letu katika ujenzi wa uchumi wa kati.

  Naye, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, ameipongeza TANROADS kwa kwa juhudi, maarifa na utendaji kazi kwa weledi ambao unaweka mbele maslahi mapana ya nchi yetu.

  “Sisi sote hapa ni mashahidi wa kuona jinsi Serikali inavyoamua miradi mingi mikubwa isimamiwe na TANROADS na katika hili hamjatuangusha”, amesema Mkuu wa Mkoa.

  Waziri Mhandisi Kamwelwe yupo mkoani Kagera kwa ziara ya siku mbili ambapo atakagua pia miradi ya barabara, madaraja, bandari inayoendelea kutekelezwa na Wizara yake.

  0 0

  Mkuu wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS), Bi. Rehema Mligo akielezea namna ambavyo wanafunzi wa uuguzi wanaosoma katika Taasisi hiyo wanavyopatiwa mafunzo ya vitendo katika maabara ya kisasa ya ujuzi iliyopo katika taasisi hiyo mbele ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dodoma. Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Afya), Bw. Gerald Chami(kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu huduma ya Maktaba inayotolewa na Taasisi hiyo toka kwa Mkuu wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS), Bi. Rehema Mligo (katikati) wakati wa ziara ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Afya) na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo leo jijini Dodoma. Kulia ni Mkutubi wa Maktaba hiyo, Andrew Gerald. Ziara hiyo ni muendelezo wa Kampeni ya Tunaboresha Sekta ya Afya inayoratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake kuelezea maboresho yanayofanywa katika sekta ya Afya chini ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. 


  Mkurgenzi wa Hospitali ya Mirembe na Taasisi ya Isanga, Dkt. Erasmus Mndeme akizungumza kuhusu mafanikio ya Taasisi anayoingoza ndani ya kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelewa na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo leo jijini Dodoma. Ziara hiyo ni muendelezo wa Kampeni ya Tunaboresha Sekta ya Afya inayoratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake kuelezea maboresho yanayofanywa katika sekta hiyo. Mkuu wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS), Bi. Rehema Mligo akifafanua jambo mbele ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Afya) na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dodoma. Ziara hiyo ni muendelezo wa Kampeni ya Tunaboresha Sekta ya Afya inayoratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake kuelezea maboresho yanayofanywa katika sekta ya Afya chini ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Taasisi hiyo inatoa masomo ya katika fani ya Uuguzi katika ngazi ya Stashahada. 
  Muonekano wa Jengo jipya la Bweni la wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS) ambalo linauwezo wa kuchukua wanafunzi 270. Jengo hilo limekuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa taasisi hiyo ambapo limetatua changamoto ya wanafunzi kukaa nje ya chuo. Ambapo awali bweni lililokuwepo lilikuwa na uwezo wa kulaza wanafunzi 180 tu kati ya wanafunzi 400 wanaosoma chuo hicho. Taasisi hiyo inatoa masomo ya katika fani ya Uuguzi katika ngazi ya Stashahada. Kiti maalumu cha kutolea huduma ya tiba ya magonjwa ya kinywa na meno ambayo inatolewa katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe. Moja ya majengo yaliyokarabatiwa katika Hospitali ya Mirembe ambayo kihistoria ilianzishwa na Mjerumani o miaka ya 1920. Jengo la kihistoria kuhusu Hospitali ya Mirembe mkoani Dodoma ambalo lilijengwa mwaka 1926. Jengo hili lilijengwa na wakoloni wa Kijerumani kwa sasa linatumiwa na wagonjwa wa afya ya akili walikatika uangalizi wa karibu. Baadhi ya mafundi wakishona sare za wanafunzi wa fani ya Uuguzi wanaosoma katika Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS) wakiendelea na kazi ya ushonaji was are hizo ikiwa ni maandalizi ya sare kwa ajili ya wanafunzi kuendea kwenye mafunzo kwa vitendo. Baadhi ya wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (DIHAS) Stashahada ya Uuguzi mwaka wa pili wakiwa darasani leo jijini Dodoma.(Picha na Wizara ya Afya

  0 0


  Na Ahmed Mahmoud,Killimanjaro.

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Annaclair Shija amewasimamisha watumishi wawili wa hospitali ya wilaya hiyo akiwemo  Afisa Tabibu kwa kudai na kupokea rushwa ya shs. 15,000/= kutoka kwa mama mwenye mtoto mchanga  mgonjwa wakike mwenye umri wa miezi mitano wa kijiji cha Vunta kilichopo ukanda wa milimani mwa wilaya hiyo.

   Shija amechukua hatua hiyo baada ya afisa tabibu huyo Kimweri kihiyo amesimamishwa kwa kumwandikia upasuaji mtoto huyo ambao hakustahili na kudai rushwa hiyo huku mlinzi daniel kihara  alimuuzia dawa kutoka bohari ya serikali kwashs. 4,500/ kwa mama wa mtoto huyo ambaye alistahili apewe mtoto wa miaka 12.

   Aidha amesema,  vitendo vya aina hiyo vimekuwa vikiidhalilisha serikaliambayo imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya dawa ambazo zinapatikana kwa asilimia 90 na kitendo cha kumwandikia dawa na upasuaji ambao hakustahili ni sawa mauaji .

  Muuguzi wa hospitali hiyo bw  Fabian Bulili  amesema kuwa afisa tabibu huyo ambaye hakuwa kazini anaonyesha alikuwa na tabia ya kuwaandikia dawa wagonjwa kwa ushirikiano na watumishi wasio waaminifu na kujipatia fedha kuikosesha mapato halmashauri

  Baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo  eliabu mgonja wameipongeza hatua hiyo na kueleza kuwa watumishi wa aina hiyo wanastahili kufukuzwa kazi ili wananchi waendelee kupata huduma bora za afya bila kudaiwa rushwa.


  0 0  0 0

  Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza mkakati wa kuwatumia Wakuu wa wilaya nchini kuhamasisha utalii wa ndani.

  Kufuatia hali hiyo jana Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu aliongozana na Wakuu wa wilaya nane kutoka wilaya mbalimbali nchini kwa ajili ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya BurigiChato iliyopo mkoani Kagera ili waweze kutambua fursa zinazopatikana ndani ya Hifadhi hiyo mpya.

  Mbali ya kutambua fursa hizo, Wakuu wa wilaya hao watatumika pia kuhamasisha wananchi wanaowaongoza katika wilaya watokazo kuhamasisha Utalii wa ndani.

  Mhe. Kanyasu amesema Sekta ya Utalii ni sekta muhimu sana katika maendeleo ya nchi hivyo Wakuu wa wilaya zote nchini wapatao 139 ni kundi muhimu katika kuwahamasisha wananchi wanaowangoza kuhusu umuhimu wa kutembelea Hifadhi zilizopo nchini.

  Akizungumzia sababu za kuwatumia Wakuu wa wilaya hao, Naibu Waziri Mhe.Kanyasu amesema mbali ya kuwatumia Waandishi wa Habari pamoja Wasanii na watu maarufu, Wakuu wa wilaya ni kundi muhimu kwa vile wao ni Wenyeviti wa kamati wa ulinzi na Usalama katika wilaya zao.

  ” Watalii wanaokuja nchini kutembelea vivutio vya utalii huzingatia ukalimu na usalama wao na Wakuu wa wilaya ndio wasimamizi wakuu wa Usalama wa watalii pamoja na Mali zao” Alisema. ” Tulianzakuwarumia Waandishi wa Habari, wakafuata wasanii na leo tumekuja na Wakuu wa wilaya lengo letu ni kuona jamii inapata mwamko wa kutembelea vivutio vya wenyewe” alisisitiza.

  Amesema Wakuu wa wilaya hao ni viongozi wanaowahakikishia usalama watalii na ndio kwenye jukumu la kuhakikisha kila mtalii anayekuja nchini kutembelea vivutio vya Utalii analala salama na anaamka salama
  Akizungumzia lengo la ziara hiyo kwa Wakuu wa wilaya, Mhe.Kanyasu amesema ameamua kuanza na Wakuu wa wilaya hao ni wawakilishi wa Wakuu wa Wilaya wenzao kwa vile vivutio vya Utalii vilivyopo nchini vipo katika maeneo hao kazi hivyo lazima watambue fursa zinazopatikana katika vivutio hivyo Aidha, Amesema kwa vile wao ni viongozi ni watu muhimu katika kutumia ushawishi walio hao kwa wananchi wanaowangoza katika kutembelea vivutio vya Utalii.

  Kwa upande wake, Damiani Salu ambayeni Mkuu wa Hifadhi hiyo amesema ujio wa Wakuu wa Wilaya hao utasaidia kuchagiza Utalii wa ndani kwa vile wao ni viongozi wanaowangoza watu hivyo watatumia ushawishi wao katika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutembelea Hifadhi nchini.
  Pia, Mkuu wa Hifadhi hiyo amewaeleza Wakuu wa wilaya hiyo kuwa Hifadhi hiyo ipo katika hatua za mwisho za kuongeza Wanyamapori mbalimbali wakiwemo simba wa kutoka familia tano.

  Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kutumia makundi mbalimbali yenye ushawishi katika jamii katika kuhamasisha Utalii wa ndani ambao umekuwa haufanyi vizuri.

  Wakuu wa wilaya waliotembelea Hifadhi hiyo ni Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Mhe.Asiya Abdallah, Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda, Mkuu wa wilaya ya Momba, Jumaa Irando pamoja na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva .

  Wengine ni Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, Mkuu wa wilaya ya Kongwa, Deogratias Ndejembi, Mkuu wa wilaya ya Musoma, Vicent Naano pamoja na Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga.
  Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato ni miongoni mwa Hifadhi mpya iliyozinduliwa mapema mwaka huu na Rais John Pombe Magufuli.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ( wa pili kulia) akiwa pamoja na baadhi ya wakuu wa wilaya kutoka wilaya nane wakijaribu kuruka juu sana ( kama inaovyoonekana pichani) kwenye eneo la ”jumping stone” katika Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato. Eneo hili ni eneo lenye mvuto sana kwa watalii, Aliyeruka juu sana upande wa kushoto wa kwanza ni Mkuu wa wilaya ya Kongwa, Deogratias Ndejembi.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( wa nne kulia) jana akiwa na Wakuu wa wilaya kutoka wilaya nane nchini wakila chakula kwenye hema pembezoni mwa Ziwa Burigi katika eneo la Mkonje mara baada ya kutembelea sehemu mbalimbali ndani ya Hifadhi ya Taifa ya BurigiChato mkoani Kagera
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na na Wakuu wa wilaya nane kutoka sehemu mbalimbali nchini nara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato akiwaelezea kuhusu umuhimu wa kuhamasisha wananchi wanaowaongoza kutembelea vivutio vya utalii. 
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe.Constantine Kanyasu akisalimiana na Afisa Utalii mara baada ya kuwasili na wakuu wa wilaya nane kufika kwa ajili ya kutembelea vivutio vya Utalii.Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Hifadhi hiyo, Damian Salu.
  Mkuu wa Hifadhi ya Burigi Chato, Damian Saru akizungungumza na Wakuu wa wilaya kuhusiana na ukubwa wa Hifadhi hiyo huku wakiwa anawasomea ramani jinsi Hifadhi hiyo ilivyo ya kipekee kwa kuwa na wantamapori wa kila aina.
  Mkuu wa wilaya ya Bariadi,Mhe.Festo Kiswaga akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea sehemu mbalimbali katika Hifadhi ya Burigi Chato. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe.Siriel Mchembe.


  0 0

  Globu ya Jamii mapema leo ilipokea taarifa ya kufuriki Dunia ,kwa aliyekuwa Katibu wa Baraza la wazee Yanga, huko Bagamoy0,Mkoani Pwani.
   
  Aidha tunawapa pole sana kwa Ndugu,Jamaa na Marafiki ikiwemo na Klabu ya Yanga sambamba na Mashabiki wake.

  Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amin

  TUTAENDELEA KUWAJUZA TAARIFA ZAIDI KUHUSIANA NA MSIBA HUU
  KWA KADIRI YA TAARIFA ZITAKAVYOKUWA ZIKIPATIKANA

  0 0  Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga akiongea katika kongamano la kutathimini na kutafakari jitihada zilizofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kuwakomboa watanzania kwenye haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni lililofanyika jijini Arusha Desemba 13-14, 2019.
  Mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Godfrey Mulisa akiteta jambo na Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga walipokutana katika kongamano hilo.

   Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, taasisi za umma na binafsi pamoja taasisi za kimataifa.


  Na Mbaraka Kambona,

  Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga amesema kuwa ili serikali iweze kutimiza haki za msingi za binadamu kwa wananchi wake kikamilifu inahitaji nguvu ya kifedha ili kujenga uchumi imara utakaoweza kutimiza haki hizo.

  Balozi Mahiga alitoa kauli hiyo kwenye kongamano la kitaifa la kutathimini hali ya haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni lililofanyika jijini Arusha Desemba 13-14, 2019.

  Mahiga alisema katika kongamano hilo kuwa ili serikali iweze kutekeleza na kutimiza haki za binadamu ni lazima ijenge mfumo wa uwajibikaji na uwazi ambao utajenga uchumi imara utakaosaidia kutekeleza haki za msingi za binadamu na utawala bora.

  Mahiga alisema kuwa kwa kutambua hilo serikali ya awamu ya tano iliamua kwa dhati kabisa kuimarisha mfumo wa ukusanyaji kodi kwa kuziba mianya yote iliyokuwa inapoteza mapato ili kupata fedha za kutosha kutoa huduma kwa jamii.

  “Serikali ya awamu ya tano imeleta sio tu mageuzi bali imeleta mapinduzi, kuna vitu ambavyo vilihitaji ujasiri wa pekee kuvitekeleza, huwezi kujenga uchumi kama huna fedha, bila kodi huwezi”,alisema Mahiga

  “Kutimiza haki za binadamu kunahitaji mtaji, lazima ujenge mfumo wa serikali bora, serikali ambayo inajenga uchumi wake kupitia mapato yake ya ndani kama serikali ya awamu hii inavyofanya”,aliongeza

  Mahiga aliendelea kusema kuwa serikali imepambana na mianya ya kuvuja kwa mapato na ndio maana leo tunashuhudia haki za kijamii, kiutamaduni na kiuchumi zinatekelezwa kwa vitendo.

  Alisema serikali imeendelea kuwapa watu wake fursa mbalimbali za kiuchumi ili kuboresha hali za maisha yao kwa mtu mmoja mmoja hata vikundi.

  Mahiga alisema serikali itaendelea kutekeleza mpango wa taifa wa miaka mitano (2016, 17-2020/21) ambao umelenga kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu.

  Alisema kuwa uamuzi wa serikali wa kujenga uchumi wa viwanda unalenga kuleta maendeleo jumuishi na endelevu kwa kutumia ipasavyo rasilimali zilizopo na hivyo kuchangia katika kukuza pato la taifa na kutoa nafasi nyingi na endelevu za ajira.

  Aidha, alisema kuwa katika kutimiza haki ya elimu, serikali imechukua hatua kadhaa ikiwemo utekelezaji wa sera yake ya elimu ya msingi na sekondari bila malipo. Sera hii imesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kutoka milioni 1.57 mwaka 2015 hadi milioni 2.08 mwaka 2016 sawa na ongezeko la asilimia 35.2.

  Kuhusu haki ya afya, Mahiga alisema serikali imeendelea kuimarisha vituo vya afya, imeongeza bajeti ya dawa kutoka bilioni 31 mwaka 2015/16 kufikia bilioni 270 mwaka 2018/19. Ongezeko hilo limeongeza upatikanaji wa dawa muhimu kufikia asilimia 96 kwa mwaka 2018/19. Tiba za kibingwa zinatolewa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, hospitali mpya za rufaa za Benjamini Mkapa na Mloganzila. Hospitali hizo zinatoa huduma za kibingwa zikiwemo upasuaji wa moyo, ubongo na uti wa mgongo ambazo awali zilikuwa zinapatikana nje ya nchi .

  Awali , Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu alisema kuwa lengo la kongamano hilo ni kutathimini na kutafakari jitihada zilizofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kuwakomboa watanzania kwenye haki za kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.

  0 0


   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na baadhi ya wavuvi katika soko la samaki manispaa ya Mtwara (hawapo pichani) wakati wa kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani Mtwara
  Baadhi ya wavuvi katika soko la samaki la Manispaa ya Mtwara wakimsikiliza Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akijibu hoja mbalimbali wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani Mtwara.
  Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akijibu hoja mbalimbali za wavuvi katika soko la samaki la Manispaa ya Mtwara wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani Mtwara
  ………………..
  Serikali imesema itaendelea kufanya marekebisho ya tozo, kanuni na sheria mbalimbali za uvuvi nchini ili wadau wa uvuvi waweze kufanya shughuli zao kwa tija zaidi na kuwataka maafisa uvuvi kuendelea kusimamia sheria zilizopo pamoja na wavuvi kutii sheria hizo.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema hayo jana (13.12.2019) Mkoani Mtwara wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani humo kwa kujionea shughuli mbalimbali za uvuvi na kuzungumza na wavuvi katika baadhi ya vijiji vya Halmashauri ya Wilaya na Manispaa ya Mtwara ambapo amesema ziara yake imelenga kukusanya maoni kutoka kwa wadau hao.
  Akizungumza na wadau wa uvuvi katika soko la samaki la Manispaa ya Mtwara, Mhe. Ulega amewataka maafisa uvuvi nchini kuwa na mahusiano mazuri na wavuvi pamoja na kuwasaidia wavuvi kutafsiri sheria mbalimbali ili wajiepushe na matumizi ya zana za uvuvi zisizotakiwa kisheria ambazo zinaweza kuwasababishia kutiwa hatiani kwa kukiuka sheria za nchi. 
  Aidha Mhe. Ulega amewataka maafisa uvuvi nchini kutojihusha na vitendo vya rushwa na kuwataka wavuvi wanaokutwa na hatia ya kujihusisha na kufanya shughuli zao kinyume na sheria ikiwemo uvuvi haramu kulipa faini wanayotozwa kwa kutumia utaratibu wa serikali uliowekwa. 
  Nao baadhi ya wavuvi wa soko la samaki la Manispaa ya Mtwara waliopata nafasi ya kuuliza maswali na kutoa maoni yao kwa Naibu Waziri Ulega wameiomba serikali ya awamu ya tano kuwaboreshea zaidi mazingira ya kufanya shughuli zao kwa kuondoa kero mbalimbali wanazokabiliana nazo ili waweze kufanya shughuli zao ziwe na tija zaidi kwa kujiongezea mapato na kulipa kodi ya serikali. 
  Wakati wa kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani Mtwara Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ametembelea pia Kijiji cha Msanga Mkuu kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara na kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho wanaojihusha na shughuli za uvuvi na kuwataka kufanya kazi kwa kufuata sheria huku akiwataka pia maafisa uvuvi wakishirikiana na vyombo vya dola kutotumia nguvu kwa mtuhumiwa wa matumizi ya zana za uvuvi zisizotakiwa kisheria ambaye anatii sheria.  

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

   Serikali imesema kuwa Soko la ajira rasmi  nchini ni dogo sana na  hivyo halikidhi mahitaji ya wahudumu wote kwa hali hiyo wahitimu hao wanatakiwa kukabiliana na changamoto ya Soko hilo kwa kuelekeza mawazo yao kwenye kujiajiri badala ya kuajiriwa.

  Hayo ameyasema Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Fedha na Mipango  Amina Shaban wakati akimwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango katika mahafali ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara yaliyofanyika katika Viwanja vya Kampasi jijini Dar es Salaam.

  Amesema kuwa kwa wale wahitimu wenye ajira msingi mkuu wa mafanikio ni kufanya kazi kwa kuzingatia sera,Sheria,Taratibu na Kanunu ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vishawishi au vitendo vya rushwa na ubadhirifu kwa kuwa vina madhara makubwa ya maisha ya mtu Mmoja moja na uchumi wa Taifa letu kwa ujumla.

  Shaban amesema elimu inayotolewa na TIA imejikita kwenye fani za Uhasibu ikiwemo Uhasibu wa Fedha za Umma, Ununuzi na Ugavi,Usimamizi  wa Biashara, Uongozi wa Rasilmali Watu pamoja na Masoko  hivyo fani hiyo ni nguzo muhimu katika kuendesha Uchumi wa Taifa hususani katika kusimamia mapato na matumizi ya Fedha za Umma.

  Naibu Katibu Mkuu huyo amesema sera yetu kwa sasa ni uchumi wa viwanda hivyo umahiri wa  wataalam wanaozalishwa  unatakiwa kuonekana ili kufanikisha azima ya serikali ya Tanzania ya Viwanda.

  Shaban amekazia katika kukabiliana na changamoto za Usimamizi wa Mapato na matumizi ya Fedha za Umma,mahitaji ya Soko ,Ushindani na Utandawazi hamna budi Taasisi ya Uhasibu nchini (TIA) Kuendesha Shughuli  kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa ya kupeana na kubadilishana taarifa kwani watalaam wanaohitajika ni wenye weledi,maarifa na umahiri wa kutatua za changamoto na si kuongeza changamoto kwa Wananchi katika kupata huduma.

  Amesema kuwa TIA izingatie  umakini wa suala la umahiri katika mitaala ili kuweza kuwa na wataalam wenye uwezo wa kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa Kipato cha kati kabla ya 2025.
  Mwenyikiti wa Bodi ya Wizara ya Fedha na Mipango Wakili Said Chiguma amesema kuwa waajiri wa sekta ya Umma na binafsi wamekuwa wakiona mafanikio kwa wahitimu wa TIA kuwa na sifa zilizotukuka katika kufanya kazi licha ya kuwapo kwa Vyuo vingi nchini na kufanya Chuo hicho kuendelea kuongeza idadi ya udahili kwa wanafunzi kusoma kwa  kila mwaka.
  Amesema Taasisi ina wanafunzi zaidi ya  19,000 katika Kampasi Sita za Kimkakati.

  Nae Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Luciana Hembe amesema kuwa wahitimu katika Chuo hicho wameweza kjfundishwa ujasiriamali ili kuweza kujiajiri katika kukabiliana na changamoto ya ajira nchini.
  Amesema Chuo kumekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakiksha wahitimu wanajiajiri katika maeneo Mbalimbali ya kuweza kukidhi mahitaji yao pamoja Taifa kunufaika na maarifa yao ya kujiajiri.

  Aidha amesema kuwa Baadhi wahitimu katika Taasisi hiyo wa miaka iliyopita wameweza kuanzisha Kampuni mbalimbali ambazo ziko katika Ushindani wa kibiashara na Kampuni zingine.

  Amesema wahitimu wa mwaka 2019 nao watumie ujuzi na maarifa yao katika kufungua milango ya ajira ya kujiajiri ili wasitumie muda mwingi wa kusubiri ajira katika sekta ya Umma na binafsi.
  Mwenyikiti wa Bodi ya Ushauri wa Wizara ya Fedha na Mipango Wakili Said Chiguma akitoa maelezo kuhusiana na uendeshaji wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika Mahafali ya 17 yaliyofanyika katika Viwanja vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Amina Shaban akizungumza katika Mahafali ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika katika Kampasi Dar es Salaam.
   Picha ya Pamoja na baadhi Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA).
   Baadhi ya Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakifatilia Hutuba ya Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 17 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika Viwanja vya Kampasi Kuu ya Jijini Dar es Salaam.
   baadhi ya Wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakiwa katika mahafali ya 17 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika Viwanja vya Taasisi jijini Dar es Salaam.
   Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wizara ya Fedha na Mipango Thabit Dokodoko akitoa shukurani kwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika Viwanja Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
   Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Amina Shaban akiwa katika picha ya pamoja na Meza Kuu mara baada ya kuhitimisha mahafali ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliofanyika katika Kampasi Kuu ya Dar es Salaam.
   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Luciana Hembe akitoa akizungumza na waandishi habari mara baada ya kuhitimishawa kwa Mahafali ya 17 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Minister of Industry and Trade in Tanzania, Hon. Innocent Bashungwa behalf of Prime Minister highly commended Huawei Tanzania’s efforts on ICT talents Eco-system development, pointing out that these efforts enhance employability and overall competitiveness of the local ICT work force.

  This commend was made at the award ceremony of Huawei Tanzania ICT Competition 2019-2020 on Dec 13th in Dar Es Salsaam. That competition aims to provide a platform for global ICT talents to showcase their ability, compete and communicate, encouraging ICT-related study and drive the growth of a robust ICT talent ecosystem. 

  The minister of Industry and Trade in Tanzania, Hon. Innocent Bashungwa said ICT is a critical part to Tanzania’s infrastructure development and a crucial enabler for Tanzania’s 2025 vision. Especially at the down of the 4th industrial revolution, ICT plays a pivotal role in shaping nation’s economy, providing answers to some social challenges, and enhancing inclusive and sustainable development by driving business growth, creating jobs and enhancing productivity and efficiency.

  With the rapid development of the global digital economy, the World Bank's latest report points out that Sub-Saharan Africa's demand for digital skills in 2030 is as high as 230 million people. In Tanzania, there is a general shortage of ICT skills in both public and private sector.

  “In developing ICT skills, talents is the most important capital. Lack of skilled people will limit our capability of adapting, managing and operating new technologies. The development of ICT human capital which needs to be addressed for full exploitation of benefits of the ICT sector by recognizing ICT professionals, and providing appropriate ICT skills and training to obtain a competent human resources base to accelerate Tanzania’s socio-economic development efforts in the information age.” said Bashungwa. 

  Frank Zhou, the CEO of Huawei Tanzania clarified that Huawei the privilege working with Tanzania government and partners to provide connectivity to uncovered rural area by building low cost, solar powered and fast deployed base stations.

  “Huawei Tanzania is proud to have been at the frontline in building a digital workforce, serving more than 35% of Tanzania’s population since our establishment in 2007, created more than 1000 jobs directly and indirectly, also provided training to more than 2000 ICT engineers.” said Frank Zhou.

  To cultivate more ICT talents, Huawei Tanzania hold 2 corresponding talents program. The first one is job fair which been held on July 2019. Second one is ICT competition which is processing to be the second executive year for Huawei Tanzania to participate the global event. Over 2500 students from the various Universities across Tanzania are expected to participate in the contest with various subjects including network, cloud computing, Artificial Intelligence and big data under the theme “Connection, Glory, Future”.

  Registration period for this competition was ends on 22th November, while preliminary ends on 27th November. Currently, Huawei Tanzania is ready to utilize all latest technology to support Tanzania digital transformation, especially in smart city and smart education. The registered students are able to access learning materials and certification portfolio provided by Huawei free of charge. Winner for preliminary will promote to a 5-days boot camp training for national final in Dar es Salaam Institute of Technology and University of Dar Es Salaam.

  “We need a comprehensive approach of skills development for employment, enhanced productivity and growth. After all, the talents and knowledge will be the key factor to Tanzania industrialization and Vision 2025.” Zhou said.

  These two initiatives epitomize Huawei Tanzania’s efforts on skill transfer and ICT skills gap bridging. The company has actively been working with government, industrial and academic partners in upskilling engineers, providing certification courses, sponsoring aboard studies and supporting government’s initiatives in promoting innovation and ICT learning. Huawei Tanzania has so far signed up 7 universities across Tanzania in establishing ICT academies, where students can access to industrially-recognized certification courses. In addition, the company has also organized together with its business partners several job fairs for over most beneficiaries of the ICT academy program and absorbed more than 80% of them.`

  0 0

  Na Said Mwishehe-Kibondo

  WANANCHI wa  Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, eneo la Station One wameiomba Serikali inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli kuwasaidia kutatua changamoto ya uhaba wa maji.

  Wakizingumza na Michuzi Blog leo Desemba 14 mwaka 2019, wananchi hao wamesema maji ndio kero kubwa kwao na kwamba wanaimani na Serikali Ikisikia kilio chao itatafuta Ufumbuzi ili waondokane na changamoto hiyo ambayo wamekuwa nayo kwa muda mrefu.

  Akizungumza zaidi kuhusu changamoto ya kukosekana kwa maji ya kutosha Mkazi wa Station One Ali Kasato amesema wanalazimika kufuata maji umbali wa wa zaidi ya  kilometa mbili kutoka katikati ya maji yanayopatikana.

  Amesema kuwa dumu moja la maji lenye ujazo wa lita 20 linauzwa Shilingi 700 kutokana na umbali wa kuyafuata  maji hayo kwa kutumia usafiri wa baiskeli.

  "Kilio chetu kikubwa hapa kwetu Kibondo ni uhaba wa maji, ni Kweli kuna changamoto nyingine makini hizo angalau kidogo tunao uwezo wa kuzitatua wenyewe lakini kwenye shida ya maji hili limetuzidi uwezo, hivyo Ombi letu Kwa Serikali itusaidie Ili tuwe na maji ya uhakika.

  "Maji tunayotumia sasa ni ya Chemchem ambayo ni salama kwani yalipimwa na wataalamu na kisha wananchi tukaelezwa yapo Salama. Hivyo hata kama watafanya utaratibu wa kutuvutia maji kutoka yalipo yakaja Mjini itatusaidia,"amesema.

  Aidha ameshauri iwapo itawezekana Serikali ya Wilaya ya Kibondo kwa Kushirikiana na Serikali Kuu iwaruhusu wananchi kuchimba Visima vingine vya maji ili kupunguza msongamano wakati wa kuchota maji,"amesema.

  Hata Hivyo amesema siku za karibuni walikuwa na kikao na viongozi wa Wilaya y Kibondo kuangalia namna ya kutatua changamoto hiyo ambapo walihakikishiwa na viongozi kuwa wataangalia uwezakano wa kutoa kibali chha kuchimbwa visima vingine viwili Ili kupunguza adha hiyo.
   
  Sehemu ya madumu ya maji ambayo hutumika kubebea maji kutoka chemuchemu iliyopo umbali wa kilometa mbili kutoka eneo la Stesheni One wilayani Kibondo

  0 0


  Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa anayemaliza muda wake Ndugu Nimka Stanley Lameck akiongea na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa saba wa Chipukizi Taifa unaofanyika katika Ukumbi wa Sekondari ya Dodoma leo tarehe 14/12/2019 jijini Dodoma.
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa saba wa Chipukizi Taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa anayemaliza muda wake Ndugu Nimka Lameck katika Mkutano Mkuu wa saba unaofanyika jijini Dodoma.
  Makamu Mwenyekiti wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana Taifa Ndugu Pili Suluhu Hassani akiaga wajumbe wa Mkutano Mkuu wa saba wa Chipukizi Taifa unaofanyika jijini Dodoma.
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa saba wa Chipukizi Taifa wakiwa katika shamrashamra za Uchaguzi wa kuchagua Viongozi wapya wa Chipukizi Taifa.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Raymond Mwangwala akitoa Hotuba katika Mkutano Mkuu wa saba wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa unaofanyika jijini Dodoma.

  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chipukizi Taifa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ndugu Mwl Raymond Mwangwala.
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chipukizi Taifa wakiwa tayari kwa Uchaguzi Viongozi wapya wa Chipukizi Taifa katika Mkutano Mkuu wa Chipukizi Taifa unaofanyika jijini Dodoma.
  Picha zote na Fahadi Siraji wa UVCCM

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (Katikati)Mwl Raymond Mwangwala akivikwa Skafu na Chipukizi wa Umoja wa Vijana alipowasili katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari DodomaUnapofanyika Mkutano Mkuu wa Chipukizi Taifa Meza Kuu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Mwl Raymond Mwangwal (katikati) kulia ni Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa anaemaliza muda wakeNdg Nimka Stanley pamoja na Mkamu mwenyekiti wa Chipukizi Taifa anae Maliza Muda wake Ndg Pili Suluhu Hassan Meza Kuu Chipukizi Wakifurahi Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndg Leonard Singo akitoa maelezo Chipukizi akifurahi
   

  0 0

  Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha 

  Shirika la Hifadhi za Taifa{TANAPA} limezindua kampeni maalumu ijulikanyo kwe jina la ‘’Talii na TANAPA msimu huu wa sikukuu ya X mass na Mwaka mpya’’ kwa kushirikisha wasanii maarufu,warembo ,watangazaji maarufu na watu maarufu lengo ni kutaka kuhamashisha watanzania kutembele hifadhi za Taifa badala ya kwenda kutalii nje ya nchi katika kipindi hicho.

  Hayo yamesemwa na Kaimu Kamishina wa Uhifadhi wa TANAPA,Witness Shoo mbele ya waandishi wa habari kwa kushirikisha viongozi mbalimbali wa uhifadhi,wasanii na watangazaji, tukio limefanyika katika Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Arusha..

  Shoo alisema kuwa lengo la TANAPA ni kutaka kila mtanzania kuwa mzalendo na nchini yake kwa kutembelea vivutio vilivyokuwa katika hifadhi 22 hapa nchini kwa kuvitembelea na kuwa balozi wakubwa wa kuvitangaza.

  Alisema kundi la kwanza la wasani,watangazaji na watu maarufu litaanza kufanya kampeni hiyo desemba 20 mwaka huu katika hifadhi sita ikiwemo Ruaha,Katavi,Mkomazi,Rubondo,Mikumi na hifadhi ya Gombe iliyopo Mkoani Kigoma.

  Kamishina huyo alisema katika Hifadhi ya Ruaha msanii Idrisa Sultan atakwenda kutalii katika mbuga hiyo na kuitangaza ndani na nje ya nchi katika mitandao ya kijamii kwani anawafuasi wengi katika mitandao ya kijamii hivyo anawajibu wa kutoa ujumbe kwa watanzania kuacha kukimbilia nje ya nchi kutalii badala yake watembelee hifadhi Taifa.

  Alisema msanii Mrisho Mpoto atakuwa katika Hifadhi ya Katavi,mrembo wa mwaka Nancy Sumary atakuwa katika hifadhi ya Mkomazi,mtangazaji kijana aliyejipatia umaarufu hapa nchini,Milard Ayo na Miss wa mwaka 2018 Elizaberth Makune watakuwa na jukumu la kuwakumbusha watanzania kutembelea hifadhi ya Robondo.

  Wengine ni pamoja na wasanii wa muziki wa Bongo flava Lulu Abas maarufu kwa jina la Lulu Diva atakuwa katika Hifadhi ya Mikumi na msani aliyetambulika kwa jina moja la Rubby atakuwa katika hifadhi ya Gombe.

  Naye Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuwataka watanzania kuwa na tabia ya kutembelea mbuga za wanyama katika vipindi vyote vya sikukuu ya X Mass na Mwaka mpya na sikukuu nyingine kwa kutumia kiasi kidogo cha fedha na pia kuvitangaza vivutio hivyo kwa faida ya nchi.

  Shelutete alisema kuwa wasanii wa fani mbalimbali,watu maarufu na watangazaji watashirikishwa katika kampeni hiyo iliyolenga kumtaka mtanzania kupenda cha nchi yake na kuacha kujali vya nje .

  Naye Msanii Idrisa Sultan alisema kuwa katika maisha yake hajawahi kufika katika hifadhi ya Ruaha hivyo kwa fursa aliyopewa atahakikisha anaitangaza hifadhi hiyo kwa kadri awezavyo lengo ni kutaka watanzania kuwa wazalendo na kupenda cha kwao na kuacha ulimbukeni wa kikumbilia nje ya nchi kama Dubai na kungine kwa kutumia mamilionin ya pesa bila ya sababu za msingi.
  Kaimu Kamishina wa Uhifadhi wa TANAPA,Witness Shoo akizindua rasmi  kampeni ya Talii na TANAPA , ambayo mabalozi wake ni baadhi ya wasanii pamoja na watangazaji ndani ya ukumbi Wa ofisi za makao makuu ya shirika hilo.
  Mabalozi  Wa kampeni hiyo ambao ni wasanii Wa muziki ,vichekesho na watangazaji pamoja na baadhi ya wafanyakazi Wa TANAPA wakiwa katika   picha ya pamoja


  0 0


  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI  Mhe.Selemani Jafo akizungumza na Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara waliohudhurua Kikao Kazi cha siku mbili (12 – 13,Desemba 2019) kilichoongozwa na Kauli Mbiu “Michezo kwa Afya,Ajira na Maendeleo ya Viwanda” wakati akifunga kikao hicho leo Jijini Dodoma.
  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi akitoa taarifa fupi  ya kikao kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara kilichofanyika kwa siku mbili (12 – 13,Desemba 2019) wakati wa ufungaji wa kikao hicho uliofanywa na Mhe. Selemani Jafo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI  Jijini Dodoma kilichoongozwa na Kauli Mbiu “Michezo kwa Afya,Ajira na Maendeleo ya Viwanda”
  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo  Bw.Bernard Patrick akitoa ufafanuzi kuhusu Muundo wa Utumishi katika kada ya Michezo kwa Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa siku mbili (12 – 13,Desemba 2019)kilichoongozwa na  Kauli Mbiu “Michezo kwa Afya,Ajira na Maendeleo ya Viwanda” leo Jijini Dodoma.
  Dkt.Jonas Tiberoha akiwasilisha mada ya “Masoko,Udhamini na Maandalizi ya Maandiko katika Michezo” wakati wa  kikao kazi cha Maafisa Michezo wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara kilichofanyika kwa siku mbili (12 – 13,Desemba 2019) Jijini Dodoma kilichongozwa na Kauli Mbiu “Michezo kwa Afya,Ajira na Maendeleo ya Viwanda”
  ………………..

  Na Anitha Jonas – WHUSM, Dodoma 

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo amewaagiza wakurugenzi wote wa Halmashauri kuhakikisha wanawawezesha Maafisa Michezo katika ofisi zao kushiriki katika kikao cha mwakani.

  Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo jijini Dodoma alipokuwa akifunga Kikao kazi cha Maafisa Michezo wa Tanzania Bara ambacho kimefanyika kwa mara ya kwanza jijini Dodoma kikilenga kuwajengea uwezo maafisa hao katika kusimamia masuala ya michezo na kujitathmini na kupeana maelekezo ya nini kifanyike kuboresha sekta ya michezo nchini.

  “Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 imejadili kwa upana  agenda ya michezo na kwa kiongozi yoyote wa serikali anayepinga suala la michezo ni mmoja ya watu wanaokwamisha utekelezaji wa ilani kwani watumishi wa umma wanatekeleza ilani ya chama kilichopo madarakani,’alisema Mhe.Jafo.

  Akiendelea kuzungumza wakati wa kufunga kikao kazi hicho Mhe.Jafo alisisitiza hivi karibuni baada ya michezo kurudishwa mashuleni tumeshuhudia vijana wadogo wakifanya mambo makubwa katika michezo mfano timu ya Serengeti Boys ambayo imekwenda mpaka AFCON U17 halikadhalika ubingwa wa Copa Coca Cola mwaka huu, na haya ni matokeo ya kazi  za Maafisa Michezo katika kuibua vipaji hivi.

  Aidha, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi alisistiza kuwa  tasnia ya michezo ni muhimu sana katika kukuza uchumi na ni moja ya sekta inayotoa ajira nyingi kwa wanamichezo na ndiyo  yenye watu wanaongozwa kulipwa fedha nyingi hivyo sekta hii ikisimamiwa vyema inaweza kulipeleka taifa mbali katika maendeleo.

  “Nimatarajio yangu kuwa kikao kazi hichi kitaleta matokeo chanya na maafisa hawa wataenda kusimamia vyema michezo katika maeneo yao na kuondoa dhana potofu ya watu kudharau michezo, pia wataibua vipaji vipya vya wanamichezo kama wanariadha mahiri zaidi ya akina Philbert Bayi,Suleiman Nyambui na Mwinga Mwanjala. Tanzania ina watu wengi sana na tuna uwezo wa kuibua vipaji vikubwa vitakavyo leta medali za dhahabu” alisema Dkt.Possi.

  Pamoja na hayo Dkt.Possi alisisitiza kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya ambao  miongoni mwao wapo wengi wenye vipaji hivyo ipo haja maafisa michezo hao kuhakikisha katika maeneo yao wanafanya kazi kubwa ya kuibua vipaji haswa kwa vijana kwani hao ndiyo nguvu kazi ya taifa. 

  Halikadhalika  Afisa Michezo kutoka Wilaya ya Siha Bibi.Neema Joseph alishukuru uongozi wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuandaa kikao kazi ambacho mbali na kuwapatia elimu ya kuandaa maandiko ya kuomba ufadhili katika michezo pia  amejifunza mambo mengi ambayo alikuwa hayajui na hivi sasa wilaya yake haitaenda kuwa kama ilivyokuwa awali kutoka na mafunzo aliyopata.

  0 0


  Mbunge Rose Tweve akishangiliwa na wabunge wenzake

  Mbunge Rose Tweve na Yosepher Komba kulia wakijiandaa kwa kuanza riadha


  Mbunge Rose Tweve kulia akiwakimbiza wakenya

  Wabunge wanaume wanamichezo toka Tanzania wakimshangilia mbunge Tweve

  Wabunge wanawake Rose Tweve na Yosepher Komba wameendelea kuing'aza nyota ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuibuka na medali za dhahabu katika mbio za mita Mia moja (100m) na mita elfu moja na Mia tano (1500m).

  Wakati Rose Tweve kutoka Mkoa wa Iringa akiwaburuza wabunge wa nchi za Kenya, Uganda, Burundi na wale wa Bunge la Afrika Mashariki EALA, Yosepher Komba kutoka Viti Maalum Mkoa wa Tanga aliwagaragaza wapinzani wake katika mbio za mita 1500.

  Wabunge Hao Vijana sasa mwaka wa Pili mfululizo wanaendelea kuipeperusha vema Bendera ya Tanzania katika mchezo wa riadha Naendelea wanatarajia kuendelea tena hapo jumapili katika mbio za kupokezana Vijiji.

  Kwa upande mwengine mwanamama Anatropia Teonest alimaliza nafasi ya Pili katika mbio za mita 400, huku wanaume kupokezana Vijiji Tanzania ilishika nafasi ya tatu.

  Michezo hiyo inaendelea Kesho katika mchezo wa Wavu wanaume na wanawake wakati Bunge la Tanzania watajitupa uwanjani kuvaana na Bunge la Afrika Mashariki

  0 0

  Na, Editha Edward -Tabora

  Wakala wa Barabara za vijijini na mjini TARURA wilayani Igunga Mkoani Tabora wanatarajia kutumia kiasi cha shilingi Milioni 455 kutengeneza Barabara 2 za kiwango cha lami mjini Igunga yenye urefu wa km 1.3 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 

  Hayo yamesemwa na meneja wa TARURA wilayani humo Mhandisi Sadick Karume katika kikao cha baraza la madiwani wa halmshauri ya wilaya huyo

  Karume ametaja Barabara zitakazotengenezwa ni Igunga-mbutu yenye urefu wa km1.0 itakayogharimu kiasi cha shilingi Milioni 380 na ile ya CCM -SingidaRoad yenye urefu wa km 0.3(mita 300)ambapo itagharimu kiasi cha pesa shilingi Milioni sabini na tano

  Pia amesema ujenzi wa Barabara hizo ni sehemu ya mkakati a wakala huyo kuboresha Barabara zote za mji huo ikiwemo kuzifanyia matengenezo makubwa Barabara mbovu zote zinazounganisha vijiji na kata zote wilayani humo

  Aidha amesema matengenezo hayo pia yataambatana na ujenzi wa mifereji makaravati na madaraja ili barabara hizo ziweze kupitika wakati wote Huku akibainisha mchakato wa kuanza ujenzi wa Barabara ya mbutu-  isakamaliwa tayari umekamilika

  Wakichangia hoja baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji miradi ya TARURA baadhi ya madiwani wamelalamikia barabara za Kata zao ambazo hazipitiki kutoingizwa katika mpango wa matengenezo kwa mwaka ujao wa fedha 

  Nao baadhi ya madiwani waloochangia hoja ni Elisha Anthony wa Kata ya kining'inila) Jilala Mipawa Kata ya humba na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Lucas Bugota wameeleza kuwa barabara nyingi za vijijini zinatengenezwa kwa kiwango cha chin sana kiasi kwamba hazikawii kuharibika hivyo wameishauri TARURA kuobgezewa bajeti ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuwataka wataalamu wa TARURA kutumia utaalamu wao ili barabara zinazojengwa ziweze kudumu tofauti na hali ilivyosasa 

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Peter Onesmo ambae pia ni diwani wa Kata ya choma amemtaka meneja wa TARURA wilayani humo kufanyia kazi ushauri anaopewa na madiwani ili kuepusha malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wananchi. 


  0 0

  Na, Editha Edward -Tabora

  Wakala wa Barabara za vijijini na mjini TARURA wilayani Igunga Mkoani Tabora wanatarajia kutumia kiasi cha shilingi Milioni 455 kutengeneza Barabara 2 za kiwango cha lami mjini Igunga yenye urefu wa km 1.3 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 

  Hayo yamesemwa na meneja wa TARURA wilayani humo Mhandisi Sadick Karume katika kikao cha baraza la madiwani wa halmshauri ya wilaya huyo

  Karume ametaja Barabara zitakazotengenezwa ni Igunga-mbutu yenye urefu wa km1.0 itakayogharimu kiasi cha shilingi Milioni 380 na ile ya CCM -SingidaRoad yenye urefu wa km 0.3(mita 300)ambapo itagharimu kiasi cha pesa shilingi Milioni sabini na tano

  Pia amesema ujenzi wa Barabara hizo ni sehemu ya mkakati a wakala huyo kuboresha Barabara zote za mji huo ikiwemo kuzifanyia matengenezo makubwa Barabara mbovu zote zinazounganisha vijiji na kata zote wilayani humo

  Aidha amesema matengenezo hayo pia yataambatana na ujenzi wa mifereji makaravati na madaraja ili barabara hizo ziweze kupitika wakati wote Huku akibainisha mchakato wa kuanza ujenzi wa Barabara ya mbutu-  isakamaliwa tayari umekamilika

  Wakichangia hoja baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji miradi ya TARURA baadhi ya madiwani wamelalamikia barabara za Kata zao ambazo hazipitiki kutoingizwa katika mpango wa matengenezo kwa mwaka ujao wa fedha 

  Nao baadhi ya madiwani waloochangia hoja ni Elisha Anthony wa Kata ya kining'inila) Jilala Mipawa Kata ya humba na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Lucas Bugota wameeleza kuwa barabara nyingi za vijijini zinatengenezwa kwa kiwango cha chin sana kiasi kwamba hazikawii kuharibika hivyo wameishauri TARURA kuobgezewa bajeti ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuwataka wataalamu wa TARURA kutumia utaalamu wao ili barabara zinazojengwa ziweze kudumu tofauti na hali ilivyosasa 

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Peter Onesmo ambae pia ni diwani wa Kata ya choma amemtaka meneja wa TARURA wilayani humo kufanyia kazi ushauri anaopewa na madiwani ili kuepusha malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wananchi. 

  (Katikati) ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Igunga Peter Onesmo wa (kwanza kushoto)ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Igunga Lucas Bugota (wa kwanza kulia ) ni mkurugenzi wa halmashauri hiyo Revocatus Kuuli wakiwa katika baraza la madiwani mjini Igunga.
  Pichani ni madiwani wa halmashuri ya igunga wakisikiliza jambo kwa makini.  0 0

  Na Zainab Nyamka, Michuzi  TV
  Katika  kuboresha huduma ya maji safi kwa wakazi wa Kigamboni Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira DAWASA wametembelea miradi ya maji ya Kijamii inayosimamiwa na Mamlaka hiyo.

  Katika ziara hiyo waliongozana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja ambapo alitembelea miradi mbalimbali inayotoa huduma na ile iliyo katika hatua za mwisho za umaliziaji.

  Luhemeja ametembelea miradi ya visima iliyopo Kigamboni ikiwemo moja ya Kisima kutoka kwenye Mradi wa Kimbiji na Mpera  kinachojengwa na Kampuni ya Serengeti.

  Baada ya kutembelea kisima hicho cha K13, Luhemeja ameshuhudia majaribio ya kuvuta maji (pump testing) ambacho kimekamilika tayari kwa kuanza mchakato wa ulazaji wa mabomba ya kusafirishia maji na yale ga usambazaji.

  Ziara hiyo imefanyika leo ikiwa ni katika kuhakikisha mji wa Kihuduma Kigamboni unapata huduma ya maji safi kutoka Mamlaka hiyo

  Mbali na kisima hicho, Luhemeja ametembelea pia mradi wa maji wa Kisima Minondo kikiwa na tanki la ujazo wa Lita 45,000, Mradi wa Kisima cha Gezaulole chenye matanki mawili ya ujazo wa Lita  45,000 na Lita 90,000.

  Luhemeja, pia ametembelea mradi wa Kisima cha Kibugumo chenye uwezo wa kuzalisha lita za maji 6800 kwa saa.

  Pia, ametembelea nyumba za NSSF zilizopo Kijichi  Vikunai ambazo Dawasa wanatarajia kupelekea maji kwenye nyumba hizo ili wakazj wa eneo hilo wafaidike kwa kupata huduma ya maji kutoka Dawasa.
  Mmoja wa wafanyakazi kutoka kampuni ya Serengeti inayochimba mradi wa maji wa Visima vya Kimbiji na Mpera akifungua koki ili kuruhusu maji wakati wa Pump testing leo.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akijaribu maji kutoka katika ch K13 kiyakachihudumia mkoa wa kihuduma Kigamboni.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuini ya Serengeti Mehrdad Talebi baada ya kutembelea mradi wa Visima vya Kimbiji na Mpera na kushuhudia majaribio ya kuvuta maji (pump testing) ambacho kimekamilika tayari kwa kuanza mchakato wa ulazaji wa mabomba ya kusafirishia maji na yale ga usambazaji.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Mehrdad Talebi baada ya kutembelea mradi wa Visima vya Kimbiji na Mpera.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Dawasa Neli Msuya baada ya kutembelea moja ya miradi ya kijamii inayofanyiwa ukarabati na Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa Kigamboni, wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya kijamii katika mkoa wa kihuduma Kigamboni.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Dawasa Neli Msuya baada ya kutembelea moja ya miradi ya kijamii  inayotoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa kihuduma Kigamboni.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Dawasa Neli Msuya baada ya kutembelea moja ya miradi ya kijamii  inayotoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa kihuduma Kigamboni.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelekezo kwa watendaji wa Mamlaka hiyo ya kuhakikisha wanafikisha maji katika nyumba za NSSF ziizopo katika hatua ya umaliziaji ili wakazi wa eneo hilo wanufaike kwa kupata huduma ya maji safi kutoka Dawasa.
  Meneja wa Mkoa wa Kihuduma Kigamboni wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Tumaini Muhondwa  akitoa maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa   Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya kijamii katika mkoa wa kihuduma Kigamboni.

  0 0   Mkurugenzi wa Habari maelezo Zanzibar Juma Mohamed akibadilishana mawazo na Mmoja kati ya Wanadiaspora Maggid Mjengwa katika Ziara ya  Wanadiaspora katika Sehemu mbalimbali ikiwemo shamba la Viungo(Spice)na kuangalia Wanyama Jozani Mkoa wa Kusini Unguja.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi (Gavu)akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na ziara ya Wanadiaspora katika Sehemu mbalimbali ikiwemo shamba la Viungo(Spice)na kuangalia Wanyama Jozani Mkoa wa Kusini Unguja.

  Mtembezaji wageni katika Shamba la Kitundu Spice Rashid Ahmada Said akiwagawia  wanadiaspora Mbegu za  Mti wa Mdalasini wakati walipofika katika shamba hilo la Viungo (SPICE)wakiwa katika Ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali Zanzibar.
  Wanadiaspora wakiwa katika ziara ya kutembelea sehemu mbalimbali za Vivutio vya Utalii Ikiwemo Viungo(Spice)Kitundu na kuangalia Wanyama Jozani Mkoa wa Kusini Unguja.
  PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0


   Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) mkoa wa Kibaha Crossman Makere wakielekea yalipo mabomba ya DAWASA yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuleta maji katika kiwanda cha TanChoice kilichopo katika wilaya ya Kibaha mkoni Pwani.
  Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) mkoa wa Kibaha Crossman Makere akitoa ufafanuzi kuhusu mambomba yaliyowekwa kwenye Kiwanda cha Kiwanda cha nyama  cha TanChoice kwa ajili ya kuunganishiwa maji kutoka DAWASA. Wa Julia ni Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  na Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Juma.
  Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Kibaha, DAWASA pamoja na viongozi wa kiwanda cha TanChoice mara baada ya kufanya ziara hapo ili kujionea uwekaji wa mabomba ya maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).
   Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akikagua mabomba ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) yaliyopo katika kiwanda cha TanChoice wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maji katika wilaya Kibaha mkoani Pwani
   Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  akitoa maelekezo kwa viongozi wa DAWASA pamoja na RUWASA mara baada ya kuleta mradi wa maji kwenye kijiji cha Kipangege uliokwamishwa na utendaji mbaya wa viongozi wa RUWASA wakati wa ziara yake katika wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
   Wananchi wa Kipangege wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  wakati akitafuta ufumbuzi wa upatikanaji wa maji katika kijiji hicho mara baada ya mradi huo kutumia miaka sita bila kukamilika ulikuwa unasimamiwa na RUWASA.
    Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Makazi Mapya wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji iliyo chini ya wizara yake katika eneo la Kibaha mkoani Pwani.
   Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA Eng.Ramadhani Mketo akitoa taarifa fupi ya namna ya wananchi wa Kitongoji cha Makazi mapya kata Kawawa wilaya ya Kibaha watakavyonufaika na mradi wa maji ya DAWASA kwa njia ya mabomba kwa kila mkazi wa eneo hilo ambapo sasa wanatumia maji ya Kisima ya DAWASA.
   Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Juma akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Makazi mapya kata Kawawa wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  ya ukaguzi wa miradi ya maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) na RUWASA. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na kulia ni Diwani wa kata ya Kawawa Salum Salum Lubawa.
   Diwani wa kata ya Kawawa Salum Salum Lubawa akitoa shukrani kwa Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) waliofika katika  Kitongoji cha Makazi Mapya ili kuweza kutatua kero ya maji katika eneo hilo.
  Baadhi ya wananchi wa Kitongoji cha Makazi Mapya kata Kawawa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya Maji iliyopo katika wilaya Kibaha mkoani Pwani.older | 1 | .... | 3284 | 3285 | (Page 3286) | 3287 | 3288 | .... | 3352 | newer