Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

PROGRAM COORDINAOR WA AGITOS FOUNDATION ATEMBELEA MAZOEZI YA WAOGELEAJI WENYE ULEMAVU (PARA SWIMMERS) NORDIC SCHOOL, DAR ES SALAAM

$
0
0
Mratibu Msaidizi wa Mfumo Pacha wa mafunzo(DATS) kutoka VETA, Challange Fihili akimuoneshea namna mfumo pacha wa mafunzo(Dual Apprenticeship Training System-DATS) unaoendeshwa kwa pande kuu mbili zinazohusisha viwanda pamoja na Vyuo vya VETA mmoja wa  wananchi waliofika kwenye maonesho ya wiki ya Viwanda yanayofanyika katika  viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
 Mhitimu wa VETA, Zadock James akitolea ufafanuzi kuhusu ubunifu wa mfumo wa kuchuja maji safi na salama kwa mmoja wa wananchi waliofika kwenye maonesho ya Viwanda yaliyoanza  Desemba 05 hadi Desemba 07, 2019.
 Mwanafunzi wa VETA Mwaka wa Pili wa Kozi ya Electrical Installation, Omary Japhari akitoa ufafanuzi kuhusu umeme mkubwa unavyofanya kazi katika sehemu mbalimbali kwa wananchi waliofika katika Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K.Nyerere
 Afisa Uhusiano  wa VETA Dora Tesha akitolea ufafanuzi kuhusu utengenezwaji wa pochi kwa wananchi waliofika katika Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K.Nyerere
 Mwanafunzi wa VETA wa Mwaka wa Tatu wa Kozi ya Automotive Mechanics, Shafii Kamugisha akiwafafanulia wananchi waliofika kwenye maonesho kuhusu mfumo wa Injini unavyofanya kazi  kwenye Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa VETA katika Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.




NCHI ZA ACP ZATAKA MAJADILIANO UPYA KUHUSU MKATABA WA EPA

$
0
0
Baraza la Mawaziri wa Nchi za Afrika,Caribbean na Pacific (ACP) Tanzania ikiwemo zimekubaliana kuwa nchi za ACP na Umoja wa Ulaya zifanye maridhiano katika maeneo yanayoonekana kuwa ni kikwazo kwa baadhi ya nchi hizo kutosaini mkataba wa EPA ama kuitekeleza.

Azimio hilo la Baraza la Mawaziri wa Nchi za Afrika,Caribbean na Pacific zimefikia makubaliano hayo katika mkutano wa 110 wa nchi hizo unaoendelea jijini Nairobi nchini Kenya.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema nchi hizo zimekubaliana kufanya mapitio mapya ya mikataba ya EPA uliyoingia na nchi za ACP.

Ameongeza kuwa mapitio hayo yanalenga kuzingatia hali halisi ya sasa duniani ikiwa ni pamoja na Malengo ya Dunia ya Maendeleo Endelevu, Makubaliano ya Mkataba wa Paris kuhusu Mazingira na uhalisia mwingine ndani na nje ya Umoja wa Ulaya.

Aidha maazimio mengine yaliyopitishwa katika mkutano huo wa 110 wa Baraza la mawaziri wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific (ACP) ni pamoja na kuifanya ACP kuwa umoja wa kisasa zaidi katika malengo yake, muundo wake na mikakati yake katika kufikia ACP tunayoitaka (The ACP we want) ikiwa ni pamoja na kubadilisha jina kutoka KUNDI la ACP na kuwa UMOJA wa ACP, yaani kutoka African Caribbean and Pacific Group of States (ACP Group of States) na kuitwa Organisation of the African Caribbean and Pacific Group of States (OACP group of states).

Prof. Kabudi amesema lengo la mabadiliko hayo ni kuifanya ACP kuwa na nguvu zaidi katika kupanga, kuweka mikakati na kutekeleza kwa ufanisi malengo ya Umoja wetu.

Pia baraza limefanya uamuzi wa kumchagua Balozi George Rebelo Pinto Chikoti kutoka Jamhuri ya Angola kuwa Katibu Mkuu wa Sekretariati ya ACP kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025.

Kuhusu suala la kujitegemea Baraza limeidhinisha uamuzi wa kuanzisha mfuko wa uwekezaji wa jumuiya ya kundi la nchi za Afrika Caribbean na Pasific kwa lengo la kukabiliana na changamoto ya utegemezi katika kuendesha jumuiya. mfuko huu utaweza kufanya uwekezaji kwa kutumia fedha za Umoja pamoja fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali badala ya kutegemea zaidi ufadhili kutoka Umoja wa Ulaya.

Katika mkutano huo Tanzania imeweza kufanya majadiliano ya pembezoni na Jamhuri ya Kenya ambaye ni nchi mwenyeji wa mkutano 110 wa nchi wanachama wa Afrika,Caribbean na Pacific na hatimaye kukubaliana kuwasilisha pendekezo ambalo limepitishwa na Baraza la Mawaziri la kutumia maneno ya kiswahili katika kaulimbiu ya Azimio la Nairobi ambayo inaiitwa “NAIROBI NGUVU YA PAMOJA DECLARATION”.
 Hatua hii ni sehemu ya kuenzi na kukuza Kiswahili ndani ya Wanachama wenzetu wa nchi 79 za ACP.Jumatatu ya Desemba 09,2019 mkutano huo unaingia katika hatua nyingine ambapo kutafanyika mkutano wa tisa wa wakuu wa kundi la nchi za Afrika,Carribean na Pacific ambapo wakuu wa nchi na serikali wapatao 79 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA, AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA ABIRIA, KATIKA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA.

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi wa jengo la abiria, linalojengwa katika uwanja wa ndege wa Mwanza, Desemba 8, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akioneshwa ramani ya jengo la abiria, linalojengwa katika uwanja wa ndege wa Mwanza, kabla ya kuweka jiwe la msingi, Desemba 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kuweka jiwe la msingi wa jengo la abiria, linalojengwa katika uwanja wa ndege wa Mwanza, Desemba 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA JENGO LA MAMA NA MTOTO JIJINI MWANZA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata Utepe na kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza leo Disemba 08,2019, ikiwa ni moja ya mfululizo wa shamrashamra ya Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri yanayotegemewa kuadhimishwa kesho  Disemba  09 katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Baadhi  ya Wauguzi Jijini Mwanza wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa  akihutubia Viongozi na Wananchi wa Nyamagana Jijini Mwanza baada ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana leo Disemba 08,2019, ikiwa ni moja ya mfululizo wa shamrashamra ya Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri yanayotegemewa kuadhimishwa kesho  Disemba  09 katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Baadhi  ya Viongozi na Wananchi Jijini Mwanza wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa  akihutubia Viongozi na Wananchi wa Nyamagana Jijini Mwanza baada ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana leo Disemba 08,2019, ikiwa ni moja ya mfululizo wa shamrashamra ya Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri yanayotegemewa kuadhimishwa kesho  Disemba  09 katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi na Wananchi wa Nyamagana Jijini Mwanza baada ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana leo Disemba 08,2019, ikiwa ni moja ya mfululizo wa shamrashamra ya Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri yanayotegemewa kuadhimishwa kesho  Disemba  09 katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi na Wananchi wa Nyamagana Jijini Mwanza baada ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana leo Disemba 08,2019, ikiwa ni moja ya mfululizo wa shamrashamra ya Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri yanayotegemewa kuadhimishwa kesho  Disemba  09 katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

SHULE YA MSINGI MWISENGE KUWA NA MAJENGO YA KISASA – MAJALIWA

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

SERIKALI imeamua kuifanyia ukarabati mkubwa shule ya msingi Mwisenge ambayo alisoma Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere ili iwe sehemu ya historia ya Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kutembelea shule hiyo jana (Jumamosi, Desemba 7, 2019), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeamua kuifanya shule hiyo iliyopo kwenye manispaa ya Musoma iwe sehemu ya historia ya Mwalimu Nyerere pamoja na historia ya Tanzania kwa ujumla.

“Shule hiyo haiwezi kubeba historia ya Mwalimu Nyerere, endapo majengo na miundombinu ya shule hiyo haitakarabatiwa na kujengwa upya,” amesema na kuongeza kuwa: “Mipango ya kuifanya shule hiyo iwe sehemu ya historia ya Tanzania inaendelea serikalini; na kwamba historia ya Baba wa Taifa itapatikana shuleni hapo.”

Amesema baada ya mchakato huo kukamilika, shule ya msingi Mwisenge itaubeba mkoa wa Mara na nchi ya Tanzania kwa ujumla.

Amesema kuwa uamuzi wa kufanya shule hiyo kuwa shule yenye historia ya Tanzania unatokana na viongozi mbalimbali wa Tanzania kusomea shuleni hapo ambapo amewataja Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba na Mzee Joseph Butiku kuwa ni miongoni mwa viongozi wa kitaifa waliosoma kwenye shule hiyo.

Amewapongeza viongozi wa mkoa wa Mara kwa kusimamia matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya shule hiyo na akawataka viongozi wengine wa umma waige mfano huo.

Mapema, akitoa taarifa ya ukarabati wa shule hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma, Bi. Fidelica Myovela amesema kuwa manispaa yake inahitaji zaidi ya sh. milioni 161 ili kukamilisha ukarabati wa shule hiyo ambao tayari umeanza.

Amesema kuwa hadi sasa wamepokea zaidi ya sh. milioni 772.6 kutoka TAMISEMI kwa ajili ya ukarabati huo ambapo hadi sasa wamekwishafanya ukarabati kwa asilimia 85 ya kazi yote.

Amesema kuwa kati ya fedha hizo, jumla ya sh. milioni 20 zilitolewa na Rais Magufuli Septemba, mwaka jana ambaye pia aliagiza tathmini ya gharama za ujenzi na ukarabati wa miundombinu shuleni hapo ianze mara moja.

Washindi wa wiki promosheni ya kishindo cha kufunga mwaka walamba mil.5

$
0
0
Mkurugenzi Wa Tigo Kanda Ya Kaskazini Aidan Komba Akimkabidhi Elizabeth Makala Mshindi Wa Milioni Tano Katika Promosheni Ya Kishindo Cha Kufunga Mwaka Mkoani Arusha Mapema Wiki Hii.
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazin Aidan Komba akimkabidhi Julita Kimaro Mshindi Wa Milioni Moja katika promosheni ya kishindo cha kufunga Mwaka mkoani Arusha Mapema wiki hii. 
Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya Akimkabidhi. Tegemeo Enos Mshindi Wa Milioni Tano katika promosheni ya kishindo ch kufunga Mwaka mkoani Mwanza Mapema wiki hii. 
Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Gwamaka Mwakilembe Akimkabidhi Mausel Magesa Mshindi Wa Milioni Tano katika promosheni ya kishindo ch kufunga Mwaka mkoani Mwanza Mapema wiki hii.

Watu tujikite katika mazoezi na kunywa maziwa, Dar es salaam kuwa mfano

$
0
0
WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam waaswa kuwa ya mfano katika kuhakikisha wanakunywa maziwa mengi zaidi.

Ameyasema hayo, Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva wakati akizungumza na wanamichezo mbalimbali katika maonesho ya nne ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya Jk. Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam leo.

"Kila jumapili ya Mwisho wa mwezi itakuwa siku ya kunywa maziwa tunaanza kwa mfano katika jiji la Dar es Salaam kwa kunywa maziwa kwa kila jumapili ya mwisho wa mwezi katika viwanja vya Sabasaba". Amesema Lyaniva.

Amesema kuwa maziwa ni mhimu na ni chanzo mhimu katika kuongeza kipato, pia ukinywa maziwa unakuwa na afya njema.

Lyaniva amesema zao pekee linaloweza kuvunwa kwa mwaka mzima ni maziwa ambayo unaweza kuvunwa kwa kila siku iendayo kwa Mungu ukilinganisha na mazao mengine yote.

"Katika mnyororo wa dhamani ya maziwa unazalisha fedha nyingi, na unapokuwa unafunga ng'ombe wa Maziwa unazalisha ajira kwa watu watakao kata majani, watu watakao kamua maziwa na watu watakao tembeza maziwa".

Hata hivyo Lyaniva amesisitiza ubora wa maziwa  kwa wadau wanaotengeneza na kuzalisha maziwa watengeneze yenye ubora wa hali ya juu kwani ubora ni mhimu sana katika afya.

Lyaniva ametoa wito kwa wananchi kuanza kufunga ng'ombe kwa wingi, ili tuweze kunywa maziwa kwa wingi kwa kuwa maziwa yanawingi wa virutubisho vingi. 

"Watu wanaokunywa maziwa wanakuwa na afya na furaha wakati wote na tuachane na kunywa maalikasusu mengine.

Aidha Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Dkt.Sophia Mlote amesema Bodi ya Maziwa inaendelea kufanya jitihada ili kuhakikisha unywaji wa maziwa unaongezeka hadi kufikia lita 200 kwa mtu kwa mwaka.

Dkt. Sophia amewapongeza wadau wote walioshiriki katika kutoa hamasa kwa wananchi kuweza kunywa maziwa hasa baada ya mazoezi kwani maziwa yana virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini ili kujenga afya.
Kauli mbiu ya mwaka huu katika maonesho ya viwanda ni tucheze tufanye mazoezi, tunywe maziwa kwa afya zetu.

Makampuni mbalimbali ya maziwa kama vile Dar fresh,Tangafresh, Asas Dairies, Woodland n.k walijitokeza kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wananchi kuweza kunywa maziwa mara baada ya mazoezi ili kuimarisha afya zao.
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza wakati wa kilele cha Tamasha la Maziwa lililofanyika kwa siku mbili (2) tar 7-8 Disemba, 2019 katika viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere (sabasaba).
Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Dkt.Sophia Mlote akizungumza na vijana wa mbio ndogondogo wa wilaya za jiji la Dar es Salaam leo baada ya kutembelea katika viwanja vya maonesho ya JK. Nyerer Sabasaba jijini Dar es Salaam. Amesema Bodi ya Maziwa inaendelea kufanya jitihada ili kuhakikisha unywaji wa maziwa unaongezeka hadi kufikia lita 200 kwa mtu kwa mwaka.

Baadhi ya wanajogging wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam mara baada ya kufika katika viwanya vya JK. Nyerere Sabasaba katika Maonesho ya viwanda ya nne.








Mkuu wa Wilaya Temeke Felix Lyaniva akitoa vyeti kwa wawakilishi wa vilau vya jogging leo wakati wa kilele cha Tamasha la Maziwa lililofanyika kwa siku mbili (2) tar 7-8 Disemba, 2019 katika viwanja vya Mwl Julius K. Nyerere (sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya Temeke Felix Lyaniva akitembelea mabanda ya  kuuza maziwa leo wakati wa kilele cha Tamasha la Maziwa lililofanyika kwa siku mbili (2) tar 7-8 Disemba, 2019 katika viwanja vya Mwl Julius K. Nyerere (sabasaba) jijini Dar es Salaam.

KIKUNDI CHA WANAWAKE 15 NDANI YA MUUNGANO WA JUMUIYA ZA WATU WANAOISHI NA MARADHI YASIOAMBUKIZA WAZUNGUMZA NA WAANDISHI ZANZIBAR.

$
0
0


Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 08/12/2019

Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake 15 ndani ya Muungano wa Jumuiya za Watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza Zanzibar (ZNCDA) Mwanakhamis Mohamed Abdalla ameiyomba Serikali kuzidisha juhudi kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na maradhi yasioambukiza .

Ameyasema hayo huko Ofisini kwake kwa Bitihamrani Zanzibar wakati wa ufunguzi wa kikao cha kikundi hicho kwa waandishi wa habari jinsi ya msimamo baada ya kumaliza mafunzo yao juu ya umuhimu wa kujumuisha elimu,uchunguzi na tiba ya maradhi yasiyoambukiza katika mfumo wa afya .

Alisema hali ya maradhi yasioambukiza Zanzibar inazidi siku hadi siku hii inatokana kuwa wananchi kukosa uwelewa wa jinsi ngani ya kuyaepuka maradhi hayo.

Akiyaelezea maradhi hayo ni maradhi ya moyo,ugonjwa wa kisukari ,saratani pamoja na magonjwa sugu ya mfumo wa kupumua ambayo yanakadiriwa kusababisha vifo vya watu million 35 kila mwaka sawa na asilimia 60 ya vifo vyote ulimwenguni .

Aidha alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya iendelee kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kuepuka maradhi yasioambukiza jambo ambalo linawezekana .

Nae Mjumbe wa Kukindi cha Wanawake hao Nunuu Kheir Saleh alisema kuengezeka kwa maradhi yasioambukiza ni moja kati ya changamoto za kiafya ambayo zinatishia maendeleo ya kiuchumi ,kijamii , maisha na afya ya mamilioni ya watu .

Alifahamisha tafiti zinaonyesha asilimia 80 ya vifo vinavyotokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati husababishwa na maradhi hayo,ambayo yanauwezo wa kuepukika,ikiwemo maradhi ya moyo kiharusi kisukari cha aina ya 2 na saratani yanaweza kuzuilika kwa asilimia 80 iwapo jamii itakuwa tayari kujiepusha na tabia hatarishi ,

“Jamii ijiepusha na matumizi mabaya ya pombe,itumie vyakula vyenye lishe kamili ikiwemo matunda na mboga mboga , kufanye mazoezi kwa wingi waachane na matumizi ya tumbaku, “alisema Nunuu

Alisema kuwa shirika la afya ulimwenguni (WHO) linakadiria kuwa vifo vinavyotokana na maradhi yasioambukiza vitaongezeka kwa asilimia 17 ulimwenguni katika kipindi cha miaka 10 ijayo ikiwa hakuna hatua madhubuti zitakazochukuliwa .

Aidha alisema ongezeko kubwa la maradhi hayo litakuwa katika nchi za Afrika kwa asilimia 27 na Nchi za Mashariki ya Mediterania kwa asilimia 25. Vile vile Benki ya Dunia inatabiri kwamba vifo vitakavyotokana na maradhi yasioambukiza vimeongezeka kutoka asilimia 28 kwa mwaka 2008 hadi asilimia 46 ifikapo mwaka 2030 hali hii inawakilisha tishio kubwa kwa mifumo dhaifu ya afya na inasisitiza hitaji la njia bora za ubunifu katika utoaji wa huduma za afya.
Baadhi ya Waandishi wa Habari na Wageni waalikwa waliohudhuria katika mkutano kuelezea Umuhimu wa kujumuisha Elimu,Uchunguzi na Tiba ya Maradhi yasioambukiza(NCDs)katika mfumo wa Afya hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio kwa bitihamran Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake 15 ndani ya Muungano wa Jumuiya za Watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza Zanzibar(ZNCDA)Mwanakhamisi Mohamed Abdalla akitoa maelezo ya makaribisho katika mkutano na Waandishi wa Habari kuelezea Umuhimu wa kujumuisha Elimu,Uchunguzi na Tiba ya Maradhi yasioambukiza(NCDs)katika mfumo wa Afya hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio kwa bitihamran Zanzibar.
Mjumbe wa kamati ya Maradhi yasioambukuza Nunuu Kheri Saleh akifafanua jambo wakati akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari kuhusiana na Umuhimu wa kujumuisha Elimu,Uchunguzi na Tiba ya Maradhi yasioambukiza(NCDs)katika mfumo wa Afya hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio kwa bitihamran Zanzibar.
Mjumbe wa kamati ya Maradhi yasioambukuza Nunuu Kheri Saleh(wapili kulia ) akisoma maelezo kwa waandishi wa Habari kuhusiana na Umuhimu wa kujumuisha Elimu,Uchunguzi na Tiba ya Maradhi yasioambukiza(NCDs)katika mfumo wa Afya hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio kwa bitihamrani Zanzibar.
 

MBUNIFU WA COSTECH AOKOA WATOTO 400 KWA KIFAA CHA KUONGEZEA JOTO

$
0
0
Mfano wa mtoto akiwa katika kifaa cha kumuongezea mtoto joto baada ya kuzaliwa .MAZAO ya Tume ya sayansi na teknolojia (COSTECH) yaonekana baada ya Mbunifu Daktari Emmanuel Mushi kuokoa watoto 400 ambao wamezaliwa wakiwa wamechoka na watoto njiti kwa kutengeneza mashine ya kuwaongezea joto (Incubator ya kuhifadhi joto la mtoto) katika hospitali ya Mkoa wa Manyara.

Akizungumza na Michuzi Blog, Mbunifu wa kifaa hicho Daktari Emmanuel Mushi amesema kuwa kifaa hicho kwa hapa nchini kinauzwa kwa bei rahisi zaidi ukitofautisha na vifaa ninavyouzwa nje ya nchi ikiwa vifaa hivyo vinafanya kazi ya aina moja.

Hata hivyo Dk. Mushi ameshauri Wizara ya Afya kumtumia kwa ufasaha katika kuzalisha mashine nyingi zaidi na kuzisambaza katika vituo vya afya ambayo hutoa huduma ya mama na mam na mtoto kwaajili ya kuokoa maisha ya watoto wengi zaidi ili kujenga taifa lenye watoto wengi na uchumi imara.

Mashine hizo ambazo zimetengenezwa kwa mfumo wa vifaa vya plastiki na kuunganishwa na umeme endapo joto la kifaa hicho litakuwa limepungua.

Dk. Mushi amesema katika kutengeneza mashine hiyo ya kuwaongezea watoto joto ambayo ameibuni mwenyewe amesema katika kufanikisha hilo ameshasaidia kujengwa kwa kituo cha afya ya mama na mtoto kilichopo katika mkoa wa Manyara ambapo wanawake wengi hufika na kujifungua katika kituo hicho.

Ameelezea kuwa kama mtoto njiti na ambaye amezaliwa akiwa amechoka joto lao hupungua kwa haraka baada ya kuzaliwa na kusababisha damu kuganda na kufariki.

Hivyo katika kupunguza vifo vya watoto njiti amesema kuwa  kifaa cha kutunza joto la mtoto pia ameshakifanyia utafiti na kugundua kifaa hicho kinafanya kazi vizuri alicho kipa jina la embranes womb kipo kwaajili ya kuokoa maisha ya watoto ambao wanasafirishwa kutoka hospitali ya kijiji hadi hospitali ya Mkoa ambacho kinafanya joto la mtoto liweze kuwepo na kufanya damu itembee kwa urahisi mwilini.

Pia Dk. Mushi amewakaribishakatika maoneshoya nne ya viwanda viongozi wa wizara ya afya katika banda la Tume ya Sayansi na Teknolojia waende wajionee vifaa vya kuwaongezea joto watoto. 

"Wizara ya afya ninawakabirisha katika maonesho haya ili mje mjionee mashine pamoja na kifaa cha kumsafirishia mtoto (embranes womb) kutoka vituo vya afya vya vijijini hadi hospitali ya mkoa kwani kimeshaanza kufanya kazi.

Amesema vifaa hivyo vikisambazwa katika vituo vya afya vilivyopo vijijini vitaweza kuokoa maisha ya watoto wengi zaidi. 

"Malengo yangu ni kuokoa mamilioni ya watoto kwa kutengeneza vifaa vya kuwaongezea joto watoto pamoja na vifaa vya kuhifadhi joto kwaajili ya kumsafirishia mtoto kutoka hospitali ya ya vijijini hadi hospitali ya Mkoa".Amesema

Hata hivyo amewaasa serikali kuwekeza katika vifaa hivyo ili waweze kutengeneza vifaa vingi zaidi kwajili ya kuokoa watoto wachanga wanaokosa joto baada ya kuzaliwa.


Mbunifu Daktari Emmanuel Mushi akizungumza na wananchi mbalimbali waliotembelea katika banda la Tume ya Sayansi na Teknolojia kwaajili ya kupata maelezo juu ya uunifu wa kifaa cha kuhifadhi joto la mtoto baada ya kuzaliwa.
Kifaa cha kuhifadhi joto ili kiweze kumfikisha mtoto kutoka hospitali za vijijini hadi hospitali ya Mkoa akiwa na joto linalotakiwa kwa afya ya mtoto.

Mtoto akiwa ndani ya kifaa  cha kuhifadhi joto na kumpeleka hospitali kwaajili ya matibabu zaidi.

Rais Magufuli aweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa meli na chelezo pamoja na ukarabati mkubwa meli 2 Ziwa Victoria

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wakimsikiliza Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria Meja Abel Gwanafyo akitoa maelezo kuhusu miradi hiyo kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa Meli mpya ya M.V Mwanza (Hapa kazi Tu) wakati wakimsikiliza Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria Meja Abel Gwanafyo akitoa maelezo kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia katika Sherehe za Uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job
Ndugai pamoja na viongozi wengine wakivuta kitambaa kuashiria uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria katika sherehe zilizofanyika eneo la
Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwachangia Kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza walipokuwa wakiimba kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza walipokuwa wakiimba kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu),
Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Muonekano wa Chelezo inayojengwa katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job
Ndugai pamoja na viongozi wengine wakiinua mikono juu kwa umoja na furaha mara baada ya uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria katika sherehe zilizofanyika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba
08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkandarasi wa Ujenzi wa Meli mpya ya M.V Mwanza Bw. Dowan Kim kutoka kampuni ya STX Engine mara baada ya sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Desemba, 2019 ameweka jiwe la msingi katika miradi ya ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, Chelezo na ukarabati wa meli za MV Victoria na MV Butiama katika Ziwa Victoria.

Sherehe za uwekaji jiwe la msingi katika miradi hiyo zimefanyika katika Bandari ya Mwanza Kusini Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai, Mawaziri na Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Wabunge, viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa, viongozi wa taasisi mbalimbali, viongozi wa Dini na viongozi wa vyama vya siasa.

Ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu utakamilika Januari 2021 kwa gharama ya shilingi Bilioni 89.764 ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 43.74 na unatekelezwa na kampuni za ukandarasi za Gas Entec Company Limitedna Kangnam Corporation za Jamhuri ya Korea kwa kushirikiana na Suma JKT. Kampuni hizi zimeshalipwa shilingi Bilioni 39.249.

MV MwanzaHapa Kazi Tu itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari makubwa 3 na magari madogo 20, inatarajiwa kufanya kazi kati ya bandari za Mwanza, Kemondo, Bukoba na Musoma pamoja na kwenda nchi jirani za Kenya na Uganda na hivyo kukabiliana na adha ya usafiri kwa wananchi na mizigo katika Kanda ya Ziwa baada ya MV Bukoba kupata ajali ya kuzama majini mwaka 1996 na meli nyingine 4 kuharibika.

Ujenzi wa chelezo unafanywa na kampuni za STX Engine Company Ltd na Saekyung Construction Company Ltd, zote za Jamhuri ya Korea kwa gharama ya shilingi Bilioni 36.4 ambapo mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 68 na wakandarasi hao wameshalipwa shilingi Bilioni 32.85 sawa na asilimia 90 ya fedha zote.

Ukarabati mkubwa wa meli za MV Victoria na MV Butiama unafanywa na kampuni za KTMI Co. Ltdya Jamhuri ya Korea na kampuni ya Yuko’s Enterprises (EA) Co. Ltd ya Tanzania kwa gharama ya shilingi Bilioni 27.71 ambapo mpaka sasa shilingi Bilioni 11.57 zimeshalipwa na kazi imefikia asilimia 65 na 60 mtawalia. 

MV Victoria ina uwezo wa kuchukua abiria 1,200 na mizigo tani 200 wakati MV Butiama ina uwezo wa kuchukua abiria 200 na mizigo tani 100. Meli hizi zitakuwa zinafanya safari kati ya Bandari za Mwanza, Kemondo, Musoma, Bukoba na Nansio-Ukerewe. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Bw. Eric Benedict Hamissi amesema ujenzi wa chelezo na ukarabati wa meli hizo ambao unafanywa kwa kiwango cha kuzirudisha kuwa meli mpya kabisa unatarajiwa kukamilika Machi 2020.

Bw. Hamissi amempongeza na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa Serikali kufanya uwekezaji mkubwa wa mara moja ambao haujawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru, ambapo katika kipindi kifupi cha miaka minne imewekeza shilingi Bilioni 152 katika usafiri kwa njia ya maji, na ameahidi kuwa MSCL itafanya kazi kwa juhudi na maarifa kuhakikisha uchukuzi kwa njia ya maji unaboreshwa ukiwemo mpango mkakati wake wa kuanzisha huduma za usafirishaji mizigo katika Bahari ya Hindi kati ya Dar es Salaam, Comoro, Madagascar, Shelisheli na maeneo mengine.

Mhe. Rais Magufuli amempongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa MSCL Bw. Hamissi kwa mageuzi makubwa anayoyasimamia ambayo yameonesha mwelekeo mzuri wa kampuni hiyo ya Serikali ambayo kwa kipindi kifupi imefufua meli nne kati ya 14 zilizoachwa na Hayati Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na amewapongeza wananchi wa Kanda ya Ziwa kwa kupata matumaini mapya ya kurejeshewa huduma za uhakika za usafiri kama alivyowaahidi wakati akiomba kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Amewapongeza Watanzania wote kwa kuchapa kazi na kulipa kodi zinazotumika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, na amesisitiza kuwa kutekelezwa kwa miradi hiyo ni uthibitisho kuwa Watanzania wanaweza hata bila kukopa au kupata ufadhili unaokuja na masharti magumu.

Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa kwa kutumia fedha za Watanzania wenyewe ikiwemo mpango wa karibuni wa kujenga reli ya Mwanza – Isaka kwa kiwango cha kisasa (standard gauge), kukarabati meli nyingine 5 na ameahidi kuwa Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kununua meli mpya itakayofanyakazi katika Bahari ya Hindi kuanzia bajeti ijayo.

Amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Aloyce Kamwelwe kwa kazi nzuri zinazofanywa na wizara hiyo zikiwemo ujenzi wa meli 3 katika Ziwa Nyasa, ukarabati wa MV Liemba utakaofanyika hizi karibuni, uanzishaji wa Wakala wa Huduma za Bandari (TASAC) na upanuzi wa Bandari za Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Kemondo, Bukoba na Nyamilembe.

Kesho tarehe 09 Desemba, 2019 Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara yatakayofanyika kwa mara ya kwanza katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Mwanza
08 Desemba, 2019

ARUSHA KWA SASA PARACHICHI HALIHARIBIKI HOVYO-MBUNIFU JESSE OLJANGE

$
0
0
 Baadhi ya bidhaa za mafuta ya Parachichi yaliyozalishwa kwaajili ya matumizi ya kawaida ya Avomeru yanayotengenezwa na Jesse Oljange.
Mwanzilishi wa wa Kampuni ya Avomeru Group LTD, Jesse Oljange akizungumza na Michuzi Blog katika maonesho ya nne ya bidhaa za viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya JK. Nyere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

TATIZO la tunda la parachichi kuharibika limepungua kwa wakazi wa Arusha kwani mbunifu Jesse Oljange ameweza kubuni Mashine ya kutengeneza mafuta ya parachichi na kupelekea thamani parachichi kuongezeka.

Akizungumza na michuzi blog, Jesse Oljange amesema kuwa katika kuhakikisha matunda aina ya parachichi hayapotei bure ameweza kununua matunda hayo kwa wingi kwaajili ya kutengeneza mafuta. 

"Kwa sasa tunda aina ya parachichi haliharibiki hovyo, wala halidharauliwi kama zamani saivi parachichi ni tunda mhimu, na maisha yake yameongezeka kutoka siku tatu hadi kufikia miezi tisa hadi miezi 12". Amesema  Oljange.

Oljange amesema ameweza kushirkiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii alivyoweza kutumia ubunifu wake na kuweza kutengeneza Mafuta ya parachichi halisi (Avomero oil).

Amesema parachichi zilikuwa zinaharibika ila kwa sasa wananchi wamepata soko la kuuzia parachichi hizo na kujipatia kipato.

"Wale wakulima wadogo walikua wanauza debe la parachichi ambalo ni sawa na parachichi 70  kwa shilingi elfu mbili sasa wananchi hao wanauza  parachichi 42 kwa shilingi elfu nane". 

Jesse amesema kuwa mpaka sasa parachichi katika eneo hilo ambapo ameweka kiwanda kidogo limekuwa na thamani kubwa kuliko ilivyokuwa mwanzo.

Hata hivyo Jesse amesema kiwango kikubwa ameweza kusaidia jamii kupinguza uzito wa kusafirisha parachichi na kuweza kusafirisha mafuta ambayo yanatumika kwa matumizi mengi.

Hata hivyo amewashukuru Tume ya Sayansi na Teknolojia kwa kuwawezesha na kupokea wazo lao kwani mpaka sasa mafuta ya Avomeru yanauzwa hadi nje ya nchi.

Hata hivyo Oljange amewakaribisha wananchi katika viwanja vya sabasaba kwaajili ya kuwaunga mkono pamoja na kwenda kuona ubunifu walioufanya katika kulipathamani Parachichi.

MAHAFALI YA CHUO CHA AFYA MUHIMBILI MUHAS YAFANA JIJINI DAR

$
0
0

Makamu Mkuu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Prof. Andrea Pembe akitoa Hotuba yake katikaMahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili. (MUHAS) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, akimtunuku Deus Charles Buma Digrii ya Udaktari wa Falsafa Doctor Of Philosophy (PhD) katika Mahafali ya Kumi na Tatu ya chuo hicho yaliyofanyika Muhimbili jijini Dar es salaam Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Andrea Pembe na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili,  Mariam Mwaffisi

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Jumla ya wahitimu  924  wamemaliza masomo yao katika  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Mahafali ya 13 ya MUHAS yamefanyikwa kwa kuhudhuriwa na Mkuu wa Chuo Rais wa Awamu ya Pili Mstaafu Alhaj Alli Hassan Mwinyi na kwuatunukiwa wahitimu waliomaliza masomo yao mwaka 2019.

Katika wahitimu hao, wanne wamefanikwia kuhitimu Digrii ya yzamivu wa Udaktari wa Falsafa  'Doctor of  Phylosophy'  PHD , na wahitimu 284 wakitunukiwa Digrii ya uzamili (masters) katika fani mbalimbali.

Wahitimu 450 walitunukiwa digrii katika fani mbaimbali na  wahitimu 190 wakimaliza masomo yao ngazi ya Diploma.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili ,Ali Hassan Mwinyi akimtunuku Shahada ya Uzamivu wa Udaktari wa Falsafa ya Chuo hicho mmoja wa Wahitimu chuoni hapo.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Mariam Joy Mwaffisi akitoa Hotuba yake katika Mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili. (MUHAS)
Mwakilishi wa Wahitimu wa Shahada ya Uzamili na Uzamivu wa Chuo hicho, Roselyne Okello akitoa Hotuba kwa niaba ya wenzake katika Mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili. (MUHAS)
Baadhi ya Wahitimu wakiwa katika Mahafali hayo ya 13 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
Baadhi ya wahitimu wa chuo hicho wakila kiapo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Andrea Pembe akiongozana na Maprofesa na Wahadhiri wa Chuo hicho katika maandamano kuelekea katika Mahafali ya Kumi na Tatu ya Chuo Kikuu kishiriki cha Afya na Sayansi MUHAS yaliyofanyika  jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, akiwa meza kuu pamoja na viongozi na wahadhiri mbalimbali wakati wa mahafali hayo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ali Hapi ni mmoja wa viongozi waliohudhuria katika mahafali ya Kumi na Tatu ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi MUHAS Muhimbili jijini Dar es salaam.

UNYANYASAJI WA KIJINSIA MKOA WA ARUSHA WAONGEZEKA KUTOKA 2456 -4334

$
0
0


Mkuu wa Kitengo cha polisi jamii mkoa wa Arusha SSP Joswam Kaijanante


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Matukio ya unyanyasaji wa Kijinsia mkoani Arusha yameendelea kuongezeka kutoka matukio 2456 ya mwaka 2018 hadi kufikia 4334 mwaka 2019 licha ya elimu mbalimbali kuendelea na wadau kutolewa kukabiliana na matukio hayo.

Mrakibu Mwandamizi wa polisi SSP Joswam Kaijanante ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha polisi jamii mkoa wa Arusha alisema jumla ya matukio 4334 yametokea mkoani hapo kwa upande wa kina mama,watoto ,wakiwemo wanaume pia katika kipindi cha mwaka 2019.

Alisema kuwa licha ya matukio hayo kuongezeka makosa yanahusiana na unyanyasaji wa kijinsia ni pamoja na ulawiti na kubaka yamepungua ambapo kubaka ni makosa 161 yaliyoripotiwa januari -septemba 2018,ambapo januari -septemba 2019 yalikuwa makosa 82,tofauti ni 79.

Alisema, makosa ya ulawiti yaliyoripotiwa Januari-septemba mwaka 2018 makosa 61 huku mwaka 2019 yaliripotiwa makosa 52 tofauti ni 9.

Alisema makosa ya kutoa mimba yameongezeka ambapo mwaka 2018 yaliripotiwa makosa 31 ambapo mwaka 2019 yaliripotiwa makosa 49 tofauti ni 18

Makosa ya kumpa mimba mwanafunzi nayo yameongezeka ambapo yaliyoripotiwa kuanzia januari -septemba 2018 yalikuwa jumla ya makosa 169, ambapo januari -septemba 2019 yaliripotiwa makosa 177 tofauti ni makosa 8.

Pia makosa ya Kumtorosha mwanafuzi yameongezeka na kwamba yaliripotiwa mwaka 2018 jumla ya makosa 30 ambapo mwaka 2019 jumla ya makosa 32 yameripotiwa na kufanya ongezeko la makosa 2.

Alisema, pia kuna makosa ya kushindwa kumuhudumia mwanafunzi ambapo mwaka 2018 yaliripotiwa makosa 889 ambapo mwaka 2019 yamepungua na kuwa makosa 32 pungufu ya makosa 857.

utumia lugha ya matusi januari-septemba 2018 jumla ya makosa 178 ambapo januari-septemba 2019 jumla ya makosa 922 tofauti 746

Kutishia kuua januari -septemba 2018 jumla ya makosa 110 yaliripotiwa ambapo januari-septemba 2019 yaliripotiwa jula ya makosa 840 tofauti ni makosa 730,kujaribu kubaka januari -septemba 2018 jumla ya makosa 104 yaliripotiwa ambapio januari -septemba 2019 jumla ya makosa 43 tofauti ni makosa 61.

Kujeruhi januari -septemba 2018 jumla ya makosa 231 ambapo januari -septemba 2019 yaliripotiwa makosa 765 tofauti ni makosa 534.Shambulio januari-septemba 2018 jumla ya makosa 349 yaliripotiwa ambapo januari -septemba 2019 1191 tofauti 842.

Kufanya mapenzi na mwanafunzi januari -septemba 2018 jumla ya makosa 1 ambapo januari -septemba 2019 jumla ya makosa 0 tofauti yake ni 12

Kumtorosha mwanafunzi januari -septemba 2018 jumla ya makosa 34 yaliripotiwa ambapo januari -septemba 2019 yaliripotiwa jumla ya makosa 10 tofauti 24,kujaribu kujiua januari -septemba 2018 jumla ya makosa 45 yaliripotiwa ambapo januari -septemba 2019 jumla ya makosa 16 tofauti ni makosa 29.

Wizi wa watoto januari-septemba 2018 jumla ya makosa 5 yaliripotiwa ambapo Januari -septemba 2019 jumla ya makosa 3 tofauti ni 2.

Kutelekeza familia januari -septemba 2018 jumla ya makosa 51 ambapo januari -septemba 2019 jumla ya makosa 102 tofauti ni makosa 51.

Kujinyonga januari -septemba 2018 juimla ya makosa 5 yaliripotiwa ambapo januari -septemba 2019 jumla ya makosa 13 yaliripotiwa tofauti ni makosa 8,Kukeketa januari -septemba 2018 jumla ya makosa 2 yaliripotiwa ambapo januari -septemba 2019 jumla ya makosa 0 tofauti ni 2.

Kutupa watoto januari -septemba 2018 jumla ya makosa 1 liiripotiwa ambapo januari -septemba 2019 jumla ya makosa 5 tofauti ni makosa 5,ambapo inaleta idadi ya makosa 2456 kwa mwaka 2018 ambapo mwaka 2019 jumla ya makosa 4334 tofauti 1878.

SSP Joswam Kaijanante alisema kuwa pia wanataarifa ya baadhi ya wazazi ambao wamebuni mbinu ya kuwakeketa watoto wachanga ambapo bado wanaendelea na uchunguzi atakayebainika sheria itachukua mkondo wake

Amesema wanaendelea kuielimisha jamii kwani jambo hilo la kukeketa watoto linafanyika kwa usiri mkubwa mtoto akiwa bado mchanga ni vigumu sana kubaini suala hilo

Amesema dawati ngazi ya mkoa linashirikiana na Ustawi wa jamii kwenye Halmashauri kwasababu wao wana watu hadi kwenye ngazi ya kata sambamba na mashirika yasiyo ya Kiserikali ambayo yanashughukika na kupinga ukatili dhidi ya vitendo vya unyanyasaji haswa wakina mama na watoto.

Amesema changamoto kubwa iliyopo kwenye unyanyasaji watu wengi wanaofikiria kwa mwanamke na mtoto tu ila wanaume

"Wanaume wananyanyaswa ila wanakuwa waoga kusema wanaona aibu kwamba jamii inayowazunguka itawachukuliaje"alisema Kaijanante

Alisema kuwa wanaendelea kuielimisha jamii ili kama wanaume wananyanyaswa watoe taarifa ,wanaume wengi wanaumia sana na wananyanyaswa,ila kwa sasa mwamko mkubwa upo kwani baadhi ya wanaume wanaripoti matukio ya kunyanyaswa ila tunawahakikishia kuwa tunayashughukikia kwa kiasi kikubwa sana.


Aidha wanaume wameaswa kujitokeza kutoa taarifa pale wanapofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia kwani dawati hilo ngazi ya mkoa wanafanya mazungumzo kwa njia ya usiri mkubwa ambao utawafanya wanaume hao kuwa salama

Kwa upande wake Insp.Lucia Mpakaseke alitaja baadhi ya unyanyasaji wa Kisaikolojia kuwa ni pamoja na matendo yanayosababisha maumivu ya kihisia ,kiakili,au kutishia kufanya fujo ,maneno ya fedheha,dharau na kutishia kutoa siri hadharani.

Alisema kuwa zipo baadhi ya ndoa nyingine ambazo kuna siri wanazifahamu wenyewe ,ila inapofikia mahali wakatofautiana mmoja wapo anatishia kuitoa siri hiyo hadharani ambapo kisaikolojia/kiakili humuathiri mmojawapo.

Matendo mengine ni pamoja na kunyang'anywa watoto,kutishiwa kuuwawa pale ambapo linatokea tatizo badala ya kusuluhisha wanatishiana,wivu wa kupindukia,ukatili wa kingono,ndoa za utotoni,usafirishaji wa mabinti kwaajili biashara za ngono,kulazimishwa kufanya biashara za ukahaba.

Aidha amesema Ukatili mwingine ni wa mila na desturi mfano ukeketaji,kuchumbia watoto wakiwa wadogo kwa baadhi ya makabila kwa kuchukua mahari,mauaji ya vikongwe,walemavu wa ngozi,matambiko ya kingono kwa watoto.

Ukatili wa kiuchumi ambao unamnyima fursa za kimaendeleo mtoto wa kike kushiriki katika maendeleo,kukatazwa kufanya kazi,unyanyasaji wawasichana au wasaidizi wa kazi majumbani,walemavu,waathirika wa VVU na Ukimwi.

Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani katika maadhimisho ya siku 16 ya kupinga Ukatili wa kijinsia ambapo yalizinduliwa rasmi mkoani Dodoma ma Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na watoto nchini Ummy Mwalimu ambapo kilele chake kitakuwa Desemba 10,2019 ambapo Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ni Kizazi chenye Usawa:Simama dhidi ya Ubakaji.


Ambapo lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuongeza ushawishi kubadilishana taarifa,uzowefu wa kujenga uwezo wa pamoja,kuelimisha,kukemea,kuchukua hatua kwa pamoja ili kupinga ukatili wa kijinsia.

BRELA WAPONGEZWA KWA KUFANYA USAJILI WA JINA LA BIASHARA KWA DAKIKA TANO

$
0
0
Naibu Waziriwa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mteja wa BRELA Cheti cha Usajili wa jina la Biashara yake alilosajili na kukamilika ndani ya dakika 5 kwenye Maonesho ya bidhaa za Viwanda (Sabasaba).
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya (wapili kutoka kulia )akikiangalia cheti cha Mteja wa BRELA cha Usajiliwa jina la Biashara yake alilosajili na kukamilika ndani ya Dakika 5 kwenye Maonesho ya nne ya bidhaaza Viwanda. 

 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Loy Mhando akimuelezea Naibu Waziri wa Viwanda Na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya majukumu mbalimbali ambayo Wakala inayafanya ya kiwemo Usajili wa Makampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma Hataza pamoja na Leseni za Viwanda.
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Loy Mhando (wapili kutoka kutoka kulia) akifurahi pamoja na Mtejawa BRELA aliyepata cheti ndani ya dakika tano.
Wafanyakazi wa BRELA wakiwa kwenye banda la Maonesho ya Bidhaa za Viwanda katika uwanja wa Mwl. J.K Nyerere ( Sabasaba).

kutoka kushoto ni  AfisaTehama,Hilary Mwenda, Afisa Leseni  Yusuph Nakapala  Afisa Habari na Mawasiliano, Robertha Makinda, Msaidizi wa Usajili Mkuu Hellen Mhina na Afisa Mwandamizi Msaidizi wa Usajili, Ruth Mmbaga.

Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wanawakaribisha katika maonesho ya nne (4) ya bidhaa za Viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salama ambayo ya tahitimishwa Desemba 9, 2019.

SOMO LA UJASILIAMALI SASA KUMFIKIA KILA MWANANCHI, UDSM KUWA KITOVU

$
0
0








KUTOKANA na somo la Ujasiliamali kuwa na umhimu katika kuzalisha wataalamu mbalimbali chuo kikuu cha Dar es Salaam kunafundisha somo la ujasiliamali kwa kila mwanafunzi na mwananchi anayetaka kusoma kozi hiyo.

Hayo ameyasema Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uvumbuzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk.Ameria Buriyo wakati akizungumza na michuzi blog katika maonesho ya nne ya bidhaa za viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa chuo kimeweka utaratiu mzuri kikishirikiana na shule ya biashara ya chuo kikuu cha Dar es Salaam, kwaajili ya kuhakikisha kwamba kila mwananfunzi katika chuo hicho anapata mafunzo ya ujasiliamali.

"Kwahiyo zimeshatengenezwa kozi za mwaka wakwanza kwa wanafunzi wote wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, kwa mwaka wa tatu, kwa mwaka wa nne, kwa mwaka wa tano ikiwa na maana kwamba wale wa mwaka wa mwisho". Amesema Hata hivyo Dk.Ameria

  Dk.Ameria  amesema kuwa  kwa sasawameanza kutengeneza kozi kwaajili ya wanafunzi wa shahada za juu kwa kila mwanafunzi anayepita katika chuo kikuu cha Dar es Salaam aweze kusoma Ujasiliamali.

Hata hivyo Dk.Ameria ametoa wito kwa watu wote waliopo mitaani kuwa wameanzisha programu maalumu  ya ubunifu na ujasiliamali ambayo itakuwa ikiendeshwa kila mwaka ifikapo Agosti na Septemba maalumu kwaajili ya wanaomaliza masomo yao katika vyuo vikuu vyote.

Amesema kuwa kwa mwaka huu wameshawafikia wananchi zaidi ya 2,000 katika mikoa nane ya Tannzania bara na mikoa 2 ya Zanzibar ambapo waliweza kuwafundisha somo la ubunifu na ujasiliamali.

Kwa upande wake Hezekiah Sawa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaa, amesema kuwa somo la ujasiliamli limemwezesha katika kutengeneza jiko linalotumia mionzi ya jua kupika chakula (Solar Cooker).

Amesema kuwa jiko hilo linasaidia katika utunzaji wa mazingira, utunzaji hewa pamoja na afya ya kila mtumiaji kwani halitoi moshi wa kuathiri mazingira.

Nae Mwanzilishi wa wa kifaa cha kutunzia kumbukumbu za mauzo na manunuzi(Smart Stock), Joshua Mshana na Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, amesema kuwa kifaa hicho kinamanufaa makubwa kwa mfanyabiashara mdogo na mkubwa kwaajili ya kutunza kumbukumbu za bidhaa anazouza au kununua kwa miaka mingi zaidi kuliko kuiandika kwenye daftari zinazo lowa na kuchakaa au kuungua.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uvumbuzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk.Ameria Buriyo akizungumza na michuzi Blog jijini Dar es Salaam leo katika maonesho ya nne ya bidhaa za viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K. Nyerere maarufu kama sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Mbunifu kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Joshua Mshana akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika katika maonesho ya nne ya bidhaa za viwana yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam. Joshua anaelezea kuhusiana na kifaa kinachoweza kumwezesha mfanyabiashara mdogo na wakati kuhifadhi taarifa za mauzo na manu nunuzi ya bidhaa katika biashara yake kifaa hicho chenye jina la SMART STOCK.

 Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza na mmoja ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam leo mara baada ya kutemelea banda la chuo hicho leo katika maonesho ya nne ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
 
 Wananchi wakipata maelezo ya bidhaa malimbali zinazopatikana katika banda la chuo kikuu cha Dar es Salaam. 
 Mwananchi akipewa maelekezo ya jiko linalotumia mionzi ya jua kupikia chakula. Katika Maelezo ya Jiko hilo linaweza kupika chakula chochote ila kwa kutegemea hali ya jua la siku hiyo.

Hata hivyo jiko hilo linatakiwa liwe juani ndipo lipike chakula kinachohitajika kwa siku hiyo.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO DESEMBA 9,2019

NGOMA AFRICA BAND INAWATAKIA HERI YA MIAKA 58 YA UHURU WA TANZANIA BARA

$
0
0
 Bendi maarufu ya muziki wa dansi Ngoma Africa Band almaarufu FFU-Ughaibuni yenye makao nchini Ujerumani,inawatakia kila la heri katika kusherehekea miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania bara . Salam hizi za heri ya 9 Disemba ziwafikie watanzania wote walio nyumbani na nje ya nchi.Ngoma Africa band chini ya uongozi wake Kamanda ras Makunja unaweza kuwasikiliza pia katika kambi yao ya FFU-ughaibuni bofya http://www.ffacebook.com/ngomaafricaband
 

maafisa kilimo na viongozi wa amcos wapewa mafunzo Inbox x

$
0
0
Viongozi wa vyama tisa(9) vya Ushirika vya Msingi vya mazao (AMCOS ) katika Wilaya ya Nyasa na Mbinga wamepatiwa mafunzo ya kukuza njia asilia za kilimo ili kuwa saidia wakulima kuongeza ubora na kuhakikisha kunakuwa na kuhakikisha kunakuwa na kahawa bora kwa sasa na kwa baadaye kwa mtumiaji yeyote.

Mafunzo hayo yamefanyika leo katika Ukumbi wa WALIOCHONACHO NA WASIOKUWANACHO uliopo Mtaa wa Ruhuwiko Mjini Mbinga yaliyotolewa na Kampuni ya Kahawa ya Starbucks yenye makao yake makuu jijini Mbeya na lengo lamafunzo hayo ni kukuza njia asilia za kilimo cha kahawa, ili kuwasaidia wakulima kuboresha zao la kahawa, na kuongeza ubora na kuhakisha kunakuwa na kahawa bora kwa sasa na kwa baadaye

akifungua mafunzo hayo,Mkuu wa Idara ya kilimo,Umwagiliaji na Ushirika Bw.Menance Ndomba alisema Halmashauri ya Wilaya ya Nyasaitawachukulia hatua kali maafisa kilimo wote ambao hawatawasaidia wakulima kuongeza ubora wa kahawa ili kuwapa maendeleo wananchi.

Bw. Ndomba amefafanua kuwa atahakikisha Maafisa kilimo wote Wilayani Nyasa, ambao watashindwa kuwapa elimu wakulima ili wazalishe kahawa yenye ubora atahakikisha anawachukulia hatua za kinidhamu pamoja na kuwafukuza kazi.

Aliongeza kuwa kahawa ni zao la kimkakati ambalo Serikali imelipa kipaumbele hivyo maafisa kilimo wanatakiwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kuwapa elimu wakulima na kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili ili kuzalisha kahawa yenye ubora na nyingi na kupelekea wananchi wanapata maendeleo.

“Maafisa kilimo wa Wilaya ya Nyasa nitawapima kwa kuangalia wananchi wamepata ubora gani wa kahawa. Afisa kilimo mmeajiriwa kwa kazi ya kuhakikisha wananchi/wakulima wanakuwa na maendeleo kwa kuzalisha mazao yenye ubora na yakutosha.Tunapozungumzia maendeleo ni pamoja na kuhakikisha Wakulima wanakuwa na elimu ndelevu ya mazao mbalimbali hasa mazao ya kimkakati. Nichukue fursa hii kuwaambia Nyasa hatumtaki Afisa kilimo asiyetoa elimu kwa wakulima wake ili waweze kuzalisha mazao bora.

Aidha bw.Ndomba ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuimarisha na kusimamia mfumo wa Vyama vya Msingi vya Ushirika vya Mazao (AMCOS) kwa kuwa wakulima wameweza kuuza kahawa zao kwa pamoja kwa bei mzuri, kuweza kufanya manunuzi ya Pembejeo kwa pamoja (Bulk purchase) hususani mbolea ambapo AMCOS zilizopo Nyasa tayari zimeshanunua mbolea na kusambaza kwa wanachama wake.

Naye Meneja wa Kampuni ya Stabucks Farmers Center amesema kahawa inayotoka Wilaya ya Mbinga na Nyasa ni nzuri na inapendwa katika soko la Dunia kwa kuwa ni ya asili, hivyo tunatakiwa kuongeza ubora wa kahawa yetu na kuulinda ili bei iwe nzuri, mkulima anufaike zaidi kwa kuuza bei ya juu kwa kuwa ubora wa kahawa unaongeza Bei katika soko la Dunia.

Aliwapongeza wakulima hao kwa kazi nzuri ya kuzalisha kahawa nzuri, na kuwataka kuongeza uzalishaji wa kahawa inayolimwa katika Wilaya ya Nyasa na Mbinga.

Mafunzo haya ni ya siku moja yaliyowakutanisha Viongozi wa vyama vya msingi vya wakulima wa kahawa,vya Tingi,Upolo,Luhangarasi,Kingerikiti,Nambawala,Mapendo na Lipo kwa Wilaya ya Nyasa na Ngaka na Mahenge kwa Wilaya ya Mbinga, Maafisa kilimo na wadau wa zao la kahawa.

NMB ILIVYOSHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA UHURU JIJINI MWANZA

$
0
0



Hivi ndivyo benki ya NMB ilivyoshiriki Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa miaka 58 yanayoendelea leo katika uwanja  wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.



Taliss-IST yatwaa ubingwa wa U-12 kuogelea Taifa

$
0
0

 Waogeleaji chipukizi wakichumpa wakati wa mashindano yaliyofanyika kwenye bwawa la kisasa la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST)- Masaki.
Waogeleaji chipukizi wakiwa katika pozi baada ya kuzawadiwa medali zao kwa kushinda ‘relay’
Mama na Mwana! Meneja wa timu ya Taliss-IST, Hadija Shebe akisheherekea na mwanaye, Nawal Shebe wakati wa mashindano ya kuogelea ya yoso chini ya miaka 12.
Waogeleaji chipukizi wakiwa katikan pozi baada ya kuzwadiwa medali zao.
……………
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Klabu ya kuogelea ya Taliss-IST imefanikiwa kutwaa ubingwa wa taifa kwa waogeleaji wenye umri chini ya miaka 12.
klabu hiyo imezipiku klabu tisa baada ya kupata  jumla ya pointi 1,736 katika mashindano yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la kisasa la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST)- Masaki.
Waogeleaji wavulana wa klabu hiyo wamechangia pointi nyingi kwa timu yao baada ya kukusanya 948 huku upande wa wanawake  wakipata pointi 788.
Meneja wa Taliss-IST, Hadija Shebe  aliwapongeza wachezaji wake kwa kuendeleza ushindi katika mchezo huo na kuiletea sifa klabu yao.
“Siri kubwa ya  ushindi kwa klabu yetu ni ushirikiano baina ya wazazi, makocha na moyo wa kujituma kwa waogeleaji, nawapongeza wachezaji kwa kufanya vyema,” alisema Hadija.
Klabu inayokuja kwa kasi ya Bluefins imemaliza nafasi ya pili kwa kukusanya pointi 1,521 ambapo kwa upande wa wanawake, klabu hiyo imekuwa ya kwanza kwa kupata pointi 798 na pointi 723 zilikusanywa na waogeleaji wanaume.
Nafasi ya tatu imechukuliwa na klabu ya Dar Swim Club (DSC) kwa kupata pointi 779 ambapo kwa upande wa wanawake  klabu hiyo ilikusanya pointi 385 na wanaume walikusanya pointi 394.
Klabu mpya kabisa katika mchezo huo, FK Blue Marlins imeshika nafasi ya nne kwa kupata pointi 778 ambapo kwa upande wa wanawake, klabu hiyo ilipata jumla ya pointi 597 na wanaume pointi 181.
 Nafasi ya tano ilichukuliwa na klabu ya Uwcea ya Moshi kwa kupata pointi  294 huku Champion Rise ikishika nafasi ya sita kwa pointi 220, Mis Pirahnas ya Morogoro (150 pointi, nafasi ya saba), Wahoo Zanzibar (106 pointi, nafasi ya nane), Mwanza (98 pointi, nafasi ya tisa na nafasi ya 10 ilishikwa na klabu ya Arusha iliyopata pointi tano.
Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya waogeleaji zaidi ya 150 ambao walishindana katika staili mbalimbali ambazo ni freestyle, butterfly, backstroke, Breaststroke na Individual Medley (IM).
Waogeleaji hao pia walishinda katika ‘relay’ ambayo ilikuwa ya kusisimua na ushidano mkubwa.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images