Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

BABU SEA, PAPII KOCHA MARIOO WANOGESHA KASIBANTE FESTIVAL

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Jana Usiku Desemba 07 imeandikwa tena Historia kwa wapenzi wa Burudani ndani ya Manispaa ya Bukoba na Viunga vyake, katika Tamasha kubwa linaloandaliwa na Kituo cha Redio Kasibante Fm, kilichopo Mkoani Kagera, ambalo hufanyika Desemba kila Mwaka, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kuanzishwa kwa kituo hicho.

Burudani hiyo ya kiwango cha aina yake imefanyika ndani ya Kumbi za Lina's Night Club kwa kuwakutanisha mamia ya wapenzi wa Burudani hususani wasikilizaji wa kituo hicho pendwa, pamoja na wasanii nguli wa muziki wa Dansi na Bongo Fravoul.

Burudani ilianza majira ya saa tatu usiku kwa kutanguliwa na wasanii wa nyumbani (wenyeji) akiwemo msanii anaefanya vizuri katika kiwanda cha Bongo fravoul HarmyD planet, na kisha baadae kutoka Jijini Dar es salaam orodha ilifunguliwa na Baddest 47 mzee wa nikagongee.

Katika kuhakikisha kila aliyefika ukumbini pale anapata burudani aliyostahili, Mzee wa Kitambaa cheupe King Kikii alionesha umahiri wake na kudhihirisha kuwa Ng'ombe hazeeki maini pale alipowakumbusha wapenzi wake Kitambaa cheupe.

Shangwe zilidishwa na kunogeshwa zaidi na Baba na mwana Nguza Viking na Papii Kocha, walioonekana kuuteka usiku wa burudani kwa kuwanyanyua mamia ya wakazi wa Kagera kwenye viti vyao na kuimba nao nyimbo zao zilizowahi kutamba Salima, Fanta, Sea na nyingine. 

Mwisho Marioo kutoka sekta ya  Bongo fravoul akafunga kazi kwa kubembelezana na wadau wake kupitia ngoma zake kalii ikiwa ni hitimisho la burudani hiyo ya kumbukizi ya kuanzishwa kwa matangazo ya kituo hicho cha Redio mnamo Tarehe 07, Desemba 2008 ikiwa imetimiza miaka 11 sasa mlangoni kwako.


Pichani ni Papii Kocha mtoto wa Mfalme akizidi kuwateka mashabiki waliofurika katika usiku wa Kasibante Festival 2019 katika viwanja vya Lina's kwa burudani muruwaa.

Pichani Ni mzee wa Kitambaa Cheupe Nguza Viking akichungulisha mashabiki kwa staili yake ya "Chunguliaaa"

Pichani Marioo akiendelea kusuuza nafsi za mashabiki kwa kukonga nyoyo zao na ngoma zake kalii ikiwemo "INATOSHA"

Pichani ni mashabiki wakiendelea kuchukua kumbukumbu katika simu zao pamoja na Msanii Baddest 47 baada ya kugongewa Banana
Mashabiki wakiendelea kuserebuka ukumbini humo

Mmoja wa wapenzi wa Muziki akimtunza Mkongwe wa Muziki Mzee Nguza kwa namna anavyomudu kulicharaza gitaa na kuimba kwa wakati mmoja.
Mzee Nguza pamoja na kubarikiwa sauti ya kuimba pia ni hodari wa Gitaa, kama anayoonekana akicharaza gitaa la solo akimpa tafu mwanae kwenye ngoma ya Sea


Pichani wanaoneka vibonge Staff wa Kasibante FM wakiongozwa na Madame Abella Mkurugenzi Mtendaji wa Kasibante FM wakiangusha moja moja jukwaani pale Fanta ya Papii Kocha ilipokuwa ikirindima.
Burudani ikiendelea kutolewa ukumbini humo
Wapenzi wa Muziki wa Dansi wakiendelea kujimwaya mwaya ukumbini

.

Equinor yafanya mahafali ya tano kwa wanafunzi iliyowafadhili

$
0
0
Mgeni rasmi Balozi wa Norway nchini Tanzania , Elisabeth Jacobsen akizungumza na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kwenye sherehe za mahafali ya tano kwa wahitimu 14 waliofadhiliwa kusoma na kampuni ya Equinor Tanzania kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili katika masomo ya Petroleum Geosciences, Petroleum Engineering na Project Management UDSM. Wengine ni Prof. Ulingeta Mbamba wa UDBS, Meneja Mkazi wa Equinor Tanzania, Dkt. Mette Halvorsen Ottøy, Prof. Egil Tjland wa NTNU, Prof. Prof. Jon Kleppe wa NTNU na Mwakilishi wa bodi ya Norad, Erik Holtar 
Meneja Mkazi wa Equinor Tanzania, Dkt. Mette Halvorsen Ottøy akizungumza na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kwenye sherehe za mahafali ya tano kwa wahitimu 14 waliofadhiliwa kusoma na kampuni ya Equinor Tanzania kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili katika masomo ya Petroleum Geosciences, Petroleum Engineering na Project Management UDSM 
Prof. Ulingeta Mbamba wa UDBS akizungumza na wageni waalikwa 
Mwakilishi wa bodi ya Norad, Erik Holtar akipokea picha ya zawadi kwenye mahafali hayo 
Wahitimu wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi Balozi wa Norway nchini Tanzania , Elisabeth Jacobsen, Prof. Ulingeta Mbamba wa UDBS, Meneja Mkazi wa Equinor Tanzania, Dkt. Mette Halvorsen Ottøy, Prof. Egil Tjland wa NTNU, Prof. Prof. Jon Kleppe wa NTNU na Mwakilishi wa bodi ya Norad, Erik Holtar. 
Mhitimu wa shahada ya Uzamili, Anita Otto Ringia akiwa kwenye picha ya pamoja na Prof. Egil Tjland wa NTNU 
Mhitimu wa shahada ya Uzamili Beatrice Issara akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wahitimu wenzie kwenye sherehe za mahafali ya tano kwa wahitimu 14 waliofadhiliwa kusoma na kampuni ya Equinor Tanzania kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili katika masomo ya Petroleum Geosciences, Petroleum Engineering na Project Management UDSM kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam 
Mhitimu wa shahada ya Uzamili, Pendaeli Mbise akiwa kwenye picha ya pamoja na Prof. Egil Tjland wa NTNU 

………………………………………………… 

Kampuni ya Equinor Tanzania inafuraha kufanya mahafali ya tano kwa wahitimu 14 waliowafadhili kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili katika masomo ya Petroleum Geosciences, Petroleum Engineering and Project Management. 

Wahitimu hao wamefadhiliwa kupitia programu ya ufadhili ya Equinor Tanzania, inayofahamika kama ‘Angola Tanzania Higher Education Initiative’ (ANTHEI). Programu hiyo inayosimamiwa na Equinor inatoa ufadhili kamili kwa wanafunzi kumi kila mwaka kusoma Shahada ya Uzamili (MSc) katika masomo ya Petroleum Geoscience and Petroleum Engineering katika Chuo Kikuu cha Norwegian University of Science and Technology (NTNU), ambacho kinafanya kazi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) 

Programu hiyo imetengenezwa katika muundo ambao wanafunzi wanasoma mwaka mmoja Norway na mwaka wa mwisho wa Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mkataba wa makubaliano uliosainiwa kati ya Equinor, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na NTNU, Programu hiyo ya msaada wa elimu chini ya Equinor, ulianza mwaka 2012 na unafikia mwisho mwaka huu. Jumla ya wahitimu 64 tayari wamefaidika na program hii, kwa na kubahatika kufanya kazi katika vitengo mbalimbali vya serikali pamoja na sekta binafsi. 

Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Makamu wa Rais Mwandamizi ambaye pia ni Meneja Mkazi wa Equinor hapa nchini Dkt. Mette Halvorsen Ottøy, alisema, “Equinor inafuraha kufanya kazi kwa kushirikiana na vyuo vikuu ili kufikia lengo lake la kujenga uwezo ambalo ni jambo muhimu katika maendeleo ya sekta muhimu ya gesi nchini Tanzania. Lengo letu ni kuona watanzania wanapata mafunzo ili kuwa na sifa stahiki ili kutoa mchango wao katika ukuaji wa sekta hii kwa namna zote, moja kwa moja na isivyo moja kwa moja .” 

“Hapa Equinor tunatilia mkazo zaidi katika utendaji endelevu duniani kote. Mbinu ya Equinor ni kujenga mazingira endelevu ya shughuli zetu za msingi na kuchangia maendeleo pasipokuwa na kikomo mahali tunapofanya kazi,” aliongeza kusema Dkt. Mette. 

Wakati wa kipindi cha miaka sita ya Equinor kupitia programu yake ya uwezeshaji kumekuwapo na mafanikio ikiwa ni pamoja na maendeleo ya tafiti za Mafuta na Gesi, ambavyo vilipelekea uwepo wa Shahada ya Uzamili katika Fedha na Uhasibu kwenye Mafuta na Gesi (Master for Finance and Accounting in Oil and Gas -MFA-OG) vikitolewa kwa ushirikiano wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Stavanger. 

Halikadhalika Equinor imetoa msaada wa kiufundi katika Chuo Kikuu cha Barcelona pamoja na kuhakikisha uwepo wa Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Petroleum Geosciences kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Hii pia ilijumuisha mafunzo wa wakufunzi, ufundishaji kwa njia ya mtandao, na ujenzi wa maabara ya analojia 

Katika nyongeza ya ufadhili, mwaka huu Equinor imejenga maabara ya na kutoa mafunzo kwa mtu wa maabara katika Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Uhandisi Dar es Salaam (UDSM), na kuwezesha ufundishaji wa Shahada ya Uzamili katika Uhadisi wa Petroli katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

TAASISI YA USTAWI WA JAMII MABINGWA WA KUANDAA TAARIFA ZA FEDHA MWAKA 2018

$
0
0
 Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni akipokea Tuzo ya Mshindi wa Kwazna ya uandaaji taarifa za fedha kwa mwaka 2018 katika kundi la Vyuo vya elimu ya Juu,
 Kutoka Kushoto Dkt. Joyce Nyoni Mkuu wa Taasisi, Dkt. Zena Mabeyo Kaimu mkuu wa Taasisi fedhaUtawala, CPA Aisha Kapande Mhasibu,CPA Manase Shunashu Mhasibu, Na nyuma CPA Athman senzota Mhasibu Mkuu 
Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii na timu yake wakifurahia ushindi wa Tuzo ya kwazna ya Uandaaji wa taarifa za fedha 2018

Taasisi ya Ustawi wa Jamii imenyakua nafasi ya kwanza na kupata tuzo ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha  ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) katika hafla iliyofanyika Disemba 7, jioni katika viwanja vya NBAA Bunju.
Kwa mara ya nne mfululizo Taasisi ya Ustawi wa Jamii inashiriki na Kunyakua ushindi kwenye tuzo hizi muhimu katika taaluma ya Uhasibu Tanzania.
Akiongea baada ya Kupokea tuzo  Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni amesema ni furaha kubwa kwa Taasisi kutunukiwa tuzo hii ambayo ni kielelezo cha weledi na umahiri wa hali ya juu wa utunzaji wa taarifa za fedha na menejimenti nzuri za fedha za serikali katika Taasisi Yetu.
"Tumekuwa tukitoa huduma ya taaluma ya elimu, na ni manguli wa kutoa na kufundisha katika taaluma ya ustawi wa Jamii lakini sasa tunaonyesha weledi mkubwa katika fani ya uhasibu na utunzaji taarifa za fedha, naipongeza sana timu yangu ya Uhasibu ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii ikiongozwa na CPA Athuman Senzota." alisema Dkt. Joyce.

Vodacom kuwaunganisha Watanzania wengi zaidi kwenye intaneti katika msimu huu wa Sikukuu

$
0
0
Meneja wa Vodashop, Mlimani City, Dar es salaam, Vanessa Mlawi (Wapili kulia) na Afisa Mauzo Waziri Khalid (Wapili kushoto) wakizindua ofa ya msimu wa sikukuu inayowezesha fursa ya wateja kuunganishwa na uwapendao kupitia simu ya Smart Kitochi inayopatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini kwa bei nafuu ya TSH 45,000 tu. Hatua hii inalenga kuwezesha Watanzania wengi zaidi kuunganishwa na mtandao wa intaneti na kukuza matumizi ya kidigitali nchini kupitia mtandao Supa wa Vodacom wenye kasi na unaominika zaidi.
Meneja wa Vodashop, Mlimani City, Dar es salaam, Vanessa Mlawi (Kulia) na Mteja wa Vodacom Elvira Kamuzora (Kushoto) wakati wa uzinduzi wa ofa ya msimu wa sikukuu inayowezesha fursa ya wateja kuunganishwa na uwapendao kupitia simu ya Smart Kitochi inayopatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini kwa bei nafuu ya TSH 45,000 tu. Hatua hii inalenga kuwezesha Watanzania wengi zaidi kuunganishwa na mtandao wa intaneti na kukuza matumizi ya kidigitali nchini kupitia mtandao Supa wa Vodacom wenye kasi na unaominika zaidi. 
Meneja wa Vodashop, Mlimani City, Dar es salaam, Vanessa Mlawi (Kulia) na Afisa Mauzo Waziri Khalid (Kushoto) wakizindua ofa ya msimu wa sikukuu inayowezesha fursa ya wateja kuunganishwa na wapendao kupitia simu ya Smart Kitochi inayopatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini kwa bei nafuu ya TSH 45,000 tu. Hatua hii inalenga kuwezesha Watanzania wengi zaidi kuunganishwa na mtandao wa intaneti na kukuza matumizi ya kidigitali nchini kupitia mtandao Supa wa Vodacom wenye kasi na unaominika zaidi. 



*************************************** 
 Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC inatoa fursa kwa wateja wake kutoa zawadi ya simu ya Smart Kitochi kwa ndugu, jamaa na marafiki wakati wa Msimu huu wa Sikukuu. 

Hatua hii ya kipekee inalenga kuwawezesha watanzania wengi kujiunga na matumizi ya digitali kama kampuni inayojiendesha kidigitali kwa lengo la kuongeza idadi kubwa ya watumiaji wa intaneti na kupata habari mtandaoni, kupitia mtandao Supa wa Vodacom wenye kasi na inaoaminika zaidi nchini kote. 

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofa hiyo katika Viwanja vya Igoma jijini Mwanza, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Vodacom, George Lugata alisema, Wakati wa msimu huu wa Sikukuu Vodacom inatambua kuwa kuna umuhimu wa kutoa zawadi lakini pia kuwaunganisha wapendanao, ndiyo maana ya ofa hii. “Wakati wa msimu huu wa Sikukukuu. 

Vodacom inatoa fursa ya kipekee kusambaza upendo nchini kote kwa kumiliki au kumpa zawadi ya simu ya Smart Kitochi ndugu, jamaa na rafiki kwa bei nafuu kabisa ya Sh. 45,000 kutoka Vodacom. 

Katika maono ya kuipeleka Tanzania katika zama za kidigitali, Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kiasi kikubwa imewekeza katika miundombinu ya mawasiliano kupitia mtadao wake wa Supa Network wenye kasi na ambao unawafikia watanzania waliowengi kwa zaidi ya asilimia 92 katika viwango vya 3G, 4G na 4G plus nchi nzima. Hata hivyo jitihada hizi bado zinakwamishwa na uwepo wa matumizi madogo ya simu janja kwa watanzania walio wengi. 

“Tunataka kila mmoja apate uzoefu wa kutumia mtandao wetu wa Supa Network lakini pia afaidike na huduma ya intaneti. Pata Simu ya Smart Kitochi wewe na umpendaye na Vodacom watahakikisha kuwa unaunganishwa katika kipindi chote hiki cha msimu wa sikukuu kwa kukupa Data yenye GB 24, dakika 500 za muda wa maongezi na SMS 200 bure kwa muda wa miezi sita, vyote kutoka Vodacom. Pia utarejeshewa asilimia 10 kwa kila muamala utakaofanya kupitia MPesa, Naomba Watanzania wengi kujitokeza katika promosheni hii iliwaweze kuunganishwa katika huduma hizo muhimu,” alisema Lugata. 

Ikiwa na betri yenye nguvu ya 1400mAh ambayo inaiwezesha kukaa kwa muda wa masaa sita ya mazungumzo, Smart Kitochi inatumia laini mbili za simu, lakini pia ni chaguo sahihi kwa watanzania waliowengi katika soko la simu hapa nchini. 

Smart Kitochi ina apps maarufu kama Facebook, WhatsApp, YouTube, Instagram, Google Assistant na nyingine nyingi zitakazomuwezesha mtanzania kuwa katika jamii ya watumiaji wa intaneti. 

“Wateja wetu wanaweza kupata simu ya Smart Kitochi katika maduka yetu yote ya Vodashop nchi nzima, na kupitia katika magari yetu maalumu wakati wa msimu huu wa sikukuu, matamasha yetu yatafanyika katika mikoa mitano ambayo ni Mwanza, Arusha, Dodoma,
Mbeya na Dar es Salaam. 

Msimu huu wa Smart Kitochi unaambatana na matukio kadhaa ya kusisimua kama vile mashindano ya dansi, na burudani mbalimbali za katika mikoa hiyo mitano. Lengo la promosheni ni kuhakikisha kuwa tunawafikia watanzania wengi kwa kuwaunganisha katika maisha ya kidigitali,” 

Pamoja na ofa hii, Vodacom itakuwa ikifanya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole. ‘Wateja wetu wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwa kuzingatia umuhimu wa zoezi hili. alisema Lugata

Mgalu aliridhishwa na miundombinu ya umeme mradi SGR

$
0
0

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( mwenye kilemba) akiangalia kazi
ujenzi wa msingi wa kusimika nguzo kubwa ya umeme wa kV 220
utakaotumika katika reli ya kisasa, unayoendelea katika njia ya kusafirisha
umeme.


Muonekano wa Moja ya nguzo kubwa ya umeme wa kV 220 baada ya
kusimamishwa tayari kwa kupitisha nyaya.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akitoa maelekezo kwa wasimamizi
wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme mkubwa utakaotumika katika reli ya kisasa baada ya kutembelea na kukagua ghala la kuhifadhia vifaa hivyo
lililopo Kibaha, mkoani Pwani.


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na baadhi ya
wafanyakazi/ vibarua katika ghala la kuhifadhi vifaa vya ujenzi wa njia ya
kusafirisha umeme mkubwa utakaotumika katika reli ya kisasa, lililopo
Kibaha, mkaoani Pwani.
Baadhi ya vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme
mkubwa utakaotumika katika reli ya kisasa vilivyohifadhiwa katika ghala
lililopo kibaha mkoani Pwani.

*********************************



Na Zuena Msuya, Dar es salaam

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema ameridhishwa na ujenzi
wa miundombinu ya njia ya kusafirisha umeme wa kV 220 inayoendelea
kujengwa katika Reli ya kisasa kutoka jijini Dar es salaam hadi mkoani
Morogoro .

Mgalu alieleza hayo Desemba 7,2019 baada ya kufanya ziara ya kukagua
maendeleo ujenzi wa miundombinu hiyo kuanzia Kituo cha Kinyerenzi,
Pugu hadi Kisarawe jijini Dar es salaam ambapo asilimia 70 ya kazi hiyo
imekamilika.

Alitumia ziara hiyo kuwathibitishia watanzania kuwa mradi huo wa ujenzi
wa njia ya umeme utakamilika kwa wakati kulinga na makubaliano ya
mkataba na umeme upo mwingi na wa kutosha kuwezesha reli hiyo
kufanya kazi yake wakati wote.

Alifafanua kuwa ujenzi wa miundombinu ya njia ya kusafirisha umeme
inatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2020 ili kutoa fursa ya kuanza
majaribio ya safari kwa kutumia Treni ya umeme, kabla ya kuanza rasmi
kwa safari hizo mwezi Julai, 2020.

“Niwatoe hofu wale wote wenye mashaka na usafiri wa reli kwa kutumia
umeme, umeme upo mwingi na wa kutosha nchini, kwa sasa tunazalisha
zaidi ya megawati 1601, tunazotumia ni megawati 1116 tu, pia kazi ya
kujenga miradi mikubwa ya kuzalisha umeme mwingi zaidi inaendelea,
ukiwemo Mradi wa Julias Nyerere katika bonde la mto Rufiji, Rusumo na
Kinyerezi”, alisisitiza Mgalu.

Pia alikagua ghala za kuhifadhia vifaa mbalimbali vinavyotumika katika
ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme lililopo Kibaha mkoani Pwani na
kushuhudia uwepo wa vifaa vya kutosha kukamilisha ujenzi wa njia hiyo.

Aidha aliwataka wasimamizi wa mradi huo kuwalipa vizuri wafanyakazi
/vibarua wanaofanya kazi katika mradi huo ili na wao wafurahie na
kunufaika kuwepo kwa mradi huo, vilevile aliwataka vibarua hao kufanya
kazi kwa bidii, kuwa walinzi wa vifaa hivyo na miundombinu na kuweka
mbele maslahi ya taifa.

Aidha alilipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kazi nzuri
ya kusimamia utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya njia ya kusafirisha umeme mkubwa katika reli ya kisasa, na kuwataka kuongeza kasi zaidi ya
ujenzi huo ili ikiwezekana ujenzi huo ukamilike kabla ya muda waliopewa.

Kwa upande msimamizi wa mradi huo kutoka Tanesco, Mhandisi
Deogratius Msaki alisema kuwa kazi hiyo inaendelea vizuri licha ya
changamoto ya kigiografia ya ardhi katika baadhi ya maeneo na hali ya
hewa ya mvua.

Aliweka wazi kuwa mpaka sasa tayari wamesimamisha nguzo zaidi 120
kati ya 456 zitakazotumika kutoka Dar es salaam hadi Morogoro, pia kazi
ya kuweka vikombe na kuanza kuvuta nyaya imekwisha anza katika
maeneo ambayo tayari usimikwaji wa nguzo umekamilika huku kazi hiyo
ikiendelea, matarajio yao ni kuukabidhi mradi huo Tar 28 Februari 2020.

RAIS MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WASALI MISA TAKATIFU DOMINIKA YA PILI YA MAJILIO KATIKA KANISA KUU LA EPIFANIA PAROKIA YA BUGANDO JIJINI MWANZA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Mhashamu Renatus Nkwande leo tarehe 8/12/2019.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Mhashamu Renatus Nkwande akihubiri katika Misa Takatifu ya Dominika ya pili ya Majilio iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania Parokia ya Bugando jijini Mwanza leo tarehe 8/12/2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wamejumuika pamoja na waumini wengine wa Kanisa Kuu la Epifania Parokia ya Bugando jijini Mwanza katika Misa Takatifu ya Dominika ya pili ya Majilio iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza MhashamuRenatus Nkwande leo tarehe 8/12/2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikusanya Sadaka ya Ujenzi wa Kanisa katika Misa Takatifu ya Dominika ya pili yaMajilio iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania Parokia ya Bugando jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Kuu la Epifania Parokia ya Bugando jijini Mwanza katika Misa Takatifu ya Dominika ya pili ya Majilio iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Mhashamu Renatus Nkwande leo tarehe 8/12/2019.
 PICHA NA IKULU

TRA YANG’ARA TUZO ZA NBAA, YAPATA USHINDI WA JUMLA

$
0
0
Na Veronica Kazimoto ,Dar es Salaam

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeshinda tuzo mbili ikiwemo mshindi wa jumla katika uandaaji bora wa taarifa za hesabu mwaka 2018 kwa kufuata viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu katika Taasisi za Umma yaani mfumo wa IPSASs.

Katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju jijini Dar es Salaam, TRA imeibuka mshindi wa kwanza katika uandaaji bora wa taarifa za hesabu kwenye kipengele cha Wakala wa Serikali na mshindi wa jumla kwa taasisi, wakala, kampuni na mashirika mbalimbali ambayo yamefanya vizuri katika kuandaa taarifa za fedha katika shughuli zao za kila siku.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hizo, Kamishna Mkuu wa TRA Dkt. Edwin Mhede, ameipongeza Idara ya Fedha na idara nyingine ndani ya mamlaka hiyo kwa kufanikisha upatikanaji wa tuzo hizo.

“Nachukua nafasi hii kumshukuru mkuu wa idara anayehusika na Idara ya Fedha pamoja na wakuu wa idara nyingine ndani ya mamlaka maana zote zinatoa mchango mkubwa kuhakikisha idara hii inatoa taarifa sahihi na zenye kuleta mipango sahihi kwa mamlaka na serikali kwa ujumla,” alisema Dkt. Mhede.

Dkt. Mhede alieleza kuwa, taarifa sahihi ni msingi wa mipango kwa kuwa taasisi isiyopanga kushinda ni sawa na taasisi inayopanga kushindwa hivyo suala la uandaaji bora wa taarifa za hesabu ni moja ya ufanisi wa ofisi yoyote hapa ulimwenguni.

Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) ndio hutoa tuzo hizo kila mwaka ambapo mwaka 2017 TRA iliibuka mshindi wa kwanza tena katika uandaaji bora wa taarifa za hesabu katika kipengele cha Wakala wa Serikali.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede akipokea tuzo ya ushindi wa jumla ya uandaaji bora wa taarifa za hesabu kati ya taasisi, wakala, kampuni na mashirika mbalimbali kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaabani wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede akionyesha tuzo ya mshindi wa kwanza ya uandaaji bora wa taarifa za hesabu katika kipengele cha Wakala wa Serikali aliyopokea kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaabani wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede (katikati aliyeshika tuzo) akiwa na Naibu Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo (wa pili kushoto kwake) pamoja na watumishi wa Idara ya Fedha mara baada ya kupokea tuzo mbili za uandaaji bora wa taarifa za hesabu wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju jijini Dar es Salaam.

KIJANA WA KAZI AMUIBIA BOSI WAKE HATI NA KUIKOPEA

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
 
 
Na. Hassan Mabuye, WIZARA YA ARDHI
Iringa 

Mkazi wa Iringa mjini Bi. Lugano Mwadini amejikuta katika deni linalopelekea karibu nyumba yake kupigwa mnada baada kijana wake wa kazi kukopa pesa kiasi cha shilingi 1,000,000 kwa kutumia hati yake ya umiliki wa ardhi ambayo amemuibia.

kadhia hiyo imetokea wakati wa mkutano wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kupitia programu yake ya ‘Funguka kwa Waziri’ mkoani Iringa alipokuwa akisikiliza na kutatua kero za ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Iringa katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo katika Manispaa ya Iringa. 

katika mkutano huo Bi. Lugano alimtuhumu Kijana wake wa kazi kwa kumuibia hati na kuenda kukopa kwa Bw. Laurence Panklas ambaye ni askari wa jeshi la polisi mkoani Iringa anayekopesha kwa riba ya 400,000 kila mwezi ambazo kijana huyo hakuweza kuzirudisha kwa wakati jambo lililopelekea kutaka kuuzwa kwa nyumba yake ili kufidia deni hilo. 

Bi. Lugano Mwadini aligundua hayo baada ya kupigiwa simu na mkopeshaji huyo kumtaka kwenda kubalisha umiliki wa hati hiyo ili apewe mtu mwingine kwa kuwa hati yake imekopewa na inadaiwa shilingi 1,400,000. 

“Mi nilikuwa sipo lakini nikaja kupata taarifa kwa kupigiwa simu kwamba kijana wangu wa kazi ameniibia hati yangu wakati nikiwa katika kazi zangu na amekopea kwa askari mmoja ambaye anakopesha kwa riba ya laki nne kila mwezi, kwa hiyo kijana wangu anadaiwa 1,400,000 na hajalipa hadi sasa” Alisema Bi. Lugano Mwadini. 

Waziri Lukuvi alimuagiza Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire kushughulikia suala hilo, kwanza kwa askali wa jeshi la polisi ambaye anafanya biashara ya pesa na kama ana kibali cha biashara hiyo na analipa kodi, kama halipi basi alipe kodi kwa miamala yote aliyowahi kufanya.

Aidha Waziri Lukuvi aliagiza kukamatwa kwa kijana huyo wa kazi ili alipe deni hilo kwa Bosi wake na kueleza kwanini amefanya uhalifu huo wa kuiba hati ya mtu mwingine. 

Katika mkutano huo Waziri Lukuvi aliweza kusikiliza na kutatua migogoro ya wakazi wa mkoani Iringa takribani 200 kwa siku moja ambapo baadhi ya wananchi walieleza kuridhishwa kwa juhudi za waziri lukuvi kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi ya wakazi wa maeneo mbali mbalibila nchini bila kubagua

EACJ CONGRATULATES THE DEPUTY PRINCIPAL JUDGE DR FAUSTIN NTEZILYAYO UPON HIS NEW APPOINTMENT AS THE CHIEF JUSTICE OF THE REPUBLIC OF RWANDA

$
0
0

Hon Justice Dr Faustin Ntezilyayo appointed as the Chief Justice of the Republic of Rwanda, taking the Oath.His Excellence President Paul Kagame of the Republic of Rwanda congratulating His Lordship Dr Ntezilyayo, after taking the Oath (5)-page-001 

The East African Court of Justice warmly congratulates Hon Justice Dr Faustin Ntezilyayo, Deputy Principal Judge of the First Instance Division, upon his new appointment as the Chief Justice of Rwanda and will be replacing His Lordship Justice Prof Sam Rugege who has retired.

The EAC Heads of State summit appointed His Lordship Dr Ntezilyayo a judge to East African Court of Justice in April 2013 by and consequently he was designated the Deputy Principal Judge in July 2018, a position he still holds to date Justice.

The President of the Court, Hon Justice Dr Emmanuel Ugirashebuja, on behalf of the Court and on his own behalf congratulates His Lordship Dr Ntezilyayo and commends his dedicated and recommendable work as a judge and the exemprary leadership as the Deputy Principal Judge of the First Instance Division, which has greatly contributed to rising the jurisprudence and steady growth of the Court.

His Lordship Dr Ugirashebuja further said that, Justice Ntezilyayo’s new elevation to the Chief Justice demonstrates his hard work in the judiciary of Rwanda and entrusting him with greater assignment. I once again congratulate His Lordship and wish him good cooperation in implementing the role of the judiciary of Rwanda. The East African Court of Justice has no doubt in his support in implementing its role of ensuring adherence to the law through interpretation, application and compliance of the Treaty in the EAC region and in particular the Republic of Rwanda.

His Excellency, President Paul Kagame of the Republic of Rwanda swore in Justice Dr Faustin Ntezilyayo as the Chief Justice of Rwanda today 6th December 2019.

Justice Ntezilyayo previously before being appointed to EACJ, served as the Assistant Lecturer at the National University of Rwanda; Senior Legal Advisor, Ministry of Trade and Industry Rwanda; Minister of Justice of Rwanda; Vice Governor of the Central Bank of Rwanda; Managing Director of the Rwanda Utility Regulatory Agency; Independent Consultant and Visiting Lecturer at the University of Ottawa, Canada and Managing Director of AGASEKE Bank. His Lordship holds a PhD in Law, University of Antwerp, Belgium 1994; LLM in Fiscal Law, Free University of Brussels, Belgium, 1996; M.A in International Affairs with specialization in International Trade Policy, Carleton University, Canada, 2009.

DATA TAMASHA 2019 LAWANUFAISHA VIJANA

$
0
0
Mkurugenzi wa Taasisi ya TSDT Sosthenes Kewe akizungumza wakati wa kufunga tamasha la Data Tamasha kwa mwaka 2019 ambapo amewashauri vijana kutumia maarufa ya kidigiti vyema katika kujenga taifa, leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Data Lab, Dkt. Blandina Kilama akitoa cheti cha pongezi kwa mmoja wa washiriki waliohudhuria Tamasha hilo, ambapo amesema kuwa makundi maalumu wakiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ni muhimu kushirikishwa katika ukusanyaji wa taarifa na takwimu, leo jijini Dar es Salaam.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IMEELEZWA kuwa ushirikishwaji wa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ni katika kukusanya na kutumia takwimu na taarifa kwa jamii ya sasa ni muhimu na yenye kuleta tija kwa jamii na hiyo ni kutokana na sekta ya kidigitali kukua na kuhitaji kuzibwa kwa ombwe la ushirikishwaji lililopo ili kujenga taifa imara.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga tamasha la Data Tamasha ambalo limewakutanisha watu wa kada mbalimbali Mkurugenzi wa  Financial Sector Deepening Trust (FSDT) Sosthenes Kewe  amesema kuwa tamasha hilo limekuwa moja ya  tamasha kubwa na kueleza kuwa washiriki  lazima wametoka na  maarifa ambayo  yatawasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii zao.

Kewe amesema kuwa baada ya kupata maarifa hayo ni vyema washiriki  watumie changamoto wanazokutana nazo kama kama fursa na  wakaibadilishe jamii na taifa kupitia maarifa hayo na hiyo ni pamoja na kufanya gunduzi zenye tija katika jamii.

Aidha amesema kuwa sekta ya uchumi inaenda sambamba na gunduzi hivyo wanafunzi lazima wajikite katika kufanya hilo kwa kuwa nafasi hiyo kwao ipo wazi na kwa kufanya hivyo  wataacha alama kwa kizazi  cha sasa na baadaye na historia yao haitofutika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya taasisi ya Tanzania Data Lab  Dkt. Blandina Kilama amesema siku tatu za Tamasha hilo zimetumika katika kujifunza mambo mengi ikiwemo ushiriki wa wanawake, watu wenye ulemavu na vijana hivyo kilichobaki ni kutumia vyema maarifa hayo ambayo wanaamini yataleta Mabadiliko chanya.

Amesema kuwa katika kusheherekea siku ya takwimu na taarifa wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi wametoa uzoefu ikiwa ni pamoja na matumizi ya vyombo mbalimbali ikiwemo ofisi ya takwimu na taarifa katika kushirikiana na kupeana taarifa za kitakwimu.

Vilevile amesema kuwa siku hizo tatu zimekuwa na faida kwa vijana ambapo wamepata uzoefu na njia mbalimbali za ubunifu ambazo zitawasaidia kijijenga na kuleta matokeo chanya katika jamii na taifa kwa ujumla.

Pia Mkurugenzi wa Tanzania Data Lab, Stephen Chacha amesema kuwa wamekuwa wakisherekea siku ya takwimu na taarifa kila baada ya miaka miwili ila kuanzia mwakani wataadhimisha siku hiyo kila mwaka na hiyo ni kutokana na mwamko na mahitaji ya wadau katika kujenga tasnia hiyo yenye tija kwa jamii.

Chacha ameishukuru Serikali kupitia ofisi ya Takwimu kwa  kwa ushirikiano wanakutoa katika kuendeleza mbele tasnia hiyo muhimu.

KATIBU MKUU DKT. JINGU AIPELEKA KAMPENI YA MAKAZI BORA MONDULI

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu (kulia) akifungua kisanduku kuashiria uzinduzi wa kikoba cha Kikundi cha wanawake cha Tuinuane mbele ya Mwenyekiti wake Bi. Anna Lusoloi (kushoto) wakati alipotembelea kujionea shughuli zinazofanywa na kikundi hicho kilichopo wilayani Monduli mkoani Arusha.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Monduli Juu Orphane Project Bw. Thomas Millay (kulia) wakati alipotembelea kujionea shughuli zinazofanywa na Shirika hilo lililopo wilayani Monduli mkoani Arusha.



Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Mandeleo ya Jamii Monduli alipotembelea miradi ya maendeleo Chuoni hapo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Tunahaki Bi. Christina Kami (kushoto) wakati alipotembelea kujionea shughuli zinazofanywa na kikundi hicho kilichopo wilayani Monduli mkoani Arusha.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu (kushoto) akipokea zawadi ya picha yake kutoka kwa Mkufunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli Bi. Mariah Lashau (kulia) wakati alipotembelea Kituo cha ubunifu cha kidijitali cha Chuo hicho.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

************************************


Na Mwandishi Wetu Arusha

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewataka wananchi kuhakikisha wanaboresha makazi yao kutoka makazi ya nyumba za nyasi na tembe kwenda nyumba za tofali na bati.

Aliyasema hayo leo Wilayani Monduli mkoani Arusha alipokuwa akitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoamasishwa na wataalam kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli kwa kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika miradi ya Maendeleo.

Dkt. Jingu aliwataka wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini kuhakikisha wanakuwa chachu ya mabadiliko na wanawezesha jamii kuwa na mawazo chanya ya kujiletea maendeleo na kubadili changamoto kuwa fursa za kimaendeleo.

“Wataalam wa Maendeleo ya Jamii tuweke nguvu katika kuhakikisha tunabadili jamii zetu kuwa na mawazo chanja hasa ya kujitegemea na kujiletea maendeleo” alisema Dkt. Jingu.

Dkt. Jingu aliongeza kuwa Sekta ya Maendeleo ya Jamii inapaswa kuwa chachu ya maendeleo katika taifa letu hivyo Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vinatakiwa kutoa wataalam wenye weledi na stadi za kubwa za kuleta mabadiliko katika jamii.

“Vyuo vya Maendeleo ya Jamii tutoe wataalam wenye weledi wa kuhakikisha tunatumia fursa zilizopo katika jamii kutatua changamoto zilizopo” alisema Dkt. Jingu.

Wakati huohuo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli Dkt. Jingu amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanatumia stadi watakazopata kubadilisha maisha yao na jamii kwa ujumla.

Dkt. Jingu aliwataka wanafunzi hao kuitumia bahati ya kuwa mmoja ya wanafunzi katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli kwa kuhakikisha wanafanikisha ndoto zao walizozilenga kuzitimiza katika maisha yao kwa kuzingatia masomo na nidhamu.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli Bw. Elibariki Ulomi alimuhakikishia Katibu Mkuu kuwa Chuo hiyo kitahakikisha kinashirikiana na wananchi wa Wilaya ya Monduli katika kutekeleza Kampeni ya Makazi Bora ili kuwawezesha wananchi kuboresha makazi yao na kuhakikisha kinatoa Wataalam wa Maendeelo ya Jamii watakosaidia kuleta mabadiliko katika taifa.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Monduli Bi. Rose Mhina alisema kuwa Halmashauri hiyo imeshaanza kutekeleza kampeni ya Makazi bora kwa kuipeleke ajenda hiyo kwa madiwani na kutoa michoro maalum kwaajili ya ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu.

Aliongeza kuwa Kampeni hiyo ya kuhamaisha ujenzi wamakazi bora itahamasishwa na katika jamii na maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka wilayani maoaka kwemye kata ili kuhakikisha wananchi wanajitoa na kuboresha makazi yao.

Kampeni ya Kuboresha makazi inalenga kuiwezesha jamii ambayo inaishi katika makazi yasiyo bora kuweza kuboresha makazi yao kwa kutumia ramani ziliziotolewa na Halmashauri walizopo zikiwa ni nyumba za gharama nafuu.

EALA HAILS MESSRS KENNETH MADETE & ALEX OBATRE LUMUMBA

$
0
0
Hon Paul Musamali presents the Resolution paying tribute to the Clerk and the Deputy Clerk whose tenure of service at the Assembly (and the Community) ended last week
· Mr Kenneth N. Madete, outgoing Clerk of the EALA
· Mr Alex Obatre Lumumba, outgoing Deputy Clerk, EALA

***************************

East African Legislative Assembly, Arusha, December 6th 2019: The East African Legislative Assembly late yesterday paid special tribute to the Clerk, Mr Kenneth Namboga Madete and the Deputy Clerk, Mr Alex Obatre Lumumba, upon completion of their tenure of service to the Community last week (on November 30th, 2019), for their dedicated service. The motion moved by Hon Paul Musamali commended the duo for their steadfast and loyal service to the Assembly and wished them well in their future endeavor.

Hon Musamali cited human resources as key to the Community and said both Mr Madete and Mr Lumumba had exemplified total commitment and dedication. “Due to the very nature of their work and because of their attitude and the value attached to the people they served, the accolades were deserving”, Hon Musamali said.

The legislator cited a number of achievements realized over the period the Clerk and his Deputy were at the helm.

“During the tenure of Mr Madete, EALA was granted a sub-accounting status and for the entire period, the Assembly audited accounts were never qualified. It is during the period that the Assembly pursued a proactive approach to ensure the growth of the staffing levels bringing on board six senior clerks/committee clerks, the creation of two deputy clerk positions, creation of a senior public relations office and the elevation and grading of some positions from the general staffing category to that of the professional level”, Hon Musamali said.

The mover also attributed the negotiating skills of the two Executives as key resulting in among others, in growth of budget and activities of the Assembly. “Through the skills of the Clerk and Deputy Clerk, the Assembly attracted support of USD 5 million (spread over five years from the Association of European Parliamentarians with Africa (AWEPA) in 2009 in support of the public hearings and the capacity building needs of EALA Members, staff and committees”, Hon Musamali said.

“The success of the first EALA-AWEPA programme will soon pay off with a new programme following new designs which have already been discussed”, Hon Musamali added.

The Member moved the motion under Articles 49 and 59(1) of the Treaty and Rule 26 of the Rules of Procedure.

During debate, Hon Dr Pierre Celestin Rwigema said the outgoing Clerk and Deputy Clerk had gained vast experience and urged the Partner State from which they hail to take advantage of their skills and utilize them effectively.

Hon Kasamba Mathias reminded the House that a number of colleagues had also exited the Assembly upon expiry of their terms. Last year when in Nairobi, the Assembly reminded the Council of Ministers to extend contracts of exiting officers in the interim period, although it was not possible”, he said. “We pray that they (exiting officers) will join the community of experts given their accumulated years of experience. Movement is part of organizational growth and maturity and we must appreciate such aspects”, Hon Kasamba stated.

Hon Rose Akol said it was necessary for the Assembly (and the East African Court of Justice) to be granted independence/autonomy to carry out their own decisions. The Member further called for secondment of clerks from the Parliaments to avoid the loss/wastage of skills. 
 
The legislator said the recently concluded institutional review exercise which was done for a decade, (although was yet to be formally presented), had anticipated downgrade of some of the positions. During the period under review, the Council of Ministers had placed a moratorium on recruitment. 
 
“There is now need to handle very urgently, the recruitment of staff. I further suggest the report of the Institutional review exercise also to be brought to this august house for scrutiny”, she said. In his update to the Assembly, the Speaker confirmed that Council of Ministers had agreed to pursue the matter of staff recruitment immediately.

Hon Pierre Claver Ruakamvye hailed the out-going Clerk as a good social mobiliser who contributed immensely to the development of sporting activities in the Parliament while Hon Dr Abdulla Hasnuu Makame, and Hon Dr Woda Jeremiah Odok commended other clerks and staff whose tenure of service ended earlier.

Mr Madete has been a Parliamentary Officer since February 1995 and rose to the ranks at the Parliament of Uganda before he joined EALA in November 2002 as a Principal Clerk Assistant. On his part, Mr Alex Obatre Lumumba joined the Assembly in August 2007 as Senior Clerk Assistant, twelve years after serving as a Clerk Assistant at the Parliament of Uganda.

Both Officers were later elevated as Clerk and Deputy Clerk respectively following a competitive process in 2009. The Clerk is the Chief Executive of the Assembly who in line with guidelines from the EALA Commission is responsible for preparing and planning the strategic programmes and activities of the Assembly and rendering professional advise to the Speaker and Members of the Assembly and other persons in respect of the procedural and legislative matters. Under the current Staff Rules and Regulations, all Professional staff are entitled to serve the Community in the same capacity for a period of 5 years renewable, once (totaling 10 years)

REGIONAL ECONOMIC AND SOCIAL INTEGRATION SUPPORTED BY TWO NEW GIZ PROGRAMMES IMPLEMENTED WITH THE EAC

$
0
0



The East African Community Secretariat and the EAC GIZ programme supporting East African Integration on behalf of the German Government, today signed an implementation agreement worth US$16 million for continuing support for EAC regional integration through their SEAMPEC and Pandemic Preparedness programmes.

The programmes are managed through the EAC-GIZ partnership to continue to grow regional economic and social integration which already has a significant impact in the region.

The SEAMPEC programme, through its multiple cross-cutting initiatives, takes a holistic approach to regional integration that encompasses civil society as well as the public and private sectors. Through targeted work in sectors including agro-processing, pharmaceuticals as well as services sectors such as tourism and ICT, SEAMPEC aims to facilitate the improvement of framework conditions to help create more competitive industries and cross border opportunities.

“GIZ and the Secretariat have been developing and managing key projects working with partners across the EAC region with a focus on making the Common Market, Customs Union and integration a reality.

Through the SEAMPEC programme many businesses and civil society organisations have all benefited from collaborating on the ground and high-level networking and coalition activities. We are proud to continue to implement programmes which are showing real results and bringing tangible benefits to the citizens of the EAC,” said Dr Mike Falke, GIZ Country Director for Tanzania and EAC.

Another US$3 million of the funding are going towards the ‘Support to Pandemic Preparedness in the EAC Region’ project, which started in March 2017 and entered its second phase in September 2019. This project is working closely with the EAC to implement the Regional Contingency Plan under the interdisciplinary and multi-sectoral One Health approach and to establish the discipline of risk and crisis communication in the region.

The project supports the EAC Secretariat in its coordinating and advisory role in the prevention and response to cross-border outbreaks. The project builds on important preparatory work and ensures that when pandemic health threats become a reality, EAC countries are in the best position to respond.

“Diseases such as Ebola and Dengue Fever are claiming lives and destroying livelihoods right now. High population density, increasing cross-border trade, climate change and many other factors increase the risk of spreading these infectious diseases. Being ready to respond and having the tools and expertise to be effective in emergency situations is crucial,” said Irene Lukassowitz, GIZ project manager. Following a successful cross border field simulation exercise between Kenya and Tanzania in June 2019, another field simulation exercise at the border between South Sudan and Uganda in 2020 will prepare the region even better.

“Germany’s development cooperation, on behalf of the German Federal Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ) and the European Union (EU), has to date contributed to the regional integration in East Africa through a variety of programmes and projects aimed at building up regional expertise and value adding to trade, industrial development, innovation and investment. GIZ has been working with the EAC for over 20 years, building capacities and expertise at the EAC Secretariat and for regional stakeholders.



SEAMPEC and the Pandemic Preparedness programme already have many achievements, and by continuing to grow these initiatives and invest in their successes we are confident that real EAC development is happening,” said Dr Kirsten Focken, GIZ Cluster Coordinator.

RAIS DKT MAGUFULI AMLILIA ALI MUFURUKI

Vodacom yawapelekea ofa mbalimbali wakazi wa mkoa Kilimanjaro msimu huu wa sikukuu

$
0
0

Meneja wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Brigita Stephen(kushoto) akizindua simu ya mkononi aina ya smart kitochi kwa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini yenye uwezo mkubwa wa internet ya 4G iliyozunduliwa Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom wakiwa kwenye hafla ya  uzinduzi wa  simu ya mkononi aina ya smart kitochi kwa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini yenye uwezo mkubwa wa internet ya 4G iliyofanyika viwanja vya kituo cha mabasi Mjini Moshi.
Baadhi wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom wakifurahia uzinduzi wa  simu ya mkononi aina ya smart kitochi kwa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini yenye uwezo mkubwa wa internet ya 4G iliyofanyika viwanja vya kituo cha mabasi Mjini Moshi


DATA TAMASHA 2019 LAWANUFAISHA VIJANA DAR

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Data Lab, Dkt. Blandina Kilama akitoa cheti cha pongezi kwa mmoja wa washiriki waliohudhuria Tamasha hilo, ambapo amesema kuwa makundi maalumu wakiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ni muhimu kushirikishwa katika ukusanyaji wa taarifa na takwimu, leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya TSDT Sosthenes Kewe akizungumza wakati wa kufunga tamasha la Data Tamasha kwa mwaka 2019 ambapo amewashauri vijana kutumia maarufa ya kidigiti vyema katika kujenga taifa, leo jijini Dar es Salaam.
 Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa katika tamasha la Data Tamasha lililofanyika kwa siku tatu jijini Dar es Salaam.


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IMEELEZWA kuwa ushirikishwaji wa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ni katika kukusanya na kutumia takwimu na taarifa kwa jamii ya sasa ni muhimu na yenye kuleta tija kwa jamii na hiyo ni kutokana na sekta ya kidigitali kukua na kuhitaji kuzibwa kwa ombwe la ushirikishwaji lililopo ili kujenga taifa imara.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga tamasha la Data Tamasha ambalo limewakutanisha watu wa kada mbalimbali Mkurugenzi wa Financial Sector Deepening Trust (FSDT) Sosthenes Kewe amesema kuwa tamasha hilo limekuwa moja ya tamasha kubwa na kueleza kuwa washiriki lazima wametoka na maarifa ambayo yatawasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii zao.

Kewe amesema kuwa, baada ya kupata maarifa hayo ni vyema washiriki watumie changamoto wanazokutana nazo kama kama fursa na wakaibadilishe jamii na taifa kupitia maarifa hayo na hiyo ni pamoja na kufanya gunduzi zenye tija katika jamii.

Aidha amesema kuwa sekta ya uchumi inaenda sambamba na gunduzi hivyo wanafunzi lazima wajikite katika kufanya hilo kwa kuwa nafasi hiyo kwao ipo wazi na kwa kufanya hivyo wataacha alama kwa kizazi cha sasa na baadaye na historia yao haitofutika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya taasisi ya Tanzania Data Lab Dkt. Blandina Kilama amesema siku tatu za Tamasha hilo zimetumika katika kujifunza mambo mengi ikiwemo ushiriki wa wanawake, watu wenye ulemavu na vijana hivyo kilichobaki ni kutumia vyema maarifa hayo ambayo wanaamini yataleta Mabadiliko chanya.

Amesema kuwa katika kusheherekea siku ya takwimu na taarifa wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi wametoa uzoefu ikiwa ni pamoja na matumizi ya vyombo mbalimbali ikiwemo ofisi ya takwimu na taarifa katika kushirikiana na kupeana taarifa za kitakwimu.

Vilevile amesema kuwa siku hizo tatu zimekuwa na faida kwa vijana ambapo wamepata uzoefu na njia mbalimbali za ubunifu ambazo zitawasaidia kijijenga na kuleta matokeo chanya katika jamii na taifa kwa ujumla.

Pia Mkurugenzi wa Tanzania Data Lab, Stephen Chacha amesema, wamekuwa wakisherekea siku ya takwimu na taarifa kila baada ya miaka miwili ila kuanzia mwakani wataadhimisha siku hiyo kila mwaka na hiyo ni kutokana na mwamko na mahitaji ya wadau katika kujenga tasnia hiyo yenye tija kwa jamii.

Chacha ameishukuru Serikali kupitia ofisi ya Takwimu kwa kwa ushirikiano wanakutoa katika kuendeleza mbele tasnia hiyo muhimu.

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YANG’ARA UANDAAJI WA RIPOTI BORA ZA MAHESABU KWA MWAKA 2018.

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi tuzo Mhasibu Mkuu fungu 50,Christopher Mkupama mshindi wa pili wa uandaaji Bora wa mahesabu kwa kuzingatia viwango vya kimataifa ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Prof. Isaya Jairo.


Na Ramadhani Kissimba, WFM, Dar es Salaam

Wizara ya Fedha na Mipango, Fungu 50 imepata tuzo ya uandaaji bora wa mahesabu (Finacial statements) kwa mwaka 2018, kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uandaaji wa hesabu serikalini (IPSAS).

Tuzo hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban, wakati akifunga mkutano wa mwaka wa wahasibu uliyofanyika Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo

Mkutano huo wa siku tatu uliowashirikisha wataalamu wa fani ya uhasibu zaidi ya 2,500 kutoka Serikali Kuu, Taasisi za Serikali, Halmashauri na Sekta Binafsi za hapa nchini pamoja na nchi za Kenya, Uganda,Burundi na Zambia, ulikuwa na lengo la kubadilishana uzoefu kwa wataalmu hao kulingana na mabadiliko ya sekta hiyo yanayotokea ulimwenguni.

Aidha, Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwawezesha wataalam hao kuwa na lugha ya pamoja katika uaandaaji wa hesabu unaozingatia viwango vya kimataifa.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo Mhasibu Mkuu wa Fungu 50 Bw. Christopher Mkupama alisema Wizara ya Fedha na Mipango, Fungu 50 imekuwa ikifanya vizuri katika uaandaji wa hesabu za mwaka kwa kipindi cha miaka minne mfufulizo na kupelekea kupatikana kwa tuzo hizo.

Alisema kuwa Tuzo hizo zimekuwa zikiiletea sifa Wizara ya Fedha na Mipango hasa Fungu 50 na kuchochea morali ya ufanyaji kazi kwa watumishi wa fani ya uhasibu.

‘’Nawashukuru sana viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango na watumishi wa Kitengo cha uhasibu kwa kutufanya tuwe washindi wa pili kwa mara nyingine katika uaandaaji bora wa hesabu kwa mwaka 2018, tuzo hii ni shukrani kwa watumishi wote wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa mchango mkubwa wanaotoa kwa wahasibu katika uandaaji wa taarifa za hesabu za kila mwaka’’ alisema Bw.Mkupama.

Mkutano wa mwaka wa wahasibu ulianza tarehe 5 hadi 7 Disemba,2019 kwa kufunguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG), Bw. Charles Kichere kwa niamba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpnago (Mb) na kufungwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban.

katibu mkuu wizara ya maendeleo ya jamii avifunda vyuo vya maendeleo ya jamii kujiongeza

$
0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Katibu Mkuu idara kuu ya maendeleo ya jamii,Dokta John Jingu amevitaka vyuo vya maendeleo ya jamii nchini kutoa elimu ambayo itakuwa ni nyenzo na silaha ya kupambana na changamoto zilizopo katika jamii na kuweza kuleta matokeo chanja.

Dkt Jingu aliyasema wakati alipotembelea chuo Cha maendeleo ya jamii Monduli Mkoani Arusha ambapo pia ametembelea na kujionea miradi mbalimbali ya wananchi iliyofanikishwa na chuo hicho kwa kushirikiana na wananchi kupia kitengo cha ujasiamali cha chuoni hapo. .

Alisema kuwa,kama wizara imekuwa ikisisitiza vyuo hivyo kuhakikisha wanatoa elimu ambayo itakuwa ni silaha ya utatuzi wa changamoto mbalimbali katika jamii ili uwepo wa vyuo hivyo uweze kutambulika kwa vitendo zaidi.

"unajua unaposema upo chuo unasomea kozi fulani mjue kabisa elimu sio sifa tu ama cheti bali jamii yenyewe inatakiwa ikutambua kwa kazi zako unazozifanya kwani ndizo zitaweza kukutambulisha kwa jamii katika kuhakikisha elimu uliyoipata italeta majibu kwenye matatizo yaliyopo."alisema

Hata hivyo katibu mkuu huyo alifurahishwa na miradi mbalimbali ya kijamii iliyoanzishwa na chuo hicho ambayo bado wananchi wanaendelea kuitekeleza ambayo imewasaidia Sana kujikwamua kiuchumi hivyo kukimwagia sifa chuo hicho kwa ubunifu mkubwa wa kuleta mabadiliko katika jamii.

Naye kaimu Mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii Monduli ,Elibariki Ulomi alisema kuwa,wamekuwa wakitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jamii inayowazunguka ikiwemo ufugaji wa kuku,ng'ombe,ambayo imewasaidia kwa kiasi kikubwa Sana kujikwamua kiuchumi.

Alisema kuwa,chuo hicho kimekuwa kikitekeleza kwa vitendo elimu wanayoitoa chuoni hapo ambapo wameweza kuibadili jamii hiyo ya wafugaji kwa kusaidia miradi mbalimbali ya ujasiriamali sambamba na kutoa elimu namna ya kuhifadhi fedha zao wenyewe na kuweza kukopeshana.

Wakizungumzia namna walivyonufaika na chuo hicho wanakikundi cha Tuinuane kilichopo Monduli juu ,walisema kuwa,chuo hicho kimeweza kuwapatia mafunzo mbalimbali namna ya ufugaji bora wa kisasa wa ng'ombe na kuku ambapo wameweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mradi huo na kuondokana kuwa tegemezi.

Katibu wa kikundi hicho ,Anna Losiloyi alisema kuwa,kikundi hicho kina jumla ya wanachama 30 ambapo wameweza kuwa na kuku Mia moja na ng'ombe mmoja huku wakijishughulisha na biashara ya kushona shanga pamoja na bangili ambazo wamekuwa wakiwauzia watalii na kuweza kutunisha kikundi chao.

Aidha kikundi hicho kimefika mbali zaidi kwa kumwomba Katibu Mkuu kuwazindulia rasmi kikoba ambacho kitawasaidia kuweka fedha zao ili waweze kukopeshana 

  Katibu Mkuu idara kuu ya  maendeleo ya jamii,Dkt John Jingu  akitembelea na kukagua miradi mbalimbali wakati alipotembelea Chuo cha maendeleo ya jamii monduli
 

WAHITIMU WASHAURIWA KUZINGATIA MAADILI MEMA,UWADILIFU KUTETEA TAIFA LAO

$
0
0
Na Pamela Mollel,Arusha

Wahitimu nchini wameshauriwa kuzingatia maadili Mema ,uwaadilifu, kutetea Taifa lao Pamoja na kuwa mabalozi Wazuri .

Hayo yamesemwa  Na Naibu Katibu mkuu wa wizara Ya fedha na Mipango Mh.  Mery Maganga mapema jana katika mahafali ya 21 ya Chuo Cha Uhasibu kilichopo njiro Mkoani Arusha ambapo amewatunukuu vyeti wahitimu zaidi ya 1000 wa Kozi mbalimbali kwa Ngazi Ya stashahada Na shahada.
 
Dkt.Mery  Ameongeza kuwa elimu bora ni msingi wa Maisha hivyo Elimu waliyo ipata watumie katika kuboresha Maisha yao na Jamii inayo wazunguka.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika mahafali hayo,  amewapongeza wahitimu kwa kuhitimu masomo yao huku akiwataka kutetea vyeti walivyonavyo kwa vitendo ili kuendana na kasi ya  soko la Ajira nchini.

"vyeti ulivyo navyo havina maana Kama Huna uwezo wa kuvitetea kwa vitendo kwani wapo wasomi wengi na wana vyeti visafi lakini ukiwaajiri hawana uwezo wa kufanya kazi yako Kama ulivyo tarajia hivyo unalazimika kuwafukuza" alisema Gambo.

Gambo Ameongeza kuwa vyuo vikuu Ndio sehemu inayozalisha mawazo mbadala lakini bado kuna changamoto ya kutokuyatendea kazi jambo ambalo hukwamisha maendeleo ya Nchi.

Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Prof. Eliamani Sadoyeka amewaasa wahitimu hao kuwa wabunifu katika kazi zao Na kujijengea utaratibu wa kusoma vitabu kwa wingi ili kuongeza maarifa kwani Soko la Ajira la sasa linaitaji watu werevu .

Amesema kuwa  katika uboreshaji wa miundombinu ya chuo wameanza ujenzi wa dhahanati , Bwalo la chakula ambavyo  vitasaidia kuboresha huduma kwa wanafunzi.

Kwa upande wake  meneja wa Benk Ya posta mkoa wa Arusha,  Ayubu Mkwawaambaye pia ameshiriki mahafari hayo amesema kuwa katika kushiriki maendeleo ya kielimu nchini Benk hiyo imetenga milioni Saba kwa wanafunzi Saba bora ili kuwapa motisha  na kuwafanya waone umhimu wa Elimu.

Hata hivyo Ametowa wito kwa Taasisi mbalimbali kuwekeza nguvu zao katika Elimu ili kuwezesha utafiti unaofanyika vyuoni nahatimae  kuibuwa hoja kwaajili yamaendeleo ya nchi.



Katika ni muhitimu katika chuo cha uhasibu njiro Trudeline Saning'o ambaye alishika nafasi ya kuwa mwanafunzi bora upande wa wanawake pamoja na zawadi zingine pia alizawadiwa na benki ya Posta shilingi milioni moja.
Upande wa wazazi wakionekana kuchukua baadhi ya matukio katika mahafali hayo
Godfrey Namani ambaye ni muhitimu katika chuo alishika nafasi ya kuwa mwanafunzi bora upande wa wanaume pamoja na zawadi zingine pia alizawadiwa na benki ya Posta shilingi milioni moja
Muonekano wa wahitimu katika picha



Sehemu ya wahitimu katika picha


Baadhi ya wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu
Naibu katibu mkuu wizara ya fedha na mipango,Dkt Mary Maganga akisoma hotuba yake kwenye mahafali ya 21ya idara ya usimamizi wa biashara yaliyofanyika leo katika chuo cha uhasibu njiro Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo akizungumza ambapo pamoja na Mambo mengine aliwataka wahitimu kujiamini na kuwa na uthubutu




Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka akizungumza katika mahafali hayo


Katikati ni meneja wa benki ya Posta Arusha,Ayub MKwawa akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu walioshika nafasi ya kuwa wanafunzi bora katika chuo hicho ambapo benki hiyo ya Posta iliwazawadia shilingi milioni moja kwa Kila mtu.

SINA WASIWASI NANYI CHAPENI KAZI-NAIBU WAZIRI MANYANYA

$
0
0



Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Mhandisi Stella Manyanya (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Roberta Feruzi Afisa Habari Mwandamizi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba wakati alipotembelea banda hilo mara baada ya ufunguzi wa Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANTRADE Dkt Ng’wanza Kamata na katikati ni Edwin Rutageruka Mkurugenzi Mtendaji wa TANTRADE.

................................................

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema hana wasiwasi na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kutokana na utendaji wao mzuri wa kazi.

Naibu Waziri Injinia Manyanya amesema hayo wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere.

"Sina wasiwasi na ninyi kwa sababu sijawahi kusikia malalamiko yoyote mkilalamikiwa kuhusu utendaji wenu hivyo nina imani na ninyi chapeni kazi" Alisikika akimuambia Roberta Feruzi Afisa Habari Mwandamizi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) wakati alipokuwa akipata maelezo ya taasisi hiyo katika banda hilo.

(TMDA) inashiriki maonesho hayo ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma zinazotolewa na taasisi hiyo muhimu nchini katika udhibiti wa ubora wa dawa na vifaa tiba katika kuhakikisha mlaji anapata huduma ya dawa zenye ubora na viwango viliyowekwa.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Mhandisi Stella Manyanya (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Roberta Feruzi Afisa Habari Mwandamizi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba huku akisoma kipeperushi wakati alipotembelea banda hilo mara baada ya ufunguzi wa Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere kushoto ni Sigifrid Mtey Afisa Uelimishaji Jamii TMDA.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Mhandisi Stella Manyanya (Mb) akisoma kipeperushi huku Roberta Feruzi Afisa Habari Mwandamizi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba akifurahia mara baada ya kusikia maneno mazuri kutoka kwa Naibu waziri hukusu TMDA kushoto ni Sigifrid Mtey Afisa Uelimishaji Jamii TMDA.

Maofisa wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Roberta Feruzi Afisa Habari Mwandamizi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba kulia na Sigifrid Mtey Afisa Uelimishaji Jamii wakiwa tayari kabisa kwa kupokea Naibu Waziri Injini Stella Manyanya.
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images