Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

RC MTAKA AIPONGEZA AGPAHI KWA KUTEKELEZA KIKAMILIFU MIRADI YA UKIMWI SIMIYU

0
0


RC MTAKA AIPONGEZA AGPAHI KWA KUTEKELEZA KIKAMILIFU MIRADI YA UKIMWI SIMIYU Inbox x Kadama Malunde 15:51 (5 hours ago) to Ahmad, Krantz, Cathbert, Khalfan, John, me, BINAGI, Bashir, BMG



Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ameipongeza Asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa kutekeleza kikamilifu miradi ya UKIMWI na kuwagusa wananchi moja kwa moja.

Mhe. Mtaka ametoa pongezi hizo Desemba 6,2019 kwenye kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa UKIMWI mkoani Simiyu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu.

Mtaka alisema AGPAHI ni taasisi maarufu mkoani Simiyu kutokana na kwamba imekuwa ikifanya vitu vinavyoonekana katik sekta ya afya mkoani humo kwa kusaidia wananchi.

“Nawapongeza sana AGPAHI kazi yenu inaonekana,kazi yenu haihitaji tochi ili kuona mnachofanya. Huwezi kuzungumzia mafanikio ya mkoa wa Simiyu kwenye sekta ya afya bila kuwataja AGPAHI”,alisema Mhe. Mtaka.

“Tunazo taasisi 14 zinazojishughulisha na masuala ya afya mkoani Simiyu. Hawa wadau 13 wangefanya walau robo tu ya kilichofanywa na AGPAHI,tungekuwa na maendeleo makubwa sana katika mkoa wetu na nchi kwa ujumla”,aliongeza Mtaka.

Mkuu huyo wa mkoa aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI inayoongozwa na Watanzania kwa kutekeleza miradi inayogusa maisha ya wananchi huku akizitaka taasisi zingine kuiga mfano wa AGPAHI.

“Wajumbe wa bodi ya AGPAHI mna ujasiri wa kutembelea miradi yenu kwenye mikoa kwa sababu miradi ipo.Nyinyi mna vitu,magari yenu pia yamekuwa yakitusaidia sana.Kuna baadhi ya taasisi hazina ujasiri wa kutembelea miradi kwa sababu hawana miradi,wengine kazi yao ni kugonga semina tu mwaka mzima.Hebu tufanye kazi zinazogusa wananchi tubadilishe mkoa huu”,alieleza Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka alisema serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote wa maendeleo mkoani humo ili katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Mtaka alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kutumia kondomu ili kupunguza maambukizi ya VVU huku akibainisha kuwa kuwa upo umuhimu wa kuvunja ukimya,vijana waelezwe ukweli kuhusu UKIMWI kwamba upo na unaua hivyo wachukue tahadhari.


Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Dkt. Edith Ngirwamungu alisema AGPAHI inatekeleza miradi yake ya UKIMWI kwa kushirikiana na serikali lengo likiwa ni kuhakikisha fedha zinazotolewa na wafadhili zinawanufaisha watanzania.

“Tunaushukuru mkoa wa Simiyu kwa ushirikiano mnaotupatia,tunajitahidi kufanya kazi kuwafikia wananchi,AGPAHI tunataka mtoto asizaliwe na maambukizi ya VVU,hivyo tutaendelea kushirikiana na serikali katika kutoa huduma za VVU na UKIMWI kwa wananchi”,alisema Dkt. Ngirwamungu.

Alisema AGPAHI inaendelea kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma za matunzo na tiba za VVU kwa watoto wachanga,vijana na watu wazima katika mikoa ya Simiyu,Mwanza,Mara na Shinyanga.

Meneja Miradi AGPAHI mkoa wa Simiyu Dkt. Julius Sipemba alisema AGPAHI inatoa huduma za VVU na UKIMWI kwa mkoa mzima wa Simiyu ambapo Mkoa wa simiyu una vituo 233 vya kutolea huduma za afya na 73 kati ya hivyo hupata usimamizi wa moja kwa moja kutoka AGPAHI. Alisema wagonjwa wanaopata huduma kwenye vituo 73 ni sawa na 95% ya wagonjwa wote walioko kwenye vituo 233. 
 
"AGPAHI inaboresha miundombinu kwa kujenga na kukarabati majengo, huduma za maabara kwa kununua madawa na vifaa 'iliwezesha maabara za wilaya kutoka nyota moja mpaka tatu', imetoa magari mapya kwa halmashauri 4 kati ya 6, imetoa pikipiki, msaada wa kuchunguza kifua kikuu, Saratani ya mlango wa kizazi",alieleza Dkt. Sipemba. Aliongeza kuwa AGPAHI pia inaajiri watoa huduma wa afya kwenye maeneo yenye uhitaji na inatoa mafunzo kwa watoa huduma kulingana na miongozo ya wizara ya afya.


Wakiwa mkoani Simiyu,Wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI wametembelea Kituo cha Tiba na Matunzo cha Hospitali ya wilaya ya Bariadi,kukutana na Mganga Mkuu wa mkoa wa Simiyu na Mkuu wa mkoa wa Simiyu pamoja na wadau wa VVU na UKIMWI mkoani Simiyu.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu Desemba 6,2019. Kushoto ni Mkurugenzi wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa,kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Dkt. Edith Ngirwamungu. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akiipongeza AGPAHI kwa huduma za VVU na UKIMWI inazotoa mkoani Simiyu.
Katibu Tawala mkoa wa Simiyu mhe. Jumanne Sagini akiipongeza AGPAHI kwa kutekeleza miradi inayogusa wananchi mkoani Simiyu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Dkt. Edith Ngirwamungu akizungumza katika kikao cha wadau wa afya na kueleza kuwa AGPAHI itaendelea kushirikiana na serikali katika kutoa huduma za VVU na UKIMWI.

Mkurugenzi wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akielezea shughuli zinazofanywa na AGPAHI mkoani Simiyu.

Awali Mkurugenzi wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa akiwashukuru viongozi wa mkoa wa Simiyu kwa kuendelea kushirikiana na AGPAHI katika kutekeleza miradi ya VVU na UKIMWI.

Meneja Miradi AGPAHI mkoa wa Simiyu Dkt. Julius Sipemba akiwasilisha mada kuhusu shughuli zinazofanywa na asasi ya AGPAHI mkoani Simiyu.

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja wakati wa kikao cha wadau wa afya mkoani Simiyu.

Mganga Mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt. Festo Dugange akichangia hoja wakati wa kikao cha wadau wa afya mkoani Simiyu.

Kikao kinaendelea.

Kijana James Leonard akielezea jinsi alivyonufaika na Klabu za watoto na vijana zinazohudumiwa na AGPAHI. Aliwataka vijana wajitokeze kupima afya zao na pale wanapobainika kuwa na maambukizi ya VVU basi watumie dawa za kufubaza makali ya VVU kwani kuwa na maambukizi ya VVU siyo mwisho wa maisha.
Minza Manyama akiwahamasisha wazazi na walezi kuwa wawazi kwa watoto waliozaliwa na maambukizi ya VVU. Alitumia fursa hiyo kuipongeza AGPAHI kwa huduma za VVU na UKIMWI inazoendelea kutoa kwa wananchi.

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI wakiwa kwenye kikao cha wadau wa afya mkoani Simiyu.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI wakiwa kwenye kikao cha wadau wa afya mkoani Simiyu.
Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya AGPAHI wakiwa nje ya kituo cha Tiba na Matunzo cha Hospitali ya wilaya ya Bariadi.
Picha ya pamoja uongozi wa mkoa wa Simiyu,AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu.

Picha ya pamoja uongozi wa mkoa wa Simiyu,AGPAHI na wanufaika wa miradi inayotekelezwa na AGPAHI mkoani Simiyu.

Picha ya pamoja uongozi wa mkoa wa Simiyu na AGPAHI.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

MKUU WA TAKWIMU ZA BEI ATOA TAKWIMU ZA BEI ZANZIBAR.

0
0

Mkuu wa Takwimu za Bei kutika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Abdul-Rahman Msham(katikati)akitoa takwimu za Bei ambapo imeonekana  kupanda Asilimia 3.1 kwa mwezi wa Novemba 2019 ukilinganisha na 2.4 kwa mwezi wa Octoba 2019 hafla iliofanyika ukumbi wa Mtakwimu mkuu mazizini Zanzibar.
Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Suleiman Simai Msaraka akifafanua baadhi ya maswala yalioulizwa  katika hafla ya utoaji wa  takwimu za Bei ambapo imeonekana  kupanda Asilimia 3.1 kwa mwezi wa Novemba 2019 ukilinganisha na 2.4 kwa mwezi wa Octoba 2019 hafla iliofanyika ukumbi wa Mtakwimu mkuu mazizini Zanzibar.

Meneja Uchumi Benki kuu ya Tanzania Tawi la Zanzibar Moto N’winganele Lugobi akijibu maswali yalioulizwa na Waandishi katika hafla ya utoaji wa  takwimu za Bei ambapo imeonekana  kupanda Asilimia 3.1 kwa mwezi wa Novemba 2019 ukilinganisha na 2.4 kwa mwezi wa Octoba 2019 hafla iliofanyika ukumbi wa Mtakwimu mkuu mazizini Zanzibar. 
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

MKUU WA MKOA WA KUSINI UNGUJA AMEKUTANA NA VIKUNDI VYA UJASIRIYAMALI MAKUNDUCHI

0
0
Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Haroun Ali Suleiman akitoa ufafanuzi kwa Vikundi vya Ujasiriamali vya kuweka na kukopa vya shehia ya Ng’anani na Kajegwa Makunduchi kuhusu kuvisaidia zaidi Vikundi hivyo.
Miongoni mwa Wanavikundi vya Ujasiriamali vya kuweka na kukopa vya shehia ya Ng’anani na Kajegwa Makunduchi Bimkubwa Bereka akisoma risala ya Vikundi hivyo katika hafla iliyofanyika Skuli ya Msingi Kajegwa Makunduchi.


Baadhi ya Wanavikundi vya Ujasiriamali vya kuweka na kukopa vya shehia ya Ng’anani na Kajegwa Makunduchi Wakimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Haroun Ali Suleiman huko Skuli ya Msingi Kajegwa Makunduchi.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi pesa Baadhi ya Wanavikundi vya Ujasiriamali vya kuweka na kukopa kutoka shehia ya Ng’anani na Kajegwa Makunduchi katika hafla iliyofanyika Skuli ya Msingi Kajegwa Makunduchi.

Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

……………………

Na Mwashungi Tahir

MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amevitaka vikundi vya wajasiriamali vya kuweka na kukopa shehia ya Ng’anani na Kajengwa Makunduchi kuwa na mashirikiano ili kufanya kazi zao kwa vizuri.

Aliyasema hayo huko Skuli ya Msingi Kajegwa Makunduchi Wilaya ya Kusini wakati wa kutambulishwa kwenye vikundi hivyo vya Ujasiriamali vya kuweka na kukopa na kuwataka kuendelea kufanya kazi zao kwa kuwa na mashirikiano ili kupata ufanisi zaidi.

Amesema iwapo watakuwa na mashirikiano katika utendaji wao wa kazi kutaweza kuwapatia fursa za kuongeza kipato chao na kujikwamua kimaisha pia kuacha kuwa tegemezi kwani akinamama ndio wenye mipango mingi ya maendeleo. Aidha amesema wajasiriamali wana uwezo mkubwa wa kubadilisha maisha yao kwa kazi zao wanazozifanya hadi kujikuta wanakuwa matajiri , kwani matajiri wote wameanza biashara ndogo ndogo mpaka wamefika katika hali nzuri.

“Wengi walikuwa kipato chao cha chini na wameanza kufanya biashara ndogo ndogo hadi sas wamekuwa matajiri wakubwa hivyo msivunjike moyo”, aliwaasa Mkuu wa Mkoa huyo wa Kusini. Pia amesema Serikali imeweka Sera katika Ilani ya Utekelezaji wa CCM kwa vikundi vya ujasiriamali na kupatiwa mikopo ya kuweka na kukopa kwa lengo la kujiletea maendeleo.

Ayoub ameahidi kuvisaidia vikundi hivyo vya wajasiriamali vya kuweka na kukopa kama vile mabusati, kuwandalia mafunzo ya ujasiriamali ili waweze kufanya shughuli zao zaidi na kuwa na taaluma nzuri na kuwahimiza wajitahidi kurudisha mikopo kwa haraka ili mitaji iweze kukua kwa vizuri.

“Nawaombeni sana mujitahidi kurejesha mikopo kwa wakati ili matarajio yenu yaweze kufikia katika kujikwamua kimaisha”, alisema Ayoub. Jumla ya vikundi hivyo ni 5 ambavyo amewapa sh laki tano kwa kila kikundi ambapo vikundi hivyo ni Kubihi moyo, Tuwe wakweli , Fikira zetu , Anacho hapokonyeki na Tuaminiane kwa lengo la kuendeleza kazi zao.

Nae Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Haroun Ali Suleiman amesema vikundi hivyo vya akinamama viko katika hali nzuri na kuvitaka vizidi kuimarika ili viwe mifano kwa vikundi vyengine. Amesema atazidi kuvisaidia ili vizidi kuwa imara na kuwataka wawe mstari wa mbele kutoa taaluma waliyonayo kwa wale wanaotaka kupotea katika maadili yao ndani ya Mkoa huo.

Amewataka wazidi kuendelea kupendana na kila kikundi amewazawadia sh Laki tano kwa kila kikundi kwa lengo kujiimarisha zaidi. Kwa upande wa msoma risala wa vikundi hivyo Bimkubwa Bereka Mbaraka alisema kila kikundi kina wanachama 30 na wanafarijika kwa kupata muongozo mzuri kwa Mwakilishi wao na kumshukuru kuwa muadilifu kwao.

Alisema kwa upande wa mafanikio wameweza kuunganika na kuwa kitu kimoja katika harakati zote za kijamii. Pia alielezea changamoto zao zinazowakabili ni pamoja na wanachama kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati , kuwa na uhaba wa elimu ya ujasiriamali na kuendeha vikundi na uwekaji wa kumbukumbu kwa mfumo wa kitaaluma.

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA KIKOMINISTI CHA VIETNAM BUNGENI JIJINI DODOMA

0
0

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimvalisha shuka la kimasai ambayo ni moja ya zawadi aliyompatia Mjumbe wa Kamati Kuu ya Siasa, Katibu wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Organaizesheni ya Chama cha Kikoministi cha Vietnam, Mhe. Pham Minh Chinh alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Siasa, Katibu wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Organaizesheni ya Chama cha Kikoministi cha Vietnam, Mhe. Pham Minh Chinh alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akipokea zawadi ya chungu cha kuwekea maua kutoka kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Siasa, Katibu wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Organaizesheni ya Chama cha Kikoministi cha Vietnam, Mhe. Pham Minh Chinh alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na Wajumbe wa kamati kuu ya Chama cha Kikoministi cha Vietnam walioongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Mhe. Pham Minh Chinh (wapili kulia) walipotembelea ukumbi wa Bunge leo Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiongozana na Wajumbe wa kamati kuu ya Chama cha Kikoministi cha Vietnam walioongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Mhe. Pham Minh Chinh (wa pili kulia) wakati wanatoka katika ukumbi wa Bunge leo Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wanne kulia) katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati kuu ya Chama cha Kikoministi cha Vietnam walioongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Mhe. Pham Minh Chinh (katikati) nje ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.

MAZINGIRA YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI YABORESHWA ZAIDI

0
0
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akizungumza katika moja ya mikutano ya mashauriano kati ya serikali, wawekezaji na wafanyabiashara iliyofanyika katika Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam. 
 
Na. Edward Kondela

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema serikali ya awamu ya tano imefanya kazi kubwa ya kuandaa mazingira ya biashara za ndani ziweze kufanya vizuri zaidi.

Akizungumza jana (06.12.2019) wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya serikali, wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Ulega amesema serikali imeweza kudhibiti matumizi ya fedha kununua nyama, maziwa na samaki kutoka nje ya nchi ili kutosheleza soko la ndani.

Akifafanua katika kikao hicho ambacho kimeongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki ambaye amekuwa mwenyekiti katika mikutano ya namna hiyo iliyofanyika pia katika mikoa ya Morogoro na Pwani, Mhe. Ulega amesema serikali imekuwa ikitumia takriban Shilingi Bilioni 10 kuagiza nyama kutoka nje ya nchi, Shilingi zaidi ya Bilioni 100 kuagiza samaki na zaidi ya Shilingi Bilioni 50 kuagiza maziwa, kitendo ambacho kwa sasa serikali haitumii fedha hizo tena kuagiza bidhaa hizo kutoka nje ya nchi.

Katika mkutano huo ambao umehusisha mawaziri na naibu mawaziri kutoka zaidi ya wizara 10, Mhe. Ulega amesema serikali imeendelea kuweka mazingira shindani ili kutoa fursa ya uwekezaji katika sekta ya ufugaji na uvuvi, hatua ambayo katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano Benki ya Kilimo (TADB) imeweza kupata maombi ya mikopo ya zaidi ya Shilingi Bilioni 90 na kufanikiwa kusajili na kutoa mikopo ya Shilingi Bilioni 25.3 ambapo Shilingi Bilioni 23 kwa ajili ya sekta ya mifugo na takriban Shilingi Bilioni Mbili kwa sekta ya uvuvi ambayo miaka iliyopita haikuwahi kukopeshwa kiasi chochote cha fedha ilhali sekta ya mifugo iliwahi kukopeshwa kiasi kisichozidi Shilingi Bilioni Tisa pekee.

Naibu Waziri huyo ametoa fursa kwa wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaotaka kuwekeza katika sekta ya uvuvi kupitia ufugaji wa samaki, ambapo hitaji la samaki kwa mwaka ni Tani 800,000 wakati Tanzania inaweza kuzalisha wastani wa Tani 400,000 hadi 450,000 aidha amewataka pia kuwekeza katika viwanda vya maziwa, nyama na ngozi.

Katika kuhakikisha wanapata miongozo sahihi ya uwekezaji Naibu Waziri Ulega amewataka wadau kutumia Dawati la Sekta Binfasi lililo chini ya wizara hiyo, ili kufahamu juu ya kanuni, miongozo na tozo wakati wa uwekezaji wao.

MKOA WA KUSINI UNGUJA UNATARAJIA KUKUSANYA ZAIDI YA CHUPA 1003 ZA DAMU SALAMA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud akizungumza na Waandishi wa habari huko Ofisini kwake Tunguu kuhusu zoezi la uchangiaji wa Damu Salama litalofanyika Bungi Miembe mingi Mkoa wa Kusini Unguja.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud akizungumza kuhusu zoezi la uchangiaji wa Damu Salama litalofanyika Bungi Miembe mingi Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrissa Kitwana akimkabidhi Mifuko ya Saruji 10 kwa niabaya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud  Mwenyekiti wa Maskani ya Ayoub Muhamed Mahmoud ya Uzi Ng’abwa Talib Khamiss Issa huko Ofisi za Mkuu wa Mkoa huyo Tunguu.
Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
…………………….

Na Mwashungi Tahir  – Maelezo.      
    
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud amesema mkoa huo unatarajia  kukusanya zaidi ya chupa elfu moja na tatu  za damu salama katika zoezi la uchangiaji damu linalotarajiwa kufanyika tarehe 8 mwezi huu bungi miembe mingi.

Akizungumza na Waandishi wa habari huko Ofisini kwake Tunguu wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu zoezi hilo ambalo litaanza na matembezi kuanzia Kibele hadi Bungi Miembe mingi alisema hatua hiyo imefauatia kuwepo kwa upungufu mkubwa wa damu salama katika kitengo cha damu salama hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya watu walio wengi hasa akina mama na watoto.

Amesema  maisha ya mwanadamu yanategemea damu hivyo ni vyema kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu kwa lengo la kupata radhi za allah kutokana na kuokoa maisha ya watu. Aidha amewaomba viongozi mbali mbali wakiwemowa kidini, siasa na wengine kwa ujumla kwani hilo  linawahusu watu wote na siola watu maalum.  

“Lengo la kutoa Damu salama halilengi kwa watu maalumu litafanyika kwa Makundi yote yakiwemo,Vyama vya siasa, Dini, na Makabila na sio suala la siasa”alisema Ayoub.Vile vile alisema Wanawake 50 wataojitokeza kutoa damu mwanzo atawazawadia zawadi mbali mbali ikiwepo Chupa za chai na Kanga na Vijana atawazawadia Fulana na Mwamvuli.

Hata hivyo alisema dhamira ya Bonaza hilo ni kuhakikisha damu salama inapatikanwa kwa wingi katika Mkoa huo ili kuondosha changamoto zinazoweza kujitokeza hasa kwa kina mama.

 Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrissa Kitwana alikabidhi Mifuko ya Saruji 10 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud kwa ajili ya ujenzi wa Maskani ya Ayoub iliopo Uzi Ng’abwa iliopo Mkoa wa Kusini Unguja.

KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI YASEMA HAKUNA MELI HATA MOJA, INAYOJIENDESHA KWA HASARA

0
0


 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli(MSCL) Eric Hamissi akizungumza leo Desemba 7,2019 kuhusu meli zao zote nne zinavyojiendesha kwa faida baada ya kuweka mfumo mzuri wa kusimamia mapato yatokanayo na utoaji huduma ya usafiri wa meli.




Baadhi ya meli zinazotoa huduma ya usafiri katika bandari ya Ziwa Victoria jijini Mwanza.



Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii-Mwanza


OFISA Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli(MSCL) Eric Hamissi amesema kuwa kampuni hiyo kwa sasa meli zake zote nne ambazo zinaendelea kutoa huduma kati ya meli 14 walizonazo zinajiendesha kwa faida.

Na kwamba moja ya mkakati walionao ni kuhakikisha wanajipambanua kama kampuni ambayo itakuwa inatoa huduma zake kibiashara na huko mbele ya safari matarajio yao ni kutoa gawio kwa Serikali.

Ameyasema hayo leo Desemba 7,mwaka 2019 akiwa ofisini kwake jijini Mwanza wakati akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari nchini waliopo kwenye ziara ya

kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari(TPA) katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano.

"Meli zetu zote nne ambazo ni Mv.Wimbi, Mv. Sangara, Mv. Umoja na Mv. Clarias zote zinajiendesha kwa faida, hakuna hata meli moja ambayo inaendeshwa kwa hasara.Tumeweka mkakati madhubuti wa kuhakikisha hatupati hasara na kwa kweli hili limewezekana".

"Ni mtarajio yetu kwa muelekeo huu nasi tutakuja kutoa gawio hata kama la Sh.milioni 20 lakini tuonyeshe kutambua kazi nzuri ambayo inafanywa na Rais wetu mpendwa katika kuimarisha usafiri wa majini".Amesema Hamissi.

Amesema kuwa chini ya Serikali ya Awamu ya Tano Kampuni hiyo mbali ya meli zake kutojiendesha kwa hasara imefanikiwa pia kuimarisha ukusanyaji mapato kwa kutumia mfumo wa ulipaji kwa njia ya kieletroniki sambamba na kudhibiti mianya yote iliyokuwa inasababisha fedha za kampuni kupotea.

Amesisitiza kuwa tayari wameshafunga mafumo wa kukusanya mapato wa kielekroniki katika Bandari za Mwanza na Nansio Ukerewe ambapo sasa yamepanda kwa asilimia 50.

"Si hilo tu kwa kushirikiana na TPA sasa kazi yetu imekuwa na ufanisi mkubwa, tumeongeza mapato.





Pia tumeshafunga mfumo wa kielekroniki sambamba na utoaji elimu kwa watumiaji wetu"

Amesema kila shilingi inayoingia wanaiona katika mtandao na hakuna kificho tena kwani wameweka uwazi na hivyo kila kinachoingia kinaonekana.

Ameongeza kutokana na mafanikio ambayo wanayo wanafikiria kuwa na meli mpya ya Tanzania katika Bahari ya Hindi ambayo itatoa huduma ya kusafirisha mizigo kati ya Tanzania na nchi za Mashariki ya mbali pamoja na nchi ya Comoro.

Wakati huo huo amesema kuwa usafiri wa meli unapokuwa imara maana yake ni kuimarisha uchumi wa nchi, hivyo mikakati inayoendelea hivi sasa nchini kutasaidia kujenga uchumi imara kutokana na kuendelea kuboreshwa kwa miundombinu ya meli nchini.

"Kutokana na umuhimu na urahisi wa usafiri wa meli pia Serikali ya Rais Magufuli, imetenga Shilingi bilioni 16 kwa ajili ya kujenga chelezo kubwa ambayo itabeba meli kubwa yenye uwezo wa tani 4,000".Amesema Hamissi

Amesema kwa muda mrefu ukarabati wa meli haujafanyika ambapo kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 1960 kwa meli ya Mv. Victoria.




TVMC YAKUTANA NA WADAU KUJADILI UTEKELEZAJI WA MTAKUWWA SHINYANGA Inbox x

0
0


Wadau wanaotetea haki za wanawake na watoto wametakiwa kutimiza wajibu wao ili kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatokomezwa katika jamii.


Rai hiyo imetolewa leo Jumamosi Desemba 7,2019 na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania (TANLAP), Christina Kamili wakati wa kikao cha wadau wa haki za wanawake na watoto kilichoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC). Kikao hicho kilicholenga kupata mrejesho kutoka kwenye jamii juu ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kupitia kamati zilizoundwa na TVMC katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Kamili ambaye ni Mwanasheria alisema ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ni vyema kila mmoja akatimiza wajibu wake na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani wanaotenda ukatili wapo katika jamii.

“Kila mmoja akisimama bila kuwa na huruma,akasimamia sheria kama inavyotakiwa hizi tabia za ukatili dhidi ya wanawake na watoto zitakomeshwa.Hawa wanaofanya vitendo vya ukatili wapo katika jamii,wapo katika familia,kinachotakiwa ni kila mtu atimize wajibu wake”,alisema.

“Tunataka kuhakikisha ustawi wa mtoto na mwanamke unalindwa.Tunaomba pia utaratibu wa kuendesha kesi za jinai ufuatwe,tuache huruma kwenye kesi za jinai.Tukifanya mazoea hatumaliza kesi hizi.Kama kesi zimeharibiwa kuanzia mwanzo hata mwisho wa kesi pia utakuwa mbaya”,aliongeza Kamili.

Naye Mkurugenzi wa TVMC,Mussa Jonas Ngangala alisema changamoto iliyopo ni kwamba kamati zimeundwa lakini hazikutani kama mwongozo unavyoelekeza kwa madai kuwa hakuna pesa kwa ajili ya kuendesha shughuli za MTAKUWWA ngazi ya kata.

Katika hatua nyingine Ngangala alisema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake bado vinaendelea kujitokeza kwa sababu ya imani potofu iliyojengeka kwenye jamii.

"Tufichue uovu na asiyewajibika achukuliwe hatua ili kumaliza vitendo vya ukatili katika jamii ikiwemo kuozesha watoto katika umri,kutumikisha watoto,kutopeleka watoto wa kike shule. Wengine wanabaka watoto ili wapate mali kutokana na imani za kishirikina. Vitendo hivi kavikubaliki",alisema Ngangala.

Kikao hicho kimehudhuriwa na maafisa ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii watendaji wa kata,maafisa wa polisi kutoka dawati la jinsia na watoto,mahakimu wa mahakama za mwanzo,maafisa elimu na wadau wengine ikiwemo Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) linalohusika na utetezi wa haki za wanawake,watoto na ujenzi wa tapo ya wanawake nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC),Mussa Jonas Ngangala akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa haki za wanawake na watoto kilicholenga kupata mrejesho kutoka kwenye jamii juu ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kupitia kamati zilizoundwa na TVMC katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC),Mussa Jonas Ngangala akizunnguza katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania (TANLAP),Christina Kamili akizungumza katika kikao cha wadau wa haki za wanawake na watoto kilicholenga kupata mrejesho kutoka kwenye jamii juu ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kupitia kamati zilizoundwa na TVMC katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania (TANLAP), Christina Kamili akiwasisitiza wadau wa haki za wanawake na watoto kutokuwa na huruma panapotokea vitendo viovu ikiwa ni pamoja kufuata taratibu za kuendesha kesi za jinai.

Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.

Afisa Ustawi wa Jamii kata ya Didia, Felister Melli akitoa mrejesho kuhusu shughuli za utekelezaji wa MTAKUWWA katika kata hiyo. Alisema changamoto iliyopo sasa ni wanaume wengi wanatelekeza familia zao.
Afisa Mtendaji kata ya Samuye, Melchades Oswald Kamuzora akitoa mrejesho kuhusu utekelezaji wa MTAKUWWA katika kata yake. Alisema kesi za mimba kwa wanafunzi zimepungua katika kata hiyo.
Wadau wakiwa ukumbini.
Afisa Mtendaji kata ya Tinde, Latifa Mwendapole akitoa mrejesho kuhusu utekelezaji wa MTAKUWWA katika kata yake.
Afisa Elimu kata ya Masengwa,Juma Chiamba akichangia hoja katika kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya jamii kata ya Samuye,Magai Magai akichangia hoja katika kikao hicho.
Afisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri ya Shinyanga ,Elizabeth Mweyo akichangia hoja katika kikao hicho.


Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Shinyanga,Victoria Maro akielezea namna ya kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.



Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, unaotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT), Glory Mbia akichangia hoja katika kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Ilola,Bandi Sospeter ambaye pia ni Msaidizi wa Kisheria akichangia hoja kwenye kikao hicho.


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

EURO MILIONI 140 ZA ACP KUWANUFAISHA WAKULIMA WA MAHINDI NA KOROSHO

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi.
 
Jumla ya Euro milioni 140 zimetengwa ili kuwanufaisha wakulima wa mazao ya korosho na mahindi katika mpango maalum wa kutoa mikopo,kujenga uwezo katika uzalishaji,masoko,uwekezaji na kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao hayo kwa wakulima wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific jambo litakalosaidia kupunguza umasikini na njaa katika nchi hizo.

Akizungumza katika mkutano wa 110 wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific uliofunguliwa na makamu wa rais wa Kenya Mhe. William Ruto jijini Nairobi nchini Kenya,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema Tanzania imetoa hoja ya kutaka mazao ya korosho na mahindi kuongezwa katika mazao ya vipaumbele kwa nchi za ACP jambo ambalo limeridhiwa na kuungwa mkono nan chi za Benin na Burkinafaso.

Ameongeza kuwa kukubalika kwa hoja hiyo iliyowezesha mazao hayo kuingizwa katika moja ya mazao ya vipaumbele kwa nchi za ACP Serikali ya Tanzania itajipanga kupitia wizara husika ili kuandaa mapendekezo ya namna ambayo wakulima wa Tanzania watanufaika na program hiyo sambamba na mazao mengine yakiwemo pamba,miwa na kahawa.

Aidha,Waziri Kabudi amesema kuwa kupitia program hiyo maalum ya ACP wakulima wa korosho na mahindi watawekewa mikakati ya kusaidiwa katika uzalishaji,kutafutiwa masoko na mbinu za uwekezaji sanjari na kuongeza mnyororo wa thamani na kusaidiwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayoweza kuathiri uzalishaji wa mazao hayo.

Program hiyo ya ACP imetajwa kuwa mkombozi kwa nchi hizo katika jitihada za kupunguza umasikini na ukosefu wa chakula kwa kuwa unalenga zaidi wakulima wa chini na wa kati hususani wanawake na vijana.

Mazao mengine yaliyopo katika mpango wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific kwa muda mrefu sasa licha ya kuwa Tanzania haijatumia fursa hiyo kikamilifu ni pamoja na Pamba,kahawa na cocoa kwa nchi nyingi za Afrika nan dizi,miwa,kava na raum kwa nchi za Caribbean na Pacifiki.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Kenya Balozi Pindi Chana amesema Ubalozi wa Tanzania Nchini humo unafuatilia kwa ukaribu mkutano huo kwa kuwa utatoa fursa mbalimbali ambazo zitaiwezesha Tanzania kunufaika nazo hususani kupitia mazao ya kilimo jambo ambalo litasaidia kupunguza umasikini na ukosefu wa ajira hususani kwa akina mama na vijana.

Shibuda atoa neno ripoti uchaguzi Serikali za Mitaa

0
0
Na Ripota Wetu-Michuzi TV
-DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, John Shibuda amesema kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni fursa ya kujenga mwamko mpya wa kusahihisha makosa ili yasiendelee kutokea kwenye chaguzi zijazo.

Shibuda ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Chama cha Ada Tadea, ameyasema hayo katika taarifa yake wakati akipokea taarifa ya ripoti ya uangalizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji  iliyofanywa na asasi ya kirai ya Tafeyoco.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Novemba 24, 2019 vyama vya upinzani vya Chadema, CUF, ACT- Wazalendo, UPDP na Chaumma vilisusia kushiriki kutokana na kile walichodai kutoridhishwa na mwenendo mzima wa uchaguzi huo huku vyama vya NRA, DP, AAFP na TLP vikishiriki.

Miongoni mwa mambo yaliyojitokeza katika mchakato ni asilimia kubwa ya wagombea wa vyama vya upinzani kuenguliwa baada ya kukosa sifa huku baadhi ya waliochukua fomu wakijikuta wakishindwa kurudisha baada ya ofisi za Serikali kufungwa.

Akizungumza huku akitumia nahau na methali, Shibuda alisema kuwa ukweli uliopo Taifa lina fadhaa ya mgogoro wa kuhusu kuwepo kwa kasoro ya uborongwaji na uparaganishwaji wa ndiyo na wa siyo kwa kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Kwa hiyo sasa, msemo wa hakuna chema kisicho na kasoro umetua vyema katika uchaguzi wa serikali za mtaa wa mwaka huu. Kwa kutambua kwamba leo kusema uchaguzi wa serikali za mitaa haukuwa na kasoro ni sawa na kujaribu kuficha kaa la moto kwenye mfuko wa kanzu.”

“Kwa kutambua wadau wa vyama vya siasa na umma wa wakereketwa wa masuala haya wana fikra ya taftishi za kusaka suluhu, suluhu inayohitajika ni kujenga utulivu wa fikra kwa uwazaji wa kuelekea katika dira ya msimu wa duru za siasa za uchaguzi wa mwakani,” amesema Shibuda.

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Vyama  vya Siasa, alipokea maoni ya Tafeyoco, ambapo alisema ni sehemu ya taarifa itakayoondoa ukomo na ulegevu kwa mambo ya mtu mwenye taarifa za kutaka kujua asiyoyajua.

“Msema kweli ni mpenzi wa Mungu sasa tukiri ndani ya jamii yetu pana kuna gumzo za kimya kimya na mijadala ya uwazi ya kuhusu fikra za kutangatanga za hoja ya kutaka kujua endapo kuna uongo au ukweli unaogusa changamoto za Serikali za mtaa,” amesema Shibuda.

Akiwasilisha ripoti ya uangalizi wa uchaguzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tafeyoco, Elvice Makumbo alisema miongoni mwa mambo waliyoyabaini ni baadhi ya vyama vya siasa kushinda kushirikiana na wagombea wa vyama.

Hata hivyo alipongeza vyama vilivyoshiriki uchaguzi huo na kusema kuwa sasa ni vema Serikali irekebishe kasoro zilizojitokeza ili sisijirudie wakati mwingine.

SERIKALI AWAMU YA TANO KUTUMIA BILIONI 152/- KUIMARISHA HUDUMA ZA MELI KATIKA MAZIWA MAKUU

0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii-Mwanza 
SERIKALI ya Awamu ya Tano imeamua!Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Serikali kutenga Sh.bilioni 152 kwa ajili ya kutekeleza miradi minne ikiwemo ya kukarabati meli kubwa, kujenga meli mpya pamoja na chelezo ya kisasa. 

Akizungumza leo Desemba 7,mwaka 2019 jijini Mwanza, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Eric Hamissi amesema chini ya Rais Dk.John Magufuli ambaye amekuwa na maono ya kuifikisha Tanzania mbali kiuchumi na kimaendeleo, kuna miradi mikubwa minne inayoendelea katika kuboresha huduma za meli nchini. 

"Tangu Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha sekta ya meli inakuwa bora na imara.Hivyo kwa mara ya kwanza Serikali ndani ya kipindi kifupi imetenga Sh.bilioni 152 kwa ajili ya kutekeleza miradi minne ya kujenga meli mpya na kukarabati meli nyingine za zamani,"amesema. 

Amefafanua zaidi amesema Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Eric Hamissi kwa sasa wana meli 14 na boti moja ambazo zipo katika Maziwa Makuu ya Victoria, Nyasa na Tanganyika.Amezitaja meli hizo ni Mv.Wimbi, Mv. Sangara, Mv. Umoja na Mv. Clarias. 

"Tuna meli nne ambazo zinafanyakazi kwa sasa ambazo ni Mv. Wimbi, Mv. Sangara, Mv. Umoja na Mv. Clarias. Pia tuna wakandarasi ambao sasa wanaendelea na kazi ikiwamo ujenzi wa chelezo ambapo Kampuni ya Six Engine na Saekyung Construction zinaendelea na kazi hiyo ambayo kwa sasa imefika zaidi ya asilimia 68. 

"Ujenzi meli mpya ya Mv. Mwanza Hapa Kazi Tu, inafanywa na Kampuni ya Gas Entec na Kangnam Corporation za nchini Korea Kusini ambapo wanafanya kazi hii kwa kushirikiana na Suma JKT na ukarabati wa meli za zamani kazi hii inafanywa na Kampuni ya KTM ambayo inakarabati meli mbili za Mv. Victoria na Mv. Butiama," amesisitiza Hamissi. 

Wakati huo huo amesema pindi meli ya Mv. Mwanza itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200, magari madogo 20 na malori makubwa matatu. "Meli hiyo itakuwa na uzito wa tani 3,500 huku chelezo ya kisasa inayojengwa ikiwa na uwezo wa kubeba tani 4,000.Ujenzi wa chelezo hiyo ya kisasa ni sehemu ya miradi ya kuboresha huduma za meli." 

Kuhusu Kampuni hiyo amesema awali hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) mwaka 1997.Hata hivyo miaka michache baadae Serikali ikaingia katika mchakato wa kutaka kulibinafsisha Shirika. 

Hata hivyo amesema kuwa Kampuni hiyo kwa nyakati tofauti imepita katika kipindi kigumu na ilipofika mwaka 2015, Rais Magufuli alipokuwa akiomba ridhaa ya Watanzania aliahidi kufufua meli na kuleta meli mpya katika maziwa yote makuu nchini. "Hivyo ili kuhakikisha ahadi hiyo na nyingine zinatekelezwa Serikali ilimua kutoa jukumu hilo kwa kampuni yetu na sasa tumesimama na tunaendelea kutoa huduma".
 Meli ya MV.Victoria ikiwa katika chelezo kwa ajili ya kukarabatiwa ikiwa ni mkakati wa Serikali kuboresha usafiri wa meli katika Ziwa Victoria.
 Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Eric Hamissi akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mikakati mbalimbali inayoendelea katika kuimarisha usafiri wa meli nchini. 
 Meli ya MV.Victoria ikiendelea kukarabatiwa  ambapo inatarajia kukamilika mwakani ili kuanza kutoa huduma.


 Ujenzi wa eneo la chelezo inayojengwa katika eneo la Bandari ya Ziwa Victoria Mjini Mwanza ukiendelea. Inaelezwa Rais Dk.John Magufuli kesho Desemba 8,2019 anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo.
Baadhi ya mafundi wanaotengeneza meli ya MV.Victoria wakiendelea na majukumu yao.
Picha zote na Said Mwishehe

KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI YASEMA HAKUNA MELI HATA MOJA INAYOJIENDESHA KWA HASARA

0
0



Baadhi ya meli zinazotoa huduma ya usafiri katika bandari ya Ziwa Victoria jijini Mwanza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli(MSCL) Eric Hamissi akizungumza leo Desemba 7,2019 kuhusu meli zao zote nne zinavyojiendesha kwa faida baada ya kuweka mfumo mzuri wa kusimamia mapato yatokanayo na utoaji huduma ya usafiri wa meli.
 
Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii-Mwanza

OFISA Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli(MSCL) Eric Hamissi amesema kuwa kampuni hiyo kwa sasa meli zake zote nne ambazo zinaendelea kutoa huduma kati ya meli 14 walizonazo zinajiendesha kwa faida.

Na kwamba moja ya mkakati walionao ni kuhakikisha wanajipambanua kama kampuni ambayo itakuwa inatoa huduma zake kibiashara na huko mbele ya safari matarajio yao ni kutoa gawio kwa Serikali.

Ameyasema hayo leo Desemba 7,mwaka 2019 akiwa ofisini kwake jijini Mwanza wakati akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari nchini waliopo kwenye ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari(TPA) katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano.

"Meli zetu zote nne ambazo ni Mv.Wimbi, Mv. Sangara, Mv. Umoja na Mv. Clarias zote zinajiendesha kwa faida, hakuna hata meli moja ambayo inaendeshwa kwa hasara.Tumeweka mkakati madhubuti wa kuhakikisha hatupati hasara na kwa kweli hili limewezekana.

"Ni mtarajio yetu kwa muelekeo huu nasi tutakuja kutoa gawio hata kama la Sh.milioni 20 lakini tuonyeshe kutambua kazi nzuri ambayo inafanywa na Rais wetu mpendwa katika kuimarisha usafiri wa majini,"amesema Hamissi.

Amesema kuwa chini ya Serikali ya Awamu ya Tano Kampuni hiyo mbali ya meli zake kutojiendesha kwa hasara imefanikiwa pia kuimarisha ukusanyaji mapato kwa kutumia mfumo wa ulipaji kwa njia ya kieletroniki sambamba na kudhibiti mianya yote iliyokuwa inasababisha fedha za kampuni kupotea.

Amesisitiza kuwa tayari wameshafunga mafumo wa kukusanya mapato wa kielekroniki katika Bandari za Mwanza na Nansio Ukerewe ambapo sasa yamepanda kwa asilimia 50. "Si hilo tu kwa kushirikiana na TPA sasa kazi yetu imekuwa na ufanisi mkubwa, tumeongeza mapato. Pia tumeshafunga mfumo wa kielekroniki sambamba na utoaji elimu kwa watumiaji wetu".

Amesema kila shilingi inayoingia wanaiona katika mtandao na hakuna kificho tena kwani wameweka uwazi na hivyo kila kinachoingia kinaonekana.

Ameongeza kutokana na mafanikio ambayo wanayo wanafikiria kuwa na meli mpya ya Tanzania katika Bahari ya Hindi ambayo itatoa huduma ya kusafirisha mizigo kati ya Tanzania na nchi za Mashariki ya mbali pamoja na nchi ya Comoro.

Wakati huo huo amesema kuwa usafiri wa meli unapokuwa imara maana yake ni kuimarisha uchumi wa nchi, hivyo mikakati inayoendelea hivi sasa nchini kutasaidia kujenga uchumi imara kutokana na kuendelea kuboreshwa kwa miundombinu ya meli nchini.

"Kutokana na umuhimu na urahisi wa usafiri wa meli pia Serikali ya Rais Magufuli, imetenga Shilingi bilioni 16 kwa ajili ya kujenga chelezo kubwa ambayo itabeba meli kubwa yenye uwezo wa tani 4,000,"amesema Hamissi

Amesema kwa muda mrefu ukarabati wa meli haujafanyika ambapo kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 1960 kwa meli ya Mv. Victoria.


IN MEMORIAL ROSE SHOMARI

0
0
Today is 14 years since you departed to the Lord. As this day comes around it will be always remembered that a heart of Gold stopped beating, two shining eyes at rest. God broke our hearts to prove he only takes the best. Not a day goes by when you are not loved and missed.
 
 You are held in our hearts forever. You will always be remembered by your kids Franco, Terry, Sunday, Lulu and grand kids as well as the Shomari clan and many others. We thank God for your wonderful care, parenthood, advice and your great smile. May the Lord rest your soul in eternal bliss. Till memory fades and life departs, you live forever in our hearts. Amen.

SERIKALI KUWALINDA WAWEKEZAJI WALIOAMUA KUANZISHA VIWANDA NCHINI

0
0
SERIKALI ya Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mikakati mahsusi ya kuimarisha na kuendeleza sekta ya viwanda ili kuongeza ajira na kuwapunguzia umaskini kwa wananchi wake huku kusisitiza kuendelea kuwalinda wawekezaji wote wanaoamua kuanzisha viwanda hapa nchini kwa kuwapatia vivutio maalumu ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira muafaka ya uwekezaji na biashara.

Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Mhandisi Stella Manyanya (Mb) wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere.

“Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa bidhaa zisizo na viwango na bandia hazitakuwa na nafasi katika soko la Tanzania, hivyo ni muhumi kuhakikisha bidhaa zinazoingia nchini zinakuwa na viwango vya kimataifa ili kuvipa changamoto viwanda vya ndani kuzalisha bidhaa zenye ubora” amesema Mhe Mhandisi Manyanya

Ameendelea kuwaomba wawekezaji kuendelea kuwekeza Tanzania kwasababu ina maeneo mazuri ya kujenga viwanda, fursa za malighafi na kuna walaji wa kutosha kwasababu Watanzania wapo takriban million hamsini na tano hivyo kuna soko kubwa la bidhaa zao.

Ameendelea kusema kuwa, serikali ya Tanzania imeshatambua na kufahamu umuhimu wa mazingira wezeshi kwa mfanyabiashara na mwekezaji wa viwanda, imechukua jukumu la kuweka miundo mbinu wezeshi kwa kuhakikisha kwamba umeme unapatikana."Ndio maana tunajenga mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji takriban megawat 2500 lakini vilevile kuna umeme ulioongezwa pale Kinyerezi na kuchangia ongezeko la takriban megawatt 1600 na kufanya nchi yetu kuwa na umeme wa kutosha hivyo kiwanda kinaweza kuanzishwa sehemu yoyote."

Pia amesema Serikali imeendelea kuondoa mikanganyiko ya kodi na mikanganyiko ya taasisi za udhibiti kwa kuhakikisha kuwa inapunguza kodi na mpaka sasa kodi takribani 168 zimeondolewa kwaajili ya kuweka mazingira wezeshi na Mamlaka nyingi kama vile Taasisi ya Tume ya Ushindani (FCC) na nyingine zote zinazohusika na ukaguzi zinazingatia bidhaa zinazoingia nchini zinakuwa bidhaa halisi na haziui soko la ndani.

Ameongeza kwa kueleza kama ambavyo ilivyo kwenye dira ya Taifa, ifikapo 2025 tunatamani kuona Tanzania inafikia uchumi wa kati lakini kufikia hapo ni pale taasisi za serikali zitakapokuwa na msimamo mmoja kuhakikisha kwamba tunaisaidia sekta binafsi ambao ndio watekelezaji na watendaji katika uzalishaji na kuwezesha upatikanaji wa uzalishaji wenye tija na kufanya bidhaa zetu ziwe na bei zinazoweza kumfikia mlaji na hivyo kukuza uchumi wetu.

Ametoa rai kwa wadau na washiriki wanaoonesha bidhaa zao kuhakikisha kila wanachozalisha wanazingatia ubora unaostahili na amelitaka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Viwanda (UNIDO) kufadhili mradi wa kuunda kanzidata ya viwanda vinavyoanzishwa na vinavyokuwa kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake Dkt Stephen Kargbo ambaye ni Mwakilishi wa UNIDO nchini Tanzania amesema kuwa uwepo wa siku ya viwanda vya ndani ni muhimu kwani hufanya kujua changamoto ambazo watu wenye viwanda wanakutana nazo na ni fursa kwa wadau kubadilishana mawazo kuhusu viwanda na njia bora za kutumia jambo ambalo linaloakisi ukuaji na ushirikiano katika nchi za Afrika.

Ameongeza kwamba katika kuendeleza muingiliano wa kibiashara katika nchi ya Afrika soko la pamoja la AFCFTA linatarajiwa kuongeza ushindani na kusisimua sekta ya uzalishaji

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania Dk.Ng’wanza Kamata amewashukuru washiriki wa Maonesho hayo kwa kuitikia wito wa kuja kushiriki na amesema kuwa uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano inasisitiza ujenzi wa uchumi wa viwanda hivyo iwe agenda ya kuduma hadi nchi itakapo simama imara katika ujenzi wa viwanda.
Naibu Waziri wa Viwanda na Bishara Mhandisi Stella Manyanya akizungumza wakati wa mkutano uliofanyika leo Desemba 7 mwaka 2019 ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea mikakati ya Serikali kuboresha mazingira ya biashara

ANTHONY JOSHUA WA MAREKANI AMDUNDA ANDY RUIZ JNR WA MAREKANI


TANESCO KWA MARA YA TATU YAWA MSHINDI WA KWANZA KATIKA TUZO ZA UBORA KATIKA UANDAAJI WA TAARIFA ZA FEDHA KWA TAASISI ZA UMMA

0
0

NA MWANDISHI WETU
SHIRIKA la Umeme nchini Tanzania, TANESCO limeshika nafasi ya kwanza na kunyakua tuzo ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha  ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi.Amina Khamis Shaaban amemkabidhi tuzo hiyo Afisa Mkuu wa Fedha (CFO) wa TANESCO, Bi. Renatha Ndege katika hafla ya kutoa tuzo kwa taasisi za umma na binafsi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Desemba 7, 2019.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Bi. Renatha alisema, TANESCO imetwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.

“Sisi kama Shirika tumefurahi sana, huu ni ushindi mkubwa, ili upate tuzo hii, kuna vigezo vinavyotumika na kubwa kuliko yote lazima uwe na hati safi, hii inamaanisha kwamba hela za Watanzania ziko salama.” Alisema.

Aliishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweza kuendelea kuliamini Shirika pamoja na Wizara kwa kutoa fedha nyingi kujenga miradi mingi na mikubwa ya uzalishaji umeme.

“Kama mnavyoona miradi ya umeme ni mingi Shirika liko salama, na hivi sasa umeme ni wa uhakika, hii inamaanisha kuna mambo mazuri yako TANESCO.” Alisisitiza.

Aliipongeza timu nzima ya idara ya Uhasibu na ukaguzi TANESCO kwa kufanya kazi nzuri iliyo pelekea Shirika kupata ushindi huu mkubwa.
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), akimkabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha  ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Afisa Mkuu wa Fedha (CFO) wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, Bi.Renatha Ndege katika hafla ya kutoa tuzo kwa taasisi za umma na binafsi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Desemba 7, 2019.
 Bi.Renatha Ndege, akiwa amebeba tuzo hiyo, huku akisindikizwa na watumishi katika idara yake wakati wa hafla hiyo.
 Bi.Renatha Ndege, akiwa amebeba tuzo hiyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari.
 Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa TANESCO wakiwa na tuzo hiyo.
 Wafanyakazi wa TANESCO wakiwa na tuzo hiyo wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi.
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi.Amina Khamis Shaaban, akitoa hotuba yake.
 Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Meza kuu.
 Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, Profesa Isaya Jairo, akitoa hotuba yake.
 Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Bw. Pius Maneno, akitoa hotuba yake.
  Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO wakiwa kwenye hafla hiyo.
Picha ya pamoja ya washindi wa tuzo wakiwa na mgeni rasmi.

NBAA YATOA TUZO ZA UMAHILI KATIKA UANDAAJI WA TAARIFA ZA FEDHA YA MWAKA 2018 KWA MAKAMPUNI, TAASISI PAMOJA NA MASHIRIKA

0
0
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani akisoma hotuba yake ya kufunga mafunzo pamoja na kutoa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye hafla iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Prof. Isaya Jairo akizungumza akitoa historia fupi ya utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mgeni rasmi pamoja na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Pius Maneno akizungumza wakati wa kufunga mafunzo pamoja na utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango,  Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt Joyce Nyoni(kulia) tuzo ya mshindi wa kwanza kwenye kipengele cha Vyuo Vikuu katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango,  Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka tuzo ya mshindi wa Pili kwenye kipengele cha Vyuo Vikuu katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi tuzo Afisa Mkuu wa Fedha (CFO) wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, Bi.Renatha Ndege ya mshindi wa kwanza ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)  zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi tuzo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk Edwin Mhede mshindi wa pili ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)  zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Prof. Isaya Jairo. 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi tuzo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)  zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Prof. Isaya Jairo. 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani (kushoto), akimkabidhi tuzo kwa Viongozi mbalimbali wa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika yaliyofanya vizuri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) zinayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)  
Baadhi ya wadau waliofika kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)  zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya  washindi wa Tuzo za uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). 

WAJUMBE BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA ARUSHA DC WAWANYOOSHEA KIDOLE BAADHI YA WAFANYAKAZI WAZEMBE UKUSANAYAJI MAPATO

0
0

ALAMIKIA UKUSANYAJI HAFIFU MAPATO 

Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

WAJUMBE kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Arusha DC wamesema uzembe wa  ukasanyaji mapato  kwa baadhi ya wafanyakazi wa halmashauri hiyo umekuwa moja ya sababu ya kutofikia malengo ya makadirio ya makusanyo kwa mwaka .
 
Hayo yamezungumzwa leo katika kikao  cha baraza la madiwani  wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji Wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya kwanza ya Julai -September 2019 kilichofanyika katika ukumbi Wa halmashauri hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho  Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Baraka Simon amesema kuwa baadhi ya wafanyakazi wamekuwa hawafanyi kazi vizuri ya ukusanuaji wa mapato  na wamekuwa hawafatilii  wakandarasi waliopewa zabuni za kukusanya mapato hali  inayoikosesha halmashauri fedha zamapato,hivyo kuifanya hata halmashauri kushidwa kulipa baadhi ya madeni ambayo wanadaiwa.

"Changamoto ya mapato ni kubwa mno kwani hata hawa  wakandarasi waliopewa zabuni za kukisanya ushuru mbalimbali wamekuwa hawazileti kama ipasavyo  hali inayofanya halmashauri tukose mapato , na mapato yetu kushuka ,"amesema.

Ameongeza wameweza kubaini baadhi ya changamoto ambazo zinasababisha mapato hayo kushuka  ,ambapo kwa asilimia kubwa sana ni pamoja na uvivu wa baadhi ya wataalamu wao wa halmashauri hiyo ambapo katika kutatua  hilo wao kama baraza la  madiwani  wametoa maelekezo  kuhakikisha ,ukusanyaji mapato unaongezeka.

Kwa upande wake Wa Diwani Wa kata ya Ilikiding'a Loth Mungaya  alisema kuwa halmashauri hiyo inavyanzo   vyanzo vingi vya mapato ikiwemo ,machimbo ya moramu  ,maegesho ya magari,pamoja na mchanga na kwa upande wa mchanga  na Moramu watu wamekuwa wanachota usiku na mchana lakini wanashangaa kuona halmashauri  haiingizi mapato na ikiendelea hivi  itapelekea halmashauri kushidwa kujiendesha na mwishowe kufutwa kabisa.

Akizungumzia suala hilo Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Arusha Dc Alvera Ndabagoye amesema atafanyia kazi na iwapo atabaini mfanyakazi yeyote anajinufaisha na fedha za mapato ya halmashauri atachukuliwa hatua kali ikiwemo na kufukuzwa kazi.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha,Alvera Ndabagoye akijibu maswali yaliyoulizwa na madiwani Wa halmashauri hiyo katika kikao cha madiwani wakati Wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji Wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya kwanza ya Julai -September 2019.(picha na Woinde Shizza, Arusha ).

Mwenyekiti Wa halmashauri ya Arusha Baraka Simon  akiongea katika kikao cha kawaida cha  madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji Wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya kwanza ya Julai -September 2019

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA, AMWAKILISHA RAIS KWENYE MAZISHI YA KAKA WA MAMA MARIA NYERERE MUSOMA. Inbox x

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwa na Mkewe Mary, wakiweka mashada ya maua, kwenye kaburi la Kaka wa Mama Maria Nyerere, Mzee Inyasi Gabriel, aliyefariki tarehe 4.12.2019, huko Musoma, mkoani Mara, Desemba 7, 2019
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwa na Mkewe Mary (kushoto), wakizungumza na Mama Maria Nyerere, baada ya mazishi ya Kaka wa Mama Maria Nyerere, Mzee Inyasi Gabriel, aliyefariki tarehe 4.12.2019, huko Musoma, mkoani Mara, Desemba 7, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwa na Mkewe Mary (kulia), wakimpa pole, Mjane wa Mzee Inyasi Gabriel, aliyefariki tarehe 4.12.2019, huko Musoma, mkoani Mara, ambaye ni Kaka wa Mama Maria Nyerere, baada ya mazishi, Desemba 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Makongoro Nyerere, kwenye msiba wa Kaka wa Mama Maria Nyerere, Mzee Inyasi Gabriel, aliyefariki tarehe 4.12.2019, huko Musoma, mkoani Mara, Desemba 7, 2019
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mtoto wa Baba wa Taifa, Mdaraka Nyerere, kwenye msiba wa Kaka wa Mama Maria Nyerere, Mzee Inyasi Gabriel, aliyefariki tarehe 4.12.2019, huko Musoma, mkoani Mara, Desemba 7, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimpa mkono wa pole Mama Maria Nyerere, kwenye msiba wa Kaka yake, Mzee Inyasi Gabriel, aliyefariki tarehe 4.12.2019, huko Musoma, mkoani Mara, Desemba 7, 2019
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Mama Maria Nyerere, kwenye mazishi ya Kaka yake, Mzee Inyasi Gabriel, aliyefariki tarehe 4.12.2019, huko Musoma, mkoani Mara, Desemba 7, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka udongo, kwenye kaburi la Kaka wa Mama Maria Nyerere, Mzee Inyasi Gabriel, aliyefariki tarehe 4.12.2019, huko Musoma, mkoani Mara, Desemba 7, 2019

Bilioni 205 za Dhihirisha “Utakimu” wa Biteko

0
0







Issa Mtuwa – “WM” Nzega

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema ataendelea kuongea kwa namba (takwimu) badala ya maneno huku akitamba kuwa wizara yake itavuka malengo ya makadirio ya makusanyo ya fedha zilizopangiwa na wizara yake kukusanya ambayo ni bilioni 475 katika mwaka wa 2019/20 huku akibainisha kuuwa ndani ya miezi 5 tu teyari wizara yake imeshakusanya bilioni 205.

Ameyasema hayo leo tarehe 7/12/2019 Wilayani Nzega alikokwenda kukabidhi Leseni 11 kwa vikundi 10 vya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu. Ameongeza kuwa kuongea ongea hakusaidii zaidi ya kufanya kazi na ukifanya kazi acha namba zikusaidie kueleza unachokifanya.

Pamoja na kukabidhi leseni hizo, Biteko ametoa masherti kwenye eneo moja la uchimbaji aliloliwekea mashaka kuhusu usalama wake kutokana na hali yake huku akiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya chini ya mwenyekiti wake ambae pia ni Mkuu wa Wilaya Godfrey Ngupula kuhakikisha utaratibu wa usalama umezingatiwa kabla ya kuanza kuchimba.

Vikundi vilivyokabidhiwa leseni hizo ni pamoja na; Msilale Miners Group, Jimbo la Nzega Vijijini, Undomo Miners Group, Hapa Kwetu Group, Umoja wa Wachimbaji Mwanshina, Mkombozi Mining Group, Imalamakoye Miners Group, Salama Miners, Makalanga Minerals Group na Nzega Miners Association.

Biteko amesema uthubutu wake na viongozi wenzake wa wizara nzima ndio unaopelekea kuiweka sekta ya madini kwenye mwendo “mdundo” huku akiahidi yeyote anayetaka kurudisha nyuma mwendo huo hatokubaliana nae.

Ameongeza kuwa, mara kwa mara halali usiku kwa ajili ya kupokea simu za wananchi wakimpa taarifa za utoroshaji wa madini na taarifa mbalimbali. Hata hivyo amesema anakerwa na vitendo vya uchonganishi kwa kutoa taarifa za uongo huku akiwaomba wananchi kutoa taarifaa zenye ukweli na usahihi ili kulisaidia tafia.

“Madini haya si yangu mimi wala ya Rais John Pombe Magufuli, ni madini ya Watanzania na sote tunawajibu wa kuyalinda, kazi yangu ni kusimamia maekezo ninayopewa na Mhe. Rais na kuhakikisha sekta hii inachangia kwenye pato la taifa kama inavyostahili. Narudia tena, anae stahili sifa katika haya yote yanayofanyika kwenye madini sio Mimi Doto Biteko, anaye stahili sifa na pongezi zote ni Rais John Pombe Magufuli kwani yeye ndiye anaye elekeza na mimi ni msimamizi tuu wa kutekeleza yale anayo yaagiza.”. Alisema Biteko.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Leseni kutoka Tume ya Madini Mhandisi Yahaya Semamba amewaambia wanavikundi waliopatiwa leseni kuwa pamoja na kupatiwa leseni hizo wanapaswa kuzingati masherti ya leseni hizo na kwamba watakao kiuka watawafutia leseni yao. Miongoni mwa masherti hayo ni kuhakikisha ulipaji wa maduhuli ya serikali, kutunza mazingira, kuzingatia usalama na masherti mengine yote.

Akiongea kwa niaba ya wanavikundi wenzake waliokabidhiwa leseni Aluna Mgalula amemshukuru Waziri wa Madini na Mkuu wa Wilaya kwa kuwaondelea kero yao ya kupatiwa leseni. Ametoa ushuhuda wa namna alivyokuwa anamsumbua waziri Biteko kwa kumpigia simu hata usiku wa manane huku akipokea na kumsikiliza.

Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wilayani Nzega ametoa pongezi kwa serikali na wizara ya madini huku akimshukuru waziri Biteko kwa namna anavyo wasaidia wachimbaji wadogo katika kuwapatia maeneo mbalimbali na kuwafanya wachimbaji kuwa na utulivu katika kazi zao.
Waziri wa Madini Doto Biteko akikabidhi Leseni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu kwa mmoja wa mwakilishi wa moja kati ya vikundi 10 vilivyo kabidhiwa leseni.
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images