Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

WAZIRI UMMY ATAKA WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII WALETEA MABADILIKO

$
0
0


 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwahutubia wahitimu wa Astashahada, Stashahada na Shahada katika Mahafali ya Tisa ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru yaliyofanyika leo mkoani Arusha.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifungua Kusanyiko la Mahafali ya Tisa ya Taasisi ya Maendeleo ya jamii Tengeru yaliyofanyika leo mkoani Arusha.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisema maneno maalum ya kuwatunuku wa Astashahada, Stashahada na Shahada katika Mahafali ya Tisa ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru yaliyofanyika leo mkoani Arusha na jumla ya wahitimu jumla ya wahitimu 918 walitunikiwa vyeti hivyo.
Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akitoa neno kwa wahitimu wa Astashahada, Stashahada na Shahada katika Mahafali ya Tisa ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru yaliyofanyika leo mkoani Arusha.
Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt Bakari George akieleza  mafanikio ya Taasisi yake katika masuala ya kitaaluma wakati wa Mahafali ya Tisa ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru yaliyofanyika leo mkoani Arusha.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu wakati wa sherehe za Mahafali ya Tisa ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru yaliyofanyika leo mkoani Arusha. 
Baadhi ya Wahitimu kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru wakisiliza hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa Mahafali ya Tisa ya Taasisi ya hiyo yaliyofanyika leo mkoani Arusha.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na waadhiri na wahitimu kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru mara baada ya kumalizika kwa Mahafali ya Tisa ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru yaliyofanyika leo mkoani Arusha.
  
Picha Zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
********************************************
Na Mwandishi Wetu Arusha
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka wahitimu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuleta mabadiliko katika jamii zinazowazunguka kwa kuzihamasisha kutafuta fursa za maendeleo.
Ameyasema hayo leo mkoani Arusha wakati akiwatunuku wahitimu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kwa ngazi ya Astashahada, Stashahada na Shahada katika mahafali ya tisa ya Taasisi hiyo.
Amewaambia wahitimu hao kuwa wataalam wa Maendeleo ya Jamii ni watalaam muhimu sana katika kuhamasisha jamii katika kujiletea maendeleo yao hivyo wakatumike katika jamii zao kuleta mabadiliko chanya kwa jamii na taifa.
“Mkatumike katika jamii zenu mkalete mabadiliko lazima muoneshe kama mnaweza msibaki mnalalamika fanya jambo linaloonekana fursa zitakuja” alisema Mhe. Ummy
Waziri Ummy amewaasa wahitimu hao kuanza kwa kujitolea katika kazi na kuzingatia maadili katika maeneo watakayokuwa wanafanya kazi au kuisaidia jamii kwani hakuna njia ya moja kwa moja ya uhakika wa kupata ajira kama hawatojitolea.
Pia Waziri Ummy amewataka Wahitimu hao kuonesha utaalam wao katika maisha yao na maisha ya jamii inayowazunguka katika kutatua changamoto zao na za jamii zao kwa kuleta mawazo chanja kwa wananjamii ikiwa na jinsi ya kufanya changamoto kuwa fursa za kimaendeleo.
Aidha Waziri Ummy ameitaka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii kuongeza nguvu katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii inayowazunguka katika kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili na kuazisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Tuoneshe namna gani wataalam wa maendeleo ya jamii tunaweza kusaidia jamii katika kufikia kipato cha kati na kuwa na Tanzania ya uchumi wa viwanda” amesema Mhe. Ummy.
Pia Waziri Ummy aliwataka wahitimu hao waliopata mikopo ya Serikali kuhakikisha wanarudisha mikopo ili kuwezesha watanzania wengine wanaohitaji elimu kupata mikopo kama Serikali ilivyowapatia wao mikopo iliyowasaidia kufikia kuhitimu.
Naye Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewataka wahitimu hao kuitumia elimu walioipata kuwa nyenzo, zana na funguo ya fursa mbalimbali katika kukabiliana na changamoto za kimaisha ili kutumia utaalamu wao kupata majawabu ya changamoto na suluhisho la matatizo mbalimbali kwa maendeleo yao na jamii zao.
Ameongeza kuwa Kada ya Maendeleo ya Jamii ni nyenzo muhimu sana katika maendeleo ya nchi yoyote na Serikali inathamini sana Taaluma ya Maendeleo ya Jamii kwani imekuwa msaada mkubwa katika kutekeleza miradi mbalimbali hapa nchini.
“Msiwe na hofu wahitimu kwani nyinyi ni watu muhimu katika jamii yetu na elimu mliyoipata ikawe nyenzo, funguo na fursa ya maendeleo katika nchi yetu” alisema Dkt. Jingu
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George amewasa wahitimu hao kwenda kuleta mabadiliko katika jamii na kuhakikisha wanakuwa chachu ya mabadiliko na kutengeneza fursa za ajira kwa wengine.
“Vyeti mtakavyopata sio njia au mlango wa ajira nikielelezo cha kusoma sasa mkaitumie kuhamasisha jamii katika kukabiliana na changamoto za maisha” alisema Dkt. Bakari
Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru katika mahafali ya tisa kwa mwakawa masomo 2018/2019 imewatunuku jumla ya wahitimu 918 wa Astashahada, Stashahada na Shahada mbalimbali ikiwemo za Maendeleo ya Jamii, jinsia na upangaji wa miradi.

JAPAN YAAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA MAENDELEO YA TANZANIA

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akipeana mkono na  mgeni wake, Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Nobuko Kayashima, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Jijini Dodoma ambapo Japan imeahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali za maendeleo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akisikiliza maelezo kutoka kwa mgeni wake, Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Nobuko Kayashima (hayupo pichani) walipokutana Jijini Dodoma ambapo Japan imeahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali za maendeleo.
Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Nobuko Kayashima akisisitiza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) Jijini Dodoma ambapo JICA imeahidi kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake, Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Nobuko Kayashima (wa tano kulia), pamoja maafisa wengine waandamizi kutoka JICA, Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Uchukuzi baada ya mazungumzo yaliyofanyika Jijini Dodoma kati ya pande hizo mbili.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adolf Ndunguru nje ya Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Nobuko Kayashima.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akimwongoza mgeni wake kutoka nje ya Ofisi ya Wizara ya Fedha na Mipango (jengo la Treasury Square), Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Nobuko Kayashima, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati) akiagana na mgeni wake, Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Nobuko Kayashima (kulia) pamoja na kurugenzi Msaidizi wa JICA, Bi. Yuriko Doi, nje ya jengo la Treasury Square, Jijini Dodoma.

*************************************
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma.

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameiomba Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa la Japan (JICA) kusaidia upatikanaji wa fedha kwa njia ya mikopo nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ikiwemo reli ya kisasa, nishati na kilimo.

Dkt. Mpango ametoa maombi hayo Jijini Dodoma, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa JICA, Dkt. Nobuko Kayashima, ambapo wawili hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa miradi inayokusudiwa kufadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia Shirika hilo.

Amesema kuwa hivi sasa Serikali imeelekeza nguvu na  fedha zake za ndani kujenga Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme kwa njia ya maporomoko ya maji ya Mto Rufiji mkoani Pwani (Nyerere Hydral Power Plant), na kwamba miradi  inahitaji fedha nyingi ambazo anaamini Japan inaweza kusaidia upatikanaji wake.

“Tumeanza kutekeleza miradi hii kwa kutumia fedha zetu za ndani na tunaiomba Serikali ya Japan kuzishawishi taasisi zake za fedha kwa kushirikiana na taasisi nyingine kutupatia mikopo yenye masharti nafuu ili tuweze kukamilisha miradi hiyo muhimu kwa Taifa” alisema Dkt. Mpango
Alifafanua kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutaongeza shughuli za kiuchumi na kibiashara hapa nchini pamoja na nchi jirani ambazo hazijapakana na Bahari huku nishati ya umeme ikitarajiwa kuboresha upatikanaji wa umeme kwa ajili ya kuendesha reli hiyo pamoja viwanda.

Aidha, Dkt. Mpango amemwomba kiongozi huyo wa JICA kusaidia Wizara na Serikali kwa ujumla kuendeleza rasilimali watu ama nguvu kazi kwa kuwapatia fursa ya masomo nchini Japan wataalam kutoka Wizara yake na maeneo mengine serikalini ili kuongeza ubobezi wa wataalam hao katika sekta ya uchumi, fedha, pamoja na tiba hususan matibabu ya moyo na figo.

“Pia ninaliomba Shirika lako lisaidie kuboresha miundombinu ya barabara za kuzunguka Jiji la Dodoma kutokana na mahitaji makubwa baada ya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi, pamoja na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nsalato-Dodoma” aliongeza Dkt Mpango
Alisema kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa-Msalato unahitaji kujengwa njia ya kuruka na kutua ndege pamoja na ujenzi wa majengo ya abiria.

“ Pia nimewaomba wenzetu ambao wanauzoefu mkubwa watusaidie katika kilimo cha mpunga na nimetoa mfano wa Bonde la Ruvu ambalo ni kubwa na lina fursa ya kuzalisha mchele wa kutosheleza mahitaji ya ndani na nje na tukichagua eneo moja na kulitumia vizuri tutamaliza mahitaji ya mchele katika Taifa letu” alisisitiza Dkt. Mpango

Akijibu maombi ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Makamu huyo wa Rais wa JICA, Dkt. Nobuko Kayashima, alikubali maombi ya kusaidia kuendeleza rasilimali watu ambapo kwa kuanzia Shirika hilo limeahidi kutoa nafasi ya watumishi 15 kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na  Sekta nyingine kupata ufadhili wa masomo nchini Japan.

Amesema Serikali ya Japan kupitia Shirika lake litaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi ambapo miradi mipya inayokusudiwa kufadhiliwa na Shirika lake ni Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Kigoma, Ujenzi wa Barabara ya Arusha-Holili na Mradi wa Maji safi na Usafi wa Mazingira Zanzibar.

Kuhusu uendelezaji wa kilimo, Dkt. Kayashima ameahidi kuwa Shirika lake litaendelea kujihusisha na kuendeleza zao la mpunga hapa nchini ili kuwasaidia wakulima kujikimu kimaisha pamoja na kusaidia nchi ijitosheleze kwa chakula.

WAZIRI UMMY AMTEMBELEA MTOTO ANNA

$
0
0

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akiwa na Mtoto Anna Zambi alipomtembelea nyumbani kwa mama yake Mdogo Mkoani Arusha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akiwa na Mtoto Anna Zambi na mama mdogo yake Anna Bi. Isabella Lyimo alipomtembelea nyumbani kwa mama yake Mdogo Mkoani Arusha. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
************************************

Na Mwandishi Wetu Arusha

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu leo amtembelea mtoto Anna Zambi ambae alipoteza wazazi wake wote wawili na wadogo zake watatu katika ajali iliyotokea Korogwe  Tanga, mwezi Octoba 2019.  

Waziri Ummy amemishi Mtoto Anna Zambi kujipa moyo na kujikaza na kumuomba Mungu amsaidie kumpa faraja katika kipindi kigumu anachokipitia baada ya kupotea wazazi wote na ndugu zake.

“Mimi nikutie moyo mtoto wangu tuko pamoja na Serikali haitokuacha peke yako tutajitaidi kukupa faraja kuwezesha kupata msaada wa huduma za msaada wa kisaikolojia taratibu na kwa uweza wake Mungu utarudi katika hali yako ya kawaida” alisema Mhe. Ummy Kwa upande mama yake mdogo  mtoto Anna  Bi. Isabella Lyimo wamemshukuru Mhe Ummy kwa kumtembelea Anna na kuendelea kuwapa faraja.

Wazazi wa Anna- Lingston Zambi na Winfrida Lyimo pamoja na ndugu zake watatu Lulu, Adrew na Grace walifariki Dunia Oktoba 26 mwaka huu wakiwa njiani kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro, kwenye mahafali ya Kidato cha Nne ya Anna, ambapo gari waliokua wakisafiria lilisombwa na maji na mafuriko yaliyotokea wilayani Handeni mkoani Tanga.

WARATIBU ELIMU WAZEMBE KUCHUKULIWA HATUA KALI MKOANI SONGWE

$
0
0

 Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila akizungumza na Waratibu Elimu kata na Wasimamizi wa Sekta ya Elimu Mkoa wa Songwe ambapo amesema atawachukulia hatua kali za kinidhamu waratibu wazembe.

Waratibu Elimu kata na Wasimamizi wa Sekta ya Elimu Mkoa wa Songwe wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila (Hayupo pichani) wakati wa kikao cha kutathmini Maendeleo ya Sekta ya Elimu kwa mwaka 2019 na kupanga mikakati ya kuboresha elimu kwa mwaka 2020.

************************************
Waratibu Elimu kata na Wasimamizi wa Sekta ya Elimu Mkoa wa Songwe waliobainishwa katika ripoti ya uchunguzi wa hali ya sekta ya Elimu kuwa ni wazembe katika kusimamia maendeleo ya elimu watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amesema hayo jana wakati wa kikao na Waratibu Elimu Kata na Maafisa Elimu ili kutathmini maendeleo ya Sekta ya Elimu kwa mwaka 2019 na kupanga mikakati ya kuboresha elimu kwa mwaka 2020.

“Tuliwapa kazi wadhibiti ubora ya kufanya uchunguzi kwanini Mkoa wetu haufanyi vizuri kielimu na ripoti yao imebainisha uwepo wa uzembe wa waratibu elimu Kata katika usimamizi, sasa nitachukua hatua kali kwa waratibu elimu wote wazembe.”, amesema Kafulila.

Kafulila amesema Waratibu Elimu kata wote walisaini Mkataba ambao uliwataka kusimamia Sekta ya elimu na kuhakikisha kiwango cha elimu kinapanda lakini pia serikali imewawezesha posho na usafiri lakini wapo baadhi yao ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao.

“Serikali imewapa posho na Waratibu Elimu Kata lakini baadhi yao wamebainishwa katika ripoti kuwa wanafanya kazi kwa kuogopana na kuendekeza urafiki, hawawachukulii hatua walimu na wakuu wa shule ambao hawatimizi majukumu yao, hao hatuwezi kuwavumilia.”, amesisitiza Kafulila.

Naye Mwenyekiti wa Wadhibiti Ubora wa Elimu Mkoa wa Songwe Mwalimu Jackson Lwafu amesema walitathmini kwanini baadhi ya shule katika Mkoa wa Songwe zimeshuka kielimu na walibaini kuwa usimamizi dhaifu umechangia kwa kiasi kikubwa.

Lwafu amesema endapo wasimamizi wa Elimu Mkoa wa Songwe watatambua majukumu yao na kuyasimamia, maendeleo ya sekta ya Elimu Mkoa wa Songwe yatakuwa mazuri.

Mratibu Elimu Kata ya Mkukwe Wilayani Songwe Mwalimu Judith Mwasoke amesema taarifa ya wathibiti ubora inasikitisha kwakuwa ili kuwe na mafanikio lazima taratibu zifuatwe hivyo suala la kuoneana aibu na kuogopana halifai na waratibu Elimu Kata wenye tabia hiyo waache.

Afisa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma Mtafya Wilson amesema kwa mwaka 2020 watahakikisha walimu wanafundisha vipindi vyote pamoja na kuwasimamia Waratibu Elimu Kata wanatimiza wajibu wao.
Afisa Elimu Mkoa wa Songwe Juma Japhet Kaponda amesema Matokeo ya darasa la saba mwaka 2019 hali haikuwa nzuri kwakuwa Mkoa ulipanda ufaulu kwa asilimia 1.65 kwa kuwa na ufaulu wa asilimia 75 na Mkoa ukishika nafasi ya 21 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2018 wa asilimia 73 na nafasi ya Mkoa wa Songwe ilikuwa 17.

Utoro, Uvivu na kutoshirikisha wazazi kwatajwa kuwa kikwazo cha ufaulu Rukwa.

$
0
0









***********************************

Pamoja na ufaulu wa matokeo ya darasa la saba kupanda kwa asilimia 8.01 kwa mwaka 2019 katika mkoa wa Rukwa na kupelekea kushika nafasi ya 13 kitaifa baada ya kufanyika mtihani wa darasa la saba mwezi septemba mwaka huu viongozi wa ngazi mbalimbali katika mkoa wameendelea kutaja utoro na uvivu wa waalimu kuwa ni kikwazo katika kuinua ufaulu katika Mkoa wa Rukwa.

Hayo yalianza kusemwa na Afisa Elimu Mkoa wa Rukwa Nestory Mloka baada ya kutoa taarifa ya matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 pamoja na taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2020 katika Mkoa huo.

“ Mwalimu kutokuwepo shuleni, kutokuja kabisa shuleni, watoro wapo, pwngine hawaripotiwi ipasavyo katika vyombo vya maamuzi vyenye kutoa maamuzi kwa wakurugenzi hawajui na yawezekana hata maafisa elimu hawajui, wapo waalimu anatoroka yupo Mbeya anafanya mambo yake, lakini mwalimu Mkuu hasemi. Sasa hili ni tatizo,” Alisema

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Kalolo Ntila alisema kuwa waaalimu wengi wamekuwa wakifika shuleni na kufanya kazi ya ‘kuchati’ na sumu zao mpaka muda wa kazi unakwisha na kwenda nyumbani na hivyo kuutaka uongozi wa mkoa kutafuta mwarobaini wa tabia hizo za waalimu.

“Bado naendelea kujitafakari hivi hao waalimu wamesomea mbinguni, hao wanaofundisha shule za binafsi, nidhamu na uwajibikaji ni kubwa sana katika hizi shule binafsi, waalimu hawa watuambie ni mambo gani yanayowapelekea kutowajibika ili tuelewe,” Alisema.

Aidha, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Apolinary Macheta alisema kuwa shule ambazo waalimu hawana mahusiano na wazazi kitaaluma, shule hizo daima huwa chini sana kitaaluma na kuongeza kuwa waaalimu wanahitajika kufanya vikao na wazazi ili kutambua changamoto mbalimbali za shule na kuweza kushirikiana kuzitatua.

Ambapo katika kuunga mkono jambo hilo mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga John Msemakweli amezitupia lawama bodi za shule kushindwa kutatua matatizo ya utoro wa wanafunzi, waalimu pamoja na kuona namna ya wanafunzi hao kupata chakula mashuleni ili kuweza kuongeza ufaulu kwakuwa wanafunzi hao hushinda njaa jambo linalowafanya kushindwa kuwa makini na masomo.

Katika kulitafutia mwarobaini suala hilo la chakula masuleni mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mazwi Godson Mwaibingila ameuomba uongozi wa mkoa kutoa maelekezo kwa halmashauri ili suala hilo la chakula liwekwe katika sheria ndogo za halmashauri na kuweza kuwalazimisha wazazi kuchangia chakula katika shule za msingi na sekondari ndani ya mkoa.

Aidha, Diwani wa Kata ya Chala, Wilayani Nkasi Michael Mwanalinze alisema kuwa sera ya elimu bure itolewe kwa upana wake ili kuhakikisha wazazi wanaielewa, tofauti na hali ilivyosasa kuwa wazazi hawachangii chochote wakisema kuwa elimu ni bure na kuonya kuwa endapo hali hiyo itaendelea basi ufaulu utaendelea kushuka.

Kwa upande wake kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Winnie Kijazi aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanashughulikia matatizo hayo kwani yapo chini ya mamlaka yao kama halmashauri pamoja na mabaraza yao na kuongeza kuwa mkoa umekuwa ukitoa ushirikiano katika kuhakikisha wanafunzi wanaodhulumu haki za kusoma za wanafunzi wanafikishwa katika vyombo husika kwa taratibu za kisheria.

Jumla ya Watahiniwa 16,069 sawa na asilimia 81.01 wakiwemo wavulana 7,953 na wasichana 8,116 wamefaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019. Huku ufaulu huo ukipanda kwa asilimia 8.01 ukilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2018 uliokuwa asilimia 73.00 na kupelekea kushika nafasi ya 13 kitaifa kati ya mikoa 26.

Madhimisho Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kufanyika Desemba 11 Jijini Dodoma Inbox x

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimeniti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maadili na Hakli za Binadamu leo tarehe 6 Desemba 2019 jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yameanza tareh 6 hadi 11 Desemba 2019 ambapo kauli mbiu yake ni “Maadili katika utumishi wa umma ni nguzo muhimu katika kuimarisha utawala bora na haki za binadamu”. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Amon Mpanju. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Amon Mpanju akijibu swali toka kwa waandishi wa habari wakati wa Mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimeniti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika(katikati) na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu leo tarehe 6 Desemba 2019 jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yameanza tareh 6 hadi 11 Desemba 2019 ambapo kauli mbiu yake ni “Maadili katika Utumishi wa Umma ni nguzo muhimu katika kuimarisha utawala bora na haki za binadamu”.Kulia ni Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela. Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimeniti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika(kulia) na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu leo tarehe 6 Desemba 2019 jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yameanza tareh 6 hadi 11 Desemba 2019 ambapo kauli mbiu yake ni “Maadili katika Utumishi wa Umma ni nguzo muhimu katika kuimarisha utawala bora na haki za binadamu”.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Amon Mpanju. Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mathew Mwaimu akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimeniti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika(kulia) na waandishi hao kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu leo tarehe 6 Desemba 2019 jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yameanza tareh 6 hadi 11 Desemba 2019 ambapo kauli mbiu yake ni “Maadili katika Utumishi wa Umma ni nguzo muhimu katika kuimarisha utawala bora na haki za binadamu”. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Amon Mpanju. Mkurugenzi wa akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimeniti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika(kulia) na waandishi hao kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu leo tarehe 6 Desemba 2019 jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yameanza tarehe 6 hadi 11 Desemba 2019 ambapo kauli mbiu yake ni “Maadili katika Utumishi wa Umma ni nguzo muhimu katika kuimarisha utawala bora na haki za binadamu”. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Amon Mpanju. Baadhi ya viongozi toka Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakifuatilia wa Mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimeniti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika(kulia) na waandishi hao kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu leo tarehe 6 Desemba 2019 jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yameanza tareh 6 hadi 11 Desemba 2019 ambapo kauli mbiu yake ni “Maadili katika Utumishi wa Umma ni nguzo muhimu katika kuimarisha utawala bora na haki za binadamu”. : Baadhi ya watendaji kutoka taasisi zinazoshiriki maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu wakifuatilia wa Mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimeniti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika(kulia) na waandishi hao kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu leo tarehe 6 Desemba 2019 jijini Dodoma. Taasisi hizo ni Ofisi ya Rais –Utummishi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, PPRA, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Wizara ya Katiba na Sheria na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Baadhi ya watendaji kutoka taasisi zinazoshiriki maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu wakifuatilia wa Mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimeniti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika(kulia) na waandishi hao kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu leo tarehe 6 Desemba 2019 jijini Dodoma. Taasisi hizo ni Ofisi ya Rais –Utummishi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, PPRA, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Wizara ya Katiba na Sheria na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina yao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimeniti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika(kulia) na waandishi hao kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu leo tarehe 6 Desemba 2019 jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yameanza tareh 6 hadi 11 Desemba 2019 ambapo kauli mbiu yake ni “Maadili katika Utumishi wa Umma ni nguzo muhimu katika kuimarisha utawala bora na haki za binadamu”. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimeniti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Huruma Mkuchika akisalimiana Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere mara baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu leo tarehe 6 Desemba 2019 jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yameanza tareh 6 hadi 11 Desemba 2019 ambapo kauli mbiu yake ni “Maadili katika Utumishi wa Umma ni nguzo muhimu katika kuimarisha utawala bora na haki za binadamu”.Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu. (Picha na Idara ya Habari – MAELEZO)

Wananchi Mkoani Tabora Watakiwa Kujiunga Na Mfuko Wa jamii Iliyoboreshwa (CHF)

$
0
0
Na, Editha Edward -Tabora

Wananchi mkoani Tabora wametakiwa Kujiunga na mfuko wa afya ya jamii Iliyoboreshwa (CHF) jambo ambapo litawasaidia kupata huduma ya afya kwa bei nafuu ya shilingi elfu thelathini kwa kila Maya watu sita

Ameyaeleza hayo mkuu wa mkoa huo Aggrey Mwanri wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kuwasisitiza wananchi Kujiunga na mfuko huo wa afya na kuwahakikishia upatikanaji wa dawa

Mwanri amesema mfuko huo utawasaidia wananchi wenye kipato cha chini kuweza kupata huduma ya afya kila mahali hapa nchini ukitofautisha na zamani ambapo mwananchi alipokuwa akijiunga kwa ajili ya kupata huduma ya afya ndipo anapotibiwa

"Mtu yeyote unapojiunga na mfuko huwa afya ya  jamii Iliyoboreshwa utatibiwa nchi nzima uwe bodaboda mama ntiliye mjasiriamali mkulima na kila Mtu atapata dawa kulingana na maelezo ya daktari "Amesema Mwanri 

Aidha Mwanri ametoa onyo kwa watumishi ya sekta ya afya ambao watahusika kwa kukwamisha zoezi hili kwa kuwabugua watu walio jiandikisha hatua kali zitachukuliwa hasa kwa upande wa Rushwa kwani ni kinyume na maadili

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora Baraka Mackona amebainisha jinsi ya Kujiunga na mfuko huo kwa wananchi ni kufika katika serikali za mitaa  na kujiandikisha ili kupata huduma hiyo

Aidha jumla ya Kaya elfu sita zimeshajiunga na mfuko wa (CHF)  Iliyoboreshwa  kwa mkoa mzima wa Tabora na zinaendelea kufaidika na huduma zinazotolewa na mfuko huo.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na wananchi Kujiunga na mfuko wa afya ya jamii Iliyoboreshwa CHF.


Afisa ustawi wa jamii ofisi ya mkuu wa mkoa Baraka Mackona akizungumzia jinsi ya wananchi wakitaka Kujiunga na mfuko huo wa afya ya jamii Iliyoboreshwa CHF.

SBL yatoa punguzo kubwa la bei kwa wateja wa vinywaji vikali

$
0
0
Watumiaji wa pombe kali zinazosambazwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), wana kila sababu ya kufurahi msimu huu wa sikukuu, baada ya kutangazwa kwa punguzo kubwa la bei kwa aina mbali mbali ya vinywaji vikali.

Ikiwa ni sehemu ya kuonyesha kuwajali katika msimu wa sikukuu, SBL jana ilizindua punguzo kubwa la bei kwa vinywaji vyake vikali ili kuwawezesha wateja wake kuwanunulia ndugu jamaa na marafikizawadi za  vinywaji vyenye ubora wa kimataifa kwenye sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya.

Akiongea na waandishi wa habari waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kilichopo Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti alisema kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha wateja wake kufurahia sikukuu pamoja na wawapendao kwa kuwanunulia pombe kali zinazosambazwa na kampuni hiyo kama Johnnie Walker, Captain Morgan, Ciroc, Smirnoff Vodka na nyinginezo kwa punguzo kubwa la bei.

“Kampeni hii ya kutoa zawadi, inaenda sambamba na wito wetu wa kunywa kistarabu ambapo tunawaelimisha wateja wetu kuepuka kutumia vilevi na kisha kuendesha vyombo vya moto,” alisema Ocitti.

Ni mwaka wa tano sasa kampuni ya SBL inaendesha ya kampeni ya unywaji wa kistarabu kwa kushirikianba na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama barabarani pamoja na wadau wengine wa usalama barabarani.

Kwa upande mwinginre, Ocitti alizungumzia mwenendo wa kibiasahara wa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na upanuzi wa viwanda vyake vya Dar es Salaam na Moshi unaogharimu Pauni za Uingereza milioni 14. Upanuzi huo utakapokamilika,  utaiongezea kampuni hiyo uwezo wa uzalishaji kwa asilimia 34 zaidi.
  
“Upanuzi tunaofanya, unaonyesha nia yetu ya kupanuka na kuongeza upatikanaji wa bidhaa zetu pamoja na kutengeneza ajira zaidi. Upanuzi huu pia utaongeza mahitaji ya malighafi tunazonunua kutoka kwa wakulima wa ndani kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zetu,” aliongeza.

Kampuni ya SBL imenunua tani 17,000 za ujazo za mahindi na uwele kutoka kwa wakulima wa ndani sawa na asilimia 70 ya jumla ya mahitaji yake yote ya malighafi kwa mwaka. SBL pia imelipa jumla ya shilingi 121bn/- kama kodi za aina mbali mbali kwa mujimu wa Ocitti.
 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Mark Ocitti, akizungumza na wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo cha Dar es Salaam kujionea upanuzi mkubwa unaoendelea kiwandani hapo.
 
Meneja Afya na Usalama Mahali pa Kazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) David Mwakalobo (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari waliotembelea kiwanda cha Dar es Salaam kujionea upanuzi mkubwa unaoendelea kiwandani hapo.


NBC yaendelea kuwapa mbinu za kibiashara wafanyabiashara jijini Dar

$
0
0
 Meneja Ukuzaji wa Biashara wa NBC, Jonathan Bitababaje akichangia mada wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Benki hiyo ya wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji wa biashara zao  jijini  Dar es Salaam juzi.

 Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakisikiliza kwa makini baadhi ya mada zilizokuwa zikitolewa katika Semina hiyo kutoka wadau mbalimbali wakiwemo Mamlaka ya Mapato (TRA), Wakala wa Usajili wa Biashara na Makampuni (Brela), Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA),  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) pamoja na wengineo.

Baadhi ya wafanyabiashara wa maeneo ya Ubungo jijini Dar es Salaam wakisikiliza baadhi ya watoa mada katika semina iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wafanyabiashara hao juzi. 
Msaidizi wa Msajili Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), George Chuwa akizungumza wakati semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Ubungo jijini Dar es Salaam jana.

 Mkurugenzi wa Bima wa Benki ya NBC, Benjamin Nkaka (kulia) akisalimiana na wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Ubungo katika semina ya siku moja ilyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji za mbinu za kufanya biashara zao  jijini  Dar es Salaam jana.
 Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Benki ya NBC, Rachel Mwalukasa (kulia), akizungumza na wafanyabiashara wa maeneo ya Ubungo jijini humo jana kuhusu huduma na bidhaa zotolewazo na benki hiyo hususani wakati wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na wadau muhimu kutoka taasisi mbalimbali zinazuhusika na masuala ya biashara.
 Mwakilishi kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Gwakisa Bapala (kulia), akizungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na baraza hilo wakati wa semina kuhusu mbinu mbalimbali za kufanya biashara iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati katika Ukumbi wa Hoteli ya Millenium Towers jijini Dar es Salaam juzi.
 Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashra wa Kati na Wadogo wa Benki ya NBC, Evance Luhimbo akizungumza katika semina ya siku moja ya  wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Ubungo  iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji wa biashara zao  jijini  Dar es Salaam juzi.

TAARIFA YA KUPOTEA KWA MTUMISHI WA TAEC

MWENYE NJAA USIMPE SAMAKI MPE NDOANO, MAFUNZO YA UBUNIFU YAFUNGWA JIJINI DAR LEO

$
0
0










MWENYE njaa usimpe samaki mpe ndoano ili aweze kuvua samaki wengine ili akila apate nguvu na kwenda kuvua samaki wengi zaidi.

Kauli hiyo ameitoa Katibu Mkuu Sayansi wa wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia, Dkt.James Mdoe wakati akifunga mafunzo ya washindi wa shindano la kitaifa la Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam leo, Amesema kuwa  sio utaratiu wa serikali kugawa fedha kwa wabunifu bali serikali inajukumu la kuwajengea uwezo ili waweze kumiliki bunifu zao kisheria ili mtu mwinvgine asije kujitokeza kufanya kitu alicho kibuni mtu mwingine.

Dkt. Mdoe amesema kuwa wabunifu wengi kuwaendeleza haina maana kuwa tuwape pesa, ni kitendo cha kuwajengea uwezo ili waweze kuendeleza ubunifu ule kwani ni wa mbunifu mwenyewe.

"Sasa jukumu letu kam serikali ni kuwezesha ili uweze kutoka hatua moja kwenda nafasi bora zaidi ili uunifu ule uweze kusaidia zaidi" Amesem Dkt. Mdoe.

Amesema kuwa kunavitu amavyo mbunifu anahitaji ili aweze kuendeleza ubunifu wake  na kuwe na mwekezaji  ambaye atachukuwa ubunifu wa mbunifu na kufanya kuwa kitu kikubwa na kuwekeza ili biashara iweze kufanyika.

MAfunzo hayo kwa wabunifu wa shindano la MAKSATU yametolewa na Baraza la uwezeshaji uchumi taifa la Sayansi na Teknolojia, Brela, SIDO, TBS na Cosota ambayo yalitolewa kwa siku nnne kwajili ya kuwajengea uwezo  na kuonesha fursa mbalimali zilizopo.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha miongozo ya kibunifu, maombi mbalimbali ya ubunifu, ili tuweze kupata wabunifu wengi zaidi kwaajili ya manufaa ya nchi ya sasa na ya baadae.

Kwa upande wa wabunifu, Halima Mpita, amesema kuwa yale yote yaliyoanzishwa na wabunifu lazima yatekelezeke kwaaajili ya kuisaidia jamii yetu, katika mahali wanapoelekea wabunifu hao.

"Safari yetu ya MAKSATU ilianzia  aada ya serikali kupitia wizara ya elimu kuundua vipaji 337 na katika kupitia hilo ziliunganishwa na DSI, VETA, COSTECH, DIT,wote hawa walifanya kazi ya pamoja katika kutafuta wabunifu hawa na hatimaye kukawa na mashindano ambayo yalianza machi mwaka huu ndiyo yaliyotupelekea kuwepo hapa leo". Amsema Halima.




Katibu Mkuu Sayansi wa wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia,Dkt.James Mdoe akizungumza na washindi wa shindano la kitaifa la ubunifu wa Sayansi na Teknolojia (2019) (MAKSATU) jijini Dar es Salaam leo wakati wa kufunga mafunzo ya siku nne kwa wabunifu hao.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH)Dkt. Amos Nungu akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa washindi wa shindano la kitaifa la ubunifu wa Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam leo.

Mbunifu wa mkaa mbadala, Halima Mpita Akizungumza kwa niaba ya wabunifu wengine na  kutoa shukurani kwa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),jijini Dar es Salaam leo wakati wa kufunga mafunzo kwa wabunifu walioshinda katika shindano la kitaifa la Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia

 Baadhi ya wabunifu wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu Mkuu Sayansi wa wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia,Dkt.James Mdoe wakati wa kufunga mafunzo ya siku nne kwa waunifu wa shindano la  MAKSATU jijini Dar es Salaam leo.

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 58 ya UHURU NA MIAKA 57 YA JAMHURI UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA YANOGA

$
0
0

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akimueleza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, juu ya umuhimu wa kukamilisha kwa wakati shughuli zitakazo fanyika siku ya sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba, wakati alipofika uwanjani hapo kukagua maandalizi ya sherehe hizo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko na Mkuu mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Christopher Kadio wakiwa katika viwanja vya CCM Kirumba, wakati alipofika uwanjani hapo kukagua maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani humo 
Kikundi cha Kwaya cha MVC kikifanya mazoezi kwa ajili ya siku ya sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba tarehe 9 Desemba 2019. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa letu”.
Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, leo, tarehe 5 Desemba, baada ya kukagua shughuli za maandalizi za Majeshi ya Ulinzi kwa ajili ya siku ya sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani humo tarehe 9 Desemba 2019, katika viwanja vya CCM Kirumba. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa letu”.
Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo akishuka katika jukwaa la Uwanja wa CCM Kirumba, mkoani Mwanza mara baada ya kukagua shughuli za maandalizi za Majeshi ya Ulinzi kwa ajili ya siku ya sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani humo tarehe 9 Desemba 2019. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa letu”.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO-BUSISI LINALOUNGANISHA WILAYA YA MISUNGWI NA SENGEREMA MKOANI MWANZA

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisogea kuangalia picha ya mfano wa Daraja hilo litakalojengwa kutokea Kigongo Misungwi hadi Busisi Sengerema mkoani Mwanza. Daraja hilo litakalopita ziwani litakuwa na urefu wa km 3.2 na kufanya kuwa Daraja refu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti walipokuwa wakiangalia picha ya mfano wa Daraja hilo litakalojengwa kutokea Kigongo Misungwi hadi Busisi Sengerema mkoani Mwanza. Daraja hilo litakalopita ziwani litakuwa na urefu wa km 3.2 na kufanya kuwa Daraja refu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine akivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kutoka Kigongo hadi Busisi lenye urefu wa km 3.2 katika sherehe zilizofanyika katika eneo la Kigongo Misungwi mkoani Mwanza.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Daraja hilo refu kupita yote katika ukanda wa Afrika Mashariki lenye urefu wa km 3.2 katika sherehe zilizofanyika katika eneo la Kigongo Misungwi mkoani Mwanza.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia picha ya mfano wa Daraja hilo litakalojengwa kutokea Kigongo Misungwi hadi Busisi Sengerema mkoani Mwanza. Daraja hilo litakalopita ziwani litakuwa na urefu wa km 3.2 na kufanya kuwa Daraja refu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Daraja la kutoka Kigongo hadi Busisi Misungwi mkoani Mwanza.

 Mbunge wa Misungwi Mhe. Charles Kitwanga akicheza ngoma ya Gobogobo wakati wa sherehe ya uwekaji wa  jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Daraja la kutoka Kigongo hadi Busisi Misungwi mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati akiwa na Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Iseni B Salma Yasin ambaye alielezea vizuri kero mbalimbali za Shule yao na kufanikiwa kuchangiwa kiasi cha Shilingi milioni 5 na Mhe. Rais Dkt. Magufuli. PICHA NA IKULU




WAZIRI KAIRUKI ATEMBELEA MAONESHO YA NNE YA BIDHAA ZA VIWANDA VYA TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki (wa pili kulia) akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stela Manyanya pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) , Edwin Rutageruka wakati wakitembelea Maonesho ya Nne ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere (Sabasaba) uliopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. 

TASWIRA MBALIMBALI KATIKA UDSM MARATHON JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Sehemu ya Washiriki wa Mbio ndefu (Marathon) walipokuwa wakianza kukimbikia kwenye UDSM Half Marathon, iliyofanyika leo Desemba 7, 2019 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.










BRELA YAWAKARIBISHA KWENYE MAONESHO YA VIWANDA KATIKA VIWANJA VYA SABASABA JIJINI DAR

$
0
0
WAKALA ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wanawakaribisha katika maonesho ya nne (4) ya Viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salama .

Akizungumza na michuzi Blog Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Loy Mhando amesema usajili wa makampuni, majina ya biashara, alama za biashara na huduma hataza pamoja na leseni za viwanda zinapatikana katika viwanja vya sabasaba ambapo maonesho ya bishara za viwanda yanafanyika.

Loy amesema leseni za biashara za kundi A nazo zinapatikana katika maonesho hayo hivyo wananchi wote wenye mpango wa kuanzisha biashara wafike katika viwanja hivyo ili wakapate huduma hiyo kwa urahisi zaidi na bila kupoteza muda.

Natoa rai kwa watanzania wote, wadau wote wa biashara na viwanda pamoja na wawekezaji wanaohitaji huduma zinazotolewa na BRELA kufika katika viwanja vya sabasaba kwa ajili ya kuangalia bidhaa zinazotengenezwa pamoja na kujipatia huduma mbalimbali zinazotolewa katika maonesho hayo". Amesema Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu (BRELA), Loy Mhando.

Hata hivyo Afisa Leseni za viwanda kutoka BRELA, Yusuph Nakapala amesema kuwa katika maonesho hayo utapata huduma ya kufanya usajili na kurasimisha biashara yako kwa njia ya mtandao na kupata cheti chako papo kwa papo.

Kwa upande wake Afisa Habari na Mawasiliano kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Robertha Makinda amewakaribisha wananchi kwa ujumla katika maonesho ya Nne (4) ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaama ili waweze kufanya usajili na kurasimisha biashara zao.

Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inawakaribisha wote kutembelea Banda lao  lililopo katika ukumbi wa Karume, banda namba 105 katika viwanja vya Mwl. J. K. Nyerere (sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa mtendaji Mkuu wa  Wakala ya usajili wa biashara na leseni (BRELA), Loy Muhando akiwa na wafanyakazi wengine wakionesha jinsi mfumo wa zamani wa kusajili Biashara na majina ya biashara ilivyokuwa ikifanyika kwa njia ya kujaza fomu.
 Picha ya pamoja katika maonesho ya nne ya idhaa za viowanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Leseni za viwanda kutoka  wakala ya usajili wa biashara na leseni (BRELA), Yusuph Nakapala akizungumza na mteje aliyetembelea katika banda lao katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 
 Mteja akipata maelekezo jinsi ya kusajili biashara katika maonesho ya viwana yanayoendelea katika viwanja vya saasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari na Mawasiliano kutoka wakala wa usajili wa biashara na leseni(BRELA), Robertha Makinda Katikati akizungumza katika maonesho ya viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

TRA YATOA ELI MU YA MLIPA KODI TANDIKA SOKONI-TEMEKE JIJINI DAR

$
0
0
 Afisa huduma na elimu kwa mlipakodi kutoka TRA, Catherine Mwakilagala, akitoa maelezo kwa wafanyabiashara wa eneo la Tandika sokoni wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea katika jiji la Dar es Salaam.
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa TRA Rachel Mkundai akitoa elimu kwa mfanyabisaha wa Tandika aliyefika katika banda la TRA eneo la Tandika Sokoni wakati wa kampeni.
 Afisa huduma na elimu kwa mlipakodi mkoa wa kikodi Temeke kutoka TRA, Catherine Mwakilagala (kushoto) akikabidhi Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi kwa mfanyabiashara wa Tandika Sokoni Patrick Mosses mara baada ya kujisajili kuwa mlipakodi katika kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea jijini Dar es Salaam.
Afisa huduma na elimu kwa mlipakodi wa mkoa wa kikodi wa Temeke Jackson Museti akitoa elimu ya kodi kwa mlipakodi wa Tandika sokoni katika kampeni ya elimu kwa mlipakodi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, AKAGUA UJENZI WA MRADI WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA ZIWA, ILIYOPO MUSOMA,MKOANI MARA

$
0
0



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na  Mkurugenzi wa Uendeshaji (MIUKI) NHC, Haikamen Mlekio, wakati alipokagua Mradi wa Ujenzi wa Hospital ya Rufaa Kanda ya Ziwa, iliyopo katika Manispaa ya Musoma Mjini, mkoani Mara, Desemba 7, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua Mradi wa Ujenzi wa Hospital ya Rufaa Kanda ya Ziwa, iliyopo katika Manispaa ya Musoma Mjini, mkoani Mara, Desemba 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 
SERIKALI KUFUNGUA TIBA ZA MIFUPA NA MISULI HOSPITALI YA MKOA WA MARA - MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inatarajia kufungua kitengo cha tiba za mifupa na misuli katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara Kwangwa mara hospitali hiyo itakapokamilika kujengwa.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa hospitali hiyo iliyopo Manispaa ya Musoma mkoani Mara, leo mchana (Jumamosi, Desemba 7, 2019), Waziri Mkuu amesema kitengo hicho kitakuwa cha pili kwa ukubwa kikifuatia cha MOI Muhimbili.

“Lengo la kufungua kitengo hiki kwenye hospitali hii ni kusogeza huduma karibu na wananchi hususan wa Kanda ya Ziwa ambao kwa sasa wanategemea huduma hizo kutoka hospitali ya Bugando, jijini Mwanza ambayo pia imezidiwa kutokana na udogo wa kitengo hicho kwenye hospitali hiyo,” amesema.

Amesema kuwa ujenzi wa hospitali ya Kwangwa ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano ambapo mbali na kutoa huduma za afya lakini pia hospitali hiyo itafungua fursa zaidi za kiuchumi kwa mkoa wa Mara.

Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliagiza kutolewa kwa shilingi bilioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo uliokwama kwa zaidi ya miaka 40 na ameridhishwa na ujenzi wake unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Bw. Adam Malima alisema hospitali hiyo inatarajiwa kuanza kutoa huduma ya mama na mtoto ifikapo Februari, mwakani baada ya kukamilika kwa jengo A (wing A) mapema mwakani.

Bw. Malima alisema kuwa huduma za rufaa za hospitali ya mkoa wa Mara zinatarajiwa kuanza kutolewa Mei, mwakani huku huduma za kibingwa zikitarajiwa kuanza kutolewa kabla ya mwisho wa mwaka 2020.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa baada ya Rais Magufuli kupokea ombi kutoka mkoa wa Mara kuhusu kusaidia mkwamo wa ujenzi huo, Serikali ilitoa fedha zote (sh. bilioni 15) kwa mara moja ili kukamilisha ujenzi huo.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu akiwa ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa, ameiwakilisha Serikali kwenye mazishi ya kaka wa mke wa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania, Mama Maria Nyerere katika kijiji cha Kinesi kilichopo wilayani Rorya, mkoani Mara.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, ATEMBELEA SHULE YA MSINGI ALIYESOMA MWALIMU JULIUS NYERERE

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi , kwenye Shule ya Msingi Mwisenge, ambayo alilokua akisoma Mwalimu, Julius Nyerere, katika Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, Desemba 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwa na mkewe Mary, wakiwa wamekaa kwenye dawati ambalo alikua akilpenda kulikalia Mwalimu Julius Nyerere, wakati akisoma kwenye Shule ya Msingi Mwisenge, iliyopo katika Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, Desemba 7, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizumza na wananchi, baada ya kukagua Shule ya Msingi Mwisenge, ambayo alilokua akisoma Mwalimu, Julius Nyerere, katiaka Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, Desemba 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma, mkoani Mara, Desemba 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia darasa la Shule ya Msingi Mwisenge, alilokua akisoma Mwalimu, Julius Nyerere, iliyopo katiaka Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, Desemba 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Afisa Elimu Mkoa wa Mara, Emanuel Kisongo,wakati alipotembelea Shule ya Msingi Mwisenge, alilokua akisoma Mwalimu, Julius Nyerere, iliyopo katika Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, Desemba 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MASHINDANO YA MWEZI YA GOFU YAFANYIKA LUGALO

$
0
0
mcheza Golf ya Stephen Chuwalo, wa Lugalo akicheza wakati wa Mashindano ya Ndani ya Mwezi yaliyofanyika katika Viwanja vya Lugalo Jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Zantel anayemtazama ni mchezaji mwenzie,Nathan Mpangala. Picha na luteni Selemani Semunyu.
Mkurugenzi huduma za fedha na Masoko wa Zantel Tanzania Sakyi Opoku (watatu kulia) wakiangalia mpira na wachezaji wenzake wa Golf wakati wa mashindano ya mwezi yaliyoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel katika viwanja vya TPDF Lugalo Golf jijini Dar es Salaam, wa kni mchora vibonzo wa ITV ,Nathan Mpangala, Tinashe Motsi na Stephen Chuwalo. Picha na Luteni Selemani Semunyu
Mchezaji wa timu ya Golf ya Lugalo Khadija Selemani akipiga Mpira wakati wa mashindano golf ya mwezi yaliyoandaliwa na Zantel katika viwanja vya TPDF Lugalo Golf jijini Dar es Salaam. Pich na Luteni Selemani Semunyu. Mkurugenzi huduma za fedha na Masoko wa Zantel Tanzania (MFS) Sakyi Opoku (wapili kulia) wakiandika matokeo na wachezaji wenzake wa Golf wakati wa mashindano ya mwezi yaliyoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel katika viwanja vya TPDF Lugalo Golf jijini Dar es Salaam, anayeandika ni mchora vibonzo wa ITV ,Nathan Mpangala, Tinashe Motsi wa Kampuni ya C.A.O Agent Group na mchezaji wa timu ya Golf ya benki ya NMB Stephen Chuwalo. Picha na Luteni Selemani Semunyu
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images