Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 3268 | 3269 | (Page 3270) | 3271 | 3272 | .... | 3352 | newer

  0 0

  Charles James, Michuzi TV

  SERIKALI imetangaza idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya Sekondari kwa kidato cha kwanza mwaka 2020 kuwa ni 700, 138 sawa na asilimia 92.27.

  Katika idadi hiyo mikoa 13 ya Tanzania bara ikiwemo Dodoma, Shinyanga, Geita, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Morogoro, Mtwara, Njombe, Ruvuma, Singida na Mwanza imeweza kuchagua wanafunzi wote waliofaulu mitihani yao ya Darasa la saba na kujiunga na kidato cha kwanza.

  Akitangaza mchanganuo huo jijini Dodoma leo mbele ya wandishi wa habari, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Mhe Selemani Jafo amesema kati ya wanafunzi hao waliochaguliwa wavulana ni 335513 sawa na asilimia 13 wakati wasichana wakiwa ni 365525 sawa na asilimia 52.14.

  Waziri Jafo ameongeza kuwa kati ya wanafunzi 1161 waliochaguliwa kati ya waliofaulu ni wale wenye ulemavu ambao ni sawa na asilimia 0.41.

  " Wanafunzi 3145 sawa na asilimia 0.41 ya waliofaulu wamechaguliwa kujiunga na bweni,ambapo wanafunzi 970 watajiunga  na shule ya vipaji maalum,huku 1095 watajiunga na shule za ufundi na 1080 watajiunga na shule za bweni za kawaida.

  Hata hivyo,wanafunzi laki 6 na 97 elfu mia 893 sawa na asilimia 99.59 wakiwemo wavulana laki 3 na 61 elfu 866 na wasichana laki 3 95 elfu mia 6 92 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kutwa katika kata mbalimbali nchini," Amesema Waziri Jafo.

  Mhe Jafo amesema kutokana na baadhi ya maeneo nchini kuwa na changamoto ya uhaba wa madarasa imechangia wanafunzi 58,699 sawa na asilimia 7.73 wakiwemo wavulana 28,567 na wasichana 30,132 kukosa nafasi za kujiunga na masomo yao ya kidato cha kwanza.

  Ameitaja Mikoa yenye uhaba wa vyumba vya madarasa ni pamoja na Arusha, Dar es Salaam, Iringa, Kigoma, Lindi, Manyara, Mara, Mbeya, Pwani, Simiyu, Rukwa, Songwe na Tanga ambapo pia amewapongeza Wabunge kwenye baadhi ya maeneo ambao wamechangia kuweza kupatikana kwa vyumba vya madarasa.

  Amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kote nchini kuhakikisha wanafanya maandalizi ya kuwapokea wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza huku pia akiwaagiza viongozi wa maeneo yenye changamoto ya madarasa kumaliza changamoto hiyo ili wale ambao hawajapata nafasi waweze kujiunga na wenzao ifikapo Machi 2020.

  " Kumekuepo na mkanganyiko wa michango gani ambayo wazazi wazazi wanapaswa kutoa pindi watoto wao wanapojiunga na kidato cha kwanza, niwatake wazazi kugharamia mahitaji binafsi ya watoto wao ikiwemo madaftari, sare za shule na wasitoe michango yoyote bila kuwa na ridhaa ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya wa eneo husika," Amesema Jafo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dodoma wakati akitangaza uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020 Tanzania bara.

  0 0  MWENYEKITI wa Baraza la Wazee la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Ndugu Khadija Jabir, na Vyombo vya Habari juu ya taarifa za uchochezi wa kisiasa dhidi ya CCM zilizotolewa hivi karibuni na Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Seif Sharif Hamad.

  **********************************

  NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

  BARAZA la Wazee la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar limelaani vikali taarifa za uchochezi wa kisiasa dhidi ya CCM, zilizotolewa hivi karibuni na Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Seif Sharif Hamad na kueleza kuwa mwanasiasa huyo ana lengo la kuingiza nchi katika machafuko ya kisiasa.

  Kauli hiyo imetolewa jana Mwenyekiti wa Baraza hilo,Khadija Jabir Mohamed wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kuu ya CCM kisiwandui ambapo alisema mwanasiasa huyo ameanza kupotosha umma kuhusu mgogoro wao dhidi ya CUF na kuingiza CCM.

  Alisema kauli zilizotolewa na mwanasiasa huyo ni za uchochezi na kwamba analeta fitina ndani ya Zanzibar lakini wazee wa CCM wanampa onyo kali kuhusu maneno anayoyatoa.

  “Baraza la wazee linakemea kauli zake za Seif Sharif Hamad kwa ukali sana tunamuonya kutokana na kuwa yeye ni mtoto mdogo na amelelewa na CCM wakati akitoka kusoma chuo kikuu hakachukuliwa hivyo anafanya mambo bila ya kujua anachokifanya,”alisema

  Alisema mwanasiasa huyo hajui kuongoza katika siasa kutokana na kuwa anafanya mambo hasiyojua mbele yake na kwamba anachokifanya ni kuleta mtafaruku ndani ya Zanzibar.

  “CCM ina wazee si chama ambacho kama vingine ambavyo havina wazee wakuweza kukemea mambo ambayo hayakwendi vizuri hivyo kwa niaba ya Baraza la Wazee tutaendelea kumkemea dhidi ya kauli zake za uchochezi,”alisema Mwenyekiti huyo.

  Naye Katibu Msaadizi wa Baraza hilo la Wazee Haji Machano Haji alisema hivi karibuni mwanasiasa huyo alisikika akiwasingizia vijana wa CCM kuwa wanandoa bendera za chama cha ACT Wazalendo kwenye matawi jambo ambalo ni la uzushi na kwamba ugombi wa majengo ya matawi kati ya vyama hivyo unawahusu wao wenyewe.

  Katika maelezo yake alisema Baraza la wazee linampa tahadhari Seif Sharif kuwa anapokaa na wafuasi wake asitoe maneno ya uzushi ama ya fitina hivyo wazee wanamuona mwanasiasa huyo anapaswa kupumzika ili kulinda heshima yake.

  “Sisi wazee tumesikia maelezo ya Seif Sharif Hamad aliyoyatoa kwa waandishi wa habari Desemba 2 mwaka huu kwa kukisingizia CCM kwamba inapanga njama ya kuwakamata viongozi wa ACT Wazalendo na kuwambambikizia kesi tunachosema ni mawazo yake,”alisema

  Aliongeza kuwa Baraza la Wazee linamuhakikishia Seif Sharif Hamad kuwa CCM haia mkono wowote ndani ya CUF na kwamba wazee wanakitambua chama hicho ni chama cha upinzani kama ilivyo vyama vyengine vya upinzani na mapambano ya chama ni kuvishinda vyama vya upinzani.

  Desemba 2 mwaka huu Seif Sharif Hamad alizungumza na waandishi wa habari ofisi ya chama chake cha ACT-Wazalendo ambapo alitoa kauli za uchochezi kwa kuwahamasisha wafuasi wake watumie silaha za jadi kwa ajili ya kuzilinda ofisi za chama chake dhidi ya chama cha CUF ambacho wapo katika mgogoro wa umiliki wa majengo ya ofisi za vyama hivyo.

  Seif Sharif Hamad aliwataka viongozi na wanachama wa ngazi zote za chama chake kwa maeneo ya mijini na vijijini kwa upande wa Unguja,Pemba kuzilinda ofisi zote za chama chao na kutoruhusu kuchukuliwa kwa ofisi hizo.

  Katika mkutano huo Seif Sharif Hamad alisema wamevumilia vya kutosha na kwamba sasa kutokana na kuwa ni muda mrefu wamevumilia kutokana na maslahi ya nchi lakini wameona wenzeao hawako tayari kuilinda amani.

  Maalim Seif alisema wako tayari kumwaga mboga wenzao wakimwaga mchuzi na kwamba alisema chama cha CUF kwa upande wa Pemba kimeanza kuvamia ofisi za ACT-Wazalendo kwa lengo la kuzichukua na kuzifanya ofisi za chama chao kwa madai ni ofisi zao.

  0 0


  NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA 

  MKUU wa wilaya ya Kibaha ,mkoani Pwani ,Assumpter Mshama ameeleza iko haja ya kuwa na usawa wa kijinsia kwa watoto wa kike na wa kiume pindi mwanafunzi wa kike anapopata mimba akiwa shuleni,ili iwe fundisho kwa wanafunzi wengine . 

  Ameeleza, inapaswa mtoto wa kike nae achukuliwe hatua sawa na mtoto wa kiume kwani ujauzito hautokani na upande mmoja bali ni ushirika wa watu wawili wa jinsia mbili tofauti. 

  Akizungumza katika mahafali ya wanafunzi wa chuo cha ufundi stadi VETA Pwani , pamoja na mambo mengine, Mshama anasema ifikie hatua kila mwanafunzi apate adhabu sawa baada ya kupeana mimba ili kukomesha tabia hiyo. 

  “Kwa wilaya hii wote mtapata adhabu, haiwezekani mtoto wa kike aendelee kutamba wakati muda mwingine unakuta mtoto huyo ndio alikuwa chanzo cha kumtongoza mwalimu au mwanafunzi mwenzie,hamjawahi kuona hilo

  Aidha Mshama alishauri Vijana hao waliomaliza chuo cha ufundi stadi VETA, kujiajiri kwa kufungua viwanda vidogo vidogo na kutengeneza vifaa vyenye ubora ili waweze kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira. 

  Mapema wakisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi wanachuo ZAHARA ABDUL na IDD ATHUMANI waliiomba serikali ya mkoa huo,kutoa kipaumbele cha ajira na fursa mbalimbali zilizoko ndani ya mkoa.
  Nae kaimu mkuu wa chuo hicho ,Karim aliainisha changamoto kubwa inayoikabili chuo ni upungufu wa mabweni.
   

  0 0


  Maafisa wa Wizara wakiwa ndani ya Banda la Wizara tayari kwa ajili ya kuwahudumia wananchi watakaotembelea Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji Biashara Tanzania (TANTRADE) yaliyoanza tarehe 5, Desemba 2019 katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
  Maafisa wa Wizara wakiwa ndani ya Banda la Wizara tayari kwa ajili ya kuwahudumia wananchi watakaotembelea Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji Biashara Tanzania (TANTRADE) yaliyoanza tarehe 5, Desemba 2019 katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
  Afisa wa Wizara akiwa ndanii ya Banda la Wizara tayari kwa ajili ya kuwahudumia wananchi watakaotembelea Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji Biashara Tanzania (TANTRADE) yaliyoanza tarehe 5, Desemba 2019 katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

  ………………

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inashiriki katika Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).

  Kupitia Maonesho hayo, Wananchi wanaelimishwa kuhusu majukumu ya Wizara na utekele zaji wake na namna wizara na balozi za Tanzania zinavyofanya kazi ya kuvutia watalii na wawekezaji kuja nchini kutembelea vivutio vya kitalii na kuwekeza nchini.

  Maonesho hayo ni utekelezaji kwa vitendo kwa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Viwanda ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2021.

  Kauli mbiu ya maonesho hayo ya Tanzania sasa Tunajenga Viwanda inalenga kujenga na kuimarisha utamaduni wa Watanzania kutambua, kununua na kuthamini bidhaa zinazozalishwa nchini.

  Maonyesho ya Nne ya Viwanda yanahusisha wadau wa Sekta ya Viwanda na yataonesha fursa zilizopo katika katika sekta ya viwanda na yatatoa fursa kwa wadau kuzungumza na kujadili namna ya kujenga mahusiano endelevu ya biashara.

  Maonyesho hayo pia yatawezesha kufanyika kwa mikutano ya wafanyabiashara ambayo itawakutanisha wauzaji na wanunuzi .

  0 0

  Charles James, Michuzi TV

  WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais menejimenti na utumishi wa Umma Kapteni John Mkuchika ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU)  kudhibiti vitendo vya rushwa katika Vyama vya Ushirika kutokana na ubadhilifu unaofanywa na wafanyakazi.

  Hayo yamesemwa na Waziri Mkuchika wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa Takukuru wenye kaulimbiu ya kupambana na rushwa ni wajibu wa kila mtu uliofanyika jijini hapa.

  Mhe Mkuchika amesema, pamoja na kazi nzuri inayofanywa na TAKUKURU lakini bado yapo malalamiko mengi ya wakulima kutolipwa kwa wakati, ikiwemo kudaiwa rushwa ili waweze kulipwa, fedha zao ambazo ni haki yao.

  "Vyama kupokea fedha na kutowalipa kabisa baadhi ya wakulima, ni ukosefu wa uadilifu kwa viongozi na watumishi wa Vyama vya Ushirika ikiwa ni pamoja na kujilimbikizia mali ambazo sio halali,'amesema Mkuchika..


  Amesema TAKUKURU mnapaswa kufuatilia na kuchukua hatua stahiki ili Vyama vya Ushirika visiwe ni kichaka cha wala rushwa,wezi na wala rushwa za haki ya wakulima.

  Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa katika Vyama vya Ushirika, wapo baadhi ya wafanyakazi wamejilimbikizia mali ambazo wanashindwa kuzitolea maelezo ya jinsi walivyozipata, hivyo ameitaka TAKUKURU kuchukua hatua stahiki na kuwasilisha mapendekezo ya nini kifanyike.

  Aidha, Mhe Mkuchika ameipongeza TAKUKURU kwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 950 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa Wilayani Ruangwa Oktoba, 2019 ya kuitaka TAKUKURU kufuatilia fedha zote walizodhulumiwa wakulima wa ufuta mkoani Lindi.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Generali  John Mbungo amesema katika tathmini ya utendaji  wao mwaka huu wamefanikiwa kwa asilimia 88.1 kitu ambacho ni kiwango cha juu kuwahi kufikia.

  Amesema kutokana na agizo la Rais Dk John Magufuli la kukusanya fedha za wakulima wa ufuta zilizoibiwa na vyama vya ushirika wamefanikiwa kukusanya sh zaidi ya million 900 ambazo zitakabidhiwa kwa wakulima.

  Amesema awali Rais Magufuli amesema wakulima hao waliibiwa sh million 423 na vyama 10 vya ushirika,lakini katika uchunguzi wa Takukuru wamebaini sh billion 1.43 ambazo zimeibiwa na vyama 31 vya ushirika.

  “Tumebaini ni vyama 31 vya ushirika na fedha zilizoibiwa ni zaidi y sh billion moja na hadi sasa milioni 900 tayari zimereshwa na zilizosalia zitarejeshwa zote kwa sababu tarehe ya mwisho ni leo," Amesema Mbungo.

  Mbali na hilo amesema jumla ya miradi 1,106 katika sekta ya maji,elimu,Afya na ujenzi ambayo inathamani y ash Trion 1.5,katika ufuatiliaji wao kiasi cha sh billion 43.3 kimebainika kufanyiwa ubadhilifu na hatua stahiki dhidi ya wahusika zinaendelea kuchukuliwa.

  Amesema sh billion 23.7 zimeokolewa kutokana na oparesheni mbalimbali za uchunguzi na uzuiaji rushwa na kuongeza kuwa mali zenye thamani y ash billion 10.1 zilizopatikana kwa njia ya rushwa zimetaifishwa na mali za washtakiwa zenye thamani y ash billion 25.27 na Dola za Marekani million 5.67ziliwekewa zuio kwa lengo la ukamilishaji wa taratibu za kisheria kwa ajili ya utaifishaji wake.

  Mbali na hilo alisema katika utekelezaji wake kesi 497 zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini,zikiwemo rushwa kubwa nne zilizofunguliwa katika mahakama ya mafisadi nchini,ambapo kati ya hizo wameshinda kesi  206 ambapo ni sawa na asilimia 60.4 jambo ambalo ni mafanikio makubwa
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika ,akizungumza wakati  akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika jijini Dodoma leo.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo akitoa taarifa ya utekelezaji ya TAKUKURU Wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika  jijini Dodoma leo

   

  0 0

  TAASISI ya kutetea masuala ya ukatili wa kijinsia (PHLI) ya Dar es salaam kwa kushirikiana na jeshi la polisi wameazimia namna ya kuifikia jamii katika kuipa uelewa dhidi ya vitendo vya rushwa ya ngono ambavyo vimeongezeka kwa watoto na wanawake.

  Mjadala huo uliofanyika katika kituo cha polisi kati Dar es salaam kiliibua hoja mbalimbali kwa washiriki katika kukomesha na kutokomeza ukatili wa kijinsia ambapo maazisho yalianza novemba 25 hadi kilele chake disemba 12 mwaka huu.

  Akizungumza katika kikao hicho mtaalamu kutoka taasisi ya Prosperous health life initiative (PHLI) wakili Hilda Dadu alisema inapaswa kuwa na mijadala ya pamoja kati ya asasi na jeshi la polisi namna ya kuwafikia wananchi kwa kuwapa uelewa wa matukio ya unyanyasaji yatokanayo na rushwa ya ngono.

  "Vyombo hivi vinatakiwa vikutane pamoja kwa kuweka mikakati madhubuti ya kuweza kuifikia na kuielimisha jamii kuhusiana na matukio ya kikatili yanayofanywa na baadhi ya watu," alisema Dadu

  Dadu amesema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la matukio yatokanayo na rushwa ya ngono  katika maeneo ya kazi,  mashuleni, mavyuoni na hata kwenye vituo vya afya yanayofanywa na baadhi ya watu kuweza kujinufaisha kimwili.

  Kwa upande wake RPO wa mkoa wa kipolisi ilala Emmanuel Pango amesema kuwa chanzo kikubwa cha rushwa ya ngono inatokana na mmomonyoko wa maadili katika jamii na kufanya mdogo kuto muheshimu mkubwa na mkubwa kuto muheshimu mdogo.

  Amesema kuwa kwa umoja wanatakiwa kuifikia jamii kwa kuiambia na kuihakikishia kuwa matendo maovu yatokanayo na rushwa ya ngono yanaweza kuepukika kwa wahusika kuweza kuchukuliwa hatua stahiki baada ya tukio kutokea.

  Aliendelea kwa kusema suala la rushwa makazini ni jambo ambalo haliwezi kuvumilika wala halikubaliki ndani ya jamii hivyo basi kila mmoja anatakiwa kuwa makini kwa kulitolea taarifa kwa haraka kwenye  madawati ama vituo vya polisi ama vya kisheria.

  Naye kamishna msaidizi mnadhimu namba moja katika mkoa wa kipolisi Ilala Janeth Stephano amesema kuwa mjadala huo uwe ni muendelezo wa kuchukua hatua za kuifikia kwa kuipa uelewa wa kutosha kwa minajili ya kupunguza na kutokomeza masula ya ukatili na rushwa ngono kwa Watoto na wanawake.

  Kikosi cha jeshi la polisi pamoja na wanaharakati wa masula la kupinga ukatili wa kijinsia mara baada ya kumaliza kikao

  0 0


  Na Said.Mwishehe, Michuzi TV-Mwanza

  UONGOZI wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania  (TPA), Kanda ya Ziwa jijini Mwanza umesema umeweka mikakati ya kukomesha utitiri wa bandari bubu karibu 300 katika ziwa Victoria.

  Umesema katika kuhakikisha bandari ya Kanda ya Ziwa anaongea ,ukusanyaji wa mapato kutokana na huduma inazotoa,umeamua kuwa na malengo ya kuhakikisha bandari hizo zinatambulika na kuwa vyanzo cha mapato.

  Akizingumza leo akiwa ofisini kwake jijini Mwanza, Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Morris Machindiuza amesema wameamua kukabiliana na changamoto ya uwepo wa bandari bubu na watazichukulia hatua kwa mujibu wa sheria ambayo inaeleza wazi shughuli zote upakiaji,upakuaji na usimamizi wa shughuli za bandari ziko chini ya mamlaka ya TPA.

  Hata hivyo amesema kuwa pamoja na kukabiliana na bandari bubu, pia TPA imepewa jukumu ya kuendeleza bandari na kuendesha, kutangaza huduma za bandari kwa kushirikiana na sekra binafsi katika uendeshaji wa bandari.

  “Katika mwambao wa Ziwa Victoria TPA inamiliki na kusimamia bandari kubwa za Mwanza Kaskazini na Kusini, Nansio, Kemondo Bay, Bukoba na Musoma pia kuna bandari zingine ndogo za mwambao zaidi ya 15 ambazo zote tunazihudumia kwa kuwa chini ya usimamizi wetu,” amesema Machindiuza.

  Pia amesema TPA inaendesha Bandari Kavu ya Isaka ambayo inamilikiwa na Shirika la Reli Tanzania ambapo kuwa ghala kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi shehena ya tani 3,000, yadi ya makasha na yadi ya Rwanda yenye eneo la ekari 17.05.

  Kuhusu hali ya mapato amesema imepanda kutoka Sh milioni 600 hadi kufikia Sh bilioni 1.4 jambo ambalo ni la kutia moyo katika uendeshaji wa shughuli za bandari.
   
  “Kwa sasa Serikali ya Awamu ya Tano mkakati mkubwa ni kukusanya mapato ya ndani, nasi TPA kama wadaui taasisi muhimu tunalizingatia hilo kwa kuhakikisha tunatafuta wafanyabishara ambao ilin waweze kutumia bandari zetu,” ameongeza Machindiuza
   Moja ya meli ya mizigo ambayo imekuwa ikitumika kubeba mabehewa yenye konteza za mizigo ambayo inatoka jijini Dar es Salaam kwa kutumia reli ya kati na kisha kuingizwa kwenye meli hiyo kuelekea nchini Uganda.
   Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Morris Machimbiuza akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Desemba 5, mwaka 2019 kuhusu mikakati iliyowekwa katika kuhakikisha wanaendelea kuboresha utoaji huduma katika bandari za kanda ya Ziwa.Pia amezungumzia mafanikio ambayo yamepatikana katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.
   Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Morris Machimbiuza akiwa na baadhi ya maofisa wa Bandari za Ziwa Victoria pamoja na waandishi wa habari baada ya kuonesha daraja la reli ambalo linatumika kupitisha kontena kutoka katika behewa za treni kwenda katika meli za mizigo bandarini hapo.

   Sehemu ya reli inayotumika kwa ajili ya kupitisha behewa za mizigo kuingizwa kwenye meli za mizigo katika Bandari ya Kanda ya Ziwa jijini Mwanza.
   Daraja la reli ya kupitisha mabehewa yenye mizigo kupandishwa katika meli kwa ajili ya kusafirisha katika nchi jirani ambazo zinatumia bandari ya Ziwa Victoria kusafirisha mizigo yake.
   Muonekana wa sehemu ya Bandari ya Kanda ya Ziwa huku baadhi ya watumishi wa bandari hiyo wakionekana kwa mbali wakiendelea na majukumu yao ya kila siku.PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE

  0 0

  UTAFITI uliyofanywa na Shirika linalohusika na usalama  na Ustawi wa wanyama Duniani (World Animal Protection) umebaini kuwa kuku wengi wanaouzwa katika maeneo mbalimbali nchini wakidaiwa kuwa ni wa kienyeji si wa kienyeji kama inavyosemwa.

  Utafiti huo umebaini kuku hao si wa kienyeji bali ni kuku wa kisasa maarufu kama kuku wa kizungu wanaofungwa majumbani kwa kupewa majani pamoja  na dawa mbalimbali za kuwakuza na kuwafanya kuwa wagumu.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati akiwasilisha ripoti ya utafiti huo uliyofanywa katika nchi nne Tanzania ikiwamo, Msemaji Mkuu wa Shirika hilo, Victor Yamo alisema utafiti huo ambao ulifanywa Juni hadi Julai mwaka huu katika mikoa ya Arusha na Dar es Salaam umebaini jambo hilo hivyo watumiaji wanapaswa kuwa makini.

  Yamo amesema kuku wengi wanauzwa katika mikoa hiyo wamekuwa wakupewa dawa za kuwakuza  ambazo zina madhara kwa binadamu pindi wanapotafuna mifupo yao

  "Wakati watu wetu wakitembelea kwenye masoko mbalimbali kuulizia bei ya kuku na wakabaini uwepo wa kuku wa kisasa wengi na mwananchi uuziwa kwa kuambia kuwa ni wa kienyeji jambo ambalo ni uongo," alisema.

  Amesema utafiti huo ulifanyika kwa lengo la kujua walaji wananunua nyama za aina gani, kutoka wapi pamoja na  kuangalia kama wanafahamu ubora wa chakula na matumizi ya dawa za wanyama.

  "Tunaamini kuwa mteja ataelewa nyama anayotaka kununua au kula inaubora au tatizo kiasi gani itakuwa rahisi kujiepusha nayo na kutafuta kitu kingine mbadala cha kula," alisema

  Aidha Yamo amesema kwa sasa Shirika lao linafanya jitihada kubwa kuhakikisha linaimarisha ustawi na haki za wanyama na sheria za kuwalinda wanyama hao zinapitishwa na serikali husika katika kila nchi.

  Amesema pamoja na kuyafanya hao wanatoa wito kwa watanzania waanze kuelewa kuwa kama watashindwa kuangalia ustawi wa wanyama hasa wanaoliwa kuna hatari kubwa ya kupotea.

  "Ni ukweli uliyowazi kuwa ustawi wa wanyama ni muhimu sana na kwa kutambua hilo tumekuwa tukienda mashuleni kufundisha jambo hilo na masuala ya usalama wa chakula na ubora wa dawa," alisema.
  Mtaalamu wa masuala ya kutetea Haki na Ustawi wa Wanyama kutoka shirika la World Anima Protection ,Dkt Victor Yamo akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar,alipokuwa akiwasilisha ripoti ya utafiti uliyofanywa katika nchi nne Tanzania ikiwamo, kuhusu kubainika kwa kuku wengi wanaouzwa katika maeneo mbalimbali nchini wakidaiwa kuwa ni wa kienyeji kumbe si wa kienyeji kama inavyosemwa.
   Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza mtaalamu huyo wa Haki na Ustawi wa Wanyama kutoka shirika la World Anima Protection ,Dkt Victor Yamo alipokuwa akiendelea kufafanua mambo mbalimbali yahusuy haki na ustawi wa Wanyama nchini Tanzania 
   Mtaalamu wa masuala ya kutetea Haki na Ustawi wa Wanyama kutoka shirika la World Anima Protection ,Dkt Victor Yamo akifafanua jambo kwa msisitizo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar,alipokuwa akiwasilisha ripoti ya utafiti uliyofanywa katika nchi nne Tanzania ikiwamo, kuhusu kubainika kwa kuku wengi wanaouzwa katika maeneo mbalimbali nchini wakidaiwa kuwa ni wa kienyeji kumbe si wa kienyeji kama inavyosemwa.


  0 0

  Katika kuelekea Msimu wa Sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa ofa kabambe kwa wananchi wote wenye magari kufanyiwa ukaguzi wa magari yao na kupatiwa ushauri wa kitaalamu bure kwa muda wa siku tano kuanzia Jumanne ya Disemba 10 hadi 15 kwenye zaidi ya Garage100 zilizopo jijini humo.

  RC Makonda amesema lengo la kutoa ofa hiyo ni kuwawezesha wananchi wanaopenda kusafiri na familia zao kula sikukuu kusafiri salama na kurudi salaam wakiwa na uhakika na usalama wa vyombo vyao vya usafiri ili kuepusha ajali zitokanazo na ubovu wa magari.

  Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kufanya kikao na Wamiliki wa Garage na mafundi na kuwapa ombi la kumsaidia kufanya ukaguzi wa magari ambapo wamiliki hao wamepokea kwa mikono miwili ombi hilo la Mkuu wa Mkoa kwakuwa linalenga kuepusha ajali.

  Aidha RC Makonda amesema licha ya zoezi hilo kuwasaidia wananchi pia litawafanya wenye Garage kujitangaza na kuongeza idadi ya wateja wapya.

  Hata hivyo RC Makonda ameeleza mpango wa kuwaunganisha watu wa Garage na Chuo cha ufundi Stadi VETA ili watoe mafunzo na vyeti jambo litakalowafanya kuongeza ujuzi na Maarifa ya kazi na kujenga imani kwa wateja huku akiwahimiza wenye Garage kuzirasimisha Garage zao ili waweze kulipa kodi serikalini na kutambulika.

  Pamoja na hayo RC Makonda amesema kuwa majina ya Garage zitakazotoa huduma hiyo zitatangazwa kwenye vyombo vya habari siku yoyote kuanzia leo ili Mwananchi achague wapi Kwa kupeleka Gari lake.

  0 0  Deogratias Maneno Mkurugenzi wa Huduma za Biashara Wakala wa Vipimo (WMA) akiweka vizuri moja ya jiwe  linalotumika kupima uzito wa madini baada ya kulitoa kwenye sanduku maalum leo katika maonesho ya bidhaa yanayofanyika kwenye banda la Karume viwanja vya Sabasaba barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam ambapo taasisi hiyo inashiriki kushoto anayetazama ni Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Vipimo (WMA).
  Kutoka kushoto Deogratias Maneno Mkurugenzi wa Huduma za Biashara Wakala wa Vipimo (WMA) Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Vipimo (WMA) na Almachius Pastory Kaimu Meneja Sehemu ya Ukaguzi na Ufuatiliaji Wakala wa Vipimo (WMA) wakitoa maelezo kwa mwandishi wa habari wa TBC Stanley Ganzel pamoja na Rose Eric mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda hilo leo kwenye maonesho ya bidhaa yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam leo.
  Almachius Pastory Kaimu Meneja Sehemu ya Ukaguzi na Ufuatiliaji Wakala wa Vipimo (WMA) urefu na upana wa nondo ili kumlinda mtumiaji huku mwandishi wa habari wa TBC Stanley Ganzel pamoja na mmoja wa wananchi Rose Eric waliotembelea katika banda hilo wakishuhudia kushoto ni Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Vipimo (WMA).
  Almachius Pastory Kaimu Meneja Sehemu ya Ukaguzi na Ufuatiliaji Wakala wa Vipimo (WMA) urefu na upana wa bati (Guage) ili kumlinda mtumiajihuku mwandishi wa habari wa TBC Stanley Ganzel pamoja na Rose Eric mmoja wa wananchi  waliotembelea katika banda hilo wakishuhudia kutoka kushoto ni Deogratias Maneno Mkurugenzi wa Huduma za Biashara Wakala wa Vipimo (WMA) na Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Vipimo (WMA).
  Almachius Pastory Kaimu Meneja Sehemu ya Ukaguzi na Ufuatiliaji Wakala wa Vipimo (WMA) akitoa maelezo namna  ujazo wa vimiminika unavyopimwa.
  Deogratias Maneno Mkurugenzi wa Huduma za Biashara Wakala wa Vipimo (WMA) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akifafanua zaidi kwa wananchi waliotembelea banda hilo namna ujazo wa vimiminika unavyopimwa.
  Muonekano wa banda la Wakala wa Vipimo WMA.

  0 0     


   
   
   

  0 0

  BENKI ya NMB imekabidhi zawadi kwa washindi tisa wa MastaBoda kama washindi wa wiki baada ya kufikisha miamala hamsini kupitia mfumo wa malipo wa Mastercard QR katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. Zoezi hilo liliendeshwa na Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi- Yusuph Achayo na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda- Michael Massawe. 

  MastaBoda ni kampeni inayoendeshwa na NMB kwa ajili ya kuwawezesha waendesha Bodaboda kuunganishwa katika mfumo wa kibenki ili waweze kupokea malipo kupitia mfumo wa Mastercard QR pamoja na mitandao ya simu iliyo unganishwa na mfumo wa malipo wa Mastercard QR. 

  Akikabidhi zawadi hizo Achayo ametoa wito kwa waendesha Bodaboda ambao hawajajiunga na mfumo wa MastaBoda kujiunga ili kuendesha biashara zao kisasa kwa usalama wa fedha zao. 

  Nao washindi walioibuka na kitita cha Sh, 50,000. Wameimwagia sifa NMB kwa kutimiza ahadi, kwani zinawaongezea nguvu ya kupambana ili kufika mbali zaidi katika kuendesha biashara zao. 

  “Tangia nijiunge na mfumo huu, hii ni mara yangu ya pili kushinda, najisikia furaha sana. Tangu nianze kufanya miamala na QR nina amani, badala ya kutembea na pesa sasa fedha yangu inaingia moja kwa moja benki, mfumo huu pia unaookoa muda hasa katika kutafuta chenchi. .”alisema Ebenezer Elisha (Mwenge) ambaye pia ni mmoja wa washindi. 

  Washindi wengine waliojizolea kitita hicho ni Goodluck Ntaya (Kawe Ukwamani), Mohamed Abdallah (Buguruni Rozana) Twaliha Mfinanga(Rozani Mafleti) na Frorian Byabato (Roziani Mafleti).
   Meneja Mahusiano wa Kitengo cha Kadi Benki ya NMB - Yusuph Achayo (kushoto) akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu 50,000 dereva Bodaboda wa Kituo cha Kibamba Hospitali-Jonas Ruben. Akishuhudia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam, Michael Massawe.
   Bodaboda wa Kituo cha Kimara kwa Msuguri - Gasper Ngoh akipokea zawadi ya fedha taslimu 50,000 kwa kufanya miamala mingi ya kulipwa na wateja wake kupitia mfumo wa Mastercard QR. 
   Dereva wa Bodaboda wa kituo cha Ubungo Plaza- Abubakar Mohamed, akipokea pesa taslimu 50,000 Kwa kuibuka mshindi kwa kufanya miamala mingi - kulipwa na wateja wake kupitia mfumo wa Mastercard QR. 
  Dereva wa Bodaboda wa Kituo Sayansi Adam nae alikabidhiwa zawadi ya fedha taslimu 50,000 kwa kufanya miamala mingi ya kulipwa na wateja wake kupitia mfumo wa Mastacard QR

  0 0

  WABUNIFU wametakiwa kujua jinsi ya kulinda bunifu zao kwa kutumia mihimili ya miliki bunifu ikiwa ni pamoja na kujua nyenzo wanazoweza kuzitumia, hatua na aina gani ya miliki bunifu zinazohitajika kwa bunifu zao.

  Mshauri wa masuala ya mambo ya hakimiliki bunifu, kutoka Kituo cha uendelezaji na uhaulishaji wa teknolojia katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Judith Kadege alisema Tume hiyo ipo kwa ajili ya kuwajengea uwezo na kuwashauri wadau tofauti katika sekta ya utafiti na ubunifu nchini.

  Alisititiza kuwa, elimu ya miliki bunifu inasaidia kujua haki za wabunifu kabla ya kuanza kubuni kitu ambacho wanakifikiria, pia hapo alipobuni akitaka teknolojia hiyo au bunifu yake itumike sehemu nyingine anatakiwa afanya kitu kipi kabla.

  “Yote hayo tunafundisha ili kulinda ile miliki bunifu yake isije ikaibiwa, au ikatupwa au ikatumiwa ndivyo sivyo bila ya idhini yake ama kibiashara au kwa matumizi mengine,” alisema.

  Kwa maelezo yake wabunifu wengi wana mlengo wa ujasiriamali kwa hiyo kwenye kusaidia hizo teknolojia zao katika mlengo wa kujua haki zao za ulinzi wa miliki bunifu itasaidia kujua wapeleke wapi bunifu ambayo imepata ulinzi wa miliki bunifu ili iweze kufanyiwa kazi.

  “Hii inafanyika duniani kote kuwa ulinzi wa miliki bunifu unakupa wewe mmiliki wa hiyo bunifu uwezo wa kuweza kujua jinsi gani unaweza kuongea hata na makampuni makubwa waweze kutumia hiyo teknolojia yako,” alisema.

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeleshaji na Uhaulishaji wa Teknolojia katika Tume hiyo, Dkt.Athuman Mgumia alisema waliandaa mafunzo hayo kwa wabunifu 60 walioshiriki na kushinda Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi na Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) ili kuendeleza bunifu zao.

  Alisema mafunzo hayo yatawasaidia katika kuboresha teknolojia zao na kuweza kuhakikisha kama zinawafikia walengwa wao waliowakusudia.

  Mhandisi wa Mitambo ambaye ni mbunifu Kennedy Mwakatundu, alikiri kuwa kama wabunifu kuna vitu ambavyo hawavilindi kisheria au sheria haiwalindi hivyo kupitia mafunzo hayo kutawawezesha kuwa na ujuzi wa kulinda kazi zao.

  “Kuna wakati ambapo migogoro inaweza kutokea lakini kumbe inaweza kuepukika bila matatizo yoyote na watu kupelekana hatua zingine, kama mbunifu unatakiwa kuelewa jinsi ya kuepuka hiyo migogoro ili usipotezewe muda wa kuihangaikia,” alisema.

  Mbunifu huyo ambaye ametengeneza mashine ya kusafisha fukwe za bahari ambazo hali yake siyo nzuri alishauri mafunzo hayo pia yawe ni sehemu ya kuwaandaa watoto wadogo kuweza kujua ikiwa wana kipaji fulani na kama akikitumia kipaji alichonacho kitamnufaishaje na nani atakuwa mlinzi wake.

  Mbunifu mwingine wa kitanda cha kuweka kwenye gari la wagonjwa ambachokinajiendesha chenyewe, Diana Kaijage alisema mafunzo waliyoyapata yatawasaidia katika kulinda kazi zao walizozifanya.
   Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeleshaji na Uhaulishaji wa Teknolojia (COSTECH) Dkt.Athuman Mgumia katika akieleza waandishi wa habari lengo la mafunzo hayo.
   Mshauri wa masuala ya mambo ya hakimiliki bunifu, kutoka Kituo cha uendelezaji na uhaulishaji wa teknolojia katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Judith Kadege akifafanua juu ya umuhimu wa haki miliki bunifu. 
   Wa kwanza kulia ni mbunifu wa kitanda cha kuweka kwenye gari la wagonjwa ambachokinajiendesha chenyewe, Mhandisi Diana Kaijageakizungumzia kuhusiana na kitnda hicho katika magari.
   Wa pili kushoto ni Mhandisi Kennedy Mwakatundu Mbunifu ambaye ametengeneza mashine ya kusafisha fukwe za bahari akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jinsi alivyotengeneza mashine ya kusafishia fukwe za bahari.

  0 0

  BAADHI ya  watumiaji wa Barabara ya Kibaoni-Stalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi, wameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa ujenzi wake ili kuwaondolea kero wanayokutana nayo hasa msimu huu wa masika.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Ripota Wetu walisema, barabara hiyo yenye urefu wa km 71 inayopita katika ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi  kwa sasa imekuwa kero kubwa kutokana na utelezi  na mashimo,jambo linalo sababisha magari kukwama na kupoteza muda mwingi  wa kufanya shughuli za maendeleo wakiwa njiani.

  Athanas John na Miriam Daniel wameiomba Serikali kupitia wakala wa Barabara (Tanroad) mkoa wa Katavi kutafuta fedha ili kuijenga barabara hiyo ambayo  inachangia kurudisha nyuma uchumi wa mkoa wa Katavi na mikoa mingine  ya Rukwa, Kigoma na Tabora.

  Athanas alisema, kama barabara hiyo ingejengwa kwa kiwango cha lami basi  kungekuwa na fursa kubwa ya usafiri na usafirishaj bidhaa za mashambani  hivyo kutoa nafasi kwa wananchi kuwahi katika majukumu yao ya  kimaendeleo tofauti na sasa ambapo wanalazimika kutumia masaa mawili hadi matatu.
  Baadhi ya  magari yakiwa yamekwama katika Barabara ya Mpanda -Sumbawanga mkoani Katavi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa wingi katika mikoa ya Nyanda za juu na hivyo kusababisha magari kukwama na kupelekea kero kubwa kwa wasafiri.

  Mmoja wa Dereva anayefanya safari zake kati ya mkoa wa Katavi na mkoa  wa Rukwa ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema, barabara imekuwa chanzo cha kuharibika magari yao na hivyo kuwaongezea hasara kubwa.

  Alisema, wakati umefika kwa Serikali  kuiangalia barabara hiyo ambayo ni kiungo kikubwa kwa uchumi wa mkoa,  kupitisha mazao na hata kurahisisha shughuli za utalii katika hifadhi  maarufu ya Katavi.

  Kwa upande wake Meneja wa Tanroad mkoa wa Katavi Martin Mwakabende alisema, ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa km 71 na kati ya hizo km 44 inapita kwenye hifadhi ya Katavi haujaanza,hata hivyo Ofisi ya Wakala wa Barabara Tanroad imeandaa ripoti ya awali itakayosaidia usanifu wake.

  Alisema, Rais Dkt John Magufuri akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Katavi Mwezi Novemba mwaka huu  aliahidi kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

  Aidha alitaja barabara ya Kizi Lyambamfipa hadi Sitalike yenye urefu wa km86.5 kati ya hizo km 50 zipo kwenye hifadhi ya Katavi bado haujaanza ambapo zoezi la upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ulikamilika tangu mwaka 2009 na Serikali inafanya jitihada kutafuta fedha za ujenzi kwa kiwango cha lami.

  0 0

  Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, akikabidhi vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wa kijiji cha Kabukome, wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera, alipokuwa katika ziara ya kazi, Desemba 5, 2019.
  Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabukome, wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera, akiwa katika ziara ya kazi, Desemba 5, 2019.
  Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ambao waliambatana na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), katika ziara yake kijijini Kabukome, Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera, Desemba 5, 2019 wakiwa wamesimama mbele ya wananchi kwa ajili ya utambulisho.

  Veronica Simba – Biharamulo

  Wananchi wa kijiji cha Kabukome, Kata ya Nyalubungo, wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera, wameruka kwa nderemo na vifijo, wakifurahia maagizo aliyoyatoa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani Desemba 5, 2019, kuwa kijiji hicho kiwe kimewashiwa umeme ifikapo Januari 30 mwakani.

  Waziri alitoa maagizo hayo mbele ya umati wa wananchi wa kijiji hicho, kwa watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Mkandarasi anayetekeleza miradi ya umeme vijijini wilayani Biharamulo.

  “Leo ni tarehe 5 Desemba; Nataka kuona ikifika tarehe 20 mwezi huu, nguzo ziwe zimeshaanza kusimikwa hapa Kabukome, na tarehe 2 Januari, zianze kupelekwa kijiji cha Lusabya,” aliagiza Waziri.

  Akieleza kuhusu mpango wa upelekaji umeme katika vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo, Dkt Kalemani alisema, vijiji hivyo viwili ambavyo ndivyo pekee havijapata umeme kati ya sita vya kata husika; havikuwa kwenye mpango wa awamu ya kwanza ya uunganishaji umeme vijijini na kwamba viko katika awamu ya pili inayotarajiwa kuanza Aprili, 2020.

  “Lakini kwa kutambua shauku kubwa ya umeme mliyonayo wananchi wa Kabukome na Lusabya,  serikali imeamua kuwawahishia huduma hiyo muhimu, ili nanyi mnufaike kama wananchi wengine walio na umeme.”

  Vilevile, Waziri aliwataka TANESCO kuanzisha ofisi ndogo eneo hilo mahsusi kwa wananchi kulipia gharama za kuunganishiwa umeme ili kuwaepusha na usumbufu wa kusafiri mwendo mrefu kufuata huduma hiyo.

  Aidha, aliwahamasisha wananchi kuanza mara moja maandalizi ya kuunganishiwa umeme kwa kusuka mfumo wa nyaya (wiring) katika makazi yao pamoja na majengo mbalimbali ya taasisi za umma zikiwemo shule, nyumba za ibada na vituo vya afya.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi mbalimbali wa kijiji hicho, akiwemo mwenyekiti wake, Kisabo Dominic, walipongeza kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano, chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli, kuhakikisha wananchi wanyonge wanafikiwa na huduma mbalimbali za kimaendeleo hususan nishati ya umeme.

  Pia, walimpongeza Waziri Kalemani pamoja na watendaji wengine wote wa wizara kwa uchapakazi wake na ushirikiano ambao wamekuwa wakitoa kwa wananchi.

  Takwimu zinaonesha kuwa, hadi sasa vijiji 51 kati ya 74 vya Wilaya ya Biharamulo vimekwishaunganishiwa umeme.

  0 0

  Kilele cha Fursa 2019 kinatarajia kufanyika kesho Desemba 7  kwenye ukumbi wa Julius Nyerere vConvetion Cente (JNICC) Dar Es Salaam 
  Katika semina hiyo ya fursa utasikia watu mbalimbali wakielezea mafanikio yao  na namna walipoanzia na kupata mafanikio ikiwemo wasukuma mikokote mpaka wauza miguu ya kuku na mtengeneza kucha.

  Dar ya ndoto itaendeshwa na Mkurugenzi wa fursa Suma Mwaitenda,Mkuu wa Mkoa wa Dar Salaam Paul Makonda na Joseph Kusanga Mkurugenzi wa Clouds 
  Fursa  2019 ambayo imeletwa kwenu na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni-Brela, usichukulie poa nyumba ni choo, clouds, vijana think tank, tacaids, uhuru hospital, R ¥O Tours and Safarisô


  0 0  KWA zaidi ya Muongo mmoja sasa, Mitandao ya kijamii imetumika kama njia ya mawasiliano kwa marafiki zetu tuliopotezana siku nyingi mitandao imekuwa zana ya kupata taarifa iwe  kuhusu biashara, jabari, masoko hata utani; watu ulimwenguni pote wanatumia mitandao ya kijamii kwa madhumuni mbalimbali na  kupatikana kwake ni rahisi kuliko hapo nyuma, na kuna nchi na baadhi ya maeneo imefikiwa zaidi na mitandao kuliko kwingine. 

  Takwimu zinaonyesha kwamba, matumizi ya mitandao ya kijamii yamekuwa ni njia bora ya Kidigitali ya masoko ya Kimataifa na hiyo ni kutokana na namna inavyoweza kutangaza na kukuza masoko ndani na nje ya nchi pamoja na uteuzi wa mtandao upi ambao utafikisha taarifa kwa haraka na kuleta matokeo chanya.

  Ni nchi gani zinatumia zaidi mitandao ya Kijamii? 

  Umewahi kujiuliza au kudadisi kuwa ni nchi ipi ni kinara wa mitandao ya kijamii?  Ufilipino ndio nchi yenye watu wanaotumia zaidi mitandao ya kijamii. Mpaka kufikia mwaka 2018, Ripoti ya Masuala ya Digitali ya Ulimwengu(Global Digital Report) iliitaja Ufilipino kama mtumizi mkuu wa mitandao ya kijamii. Ni kwa miaka miwili, Ufilipino imebaki kuwa kinara. 

  Watumiaji wa Mitandao huko Ufilipino wanatumia wastani wa saa 3 na dakika 57 kila siku kwenye mitandao ya kijamii. Hii ni theluthi moja tu ya muda ambao wanatumia inteneti kila siku (Saa9 na dakika 29) na kuifanya Ufilipino kuwa nchi ya pili kwa matumizi ya inteneti baada ya Thailand.

  Wakazi milioni 67 nchini humo wanatumia mtandao wa Facebook sambamba na wengine milioni 10 wanaotumia Instagram. Asilimia 10% ya watumiaji wa Mitandao ya kijamii pia ni watumiaji wa YouTube ndani ya Taifa hilo.

  Kwa ujumla, Bara la Asia lina watumizi wengi wa mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa. 

  Kwa ufupi huu ndio muda watu hutumia mitandao ya kijamii kulingana na Ripoti ya Masuala ya Digitali ya Ulimwengu(Global Digital Report) 2018

  Indonesia – Saa 3 na dakika 23, hii ni nchi ya tatu ulimwenguni kwa wastani wa matumizi ya mitandao ya kijamii. 

  Thailand – Saa 3 na dakika 10, inashika namba 4 ulimwenguni kwa wastani wa matumizi ya mitandao ya kijamii.  

  Malaysia – Saa 3 kila siku, inatajwa kuwa nambari 8 Ulimwenguni

  Umoja wa Falme za Kiarabu, Emerati- saa 2 na dakika 56 ikishika namba 9 ulimwenguni. 

  Mitandao ya Kijamii imeendelea kutumika zaidi barani Asia hasa Saudi Arabia, ambayo imeonesha maendeleo makubwa, kati ya Januari 2017 na 2018, Matumizi ya mitandao yaliongezeka kwa asilimia 32, asilimia moja zaidi mbele ya India. Indonesia ikiwa na asilimia 23 na Vietnam 20.  

  Vipi kuhusu Marekani na Canada?

  Ungetarajia kuwa Marekani ingekuwa juu zaidi katika matumizi ya mitandao kwa kuwa ndipo mitandao hii inapozaliwa, Sivyo? Ushahidi unaonyesha kwamba, Marekani haikaribii hata kidogo takwimu za matumizi ya inteneti na mitandao kama ilivyo kwa Asia.  
  Marekani ni nchi ya 24 kwa wastani wa matumizi ya saa 2 na dakika 1 tu kwa siku, wakati huo huo, Canada ipo nafasi ya 30 Ulimwenguni kwa wastani wa saa 1 na dakika 48 na hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Global Digital Report ya 2018 iliyoeleza kwamba nchi zote mbili hazina idadi kubwa ya watumiaji wapya. Januari 2017 na Januari 2018, kulikuwa na watumiaji wapya kwa asilimia 9 nchini Canada na asilimia 7 nchini Marekani. 

  Kwa kuwa mitandao ya kijamii ilianza kuwa maarufu Marekani na intaneti yenye kasi zaidi, inafanya uwekaji wa vitu mitandaoni kuwa wa haraka na na hivyo muda mchache kutumika kulinganisha na maeneo mengine. 

  Kulingana na kituo cha Utafiti cha Pew, Mitandao ya Kijamii imekuwa ni muunganiko wa tabia zinazoibuka na zile za umaarufu ambazo zimekuwepo kwa kipindi kirefu ndani ya Marekani. Facebook na YouTube zinatumika zaidi, angalau  73% ya watu wazima wote hupachika maandiko kwenye Facebook, na 68% kutazama video kwenye YouTube. Vijana wengi kati ya umri wa miaka 18 had 24, wanatumia Snapchat kwa 78%, na 71% huingia mara tatu kwenye mtandao huo kila siku. Pia kuna 71% ya vijana ambao hutafuta au kupakia picha kwenye mtandao wa Instagram, 29% hutumia Pinterest na karibu 25% hutumia mtandao wa kibiashara na kazi wa LinkedIn.


  Huko Canada, Facebook imekuwa mtawala zaidi kuliko hata ilivyo Marekani. Mamlaka ya Uthibiti ya Canada (Canadian Internet Registration Authority-CIRA) inaeleza kwamba 77% ya wakanada wote wapo Facebook. Lakini baada ya Facebook raia wa Canada wanapendelea mitandao ya Instagram na LinkedIn (35%), kisha mtandao wa Twitter (26%), na Snapchat (19%). Canada ni namba tatu kwa umaarufu wa shughuli za mitandaoni, na kuifanya mtumizi mkubwa wa Inteneti karibu 67%. 

  Kupokelewa kwa Mitandao ya Kijamii

  Ukitazama ulinganifu wa matumizi ya mitandao ya kijamii, utajiri wa Taifa Fulani sio kigezo kabisa, Unaweza kufikiri nchi tajiri ndio itakuwa na watumiaji wakubwa wa mitandao. Sivyo, na sio lazima iwe hivyo. 

  Nchi za Mashariki ya Kati zina sifa ya uchumi ambao unaendelea, Lakini Ukanda huo una matumizi makubwa ya Mitandao ya Kijamii kuliko pengine popote. Pew Research Center inaeleza kwamba 75% ya watu wa Jordan wanatumia mitandao ya kijamii, Lebanon ni 72%.

  Nchi zenye uchumi imara zina matumizi madogo ya mitandao ya kijamii, mfano Ujerumani ni 40% na Japani ni 39%. Hii ni chini wa Wastani wa matumizi ya mitandao ya kijamii ulimwenguni ambayo ni 53%.

  Uingereza pia watu wanatumia muda mchache kati katika mitandao ya kijamii kulinganisha na Marekani ingawa 85% ya watu wote wanatumia mitandao. 

  Ripoti za hivi karibuni zinaonesha kwamba Facebook, Facebook Messenger, WhatsApp, na Instagram inatumiwa sana Uingereza ingawa Facebook inatumika zaidi lakini Instagram na WhatsApp zimejikusanyia watumiaji wengi miaka ya karibuni. 

  Jambo lingine muhimu ni kwamba, katika nchi zilizoendelea, Wanawake wanatumia zaidi Mitandao kuliko wanaume. Mfano Sweden, Wanawake wanaotumia mitandao ni 72% ukilinganisha na Wanaume ambao ni 63%. Ingawa Wanaume wanatumia zaidi intaneti kwa 94% huku wanawake ni 90%

  Kwa nini Mataifa yanatumia Mitandao ya Kijamii? 

  Sababu kubwa ya Ufilipino kuwa na matumizi makubwa ya Mitandao ni idadi kubwa ya watumiaji wanaopakia maandiko kila kukicha lakini pia idadi kubwa ya watu wanaoitembelea nchi hiyo. 

  Huko Ulaya, Wengi hupata habari kupitia mitandao mfano tu, Nchini Italia, Nusu ya Raia wote wanatumia mitandao kupata Habari.  Angalau 40% ya watu wanapata habari kupitia mitandao katika nchi hizi Uhispania, Denmark, na Sweden. Facebook ndio inatumika zaidi kupata Habari mbalimbali.

  Ikiwa na mionekano mipya na ya kuvutia, Wafanyabiashara wengi sasa wanaitumia Mitandao kuwasiliana na wateja wao. Nchi kadhaa zinatumia Mitandao kwa biashara. Ingawa sababu za matumizi ya mitandao zinatofautiana kulingana na watumiaji, ukubwa wa matumizi na mengineyo lakini ukweli ni Kwamba mitandao imekuwa na thamani kubwa sana wakati huu kuliko kipindi chochote kihistoria.

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewapongeza waandaji wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon kwa kukuza utalii wa michezo kwa kupitia mbio hizo na kuwataka waandaaji wengine nchini kuiga mfano huo.

  Alitoa pongezi hizo wakati wa Kikao maalumu na waandaaji hao wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon kufuatia uzinduzi wa kufana uliofanyika mwezi uliopita jijini Dar es Salaam ambapo waziri Mwakyembe ndiye alikuw amgeni rasmi na baada ya hapo aliamua kuwaalia waandaaji hao ofisini kwake ili kujadili masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kukuza riadha nchini.

  Kamati ya maandalizi ya Kilimanjaro Marathon iliwakilishwa na Muandaaji Mkuu John Addison ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wild Frontiers na pia aliyebuni wazo la Kilimanjaro Marathon, Aggrey Marealle ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Executive Solutions kampuni inayoratibu mbio hizo kitaifa na John Bayo ambaye ni mkurugenzi wa mbio hizo kitafa. Wote hawa ni waanzilishi wa mbio hizo zilizoanza 2003.

  Kwa kuzingatia kuwa Kilimanjaro Marathon ina washiriki zaidi ya 11,000 kutoka nchi 58 duniani, Waziri Mwakyembe alisema kuna haja ya kuwepo ushirikiano wa karibu kati ya Wizara yake na ile ya Maliasili na Utalii ili kukuza maendeleo ya michezo na utalii.

  “Kilimanjaro Marathon imekuza utalii wa michezo kwa kiasi kikubwa kwani washiriki wanaweza kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii katika mkoa wa Kilimanjaro na maeneo mengine nchini ambapo kuna vivutio vya utalii,” alisema na kuongeza kuwa riadha ni nzuri kwa afya lakini pia ni moja ya chanzo cha fedha za kigeni kwa Tanzania.

  Waziri Mwakyembe alitoa wito kwa miko ayote inayoandaa mbio mbalimbali kuhakikisha wanazingatia faida yam bio hizo kiuchumi kwa kuandaa shughuli mbalimbali za kitamaduni na kijamii kwa wenyeji na watalii kabla na baada yam bio  ili kuongeza kipato na ajira kutokana na shughuli hizo za wiki nzima.

  Alionesha pia kufurahishwa na namna mbio mbalimbali zinaanzishwa mikoani ila akatoa tahadhari kuwa ni muhimu kuwepo na miongozo na vigezo  kuzingatiwa huku akimtaka Mkurugenzi wa Michezo kuhakikisha hili linasimamiwa vikamilifu.

  Wadhamini wa Kilimanjaro Marathon 2020 ni Kilimanjaro Premium Lager-42 km, Tigo-21 Km, Grand Malt-5km. Wengine ni  Kilimanjaro Water, TPC Limited, Simba Cement, Barclays Bank na watoa huduma maalumu ni Kibo Palace Hotel, Keys Hotel, GardaWorld Security, Precision Air na CMC Automobiles.                            

  Katika hatua nyingine, Waziri Mwakyembe ametoa pongezi nyingine kwa waandaaji wa Kilimanjaro Marathon kwa kukubali kusaidia kufanyika kwa Mbio za John Steven Akhwari ambazo zinatarajiwa kufanyika Juni mwakani.

  Waandaaji hao wanafanya kazi na wadau wengine wakiwemo Chama Cha Riadha Tanzania na Taasisi ya John Steven Akhwari ili kuweka vigezo mbalimbali  na kuhakikisha mbio hizi zinafanikiwa ili kumtambua Bw. Akhwari ambaye anatambulika na  Olympiki kama mwanarisha anayewakilisha dhamira ya Olympiki.

  Akizungumza kwa niaba ya waandaaji, Bw. Marealle alimshukuru Waziri Mwakyembe kwa kuunga mkono mbio hizo miaka yote  jambo ambalo limewapa waandaaji na wadhamini heshima ya kipekee. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dr. Harison Mwakyembe (katikati) na Mkurugenzi wa Michezo Yussuf Singo (kushoto) wakiwa na waandaaji wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager baada ya Kikao cha pamoja kilichoitishwa na Waziri ili kujadili namna ya kuendeleza riadha nchini. Wengine kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Executive Solutions ambao ndio waratibu wa mbio hizo kitaifa, Aggrey Marealle, Muandaaji Mkuu wa mbio hizo ambaye pia ni Afrisa Mtendaji Mkuu wa Wild Frontiers, John Addison na Mkurugenzi wa Mbio hizo Kitaifa, John Bayo.

  0 0
  Mwenyekiti wa bodi ya TASAF, Dr. Moses Kusiluka (aliyevaa shati nyeupe) akikagua baadhi ya bidhaa zinazouzwa na baadhi ya walengwa wa TASAF katika kijiji cha Khusumay wilayani Karatu kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.


  Mwenyekiti wa Bodi ya TASAF Dr.Moses Kusiluka ambaye pia ndiye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Ikulu ( aliyevaa koti ) akikagua moja ya majengo  ya Shule ya Sekondari yaliyojengwa na TASAF katika kijiji cha Khusumay wilaya ya Karatu.

  Nyumba za Walimu na hosteli ya wanafunzi ( picha ya juu na chini ) yaliyojengwa na TASAF katika Shule ya Sekondari ya Khusumay yanaelezwa kuhamasisha wanafunzi kuhudhuria masomo na kupunguza tatizo la mimba kwa watoto  wa kike.


  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladisilaus Mwamanga akifungua bomba la maji kwenye moja ya nyumba zilizojengwa na TASAF katika Shule ya Sekondari Khusumay wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

  Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya TASAF,Wadau wa Maendeleo na Menejimenti ya TASAF akiangalia ujenzi wa daraja linalojengwa na walengwa wa TASAF katika kijiji cha Nala wilaya ya Karatu mkoani Arusha kwa utaratibu wa Ajira ya Muda.
   Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Uongozi ya TASAF, Maafisa wa Serikali na Wadau wa Maendeleo wakiangalia ng’ombe wa mmoja ya Walengwa ambao amewapata baada ya kujumuishwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Nala wilaya ya Karatu mkoani Arusha.
  Na Estom Sanga- Karatu

  Katibu Mkuu ofisi ya Rais-Ikulu -Dr. Moses Kusiluka ametoa wito kwa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuondokana na umaskini uliokithiri.

  Dr. Kusiluka ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya taifa ya Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipotembelea na kukutana na baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kukagua miradi inayotekelezwa na TASAF katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha ambako aliambatana pia na baadhi ya Wajumbe wa bodi .

  Amesema Serikali inatambua changamoto ya Umaskini unaowakabili wananchi ,lakini akasisitiza kuwa ili kuitokomeza changamoto hiyo wananchi wanapaswa kujituma kwa kufanyakazi kwa bidii na maarifa na kutumia vizuri mazingira wezeshi yaliyowekwa na Serikali kuinua mapato yao.

  Aidha Dr. Kusiluka amehimiza wazazi kutilia mkazo suala la elimu kwa watoto wao ambao amesema Hiyo ndiyo njia ya uhakika ya kujenga jamii bora ya baadaye itakayoleta ukombozi wa kweli wa ujenzi wa uchumi thabiti wa kaya husika na taifa kwa ujumla huku ikikemea vikali vitendo vyovyote vinavyoathiri maendeleo ya wanafunzi hususani watoto wa kike.

  ‘’tumieni vizuri fursa mliyoipata ya kuwa shuleni ili mtimize ndoto zenu za kuwa wataalamu wa fani mnazozitaka katika utumishi wa taifa hapo baadaye’’ alisisitiza Dr. Kusiluka baada ya kukagua nyumba na hosteli ya wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya Khusumay ambayo yamejengwa na TASAF.

  Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa Bodi ya taifa ya Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa Shughuli za Mfuko huo , Serikali imeanza kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha kuwa Mfuko huo unaendelea kuwa nyenzo muhimu katika kusaidia jitihada za kupunguza umaskini nchini.

  Wakiwa katika kijiji cha Khusumay,Wajumbe hao wa bodi ya taifa ya Uongozi ya TASAF ,walitembelea kaya za baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kujionea namna walengwa hao walivyofanikiwa kuboresha makazi yao, kununua mifugo hususani mbuzi, ng’ombe ,kuku na nguruwe kwa kutumia ruzuku waliyoipata kutoka TASAF kama njia mojawapo ya kukuza uchumi wa kaya za Walengwa hao.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- Bw. Ladislaus Mwamanga ameishukuru serikali kwa kuendelea kuuthamini Mfuko huo na kuridhia utekelezaji wake kuendelea katika sehemu ya pili ambayo amesema imeagizwa kutekelezwa katika maeneo yote nchini.

  0 0


  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo (katikati aliyevaa miwani) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kodi wa mamlaka hiyo baada ya kupanga mikakati ya Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi kwa wafanyabiashara wa eneo la Mabwepande Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo inayoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Dar es Salaam itamalizika tarehe 14 Desemba, 2019.
  Mfanyabiashara wa duka la rejareja wa eneo la Mabwepande Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Cathbert Kagirwa akitoa maoni yake kwa Afisa Kodi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Rose Mahendeka wakati wa Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Dar es Salaam ambayo itamalizika tarehe 14 Desemba, 2019.
  Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Isihaka Shariff akitoa elimu ya kodi kwa mmoja wa wafanyabiashara wa Kariakoo Wilaya ya Ilala wakati wa Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Dar es Salaam ambayo itamalizika tarehe 14 Desemba, 2019.
  Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Catherine Mwakilagala akitoa elimu ya kodi kwa baadhi ya wafanyabiashara wa eneo la Tandika Wilaya ya Temeke wakati wa Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Dar es Salaam ambayo itamalizika tarehe 14 Desemba, 2019.
  Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zakeo Kowero akitoa elimu ya kodi kwa mmoja wa wafanyabiashara wa eneo la Kivule Wilaya ya Ilala wakati wa Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Dar es Salaam ambayo itamalizika tarehe 14 Desemba, 2019. (PICHA ZOTE NA TRA)

older | 1 | .... | 3268 | 3269 | (Page 3270) | 3271 | 3272 | .... | 3352 | newer