Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

TAKUKURU YATOA SIKU KUMI MRADI WA MAJI WA KELEMA KUU UKAMILIKE

$
0
0
Na Charles James,Michuzi TV

Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, amemuagiza Mkandarasi wa Kampuni ya JUAN, inayotekeleza mradi wa Maji wa Kelema Kuu, katika Kijiji Cha Kelema Balai Wilayani Chemba, Mkoa wa Dodoma, kuhakikisha ndani ya siku kumi mradi huo uwe umekamilika.

Awali mradi huo ulioanza kutekelezwa tokea 2014 wenye thamani ya sh mil 223 ulikamilika lakini ulifanya kazi ndani ya wiki moja kutokana na mabomba yaliyowekwa yalikuwa chini ya kiwango.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo wameamua kutoa siku hizo ili kusaidia wananchi wa kitongoji cha Ndoroboni kilicho ndani ya kijiji cha Kelema Kuu wilayani Chemba wapate maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya kila siku.

"Tumetoa siku hizo kwa wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha mradi huo,hatutaki visingizo kwa sababu mitaro tayari imeshachimbwa,"alisema Kibwengo.Alifafanua kuwa wanatakiwa kwenda kwa kasi katika uwekeaji mambomba hayo.ili kukwepa tope kuyafukia kutokana na kwamba msimu wa mvua umeanza.

Akitoa ufafanuzi baada ya kufanya uchunguzi wao amesema walichokibaini ni kwamba mambomba yaliyonunuliwa kuweka katika mradi huo yalikuwa na kiwango chenye presha ya kawaida (Normal Presha)PN 6 badala ya PN 12.5 kama ilivyoidhinishwa katika mkataba wa kutekeleza mradi huo.

Kutokana na hilo amesema siku hizo walizotoa hakutakuwa na msamaha wowote kwa kampuni hiyo kwasababu ni uzembe na udanganyifu uliofanywa na mkandarasi huyo katika mradi huo,kinachotakiwa ni wao kufanya kazi haraka iwezekanavyo hasa ukizingatia mitaro tayari imechimbwa.

Naye Mhandisi wa wakala wa maji vijijini (RUWASA) wilayani Chemba Robert Mganga amesema kazi iliobakia ni nyepesi sana hivyo wiki moja inatosha kukamilisha kufanya utandikaji huo wa mabomba.

"Hakuna kazi ngumu hapa sema hii kampuni inaleta uzembe,tuko nao pamoja hivi sasa kuhakikidha wanakamilisha ujenzi wa mradi huo,"amesema Mganga.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa kitongoji cha Ndoroboni amesema kitongoji hiko kina shida ya maji inayopelekea wakazi wa eneo hilo kuafuata kijiji cha Kelema Balai kama maili mbili kutoka Kelema Kuu.

Hata hivyo ameiomba serikali kwa kishirikiana na serikali ya mtaa kusimamia mradi huo ukamilike ili wakazi waweze kupata maji safi kwa ajili ya matumizi ya kila siku.Amesema wakazi wengine hushindwa kwenda umbali mrefu na badala yake wanatumia maji ya mabwawa ambayo ni machafu na si salama kutumia kwa binadamu.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa kampuni ya Juan Mhandisi Inocent Benard amesema wakazi wa eneo hilo wategemee mwezi huu kupata maji kutokana na kuwa watakamilisha ndani ya siku ambazo wametakiwa kukamilisha.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo akizungumza na wandishi wa habari.

Benki ya NBC yatoa mafunzo kwa wafanyabiashara jijini Dar.

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara wa Kati na Wadogo wa Benki ya NBC, Evance Luhimbo akizungumza na wafanyabiashara  wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo, katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwawezesha kimafunzo yatakayosaidia katika ukuaji wa biashara zao jijini Dar es Salaam jana.
 Meneja Maendeleo ya Viwanda wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Patrick Magai akitoa elimu kuhusu fursa za viwanda katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo jana. 
 Msaidizi wa Msajili Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), George Chuwa akizungumza katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo jiijini Dar es Salaam jana. 
  Ofisa Msimamizi wa Walipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Joyce Ng`oja akitoa elimu kuhusu kodi katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam jana.

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin akitoa elimu kuhusu uhifdhi wa bidhaa katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoojiji jijini Dar es Salaam jana.
  Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru (wa pili kushoto) akizungumza jambo na wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam wakati wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo yenye lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji wa biashara zao jijini humo jana.
 Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru (kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam katika semina ya siku moja yenye lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji wa biashara zao, masuala ya kodi, mitaji na taratibu nyingine za uendeshaji wa biashara jijini  Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashra wa Kati na Wadogo wa Benki ya NBC, Evance Luhimbo (kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Kariakoo  katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji wa biashara, masuala ya mitaji, kodi na jinsi nyingine ya kuendesha biashara jijini Dar es Salaam jana.

Ulinzi waimarishwa soko la Madini Chunya-DC Mahundi Inbox x

NAIBU WAZIRI AWESO AVUNJA BODI YA MAMLAKA YA MAJI MJI MDOGO MISUNGWI

$
0
0

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akipita kukagua kazi ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Magu, mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (wa tatu kutoka kushoto) walipokuwa wakikagua Mradi wa Maji wa Magu, mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Dkt. Philemon Sengati akitoa taarifa ya Sekta ya Maji ya wilaya kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga wakibadilishana mawazo wakitoka kukagua Mradi wa Maji wa Magu, mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na wananchi katika Mji Mdogo wa Misungwi, mkoani Mwanza.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Leonard Msenyele akitoa maelezo kuhusu chanzo cha Mradi wa Maji wa Magu kwa Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akimsikiliza, mkoani Mwanza.

………………

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amevunja Bodi ya Mamlaka ya Maji ya Mji Mdogo Misungwi (MIUWASA) kutokana na uendeshaji na usimamizi usioridhisha hali iliyosababisha huduma ya maji katika mji wa Misungwi kuzorota na kuwa kero kwa wananchi.

Akitangaza uamuzi huo, Aweso amesema amechukua maamuzi hayo baada ya kubaini mapungufu makubwa ya kiutendaji katika mamlaka hiyo na kujiridhisha kupitia taarifa iliyotokana na kikao alichokaa na viongozi wa Wilaya ya Misungwi.

“Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu hali ya upatikanaji wa maji katika mji wa Misungwi na uchunguzi uliofanyika tumegundua kuna tatizo kwenye mamlaka na uongozi wa wilaya umetuthibitishia baada ya kufanya mazungumzo’’, amesema Aweso.

“Kuanzia leo mji wa Misungwi utakuwa chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), lakini pia Mkaguzi wa Ndani kutoka wizarani atakuja kufanya ukaguzi wa hesabu za MIUWASA na kutupa taarifa yote ya mapato na matumizi yao’’, ameelekeza Aweso.

Awali, Naibu Waziri Aweso alisema wizara imetekeleza agizo la Mhe. Rais, Dkt. John Magufuli kwa kutoa kiasi cha Shilingi milioni 623 kama malipo ya mkandarasi Kampuni ya Shanxi Construction Engineering Corporation ya China anayefanya kazi ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Mbalika wilayani Misungwi chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Kahama-Shinyanga (KASHWASA).

Akisema na kiasi cha milioni 350 kimeshatolewa na milioni 273 iliyobaki itamaliziwa wiki ijayo, akifafanua kuwa fedha hizo ni ajili ya kukamilisha kazi zote zilizobaki na kuagiza mradi uwe umekamilika ifikapo Machi, 2020 kulingana na mkataba.

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AFUATILIA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS

$
0
0
Kazi ya usafishaji wa barabara ya Mang’ombe – Iloganzala Km 1.2, inayojengwa kwa kiwango cha lami wilayani Mbogwe mkoani Geita ikiendelea ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli kuwataka TARURA kujenga barabara za lami zenye urefu wa km 3 wilayani humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli wa kuwataka TARURA kujenga barabara za lami zenye urefu wa Km 3 wilayani Mbogwe.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa Mbunge wa Mbogwe mhe, Augustino Masele alipokagua utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli la kuutaka Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA), wilayani Mbogwe kujenga kilometa 3 za barabara za lami katika makao makuu ya wilaya hiyo kulia ni mkuu wa wilaya hiyo Bi. Martha John Mkupasi.
Meneja wa (TARURA), wilayani Mbogwe mkoani Geita Eng. Justine Lukaga, akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua barabara ya Mang’ombe-Iloganzala Km 1.2, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umeanza katika mji wa Masumbwe Wilayani humo.
Muonekano wa barabara ya Mang’ombe-Iloganzala Km 1.2, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umeanza katika mji wa Masumbwe Wilayani Mbogwe Mkoani Geita.
Mkuu wa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita Bi, Martha John Mkupasi (wapili kushoto), akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua barabara zinazojengwa na TARURA kwa kiwango cha lami wilayani humo.

………………….

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa amewataka viongozi wote wa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kushirikiana na Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA), kuhakikisha ujenzi wa barabara za lami katika mji wa Masumbwe unakamilika kwa wakati.

Amesema uwepo wa barabara nyingi za lami katika wilaya za Mbogwe na Kahama utachochea fursa nyingi za utalii, ufugaji, uchimbaji madini na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na hivyo kukuza uchumi wa jamii na taifa kwa ujumla.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara zinazosimamiwa na TARURA wilayani humo mhe. Kwandikwa amesema atahakikisha ujenzi wa kilomita zote tatu zilizoahidiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli unakamilika kama ilivyopangwa.

“Hakikisheni mnawaelimisha wananchi ili wapishe maeneo yote zitakapopita barabara hizo ili kusiwe na vikwazo kwa wajenzi wa barabara hizo”, amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.

Hivi karibuni katika ziara yake wilayani humo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli aliagiza utekelezwaji wa haraka wa ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa tatu alizoahidi katika makao makuu ya wilaya ya Mbogwe na kusisitiza kazi hiyo ifanyike haraka.

Naye mkuu wa wilaya ya Mbogwe Bi, Martha John Mkupasi amesisitiza umuhimu wa wananchi kutoa ushirikiano wakati wa ujenzi wa barabara hizo na kuzilinda pindi zitakapokamilika ili kuboresha miundombinu ya wilaya hiyo na kukuza shughuli za biashara.

Amehimiza wananchi kutovamia maeneo ya hifadhi ya barabara ili kuepuka usumbufu wakati zoezi la ujenzi linapoendelea.

Kwa upande wake meneja wa TARURA wilayani humo Eng. Justine Lukanga ameahidi ujenzi wa kilometa tatu za lami katika barabara ya Mashineni-Kasandalala km 1.3 na Mang’ombe-Iloganzala 1.2 na kituo cha afya-shuleni km 0.5 zitajengwa kwa kasi na ubora unaozingatia thamani ya fedha.

Mradi wa REGROW kuanza kumaliza changamoto za miundo mbinu hifadhi ya Taifa ya Ruaha Inbox x

$
0
0
Na Francis Godwin ,Iringa


KATIBU mkuu wizara ya maliasilia na utalii Prof Adolf Mkenda amesema wizara yake imejipanga kupitia mradi wa kuendeleza Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania(REGROW) kuboresha miundo mbinu ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa ili kuweza kuvutia idadi kubwa ya watalii zaidi .

Akizungumza jana baada ya kuzindua vitendea kazi vya mradi wa REGROW katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha katibu mkuu huyo alisema kuwa wizara hiyo imeelekeza nguvu zake kutangaza na kuboresha miundo mbinu katika hifadhi ya Ruaha ili kuiwezesha hifadhi hiyo na hifadhi nyingine kuendelea kujiendesha kwa faida na kutoa gawio lake serikalini .

Kwani alisema changamoto ya miundo mbinu katika maeneo ya hifadhi mbali mbali hapa nchini imekuwa kikwazo kikubwa kwa watalii kufika kutembelea hifadhi nchini na kama miundo mbinu itaboreshwa watalii zaidi wanaweza kufika kwa urahisi zaidi .

Alisema changamoto kubwa ya hifadhi ya Ruaha ni pamoja na ubovu wa miundom mbinu na kuwa kupitia mradi wa REGROW wizara imejipanga kuanza kuboresha miundo mbinu hiyo na kutangaza hifadhi ya Ruaha ili kuwezesha kuongeza kasi ya watalii kufika .

Prof Mkenda alisema changamoto ya utalii ina vitu viwili vikubwa kwanza kufungua miundo mbinu ndani ya hifadhi yenyewe na namna ya kufikia ndani ya hifadhi hivyo mradi huo unasaidia mambo makubwa mawili kutangaza na kuboresha miundo mbinu yake .

Alisema ndani ya hifadhi ya Ruaha wanategemea kupitia mradi huo wa REGROW kufungua barabara ya kuunganisha mkoa wa Mbeya na Dodoma kwa kujenga daraja kubwa katika eneo la Othuman ambalo kuna mzungu alipata kujenga daraja kabla ya hifadhi hiyo kutangazwa rasmi kuwa kujengwa kwa daraja eneo hilo kutawezesha kuunganisha hifadhi hiyo na watalii wakaweza kuingia kutokea Dodoma na kutokea Mbeya kwenda hifadhi nyingine kama Katavi na Kitulo .

Hata hivyo alisema wakati wizara inaendelea kufanya jitihada za kutangaza utalii na kuboresha miundo mbinu mbali mbali kwenye hifadhi nchini bado itatoa wito kwa wadu wa utalii nchini kuunga mkono jitihada za kutangaza utalii kwa kutenga gharama zao wenyewe badala ya kusubiri kuwezeshwa na wizara ya maliasi na utalii kwa kila jambo wanalotaka kufanya .

Kwani alisema wapo baadhi ya wadau wa ndani ya nchi na nje ya nchi ambao wameendelea kutangaza utalii nchini kwa kutumia gharama zao wenyewe .

Japo alisema wizara itaendelea kuwatumia watu wa makundi mbali mbali watu maarufu kwa ajili ya kutangaza utalii nchini japo watafanya hivyo kwa kushirikisha idara mbali mbali zinazohusiana na makundi hayo ili kuweka vigezo vya kuwapata wale watakaofanya kazi ya kutangaza utalii na mwisho wa siku kuja na matokeo ya kazi hiyo .

Prof Mkenda alisema kuwa wakati wanaendelea na uboreshaji wa miundi mbinu katika hifadhi nchini bado wizara inaangalia jinsi ya kuanzisha utalii wa meli na fukwe ili kuvutia watalii zaidi nchini kwani wapo baadhi ya watalii ambao wanatamani kuja kutalii katika hifadhi za fukwe na utalii wa meli na kuwa jitihada zitakazofanyika ni kujenga magati kwa ajili ya utalii wa meli na kuboresha maeneo ya fukwe .

Kamishna mwandamizi wa uhifadhi wa hifadhi za Taifa (TANAPA ) kanda ya kusini Dk Christopher Timbuka alisema kuwa ujio wa mradi wa REGROW umetokana na changamoto ambazo hifadhi za kusini zilikuwa zikikabiliwa nazo .

Kuwa changamoto hizo ni miundo mbinu kuwa mibovu na watalii kushindwa kufika katika hifadhi hivyo mradi huo utawezesha kufungua utalii nyanda za kusini .Hivyo alisema ujio wa mradi huo ambao unaanza kazi utasaidia kuongeza idadi ya watalii na kuongeza idadi ya vitanda kutoka vitanda 400 vilivyopo na kuongezeka zaidi ili watalii kuweza kupata maeneo ya kufikia .

Alisema kupitia mradi huo ulinzi ulinzi didhi ya ujangili kwenye hifadhi utapungua zaidi kutokana na mradi huo kuwezesha vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi .

Mratibu wa mradi wa REGROW Saanya Aenea alisema kuwa vifaa mbali mbali vimezinduliwa kwa ajili ya mradi huo na kuwa changamoto kwa asilimia 100 zitakwenda kumalizika .

Pia alisema kwa kupitia mradi huo wananchi watajengewa miradi ya kiuchumi kama ya ufugaji samaki ,ufugaji nyuki na mingine ili kuwawezesha kiuchumi na wasiwe chanzo cha kujihusisha na ujangili .
 Kamishina mwandamizi wa hifadhi za Taifa (TANAPA) kanda ya nyanda za juu kusini Dkt Christopher Timbuka wa pili kulia akimkabidhi baadhi ya vifaa vya mradi wa Regrow, katibu  mkuu wizara ya maliasili na utalii Prof Adolf Mkenda ,mradi wa Regrow umekabidhi vifaa vya ulinzi hifadhi ya Ruaha vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.2
 

Changamoto Biashara ya Mtandaoni,Tume ya Ushindani (FCC) yajipanga kuchukua hatua

The first Absa branded branch launched in Dar

$
0
0
Barclays bank Tanzania has started to rebrand its properties in the country following a take-over by ABSA Group Limited last year.

Yesterday the banks unveiled its first Absa branded branch at Palm Village along Mwai Kibaki Road in Dar es Salaam and with the bank’s Managing Director, Abdi Mohamed, assuring customers that the changes would not affect the quality of service attached with the bank.

“We are getting ready to change our name from Barclays Bank Tanzania to Absa Bank Tanzania. This is in line with our parent company Absa Group Limited’s decision to rebrand all its operations to Absa, as announced in July 2018,” said the MD during the ceremony to unveil the new Absa branded branch.

he noted that over the coming weeks, people in the country will witness more of Absa branded branches, ATMs and some other branded assets take on the warm, vibrant red colour palette of the Absa brand, symbolic of the many shades under our hot African sun.“This is the look-and-feel we will be rolling out across our Tanzania branch network,” he declared.

According to Mr Mohamed the change was part of one of the largest rebranding projects in Africa scheduled to be completed by mid-2020 and part of a broader, multi-country rebrand programme happening at Group-level.

Appreciating the size of the task ahead and in preparation to change their name, the bank started to introducing Absa’s warm, vibrant red colour palette on some of its assets, including bank branches and ATMs, to ensure that they make their clients and the general public aware of the changes ahead of before new legal name changes.He noted that the bank will continue to be known as Barclays Bank Tanzania until the process was officially concluded.

“We will continue to listen to our customers and use their feedback to create a business that is relevant and meets their needs. There will always be a demand for physical branches in Tanzania, and branch-based banking remains a key part of our offering,” he said.

Unveiling the branded branch on behalf of the Minister for Finance and Planning, Dr Phillip Mpango, the Assistant Commissioner for External Finance, Ms. Mamelta Mutagwaba, noted that the move was a clear testimony of how the bank is committed to continue doing business in the country.

“It is important to note that customers are usually sensitive, and jittery when it comes to re-branding because of the fear that they will lose the services, value for money, reliability that made them loyal.

We call upon banking consumers in Tanzania to have confidence in Absa, and that they will get the same standard of services they have been getting from Barclays. On your part, we expect Absa to reciprocate this trust by making sure that the transition over rebranding is smooth and as flawless as can be”, she said.

She noted; “The government has embarked on a drive to make Tanzania a middle income industrial economy. Such endevour requires concerted efforts involving both the private sector and the public sector. Within this context, private public partnership is needed especially by engaging the banking sector. To achieve this ambition, the country needs to invest heavily in infrastructure, business support, manpower training, and in social amenities.

“The ascendancy of Tanzania onto this industrialization route has seen the launching of infrastructural mega projects, as manifested by the on-going construction of the Standard Gauge Railway, Stigler’s Gorge Hydroelectric power. Construction of Chato airports and Terminal 3 at Mwalimu Nyerere International Airport. Such projects require massive investments. It is our expectation that the banking sector will take the initiative and expand its credit portfolio to accommodate financing of such projects. 

“This is one aspect of public finance demand, the other is on productive sectors that are crucial to creating the needed linkages in the industrialization mix, especially agriculture. Traditionally, commercial banks has not been able to adequately finance agriculture, either because of the risk involved in crop failure or the long production cycle which delays the commencement of loan repayment.

“We call upon banks to come up with innovative financing packages that can cater for the agricultural sector. In addition, banks should try to deal with the various obstacles that have tended to make the agricultural sector not bankable. On our part, the government, and the ministry of finance in particular, will work with other ministries to make sure that impediments to advancing loans to the agricultural sector are removed”, added Ms. Mamelta.
Ministry of Finance and Planning Assistant Commissioner for External Finance who was representing Finance’s Minister, Mrs. Mamelta Mutagwaba (second left), cuts a ribbon to official launch the first Absa branded branch in Tanzania at Palm Village, Mwai Kibaki Road in Dar es Salaam on Tuesday. Looking on from left are; Barclays Tanzania Board Chairman, Simon Mponji, BBT Managing Director, Abdi Mohamed, Chinese Business Chamber Chairman, Janson Huang, BBT Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi and BBT Head of Communications and Corporate Relations, Aron Luhanga.



SIKONGE WATAKIWAKUWA KUANZA MCHAKATO WA KUJENGA KIWANDA CHA KUSINDIKA ASALI

$
0
0




Mkuu  wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akihutubia kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge hivi karibuni.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani hivi karibuni.
………………………………………………

NA TIGANYA VINCENT

MADIWANI na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wametakiwa kuachana na mpango waliokusudia wa kutenga Kituo cha ukusanyaji wa asali bali wafikirie wazo la ujenzi wa Kiwanda cha kusindika asali ili kuongeza thamani ya asali hiyo.

Ushauri huo umetolewa juzi wilayani Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.

Alisema utaratibu wa ujenzi wa Kiwanda utawasaidia wafugaji wa nyuki kupata faida kubwa na  kuwa na bidhaa ambazo zinajulukiana asili yake zinazalishwa na Kiwanda cha Sikonge(Made in Sikonge)
Mwanri alisema kitendo cha kuruhusu Sikonge kugeuka kuwa sehemu ya kukusanya asali ambayo haijasindikwa utasababisha watu kutoka nje kuingia katika eneo la kukusanya asali yote na kuwaacha wafugaji wakiwa na faida kidogo huko ikienda kunufaisha maeneo mengine.

 “ Naona Sikonge hatuelewani mimi nazungumzia uanzishaji wa Kiwanda cha kusindika asali na kuiweka kwenye vifungashio kama vile Chupa ambazo zina nembo ya Sikonge, nyie mnafikiria kuwa na ‘collection centre’ ambapo asali itauzwa kabla ya kuongezewa thamani na kwenda kunufaisha watu wa sehemu nyingine na kuwacha watu wakiwa maskini “ alisema.

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LASHAURI NCHI WANACHAMA KUONGEZA VIFAA ZAIDI MIPAKANI ILI KUBAINI WAGONJWA WA EBOLA NA DENGUE

$
0
0

Na Mwandishi wetu Arusha.

Kamati ya mambo ya jamii katika Bunge la Afrika Mashariki imeshauri nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuhakikisha wanaboresha na kuongeza vifaa maalumu mipakani ili kuwabaini wagonjwa wa magonjwa ya milipuko kama vile homa ya Dengue na Ebola ili kuepusha kasi ya maambukizi baina ya nchi na nchi.

Aidha kamati hiyo ilitoa wito huo mapema jana kwenye bunge la nne la afrika mashariki linaloendelea jijini Arusha.

Akiongea na vyombo vya habari mapema jana mara baada ya kuwasilisha taarifa ya kamati hiyo ambayo ilihusisha nchi 3 mjumbe wa kamati hiyo bi Pamela Maassay,alisema kuwa wao kama kamati waliweza kutembelea nchi wanachama kwa ajili ya kukusanya na kujua mambo mbalimbali yahusuyo magonjwa hasa ya mlipuko.

Alidai kuwa katika mipaka ya nchi wanachama wa jumuiya ya afrika mashariki bado kunaitajika nguvu kubwa sana kwa kuwa kwa mujibu wa taarifa ambazo wamekusanya wameweza kubaini kuwa zipo nchi ambazo wakati mwingine zinapata magonjwa kupitia Mipaka hivyo usalama unahitajika sana.

“Katika ripoti yetu tumeweza kuona nchi kama Rwanda ambayo kupitia mipaka yake ambayo ipo karibu na Kongo wamekuwa wakipata magonjwa sana kwa kuwa wapo karibu lakini tena kwa nchi kama Uganda nako hivyohivyo sasa taadhari inatakiwa ichukuliwe na kuimarishwa zaidi” aliongeza.

Katika hatua nyingine alisema hata kwa upande wa nchi ya Tanzania napo pamoja na kuwa kuna jitiada kubwa ambazo zimekwa kwenye mipaka lakini jitiada hata kuanzia ngazi za vijiji hadi taifa ni muhimu sana.

“Kwa nchi nyingine magonjwa ya mlipuko tahadhari kubwa sana imechukuliwa kwenye mipaka wameweka vifaa maalumu ambavyo mtu akipita tu na ugonjwa anafahamika lakini pia hata kila zahanati ina jengo kabisa la wagonjwa hawa wa magonjwa ya milipuko tuige hili maana afya ya wananchi ni jukumu la kila kiongozi” aliongeza bi Pamela.

Alimalizia kwa kusema kuwa Wizara ya afya na maendeleo ya jamii hapa nchini iinatakiwa kuiga mfano huo kwa kujenga majengo lakini pia kuongeza vifaa mipakani kwa ajili ya kuepusha nchi na magonjwa hasa ya mlipuko yanayoweza Kutokea na kuathiri maisha ya wananchi.

Serikali inawahimiza wadau na jamii nzima kutunza, kulinda na kuhifadhi maeneo ya kihistoria

$
0
0

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Ndaki ya Sayansi na Elimu Kampasi ya Solomon Mahlangu Prof. Allen Malisa akiwa kwenye ziara ya kikazi siku mbili alipotembelea eneo la Mazibu Morogoro lililotumiwa na wapigania uhuru wa “African National Congress” (ANC) wa Afrika ya Kusini.


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza (wa kwanza kulia) akitembelea Kampasi ya Solomon Mahlangu Mazibu Morogoro ambalo ni moja ya eneo lililotumiwa na wapigania uhuru wa “African National Congress” (ANC) wa Afrika Kusini. Nyuma ya picha hiyo ni Ukumbi wa Mikutano wa Nelson Mandela uliotumiwa kwa mikutano ya kuhamasisha harakati kudai uhuru wa Afrika Kusini.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akisoma kibao kinachotambulisha yalipo makaburi ya wapigania uhuru wa “African National Congress” (ANC) wa Afrika Kusini yaliyopo Kampasi ya Solomon Mahlangu Mazibu mkoani Morogoro
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akisoma maneno yaliyotamkwa na kijana mpigania uhuru machachari wa Afrika Kusini aliyejulikana kwa jina la Solomon Kalushi Mahlangu, kukamatwa na kutiwa kizuizini mwaka 1977 na hatimaye kunyongwa hadi kufa mwezi Aprili 1979.
Mkuu wa Ndaki ya Sayansi na Elimu Kampasi ya Solomon Mahlangu Prof. Allen Malisa (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza (wa tatu kushoto) kuhusu makaburi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini yaliyopo Kampasi ya Solomon Mahlangu Mazibu mkoani Morogoro.


Mkuu wa Ndaki ya Sayansi na Elimu Kampasi ya Solomon Mahlangu Prof. Allen Malisa (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza (wa tatu kushoto) kuhusu makaburi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini yaliyopo Kampasi ya Solomon Mahlangu Mazibu mkoani Morogoro.

(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Morogoro)

…………………………………..

Na Eleuteri Mangi, WHUSM Morogoro

Serikali inawahimiza wadau na jamii nzima kutunza, kulinda na kuhifadhi maeneo ya kihistoria ambayo yalitumika wakati wa harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika ili historia hiyo isipotee na iweze kutumika kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza alisema hayo jana mkoani wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi siku mbili alipotembelea maeneo Dakawa na Mazibu yaliyotumiwa wapigania uhuru wa “African National Congress” (ANC) wa Afrika Kusini.

“Kazi ya kulinda, kuhifadhi na kuendeleza urithi wa Ukombozi wa Afrika uliopo Tanzania ni jukumu la jamii nzima, mashirika ya umma na watu binafsi ili kuthamini na kuenzi urithi huu muhimu wa Afrika” alisema Naibu Waziri Shonza.

Ili kutunza na kuhifadhi maeneo, nyaraka, vifaa na vielelezo vingine vilivyotumiwa na Wapigania uhuru, Serikali kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeanzisha Programu ya uhifadhi na uendelezaji wa historia ya Ukombozi wa Afrika ambayo pamoja na mambo mengine;inalenga kuthamini na kuenzi mchango wa Tanzania katika kuongoza harakati za mapambano ya kudai uhuru.

“Tunawashukuru sana wenzetu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuendelea kutumia na kuhifadhi maeneo haya, tumeona pamoja na kwamba yalitumika katika harakati za ukombozi, lakini kimsingi miundombinu mikubwa imebaki ikiwemo shule za msingi na sekondari, zahanati pamoja na vyuo katika maeneo yote ya Dakawa na Mazimbu ambayo yanaendelea kuhifadhiwa na kutumika ili kuhakikisha historia hii haipotei” alisema Naibu Waziri Shonza.

Aidha, aliwasisitiza na kuwahimiza Watanzania kutumia fursa ya kuwepo kwa utajiri huo wa kihistoria kwa kuya tembelea maeneo hayo wakiwemo wanafunzi wa ngazi za shule ya msingi, sekondari, vyuo vya kati pamoja na vyuo vikuu ili kujifunza historia hiyo sio tu kwa nadharia, bali kwa kujionea maeneo halisi pamoja na vifaa vilivyotumiwa na wapaingania uhuru hao.

Kwa upande wa eneo la Dakawa, upo utajiri mkubwa wa kihistoria ambao una manufaa kwa vijana na Watanzania kwa ujumla. Eneo hilo lina taasisi tano ambazo zinatumika hadi sasa ikijumuisha; shule ya msingi na shule ya sekondari ya wasichana Dakawa, chuo cha VETA, Chuo cha ualimu pamoja na Kituo cha afya.

Naye Mkuu wa Ndaki ya Sayansi na Elimu Kampasi ya Solomon Mahlangu Prof. Allen Malisa alisema Kampasi hiyo ilianzishwa mwaka 1978, wakati huo eneo hilo likijulikana kama makazi ya wapigania uhuru wa ANC wa Afrika ya Kusini.

Wapigania uhuru hao ambao wengi wao wakiwa ni vijana, walilazimika kukimbia Afrika ya Kusini ili kukwepa kukamatwa na Utawala wa Makaburu, kufuatia mgomo wa vijana wa Soweto wa mwaka 1976 hatua iliyopelekea vijana wengi kukimbilia Tanzania, ambapo awali walijikuta wamekuwa wengi kwenye mji wa Dar es Salaam kiasi cha kuhatarisha usalama baina yao na vijana wazawa.

Katika kutatua tatizo hilo, mamlaka ya utawala wa wakati huo iliwahamishia wapigania uhuru hao Mkoani Morogoro, na kwa vile kulikuwepo na haja ya kuwalinda na Makaburu ambao walikuwa wanafanya kila mbinu kuwatafuta popote walipo, waliwekwa jirani na kikosi cha jeshi la wananchi cha Mzinga kwa muda. Hatimaye, walihamishiwa eneo la Mazimbu ambalo liko uwanda wa chini na hivyo kutokuonekana kirahisi kutokea mjini Morogoro.

Kwa kuwa idadi ya vijana hao ilikuwa ni kubwa, na kutokana na ugeni katika makazi hayo mapya, hawakuwa na kazi za kufanya, hivyo kutumia muda mwingi kufundishana; wakubwa wakichukua nafasi ya ualimu na kuwafundisha wadogo.

Jambo hilo liliporipotiwa kwa uongozi wa ANC kule Afrika ya Kusini, liliwagusa Viongozi na kufanya aliyekuwa Rais wa chama, Ndugu Oliva Tambo, kuagiza makazi hayo waliyopewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ijengwe shule. kwa kutekeleza maagizo hayo ya ANC, eneo hilo lilijengwa shule iliyojulikana kama “ANC school” Mazimbu.

Kufuatia kijana aliyekuwa mpigania uhuru machachari, aliyejulikana kwa jina la Solomon Kalushi Mahlangu, kukamatwa na kutiwa kizuizini mwaka 1977 na hatimaye kunyongwa hadi kufa mwezi Aprili 1979, Uongozi wa ANC ulibadilisha jina la Mazimbu “ANC school” kuwa “Solomon Mahlangu Freedom College” (SOMAFCO) ili kutambua mchango wa wapigania uhuru wa ANC kwenye kutafuta uhuru.

Naibu Waziri Shonza yupo katika ziara ya kikazi kutembelea maeneo ya ya historia ya ukombozi wa Afrika katika mikoa ya Dodoma wilaya ya Kongwa, Morogoro wilaya Kilosa, Manispaa ya Morogoro pamoja na Mkoa wa Pwani wilaya za Chalinze na Bagamoyo.

SHIRIKA LA ‘ESTL’ MKOANI SINGIDA LATOA WITO KWA JAMII KUUNGANA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA, UKEKETAJI KWA MTOTO WA KIKE.

$
0
0

 Mratibu wa Mradi maarufu ‘Kick FGM out of Singida kutoka Shirika lisilo la kiserikali la ESTL, Rosemary Mfui akitoa mada mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ya Kata ya Mwankoko, Singida MC jana kuhusu athari za ukatili wa kijinsia na masuala ya ukeketaji.
 Mthamini Mradi wa ‘Kick FGM out of Singida kutoka Shirika lisilo la kiserikali la ESTL, Philbert Swai akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ya Kata ya Mwankoko, Singida MC jana, juu ya hatua mbalimbali za awali za kuchukua endapo mtoto wa kike amebakwa.
 Afisa Mendeleo ya Jamii, Singida MC, akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kamati ya kata ya kupinga vitendo vya ukatili kata ya Mwankoko, Singida MC jana (hawapo pichani) kuhusiana na matakwa ya Mwongozo uliopo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA)
 Wajumbe wa  Kamati ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ya Kata ya Mwankoko, Singida MC wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasiliswa na wataalamu wa ESTL (hawapo pichani) kuhusu athari za ukatili wa kijinsia na ukeketaji ndani ya jamii.
 Wajumbe wa  Kamati ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ya Kata ya Mwankoko, Singida MC wakisikiliza mada mbalimbali zinazowasiliswa na wataalamu wa ESTL (hawapo pichani) kuhusu athari za ukatili wa kijinsia na ukeketaji ndani ya jamii.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wajumbe wa MTAKUWWA kata ya Mwankoko, Singida MC, na wataalamu wa ESTL, mda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano uliojadili na kuweka mikakati ya namna bora ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike.

Na Dotto Mwaibale,  Singida
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Empower Society Transform Lives (ESTL), limetoa wito kwa watanzania kuungana pamoja katika kukabiliana na vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia kwa mwanamke na mtoto wa kike ikiwemo ukeketaji, ambavyo bado hufanyika kwa siri sana kwa baadhi ya maeneo.
Ifahamike ukeketaji ni aina yoyote ya kutoa kidogo au kutoa kabisa viungo vya nje vya uzazi vya mwanamke au mtoto wa kike bila sababu za kimatibabu. Ukatili wa aina hiyo hupelekea madhara makubwa kwa ustawi wa ukuaji wa mtoto wa kike kiafya, kimwili, kiuchumi na kiakili
Awali, mtindo wa ukeketaji uliokuwa ukitumika ni kumuwahi mtoto tangu akiwa mchanga, lakini kupitia juhudi kubwa za ukaguzi wanaofanyiwa watoto mara kwa mara wanapoletwa zahanati zimewashtua wahalifu wa vitendo hivyo. Sasa mbinu inayotumika kutekeleza uhalifu huo ni kushughulika na wale wenye umri wa kuanzia miaka 5 na kuendelea ambao hawapelekwi tena zahanati.
Akizungumza mbele ya Kamati ya Kutokomeza Ukatili wa kijinsia, hususan dhidi ya Wanawake na Watoto Kata ya Mwankoko, Singida MC, mkoani hapa jana, Mratibu wa mradi wa Kupinga Ukeketaji na Ukatili wa kijinsia kupitia ESTL maarufu 'Kick FGM Out of Singida,’ chini ya ufadhili wa Foundation for Civil Society, Rosemary Mfui, alisema ukatili huo unachangiwa zaidi na mambo ya kiimani anayoaminishwa mtu, sambamba na mila na desturi zilizopitwa na wakati
"Tatizo la ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji ni changamoto kubwa ndani ya mkoa wa Singida, baadhi ya watu bado wanafanya kwa siri, kitaifa tatizo linaonyesha kupungua lakini kwa mkoa wa Singida tatizo linaongezeka. Nichukue nafasi hii kuwasihi sana viongozi wa kimila, wazazi, viongozi wa dini, Jeshi la Polisi na jamii kwa ujumla tushikamane ili kwa pamoja tuweze kutokomeza vitendo vya ukeketaji kwa watoto wetu hawa wa kike," alisema Mfui
Alisema kinachosikitisha zaidi ukatili huo hufanyika kwa siri sana kwa wahusika kuogopa mkondo wa sheria, hali inayopelekea ugumu wa kubaini vitendo hivyo kutokana na watu walio wa karibu ya mwathirika wa tukio hilo kutoonyesha ushirikiano ipasavyo, na kuendelea kukumbatia na kuzipa hadhi mila potofu na kandamizi ndani ya baadhi ya jamii kwa kuzigeuza kuwa kama ndio sheria halali za kimila
Mfui alibainisha kwamba madhara ya ukeketaji ni mengi, ikiwemo kuweza kusababisha vifo kutokana na mwathirika wa tukio hilo kutokwa na damu nyingi, maambukizo ya magonjwa na hasa UKIMWI kutokana na vifaa vinavyotumika kwa ukeketaji kutokuwa safi na salama, maumivu makali wakati wa kujamiiana na kujifungua, ongezeko la mimba za utotoni na madhara ya kimwili na kisaikolojia
Aidha, akizungumzia kuhusu ukatili wa kijinsia, alisema ni kitendo anachofanyiwa mtu yeyote mwanamke au mwanaume kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza kisaikolojia, kimwili, kiafya, kingono au kiuchumi, kitendo kinachohusisha kutishia usalama na uhuru katika maisha ya mtu binafsi au jamii, huku wahanga wakubwa wa ukatili huo wakiwa ni wanawake na watoto wa kike
Kwa upande wake, Afisa Mthamini wa Mradi huo kutoka ESTL, Philbert Swai, pamoja na mambo mengine, alitoa mwongozo wa hatua za kuchukua pindi mwanamke au mtoto wa kike amebakwa au kulatiwa kuwa ni kwanza kuhakikisha anakimbilia sehemu salama.
Swai alisema baada ya hapo mhanga anapaswa kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola na ahakikishe anapewa fomu ya Polisi namba 3, kisha afike zahanati au kituo cha afya ndani ya masaa 72 kwa lengo la kupewa dawa za kuzuia maradhi na mimba.
Aidha, alitahadharisha kuwa kamwe mwathirika baada ya kufanyiwa tukio la ukatili asikubali kuwekwa chini na kufanyiwa vikao vya usuluhishi kutoka kwa yeyote, na aliyebakwa au kulatiwa akumbuke mda wote kuchukua ushahidi
“Usifue nguo, usioge, usichane wala kuosha nywele, na usibadilishe nguo baada ya kitendo cha ubakaji, endapo utabanwa na haja ndogo fanya hivyo kwenye chombo,” alisisitiza Swai
Alisema azma iliyopo kwa ESTL ni kuhakikisha wanatokomeza kabisa vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukeketaji ndani ya maeneo yote ya mkoa huo, na hivi karibuni kwa kushirikiana na serikali kupitia Manispaa ya wilaya ya Singida wanatarajia kuendelea kutoa elimu hiyo ya ukatili wa kijinsia na masuala ya ukeketaji kwa makundi tofauti ndani ya jamii
Swai alisema kwa mujibu wa takwimu za kitafiti, mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa mitano kitaifa ambayo masuala hayo ya ukeketaji yameonyesha kushamiri. Takwimu zinaonyesha asilimia 31 ya wanawake wa mkoa huo wamekumbwa na kadhia hiyo, jambo ambalo alisisitiza kuwa jamii inapaswa kukataa hali hiyo na kubadilika
Awali, akifafanua mwongozo wa uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto 2017/2018-2021/22 (MTAKUWWA), Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Tumaini Sabbi Christopher, alisema lengo la mpango huo ni kukabiliana na changamoto za ulinzi wa wanawake na watoto nchini
Christopher kupitia mwongozo wa mpango huo, alibainisha kwa mujibu wa takwimu za kitafiti zinaonyesha kwamba mwanamke 1 kati ya 5 ametoa taarifa ya kufanyiwa ukatili wa kingono katika maisha yake, msichana 1 kati ya 3 na mvulana 1 kati ya 7 walifanyiwa ukatili wa kingono kabla ya umri wa miaka 18
Katika kutekeleza mpango huo kwa ufanisi, serikali imeandaa mwongozo wa uratibu, usimamizi, na ufuatiliaji. Aidha, mwongozo huo unatoa maelekezo kuhusu uundwaji wa kamati mbalimbali, mfumo wa mawasiliano na uwasilishaji wa taarifa kutoka ngazi ya taifa mpaka kijiji
“Hata hivyo pamoja na uhaba wa rasilimali fedha za kuhudumia kamati zote za mtakuwwa nchi nzima, serikali kwa kushirikiana na wadau mpaka sasa tayari imeandaa sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia (2000), na sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008), kupitishwa kwa Sheria ya Mtoto Na. 21 na kanuni zake,” alisema
Christopher aliongeza kuwa, juhudi nyingine zilizofikiwa ni pamoja na kuanzishwa Dawati la Jinsia kwenye wizara zote, kuanzishwa kwa mifumo ya ulinzi wa mtoto katika halmashauri 63 nchini, kuanzishwa kwa Dawati la Jinsia na Watoto kwenye vituo vya Polisi 417, sambamba na kuanzishwa kwa mahakama za kusimamia kesi za watoto katika halmashauri 131.

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA JELA AU FAINI YA MILIONI MBILI KWA KUKUTWA NA VIUATILIFU VISIVYO SAJILIWA

$
0
0


Na innocent Natai, Morogoro

Mahakama ya Wilaya ya  Ifakara Mkoani Morogoro imemuhukumu kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela au faini ya shilingi Milioni Mbili pamoja na kuviteketeza viuatilifu kwa gharama zake mwenyewe, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Yerusalem Mwamaja miaka 49 (Mhehe) baada ya kupatikana na hatia ya kupatikana na viuatiliafu visivyo sajiliwa
Hukumu hiyo imetolewa  Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Binge Njaga Mashabara, baada ya kujiridhisha na hoja za mashahidi watatu wa upande mshtaka, bila kuacha shaka yeyote.

Hakimu Mashabara alisema vitendo kama hivyo vinawasababishia hasara wakulima na seikali kwa ujumla ukiachilia mbali kuendelea kusababisha madhara kwa mazingira na kwa Afya za binadamu wanyama na mimea. Hivyo alitoa adhabu hiyo ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo.

Awali, Wakili wa Serikali, alidai kuwa hakukuwa na kumbukumbu za mashtaka ya nyuma dhidi ya mshatakiwa na hivyo kuiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo.

Katika utetezi wake Yerusalem Mwamaja alikubali mashtaka na aliomba apunguziwe adhabu kwani ni mara yake ya kwanza kufanya kitendo hicho na hata rudia.

Akizungumzia hukumu hiyo baada ya kutoka Mahakamani hapo Bw Solomon Shedrack Mungure amabaye ni Mkurugenzi wa Viuatilifu kutoka ofisi ya TPRI Dar es Saalam ameipongeza Mahakama hiyo kwa adahabu iliyotoa kwani itakuwa ni fundisho kwa wengine wenye tabia za kufanya biashara za viuatilifu visivyo Sajiliwa.


Aidha ametoa rahi kwa wauzaji na wasambazaji wa Viuatilifu nchi nzima wenye tabia za kuuza na kusambaza viuatilifu visivyo sajiliwa na kukaguliwa na TPRI kuacha mara moja kwani zoezi la ukaguzi na kuwabaini watu kama hao halikomi ni la kila siku na kila saa hivyo watakamatwa mara moja na kuwafikisha mahakamani.


Aidha amehitimisha kwa kusema kuwa kuuza au kusambaza viuatilifu bila kwa na elimu pia ni kosa kwani kunaweza kumsababishia madhara msambazaji au muuzaji wakati wa ufanyaji biashara bila kuwa na elimu ya namna bora na salama ya kufanya biahara hiyo, hivyo ni vyema wasio na taaluma hiyo kuacha kufanya biashara hizo mara moja na wafuate kanuni na taratibu za kupata mafunzo na kibali cha kufanya biashara hizo.

Babawatoto organization yakutana wadau kujadili upigaji vita unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa mitaani jijini Dar

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la Babawatoto, Mgunga Mwamnyenyelwa akizungumza katika mkutano wa kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto wa mitaani uliowahusisha wadau wa kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa mitaani uliofanyika kwenye Ukumbu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam hivi karibuni. Mkutano huo uliandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Babawatoto.
 Mkuu wa kituo cha Polisi Magomeni, OCS Laurent Idowa  akitoa maelezo ya namna ya kukabiliana na changamoto za kijinisa zinazowakabili watoto wa mitaani katika mkutano wa wadau wa kujadili unyanyasi wa kijinsia kwa watoto wa mitaani, uliofanyika kwenye Ukumbu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam hivi karibuni.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la BabawatotoMgunga Mwamnyenyelwa (kulia) akiwa pamoja na washiriki wengine wakati wasikikiza maoni ya wadau wakati wa mkutano wa kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa mitaani uliofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Afisa wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia kanda maalumu, Mudathir Kato akitoa maelezo wakati wa mkutano wa wadau ww kujadili upigaji vita unyanyasaji wa kinjisia kwa watoto wa mitaani huo ulioratibiwa na taasisi ya Babawatoto organization hivi karibuni.
Picha ya pamoja ya wadau waliohudhira mkutano wa wadau wa kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa mitaani uliofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni

TMDA yang’ara Kimataifa

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo pichani), kuhusu mafanikio ya Mamlaka hiyo katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam.


Mamlaka ya Dawa na vifaa tiba nchini TMDA , imetambulika na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika ubora wa udhibiti wa dawa na kuifanya Tanzania kupitia mamlaka hiyo kuwa ya kwanza barani Afrika kufikia mafanikio hayo na imekuwa mshindi wa kwanza kwa ubunifu wa mfumo wa utoaji huduma kwa wananchi katika wiki ya Utumishi wa umma barani Afrika mwaka 2019.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo, alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia mafanikio ya Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne.

Amesema katika kipindi hicho TMDA imefanikiwa kushikilia cheti cha kimataifa cha ithibati cha ISO 9001:2015 ambapo maabara ya Taasisi hiyo inatambuliwa na shirika la Afya Duniani kutokana na ubora na umadhubuti wa kazi zake.

“Katika kipindi cha Miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, sisi kama taasisi tumefanya mambo mengi makubwa ambayo yameleta mageuzi katika masuala ya udhibiti na usalama wa Dawa na vifaa tiba, na tumeimarisha na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato” Alisema Kaimu Mkurugenzi huyo wa TMDA.

Aidha amesema TMDA imesajili zaidi ya bidhaa 20,247 za dawa na vifaa tiba baada ya kujiridhisha ubora ,usalama na ufanisi wake hivyo kuongeza wigo wa upatikanaji wa bidhaa kwaajili ya kulinda afya za watanzania.

Mamlaka pia imeimarisha udhibiti wa bidhaa kwa asilimia 96 katika kipindi cha mwaka 2015 hadi Novemba 2019 hivyo kuifanya nchi yetu kuwa salama, pia mamlaka imeweza kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kujenga maabara ya kisasa Jijiji Mwanza.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo wa TMDA amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuwekeza katika taasisi hiyo ili kulinda afya za watanzania , kwa kuongeza bajeti kutoa Shilingi Bilioni 34.64 mwaka 2015/16 hadi Shilingi Bilioni 53.31 kwa mwaka 2018/19 ambayo ni sawa na asilimia 53.8.

Mafanikio hayo yamewezesha kuimarika kwa huduma pamoja na kiuwezesha taasisi kutoa gawio kwa serikali kila mwaka hadi kufikia shilingi Bilioni 29.1 katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Katika kuelekea Tanzania ya Viwanda TMDA imetoa msaada wa kiufundi katika kuanzishwa kwa viwanda vipya 12 vya dawa na vifaa tiba hivyo kuchangia katika juhudi za kukuza uchumi kupitia viwanda, na katika kutimiza adhma hiyo imeanza kutumia mfumo wa kielektroniki katika utoaji wa vibali ambapo hutolewa kwa saa 24.

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA ni Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Afya iliyoundwa kwa mujibu wa Sheria baada ya kufanyiwa marekebisho ya kiutendaji ya aliyokuwa Mamlaka ya na baadhi ya majukumu yake kuhamishiwa katika shirika la Viwango Tanzania TBS.

DIRA YA SERIKALI YAZIDI KUWAVUTIA WAWEKEZAJI NCHINI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
DIRA ya Serikali ya awamu ya tano ambayo imejikita katika ujenzi wa viwanda imezidi kuwavutia wawekezaji wengi zaidi wenye uhitaji wa kuwekeza na kutengeneza masoko zaidi nchini, ambapo leo Desemba 05 kampuni ya JK White cement (Afrika) Limited ambayo ni sehemu ya kampuni ya JK ya nchini India imetangaza rasmi kuungana kibiashara na kampuni ya uzalishaji wa rangi ya Goldstar Paints ya Tanzania ili kuingiza sokoni bidhaa mpya ya JK Wall Putty bidhaa ambayo ni poda laini itokanayo na saruji nyeupe yenye kutoa mwonekano mzuri kwa kuta na dari ambayo itaenda sambamba na mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa JK cement Amit Kothari amesema, ushirikiano huo wa kibiashara umelenga kukata kiu ya wananchi kwa kutoa bidhaa bora yenye kuendana na mazingira.

"JK cement ni moja kati ya wazalishaji bora wa cement na tumepata  washirika makini ambao tutaziba ombwe lililopo pamoja na kutoa ajira, na kubwa zaidi ni kufungua ofisi na kupandisha bendera Tanzania kwa mara ya kwanza katika ukanda wa Afrika na dunia, na hiyo ni kutokana na ushirikiano mzuri tunaooneshwa na Serikali ya Tanzania" ameeleza Kothari.

Amesema kuwa wanajivunia kuwa sehemu ya watanzania na kueleza kuwa kampuni hiyo isiitwe ya wahindi bali watanzania kwa kuwa Goldstar Paint wamekuwa kwenye safari na dhamira ya kutoa bidhaa zenye ubora zenye kukidhi mahitaji ya watanzania kupitia bidhaa zao.

Kwa upande wake  Mkurugenzi Mtendaji wa Goldstar Srinivasan amesema kuwa  kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele  hasa katika masoko kwa Kuhakikisha kwamba inaleta bidhaa zenye viwango stahiki na kwa sasa wameongeza bidhaa nyingine kwenye soko jambo ambalo wanaamini litaleta mabadiliko na mapinduzi katika kuwahudumia wateja.

Amesema kuwa, JK ikiwa moja kati ya kampuni kubwa za uzalishaji wa saruji nyeupe duniani na mzalishaji mkuu wa bidhaa ya Wall Putty nchini India  wataendelea kuwahudumia watanzania kwa kuwapa bidhaa bora zaidi ambazo zinaendana na mazingira.

Kampuni ya JK cement yenye makazi yake Fujairah (UAE) wamekuwa wadau kwa nchi za Afrika na katika kujipapanua zaidi  wamejiegemeza zaidi katika kukuza soko lake Tanzania kupitia muungano huo wa kibiashara na kampuni ya Goldstar iliyoanzishwa mwaka 1988 ambao wamekuwa maarufu zaidi kupitia rangi ya Goldstar ambayo hupatikana kote nchini na ilichaguliwa miongoni mwa makampuni 50 bora zaidi nchini na TBS na TPSF mwaka 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa JK cement Amit Kothari akizungumza wakati wa hafla ya makubaliano ya kibiashara yaliyofanyika kati ya kampuni ya JK cement na kampuni ya Goldstar Paints ambapo ameeleza kufurahishwa na Serikali katika suala zima uwekezaji, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Goldstar Paints K. Srinivasan akizungumza wakati wa hafla ya makubaliano ya kibiashara yaliyofanyika kati ya kampuni ya JK cement na kampuni ya Goldstar Paints ambapo amesema kuwa wataendelea kutoa huduma kwa Bora kwa watanzania, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Goldstar Paints K.Srinivasan (kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya JK Cement Amit Kothari kama ishara ya kupongezana na kufanya kazi pamoja, leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa kampuni hizo  na wadau wa 5mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.

MADAKTARI BINGWA WA WATOTO WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA NA PROF. PAN XIANG BIN KUTOKA CHINA

$
0
0

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani na wenzake kutoka Jamhuri ya watu wa China wakimpima mtoto kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiogram) kabla ya kumfanyia upasuaji mdogo wa kuziba tundu la moyo kupitia mshipa wa damu wa kwenye paja kwa kutumia mashine ya (ECHO machine) bila ya kutumia mionzi (Transthoracic Echocardiography – TTE). Mara nyingi upasuaji huo hufanyika kwa njia ya mionzi kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization Laboratory).
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Jamhuri ya watu wa China Prof. PAN Xiang Bin akimfanyia mtoto mwenye umri wa miaka minne ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) upasuaji mdogo wa kuziba tundu la moyo bila kufungua kifua kupitia mshipa wa damu wa kwenye paja kwa kutumia mashine ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO machine) bila ya kutumia mionzi (Transthoracic Echocardiography – TTE). Mara nyingi upasuaji huo hufanyika kwa njia ya mionzi kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization Laboratory).
Madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Jamhuri ya Watu wa China wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumfanyia mtoto upasuaji mdogo wa kuziba tundu la moyo bila kufungua kifua kupitia mshipa wa damu wa kwenye paja kwa kutumia mashine ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO machine) bila ya kutumia mionzi (Transthoracic Echocardiography – TTE). Mara nyingi upasuaji huo hufanyika kwa njia ya mionzi kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization Laboratory).(Picha na JKCI).

DKT. ABBASI AWAPIGA MSASA MAAFISA HABARI UANDAAJI WA TAARIFA KWA UMMA

$
0
0

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiwasilisha mada kuhusu uandaaji wa taarifa kwa umma wakati wa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali Jijini Dodoma leo tarehe 3 Desemba 2019. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni awamu ya pili kufanyika yameandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO). Majadiliano ya vikundi Baadhi ya Maafisa wakifanya mazoezi kwa vitendo ya namna ya uandishi wa Taarifa kwa Umma/Vyombo vya Habari wakati wa mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari kutoka wizara, taasisi, mashirika ya umma na halmashauri nchini leo tarehe 03 Desemba 2019 Jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni awamu ya pili kufanyika yameandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO). Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), Bw. Twaha Twaibu akichangia mada wakati wa mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari kutoka wizara, taasisi, mashirika ya umma na halmashauri nchini leo tarehe 03 Desemba 2019 Jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni awamu ya pili kufanyika yameandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO). Mjumbe wa kamati tendaji ya Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Bw. Innocent Byarugaba akiwaongoza Maafisa Habari kumpongeza Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (mwenye suti nyeusi) mara baada ya kumaliza kuwasilisha mada kuhusu uandaaji wa taarifa kwa umma/vyombo vy habari wakati wa mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati Maafisa hao leo tarehe 03 Desemba 2019 Jijini Dodoma.Kulia ni Katibu Mtendaji wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni awamu ya pili kufanyika yameandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO). (Picha zote na: Idara ya Habari – MAELEZO)

TAZAMA SAFARI NZIMA YA TRENI YA MAJARIBIO YA DELUXE YA DAR ES SALAAM HADI MOSHI

MKUU WA WILAYA YA ILEJE AMPATIA BAISKELI YA MIGUU MITATU KIJANA MLEMAVU

$
0
0

Na Dan Mwambene, Ofisi ya DC Ileje
Wakati Siku ya Walemavu Duniani imeadhimishwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje amemtembelea na kumkabidhi baiskeli ya tairi tatu kijana aliyekatwa miguu yote baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Waswahili husema,kabla hufajafa,hujaumbika usemi huu unamwangukia kijana mwenye umri mchanga akiwa na ndoto zenye kumfikisha mbali kimaisha ambazo sasa zimepunguzwa kasi na ulemavu huo.
Akiwa mwenye umri wa miaka 23 mtoto wa nne kati ya watoto saba wa Mzee Odeni Mwambene kijana Costa Mwambene mkazi wa Kitongoji cha Ipapa Kijiji cha Isongole Ileje ameshapoteza miguu yote na kuwa tegemezi.
“Nimeugua kwa karibu miaka mitatu kilianza kijipu kidogo mguu wa kulia na badaye mguu wa kushoto hali iliyomsababishia vidonda na kupelekea nikatwe miguu yote miwili”alisema kijana huyo akiuguza majeraha muda wote kitandani.
Baada ya kupokea ombi la mlemavu huyo hatimaye Mkuu wa Wilaya ya Ileje Ndg.Joseph Mkude alifika nyumbani kwa wazazi wa Costa na kukabidhi baiskeli ya tairi tatu itakayomsaidia.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi baiskeli hiyo kiongozi huyo aliitaka jamii kutambua kuwa kila mmoja anaweza kuwa mlemavu akashukuru watu walioweza kutoa michango yao wakati wa kumhudumia kijana Costa aliyeanza kuugua mwanzoni mwa mwaka 2017. 
Mdogo wa mlemavu huyo alisema kuwa kutokana na maradhi hayo mke wa kaka yake alishaondoka baada ya kumwuguza miaka miwili tu.
‘’Mwanzo aliomba kwenda kwao kupumzika,lakini katikati ya mwaka huu tukiwa Hospitali ya Ikonda mkoani Njombe alikokatwa miguu tulipigiwa simu na mama yetu kuwa amechukua talaka”alisema kwa masikitiko.
Aliongeza kuwa wametumia fedha nyingi ikiwemo kuuza nyumba ya mgonjwa,kuuza ng’ombe wanne wa familia wakihangaika kuponya maradhi ya ndugu yao wakitibiwa katika hospitali za Ileje,Kyela,Chitipa-Malawi  na Ikonda Njombe.
Alisema kwa sasa mipango ya maendeleo ya kifamilia imesimama kutokana hali inayowasibu kwani kila baada ya siku mbili hulazimika kukodi gari kwa elfu saba ili kwenda kuhudumiwa Hospitali ya Wilaya umbali wa kilometa saba.  
 kijana Costa Mwambene enzi hizo kabla hajapata ulemavu wa kukatwa miguu yote.

 kijana Costa Mwambene enzi hizo kabla hajapata ulemavu wa kukatwa miguu yote.

DC Joseph Mkude (kushoto)akiwa na Costa Mwambene siku alipomtembelea na kumkabidhi baiskeli ya tairi tatu. 
Kijana Costa Mwambene baada ya kupata ulemavu.

Kijana Costa Mwambene baada ya kupata ulemavu.

 Kijana Costa Mwambene baada ya kupata ulemavu.
DC Joseph Mkude wa Ileje (aliyevaa shati la bluu) akizungumza mara baada ya kumwona na kukabidhi baiskeli kwa wazazi wa mlemavu Costa Mwambene. 

 Mzee Odeni Mwambene na mkewe Luhobokelo Nyondo wakazi wa Isongole Ileje(kulia) wakimshukuru DC wa Ileje aliyefika nyumbani  kwao kumwona kijana wao mlemavu na kumkabidhi baiskeli ya taili tatu.

Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images