Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109572 articles
Browse latest View live

DC CHONGOLO KUTOA TUZO KWA MITAA IKAYONG’ARA KWENYE USAFI, AWATAKA KUSIMAMIA SHERIA VIZURI KWA WANAOTUPA TAKA HOVYO

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amesema kuwa ameanzisha kampeni ya utoaji tuzo kwa mitaa itakayofanya vizuri kwenye suala la usafi ambapo kila mtaa utapatiwa zawadi ya fedha tathilimi.

Aidha Chongolo amewaonya wananchi wanaotupa taka hovyo na hivyo kuwataka watendaji hao kusimamia sheria kwa watakaojihusisha na uharibifu huo wa mazingira ikiwemo kulipa faini kwa mujibu wa sheria.

 Mhe. Chongolo ametoa kauli hiyo leo, wakati wa ufunguzi wa semina elekezi kwa wenyeviti wa serikali, wajumbe wa mitaa pamoja na watendaji kata iliyofanyika katika ukumbi wa King Solomi Ostarbey.

Mhe. Chongolo amesema kuwa lengo la kampeni hiyo, ni kuongeza motisha katika kuboresha Halmashauri hiyo kuwa katika muonekano mzuri, na kuwasisitiza watendaji hao pamoja na wenyeviti wa mitaa kusimamia kwa ukamilifu.

Amefafanua kuwa tuzo hiyo itatolewa  kila maada ya miezi mitatu ambapo mtaa utakaoibuka na ushindi itapatiwa fedha tathilimu kiasi cha shilingi 500, 0000, mshindi wa pili 300,000 huku mshindi wa tatu akipata shilingi 200,000.

“ Halmashauri ya Kinondoni ni safi, lakini tunatakiwa kufanya vizuri zaidi , kwa mantiki hiyo tunakuja na kapmeni ya usafi wa kila mtaa, watakaofanya vizuri watapatiwa zawadi ya fedha, na fedha hizo zitabaki kwenye mitaa yenu kwa ajili ya shuguli nyingine” amesema Mhe. Chongolo.

”Watakaoendesha mchakato huo ni nyie wenyeviti na wajumbe wa mitaa, kazi yangu mimi ni kuweka fedha kwa ajili ya kutoa zawadi, na kampeni hiyo tunaianza leo hii arehe nne mwezi wa 12 kwa hiyo ikifika tarehe nne mwezi watatu 2020 tutatoa tuzo hiyo kwa mitaa itakayokuwa imeshinda.

Aidha Mhe. Chongolo ameongeza kuwa pamoja na tuzo hizo kutolewa amewataka watendaji  kusimamia sheria na kanuni za utunzaji mazingira ikiwemo kutoza faini kwa watu wanaotupa taka hovyo kwani kwakufanya hivyo wataongeza ufanisi na ubora wa mitaa kuendelea kuwa misafi.

“ Zipo sheria za usafi ambazo zimewekwa kwa mujibu wa sheria lakini hazifuatwi, watendaji, wenyeviti na wajumbe mliopo hapa nendeni mkazisimamie vizuri”amesisitiza.

Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amewataka viongozi hao kusimamia mapato vizuri sambamba na kuepuka rushwa kwa kuwa kufanya hivyo kutawaingiza kwenye matatizo makubwa.

“ Kunasuala la rushwa, ni waonye msijihusishe na mambo hayo, leo hii hapa kuna maafisa kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wapo hapa nawao wata waeleza madhara ya kupokea au kutoa rushwa, niwaombe sana msikilize kwa makini na mkayafanyie kazi” ameongeza Mhe. Chongolo.

Kwa upande wake Afisa utumishi mkuu wa Halmashauri hiyo Bi Faudhia Nombo amesema kuwa lengo la mafunzo hayo elekezi ni kuwawezesha viongozi hao ili waweze kutekeleza majukumu ya usimamizi na undeshaji wa shughuli mbalimbali katika mitaa yao kwa kuzingatia Sera, Sheria , Taratibu ,Kanuni na miongozo iliyopo ilikuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akitoa nenowakati wa ufunguzi wa semina elekezi kwa wenyeviti wa serikali, wajumbe wa mitaa pamoja na watendaji kata iliyofanyika katika ukumbi wa King Solomi Ostarbey.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni Ndugu Harodi Maruma akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina elekezi kwa wenyeviti wa serikali, wajumbe wa mitaa pamoja na watendaji kata iliyofanyika katika ukumbi wa King Solomi Ostarbey.
Wajumbe wakifuatilia mafunzo yaliokuwa yakitolewa katika ukumbi wa king Solomon leo.

Tamasha la Twenzetu Kilimanjaro Fest laja

0
0
 Wenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro watakaoenda likizo mwaka huu kwa msimu wa sikukukuu wameandaliwa burudani mbalimbali kwenye Tamasha  kubwa linalotarajiwa kufanyika  tarehe 22 Disemba 2019 kwenye Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi.

Tamasha hilo linalojulikana kama ‘Twenzetu Kilimanjaro Fest’ 2019 limendaliwa na Kampuni ya Real PR Solutions ya jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia Tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuzinduliwa rasmi hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo Bw Clement Mshana amesema ni sehemu ya mkakati wa kufanikisha Mpango wa Kuendeleza Utalii wa Ndani (Domestic Tourism Promotion Initiative (DTPI) unaotarajiwa kufanyika mikoa mbalimbali nchi nzima kwa kuanza  na Mkoa wa Kilimanjaro.
“Tamasha hili la Twenzetu Kilimanjaro Fest  linatarajiwa kupambwa na matukio kadhaa ya burudani zikiwemo, Mbio za kujifurahisha za Capital Mountain Run zitakazohusisha Km 5, Km 10 pamoja na mbio za watoto za Km 3 na Mbio za Baiskeli za KM 60, Maonesho ya Utalii na Biashara, Burudani na viburudisho mbalimbali ikiwemo michezo ya watoto, vyakula vya asili na muziki.’’ Alitaja.
Alisema katika Mkoa wa Kilimanjaro Tamasha hilo hasa litahusisha agenda kuu tatu ambazo ni pamoja na kutangaza Utalii wa ndani, upandaji wa miti  pamoja na kuhamasisha uwekezaji wa viwanda katika mkoa huo.
Aidha katika mkakati wake wa kufanikisha agenda hizo, kampuni hiyo ya Real Pr Solutions imeandaa matukio kadhaa ya kijamii ili kuunganisha wadau mbalimbali wa mkoa huo kama utembeleaji wa vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo mkoani Kilimanjaro ikiwemo, Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na maporomoko mbalimbali ya maji yaliyopo mkoani humo.
“Tutukio hili la  utembeleaji wa vivutio na upandaji miti linatarajiwa kufanyika Disemba 21, 2019 yaani siku moja kabla ya Tamasha,’’ alisema huku akitaja tukio jingine kuwa ni upandaji wa miti zoezi ambalo litatekelezwa kwa uratibu wa pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) likihusisha wadau mbalimbali ikiwemo mashirika na taasisi za umma ikiwemo shule na vyuo mbalimbali mkoani Kilimanjaro.
Mbali na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)aliwataja baadhi ya wadau muhimu katika ufanikisha tamasha hilo kuwa ni pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
“ Wengine ni pamoja na Kampuni ya Ujenzi ya CRJE (East Africa) Limited, HAL, Kilimanjaro Wonders Hotel, Nyumbani Hotels na Afrimax Strategic Partnerships.”
 “Kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya Tamasha hili ninawaomba sana wadau mbalimbali wajitokeze kutuunga mkono ili tuweze kufanikisha maandalizi ya Utekelezaji wa Mpango huo.’’ Alisema.

WIZARA YA MAJI YAWEKA KAMBI MISUNGWI

0
0
UONGOZI wa Wizara ya Maji ukiongozwa na Naibu Waziri, Jumaa Aweso na Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Anthony Sanga umeweka kambi Wilayani Misungwi kwa lengo la kupata ufumbuzi wa miradi ya maji inayotekelezwa kwa kusuasua wilayani humo. 

Uamuzi huo umefikiwa wakati wa ziara ya viongozi hao Desema 3, 2019 ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa Wilayani Misungwi ambapo walionyesha kutoridhishwa na hali ya utekelezaji wake. 

Akizungumza juu ya uamuzi huo wa kuweka kambi wilayani humo, Jumaa Aweso alisema hali aliyoishuhudia ya utekelezaji wa miradi ya maji unakwenda kinyume na dhamira ya Rais John Pombe Magufuli ya kuhakikisha wananchi wanaondokana na kero hiyo haraka iwezekanavyo. 

Wakati wa ziara hiyo, Aweso na Naibu Katibu Mkuu Sanga walikuta ujenzi wa mradi wa Ihelele na Mbarika unaotekelezwa na Mkandarasi Shanxi Construction Engineering Corporation ya China ukiwa umesimama kwa madai ya kuchelewa kufika kwa mabomba ya chuma (steel pipes) kutoka kwa mtoa huduma kiwanda cha Tanzania Steel Pipe (TSP) jambo ambalo liliwalazimu kuitisha kikao cha dharura kitakachohusisha wadau wanaohusika na ujenzi wa mradi. 

"Hili suala halikubaliki, Serikali imetoa fedha lakini hakuna kinachoendelea, ninaagiza kesho nikutane na TSP, Mkandarasi na Msimamizi wa mradi KASHWASA ili tupate ufumbuzi wa pamoja," alisisitiza Naibu Waziri Aweso. 

Aweso alisisitiza kuwa hatoondoka Wilayani humo hadi hapo utatuzi wa bomba hizo utakapopatikana ikiwa ni pamoja na TSP kuthibitisha lini watakamilisha na kuleta mabomba hayo. 

"Nimeelezwa kwamba TSP bado inadai kiasi cha fedha ili kukamilisha mabomba, niwathibitishie wananchi wa Misungwi Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametupatia fedha sasa tunataka kiwanda kituthibitishie lini kitakamilisha mabomba haya ya mradi," alisema Aweso. 

Mbali na hilo, Aweso alimuagiza Mkandarasi kuhakikisha ifikapo Machi, 2020 mradi uwe umekamilika na wananchi wanapata huduma

Kwa upande wake Mhandisi Sanga alisisitiza kuwa fedha za kutekeza miradi ya maji Wilayani Misungwi ilikwishatengwa na alisisitiza Mkandarasi kuhakikisha anakamilisha kazi kama alivyoelekezwa. 

Mhandisi Sanga alishukuru jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha wananchi wanaondokana na kero ya maji ambapo alisema fedha imekuwa ikitoka kwa wakati na hivyo hakuna sababu ya kuchelewesha miradi. 

"Namshukuru sana Mhe. Rais kwani hajawahi kuchelewa kutupatia fedha ya kukamilisha miradi na amekuwa mstari wa mbele kufuatilia na kila anapoahidi hajaacha kutekeleza," alisema Mhandisi Sanga. 

Mradi wa Maji Ihelele utanufaisha zaidi ya wananchi 81,000 kutoka vijiji vya Nyang'omango, Isesa, Igenge na Mbarika.
 Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Maji Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Leonard Msenyele wakati wa ziara kwenye mradi wa maji wa Nyahiti
 Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akielekeza jambo wakati wa ziara yake kwenye mradi wa maji wa Nyahiti, Wilayani Misungwi
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (wa pili kulia) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Anthony Sanga (kulia) wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga (wa pili kudhoto) akieleza jambo wakati wa ziara yao wilayani Misungwi.

SIMBA SC KUIVAA ARUSHA FC, YANGA SC NA IRINGA UNITED RAUNDI YA TATU YA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM SPORTS

0
0
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Droo ya Raundi ya Tatu ya Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) imeendeshwa leo jijini Dar es Salaam, ikihusisha timu 64: Timu 20 kutoka Ligi Kuu, Timu 24 kutoka Ligi Daraja la kwanza na timu 20 zilizofuzu kutoka madaraja ya chini.

Katika Droo hiyo, timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Michuano hiyo, Azam FC  watakumbana na timu ya African Lyon ya Dar es Salaam. Simba SC yenyewe itavaana na Arusha FC ya Arusha wakati Watani wao wa Jadi, Yanga SC watavaana na Iringa United ya Iringa.

Timu kutoka Tanga (Tanga Derby), Coastal Union ya mjini humo yenyewe itacheza na African Sports, mchezo utakaopigwa katika dimba la CCM Mkwakwani ikiwa ni Raundi hiyo ya Tatu ya Kombe ya Shirikisho (ASFC).

Timu nyingine za Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ambazo zipo juu katika Msimamo wa Ligi hiyo ni Lipuli FC ya Iringa wataikaribisha Dar City ya Dar es Salaam, Kagera Sugar katika dimba la Kaitaba Stadium watacheza na Rufiji United, Tanzania Prisons wakiwa katika Dimba la Sokoine wataikaribisha Mlale FC.

Mtibwa Sugar wakiwa nyumbani Morogoro wataikaribisha Rhino Rangers, Namungo FC wakiwa katika dimba la Majaliwa Stadium watacheza na Green Warriors na JKT Tanzania watapepetana na Boma FC ya Mbeya.

Timu nyingine za Ligi Kuu ni Mbeya City dhidi ya Migombani, Polisi Tanzania watacheza dhidi ya Top Boys, Mwadui ya Shinyanga watacheza dhidi ya Mkamba Rangers ya Morogoro na Singida United itakuwa ugegeni kukabiliana na Tukuyu Stars ya Mbeya katika dimba la Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. 


Michezo mingine ni:-
KMC v Mbuni FC
Alliance FC  VS Transit CAMP
Ndanda FC VS Cosmopolitan
Ruvu Shooting VS Milambo FC
Mbao FC VS Stand UNITED
Biashara United VS Nyamongo

Mawenzi FC VS Mtwivila City
Mpwapwa VS Kitayosa
Friends Rangers VS Talinega FC
Kasulu Red Star VS Ihefu FC
Gipco VS Toto Africans
The Mighty Elephant VS Mashujaa FC
Jeshi Warriors VS Dodoma FC
Majimaji VS Pamba FC
Area C United VS Panama FC
Gwambina FC VS Mbeya Kwanza
Geita Gold VS Pan African
Sahare All Stars VS Njombe Mji

Mkurugenzi wa Mashindano wa Shrikisho la Soka nchini (TFF), Salum Madadi amesema mchakato wa sehemu ambapo itachezwa Fainali bado unaendelea, amesema michezo ya Raundi hiyo ya Tatu ya Michuano hiyo itaanza kucheza Desemba 22 na 23, 2019.

TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada wilayani Babati yashika kasi katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole.

0
0
Wakazi wa wilayani Babati mkoani Manyara na viunga vyake wamejitokeza katika kupata namba za vitambulisho vya Taifa ili kukidhi matakwa ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA ipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya Uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole na kuongeza kuwa ambaye hatatimiza matakwa ya kisheria ya kusajili laini ya simu kwa alama za vidole laini hiyo itafungwa

Kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika maeneo ya miji na Mkoa lengo Wananchi kutumia fursa ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole ambayo unakwenda nchi nzima 

Akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Babati katika Stendi ya mabasi ya Zamani ya Magugu Mkuu wa Kanda ya Kasikazini wa TCRA Mhandisi Emelda Salum amesema ni fursa kwa wananchi wa Babati na maeneo Mbalimbali wamefika katika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya Magugu kupata namba ya kitambulisho cha Taifa katika mfumo wa NIDA na kuweza kusajili laini ya simu kwa alama za vidole.

Mhandisi Salum Amesema katika Kampeni hiyo imekuwa inafanywa na kanda hiyo ikiwa kila mwananchi aweze kuwa na namba ya Kitambulisho au Kitambulisho cha Taifa kutokana Ushirikiano na NIDA kuwa katika Kampeni hiyo.Amesema kuwa Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa kwa pamoja kwa huduma za mawasiliano na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika huduma za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi na kuongeza kuwa muda ulioabakia ni 27 mdogo hivyo kila mtu atumie kutafuta taarifa zinazokidhi usajili wa laini kwa alama za vidole.

Hata hivyo amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Hata hivyo amesema kuwa kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana makosa ya jinai ya matumizi ya simu yasiofuata sheria.

Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia wananchi kuhakikisha kila mwananchi anasajili laini ya simu kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa au namba ya kitambulisho hicho.Salum amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa kupitia Kampeni ya Mnada kwa mnada.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31 kwa kufika katika maduka ya watoa huduma wa Kampuni za Simu za Mkononi."TCRA tutahakikisha tunawafikia wananchi wote kupata elimu ya utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema Mhandisi Salum.

Ameongeza kuwa Kampeni iko katika mikoa yote iliopo katika kanda ya Kaskazini.Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Makao Makuu Mabel Masasi amesema kuwa wananchi wameitikia kwa kujitokeza kwa wingi kuangalia namba vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole na wengi wamepata namba hizo na kufanya usajili kwa watoa huduma wa Kampuni za Simu za Mkononi.

Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata utaratibu wa vitambulisho vya Taifa.

Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Emelda Salum akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara wa Katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika katika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi ya Magugu ya usajili wa Laini za Simu kwa Alama za vidole.
 Afisa Habari Mwandamizi wa  Mamlaka ya a Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa maelezo kwa Wananchi namna ya kufuata utaratibu wa kuangalia namba ya kitambulisho cha Taifa kwa maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.
 Wananchi wakipata huduma ya usajili wa Laini za simu wakati Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.
 Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa maelezo kwa Wananchi wa Babati.
 Wananchi wakihudumiwa usajili wa Laini za simu wakati Kampeni ya Mnada kwa Mnada wa TCRA uliofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara. 
 Bibi zetu ambao wamezaliwa mapacha  wamejitokeza  kupata namba zao za vitambulisho vya Taifa  (NIDA) na kisha kujisajili kwa njia ya alama za vidole.
 Mwananchi akisajili laini ya simu kwa alama za vidole moja ya Kampuni ya huduma za Simu za Mkononi wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.
 

WAZIRI SIMBACHAWENE AKUTANA NA MKUU WA SHIRIKA LA CHAKULA DUNIANI (WFP)

0
0

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. George Simbachawene akifurahia jambo na Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani  (WFP) ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UN Nchini Tanzania,  Bwana Michael Dunford alipomtembelea Ofisini kwake  barabara ya Luthuli mapema hivi leo. Lengo la mazungumzo hayo ilikua ni kuhusu ushirikiano katika programu za Mazingira hususan mabadiliko ya tabianchi ambayo huathiri usalama wa chakula.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh. George Simbachawene akizungumza na Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (WFP)  ambaye ni pia ni Kaimu Mkurugenzi Mkazi UN Nchini Tanzania,  Bwana Michael Dunford,  alipomtembelea Waziri katika Ofisi yake Luthuli jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo kuhusiana na ushirikiano katika programu za Mazingira hususan mabadiliko ya tabia Nchi ambayo huathiri usalama wa chakula.

SERIKALI KUSHUGHULIKIA HARAKA CHANGAMOTO ZA WAWEKEZAJI

0
0
Wamiliki wa viwanda mkoa wa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji,Mhe Angela Kairuki wakati akifanya ziara ya kutembelea viwanda mkoani morogoro orogoro walalmikia sheria ya ushuru wa forodha ya East Africa sambamba na VAT  kukwamisha ukuaji wa viwanda  vya ndani hali inayo fanya washindwe kushindana na viwanda vya nje ya nchi.

Wamiliki hao wameeleza changamoto hizo mbele ya Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji,Mhe Angela Kairuki wakati akifanya ziara ya kutembelea viwanda mkoani Morogoro na kujua changamoto zao sambamba na namna gani ya kutatua.

Aidha badhi ya changamoto zilizo lalamikiwa ni pamoja na sheria ya ushuru ya Afrika Mashariki zinazo daiwa kutoa nafuu kwa bidhaa za nje hali inayopelekea viwanda vya ndani kushindwa kushindana  na wengine wakabainisha changamoto ya vat kuwa juu pamoja na malipo ya osha kuwa ni kikwazo kikubwa.

Hali hiyo wameeleza kuwa imewafanya wapate woga kwa wawekezaji kwa kuhofia kushindwa kufanya biashara nchini na kupelekea nchi kuendelea kuagiza nguo na vitu mbalimbali kutoka nje ya nchi.
 
kwa upande wake Waziri Kairuki amewahakikishia Wawekezaji hao kuwa Serikali imeyapokea yote na kujiandaa kuzifanyia kazi mapeMa changamoto zao,  ambapo ameahidi kushirikisha Mawaziri wote husika katika kupitia kanuni na miongozo mbali mbali ili kurekebisha
 Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji,Mhe Angela Kairuki akikagua moja ya kiwanda wakati akifanya ziara ya kutembelea viwanda mkoani morogoro.

THE 3RD ANNUAL HEALTH CONFERENCE HELD IN DODOMA FROM 23RD-25TH SEPTEMBER 2019


MFUMO WA JESHI LA POLISI 'ONE STOP CENTER' UMEISAIDIA JAMII KATIKA UWASILISHAJI TAARIFA ZA MATUKIO YA UKATILI WA KIJINSIA

0
0
MFUMO wa One stop centre unaoendeshwa na jeshi la polisi umeisaidia jamii ya watanzania hususani wakazi wa Ilala katika uwasilishaji wa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es salaam na kamishna msaidizi wa polisi Zuberi Chembera wakati wa kongamano la siku 16 dhidi ya ukatili wa kijinsia uliofanyika kwenye viwanja vya kampala vilivyopo katika maeneo ya Gongo la mboto.

Amesema kutokana na uanzishwaji wa kituo hicho kumekuwa na uelewa kwa wananchi katika ufatiliaji pamoja na utoaji wa taarifa za matukio ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia unaofanywa na baadhi ya watu ndani ya jamii.

"Matukio ya kikatili dhidi ya wanawake na watoto yamekuwa yakiongezeka kwa kadiri miji inavyopanuka na makazi kuongezeka ambapo baadhi ya wanajamii zikiwemo familia huishi kwa kuwekeana chuki, fitina ,wivu na imani mbalimbali za kidini," alisema Chembera

Chembera amesema kuwa jeshi la polisi limekuwa bega kwa bega na kikosi cha ulinzi shirikishi sambamba na wananchi katika kuhakikisha taarifa za matukio ya ukatili zinazowafikia zinachukuliwa hatua za kisheria.

Amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi  na wadau mbalimbali wameanzisha madawati ya kijinsia yapatayo 25 kimkoa katika kuwezesha taarifa kufika kwa haraka.

Aidha takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2018 matukio ya makosa ya ubakaji yalikuwa 926 ambapo mwaka 2019 yalifikia 725,huku makosa ya ulawiti kwa watoto yakiwa idadi ya 471 kwa mwaka 2018 na kuongezeka kwa idadi ya 571 mwaka 2019, upewaji ujauzito Watoto wa kike mwaka 2018 ilikuwa 54 ambapo mwaka 2019 kupungua kwa idadi ya 51.

Kwa upande wake diwani wa gongo la mboto Jackob Kissi alisema kuwa matendo ya unyanyasaji wa kijinsia yameongezeka kutokana na malezi mabaya ya baadhi ya familia.

Amesema changamoto za kijinsia dhidi ya watoto na wanawake vinachangiwa na mfumo dume kuchukua nafasi kutenda ama kufanya matendo mabaya ndani ya  familia hizo.

Naye kamishna msaidizi wa polisi mnadhimu namba moja katika mkoa wa kipolisi Ilala Janeth Stephano alisema wananchi washiriki kikamilifu katika utoaji wa taarifa hivyo wasiwaogope polisi katika kuwalipoti wahusika waovu.
Kamishina msaidizi wa polisi Zuberi Chembera ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye  kongamano la siku 16 za kuadhimisha ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto

CAMFED YAFUNGUA MKUTANO WAKE WA MWAKA

0
0
 Na Irene Mwidima, Yassir Simba - Globu ya Jamii.

Serikali imetoa wito kwa taasisi zake kama SIDO, Bodi ya mikopo ya elimu ya juu, taasisi za vijana na halmashauri kuweza kuona ni jinsi gani watashirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la kusimamia haki za mtoto wa kike nchini (CAMFED) ili kuwawezesha vijana hasa wasichana kupata fursa zinazotolewa na shirika hilo.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa, jijini Dar-es-salaam, Katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi na teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo, amesema kuwa mkutano huo utatoa fursa ya kupata mrejesho wa utekelezaji wa mipango mkakati wa CAMFED 2015 - 2029 pia kujadiliana na kupata maoni yatakayoboresha mpango mkakati wa shirika kwa miaka mitano ijayo.

Amesema kwamba ni matumaini yake kuwa taasisi za serikali pamoja na wadau wa mkutano huo watatumia fursa hizo kuishauri vyema CAMFED ili iweze kufanya vizuri zaidi katika mikakati ya kuwasaidia wasichana kupata fursa mbalimbali kama za ajira, elimu, mikopo ya vijana serikalini, mikopo ya elimu ya juu, elimu ya ufundi na ujuzi ili waweze kufikia malengo yao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa CAMFED, Lydia Wilbard ametoa wito kwa wazazi kushirikiana kikamilifu kuhakikisha suala la uwezeshaji wa elimu kwa watoto wa kike katika jamii zao na kukemea vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia miongoni mwa watoto wa kike katika jamii.

Pia amesema kuwa mtandao wa kusimamia haki za mtoto wa kike, unahamasisha ushiriki wa jamii katika kuboresha miundombinu ya kufundisha na kujifunza shuleni ikiwemo utoaji wa chakula, vifaa vya shule kwa wanafunzi, kuboresha miundombinu kama madawati, vitanda, ukarabati wa mabweni ya wasichana na nyumba za walimu, hii imechangia kuongeza uelewa kwa jamii katika utekelezaji wa waraka wa elimu bila malipo.

Ameongeza kwa kusema "Niwapongeze pia kwa kuanzisha elimu ya stadi za maisha katika shule za sekondari. Elimu hii imewezesha wanafunzi kujitambua, kuboresha ustawi wao na kufahamu, kuboresha mahudhurio na kupunguza utoro mashuleni".

Kaimu mwenyekiti wa CAMFED, Bw. Msigwa yeye azungumzia kuhusu hali halisi ya maendeleo ya CAMFED katika mikoa iliyofikiwa na shirika hilo na kueleza ya kwamba maendeleo ni mazuri na bado wanapiga vita vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, pia kuisaidia mikoa ambayo haijafikiwa na shirika hilo.
 Katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi na teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza katika mkutano wa Mwaka wa Shirika lisilo la kiserikali la kusimamia haki za mtoto wa kike nchini (CAMFED), uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es salaam. Picha zote na Al Hassan Muhidin.
 Baadhi ya waalikwa na wanafunzi waliohudhulia Mkutano huo, wakifatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa CAMFED, Lydia Wilbard.
Katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi na teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Bodi ya CAMFED, baada ya kumalizika kwa Mkutano huo.

NDALICHAKO AAGIZA UJENZI CHUO CHA UALIMU MPUGUSO KUKAMILIKA DESEMBA 30

0
0



KUSUASUA kwa ukamilishaji wa ujenzi wa baadhi ya miundombinu katika Chuo cha Ualimu Mpuguso, Mkoani Mbeya unaotekelezwa na mkandarasi Lukolo Construction Company umepelekea Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako kutoa agizo kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo kusimamia kwa karibu ukamilishaji wa kazi hiyo ili majengo hayo yaweze kutumiwa na walimu tarajali.

Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua mradi huo na kukuta ukitekelezwa kwa hali isiyoridhisha na katika baadhi ya maeneo kuwa chini ya kiwango.

Amesema mkandarasi huyi pamoja na kushindwa kukamilisha kazi yake kwa wakati aliepewa muda zaidi ili kukamilisha kazi hiyo lakini bado hajakamilisha hivyo kupelekea chuo kushindwa kutumia miundo mbinu na Serikali kuchelewa kufikia malengo yake ya uboreshaji na upanuzi wa Chuo hicho.

"Naelekeza mradi huu ukamilike ifikapo Desemba 30 tena kwa ubora kama ilivyopangwa hivyo Katibu Mkuu afuatilie kwa karibu kazi hii na makandarasi akishindwa kukamilisha mchukulie hatua," amesema Ndalichako

Kiongozi huyo alisema kwa mujibu wa makubaliano mapya baada ya kurudishwa kazini ni kukamilisha kazi hiyo Desemba 30, 2019 lakini hata sasa haonekani kuwepo eneo la mradi na hakuna kinachoendelea.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa mbeya Albert Chalamila amemweleza waziri kuwa mkandarasi huyo asipokamilisha kazi hiyo kwa muda uliopangwa atachukuliwa hatua na kuwa kama Mkoa watafuatilia pia utekelezaji wake kwa karibu.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Mbeya pia amemwomba waziri wa elimu kukipatia Chuo hicho gari ili kusaidia katika huduma mbalimbali jambo ambalo Waziri aliridhia na kusema kuwa tayari Wizara imenunua magari kwa ajili ya vyuo vya ualimu ambavyo havina huduma hiyo.

Nae mkuu wa chuo cha ualimu Mpuguso Dorothy Mhaiki ameishukuru Serikali kwa namna inavyoboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika chuo hicho na kuomba kukarabati maeneo mengine yaliyobakia kwa kuwa bado kuna uhitaji ikiwa ni pamoja na kusaidia kupatikana watumishi wa kudumu Upande wa walinzi na wapishi ili kupunguza gharama ya uendeshaji.

Ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu katika Chuo cha Ualimu Mpuguso ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu katika Chuo hicho ambao umegharimu kiasi cha sh bilioni 10 unaotekelezwa na serikali ya Tanzania na ile ya Canada.

Mradi huo umetekelezwa na kandarasi mbili Salem Construction Ltd ambao wamekalilisha kazi zao kwa ubora na majengo kuanza kutumika na Lukolo Construction Company ambao bado kazi yao haijakamilika.

Nyumba za walimu zilizojengwa katika Chuo cha Ualimu Mpuguso na kukamilika kwa ubora


 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce  Ndalichako akikagua mlango  uliowekwa katika moja ya jengo linalojengwa katika Chuo cha Ualimu Mpuguso ambao uko chini ya viwango.
 Waziri wa Elimu, Sayansi  na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Ualimu  Mpuguso Wilayani Rungwe Dorothy Mhaiki alipowasili chuoni hapo kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi unaotekelezea Chuoni hapo.
 Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila wakikagua moja ya jengo lenye madarasa linalojengwa katika Chuo cha Ualimu Mpuguso Tukuyu Mbeya.

KAGERA WAZINDUA MIAKA 58 YA UHURU KWA KUFANYA SHUGHULI ZA KIJAMII.

0
0
Anaandika Abdullatif  Yunus wa Michuzi TV.

Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru, na Miaka 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti kwa kufanya shughuli za Kijamii ikiwemo usafi wa Mazingira na Uchangiaji wa Damu, ikiwa ni kumbukumbu ya Sherehe ambazo hufanyika Desemba 9 ya kila Mwaka.

Shughuli hizo zimefanyika mapema Desemba 4, 2019 kwa kuishirikisha Kamati ya Ulinzi na Usalama, pamoja na watumishi na watendaji wa Serikali, shughuli hizo zikianzia Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  kuelekea Barabara ya Soko Kuu Bukoba, ambapo umefanyika Usafi kuzunguka maeneo yote ya Soko hilo, na kisha kuelekea Hospitali ya Rufaa Mkoa Kagera kwa ajili ya Uchangiaji Damu.

Akizungumza na wananchi na Wafanyabiashara Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amezidi kuwakumbusha umihimu wa kufanya Kazi kwa bidii na ubunifu ili kuongeza chachu ya Uchumi, kuwa wazalendo wa Taifa, na mara nyingi akizidi kuwakumbusha mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ndani ya Miaka minne Mkoani Kagera ikiwemo yaliyofanywa katika Sekta ya Afya, Elimu, Utalii, Kilimo na Miundo mbinu ikiwa ni pamoja na Ujenzi na Ukarabati wa Meli Mpya itayosaidia urahisi wa biashara zao.

Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameongoza kuwa watumishi wengine katika zoezi la kujitolea Uchangiaji Damu, lililofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kagera sambamba na kutembelea baadhi ya maeneo ya Hospitali  wodi ya akina mama, na kushuhudia ujenzi wa Wodi hiyo inayoendelea kujengwa.

Akiwa Hispitalini hapo amewasihi bodaboda kuendelea kufuata na kutii sheria za barabarani kwa kufanya hivyo watasaidia kupunguza ajali ambazo hupelekea mahitaji makubwa ya Damu.

 Pichani shughuli za Usafi zikiendelea maeneo mbali mbali ya Soko Kuu la Bukoba katika uzinduzi wa Wiki ya Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru kwa Mkoa Kagera.
 Pichani Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akionekana kushiriki zoezi la Uchangiaji Damu, mapema Desemba 04, 2019 katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru, 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kimkoa.
Pichani Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza na Wananchi pamoja na wafanyabiashara Mara baada ya kumalizika shughuli ya Usafi katika uzinduzi wa Wiki ya Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru kwa Mkoa Kagera
 

WAFANYABIASHARA, WAWEKEZAJI MKOANI MOROGORO WAWASILISHA CHANGAMOTO ZAO KWA MAWAZIRI.

0
0

Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara mbalimbali wakiwasili ukumbini kwa ajili ya Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji kwa lengo la kusikiliza changamoto zao uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Glonency Mkoani Morogoro tarehe 12 Disemba, 2019. Kushoto ni Mkuu wa mkoa huo Mhe. Loata Ole Sanare.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (wa kwanza kulia) wakiwa pamoja na Manaibu Waziri wakipata maelezo kutoka kwa Sajenti Esther Mbugura kuhusiana na vifaa vinavyotumika kwa ajili ya kuzimia moto wakati wa Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji Morogoro.


Baadhi ya Manaibu Waziri na Mawaziri wa Wizara walioshiriki katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji wakiwasikiliza wachangiaji mbalimbali walioalikwa katika mkutanouliolenga kusikiliza changamoto za Wafanyabiashra uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro tarehe 12 Disemba, 2019.
Baadhi ya Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali wakifuatilia majadiliano ya Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji uliolenga kusikiliza na kutatua changamoto zao katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro
Afisa Masoko wa Royal Agri Company, Elizabeth Priscus akichangia hoja ya kuwawezesha Wahitimu kujihusisha katika shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali mkoani Morogoro katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji uliolenga kusikiliza changamoto zao katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency.
Waziri wa Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki wakiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole Sanare wakiwa katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji uliolenga kusikiliza changamoto zao katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji wakifuatilia majadiliano ya Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji uliolenga kusikiliza na kutatua changamoto zao katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro.
Mjumbe wa TCCIA, Anthony Fuime akichangia hoja kuhusu umuhimu wa kuwa na mipango inayotekelezeka katika ngazi ya Halmashauri wakati wa Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji uliolenga kusikiliza changamoto zao katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency.


Baadhi ya Watendaji wakuu wa Serikali wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuingia ukumbini kwa ajili ya Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji kwa lengo la kusikiliza changamoto zao uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro.



(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

KATIBU MKUU WA CCM DKT. BASHIRU AHITIMISHA ZIARA NA WAZEE WA KISIWA CHA PEMBA

0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally leo tarehe 04 Desemba, 2019 amehitimisha ziara yake ya siku tisa Visiwa vya Unguja na Pemba kwa kuzungumza na wazee wa Pemba.

Katibu Mkuu ameitumia fursa hiyo kusikiliza maoni ya wazee, ushauri, mapendekezo, na changamoto mbalimbali katika kuboresha zaidi huduma kwa wananchi na kufahamu ni kwa kiasi gani wazee wameridhika na mwenendo wa serikali zote mbili za Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais  Dkt. Ali Mohamed Shein na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Wazee hao wa Pemba katika mazungumzo hayo kwa kauli moja, wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwa ufanisi wao wa kusogeza karibu huduma za jamii pamoja na  kudumisha Muungano wakati wote.

"Sisi tunampongeza sana Rais wetu Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya, kazi tuliompatia anaifanya vizuri sana na tunasema kwa  kauli moja, tunamtaka aendelee hivo, Pia tunamshukuru sana Rais wetu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kudumisha umoja wetu, upendo, amani na utulivu katika kipindi hiki cha miaka tisa ya uongozi wake hakika tunafarijika sana". Mzee Hamis Ali Mzee.

Katibu Mkuu akizungumza ma wazee hao, ameeleza umuhimu wa kuwa karibu na wazee wetu ambao muda mrefu wa maisha yao wameutumia katika ujenzi wa Nchi na Taifa tulilonalo sasa.

"Viongozi wenzangu ni lazima tuwe na utaratibu wa kukutana na wazee wetu, wazee hawa wana mambo mazuri ya kujifunza kwao katika kipindi hiki ambacho bado wananguvu za kuzungumza na kufundisha ili tuzidi kupata maarifa mengi walionayo." Katibu Mkuu ameeleza

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu  amezuru  kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt. Omary Ali Juma aliyefariki mwaka tarehe 04 Julai,  2001.

Dkt. Bashiru ametumia wasaa huo kueleza kwa ufupi wasifu wa hayati Dkt. Omari ambapo amesema, 

"Dkt. Omari Ali Juma alisimamia dhana ya kuishi pamoja kwa upendo, amani, kuvumiliana na kuhimiza maendeleo, nakumbuka pia alivyosimamia kwa uthabiti kampeni ya mazingira akiwa Makamu wa Rais." Ameeleza

"Ndani ya Chama Chetu, viongozi na wanachama wote waliotoa mchango wao katika kukijenga Chama tutaendelea kuwaenzi na vijana ni lazima mpangilie maisha yenu vizuri ili mtoe mchango mkubwa zaidi kwa Taifa letu." Ameongeza.

Aidha, Katibu Mkuu amewatembelea wazee na wagonjwa mbalimbali Mkoa wa Kusini Pemba wakiwemo Mzee Khalidi Ali Khalid na Mzee Ali Suleimani Makasi.

Ziara hii ya siku tisa ambayo imehitishwa leo  kisiwani Pemba imelenga katika kuimarisha Uhai wa Chama na Jumuiya zake na kuimarisha mahusiano baina ya viongozi wa Chama na Serikali pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015 - 2020.




WAKIMBIZI KUREJEA MAKWAO NI JAMBO LA HIARI

0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IMEELEZWA kuwa haki ya wakimbizi kurejea nchini mwao au kubaki kwa wakimbizi waishio nchini wakitokea Burundi itaendelea kuwepo na kuwa la hiari na hiyo ni pamoja na kupata  huduma za msingi ikiwepo ulinzi kwa wakimbizi watakaobakia nchini na kwa wale watakaorejea nchini mwao watahakikishiwa usalama wa kurejea nchini mwao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George Okoth Obbo amesema, kupitia kikao cha siku tatu cha mkutano wa 21 wa Tripartite commission kilichowakutanisha na Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Kangi Lugola na wawakilishi kutoka Burundi na Shirika linalohusika na masuala ya wakimbizi duniani (UNHCR) walipata wakati mzuri wa kujadili masuala yahusuyo wakimbizi ikiwemo kuheshimu uhuru wa wakimbizi hao kubaki au kurejea makwao.

"Wakimbizi kurejea Burundi ni hiari na watakaoamua  kurejea katika nchi zao tutashirikiana nao kwa Kuhakikisha wanarejea nchini mwao salama kabisa,  tutawafikisha kwenye mipaka ya nchi zao na wale watakao endelea kubaki nchini UNHCR kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania na Burundi tutaendelea kushirikiana nao kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yote ya msingi" ameeleza Okoth -Obbo.

Pia amesema kuwa kupitia mkutano huo wamekubalina kuwa Tanzania iendele kutoa taarifa za wakimbizi hasa vyeti vya kuzaliwa, vifo na vyeti vya wakimbizi katika shirika la UNHCR.

"Taarifa zinazowahusu wakimbizi ni muhimu sana katika kuisaidia kutoa mahitaji ya msingi ni vyema Tanzania ikaendelea kutoa taarifa kupitia nyaraka mbalimbali zinazoonesha  ndoa, uzazi na vifo"

Amesema kuwa UNHCR Tanzania inahitaji dola za kimarekani 126 na kueleza kuwa wadau mbalimbali wamekuwa wakishiriki kwa namna moja au nyingine kwa Kuhakikisha wakimbizi hao wanapata huduma muhimu hasa zile za kijamii.

Okoth amesema kuwa  baada ya mkutano huo alitembelea kambi za Nduta na Mtendeli zilizopo Mkoani Kigoma ambapo alipata wasaa wa kuzungumza na wakimbizi pamoja na viongozi na washiriki wanaohudumia wakimbizi katika nchi hizo.

" Niipongeze Serikali ya Tanzania na wananchi wake kwa kubeba jukumu la kubeba wakimbizi wapatao 246,000 katika nchi yao na katika kambi nilizopita Kigoma nilipata kushuhudia wakimbizi wakijiandikisha kwa hiari ili wapate kurejea makwao." Ameeleza.

Ikumbukwe kuwa idadi kubwa ya wakimbizi wanatoka katika nchi za Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo huku 87 ya wakimbizi hao wakiishi katika kambi tatu zilizopo Mkoani Kigoma.
 Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George Okoth Obbo akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),jijini Dar  kuhusu mambo mbalimbali yaliyojadiliwa kwenye kikao chao cha siku tatu kilichowakutanisha Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Mhe.Kangi Lugola,Wawakilishi kutoka Burundi na Shirika linalohusika na masuala ya wakimbizi Duniani (UNHCR),namna walivyojadili  masuala yahusuyo wakimbizi ikiwemo kuheshimu uhuru wa wakimbizi hao kubaki au kurejea makwao. 
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumza na  Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George Okoth Obbo,jana jijini Dar es Salaam.

Mvua Zinazoendelea Kunyesha Nchini Zasababisha Mafuriko Kwa Wakazi Wa Tabora

0
0
Na  Editha Edward -Tabora

Mvua Zinazoendelea Kunyesha nchini zimesababisha Mafuriko Kwa Wakazi Tabora wanaoishi katika mtaa wa Mwalitani (Freemason) Kata Ya mpera manispaa ya Tabora ambapo mvua hiyo imeanza kunyesha usiku wa kuamkia Leo ambapo imepelekea wakazi wa mtaa huo kushindwa kulala usiku kucha na nyumba zao kujaa maji

Jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Tabora lilifika katika eneo hili na Kuanza kuwokoa baadhi ya watu walioshindwa kuvuka maji yaliyokuwa yamewazingira

Aidha Mkuu wa mkoa Agrrey Mwanri ambaye pia alifika katika tukio hilo usiku huo amewaomba wananchi waliopata maafa hayo wasirudi katika nyumba zao zilizojaa maji hadi pale oparesheni itakapokamilika.
PichaniJeshi la zimamoto na uokoaji wakiokoa wananchi ambao nyumba zao zimefurikwa na maji usiku wa kuamkia leo.
Nyumba zilizofikwa na mafuriko mtaa wa Mwalitani maarufu kama Freemason Kata ya mpera.
Pichani ni mtaa wa Mwalitani uliokumbwa na mafuriko
Mvua Zinazoendelea Kunyesha Nchini Zasababisha Mafuriko Kwa Wakazi Wa Tabora

MKAKATI WA KITUO MAHIRI CHA RASILIMALI ZA MAJI WAPITIWA

0
0


 Katibu Mkuu mstaafu na mwenyekiti wa kikao Mhandisi Mbogo Futakamba, kushoto akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali za Maji, Wizara ya Maji  Dkt. George Lugomela wakifuatilia uwasilishaji wa Mkakati wa Kituo Mahiri cha Rasilimali za Maji (Water Resources Centre of Excellence-WRCE).
Mtaalam Bw. Vincent Ssebuggwano akiwasilisha Mpango Mkakati wa Kituo Mahiri cha Rasilimali za Maji kwa wadau wa rasilimali za maji nchini
Wataalam na wadau wa Rasilimali za Maji wakifanya mapitio ya Mpango Mkakati wa Kituo Mahiri cha Rasilimali za Maji (Water Resources Centre of Excellence-WRCE), kilichoanzishwa na Wizara ya Maji. WRCE itahusika, pamoja na mengine, masuala ya kitaalam na utafiti wa kina katika sekta ya maji nchini.

CGP KASIKE ATETA NA MAOFISA MAGEREZA WAANDAMIZI MKOANI MWANZA AWATAKA KUONGEZA UWAJIBIKAJI NDANI YA JESHI HILO

0
0

Kamishna Jenerali wa Magerezanchini, CGP – Phaustine Kasike(kushoto vazi la kiraia) akiteta jambo na Mkuu wa Magereza Mkoani Mwanza, SACP. Hamza Hamza.Picha zote na Jeshi la Magereza
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP –  Phaustine Kasike akisisitiza jambo wakati akizungumza na  Maafisa waandamizi wa Magereza Mkoani Mwanza alipowasili  leo Desemba 4, 2019 akitokea Mkoani Geita kwa shughuli za kikazi.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza wakifuatilia mazungumzo ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike(hayupo pichani) leo Desemba 4, 2019 alipowasili jijini Mwanza akitokea Mkoani Geita kwa shughuli za kikazi.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akisalimiana na Maafisa waandamizi wa Magereza Mkoani Mwanza alipowasili  leo Desemba 4, 2019 akitokea Mkoani Geita kwa shughuli za kikazi.


TUMEAMUA UJENZI WA MELI MPYA NA CHELEZO ZIWA VICTORIA NI UKOMBOZI WA WENGI AFRIKA MASHARIKI

MAFINGA ACADEMY KINARA WA MAGOLI WA ASAS SUPER LEAGUE 2019/2020 MZUNGUKO WA TATU WA NANE BORA

0
0

Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwasalimia wa wachezaji wa timu ya IUO wakati wa mchezo katika yao dhidi ya Irole fc(PICHA KUTOKA MAKTABA)
Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiongea wa wachezaji wa timu ya IUO wakati wa mchezo katika yao dhidi ya Irole fc(PICHA KUTOKA MAKTABA)




NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


Asas Super League 2019/2020 hatua nane bora imemaliza hatua ya mzunguko wa tatu kwa timu ya mafinga academy kuongoza kundi B na Isiman Fc kuongoza kundi A huku timu ya mafinga academy wakiongoza kwa kufunga magoli kumi.


Kufuatia kutamatika kwa mzunguko wa tatu wa Asas Super League 2019/2020 kundi Alinaongozwa na timu ya Isimani fc yenye alama saba na magoli ya kufunga matano huku ikiwa imefungwa goli moja tu katika michezo mitatu ya awali.

Kidamali fc na kalinga fc wanalinga alama kwa kila timu kwa kuwa na alama nne huku wakitofautiana kwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa huku Kidamali fc akiwa na magoli ya kufunga matano na wamefungwa magoli mawili tu na timu ya kalinga wakiwa wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli manne.

Timu ya Young Stars wakiwa wanaburuza mkia kwenye kundi hilo wakiwa wana alama moja huku wakiwa wamefungwa jumla ya magoli sita katika michezo mitatu waliyocheza katika mzunguko wa kwanza wa Asas Super League 2019/2020

Kwa upande wa kundi B,timu ya Mafinga Academy wanaongoza kundi B wakiwa wamekusanya jumla ya alama tisa huku wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja huku wakiwa wamefunga jumla ya magoli kumi na kufungwa magoli mawili kwenye michezo mitatu ya awali ya kundi B.

Timu ya Mkimbizi fc,Nzihi fc na Irole Fc zote zimekusanya jumla ya alama mbili kwenye michezo mitatu huku wakiwa wametofautiana kwenye magoli ya kufunga na kufungwa,ukiangalia Mkimbizi Fc wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli matatu,Nzihi fc wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli manne na Irole Fc wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli saba na ndio timu inayongoza kwa kufungwa magoli mengi kuliko timu yeyote ile kwenye hatua ya nane bora.

Asas Super League 2019/2020 itaendelea siku ya ijumaa tarehe sita mwenzi wa kumi na mbili kati Kidamali Fc na Isimani fc mchezo utachezwa katika uwanja wa Kidamali na ikumbukwe kuwa kwenye nmchezo wa awali timu ya Isimani ilishinda kwa goli moja bila.
Viewing all 109572 articles
Browse latest View live




Latest Images