Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

MAHAKAMA KUTOA UAMUZI WA KUPOKEA KILELEZO CHA CD KESI YA ZITTO KABWE KESHO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu kesho Desema 4,2019 inatarajia kutoa uamuzi wa kama ipokee kielelezo cha CD iliyohifadhi video iliyorekodiwa wakati wa mkutano wa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe au la.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa utetezi katika kesi hiyo ya uchochezi dhidi ya Zitto inayounguruma mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kupinga kupokelewa kwa kielelezo hicho kwa madai kuwa  shahidi anayepataka kutoa kielelezo hicho mahakamani hajaeleza ni namna gani video hiyo ilirekodiwa.

Akiwasilisha hoja zake za kupinga, wakili wa utetezi, Jebra Kambole amedai kuwa nyaraka inayotakiwa kutolewa na Sajent James ambaue ni shahidi wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo ni ya kielektroniki hivyo inatakiwa kufuata maelekezo ya sheria yanayohusu utoaji wa kielelezo cha kielektroniki.

Amedai CD ambayo inatakiwa kupokelewa mahakamani haijarekodiwa na shahidi huyo hivyo ameshindwa kukithi matakwa ya kifungu cha 18 (2) (a) cha sheria hiyo ya kielektroniki na kwamba shahidi huyo ameshindwa kuonesha mashine iliyotumika kurekodi na kama ilikuwa inafanya kazi vizuri hivyo ameiomba mahakamani isipokee kielelezo hicho.

Akipinga hoja hizo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga amekiri kuwa kielelezo ambacho shahidi wao anataka kipokelewe na kitumike kama ushahidi mahakamani ni cha kielektroniki.

Amedai kitu ambacho shahidi amekuja kukielezea mahakamani hapo ni kuhusu uchunguzi walioufanya katika video kama ni halisi au la na kwamba hakuna kifungu ambacho upande wa utetezi wamekielezea  kwamba aliyerekodi video ndio anayepaswa kutoa kielelezo hicho.

Kufuatia mabishano hayo, Hakimu Shaidi amesema atatoa uamuzi kesho kama kielelezo hicho kipokelewe au la.

Mapema,  shahidi wa 14 ambaye ni Mtaalamu wa Uchunguzi wa Kisayansi kutoka Makao Makuu ya Polisi, Sajent James (52) alidai alipata barua iliyoambatanishwa na CD  kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ikielekeza kufanya uchunguzi wa picha iliyomo kwenye kielelezo hicho.

Alidai barua hiyo ilipewa namba OB/IR/8291/2018 ya Oktoba 10,2018 ililetwa na Koplo Faraji na baada ya kuipokea,  mkuu wake wa kazi, SP Tumaini alimpa jukumu la kufanya uchunguzi ambapo baada ya uchunguzi aligundua kuwa video iliyohifadhiwa kwenye CD ni halisi hivyo aliandaa hati kwa mujibu wa kifungu cha 202 (1) cha Sheria ya Mwendendo wa Makosa ya Jinai (CPA) na katika ripoti ya uchunguzi wa kielelezo hicho aliandika Desemba 6, 2018 na kuiomba mahakamani ikipokee kielelezo hicho na kioneshwe kilichomo ndani ya CD.

Katika kesi hiyo, Zitto anadaiwa Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliyofanyika katika Makao Mkuu ya ofisi ya Chama cha ACT Wazalendo alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.

Inadaiwa alisema " Watu ambao walikuwa ni majeruhi katika tukio la mapambano baina ya wananchi na polisi wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya Nguruka, Polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospitali kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua".

CCM ZANZIBAR YAMJIBU MAALIM SEIF

$
0
0

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao,imelitaka Jeshi la Polisi kumuhoji,kumchunguza na kumchukulia hatua za kisheria Mshauri Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo Seif Sharif Hamad kwa kauli zake za uchochezi alizotoa kwa kuwahamasisha wafuasi wake watumie silaha za jadi kuanzisha vurugu visiwani hapa.

Hatua hiyo inatokana na kiongozi huyo kutoa matamshi mbele ya vyombo vya habari kwa kuwataka viongozi na wanachama wa ngazi zote za chama chake kwa maeneo ya mijini na vijijini kwa upande wa Unguja,Pemba kuzilinda ofisi zote za chama chao na kutoruhusu
kuchukuliwa kwa ofisi hizo.

Katika mkutano huo ambao aliufanya juzi kwenye ofisi ya chama hicho mjini Unguja Maalim Seif alisema wamevumilia vya kutosha na kwamba sasa wanasema basi kutokana na kuwa ni muda mrefu wamevumilia kutokana na maslahi ya nchi lakini wameona wenzao hawako tayari
kuilinda amani.

Maalim Seif alisema wako tayari kumwaga mboga wenzao wakimwaga mchuzi na kwamba alisema chama cha CUF kwa upande wa Pemba kimeanza kujaribu kutaka kuvamia ofisi za ACT-Wazalendo kwa lengo la kuzichukua na kuzifanya ofisi za chama chao kwa madai ni ofisi zao.

Akizungumza jana na vyombo vya habari Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu Taifa ya CCM,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao,alisema kutokana na kauli za Hamad ambaye aliyotoa katika vyombo vya habari ni lazima jeshi la Polisi lichukue hatua za haraka za kumthibiti kiongozi huyo kabla nchi haijaingia katika machafuko.

Katibu huyo amelaani taarifa hiyo ya Maalim Seif kuwa inalenga kuvuruga hali ya amani na mshikamano wa wananchi na kuirejesha Zanzibar katika machafuko ya kisiasa.

Aliongeza kuwa katika taarifa hiyo ya Maalim Seif alimtaja Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru Ally kuwa moja ya mikutano yake ya ndani iliwahamasisha viongozi wa CCM kuratibu mipango ya vurugu,jambo ambalo si kweli kwani kiongozi huyo alifanya ziara yake kwa lengo la kuimarisha chama katika kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020.

Pia,Katibu huyo alisema taarifa alizotoa Maalim Seif za kumtuhumu Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru kuwa ziara yake za visiwani Zanzibar imelenga kuhamasisha Vurugu na kwamba jambo hilo ni la upotoshaji na si za si za kweli.

Alisema Maalim Seif ni mwanasiasa aliyetawaliwa na ubinafsi pamoja na ukatili wa kupindukia kutokana na kuwa furaha yake ni kuona damu za wananchi wa Zanzibar zinamwagika bila hatia na kwamba ndio maana kila anapoona hali ya amani inaimarika visiwani hapa yeye anaanzisha vurugu kwa kusudi.

Katibu Catherine, alimtaja Maalim Seif kuwa ni bingwa wa migogoro toka wakati wa Rais wa awamu ya pili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambapo Maalim Seif alitengeneza mgogoro akiwa ndani ya CCM na
hatimaye akatimuliwa.

Aliongeza kuwa maisha ya kisiasa ya kiongozi huyo wa upinzani Maalim Seif yametawaliwa na usaliti,uongo,chuki binafsi na hata katika uchaguzi wa kwanza Tanzania uliofanyika katika kipindi cha mwaka 1995, aliibuka na kudai ameshinda wakati akijua hakuwa
na uwezo huo.

Katika maelezo yake Catherine, alisema Maalim Seif aseme ukweli wa kuwa ameogopa ujio wa Katibu Mkuu Dk.Bashiru Zanzibar kuja kufunga mitambo ya kufanikisha uchaguzi wa mwaka 2020.

Alisema kuwa hakuna wa kuizuia CCM kushinda katika uchaguzi huo kwani tayari imemaliza kazi na kwa sasa inajipanga kwa ushindi mkubwa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

Pia,alisema ushindi huo utatokana na Utekekelezaji Mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, alivyoimarisha Nyanja mbalimbali za kiuchumi,kisiasa,kijamii na kimaendeleo.

Katibu huyo Catherine, alisema Dk.Shein amekuwa ni kiongozi wa mfano ambaye ni mwadilifu, mchapakazi, mwenye hekima na shujaa wa kuasisi maendeleo.

“ Maalim Seif eti anasema kuwa Dk.Shein anawagawa wananchi hilo si kweli kwani Rais wetu amefanya mambo mengi ya maendeleo yanayowanufaisha wananchi wote hata huyo Maalim Seif anayebeza na kumtukana Rais wetu pia naye ananufaika na maendeleo haya,”
alisema Catherine.

Hata hivyo Katibu Catherine alimuonya Maalim Seif, alihamishie mgogoro wa chama cha ACT-wazalendo na CUF akaupeleka CCM kwani taasisi anayopambana nayo si ya kiwango chake.

Pia alihoji taarifa aliyotoa ambayo alidai kuwa takwimu za ACT- Wazalendo kukubalika Zanzibar kwa asilimia 64 na CCM kukubalika kwa asilimi 34, kuwa zimefanywa na taasisi gani kupitia vyanzo gani vya uhakika kwani hizo ni takwimu za uongo zinazotumiwa na Maalim Seif.

Alisema kwa takwimu hizo ambazo hazikuzingatia uwepo wa vyama vingine vya kisiasa ambavyo vina usajili na wanachama nchini kama vile ADA,TADEA, TLP,CHADEMA na CUF ni takwimu za kupuuzwa.

Catherine alisema kila siku zikienda Maalim Seif anaendelea kufilisika kisiasa ndio maana akapewa nafasi ya ushauri ndani ya Chama Cha ACT-Wazalendo kinachojipanga kushindana na CCM huku Zanzibar hakina hata balozi wala Diwani.

Pamoja na hayo Katibu huyo, aliwambia wafuasi wa Maalim Seif kuwa makini na kiongozi huyo ambaye amekisaliti chama alichokianzisha cha CUF hivyo hawezi kushindwa kusaliti ACT-Wazalendo.

Catherine alisema maalim Seif hana sifa za uongozi kwani uongozi ni wito na unatoka kwa mwenyezi mungu lakini kiongozi huyo amekuwa akilazimisha kupata nafasi hiyo kupitia njia haramu.

Alisema siasa za maji taka zimepitwa na wakati na viongozi wa kisiasa wanaondelea na siasa hizo watadhibitiwa na Vyombo vya Dola.

Catherine alisema CCM itaendelea kushindana kwa sera,hoja,na utendaji wa kazi na sio marumbano na porojo kwani wananchi wanahitaji maisha bora.

“Dk.Shein ametekeleza Ilani ya CCM kwa kununua boti za kisasa,majengo ya kisasa, huduma za afya bure,elimu bure, barabara za lami zipo kila sehemu na mengine mengi …lakini
ukimuuliza Maalim  Seif kafanya nini hata kisima kimoja cha maji hajachimba,”alisema.

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao akizungumza na Vyombo vya Habari Ofisini kwake Kisiwandui Zanzibar.

BMT YAWAFUNGIA MWAKA MMOJA WAANDAAJI WA KIGAMBONI INTERNATIONAL MARATHON

$
0
0
Na Zainab  Nyamka, Globu ya Jamii

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeifungia mbio ya “Kigamboni International Marathon” kwa muda wa mwaka mmoja, baada ya kufanyika kwa mbio hiyo tarehe 1 Disemba, 2019 bila kufuata Sheria na kanuni za uendeshaji wa mbio za Marathoni.

Muandaaji wa mbio hizo anatakiwa kuhakikisha anakamilisha kulipa zawadi alizotakiwa kutoa katika mbio hizo kabla ya tarehe 12 Disemba, 2019.

BMT kupitia Kaimu Katibu Mkuu, Neema Msitha, amesema kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la uandaaji za Marathoni pamoja na mbio nyingine za barabarani nchini, ambapo zimekuwa na mchango mkubwa sana katika kuendeleza mchezo wa riadha pamoja na kukuza uchumi nchini.

Amesema, hata hivyo pamoja na mchango mkubwa; kumekuwa na changamoto nyingi za uendeshaji wa mbio hizo zikiwemo baadhi ya waandaji kuandaa mbio bila kusajiliwa, kukosa ulinzi barabarani (traffic control), kukosekana kwa huduma za afya (ambulances).

Msitha amesema pia mbio hizo zimekuwa zinakosa huduma ya maji ya kunywa katika vituo vya kukimbilia pamoja na baadhi ya wandaaji kushindwa kulipa zawadi kwa washindi, kukosa wataalam/wasimamizi wenye weledi, jambo ambalo linapelekea kuwepo kwa udanganyifu.

Ameeleza, kushindwa kukamilisha taratibu zote zimekuwa zinasababisha Changamoto ambazo zimepelekea mgogoro mkubwa baina ya wandaaji, washiriki wa mbio hizo (wakimbiaji) pamoja na wadau wengine wa mchezo wa riadha.

BMT wasema, kutokana na kuwepo kwa changamoto hizo kuanzia tarehe 1 Januari 2020, vibali vyote vya kuendesha mbio za Marathoni na mbio nyingine za Barabarani ngazi ya Taifa, mkoa na wilaya vitatolewa na Baraza la Michezo la Taifa baada ya kupitiwa na Shirikisho la Riadha Tanzania. 

Vibali hivyo vitatolewa baada ya Baraza kujiridhisha kuwa muandaaji wa mbio hizo amekidhi matakwa ya uendeshaji wa mbio hizo.

Aidha BMT limezielekeza mamlaka za usimamizi wa Michezo ngazi ya Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa hamna mbio yoyote ya barabarani inafanyika bila kibali cha BMT.

Kwa mujibu wa Sheria ya BMT waandaji wote wa mbio hizo wanapaswa kulipia asilimia moja (1%) ya tiketi/viingilio vya mbio, kwenda katika mfuko wa maendeleo ya Michezo BMT,Vilevile kuanzia leo tarehe 3 Disemba 2019.

WAZIRI MKUU AAGIZA UJENZI WA MACHINJIO UKAMILIKE MWEZI HUU MWISHONI KAMA ILIVYOAMRIWA NA RAIS MAGUFULI

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka mkandarasi anayejenga machinjio ya kisasa ya Vingunguti jijini Dar es Salaam ahakikishe kwamba anakamilisha ujenzi huo mwishoni mwa mwezi huu kama alivyoamriwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo leo (Jumanne, Desemba 3, 2019), Mheshimiwa Majaliwa amesema amefurahishwa na hatua ya mkandarasi huyo ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ya kuongeza idadi ya watalaam na mafundi ili kuhakikisha kwamba kazi hiyo inafanyika haraka na kukamilika kwa wakati ulioamriwa na Rais Magufuli yaani Desemba 30, mwaka huu.

Amesema amefurahi pia kuona kwamba mkandarasi huyo ameamua kufanya kazi usiku na mchana, hatua ambayo imeongeza kasi ya ujenzi huo na anaamini kuwa kazi hiyo itakamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Majaliwa amemtaka  Mshauri Mwelekezi wa mradi huo ambaye ni M/SCONS AFRIKA LIMITED na FB Consultant wa Dar es Salaam  asimamamie kwa karibu ili  kujiridhisha  kuwa maelekezo yote yaliyopo kwenye michoro ya ujenzi huo yanazingatiwa na mkandarasi.

Amesema Serikali imeamua kujenga machinjio hayo ya kisasa ya Vingunguti baada ya kugundua kwamba wafanyabiashara wa mifugo na mazao yake  katika machinjio hayo, walikuwa wakifanya kazi zao kwenye mazingira duni na  kwamba nyama iliyokuwa ikitoka kwenye machinjio hayo ilikuwa haikubaliki kwenye soko la nje ya nchi.

“Uamuazi wa Serikali kujenga machinjio haya, utaifanya nyama inayotoka hapa ikubalike kwenye masoko ya nje ya nchi, hatua ambayo itaongeza mzunguko wa fedha kwenye eneo hili wakati Serikali na Manispaa watanufaika kwani kutakuwa na ongezeko la makusanyo ya kodi,” aliongeza Mheshimiwa Majaliwa.

Waziri Mkuu pia ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Manispaa ya Ilala wafanye mazungumzo na uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) ili ijengwe reli ya mchepuko kutoka reli ya kati kwenda kwenye machinjio ya Vingunguti ili mifugo iingizwe moja kwa moja kwenye machinjio hayo badala ya kuteremshiwa Pugu halafu ikapelekwa  kwa magari.

Amewahakikishia wafanyabiashara wote wanaoendesha shughuli zao kwenye machinjio hayo kuwa ujenzi wa machinjio ya kisasa  ya Vingunguti hautawafanya wapoteze fusa zao za biashara au kuajiriwa kwenye eneo hilo kwani  machinjio hayo yatafungua fursa zaidi za biashara na ajira kwao.

Amewaagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala wahakikishe kwamba wanaushirikisha uongozi wa wafanyabiashara wa mifugo na mazao yake wa Vingunguti ili wanachama wao wenye sifa za kuajiriwa, waajiriwe na pia wawaandalie mazingira ya kufanya biashara mbalimbali karibu na machinjio hayo.

Akizungumzia soko na bei duni ya ngozi za mifugo nchini, Waziri Mkuu amekemea tabia ya wafugaji ya kuweka alama kwenye ngozi za mifugo yao hasa ng’ombe kwani kufanya hivyo kunashusha thamani ya ngozi za Tanzania na badala yake amewataka waweke alama za hereni kwenye masikio ya mifugo yao ili kulinda ubora wa ngozi za mifugo yao.

Amesema Serikali tayari imekwishampata mwekezaji kutoka Misri ambaye amekubali kuwekeza kwenye kiwanda cha ngozi cha Mwanza hatua ambayo italihakikishia Taifa soko la ngozi.

Mapema, akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri amesema ujenzi wa machinjio hayo ulianza Julai 8, mwaka huu na mkandarasi alitakiwa akamilishe ujenzi huo ifikapo  Januari 6, 2021. Amesema kufuatia agizo la Rais Magufuli alilolitoa Septemba 16, mwaka huu, ujenzi huo unatakiwa ukamilike ndani ya miezi mitatu yaani ifikapo Desemba 31, 2019.

Bw. Shauri amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo itagharimu sh.  12, 498,916,063.00 ambapo sh. 8,528,486,470.00 ni ruzuku kutoka Serikali Kuu na sh. 3, 970,429,593.00 zimetokana na mapato ya ndani ya Halmashauri na kwamba ujenzi wa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 60.

Akisoma risala  ya Ushirika wa Wafanyabiashara ya Mifugo na Mazao yake  wa Vingunguti (UWAMIVI), Mwenyekiti wao, Bw. Joel Meshaki aliiomba Serikali  iwaandalie wafanyabiashara hao eneo mbadala la kufanyia shughuli zao  ili  ajira yao isipotee.

Alipendekeza kwa Waziri Mkuu maeneo matatu yaliyoko karibu  eneo hilo, ambayo yangewafaa wafanyabiashara hao wakati watakapoondoka  kwenye maeneo yao sasa yanapojengwa machinjio ya kisasa kuwa ni Dampo la zamani ambalo kwa sasa halitumiki,  eneo la Wizara ya Kilimo ambalo kwa sasa ni sehemu ndogo tu inayotumika  na jengo la Kilimo ambalo kwa sasa linatumika kama ghala.

Alisema idadi ya mifugo inayochinjwa katika machinjio hayo kwa sasa ni ng’ombe 550 hadi 600 kwa siku za kawaida na siku za sikukuu ni ng’ombe 1,000 hadi 1,500. “Halmashauri yetu ya Ilala  hukusanya  zaidi ya sh.  milioni 118 kwa mwezi  wakati Serikali Kuu hukusanya milioni 117 kila mwezi,” alisema Meshaki.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kukagua Machinjio ya zamani yaliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, baada ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa Vingunguti, Desemba 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tanzania imepiga hatua katika kuwajumuisha watu wenye ulemavu - Mbunge Amina Mollel

KONGAMANO LA TATU LA KIMATAIFA LA KISWAHILI KUFANYIKA ZANZIBAR

TASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE YAZIDI KUICHANJA MBUGA

WANANCHI VIJIJINI RUKSA KULIPIA UMEME KWA KUDUNDULIZA

$
0
0
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, akiwasha rasmi umeme katika kijiji cha Mnekezi, wilayani Chato, Mkoa wa Geita, akiwa katika ziara ya kazi, Desemba 3, 2019.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati-mwenye kipaza sauti), akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mnekezi, wilayani Chato, Mkoa wa Geita, kabla ya kuwasha rasmi umeme kijijini hapo, Desemba 3, 2019. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Charles Kabeho.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (mwenye miwani), akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Charles Kabeho (wa tatu-kulia), kwenda kuwasha umeme katika moja ya nyumba za wananchi wa kijiji cha Mnekezi, wilayani Chato, Mkoa wa Geita, Desemba 3, 2019.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa mkandarasi wa umeme vijijini, anayetekeleza mradi huo katika kijiji cha Mnekezi, wilayani Chato, Mkoa wa Geita, akiwa katika ziara ya kazi, Desemba 3, 2019. Waziri aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.
Wafanyakazi wa kampuni ya mkandarasi wa umeme vijijini ambaye anatekeleza mradi huo katika kijiji cha Mnekezi, wilayani Chato, wakiendelea na kazi husika, baada ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), kukagua kazi hiyo na baadaye kuwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.
Msikiti uliopo katika kijiji cha Mnekezi, wilayani Chato, Mkoa wa Geita. Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), Desemba 3, 2019, akiwa kijijini hapo, alisisitiza taasisi za umma, nyumba za ibada kama hiyo na miradi ya wananchi ipewe kipaumbele katika kuunganisha umeme.

Veronica Simba – Chato
Wananchi wa maeneo ya vijijini ambao hawana uwezo wa kulipia shiingi 27,000 za kuunganishiwa umeme kwa mkupuo, sasa wanaweza kulipia huduma hiyo kwa kudunduliza kidogo kidogo.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani aliyasema hayo Disemba 3, 2019 kijijini Mnekezi, wilayani Chato, ambapo alikuwa akizungumza na wananchi kabla ya kuwasha rasmi umeme kijijini hapo.

Alikuwa akitoa maelekezo kwa wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwamba, wahakikishe wananchi wote wanaunganishiwa umeme bila kubagua hali zao kiuchumi kama ilivyo azma ya serikali.

Alisema kuwa, pamoja na serikali kupunguza gharama za kuunganisha umeme vijijini hadi shilingi elfu 27 tu lakini bado wako wananchi ambao kipato chao hakiwezi kuwaruhusu kulipa pesa hiyo kwa mkupuo, hivyo akawataka watendaji hao kupokea malipo ya wananchi husika kwa mtindo wa kudunduliza.

“Akipata elfu 10 akaleta, pokea umwandike; kesho akileta nyingine elfu tano pokea hadi pale atakapotimiza kiwango kinachotakiwa cha elfu 27.”

Katika hatua nyingine, Waziri alitoa hamasa kwa wananchi wa kijiji hicho na vingine vyote nchini ambako miradi mbalimbali ya umeme inatekelezwa, kutochagua kazi.

Alitoa hamasa hiyo baada ya kutoa maagizo kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini nchi nzima, kuhakikisha wanaajiri vibarua kutoka maeneo husika ili kuharakisha kazi lakini pia kuinua kipato cha wananchi, hususan vijana wa maeneo hayo.

Aidha, aliwataka wananchi kuachana na kasumba ya kulalamika kuwa hawajaunganishiwa umeme wakati hawajalipia huduma husika kwa visingizio tofauti, ikiwemo madai ya ukosefu wa nguzo.

“Wananchi, suala hili narudia tena kulisemea; ninyi mnachotakiwa kufanya ili muunganishiwe umeme ni kulipia tu na kuandaa nyumba zenu kwa kuweka mfumo wa nyaya. Suala la nguzo na vifaa vingine haliwahusu. Lipieni ili mletewe umeme,” alisisitiza.

Waziri Kalemani, ambaye pia ni Mbunge wa eneo husika (Chato), aligawa kwa wananchi wa Mnekezi, vifaa 50 vya Umeme Tayari (UMETA) bure, mbali na vile 250 ambavyo kila mkandarasi wa miradi ya umeme vijijini hutakiwa kugawa katika eneo lake.

Katika ziara hiyo, Waziri alifuatana na viongozi mbalimbali, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Chato, Charles Kabeho.

RC MWANRI AAGIZA UCHUNGUZI WA UJENZI WA NYUMBA YA DC KALIUA BAADA YA KUBAINI MAPUNGUFU

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora aggrey Mwanri amemwagiza Mhandisi wa ujenzi wa Ofisi yake kuchunguza vipimo vya nyumba ya  makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua ili kujiridhisha kama Mkandarasi amefuata maelekezo yaliyopo kwenye ramani ya ujenzi.

Amechukua hatua hiyo baada ya kubaini sehemu ya ukuta wa sebule katika nyumba hiyo kurudishwa ndani mita moja na kuwa sita badala ya saba ambazo ndio zinaoonyeshwa kwenye mchoro wa ramani ya ujenzi.

Mkuu wa Mkoa ametoa agizo hilo  Wilayani Kaliua wakati alipoongoza Kamati ya Mkoa wa Tabora ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa baada ya kupata fedha toka Serikalini.

Amesema kama itabainika kuwa Mkandarasi amesogeza ndani ukuta kwa ajili ya kupunguza vipimo itabidi akatwe sehemu ya fedha zake ili kufidia sehemu ambayo imepunguzwa.

“Kwa sababu jengo limeshafika hatua ya uezekaji , hatuwezi kumwambia abomoe lakini tunachotaka kujua vipimo vya upana na urefu wa vyumba kama viko sawa na kama haviko sawa kulingana na mchoro tumkate fedha” alisema.

Nyumba hiyo ya makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua inaendelea kujengwa na Mkandarasi ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) inatarajia kutumia shilingi milioni 199.6 hadi itakapokamilika.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alimwagiza Mkandarasi huyo kuhakikisha anafanyia marekebisho eneo la ndani ya Choo katika nyumba ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaliua kabla ya kuikabidhi kwa uongozi wa Wilaya ili kuondoa mapungufu yaliyoonekana.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema kuwa mchakato wa awali wa ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua umeanza na tayari wameshapokea shilingi milioni 350 kwa ajili ya kuanza kazi za awali za ujenzi wa Ofisi hiyo ambapo tayari uchunguzi udongo umeshafanyika.

Aidha Katibu Tawala huyo wa Mkoa alisema kuwa awali walitaka kutumia Shirika la Nyumba la Taifa katika ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya lakini wakadai shilingi bilioni 1.400 ikiwa ni gharama za ujenzi pekee tu bila kuweka gharama za ununuzi wa vifaa.

Alisema hatua hiyo iliwafanya kuachana nao na kuendelea kutafuta Wakandarasi wengine ambao watajenga jengo hilo kwa ubora unaotakiwa kwa gharama za chini.
 Viongozi wa Mkoa wa Tabora na Wilaya ya Kaliua wakiwa nje ya jengo la Makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua wakati wa ziara yao ya kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi huo unaoendelea.
 Mkuu wa Mkoa  wa Tabora Aggrey Mwanri (katikati) akitoa maelekezo kwa Watendaji na viongozi mbalimbali mara baada ya kukagua maendeleleo ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua.
 
  Mkuu wa Mkoa  wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia)  akipima urefu wa kuta mbalimbali wakati wa ukaguzi wa maendeleleo ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua.
Mkuu wa Mkoa  wa Tabora Aggrey Mwanri (kushoto) akitoa maelekezo kwa Watendaji na viongozi mbalimbali mara baada ya kukagua maendeleleo ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua . Picha na Tiganya Vincent

Ubakaji, Udhalilishaji waundiwa Mkakati Maalumu Zanzibar

$
0
0
Na Abubakari Akida, MOHA
Katika kukabiliana na Matendo ya Udhalilishaji,Ubakaji na Ulawiti  Visiwani Zanzibar, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeunda mkakati maalumu lengo  ikiwa ni  kukomesha matendo hayo ambayo yameota mizizi visiwani humo huku wengi wa waathirika wa matendo hayo wakitajwa kuwa ni watoto wadogo hali inayopelekea kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

Akizungumza katika Ukumbi wa Polisi Madema baada ya Kikao cha Ndani na Maafisa wa Juu wa Jeshi la Polisi Visiwani humo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema zinahitajika juhudi za makusudi ili kuweza kukomesha vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya wazanzibar na watanzania kwa ujumla

“Jumla ya kesi 280 zimeripotiwa hapa tu Mkoa wa Mjini Magharibi na tatizo hili linaendelea kukua kwa kasi na inasikitisha sana, jambo hili linachafeua heshima ya nchi yetu, sasa serikali tunakuja na mkakati maalumu ikiwa ni dhamana tuliyopewa kama viongozi,tumeamua kuja na mkakati maalumu na wa kipekee wa kupambana na changamoto ya udhalilishaji,ubakaji na tunaomba mamlaka nyingine zituunge mkono katika mkakati huu sisi kama wizara kupitia Jeshi la Polisi tunaamini mapambano haya hatuwezi kufanya peke yetu..” alisema Masauni

“...pia tunaunda kikosi kazi maalumu ambacho kitaratibu mkakati huo huku kikisimamia uandaaji mafunzo kwa askari wetu hasa wapelelezi wa makosa ya udhalilishaji,kufuatilia kesi zote zilizoenda mahakamani na kuhakikisha zinaenda vizuri hatua kwa hatua,kuhakikisha kesi za udhalilishaji zinapewa kipaumbele badala ya kesi hizo kuchukua muda mrefu hali inayopelekea waathirika wa matendo hayo kukata tama na tunataka kikosi kazi hicho kiwe kiungo na mamlaka nyingine zinazoshughulika na kesi hizo.” Aliongeza Masauni

Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mohamed Hassani Haji anaweka wazi Utekelezaji wa Mkakati huo ambao ni maagizo toka serikalini huku akikiri tatizo hilo la Ubakaji,Udhalilishaji na Ulawiti kukua kwa kasi Visiwani Zanzibar huku akikwaonya wazazi kufika polisi na kuripoti pindi watoto wao wanavyofanyiwa vitendo hivyo.

“Sisi kama jeshi la polisi tnaenda kuunda kikosi kazi hicho,na leo tumepitia majalada hapa na kuona kesi nyingi zimekwama,kwahiyo kikosi kazi hicho kitaanza kazi ndani ya mwezi huu na tunatoa onyo kwa wale wote wanaoshiriki,kusaidia au kuficha matendo haya ya udhalilishaji waache mara moja kwani hakutakua na kuchekeana” alisema Kamishna Hassani

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa visiwa hivyo wameiomba serikali kupeleka elimu juu ya kupambana na udhalilishaji mashuleni ambako watoto wamekua wakirubuniwa na vitu mbalimbali ambavyo vimewapelekea kutumbukia katika matendo ya udhalilishaji ambayo yamekua na madhara makubwa Visiwani Zanzibar huku wakiasa kuchukuliwa hatua kwa baadhi ya wazazi wanaowatetea watuhumiwa na kuyamaliza masuala hayo kifamilia kwani hilo upelekea matendo hayo kuendelea kuota mizizi katika jamii.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiongoza Kikao Maalumu na Viongozi wa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar, ambapo kikao hicho kiliazimia kuanzishwa kwa Mkakati Maalumu wenye lengo la kupambana na Matendo ya Udhalilishaji, Ubakaji na Ulawiti visiwani humo ambapo waathirka wakubwa wa vitendo hivyo wakitajwa ni watoto huku jumla ya Kesi 280 zikiwa zimeripotiwa ndani ya mwaka huu kwa Mkoa wa Mjini Magharibi pekee.Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Kituo cha Polisi Madema,Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi

Kabendera aendelea kusota, ni baaada ya makubaliano yake na DPP kutofikiwa muafaka

$
0
0
 Allen Christian na Collin Ndanzi (DSJ)
MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi kisutu imeuambia upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera kuwa waende wenyewe kwa mkurugenzi wa mashtàka nchini (DPP) ili kujua hatma ya barua ya mshtakiwa ya makubaliano ya kuomba msamaha na kukiri kosa ( pre- baggening).

Hatua hiyo imefikiwa wakati kesi hiyo leo Desemba 4, 2019 ilipoitwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega  kwa ajili ya kutajwa na kudaiwa kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo upande wa utetezi wakawasilisha hoja zao.

Mapema wakili wa utetezi Jebra Kambole alidai mahakamani hapo kuwa, Oktoba 11, 2019 waliitaarifu mahakama juu mshtakiwa kuandika barua ya kuomba msahama na kukiri kosa kwenda kwa DPP lakini mpaka leo ni miezi miwili hawajapata mrejesho wowote kutoka kwa DPP .

"Ni lini tutakamilisha mchakato wa majadiliano hayo kwani mpaka sasa hakuna chochote ambacho kimefanyika na mtuhumiwa bado yuko gerezani na ni mgonjwa", ameuliza Kambole

Akijibu hoja hizo wakili wa serikali Easter Martin amekiri kwamba ni kweli maombi yao hayo yapo kwa DPP toka Oktoba 11 hadi leo lakini suala la makubaliano si maamuzi yanayoweza kutolewa mara moja,  ni vema waende katika ofisi ya DPP ili wajue kinachoendela.

Hakimu Mtega nae amesema, kufuatia hoja hizo,  amewataka upande wa utetezi waende wenyewe kufuatilia jalada la kesi kwa DPP ili wajue kinachoendelea na ameiahirisha kesi hiyo hadi itakapotajwa tena Desemba 18, mwaka huu.

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh milioni 173.

Katika mashtaka ya kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha  na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Inadaiwa kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya Sh 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Pia inadaiwa Kabendera alitakatisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji kodi.

Mwimsamaha na kukiri kosa ( pre- baggening).

Hatua hiyo imefikiwa wakati kesi hiyo leo Desemba 4,2019 ilipoitwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega  kwa ajili ya kutajwa na kudaiwa kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo upande wa utetezi wakawasilisha hoja zao.

Mapema wakili wa utetezi Jebra Kambole alidai mahakamani hapo kuwa, Oktoba 11,2019 waliitaarifu mahakama juu mshtakiwa kuandika barua ya kuomba msahama na kukiri kosa kwenda kwa DPP lakini mpaka leo ni miezi miwili hawajapata mrejesho wowote kutoka kwa DPP .

"Ni lini tutakamilisha mchakato wa majadiliano hayo kwani mpaka sasa hakuna chochote ambacho kimefanyika na mtuhumiwa bado yuko gerezani na ni mgonjwa", ameuliza Kambole

Akijibu hoja hizo wakili wa serikali Easter Martin amekiri kwamba ni kweli maombi yao hayo yapo kwa DPP toka Oktoba 11 hadi leo lakini suala la makubaliano si maamuzi yanayoweza kutolewa mara moja,  ni vema waende katika ofisi ya DPP ili wajue kinachoendela.

Hakimu Mtega nae amesema, kufuatia hoja hizo,  amewataka upande wa utetezi waende wenyewe kufuatilia jalada la kesi kwa DPP ili wajue kinachoendelea na ameiahirisha kesi hiyo hadi itakapotajwa tena Desemba 18, mwaka huu.

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh milioni 173.

Katika mashtaka ya kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha  na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Inadaiwa kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya Sh 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Pia inadaiwa Kabendera alitakatisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji kodi.

SUMAYE AONDOKA CHADEMA

Yutong yatoa Mafunzo kwa Maafisa na Askari wa Zimamoto

$
0
0
Kampuni ya kutengeneza Mabasi aina ya Yutong imetoa mafunzo kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji nchini, namna mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto inavyofanya kazi katika mabasi hayo yanayofanya safari zake mikoani na nje ya nchi ili kuweza kujikinga pindi yanapopata hitilafu na kuwaka moto lengo ikiwa ni kupunguza ajali za moto.

Mafunzo hayo  ya siku mbili yanafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma yamefunguliwa  leo na Mkuu wa Kitengo cha Usalama,Majanga ya Moto na Uchunguzi,Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Fikiri Salla huku washiriki hao wakifundishwa nadharia na vitendo katika kudhibiti majanga ya moto na ikiwa pamoja na kuangalia mifumo ya magari hayo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Naibu Kamishna Fikiri alisema sasa ni wakati wa sayansi na teknolojia na jeshi halina budi kuanza kujifunza njia mbalimbali za udhibiti wa majanga kwa kutumia teknolojia huku akiishukuru kampuni ya Yutong kwa mafunzo hayo.

“Tunapitia kipindi cha mabadiliko ya sayansi na teknolojia naamini mafunzo haya yatawawezesha askari wetu kujifunza njia hizo za kisasa sambamba na kuelewa mfumo mzima wa mabasi hayo ambayo yamekua mengi hivi sasa hapa nchini na yakitumika katika usafiri wa kwenda mikoa mbalimbali” alisema Naibu Kamishna Fikiri

Aidha mafunzo hayo yanaendeshwa na Wakufunzi kutoka Kampuni ya kutengeneza mabasi aina ya Yutong wakiongozwa na Meneja Huduma wa Kampuni hiyo, Lang Chang Ling,Mtaalamu wa Usalama kwenye gari,Ma Jiong  na Mhandisi wa Huduma, Zhao Le Hui

Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo ya siku mbili walisema wanaamini baada ya mafunzo kumalizika watakua wamepata elimu ambayo itawaongezea kitu katika shughuli zao za kila siku zinazohusiana na majanga ya moto na uokoaji.
 Mkuu wa Kitengo cha Usalama,Majanga ya Moto na Uchunguzi Naibu Kamishna Fikiri Salla, akizungumza na Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji(hawapo pichani), wakati akifungua mafunzo ya namna mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto inavyofanya kazi kwenye mabasi aina ya Yutong. Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma yakiendeshwa na Wakufunzi kutoka Kampuni ya kutengeneza mabasi aina ya Yutong.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Mkufunzi  kutoka Kampuni ya Mabasi ya Yutong Lang Chang Ling akitoa ufafanuzi jinsi mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto inavyofanya kazi kwenye mabasihayo  kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini  katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma ,leo ambapo mafunzo hayo ya siku mbili yameanza.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

VYAMA VYA USHIRIKA ROMBO VINAFANYA VIZURI

$
0
0
 Meneja wa Chama cha Ushirika cha Msingi Mamsera AMCOS, Mary Shayo akiwasilisha taarifa ya chama hicho kwa Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Titus Kamani wilayani Rombo,mkoa wa Kilimanjaro.
  Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Titus Kamani, akizungumza na Wanachama wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Kilimo na Masoko Mamsera Desemba 03, 2019 wilayani Rombo,mkoa wa Kilimanjaro.
Wanachama wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Kilimo na Masoko Tarakea AMCOS  wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Titus Kamani Jumanne, Desemba 03, 2019 wilayani Rombo,mkoa wa Kilimanjaro.

Vyama vya Ushirika katika wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro  vinakubalika  kwa wananchi  kutokana  na huduma  nzuri na shirikishi zinazotolewa kwa wanachama  na viongozi wa Bodi za vyama hivyo kwa  jamii nzima. Vyama hivi vimepata mafanikio mbalimbali tangu kuanzishwa kwake ikiwemo kuongezeka kwa mitaji pamoja na uanzishwaji wa  miradi mbalimbali ya maendeleo inayowaingizia kipato wananchama wa vyama vya ushirika

Taarifa zilizotolewa kwa Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Titus Kamani, Jumanne, Desemba 03, 2019 wilayani Rombo, kwenye vyama vya ushirika alivyovitembelea zinaonyesha  uwepo wa ongezeko kubwa la wanachama  wanaojiunga na vyama vya  ushirika ambavyo vimekuwa mkombozi mkubwa kwa  wananchi kujikwamua kiuchumi.
“Hali ya Ushirika niliyoiona na maendeleo yaliyopatikana katika vyama vya ushirika hapa Rombo imenipa faraja kubwa sana, kuwa kuna  baadhi ya Watanzania bado wanauishi Ushirika , na ninawapongeza viongozi wa vyama hivi kwa kusimama imara katika kuvisimamia  kwa   kufuata Sheria na taratibu za Ushirika,” amesema Dkt. Kamani.
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika  anaeleza kuridhishwa na uendeshwaji wa vyama vya ushirika alivyovitembelea katika  wilaya  Rombo  na kuvitaja kuwa  Shamba Darasa la vyama vya msingi vinavyosimamiwa vizuri na kwamba popote atakapokwenda katika mikoa mbalimbali hapa nchini atawataka wanaushirika kuja Kilimanjaro katika wilaya ya Rombo kujifunza na kujionea mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia ushirika

 Vyama vya ushirika  ambavyo  Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania amepata fursa ya kuvitembelea  katika ziara yake ni  pamoja na Chama cha Ushirika cha Msingi cha Kilimo na Masoko Mamsera, Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Mashati na Chama cha Ushirika cha Msingi cha Kilimo na Masoko Tarakea.

Meneja wa Chama cha Ushirika cha Msingi Mamsera AMCOS, Mary Shayo alisema idadi ya wanachama imeongezeka kutoka 934 mwaka 1995 na kufikia wanachama 2,000 mwaka 2017/2018 na kwamba chama hicho kinahudumia wakulima zaidi ya 10,000. 
Aidha, Mamsera AMCOS kimekuwa kikitoa gawio kila mwaka kwa wanachama wake na chama kimetenga mafungu kila mwaka kwa ajili ya kusomesha wanafunzi yatima na walio katika mazingira magumu  ambapo mwanafunzi mmoja amesomeshwa hadi kuhitimu chuo kikuu (UDOM) na wengine wawili wamemaliza kidato cha nne huku wengine  wanaendelea kusomeshwa pamoja na chama vilevile kimejenga jengo kubwa  la kitega uchumi.

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Mashati SACCOS kilianza na wanachama 17 mwaka 1987 na hivi sasa kina wanachama 3,511, Akiba za Wanachama Shilingi 3,101,832,070, Hisa za Wanachama Shilingi 225,318,000 na Amana za Wanachama Shilingi 45,131,552. Aidha, chama hicho kimewekeza fedha za hisa za Wanachama katika makampuni mbalimbali Zaidi ya Shilingi 234,439,552 na chama kimeweka Bondi Benki Kuu ya Shilingi 1,329,786,002 na Mtaji wa chama ni Shilingi 336,530,238.

Idadi ya Wanachama katika Chama cha Ushirika cha Msingi cha Kilimo na Masoko Tarakea AMCOS wameongezeka kutoka 55 mwaka 1961 na kufikia wanachama 2,870 hivi sasa. Aidha, Chama kimeweza kujenga Ukumbi wa Mikutano na Ukuta kwa ajili ya kuimarisha usalama wa chama bila kuchangisha mwanachama, gharama za ujenzi mpaka sasa imefikia Shilingi 197,349,701. Vilevile Chama kiliweza kuwalipia sehemu ya ada wanafunzi 12 kila mwaka kwa kipindi cha miaka 12 kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano haijafuta ada kwenye shule za msingi na sekondari za Serikali.

Yutong yatoa Mafunzo kwa Maafisa na Askari wa Zimamoto

$
0
0


Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya kutengeneza Mabasi aina ya Yutong imetoa mafunzo kwa
Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji nchini, namna mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto inavyofanya kazi katika mabasi hayo yanayofanya safari zake mikoani na nje ya nchi ili kuweza kujikinga pindi yanapopata hitilafu na kuwaka moto lengo ikiwa ni kupunguza ajali za moto.

Mafunzo hayo  ya siku mbili yanafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma yamefunguliwa  leo na Mkuu wa Kitengo cha Usalama,Majanga ya Moto na Uchunguzi,Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Fikiri Salla huku washiriki hao wakifundishwa nadharia na vitendo katika kudhibiti majanga ya moto na 
 ikiwa pamoja na kuangalia mifumo ya magari hayo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Naibu Kamishna Fikiri alisema sasa ni wakati wa sayansi na teknolojia na jeshi halina budi kuanza kujifunza njia mbalimbali za udhibiti wa majanga kwa kutumia teknolojia huku akiishukuru kampuni ya Yutong kwa mafunzo hayo.

“Tunapitia kipindi cha mabadiliko ya sayansi na teknolojia naamini mafunzo haya yatawawezesha askari wetu kujifunza njia hizo za kisasa sambamba na kuelewa mfumo mzima wa mabasi hayo ambayo yamekua mengi hivi sasa hapa nchini na yakitumika katika usafiri wa kwenda mikoa mbalimbali” alisema Naibu Kamishna Fikiri

Aidha mafunzo hayo yanaendeshwa na Wakufunzi kutoka Kampuni ya
kutengeneza mabasi aina ya Yutong wakiongozwa na Meneja Huduma wa Kampuni hiyo, Lang Chang Ling,Mtaalamu wa Usalama kwenye gari,Ma Jiong  na Mhandisi wa Huduma, Zhao Le Hui

Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo ya siku mbili walisema wanaamini baada ya mafunzo kumalizika watakua wamepata elimu ambayo itawaongezea kitu katika shughuli zao za kila siku zinazohusiana na majanga ya moto na uokoaji.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama,Majanga ya Moto na Uchunguzi Naibu Kamishna Fikiri Salla, akizungumza na Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji(hawapo pichani), wakati akifungua mafunzo ya namna mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto inavyofanya kazi kwenye mabasi aina ya Yutong. Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma yakiendeshwa na Wakufunzi kutoka Kampuni ya kutengeneza mabasi aina ya Yutong.
 
Mkufunzi  kutoka Kampuni ya Mabasi ya Yutong Lang Chang Ling akitoa ufafanuzi jinsi mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto inavyofanya kazi kwenye mabasihayo  kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini  katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma ,leo ambapo mafunzo hayo ya siku mbili yameanza.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

TCRA YAENDELEA KUHAMASISHA USAJILI WA LAINI ZA SIMU KWA ALAMA ZA VIDOLE MKOANI SINGIDA

$
0
0

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kampeni ya kuhamasisha usajili wa laini za simu kwa alama za vidole iliyofanyika katika viwanja vya Stend ya Zamani mjini Singida akizungumza na wananchi juzi kwenye kampeni hiyo. Kushoto ni  Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati,  Antonio Manyanda.
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kwenye kampeni hiyo.
 Kampeni ikiendelea.
Muonekano wa vibanda vya makampuni ya Simu katika kampeni hiyo.

Na Waandishi wetu, Singida.  
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wananchi kusajili laini zao za simu kwa alama za vidole kwa lengo la kuondoa uhalifu unaofanywa mitandaoni. 
Aliyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi katika kampeni ya kuhamasisha usajili wa laini za simu kwa alama za vidole iliyofanyika katika viwanja vya Stendi ya Zamani mjini Singida. 
Dkt. Nchimbi aliwapongeza wananchi wa mji huo kwa kujitokeza kwa wingi ili kusajili laini zao za simu na kueleza umuhimu wa simu na manufaa yake ambapo licha ya umuhimu huo wapo watu wamekuwa wakutumia manufaa hayo Vibaya kwa kufanya uhalifu hivyo ili kudhibiti uhalifu huo serikali ameagiza kila anayemiliki simu asajili laini yake kwa alama za vidole. 
"Taifa limeona kuna umuhimu wa simu licha ya kuwa hatarishi katika usalama ndio maana limeamua kuboresha huduma hizi, tuunge mkono juhudi hizi."alisema Dkt Nchimbi. 
Hata hivyo aliziagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) kuwafuata wananchi huko waliko ili kutoa elimu juu ya umuhimu wa kusajili laini zao kwa alama za vidole kabla zoezi hilo halijaisha ambapo linatarajiwa kuhitimishwa Disemba 31 mwaka huu. 
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati,  Antonio Manyanda alisema takwimu zinaonyesha takribani watanzania 45 milioni wanamiliki simu lakini mpaka sasa waliosajili laini zao za simu kwa alama za vidole ni watanzania 19 milioni tu, hivyo aliwaomba waendeleze kujitokeza ili wakamilishe zoezi hilo kwani tofauti na hapo hawataruhusiwa kutumia laini ambazo hazijakamilishwa.

Mganda kuwakilisha Afrika Mashariki Mashindano ya Pool Kimataifa Nchini China.

$
0
0

Amos Ndyagumanawe kutoka Nchini Uganda amefuzu kushiriki mashindano ya Kimataifa ya mchezo wa Pool yajulikanayo  “Chines 8 Ball WeMasters Championship 2020” yanayotarajiwa kufanyika Qinhuangdao City Nchini China Januari 3 – 8,2020 kwa kushirikisha Mataifa 42.
Amos alifuzu nafasi hiyo katika mashindano ya Afrika Mashariki yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Whisky River  Nairobi nchini Kenya kwa kushirikisha nchi tatu yaani Tanzania, Uganda na wenyeji Kenya na kwa kufuzu huko alizawadiwa pesa taslimu za Kenya shilingi 200,000/= sawa na milioni 4,478,721.73 za Kitanzania, Saa ya Ukutani ya kisasa inayoashilia mchezo swa Pool,Ticket ya Ndege ya kwenda na kurudi nchini China pamoja na huduma zote za chakula na maladhi.
Amos ataambatana na Mchezaji mmoja kutoka Tanzania, Amos Boniphace ambaye ni mlemavu wa mkono na mguu aliyepewa nafasi ya upendeleo kushiriki mashindano hayo nchini China kwa ufadhili wa Uongozi wa Chines 8 Ball wa nchini Kenya.
Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni Joseph Kasozi pia kutoka Uganda ambaye alizawadia pesa taslimu za kikenya shilingi 100,000 sawa na shilingi milioni 2,239,360.87 za Tanzania, mshindi wa tatu ni Morgan Muema kutoka Kenya ambaye alizawadiwa pesa taslimu za Kenya shilingi 50,000 zawa na milioni 1,119,680.43 za Tanzania, mshindi wa nne ni Baraka Jackson kutoka Mkoa wa Mayara nchini Tanzania ambaye alizawadia pesa taslimu za Kenya 30,000 zawa na shilingi 6,71,808.26 za Tanzania,mshindi wa tano mpaka wa nane walizawadiwa pesa taslimu za kesha shilingi 10,000 ambazo ni sawa na 2,23,936.09 za Tanzania ambao ni Simoni Lubulwa kutoka Uganda, Caesar Chandiga kutoka Uganda, Collins Tuwei kutoka Kenya, AlfredGumikiriza kutoka Uganda.
Mshindi wa tisa mpaka kumi na sita walizawa pesa taslimu ya Kenya shilingi 5,000 sawa na shilingi 1,11,968.04 ya Tanzania ambao ni Stephen Kyalo kutoka Kenya, Bwanika Mansoor kutoka Uganda, John Kyalo kutoka Kenya, Henry Mwangi kutoka Kenya, Lucas Mbugua kutoka Kenya, Geoffrey Setumba kutoka Uganda, Kituku Munguti kutoka Kenya na  David Njane kutoka Kenya.
Mashindano hayo yalijumuisha jumla ya Wachezaji 64 kutoka nchi hizo ambapo Tanzania iliwakilishwa na Wachezaji waanne ambao ni Abdallah Hussein(Dar es Salam), Ahmed Sahil(Dar es Salaam), Amos Boniphace(Dar es Salaam) na Baraka Jackson(Manyara).
Akizungumza na Wachezaji pamoja na waandishi wa habari,Mratibu wa mashindano ya Afrika Mashariki, Peter Kinyua kwanza aliipongeza kamati ya maandalizi iliyoendesha mashindano kwa ushumla mpaka kumalizika kwa usalama, pili aliwapongeza wachezaji wote walijitokeza kushiriki mashindano hayo ya funga mwaka 2019, lakini zaidi aliwapongeza washindi wote waliopata zawadi  na zaidi alimpongeza Bingwa, Amos Ndyagumanawe kwa ushindi na kumuomba ajiandae vyema sasa kuwawakilisha wana Afrika mashariki kwanye fainali za Kimataifa Nchini China hapo Januari 2020.Lakini pia aliwaomba wapenzi na wadau wote kwa sasa tuelekeze hakili na masikio yetu kwenye fainali za Kimataifa zijulikanazo kama “Chines 8 Ball WeMasters Championship 2020” zinazo tarajiwa kuanza Januari 3-8,2020.






Benki ya NBC na T-Pesa zaingia ushirikiano kutoa huduma za kifedha.

$
0
0
Mkurugenzi wa T-Pesa, Lulu Mkudde (kulia), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa huduma za kifedha kati ya NBC na T-Pesa ambapo wateja wa NBC wataweza kutoa na kutuma pesa kutoka katika akaunti zao kupitia huduma ya simu za mkononi ya T-Pesa. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Kibenki Kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha.

Mkurugenzi wa Huduma ya T-Pesa, Lulu Mkudde (kulia), akionyesha jinsi ya kufanya muamala wa kifedha kutoka katika akaunti ya Benki ya NBC kupitia huduma ya kifedha kupitia T-Pesa ya Kampuni ya TTCL, katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa huduma za kifedha kati ya T-Pesa na NBCambapo wateja wa NBC wataweza kutoa na kutuma pesa kutoka katika akaunti zao kupitia huduma ya simu za mkononi ya T-Pesa. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Kibenki Kidigitali wa NBC, Deogratius Mosha. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Huduma za Kibenki Kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa huduma za kifedha kati ya NBC na T-Pesa ambapo wateja wa NBC wataweza kutoa na kutuma pesa kutoka katika akaunti zao kupitia huduma ya simu za mkononi ya T-Pesa. Kulia ni Mkurugenzi wa T-Pesa, Lulu Mkudde.
Mkurugenzi wa T-Pesa, Lulu Mkudde (kulia), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa huduma za kifedha kati ya NBC na T-Pesa ambapo wateja wa NBC wataweza kutoa na kutuma pesa kutoka katika akaunti zao kupitia huduma ya simu za mkononi ya T-Pesa. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Kibenki Kidigitali wa Benki ya NBC, Deogratius Mosha.

DATA TAMASHA LAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI UMUHIMU WA TAKWIMU NA TAARIFA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
KONGAMANO la kwanza kufanyika barani Afrika na kuwakutanisha   wanawake katika masuala ya data limefanyika leo katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam tawi Kijitonyama huku mlengo mkubwa ukiwa ni kujadili masuala ya wanawake ambapo tafiti zinaonesha kuwa asilimia 30 ya wanawake   pekee ndio wanaoshiriki katika masuala ya data jambo lililowapa  kiu ya kuwakutanisha vijana na wanawake waliofanya vizuri katika masomo hayo ili iwe chachu kwa vijana hao.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tanzania Data Lab Stephen Chacha amesema kuwa leo wanasherehekea  taarifa na takwimu kupitia jukwaa la Data Tamasha ambalo limewakutanisha wadau mbalimbali na baada ya hilo na wanaamini sera na maamuzi wanayoyafanya kupitia katika mifumo maalumu na kutoa taarifa sahihi za maendeleo kwa taifa hasa katika ujenzi wa taifa la viwanda.

Amesema kuwa tamasha hilo pia litajadili ushiriki wa wanawake katika masuala ya taarifa na takwimu na kwa namna zinasaidia katika  kufanya maamuzi, pia watajadili kuhusiana na uelewa wa wananchi katika masuala ya taarifa na takwimu na namna ya taarifa zinazowanufaisha wananchi kimaendeleo.

" Pia wadau kutoka nchi mbalimbali wapo na tutabadilishana uzoefu hasa kuhusiana na teknolojia katika ngazi mbalimbali na hiyo ni pamoja na kukuza uelewa kwa wananchi na kupokea taarifa zinazotoka kwa wananchi" ameeleza.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa mafunzo kutoka Tanzania Data Lab   Mahadia Tunga amesema kuwa Data Lab imekuwa ikihimiza matumizi sahihi ya data katika kuleta tija katika maendeleo ya kiuchumi, na ameeleza kuwa data ni mkombozi katika jamii hasa katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii na maendeleo zikiwa zimechakatwa kiutaalamu zaidi.

Amesema kuwa data imekuwa zimekua zikitatua changamoto kadha wa kadha katika taasisi za umma na binafsi na ameshauri taasisi hizo kuendeleza matumizi ya data kwa usahihi ili kuweza kutatua changamoto za aina hiyo.

"Katika biashara pia Kuna uhitaji mkubwa wa matumizi ya data, pia hata kwa wanafunzi wa Sekondari, Serikali na taasisi nyingine zinazoshughulikia masuala  ya kijamii ndani na nje ya nchi na ili  kuleta maendeleo data lazima zihusike" ameeleza.

Hafla hiyo ilienda sambamba na maonesho ya data katika nyanja mbalimbali yaliyooneshwa na wanafunzi kutoka Chuo kikuu Dar es Salaam wanaosomea masuala ya data.
 Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Data Lab nchini Stephen Chacha Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana sherehe ya Data Tamasha ambapo ameeleza umuhimu wa data katika shughuli za kijamii ikiwemo utunzaji wa kumbukumbu zenye kusaidia jamii, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa mafunzo kutoka Tanzania Data Lab Mahadia Tunga akizungumza na waandishi kuhusiana na hafla hiyo ambapo ameeleza kuwa data husaidia sana katika kufanya maamuzi, leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wakiwemo wanafunzi wakifuatilia mada mbalimbali katika sherehe za Data Tamasha lililofanyika katika Chuo kikuu Cha Dar es Salaam tawi la Kijitonyama, leo jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa Tamasha la Data Tamasha wakiwa katika picha ya pamoja.

RAIS DKT.SHEIN AZUNGUMZA NA KATIBU WA KAMATI KUU YA UONGOZI WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA VIETNAM IKULU ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Ujumbe alioongazana nao Katibu wa Kamati Kuu ya Uongozi wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam. Pham Minh Chinh, walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika leo 4-11-2019.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitowa maelezo ya mlango wa Zanzibar (Zanzibar Door) kwa Katibu wa Kamati Kuu ya Uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam. Pham Minh Chinh,baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na ( kulia) ujumbe aliofuatana nao.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiagana na Katibu wa Kamati Kuu ya Uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam. Pham Minh Chinh, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo leo,4-12-2019(Picha na Ikulu)
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images