Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

BENKI YA CRDB YAIPIGA TAFU HOSPITALI YA MJI WA MBULU

$
0
0
Na Woinde Shizza, Globu ya Jamii.

Hospitali ya mji wa Mbulu Mkoani Manyara inayokabiliwa na uchakavu wa miundombinu ikiwemo majengo,samani na upungufu wa vifaaa kutokana na hospitali hiyo kujengwa zaidi ya miaka 50 iliyopita hivyo kusababisha usumbufu kwa wagonjwa wanaotumia hospitali hiyo.

Licha ya serikali kuanza uboreshaji wa miundombinu kwa kukarabati majengo ya hospitali  hiyo baadhi ya wadau wameanza kujitokeza kuunga mkono jitihada hizo kuhakikisha ukarabati huo  unaenda sambamba na uwekaji wa vifaa ikiwemo vitanda na magodoro, ambapo benki ya CRDB kupitia tawi la Mbulu katika kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii imetoa msaada wa vitanda vitano na magodoro vya wagonjwa kwa ajili ya hospitali hiyo na mabati sitini kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi.

Akikabidhi msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga, katika hafla iliyofanyika kwenye hospitali ya mji wa Mbulu, Meneja wa benki ya CRDB kanda ya kaskazini, Chiku Issa amesema benki hiyo inatambua kuwa vitanda ni nyenzo muhimu sana katika utoaji wa huduma za afya lakini pia mabati katika kuboresha miundombinu ya utoaji huduma nchini kote.
Alisema aliposikia kuwa halmashauri ya mji wa Mbulu ina uhitaji wa vitanda na mabati ili kuboresha huduma za afya  hawakusita kama benki kuunga mkono ombi hilo kuwezesha katika kufanikisha jitihada hizo.

“Benki ya CRDB ni muumini mkubwa wa falsafa ya kusaidia jamii ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazorudisha nyuma juhudi za maendeleo yaani kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii hivyo imepelekea benki kujiwekea sera maalum ya kusaidia jamii yenye kuagiza na kuelekeza kutenga asilimia moja ya faida yake kila mwaka ili ziende katika shughuli za kusaidia jamii katika Nyanja mbalimbali”alisema Chiku.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga aliishukuru benki ya CRDB kwa msaada huo ambao amesema umekuja kwa wakati na utasaidia kutatua changamoto ya upungufu wa vitanda na magadoro iliyokuwa ikiwakabili hospitalini hapo ambapo wakati mwingine kulazimu wagonjwa wanapozidi kulala zaidi ya mtu mmoja lakini pia msaada wa mabati utasaidia kuboresha sekta ya elimu.

“Hili ni tukio muhimu sana kwa maana msaada huu  unatimiza falsafa yenu ya ulipo tupo huu ndio utekelezaji wa kusogea kwa wale wadau wenu muhimu na kuweza kuwachangia kile kitu cha ziada kinachotokana na biashara yenu”alisema Mofuga

Awali Kaimu mganga mfawidhi hospital ya mji wa Mbulu daktari Charles Shija alisema msaada huo utawapunguzia kazi wao kama watumishi kwa kuwa walikuwa wakabiliwa na upungufu wa vitanda ishirini na mbili hivyo kusababisha wagonjwa wanapofurika kuwalazimu kulala Zaidi ya mmoja jambo ambalo amesema si salama kwa afya za wagonjwa.  

Alisema Hospitali hiyo bado inakabiliwa na upungufu wa vitanda na magodoro 17 ambapo endapo vitapatikana vitasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa haswa kina mama wanapokuja kujifungua ambao wakati mwingine wanalazimika kulala watatu kwenye kitanda kimoja pamoja na watoto wao.

WAFUGAJI JIUNGENI KATIKA VYAMA VYA USHIRIKA – DKT. KAMANI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Titus Kamani (Wa kwanza kulia) akipatiwa maelezo kuhusu usindikaji katika kiwanda cha maziwa cha Chama cha Ushirika wa Maziwa wa Wanawake Nronga kutoka kwa Katibu Meneja wa chama hicho, Hellen Usiri.
  Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Kilimanjaro, John Henjewele akiongea kwenye ziara ya Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Titus Kamani kwenye kiwanda kusindika maziwa cha Chama cha Ushirika wa Maziwa wa Wanawake Nronga.
 Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Titus Kamani (Wa kwanza kulia) akinywa maziwa yanayosindikwa na kiwanda cha Chama cha Ushirika wa Maziwa wa Wanawake Nronga, kwenye ATM ya Maziwa ya Nronga Youth Service Group.
 Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Titus Kamani (Mwenye tai) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa kiwanda cha kusindika maziwa cha Chama cha Ushirika wa  wa Wanawake Nronga.

Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Titus Kamani amewataka Wafugaji kote nchini kujiunga pamoja katika Vyama vya Ushirika ili kuwa na nguvu ya pamoja na kuweza kuyaaongezea thamani mazao ya mifugo ikiwemo kuanzisha Vyama vya Ushirika wa Maziwa.

Dkt. Kamani ametoa wito huo leo Jumatatu, Desemba 2, 2019 kwenye ziara ya kutembelea na kujionea mafanikio na changamoto za Chama cha Ushirika wa Maziwa wa Wanawake Nronga (Nronga Women Dairy Cooperative Society) kilichopo wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro. 

“kutokana na nilichojionea hapa kwenye kiwanda cha kusindika maziwa cha Chama cha Ushirika wa Maziwa wa Wanawake Nronga, na kwa kuwa nchi hii ina utajiri mwingi wa ng’ombe wa  asili na kisasa, nawasihi wafugaji wajiunge pamoja katika ushirika na kuanzisha viwanda vidogo na vikubwa vya kusindika maziwa na bidhaa zake na kuwanufaisha wananchi wengi Zaidi kwa kuwapatia ajira na kuwaongezea kipato,” amesema Dkt. Kamani.

Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania amesema kuwa mfano uliooneshwa na wanawake wa Nronga hauna budi kuigwa na wafugaji katika mikoa inayosifika kwa kuwa na mifugo mingi ili waweze kujiunga pamoja katika ushirika na kuweza kupata manufaa makubwa kutokana na kusindika maziwa na kujipatia bidhaa nyingine zinazotokana na maziwa.

“Ni vigumu mfugaji mmoja mmoja kuweza kuanzisha kiwanda cha kusindika maziwa, lakini wafugaji wakijiunga katika ushirika wataweza kukusanya maziwa yao kwa pamoja na kutafuta mashine zitakazowawezesha kufanya usindindikaji na kukuza mataji na hatimaye kuweza kumiliki kiwanda chao wenyewe,” amesema Dkt. Kamani.

Akitoa maelezo kuhusu Chama cha Ushirika wa Maziwa wa Wanawake Nronga kwa Dkt. Kamani, Katibu Meneja wa chama hicho, Hellen Usiri amesema kuwa chama chake kilianzishwa na wanawake 6  mwaka 1987 na hivi sasa kina wanachama 462. 

Tangu Nronga Women Dairy Cooperative Society ianzishwe imeweza kupata mafanikio mbalimbali kwa jamii ndani na nje ya Nronga ikiwemo: ongezeko la kipato kwa kaya, kusomesha Watoto, kuboresha mifugo ya wanachama, kuboresha makazi (nyumba bora), wanachama kufungiwa mitambo ya biogas na kutengeneza mbolea hai itokanayo na mbolea itokayo kwenye mitambo ya biogas.

Mafanikio mengine ya Chama cha Ushirika wa Maziwa wa Wanawake Nronga ni pamoja na Kutekeleza Mradi wa unywaji maziwa shuleni kwa baadhi ya shule za msingi zilizopo katika wilaya ya Hai, Kuanzisha SACCOS, kutoa mafunzo kwa vyama na vikundi vya maziwa ndani na nje ya Nronga na kuongoza jitihada za uanzishwaji wa Joint Enterprise (JE) kwa vikundivilivyokowilaya ya Hai vinavyojishughulisha na ukusanyaji na usindikajiwa maziwa.

Aidha, Chama cha Ushirika wa Maziwa wa Wanawake Nronga kimefanikiwa kuanzisha kiwanda cha maziwa na kimeweza kutengeneza bidhaa mbalimbali na bora zinazotokana na maziwa kama vile mtindi, yogati pamoja na siagi.

WASICHANA WAASWA KUTOPOKEA ZAWADI AMBAZO ZITAHATARISHA MAISHA YAO

$
0
0
WASICHANA Mkoani Tabora wametakiwa kuwa na ujasiri wa kusema hapana pindi wanaposhaushiwa na wanaume kupokea zawadi kwa lengo la kuwataka wajiingize katika vitendo vya kujamiana ambavyo vinawaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vinavyosababisha UKIMWI.

Kauli hiyo imetolewa juzi wilayani Igunga  na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa maadhimisho ya UKIMWI Duniani ambapo kimkoa yalifanyika wilayani humo ambapo kauli mbiu ilikuwa Jamii ni chachu ya mabadiliko , tuungane kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.

Alisema wanapochukua  zawadi zenye hila na kupakizwa katika vyombo mbalimbali vya usafiri wanakuwa wamejiingiza katika mtego wa kudaiwa jambo ambalo litawaingiza katika vitendo vinavyo hatarisha maisha yao.

“Ukizoea kupokea zawadi na kupewa ‘rift’ za magari na pikipiki , ipo siku na wewe utaombwa ‘rift’ ndipo kitakuwa chanzo cha kujiweka katika hatari na kupata maambuzi ya UKIMWI na wakati mwingine kupoteza ndoto yako ya kupata elimu” alisisitiza.

Aidha Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliitaka jamii kuendelea kuzingatia ushauri na elimu wanayopata ya kujikinga na maambukizi mapya ya VVU kwa ajili ya kujikinga wao na familia zao na kuwa na jamii yenye afya njema.

Alisema maambukizi ya VVU yamekuwa na athari kubwa ya kiuchumi na hata watoto wengine wanalazimika kuacha masomo kwa ajili ya kuwahudumia wazazi wao na wengine kujiingiza katika utumikishwaji kwa sababu ya kutafuta fedha za kuwasaidia wadogo wao waliachwa na wazazi.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo alisema katika kukabiliana na kuenea kwa maambukizi mapya miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari wilayani humo amepiga marufuku sherehe za wanafunzi ambazo sio rasmi ambazo zinawachochea kufanya vitendo viovu.

Alisema kumezuka utaratibu ambao ni hatari kwa baadhi ya wanafunzi wanaohitimu Kidato cha Nne na Sita kuchangishana fedha na kukodi kumbi na vyumba kwa ajili kuwafanya sherehe ambayo hata walimu na wazazi hawana taarifa.

Mwaipopo alisema katika sherehe hiyo ambayo sio rasmi kuna vitendo hatari vinafanyika humo ambavyo vinaweza kuwasababisha kupata maambukizi ya VVU.
Baadhi ya wakazi wa Igunga mjini wakiwa wamejipanga mstari kwa ajili ya kuchunguza afya zao ikiwa sehemu ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani juzi ambapo kwa Mkoa wa Tabora imefanyika Igunga.
Mratibu wa Kifua Kikuu na UKIMWI wilaya ya Igunga, Dkt. Joachim Kabeya akitoa maelezo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (mwenye skafu) juu ya zoezi linaloendelea la upimaji Kifua mjini Igunga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani. Imeandikwa na TIGANYA VINCENT.

PAKA ALIYETEKA MITANDAO YA KIJAMII AFARIKI DUNIA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
Ni ajabu na nadra  kutokea katika jamii ya sasa kuona wanyama au ndege wakipata nafasi ya kutambulika kutokana na muonekano wa kuvavuta wengi, Lil Bub amevunja rekodi ya kuwa  mashuhiri hasa katika mtandao wa Instagram ambako amekuwa akifuatiliwa na wafuasi zaidi ya milioni mbili, Lil Bub amefariki akiwa na umri wa miaka nane, mmiliki wa Paka huyo Mike Bridavsky amethibitisha kupitia ukurasa wa Instagram wa Paka huyo na kueleza kuwa Lil alifariki akiwa usingizini.

Lil Bul ambaye aliwavuta wengi kwa muonekano wake wa kuwa na ulimi mdogo, picha zake pamoja na kutokuongezeka kimo jambo lililomfanya aendelee kuwa na muonekano mdogo na hiyo ilimfanya kuwa paka pekee kugundulika kuwa na tatizo hilo la homoni (dwarfism)

Wengi wamemwelezea Lil kuwa ni mtunzi, mtangazaji wa Televisheni na msemaji wa wanyama ulimwenguni.

Kupitia Lil Bub dola za kimarekani zipatazo 700,000 zilipatikana ili kuwasaidia wanyama wenye mahitaji maalumu kama yake.

MAKATIBU WAKUU SMT NA SMZ WAKUTANA ZANZIBAR

$
0
0
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Balozi John Kijazi (katikati) akifuatilia Kikao cha pamoja cha Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika katika ukumbi a zamani wa Baraza la Wawakilishi Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na kulia ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ Dkt. Abdulhamid Y. Mzee.
 Baadhi ya Makatibu wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) wakifuatilia kikao cha pamoja ana Makatibu wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 Makatibu wakuu kutoka Serikali Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wakiwa katika kikao cha pamoja na Makatibu wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) kilichoketi katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Katibu MKuu Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga akichangia katika kikao cha pamoja ana Makatibu wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika katika ukumbi wa Amani wa Baraza la Wawawilishi Zanzibar.

RAIS DK.SHEIN AZINDUA BOTI YA UVUVI YA KAMPUNI YA UVUVI ZANZIBAR (ZAFICO)

$
0
0
BOTI Mpya ya ya Uvuvi ya Sehewa ikiwa katika eneo la ufukwe wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikata Utepe kuashiria kuizindua Boti Mpya ya Kampuni ya Uvuvi Zanzibar (ZAFICO) hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar (kushoto kwa Rais) Naibu Waziri wa Kilimmo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar.Dkt. Makame Ali Ussi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Nahodha wa Boti ya Uvuvi ya Sehewa Ndg. Rashid Abdalla Rashid, akiada ya uzinduzi huo uliofanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Nahodha wa Boti ya Uvuvi ya Sehewa Ndg. Rashid Abdalla Rashid, akiada ya uzinduzi huo uliofanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Nahodha wa Boti ya Uvuvi ya Sehewa Ndg. Rashid Abdalla Rashid, akiada ya uzinduzi huo uliofanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza MKURUGENZI Mtendaji Kampuni ya Uvuvi ya Zanzibar (ZAFICO) Ndg.Zahor Kassim Mohamed, wakati akitembelea Boti hiyo ya Sehewa baada ya kuizindua leo katika ufukwe wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Zanzibar.Ndg. Mussa Aboud Jumbe, akionesha aina ya samaki watakaovuliwa na Boti hiyo ya Kisasa ya Uvuvi ya Sehewa wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Desemba 2, 2019. Katika ufukwe wa bahari ya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.(PICHA NA IKULU)

HASUNGA AZINDUA MASHINE YA KUKOBOA MPUNGA KIJIJINI MKINDO WILAYA YA MVOMERO

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb) akikagua mashine kukoboa mpunga katika kijiji cha Mkindo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Jana Tarehe 2 Disemba 2019. 
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizindua mashine ya kukoboa Mpunga katika kijiji cha Mkindo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ambayo ni moja ya mashine kubwa nne zilizonunuliwa na kusimikwa kupitia mradi huo, Jana Tarehe 2 Disemba 2019. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro

Serikali imelipongeza Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa-FAO, Serikali ya Venezuela, Halmashauri za Wilaya za Kilosa, Mvomero na Kilombero kwa utekelezaji wa mradi wa ubia wa maendeleo ya mifumo ya uzalishaji endelevu wa mpunga Afrika chini ya jangwa la Sahara.

Pamoja na majukumu mengine mradi huo ulikuwa na majukumu ya kuwafundisha vijana kilimo shadidi cha mpunga ambacho kinatumia mbegu kidogo zenye ubora na maji kidogo huku kikiwahakikishia wakulima mavuno zaidi.

Mradi huo pia ulitoa na kuwafundisha vijana kutumia zana za kilimo zenye kujali masuala ya jinsia, kurahisisha kazi na kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb) ametoa pongezi kwa taasisi hizo jana tarehe 2 Disemba 2019 wakati akizindua mashine ya kukoboa Mpunga katika kijiji cha Mkindo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ambayo ni moja ya mashine kubwa nne zilizonunuliwa na kusimikwa kupitia mradi huo.

Amesema kuwa lengo la serikali kwa kushirikiana na taasisi hizo ni kuhakikisha kuwa wakulima katika eneo hilo wanatunza ubora wa mazao yao na kupunguza upotevu wa mazao yao baada ya mavuno ikiwa pia ni kuyaongezea thamani ili kupata faida zaidi. 

Amesema kuwa Sanjali na jitihada hizo, Wizara ya Kilimo imeanzisha kitengo cha masoko ya mazao ya kilimo ambacho kinahusika na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi kwa mazao mbali mbali yanayozalishwa hapa nchini ili mbegu zitakazozalishwa na kuwa na mafanikio makubwa katika kilimo uweze kuimarisha kipato cha wananchi.

Takwimu zinaonesha kwamba wastani wa kitaifa wa matumizi ya zana bora za kilimo umeongezeka hadi kufikia asilimia 20 kwa matrekta na asilimia 27 kwa wanyama kazi ikilinganishwa na asilimia 14 ya matrekta na asilimia 24 ya wanyama kazi mwaka 2013. 

Amesema kuwa Kutokana na ongezeko hilo, matumizi ya jembe la mkono yamepungua na kufikia asilimia 53 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na asilimia 62 kwa mwaka 2013. Aidha, kupitia Mfuko wa Taifa wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) Wizara imeendelea kutoa mikopo ya pembejeo na zana za kilimo. 

Waziri Hasunga amesema kuwa mradi huo umekuwa ukitekeleza kwa vitendo Mkakati wa Kitaifa wa Kuwahusisha Vijana katika Kilimo wa mwaka 2016 pamoja na Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP-II), Sera na Miongozo mbalimbali ya kilimo hapa nchini. 

Alisema kuwa kupitia miongozo hiyo mbalimbali, Wizara ya Kilimo imeendelea kuratibu utekelezaji wa mikakati ya maendeleo ya kilimo hapa nchini kwa kuimarisha huduma za utafiti, upatikanaji na utumiaji wa pembejeo na zana za kilimo, udhibiti wa visumbufu vya mazao, huduma za ugani, uongezaji wa thamani na upatikanaji wa masoko. 

“Nafarijika kutambua kuwa vijana walionufaika na mradi huu pia walipata mafunzo ya kuongeza thamani kwa mavuno yao, ufikiaji na upatikanaji wa masoko ili kuweza kuuza mazao yao kwa faida” Alikaririwa Mhe Hasunga 

Alisisitiza kuwa zao la mpunga ni la pili kwa umuhimu hapa nchini linapokuja suala la chakula likifuatia kwa mahindi ambayo ndio zao kuu la chakula kwa Watanzania wengi. “Kama ilivyo kwa mazao mengine, Serikali imeweka mikakati kadhaa ya kuhakikisha uzalishaji wake unaongezeka. Kwa sasa nchi yetu inazalisha karibu asilimia mia moja ya mahitaji yetu ya mchele kwa mwaka tukiwa ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa mpunga Afrika baada ya Madagascar” Alisema 

Alisema kuwa kukosekana kwa miundombinu dhabiti ya umwagiliaji, zana na teknolojia duni, athari mabadiliko ya tabia nchi pamoja na mbegu zenye ubora hafifu ni miongoni mwa sababu zinazotuzuia tusizalishe zaidi na kwa tija, hivyo serikali imeweka msisitizo madhubuti katika kukabiliana nazo.

Serikali inaandaa sheria ya kulinda na kuhifadhi urithi wa Ukombozi wa Afrika

$
0
0
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza  akiangalia hanadaki lililotumiwa na Samora Mashel lililopo wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakati akitembelea maeneo ya historia ya Ukombozi wa Afrika.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akiwa ndani ya hanadaki lililotumiwa na Samora Mashel lililopo wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakati akitembelea maeneo ya historia ya Ukombozi wa Afrika.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza  akiongea na Mama Loisa Kamwaya (aliyevaa kilemba) akiwa miongoni mwa Watanzania walioolewa na Wanamimbia waliokaa Wilaya ya Kongwa mkoa wa Dodoma wakati wa kupingania uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratius Ndejembi.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza  akimsikiliza Mama Loisa Kamwaya (aliyevaa kilemba) akiwa miongoni mwa Watanzania walioolewa na Wanamimbia waliokaa Wilaya ya Kongwa mkoa wa Dodoma wakati wa kupingania uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratius Ndejembi (aliyevaa kaunda) akiongea na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza (wa pili kulia) wakati akitembelea maeneo ya historia ya Ukombozi wa Afrika wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. 
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akiwa ziara ya kikazi wilayani Kongwa kutembelea maeneo ya harakati za ukombozi wa Afrika katika sehemu ambayo ilitumiwa kwa kujifunzia kulenga shabaha.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akiangalia moja ya masalia ya mabomu yaliyotumiwa wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika eneo la Kongwa mkoani Dodoma.
 Moja ya masalia ya mabomu yaliyotumiwa wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika eneo la Kongwa mkoani Dodoma.
 Kaimu Afisa Utamaduni Obadia Ngole wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma akimuonesha Naibu Waziri wa Habari, Utamauni, Sanaa  na Michezo (wa kwanza kulia) eneo ambalo lilitumiwa na wapigania uhuru wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamauni, Sanaa  na Michezo akisaini kitabu cha wageni ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kongwa.
(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Kongwa)

Na Eleuteri Mangi, Kongwa
Serikali inaendelea kubainisha maeneo yaliyotumiwa na wapingania uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika ambayo yanasimamiwa kupitia Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika iliyopo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Akiwa katika ziara ya kikazi wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakati akitembelea maeneo ya historia ya Ukombozi wa Afrika, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema kuwa Serikali kupitia wizara hiyo inaandaa sheria ya kulinda na kuhifadhi urithi wa ukombozi wa Afrika unaopatikana nchini.

“Lengo kubwa ni kuhakikisha maeneo haya yanalindwa kisheria ili yaweze kutumika kama vivutio vya utalii wa kiutamaduni pamoja na utalii wa kihistoria kwa sababu huu ni urithi muhimu wa historia nzuri ya nchi yetu, haya ni maeneo yaliyotumika kusaidia ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika” alisema Naibu Waziri Shonza. 

Katika kutekeleza Programu ya Uhifadhi na Uendelezaji wa historia ya Ukombozi wa Afrika, Wizara inaendelea kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo, ukarabati wa jengo lililokuwa la Kamati ya Ukombozi ya iliyokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ambayo kwa sasa ni Umoja wa Afrika (AU).

Kazi nyingine ambazo Serikali imekamilisha ni uandaaji wa tovuti ya Programu, ubainishaji wa maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi, utambuzi wa nyaraka na vitu mbalimbali vinavyohusiana na harakati hizo pamoja na kufanya mahojiano na watu walioshiriki au kushuhudia harakati za ukombozi wa Afrika ambayo yamehifadhiwa kwa njia ya kidigitali.

Mji wa Kongwa kihistoria ni kitovu cha harakati za Ukombozi wa Afrika kwani harakati zote za mapambano ya kutafuta uhuru zilianzia Kongwa na baadaye zikaendelea katika maeneo mengine nchini kama sehemu ya kupanua wigo wa harakati hizo na huduma kwa Wapigania Uhuru.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Deogratius Ndejembi amesema kuwa Kongwa ni eneo kongwe lililotumiwa na Wapigania uhuru kutoka vyama mbalimbali vya Ukombozi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika.

Aidha, Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa eneo hilo lilitumika kwa ajili ya mafunzo kwa wapigania uhuru ambapo kwa sasa lina vielelezo muhimu vya kihistoria vilivyopo katika eneo hilo yakiwemo maeneo ya Handaki alilokuwa akilitumia Samora Mashel, nyumba za Makazi kwa wapigania uhuru, majengo ya shule ya sekondari Kongwa, eneo la Mafunzo ya kijeshi, kiwanja cha ndege na makaburi ya wapigania uhuru.

Maeneo mengine ya kihistoria ni makaburi ya mashujaa wa harakati za ukombozi ambayo jumla yake ni 11; makaburi matano ya wapigania uhuru kutoka Msumbiji, makaburi matatu ya wapigania uhuru kutoka Afrika Kusini na makaburi matatu ya wapigania uhuru kutoka Namibia.

Naibu Waziri Shonza yupo katika ziara ya kikazi kutembelea maeneo ya ya historia ya ukombozi wa Afrika katika mikoa ya Dodoma wilaya ya Kongwa, Morogoro wilaya Kilosa, Manispaa ya Morogoro pamoja na Mkoa wa Pwani wilaya za Chalinze na Bagamoyo. 

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII AWATAKA WATANZANIA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA UTALII

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda, akizungumza na watumishi wa Tanapa katika -Hifadhi ya Ruaha mkoani Iringa pamoja na watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani )waliohudhiria hafla ya Makabidhiano ya vifaa vya doria kutoka mradi wa REGROW kuimarisha Uhifadhi na Kukuza Utalii

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda koine mbali(darubini) kutazamia Wanyama.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Adolf Mkenda Akitoka kwenye moja hema katika Hifadhi hiyo ya Ruaha iliyopo mkoani Iringa.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda akikagua vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na mahema, mabegi, vifaa vya kukusanyia taarifa (camera, GPS), sare, magodoro, buti, vifaa maalumu vya kufanyia doria usiku na vinginevyo vyote vikiwa vimenunuliwa kupitia mradi wa REGROW.


Na Vero Ignatus, Ruaha
KATIBU Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda amewataka watanzania kuendelea kuwa sehemu ya mafanikio makubwa yanayofikiwa katika sekta ya utalii kwa kuwekeza kwenye sekta hiyo ambayo ina utajiri mkubwa wa rasilimali ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi kwa Taifa.

Prof. Mkenda ameyasema hayo wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 1.2 bilioni kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa wanyamapori katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Kwa Hifadhi nyingine zilizoko chini ya mradi wa REGROW.

Amesisitiza kuwa, ni vizuri kila mmoja kwa nafasi yake akaona umuhimu wa kushiriki kuitangaza nchi kupitia utajiri wa rasilimali iliyojaliwa kuwa nayo jambo ambalo litakuwa na mchango katika ukuaji wa sekta ya utalii na uchumi kwa ujumla.

Vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na Mahema, Vifaa vya kukusanyia taarifa (camera, GPS), sare, magodoro buti, vifaa maalumu vya kufanyia doria usiku na vinginevyo vimenunuliwa kupitia mradi wa REGROW.

Awali, Mratibu wa Mradi wa REGROW Saanya Aenea amesema serikali kupitia mradi huo imedhamiria kumaliza changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikabili hifadhi katika ukanda wa kusini mwa nchi na hasa eneo la miundombinu.

Hifadhi ya Taifa ya Ruaha inapatikana kwa sehemu kubwa mkoani Iringa na ni ya pili kwa ukubwa ikiwa na kilomita za mraba zaidi ya elfu 20

SPIKA ZANZIBAR AMNG’ATA SIKIO MWENYEKITI THBUB NA MBARAKA KAMBONA, ZANZIBAR

$
0
0
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Visiwani Zanzibar, Zubeir Ali Maulid amemueleza Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu kuwa kazi aliyopewa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ni kubwa na ngumu.

Spika Maulid alieleza hayo katika kikao kilichofanyika kwenye ofisi za Baraza la wawakilishi mapema  (Desemba 2, 2019) alipotembelewa na Mwenyekiti huyo.

Akiongea na Mwenyekiti huyo, Spika Maulid alisema kuwa kazi ya tume sio nyepesi, kwa kuwa ni miongoni mwa vyombo vinavyotegemewa katika kuleta amani na usalama wa nchi.

“Tume ni chombo kinachotegemewa kusaidia wananchi kupata haki zao, kutoa miongozo kwa jamii namna gani wanaweza kupata haki zao”alisema Maulid

Maulid aliendelea kusema kuwa usalama na amani iliyopo nchini ni kwa sababu ya uwepo wa taasisi kama tume ambazo zinasaidia kutatua kero za wananchi.

“Hichi ni chombo cha msaada mkubwa kwa nchi, kinachoweza kuona viashiria mbalimbali vya uvunjifu wa haki za binadamu na kuweza kuishauri serikali namna nzuri ya kudhibiti kabla ya mambo kuharibika”aliongeza

Kazi hii msiichukulie kwa wepesi, ni ngumu lakini inafanyika, ipeni umuhimu mkubwa ili muweze kuishauri vizuri serikali, nina imani na wewe mwenyekiti pamoja na wenzako kuwa mnao uwezo mkubwa wa kuifanya kazi hii na kufikia malengo tarajiwa, aliendelea kusema

Aidha, Spika Maulid alimueleza Jaji Mwaimu kuwa ofisi yake ipo tayari kumpa ushirikiano wowote atakaouhitaji na pale ambapo atakuwa na ushauri wowote awaeleze nao wataupokea.

“Tupeni ushauri pale mtakapoona kuna haja ya kufanya hivyo, na sisi tutawashauri, hii sio AZAKI, ni taasisi ya serikali hivyo fanyeni kazi zenu vizuri ili muendelee kusaidia wananchi”alisisitiza

Katika ziara hiyo, Jaji Mwaimu akiongozana na viongozi wenzake wa tume, alikutana pia na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omary Othman Makungu.
Mwenyekiti wa THBUB Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akiongea katika kikao kilichofanyika Desemba 2, 2019 katika ofisi za Baraza la Wawakilishi. Kulia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Visiwani Zanzibar, Zubeir Ali Maulid.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Visiwani Zanzibar, Zubeir Ali Maulid akiongea katika kikao baina yake na Mwenyekiti wa THBUB.
Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akisimama kutoa salamu za heshima alipokuwa akitambulishwa katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wakati kikao kinaendelea Desemba 2, 2019. Mwenyekiti alikuwa ni mgeni wa Spika.
Kamishna wa THBUB, Nyanda Shuli akiteta jambo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Visiwani Zanzibar, Zubeir Ali Maulid mara baada ya kikao.

Tanzania, Namibia zajidhatiti kukuza sekta ya biashara

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah wakisaini hati ya makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na biashara leo jijini Dar es Salaam

Serikali ya Tanzania na ya Namibia zajidhatiti kukuza na kuendeleza kiwango cha biashara na uchumi kwa kutumia rasilimali zinazopatikana kati ya mataifa hayo.

Makubaliano hayo yamefikiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah wakati wa kuhitimisha Mkutano wa pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Namibia jijini Dar es Salaam.

Prof. Kabudi amesema kuwa kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Namibia bado ni kidogo kikilinganishwa na fursa zilizopo, licha ya kiwango hicho kukuwa kutoka shilingi milioni 2,562.81 kwa mwaka 2010 hadi shilingi milioni 21,830.3 kwa mwaka 2018.

Kutokana na takwimu hizo, Prof. Kabudi amesema ni dhahiri kwamba mamlaka husika zinatakiwa kufanya jitihada za kutosha kwa kuhamasisha na kukuza uwekezaji baina ya nchi hizo. Aidha, pamoja na mambo mengine, Prof. Kabudi ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka Namibia kuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo, sekta ya mafuta na gesi, kilimo na biashara, viwanda vya dawa, ujenzi na utalii pamoja na uvuvi.

" Serikali ya Tanzania inafanya jitihada mbalimbali za kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ili kuhakikisha kuwa wawekezaji wanawekeza mahali salama. Jitihada hizo ni pamoja na utekelezaji wa blue print ambao unasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji" amesema Prof. Kabudi Ameongeza kuwa kutokana na jitihada hizo, ripoti ya Benki ya Rand Merchant ya Afrika Kusini imeonesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya saba (7) bora kwa uwekezaji kati ya nchi 52 za Afrika. Aidha, ripoti ya The African Index (AII) 2018 imeonesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 13 kati ya nchi 54 kwa kuwa na masoko na vivutio vya utalii.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah amesisitiza umuhimu wa ushirikiano na kwamba ushirikiano wa Namibia na Tanzania ni wa kindugu,kidiplomasia,kiuchumi na ni wa kudumu.

"Napenda kutumia fursa hii kuwasihi sana wafanya biashara kutoka nchini Namibia na Tanzania kushirkiana na kuona namna ya kukuza sekta ya biashara, utalii, kilimo, viwanda vya dawa, ujenzi pamoja na uvuvi kwani kupitia uwekezaji huo tutaweza kukuza kiwango cha mapato kati ya mataifa yetu," amesema Nandi-Ndaitwah.

katika mkutano huo, nchi hizo zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika Utamaduni, Sanaa na Michezo; Ushirikiano katika sekta ya Utalii pamoja na ushirikiano kwenye maendeleo ya vijana. Katika maeneo mengine, majadiliano yanaendelea na pande hizo mbili zimekubaliana hadi kufikia mwezi Machi 2020, Hati za Makubaliano ziwe zimesainiwa katika maeneo hayo.

Mkutano huo wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Namibia ulianza katika ngazi ya maafisa waandamizi wa Serikali na kufuatiwa na ngazi ya Makatibu Wakuu na kuhitimishwa na Mawaziri wa Mambo ya nje jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), akibadilishana hati ya makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na biashara na Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Namibia, Mhe. Netumbo Nandi- Ndaitwah wakisaini leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah wakionesha hati za makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na biashara mara baada ya kusaini hati hizo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasilisha hotuba yake wakati wa kuhitimisha Mkutano wa pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Namibia leo jijini Dar es Salaam. Wengine kulia ni Balozi wa Namibia nchini Tanzania Mhe. Theresia Samaria, Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko, (Mb) pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, (Mb).
Baadhi ya Makatibu wakuu, maofisa waandamizi, maofisa wa serikali pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa JPC leo jijini Dar es Salaam.

RC MARA AKAGUA MAENEO YALIYOATHIRIWA NA MVUA

$
0
0
Mvua hizo zilizosababisha kifo cha mkazi mmoja pia zilipelekea nyumba nyingi kuwa chini ya maji kwa muda wa siku ya Jumamosi Novemba 30 mwaka huu. 

Baada ya kufanya ziara hiyo ambapo aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mara, imebainika kuwa mafuriko hayo katika maeneo hayo yamechangiwa na ujenzi holela juu ya njia asili za maji ambapo pia imebainika kwamba ujenzi huo umefanywa kwa ridhaa ya baadhi ya watu katika nafasi za Mamlaka husika.

Mkuu wa Mkoa.ameagiza kwamba Viongozi wa Manispaa ya Musoma chini ya usimamizi wa Mkuu wa wilaya wafanye tathmini mara moja kubaini uzembe huo uliofanyika na wahusika na hatua stahili zichukuliwe.

Aidha.ametumia nafasi hiyo kuongea na wananchi na kuwasihi kuchukua tahadhari na taratibu za usalama wa maeneo yao. Amewakumbusha kutumia nafasi hiyo kumshukuru Mwenyezi Mungu kwamba maji hayo yalifurika saa za mchana na watu walipata nafasi ya kujiokoa, kwani kama maji hayo yangevamia maeneo hayo usiku wananchi wakiwa wamelala maafa yangekuwa makubwa sana.

39TH MEETING OF THE COUNCIL OF MINISTERS APPROVES CRUCIAL COTTON, TEXTILE AND APPARELS STRATEGY

$
0
0
East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania, 2nd December, 2019: The 39th Meeting of the EAC Council of Ministers has approved the Final Draft Cotton, Textiles and Apparels (CTA) Strategy and its Implementation Roadmap.

The strategy whose vision is to have “An integrated and globally competitive cotton, textiles and apparels industry,” makes a critical analysis of the CTA sector along the following key levels of the value chain: Cotton Seed (Production); Seed Cotton (Ginning); Cotton lint (Spinning); Yarn (Weaving/Knitting/Printing/Dyeing/Finishing), and; Fabrics (Garments/Apparels/Fabrication/Manufacturing) level.

The 39th Council which was chaired by Rwanda’s Minister of State for Foreign Affairs, Regional Cooperation and East African Community Affairs, Amb. Olivier Nduhungirehe, was attended by line Ministers from all the EAC Partner States and EAC Executives.

The Council further approved the Final Draft Leather and Leather Products Sector Strategy and its Implementation Roadmap. The Council which met at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania, further directed EAC Partner States to give priority to the implementation of the (CTA) and the Leather Products Sector Strategy.

In an effort to promote the textiles and apparels sector in East Africa, the Ministers directed Partner States to encourage sustainable procurement of all institutional uniforms, beddings, draperies by state institutions from textiles and fabric industries the region.

The Council directed the Sectoral Council on Agriculture and Food Security to develop a strategy to boost the production of cotton in the region.

In their deliberations, the Ministers observed that the seed cotton sector was constrained by low and declining production, low productivity, low quality and fluctuating farm gate prices. Textile mills were further constrained by outdated technology; low spinning capacity, availability of cotton lint, high cost of energy and low skill levels.

The Ministers were informed that inadequate supply of cotton lint forces millers to either buy or hold stock covering a one-year production cycle, or to shut down their production during off-seasons when they lack funds for bulk purchases.

The apparels sector on the other hand suffers mainly from low skills, low local market penetration by local producers and unfavourable trade practices particularly contraband and used clothes.

The EAC Strategy and Implementation Roadmap for Leather, Leather Products and Footwear Sector is a response to directive by the 19th Summit of EAC Heads of State held in 2018 concerning the promotion of the cotton, textile, apparel and leather industries in the region, with a view to making the region more competitive and creating jobs.

The Summit further directed the Council to implement the directive and put in place a mechanism that supports textile and leather manufacturing in EAC.

The strategy whose vision is to have “An integrated and globally competitive leather and leather products industry” makes a critical analysis of the sector along all other levels of leather and leather products value chain.

The Council referred the request for admission to the EAC from the Democratic Republic of Congo to the 21st Summit of the EAC Heads of State for consideration.

The Session had been informed that Chairperson of the Council had written to the EAC Secretariat on the request of the Democratic Republic of Congo to join the Community. The Council noted that Article 3 of the Treaty provides the matters to be taken into account by Partner States in considering the application by a foreign country to become a member of the Community.

On investment promotion within the region, the Council approved the Draft EAC Export Promotion Strategy 2020 – 2025 for implementation. The EPS 2020-2025 contains the following strategic interventions: Stimulate exports through acquired market intelligence for enterprises and improved visibility on international markets; Improve market access and conditions for EAC Export; Strengthen export competitiveness through interventions like improved access to finance and technology for enterprises, in particular SMEs, and; Strengthen the trade support institutions and partnerships. 

The Council was informed that 60 students from five Partner States had been awarded fully paid postgraduate scholarships under KFW scholarship programme tenable at various institutions of higher learning within the EAC from September this year.

The scholarship programme, an initiative of a Tripartite Financing Agreement between the Government of the Federal Republic of Germany (KFW), the EAC and Inter-University Council for East Africa (IUCEA) for a non-repayable grant of 5 million Euros, was signed in April 2018, with IUCEA being selected as the Project Executing Agency (PEA).

The programme’s objective is to enable poor and disadvantaged but academically gifted students pursue graduate studies in the EAC (so-called Change Agents) to foster regional integration. The scholarship programme supports postgraduate students in Mathematics, Engineering, Informatics, Science, Technology and Business Science programmes.

MAWAZIRI 12 WAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA VIWANDA KUTATUA KERO ZA WAWEKEZAJI

$
0
0

 Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angela Kairuki akizungumza  na waandishi wa habari wakati wa kutembelea kiwanda cha kuzalisha magunia Mkoani Morogoro.

 
 Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angela Kairuki akipata maelezo kutoka kwa meneja uzalishaji Benjamini Masinde baada ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha magunia Mkoani Morogoro

Mawaziri 12 kutoka wizara mbalimbali wamefanua ziara ya kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero zinazowakabili wawekezaji wa kada zote katika mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili mkoani Morogoro Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji Angela Kairuki amesema lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha migogoro hasa ya wananchi na wawekezaji pamoja na changamoto zinazowakabili wawekezaji zinafanyiwa kazi ,nyingine papo hapo na ambazo ni za kiujumla zitaenda kufanyiwa kazi na Mawaziri wote 12 na utatuzi utapatikana.

Baada ya mkutano huo na waandishi wa habari Mh Waziri aalitembelea baadhi ya viwanda zaidi ya 10 na kujionea hali halisi ya uzalishaji wa viwanda hivyo na kuzungumza na uongozi wake pamoja na kusikiliza changamoto zao.

Aidha amewaeleza watendaji wa umma kuwa wana deni kubwa la kuhakikisha wanawatumikia wananchi kikamilifu pamoja na kushughulikia changamoto za wafanyabiashara na wawekezaji ili kutekeleza majukumu yao bila vikwazo kwa maendeleo ya Taifa.

WATAALAMU WA MAABARA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUBORESHA MAABARA NCHINI

$
0
0
Wataalamu wa maabara nchini kutoka sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori, mifugo na mazingira wameipongeza serikali ya awam ya tano kwa jitihada zake za kuboresha maabara za sekta hizo kwa kuziwezesha kuwa na  vitenganishi, vifaa vya kisasa, teknolojia  na kuwajengea ujuzi wataalam hao ili kuweza kufanya utambuzi na uchunguzi ndani ya maabara.

 Akiongea wakati wa mkutano wa mwaka wa Mtandao wa wataalam wa maabara nchini (LABSNET),Jijini Arusha,  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara ya Vetenari Tanzania, Dkt. Furaha Mramba amefafanua kuwa kutokana na jitihada za serikali katika kuimarisha kuboresha utendaji wa maabara nchini, tayari maabara za hapa nchini zinao uwezo wa kutambua magonjwa yote yanayowapata mifugo lakini pia na magonjwa yanayowapata binadamu.

“Zamani tulikuwa tunapeleka sampuli nje ya nchi hususani katika nchi ya Kenya na katika nchi ya Afrika kusini, lakini miaka ya hivi karibuni kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na serikali katika kuboresha utendaji wa maabara tulizonazo, tayari tunazo maabara za rufaa ambazo zinauwezo mkubwa wa kufanya utambuzi na uchunguzi wa magonjwa” Amesisitiza Dkt. Mramba.

Dkt. Mramba ameongeza kuwa lengo la kukutana kwa wataalam wa maabara nchini kutoka katika sekta zote za Afya ni kujadiliana na kuona mbinu bora za kufanya uchunguzi na kutambua kwa wepesi na kwa  haraka magonjwa kabla hayajaleta madhara makubwa kwa mifugo na binadamu. Amefafanua kuwa katika mkutano huo wameshiriki wadau wa maendeleo katika sekta ya maabara kutoko Marekani na Finland.

“Tunapokutana na wadau hawa ambao hutufundisha teknolojia za kisasa za maabara na hutupatia vifaa vyenye uwezo mkubwa wa utambuzi wanaweza kujua ni teknnolojia gani tunaihitaji kwa sasa na maabara gani zinahitaji kujengewa uwezo katika uchunguzi na utambuzi. Wadau hawa kwa jinsi wanavyo unga juhudi za serikali ndio maana sekta ya maabara hapa nchini  imekuwa bora” Amesema Dkt. Mramba.

Kwa upande wake Mratibu kutoka Finland wa Mradi unaotekelezwa hapa nchini wa Kuimarisha Afya na Usalama katika Maabara kwa kujenga uwezo wa Utambuzi, Dkt.Lina Voutilainen, amebainisha kuwa wamekuwa wakiunga  mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuboresha utendaji wa maabara nchini kupitia Wakala wa Maabara ya Vetenari Tanzania kwa kuwajengea uwezo wataalam wa maabara na kuwapatia vifaa vyenye uwezo mkubwa wa utambuzi na uchunguzi wa magonjwa.

“Tayari kupitia Wakala wa Maabara ya Vetenari Tanzania tumetoa vifaa  sita  vya QPCR vinavyohamishika kwa maabara zake za kanda ya Mwanza, Arusha na Iringa, Tutaendelea kutoa vifaa hivyo vya kisasa na vitenganishi pamoja na kuendelea kuwajengea uwezo wataalam wa maabara katika kipindi tutakachotekeleza mradi huu hadi 2023 ” Amesisitiza Voutilainen

Naye,  Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Uchunguzi, kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Alex Magesa, amefafanua kuwa katika kuhimarisha Huduma za uchunguzi imebainika kuwa usugu wa vimelea dhidi ya dawa ni changamoto kubwa hivyo tayari serikali imeandaa mpango mkakati wa kukabiliana na changamoto hiyo ambapo wafamasia na wanafuzi  na jamii kwa ujumla wanahusishwa katika kukabili changamoto hiyo.

Mkutano huo ulioratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja, uliwakutanisha wataalam wa maabara hao kwa kuzingatia dhana ya Afya moja ambayo ni wataalam wa maabara kutoka sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara ya Vetenari Tanzania, Dkt. Furaha Mramba akifafanua umuhimu wa kuwa na maabara zenye uwezo wa uchunguzi na utambuzi wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara waliokutana kwa kutumia dhana ya Afya  moja  inayojumuisha  sekta za Afya ya Binadamu , Wanyamapori, Mifugo na mazingira, jijini Arusha.
 Mratibu wa Mradi wa Kuwezesha Maabara nchini kutoka Finland, Dkt. Mika Aho , akifafanua umuhimu wa mradi huo katika kuimarisha maabara kwenye uchunguzi na utambuzi wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara waliokutana kwa kutumia dhana ya Afya  moja  inayojumuisha  sekta za Afya ya Binadamu , Wanyamapori, Mifugo na mazingira, jijini Arusha.
 Baadhi ya Wataalam wa Maabara kutoka nchin Marekani na Kutoka hapa nchini wakifuatilia mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara waliokutana kwa kutumia adhana ya Afya  moja  inayojumuisha  sekta za Afya ya Binadamu , Wanyamapori, Mifugo na mazingira, jijini Arusha.
 Mratibu wa Mradi wa Kuwezesha Maabara nchini kutoka Finland, Dkt.Lina Voutilainen, akifafanua umuhimu wa mradi huo katika kuimarisha maabara kwenye uchunguzi na utambuzi wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara waliokutana kwa kutumia dhana ya Afya  moja  inayojumuisha  sekta za Afya ya Binadamu , Wanyamapori, Mifugo na mazingira, jijini Arusha.
 Mtaalam wa Maabara kutoka sekta ya mifugo akifafnunua umuhimu wa kutumia Dhana ya Afya moja katika kuimarisha na kuboresha utendajiwa maabara nchini wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara waliokutana kwa kutumia dhana ya Afya  moja  inayojumuisha  sekta za Afya ya Binadamu , Wanyamapori, Mifugo na mazingira, jijini Arusha.
 Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Uchunguzi  wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Alex Magesa akifafnunua umuhimu wa kutumia Dhana ya Afya moja katika kuimarisha na kuboresha utendajiwa maabara nchini wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara waliokutana kwa kutumia dhana ya Afya  moja  inayojumuisha  sekta za Afya ya Binadamu , Wanyamapori, Mifugo na mazingira, jijini Arusha.
 Baadhi ya Wataalam wa Maabara kutoka sekta ya Afya ya Binadamu ,Wanyamapori na Mifugo wakifuatilia mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara waliokutana kwa kutumi dhana ya Afya  moja  inayojumuisha  sekta za Afya ya Binadamu , Wanyamapori, Mifugo na mazingira, jijini Arusha.
 Mtaalam wa Maabara kutoka nchiniMarekani, Dkt. Saindon, akifafanua umuhimu wa mradi huo katika kuimarisha maabara kwenye uchunguzi na utambuzi wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara waliokutana kwa kutumia dhana ya Afya  moja  inayojumuisha  sekta za Afya ya Binadamu , Wanyamapori, Mifugo na mazingira, jijini Arusha
 Mtaalam wa maabara kutoka Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Jacob Lusekelo akifafanua umuhimu wa kuwa na maabara zenye uwezo wa uchunguzi na utambuzi wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara waliokutana kwa kutumia dhana ya Afya  moja  inayojumuisha  sekta za Afya ya Binadamu , Wanyamapori, Mifugo na mazingira, jijini Arusha.
 Baadhi ya Wataalam wa Maabara kutoka sekta ya Afya ya Binadamu ,Wanyamapori na Mifugo wakifuatilia mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara waliokutana kwa kutumia dhana ya Afya  moja  inayojumuisha  sekta za Afya ya Binadamu , Wanyamapori, Mifugo na mazingira, jijini Arusha.
 Mtaalam wa maabara sekta ya Afya, Charles Masambu akifafanua umuhimu wa kuwa na maabara zenye uwezo wa uchunguzi na utambuzi wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara waliokutana kwa kutumia dhana ya Afya  moja  inayojumuisha  sekta za Afya ya Binadamu , Wanyamapori, Mifugo na mazingira, jijini Arusha.
 Washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa Maabara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa  mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara waliokutana kwa kutumia dhana ya Afya  moja  inayojumuisha  sekta za Afya ya Binadamu , Wanyamapori, Mifugo na mazingira, jijini Arusha. 

WAZIRI LUKUVI AWATAKA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KUJITATHMINI KATIKA UTOAJI HATI ZA ARDHI

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM IRINGA
Waziri wa Adhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuanza kujitathmini katika idadi ya hati za ardhi wanazotoa kwa wamiliki wa ardhi kwenye halmashauri zao.

Alisema Wizara yake itaanza kutangaza wilaya itakayoongoza katika Upangaji, Umilikishaji na Utoaji Hati za ardhi kwa wananchi ili kubaini hamashauri ambazo ziko nyuma katika kutoa hati za ardhi kwa wananchi.

Lukuvi alisema hayo jana katika mkutano wake wa kusikiliza na kutatua kero za ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Iringa kupitia programu ya Funguka kwa Waziri uliyofanyika ukumbi wa Siasa ni Kilimo katika Manispaa ya Iringa,

‘’Mkurugenzi ajione fahari kuwaezesha wananchi kwa kupima na kuwapatia hati, kama Mkurugenzi huwezi kutoa hati miliki hata mia moja basi wewe hufai’’ alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, kumilikisha na kumpatia mwananchi hati ya ardhi ni kumuwezesha kiuchumi kwa kuwa anaweza kuitumia hati kwenye shughuli za kimaendeleo na kusisitiza kuwa wakurugenzi wa halmashauri wahakikishe wanapanga na kuwamilikisha maeneo wananchi.

Aidha, Lukuvi alisema kwa sasa wizara yake imejipanga kuhakikisha inasogeza huduma za ardhi karibu na wananchi kwa kuanzisha ofisi za mikoa zitakazokuwa na watendaji wote wa sekta ya ardhi kama vile Wapimaji, Wathamini, Wataalamu wa Mipango Miji pamoja na Wasajili.

‘’Sasa Wapimaji, Wathamini na Wapangaji watakuja hapa Iringa, muundo unaanza mwezi ujao lengo ni kuwapunguzia usumbufu wananchi katika kupata huduma za ardhi’’ alisema Lukuvi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, katika kuboresha huduma za sekta ya ardhi, Wizara yake itatumia mifumo unganishi itakayorahisisha utendaji kazi kwa wataalamu wa sekta ya ardhi ambapo kazi kubwa itakuwa ikifanyika kielektroniki badala ya kutumia makaratasi aliyoaeleza kuwa wakati mwingine husababisha tamaa kwa maafisa ardhi.

Alitolea mfano mkoa wa Dar es Salaama kuwa, ushaanza kutumia mfumo unganishi ambapo sasa wamiliki wa ardhi katika mkoa huo wanapatiwa hati za kielectroniki na kubainisha kuwa lengo la kuwa na mfumo unganishi ni kuondoa urasimu na kurahisisha utendaji kazi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi alieleza kuwa mkoa wake umejitahidi kupunguza kero na migogoro ya ardhi iliyokuwepo miaka ya nyuma kwa kuanzisha utaratibu wa kuwafuata wananchi kwenye maeneo yao kupitia programu ya Iringa Mpya.

Alimueleza Waziri Lukuvi kuwa, kama angekuja mwaka mmoja na nusu uliopita basi ukumbi aliofanyia mkutano wa Funguka kwa Waziri ungekuwa umejaa wananchi wenye kero za ardhi lakini jitihada za mkoa wake zimesababisha mkutano huo kutokuwa na idadi kubwa ya wananchi wenye migogoro ya ardhi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

‘’Muda mwingi nautumia kwenda kwa wananchi na kazi za ardhi zina changamoto kubwa na njia pekee ya kukabiliana nazo ni kutenda haki bila kujali uwezo, kabila ama dini ya mtu’’ alisema Hapi.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela (Kushoto) wakati wa mkutano wa kusikiliza kero za ardhi kwa wananchi wa Iringa kupitia programu ya Funguka kwa Waziri katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo uliopo Manispaa ya Iringa jana. Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi.
Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Iringa waliojitokeza kuwasilisha kero za ardhi kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kupitia programu ya Funguka kwa Waziri katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Siasa ni Kilimo uliopo Manispaa ya Iringa jana.
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akisisitiza jambo kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi baada ya mkutano wa kusikiliza kero za ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Iringa kupitia programu ya Funguka kwa Waziri jana. 
Baadhi ya akina mama wa mkoa wa Iringa waliojitokeza kuwasilisha kero za ardhi kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kupitia programu ya Funguka kwa Waziri katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Siasa ni Kilimo uliopo Manispaa ya Iringa jana.(PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

UJENZI WA MKEKA MPYA WA BAMAGA MPAKA SHEKILANGO WAENDELEA KWA KASI

$
0
0
Upanizu wa barabara ya Bamaga - Shekilano umeana na kuendelea kwa kasi kama kamera ya Globu ya Jamii ilivyoweza kuzinasa taswira kadhaa wakati ujenzi huo ukiendelea. Pichani ni katapila likiwa katika zoezi la kusawazisha vifusi vilivyomwagwa barabarani hapo mchana wa leo. Barabara hii ina urefu wa kilomita 3.7 Picha na Emmanuel Massaka.

Muonekano wa Barabara ya Shekilango inayoendela kujengwa.

Joshua vs Andy Ruiz Jr kukosa Boxing Ring Girls

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kutokana na tamaduni za nchi ya Saudi Arabia, Pambano la ngumi kati ya Antony Joshua na  Andy Ruiz Jr hakutakuwa  wasichana (Boxing Ring Girls) wanaopita kuonyesha raundi kila linapotaka kuanza.

Pambano hilo litakalofanyika Jumamosi usiku Disemba 7,  kwa mara ya kwanza hakutakuwa na wale wasichana wanaopita kuonyesha raundi kila inapotaka kuanza.

Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na kuheshimu utamaduni wa Saudi Arabia, ambao sheria zao zinakataza wanawake kujitokeza hadharani wakiwa na mavazi yanayoonyesha mwili wao.

Joshua atakuwa na hamu kubwa ya kupata ushindi jijini Diriyah baada ya Ruiz kushangaza ulimwengu wa ngumi Juni mwaka huu kwa kumchapa Muingereza huyo katika raundi ya saba kwenye Ukumbi wa Madison Square Garden.

Mwanzoni ilikuwa inaonekana Joshua na Ruiz wangepigania Cardiff kabla ya Saudi Arabia kunyakuwa pambano hilo. Joshua, tayari amewasili Saudia kwa lengo la kumalizia mazoezi yake ya mwisho kuelekea katika pambano hilo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA MACHINJIO YA KISASA-VINGUNGUTI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati akiwasili kwenye Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa, Vingunguti jijini Dar es Salaam, Desemba 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mshauri wa Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa Vingunguti, Henry Mwoleka, wakati alipokagua mradi huo, Desemba 3, 2019, jijini Dar es Salaam. 
 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa, yaliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, Desemba 3, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifafanuliwa Mkandarasi wa Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa Vingunguti, Mhandisi Elisante Ulomi, wakati alipokagua mradi huo, Desemba 3, 2019, jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua Machinjio ya zamani yaliyopo Vingunguti, baada ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa, jijini Dar es Salaam, Desemba 3, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Afisa Mfawidhi wa Machinjio Vingunguti, Jihadhari Mgeni, wakati alipokagua machinjio hayo, Desemba 3, 2019, jijini Dar es Salaam. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akioneshwa jambo na Afisa Mfawidhi wa Machinjio Vingunguti, Jihadhari Mgeni, wakati alipokagua machinjio hayo, Desemba 3, 2019, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kukagua Machinjio ya zamani yaliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, baada ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa Vingunguti, Desemba 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JAMII IMETAKIWA KUACHANA NA BIASHARA HARAMU ZA MADAWA YA KULEVYA NA KUGUSHI NYARAKA ZA SERIKALI

$
0
0
Na Farida Saidy, Morogoro 
Jamii imetakiwa kuachana  na biashara haramu za madawa ya kulevya na kugushi  nyaraka za serikali badala yake kufunya  shughuli halali ambazo zinaweza kuwaingizia kipato hususani katika kipindi hiki cha kuelekea katika sikukuu za mwisho wa mwaka

Lai hiyo imetolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro wilboad William Mtafungwa ofisini kwake, baada ya watu tisa kukamatwa kwa makosa tofauti yakiwemo kusafirisha madawa ya kulevya aina ya bhangi na kugushi nyaraka za serikali pamoja na wizi wa thamani za dani zikiwemo runinga.

Jeshi la polisi mkoa wa morogoro tunawashikilia watu tisa kwa matukio mbalimbali ya uharifu pia tumefanikiwa kukamata bhangi gunia 6, kg 6 na kete 50 ya bhangi, roli lililokuwa likisafirisha bhangi, TV 08, Computer 02 na pia tunaendelea na uchunguzi wa matukio mbalimbali ya jinai yaliyojitokeza alisema kamanda mtafungwa. 

Aidha amesema kuwa mnamo tarehe  30/11/2019 majira ya 00:30 katika kijiji cha dala kata na tarafa ya mvuha askari polisi wakiwa doria wamefanikiwa kuwakamata wasafirishaji bhangi kwa kutumia roli aina ya fuso lenye namba T.671 CPM.

Amesema Wasafirishaji hao ni Respice Joachimu deleva wa gali, Iddi Boga utingo wa gali hilo, Abdalla Azizi bodaboda wote wakiwa wakazi wa manispaa ya morogoro,ambapo walisafilisha bhangi hizo ndani yake kukiwa na mfuko wa pumba za mpunga.

Katika hatua nyingine kamanda Mtafungwa amesema kuwa wanamshikilia  mkurugenzi wa kampuni ya MOROSIGN, Bwana omari Kassim Mataka na Bwana Mussa Salim Mshana afisa masoko wa kampuni ya SUPER TECH ENTERPRISES   kwa kosa la kukutwa na vifaa vya kugushi nyaraka serikali zikiwemo za TRA na TANESCO

Hata hivyo  kamanda mtafungwa amewataka watanzania kuachana na imani za kishirikina baina yao badala yake kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pale wanapoona kunawalakini katika jamii.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images