Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Mloganzila yapewa msaada wenye thamani ya Tsh. Milioni 10

$
0
0
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi
akikabidhiwa hati ya msaada wenye thamani ya milioni 10 uliotolewa na Benki ya NMB PLC, kulia ni Meneja wa Benki hiyo Tawi la Kibaha Bw. Hosea Lyatuu.
Mkuu wa Idara ya Huduma za Ukunga, Afya ya Uzazi Mama na Mtoto MNH-
Mloganzila Bi. Christina Mwandalima (kushoto) akiishukuru NMB kwa msaada huo, katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. Mohamed Mohamed.
Bw. Hosea Lyatuu (wa pili kulia) akizungumza na uongozi wa Hospitali ya
Mloganzila wakati akikabidhi msaada kwa niaba ya Benki ya NMB.
Baadhi ya viongozi wa MNH-Mloganzila wakiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa NMB mara baada ya kukabidhiwa msaada.
Vitanda 10, magodoro 10 na strecha mbili zilizokabidhiwa hospitalini hapa naBenki ya NMB.

*********************************

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imepokea msaada kutoka Benki ya NMBwenye thamani ya Tsh. Milioni 10 ambao unalenga kuunga mkono juhudi zaserikali za kuboresha huduma za afya nchini.

Akikabidhi msaada kwa niaba ya Benki ya NMB PLC, Meneja wa Benki hiyo tawila Kibaha, Bw. Hosea Lyatuu ametaja msaada huo ni vitanda 10, magodoro 10pamoja na strecha mbili ambapo ameeleza kuwa NMB imekuwa ikitoa misaadakatika sekta tatu ikiwemo elimu na afya kwa lengo la kuisaidia jamii.

“Tumeamua kutoa msaada huu katika hospitali ya Mloganzila ili kuhakikisha kuwa kuna vitanda vya kutosha kwa ajili ya kutoa huduma za afya na benki yetu hufanya hivi ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii,” amesema Bw. Lyatuu.

Bw. Lyatuu amefafanua kuwa wanatambua mchango unaotolewa na watoa
huduma za afya hivyo wameamua kutoa msaada katika sekta hii ili kuhakikishajamii inapata huduma pasipo shida yoyote.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo ambao utaongeza idadi ya vitanda vitakavyotumika kwa ajili ya kutolea huduma hospitalini hapa.

“Tunawashukuru kwa msaada huu kwani umekuja wakati muafaka wakati hospitali hii inajikia katika kuanzisha huduma mpya hivyo tunatumaini NMB mtaendelea na juhudi hizi kwani hospitali yetu bado inahitaji msaada wenu kwa lengo la kuhudumia jamii,” amesema Dkt. Magandi.

WAZIRI MWAKYEMBE ATUMA SALAMU ZA POLE KWA MKUU WA MKOA WA TANGA KUFUATIA VIFO VYA MASHABIKI WA BONDIA HASSAN MWAKINYO

Mkoa wa Mara Wajivunia Mafanikio Miaka 4 ya Serikali ya Awamu ya Tano

$
0
0
Serikali ya Awamu ya Tano imeuwezesha mkoa wa Mara kujenga Hospitali 4 za Wilaya, Vituo vya Afya 13 kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Akizungumza katika kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Malima amesema mkoa huo umepiga hatua kubwa katika kuimarisha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo sekta ya afya kutokana na kutekelezwa kwa ujenzi wa miundombinu ya sekta hiyo kwa ufanisi.

“Mradi wa Hospitali ya Kanda ya Mwalimu Nyerere unaendelea vizuri na utawezesha wananchi kupata huduma za kibingwa ikiwemo za mifupa na nyingine hali itakayoondoa adha ya wananchi kusafiri hadi Hospitali ya Bugando kufuata huduma hizo” Alisisitiza Malima.

Akifafanua amesema kuwa mkoa huo umepata mafanikio makubwa katika sekta nyingine kama vile elimu kwa kujenga miundombinu ya kisasa yakiwemo madarasa na maabara hali iliyochangia kukua kwa kiwango cha elimu katika mkoa huo ikilinganishwa na miaka iliyotangulia kabla ya uwekezaji huo.

Kwa upande wa sekta ya madini amesema kuwa kuwepo kwa sheria nzuri na taratibu zilizowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano, mkoa huo umezalisha kilo 130 za dhahabu kufikia Septemba mwaka huu hali inayochangia kukuza sekta ya madini na uchumi kwa ujumla.

Akizungumzia mikakati yake ya kukuza kilimo na uvuvi, Mhe. Malima amesema kuwa dhamira ya mkoa huo ni kuona sekta hizo zinatoa mchango stahiki katika uchumi kutokana na hatua zilizochukuliwa katika kokomesha uvuvi haramu katika mkoa huo.

Aidha, Mhe. Malima amebainisha kuwa wamejipanga kukuza sekta ya utalii katika mkoa huo ili kuongeza pato la mkoa huo hatua itakayowasaidia kuwainua wananchi kiuchumi na Taifa kwa ujumla.

Kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ kinarushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kuratibiwa na Idara ya Habari MAELEZO ambapo awamu hii inawashirikisha wakuu wa mikoa yote Tanzania Bara.

SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI MKUTANO WA VIONGOZI KUHUSU FAMILIA YENYE BARAKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waheshimiwa Wabunge, wageni waalikwa wakati wa Mkutano wa Viongozi kuhusu familia yenye baraka tukio lililofanyika leo katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akionyesha tuzo maalum ya udumishaji wa amani aliyopatiwa leo katika Mkutano wa viongozi kuhusu familia yenye baraka tukio lililofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Universal Peace Foundation Bara la Afrika, Rev. Bakary Camara na kushoto ni Mbunge wa Sengerema, Mhe. William Ngeleja



Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akizungumza na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum (kushoto) walipokutana leo katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam. Kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Viongozi kuhusu familia yenye baraka, Wa pili kushoto ni Mbunge wa Igagula, Mhe. Mussa Ntimizi na Mbunge wa Sengerema, Mhe. William Ngeleja.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

DAWASA WASHIRIKI MBIO ZA KIGAMBONI MARATHON, YAWAKARIBISHA WANANCHI KUJIUNGA NA HUDUMA YA MAJI KWA MKOPO

$
0
0
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)  Neli Msuya (kushoto) akiwa moja ya washiriki wa mbio za Kigamboni International Marathon zilizofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA wameshiriki katika mbio za Kigamboni International  Marathon na kuwataka wananchi wajiunge na huduma za maji safi.

Dawasa katika mbio hizo wamewaomba wananchi wa Mkoa wa Kihuduma Kigamboni kujiunga na huduma ya maji safi.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Dawasa Neli Msuya amesema kwa sasa wameanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi ambapo miradi ya Dawasa imepita kwenye mitaa ya Gezaulole, Kizani, Mbwamaji, Vijibweni kata ya uzunguni.

"Tumefungua mkoa wa kihuduma Dawasa Kigamboni ambapo kuna miradi ya maji imeanza kutoa huduma kwa wananchi wa maeneo mbalimbali na mingine ikiwa bado inaendelea na ujenzi,"amesema Neli.

Amesema, kwa sasa ofisi za Dawasa zinapatikana kwenye bustani ya Gezaulole na utaweza kupata taarifa za namna ya kuunganishiwa huduma ya maji.

"Utakapofika kwenye ofisi zetu zilizopo Bustani ya Gezaulole utajaza fomu ya kuomba huduma ya maunganisho mapya  na ndani ya siku saba utapatiwa taarifa ya siku ambayo fundi atakuja kufanya usanifu na utaunganishiwa maji kwa mkopo,"

Mamlaka Dawasa imekuwa inatekeleza ahadi ya rais ha kufikia asilimia 95 ya watumiaji wa maji kwa mwaka 2020 na mpaka kufikia sasa asilimia 85 ya wakazi wa Dar es Salaam wanapata maji safi kutoka Mtambo wa Ruvu Chini, Ruvu Juu na  Visima virefu.
 Meneja wa DAWASA Mkoa wa kihuduma Tegeta Boniface Philemon (katikati) akiwa na Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Kinondoni Christian Kaoneka (kushoto) wakati wa Kigamboni International Marathon 2019 Km 10 zilizofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakishiriki mbio za Kigamboni International  Marathon zilizofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakishiriki mbio za Kigamboni International  Marathon zilizofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA Neli Msuya akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo baada ya kumaliza mbio za Kigamboni International Marathon 2019 zilizofanyika leo Jijini Dar
Meneja wa DAWASA Mkoa wa kihuduma  Tegeta Bonifave  Philemon (kushoto) akiwa na Meneja wa DAWASA Mkoa wa  Kihuduma Kinondoni Christian Kaoneka (kulia) pamoja na Mhandisi wa Mkoa wa Kihuduma Ilala Sirila  Josephat Baada ya kumaliza mbio za Kigamboni International Marathon 2019 Km 10 zilizofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa DAWASA akigawa vipeperushi vyenye miradi mbalimbali ya Mamlaka hiyo kwa  washiriki wa Mbio za Kigamboni International Marathon 2019 baada ya kumalizika kwa mbio hizo leo Jijini Dar.

Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Vyuo Vikuu Afrika Mashariki chazinduliwa nchini Uganda

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Dkt. Aziz Ponary Mlima akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Vyuo Vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA), uliofanyika jana tarehe 30 Novemba 2019, katika Chuo Kikuu Cha Ndejje, kilichopo Luwero nchini Uganda.

Tukio hilo lilihudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria wa Uganda,  Jenerali Kahinda Otafiire, Jenerali Salim Saleh, Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo Prof. Semakula Kiwanuka, Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Eriabu Lugujjo. Zoezi hilo pia lilihudhuriwa na Prof Aldin Mutembei kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. 

Katika hotuba ya aliyoitoa Balozi Aziz P. Mlima, alizungumzia mchango wa Mwalimu Julius Nyerere kwa harakati za ukombozi wa Afrika kusini na Uganda na mchango wa Kiswahili kwa umoja wa kitaifa.

Prof. Aldin Mutembei alizingumzia maendeleo ya lugha ya Kiswahili kama moja ya lugha adhimu katika umoja wa nchi za kiafrika na jinsi kiswahili kinavyoweza kutumika bila kudhoofisha lugha zingine za kiasili. 

Jenerali Kahinda Otafiire alimwakilisha Rais Yoweri Museveni kwenye mdahalo huo.

Wanafunzi na uongozi wa Chawakama kutoka Chuo Kikuu cha Makerere walishiriki katika uzinduzi na mdahalo huo.

WASANII MAARUFU NCHINI WAJIPANGA KUTANGAZA UTALII WA NDANI.

$
0
0

Na Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.
Jumla ya Wasanii wapatao Saba wanaendelea na ziara yao ya kutembelea Baadhi ya Hifadhi za Taifa hapa Nchini, lengo ikiwa ni sehemu ya kujionea Vivutio katika Hifadhi hizo ili kuendelea kuzitangaza na kuhamasisha wageni na wenyeji kufika Nchini kwetu kwa ajili ya kufanya Utalii.
Ziara hiyo iliyoanzia katika Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato, mara baada ya Uzinduzi wa Hifadhi za Taifa za Ibanda - Kyerwa na Rumanyika Karagwe, ikiongozwa na Waziri mwenye dhamana Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangala (MB), pamoja na wasanii wa Muziki na  Maigizo  (Bongo Movie) ambao ni Steve Nyerere, Dude, Richie, Shilole, Ebitoke,  Shetta huku kutoka Visiwa vya Zanzibar wakiwakilishwa na Msanii wa Muziki AT.
Wakiwa Katika Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato, wamejionea wanyama mbali mbali kama Twiga, Swala, Pundamilia, na Pofu, Wasanii hao baada ya kufanya Game Drive pamoja na matembezi ya Miguu (walking safari)wamekiri kufurahishwa na mandhali nzuri ya Hifadhi ya Burigi - Chato, kwa kujionea uzuri wa ziwa Burigi, huduma nzuri na ukarimu kutoka kwa wahifadhi, na zaidi huduma ya Malazi na mapumziko kwenye mahema mazuri ya kisasa ya Mwekezaji wa kwanza katika hifadhi hiyo aitwae Wilbard Chambulo.
Kumalizika kwa Ziara hiyo katika Hifadhi hiyo ya Burigi - Chato, na kuelekea katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo ambapo huko wamefanya utalii wa kwenye Maji kwa kutembelea maeneo mbalimbali, huku wajionea Viboko, Mamba,  na Ndege wazuri wa kila aina, akiwemo Ndege aina ya Conorad wenye uwezo wa Kusafiri kwa kuhama kwenda Ulaya na kurudi, lakini zaidi wakipata nafasi ya kufanya Utalii wa Uvuvi (Sport Fishing).
 Twiga hifadhini Burigi
 Msanii Steve Nyerere akionekana m wenye wasiwasi wakatiu wa game drive. Ni hadi wahifadhi walipomhakikishia kwamba wanyama hawana nongwa na binadamu ndipo akatulia...
Twiga anayepatikana ndani ya Burigi - Chato, ambae kwa mujibu wa Steve Nyerere, amedai amemsikia akiongea kingereza.... 
Pundamilia wakionekana kufurahia baada ya kuwaona (bure) wasanii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya  Burigi - Chato. 
 Tumbili akimshangaa msanii JB
Kambi ya kitalii ya Mahema mazuri na ya kisasa ya Mwekezaji wa kwanza katika hifadhi ya Taifa ya Burigi aitwae Wilbard Chambulo.
 Ndege aina ya Conorad mwenye uwezo wa kusafiri kutoka Ulaya au kwenda kulingana na msimu wa hali ya hewa, akiwa ametulia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Rubondo


Wasanii wakiwa wameongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala katika matembezi ya Kitalii (walking) Mara baada ya kuwasili katika hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato

 Wasanii wakiwa wameongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala katika matembezi ya Kitalii (walking) Mara baada ya kuwasili katika hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala na wasanii wakiwa katika walking safari baada ya kuwasili katika hifadhi ya Taifa ya Burigi, Chato
Mnyama aina ya Sitatunga kama alivyokutwa na Kamera yetu ndani ya hifadhi ya Taifa ya Rubondo

MABALOZI KUINGILIA MASUALA YA NDANI YA NCHI SIO SAWA


Kumbukumbu ya miaka 32 ya baba mzazi wa Emmy Marealle

$
0
0
You touched so many lives. You held so many hands, You were a miracle to so many people, we can’t believe that it has been 32 years without you in our lives.
You are deeply missed by your family and children.
WifeMargareth, Children: Emmy, Leonard, Maposha, Ened, Matilda,& Sia.
Missed also by your beloved grandchildren, Godfrey, Karim, Lilian, 
Mackdonald, Jackline, Vanessa, Joyceline, Eve, Hellen, Ryian, Dereck,Mackline,Mitchel, Milton, & Margareth and great grandchildren
Your legacy will always remain in our lives.

Waziri Simbachawene aiagiza TAREA kutafiti matumizi nishati jadidifu Dar, Ataka mataifa yasimwage Tv na Friji mbovu Afrika

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene akifungua Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene akifungua Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TAREA, Mhandisi Prosper Magali.
Makamu Mwenyekiti wa TAREA, Mhandisi Prosper Magali(kulia) akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Jeroen Verheul akizungumza kwenye uzinduzi wa Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene akiangalia majiko yaliyotengenezwa kitaalamu kulinda mazingira na yanatumia mkaa na kuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene akitembelea mabanda mbalimbali kwenye Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu yanayofanyika Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene akiangalia jiko linalolinda mazingira kwenye moja ya mabanda katika Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu yanayofanyika Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene, ameiagiza Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) kufanya utafiti katika Jiji la Dar es Salaam ili kubaini kiasi cha matumizi ya nishati jadidifu.

Alitoa agizo hilo wakati akifungua Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam yakiwa na kauli mbiu: “NISHATI JADIDIFU KUFIKIA TANZANIA YA VIWANDA 2025” yaliyoandaliwa na TAREA na kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar Salaam.

Aidha, ameyataka mataifa yaliyoendelea kuacha kuleta bidhaa chakavu za kielektroniki zikiwamo runinga na friji katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania kuacha kwa kuwa ni majanga.

Alikuwa akijibu risala ya TAREA iliyosomwa kwake na Makamu Mwenyekiti wa TAREA, Mhandisi Prosper Magali aliyesema licha ya TAREA na wadau mbalimbali kuhamisisha matumizi teknolojia ya nishati jadidifu, zipo changamoto kubwa za kudhibiti taka zitokanazo na bidhaa za kielektroniki zikiwamo runinga na friji.

Simbachawene alisema inasikitisha kuona vifaa vilivyotumika na kuchakaa katika mataifa yaliyoendelea bado zikiwamo friji na TV bado zinaletwa katika mataifa yaliyoendelea ikiwamo Tanzania.

Akasema: “Kwa nchi zilizoendelea, kama kitu ni kibaya, tusikitumie wote; tusione ni kibaya tukapeleka Afrika maana madhara yake tabaka la ozini ni makubwa. Uchafuzi wa hali ya hewa husababisha kumomonyoka kwa tabaka la ozoni na kubadilika kwa tabianchi huathiri watui wote.”

Alisema serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira, imeandaa kanuni mpya za udhibiti na usimamizi wa taka hatarishi za mwaka 2019 zilizoanza kutumika Septemba mwaka huu.

“Kanuni hizi zinasimamia taka hatarishi mbalimbali zikiwamo betri chakavu, hivyo serikali inawahakikishia kuwa itaendelea kusimamia kanuni hizo ipsavyo ili kudhibiti uchafuzi unaoweza kutokea na utupaji usio salama,” alisema na kuongeza kuwa, matumizi ya niashati ya kuaminika na endelevu hayaepukiki kwa maendeleo ya taifa na kuelekea uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Simbachawene alisema: “Mafanikio katika sekta zote za uchumi, huduma za jamii na maendeleo yanategemea upatikanaji wa kuaminika na endelevu wa nishati ya kutosha usiokuwa na madhara katika mazingira.”

Alisema sekta ya viwanda kutumia fursa hiyo kujipatia umeme katika vyanzo vya nishati safi na nafuu kwa shughuli za viwanda kwa mifumo na kazi kama kuchemsha mahji, kuvuta maji kwa ajili ya umwagiliaji na majiko sanifu kwa taasisi za umama kama shule na majeshi.

“Natoa mwito kwa taasisi za umma kama majeshi, magereza, hospitali, shule na vyuo kuingia katika matumizi ya teknolojia ya nishati jadidifu maana miti mingi inakatwa na magereza na shule hivyo, uharibifu wa mazingira ni mkubwa,” alisema

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Jeroen Verheul alisema ili teknolojia ya nishati jadidifu isambae na kutumika zaidi kwa umma, lazima kuwepo mazingira rafiki zaidi ya kisera na kisheria na kwamba, sula hjili linahitahji ubia wa dhati.

Alisema nchi yake itaendelea kushitrikiana na Tanzania katika kusaidia matumizi ya teknolojia ya nishati jadidifu am,bayo ni msaada katika mapambano ya kidunia dhidi ya majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.

Awali, Mhandisi Magali ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa TAREA na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maonesho hayo, alimwambia waziri kuwa, licha ya TAREA na wadau mbalimbali kuhamisisha matuimizi yteknolojia ya nishati jadidifu, zipo changamoto kubwa za kudhibiti taka zitokanazo na bidhaa za kielektrponiki zikiwamo runinga na friji.

“Taka za kielektroniki zimeendelea kuongezeka na tupo kwenye hatari kubwa ya uchafuzi wa mazingira kupitia taka hizi,” alisema magali.

Akaongeza: “Tunaomba Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira kukamilisha utungaji wa sheria za kusimamia biashara ya taka za kielektroniki ili kuwezesha shughuli za urejelezaji wa taka hizo ili kuhifadhi mazingira”.

SHIRIKA LA MEDO SINGIDA LAENDESHA MJADALA WA KUTATUA CHANGAMOTO KWA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU WA AKILI MASHULENI

$
0
0
Mratibu wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la MEDO, Idd Hashim, akiongoza majadiliano katika kongamano la kujadili changamoto dhidi ya wanafunzi wenye ulemavu wa akili katika Shule ya Msingi Mchanganyiko ya Ilongero Halmashauri ya Wilaya ya Singida jana. 
Baadhi ya majengo yenye ubora yaliyo jengwa katika shule hiyo.

Na Waandishi wetu Singida. 

SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la MEDO limeendesha majadiliano na wadau wa elimu katika Shule ya Msingi Mchanganyiko ya Ilongero Halmashauri ya wilaya ya Singida kwa lengo la kuondoa changamoto zinazowakabili walemavu wa akili.

Akizungumza kwenye majadiliano hayo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani ambayo hufanyika Disemba 3 kila mwaka, Mratibu wa shirika hilo Idd Hashim alisema lengo la kukutana na wadau hao ni kuhakikisha watoto wenye ulemavu wa akili kutokubaguliwa katika Jamii. 

Alisema jamii ni lazima itambue walemavu ni watu kama watu wengine na kwamba ulemavu walionao hawakuhitaji bali unaweza kumpata mtu yeyote, hivyo jamii iache kuwaficha watu hao badala yake wawapatie haki zote za msingi ikiwemo elimu. 

"Wadau tuendelee kuelimisha jamii juu ya watoto wetu hawa tusiwafiche, na tuendelee kuiomba serikali iboreshe miundombinu ya shule."alisema Hashim. 

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Sijaona Nkurukwa alisema shule hiyo imeanzishwa mwaka 1951 huku elimu ya kitengo maalumu ikianzishwa mwaka 2015 ambapo watoto wenye ulemavu wa akili ni 29 wavulana wakiwa 18 wasichana 11.

Diwani wa kata ya Ilongero Mh:Issa Mwiru aliwasisitiza wananchi kulipa kodi ili serikali iendelee kuboresha miundombinu ya shule hasa kwa upande wa watoto wenye ulemavu wa akili, na kuwaomba viongozi na jamii kwa ujumla kuwajibika ili kuwaibua wazazi wanaowaficha watoto wao wenye ulemavu huko majumbani. 

Alisema kutokana na shule hiyo kupokea watoto katika maeneo mengi ya Halmashauri hiyo, hivyo jamii nzima kushirikiana kwa pamoja ili kuwaboreshea miundombinu ya kujifunzia watoto hao.

Aidha wazazi na wadau kwa ujumla walisema kuna baadhi ya wazazi wenye watoto wenye ulemavu huo wanashindwa kuwapeleka watoto wao shuleni kutokana na shule kutokuwa na mabweni ambapo inamlazima mzazi kumpeleka na kumrudisha nyumbani mtoto jambo ambalo ni gumu kwao hivyo serikali ingewajengea watoto hao mabweni.
Mratibu wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la MEDO, Idd Hashim, akikagua miundombinu ya shule hiyo akiwa na viongozi wa kamati ya shule na wadau wa elimu wa Kata ya Ilongero.
Mwalimu wa Kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili katika Shule ya Msingi Mchanganyiko ya Ilongero, akizungumzia jinsi wanavyo wahudumia wanafunzi hao.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo akizungumza.
Mjadala ukiendelea.
Wanafunzi wakiimba shairi.
Mwenyekiti wa shule hiyo, Rehema Mbura akizungumza.
Choo cha kisasa kilicho jengwa shuleni hapo. 
Diwani wa Kata ya Ilongero, Issa Mwiru, akijibu maswali ya wadau.
Muonekano wa choo kilicho chakaa shuleni hapo.
Ukaguzi wa choo kipya ukifanyika.
Wanafunzi wakiwa darasani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Ilongero, Ibrahimu Mohammed akizungumza.

Lindi wazindua mwongozo wa uwekezaji

$
0
0
 Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuzindua wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
 Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Rehema Madenge akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa na kutambulisha meza kuu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Godfrey Zambi akitoa salamu kwa mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za  Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida Dk. Hoseana Lunogelo akitoa salamu za ESRF kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo wakati wa hafla ya kuzindua wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
 Mkuu wa Ukuaji wa Maendeleo Jumishi na Mtaalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Miradi ya Maendeleo (UNDP), Ernest Salla akitoa salamu za UNDP kwa niaba ya Mwakilishi Mkaazi wa UNDP nchini Tanzania.Bi. Christne Musisi wakati wa hafla ya kuzindua wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida Dk. Hoseana Lunogelo akikabidhi Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa tayari kuzinduliwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwongozo huo wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
 Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi sambamba na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Godfrey Zambi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwongozo huo uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg.Shaibu Issa Ndemanga pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Rehema Madenge
 Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa (katikati) akionyesha nakala  za Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi mara baada ya kuzindua rasmi wakati wa  hafla iliyofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg.Shaibu Issa Ndemanga, Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Rehema Madenge Mstahiki Meya wa Lindi mjini Ndugu Mohamed Liumbwe pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg.Shaibu Issa Ndemanga.
 Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akikabidhi nakala ya Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi kwa Mkuu wa Ukuaji wa Maendeleo Jumishi na Mtaalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Miradi ya Maendeleo (UNDP), Ernest Salla wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo huo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
 Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akikabidhi nakala ya Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi kwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) - Utalii na Huduma za Biashara Bw. Imani Nkuwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo huo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
 Mtafiti Mwandamizi wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo (kulia) pamoja na Mtafiti mshiriki kutoka ESRF Musa Martine wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
 Mwekezaji wa hoteli za fukwe za bahari mkoani Lindi Bw. Sultan Ahmed kutoka Kilwa akitoa ushuhuda kuhusu fursa zilizopo ndani ya mkoa wa Lindi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.


Pichani juu na chini ni sehemu ya wageni waalikwa walioshiriki hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
 Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa na meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa wilaya za Lindi na Wilaya za Mtwara wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
 Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa na meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau waliowekeza kwenye mkoa wa Lindi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.
 Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa na meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau kutoka ESRF, UNDP, Equinor, Shell, taasisi mbalimbali za serikali na sekta binfasi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa na meza kuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya mkoa wa Lindi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji wa mkoa wa Lindi uliofanyika katika hoteli ya Sea View Beach Resort mkoani Lindi.

Na Mwandishi Wetu, Lindi
MKOA wa Lindi umezindua Mwongozo wa Uwekezaji mkoani humo ambao umeanisha fursa za uwekezaji zilizopo Lindi ili kuvutia wawekezaji kwa lengo la kukuza uchumi wa mkoa na kuimarisha pato la mtu mmoja mmoja na taifa. Mwongozo huo umezinduliwa tarehe 27 Novemba 2019 na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa.
Mwongozo huo umeandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na wataalam wa Mkoa wa Lindi chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Akizindua mwongozo huo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa alitaka fursa hizo zilioanishwa kutekelezwa kimkakati ili kuongeza kipato cha wananchi na Mkoa wa Lindi.
Alisema mkoa wa Lindi umefanyakazi kubwa ya kuongeza kilimo cha korosho na ufuta na kusema hiyo ni fursa kubwa kama ilivyo katika utalii kutokana na kuwa na misitu mingi ya hifadhi na fukwe nzuri zaidi za kitalii nchini na duniani. Alisema inawezekana pia kuanzisha siku maalum ya kula nyama pori wilayani Kilwa ili kuchochea utalii.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi M kuu wa  Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema Kongamano la Biashara na Uwekezaji lililoandaliwa na Mkoa kwa kushirikiana na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Machi mwaka huu limeleta wawekezaji wa ndani na nje ya mkoa kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Alisema Chuo cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es Salaam ni kati ya taasisi zilizoonesha nia ya kuwekeza na kimepewa ekari 150 za ardhi bure kwa ajili ya  Chuo cha Kujenga Boti na Meli. Mwekezaji mwingine ni Sarah Masasi anayetaka kujenga Kiwanda cha kubangua korosho na amepatiwa ekari 50 bure za ujenzi huo.
Alisema kampuni ya kimataifa ya Norway inatarajia kuwekeza kituo cha sayansi, ufugaji na kilimo na kampuni kutoka India kuwekeza kwenye uvuvi. Hakutaja majina ya kampuni. Aidha kampuni kutoka Ujerumani, Filloship  inafanya mazungumzo  kuwekeza mkoani hapa.
Katika hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, kampuni za mafuta na gesi za Equinor, Shell, wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya na manispaa, taasisi za umma, wawekezaji na sekta binafsi, Zambi alisema kutokana na kongamano hilo walianzisha ofisi ya uratibu wa uwekezaji.
''Tunaishukuru TSN (wachapishaji wa magazeti ya HabariLEO, Daily News na SpotiLeo) kutufungulia mlango kupata wawekezaji Marekani, Ujerumani, India na nchini,'' alisema Zambi. Pia, aliwashukuru Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Lindi.
Alisema kuna miradi mikubwa ambayo inashughulikiwa na serikali kuu hapa mkoani ikiwa ni pamoja na  mradi wa kiwanda cha mbolea Kilwa. Mkoa una fursa ya kuwa na kiwanda cha usindikaji chumvi, utengenezaji wa mvinyo kw akutumia korosho, viwanda vya vifungashio, viwatilifu, kubangua korosho na usindikaji wa mafuta ya nazi, alizeti, nishati mbadala nk.
Aidha alisema kwamba fursa katika ngazi ya halmashauri ni pamoja na makundi madogo ya wachambuaji korosho, misitu na utalii na pia kuongeza mnyororo wa thamani katika bidhaa mbalimbali za Kilimo katika ngazi za wilaya na halmashauri.
Alisema kuna utajiri mkubwa wa urithi wa utamaduni na wanamatarajio taaaisi za kitaifa kama Tawa zitasaidia kuwepo na utalii unaowezesha kuchangia kwa kiasi kikubwa pato.
Katika masuala ya uwekezaji katika utalii, mmoja wa wafanyabiashara mkoani Lindi, Sultani Ahmed Sultani  alizungumzia kwa kina katika mada yake namna bora ya kuwezesha sekta ya utalii akitaka sekta binafsi kuwezeshwa ili kushiriki katika nafasi hiyo.
Alisema Lindi ina nafasi kubwa ya kuleta watalii kutoka kaskazini na Kusini mwa Afrika kupitia mpango maalumu unaoweza kuungwa na Zanzibar na matunda yake yataonekana.
Dkt. Hoseana Lunogelo, Mtafiti Mwandamizi akizungumzia Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Lindi kwa niaba ya Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), alisema  watafiti wake wameona fursa nyingi sana na ziko katika sekta na ngazi zote.
 “Kwa hapa Lindi fursa kubwa ipo kwenye mnyororo wa thamani wa zao la Korosho, utalii na madini bila kuisahau gesi. Pia kuna fursa nyingi katika Sekta ya Viwanda, Kilimo, Uvuvi, Miundombinu na Huduma. “ alisema Dk Kida katika hotuba yake iliyosomwa na Dkt. Lunogelo.
Alisema fursa hizo zilizoainishwa katika mwongozo zikitumika vizuri zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha ya wananchi.
Mpaka sasa ESRF imesaidia Mikoa 24 kuandaa Miongozo ya Uwekezaji ambapo mikoa 14 imekamilisha na Mikoa 10 iko katika hatua mbalimbali. ESRF tayari imeanza kusaidia zoezi hili katika mikoa iliyobaki.
Naye Bw. Ernest Salla akitoa neno kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Christine Musisi ameisihi mikoa iliyokwisha tengenezewa miongozo kuhakikisha kwamba wanafanyaia kazi miongozo hiyo ili kuleta tija.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Bw. Ernest Salla alisema kwamba baada ya kuzinduliwa kwa amwongozo ipo haja kwa mkoa wa Lindi sasa kuangalia vipaumbele na kuchambua vilivyotayari ili kuyafanyiakazi kwa haraka.
Aidha hatua nyingine ya pili ni kutangaza fursa zilizopo na kuandaa mikutano ya uwekezaji kwa kuwakutanisha wawekezaji. Pia watumishi wanaoshughulikia uwekezaji ni vyema wakaandaliwa kusaidia kusukuma mbele gurudumu hilo na kutayarisha nyaraka mbalimbali kielektroniki ili kila mmoja aweze kuzipata.
Pia aligusia haja ya kuhakikisha fursa hizo zinatambuliwa kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na mabalozi wetu nje ili kuuza fursa hizo na kutafuta mitaji ili kuiwezesha sekta binafsi inashiriki kikamilifu.
Mwakilishi Mkazi wa UNDP alisema shirika lake litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania na ESRF katika kuhakikisha kwamba wanakamilisha kutengeneza Miongozi kwa mikoa iliyobaki.

Waziri Dkt. Mwakyembe ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Michezo na BMT kufanya uchunguzi wa mbio ndefu za Kigamboni

4,076 WAJITOKEZA MANYARA KUPIMA MAGONJWA MBALIMBALI

$
0
0
Wakazi 4,076 wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wamepima magonjwa mbalimbali katika kuadhimisha siku ya ukimwi duniani yenye kauli mbiu ya jamii ni chachu ya mabadiliko tuungane kupunguza maambukizi mapya ya VVU. 

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Zephania Chaula akizungumza kwenye maadhimisho hayo ambayo kimkoa yamefanyika mji mdogo wa Mirerani jana alisema wananchi hao wamejitokeza kupima magonjwa tofauti. 

Chaula alisema waliopima VVU ni 2,739 wakiwemo wanawake 1,168 na wanaume 1,571 na waliogundulika na virusi ni 98 sawa na asilimia 3.6.

Alisema waliofanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa kifua kikuu (TB) ni 337 wakiwemo wanaume 139 na wanawake 198 ila bado majibu hayajatoka. 

Alisema wanawake 178 walifanyiwa uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na 68 wakakutwa na dalili za kansa na walipatiwa tiba ya mgandisho papo hapo. 

"Watu 78 walipimwa magonjwa ya zinaa na 11 wakakutwa na maambukizi, wanawake 226 walipata huduma ya uzazi wa mpango, watu tisa walichangia damu na watu 507 walipima uzito na urefu," alisema. 

Mkurugenzi wa Tanzanite Founder Foundation, Asha Ngoma, ambaye ni mmoja kati ya waandaaji wa maadhimisho hayo aliwashukuru wote walioshiriki kuyafanikisha ikiwemo serikali. 

Ngoma alisema lengo lao ni kuhakikisha wanatoa elimu kwa watoto wachimbaji wa madini, wamiliki wa migodi na wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanayozunguka migodi juu ya suala la afya na usalama maeneo ya kazi. 

Alisema wananchi wengi walishiriki maadhimisho hayo ikiwemo maandamano, kuvuta kamba, kukimbia mbio fupi, kusikiliza mashairi, ngojera, nyimbo, hotuba na ujumbe wa kupiga vita maambukizi mapya ya VVU. 

Hata hivyo, aliomba radhi endapo kumetokea mapungufu kwenye maadhimisho hayo kwani jambo lolote lililopangwa kwa ajili yao lilikuwa ni geni hivyo watajifunza kwenye wakati mwingine. 

Kaimu mratibu wa ukimwi mkoani Manyara, Scola Mwalyanzi alisema lengo la kufikia 90 tatu kwenye mkoa huo litatimia ifikapo mwaka 2020.

Mwalyanzi alisema mkoa wa Manyara unaonyesha kiwango cha maambukizi ya VVU kimeongezeka kutoka asilimia 1.5 mwaka 2011/2012 na kufikia asilimia 2.3 mwaka 2016/2017. 
 Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, mhandisi Zephania Chaula akizungumza kwenye siku ya Ukimwi duniani ambapo katika Mkoa wa Manyara, imefanyika Mji mdogo wa Mirerani. 
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wakishindana kuvuta kamba na wanajeshi wa JWTZ kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambapo katika Mkoa wa Manyara, zilifanyika Mji mdogo wa Mirerani.  

Hatuwafukuzi Wakimbizi-Lugola

$
0
0
Na Abubakari Akida,MOHA
Serikali ya Tanzania imepinga tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba imekua ikiwafukuza wakimbizi kutoka nchini Burundi wanaoishi katika makazi na kambi mbalimbali katika mikoa ya Kigoma,Tabora na Katavi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam kikihusisha pande tatu;Serikali ya Tanzania,Serikali ya Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi(UNHCR),huku mkataba maalumu ukisainiwa na pande hizo tatu lengo ni kuwezesha urejeshwaji wa wakimbizi walioomba kurejea nchini kwao baada ya amani kurejea.

“Ni vyema tukaliweka hili wazi ili jumuiya za kimataifa na Mataifa mengine yajue kwamba tunaposema tunawarejesha wakimbizi wa Burundi sisi na Serikali ya Burundi tunachofanya ni kuhamasisha,kuhimiza wale ambao wako na hiari warudi Burundi,baada ya kugundua amani imerejea Burundi,sasa tunapofanya hivyo wenzetu wanatafasiri kwamba tunawafukuza wakimbizi,hiyo sio sahihi,serikali ya Tanzania na wananchi wake kwa ujumla wamekua wakipokea wakimbizi kutoka nchi mbalimbali na hatujaanza leo tumekua tukiwahifadhi na amani inaporejea wanaomba warejee katika nchi zao” alisema Lugola

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Mambo ya Ndani kutoka nchini Burundi,Pascal Barandagiye amesemaBurundi sasa ina amani na wameona ipo haja ya raia wake warejee ili kuweza kuijenga nchi yao.

“Tunawahakikishia kwamba kama nchi tuna uwezo wa kupokea warundi 2000 kwa wiki na sisi tutahakikisha warundi wote wanarejea nyumbani,tutawafuata popote walipo,tunawahitaji warudi nyumbani ili tuje tujenge nchi yetu pamoja,” alisema Barandagiye

Kwa upande wa Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi(UNHCR),George Okoth Obbo alisema wameshirikiana na nchi mbili za Tanzania na Burundi katika kuhakikisha yanakuwepo mazingira salama na yenye utu katika uendeshaji wa zoezi hilo huku akiwashukuru Watanzania kwa mwema wao wa kuendelea kuwapokea wakimbizi.

“Tanzania imekua nchi rafiki kwa wakimbizi,mawaziri wote wawili wamekubaliana suala la kurudi wa warundi nchini kwao,tuko hapa kuhakikisha zoezi hilo litaenda salama likizingatia ustawi wa pande zote tatu” alisema Okoth

Ni takribani mwezi mmoja umepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli kwenye ziara yake katika mkoa wa Katavi kuagiza pande zote zinazohusiana na masuala ya wakimbizi wakutane ili kuweza kujadili suala la warundi wanaojiandikisha kwa hiari kurudi nchini kwao,akiwaambia umefika wakati sasa wakurudi katika nchi zao kwenda kuzijenga   huku akiwaonya wakimbizi wanaoshiriki katika matukio ya uhalifu hapa nchini.
 Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Burundi, Pascal Barandagiye (kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George  Okoth  Obbo  wakibadilishana mkataba unaohusu makubaliano ya pande hizo tatu katika kuhakikisha urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi  wanaotaka  kurejea  nchini  kwao  kwa  hiari. Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. 
 Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Kangi  Lugola,  akisaini moja ya mkataba  unaohusu  makubaliano  katika  kuhakikisha  urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi  wanaotaka  kurejea  nchini  kwao  kwa  hiari.Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi  wa  Idara ya Wakimbizi,Sudi Mwakibasi na Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma,Rashid Mchata. Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Burundi, Pascal Barandagiye, akisaini moja ya mkataba unaohusu makubaliano katika kuhakikisha urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi  wanaotaka  kurejea  nchini  kwao  kwa  hiari. Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. 
 Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), George  Okoth  Obbo, akizungumza wakati wa Kikao cha makubaliano katika kuhakikisha urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi  wanaotaka  kurejea  nchini  kwao  kwa  hiari. Kulia ni Mwakilishi wa UNHCR nchini Tanzania,Chansa Kapaya.Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akizungumza wakati wa Kikao cha makubaliano katika kuhakikisha urejeshwaji  wa  wakimbizi  wa Burundi  wanaotaka  kurejea  nchini  kwao  kwa  hiari.Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Nchi za Tanzania,Burundi na DRC Congo zimeingia kwenye makubalino ya Uje...

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe.

TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD YAZIDI KUIMARISHA HUDUMA ZAKE KWA WANANCHI

$
0
0
 SERIKALI kupitia Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) imenunua na kusimika mashine mbili za kisasa za huduma ya uchunguzi na tiba za kutibu saratani aina ya LINA na CT Simulator zenye thamani ya Tsh Bilioni 9.5/-  hatua inayolenga kupunguza muda wa kusubiri tiba mionzi kutoka wiki sita hadi kufikia wiki mbili.

Hayo yamebainishwa  leo Jumatatu (Desemba 2, 2019) Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dkt. Julius Mwaiselage  wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya ORCI katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano unaoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.

Dkt. Mwaiselage alisema mashine hizo za kisasa zinazotumia teknolojia ya 3D zinapatikana katika hospitali yoyote kubwa ya saratani duniani kama India, Ulaya na Marekani, ambapo tangu mashine hizo zianze kutoa huduma za uchunguzi na tiba mwezi Septemba 2018 tayari wagonjwa 1,141 wamepatiwa matibabu.

‘’Kwa wagonjwa 1,141 waliotibiwa kwa kipindi hicho, takribani wagonjwa 208 wangepelekwa nje ya nchi kama  mashine hizi zisingekuwepo na hivyo Serikali imeweza kuokoa Tsh. Bilioni 10.4 ambazo zingetumika kutibu wagonjwa hao nje ya nchi ambapo mgonjwa mmoja hugharimu Tsh Milioni 50’’ alisema Dkt. Mwaiselage.

Dkt. Mwaiselage alisema mshine ya CT Simulator imesaidia kuanzisha huduma za kupima CT Scan katika taasisi hiyo ambapo hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu, jumla ya wagonjwa 1,430 walikuwa wamepata kipimo cha CT Scan, hivyo kupunguza usumbufu kwa wagonjwa ambao walitakiwa kwenda hospitali nyingine kupata huduma hiyo.

Kuhusu rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi, Dkt. Mwaiselage alisema katiks mwaka 2015, jumla wagonjwa 164 wa saratani walipatiwa rufaa kwenda nje ya nchi, lakini baada ya kuboresha huduma za saratani nchini, kuanzia  mwaka 2018 hadi 2019 ni wagonjwa 39 pekee waliosafirishwa nje ya nchi, ambapo wagonjwa hao wengi walikuwa wakienda nje kwa upasuaji na tiba mionzi ya kisasa.

Akibainisha mafanikio mengine, Dkt. Mwaiselage alisema ORCI pia imekarabati wodi mbili za kutolea tiba kemia ikiwemo kufungwa viyoyozi na kununua vitanda maalum vya kutolea tiba kemia hivyo kuongeza utoaji wa tiba kemia kutoka wagonjwa 40 kwa mara moja hadi wagonjwa 100 kwa mara moja, ambapo awali huduma hiyo ilikuwa inatolewa katika wodi 1 pekee.

‘’Kuongezeka kwa wodi na vitanda imesaidia kupunguza muda wa kuanza tiba kemia kutka siku 10 hadi tatu pekee, ikimaanisha mgonjwa anaweza kuanza tiba ndani ya siku tatu kama majibu ya vipimo vyake vyote vitakuwa sawa kupata tiba hiyo’’ alisema Mwaiselage.

Aidha Dkt. Mwaiselage anasema Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia na Wazee na Watoto imewezesha kuimarisha uhakika wa upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 4 mwaka 2014/15 hadi kufikia  asilimia 95 mwaka 2018/19, na upatikanaji wa dawa upo kwa asilimia 100 kwa wagonjwa wenye saratani za mlango wa kizazi, matiti, Kaposi sarcoma, tezi dume, njia ya chakula, kooni, damu, matezi, ngozi na kibofu cha mkojo.

Akifafanua zaidi Dkt. Mwaiselage alisema asilimia 5 ya dawa  zinazopungua, hupatikana katika Duka la Dawa la Jamii la Taasisi ililolianzisha ili kuimarisha upatikanaji wa dawa za saratani na dawa zake hupatikana kwa bei nafuu sana ulikinganisha na maduka mengine ya binafsi.

Dkt. Mwaiselage alisema kuwa kutokana na kuimarika kwa huduma za saratani katika taasisi hiyo, wagonjwa kutoka nchi jirani za Kenya, Comoro, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Burundi wameongezeka kuja kupata huduma za tiba saratani na hivyo kuongeza mapato ya Taasisi kwani wananchi wasio raia wanalipia huduma hizo.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAANDAA MAFUNZO KWA WAKUFUNZI WA VYUO VYA VETA JUU

$
0
0
 Injinia Julius Enock kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Idara ya Mazingira akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo kwa wakufunzi kutoka vyuo vya VETA juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi bila kuachia angani kemikali zinazoaathiri mazingira. Mafunzo hayo  yamefanyika katika ukumbi wa CCEMI jijini Dar es Salaam na  yameandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
 Sehemu ya Washiriki waliohudhuria warsha ya mafunzo kwa wakufunzi kutoka vyuo vya VETA juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi bila kuachia angani kemikali zinazoaathiri mazingira  wakifuatilia kwa umakini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na mtoa mada (hayupo pichani)  wakati wa mafunzo hayo yalioandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu mwelekezi wa mpango wa kupunguza Matumizi ya kemikali jamii ya hydrochlofluocar-cons(HCFCs) kemikali zinazotumika  kweny viyoyozi na majokofu, Bwana Marvin Kamurthuzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira (UNEP)  akiwasilisha mada wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
 Washiriki waliohudhuria warsha ya mafunzo kwa wakufunzi kutoka vyuo vya VETA juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi bila kuachia angani kemikali zinazoaathiri mazingira  wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mafunzo hayo, yaliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

BENKI YA CRDB YAKABIDHI MADAWATI 240 KWA SHULE SITA WILAYANI CHUNYA, MBEYA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntimika ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, akipokea sehemu ya madawati kutoka kwa Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB anayeshughulikia masuala ya Serikali za Mitaa, Suzan Shuma katika hafla iliyofanyika Novemba 30, 2019 katika kitongoji cha LUPA Wilayani Chunya, mkoani Mbeya kwa ajili ya Shule za Sekondari na Msingi zilizomo katika Kata Sita za LUPA, yaliyotolewa na Benki ya CRDB. Jumla ya madawati na Viti 240 vilivyotolewa.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntimika akimkabidhi Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sophia Kumbuli Madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya kata Sita za LUPA Wilayani Chunya katika hafla fupi iliyofanyika Novemba 30, 2019 katika kitongoji cha LUPA Wilayani Chunya, mkoani Mbeya. Kulia ni Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB anayeshughulikia masuala ya Serikali za Mitaa, Suzan Shuma.
Picha ya pamoja.

MTANZANIA VICTOR JOSEPH AIBUKA MSHINDI TANZANIA OPEN 2019

$
0
0
Mshindi wa jumla wa mashindano ya gofu ya Tanzania Open 2019 Victor Joseph kutoka klabu ya Gymkhana mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mh Dumbaro katika mashindano yaliyomlizika katika Uwanja wa Kili Jijini Arusha jana.
Mshindi wa Mikwaju ya jumla wa mashindano ya gofu ya Tanzania Open 2019, M Chadha kutoka klabu ya Kili akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi kutoka kampuni ya Oryx Energy, Sira Muhele katika mashindano yaliyomalizika katika Uwanja wa Kili Jijini Arusha jana.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Damas Ndumbaro amehitimisha Mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania Open jijini Arusha huku mcheza gofu Victor Joseph kutoka klabu ya Gymkhana ya Dar es Salaam akitwaa ubingwa wa mashindano hayo.

Mchezaji huyo kutoka Klabu  ya Dar es Salaam Gymkhana alifanikiwa kubakiza kombe baada ya kuibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyoshirikisha wachezaji toka Nchi Sita kwa kupata Mikwaju (Gross) 294.

Siku ya kwanza Mchezaji huyo alicheza 75,74,71 na 74 akifuatiwa  Joseph Chinywai kutoka Uganda aliyepata mikwaju  308 na kuwashinda wachezaji wengine wa  divisheni A walioshiriki mashindano hayo.

Katika  Mikwaju ya jumla Net Manraj Chadha wa kili golf aliibuka na Ushindi baada ya kupata  Mikwaju ya Jumla 291 huku akiwa amecheza 72,74,71 na 74 katika mzunguko wa Mwisho.

Mshindi katika Divisheni B ni  Joe Lee ambaye alipata mikwaju ya jumla 149 baada ya kucheza 71 na 78 katika  mzunguko wa pili huku kiwango chake cha makosa kikiwa ni 18.

Mshindi katika  kundi la senior ni Boniface Nyiti wa Lugalo aliyepiga Mikwaju yaa Jumla 162 baada yaa mzunguko wa kwanza kupata mikwaju 81 sawa na mzunguko wa pili huku kiwango cha makosa kikiwa ni Nane.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mwenyekiti wa TGU Criss Martin alisema mashindano haya ni mashindano ya 69 tangu kuanzishwa kwake lakini kumekuwa na Changamoto nyingi na kuomba Rais Magufuli kutupia Jicho mchezo huo.

“ tunatambua kazi kubwa ya Mh Rais katika Majukumu mbalimbali ambayo amekuwa akifanya lakini tunaomba atupie jicho pia Mchezo huu umekuwa  na mafanikio” Alisema Mwenyekiti.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ndumbaro aliahidi kufikisha kilio chao kwa wahusika ili kuendeleza mchezo huu nap engine kwa kuanzia ngazi yaa Mashuleni ili kupata vipaji na kuzalisha wachezaji bora wakiwemo wa kulipwa

“ Nitafikisha Kilio chenu Serikali ili kuboresha Mchezo huu lakini pia hakikisheni mnasajili viwanja ili viwango vya Uchezaji viweze kutambulika Kimataifa “. Alisema Naibu Waziri Ndumbalo

Aidha alisema Mashindano yamefanikiwa  na hiyo ni kutokana na Kazi nzuri waliyofanya kwa kushirikiana na na kamati ,waratibu Verge Africa na wadhamini ambaao wamefanya Zawadi kuwa Bora hivyo inahitaji kuendelezwa.

Klabu za Tanzania zilzoshiriki mashindano haya yaliyodhaminiwa na Oryx, Super Doll, Garda word, Coca Cola, Tanfoam, Hal na Serengeti ni Lugalo, Dar es Salaam Gymkhana zote za Dar es Salaam, Morogoro Gymkhana, Arusha Gymkhana, TPC, Moshi na Zanzibar Sea Cliff .
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images