Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110027 articles
Browse latest View live

IGP SIRRO AWAONYA WANAOENDELEA KUWANYANYASA WANAWAKE NA WATOTO BUNDA, MARA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameendelea kuwaonya watu wanaonyanyasa wanawake na watoto, kwa kuwasababisia vipigo na ukatili wa aina nyingine ambao ni kinyume cha sheria za nchi. 

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizindua Ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto wilayani Bunda mkoani Mara, ujenzi uliofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani UNFPA pamoja na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto yaani CDF. 

Katika sherehe hizo za uzinduzi IGP Sirro amewataka wananchi kutumia ofisi hiyo ya Dawati la kijinsia na watoto ili kuendelea kukomesha vitendo vya ukatili sambamba na kuwataka wazazi kuwaendeleza kielimu watoto wao jambo ambalo litasaidia jamii kuwa na viongozi bora. 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Lydia Bupilipili amesema kuwa, Jeshi la Polisi limeweza kuchukua hatua madhubuti hususani katika kudhibiti vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, ukatili, mimba za utotoni, ulawiti, na ubakaji 

Aidha, katika ziara yake mkoani Mara, IGP Sirro tayari amekwisha zindua jumla ya Ofisi nne za Dawati la Jinsia na Watoto hatua ambayo itarahisisha upatikanaji wa taarifa zinazoripotiwa kwenye madawati hayo kuhusiana na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia.


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KATIKA MAHAFALI YA 45 YA IFM UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, wakati aliwasili kwenye kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha IFM, Dkt. Benson Bana, wakati aliwasili kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha IFM, kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini .


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na Wahitimu wa Chuo cha IFM, kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ,Novemba 29, 2019. 


Wahitimu wa Chuo cha IFM, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ,Novemba 29, 2019


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha IFM, kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ,Novemba 29, 2019. 


Wahitimu wa Chuo cha IFM, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ,Novemba 29, 2019


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa anaingia kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ,Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WANAHABARI MTAKUWA VIBARUA MPAKA LINI - WAZIRI MWAKYEMBE

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe na Mwakilishi wa UN Women nchini, Bi. Hodan Addou, wakionyesha nakala ya kitabu cha Masuala ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye vyombo vya habari, kilichozinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Jukwa la Waandishi wa Habari Wanawake lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe akizungumza na washiriki wa Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Mwakilishi wa UN Women Nchini, Bi. Hodan Addou akizungumza na washiriki wa Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Mwandishi wa Habari Mkongwe, Bi. Pili Mtambalike akichangia mada katika Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.(PICHA NA MAELEZO).

NA JUDITH MHINA -MAELEZO

WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrisom Mwakyembe amezindua kitabu cha Gender and Media Handbook in Tanzania wakati wa maadhimisho ya miaka miwili ya Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano.

Akizindua kitabu hicho katika ukumbi wa Kibo ndani ya hoteli i ya Kimataifa ya Hyatt Regence - The Kilimanjaro leo Jijini Dar-es-salaam Waziri Dkt Mwakyembe amesema “Wana habari mtakuwa vibarua mpaka lini”.

Hebu tujaribu kutekeleza sheria mbili ya Habari na ile ya haki ya kupata taarifa, ambapo Tanzania ni kati ya nchi chache ambazo zimeiga kiila kitu kilichoandikwa kwenye sheria husika ya kimataifa, badala yake wanaleta mada yao pendwa ya jinsia moja, hatuwezi kukubali. Amesema Waziri Mwakyembe.

Akijibu risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano- Tanzania Women Media and Public Relation Networ,. Bevin Bhoke Chacha Mwita ambaye amesema kuwa waandishi wa habari wanawalke wananyanyaswa kijinsia katika vyumba vya habari . Hii ikiwa ni pamoja na kutolipwa mshahara stahiki kulingana na sifa walizonazo, kutopandishwa madaraja, lugha chafu na kubaguliwa katika majukumu ya kazi kama waandishi wa kiume na kujikuta wengi wao wakiwa waadhirika wa kunyanyaswa kijinsia.

Waziri mwakyembe aliongeza kwa kusema “Tunaomba wahisani watenge nusu ya fedha wanazotoa ili kuangalia masilahi ya waandishi wa habari na kuboresha mazingira ya kazi kutokana na kuwa na vitendea kazi duni katika vyombo vyao vya Habari.

Ninashangaa waandishi wa Habari ambao wanashangilia kuwa na taaluma isiyo na mpangilio, sheria wala kanuni, katika kuimarisha taaluma yao na ndio maana leo hii mnalalamika masilahi madogo yasiyolingana na kazi mnayofanya au hatopata mishahara kabisa .

Akisisitiza jambo hilo Waziri amesema “Ni agfadhali kuwa na vyombo vya Habari vichache vinavyojali na lulinda masilahi ya Waandishi wa Habari kuliko kuwa na vyombo vingi ambavyo , haviangalii masilahi ya waandishi wa Habari, kuwalipa mishahara stahiki kwa wakati .

Akitoa agizo kwa kukabiliana na suala la kupiga vita unyanyasaji kijinsia Waziri Mwakyembe amesema kuwa nimefurahi kwa kuwa mmeonyesha namba mbili maalum za simu ambazo yeyote atakayenyanyaswa kijinsia azipige ili kupata msaada. Aidha, Wizara yangu naiagiza kuwa na namba maalum ya simu ambayo mtanipigia mimi moja kwa moja na kuwatangaza wale wote wanaomnyanyasa wanahabari wanawake ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji kwenye vyumba vya habari.

Akisisitiza agizo hilo amesema dirisha la Waziri lipo wazi kwa kila mtu bila mashariti yeyote na naomba wanahabari walitumie kweli kweli, mimi nikiwa kama mzazi na kiongozi ni lazima kuhakikisha suala hili linakuwa historia.

Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa wanahabari wanawake na maafisa uhusiano Bi Chacha ameongeza kwa kusema kuwa wanawake wana

Katika hizi siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika vyumba vya Habari Mshauri wa masuala ya wanawake wanahabari Bi Pili Mtambalike amesema “Wanahabari wanawake wananyanyaswa kijinsia ikiwa ni pamoja na kutengwa kwa kupewa kazi nyepesi ikilinganiswha na waandishi wa kiume katika vyombo vya habari kutokana na kutokujiamini

Aidha , katika vyombo vingi vya Habari utafiti unaonyesha kuwa wahariri wengi ni wa jinsia ya kiume japo wapo wanawake ambao wanastahili kuwa wahariri na wanalingana hata kwa taaluma walizonazo ila hawapewi madaraka na hata hawapandishwi madaraja kama wenzao wa jinsia ya kiume.

Vilevile waandishi wanahabari wachanga wakike wananyanyaswa kingono na waliowengi wanafanya kazi kwenye vyombo hivyo kama correspondence na kulipwa kulingana na stori ambayo haiwatoshelezi kimaisha. Pia, Lugha wanazotumia wahariri katika vyumba vya habari ni lugha chafu za kudhalilisha na vitisho.

Akiongelea upande wa pili kama ushauri kwa wanahabari wachanga wanawake amesema kuwa ipo tabia ya wanahabari hawa wa kike wachanga kujiendekeza ili wapate wepesi wa kufanya kazi bila kuwa wabunifu kujituma na kuhakikisha wanajifunza kila mara ili kukomaa kitaaluma.

Pili Bi Mtambalike amesema kuwa ipo haja ya kuwa na sera ya jinsia katika vyombo vya Habari na kuhakikisha sera hizo zinatumika . Utafiti uliofanywa katika vyombo 23 vya Habari sita tu ndio vilikuwa na sera inayoeleweka ambayo haitumiki.

Hivyo tunaomba Jukwaa la Wahariri Tanzania –TEF liangalie namna gani linaweza kuleta usawa wa kijinsia katika kuwa na idadi sawa ya wahariri kwa kuwa wanawake walio wengi wanaishia katika ngazi ya Wahariri wasaidizi . Akitoa Takwimu amesema asilimia 26 ya wanawake ndio wahariri wasaidizi waliosalia wote ni jinsia ya kiume wakiwemo wahariri wakuu wa jinsia ya kiume.

Pia, unyanyasaji huu wa wanawake unafanyika hata kwenye upande wa vyanzo vya Habari ambavyo kwa wanawake ni asilimia 36 ,a silimia 64 ya vyanzo vya Habari hutokana na wanaume. Hivyo tunaomba hata wanawake wanahabari walione hili na kuhakikisha wanawahoji wanawake wenzao kama chanzo cha Habari badala ya kujikita zaidi kwa wanaume. Amesema Bi Mtambalike.

Naye Mhariri Mtendaji Bakatri Machumu ambaye hakuweza kufika katika hafla hiyo na kuwasilisha taarifa yake kupitia video iliyorekodiwa amesema kuwa kutokana na uzoefu wangu katika tasnia ya Habari waandishi wanawake ni wabunifu na wananafasi kubwa ya kuangalia wanawake ambao wako katika jamii na kusaidiana.

Naye Muwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bibi Hodan Addou amesema “ Vyombo vya Habari ni kati ya vyombo vyenye nguvu kubwa hivyo vitumike katika kuhakikisha vinaondoa kabisa suala zima la unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia katika vyomvo vya Habari”.

Pia, ameongeza kwa kusema kuwa ni lazima kuhakikisha wanahabari wanawake wanashiriki kikamilifu katika kuhakikisha wanatumia taaluma yao bila vikwazo ili kuwaletea maendeleo mtu momoj ammoja na Taifa kwa ujumla.

Akiongelea kauli mbiu ya mwaka katika maadhimisho ya miaka miwili ya Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano. Unaosema “Changamkia Fursa sasa” Grabbing Opportunity now Katibu wa Kamati Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano, Bi Leah Mushi amesema nafasi za mafunzo ambazo hutolewa na wadau mbalimbali wa sekta wa Habari wakiwemo Wanawake wa Umoja wa Mataifa, pamoja na Shirika la Mitandao ya Habari- Internews.

Aidha, kuna fursa nyingi za mafunzo ya Mitandao ya kijamii na pia wanatoa vitendea kazi kwa waandishi wachanga wake kwa waume ili waweze kujitegemea katika kufanya kazi zao na kujiendeleza kitaaluma.
Naye Afisa Uhusiano wa Kituo cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bi Stela Vuzo, amesema kuwa huu ni wakati muafaka kwa wanahabari wachanga wanawake Tanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo kwa ajili ya kusimamia taaluma ya Habari na kujiendeleza, ikiwa ni pamoja na kupata kazi sehemu mbalimbali duniani na kuacha kulalamika kuhusu masilahi na mishahara midogo.

Haya tunayoyaona sasa inatokana na mfumo dume ambao tumeuishi kwa miongo kadhaa ambayo adhari zake zinajitokeza , hivyo sio kitu cha ajabu katika jamii zetu, na hayatokei kwenye tasnia ya Habari peke yake bali ni mfumo wa malezi kwenye jamii zetu ambao unatakiwa ukemewa, upigwe vita na uache kubagua mtoto wa kike na yule wa kiume. Amesema Mhariri Jesse Kwayu.

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA MAMA MZAZI WA NAIBU WAZIRI MABULA

$
0
0

Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA

Mamia ya wananchi wa jiji la Mwanza na vitngoji vyake wamejitokeza kwa wingi kumzika mama mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula.

Mazishi ya Mama Mzazi wa Dkt Mabula Bi Cecilia Lubala yamefanyika jana kwenye makaburi ya familia yaliyopo kijiji cha Mnyengeja kata ya Sumve wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

Kabla ya mazishi hayo yaliyohudhuriwa pia na viongozi wa Chama na Serikali kulifanyika ibada maalum ya kumuombea marehemu Cecilia Lubala kwenye Kanika Katoliki Parokia ya Kirumba na baadaye shughuli ya kuaga mwili eneo la Ishungisha wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo William Lukuvi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kilagi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Herry Jemes, Katibu wa UWT Queen Mlozi, Mkuu wa mkoa wa Katavi Anthony Mtaka, Wakuu wa wilaya na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Marehemu Cecilia Lubala alifariki dunia jumamosi iliyopita tarehe 23 Novemba 2019 baada ya kuugua kwa muda mrefu na kulazwa kwa nyakati tofauti katika hospitali za Muhimbili, Dodoma na Bugando mkoani Mwanza ambako umaiti ulimkuta. 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa kwanza kulia) pamoja na ndugu zake wakiweka shada la maua katika kaburi la mama yake mzazi bi Cecilia Lubala baada ya kukamilika kwa mazishi katika kijiji cha Mnyengeja kata ya Sumve wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitoa heshima za mwisho kwa mama mzazi wa Naibu wake Dkt Angeline Mabula aliyefiwa na mama yake mzazi Bi Cecilia Lubala wakati wa kuaga mwili wa marehemu eneo la Ishungisha wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa pili kushoto) wakati wa mazishi ya mama yake mzazi Bi Cecilia Lubala baada ya kukamilika kwa mazishi katika kijiji cha Mnyengeja kata ya Sumve wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza jana. Wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Qween Mlozi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa na viongozi wengine katika mazishi ya mama mzazi wa Naibu wake Dkt Angeline Mabula Bi Cecilia Lubala katika mazishi yaliyofanyika kijiji cha Mnyengeja wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza. 

WAUGUZI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) WAADHIMISHA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WAGONJWA, NI WA WODI NAMBA TATU

$
0
0

Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi wa Taasisi hiyo Robert Mallya (aliyevaa safari suti) mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi namba tatu.
Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tulizo Shemu akiwaeleza wauguzi wa wodi namba tatu jinsi ya kuwahudumia wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo ili waweze kujikinga na maambukizi (infection) kwenye eneo ambalo limefanyiwa upasuaji (kidonda) wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akiwapongeza wauguzi wa wodi namba tatu kwa upendo waliokuwa nao kwa wagonjwa wanaowahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.

Msimamizi wa wodi namba ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Afisa Uuguzi Anastazia Moshi akieleza namna wauguzi wa wodi hiyo wanavyofanya kazi ya kuwahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika Taasisi hiyo.


Maafisa Uuguzi wa wodi namba wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Dkt. Tulizo Shemu na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi Robert Mallya wakimkabidhi dawa zilizotolewa na wauguzi wa wodi hiyo Mkuu wa kitengo cha Ustawi wa Jamii Asha Salum kwa ajili ya wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kulipia gharama za matibabu wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.


Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi Robert Mallya, Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Dkt. Tulizo Shemu na Mkuu wa kitengo cha Ustawi wa Jamii Asha Salum wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wakiwaongoza wauguzi wa wodi namba tatu kukata keki ikiwa ni ishara ya kuonesha upendo kati yao na wagonjwa wanaowahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.


Afisa Uuguzi wa wodi namba tatu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jumaa Omary akimlisha keki mgonjwa aliyelazwa katika wodi hiyo ikiwa ni ishara ya kuonesha upendo kwa wagonjwa wanaowahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.


Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi wa Taasisi hiyo Robert Mallya (aliyevaa safari suti) mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi namba tatu. (PICHA NA: GENOFEVA MATEMU – JKCI)

MADHEHEBU YA DINI YAMEISAIDIA SERIKALI KUPATA VIONGOZI WAZURI - WAZIRI MKUU

$
0
0

NA OWM, DAR ES SALAAM
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema madhehebu ya dini yametoa mchango mkubwa katika kuwapata viongozi wa Serikali wanaofuata maadili mema na miiko ya uongozi.

Akizungumza wakati alipofungua Msikiti wa Haq – Kionga ulioko Magomeni, jijini Dar es Salaam leo mchana (Ijumaa, Novemba 29, 2019), Mheshimiwa Majaliwa amesema imedhihirika kwamba waumini wazuri wa dini mbalimbali wamebainika kuwa ni viongozi wazuri na waadilifu ndani ya Serikali. 

Amewasihi viongozi wa dini waendelee kuwafundisha maadili mema waumini wao ili Taifa liendelee kuwa na raia wema ambao baadhi yao ndiyo watakakuwa viongozi katika ngazi mbalimbali hapo baadaye.  

“Nyumba za ibada ndiyo mahali sahihi panapojengwa maadili mema kwa watu wa rika zote, hivyo nawaomba Watanzania wawe waumini wazuri wa dini zao kwani kwa kufanya hivyo watakuwa pia ni raia wema,” amesema Mheshimiwa Majaliwa.

Amesema wazazi na walezi wanawajibika kuwarithisha watoto wao imani za dini vizuri kwani anaamini kwa kufanya hivyo watoto watajengewa misingi mizuri ya imani ya dini na maadili mema na watakapokuwa watu wazima watakuwa ni raia wema.

Mheshimiwa Majaliwa aliwasilisha mchango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli wa sh. milioni 10 na yeye pia alichangia sh. milioni tano ili zisaidie katika awamu ya pili ujenzi wa msikiti huo.  

Naye Sheikh Masoud Jongo ambaye alimwakilisha Sheikh Mkuu wa Tanzania katika ufunguzi wa msikiti huo, alisema uhuru mkubwa wa kuabudu uliopo nchini ndiyo sababu kubwa inayoifanya Tanzania iwe ni nchi ya amani na utulivu. 

Sheikh Jongo amewaomba Watanzania wautumie vizuri uhuru mkubwa wa kuabudu uliopo nchini kwani ni nchi chache duniani zinazotoa uhuru mkubwa wa kuabudu kwa wananchi wake kama ilivyo hapa Tanzania.

Baadhi ya viongozi walioshiriki katika ufunguzi wa msikiti huo ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia na mbunge wa Kibaha Vijijini, Abuu Juma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kufungua rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, wakati akifungua rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, wakati aliwasili kwenye Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, ambao ameufungua rasmi, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, wakati aliwasili kwenye Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, ambao ameufungua rasmi, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwakilishi wa Mufti wa Tanzania na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa na Sheikh Hamid Jongo, kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, kabla ya kuufungua rasmi, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Sheik Jongo, akizungumza na Waumini wa Kiislamu, kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Waumini wa Kiislamu, kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Waumini wa Kiislamu, kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waumini wa Kiislamu, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiingia msikitini, baada ya kufungua rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisikiliza mawaidha kwenye swala ya Ijumaa, baada ya kufungua rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DISEMBA MOSI, 2019

Historia ya Wachaga wa Old Moshi ikisimuliwa na Esaria Meli, mjukuu wa Mangi Meli


KAMPENI YA ELIMU KWA MLIPAKODI KUANZA KESHO DAR

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inatarajia kuanzisha Kampeni ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi katika Mkoa wa Dar es Salaam itakayodumu kwa siku 13 kuanzia kesho tarehe 2 hadi 14 Desemba, 2019.

Akizungumzia kampeni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amesema kuwa lengo ni kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na kupokea maoni kutoka kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

"Kampeni hii ni mwendelezo wa kampeni ambayo imemalizika katika Mikoa ya Morogoro na Pwani na sasa tunaingia katika Mkoa wa Dar es Salaam tukiwa na lengo la kuwaelimisha walipakodi na wananchi masuala yanayohusu kodi, kupokea maoni yao, kusikiliza changamoto na malalamiko ili tuweze kuyatafutia ufumbuzi", alisema Kayombo.

Kayombo ameongeza kuwa kampeni hiyo itaambatana na huduma ya usajili wa wafanyabiashara wapya wasiokuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi yaani TIN.

"Pamoja na kutoa elimu ya kodi, kupokea maoni na kusikiliza changamoto za walipakodi pia tutatoa huduma ya usajili wa walipakodi wapya ambapo tutawapatia cheti cha Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi tukiwa na dhumuni la kupanua wigo wa walipakodi hapa nchini", aliongeza Kayombo.

Mkurugenzi Kayombo amebainisha maeneo ambayo yatafikiwa katika kampeni hiyo kuwa ni Ilala, Kinondoni, Temeke na Kariakoo na itafanyika kwa njia ya semina katika vituo vilivyopangwa kwenye maeneo hayo pamoja na kuwatembelea walipakodi katika biashara zao yaani duka kwa duka.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo

CHEKI MPAMBANO WA MMAREKANI FLOYD MAYWEATHER NA MFILIPINO MANNY PACQUIAO, KISHA LINGANISHA NA WA MWAKINYO

SHIMUTA 2019:TANESCO YAAPA KUSOMBA VIKOMBE VYOTE

$
0
0
MWENYEKITI wa TANESCO Sports Club , Omary Shabani amesema kuwa mwaka huu TANESCO imejiandaa kuchukua makombe yote katika mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma , Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) yanayoendelea jijini Mwanza.

Mashindano ya SHIMMUTA kwa mwaka huu 2019 yanafanyika katika viwanja tofauti huku jijini humo yakihusisha jumla ya timu 46 ikiwa ni ongezeko la klabu 20 kwani ya mwaka jana yaliyo fanyika Jijini Dodoma yalikuwa na timu 26.

Akizungumzia maandalizi ya TANESCO, Shabani alisema maandalizi ya timu zote yamekamilika na mpaka sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja hivyo ndoto ni kuchukua mataji ya michezo yote inaanza kutimia taratibu.

"Mwaka Jana kule Jijini Dodoma tulikuwa mabingwa wa jumla, pia msimu huu tunataka kufanya hivyo na kuongeza vikombe zaidi katika michezo yote ambayo tunashiriki, maandalizi yalifanyika mazuri , hatuna shaka tutafanya hivyo" alisema Shaban.

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO katika mchezo wa Netball, Nazareth Mwanjala alisema mashindano hayo ni muhimu kushiriki kwani husaidia kuleta maendeleo pia hupelekea kufahamiana miungoni mwa Washiriki hivyo hubadilisha mawazo na uzoefu wa kazi.


UFUNGUZI WA JENGO LA TUME YA HAKI ZA BINAADAMU NA UTAWALA BORA

$
0
0

Na Mwashungi Tahir Maelezo 

MWENYEKITI wa Tume ya Haki za binaadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu, Mathew Pauwa Mhina aliwataka watendaji wa Tume ya Haki za binaadamu na Utawala Bora kusimamia majukumu yao kwa mujibu wa madai ya malalamiko kwa Wananchi . 

Hayo aliyasema huko kwenye Ukumbi wa Jengo la Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala bora lilioko Mbweni Wilaya ya Magharibi B Unguja wakati alipokuwa akiwatambulisha Makamishna wapya walioteuliwa hivi karibuni na kukagua jengo lililofanyiwa matengenezo.

Alisema malalamiko na madai ya Wananchi hutokezea pale ambapo wamecheleweshewa malipo kupunwa au kutolipwa kabisa fidia ya mali zao ili waweze kuzifanyia ufumbuzi kwa haraka. 

Aidha Mwenyekiti huyo alisema iko haja ya wananchi kupewa elimu kwa kufanyiwa mikutano katika shehia zao ili kupata uelewa wa jinsi ya kutetea haki zao kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi wakati wanapopeleka malalamiko yao katika Tume hiyo.

“Wananchi iko haja ya kupatiwa elimu na kufahamishwa majukumu ya Tume hii ili waweze kupata uelewa wa sehemu gani ya kuyapeleka malalamiko yao na kuweza kupatiwa ufumbuzi”, alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha alisema Serikali inapofanya shughuli zake za maendeleo kama vile ujenzi wa miundombinu katika maeneo ya wananchi hujitokeza malalamiko mengi ya madai ikiwemo kucheleweshwa kwa malipo au kutolipwa kabisa fidia za mali zao.

Hivyo alisema pamoja na kazi ya kupokea na kuchunguza malalamiko Tume inaendelea kutekeleza shughuli nyengine kwa mujibu wa sheria kwa kutembelea sehemu mbali mbali ikiwemo Hospitali za watu wenye matatizo ya akili, nyumba za waathirika wa madawa ya kulevya.

Akisoma taarifa fupi Mratibu wa mradi wa UNDP ya Ukarabati wa jengo la Tume za Haki za Binaadamu na Utawala Bora Laurant Burilo amesema jengo hilo limefanyiwa ukarabati kwa lengo la kuwa na haiba nzuri kwa wafanyakazi .

Alisema ukarabati huo ni pamoja na utiaji wa rangi , uwekaji wa mabango na mageti , utengezaji wa vyoo pamoja na huduma nyengine zote muhimu za kiofisi ambapo jumla yaTsh, Milioni 18 zimetolewa kwa msaada wa UNDP na Denmark.

Kwa upande wake Kamishna wa Tume za Haki za Binaadamu na Utawala Bora Amina Salum Ali alipokuwan akitambulishwa aliomba mashirikiano ya pamoja kwa kuwasaidia wananchi katika kutetea madai ya haki zao ili kupunguza changamoto .
Muonekano wa Jengo la Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora lilifunguliwa  baada ya kufanyiwa matengenezo  huko Bweni Wilaya ya Magharibi B ,Unguja    



Tigo wazindua kampeni ya wakala kinara

$
0
0
Tigo yazindua kampeni ya kufunga mwaka kwa ajili ya mawakala iitwayo Wakala Kinara. Kampeni hiyo itakayo anza rasmi tarehe 1 disemba hadi 31 disember itahusisha mshindi wa kwanza kupokea milioni 20 akifuatiwa na wa pili milioni 10. #TigoWakalaKinara

Kampuni ya Mawasiliano Tigo jana yakutana, yawapongeza mawakala wa Tigo pesa pamoja na kuzindua promosheni mpya ya mawakala iitwayo Wakala Kinara.

“Kama tunavyofahamu tulizindua kampeni ya ‘Kishindo Cha Kufunga Mwaka’ kwa ajili ya mteja wa Tigo pesa hivyo kampeni tunayozindua leo ni mahususi kwa ajili ya mawakala wa Tigo pesa.”‬‪Kaimu Mkuu wa kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha‬ 




Tigo yazindua kampeni ya kufunga mwaka kwa ajili ya mawakala iitwayo Wakala Kinara. Kampeni hiyo itakayo anza rasmi tarehe 1 disemba hadi 31 disember itahusisha mshindi wa kwanza kupokea milioni 20 akifuatiwa na wa pili milioni 10. #TigoWakalaKinara

Baadhi ya mawakala wa Tigo pesa wakiwa pamoja uongozi wa kampuni ya mawasiliano Tigo, baada ya kupokea tuzo za mawakala wa Tigo pesa waliofanya vizuri katika mwaka 2019.

Benki Ya Exim Yatoa Msaada Wa Taulo Za Kike Kwa Wanafunzi Wa Sekondari na Msingi Mkoani Shinyanga.

$
0
0
  Benki ya Exim Tanzania imetoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 2,400 wa Shule za Sekondari na Msingi zilizopo Mkoani Shinyanga.

Shule hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Kiislamu Istiqaama, Shule ya Msingi Mwenge, Shule ya Msingi Mapinduzi, Shule ya Msingi Jomu, Shule ya Msingi Ibadhi pamoja na Kituo cha Agape aids control Programme zilizopo mkoani humo.

Akizungumza wakati wa akikabidhi msaada huo mwishoni mwa wiki, Meneja wa Benki hiyo tawi la Shinyanga, Bi Sarah Paul alisema hatua hiyo ni muendelezo wa mpango wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) wa benki hiyo unafahamika kama Exim Cares.

Alisema benki hiyo imekuja na mpango huo ili kusaidia wanafunzi wa kike kwa kuwapatia hitaji hilo muhimu kiafya sambamba na kutoa elimu kuhusu hedhi salama kwa wanafunzi wa kike pindi wakiwa shuleni.

Kwa mujibu wa Bi Sarah, kupitia mpango huo, benki hiyo inatarajia kutoa misaada mingine kama hiyo kwa shule kadhaa katika mikoa mingine ikiwemo Tabora na Iringa.

"Benki ya Exim inafarijika sana kuwa sehemu ya agenda muhimu za kijamii na hiyo ni moja ya imani yetu, kwa hiyo tumeamua kuja na mpango wa kusaidia mtoto wa kike na ili kuhakikisha kwamba msaada huu unakuwa na tija zaidi taulo hizi tulizotoa zinaweza kutumika zaidi ya mara moja na itawasaaidia zaidi wahusika,’’ alisema.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNESCO inakadiriwa kuwa msichana mmoja kati ya kumi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara anakosa kwenda shule wakati wa mzunguko wa hedhi.

Aidha katika baadhi ya tamaduni suala la hedhi linapewa tafsiri potofu zaidi na hivyo kuongeza changamoto kwa watoto wa kike na hivyo kuathiri maudhulio yao mashuleni na hatimaye kuathiri taaluma zao.

"Benki ya Exim imejitolea kikamilifu kuhakikisha kuwa vijana wa Kitanzania wanapata elimu, licha ya changamoto zinazowakabili na hili tutalifanikisha kwa kuhakikisha tunakuwa sehemu ya kuwasaidia kuzitatua changamoto hizo na utoaji wa taulo hizi ni sehemu ya mkakati wa kukamilisha adhima hiyo,’’ alisema.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Istiqaama Bw Mbaraka Songoro alisema msaada huo kutoka benki ya Exim si tu unaonyesha utu bali pia ni unaonyesha heshima kwa watoto wa kike.

"Sisi kama shule tunaona hii kama heshima kubwa kwa wapokeaji wa msaada huu na kwa jamii kwa ujumla. Misaada ya namna hii inaonesha namna watu na taasisi makini kama Benki ya Exim zinavyowachukulia watoto wa kike…tunashukuru sana '' Alisema

Akitoa neno la shukrani kwa benki hiyo kwa niaba ya wanafunzi wenzie, Mwananfunzi Fathihiya Faiz, kidato cha tatu .kutoka Shule ya Sekondari Istiqaama.alisema mbali na uhitaji walio nao kwa bidhaa hiyo muhimu pia wameupokea msaada huo kama ishara ya upendo na heshima kutoka kwa benki hiyo hatua ambayo itawafanya wasome wakitambua kuwa zipo taasisi na watanzania wanaowajali na kutambua changamoto za kijinsia wanazopitia.

"Kwa msaada huu tunaamini hatutakabiliwa tena na magonjwa ambayo yanaweza kutokea kwa ukosefu wa taulo za hedhi. Pia msaada huu utaziba pengo ambalo wazazi wetu hawawezi kuliziba kwa sababu ya changamoto kadhaa zinazowakabili zikiwezo za kiuchumi,’’ alisema.
 Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, wakiongozwa na Meneja wa Tawi hilo Bi Sarah Paul wakiwa kwenye picha ya pamopa na walimu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu Istiqaama iliyopo Mkoani Shinyanga baada ya kukabidhi msaadawa taulo za kike kwa wanafunzi hao mwishoni mwa wiki.
 Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, wakiongozwa na Meneja wa Tawi hilo Bi Sarah Paul (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamopa na walimu pamoja na wanafunzi wa Kituo cha Agape aids control Programme kilichopo Mkoani Shinyanga baada ya kukabidhi msaadawa taulo za kike kwa wanafunzi hao kituo hicho mwishoni mwa wiki.
 Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, wakiongozwa na Meneja wa Tawi hilo Bi Sarah Paul (katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na walimu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapinduzi iliyopo Mkoani Shinyanga baada ya kukabidhi msaadawa taulo za kike kwa wanafunzi hao.Kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) unaofahamika kama Exim Cares,  benki hiyo iliweza kutoa msaada taulo hizo kwenye shule sita zikiwemo za Msingi na Sekondari mkoani humo,mwishoni mwa wiki
 Ofisa Mauzo wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, Bi Stella Malebetoh (Kulia) akifurahi pamoja na baadhi ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu Istiqaama iliyopo Mkoani Shinyanga baada ya kukabidhi msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi hao. Kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) wa benki hiyo unafahamika kama Exim Cares, iliweza kutoa msaada taulo hizo kwenye shule sita zikiwemo za Msingi na Sekondari mkoani humo mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, Bi Sarah Paul (Kushoto) akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa walimu wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu Istiqaama iliyopo Mkoani Shinyanga ikiwa ni msaada wa benki hiyo kwa wanafunzi wa kike wanaosoma shule hiyo. Kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) unaofahamika kama Exim Cares,  benki hiyo iliweza kutoa msaada taulo hizo kwenye shule sita zikiwemo za Msingi na Sekondari mkoani humo,mwishoni mwa wiki.

KUNAMBI KUANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS MAGUFULI LA KULIPA FIDIA WANANCHI

$
0
0
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema Sh. Bil. 3.399 za kulipa fidia wananchi 1,526 wa Kikombo ili wapisha eneo la Kikombo
linalojengwa Makao Makuu Jeshi, anazo mkononi.

Amesema utekelezaji wa agizo hilo la Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ulianza Novemba 26 Mwaka huu, siku Moja tu baada ya agizo
kutolewa kwake likimtaka ifikapo Leo, Desemba 1 Mwaka huu awe ameanza kulipa fidia hiyo.

Lakini amesema wanufaika wa zoezi hilo hawajaanza kupokea malipo yao, kutokana na taratibu za ulipaji wa fedha za serikali ambao hata hivyo, Kunambi amesema zipo kwenye hatua za mwisho na wale ambao taratibu zitakuwa zimekamilika wataanza kupokea malipo wiki inayoanza kesho.

“Tupo tayari kulipa fidia lakini  zipo taratibu ambazo zinakamilishwa ili zoezi lianze, uhakiki wa malipo unafanywa na wizara ya fedha,
nimeambiwa umekamilika na nitakabidhiwa wiki ijayo.

Pia  kuna ambao hawakuwa na akaunti benki huku wengine walionazo zikiwa haziko ‘active’ watendaji wa mitaa wanaendelea kuwasaidia
katika kukamilisha hayo na ninahakika wiki ijayo watakaokuwa tayari wataanza kulipwa," Amesema Kunambi.

Kunambi amesema Kikombo ndiyo utakaokuwa mji mpya wa jiji hilo ambalo litakuwa na miji miwili; wa sasa ambao utakuwa mji wa zamani na
huo mpya.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma kuhusiana na utekezaji wa agizo la Rais Magufuli la kulipa fidia wananchi.

NBC kusaidia wanafunzi wanaoshindwa kumudu gharama za ada chuo kikuu

$
0
0


Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Emmanuel Mapunda (katikati) akisalimiana na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( DARUSO ) Bw. Hamis Mussa katika hafla ya kuchangisha fedha kwa njia ya vichekesho na burudani iitwayo ‘Cheka Nisome’ iliyodhaminiwa na NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada. . Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC Bw. David Raymond.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa Benki ya NBC Bw. David Raymond (kulia), akisalimiana na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( DARUSO ) Bw. Hamis Mussa katika hafla ya kuchangisha fedha kwa njia ya vichekesho na burudani iitwayo ‘Cheka Nisome’ iliyodhaminiwa na NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada. Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni Meneja wa NBC Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Emmanuel Mapunda.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond (kulia), akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika hafla ya kuchangisha fedha kwa njia ya vichekesho na burudani iitwayo ‘Cheka Nisome’ iliyodhaminiwa na NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada. Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Hafla hii iliratibiwa na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( DARUSO ).
Baadhi ya wahudhuriaji wakishangilia moja ya onesho lililokuwa likifanywa na mmoja wa wachekeshaji mahiri kutoka Kenya, Erick Omondi katika hafla iliyoandaliwa mwishoni mwa juma lililopita na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( DARUSO ) na kudhaminiwa na Benki ya NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada chuoni hapo.



SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA MUANZILISHI WA MASHIRIKISHO YA AMANI DUNIANI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Muanzilishi wa Mashirikisho ya Amani Duniani, Dkt. Hak Ja Han Moon walipokutana leo katika hoteli ya Serena ya Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akifurahia jambo na Muanzilishi wa Mashirikisho ya Amani Duniani, Dkt. Hak Ja Han Moon walipokutana leo katika hoteli ya Serena ya Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Muanzilishi wa Mashirikisho ya Amani Duniani, Dkt. Hak Ja Han Moon (wanne kulia) baada ya kuagana leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Wengine ni Waheshimiwa wa Bunge la Tanzania na Maafisa Waandamizi kutoka Mashirikisho ya Amani Duniani.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza jambo na Muanzilishi wa Mashirikisho ya Amani Duniani, Dkt. Hak Ja Han Moon walipokutana leo katika hoteli ya Serena ya Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Mashirikisho ya Amani Duniani, Ndg. Young Ho Yun.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

NAIBU WAZIRI SHONZA ASHIRIKI TAMASHA LA MAVAZI RED RIBBON FASHION SHOW 2019 JIJINI DAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wabunifu wa mavazi pamoja na wanamitingo wakati wa Tamasha la maonesha ya mitindo la Tanzania Red Rebbon Fashion Show 2019 lililofanyika jana Novemba 30/2019 Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo lilikuwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana liliandaliwa na Mwanamitindo mkongwe Bi. Khadija Mwanamboka kwakushirikiana na wanamitindo mbalimbali nchini.



WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA UHURU MWANZA.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na wajumbe wa kamati ya maandilizi ya Sherehe ya Uhuru zitakazofanyika Kitaifa Mkoa wa Mwanza wakiwasili kwa ajili ya Ukaguzi wa Uwanja wa CCM Kilumba utakaotumika kwa ajili ya sherehe hizo.Alitembelea tarehe 30 Novemba 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Afisa Maadhimishi kutoka ofisi yake, Bw.Stephen Magoha alipowasili katika Kijiji cha Hunghumalwa Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza ili kukagua jeshi la jadi (sungusungu) walioandaliwa kwa ajili ya kufanya onesho lao wakati wa kilele cha sherehe za Uhuru (9 Desemba, 2019).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Mkuu wa itifaki Balozi Kanali Wilbert Ibuge wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Kwimba apotembelea kukagua maandalizi ya Jeshi la Jadi (Sungusungu) wanaoendelea na maandalizi ya onesho maalumu katika sherehe za Uhuru mwaka huu.
Mkuu wa Itifaki Balozi Kanali Wilbert Ibuge akizungumza na Jeshi la Jadi (hawapo pichani) wanaoendelea na maandalizi ya onesho maalumu katika sherehe za Uhuru mwaka huu mkoani Mwanza.

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga na Mtemi wa Sungusungu wa Wilaya hiyo Bw. Mogan Shimbi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara yake kukagua maandalizi ya onesho maalum la sungusungu katika wilaya hiyo.

Sehemu ya wajumbe walioshiriki kukagua onesho la sungusungu Wilaya ya Kwimba (hawapo pichani) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimishi ya miaka 58 ya Uhuru kwa mwaka 2019.

Baadhi ya wajumbe wa Jeshi la Jadi (sungusungu) wakiimba mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na viongozi alioambatana nao wakati wa ukaguzi wa maandalizi ya Maadhimishi ya 9 Desemba, 2019 mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Christopher Derek wakiangalia Gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama nchini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sherehe Uhuru kwa mwaka 2019.
Mtemi wa Sungusungu wa Wilaya Kwimba mkoani Mwanza Bw.Mogan Shimbi akiwaongoza wajumbe wa jeshi hilo kuimba wimbo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya onesho lao la Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

****************************************

NA.MWANDISHI WETU

Maandalizi ya maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru yamefikia hatua za kuridhisha huku Serikali ikieleza kuwa sherehe hiyo itapambwa na onesho maalum la Jeshi la Jadi la sungusungu kutoka Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameeleza itakuwa ni mara ya kwanza kwa jeshi hilo kuonesha namna wanavyofanya kazi za ulinzi katika maeneo yao ili kuendelea kuenzi nia ya Rais wa Awamu ya Tano Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ya kuilinda amani na utulivu uliopo nchini.

Waziri alieleza hayo mapema Novemba 30, 2019 alipotembelea na kukagua maandalzii ya onesho hilo yanayoendelea katika Kijiji cha Hunghumalwa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

“Hii itakuwa ni mara ya kwanza kuwa na onesho hili maalum ambalo linatukumbusha nia ya Mhe. Rais ya kuilinda amani iliyopo na kuhakikisha haichezewi kwa gharama yoyote na kuona namna tunavyojivunia jeshi hili lililoundwa katika misingi na maadili mema ya amani na utulivu,” alisema waziri Mhagama

Aliongezea kuwa, Jeshi hilo litajumuisha zaidi ya sungusungu 1300 watakaoshiriki kwa siku hiyo kwa kuongozwa na Manji wao pamoja na Mtemi wa Wilaya Mogan Shimbi.

Sambamba na hilo maandalizi mengine ikiwemo, uandaaji wa uwanja wa CCM Kilumba, mazoezi ya Majeshi (Gwaride), Usafi wa mazingira pamoja na vikundi vya burudani yanaendelea mkoani hapo.

“Maandalizi muhimu ikiwa ni pamoja na marekebisho ya miundombinu katika uwanja yanaendelea pamoja na maandalizi muhimu ikiwemo, kutoa mialiko, kuandaa malazi kwa wageni, kuandaa vikundi vya ngoma za asili, kuandaa gwaride , kuandaa wanafunzi wa watakaoumba umbo la bendera, pamoja na nyimbo za kizazi kipya na mahitaji mengine muhimu yapo katika hatua za kuridhisha,” alisema Waziri Mhagama

Aidha, kutakuwa na vikundi vya burudani ikiwemo; ngoma za asili kutoka mkoa wa Mara (Ritungu) na mkoa wa Mwanza, wimbo maalum kutoka Zanzibar pamoja na kwaya ya AIC Mwanza na bendi ya Tanzania One Theatre (T.O.T) vitatumbuiza.

Alifafanua kuwa maonyesho hayo yatakayofanyika Desemba 9 yatajumuisha gwaride maalumu la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama nchini.

“Watoto 3200 kutoka shule za msingi na sekondari za mkoa wa Mwanza wataonesha umbo la bendera ya Taifa letu,” alisema Waziri Mhagama

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella aliwasihi Watanzania kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuendelea kuilinda amani iliyopo kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu pamoja na kuendelea kuwa na uzalendo na kufanya kazi kwa bidiii kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

Pia, aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo na kuendelea kujiandaa kwa bidii, usanifu na ubunifu wa kipekee katika kuiadhimisha siku hiyo muhimu.

“Ninamshukuru sana Mhe. Rais kwa kuelekeza maadhimisho haya kufanyika mkoani kwetu, niiwaase wananchi wa Mwanza kuitumia heshima tuliyopewa kwa kujitokeza kwa wingi katika siku hiyo ili kuunga mkono jituhada za Mhe. Rais wetu,” Alisisitiza Mongella.

Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri kwa mwaka huu (2019) kitaifa yatafanyika Mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kilumba ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli na kupambwa na kauli mbiu inayosema “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Tifa letu”.

SEKTA YA ARDHI YATAKIWA KUPEWA KIPAUMBELE KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Eng. Stellah Manyanya amezitaka idara mbalimbali za Serikali kuipa kipaumbele sekta ya ardhi katika mipango ya maendeleo inayofanyika nchini.

Eng. Stellah Manyanya ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano mkuu wa sita wa Mwaka wa Wataalaamu wa Mipangomiji ulioanza tarehe 27 hadi 29 Novemba 2019 jijini Dodoma.

Eng. Stellah Manyanya amesema, kumekuwepo na miradi mingi nchini inaanzishwa na Serikali inatumia gharama kubwa katika kuikamilisha matokeo yake imekuwa haitumiki na wakati mwingine inaingiliana na shughuri nyingine za kijamii hali inayopelekea kuzuka kwa migogoro katika jamii.

Akitolea mfano Jengo la Machinga Complex lililopo Ilala Jijini Dar es Salaam, Eng. Stellah Manyanya amesema kuwa kutokuwepo kwa mipango kina ya muda mrefu na utafiti duni ndio chanzo kikubwa hadi leo hii jengo hilo kushindwa kufikia lengo walilojiwekea la kuwa saidia wafanyabiashara wadogowadogo kuwa na sehemu yao ya kufanyia shughuri zao.
Viewing all 110027 articles
Browse latest View live




Latest Images