Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

SIMBA SC YAACHANA NA KOCHA AUSSEMS, MWAMBUSI AJIUZULU MBEYA CITY

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Klabu ya Soka ya Simba rasmi imeachana na Kocha wake Mkuu, Patrick Aussems baada yakuvunja mkataba wake kutokana nakushindwa kutekeleza majukumu yake kwa viwango na malengo ambayo Klabu hiyo ilikubaliana naye kwenye mkataba wa ajira.

Taarifa ya Klabu hiyo iliyotolewa leo kuhusu kuachwa kwa Kocha huyo imeeleza kuwa licha ya jitihada za Bodi ya Klabu hiyo kumpa ushirikiano Kocha huyo alisimamia timu hiyo bila kujali malengo ya Klabu, maamuzi hayo yamefanywa siku tano tangu kusimamishwa kwake kwa maswala yakinidhamu.

Taarifa hiyo imeeleza maelezo ya Kocha huyo yaliyotolewa mbele ya Kikao cha Kamati ya Nidhamu Novemba 28 mwaka huu hayakuiridhisha Kamati hiyo dhidi ya tuhuma za Kocha huyo kuondoka Kiktuo cha Kazi bila ruhusa ya Uongozi wa Klabu licha yakukataa kuiambia Kamati sehemu alipokuwa na sababu za kwenda bila ruhusa.

Simba SC kupitia taarifa hiyo imesema itaanza mara moja mchakato wakutafuta mbadala wa Kocha Mkuu, tayari Kocha Msaidizi, Dennis Kitambi ameteuliwa Kukaimu nafasi hiyo ya Kocha Mkuu hadi atakapopatikana mwengine.

Katika hatua nyingine, Klabu ya Mbeya City ya Mbeya imeridhia kujiuzulu kwa Kocha Mkuu, Juma Mwambusi baada yakuwasilisha ombi lake lakujiuzulu tangu Novemba 26 mwaka huu.

Kupitia taarifa ya Klabu hiyo iliyotolewa leo  imeeleza kuwa Mwalimu Mwambusi aliwasilisha ombi hilo kufuatia mwenendo wa timu usioridhisha tangu kuanza kwa Ligi Kuu msimu huu.

Pia, Mbeya City imemkabidhi timu hiyo, Kocha Msaidizi, Mohammed Kijuso wakati mchakato wakutafuta Kocha mpya ukiendelea.

Tanzania na Namibia Zaweka Mikakati ya Kujiimarisha Kiuchumi

$
0
0
Viongozi katika Meza Kuu. Kutoka kulia ni Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Mhe. Theresia Samaria; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Namibia, Balozi Selma Ashipala-Musavyi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Joseph Buchweishaija. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano wa JPC ngazi ya Makatibu Wakuu akisoma hotuba ya ufunguzi ya Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia. 
Dkt. Mnyepe akiendelea kusoma hotuba, huku wajumbe wakimsikiliza. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Namibia, Balozi Selma Ashipala-Musavyi ambaye ni Mwenyekiti mwenza akisoma hotuba ya ufunguzi katika mkutano huo. 

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Wilbroad Kayombo akifanya utambulisho wa viongozi wa Tanzania wanaoshiriki mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC). 
Waliokaa mstari wa mbele ni Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wanaoshiriki mkutano wa JPC ambao walikuwa wanatambulishwa na Bw. Kayombo. 
Wajumbe wanaoshiriki kikao cha JPC wakifuatilia hotuba za viongzo zilizokuwa zinawasilishwa.
Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za Tanzania na Namibia, Dkt. Faraji K. Mnyepe na Balozi Selma Ashipala-Musavyi wakipongezana baada ya kuwasilisha hotuba za ufunguzi katika Mkutano wa JPC kati ya Tanzania na Namibia. 
Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Elizabeth Rwetunga akiongoza wajumbe wa mkutano kupitia rasimu ya taarifa ya masuala waliyoyajadili na kukubaliana. 
Watumishi kutoka Taasisi za Serikali wakifuatilia Mkutano wa JPC. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Wilbroad Kayombo akiongea na vyombo vya habari kuhusu mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Namibia. 
Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za Tanzania na Namibia, Dkt. Faraji K. Mnyepe (mwenye suti) na Balozi Selma Ashipala-Musavyi wakiongea na waandishi wa habari kuhusu JPC kati ya Tanzania na Namibia. 
Viongozi wa Tanzania na Namibia wakiwa katika picha ya pamoja. 




SHIRIKA LA FIKRA MPYA LAENDESHA KONGAMANO KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

$
0
0
Shirika lisilo la kiserikali liitawalo Fikra Mpya la Mkoani Shinyanga, linalofanya shughuli ya kutoa elimu ya kujitambua kwa mtoto wa kike, limeendesha Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa kike kutoka Shule za Sekondari Nane Mjini Shinyanga.

Kongamano hilo limefanyika leo Novemba 30, 2019, kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ualimu mjini Shinyanga (Shycom), na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo, wakiwemo maofisa ustawi jamii, maendeleo, dawati la jinsia kutoka polisi, walimu, pamoja na wazazi. Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah, amesema wameendesha Kongamano hilo kwa wanafunzi wa kike, ili kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, ikiwemo kutokomeza tatizo la mimba na ndoa za utotoni, ambalo limekuwa likizima ndoto za wanafunzi walio wengi. 

Amesema wameendesha Kongamano hilo kama sehemu ya kuadhimisha siku 16 za kupinga Ukatili wa kijinsia, ambayo ilianza kuadhimishwa Novemba 25 mwaka huu na itahitimishwa Desemba 10, kwa kufanya mijadala mbalimbali ya kujadili namna ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake. “Shirika letu tumeamua kuendesha Kongamano hili la kupinga vitendo ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa kike, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, ambapo tunajadili kwa pamoja na wanafunzi ili kupata suluhu ya kutokomeza ukatili na wanafunzi wapate kutimiza ndoto zao,” amesema Josiah. 

“Mkoa wetu wa Shinyanga na Kanda ya ziwa inatajwa kuongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake, ambapo takwimu zinaonyesha kuanzia Januari hadi Juni 2019 kanda ya ziwa inaongoza kwa asilimia 38, ikifuatiwa na mikoa ya nyanda juu kusini asilimia 32, Pwani asilimia Tisa (9), “Kanda ya kaskazini asilimia Tisa (9), Kanda ya Kati asilimia Saba (7), pamoja na Kanda ya Magharibi asilimia Tano (5),”ameeleza Josiah. 

Naye mgeni Rasmi kwenye Kongamano hilo Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Kamara Beda, akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewataka wanafunzi wanapokuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili wasikae kimya, bali watoe taarifa ili wahusika wapate kuchukuliwa hatua na kukomesha vitendo hivyo.

 Nao baadhi ya wanafunzi akiwemo Mariamu Charles kutoka Shule ya Sekondari Mwasele, wameshukuru kuendeshwa kwa Kongamano hilo, ambalo wamedai limewasaidia kuwapatia upeo namna ya kupinga vitendo ya ukatili wa kijinsia, pamoja na wapi pa kwenda kutoa taarifa hizo. Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Mkoani Shinyanga Leah Josiah akizungumza kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia leo Jumamosi Novemba 30,2019. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Mkoani Shinyanga Leah Josiah akizungumza kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia. Mgeni Rasmi Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Kamara Beda akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye Kongamano la Kupinga ukatili wa kijinsia. Wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia. Wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia. Mratibu kutoka Shirika la Women Fund Tanzania Mkoani Shinyanga Glory Mbia, akifungua mjadala wa kujadili juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutafuta suluhu ya kuvitokomeza. Mwenyekiti wa baraza la watoto manispaa ya Shinyanga Rose Matiku akichangia mada kwenye Kongamano hilo la kupinga ukatili wa kijinsia. Afisa wa Jeshi la Polisi kutoka dawati la Jinsia wilaya ya Shinyanga Joseph Christopher, akichangia mada kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia, wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah. Mzazi Aida Luben akichangia mada kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia. Mwanafunzi Mariam Charles kutoka Shule ya Sekondari Mwasele akichangia mada kwenye Kongamano hilo la kupinga ukatili wa kijinsia. Awali wanafunzi wakiingia kwa maandamano kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa Kijinsia. Mgeni Rasmi afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Kamara Beda akipokea maandamano kwenye Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia. Wageni waalikwa wakiwa na mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia. Wageni waalikwa, wanafunzi pamoja na mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya ,wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

PINDA AKUMBUSHIA ALIVYOTESWA NA MAUAJI YA WENYE UALBINO, SAKATA LA KUCHINJA KANDA YA ZIWA

$
0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Agri Thamani Foundation Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza kwenye hafla ya viongozi wa dini kusaini makubaliano ya mapambano ya ugonjwa wa Kifua Kikuu kupitia majukwaa ya nyumba za ibada jana jijini Mwanza.
…………….



NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

MWENYEKITI wa Taasisi ya AGRI THAMANI Foundation, Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda, amesema mauaji ya watu wenye ualbino na sakata la kuchinja Kanda ya Ziwa lilimfanya auone Uwaziri Mkuu mchungu.

Pinda alisema jana jijini Mwanza wakati akizungumza kabla alisema viongozi wa dini kabla ya kusaini makubaliano ya kutumia nyumba za ibada kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa wa Kifua Kifuu (TB).

Alidai anafarijika na kupata matumaini mkutano huo kufanyika Mwanza kwa sababu wakati akiwa Waziri Mkuu yaliibuka mauaji ya watu wenye ualbino lakini pia ubishani wa nani achinje kati ya Wakristo na Waislamu mambo ambayo yalimfanya Uwaziri Mkuu auone mchungu lakini yaliisha salama baada ya kushirikiana na viongozi wa dini na kukafanikiwa na leo hayapo.

Alisema viongozi wa dini wana nguvu mbili, moja ni ukaribu wao na Mungu, wanapowaombea watu kiroho wanapona, ya pili wamebeba kundi kubwa la jamii, wanasikilizwa na wakisema jambo linakwenda sawia hivyo ushiriki wao kwenye vita ya kupambana na TB utakuwa na tija na makubaliano hayo kusainiwa Kanda ya Ziwa, unaweza kuwa uwanja mzuri wa vita ya TB kutokana na kanda hiyo kuwa na watu milioni 12 ambapo asilimia 20 ikiwekwa pamoja inawezekana kupata matokeo chanya..

Alisema ugonjwa huo unasumbua taifa kwa sababu ya maadui waliotajwa na Mwalimu Nyerere ( umaskini, ujinga na maradhi) hivyo umaskini na ujinga ukiondolewa TB itatokomezwa na kushauri kila halmashauri kujenga uwezo wa watendaji na mifuko ya lishe itumike ipasavyo na kutafuta mbinu ya kuzungumza lugha moja.

Utiaji saini huo ulishuhudiwa na Spika wa Bunge Job Ndugai ambaye alikuwa mgeni rasmi, Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda,Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Jenister Mhagama, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Serikali za Mitaa na Tawala za mikoa Joseph Kandege na mwenyekiti wa Kamati ya wabunge hao, Oscar Mukasa.

Miongoni mwa viongozi wa dini waliosaini makubaliano ya mapambano ya TB yalioasisiwa na Mtandao wa Wabunge walio kwenye mapambano ya kudhibiti ugonjwa huo wa Kifua Kikuu nchini ili kutumia nyumba za ibada kufikisha ujumbe na elimu kwa jamii ni kutoka Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC), Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste (CCT), Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA).

Aidha, Askofu Renatus Nkwande (TEC), Askofu Mark Malakana (SDA), Sheikh Hassan Chizenga (BAKWATA) na Askofu Cheyo,walisema kwa nyakati tofauti kuwa jukumu hilo wamelibeba kwa maslahi ya watanzania kuhakikisha hawaathiriwi na vimelea vya TB.

“Kujadili na kuunganisha nguvu na viongozi wa dini kupamban na TB ni wazi watafikisha ujumbe kwa waumini sababu kanisa tiba kwao ni wajibu .Kutuhusisha kuelemisha jamii ni wazi jambo hili litakwisha,”alisema Askofu Nkwande.
“Jambo hili tumelipokea kwa mikono miwili, kwangu na wachungaji wa SDA suala la mafundisho ya afya ni sawa na kumsukuma mlevi.Magonjwa yanaletwa kwa kukiuka misingi iliyowekwa na Mungu.Tunataka Tanzania bila TB inawezekana, hivyo vita hiyo ni wajibu wa kila mmoja kuibeba ili tulifute;tutalifikishaje, ni kutoa elimu kwani watu kufa si heshima, waliumbwa wafurahie maisha yao,”alisema Askofu Malekana.

Mwenyekiti wa mtandao wa wabunge hao Oscar Mukasa kabla ya hafla hiyo alisema majukwaa ya nyumba za ibada yanalenga kuifikia jamii elimu itakayosaidia kuongeza ufahamu wa TB, namna ya kujikinga na kupata tiba lakini pia maelekezo ya serikali yatafika kwa usahihi , eliemu ambayo itawafikia watanzania wengi na itakuwa endelevu

Kwa mujibu wa takwimu watu milioni 18 nchini wanavimelea vya TB ambapo watu 100,000 kati ya 142,000 wana tatizo hilo, pia mwaka 2018 watu 75000 waligundulika kuwa na TB, asilimia 67 hawakuwa kwenye tiba, 39,000 walipoteza maisha na watu 60 hufariki kila siku mtu mmoja anaweza kuambukiza watu 10 hadi 20 kwa mwaka.

Aidha, watu milioni 1.5 walipoteza maisha mwaka 2018 ambapo watu milioni 7 walikuwa kwenye tiba huku milioni 3 wakiwa hawajulikani walipo ama walikufa jambo linaloonyesha TB bado ni tishio ikizingatiwa theluthi moja ya watu duniani wameambukizwa vimelema vya ugonjwa huo.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema jumuiko na dhamira ya viongozi wa dini kwenye mapambano ya TB litaongeza chachu, kuja na ubinifu na jamii kuacha mazoea ambapo serikali kupitia wizara hiyo itaendelea kuchukua hatua ya kupambana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja kutoa dawa bure, vifaa tiba na vitendanishi.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Vijana na Ajira, Jenister Mhagama, alisema tatizo la TB ni pacha na Ukimwi pamoja na dawa za kulevya nchini hivyo nguvu inayotumika kuhakikisha maambukizi mapya hayatokei ipelekwe kwenye vita hiyo.

Alisema nguvu kazi ya taifa ni vijana ambao ni asilimia 56 ndio waathirika wakubwa na bila kujipanga vizuri tutajikuta tunaingia kwenye uchumi wa viwanda tukiwa na tatizo na kupoteza malengo tunayoweka lakini serikali itaendelea kutoa mchango mkubwa ili kupambana na maradhi hatarishi.

Mgeni rasmi Ndugai alisema aliamua mkutano huo ufanyike Mwanza ili kufikisha elimu vizuri na kuwaeleza wananchi wa Kanda ya Ziwa kuna tatizo kubwa la TB na kuonya waachane na imani potofu za kuamini kila ugonjwa na kifo una mkono wa mtu.

KITUO CHA AFYA KOME KUPEWA X-RAY YA KIDIGITALI

$
0
0
Waziri Ummy Mwalimu akimjulia hali Bi Adela Deus aliyekuwa akipokea huduma baada ya kujifungua katika kituo cha Afya Kome.

Waziri Ummy Mwalimu akimjulia hali Bi. Ester Juma, mzazi aliyejifungua katika kituo cha Afya Kome, kisiwa cha Kome kilichopo Mkoa wa Mwanza.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Wananchi waliofika kwenye mkutano, wakati alipofanya ziara katika Kisiwa cha Kome Jijini Mwanza.
Mbunge wa Buchosa Mhe.Charles Tizeba akiongea na wananchi wa kisiwa cha Kome, wakati wa ziara ya Waziri wa Afya Mhe.@umwalimu (hayupo kwenye picha) katika kisiwa hicho.
Wananchi waliofika kwenye mkutano, kumsikiliza Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara katika Kisiwa cha Kome Jijini Mwanza.

………………….

Na.Catherine Sungura,Buchosa

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameahidi kuwapatia mashine ya x-ray ya kisasa ya kidigitali kituo cha afya kome kilichopo halmashauri ya Buchosha wilayani Sengerema.

Waziri Ummy ametoa ahadi hiyo akiwa kwenye ziara ya kikazi kisiwani hapo ya kujionea hali ya utoaji huduma za afya.

“Ninawaahidi wananchi nitaleta x-ray mashine ya kidigitali kwenye kituoa hichi cha afya ili msivuke maji kwenda kupata huduma za vipimo wilayani sengerema”.Alisema Waziri Ummy

Aidha, alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosha Crispian Luanda pamoja na Mganga Mkuu wake Dkt. Ernest Chacha kwa jitihada kubwa wanazofanya za kuboresha huduma za afya kwenye halmashauri hiyo”Nimefurahi kumuona daktari wa upasuaji kwenye kituo hiki na hongereni kwa kumpatia mafunzo ya mwaka mzima kwenye eneo hili,sasa mnatakiwa kuweka vifaa na huduma za mtoto njiti ili kusiwepo na vifo vya watoto hao endapo itatokea”.

Hata hivyo Waziri Ummy aliwataka akina mama wa kisiwa hicho kuhudhuria kliniki mara nne mara wanapokuwa wajawazito ili kuepukana na vifo vya wajawazito na watoto pamoja na kuepusha kuzaa watoto walemavu.

“Tumeanzisha huduma za upasuaji kwenye kitua hiki cha afya tunataka mama mjamzito wa Kome akipata tatizo la mtoto kukaa vibaya tumboni au mama akipata kifaa cha mimba asaidiwe hapa hapa”Alisisitiza Waziri Ummy.

Naye Mbunge wa Buchosa Dkt. Charles Tizeba ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kuwajengea jengo la upasuaji pamoja na vifaa hivyo kuondoa tatizo kubwa la upasuaji lililokuwa linawakabili wananchi wa Kome na kuomba wizara kuwapatia vifaa vya vipimo katika vituo vya huduma za afya kwenye halmashauri hiyo kwani wananchi wameanzisha ujenzi wa zahanati 30 kwa nguvu zao hivyo wakikamilisha miundombinu huduma za afya zitakuwa zimeboreshwa kwenye jimbo lake.

Kisiwa cha Kome kimeongeza idadi ya akina mama wanaojifungulia kwenye vituo vya huduma za afya kutoka asilimia 42 mwaka 2015 kati ya akina mama 100 hadi kufikia asilimia 80 kwa mwaka ambapo wastani wa akina mama 50 wanajifungua kwa mwezi.

Barclays Bank hosts its Zanzibar customers to a thanks-giving cocktail event

$
0
0
Barclays Bank Tanzania Limited (BBT) on Tuesday, 26th of November hosted its Zanzibar customers to a cocktail event. The event was not only a platform to appreciate the continued support of its customers but was also used to provide an opportunity for clients to join BBT in its transition journey and be informed of the expected milestones as the Bank prepares to rebrand into Absa.

Speaking during the event, the bank’s Managing Director, Mr. Abdi Mohamed said, “Our brand and name change to Absa is proceeding as planned. We have taken a sequenced approach and expect some branches to reflect several elements of the new brand in the first half of December, while some branches will retain the current look. The intention is to take our customers and the public with us through the transformation journey visually. We will however continue to operate and trade as Barclays Bank Tanzania Limited until our name officially changes, as approved by the Regulator.”

Speaking on the bank’s commitment to Tanzania, Mr. Mohamed said, “Barclays is committed to serving its customers and we are proud of the momentum we have built over the past 3 years. Our commitment to our clients has been demonstrated in the successful execution of key financing transactions amounting to TZS 529bn, across sectors such as Oil & Gas, Public Sector, Manufacturing and Agriculture. In addition, our non-funded strategy and focus has been reaffirmed by The Asian Banker 2019 recognition of BBT as the best ‘Cash Management Bank in Tanzania’.

Responding to a question on whether customers can have the same confidence in Absa as they had in Barclays, the bank’s Head of Retail Banking, Mr. Oscar Mwamfwagasi said ”Absa Group is committed to building on Barclays' heritage in Africa and the strengths that we already have on the continent. We have a deep history and local knowledge in Tanzania. Our main products and services haven’t changed. Our customers can bank with us as confidently as they always have.

You can bank with us as safely as you always have. Absa Group is one of the largest banking groups in Africa, with a balance sheet of more than USD 91 billion, as well as new systems with robust security provisions. ”

In conclusion, Mr. Mwamfwagasi; called for clients to remain vigilant, saying “We will not ask any customer for additional information during this time, and all customer account details will remain the same before and after the transition.”

Barclays Bank’s Managing Director, Abdi Mohamed (on the right) in conversation with a client during the cocktail event.
Barclays Bank’s Finance Director, Obedi Solomon Laiser (in the middle) engaging with clients during the cocktail event.

Barclays Bank’s Human Resource Director, Patrick Foya ( right) engaging with customers during the cocktail event


Barclays Bank’s Chairman, Simon Mponji (left) and Dr Suleiman Rashid Mohamed (extreme right) in conversation with clients during the cocktail event.

Barclays Bank’s Corporate Director, Brian Kalero (Right) in conversation with clients during the cocktail event.

MWANA FA: MIMI SINA OFISI BASATA, SIFUNGII WIMBO WA MTU....

$
0
0

Na Khadija Seif, Michuzi TV

MWAMUZIKI  nguli wa Bongofleva Hamis Mwinjuma  a.k.a Mwana FA amesema wasanii waache lawama kipindi kazi zao zinapofungiwa katika baraza la Sanaa (BASATA).

Mwana FA  (pichani) ameyasema hayo katika mahoijiano maalumu, kufuatia minong'ono inayoendelea ya yeye kuhusishwa na ufungiwaji wa kazi za wasanii Basata.

"Mimi ni mjumbe tu wa baraza la Sanaa (BASATA) sihusiki na jukumu la kumfungia mtu kazi zake na wala sina ofisi pale basata kwahiyo wasanii wasinitupie lawama najaribu kufanya kazi na utaratibu ambao baraza kama baraza huwa wananipangia na mara nyingi nimekua  kama mshauri kwa wasanii wenzangu linapotokea tatizo lolote lile", amesema.

Mwana FA  ametaja changamoto kadhaa ambazo wanazipata wasanii wachanga ni ikiwa ni pamoja na tuzo zinazotolewa na kuwepo dhana na ukandamizwaji au kubaguliwa na amemtaja Marehemu Sam wa Ukweli kama kielelezo tosha.

"Kuna tuzo zilikuwepo na katika kinyang'anyiro hicho Marehemu Sam wa Ukweli alikua akishiriki na ikaonekana wazi wazi kuwa wamembania na kumnyima tuzo wakati ni kitu ambacho Mashabiki wanajua alistahili hivyo kwa namna moja au nyingine ilimvunja moyo na kumrudisha nyuma kimuziki," ameelez.

Mwana  FA alichukua nafasi hiyo kuwapongeza  Watanzania wote kwa uzalendo walioonyesha na kuhamasika kujaa uwanjani na kumshangilia bondia Hassan Mwakinyo usiku wa kuamkia  novemba 30 Mwaka huu.

"Wakati mwengine tukiwa pamoja na tukijenga nguvu katika michezo yetu na kuwapa moyo wachezaji huwa wanajitoa na kuona nia ya kuwakilisha Taifa na kulitoa kimasomaso kutokana na hamasa wanazozipata", ameeleza Mwana FA ambaye pamoja na msanii Ommy Dimpoz, Ney wa Mitego na Profesa Jay walikuwa mstari wa mbele  katika kutoa hamasa kwenye mpambano huo ambao Mwakinyo alishinda kwa pointi.


MUONEKANO MPYA WA CRISTIANO RONALDO


WATAKAOAJIRI WATOTO CHINI YA MIAKA 18 KWENYE TUMBAKU KUKIONA CHA MOTO – MHE HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari tarehe 30 Novemba 2019 kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesisitiza marufuku yake aliyoitoa hivi karibuni kuhusu ajira kwa watoto ambao wapo chini ya miaka 18.


Mhe Hasunga amepiga marufuku hiyo leo tarehe 30 Novemba 2019 wakati akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam.


Alisema kuwa suala la ajira kwa watoto ni miongoni mwa mambo yanazuiliwa kwenye Sheria za kimataifa kupitia Shirika la Kazi Duniani (International Labour Organization) na Sheria za Ajira hapa nchini hivyo mdau yeyote atakayebainika kukiukwa maelekezo hayo atashtakiwa.


“Nawasihi wadau wote hususani wakulima wa Tumbaku tuendelee kupiga vita ajira kwa watoto kwa kuwa ni eneo ambalo limeendelea kulalamikiwa na wadau wengi” Alikaririwa Mhe Hasunga


Kadhalika, Mhe Hasunga alisema kuwa katika kuhakikisha zao la tumbaku linaendelea kutoa mchango mkubwa katika pato la mkulima na Taifa, Wizara imejiwekea malengo ya haraka yanayopaswa kutekelezwa ambayo ni pamoja na usajili wa wakulima wote wa tumbaku, kuwapatia vitambulisho na kuwaingiza kwenye kanzidata ili kupata takwimu za uhakika za maeneo wanayolima na kuiwezesha serikali kusimamia upatikanaji wa pembejeo kulingana na mahitaji yao.


Aidha, mipango mingine ni kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo kwa wakati kwa kuweka utaratibu wa kumwezesha mkulima kujitegemea kwa pembejeo ili aache kuwa tegemezi wa mikopo ya mabenki yenye riba kubwa.


Pamoja na malengo hayo ya haraka, Wizara ya Kilimo inasimamia utekelezaji wa malengo ya muda mrefu yakiwemo Upatikanaji wa wanunuzi wapya wa tumbaku kwa sasa na kwa miaka ijayo kabla ya Juni, 2020, Kuongeza ubora wa zao la tumbaku kutoka asilimia 87 ya sasa hadi asilimia 92 ifikapo Juni 2022 na Kuongeza mbegu mpya na bora za tumbaku ili tuweze kupata masoko katika nchi nyingine kama vile China.


Alisema ili kufikia malengo hayo wadau wote wa tasnia ya tumbaku wanapaswa kushirikiana ili kufikia malengo hayo na wakulima kunufaika na jasho lao.


Tumbaku ni miongoni mwa mazao makuu ya kimkakati ya yaliyopewa kipaumbele na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mazao mengine ni pamoja na Tumbaku,  Kahawa, Pamba, Korosho, Chai, michikichi na alizeti.  


Mhe Hasunga alisema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa malengo ya uzalishaji yanafikiwa kwa kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo kwa wakati, kuboresha huduma za ugani na kutafuta masoko mapya ya tumbaku.


Waziri Hasunga amesema kuwa katika msimu wa kilimo 2019/2020 ambao masoko yake yataanza mwezi Mei 2020, kampuni za ununuzi zilizopo nchini ambazo ni Alliance One Tanzania, Premium Active Tanzania na Japan Tobacco International zimetoa mikataba ya kilo 42,225,985 na tayari wakulima wapatao 33,000 wameomba kusajiliwa na Bodi ya Tumbaku kutokana na uzalishaji huo. Uzalishaji huo ni mdogo na hivyo unaacha wakulima takribani 16,000 bila kulima tumbaku msimu huu.


Kutokana na hali hiyo, Wizara ya Kilimo kupitia Bodi ya Tumbaku ilianzisha jitihada za kutafuta masoko mengine ili kuziba pengo la kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco – TLTC ambayo haijatoa makisio ya uzalishaji msimu huu.


Jihada hizo zimepelekea kupata kampuni nne (4) mpya ambazo zimeonesha nia ya kununua tumbaku ya Tanzania msimu ujao . Kampuni hizo Kampuni za Zambia kupitia kampuni ya kizawa ya MAGEFA GROWERS Ltd itanunua kilo 5,500,000, Kampuni ya TRANSAFRICQUE kupitia kampuni ya kizawa ya GRAND TOBACCO GROWERS Co. Ltd imeomba kununua kilo 9,000,000, Kampuni ya PETROBENAitanunua kilo 300,000, na Kampuni ya PACHTEC  Limited imeomba kununua kilo 500,000


Takwimu zinaonesha kwamba kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 hadi kufikia mwaka 2016 tumbaku imekuwa na mchango mkubwa wa kuliingizia Taifa fedha za kigeni.  Kwa mfano katika mwaka 2017, tumbaku iliingiza fedha za kigeni kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 195.8 ikishika nafasi ya pili baada ya zao la korosho. Licha ya faida kwa taifa, pia, uzalishaji wa tumbaku unawanufaisha wakulima, wanunuzi, viwanda vya kusindika tumbaku, mabenki, wasambazaji wa pembejeo, Halmashauri za wilaya na wadau wengine katika mnyororo wa thamani.

CWT KUJENGA KIWANDA CHA MIKATE LISHE SIMIYU

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe (mwenye tai kushoto) akimkabidhi Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania, Mwl. Deus Seif(mwenye suti nyeusi kulia) hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2) kilichopo Ng’hami wilayani humo ambacho Halmashauri imekitoa bure kwa CWT kwa ajili ya kujenga kiwanda cha mikate lishe.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe (kulia) akiwaongoza viongozi mbalimbali kwenda katika kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2) kilichopo Ng’hami wilayani humo , kilichotolewa bure na Halmashauri kwa CWT kwa ajili ya kujenga kiwanda cha mikate lishe kabla ya makabidhiano ya hati ya kiwanda hicho kati yake na Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania, Mwl. Deus Seif Novemba 29, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akitoa maelezo kwa viongozi mbalimbali katika kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2) kilichopo Ng’hami wilayani humo , kilichotolewa bure na Halmashauri kwa CWT kwa ajili ya kujenga kiwanda cha mikate lishe kabla ya makabidhiano ya hati ya kiwanja hicho kati yake na Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania, Mwl. Deus Seif Novemba 29, 2019.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza kabla ya makabidhiano ya hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2) kilichopo Ng’hami wilayani Maswa , kilichotolewa bure na Halmashauri kwa CWT kwa ajili ya kujenga kiwanda cha mikate lishe kabla ya makabidhiano ya hati ya kiwanja hicho kati Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe na Katibu M wa Chama cha Walimu Tanzania, Mwl. Deus Seif Novemba 29, 2019.

……………………

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kinatarajia kujenga kiwanda cha mikate lishe kupitia kampuni yao inayosimamia Maendeleo ya Walimu ya biashara (TDCL), katika eneo la Ng’hami wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Akimkabidhi Katibu wa Chama cha Walimu Nchini, Mwl. Deus Seif hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2), Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe amesema wilaya imetoa kiwanja hicho bure, ikiwa ni moja ya njia ya kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda ambapo kumhakikishia upatikanaji wa malighafi ya kiwanda hicho (viazi lishe)

“Tumejipanga kuzalisha viazi lishe vya kutosha vitavyotumika kama malighafi ya kiwanda hiki na tayari wakulima wamepewa mbegu za viazi hivyo, niendelee kuwakaribisha CWT wilayani Maswa, kama kuna uwekezaji mwingine mnahitaji kufanya karibuni, hata kama ni tawi la benki yenu ile ya walimu tunawakaribisha sana,” alisema Dkt. Shekalaghe.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Simiyu amesema kukamilika kwa kiwanda hicho kutasaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa lishe ambalo limekuwa ni changamoto kwa Mkoa wa Simiyu.

Aidha, Mtaka amesisitiza Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashautri na wataalam wa kilimo wahakikishe mbegu ya viazi lishe inapatikana kwa wingi ili wananchi wanapohitaji waipate

Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Taifa, Mwl. Deus Seif amesema chama hicho kinaunga mkono sera ya Tanzania ya Viwanda huku akibainisha kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utaenda haraka kwa kuwa tayari kampuni ya CWT inayosimamia miradi imeshaanza kulifanyia kazi suala hilo.

Ameongeza kuwa pamoja na kujenga kiwanda cha mikate lishe, chama hicho pia kinatarajia kuchukua uwakala katika Kiwanda cha Chaki cha Maswa ili kusambaza chaki zinazozalishwa wilayani humo katika shule zote nchini

WAZIRI MHAGAMA ATOA MIEZI MIWILI KUKAMILISHA HATUA YA KWANZA KIWANDA CHA NGOZI CHA KARANGA

Serikali yafanikiwa kupata makampuni mawili zaidi toka nje ya nchi kununua Tumbaku iliyobakia.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.
BAADA ya zao la Tumbaku kulimwa na kupitiliza malengo ambayo yalipelekea baadhi kushindwa kupata mnunuzi  hatimae serikali kwa juhudi zake imefanikiwa  kupata makampuni mawili kutoka nchi jirani ya Zambia kuja kununua zao hilo la Tumbaku iliyobakia kutoka kwa wakulima

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema zao la Tumbaku ni moja ya mazao ya kimkakati ambayo yanalimwa kwa mkataba ambapo makampuni yanajitojeza kununua mapema na kusaini mkataba.

Amesema msimu uliopita uzalishaji wa Tumbaku  ulipitiliza malengo yaliyowekwa ambapo zaidi ya tani elfu tatu zilibaki baada ya makampuni kuchukua ile waliyokuwa wameingia mkataba hivyo serikali ikalazimika kufanya juhudi za kutafuta wanunuzi.

“Katika msimu uliopita lengo la uzalishaji katika mkataba lilikuwa ni tani 57,305.1, wakulima walizalisha kilo 12,452.3 zaidi ya malengo ya mkataba lakini kutokana na mkataba kampuni  inatakiwa kununua asilimia kumi zaidi ya malengo tuliyokubaliana na mpaka kufikia mwishoni mwa msimu makampuni yalikuwa yamenunua  tani 60, 691.9. sawa na asilimia 105 ya makubaliano.

Amesema, serikali ilitafuta wanunuzi wa tumbaku iliyobaki ambapo  kampuni ya Alliance One na Premium Active ziliongeza jumla ya tani 6,305 na kufanya kiasi cha Tumbaku iliyobaki kufikia tani 3,345.1.

Ameeleza kuwa, kuwa juhudi za serikali hazikuishia hapo kwani walifanikiwa kushawishi kampuni za Topper Leaf Company na Tombwe processing kutoka Zambia kuja kununua tumbaku iliyobaki ambapo sasa hivi wako katika hatua za kusaini mkataba kwa ajili ya kununua tumbaku hiyo.

Aidha ameongeza kuwa, serikali imejipanga vema katika msimu ujao ambao masoko yake yataanza Mei mwakani na  kampuni za ununuzi zilizopo Tanzani ambazo ni Alliance One, Premium Active na Japana Tobacco International zimetoa mikataba ya tani  42,225.9 kiasi ambacho ni kidogo kutokana na kujitoa kwa kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC) katika ununuzi wa Tumbaku.

 Hasunga aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo serikali ilifanya juhudi za kutafuta kampuni zaidi na kufanikiwa kushawishi kampuni nyingine nne  kutoka Zambia zitakazowezesha kufikia matarajio ya tani 63278.6 msimu ujao.
“Tumefanikiwa kuongeza kampuni nne kutoka Zambia kupitia kampuni za kizawa na hivyo tunatarajia malengo ya mikataba ya msimu ujao yatatimia,” alisema.
Akiekeza  sababu za kujitoa kwa kampuni ya TLTC alisema ni kupungua kwa mtaji kulikotokana na deni la faini walilotozwa na Tume ya ushindani pamoja na fedha za VAT ambazo hawajarejeshewa kutokana kutofautiana kwa mahesabu na serikali.

Aidha amesema kuwa sasa hivi serikali imesema iko mbioni kununua ndege ya mizigo itakayowezesha kusafirishwa kwa mazao ya mboga mboga mboga na matunda kwenda nje ya nchi ili yaweze kufika yakiwa katika hali nzuri na kuongeza uchumi wa nchi.
 Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 30, 2019 jijini Dar es  Salaam alipokuwa akitoa taarifa juu ya kupatikana kwa makampuni mawili ya kutoka nchini Zambia yaliyojitokeza kununua Tumbaku iliyobaki msimu uliopita baada ya kupitiliza malengo.

DKT. MUHAMMED SEIF KHATIBU, MTUNUKIWA WA KWANZA WA PhD CHUO KIKUU CHA DODOMA

$
0
0
Na  Mwandishi wetu

Alipohojiwa mnamo January mwaka juzi, Dkt. Muhammed Seif  Khatib alikuwa na mengi ya kuzungumzia kuhusu umuhimu wa kuhifadhi historia, ambapo aliweka bayana kwamba wakati umefika wa kujenga makumbusho ya Taifa ya Mapinduzi ya Zanzibar, ili kizazi cha sasa na kijacho kiweze kujifunza na kuipitia historia muhimu kwa Watanzania na wageni kutoka nje.

Dkt. Khatib anasema ni vema kuonesha  katika  picha,  filamu,  maandishi  na  sura  halisi  za  historia  ya  Zanzibar ya wakati huo uliopita wa utawala wa wageni wa Waajemi, Wareno, Waarabu, Waingereza na hadi hivi sasa wakati wa Serikali ya Mapinduzi ya Waafrika inaongozwa na walio wengi. 

“Kwa kuweka makumbusho na usahihi wa historia ya nyuma ya kabla, wakati na baada ya Mapinduzi kadhalika na yanayotokea hivi sasa, hayo yote yakiwa katika makumbusho hio, yatakuwa msingi wa historia ya Zanzibar hatua ambayo itasaidia kuwekwa wazi mambo yaliyowahi kutokea, hivyo sio rahisi kwa mtu yoyote ambaye ana agenda ya kupotosha umma kufanya hivyo”,  alisema Dkt. Khatib ambaye unapokutana naye bado anaonekana ni mwenye nguvu zake na afya tele.

Ila kwa vile wazo lake la kuwa na kituo cha historia halijafanyiwa kazi, bado Dkt. Khatib tu anasikitika kwamba hivi sasa ni kweli kabisa mtu yoyote anaweza akasema vyovyote atakavyo kwa kuwa haijui historia vema na wala hana mahali pa kurejea historia ya Mapinduzi ya Zanzibar.  

“Wengi hawajui kwamba watu walitoka Kongo, Malawi, Kigoma na Tabora wakibebeshwa pembe za Ndovu na kusafiri kwa mguu, wakifuata njia ya reli ya kati, mpaka Bagamoyo na kusafirishwa na  jahazi  mpaka  Unguja  na  kuwekwa  sokoni  kuuzwa  kama  samaki  katika  soko  la watumwa. Huu ndio ukweli ambao sio tu wengi hawaujui, bali pia yapasa waujue” anasema Dkt. Khatib.

Anatoa  mfano  wa Rwanda  iliyokumbwa na  mauaji  ya  kimbari  mwaka  1994,  na kwamba kwa kutambua kuwa hicho siyo kitu kizuri kutokea tena hapa duniani nchi hiyo imeweka makumbusho ya kitaifa ambayo japo yanahuzunisha lakini ndio ukweli wenyewe. 

“Ukweli kwenye makumbusho hayo mjini Kigali utajionea maelfu ya mafuvu ya vichwa vya watu waliouwawa yalivyopangwa kiasi hata huwezi kuamini kama hiyo ndiyo iliyokuwa hali halisi ya mauaji ya kimbari yalivyotokea hapa duniani.

“Kwa Wanyarwanda na watu wengine duniani, makumbusho ya kimbari ni sehemu ya Utalii ikizingatia msemo wa waswahili wanasema kuona ni kuamini”, anasema Dkt. Khatib. 

Anaongeza kwamba siyo Rwanda tu, bali hata nchi ya Namibia kuna jumba la makumbusho la mauaji yaliyofanywa na Wajerumani kwa kabila la Waherero ambao anasema waliuwawa katika vita ya kwanza ya dunia, ambapo takribani Waherero nusu ya milioni waliuwawa na hivi karibuni Waherero wa Namibia walikuwa wanaomba fidia kwa Serikali ya Ujerumani, ingawa Ujerumani wameomba msamaha kwa mauaji hayo ya kimbari.

Dkt. Khatib anasema kwamba Uingereza ni nchi inayoongoza duniani kwa kuweka kumbukumbu zake katika makumbusho za kifalme, Kimataifa, Kitaifa, Vita, Silaha, Bahari, Mtu Binafsi, Jiji au Mji husika, ikiwa ina zaidi ya makumbusho 55 ambayo yanafahamika duniani. Mfano ikiwa ni British Museum London, Natural History Museum London, National Gallery London, Science Museum London, Victoria ana Albert Museum, National Maritime Museum, Museum of London City, National Portrait Gallery, National Army Museum, Sir Johns Soanes Museum, Wallace Collection London, National War Museum na kadhalika.

“Kujengwa kwa kituo cha makumbusho Zanzibar pia kitasaidia kuingiza fedha ikiwa kama sehemu ya Utalii wa historia kama wanavyofanya nchi zingine, ambapo mtu anayehitaji kuijua historia hiyo atapata kila kitu mahala pamoja bila kusumbuka”, anamalizia Dkt. Khatib.

Yote hayo tisa, mimi baada ya kufanya utafiti wa kina nikakuta kumbe hata yeye mwenyewe Dkt. Muhammed Seif Khatib ni mmoja wa watu ambao watafaa kuandikwa historia zao na kuwemo kwenye kituo hicho cha kumbukumbu, maana kwa kweli kapita kwingi na kufanya mengi na kuishi kwingi na kuona mengi.

Na endapo mtu akipata kibarua cha kuandika hiyo historia yake yeye kama yeye, hakika utapata taabu uanzie wapi ama fani ipi kati ya nyingi alizopitia na ambazo anazo hadi hii leo - kama ambavyo mimi nimepata shida kuandika hii sehemu tu ya historia yake hapa.

Baada ya kuongea nae kwa kina, nikawa najiuliza sijui nianze na hili jina la Daktari ambalo alilipata rasmi mnamo Novemba 25, 2011 pale alipotunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa.

“Hii ilikuwa Shahada ya Kwanza ya PhD kutoka katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Ni bahati ilioje mimi kuipata Shahada hii ya juu kitaaluma” anasema Dkt. Khatib huku akiikumbuka vyema siku hiyo katika viwanja vya UDOM, wakati aliposimamishwa na kwenda kupiga goti na mbele ya Mhe. Mkapa na kutunukiwa Shahada hiyo.

Anasema Mada yake ya kuupata udaktari huo wa Falsafa ilikuwa ni ulinganisho wa washairi Shaaban Robert wa Tanga (wa karne ya 20) na Muyaka bin Haji wa Mombasa (wa karne ya 19), akichambua jinsi wanavyomsawiri mwanamke kwa “chanjo za matakwa ya mwanamume”. 

“Nilifarijika kufikia kiwango hicho cha elimu na kutunukiwa na Rais Mkapa ambaye niliyefanya kazi nae kwa muda wa miaka 10, akiamini kuwa mmoja wa mawaziri wake aliowaita “Askari wa Miamvuli”, anasema huku akitabasamu. 

Nikajiuliza labda nianze na historia yake ki-elimu, baada ya kuniambie yeye alisoma hadi darasa la nane lakini alijiendeleza mwenyewe na hatimaye kupata Shahada yake ya Kwanza,  katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1978 na Shahada ya Pili aliipata mwaka 1982 Uingereza SOAS. 

Kwa kweli Dkt. Khatib, ambaye baada ya kuhudumu kupitia Umoja wa Vijana kama mbunge wa viti maalumu baadaye akahudumu kama mbunge wa Uzini kwa miongo kadhaa, ni changamoto kubwa kumwelezea. 

Hasa ikizingatiwa kwamba yeye pia Mwenyekiti wa BARAZA LA KISWAHILI LA ZANZIBAR (BAKIZA), Mwenyekiti wa Mapitio ya Kamusi Fasaha la BAKITA lilochapwa 2010, huku akiwa Mhadhiri wa Muda kwa wanafunzi wa Shahada ya Uzamili (Masters) katika Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA). 

Na kama hayo yote hayatoshi, hivi karibuni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein alimteua kuwa Mjumbe wa TUME ya UTUMISHI WA UMMA katika Ofisi ya Rais, Zanzibar. 

Tukija alikokopita huko nyuma, utakuta Dkt. Khatib amewahi kushika nyadhifa nyingi na kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na  kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (1978-82), Katibu Mkuu Umoja huo (1982 - 88) ambapo hapo kwa vijana amekuwa kiongozi kwa miaka 10. 

Amekuwa Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya Pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi, na awamu ya Tatu ya Mhe. Mkapa na ya nne ya Dkt. Jakaya Kikwete (1988-2010), safari hiyo akianzia toka akiwa mbunge wa viti vya Vijana na baadaye wa Jimbo la Uzini tokea mwaka 1988 hadi alipostaafu mwaka 2015. 

Vile vile amekuwa Mjumbe wa NEC ya CCM tokea 1978 hadi 2017, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho (1995-2017), na baadaye Katibu wake wa  Oganaizesheni 2012-2017. 

Licha ya kuwa mwanasiasa mwenye nyadhifa mbalimbali, Dkt. Khatib katika muda wake wa ziada alikuwa mwandishi wa makala za michezo katika gazeti la Serikali la Daily News, gazeti la chama Uhuru na katika Mzalendo akiwika na makala yake mashuhuri KIPANGA. 

Na hakuishia magazetini pekee. Huyu bwana pia ni Mwandishi mashuhuri wa vitabu vikiwemo “Fungate ya Uhuru”, “Wasakatonge”, “Chanjo”, “Vifaru Weusi”, Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar” na “Taarab Zanzibar”. 

Nilipoongea nae hivi karibuni, Dkt. Khatib amenambia kwamba amehamasika sana na kitendo cha Mhe. Mkapa kutoa kitabu cha historia ya maisha yake, na kuongezea yeye pia tayari yuko mbioni kufuata nyayo za kiongozi huyo mahiri kwa kuandaa kitabu cha maisha yake. 

Hapana shaka kwamba kitabu chake hicho kitatuhadithia sio tu alivyokiuwa na kipawa cha kufanya mambo mengi kwa wakati  mmoja, bali pia jinsi alivyokuwa mwanasoka hodari wa timu ya Kikwajuni almaarufu kama “KISK” na timu ya Taifa ya Zanzibar - bila kusahau alikuwa pia Nahodha wa timu ya soka ya Chuo cha Nkrumah. 

Dkt. Khatibu, ambaye anasema hobby zake kubwa ni kufanya jogging, kusoma vitabu na makala mbaklimbali, pia ameshatunga nyimbo kibao za taarabu zinazoimbwa na wasanii wa bendi mbalimbali ikiwemo Culture.  Baadhi yake ni "Nia yangu sigeuzi", "Paka shume", "Wewe peke yako,""Nakupenda" na nyingine kibao.

Hadi nafikia hapa, bado sijajua nianzie wapi kumwelezea huyu mwanasiasa, mwanamichezo, mwanahabari, mshairi, ambaye kwa sasa  anasimamia kwa karibu kampuni ya familia ya Zanzibar Media Corporation akiwa Mkurugenzi wa Zenj Fm na Zenj Tv. 

Mie nashauri tusubiri tu hicho kitabu cha maisha yake ili tumjue kwa undani, na vile vile mamlaka zinazohusika, zikipendezwa, zianzishe hicho kituo cha kumbukumbu na historia ya Zanzibar kama anavyoshauiri - na kujumuisha kitabu chake kuwa miongoni mwa vitu vitavyowekwa humo.  Ama hakika, kwa maoni yangu, anastahili kuwemo kama ambavyo Wazanzibari wengi wa aina yake wanavyostahili.

 Dkt Muhammed Seif  Khatib aliposimamishwa ili kwenda kupiga goti Novemba 25, 2011 pale alipotunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa. Hii ilikuwa Shahada ya Kwanza ya PhD ya Chuo Kikuu cha Dodoma toka kianzishwe. 
 Dkt Muhammed Seif  Khatib  alipotunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa, Novemba 25, 2011. Hii ilikuwa Shahada ya Kwanza ya PhD ya Chuo Kikuu cha Dodoma toka kianzishwe.
 Dkt Muhammed Seif  Khatib katika tafrija ya kifamilia baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa, Novemba 25, 2011. Hii ilikuwa Shahada ya Kwanza ya PhD ya Chuo Kikuu cha Dodoma toka kianzishwe.
 Dkt Muhammed Seif  Khatib (namba 2) akiwa  na kikosi cha "Kiski" miaka ya 1970 
Akiwa Nahodha wa timu ya Chuo cha Nkrumah Dkt. Khatib akipokea kikombe cha ubingwa toka kwa Raisw wa kwanza wa Zanzaibar Sheikh Abeid Amnani Karume

 Dkt. Khatib akimkabidhi Mwalimu Nyerere Tunzo ya Kimataifa akiwa Katibu Mkuu wa Vijana mbele ya Rais Ali Hassan Mwinyi. Anasema hakumbuki mwaka ila kabla ya 1988

Dkt Muhammed Seif  Khatib wa pili kushoto waliosimama mbele. Hili lilikuwa baraza la mawaziri la kipindi cha pili cha Rais wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa. 
Dkt Muhammed Seif  Khatib akiwa katika majukumu yake kama Mkurugenzi wa Zanzibar Media Corporation Ltd., siku kilipoingia makubaliano ya kurusha vipindi vya CCTV ya China



Dkt Muhammed Seif  Khatib akiwa katika majukumu yake kama Mkurugenzi wa Zanzibar Media Corporation Ltd., akiwa na wageni waliotembelea Zenj FM/Zenj TV kutoka Amana Bank baadfa ya kufungua Tawi lao Zanzibar. Kutoka kulia ni Nassor Ameir, Dr.Muhammed Seif Khatib,Farsy Mussa na Jamal .I.Jamal

Ni Mwaka 2005  wakati Marehemu Ali Juma Shamuhuna alipokuwa mgeni wa Heshima katika ufunguzi wa Zenj FM.  Watatu kushoto ni Meneja wa  Zenj FM, Dkt. Khatib (kushoto), mwakilishi wa Mikunguni Mhe. SulShihata na Bwana Subash Patel.

Mwaka 1973 wakati Rais wa Zanzaibar wakati huo Mhe. Aboud Jumbe alipokutana na wajumbe wa Kamati ya kukusanya, kunakili na kuandika kitabu cha hotuba za Rais wa Kwanza wa Zanzibar Sheim Abeid Amani Karume. Dkt. Khatib ni wa tatu kutoka kushoto.
Dkt Khatib akiwa ofisini kwake na Omar Mkambara mtangazaji mahiri wa Soka kutoa BBC aliyekuwa katika maandalizi ya kutangaza mashindano ya AFCON  ' live' kutoka Misri na kupiga kambi Zenj FM  kuwashirikisha Wazanzibari.

Picha ya pamoja ya viongozi wa BAKITA na BAKIZA baada ya kikao cha mashauriano. Kutoka kulia waliosimama mbele ni Bi Mwanahija (Katibu Mtendaji - BAKIZA), Dkt.Muhammed Seif Khatib (Mwenyekiti - BAKIZA), Dkt.Sewangi (Katibu Mtendaji- BAKITA) na Dkt.Samwel ( Mwenyekiti - BAKITA) na wajumbe wengine.

KONGAMANO LA TATU LA KIMATAIFA LA KISWAHILI KUFANYIKA ZANZIBAR DISEMBA 19 - 20, 2019

SERIKALI YATAKIWA KUISHIRIKISHA SEKTA YA ARDHI KATIKA MIPANGOMIJI NCHINI

$
0
0
N/Waziri wa Viwanda na Biashara Eng. Stellah Manyanya (wa pili Kushoto) akitoa maelekezo kwa Msajili wa Bodi ya Usajili Wataalamu wa Miapango Miji nchini Hellen Mtutwa (Kulia) wakati alipotembelea mabanda ya maonesho katika Mkutano wa Wataalamu wa Mipango mwishoni mwa wiki.
N/Waziri wa Viwanda na Biashara Eng. Stellah Manyanya (katikati) Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji Profesa Wilbert Kombe (Kushoto) na Msajili wa Bodi ya Wataalamu wa Mipango Miji Hellen Mtutwa ( kulia) wakiwasili katika Mkutano wa Wataalamu wa Mipango Miji Nchini uliofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
N/Waziri wa Viwanda na Biashara Eng. Stellah Manyanya (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wataalamu wa Mipango Miji na baadhi ya wajumbe kwenye Mkutano wa Wataalamu wa Mipango Miji Nchini uliofanyika
Mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)


Na Munir Shemweta, WANMM DODODMA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya ametaka kushirikishwa kwa sekta ya ardhi hasa idara ya Mipango Miji katika miradi mbalimbali inayoibuniwa na serikali ili kuondokana na miradi isiyokuwa na tija kwa jamii.

Mhandisi Stellah Manyanya aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano mkuu wa sita wa Mwaka wa Wataalaamu wa Mipangomiji uliofanyika jijini Dodoma.

Alisema, kumekuwepo na miradi mingi nchini inayoanzishwa na Serikali na kutumia gharama kubwa lakini matokeo yake imekuwa haitumiki ipasavyo na wakati mwingine inaingiliana na shughuli nyingine za kijamii hali inayosababisha kuzuka kwa migogoro kwenye jamii.

Alitolea mfano Jengo la Machinga Complex lililopo Ilala Jijini Dar es Salaam, Mhandisi Manyanya alisema, kutokuwepo kwa mipango kina ya muda mrefu na utafiti duni ndio chanzo kikubwa hadi leo jengo hilo limeshindwa kufikia lengo walilojiwekea la kuwasaidia wafanyabiashara wadogowadogo katika shughuli zao.

“ Kuna wale wenzetu waliojenga lile Jengo kubwa kabisa wakalipa jina la heshema Machinga Complex lakini kwa namna walivyopanga na kutumia fedha kwenye kujenga limebaki kuwa jengo la aibu” Alisema Mhandisi Stellah Manyanya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Profesa Wilbert Kombe alisema, Miradi Mingi nchini inafanyika bila kushirikisha wataalamu wa Mipangomiji kwani Taasisi nyingi za Serikali zinapopanga mipango yake ya kiuchumi na miundombinu hazizingatii na kuonesha mipango ya ardhi hali inayosababisha muingiliano wa shughuli za kiuchumi.

Aliongeza kwa kusema kuwa, Taasisi zote nchini zinategemea uwepo wa ardhi, hivyo hazina budi kushirikiana na Sekta zote zinazohusu ardhi kabla ya kupanga mipango yao ya kiuchumi ili kuepusha muingiliano na kupangwa vibaya kwa miji.

‘’Ukitazama eneo la Maegesho ya magari ya Mwendokasi eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam , hayo ni matokeo ya kutoshirikishana katika mipango miji kwani lilile eneo linahitaji mambo mawili ama lihamishwe au iinuliwe barabara kuanzia Magomeni “ Alisema Profesa Kombe.

Naye Msajili wa Bodi ya Wataalamu wa Mipango Miji Hellen Mtutwa alisema, taasisi zote za Serikali ni lazima ziwe na ushirikiano wa karibu wakati wa kuandaa mipango na kuitekeleza siyo sekta za ardhi tu bali Tanesco ,Tanroad Maji na taasisi nyingine ili kuepusha hasara kwa Serikali .

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa City Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed alisema, maendeleo yote yapo kwenye sekta ya ardhi hivyo Serikali inatakiwa iipe kipaumbele sekta hiyo kwani hasara ya kutokufanya mipango ni kubwa kuliko kuitekeleza.

Mamluki katika Mashindano ya Michezo ya Wafanyakazi kuchukuliwa Hatua

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza leo Novemba 30,2019 Jijini Mwanza na Wanamichezo ambao ni wafanyakazi (hawapo pichani) wakati alipofungua mashindano ya Michezo kwa Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma na Binafsi yanayofanyika Jijini humo kuanzia tarehe 27 Novemba hadi 01 Desemba 2019,yanayongozwa na Kauli mbiu “SHIMMUTA 2019 Familia Moja”lengo ikiwa ni kuimarisha afya na kubadilishana uzoefu kazini. Kulia ni Mwenyekiti wa SHIMMUTA Bw. Khamis Mkanachi na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Mhe.Dkt.Fillis Nyimbi.
Mwenyekiti wa SHIMMUTA Taifa Bw.Khamis Mkanachi akiongea kuhusu SHIMMUTA leo Novemba 30,2019 Jijini Mwanza na Wanamichezo ambao ni wafanyakazi (hawapo pichani) wakati Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) alipofungua mashindano ya Michezo kwa Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma na Binafsi yanayofanyika Jijini humo kuanzia tarehe 27 Novemba hadi 01 Desemba 2019,yanayongozwa na Kauli mbiu “SHIMMUTA 2019 Familia Moja”lengo ikiwa ni kuimarisha afya na kubadilishana uzoefu kazini.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa SHIMMUTA Bibi Roselyn Massam.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akipiga mpira wa penati leo Novemba 30,2019 Jijini Mwanza kuashiria ufunguzi wa Mashindano ya Wanamichezo ambao ni wafanyakazi alipofungua mashindano ya Michezo kwa Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma na Binafsi (SHIMMUTA) yanayofanyika Jijini humo kuanzia tarehe 27 Novemba hadi 01 Desemba 2019,yanayongozwa na Kauli mbiu “SHIMMUTA 2019 Familia Moja”lengo ikiwa ni kuimarisha afya na kubadilishana uzoefu kazini.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bibi Phillis Nyimbi akitoa salamu za Wilaya na Mkoa leo Novemba 30,2019 Jijini Mwanza wakati Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) alipofungua Mashindano ya Wanamichezo ambao ni wafanyakazi wa Mashirika ya Umma na Binafsi (hawapo pichani yanayofanyika Jijini humo kuanzia tarehe 27 Novemba hadi 01 Desemba 2019,yanayongozwa na Kauli mbiu “SHIMMUTA 2019 Familia Moja”lengo ikiwa ni kuimarisha afya na kubadilishana uzoefu kazini.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa SHIMMUTA Bibi Roselyn Massam.
Bibi Elinaike Naburi ambaye ni Afisa Utumishi kutoka TPDC akiwaapisha wanamichezo wenzake leo Novemba 30,2019 Jijini Mwanza wakati Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipofungua mashindano ya Michezo kwa Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma na Binafsi (SHIMMUTA) yanayofanyika Jijini humo kuanzia tarehe 27 Novemba hadi 01 Desemba 2019,yanayongozwa na Kauli mbiu “SHIMMUTA 2019 Familia Moja”lengo ikiwa ni kuimarisha afya na kubadilishana uzoefu kazini.
Bw.Felix Eliudi ambaye ni Muamuzi akila kiapo kwa niaba ya waamuzi wote watakaochezesha mashindano ya Michezo kwa Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma na Binafsi (SHIMMUTA) yanayofanyika Jijini humo kuanzia tarehe 27 Novemba hadi 01 Desemba 2019,yanayongozwa na Kauli mbiu “SHIMMUTA 2019 Familia Moja”lengo ikiwa ni kuimarisha afya na kubadilishana uzoefu kazini ambayo yamefunguliwa na wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Chuo cha Usimamizi wa Biashara CBE kampasi ya Mwanza leo Novema 30,2019 mara baada ya kufungua mashindano ya Michezo kwa Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma na (SHIMMUTA) yanayofanyika Jijini humo kuanzia tarehe 27 Novemba hadi 01 Desemba 2019,yanayongozwa na Kauli mbiu “SHIMMUTA 2019 Familia Moja”lengo ikiwa ni kuimarisha afya na kubadilishana uzoefu kazini.

………………

Na Shamimu Nyaki –WHUSM ,Mwanza

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ametangaza kuwachukulia hatua Wanamichezo wasiokuwa Wafanyakazi maarufu kwa jina la “Mamluki” wanaoshiriki Mashindano ya Michezo kwa Wafanyakazi inayojulikana kama SHIMUTA na SHIMIWI endapo watabainika.

Dkt.Mwakyembe amesema hayo leo Jijini Mwanza wakati akifungua michezo ya Mashirika ya Umma na Binafsi maarufu kwa jina la SHIMMUTA kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluh Hassan ambaye pia ndiye mlezi wa mashindano hayo ambapo amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuimarisha afya za wafanyakazi,kubadilishana uzoefu pamoja na kutangaza Taasisi zao.

“Kuna hili suala la Wachezaji ambao sio wafanyakazi maarufu kwa jina la MAMLUKI kushiriki karika michezo hii,tena nakumbuka kuna kiongozi aliwahi kuwaita “viongeza nguvu bambikizi”,Hapa sio mahala pao nawataka wajiondoe mapema maana tukiwabaini wao pamoja na Taasisi zao tutawachukila hatua”alisema Waziri Mwakyembe

Mhe.Waziri Mwakyembe ameongeza kuwa wakati mwaka jana mashindano hayo yalipofanyika Jijini Dodoma Mhe.Makamu wa Rais Mama Samia hakuridhishwa na idadi ya washiriki kutokana na Idadi ya Makampuni na Mashirika yaliyopo nchini,hivyo kuagiza mkutano ufanyike kujua sababu na kuzipatia majibu ambapo maazimio yameleta matunda kwani mashindano ya mwaka huu idadi imeongezeka kutoka 26 hadi 46.

Hata hivyo Mhe.Waziri amewataka waamuzi wa mashindano hayo kuchezesha michezo hiyo kwa haki na kufuata sheria zote za michezo na atakayesababisha vurugu au masononeko atawajibishwa kupitia kiapo alichoapa leo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa SHIMMUTA Bw.Khamis Mkanachi amesema kuwa Menejimenti za Taasisi za Umma pamoja na Makampuni binafsi zinatakiwa kuelewa kwamba wafanyakazi wao wanatakiwa kufanya michezo mbalimbali ili kuimarisha afya zao kwa ajili ya kuongeza ufanisi wanapokuwa kazini,hivyo ni wajibu wa kila Taasisi na mashirika kuona haja ya kutenga siku ya kufanya michezo.

“Michezo hii inafanyika kwa mwaka mara moja ni vyema viongozi wa Taasisi na Mashirika binafsi kuona umuhimu huo na kuwapa wafanyakazi wao muda wa kushiriki michezo hiyo inayoleta ari katika kufanya kazi” aliongeza Bw.Mkanachi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt.Fillis Nyimbi amesema Jiji la Mwanza hususan Wilaya ya nyamagana imeshukuru ujio wa mashindano hayo kwakua itaongeza kipato kwa wenyeji kutokana ongezeko la watu waliokuja kwa ajili ya mashindano hayo ambapo pia amewahakikishia amani na usalama.

Vilevile mwanamichezo Eliud Felix kutoka timu ya Jiji la Mwanza amesema michezo hiyo imewasaidia kujuana pamoja na kubadilishana uzoefu wa majukumu ya kila mmoja katika taasisi yake na kupendekeza iendelee kufanyika kila mwaka.

Mashindano hayo yalianza rasmi tarehe 27/11/2019 na yanatarajiwa kumalizika Desemba mosi 2019 ambapo jumla ya Mashirika na Taasisi 46 zimeshiriki ikiwemo wenyeji Ofisi ya Mkoa wa Mwanza,Chuo Kikuu Dodoma,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na nyingine.

JAJI MWAIMU ATEMBELEA OFISI ZA THBUB ZANZIBAR

$
0
0
Mwenyekiti wa (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akiongea na wafanyakazi wa tume pamoja na wageni wengine waliohudhuria hafla fupi.
Afisa Mfawidhi wa tume Zanzibar, Hussein Mbarouk akimuonesha kitu Mwenyekiti (wa kwanza kushoto) wakati wa ukaguzi wa jengo hilo.
Jaji Mwaimu (kushoto) akiongea na Kamishna Mkaazi wa tume visiwani Zanzibar, Khatib Mwinyichande wakati wakikagua ofisi hizo za tume.






Mwenyekiti wa (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (aliyeinama) akiwaongoza viongozi wengine wa tume kuwatunza waburudishaji wa kikundi cha ngoma ya kibati kutoka Zanzibar katika hiyo hafla fupi.


……………

Na Mbaraka Kambona,

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu ametembelea ofisi za taasisi hiyo zilizopo visiwani Zanzibar, ikiwa mara yake ya kwanza tangu alipokabidhiwa dhamana hiyo Novemba 4, 2019.

Jaji Mwaimu alifanya ziara hiyo mapema leo (Novemba 30, 2019) kwa lengo la kutambuana na wafanyakazi wa tume waliopo katika ofisi hizo zilizopo Mbweni, visiwani Zanzibar.

Katika ziara hiyo, Jaji Mwaimu akiongozana na Makamishna na viongozi wengine wa tume alifanya ukaguzi wa ofisi hizo ambazo hivi karibuni zilifanyiwa ukarabati mkubwa kwa lengo la kuziboresha. 

Akiongea baada ya kumaliza ukaguzi wa jengo hilo, Jaji Mwaimu alieleza kuridhishwa kwake na ukarabati huo uliofanyika na kusema kuwa watajipanga vizuri katika majukumu yao ili kuhakikisha wanazitumia vizuri ofisi zote mbili za Tanzania bara na hizo za visiwani ili kutatua kero za wananchi.

Katika ziara hiyo Jaji Mwaimu aliambatana na viongozi wafuatao; Makamu Mwenyekiti, Mohamed Khamis Hamad, Mheshimiwa, Dkt. Fatma Rashid Khalfan, Mheshimiwa Thomas Masanja, Mheshimiwa Amina Talib Ali, Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande na Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli.

WENYEVITI WAPYA WA VIJIJI NA VITONGOJI JIMBO LA KISESA MKOA WA SIMIYU WAAPISHWA

$
0
0
Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na wajumbe wao kutoka Jimbo la Kisesa wilayani Meatu Mkoa wa Simiyu wakila kiapo cha utii kwenye hafla iliyofanyika Mwandoya Makao Makuu ya Jimbo la Kisesa.
Wenyeviti wote wa Vijiji vya Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kuapishwa.
Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Ikigijo Kata ya Mwabusalu Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Itinje Kata ya Itinje Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Lingeka Kata ya Lingeka Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Matale Kata ya Tindabuligi Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Mbugayabahnya Kata ya Mbugayabahnya Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Mwashata Kata ya Mwabuma Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Ntobo Kata ya Kisesa Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Nyanza Kata ya Mwakisandu Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Semu Kata ya Isengwa Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo
Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Ming’ongwa Kata ya Sakasaka Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu baada ya kula kiapo

TAASISI YA WBM YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAFUNZI YA SHULE YA MSINGU\I KIJITONYAMA

$
0
0


Mkurugenzi na mwanzilishi wa Taasisi ya Wezesha Binti na Mama aMjasiriamali (WBM) Latifa Mohamed akizungumza na wanafunzi wakati wa utoaji wa vyeti na zawadi kwa wanafunzi 48 waliopata mafunzo ya ujasiriamali kutoka katika taasisi hiyo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo ameipongeza Taasisi ya Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali (WBM) kwa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wananfunzi wa shule za Msingi na Sekondari.

WBM imetoa elimu kwa wanafunzi 48 wa Shule ya Msingi Kijitonyama waliopatiwa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali na kupata vyeti baada ya kuhitimu mafunzo hayo. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, amesema taasisi ya WBM imeunga mkono jitihada za serikali katika kutoa elimu ya mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi na wamekuwa wa kwanza kuliona hilo hata baada ya serikali kurudisha mtaala utakaokuwa unafundisha fani mbalimbali. 

Amesema, unapompa mwanafunzi elimu ya ujasiriamali utamsaidia pindi atakapomaliza elimu yake iwe ya msingi au sekondari ataweza kiujiajiri na kuacha mawazo ya kuajiriwa kwani katika mwaka mmoja wanafunzi wengi sana wamekuwa wanahitimu elimu zao na wote wanasubiri kuajiriwa. 

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kijitonyama Beatus Amri ameishukuru taasisi ya WBM kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu kwa wanafunzi jambo ambalo litakuwa na mchango mkubwa sana katika maisha yao ya baadae.

"Jambo hili ni kubwa sana nawashukuru WBM, wameona umuhimu wa kutoa elimu ya ujasiriamali wa wanafunzi hawa kwani hata sisi upo mtaala unaofundisha masuala mbalimbali ila kuja kwa wao ni chachu nyingine,"

Naye kwa upande wa Mkurugenzi na mwanzilishi wa Taasisi ya WBM Latifa Mohamed amesema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ilikua ni katika kumjenga mtoto wake na mama wa baadae kuacha fikra za kuajira na kutakiwa kujiajiri mwenyewe. 

Amesema, wamekuwa wanatoa mafunzo kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari, ambapo lengo likiwa ni kwa wanafunzi wa darasa la tano na sita na wale wa sekondari ambapo watapata mafunzi ya ujasiriamali na kupatuwa vyeti. 

Latifa ameeleza kuwa, kwa mwaka 2020 lego lao ni kuwaa na watoto 5000 kutoka katika shule za Msingi na Sekondari ambapo kila upande watachukua shule 50 kote nchini na sio Dar es salaam tu. 



Taasisi ya WBM wamelenga hususani kwa watoto wa kike ila waliona ni bora kutoa elimu hiyo kwa jinsia zote ambapo itawasaidia kujiajiri na kuacha fikra za kuajiriwa.
Mkurugenzi na mwanzilishi wa Taasisi ya Wezesha Binti na Mama aMjasiriamali (WBM) Latifa Mohamed akiwapatia watoto vinywaji kabla ya kuanza zoezi la utoaji wa vyeti na zawadi.
MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo akitoa zawadi kwa Mlezi wa Club ya WBM Mwalimu Margareth Mnyuko kama jitihada zake katika kuunga mkono mafunzo ayo waliyoyapata wanafunzi 48 wa shule ya Msingi Kijitonyama kutoka 
MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo akikabidhi zawadi na vyeti kwa wanafunzi waliomaliza mafunzo yao ya ujasiriamali kutoka Taasisi ya Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali (WBM) ikiwa na lengo la kuondoa fikra ya kiajirwa.
MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo akikabidhi zawadi na vyeti kwa wanafunzi waliomaliza mafunzo yao ya ujasiriamali kutoka Taasisi ya Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali (WBM) ikiwa na lengo la kuondoa fikra ya kiajirwa.
MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo akikabidhi zawadi na vyeti kwa wanafunzi waliomaliza mafunzo yao ya ujasiriamali kutoka Taasisi ya Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali (WBM) ikiwa na lengo la kuondoa fikra ya kiajirwa.
MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kijitonyama baada ya kuwakaidhi vyeti na tuzo ya kumaliza mafunzo ya ujasiriamali kutoka Taasisi ya Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali (WBM) ikiwa na lengo la kuondoa fikra ya kiajirwa.
MRATIBU wa Kituo cha Walimu Mzimuni Karib Chimwejo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kijitonyama sambamba Taasisi ya Wezesha Binti na Mama Mjasiriamali (WBM).

NAIBU WAZIRI KUFUNGA MASHINDANO YA GOFU YA TANZANIA ARUSHA

$
0
0
Naibu Waziri wa mambo ya Nje Damas Ndumbaro (KATIKATI) akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Gofu tanznaia TGU kabla ya kuingia Uwanjani katikaa mashindano hayo yaliyochukua Siku Tatu .
Baadhi ya Wachezaji kutoka Vilabu Mbalimbali wakiwa tayari kwa ajili ya kuingia katika Mchuano wa mashindo ya Wazi ya Tanzania open katika Uewanja wa Kili jijini Arusha.



……………….

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mh Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika ufungaji wa mashindano ya wazi ya Gofu ya Tanzania open yanayofanyika katika Uwanja wa Kili Jijini Arusha.

Akizungumza katika Siku ya Pili ya Mchezo huo Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU) Criss Martin alisema Maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni hitimisho kesho Jumapili licha ya mvua iliyonyesha Nyakati za mchana.

“ Mvua ilinyesha lakini bahati nzuri haijaathiri kiasi cha kuvunja mchezo licha ya kuchelewesha wachezaji ambao iliwalazimu kujificja kwa ajili ya Mvua na muda kwenda lakini hali ikawa sawa “ Alisema Mwenyekiti wa TGU.

Aidha alisema anawashukuru wadau wote waliofanikisha mashindano haya makubwa wakiwemo Verge Africa ambao wamehakikisha maandalizi yote yamekamilika ikiwemo upatikanaji wa Wadhamini ambao ndi mafanikio ya mashindano.

Kwa upande wake Mchezaji Victor Joseph ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya tanznai kwa kuongoza katika wachezaji wa Divisheni A baada ya kupiga 71 nna kuendelea kuongoza na kubakiza matumaini ya Watanzania.

Victor alisema licha ya Mvua lakini bado anaendelea kupambana kuhakikisha kikombe kinabaki Tanznaia kutokana na uwepo wa wachezaji kutoka nchi Nyingine amabao wameshiriki katika Mashindano haya.

Kwa Upande wa Wachezaji wa Kulipwa kutoka Kenya Dismass Indiza ameendelea kuongoza huku kwa Wachezaji wa Ridhaa Victor joseph wa klabu ya Golf ya Dar es Salaam Gymkhana wameendelea kufanya vyema.

Kwa upande wake Dismass Indiza alisema mchezo umekuwa mgumu siku ya pili baada ya siku ya kwanza kutokana na mvua na hata ushindani haukuwa wa nguvu kufuatia hali ya hewa lakini matumaini yake yake katika hatua ya mwisho ya fainali Leo jumapili.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images