Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

WAZIRI HASUNGA AWATAKA MAWAZIRI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUDUMISHA MSHIKAMANO

$
0
0
Sehemmu ya mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika mkutano wa 39 wa Baraza la mawaziri la jumuiya ya Afrika Mashariki ulioketi Jijini Arusha tangu tarehe 21-28 Novemba 2019.
Sehemmu ya mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika mkutano wa 39 wa Baraza la mawaziri la jumuiya ya Afrika Mashariki ulioketi Jijini Arusha tangu tarehe 21-28 Novemba 2019.
Sehemmu ya mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika mkutano wa 39 wa Baraza la mawaziri la jumuiya ya Afrika Mashariki ulioketi Jijini Arusha tangu tarehe 21-28 Novemba 2019.

Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe. Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa mawaziri wenzake wa sekta ya zote ikiwemo sekta ya Kilimo kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki wanapaswa kuendeleza na kuongeza umoja na mshikamano ili kuakisi matakwa ya jumuiya katika Uzalishaji wa mazao bora ya Kilimo.

Waziri Hasunga ameyasema hayo tarehe 28 Novemba 2019 wakati akichangia mada kwenye mkutano wa 39 wa Baraza la mawaziri la jumuiya ya Afrika Mashariki ulioketi Jijini Arusha tangu tarehe 21-28 Novemba 2019 wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.

Mhe Hasunga alisema kuwa kadri ushirikiano mwema utakavyoendelezwa ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii itaimarisha tija na mafanikio ya soko la mazao katika jumuiya hiyo na dunia kwa ujumla.

Aidha, amewataka watendaji wote katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza taarifa mbalimbali zinazoandikwa kwa ustadi mkubwa kwani kwa kiasi kikubwa kumekuwa na utekelezaji duni wa mipango hiyo.

Mkutano huo umefanyika katika ngazi mbalimbali ambapo Mkutano wa wataalamu ulifanyika tarehe 21-23 Novemba 2019, Mkutano wa makatibu wakuu ulifanyika tarehe 25-26 Novemba 2019, mkutano wa Mawaziri tarehe 27 -28 Novemba 2019, Kadhalika kutakuwa na Maonesho ya biashara kuanzia tarehe 28-30 Novemba 2019. Aidha mkutano wa wakuu wa nchi uliotarajiwa kufanyika tarehe 30 Novemba 2019 umeahirishwa mpaka mwezi Februari 2020.


Katika mkutano huo kwa upande wa sekta ya kilimo maswala kadhaa ya sekta ya kilimo yamejadiliwa na kufikia maazimio Katika kikao cha wataalamu na makatibu wa wakuu walioazimia kuwa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kupitisha mfumo wa pamoja wa kufanya tathmini ya sekta ya kilimo kwa jumuiya ya afrika mashariki (Joint Sector Review Mechanism)


Waliazimia pia kupitisha mfumo wa pamoja wa kufanya uchunguzi wa magonjwa kwa mazao ya mahindi, mpunga na maharage (Pest Risk Analysis).


Pia wameazimia pia kuanzisha mahala pa kuzalisha Viuatilifu, na kuwepo kwa miongozo ya kuhifadhi taarifa za siri za usajili wa Viuatilifu kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki 


Kadhalika, katika mkutano huo wataalamu walipemdekeza makatibu wakuu kuwashauri waheshimiwa Mawaziri kuagiza sekretarieti kuwezesha upatikanaji wa rasimu, mapitio na usainishaji wa makubaliano baina ya nchi mbili au zaidi juu ya udhibiti wa pamoja wa magonjwa ya wanyama yanayoweza kuvuka mipaka na kuharakisha utekelezaji wa makubaliano hayo.


Mhe Hasunga ameeleza kuwa katika mkutano huo pia wamejadili kuhusu kujiunga kwa nchi ya Congo kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki.

Viongozi Wapya wa Serikali za Mitaa Wafundwa Baada ya Kuapishwa

$
0
0
Baadhi ya Wenyeviji wa vijiji, vitongoji, viti maalu na wajumbe mchanganyiko wakila kiapo wakati wa hafla fupi ya uapisho wa viongozi hao iliyohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (hayupo Pichani) tarehe 29.11.2019.
Baadhi ya Wenyeviji wa vijiji, vitongoji, viti maalu na wajumbe mchanganyiko wakila kiapo wakati wa hafla fupi ya uapisho wa viongozi hao iliyohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (hayupo Pichani) tarehe 29.11.2019.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiongea na viongozi wapya wa vijiji na vitongoji muda mfupi baada ya viongozi hao kula kiapo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akimsalimia baadhi ya wenyeviti wa kijiji muda mfupi kabla ya kuondoka eneo hilo baada ya viongozi hao kula kiapo tayari kwa kuwatumikia wananchi katika maeneo yao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akimkabidhi zawadi motto wa mmoja wa wenyeviti wa vitongoji muda mfupi kabla ya kuondoka eneo hilo baada ya viongozi hao kula kiapo tayari kwa kuwatumikia wananchi katika maeneo yao.

……………….

Viongozi wapya 2,766 wa vijiji na vitongoji walioshinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika tarehe 24.11.2019 katika wilaya ya Kalambo wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanatatua kero na malalamiko ya wananchi wanaowahudumia katika vijiji na vitongoji ili kupunguza msongamano wa wananchi wanaohitaji kutatuliwa kero zao katika ngazi ya wilaya na mkoa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo muda mfupi baada ya viongozi hao kula kiapo mbele yake na mbele hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Kalambo ambapo wenyeviti wa vijiji na vitongoji kutoka katika kata 10 za tarafa ya Matai wilayani humo walishiriki katika kiapo hicho.

“Katika ngazi hiyo ya vijiji, vitongoji na mitaa, wenyeviti wa maeneo hayo mimi nikipata mtu anatoka kwenye vijiji vyenu analalamika kwa jambo ambalo ni dogo sana, nitakuita. Utapata usumbufu wa kuja Sumbawanga, uhisabu kuwa utatumia gharama zako kuja na kurudi kutoka kule kweny kijiji chako. Nitakusumbua kwasababu wewe hutaki kusumbuka nikilipata tu nitakusumbua, kwahiyo nendeni mkatatue kero za wananchi katika ngazi zenu, yako mambo mengi mtusaidie sio kila kitu mkuu wa mkoa, kila kitu mkuu wa Wilaya na wengine wanakwenda wanaandika mpaka kwa Rais,”Alisisitiza.

Aidha amewataka viongozi hao kuwaumikia wananchi wote bila ya kujali vyama vyao vya kisiasa, dini wala kabila na kuwataka katika utekelezaji huo kuwa shirikishi kwani wasipofanya hivyo wananchi watashindwa kushiriki katika shughuli za kimaendeleo jambo litakalorudisha nyuma juhudi za mkoa kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma stahiki na kwa wakati.

“Mambo ambayo mnapaswa kwenda kuyasimamia katika maeneo yenu kuwashirikisha wananchi katika kupanga maendeleo, sio unakurupuka tu unasema mimi nataka hiki kifanyike bila ya kuwashirikisha wananchi , lazima wapange waamue wao wenyewe na wakishaamua wao wenyewe watashiriki katika kutekeleza lakini pia watasimamia kulinda yale maamuzi yao na hiyo ndio demokrasia na hili ndilo mkalifanye kule, viongozi wengine wakishachaguliwa kama hivi wanakuwa miungu watu, hatupendi kuona miungu watu kwenye vijiji vitongoji na mitaa,” Alisema.

Na katika kuhakikisha viongozi hao wanatekeleza majukumu yao bila ya visingizio amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri nne za mkoa huo kuwapatia mafunzo viongozi hao wapya pamoja na wale ambao ni muhula wao wa pili au zaidi jambao litakalotawasaidia kutekeleza majukumu yao kwa Mujibu wa Sera za Kisekta, Mikakati ya Kisekta, Sheria, Kanuni, Miongozo na Taratibu zinazosimamia Sekta husika.



Wakati akitoa muhtasari wa taarifa ya uchaguzi wa serikali za mitaa mratibu wa uchaguzi mkoa Albinus Mgonya alisema kuwa mitaa 165 iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga imechukuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo ni sawa na asilimia 100 wakati katika ngazi ya vijiji CCM imechukua vijiji 336 huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikichukua vijiji 2 kati ya vijiji 339 vya mkoa wa Rukwa.



“Vitongoji vilivyoshiriki katika uchaguzi ni 1,816 na kwa nafasi ya vitongoji Chama cha Mapinduzi kimepata nafasi 1,807 sawa na asilimia 99.4 Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimepata nafasi za wenyeviti wa vitongoji 8 sawa na asilimia 0.6. kwa faida ya wadau waliopo hapa nafasi hizi 8 mgawanyo wake ni kama ifuatavyo, Sumbawanga Manispaa nafasi 1, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga nafasi 1 na Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi nafasi 6,” Alimalizia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mh. Daudi Sichone wakati akitoa neon la shukurani aliwataka viongozi hao wapya kuhakikisha wanawapatia elimu ya kutosha wananchi wanaowaongoza juu ya kutatua kero na malalamiko katika ngazi hizo zao na sio kumshawishi mwananchi afike ngazi mkoa.

“Hawa viongozi wetu wanantumia mkoa na taifa, hebu ifike mahali tutoe elimu kwa wananchi wetu, kabla hajafika huko angalau akifika kule ionekane sisi sote tunasapoti kwamba kwa tatizo lako hili ni vyema ukafika kwa mkuu wa mkoa lakini sio tu unaamka tu na masimu yako unamyuhangaisha mzee wa watu anashindwa kufanya kazi za watu,”Alisema.

Maeneo yaliyofanya uchaguzi katika mkoa wa Rukwa ni vijiji 67, vitongoji 348, mitaa 9 na wananchi walioshiriki kupiga kura ni 118,887 huku zoezi hilo la uchaguzi likiwa limefanyika katika hali ya amani na utulivu.

Waziri mkuu aongoza mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) jijini Dar

$
0
0


 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanikiwa kukusanya mikopo iliyoiva yenye thamani ya shilingi bilioni 183.3 sawa na asilimia 116.2 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 157.7. 



“Natambua kwamba baadhi ya wahitimu wamepata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, hivyo natumia  fursa hii kuwakumbusha wale wote mlionufaika na mkopo wa Serikali katika kutimiza ndoto zenu za kupata elimu ya juu, mkumbuke kurejesha mikopo,” amesema.



Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Novemba 29, 2019) wakati akizungumza kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. 



Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila anayenufaika na mkopo asaidie wengine walio nyuma yake ili nao waweze kufaidika na utaratibu huo wa kukopa na kulipa. Alisisitiza  kwamba bila kufanya hivyo, ni ukweli usiopingika kuwa Serikali itashindwa kuwajengea uwezo wananchi wake wa kupata fursa zinazojitokeza za elimu katika ngazi mbalimbali. 



“Ikumbukwe kuwa, maendeleo ya Taifa lolote yanategemea uwekezaji katika rasilimali watu. Hivyo nitoe rai kuwa wote mliokopeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu mfanye hima kulipa,”  alisema Majaliwa 



Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wahadhiri na wanachuo wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu vilivyopo Dar es Salaam wachangamkie fursa ya kupata nyumba na vyumba vya kupangisha katika miradi ya ujenzi wa nyumba ya NSSF, NHC na Watumishi Housing zilizopo Kigamboni.



Amesema amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF atenge maghorofa ambayo yatakaliwa na wahadhiri na wanafuzi wa vyuo vya elimu ya juu na vyuo vikuu tena waache kuwatoza bei kubwa na badala yake wapange bei mpya za kupangisha ambazo wanachuo watazimudu.



Ili kufanikisha utekelezaji  wa jambo hilo, Waziri Mkuu amesema amewashauri viongozi wa taasisi za elimu ya juu za mkoa wa Dar es Salaam wafanye mawasiliano  na Watendaji Wakuu wa NSSF, NHC na Watumishi Housing ili wafikie makubaliano ya namna ya kupangisha au kununua nyumba hizo.



Akizungumzia suala la kuboresha usafiri kwa wanafunzi na watu wakaoishi kwenye nyumba hizo, Mheshimiwa Majaliwa amesema tayari amekwishatoa maelekezo  kwa viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo Wakuu wa Wilaya za Kigamboni na Temeke wakutane na uongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) ili wapange safari za mabasi ya abiria kutoka Tuangoma, Mtoni Kijichi hadi eneo la Ferry Kigamboni.



Mheshimiwa Majaliwa amewasihi wahadhiri na wanachuo wachangamkie fursa hiyo ili waweze kupata nyumba bora za kupanga au kununua ili kuepuka adha ambayo imewakabili kwa muda mrefu ya kupanga au kuishi katika nyumba duni.



Akiwaasa wahitimu  wa Mahafali hayo, Mheshimiwa Majaliwa alisema: “Mnao wanao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa mnatumia vizuri elimu mliyoipata  chuoni ili kuchochea maendeleo ya kweli ya nchi yetu. Hivyo basi, huko mnakoenda iwe ni kwenye Halmashauri, Mikoa, Wizara, taasisi za umma na hata sekta binafsi, mkawe chachu ya mafanikio.”



“Aidha, mtakapokuwa huko kwenye maeneo mbalimbali ya kazi, hakikisheni mnajitanabaisha kwa  weledi na ufanisi wa hali ya juu. Tunawatarajia muwe mfano kwa kuwa waadilifu, waaminifu na wachapa kazi,” alisema Mheshimiwa Majaliwa.



Aliwasihi wahitimu hao kuwa watakapoingia kwenye utumishi wa umma au kwingineko wakazingatie maadili na kujiepusha na tabia ya kujitafutia utajiri wa harakaharaka. “Kafanyeni Kazi kwa uzalendo wa hali ya juu,” aliongeza Mheshimiwa Majaliwa. 



Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza katika mahafali hayo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango alisema ili Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kiweze kuwa chachu ya mabadiliko makubwa ya kiuchumi yanayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, ni lazima uongozi wa chuo hicho utekeleze sera ya elimu kwa vitendo na kuwa wabunifu katika kupitia upya mitaala, ufundishaji na kufanya tafiti.



Waziri Mpango amelitaka Baraza la Uongozi wa Chuo cha IFM na wanataaluma waendelee kuwa wabunifu zaidi ili kuhakikisha kwamba fani zinazofundishwa Chuoni hapo zinaendana na wakati huku wakizingatia mahitaji ya nchi na wananchi wake pamoja na mabadiliko ya haraka ya kitekinolojia yanayoendelea ulimwenguni.



Jumla ya wahitimu 2,775 wametunukiwa tuzo mbalimbali na wanafunzi 20 wa Shahada ya Usimamizi wa Fedha wamepongezwa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha IFM, kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ,Novemba 29, 2019.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na Wahitimu wa Chuo cha IFM, kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ,Novemba 29, 2019.
 Wahitimu wa Chuo cha IFM, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ,Novemba 29, 2019

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati aliwasili kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha IFM, Dkt. Benson Bana, wakati aliwasili kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa anaingia kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ,Novemba 29, 2019

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, wakati aliwasili kwenye kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.

Dkt Mahiga Awataka Wakuu wa Magereza Nchini Kutumia Ujuzi wa Wafungwa Kujiendesha na Kutoa Mchango wa Gawio kwa Serikali

$
0
0

Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Balozi Dkt Augustine Mahiga amewataka Wakuu wa Magereza nchini kutumia nguvu kazi na ujuzi wa wafungwa walioko magerezani kubuni miradi mbalimbal ili kuwazalishia fedha zitakazowawezesha kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini.

Balozi Mahiga ameyasema hayo leo alipotembelea gereza la Kyela kujionea jinsi Taasisi za Haki Jinai zinavyotekeleza majukumu yake katika mahakama na magereza ikiwemo kutatua changamoto ya mrundikano wa mahabusu katika magereza pamoja na kuboresha mfumo wa utoaji haki na hali ya magereza kote nchini.

“Nguvu kazi za hawa wafungwa ni nyingi na wana ujuzi mbalimbali mnaoweza kuutumia kuanzisha miradi ambayo itawasaidia kupata fedha na mkaweza kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini, watumieni. Pale Dar es Salaam natazama yale majengo ya magereza mnajengewa na jeshi wakati mngeweza kujenga wenyewe.” 

Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la Kyela ASP. Nelson.M. Mwaifani amesema kwamba wao wamejitahidi kuhakikisha kwamba gereza hilo halina msongamano wa mahabusu na kwamba mazingira ya wafungwa na mahabusu ni mazuri salama kwa afya za watu hao kwani wana mabweni na magodoro yanayowatosha wafungwa na mahabusu wote waliopo katika gereza hilo. Pamoja na hayo ASP. Mwaifani amemwambia Waziri Mahiga aliyeambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Biswalo Mganga kwamba wameingia mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Kyela ya kuzoa taka ngumu, kuzibua mifereji na kufanya usafi katika hospitali ya Wilaya kwa makubalino ya kulipwa shilingi 6,700,000/- kwa mwezi.

Hata hivyo, Dkt. Mahiga alifurahishwa na uongozi wa gereza la Kyela chini ya ASP. Nelson.M. Mwaifani kwa kuwa wabunifu na kushirikiana vizuri na Halmashauri ya Kyela kiasi cha kufanikiwa kupata tenda ya kufanya usafi katika Halmashauri hiyo jambo linalowaingizia wastani wa cha shilingi milioni sita kwa mwezi. Aidha aliwataka wakuu wote wa Magereza nchini kuiga mfano huo na kwamba siku moja wawe sehemu ya taasisi za serikali zitakazotoa gawio mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Joseph Pombe Magufuli.

“Nataka siku moja gereza hili lichangie kwenye mgao wa pesa za Taasisi ya Mahakama kwaajili ya gawio la kwenda serikalini mbele ya Rais, nikisikia, nitafurahi sana. Nina uhakika hivi karibuni tutaulizwa mchango wenu ni nini kwenye gawio la serikali. Najua mnaweza kuwa vyanzo vingi vya kupata pesa hivyo ni matumaini yangu kuwa gawio lijalo Wizara yetu au Taasisi ndani ya wizara yetu itatoa kitu (‘very signficant’) kikubwa, na magereza nina uhakika. Kule sabasaba kila mwaka mnapata zawadi tena nzuri tu, mnaongoza, sasa hapa onesheni mfano mzuri.” Amesema Dkt. Mahiga.

Hivi Karibuni Mheshimiwa Rais Dkt. John Joseph Pombe Magufuli azitaka Taasisi za Umma zinazozalisha na kupata faida zitoe gawio kwa serikali na kuzipa siku 60 Taasisi,Mashirika na Makampuni ya serikali ambayo hajatoa yafanye hivyo ndani ya muda huo. Waziri Mahiga ameamua kutumia ziara yake ya siku saba pamoja na mambo mengine kuzipa changamoto Taasisi za utoaji haki jinai kuanza kufikiria namna ya kuweka mikakati madhubuti ili nazo zianze kutoa gawio kwa serikali. Ziara hii iliyoendelea leo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela na Gereza la Kyela, itaendelea tena kesho katika Wilaya ya Mbarali jijini Mbeya.

DOKTA KIJAJI AKITAKA CHUO CHA MIPANGO KUFANYA UTAFITI WA UMASIKINI NA UTEKELEZAJI MIRADI YA UMMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na Wahitimu na watumishi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma, katika mahafali ya 33 ya Chuo hicho ambapo aliuagiza uongozi wa chuo hicho kuongeza juhudi katika masuala ya tafiti zinazolenga kutatua changamoto mbalimbali za maendeleo na kupunguza umaskini.
Kamishina Msaidizi wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Pius Mponzi, akitoa neno la kumkaribisha mgeni rasmi wa mahafali ya 33 Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), kwa niaba ya Katibu Mkuu waWizara hiyo.
Mkuu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya akitoa hotuba katika Mahafali ya 33 Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma.
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma, wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 33 ya chuo hicho.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akimtunuku Shahada ya Mipango na Usimamizi wa Mazingira mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma, katika Mahafali ya 33 ya chuo hicho ambapo aliwasihi wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kujiajiri.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma wakivaa kofia baada ya kutunukiwa Astashahada na Shahada mbalimbali katika Mahafali ya 33 ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere chuoni hapo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akipokea zawadi ya mipira kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya katika Mahafali ya 33 ya Chuo hicho Kampasi Kuu ya Dodoma, mipira hiyo imetengenezwa katika kiwanda cha kujenga kiwanda cha kuchakata na kutengeneza bidhaa za ngozi katika kijiji cha Idifu Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma ambapo Chuo kimewekeza jumla ya shilingi milioni 396.
Mfanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango Mike Luzigah (katikati) akiwa na baadhi ya Wahitimu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu wafuatilia kwa karibu matukio mbalimbali ya kutunukiwa Astashahada na Shahada mbalimbali katika Mahafali ya 33 ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere chuoni hapo.

Jumuiya ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma, wakimsikiliza Mkuu wa Chuo hicho Prof. Hozen Mayaya, akitoa hotuba wakati wa Mahafali ya 33 ya Chuo hicho ambapo wahitimu 3,182 wa,etunukiwa Astashahada na shahada mbalimbali.



(Picha na Farida Ramadhani-Wizara ya Fedha na Mipango)

…………………..

Benny Mwaipaja, Dodoma

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amekitaka Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, kutafiti kwa kina namna wananchi wanavyoweza kuondokana na umasikini wa kipato pamoja namna Miradi mbalimbali ya Serikali inavyoweza kutekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia thamani ya fedha kuliko ilivyo sasa.

Dkt. Kijaji ametoa rai hiyo wakati akiwatunuku astashahada na shahada mbalimbali wahitimu 3,182 Wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kampasi ya Dodoma wakati wa sherehe za mahafali ya 33 ya chuo hicho.

Amesema kuwa matokeo ya tafiti hizo yataisaidia Serikali na Jamii kwa ujumla kupanga mikakati ya namna ya kukabiliana na umasikini wa wananchi hususan wa vijijini pamoja na kuharakisha maendeleo ya nchi kwa kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa na Serikali inakuwa na tija.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ni Kamishna Msaidizi wa Bajeti Bw. Pius Mponzi amemwahidi Dkt. Ashatu Kijaji, kwaniaba ya Baraza la Chuo hicho kwamba wataongeza jitihada katika eneo la utafiti na kuhakikisha kuwa matokeo ya utafiti huo yanawafikia wananchi kwa lugha rahisi

Naye Mkuu wa Chuo hicho cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya amesema chuo chake kimetimiza miaka 40 tangu kianzishwe na kimepata mafanikio makubwa kwa kutoa wahitimu mahili na wenye kukidhi mahitaji ya soko.

Amebainisha kuwa Chuo kimeongeza idadi ya kozi kutoka kozi moja mwaka 1980 hadi kufikia kozi 25 mwaka huu, huku idadi ya wanachuo wanaodahiliwa nayo imeongezeka kutoka wanachuo 13 mwaka huo hadi kufikia wanachuo zaidi ya elfu 11 mwaka huu.

JAJI MKUU ATAKA ELIMU YA SHERIA KUWA SILAHA

$
0
0


Na Magreth Kinabo – Mahakama, Lushoto

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto(IJA) kutumia silaha ya elimu ya sheria kuitumikia jamii kikamilifu.

Aidha, Jaji Mkuu amesema kwamba wahitimu hao wanapaswa kuinoa elimu hiyo kila wakati ili silaha hiyo iwe na nguvu ya kuibadilisha dunia.

Prof. Juma alisema hayo katika sherehe za mahafali ya 19 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa wahitimu wa Stashada na Astashahada ya Sheria, yaliyofanyika leo Novemba 29, mwaka huu chuoni hapo, wilayani Lushoto mkoani Tanga. 

‘Katika fani ya sheria, moja ya njia ya kuinoa silaha hiyo ni kujisomea kila wakati kwa sababu sheria na kanuni huwa zinabadilika mara kwa mara. Sio vyeti vyenu vitakavyofanya kazi ya kutoa huduma. Kwa kuhitimu hivi leo haina maana kwamba mtakuwa mmemaliza kujifunza masuala yote ya kisheria.

‘Bali mnapaswa kuendelea kuwa wanafunzi kila wakati ili kujua sheria mpya na kanuni zake pindi zinapobadilika. Mhitimu mzuri ni yule anayeacha milango wazi ya kujifunza kutoka kwa wengine’.alisema Jaji Mkuu.

Jaji Mkuu aliwaasa wahitimu hao, popote pale watakapokuwa kujifunza jambo jipya kila siku ili wasipitwe na wakati ili kutoiaibisha fani yao, hivyo wajiendeleze hadi kufikia viwango vya juu kabisa katika fani hiyo muhimu.

‘Jengeni tabia ya kujisomea wenyewe vitabu ili kuendelea kujielimisha. Kamwe usimtegemee mtu mwingine asome kisha akuelekeze. Katika kujisomea, hakikisheni mnasoma pia mambo yasiyo ya kisheria kwa mfano hivi karibuni, Mhe. Benjamin William Mkapa (Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu) alizindua kitabu chake “My Life” My Purpose, A TANZANIA PRESIDENT REMBERS”,’ alisisitiza.

Alisema kitabu hicho kitawaongezea ufahamu wa historia ya nchi yetu kupitia miaka 81 ya maisha ya Rais huyo wa Awamu ya Tatu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo hicho, lililomaliza muda wake, Mhe.Jaji Dkt. Gerald Ndika, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, alisema mahafali haya ya 19, yamefanya jumla ya wahitimu 6,037 katika ngazi ya Stashahada na Astashada ya Sheria tangu kilipoanzishwa mwaka 2001.

Naye Mkuu wa chuo hicho, Mhe Jaji Dkt.Paul Kihwelo alizitaja takwimu za wahitimu hao kwa mwaka huu, kwa upande wa Stashahada ya Sheria kati ya wahitimu 169 wanaume ni 93 (55.03%) na wanawake 76 (44.97%) na kwa upande wa Astashahada ya Sheria, kati ya wahitimu 234 wanaume ni 102 (43.59%) na wanawake ni 132 (56.41%).

Mahafali hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali, pia baadhi wahitimu walizawadiwa vyetieti, vitabu pamoja na fedha taslimu kutoka chuo hicho na Mahakama yaTanzania.

Pia wahitimu bora wawili kutoka kutoka ngazi hizo, waliopata wastani wa daraja ‘A’ katika somo la mwenendo wa mashauri ya madai na jinai walipewa zawadi kutoka kwa Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

MATUMIZI YA NISHATI MBADALA NI KITU CHA MUHIMU KWA MAENDELEO YA TAIFA -SIMBACHAWENE

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene akiongea wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya nishati jadidifu yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene akiangalia taa inayotumia mwanga wa jua wakati akitembelea mabanda mbalimbali yaliyokuepo katika viwanja vya mnazi mmoja kwenye maonyesho ya nishati jadidifu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene akiwa pamoja na Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Bwana Jeroen Verheul wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya nishati jadidifu yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja. Uholanzi ni Wafadhili wakubwa katika masuala ya nishati jadidifu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamojaj na Watumishi wa TAREA ambao ni waandaji wa maonyesho ya nishati jadidifu ambayo hufanyika kila mwaka.Mwaka huu yamefanyika katika viwanja vya mnazi mmoja.

…………………….

Matumizi ya nishati ya kuaminika na endelevu ni kitu kisichoepukika kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na kwa Taifa lolote duniani hasa tunapoelekea kufikia lengo la Uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 2025. Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene alipokua akizindua maonyesho ya 14 ya kitaifa ya nishati jadidifu yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja , jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa changamoto kubwa iliyopo ni kuhakikisha kuwa masuala yote yanayokwamisha upatikanaji rahisi, ueneaji na ongezeko la matumizi ya Nishati hizi kwa wananchi wote hasa walioko vijijini na hata mijini linashughulikiwa ipasavyo. ”Ninawashauri muwe tayari kupeleka huduma zenu vijijini kwa kuanzisha matawi ya biashara zenu huko badala ya kunga’ng’ania mijini pekee” alisema Waziri Simbachawene. 

Aidha alisititiza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inathamini juhudi za uendelezaji na uhamasishaji wa matumizi ya Nishati jadidifu na udhibiti wa ubora wa vifaa na ufungaji wa mitambo mbalimbali, ili kuwa na Teknolojia endelevu katika ustawi wa Mazingira yetu. Pia amewaagiza TAREA kufanya utafiti kubaini kwa kiasi gani jamii ya Wananchi katika mkoa wa Dar es Salaam wanatumia nishati jadidifu.

“Naye Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Bwana Jeroen Verheul amemshukuru Waziri Simbachawene lakin pia amesema kuwa wataendelea kufadhili masuala mbalimbali ya mazingira yakiwemo yanayohusu nishati mbadala kama ambavyo wamefanya kwa TAREA.

Akiongea katika ufungzi huo Katibu wa Jumuia ya Nishati jadidifu Makamu Mwenyekiti wa TARE Bwana Prosper Magali, alimshukuru Waziri Simbachawene kwa kufungua maonyesho hayo na aliongeza kuwa TAREA itaendelea kushughulika na masuala ya nishati jadidifu lakini pia wanachukua maelekezo ya Waziri aliyowapa na kuyafanyia kazi.

Maonyesho hayo ya nishati jadidifu yameandaliwa na Jumuia ya nishati jadidifu (TAREA) ambapo hufanyika kila mwaka. Kwa mwaka huu maonyesho hayo ymefanyika katika viwanja vya mnazi mmoja na mgeni Rasmi akiwa Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene.

WAZIRI WA AFYA AZINDUA CHUMBA CHA KUHIFADHI MAJOKOFU YA UMEME ZAHANATI YA NYAKASUNGWA SENGEREMA.

$
0
0

***********************************

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amezindua chumba cha kuhifadhia majokofu yanayotumia umeme wa jua kwenye zahanati ya Nyakasungwa iliyopo halmashauli ya Buchosa wilayani Sengerema.

Halmashauri ya buchosa imepata majokofu 17 kutoka Wizara ya afya mwezi oktoba 2019 kwa awamu ya kwanza na tayari yamesambazwa kwenye na kufungwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Hali ya chanjo kwa halmashauri hiyo kwa kwa mwaka huu ni asilimia 94 kutoka asilimia 79 mwaka jana na katika kampeni ya kitaifa ya chanjo ya surua na rubella mwezi oktoba mwaka huu imefanikiwa kwa asilimia 106.

Majokofu hayo yatasaidia kuimarisha mnyororo baridi na hivuo kuongeza ubora na utunzaji wa chanjo katika vituo vya kutolea huduma za afya ambayo itapelekea watoto kupata chanjo zenye ubora kama ilivyokusudiwa

TARURA watakiwa kushughulikia maeneo korofi msimu wa mvua

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa mbele) akitoka kuangalia daraja la mto Kanteza linalowaunganisha wananchi na kituo cha afya cha Laela, Wilayani Sumbawanga, daraja ambalo limetengewa shilingi milioni 163.2 katika mwaka wa fedha 2019/2020 huku kazi zikiwa zinaendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa mbele) akitoka kuangalia daraja la mto Kanteza linalowaunganisha wananchi na kituo cha afya cha Laela, Wilayani Sumbawanga, daraja ambalo limetengewa shilingi milioni 163.2 katika mwaka wa fedha 2019/2020 huku kazi zikiwa zinaendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akizungumza na baadhi ya wananchi wa mji mdogo wa Laela juu ya adha wanayoipata kabla ya dalaja la mto Kanteza kuanza kutengenezwa na kutaka kujua maoni yao juu ya ujenzi huo muda mfupi baada ya kukagua daraja hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akimkabidhi zawadi ya pesa mmoja wa mtoto wa wananchi aliokuwa akizungumza nao kupata maoni juu ya ujenzi wa daraja la mto Kanteza katika mji mdogo wa Laela.

********************************

Wakala wa Barabara za mijini na Vijijini (TARURA) wametakiwa kuhakikisha Barabara zote za Vijijini zinapitika mwaka Mzima kwa kufanyiwa matengenezo na endapo itashindikana basi ni muhimu kuyapa kipaumbelea maeneo korofi, hasa katika kipindi hiki cha Mvua jambo ambalo litawasaidia wananchi kuendelea na shughuli zao za Kiuchumi bila vikwazo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo katika kikao cha Bodi ya barabara baada ya wabunge wa mkoa huo pamoja na wenyeviti wa halmashauri kuilalamikia TARURA juu ya utendaji wake wa kazi pamoja na mipangilio yao ya bajeti katika kutekeleza majukumu yao.

“Wakala wa Barabara za Vijijini (TARURA) kuhakiki Barabara zote za vijijini katika Halmashauri zote za Mkoa wa Rukwa ili kwanza wawe na orodha kamili ya Barabara za Vijijini na zipo kwenye hali gani,Baada ya kuhakiki wawe na orodha ya Barabara zilizoingizwa kwenye Mtandao wa Barabara za TARURA na Barabara zipi hazipo kwenye mtandao wa Barabara za TARURA na kwanini?,” Alihoji

Aidha alisema kuwa kwa kufanya hivyo itawasaidia TARURA kuwa na picha ya Barabara zote za Mkoa wakati wa upangaji wa Bajeti ya mwaka 2020/2021 ili waweze kuziweka kwenye Bajeti Barabara ambazo zinahitaji Matengenezo.

Wakati wakiwasilisha malalamiko hayo miongoni mwa wabunge hao walisema kuwa hawaridhishwi na bajeti inayotengwa na TARURA na hata hiyo inayotengwa haifikishwi kwa wakati hali ambayo inasababisha hata hicho kidogo kilichotengwa kushindwa kufanya kazi iliyokusudiwa.

Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mh. Ali Kessy alisema, “Tumepanga bajeti milioni 400 wazilete zote milioni 400, hauwezi kupanga bajeti milioni 400 unaleta milioni 20, nimemuuliza mratibu wa (TARURA) Mkoa, mmeleta shilingi ngapi anasema tumeleta milioni 20 kwenye bajeti ya serikali ya milioni 400, walitenga kabia daraja la Kavunje, wakadarasai wamekwama daraja haliendelei na mvua ndio hiyo kama unavyoona.”

Naye Mbunge wa Nkasi Kusini Mh. Desderius Mipata alisema kuwa wananchi wa kata ya Ninde watatengwa kutokana na TARURA kushindwa kutenga bajeti kwaajili ya ukarabati wa barabara inayowaunganisha wananchi wa kata hiyo na kata za jirani.

“Kwahiyo naomba mtafute njia yoyote ya dharura ya kuwezesha eneo hilo lipitike hakuna namna nyingine ya kufanya, nikiwa bungeni daraja la kwenda ninde lilikuwa limevunjika, nikapiga kelele bahati nzuri walikuja wakatengeneza kwa pesa kidogo lakini barabara yake haipitiki,” Alimalizia.

Wakati akitoa malalamiko yake kwa niaba ya wakandarasi wenzie Bwana Anyosisye Kiluswa amesema kuwa wakandarasi bado wanazidai halmashauri fedha za matengenezo ya barabara kadhaa kabla ya barabara hizo hazijahamishiwa kwa TARURA na kuongeza kuwa halmashauri hizo zilishapewa fedha na serikali lakini matokeo yake wametumia kwa matumizi mengine.

“Sasa kwa sasa hivi wakandarasi tunashindwa kutekeleza wajibu wa kufanya kazi kwasababu pesa zetu wenyewe ni za kuunga unga, ukifanya kazi umelipwa halafu pesa hiyo hiyo unaichukua unakwenda kufanya kazi sehemu nyingine, sasa unapokuwa unafanya kazi bila ya kulipwa na nyingine ambazo zipo wanazitumia kwenye maeneo mengine matokeo yake wakandarasi wa mkoa wa Rukwa tunaonekana hatufanyi kazi vizuri,” Alisisitiza.

Kwa upande wake Kaimu mratibu wa TARURA Mkoa wa Rukwa alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 jumla ya fedha shilingi bilioni 4.133 kwaajili ya matengenezo ya barabara km 346.63 na vivuko 48 huku kutoka mfuko wa barabara zikitengwa shilingi bilioni 1.763 kwaajili ya miradi ya maendeleo ambapo daraja la mto Kavunja likitengewa shilingi milioni 400 na daraja la mto Kanteza lilopo Laela likitengewa shilingi milioni 163.2.

Waziri Mkuu aongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, mazishi ya Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi),

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mkono na Mjomba wa Marehemu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi) aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni Maarufu, wakati akiwasili kwenye makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, kuongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, katika mazishi ya Mfanyabiashara na Mwanazuoni huyo, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hussein Mwinyi, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. Kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiongea na wananchi baada ya mazishi ya aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), kwenye makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

***********************************

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine kwenye mazishi ya Mfanyabiashara na Mwanazuoni Maarufu wa dini ya Kiislam, Alhaj Aziz Massanga (Zingizi), yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani.



Alhaj Zingizi amefariki dunia Jumatano, Novemba 27 jijini Johanesburg nchini Afrika Kusini alikikwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Marehemu Alhaj Zingizi alikuwa akisumbuliza na ugonjwa wa saratani ya kibofu.



Akizungumza baada ya mazishi hayo yaliyofanyika jana jioni (Ijumaa, Desemba 29, 2019), Waziri Mkuu aliwaasa wananchi kumuenzi marehemu Alhaj Zingizi kwa kufanya mambo mema kama alivyokuwa akiyafanya enzi za uhai wake. “Marehemu Zingizi alikua ni mtu mwenye kusaidia jamii kwa hali na mali.”



“Marehemu ametenda mengi mema katika msikiti wake na jamii iliyomzunguka. Alisaidia wenye mahitaji, hivyo na sisi hatuna njia nyingine ya kumuenzi marehemu bali ni kutenda mema kwa jamii hususani kwa kuwajali watu wenye shida ili wale waliokua wananufaika wasione pengo kubwa. ”



Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali ipo pamoja na viongozi wote wa dini na wala wasisite kuijulisha pale wanapopatwa na jambo lolote ipo tayari kushirikiana nao kwa namna moja au nyengine.

DKT.BASHIRU KATIKA ZIARA YAKE VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt.Bashiru Ally Kakurwa, akizungumza na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mjini katika mwendelezo wa ziara yake ya kuimarisha CCM Unguja.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Ndugu Talib Ali Talib akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally katika Mkoa wa Mjini kichama.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt.Bashiru Ally Kakurwa,akizungumza na kutoa salamu za Chama Cha Mapinduzi kwa Vijana na Wanachama mbali mbali walioshiriki katika mapokezi yake katika Mkoa wa Mjini kichama.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt.Bashiru Ally Kakurwa,akivishwa Skafu na Vijana Maalum wa UVCCM baada ya kuwasili katika Ofisi ya CCM Jimbo la Jang’ombe Matarumbeta Unguja.

BODI YA URATIBU WA NGOs YATEMBELEA MIRADI YA PLAN INTERNATIONAL JIJINI MWANZA

$
0
0
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao akifafanua jambo kwa vijana wa kikundi cha Shilabela wanaonufaika na mradi wa Vijana Maisha ni Kazi unaotekelezwa na Shirika la Plan International Buhongwa jijini Mwanza wakati Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.
Mwezeshaji kutoka Shirika la Amani Girls Home Bw. Mang’olo Shoma Bahati akieleze jinsi Mradi wa Vijana Maisha ni Kazi unaotekelezwa na Shirika la Plan International ulivyowasaidia vijana wa Kikundi cha Shilabela cha Buhongwa wakati Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika.
Afisa Miradi kutoka Shirika la Plan International Bw. Nicodemas Gachu akielezea kuhusu utekelezaji wa Miradi inayotekelezwa na Shirika hilo wakati Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ilipotembelea Miradi inayotekelezwa na Shirika hilo mkoani Mwanza katika ufuatiliaji wa mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Dkt. Richard Faustine Sambaiga (Mwenye koti) akikabidhi mchango wa jamii kwa mmoja wa mjumbe wa kikundi cha Shilabela kilichopo Buhongwa jijini Mwanza wakati Bodi hiyo ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.

RC TABORA AAGIZA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA KUSIMAMIA UKUSANYAJI WA MAPATO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama(kushoto) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele(katikati) jana kabla ajafungua mafunzo ya siku mbili ya Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na wajumbe wa Serikali za Vijiji waliochaguliwa hivi karibuni wilayani humo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele akiwasisitiza jana Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji juu ya kushirikiana na Madiwani katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua jana mafunzo ya siku mbili ya Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na wajumbe wa Serikali za Vijiji waliochaguliwa hivi karibuni wilayani Kaliua.
Picha na Tiganya Vincent 

………………..

NA TIGANYA VINCENT

SERIKALI imewaagiza viongozi wa Serikali za Mitaa walioapishwa kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa ajili ya kupata fedha za kuwaletea maendeleo wananchi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Wajumbe wa Wilaya ya Kaliua waliochaguliwa hivi karibuni na kuapishwa.

Alisema kuwa kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kuhakikisha wanakusanya ushuru, kodi ,maduhuli na mapato mengine ya Serikali katika maeneo yao.

Mwanri aliongeza kuwa jukumu lao jingine ni kuratibu shughuli na miradi mbalimbali katika maeneo yao ya Vitongoji na Vijiji kwa ajili ya kuhakikisha matumaini na matarajio ya wananchi yanatimizwa.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele aliwataka viongozi wa vitongoji na vijiji waliochaguliwa hivi karibuni kutumia Sheria ndogo ndogo za Vijiji katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali yaliyo ndani ya uwezo wao.

Aidha aliwataka kushirikiana na Madiwani katika kuhakikisha wanahamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, Zahanati na utengezaji wa barababara za Vijiji.

TAASISI YA UHASIBU NCHINI (TIA) KWA MARA YA KWANZA YATUNUKU SHAHADA KAMPASI ZA SINGIDA NA MWANZA

$
0
0
.
 Mgeni rasmi wa mahafali ya 17 ya Taasisi ya uhasibu Tanzania (TIA) kwa kampasi za Singida, Mwanza na Kigoma, Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia kwenye mahafali hayo yaliyofanyika mkoani Singida jana.
 Mratibu wa Taaluma Kampasi ya Singida,  Abbas Sanga akizungumza kwenye mahafali hayo.
 Mhitimu bora wa Shahada ya Uongozi wa Rasilimali Watu kutoka Kampasi ya Singida Emmanuel Matikiti akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Dkt. Rehema Nchimbi.
 Miongoni mwa wahitimu wa kike waliofanya vizuri akipokea zawadi.
 Wahitimu wa kozi ya Astashahada ya Uhasibu muda mfupi kabla ya kutunukiwa.
 Mhitimu wa Shahada ya Uhasibu kutoka kampasi ya Singida Livingstone Ruzikamunzira  akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi Dkt. Rehema Nchimbi kwenye mahafali hayo.
 Wahitimu wa kozi ya Shahada ya Uhasibu wakiwa mbele ya mgeni rasmi kabla ya kuanza zoezi la kuwatunuku
Mgeni rasmi Dkt. Rehema Nchimbi (waliokaa katikati) akiwa na Wahitimu wa kozi mbalimbali kwenye mahafali ya 17 ya TIA mkoani Singida. 
Na Dotto Mwaibale, Singida
KWA mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Kampasi za Singida na Mwanza chini ya Taasisi mahiri na kongwe ya uhasibu nchini (TIA) hapakuwepo na kozi ya Shahada ndani ya kampasi zake za Singida na Mwanza. Hivyo wahitimu wa kozi ya shahada kwa mwaka wa masomo 2018/2019 ndio wanaofanikiwa kuandika historia ya kuhitimu kozi hiyo kwa mara ya kwanza.
Katika mahafali ya 17 ya (TIA) kwa Kampasi za Singida, Mwanza na Kigoma, na mahafali ya nane kwa kampasi ya Singida, jumla ya wahitimu 209 wamehitimu kozi ya Shahada, huku wengine 328 wakihitimu kozi ya Stashahada, Astashahada 504 na ngazi ya cheti 647 wote wakihitimu katika kozi za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Uongozi wa Rasilimali Watu na Usimamizi wa Biashara.
Akizungumza kwenye mahafali hayo, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango mkoani hapa jana, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, mbali ya kupongeza juhudi lukuki zinazofanywa na taasisi hiyo katika kuboresha ubora wa taaluma na wanataaluma, aliwasihi wahitimu hususan wale wa shahada na uongozi mzima wa TIA kuanza kutumia sifa na ubora wa kitaaluma walionao katika kuongeza thamani kwa wananchi walio mitaani hususan vijana.
Dkt Nchimbi aliwatakafarisha na kuwataka wahitimu kujiuliza je sura ya kampasi hiyo huko nje ikoje? Kampasi hii inavyosifika kwa ubora je na akina mama lishe na waendesha bodaboda wanaoizunguka na kuihudumia kila kukicha nao wamepata fursa ya kuambukizwa ubora huo? Je kampasi hizi zinaonekanaje huko nje katika kubadili na kuongeza thamani hususan kwa vijana ili kuchagiza na kuleta chachu ya mabadiliko ya fikra kufikia maendeleo stahiki na ya kiushindani
“Je haiwezekani TIA kuwa na mafunzo ya muda mfupi kwa vijana wetu, waendesha bodaboda, mama lishe na wajasiriamali angalau na wao wakawa na mahafali yao ya kila wiki itapendeza, na itaongeza ubunifu tija na ufanisi ndani na nje ya kampasi zetu kwa maendeleo ya taifa letu,” alisema Dkt Nchimbi
Alisema watumishi wa Singida wamejiwekea kauli mbiu yao inayojulikana kama “ Mshahara wangu uko wapi”? huku akichekesha wahitimu kuwa kuna watumishi ambao wameshapokea mshahara wa mwezi Novemba mwaka huu, lakini ukimuuliza mpaka sasa hauoni Zaidi ya kulalamika mshahara hautoshi! Na kutoa rai kwa wanajumuiya ya TIA kuangalia namna ya kuanzisha somo mahususi la “mshahara hautoshi,” akiamini ni taasisi hiyo pekee na wahitimu wake ndio jawabu la kutamka kwanini hautoshi, uko wapi na kutupa maarifa na stadi stahiki za siku zote kuiona mishahara yetu.
Aidha, akizungumzia kuhusu ubora wa elimu ndani ya taasisi Dkt Nchimbi alisema fani zinazotolewa na TIA ni muhimu sana katika kuendesha uchumi wa taifa, hususan katika kusimamia mapato na matumizi ya fedha za umma, hivyo aliwataka kuzidisha kasi ya umahiri huo katika kufanikisha azma ya sera iliyopo ya Tanzania ya Viwanda.
Alisema dunia ya sasa imetamalaki teknolojia na utandawazi hivyo jukumu lililopo ni kuendelea kuboresha mitaala ndani ya taasisi ili wakati wote ikidhi viwango vya kimataifa, hususan umahiri badala ya maarifa. Na kuwasihi kuzidisha kuzalisha wataalamu wenye weledi, maarifa na umahiri wa kutatua changamoto na sio kuziongeza.
“Zingatieni kwa umakini suala la umahiri katika mitaala yenu ili tuweze kuwa na wataalamu wenye uwezo wa kulifikisha taifa kwenye uchumi wa kipato cha kati kabla ya ishirini ishirini na tano (2025),” alisema Dkt Nchimbi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha na Mipango, Wakili Said Musendo Chiguma, alisema jukumu la bodi ya ushauri, pamoja na mambo mengine ni kutoa ushauri kwa TIA kwa nia ya kutekeleza na kuendeleza jitihada za serikali kulingana na malengo makuu yaliyoianzisha.
Chiguma alisema lengo hasa la taasisi hiyo ni kutayarisha wahitimu kwa uboreshaji endelevu wa mitaala, azma ikiwa ni kuandaa wafanyakazi wenye weledi na uwezo wa kujiajiri, sambamba na maboresho hayo kuzingatia juhudi za kujenga uzalendo, uaminifu na maadili, huku akisisistiza kwamba mhitimu asiye na sifa hizo siyo rasilimali kwa taifa.
Alisema kwa matokeo ya vigezo hivyo taasisi imeendelea kupendwa na kuwa kivutio kikubwa, hali iliyopelekea ongezeko kubwa la udahili wa wanafunzi kila mwaka licha ya kuwepo vyuo vingi vya ushindani idadi inayofikia jumla ya wanafunzi 18,585 katika kampasi zake zote sita ambazo zimesambaa kimkakati.
“TIA ni taasisi ya serikali, imeweza pia kuchangia bilioni mbili na milioni mia tano (2,500,000,000) kama ziada ya mapato yake serikalini,” alisema Wakili Chiguma.
Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Luciana Hembe, alisema Taasisi hiyo kwa sasa ina kampasi 6 zilizopo katika mikoa ya Dar es Salaam (Makao Makuu), Mbeya, Singida, Mtwara, Mwanza na Kigoma, zote zikiwa na jumla ya wanachuo 18, 587, huku jumla ya kozi zinazotolewa katika kampasi zote ni 20.
Hembe alibainisha kuwa, kwa mwaka 2019 katika kampasi zote kuna jumla ya wahitimu 8695 ikiwa ni ongezeko la asilimia 35.5 ikilinganishwa na wahitimu 6418 kwa mwaka 2018. Alisema mahafali hayo ni kwa wahitimu wa TIA ngazi tofauti Kampasi za Singida, Mwanza na Kigoma kwa mwaka wa masomo 2018/2019.
Alisema idadi ya wahitimu wote waliohudhuria na wasiohudhuria mahafali hayo katika kozi ya Cheti cha Awali, Astashahada na Shahada ni 1,688 wakiwemo wanawake 915 sawa na asilimia 54.21, na wanaume 773 sawa na asilimia 45.79

ELIMU YA UMEME KWA WASIOONA YAIPA TANESCO TASWIRA MPYA

$
0
0

 MKUU wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare  akizungumza wakati wa uzinduzi wa wasrha hiyo kushoto ni  Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro William Masome
 Sehemu ya wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro.
 Sehemu ya wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro Mkuu wa Mkoa huo ambaye hayupo pichani

 wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro aliyevaa suti jeusi akiwa kwenye picha ya Pamoja na washiriki wa semina hiyo kushoto ni  Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro William Masome 

SHIRIKA la Umeme Nchini TANESCO limeendesha semina maalum inayohusu masuala ya Umeme kwa wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati wa uzinduzi  wa warsha hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Loata Ole Sanare amesema kuwa Tanesco  imeonyesha mfano mzuri wa kuigwa kwa kutoa elimu hiyo kwa watu wa kundi  maalum katika jamii.

Alisema pia kupitia hili shirika limetoa taswira kuwa mashirika ya Umma yanafuata muelekeo wa Raisi John Pombe Magufuli ambae ni  Raisi wa wanyonge na kwa kujali wateja wake hata wa Makundi maalum kwa kutoa elimuYa Umeme itakayowasaidia katika maisha yao ya kila  siku.

Mkuu huyo wa Mkoa  amewataka wasioona kutokuwa wanyonge kwakudhani kuwa  Serikali haiwatambui na kusema kuwa Serikali ipo pamoja nao na kuwakaribisha katika ofisi za Mkoa, muda wowote watakapokua na changamoto zozote.


Naye Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro William Masome amesema Kuwa TANESCO chini ya Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Tito Mwinuka imetambua umuhimu wa watu wenye Ulemavu wa kutoona kupatiwa elimu ya Umeme ili waweze kutambua fursa  zitokanazo na umeme zitakazoweza kuwainua kiuchumi lakin pia kuwafundisha jinsi ya kutumia umeme vizuri (matumizi Bora ya umeme)ili wasilipe gharama kubwa
Kwenye kununua Umeme.


Naye kwa upande wake Mratibu wa idara ya maendeleo, Vijana na Chipkizi toka TLB , Bw.Kiongo Itambu ameishukuru TANESCO kwa kuwapatia elimu hiyo Maalum ambayo itawasaidia hasa katika kujiepusha na matukio ambayo yanaweza kuathiri usalama wao.

Alisema kwani wameshajua athari za kukaa karibu na miundombinu ya umeme  na  kuahidi kushirikiana na TANESCO katika kuwafichua wanaolihujumu Shirika kwa kuiba umeme na kuharibu miundombinu ya Shirika.

Aidha Bw. Kiongo alimuhakikishia Mkuu wa mkoa kuwa wao kama watu wenye ulemavu ni kama watu wengine, ni mara chache kusikika wasioona ikiwa na sifa ya kuliibia shirika la umeme na watakuwa mabalozi wa kuhakikisha Tanesco haiujumiwi ili kukuza kipato chake kwa maendeleo ya Shirika na Taifa kwa ujumla

RAIS MAGUFULI ATOA POLE KWA FAMILIA YA MZEE SUGWA ALIYEFIWA NA MKEWE BI. SABINA NDEGE KILANDA NA MWANAE SHIJA SUGWA , CHATO MKOANI GEITA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kaburi la Bi. Sabina Ndege Kilanda Mke wa Mzee Sugwa aliyefariki duni Septemba 15, 2019 katika kijiji cha Katende Wilayani Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli ametoa pole kwa Mzee
Sugwa kufuatia kifo cha Mkewe pamoja na Mwanae Shija Sugwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea Makaburini kwaajii ya kutoa heshima zake mwisho kwenye kaburi la Bi. Sabina Ndege Kilanda Mke wa Mzee Sugwa aliyefariki duni Septemba 15, 2019 katika kijiji cha Katende Wilayani Chato mkoani
Geita. Rais Dkt. Magufuli ametoa pole kwa Mzee Sugwa kufuatia kifo cha Mkewe pamoja na Mwanae Shija Sugwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama Makaburi ya Familia ya Mzee Sugwa mara baada kutoa heshima za mwisho kwenye kaburi la Bi. Sabina Ndege Kilanda Mke wa Mzee Sugwa aliyefariki duni Septemba 15, 2019 katika kijiji cha Katende
Wilayani Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli ametoa pole kwa Mzee Sugwa kufuatia kifo cha Mkewe pamoja na Mwanae Shija Sugwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waombolezaji nyumbani kwa Mzee Sugwa kijiji cha Katende Wilayani Chato mkoani Geita aliyefiwa na Mwanae Shija Sugwa,pia alimtembelea na kutoa pole kwa kufiwa na Mkewe Marehemu Bi. Sabina Ndege Kilanda aliyefariki dunia Septemba 15, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bi. Beatrice Masanilo aliyefiwa na mumewe walipokutana nyumbani kwa Mzee Sugwa kijiji cha Katende Wilayani Chato mkoani Geita, alipomtembelea na kutoa pole kwa kufiwa na Mkewe Marehemu Bi. Sabina Ndege Kilanda aliyefariki dunia Septemba 15, 2019 na mwanae Shija Sugwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshma za mwisho katika kaburi la Bi. Sabina Ndege Kilanda Mke wa Mzee Sugwa aliyefariki duni Septemba 15, 2019 katika kijiji cha Katende Wilayani Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli ametoa pole
kwa Mzee Sugwa kufuatia kifo cha Mkewe pamoja na Mwanae Shija Sugwa.
PICHA NA IKULU

RC.MWANRI AMPONGEZA MSANII ALIKIBA KWA MCHANGO WA VIFAA TIBA KATIKA MKOA WA TABORA

$
0
0
Msanii wa kizazi kipya hapa nchini AliKiba amepongezwa na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri kwa mchango wake wa vifaa tiba vya zaidi ya shilingi Milioni 6 kwa wananchi wa mkoa huo.

AliKiba alikabidhi vifaa hivyo kwa Aggrey Mwanri ikiwa ni sehemu ya kurejesha shukrani zake kwa wananchi wa Tabora katika tamasha lake ‘AliKiba Uforgetable Tour’ litakalofanyika Novemba.

Alikiba Ashiriki Mbio Za Tabora Green Marathon

$
0
0
 Na,Editha Edward –Tabora 

Msanii wa bongo fleva Ally Salehe Kiba Maarufu kama Alikiba ameshiriki mbio za Tabora green marathon kwa kukimbia km 2.5 zilizoanzia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora hadi viwanja vya Ali Hassan Mwinyi zilizofanyika hii leo mkoani humo 

Akizungumza katika mbio hizo msanii alikiba amesema mbio zimemfanya achangamshe mwili na akili kwani michezo zinajenga urafiki pia zinakutanisha watu na zinaimarisha mwili hivyo amefurahi kushiriki pamoja na mkuu wa mkoa huo na amewahimiza wananchi wa mkoa huo kuwa na utamaduni wa kukimbia ma kufanya mazoezi ili waweze kuwa imara kimwili.

 Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri naye alikuwa ni miongoni mwa wakimbia mbio hizo ambapo yeye amekimbia mbio umbali wa km2.5 ambapo amesema msanii alikiba ni mfano wa kuigwa kwani tangu afike mkoani humo katika tamasha lake la muziki linalojulikana kama unfogetabletour ameweza kufanya mambo mengi ya kijamii ‘’Msanii.

Pichani ni Msanii Wa bongo fleva Alikiba na mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakikimbia mbio za Tabora Green Marathon 
Pichani ni Msanii Wa bongo fleva Alikiba na mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakikimbia mbio za Tabora Green Marathon 
Pichani ni Msanii Alikiba akimvalisha medani mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kukimbia mbio za km 2.5
Msanii Alikiba akipanda mti nje ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi baada ya kukimbia mbio.

DKT.BASHIRU AWATAKA VIONGOZI NA WATENDAJI CCM KUBUNI MIRADI YA KUONGEZA MAPATO NDANI YA CHAMA

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Bashiru,amewataka Viongozi na Watendaji wa CCM visiwani Zanzibar kuendelea kubuni miradi itakayoongeza mapato ndani ya Chama.
Rai hiyo ameitoa katika mwendelezo wa ziara yake wakati akizungumza na Viongozi na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mjini Unguja huko Mkoa wa CCM Mjini.
Dkt.Bashiru. Bashiru,alifafanua kuwa uwepo wa miradi mbali mbali itasaidia  Chama kujitegemea kiuchumi.
Alisema rasilimali za vyanzo vya mapato zinazomilikiwa na CCM katika maeneo mbali mbali nchini zikitumiwa vizuri zitasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa fedha katika maeneo mbali mbali nchini.
"Chama chetu kimejaaliwa kuwa na rasilimali nyingi zikiwemo majengo, ardhi na vitu mbali mbali vilivyoasisiwa na Wazee wetu wa ASP na TANU,wajibu wetu kuvitunza na kuongeza vingineN ili na sisi tuache alama za uongozi kama walivyafanya viongozi waliopita.
Nasi tunaendelea kudhibiti rasilimali hizo zisihujumiwe na watu wachache kwani zipo kwa manufaa ya wanachama wote",alisema Dkt.Bashiru.
Kupitia Kikao hicho alihimiza wanachama kuendeleza utamaduni wa kuwa na mahusiano ya kijamii baina ya wanachama na wanachama pamoja na wananchi wengine.
Alisema mahusiano hayo ndio msingi wa Umoja na Mshikamano wa Chama Cha Mapinduzi unaowafanya watu wawe wamoja.
Aidha Dkt.Bashiru, alikemea siasa za ubaguzi kuwa zinatakiwa kupingwa na vyama vyote vya siasa kwani zinaharibu sifa ya nchi na kusababisha mipasuko isiyokuwa ya lazima kwa wananchi.
"Siasa za ubaguzi haziwezi kujenga umoja wa kitaifa hivyo tukiwa ni Chama kinachoongoza dola ni lazima tuwakumbushe vyama vingine vya siasa nchini waepuke dhambi hiyo kwani madhara yake ni makubwa juu ya ustawi wa maendeleo ya nchi.", alisema dokta Bashiru.
Alisema CCM sio chama cha wakati wa uchaguzi bali ni chama cha uongozi kinachoongoza wananchi wote, hivyo hakiwezi kushindwa kukemea juu ya masuala mbali mbali yanayolenga kuhatarisha Amani na Utulivu wa nchi.
Akizungumza kwa wakati tofauti wakati akipandisha bendera za chama katika mashina mbali mbali ya CCM,aliwataka Watendaji wa ngazi za wilaya kuhakikisha mabalozi wote wanapatiwa vitambulisho vitakavyowasaidia kuingiza katika ofisi za umma kuwasilisha changamoto za wananchi ili zitatuliwe.
akizungumza baada ya kukagua kazi za vikundi vya ujasiriamali katika Chuo Cha Ujasiriamali cha UWT Wilaya ya Mjini Kilichopo Miembeni,Dkt.Bashiru aliwapongeza viongozi wa CCM na kuwataka bidhaa zinazozalishwa katika Chuo hicho zitatuliwe soko la uhakika.

BODI YA URATIBU WA NGOs YATAHADHARISHA MASHIRIKA KUFANYA SIASA

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Dkt. Richard Faustine Sambaiga (Mwenye koti) akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati Bodi hiyo ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.

Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao akifafanua jambo kwa wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati Bodi hiyo ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.

Mjumbe wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Dkt. Zena Mabeyo akifafanua jambo wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati Bodi hiyo ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.

Mwakilishi wa Shirika la The Kesho Fund Bw. Petro Okoth akifafanua jambo katika kikao kati ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati Bodi hiyo ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.

Mwakilishi wa Shirika la Foundation for Farmer’s Service Bi. Lydia Kamugisha akifafanua jambo katika kikao kati ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati Bodi hiyo ilipokuwa inatembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.

Baadhi ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Mwanza wakisikiliza maelezo kutoka kwa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ilipotembelea Mashirika yaliyopo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa miradi katika Mashirika hayo.


Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Dkt. Richard Faustine Sambaiga (Mwenye koti) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Mwanza mara baada ya kikao kati ya Bodi hiyo na wadau hao.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

********************************

Na Mwandishi Wetu Mwanza

Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini imeyatahadharisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutojihususha na masuala ya kisiasa bali wasimamie Katiba zao katika kutekeleza majukumu yao ya kuisadida jamii ya watanzania.

Mwenyekiti wa Bodi Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Dkt. Richard Faustine Sambaiga ametoa tahadhari hiyo mkoani Mwanza alipokutana na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiseikali mara baaad ya kutembeea baadhi ya Mashiria hayo kujionea utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Mashriika ya mkoa wa Mwanza.

Dkt. Sambaiga amesema kuwa katika kipindi cha uchaguzi wadau wengi wa NGOs wanahama katika majukumu yao na kuanza kupeperusha bendera za watu wengine na sio kuihudumia jamii inayowazunguka kama Katiba zao zinavyoelekeza.

Pia amewataka wadau wanaofanya kazi za kutoa elimu kwa wapiga kura kutumia fursa ya uchaguzi Mkuu ujao kuchangamkia fursa hiyo na kuwataka kutoa elimu ya kupiga kura na sio kampeni za kisiasa.

“Kama unaona unataka kujiingiza katika masuala ya kisiasa achana na kazi za NGOs simama wewe kama wewe na sio kuitumia NGO kwa ajili ya kufanya kampeni au kuwafanyia watu kampeni za kisiasa” alisema Dkt. Sambaiga

Dkt. Sambaiga ameyataka Mashirika kujiendesha kitaasisi na sio kuendesha Mashirika hayo kwa maslahi ya mtu mmoja au kikundi cha watu bali watekeleze majukumu kwa mujibu wa Katiba yao waliosajili Shirika.

“Tumetembelea Shirika moja ofisi zipo nyumbani kwa Mkurugenzi tukaomba mikataba ya fedha hana sasa hili Shirika linaendeshwaje na mtu mmoja na lina wajumbe zaidi ya kumi”alisisitiza Dkt. Sambaiga

Kwa upande wake Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao amesema kuwa Ofisi yake imeamua kutembelea Mashirika mkoani Mwanza kufuatilia miradi ianyotekelezwa na Mashirka hayo kwa jamii.

“Tumekuja kwenu kwa lengo la kujionea miradi mnayoitekeleza katika jamii na kuona kwa uwazi na uwajibikaji wa Mashirika yenu kwa jamii ikiwemo Jamii husika kujua miradi inayotekelewa na gharama zake” alisema Bi. Vickness.

Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini imetembelea na kukagua utekelezaji wa miradi inayofanya na Mashirika yaliyopo mkoani Mwanza kwa lengo la kujiridhisha juu ya miradi hiyo na manufaa yake katika jamii.

Viewing all 109984 articles
Browse latest View live


Latest Images