Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live

Madaktari na wauguzi wa JKCI wajifunza jinsi ya kuokoa maisha ya mtu aliyepata tatizo la dharula la kiafya

0
0
Madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakijifunza jinsi ya kuokoa maisha ya mtoto aliyepata tatizo la dharula la kiafya wakati wa mafunzo ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano Taasisi hiyo jijii Dar es Salaam. Mafunzo hayo yanatolewa na wataalamu kutoka kituo cha Emergency Medical Services Academy kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Dkt. Sylivester Fanya kutoka kituo cha Emergency Medical Services Academy kilichopo Mkocheni jijini Dar es Salaam akiwafundisha madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi ya kuokoa maisha ya mtu aliyepata tatizo la dharula la kiafya wakati wa mafunzo ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea umuhimu wa mafunzo ya jinsi ya kuokoa maisha ya mtu aliyepata tatizo la dharula la kiafya kwa washiriki wa mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoandaliwa na kituo cha Emergency Medical Services Academy kilichopo mikocheni jijini Dar es Salaam.

Picha na JKCI

TANZANIA KUPIGA VITA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI WA BINAADAMU

0
0
Na Khadija Khamis – Maelezo 

Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM) Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Kazi, Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Zanzibar wamefanya majadiliano ya kupiga vita Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini.

Hayo aliyasema Mkurugenzi wa Ajira Ali Suleiman Ameir wakati wa Majadiliano kuhusu mipango mikakati yalifanyika huko katika Ukumbi wa Mtakwimu Mkuu Mazizini kati ya Shirika la IOM na Watendaji wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Zanzibar.

Majadiliano hayo ya Pamoja ni moja ya shughuli zitakazotekelezwa na IOM kwa mwaka huu wa miradi 2019/2020 ikiwa ni moja ya utekelezaji wa mpango huo chini ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa Zanzibar (Zanzibar Joint Programme) kuhusu Msaada wa Maendeleo (United Nations Assistance Development Plan II 2016 -2021).

Mpango huo wa utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto 2017-2022 Zanzibar, utasaidia Kutoa mapendekezo ya tafiti iliyofanywa Zanzibar na Shirika la IOM juu ya Unyanyasaji Kiuchumi ikihusisha Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

Kati mipango hiyo ni Kukuza uelewa wa jamii juu ya dhana na aina za Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto, Utambuzi wa wahanga, Vyanzo na Madhara yake, Juhudi za Serikali na wadau katika utokomezaji wa udhalilishaji huo.

Pia Mjadala huo ulihusisha Nafasi ya viongozi katika jamii juu ya utokomezaji wa ukatili na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto pamoja na biashara haramu ya usafirishaji wa Binaadamu.

Hata hivyo washiriki wa kikao hicho walipendekeza Kuimarishwa ushirikiano wa wadau katika jamii juu ya juhudi za kutokomeza, ulinzi wa pamoja na kuongeza mwitikio wa huduma kwa wahanga wa Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu .

Majadiliano hayo ya siku mbili yalihusisha jumla ya washiriki 28 kutoka katika jamii, Viongozi wa Shehia, Mtaa, Viongozi wa Dini, Walimu wa Skuli za Msingi na Sekondari na Maafisa Ustawi wa Jamii .
Mkurugenzi wa Ajira  Ali Suleiman Ameir (katikati),akitoa maelezo kuhusiana na mikakati ya biashara haramu ya binaadamu  ( kushoto)  Msaidizi wa Programu ya Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM)  Enna Lutengano  na  Afisa  mipango Msaidizi  wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Zanzibar  Sarah Abdallah, huko katika ukumbi wa Mtakwimu Mkuu Mazizini.
 Washiriki wa majadiliano ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wakimsikiliza Mkurugenzi wa Ajira  Ali Suleiman Ameir huko katika ukumbi wa Mtakwimu Mkuu Mazizini.

BENKI YA CRDB YAMPONGEZA PROF. NEEMA MORI

0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela (kulia) wakimpongeza Mjumbe wa Bodi ya Benki hiyo,  Prof. Neema Mori kwa kupata wadhifa wa uProfesa, hivi karibuni. 

Prof. Neema Mori ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB na ni mhadhiri mwandamizi katika Idara ya Fedha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia ni muasisi na mkurugenzi wa kampuni ya uwekezaji ya MTI iliyopo Tanzania na Norway. Pia ni mkurugenzi na muasisi wa Chuo cha Uongozi na Ujasiriamali (Institute of Management and Entrepreneurship Management (IMED). Amewahi pia kuwa Doctoral Research Fellow Chuo Kikuu cha Agder, Norway. Prof Mori ana Shahada ya Ubobevu (PHD) katika biashara za kimataifa (utawala wa makampuni na bodi za taasisi za fedha) kutoka chuo kikuu cha Agder Norway. 

Benki ya CRDB inafuraha kwamba sera yake ya usawa kazini, inayowapa vipaumbele wanawake katika nyadhifa mbalimbali za uongozi na kuhakikisha wanashiriki kikamimlifu katika shughuli za maendeleo inatekelezwa na kuzaa matunda.

RUDISHENI NG’OMBE ZA MAHARI-SIRRO

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka wazazi wote na walezi Mkoani Mara walioozesha watoto wadogo wakiwemo wanafunzi kurudisha ng’ombe walizopokea kama mahari vingenevyo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na watafungwa jela.

“baba wa Tanzania hauko juu ya sheria ukimpiga mkeo ni kosa la jinai ukimuozesha mwanao kabla ya umri ni kosa utashughulikiwa tu, lazima tufunge watu sasa hata kama wazazi wamekubaliana tutawagonga kwa mujibu wa sheria”amesema

Sirro ametoa agizo hilo Wilayani Bunda Mkoani mara wakati wa uzinduzi wa madawati ya jinsia Mkoani humo ambapo akiwa Bunda ametoa agizo kwa wazazi wote na walezi kuhakikisha wanawarudisha watoto wote waliowaozesha na warudishe mahari kama wanataka mali wazitafute kwa kufanyakazi na siyo kufanya watoto wa kike mtaji.

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi ameendeleza kauli mbiu yake ya polisi kutumia nguvu ya kadri kwa wanaume wote nchini wanaopiga wake zao ili kukomesha vitendo vya ukatili ambavyo amesema Mkoa wa Mara unaongoza kwa ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

“Bahati mbaya sana mimi ni IGP na natokea Mkoa huu sasa kuanzia sasa huu ukatili haukubaliki madawati haya ya jinsia yatafanyakazi saa ishirini na nne mwana mama ukipigwa muda wowote wewe nenda kituoni utapata huduma na huyo aliyekupiga atapata huduma anayostahili”ameongeza Sirro

Aidha amewaomba viongozi wa madhehebu ya dini wafanye kazi ya doria ya kiroho kwa waumini wao  ili waachane na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Mkuu wawilaya ya Bunda Bi Lidya Bupilipili akimkaribisha IGP wilayani hapa ameeleza kuwa mbali na ukatili kwa watoto lakini kuna changamoto ya wanafunzi wa kike kutumia uzazi wa mpango wakati bado wanasoma.

Amesema wazazi wamewekeza kwenye mambo ambayo hayana tija badala ya kuwekeza kwenye elimu ndiyo maana mmomonyoko wa maadili ni mkubwa.

“Sijawahi kushuhudia katika kesi nnazopokea ofisini kwangu baba amekatwa mapanga lakini kila siku ni wanawake tu na jambo la kusikitisha kuna baadhi ya viongozi wa vijiji hawalichukulii kwa uzito ukatili huu”amesema mkuu  wa wilaya

Mkurugenzi wa jukwaa la Utu wa Mtoto CDF bw Koshuma Mtengeti amewataka wana Mara kuacha vitendo vya unyanyapaa kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia na wasiogope kwenda kutoa ushahidi wanapohitajika.

Ameongeza kuwa kamati za ulinzi na usalama zinapaswa kuhakikisha sheria zinasimamiwa kikamilifu kuanzia ngazi ya chini.

Mwakilishi Mkaazi Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu (UNFPA) Jacqueline Mahon amesema madawati hayo yameanzishwa ili kuwarahisishia wahanga wa ukatili kupata haki zao.

“mtoto wa mwenzio ni wako, mlinde mwanamke wa yeyote ni mama yako muheshimu, mlinde, msichana yeyote ni sawa na binti yako au dada yako mlinde,muwezeshe atomize ndoto zake.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akikata utepe wakati wa uzinduzi wa jengo la ofisi ya dawati la jinsia wilayani Bunda Mkoani Mara, kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Bunda Lidya Bupilipili na kulia kwake ni mkurugenzi mtendaji wa jukwa la utu wa mtoto Koshuma Mtengeti na Mwakilishi Mkaazi Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu (UNFPA) bi Jacqueline Mahon

VIONGOZI WA DINI WASAINI MAAZIMIO YA MAPAMBANO DHIDI YA KIFUA KIKUU

0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongea viongozi wa dini (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa viongozi wa dini wa Taifa na wa kanda ya ziwa ambapo viongozi hao walitia saini maazimio ya mapambano dhidi ya kifua kikuu jijini Mwanza
Baadhi ya viongozi wa dini wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa mkutano huo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa OR-TAMISEMI Josephat Kandege kwenye mkutano wa viongozi wa dini katika vita dhidi ya Kifua Kikuu
Viongozi mbalimbali wa dini wakifuatilia mkutano huo ambao umefanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiongea wakati wa mkutano wa viongozi wa dini ambapo alisema wanayo imani na viongozi wa dini kwani wanawafikia wananchi wengi

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiongea na viongozi hao
Viongozi wa dini wakisaini maazimio ya kushiriki mapambano ya kutokomeza kifua kikuu.Mkutano huo umeandaliwa na Bunge kupitia mtandao wa wabunge wa kupambana na kifua kikuu

……………..
Na. Catherine Sungura, Mwanza

Serikali ya Tanzania inatenga mabilioni mengi katika kushughulikia masuala ya afya nchini hususani kwenye upande wa tiba ambapo gharama za matibabu zinakuwa kubwa sana.

Hayo yamesemwa leo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai wakati kusaini tamko la maazimio ya viongozi wa dini lililobeba ajenda ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) ,makazi na lishe bora nchini jijini hapa 

“Wananchi wanadhani kuwa wizara ya afya inasimamia tu tiba, hapana tusisahau kinga ni muhimu sana dhidi ya magonjwa nchini, tutakaposimamia kinga serikali itakua inaokoa gharama kubwa kwenye matibabu na pia kupunguza mzigo mkubwa wa kugharamia matibabu kama nchi”Alisisitiza Mhe. Ndugai

Aidha, amewashuru viongozi hao wa dini kwa ahadi pamoja na kusaini azimio la kusimamia na kusemea kwa waumini wao suala zima la TB hivyo anayo Imani watalibeba na kulitekeleza na kuwafanya wananchi wengi kupata uelewa juu ya ugonjwa huo na kujitokeza mapema kwenda kupima afya zao na hivyo kuanza dawa na kutoambukiza watu wengine.

Awali akiongea na viongozi hao Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Wizara yake inaendelea kubuni mikakati ya kutokomeza Tb nchini kama mikakati Madhubuti yaliyowekwa kwa mara ya kwanza na baraza kuu la umoja wa mataifa lililokutana Septemba mwaka 2018 na kuweka maazimio na malengo ya kuongeza kasi ya kutokomeza TB ifikapo mwaka 2030.

“Maambukizi mapya ya Tb nchini yamepungua kwa asilimia 18 kulinganisha na hali ya mwaka 2015 na hivyo kufanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi saba Duniani ambazo zipo katika mwelekeo sahihi wa kufikia malengo ya mpango mkakati wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ya kutokomeza TB kwa hatua ya kwanza ya mwaka 2020.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa vifo vitokanavyo na Tb peke yake vimepungua kutoka 30,000 mwaka 2015 hadi 22,000 mwaka 2018 na hii ni sawa na punguzo la asilimia 27,“licha ya mafanikio, nchi bado ina vifo vingi vinavyosababishwa na Tb ambapo kwa sasa takribani watu sitini hufariki kila siku hapa nchini”, alisema .

Hata hivyo Waziri huyo wa afya amesema kuwa hadi kufikia mwaka huu serikali ina vituo 103 vinavyotoa huduma za wagonjwa wenye Tb sugu ukilinganishwa na kituo kimoja mwaka 2015 pamoja na uboreshaji wa mifumo ya uchunguzi na ugunduzi wa TB kwenye vituo vya huduma za afya,upanuzi wa matumizi ya hadumini za kisasa za LED na kuongezeka kwa mashine za kisasa zinazopima vimelea vya TB kwa njia ya vina saba za GenXpert zipatazo 238 ambazo kwa sasa zinapatikana kwenye mikoa yote nchini.

Wauguzi wodi 3 JKCI Watoa Msaada wa Dawa kwa Wagonjwa Wasiokuwa na Uwezo

0
0
Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tulizo Shemu akiwaeleza wauguzi wa wodi namba tatu jinsi ya kuwahudumia wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo ili waweze kujikinga na maambukizi (infection) kwenye eneo ambalo limefanyiwa upasuaji (kidonda) wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akiwapongeza wauguzi wa wodi namba tatu kwa upendo waliokuwa nao kwa wagonjwa wanaowahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.
Msimamizi wa wodi namba ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Afisa Uuguzi Anastazia Moshi akieleza namna wauguzi wa wodi hiyo wanavyofanya kazi ya kuwahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika Taasisi hiyo.
Maafisa Uuguzi wa wodi namba wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Dkt. Tulizo Shemu na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi Robert Mallya wakimkabidhi dawa zilizotolewa na wauguzi wa wodi hiyo Mkuu wa kitengo cha Ustawi wa Jamii Asha Salum kwa ajili ya wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kulipia gharama za matibabu wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi Robert Mallya, Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Dkt. Tulizo Shemu na Mkuu wa kitengo cha Ustawi wa Jamii Asha Salum wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wakiwaongoza wauguzi wa wodi namba tatu kukata keki ikiwa ni ishara ya kuonesha upendo kati yao na wagonjwa wanaowahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.
Afisa Uuguzi wa wodi namba tatu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jumaa Omary akimlisha keki mgonjwa aliyelazwa katika wodi hiyo ikiwa ni ishara ya kuonesha upendo kwa wagonjwa wanaowahudumia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.
Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi wa Taasisi hiyo Robert Mallya (aliyevaa safari suti) mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuadhimisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi namba tatu.

Picha na: Genofeva Matemu – JKCI

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA MAMA MZAZI WA NAIBU WAZIRI MABULA

0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa pili kushoto) wakati wa mazishi ya mama yake mzazi Bi Cecilia Lubala baada ya kukamilika kwa mazishi katika kijiji cha Mnyengeja kata ya Sumve wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza jana. Wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Qween Mlozi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitoa heshima za mwisho kwa mama mzazi wa Naibu wake Dkt Angeline Mabula aliyefiwa na mama yake mzazi Bi Cecilia Lubala wakati wa kuaga mwili wa marehemu eneo la Ishungisha wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa kwanza kulia) pamoja na ndugu zake wakiweka shada la maua katika kaburi la mama yake mzazi bi Cecilia Lubala baada ya kukamilika kwa mazishi katika kijiji cha Mnyengeja kata ya Sumve wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza jana.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwa na viongozi wengine katika mazishi ya mama mzazi wa Naibu wake Dkt Angeline Mabula Bi Cecilia Lubala katika mazishi yaliyofanyika kijiji cha Mnyengeja wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza jana.

…………………

Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA

Mamia ya wananchi wa jiji la Mwanza na vitngoji vyake wamejitokeza kwa wingi kumzika mama mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula.

Mazishi ya Mama Mzazi wa Dkt Mabula Bi Cecilia Lubala yamefanyika jana kwenye makaburi ya familia yaliyopo kijiji cha Mnyengeja kata ya Sumve wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

Kabla ya mazishi hayo yaliyohudhuriwa pia na viongozi wa Chama na Serikali kulifanyika ibada maalum ya kumuombea marehemu Cecilia Lubala kwenye Kanika Katoliki Parokia ya Kirumba na baadaye shughuli ya kuaga mwili eneo la Ishungisha wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo William Lukuvi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kilagi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Herry Jemes, Katibu wa UWT Queen Mlozi, Mkuu wa mkoa wa Katavi Anthony Mtaka, Wakuu wa wilaya na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Marehemu Cecilia Lubala alifariki dunia jumamosi iliyopita tarehe 23 Novemba 2019 baada ya kuugua kwa muda mrefu na kulazwa kwa nyakati tofauti katika hospitali za Muhimbili, Dodoma na Bugando mkoani Mwanza ambako umaiti ulimkuta.

DK KALEMANI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI YA UMEME

0
0

Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imesema hadi kufikia Juni 31 mwaka 2021 kila kijiji nchini kitakua kimefikiwa na umeme hivyo kuwataka wakandarasi wote waliopewa tenda kuhakikisha wanamaliza ndani ya muda waliopangiwa.

Pia imewaonya wakandarasi wanaochelewesha miradi kwa visingizio mbalimbali kwa kuwachukulia hatua za kisheria, kimkataba na hatopewa kazi nyingine katika miradi inayofuata.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati, Mhe Medard Kalemani leo jijini Dodoma wakati alipokutana na wakandarasi wa miradi ya umeme vijijini REA na wauzaji wa vifaa nchini na kuwataka kuzingatia makubaliano waliyoingia na serikali pamoja na kufanya kazi kwa uadilifu.

Amesema kazi kubwa imefanywa na serikali katika kupeleka umeme vijijini ambapo mpaka sasa tayari vijiji 8115 vina umeme kati ya vijiji 12268.

" Kama wakandarasi wetu mkimaliza kazi kwa wakati kwa kuzingatia mikataba yetu basi kufikia Desemba mwaka huu tutakua tumewasha umeme kwenye vijiji 10446 na kubakia vijiji 1822 Nchi nzima hivyo kufikia Desemba tutakua tumewasha umeme kwa asilimia 80.

Rais wetu ana matarajio makubwa na sisi na ametuamini hivyo hivyo kwa watanzania wana imani kubwa na sisi, niwatake mzingatie mahitaji yetu kama Nchi na hasa tunapoijenga Tanzania ya viwanda mnapaswa kuelewa bila umeme hatuwezi kufanikisha hivyo nendeni mkamalize miradi kwa wakati," Amesema Dk Kalemani.

Amesema kuna viwanda vitano vya vifaa vinajengwa ambapo serikaki ikijiridisha navyo hadi kufikia Januari itasitisha uagizaji wa vifaa nje ya Nchi lengo likiwa kuwapunguzia wakandarasi gharama za uagizaji wa vifaa nje ya nchi, kuongeza mapato kwa serikali pamoja na kutoa Ajira kwa vijana.

Amewataka kutumia mkutano huo kufikia muafaka wa kutafuta njia ya kufikia malengo waliyojiwekea na kuwahakikishia kuwa serikali kupitia REA itawalipa wakandarasi fedha zao kwa wakati ili kuepuka visingizio vya kuchelewesha miradi.

Waziri Kalemani pia amewaonya watoa huduma kuacha kukwamisha miradi ya serikali kwa kuwacheleweshea vifaa wakandarasi na wakiendelea kufanya hivyo Sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.

" Rais wetu anafanya kazi kubwa kuwaletea maendeleo watanzania, tunamshukuru kwa kutupatia Bilioni 492 kwa ajili ya miradi hii, sasa ni jukumu letu kuhakikisha vijiji vyetu vyote vinawaka umeme, " Amesema Dk Kalemani.
 Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani akizungumza na wakandarasi wa umeme vijijini ambapo amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia makubaliano ya mkataba na serikali
 Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani akizungumza na wakandarasi na wauzaji wa vifaa vya umeme katika kikao cha pamoja leo jijini Dodoma.
 Mmoja wa wakandarasi kutoka mkoani Arusha, Michael Njarita akizungumza katika kikao cha wakandarasi na Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani leo jijini Dodoma
Wakandarasi wa umeme vijijini na wauzaji wa vifaa nchini ambao wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Mhe Dk Medard Kalemani leo jijini Dodoma katika kikao cha pamoja.

WAZIRI MHAGAMA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA UTEKELEZAJI YA MRADI WA UJENZI WA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI CHA KARANGA KILICHOPO KILIMANJARO

0
0
Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akipata maelezo kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga.
Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akitoa maelekezo kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga.
Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akimsikiliza Meneja wa Miradi kutoka PSSSF bw. Marco Kapinga wakati akitoa ufafanuzi
Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akipata ufafanuzi 
Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akipata ufafanuzi 
Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akisalimiana na Uongozi wa Kiwanda cha Karanga pamoja na uongozi wa PSSSF alipowasili kiwandani






Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akiongea kuhusu Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga, kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF bw. Hosea Kashimba


Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hosea Kashimba akifafanua jambo wakati wa kikao hicho


Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akisikiliza maelezo kutoka kwa Maneja wa Kiwanda hicho Bw. Masoud Omari


Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akisikiliza maelezo kutoka kwa Maneja wa Kiwanda hicho Bw. Masoud Omari


Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akiuliza swali kwa Maneja wa Kiwanda cha karanga Bw. Masoud Omari.

Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akizungumza kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga.

MATUMIZI YA POMBE YANACHANGIA ONGEZEKO LA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA- PROF PEMBE MUHAS

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Pamoja na faida zinazotajwa ndani yaa mwili matumizi ya Pombe yamekuwa yanachangia ongezeko la magonjwa yasiyo ya  kuambukiza kutokana na wingi wa matumizi hayo na kupelelekea kupata shinikizo la damu, kiria tumbo, kisukari na mengineyo.

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili (MUHAS) Prof Andreas Barnabas Pembe wakati wa bonanza la kuhamasisha wana taaluma kufanya mazoezi wakati wote pamoja na upimaji wa afya kwa watu mbalimbali.

"Matumizi ya pombe si salama kwa afya ya mtumiaji kwani mtu akiwa anafanya mazoezi huweka mwili wake vizuri, ukingalia mtu anayekunywa bia moja au glass ya wine ni sawa na kula mkate kipande kimoja na hivyo kupelekea kuleta kiriba tumbio kwa mtumiaji."

"tunaposema kiriba tumbo ni yale mafuta yaliyorundikana ndani ya mwili ambayo hayawezi kuchimwa kutokana na kazi zetu za kila siku, kwenye  miaka ya 70 wanaume walionekana wengi wana kiriba tumbo ila kwa miaka ya karibuni wanawake wamekuwa wengi sana,"

Prof Pembe amesema, kama MUHAS kimewataka wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuondokana na maradhi yasiyo yakuambukiza pamoja na kiriba tumbo.

Amesema kuwa mazoezi ni kitu muhimu sana kwani kumekuwa na ongezeko kubwa la wananchi wenye magonjwa yasiyoambukiza ambayo sio mazuri kwa afya na wingi wa matumizi ya vyakula ambayo havina faids ndani ya mwili.

Mbali na kufanya mazoezi, kupima presha pia wameweza kutoa ushauri elekezi kwa kufanya mazoezi ili kuyaepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza pia kutoa ushauri kwa wananchi kula chakula kulingana na kazi anayifanya mtu,"amesema

"Mtu anayefanya kazi ya kubeba mizigo mizito ni tofauti na yule anayekaa ofisini wanatakiwa na matumizi tofauti ya chakula kulingana na aina ya kazi anayofanya mhusika, na mara nyingi mtu anayetumia muda mwingi kukaa basi anatakiwa ale chakula kidogo,amesema Prof"

Mkurugenzi wa mfunzo endelevu na Weledi MUHAS Dkt Doreen Mloka amesema amefurahi sana kuwa moja ya washiriki wa mazoezi hayo ambapo amekiomba chuo hicho kuendelea kuandaa mabonanza kama haya mara kwa mara ili wajumuike pamoja kufanya mazoezi.

Amesema, hataishia hapa ataendelea kufanya mazoezi na kupungza kiribatumbo ambapo wameweza kupata elimu kuwa mazoezi ni afya na kwakua wanaanza mazoezi taratibu hadi pale watakapopata stamina.

Mwenyekiti kamati ya maandalizi wa bonanza hilo, Prof Kennedy Mwambeta  amesema toka mwaka 2013 hakujawai kuwa na bonanza kama hilo na miaka yote wamekuwa wanaanza yale yanayowahusisha wanafunzi hususani pindi chuo kinapofunguliwa na kufungwa, ila kwa sasa wamejifunza kuwa jambo hili ni muhimu na litakuwa ni endelevu.

Bonanza hilo walilolipa jina la michezo kwa afya MUHAS limewahussisha wanataaluma wa chuo hicho na kufanya mazoezi ya aina mbalimbali na kupima afya zao.Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili (MUHAS) Prof Andreas Barnabas Pembe  akizungumza na waandishi wa habari wakat wa bonanza la chuo hicho kwa wanataaluma wa MUHAS lililofanyika leo Jijini Dar es salaam.

 Picha ya pamoja ya wanataaluma wa MUHAS.

Mazoezi yakiendelea, wanataaluma wa MUHAS wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya kuweka afya nzuri.
  Huduma ya upimaji na kutoa ushauri nasaha kwa wanataaluma wa chuo cha MUHAS wakati wa Bonanza la chuo hicho  la kuhamasisha wana taaluma kufanya mazoezi wakati wote pamoja na upimaji wa afya kwa watu mbalimbali.




MADHEHEBU YA DINI YAMEISAIDIA SERIKALI KUPATA VIONGOZI WAZURI – WAZIRI MKUU

0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, wakati akifungua rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kufungua rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiingia msikitini, baada ya kufungua rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisikiliza mawaidha kwenye swala ya Ijumaa, baada ya kufungua rasmi, Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, wakati aliwasili kwenye Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, ambao ameufungua rasmi, Novemba 29, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, wakati aliwasili kwenye Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, ambao ameufungua rasmi, Novemba 29, 2019. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwakilishi wa Mufti wa Tanzania na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa na Sheikh Hamid Jongo, kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, kabla ya kuufungua rasmi, Novemba 29, 2019
Sheik Jongo, akizungumza na Waumini wa Kiislamu, kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Waumini wa Kiislamu, kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.
Waumini wa Kiislamu, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye ufunguzi wa Msikiti wa Haq Kionga, uliyopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. 
……………..

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema madhehebu ya dini yametoa mchango mkubwa katika kuwapata viongozi wa Serikali wanaofuata maadili mema na miiko ya uongozi.

Akizungumza wakati alipofungua Msikiti wa Haq – Kionga ulioko Magomeni, jijini Dar es Salaam leo mchana (Ijumaa, Novemba 29, 2019), Mheshimiwa Majaliwa amesema imedhihirika kwamba waumini wazuri wa dini mbalimbali wamebainika kuwa ni viongozi wazuri na waadilifu ndani ya Serikali.

Amewasihi viongozi wa dini waendelee kuwafundisha maadili mema waumini wao ili Taifa liendelee kuwa na raia wema ambao baadhi yao ndiyo watakakuwa viongozi katika ngazi mbalimbali hapo baadaye. 

“Nyumba za ibada ndiyo mahali sahihi panapojengwa maadili mema kwa watu wa rika zote, hivyo nawaomba Watanzania wawe waumini wazuri wa dini zao kwani kwa kufanya hivyo watakuwa pia ni raia wema,” amesema Mheshimiwa Majaliwa.

Amesema wazazi na walezi wanawajibika kuwarithisha watoto wao imani za dini vizuri kwani anaamini kwa kufanya hivyo watoto watajengewa misingi mizuri ya imani ya dini na maadili mema na watakapokuwa watu wazima watakuwa ni raia wema.

Mheshimiwa Majaliwa aliwasilisha mchango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli wa sh. milioni 10 na yeye pia alichangia sh. milioni tano ili zisaidie katika awamu ya pili ujenzi wa msikiti huo. 

Naye Sheikh Masoud Jongo ambaye alimwakilisha Sheikh Mkuu wa Tanzania katika ufunguzi wa msikiti huo, alisema uhuru mkubwa wa kuabudu uliopo nchini ndiyo sababu kubwa inayoifanya Tanzania iwe ni nchi ya amani na utulivu.

Sheikh Jongo amewaomba Watanzania wautumie vizuri uhuru mkubwa wa kuabudu uliopo nchini kwani ni nchi chache duniani zinazotoa uhuru mkubwa wa kuabudu kwa wananchi wake kama ilivyo hapa Tanzania.

Baadhi ya viongozi walioshiriki katika ufunguzi wa msikiti huo ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia na mbunge wa Kibaha Vijijini, Abuu Juma.

Dkt Bashiru aishauri serikali kuchunguza vyanzao vya fedha za vyama Vya Siasa vyote nchini

0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Bashiru. Bashiru Ally Kakurwa,ameishauri Serikali kuhakikisha inachunguza vyanzo vya fedha za Vyama Vya Siasa vyote nchini zitakazotumika katika uchaguzi mkuu ujao kama zinatokana na vyanzo halali vya fedha za vyama hivyo.

Alisema kuna vyama havina wanachama wala mradi ya kuwaingizia kipato lakini wakati wa uchaguzi vinatumia fedha nyingi bila ya kujulikana vyanzo vya upatikanaji wa fedha hizo.

Ushauri huo aliutoa katika mwendelezo wa ziara yake zanzibar katika Mkoa wa Kusini Kichama wakati akizungumza na Viongozi wa ngazi mbali mbali za CCM Mkoani humo.

Dkt.Bashiru,alisema Serikali ihakikishe Vyama vyote vya Siasa ikiwemo CCM vinatumia vyanzo halali vya fedha za uchaguzi mkuu ujao ili kuepuka matumizi ya fedha kutoka vyanzo haramu.

Alisema CCM inajipanga kutekeleza kwa vitendo sheria ya gharama za Uchaguzi kwa kuhakikisha inatumia fedha zake za ndani zilizotokana
na vyanzo halali vya fedha za ndani ya chama hicho.

Alieleza kuwa kuna baadhi ya vyama vya Siasa vimevikuwa na tabia zisizofaa za kupita kila kona wakiomba fedha za kufanya uchaguzi kutoka katika vyanzo haramu kwa lengo la kushindana na CCM.

"Chama Cha Mapinduzi kina wanachama wengi wanaolipa ada hivyo tunao uwezo wa kuendesha uchaguzi bila kutegemea fedha za misaada.

Lazima na vyama vya upinzani viweke wazi vyanzo vyao vya mapato kama tunavyofanya sisi bila kufanya hivyo tutakuwa na mashaka na upatikanaji wa fedha zao katika uchaguzi. "alisema Dkt.Bashiru.

Katika maelezo yake Dkt.Bashiru,alizielekeza kamati za siasa za Mikoa yote ya CCM Tanzania kuanza maandalizi ya kukusanya fedha za uchaguzi kutoka katika vyanzo vya fedha vinavyotambulika kutoka katika mikoa hiyo kwa ajili ya uchaguzi.

Aliwambia viongozi hao wa mikoa kuwa uchaguzi mkuu ujao CCM Makao Makuu haitotoa fedha za uchaguzi kila mkoa utajigharamia na CCM utakuwa na kazi kubwa ya kuratibu uchaguzi ufanyike kwa ufanisi.

Aliongeza kuwa mwaka 2020 CCM kwa mara ya kwanza itafanya uchaguzi wa gharama nafuu kwani hata katika uchaguzi wa Serikali za mitaa wa mwaka huu walitumia fedha zisizozidi shilingi Milioni 300 badala ya bilioni 8 zilizokuwa katika bajeti ya awali.

Katibu Mkuu huyo Dkt.Bashiru,akizungumza katika ziara hiyo alizitaka Kamati za Siasa za Mikoa zinazoandaa mapendekezo ya uteuzi wa wagombea Udiwani kuwasilisha katika Halmashauri za mikoa kwa ajili ya uteuzi wa wagombea katika kura za maoni kuepuka hilba na upendeleo kwa kuandaa mapendekezo ya wagombea wenye sifa na wanaokubalika kwa Wananchi.

Pia hata kwa Wabunge na Wawakilishi utaratibu wa kupatikana wagombea wa kupeperusha bendera ya CCM watapita katika mchujo na kuthiminiwa kwa kina ili wapatikane viongozi wenye sifa na uwezo unaokubalika kikatiba na wanaokwenda na kasi ya sasa CCM Mpya.

"Uchaguzi ujao ushindi wa kura za maoni hautokuwa kigezo cha kuwa kiongozi lazima tujiridhishe kwa sifa za kila mgombea kwa kuangalia rekodi yake kiutendaji na uchapakazi wake ndani na nje ya Chama",alisisitiza Dkt.Bashiru.

Kupitia Kikao hicho aliwapingeza Wabunge,Wawakilishi na Madiwani walioanza kujenga majengo ya chama na kununua vifaa mbali mbali kwa ajili ya chama kwani kufanya hivyo ni kuweka alama za kudumu za uongozi katika maeneo yao.

Sambamba na hayo Dkt.Bashiru, aliahidi kuwa CCM kwa kushirikiana na Serikali wataendelea kuandaa mazingira rafiki ya kuwaunganisha Vijana bila ya kujali tofauti zao za kisiasa kupitia sekta za michezo na sanaa ili waepuke dhambi ya kubaguana.

Aliwataka viongozi wa CCM kuwekeza kwa vijana kwa kuhakikisha wanawapatia malezi na makuzi bora ya kuwaeleza historia halisi ya Mapinduzi,Muungano na Uhuru wa Tanzania sambamba harakati za kujikomboa kutoka katika mikono ya ukoloni na usultani ili wapate ujasiri wa kulinda nchi.

SERIKALI YAKUSANYA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YA SH. BILIONI 183 - WAZIRI MKUU

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanikiwa kukusanya mikopo iliyoiva yenye thamani ya shilingi bilioni 183.3 sawa na asilimia 116.2 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 157.7. 

“Natambua kwamba baadhi ya wahitimu wamepata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, hivyo natumia  fursa hii kuwakumbusha wale wote mlionufaika na mkopo wa Serikali katika kutimiza ndoto zenu za kupata elimu ya juu, mkumbuke kurejesha mikopo,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Novemba 29, 2019) wakati akizungumza kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. 

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila anayenufaika na mkopo asaidie wengine walio nyuma yake ili nao waweze kufaidika na utaratibu huo wa kukopa na kulipa. Alisisitiza  kwamba bila kufanya hivyo, ni ukweli usiopingika kuwa Serikali itashindwa kuwajengea uwezo wananchi wake wa kupata fursa zinazojitokeza za elimu katika ngazi mbalimbali. 

“Ikumbukwe kuwa, maendeleo ya Taifa lolote yanategemea uwekezaji katika rasilimali watu. Hivyo nitoe rai kuwa wote mliokopeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu mfanye hima kulipa,”  alisema Majaliwa 


Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wahadhiri na wanachuo wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu vilivyopo Dar es Salaam wachangamkie fursa ya kupata nyumba na vyumba vya kupangisha katika miradi ya ujenzi wa nyumba ya NSSF, NHC na Watumishi Housing zilizopo Kigamboni.

Amesema amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF atenge maghorofa ambayo yatakaliwa na wahadhiri na wanafuzi wa vyuo vya elimu ya juu na vyuo vikuu tena waache kuwatoza bei kubwa na badala yake wapange bei mpya za kupangisha ambazo wanachuo watazimudu.


Ili kufanikisha utekelezaji  wa jambo hilo, Waziri Mkuu amesema amewashauri viongozi wa taasisi za elimu ya juu za mkoa wa Dar es Salaam wafanye mawasiliano  na Watendaji Wakuu wa NSSF, NHC na Watumishi Housing ili wafikie makubaliano ya namna ya kupangisha au kununua nyumba hizo.

Akizungumzia suala la kuboresha usafiri kwa wanafunzi na watu wakaoishi kwenye nyumba hizo, Mheshimiwa Majaliwa amesema tayari amekwishatoa maelekezo  kwa viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo Wakuu wa Wilaya za Kigamboni na Temeke wakutane na uongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) ili wapange safari za mabasi ya abiria kutoka Tuangoma, Mtoni Kijichi hadi eneo la Ferry Kigamboni.

Mheshimiwa Majaliwa amewasihi wahadhiri na wanachuo wachangamkie fursa hiyo ili waweze kupata nyumba bora za kupanga au kununua ili kuepuka adha ambayo imewakabili kwa muda mrefu ya kupanga au kuishi katika nyumba duni.

Akiwaasa wahitimu  wa Mahafali hayo, Mheshimiwa Majaliwa alisema: “Mnao wanao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa mnatumia vizuri elimu mliyoipata  chuoni ili kuchochea maendeleo ya kweli ya nchi yetu. Hivyo basi, huko mnakoenda iwe ni kwenye Halmashauri, Mikoa, Wizara, taasisi za umma na hata sekta binafsi, mkawe chachu ya mafanikio.”

“Aidha, mtakapokuwa huko kwenye maeneo mbalimbali ya kazi, hakikisheni mnajitanabaisha kwa  weledi na ufanisi wa hali ya juu. Tunawatarajia muwe mfano kwa kuwa waadilifu, waaminifu na wachapa kazi,” alisema Mheshimiwa Majaliwa.

Aliwasihi wahitimu hao kuwa watakapoingia kwenye utumishi wa umma au kwingineko wakazingatie maadili na kujiepusha na tabia ya kujitafutia utajiri wa harakaharaka. “Kafanyeni Kazi kwa uzalendo wa hali ya juu,” aliongeza Mheshimiwa Majaliwa. 

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza katika mahafali hayo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango alisema ili Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kiweze kuwa chachu ya mabadiliko makubwa ya kiuchumi yanayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, ni lazima uongozi wa chuo hicho utekeleze sera ya elimu kwa vitendo na kuwa wabunifu katika kupitia upya mitaala, ufundishaji na kufanya tafiti.

Waziri Mpango amelitaka Baraza la Uongozi wa Chuo cha IFM na wanataaluma waendelee kuwa wabunifu zaidi ili kuhakikisha kwamba fani zinazofundishwa Chuoni hapo zinaendana na wakati huku wakizingatia mahitaji ya nchi na wananchi wake pamoja na mabadiliko ya haraka ya kitekinolojia yanayoendelea ulimwenguni.

Jumla ya wahitimu 2,775 wametunukiwa tuzo mbalimbali na wanafunzi 20 wa Shahada ya Usimamizi wa Fedha wamepongezwa.

MUHIMBILI YAZINDUA ICU MBILI ZA WATOTO WACHANGA

0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof Charles Majinge akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa ICU mbili za watoto wanaohitaji uangalizi maalumu PICU na NICU. Kulia ni Mwakilishi wa Malkia wa Sharja, Dkt. Sawsan Abdul Salam Al Madhi akishiriki katika uzinduzi na Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini la Maisha (TLM), Bw. Gerald Mongella akishuhudia tukio hilo. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa MNH, Dkt. Ellen Senkoro naye akishudia tukio hilo leo. Mke wa Mfalme wa UAE, Shaikha Jawaher Bint Mohammed AlQasim amefadhili ujenzi wa wodi mbili za watoto chini ya siku 28 na kuanzia umri wa mwaka mmoja kuendelea kwa thamani ya shilingi bilioni 4.9.
Mojawapo ya ICU ya watoto wenye umri wa siku 29 hadi miaka 14 iliyozinduliwa leo.
Mwakilishi wa Malkia wa Sharja, Dkt. Sawsan Abdul Salam Al Madhi akizungumza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kabla ya kuzinduliwa kwa ICU mbili za watoto wanaohitaji uangalizi maalumu ya PICU na NICU. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa MNH, Dkt. Ellen Senkoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MNH, Prof. Charles Majinge akizungumza na wataalamu wa afya kabla ya uzinduzi wa wodi hizo. Kulia ni Mwakilishi wa Malkia wa Sharja, Dkt. Sawsan Abdul Salam Al Madhi na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa MNH, Dkt. Hedwiga Swai wakimsikiliza Prof. Majinge.

……………….

Tanzania ni nchi mojawapo duniani iliyofanikiwa kupunguza idadi ya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano kwa theluthi mbili na imesababisha kufikia mpango namba nne wa malengo ya millennia.



Mafanikio haya yamekuja baada ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Tumaini la Maisha (TLM) kujenga ICU mbili za watoto wanaohitaji huduma za uangalizi maalumu. Kutokana na juhudi hizo, Muhimbili imefanikiwa kupunguza vifo vya watoto waliokuwa wanahitaji uangalizi maalumu kutoka asilimia 70 ya vifo vilivyokuwa vikitokea ndani ya saa 24 na kufikia asilimia 30.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa MNH, Dkt. Hedwiga Swai kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru wakati wa uzinduzi wa ICU zinazowahudumia watoto wanaohitaji uangalizi maalumu chini ya umri wa siku 28 (Neonatal Intensive Care Unit) na watoto wenye umri wa kati ya mwezi mmoja hadi miaka 9 (Pediatric Intensive Care Unit) zenye dhamani ya shilingi bilioni 4.9 zilizojengwa kwa ufadhili wa Mke wa Mfalme wa UAE, Shaikha Jawaher Bint Mohammed AlQasim kupitia Shirika la Tumaini la Maisha (TLM).

“Hospitali ya Taifa Muhimbili ndiyo Hospitali kubwa kuliko hospitali zote nchini, idara ya watoto wenye umri siku 0 mpaka 28 kina vitanda (baby cots) 134 na umri wa siku 29 mpaka miaka 14 kina vitanda 294 na ndicho kitengo chenye vitanda vingi nchini. Kitengo hiki kinahudumia watoto wote wanaozaliwa Muhimbili na wanaoletwa kwa njia ya rufaa kutoka takribani hospitali zote za mikoa nchini,” amesema Prof. Museru.

Dkt. Swai amesema kwa kipindi kirefu watoto walikua hawana ICU maalumu kwa ajili yao hivyo kulazwa ICU ya kawaida ya watu wazima hali iliyosababisha watoto hao kukosa huduma muhimu.

“Uwepo wa ICU hizi maalumu kwa watoto utafanya watoto waweze kuonwa kwa ukaribu na madaktari na wauguzi waliobobea katika kutoa huduma stahiki kwa watoto tofauti na awali ambapo watoto walichanganywa kwenye ICU za watu wazima,” amesema Dkt. Swai.

Pia, amesema katika kuendelea kutekeleza maazimio ya mpango namba nne wa milenia wa kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano, Muhimbili imefanikiwa kuwa na muongozo wake wa kutoa huduma kwa watoto wachanga na watoto chini ya miaka 14 (PICU Guidelines). 

“Haya ni mafanikio makubwa sana kwani tumefanikiwa kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka asilimia 19.2 mwaka 2017/2018 mpaka asilimia 16.2 mwaka 2018/2019. Haya ni mafanikio makubwa kwetu katika kipindi cha mwaka mmoja,” amesema Dkt. Swai.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Charles Majinge ameshukuru Shirika la Tumaini la Maisha (TLM) na malkia wa Sharja kwa msaada huo, pia ameutaka uongozi wa Muhimbili kuhakikisha hizi ICU zinatunzwa ili watoto wote watakaopitia hapo waweze kunufaika na huduma za uangalizi maalumu.

WANA HABARI MTAKUWA VIBARUA MPAKA LINI- WAZIRI MWAKYEMBE

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe akizungumza na washiriki wa Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Mwakilishi wa UN Women Nchini, Bi. Hodan Addou akizungumza na washiriki wa Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Mwandishi wa Habari Mkongwe, Pili Mtambalike akichangia mada katika Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe, akikata utepe kuzindua kitabu cha Masuala ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye vyombo vya habari katika jukwaa la Waandishi wa habari wanawake, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe na Mwakilishi wa UN Women nchini, Bi. Hodan Addou, wakionyesha nakala ya kitabu cha Masuala ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye vyombo vya habari, kilichozinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Jukwa la Waandishi wa Habari Wanawake lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.

Mwakilishi wa UN Women nchini, Bi. Hodan Addou, akiandika anayoyasikia wakati wa Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.

……………………

Na Judith Mhina -Maelezo

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrisom Mwakyembe amezindua kitabu cha Gender and Media Handbook in Tanzania wakati wa maadhimisho ya miaka miwili ya Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano.

Akizindua kitabu hicho katika ukumbi wa Kibo ndani ya hoteli i ya Kimataifa ya Hyatt Regence – The Kilimanjaro leo Jijini Dar-es-salaam Waziri Dkt Mwakyembe amesema “Wana habari mtakuwa vibarua mpaka lini”.

Hebu tujaribu kutekeleza sheria mbili ya Habari na ile ya haki ya kupata taarifa, ambapo Tanzania ni kati ya nchi chache ambazo zimeiga kiila kitu kilichoandikwa kwenye sheria husika ya kimataifa, badala yake wanaleta mada yao pendwa ya jinsia moja, hatuwezi kukubali. Amesema Waziri Mwakyembe. 

Akijibu risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano- Tanzania Women Media and Public Relation Networ,. Bevin Bhoke Chacha Mwita ambaye amesema kuwa waandishi wa habari wanawalke wananyanyaswa kijinsia katika vyumba vya habari . Hii ikiwa ni pamoja na kutolipwa mshahara stahiki kulingana na sifa walizonazo, kutopandishwa madaraja, lugha chafu na kubaguliwa katika majukumu ya kazi kama waandishi wa kiume na kujikuta wengi wao wakiwa waadhirika wa kunyanyaswa kijinsia.

Waziri mwakyembe aliongeza kwa kusema “Tunaomba wahisani watenge nusu ya fedha wanazotoa ili kuangalia masilahi ya waandishi wa habari na kuboresha mazingira ya kazi kutokana na kuwa na vitendea kazi duni katika vyombo vyao vya Habari. 

Ninashangaa waandishi wa Habari ambao wanashangilia kuwa na taaluma isiyo na mpangilio, sheria wala kanuni, katika kuimarisha taaluma yao na ndio maana leo hii mnalalamika masilahi madogo yasiyolingana na kazi mnayofanya au hatopata mishahara kabisa .

Akisisitiza jambo hilo Waziri amesema “Ni agfadhali kuwa na vyombo vya Habari vichache vinavyojali na lulinda masilahi ya Waandishi wa Habari kuliko kuwa na vyombo vingi ambavyo , haviangalii masilahi ya waandishi wa Habari, kuwalipa mishahara stahiki kwa wakati .

Akitoa agizo kwa kukabiliana na suala la kupiga vita unyanyasaji kijinsia Waziri Mwakyembe amesema kuwa nimefurahi kwa kuwa mmeonyesha namba mbili maalum za simu ambazo yeyote atakayenyanyaswa kijinsia azipige ili kupata msaada. Aidha, Wizara yangu naiagiza kuwa na namba maalum ya simu ambayo mtanipigia mimi moja kwa moja na kuwatangaza wale wote wanaomnyanyasa wanahabari wanawake ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji kwenye vyumba vya habari.

Akisisitiza agizo hilo amesema dirisha la Waziri lipo wazi kwa kila mtu bila mashariti yeyote na naomba wanahabari walitumie kweli kweli, mimi nikiwa kama mzazi na kiongozi ni lazima kuhakikisha suala hili linakuwa historia. 

Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa wanahabari wanawake na maafisa uhusiano Bi Chacha ameongeza kwa kusema kuwa wanawake wana

Katika hizi siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika vyumba vya Habari Mshauri wa masuala ya wanawake wanahabari Bi Pili Mtambalike amesema “Wanahabari wanawake wananyanyaswa kijinsia ikiwa ni pamoja na kutengwa kwa kupewa kazi nyepesi ikilinganiswha na waandishi wa kiume katika vyombo vya habari kutokana na kutokujiamini 

Aidha , katika vyombo vingi vya Habari utafiti unaonyesha kuwa wahariri wengi ni wa jinsia ya kiume japo wapo wanawake ambao wanastahili kuwa wahariri na wanalingana hata kwa taaluma walizonazo ila hawapewi madaraka na hata hawapandishwi madaraja kama wenzao wa jinsia ya kiume.

Vilevile waandishi wanahabari wachanga wakike wananyanyaswa kingono na waliowengi wanafanya kazi kwenye vyombo hivyo kama correspondence na kulipwa kulingana na stori ambayo haiwatoshelezi kimaisha. Pia, Lugha wanazotumia wahariri katika vyumba vya habari ni lugha chafu za kudhalilisha na vitisho.

Akiongelea upande wa pili kama ushauri kwa wanahabari wachanga wanawake amesema kuwa ipo tabia ya wanahabari hawa wa kike wachanga kujiendekeza ili wapate wepesi wa kufanya kazi bila kuwa wabunifu kujituma na kuhakikisha wanajifunza kila mara ili kukomaa kitaaluma.

Pili Bi Mtambalike amesema kuwa ipo haja ya kuwa na sera ya jinsia katika vyombo vya Habari na kuhakikisha sera hizo zinatumika . Utafiti uliofanywa katika vyombo 23 vya Habari sita tu ndio vilikuwa na sera inayoeleweka ambayo haitumiki.

Hivyo tunaomba Jukwaa la Wahariri Tanzania –TEF liangalie namna gani linaweza kuleta usawa wa kijinsia katika kuwa na idadi sawa ya wahariri kwa kuwa wanawake walio wengi wanaishia katika ngazi ya Wahariri wasaidizi . Akitoa Takwimu amesema asilimia 26 ya wanawake ndio wahariri wasaidizi waliosalia wote ni jinsia ya kiume wakiwemo wahariri wakuu wa jinsia ya kiume.

Pia, unyanyasaji huu wa wanawake unafanyika hata kwenye upande wa vyanzo vya Habari ambavyo kwa wanawake ni asilimia 36 ,a silimia 64 ya vyanzo vya Habari hutokana na wanaume. Hivyo tunaomba hata wanawake wanahabari walione hili na kuhakikisha wanawahoji wanawake wenzao kama chanzo cha Habari badala ya kujikita zaidi kwa wanaume. Amesema Bi Mtambalike.

Naye Mhariri Mtendaji Bakatri Machumu ambaye hakuweza kufika katika hafla hiyo na kuwasilisha taarifa yake kupitia video iliyorekodiwa amesema kuwa kutokana na uzoefu wangu katika tasnia ya Habari waandishi wanawake ni wabunifu na wananafasi kubwa ya kuangalia wanawake ambao wako katika jamii na kusaidiana.

Naye Muwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bibi Hodan Addou amesema “ Vyombo vya Habari ni kati ya vyombo vyenye nguvu kubwa hivyo vitumike katika kuhakikisha vinaondoa kabisa suala zima la unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia katika vyomvo vya Habari”.

Pia, ameongeza kwa kusema kuwa ni lazima kuhakikisha wanahabari wanawake wanashiriki kikamilifu katika kuhakikisha wanatumia taaluma yao bila vikwazo ili kuwaletea maendeleo mtu momoj ammoja na Taifa kwa ujumla.

Akiongelea kauli mbiu ya mwaka katika maadhimisho ya miaka miwili ya Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano. Unaosema “Changamkia Fursa sasa” Grabbing Opportunity now Katibu wa Kamati Mtandao wa Wanahabari Wananawake Tanzania na Maafisa Uhusiano, Bi Leah Mushi amesema nafasi za mafunzo ambazo hutolewa na wadau mbalimbali wa sekta wa Habari wakiwemo Wanawake wa Umoja wa Mataifa, pamoja na Shirika la Mitandao ya Habari- Internews. 

Aidha, kuna fursa nyingi za mafunzo ya Mitandao ya kijamii na pia wanatoa vitendea kazi kwa waandishi wachanga wake kwa waume ili waweze kujitegemea katika kufanya kazi zao na kujiendeleza kitaaluma.

Naye Afisa Uhusiano wa Kituo cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bi Stela Vuzo, amesema kuwa huu ni wakati muafaka kwa wanahabari wachanga wanawake Tanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo kwa ajili ya kusimamia taaluma ya Habari na kujiendeleza, ikiwa ni pamoja na kupata kazi sehemu mbalimbali duniani na kuacha kulalamika kuhusu masilahi na mishahara midogo.

Haya tunayoyaona sasa inatokana na mfumo dume ambao tumeuishi kwa miongo kadhaa ambayo adhari zake zinajitokeza , hivyo sio kitu cha ajabu katika jamii zetu, na hayatokei kwenye tasnia ya Habari peke yake bali ni mfumo wa malezi kwenye jamii zetu ambao unatakiwa ukemewa, upigwe vita na uache kubagua mtoto wa kike na yule wa kiume. Amesema Mhariri Jesse Kwayu.

Iko haja ya Wadau wa Tasnia ya Habari kuongeza kwa pamoja na kuona umuhimu wa sheria , kanuni na taratibu tulizojiwekea ili kuifanya sekta ya Habari iwe na mfumo madhubuti unaowafaidisha wana taaluma ya Habari kwa jumla.

MKAWE MABALOZI WA UADILIFU NA UZALENDO - STEPHEN WASIRA

0
0

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WAHITIMU 3237 wametunukiwa Astashahada za awali, stashahada na shahada mbalimbali katika mahafali ya kumi na nne  ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, huku wanawake wakichukua asilimia 50 ya wahitimu wote na wanaume wakichukua asilimia 46 pekee ya wahitimu wote.

Akizungumza katika mahafali hayo Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa bodi ya Chuo hicho Stephen Wasira amewataka wanafunzi hao kuwa mabalozi bora wa uzalendo na uadilifu katika jamii na kueleza kuwa Chuo hicho ni tunu na hazina kubwa nchini hivyo ni vyema wahitimu hao wakajitofautisha kwa kuweka mbele maadili uzalendo.

Wasira amesema, Tangu Chuo hicho kianzishwe mwaka 1961 viongozi na wengi kutoka taasisi za umma na binafsi wamepitia mafunzo kutoka katika Chuo hicho, na amezishauri taasisi  kuendelea kupata maarifa katika Chuo hicho.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho  Profesa.Shadrack Mwakalila amesema kuwa chuo hicho kinaendeleza dira ya kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kutoa maarifa bora na elimu kuhusiana na ubunifu na uvumbuzi pamoja na kuendeleza amani na umoja wa kitaifa.

Prof. Mwakalila amesema wanatumai kuwa wanafunzi hao ambao idadi ya wanawake ni 1735 na wanaume 1502 watakuwa mstari wa mbele kwa kuwa wazalendo na kuwa na maadili yatakayoigwa na watanzania.

Amesema kuwa Chuo kimejipanga kuwa kitovu cha mafunzo ya uongozi na maadili na tayari wameanza na mkakati wa kuendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi ya uongozi, maadili na utawala bora kwa sekta za Umma na binafsi kwa ngazi zote kuanzia Kijiji, Wilaya na Kata.

Prof. Mwakalila amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho mwaka 1961 bado kinandelea kutoa mafunzo kwa viongozi chipukizi ili wawe wazalendo na wenye maadili hapo baadaye.

Akizungumza malengo ya chuo hicho kwa sasa Prof. Mwakalila amesema kuwa wapo katika mchakato wa kuboresha mazingira ya kujifunza na kujifunzia, kuongeza maktaba pamoja na kuongeza udahili kwa wanafunzi.

Aidha ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na chuo hicho na amewasihi wahitimu hao kutumia vyema maarifa waliyoyapata na kuwa wazalendo wa mfano katika jamii zao.
 Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Stephen Wasira(kushoto) katika maandamano ya kitaaluma wakati wa mahafali ya kumi na nne ya Chuo hicho kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Shadrack Mwakalila leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Stephen Wasira akikiwa na viongozi wa Chuo wakati wa mahafali ya kumi na nne ya Chuo hicho, leo jijini Dar es Salaam.

TCRA yaongeza muda wa usajili kwa Wananchi wa Makambako hadi Desemba Sita

0
0

Kufuatia na kujitokeza kwa wingi kwa wakazi wa Makambako na viunga vyake vya jirani katika zoezi la kupata namba za vitambulisho vya taifa na kusajili simu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kushirikiana na Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA na watoa huduma wote wa makampuni ya simu wameongeza muda wa zoezi hilo  ambapo  sasa zoezi hilo utafanyika kwa wiki  nzima kuanzia Desemba  2 hadi 6  2019

 Akizungumzia  maendeleo ya zoezi hilo linaloratibiwa na TCRA mkuu wa kanda ya Nyanda za juu Kusini Mhandisi Asajile John amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaopata huduma za msingi kwa urahisi hivyo kuongeza huko kwa siku kunalenga kutekeleza  malengo hayo.

Amesema huo ni muendelezo wa kampeni ya "Mnada kwa Mnada, Karibu tukuhudumie" iliyoanzishwa na kuratibiwa na TCRA na kushirikisha wadau wengine  inayolenga kutoa elimu ya utumiaji bora na salama wa huduma za mawasiliano  na kuhamasisha usajili wa laini kwa kutumia namba za vitambulisho vya taifa.
 Afisa uhamiaji akihudumia Mwananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika Mji mdogo wa Makambako.
 Kampuni za simu wakisajili  Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako laini za simu kwa alama za vidole.
Wananchi wakipata huduma ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Mji Mdogo wa Makambako.

TUME YA USHINDANI TANZANIA (FCC) NA WADAU WAKE KUADHIMISHA WIKI YA USHINDANI DESEMBA 3 HADI 5

0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

TUME ya Ushindani Tanzania (FCC) kwa kushirikiana na Mamlaka za EWURA, LATRA, PURA, FCT, TCAA, TCRA na TASAC wataadhimisha maadhimisho ya siku ya ushindani Duniani ambayo huadhimishwa Novemba 5 kila mwaka na mwaka huu itaenda sambamba  na kongamano litakalowakutanisha wadau na wananchi kwa malengo ya kuwajengea uwezo na ufahamu zaidi kuhusiana na maadhimisho hayo pamoja na shughuli zinazofanywa na Mamlaka hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa bodi ya ushindani nchini (FCC), Profesa. Humphrey Moshi amesema Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya ushindani tangu mwaka 2015 na kwa mwaka huu maadhimisho hayo yamekuja na kauli mbiu inayoendana na masuala ya kiushindani yanayojitokeza kote Duniani ya " Kuhakikisha Ushindani Madhubuti katika Ukuaji wa Dunia ya Kimtandao."

Amesema kuwa kilele cha maadhimisho hayo yatakayofanyika Desemba 5 na Waziri mwenye dhamana ya Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa atakuwa mgeni wa heshima.

Prof. Moshi amesema kuwa mitandao imekuwa ikikuza biashara kama ikitumiwa vizuri, "Biashara mtandao ni ile inayohusisha mabadilishano ya taarifa kupitia mtandao wa kompyuta, kimsingi ni jambo zuri kwa kuwa tafiti zinaonesha kuna masoko ya kutangaza bidhaa kwa urahisi hata kwa kuvuka mipaka ukilinganisha miaka iliyopita" ameeleza .

Vilevile amesema kuwa lazima jamii itambue fursa za masoko ya mtandao licha ya kuwepo na baadhi ya changamoto,lakini tume hiyo itaendelea kuhakikisha inawezesha masoko na kuwasiliana kwa urahisi, na hiyo ni pamoja na kuimarisha mifumo na uwezo wa biashara.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani nchini Godfrey Machimu amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatahusisha maonesho mbalimbali kutoka kwa wadau pamoja na kupata fursa ya kujua utendaji kazi wa Mamlaka hizo.

Machimu amesema kuwa Tume ya Ushindani kupitia maadhimisho hayo wanaamini italeta chachu katika kutatua changamoto za biashara mtandao zinazowakabili wananchi kote nchini.

Siku ya Ushindani Duniani imekuwa ikiadhimishwa na Mamlaka za ushindani Duniani kote kuanzia Mwaka 1980, wakati wa Umoja wa Mataifa uliporidhia na kukubaliana na kanuni za kuzuia mienendo potofu ya biashara.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Godfrey Machimu akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani),leo jijini Dar akieleza kuhusu tume hiyo   ikishirikiana na Mamlaka za EWURA, LATRA, PURA, FCT, TCAA, TCRA na TASAC wataadhimisha maadhimisho ya siku ya ushindani Duniani ambayo huadhimishwa Novemba 5 kila mwaka,ambapo mwaka huu itaenda sambamba na kongamano litakalowakutanisha wadau na wananchi kwa malengo ya kuwajengea uwezo na ufahamu zaidi kuhusiana na maadhimisho hayo pamoja na shughuli zinazofanywa na Mamlaka hizo.

 Mkurugenzi wa Utafiti na Muungano wa Makampuni na Urabishi Dkt. Allan Syril Mlulla akifafanua zaidi mbele ya Waandishi wa habari  namna maadhimisho hayo adhimu kwa Wadau yatakavyofanyika sambamba na kutoa elimu na kueleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Tume hiyo.
Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani Prof. Humphrey Moshi akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar, kuhusu namna Tanzania ilivyojiandaa kuadhimisha siku hiyo,amesema Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya ushindani tangu mwaka 2015 ,lakini kwa mwaka huu maadhimisho hayo yamekuja na kauli mbiu inayoendana na masuala ya kiushindani yanayojitokeza kote Duniani ya " Kuhakikisha Ushindani Madhubuti katika Ukuaji wa Dunia ya Kimtandao."
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo. Picha na Michuzi JR.

TAWI LA CHUO KIKUU WAPATA VIONGOZI WA TAWI WAPYA

0
0
Viongozi wa Serika ya Mtaa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wameapishwa leo Novemba 29,2019 katika ukumbi wa Urafiki Social Hall Ubungo,na kuahidi kufanya mabadiliko makubwa ya kimaendeleo katika mtaa wao ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuri,   inayotaka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kufikia maendeleo ya uchumi wa kati. 

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa mtaa huo Dkt. Jonas Benedict Tiboroha mara baada ya kuapishwa.

Amesema kazi ya kuwatumikia wananchi wa tawi lake imeishaanza hivyo basi wategemee mabadiliko pamoja na maendeleo. Anawaomba ushirikiano kwani kupitia ushirikiano utaleta chachu ya maendeleo.
Pichani ni Uongozi mpya wa Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwenyekiti Dr. Jonas Tiboroha ( wa nne kutoka kushoto) pamoja na wajumbe wake.

TCRA yaongeza muda wa usajili kwa Wananchi wa Makambako hadi Desemba Sita.

0
0
Afisa uhamiaji akihudumia Mwananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika Mji mdogo wa Makambako.
Kampuni za simu wakisajili Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako laini za simu kwa alama za vidole.
Wananchi wakipata huduma ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Mji Mdogo wa Makambako.

*************************************

Kufuatia na kujitokeza kwa wingi kwa wakazi wa Makambako na viunga vyake vya jirani katika zoezi la kupata namba za vitambulisho vya taifa na kusajili simu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kushirikiana na Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA na watoa huduma wote wa makampuni ya simu wameongeza muda wa zoezi hilo ambapo sasa zoezi hilo utafanyika kwa wiki nzima kuanzia Desemba 2 hadi 6 2019.

Akizungumzia maendeleo ya zoezi hilo linaloratibiwa na TCRA mkuu wa kanda ya Nyanda za juu Kusini Mhandisi Asajile John amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaopata huduma za msingi kwa urahisi hivyo kuongeza huko kwa siku kunalenga kutekeleza malengo hayo.

Amesema huo ni muendelezo wa kampeni ya “Mnada kwa Mnada, Karibu tukuhudumie” iliyoanzishwa na kuratibiwa na TCRA na kushirikisha wadau wengine inayolenga kutoa elimu ya utumiaji bora na salama wa huduma za mawasiliano na kuhamasisha usajili wa laini kwa kutumia namba za vitambulisho vya taifa.
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live




Latest Images