Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110105 articles
Browse latest View live

Uyui Yajivunia Mafanikio Miaka 4 ya Serikali ya Awamu ya Tano

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe. Gift Msuya akisisitiza kuhusu mikakati yake ya kuhakikisha wanafikia maendeleo endelevu kupitia miradi inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi.


Na mwandishi Wetu

Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kuleta mageuzi katika sekta ya Afya, Maji, Elimu na sekta nyingine zinazolenga kuwainua wananchi kiuchumi katika Wilaya ya Uyui, Mkoani Tabora.

Akizungumza katika mahojiano maalum kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka 4 ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Gift Msuya amesema kuwa moja ya miradi hiyo ni ujenzi wa Hospitali ya wilaya uliogharimu shilingi bilioni 1.6 na ujenzi umefikia asilimia 95 na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Novemba, 2019.

“ Ujenzi wa Hospitali ya wilaya umeenda sambamba na kujengwa kwa Vituo vya Afya kama kile cha Upuge kilichogharimu shilingi milioni 500,000 na kimekamilika na kuanza kutoa huduma tayari wagonjwa 62 wamefanyiwa upasuaji katika kituo hiki,” alisisitiza Msuya

Akifafanua amesema kuwa kiasi cha shilingi milioni 400 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Igalula na ujenzi umefikia asilimia 95 na kinaratajia kukamilika hivi karibuni ili kiweze kuanza kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Katika sekta ya Elimu, wilaya hiyo imefanikiwa kujenga Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Ubora wa Elimu Uyui iliyogharimu milioni 130 na imekamilika kwa asilimia 100 hali itakayochangia kukuza kiwango cha elimu wilayani humo.

Miradi mingine ni ile ya maji ambayo imegharimu zaidi ya bilioni 3 zizilotolewa ili kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo kwa lengo la kuwezesha wananchi kupata huduma bora zaidi ya maji safi na salama.

Ujenzi wa madarasa ya EQUIP na lipa kadiri ya matokeo (EP4R) umegharimu zaidi ya bilioni 1.5 na kumewezesha kupungua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika wilaya hiyo.

Akizungumzia miradi iliyotekelezwa kwa kushirikiana na wadau katika sekta za Afya na Maji, Mhe. Msuya amesema kuwa imegharimu takriban bilioni 1.1 na hivyo kutoa mchango katika kuleta ustawi wa wananchi.

Wilaya ya Uyui mkoani Tabora ni moja ya wilaya zilizopiga hatua katika kukuza sekta ya Kilimo ili kuwainua wananchi kiuchumi na kujenga uchumi jumuishi.

MIRADI YA JAMII YA MAJITAKA INAVYOSAIDIA KUPUNGUZA MAGONJWA YA MLIPUKO

$
0
0
Meneja Miradi ya Jamii (usafi wa mazingira) Bw Charles Makoye  akitoa maelezo kwa Maafisa Afya wa Manispaa za Jiji la Dar es Salaam walipotembelea  Miradi ya Jamii ya  Majitaka katika eneo la Vingunguti na Toangoma wilayani Temeke.Miradi hii imesaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko na kujenga ustawi wa maisha ya wakazi wa maeneo tajwa.
Eneo la majitaka 

WANANCHI BUTIAMA WAHOFIA MADAWATI YA JINSIA KUVUNJA NDOA

$
0
0

Mwandishi wetu Butiama Mara

Baadhi ya wakazi wa Butiama Mkoani Mara wameiomba  serikali kuongeza nguvu katika kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ili kutokomeza tatizo hilo ambalo limeonekana kuwa sugu Mkoani Mara huku baadhi ya wanaume wakidai ufunguzi wa madawati hayo yatavunja ndoa kwani baadhi ya wanawake watakuwa jeuri.

Wametoa ombi hilo wilayani Butiama baada ya Mkuu wa jeshi la polisi (IGP) Simon Sirro kufungua ofisi ya dawati la jinsia ambapo kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema licha ya madawati ya jinsia kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ukatili lakini pia wanawake wamekuwa wajeuri kwa kuwa wanajua wataenda kushitaki

Akizungumza na wananchi hao Mkuu huyo wa jeshi la Polisi amesema mfumo dume bado unasumbua wanaume wa Mkoa wa Mara na kwamba jeshi la polisi haliwezi kuvumilia mambo yaliyopitwa na wakati lazima washugulikiwe kwa nguvu zote.

"Salamu zangu kwa wanaume ubabe haulipi wakati Rais Magufuli akiniteua alikuwa na maana yake huwa nikisema jambo sitanii sasa wewe baba jaribu uone"amesema Sirro

Aidha amesema ng'ombe hana nafasi ya kuruhusu ulatili kwa mwanamke eti kwa sababu alitolewa mahari ya ng'ombe na kwamba ndiyo maana madawati yameanzishwa nchi nzima kulinda haki za wanawake na watoto lakini pia amewataka wanawake wasizidi wakasababisha balaa.

"Kina mama lindeni watoto wenu wazazi wangu wasingenilinda leo nisingekuwa IGP hujui mtoto wako atakuwa nani baadae na nyie wababa msiwarubuni watoto wadogo nendeni kwa wakubwa wenu wamejaa tele na nyie watoto wa kike msilubali kurubuniwa na vitu vidogo vikaharibu ndoto yako ukiona kuna viahashiria vya mtu mzima kukurubuni au kukutaka kimapenzi nenda kwenye dawati"alisema IGP Sirro

Naye Mkurugenzi wa  jukwaa la utu wa mtoto Koshuma Mtengeti amesema kutokomeza ukatili wa jinsia kutaleta maendeleo kwani wanawake watajishughulisha kikamilifu kujenga uchumi na kuwa uzinduzi wa dawati hilo utatoa chachu kukusanya rasilimali na kuweka nguvu pamoja kutokomeza ukatili.

"Tunapata faraja sana kuona IGP anaongoza mapambano kutokomeza ukatili nnamini tutashinda cha msingi wananchi tutoe ushahidi pale ambapo unahitajika hili ni janga letu sote" amesema Mtengeti

Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu UNFPA Jackqueline Mahon amesema lengo ni ifikapo mwaka 2030 vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia viwe vimetokomezwa.

Pia ameipongeza serikali ya Tanzania na jeshi la polisi kwa jitihada kubwa inayofanya kuhakikisha vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto vinatokomezwa. 
 Mkuu wa jeshi la polisi (IGP) Simon Sirro akifungua ofisi ya dawati la jinsia na Watoto Butiama mkoani Mara,huku wadau mbalimbali wakijitokeza kushiriki tukio hilo.

Picha ya pamoja

HIFADHI MBILI ZA TAIFA ZAZINDULIWA MKOANI KAGERA

$
0
0
Abdullatif  Yunus wa Michuzi TV.

Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe ni Hifadhi mbili nyingine zilizozinduliwa rasmi mnamo Novemba 28, Mwaka huu, na hivyo kufanya  idadi ya Hifadhi za Taifa  kufikia 22 mpaka sasa.

Tukio hilo kubwa na la kihistoria katika sekta ya Utalii, limefanyika katika Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera Chini ya Waziri mwenye dhamana Dkt. Hamisi Kigwangala (MB), huku likihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo  wajumbe Wa kamati ya Bunge ya Uwekezaji, Maafisa wa Shirika la TANAPA, Katibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adoloph Mkenda, Viongozi wengine wa Chama, Dini na Serikali pamoja na wananchi.
Katika kuhakikisha Utalii unazidi kuimarishwa Mkoani Kagera hususani katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa,

Waziri  wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala amesema suala la kulinda Hifadhi pamoja na wanyama wake ni jukumu la kila mwanchi anaepatikana katika eneo husika, hivyo wananchi pamoja na Taasisi husika hawana budi kuendelea kuweka miundo mbinu wezeshi pamoja na kuweka vivutio vingine kwa watalii ili kuwanfanya waendelee kufika katika Hifadhi hizo.

Aidha Waziri Kigwangala ameelekeza kujengwa kwa kituo cha utamaduni chenye vyumba walau kumi kwa kuanzia, kituo ambacho amewaelekeza TANAPA kukijenga kati ya Omugakorongo hadi Murongo, ili kusaidia kurahisisha safari ya Watalii kujifunza na kujionea mambo mengine ya kiutamaduni, wanapokuwa safarini kuelekea katika Hifadhi za Ibanda na Rumanyika, na kwa kufanya hivyo Itamsaidia pia mwananchi mmoja mmoja kunufaika na uwepo wa Hifadhi katika maeneo yao.

Kwa upande wake Msimamizi wa Hifadhi hizo Bwana Allen Kijazi amesema pamoja na changamoto baadhi wanazokabiliana nazo kama TANAPA, pia wapo na mpango wa kukarabati uwanja wa Ndege uliokuwa zamani ukitumiwa na Wakimbizi, na kusema kuwa baada ya kukamilika kwa Uwanja huo unaopatika Wilayani Kyerwa, utarahisisha huduma ya Usafiri wa anga kwa watalii na wawekezaji, licha ya kuwa tayari wameanza pia uchongaji wa barabara zinazoingia na kutoka hifadhini.

Mwenyeji katika Shughuli hiyo ya uzinduzi wa Hifadhi za Taifa, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Ndg. Rashid Mwaimu amesisitiza zaidi juu ya kuendelea kutunza kulinda na kuhifadhi rasilimali zote za Wilayani Kyerwa, Hifadhi ya Ibanda ikiwa ni mojawapo na huku akitangaza vita dhidi ya majangili wanaofikiria kuhujumu Hifadhi na rasilimali nyinginezo kwa namna yoyote
Pichani ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala (MB), akiwa amesimama katika jukwaa maalumu kabla kupokea heshima, kabla ya ukaguzi wa gwaride katika onesho lilifonywa na Jeshi USU, katika Uzinduzi wa Hifadhi za Taifa za Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe.
 Pichani Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Ndg. Rashid Mwaimu akitoa salaam zake kwa Wananchi na Viongozi (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Hifadhi za Taifa za Ibanda na Rumanyika..
 
 Pichani ni Gwaride kutoka Jeshi USU likiendelea kunogesha Uzinduzi wa Hifadhi za Ibanda na Rumanyika katika Shughuli ya Uzinduzi rasmi wa Hifadhi hizo uliofanyika Wilayani Kyerwa.
 Pichani ni Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi, Viongozi, pamoja na baadhi ya  Watumishi wa TANAPA wakati wa Uzinduzi wa Hifadhi za Taifa za Ibanda na Rumanyika.
Pichani ni sehemu ya Burudani kutoka TANAPA BAND ikiendelea kuburudisha katika uzinduzi wa Hifadhi za Taifa za Ibanda na Rumanyika.

MTANZANIA ASHINDA TUZO YA LEGACY JIJINI LONDON

$
0
0
Kijana Mtanzania Erick Venant, amepokea tuzo ya Legacy jijini London,Tuzo hiyo imetolewa Novemba 26/2019, wa Kutambua mchango wake katika kupambana na tatizo la usugu wa vimelea dhidi ya dawa (Antimicrobial resistance)na haswa kuongeza uelewa kwenye Jamii na kutia hamasa ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya tatizo hili, juhudi zake zinatajwa kuwa muhimu katika kuboresha afya ya ulimwengu*.

Akiwa Uingereza Erick amepata nafasi ya kukutana na Prince William katika makazi ya Kifalme, Kengstone palace ambapo walijadili kwa ufupi kuhusu tatizo la usugu wa vimelea dhidi ya dawa.

 Magazeti ya Uingereza yameripoti jinsi Prince William alivyotumia lugha ya Kiswahili mara kadhaa wakati wa mazungumzo hayo.Erick ni miongoni mwa vijana 20 duniani waliochaguliwa kupokea tuzo ya Legacy waandaji wa tuzo hiyo "The Diana award" wanasema vijana wote waliochaguliwa wana mchango mkubwa kwenye jamii.

Washindi wengine wametoka mataifa ya Uingereza, Malaysia, India,Canada, Nigeria na Nepal.Mshauri mwandamizi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Elizabeth Nyamayaro na mtendaji mkuu wa Shirika la ndege la Uingereza Alex Cruz ni miongoni mwa waliounda jopo la majaji 14 waliokutana kuchagua washindi 20 wa tuzo hii kutoka miongoni mwa washindi wa tuzo ya Diana award wa mwaka 2018 na 2019.

Sherehe za Utoaji wa tuzo zilifanyika katika ukumbi wa Old Royal Naval College,Greenwich-London na kuhudhuriwa na kaka mkubwa wa Princess Diana, Earl Spencer.Tuzo hii hufanyika kila baada ya miaka miwili.Tuzo za Diana award na Legacy award hutolewa kama kumbukumbu ya Princess Diana wa Wales aliyefariki mwaka 1997.Watu laki saba hufariki kila mwaka duniani kote kutokana na tatizo hilo.
 Kijana Erick Venant akiwa na tuzo yake  ya Legacy jijini London.
Kijana Mtanzania Erick Venant, akipongezwa na Prince William baada ya kukaribishwa kwenye makazi ya kifalme,Kingstone Palace kwa kupokea  tuzo ya Legacy jijini London.Tuzo hiyo imetolewa  Novemba 26,2019.
 Muonekano wa tuzo yenyewe.
 Picha ya pamoja na Wadau

KIJANA MTANZANIA APOKEA TUZO YA LEGACY NCHINI UINGEREZA, PRINCE WILLIAM AMMIMINIA SIFA LUKUKI

$
0
0

Na Ripota Wetu,Michuzi TV

KIJANA Mtanzania Erick Venant amepokea tuzo ya Legacy jijini London,ikiwa ni ya kutambua mchango wake katika kupambana na tatizo la usugu wa vimelea dhidi ya dawa(Antimicrobial resistance) na hasa kuongeza uelewa kwenye jamii na kutia hamasa ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya tatizo hilo.

Erick amepokea tuzo hiyo  Novemba 26 mwaka 2019, ambapo juhudi zake zinapaswa kuwa muhimu katika kuboresha afya ya ulimwengu. Akiwa Uingereza Erick amepata nafasi ya kukutana na Prince William katika makazi ya Kifalme, Kengstone palace ambapo walijadili kwa ufupi kuhusu tatizo la usugu wa vimelea dhidi ya dawa.

Kwa mujibu ya magazeti ya nchini Uingereza yameripoti jinsi Prince William alivyotumia lugha ya Kiswahili mara kadhaa wakati wa mazungumzo hayo.Erick ni miongoni mwa vijana 20 duniani waliochaguliwa kupokea tuzo ya Legacy waandaji wa tuzo hiyo "The Diana award" na kwamba inaelwzwa kwamba vijana wote waliochaguliwa wana mchango mkubwa kwenye jamii.

Washindi wengine wametoka mataifa ya Uingereza, Malaysia, India,Canada, Nigeria na Nepal.Mshauri mwandamizi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Elizabeth Nyamayaro na mtendaji mkuu wa Shirika la ndege la Uingereza Alex Cruz ni miongoni mwa waliounda jopo la majaji 14 waliokutana kuchagua washindi 20 wa tuzo hii kutoka miongoni mwa washindi wa tuzo ya Diana award wa mwaka 2018 na 2019.

Sherehe za Utoaji wa tuzo zilifanyika katika ukumbi wa Old Royal Naval College,Greenwich-London na kuhudhuriwa na kaka mkubwa wa Princess Diana, Earl Spencer.Tuzo hii hufanyika kila baada ya miaka miwili.Tuzo za Diana award na Legacy award hutolewa kama kumbukumbu ya Princess Diana wa Wales aliyefariki mwaka 1997.Watu laki saba hufariki kila mwaka duniani kote kutokana na tatizo hilo.
 Kijana Erick Venant akiwa na tuzo yake  ya Legacy jijini London,chini Uingereza.
Kijana Mtanzania Erick Venant, akipongezwa na Prince William baada ya kukaribishwa kwenye makazi ya kifalme,Kingstone Palace kwa kupokea  tuzo ya Legacy jijini London,chini Uingereza.Tuzo hiyo imetolewa  Novemba 26,2019.
 Muonekano wa tuzo yenyewe.
 Picha ya pamoja na Wadau

Lift chanzo cha ukatili wa kingono

$
0
0
UMBALI mrefu na tatizo la usafiri ni mojawapo ya mambo yanayoelezwa kuchangia kuendeleza ukatili wa kingono kwa wanawake na wanafunzi nchini.

Hali hiyo inatajwa kuwa mbinu rahisi kwa madereva wa bodaboda na magari wakiwamo utingo kutumia kama mtego wa kuwanasa watoto wa shule za msingi na sekondari ambao husafiri umbali mrefu kuisaka elimu.

Akizungumza katika mafunzo yaliyoandaliwa na Asasi ya Wanawake Katika Jitihada za Maendeleo (WAJIKI) kwa ufadhili wa Women Fund Tanzania ya kuwajengea uwezo madereva na kuwa mabalozi katika kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia nchini ambayo imeanza Novemba 25 hadi Desemba 10 mwaka huu, Katibu wa Umoja wa  Madereva wa Daladala Mbagala (UMDM), Albert Shoo anasema wanawake na wanafunzi wamekuwa waathirika wakubwa kutokana na shida ya usafiri katika mkoa wa Dar es Salaam

“ Mimi naendesha daladala ruti za Mbagala Kawe, nashuhudia mengi kwa madereva na makondakta wana msemo wa ‘Kanyagia ganda la  ndizi’ hiyo ni mida ya saa tatu, nne, unawakuta bado wanasota kituoni unampakia awezi kukataa, unamsomesha unaenda kupiga mzigo (ngono) kiulaini sana,” anasema Shoo

Kauli ya Shoo imekuja ikiwa serikali tayari imetangaza kuandaa mpango wa taifa wa kutokomeza ukatili wa kijnsia dhidi ya Wanawake na Watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000); Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Jinsia (2005); Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008); Sheria ya Makosa ya Kujamiiana – SOSPA (1998).

Kwa upande wake Mkuu wa dawati la elimu kwa umma kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru),Esther Mkokota  akizungumza katika mafunzo hayo  anasema madereva  ni wadau wakubwa hivyo wanawajibu wa kuwalinda wanawake na watoto, wavunje ukimya na kutoa taarifa na kukemea vitendo vya ngono.

Naye Mkurugenzi wa Asasi ya WAJIKI, Janeth Mawinza anasema  mbali na kudadavua mambo mbalimbali yanayochangia muendelezo wa ukatili wa kingono nchini, suala la umbali mrefu kuelekea katika shule mbalimbali nchini limechangia kuendelea kuwapo kwa ushawishi wa kushiriki ngono kwa baadhi ya wasichana na mwishowe kupata mimba.

Shabiki Yanga, Barcelona ashinda Milioni 76.2 za M-BET

$
0
0
Dar es Salaam.Shabiki wa timu ya kongwe ya soka nchini, Yanga, Barcelona na Manchester City, Samson Auzebio Mlembe (23) ameshinda Sh 76, 200, 750 kupitia mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-BET.

Msemaji wa kampuni ya M-Bet Tanzania David Malley amesema kuwa Mlembe ameshinda fedha hizo baada yakubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali duniani.

Malley alisema kuwa Mlembe ambaye ni mkazi wa Dodoma amekuwa mshindi wa tano kwa mwezi Novemba na 17 miezi 11 na kuweza kubadili maisha yao kupitia mchezo wa Perfect 1.

Alisema kuwa M-BET ni inaendelea kuwa nyumba ya mabingwa kwa kutoa washindi wengi zaidi ambapo mpaka sasa wametumia zaidi ya Sh milioni 700 kwa washindi na bonusi kwa mwezi Novemba peke yake.

“Tunazidi kuinua vipato kwa Watanzania, tumeweza kutoa zaidi ya mamilioni ya fedha kwa mwezi huu na kuwa kampuni pekee iliyoweza kutoa fedha nyingi kwa washindi,” alisema Malley.

Kwa upande wake, Mlembe alisema kuwa hakufikiria kabisa kuwa Allen Mushi kuwa ni tapeli wa mjini baada ya kupokea simu yake.Mlembe alisema kuwa anamfahamu Mushi kutokana na kumuona akiwakabidhi fedha washindi wengi Perfect 12 na kuamini kuwa ameshinda.

“Mpaka sasa sijapanga nitumie fedha hizi kwa mambo gani, ni fedha nyingi ambayo sikutegemea kuipata, nitakaa na wazazi wangu na kujua nini cha kufanya, kwa kweli siwezi kukurupuka,” alisema Mlembe.

Alisema kuwa kuna biashara mbalimbali za kufanya, lakini lazima uweke mikakati na mipango sahihi kabla ya kuanza.
Msemaji wa Kampuni ya M-BET Tanzania, David Malley (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh milioni 76.2 Mkazi wa Dodoma, Samson Mlembe aliyeshinda mchezo wa kubashiri wa Perfect 12. Katikati ni Shabani Mwanga, Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Michezo ya Kubahatisha (TRA), mkoa wa kodi wa Ilala.

4th INTERNATIONAL THERMAL & HEALTHCARE TRAVEL SUMMIT, BALIKESIR TURKEY.

$
0
0
The summit was officially opened by the Mayor of Balikesir Mr. Yücel Yilmaz and flagged by mayors of respective municipals among other government officials and high dignitaries. 

Balikesir is known as an important health destination with its resources and potential, important candidate to be “Thermal center of the Future”. 

Providing remedy for citizens and inhabitants of the region for centuries with healing waters in almost every district. Balikesir derives its power in health, tourism, not only from its healing waters but also from its unique nature. 

The guests were treated to a detailed tour of Edremit, Gonen and Sindirgi and enjoyed these facilities. Edremit, Sindirgi and Gonen are districts located at Balikesir region.THERMAL treatment is famous in Turkey with 5-star thermal hotels and facilities.
Various government leaders and stakeholders follow the 4th international thermal & healthcare travel summit held in Endremit, Turkey. The summit featured many countries including Tanzania.
Turkish Healthcare Travel Council President, Emim Cakmak invites various delegation during the 4th International Thermal Healthcare Travel Summit' held in Endremit, Balikesir in Turkey.
Turkish Healthcare Travel Council President Emim Cakmak handovers appreciation certificate to the Mayor of Balıkesir Metropolitan Municipality,Yucel Yilmaz for successfully hosting the summit
Some of healthy stakeholders discuss various matters during the summit
Delegations of 4th International Thermal Healthcare Travel Summit in a group picture after the event
Turkish Healthcare Travel Council President Emim Cakmak (middle) handovers appreciation certificate to Balikesir regional leaders for successfully hosting the summit

Delegates being entertained by special entertainment group
Participants in a group picture after the summit.

KAIMU DC MUHEZA KIJAZI ATOA WIKI MOJA KWA MAAFISA KILIMO KUSHUGHULIKIA JANGA LINALOATHIRI PILIPILI MANGA MUHEZA

$
0
0
 KAIMU Mkuu wa wilaya ya Muheza Ally Kijazi ambaye pia ni Afisa Tarafa ya Bwembwera wilayani humo akizungumza mara baada ya kufungua Jukwaa hilo la viungo
 Afisa Kilimo wilaya ya Muheza Hoyange Mbwambo  akizungumza wakati wa Jukwaa hilo 
 MENEJA wa Benki ya CRDB wilayani Muheza Shija akizungumza wakati wa Jukwaa hilo
 Mkulima wa Iliki Kata ya Zirai Ally Zubeya akichangia jambo kwenye Jukwaa hilo
 AFISA Kilimo Idrisa Kijazi akieleza jambo wakati wa Jukwaa hilo 
 MDAU wa  mazao ya viungo wilayani Muheza kutoka Baraza la Biashara za Uholanzi na Afrik akielezea uzoefu wao kwenye Jukwaa hilo
 Sehemu ya wakulima wa mazao ya viungo wilayani Muheza wakiwa kwenye kikao hicho
 Sehemu ya wakulima wa mazao ya viungo wilayani Muheza wakiwa kwenye kikao hicho


KAIMU Mkuu wa wilaya ya Muheza Ally Kijazi amewaagiza maafisa kilimo na watendaji wa Kata wilayani humo kuhakikisha ndani ya wiki moja washughulikia janga ambalo linaendelea kuathiri zao la pilipili manga ndani ya wiki moja. 

Pia alimtaka Afisa Kilimo wa wilaya hiyo Hoyange Mbwambo kushirikiana na maafisa hao kuhakikisha wanapata suluhu ya tatizo hilo ambalo linaleta athari kwa wakulima hao wa pilipili manga. 



Kijazi ambaye ni Afisa Tarafa ya Bwembwera wilayani Muheza alitoa agizo hilo wakati wa Jukwaa la wadau wa mazao ya viungo wilayani humo ambapo pia walitumika kuweka mikakati mbalimbali. 


Alisema baada ya muda huo waweze kutoa ripoti ya tatizo linalopelekea kukausha zao hilo la pilipili Manga huku likiufanya mti wa zao hilo kukauka na kuleta athari kubwa kwa wakulima. 


“Tunaweza kujaribu kufanya tathimini kukuta janga hili ni kubwa hasa kwa wakulima lakini pia mkishindwa kulitatua tupeleke ombi tuweze kusaidiwa kwenye ngazi za juu akiwemo Mkuu wa wilaya hata Mkuu wa Mkoa kuweza kuona namna ya kulitatua kwa pamoja”Alisema 

Kaimu Mkuu huyo wa wilaya alisema ufunguzi rasmi ya kuvuna zao pilipili Manga wilayani humo litakuwa ni Januari 3 mwakani huku akiwaonya watakaojaribu kuvuna kabla ya muda huo watawachukulia hatua. 

“Tunawafahamu njia ambazo mnatumia kusafirisha mazao hayo hivyo hakikisheni mnazingatia muda wa kuvuna msije kuingia matatani kwani watakaokamatwa kabla ya wakati watawashughulikia kwa mujibu wa sheria kukomesha vitendo hivyo “Alisema 

Awali akizungumza wakati wa Jukwaa hilo Afisa Kilimo wilaya ya Muheza Hayange Mbwambo alisema kwamba walipokubaliana wawe na muda wa kuvuna iliwasaidia sana kuhakikisha kwenye masoko wanapata pilipili manga iliyokomaa na yenye ubora. 

Alisema kwamba licha ya kuwepo kwa kasoro ndogo ndogo zinazungumzika na wamefikia hatua nzuri ya mahali wanapotaka kufika huku akieleza kwamba wameanza kuaminika kwamba asilimia 70 ya pilipili zinazovunwa zinasifa ya ukomavu na kuleta ubora na hivyo kupunguza malalamiko sokoni. 

“Lakini pia wiki mbili zilizopita tulitembelewa na wageni kutoka kwenye makampuni ya nje moja ya mambo ambayo walitupongeza ni kuweka utaratibu mzuri wa kufungua msimu”Alisema 

Naye kwa upande wake Mkulima wa Iliki Kata ya Zirai Ally Zubeya alisema visababishi vya iliki kuwa changa ni wakulima kuwekeza shamba lake kwa mtu kwamba ukifika muda Fulani atavuna mazao na anapokwenda kuvuna anavuna zote. 


Alisema mwarobaini wa suala hilo ni vyama vya ushirika kuhakikisha wanakagua mazao husika yanapokuwa shambani kabla ya kuvunwa kutokana na kwamba nyengine zinavunwa kabla ya kukomaa na kupelekea kukosekana kwa ubora. 

ZIARA YA RAIS WA TAASISI YA UCHUMI NA MAENDELEO YA AFRIKA WA JAPAN HAPA NCHINI

EAC-COMESA-ECOWAS LAUNCH DIGITAL PLATFORM TO EMPOWER WOMEN

$
0
0
After a one-year-long work of platform construction and information upload, the new continental women’s platform was launched on November 26, during the Global Gender Summit in Kigali, Rwanda.
Implementing team members after the platform launch.


The platform is intended to connect 50 million African women in business across 38 African countries.
The portal (www.womenconnect.org) and mobile application (50MAWSP) come to solve the information issue that African women in business face when it comes to accessing available information on financial and non-financial services.
In a joint media address that followed the launch of the platform, the Tripartite EAC-COMESA-ECOWAS told journalists that sub-Saharan Africa hosts close to 13 million formal and informal, small and medium-sized enterprises with one or more women owners, but only 16-20 percent of the women entrepreneurs are able to access long-term financing from formal financial institutions to scale up their businesses.
The platform hosts information on where to access capital, how to run a business, access training resources, get mentorship, access markets and many more relevant categories of information.
“This information is expected to help women create business opportunities and thus empower them economically”, press conference panel said.
This initiative is funded by the African Development Bank (AfDB) and implemented by the Common Market for Eastern and Southern Africa (COMESA), the East African Community (EAC) and the Economic Community of West African States (ECOWAS).
The audience appreciated the initiative but expressed concerns about who was the target group of the platform since it is technology-based and when many women in Africa don’t have access to smartphones.
“I don’t think we need to have everything in place to dream big in Africa,” Vanessa Moungar, Director of Gender, Women and Civil Society Department in the African Development Bank said. I know many projects that are running well in Africa from which the World can learn from, she added.
Hon. Christophe Bazivamo, the EAC Deputy Secretary General in charge of the Productive and Social Sectors, disclosed that the implementing partners were executing many other projects in parallel.
“This platform is one project among many others. As we work towards women empowerment, we are also working in energy, infrastructure, industry, health, and many other sectors to ensure the effectiveness of our interventions,” said Hon. Bazivamo.

The 50 Million African Women Speak platform is now up and running; it initially uses English, French and Arabic languages.

WAZIRI NDALICHAKO AZINDUA CHUO CHA MAFUNZO YA UFUNDI CHA MKOA WA KAGERA

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amezindua ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera na kusema kuwa ujenzi wa chuo hicho ni muendelezo wa jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha kunakuwa na Vyuo vya ufundi stadi vya Mikoa na Wilaya.

Akizindua ujenzi wa chuo hicho mkoani Kagera Waziri Ndalichako amesema  chuo hicho  kinajengwa  na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kutokana na uhusiano mzuri wa muda mrefu uliopo baina ya Tanzania na Nchi hiyo na kwamba ujenzi utakapokamilika vijana wengi wa kitanzania watapata fursa ya kusoma katika chuo hicho na kupata ujuzi katika fani mbalimbali zitakazo fundishwa.

"Kama nilivyosema Tanzania na China ni marafiki na rafiki yako anaangalia mahitaji yako, waswahili husema akufaaye kwa dhiki ndio rafiki wa kweli. China imeona Tanzania inajenga uchumi wa Viwanda ikiwa ni azma ya serikali ya awamu ya Tano  nao wakaamua watuunge mkono katika ujenzi wa Chuo cha Ufundi stadi ili kuandaa vijana wenye ujuzi watakaofanya kazi katika viwanda.

Nikuombe Balozi  tufikishie shukrani zetu za dhati kwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa msaada huu mkubwa na wa kihistoria ," Amesema Waziri Ndalichako.

Waziri Ndalichako amesema ujio wa mradi huo utaongeza ajira kwa vijana wa kitanzania kwa kuwa wazawa 400 wataajiriwa katika mradi huo ikiwa ni pamoja na kupata  ujuzi  kulingana na kazi watakazokuwa wakizitekeleza.

"Vijana watakaofanya kazi eneo la mradi pamoja na kufanya kazi  watapata na mafunzo, kwa hiyo ujuzi wao wa kiufundi utaimarishwa kupitia kazi ambazo watakuwa wakifanya katika mradi," Amesema waziri Ndalichako.

Katika hatua nyingine Waziri Ndalichako ameitaka Mamlaka ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kupitia upya fani zilizopangwa kutolewa katika chuo hicho ili ziendane na Mazingira halisi ya kiuchumi kwa wakazi wa eneo hilo.

"Nimepitia fani ambazo zimeanishwa kutolewa katika chuo hiki pindi kitakapokamilika, nikiangalia eneo ambalo chuo kinajengwa ni eneo la ziwa na watu wa Kagera au wazazi wa hapa ni wavuvi lakini sijaona kozi ya uvuvi sasa tunawaletea mambo ya uchomeleaji, ufundi bomba, useremala, upakaji rangi kwenye bahari, nilitegemea kuwe na fani ya uvuvi pia
 tuweke fani zinazoendana na mazingira," Amesema Waziri Ndalichako

Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania Balozi WANG Ke amesema Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania amezingatia maboresho ya sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuwaongoza watanzania kuelekea dira ya  maendeleo 2025 hivyo China iko tayari kuchangia maendeleo katika sekta ya elimu ili kufikia malengo ya elimu ambayo serikali ya tanzania imejiwekea. 

Nae Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Gaguti  amewataka wanakagera hasa vijana kushiriki vizuri katika kazi za ujenzi zitakazofanyika katika mradi huo  ili kupata ujuzi wa ufundi ambao utawasaidia kushirikia katika kazi za ujenzi zitakazojitokeza katika Mkoa wa Kagera mara baada ya mradi kukamilika. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi   VETA Dkt. Pancras Bujulu amesema Chuo hicho kinajengwa katika eneo lililotolewa na wananchi wa kijiji cha Burugo wilayani Bukoba na lina ukubwa wa hekta 40. 5 sawa na hekari 100.

Dkt. Bujulu amesema Chuo hicho pindi kitakapokamilika kitatoa fani za useremala, uchomeleaji, upakaji rangi, ufundi bomba na kitachukua wanafunzi 800 wa kozi ndefu na 2000 wa kozi fupi

Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Mkoa wa Kagera kinajengwa kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China  kwa gharama za fedha za kitanzania sh bilioni 19.4  ambapo ujenzi wake utachukua miezi 18

Gharama hizo zinajumuisha usanifu, upembuzi yakinifu na ujenzi mpaka ukamilike.
Waziri wa Elimu, Sayansi  na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizindua kuanza kwa ujenzi wa Chuo cha  Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma cha mkoa wa Kagera, mkoani Kagera.

 Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi waliohudhuria uzinduzi wa ujenzi wa chuo cha VETA  cha Mkoa wa Kagera wakifuatilia hotuba ya waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.
 Balozi wa China nchini Tanzania WANG Ke akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi  Stadi na Huduma Cha Mkoa wa Kagera.
 Waziri wa Elimu, Sayansi  na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi na  Huduma  cha Mkoa wa Kagera.

EU, EAC SIGN 10 MILLION EUROS FOR JOINT RESPONSE TO REGIONAL AND CROSS BORDER SECURITY THREATS

$
0
0
( from R-L) EAC Director General Customs and Trade, Mr Kennethe Bagamuhunda, Deputy Secretary General Planning and Infrastructure, Eng Steven Mlote, Secretary General of EAC, Amb Liberat Mfumukeko and EU Amb Manfredo Fanti during the accreditation ceremony
The EAC Secretary General Amb Liberat Mfumukeko ( R) receives credentials from the new EU Amb .Manfredo Fanti
EU Amb .Manfredo Fanti and EAC Secretary General signs financing agreement of 10 million Euros

……………………………………………….

The EU Ambassador to Tanzania and the East African Community, H.E. Manfredo Fanti, and the EAC Secretary-General, H.E. Libérat Mfumukeko, today launched a new 10 million Euros (approx. TShs25.38 billion) joint programme to address regional and cross border security threats in the region.

The programme is a regional response to the various and growing security threats across the EAC region. It will work both on enhancing the technical capacities and building trust between the law enforcement agencies in the EAC Partner States. Without mutual trust, data and information will not be shared. The shared aim is to intercept those engaged in transnational organised crime.

This 45-month programme will be implemented by the EAC Secretariat and the International Criminal Police Organization (Interpol). It will complement several other initiatives to provide peace and security to the people of the EAC.

“Cooperation in this area can work only if there is mutual trust among law enforcement agencies and this is what the programme aims at,” said the EU Ambassador to Tanzania and the East African Community.

In his remarks, Amb. Mfumukeko hailed the long standing partnership between the EAC and the EU in the peace and security sector which he said was a key enabler to the integration process in East Africa.

“The current phase of the EDF11 has set aside 85 million Euros for a variety of interventions supportive to the various integration initiatives, among them peace and security. The EAC is also a beneficiary of the 528 million Euros through a regional enveloped that also covers IGAD, COMESA, IOC and SADC,” said Amb. Mfumukeko.

“Since 2007, the EU has extended support to the EAC through various initiatives including the APSA support project (about Euro 10 million cumulative to date) whose 4th phase is still under negotiation, the Conflict Prevention, Management and Resolution Project whose implementation ended in 2012 (4.8 million Euros) and the Eastern and Southern Africa-Indian Ocean (ESA-IO) Maritime Security Project whose implementation ended on 14th October, 2019 (11.6 million Euros),” said the Secretary General.

“The project being launched today will seek to reduce opportunities for transnational and cross border threats to the integration process through support to policy development and implementation, enhanced political accountability, structured and institutional information exchange mechanisms, consolidation and extension of ballistic examination capacity, and extension of I/24-7 connectivity to as many One Stop Border Posts as possible,” he said.

The Secretary General said the efficient implementation of the proposed interventions will enable the law enforcement agencies to, at a regional level, implement information sharing mechanisms that will facilitate rapid and timely response to threats and enhance security as greater gains are made in the implementation of the EAC Customs Unions and Common Market protocols.

This project will also assist the EAC in the implementation of the recently adopted Peace and Security Protocol and feed into the broader African commitment of “silencing the guns in Africa by 2020.”

RMO KILIMANJARO AENDESHA OPERESHENI NA KUKAMATA TANI TATU ZA MADINI

$
0
0
fisa madini mkazi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Fatuma Kyando akikagua madini ya yaliyokamatwa Kata ya Hedaru Wilayani Same yakisafirishwa kwenda jijini Dar es salaam bila kibali.
Ofisa madini mkazi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Fatuma Kyando akiandika taarifa za kazi ofisini kwake.
……………………………………..

TANI tatu za madini mchanganyiko yenye thamani ya sh15 milioni yamekamatwa Mkoani Kilimanjaro, mengine yakisafirishwa kwenda kuuzwa jijini Dar es salaam bila kuwa na kibali.

Ofisa madini mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro, Fatuma Kyando alisema watu saba walikamatwa kwenye maeneo tofauti wakiwa na madini hayo. 

Kyando alisema watu watatu walikamatwa na madini aina ya Feldspar Carrot kwenye eneo la Hedaru wilayani Same wakitoa wilayani Simanjiro mkoani Manyara wakiyasafirisha jijini Dar es salaam. 

Alisema watu wawili walikamatwa wilayani Same wakiwa na madini ya vito aina ya Red garnet na Almandite bila kuwa na kibali cha aina yoyote kinachowapa haki ya kuwa na madini hayo. 

Alisema mjini Moshi waliyakamata madini tofauti ikiwemo vito mchanganyiko na madini ya viwanda na watu wawili ambao hawakuwa na kibali cha kuwa na madini hayo. 

“Tulishirikiana na askari polisi kwenye matukio hayo hapa Moshi na kule wilayani Same akiwemo OCCID na askari polisi wa kituo kidogo cha Hedaru katika kuwakamata watuhumiwa hao,” alisema Kyando. 

Mmoja kati ya wachimbaji madini wa mkoa huo, Godfrey Kiangi alipongeza ofisi ya madini ya mkoa wa Kilimanjaro kwa kazi kubwa wanayofanya na ushirikiano wanaotoa kwa wadau.

Kiangi alisema utendaji kazi wa ofisi ya madini Kilimanjaro ni mzuri kwani wanatoa huduma bora ikiwemo maelezo yaliyojitosheleza na utunzaji wa mazingira mzuri. 

“Hakuna urasimu kwenye ofisi zao na pia unaweza kupiga simu saa 24 ukapatiwa huduma kwani wanafanya kazi kwa vitendo bila ubaguzi wa kufahamiana hivyo wanastahili hongera kwa kazi nzuri wanayofanya,” alisema. 

Hata hivyo, aliwaasa wafanyakazi wa serikali wa ofisi nyingine kufanya kazi zao kwa kuiga mambo mazuri yanayofanywa na ofisi ya madini mkoani Kilimanjaro ambapo ukimaliziwa tatizo una hamu ya kurudi kwa namna huduma inavyotolewa.

NAIBU SPIKA ASHIRI KATIKA MKUTANO WA MASUALA YA AMANI JIJINI NIAMEY, NIGER

$
0
0

 Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), ashiriki Mkutano wa Masuala ya Amani, Usalama na Maendeleo ya Watu unaoendelea katika Jiji la Niamey nchini Niger. Mkutano huo wa siku tatu ambao umeandaliwa na Shirika la Universal Peace Federation, umewaleta pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali, Maspika, Manaibu Spika, Mawaziri, Wabunge, Viongozi wa Dini na Kimila pamoja na Wakuu wa Taasisi za Kibiashara wa Bara la Afrika kubaini na kujadili changamoto zinazosababisha uvunjifu wa amani na usalama katika kuwaletea maendeleo Waafrika. Katika Mkutano huo Naibu Spika ameambatana na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Zainabu Katimba.

UBINAFSI CHANZO CHA KUDORORA BIASHARA EABC

$
0
0
Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Paramagamba Kabudi 



Na Ahmed Mahmoud Arusha.

Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Paramagamba Kabudi amezitaka nchi za jumuiya ya Afrika mashariki kuwekeza katika sekta ya miundo mbinu ili kuwa na nishati ya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa viwanda .

Alisema hatua hiyo itawezesha biashara kukua kwa nchi za jumuiya hiyo kiwemo kuongeza sayansi ,Teknolojia na ubunifu kwa Vijana wenye ujuzi wa kufanyakazi kwenye viwanda hivyo.

Ameyasema hayo katika mkutano wa Wafanyabiashara zaidi ya 1000 wa nchi za Afrika mashariki ulioandaliwa na Baraza la Wafanyabiashara wa nchi za Afrika Mashariki (EABC) unaofanyika kwa siku mbili jijini Arusha na kwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 20 ya jumuiya ya Afrika Mashariki.

Prof.Kabudi amesema kuwa,nchi zilizo nyuma katika maendeleo ya viwanda zinapaswa kusaidiwa ili kupata viwanda na kuweza kuzalisha bidhaa na kuuza kwenye soko la pamoja la jumuiya ya Afrika Mashariki.

“lazima nchi ziwe na viwanda vya kutosha na kufanyabiashara nzuri ,kwa sababu jumuiya ni ya watu wote na lazima iwanufaishe wananchi wote”Amesema

Naye waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amesema kuwa uchumi wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki lazima ujengwe kupitia sekta binafsi za viwanda,kilimo, Mifugo na kuimarisha miundo mbinu .

Amesema serikali ya Tanzania inajitahidi kuweka mazingira Bora kwa wafanyabiashara ili biashara zao zinakua na kuhakikisha wanafanyabiashara nje ya Tanzania bila kikwazo chochote .

Waziri Bashingwa ametumia wasaa huo kuwakaribisha wawekezaji kuja hapa nchini kuwekeza viwanda kwa ajili ya vifungashio na kuviuza katika nchi wanachama.

Baadhi ya Wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo ,Lomayan Laizer na Jiten Shah Mwanzilishi wa kampuni ya Quickmarc wamepongeza mazingira mazuri yanayotolewa kwenye nchi za ukanda huu na kuwataka kuangalia kwa kina na kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ushuru na tozo mbalimbali

Walisema kuwa pia vikwazo katika mipaka wakati wanaposafirisha bidhaa zao kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine imekuwa ni shemu ya changamoto hususani vipimo vya ubora na kuwataka wakuu wa jumuiya hiyo kuboresha na uwezekano wa kuondoa vikwazo hivyo ili kuwarahisishia Wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa urahisi zaidi.

Naye Erhard Mlyansi ambaye ni Afisa masoko mkuu wa kampuni ya Motisun Group kutoka jijini Dar es Saalamu inayotengeneza bidhaa mbalimbali za ujenzi na juisi ya Sayona amelalamikia hatua ya kuigwa kwa bidhaa zao na kuuzwa katika nchi za jumuiya ya Afrika mashariki Jambo ambalo limekuwa likiwasababishia usumbufu kibiashara

DPP Afuta Kesi 59 Zaidi Jijini Mbeya

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) akisalimiana na afisa wa magereza wakati wa ziara ya kikazi katika gereza la Tukuyu Wilaya ya Rungwe Jijini Mbeya. Nyuma ya Waziri Mahiga ni Mkuu wa Gereza la Tukuyu ASP. Samwel J. Kaluwa (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP) Biswalo Mganga (katikati).
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) akisalimiana na afisa wa magereza wakati wa ziara ya kikazi katika gereza la Tukuyu Wilaya ya Rungwe Jijini Mbeya. Kushoto ni Mkuu wa Gereza la Tukuyu ASP. Samwel J. Kaluwa akiwatambulisha Staff wa gereza hilo mbele ya Waziri.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mh. Chalya J. Nyangidu (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka Biswalo Mganga (wa pili kulia), walipotembelea Ofisi ya Mkuu huyo wa Wilaya leo tarehe 28 Nov. 2019 wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo.
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) kulia akiwa na mwenyeji wake Kamishna Msaidizi wa Magereza Mkoa wa Mbeya Mathias Mkama (ACP) katikati, alipotembelea Gereza Kuu la Ruanda Mbeya 27 Nov. 2019. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ruanda Mbeya Vendeline Tesha wakati wa ziara ya kikazi jijini humo.

……………….

Katika mwendelezo wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) kwenye mikoa ya kusini, Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka Tanzania (DPP) Biswalo Mganga amefuta jumla ya kesi 59 katika mahakama za Mkoa wa Mbeya. 

Mkurugenzi Biswalo ameyafanya hayo katika gereza la Ruanda mjini Mbeya na gereza la Tukuyu Wilaya ya Rungwe alipoambatana na Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Mahiga ili kujionea hali halisi ya mazingira ya utoaji haki jinai katika magereza hayo na taasisi mbalimbali za haki jinai ikiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, Polisi, Mahakama na Magereza yenyewe. 

“Niliowafutia Kesi nendeni mkawe raia wema, msirudie makosa, badala yake mkawe mabalozi wema mtakaofanya kazi kwa bidii ili kumuunga mkono Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Joseph Maguli katika kauli yake ya hapa kazi tu.”

Kwa upande wake Waziri mwenye dhamana ya Katiba na Sheria Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) aliwataka wote waliofutiwa mashitaka kwenda kufurahi na familia zao huku wakimshukuru Mungu na kujutia makosa yaliyosababisha kushitakiwa kwao. Aidha, aliwaonya kutokurudia makosa hayo badala yake watumie nguvu na akili walizonazo kuzalisha mali kwa maendeleo yao na familia zao pamoja na kukuza uchumi wa Taifa. 

“Mliosamehewa leo nendeni mkafurahi na familia zenu sambamba na kuwa watu wema katika jamii inayowazunguka kwani ni matumaini yangu kuwa mmejifunza mengi na mmebadilika. Kuna watu hapa nikiwatizama misuli yao, walipaswa wakaitumie kufanya kazi na kuzalisha mali kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla badala ya kuitumia kufanya uhalifu.” 

Kwa mujibu wa kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marejeo 2002, Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka anayo mamlaka ya kuwafutia mashitaka watuhumiwa wa makosa ya jinai katika magereza mbalimbali nchini. Mpaka sasa katika ziara hii ya kikazi ya Waziri wa Katiba na Sheria katika mikoa mitatu DPP Biswalo ameshafuta jumla ya kesi 120 na bado ziara inaendelea katika Wilaya ya Kyela na baadae mkoa wa Njombe. 

WAZIRI MAHIGA -TANZANIA INAFUATA MGAWANYO WA MADARAKA

$
0
0


Na. Rajabu Singana, Mahakama Kuu Mbeya

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amesema kwamba Tanzania ina mgawanyo wa madaraka na unaofuatwa vizuri tofauti na nchi nyingine.

Akizungumza leo Novemba 28,mwaka huu wakati alipotembelea Ofisi za Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Waziri Mahiga alisema ametembea nchi mbalimbali na kujifunza kwamba katika nchi yetu mgawanyo wa madaraka (separation of power) unafuatwa.

‘Mgawanyo wa madaraka kwa mihimili ya dola, ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama upo na unafuatwa vizuri kulinganisha na nchi nyingine ambapo hata kuonekana haionekani kabisa na kama ilikuwepo basi ilikufa, alisema Waziri Mahiga. 

Akizungumzia kuhusu kazi kubwa inayofanywa na Wahe. Majaji ya kusikiliza mashauri ambapo kuna wakati wanalazimika kufanya kazi hadi kwa zaidi ya saa 18 kwa siku ili kuweza kuwahudumia wananchi na kufikia malengo ya kitaasisi, alisema anatambua mchango huo na kuwapongeza.

Pamoja na pongezi hizo, amewataka majaji hao, kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na utendaji uliotukua kiasi kwamba ikitokea mtu ameulizwa haki ni nini? katika kutoa majibu amchukue Jaji na kusema hii ndio maana ya haki.

Hivyo katika hilo amewashauri Wahe. Majaji kuwa na maadili ya ziada na kuufanya Mhimili wa Mahakama kutekeleza majukumu kwa viwango vya juu.

Vile vile Waziri Mahiga amesema kupitia kuongezeka kwa watu na kukua kwa Sayansi na Teknolojia, nchi yetu imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali zinazosababisha watu kubuni njia nyingi za uhalifu.

Alisema changamoto hizo zinasababisha kuwa na uhaba wa majaji kitendo kinachowalazimu kuwa na makadirio ya kusikiliza mashauri mengi zaidi tofauti na mipango ya kitaasisi, na kila mmoja kulazimika kufanya kazi kwa muda mrefu.

Naye Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Dkt. John Utamwa, alisema mikakati ambayo imekuwa ikitumiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya katika kuhakikisha mashauri yanaamuliwa kwa wakati na ubora unaotakiwa ni uwepo wa miongozo mbalimbali juu ya utoaji huduma kwa mfano kabla ya kufika siku 21 nakala za hukumu zinatakiwa kuwa tayari lakini Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Nakala za Hukumu hutolewa ndani ya siku ambayo hukumu hutolewa.

Waziri wa Sheria na Katiba yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, ameambatana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Mhe. Biswalo Mganga ambapo wakikagua Magereza na kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafungwa na Mahabusu.

Katika ziara hiyo, Mhe. Biswalo Mganga amewafutia mashtaka jumla ya watuhumiwa 47.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe.Dkt. John Utamwa.Picha na  Rajabu Singana, Mahakama Kuu Mbeya)
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akitembelea jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya leo. Kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe.Dkt. John Utamwa.

KILA MMOJA ANA WAAJIBU WA KUISAIDIA SERIKALI KATIKA UKUSANYAJI MAPATO-TRA

$
0
0
Na Kijakazi Abdalla-Maelezo  
Kaimu Meneja Idara ya Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (T.R.A) Mbarouk Khalid Ussi amesema kila mmoja ana wajibu wa kuisaidia Serikali katika ukusanyaji wa mapato.
Hayo ameyasema huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo wakati  akifungua semina ya Wahasibu,Afisa Manunuzi pamoja na Wakaguzi wa hesabu wa taasisi za Serikali kuhusu kodi ya zuwio.
Amesema kuwa Serikali  inategemea kodi katika ukusanyaji wa mapato hivyo ipo haja kwa wafanyakazi hao  kusimamia na kutoa ushirikiano  ili kuhakikisha Serikali inapata mapato yao.
Amesema kuwa Serikali ina viazio vingi vya ukusanyaji wa  mapato hivyo ni vyema kuisaidia katika ukusanyaji kodi ili kuhakikisha lengo lilokusudiwa katika kuengeza pato la taifa linatimia
Nae Afisa Msimamizi wa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (T.R .A) kwa upande wa Zanzibar Abdallah Seif Abdallah  amesema lengo la semina hiyo ni kuwakumbusha Wahasibu,Afisa Manunuzi pamoja na Wakaguzi wa Hesabu wa taasisi za Serikali  kujua wajibu wao wa  kuzuwia kodi ya zuwio ili kuongeza ukusanyaji wa mapato .
Aidha amewataka wafanyabiashara pamoja na watendaji hao kutoa mashirikiano kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (T.R.A)  ili kuhakikisha hakuna upotevu katika ukusanyaji wa mapato na ulipaji wa kodi.
Akiwasilisha mada ya Kodi ya Zuwio kwa Wahasibu,Afisa Manunuzi pamoja na Wakaguzi wa Hesabu wa Taasisi za Serikali Afisa Mwandamizi Elimu na Huduma kwa Walipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa upande wa Zanzibar Shuweikha S.Khalfan amesema kuwa ni wajibu kwa wafanyakazi hao kujua sheria zote za walipa kodi.
 Kaimu Meneja Idara ya Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (T.R.A) Mbarouk Khalid Ussi akifunguwa Mafunzo ya Kodi ya Zuwio kwa Wahasibu,Afisa Manunuzi na Wakaguzi wa hesabu kutoka Taasisi za Serikali huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
 Afisa Msimamizi wa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (T.R.A) kwa upande wa Zanzibar Abdallah Seif Abdallah akitowa ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa na Wahasibu,Afisa Manunuzi na Wakaguzi wa hesabu wa Taasisi za Serikali katika Semina inayozungumzia Kodi ya Zuwio huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
 Afisa Muandamizi Elimu na Huduma kwa walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (T.R.A) Kwa upande wa Zanzibar Shuweikha .S. Khalfan akitoa mada kuhusu Kodi ya Zuwio kwa Wahasibu,Afisa Manunuzi na Wakaguzi wa hesabu wa Taasisi za Serikali katika Semina inayozunguzmzia  Kodi ya Zuwio huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
Baadhi ya  Wahasibu,Afisa Manunuzi na Wakaguzi wa hesabu wa Taasisi za Serikali wakifatilia kwa makini  Semina inayozungumzia Kodi ya Zuwio huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.Picha na Maryama Kidiko – Maelezo Zanzibar.
Viewing all 110105 articles
Browse latest View live




Latest Images