Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live

WATANZANIA KUNUFAIKA NA OFA KABAMBE ZA BLACK FRIDAY KUPITIA VODACOM M-PESA

$
0
0
Meneja masoko wa Vodacom M-Pesa, Noel Mazoya (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Es Salaam kuhusu ofa ya hadi asilimia 10 itakayotolewa na Kampuni ya Vodacom tarehe 29 wiki hii,siku maarufu duniani kwa manunuzi ya bidhaa kwenye maduka na mtandaoni ijulikanayo kama BLACK FRIDAY. Wateja wa Vodacom watalipa kupitia huduma za LIPA KWA SIMU na M-PESA MASTERCARD na watarudishiwa hadi asilimia 10 papo hapo wakilipa kupitia mtandao wowote kwenye maduka mbalimbali yaliyopo kwenye malls tofauti nchini. Wengine kwenye picha, wapili toka kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Mr Price Tanzania, Paul Namuhisa, Meneja wa Easybuy Africa, Juliana Siyame na Meneja wa malipo kwa njia ya Mtandao Vodacom, Loius Maro.
Meneja masoko wa Vodacom M-Pesa, Noel Mazoya akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Uendeshaji wa Mr Price Tanzania, Paul Namuhisa, Meneja wa Easybuy Africa, Juliana Siyame na Meneja wa malipo kwa njia ya Mtandao Vodacom, Loius Maro, mara baada ya kutangaza ofa maalum ya BLACK FRIDAY itakayotolewa siku ya ijumaa wiki hii 
Baadhi ya warembo watakaohudumia wateja kwenye maduka mbalimbali yaliyoorodheshwa kote nchini siku ya ijumaa kwenye ofa ya BLACK FRIDAY.

…………….
Wateja kurudishiwa hadi 10% ya gharama za malipo siku hiyo.

Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na wafanyabiashara mbalimbali nchini imezindua kampeni kabambe inayowawezesha wateja wake kufurahia punguzo kubwa wanapofanya malipo kupitia huduma yake ya M-Pesa. Kampeni hiyo iliyoziduliwa jijini Dar es salaam inalenga kuongeza matumizi ya huduma za kidigitali kwenye kufanya malipo hasa kwenye kipindi hiki cha BLACK FRIDAY, siku maarufu duniani kwa manunuzi ya bidhaa kwenye maduka na mtandaoni. 

Kupitia huduma zake mbili za LIPA KWA SIMU na M-PESA MASTERCARD Vodacom M-Pesa wanawawezesha watanzania kufanya malipo kwa wafanyabiashara ndani ya nchi na mitandaoni kupitia simu zao na kurudishiwa hadi 10% ya gharama za malipo siku hiyo ya BLACK FRIDAY ambayo kwa mwaka 2019 itakuwa ijumaa tarehe 29 Novemba.

Meneja masoko wa Vodacom M-Pesa, Noel Mazoya alisema, ‘Black Friday hii tumeandaa ofa ya hadi asilimia 10 ya gharama ambayo wateja wetu watalipa kupitia huduma za LIPA KWA SIMU na M-PESA MASTERCARD. Kupitia huduma ya LIPA KWA SIMU, M-Pesa tutawarudishia hadi asilimia 10 papo hapo wakilipa kupitia mtandao wowote kwenye maduka mbalimbali yaliyopo kwenye malls tofauti nchini. Baadi ya maduka ni kama ifuatavyo kwa Dar es salaam: Mlimani city (Mr Price, Just Fit sports gear, Atsoko, Cassandra Julac, Joo Africa na Vodashop Mlimani, Dar Free Market (Home of events, Zurii house of beauty, Vodacom service desk) City Mall (Kanzu Point, Ley Jewerly, G Best Zone), Rock City Mall Mwanza (Street Soul, Chief Empire Classic, Café Mambo, Upendo Unique beauty shop na Vodashop Rock City) na Aim Mall Arusha (Street Soul, Supa Clean) na mengine mengi. Wauzaji pia watatoa punguzo kabambe la Black Friday. 

Meneja uendeshaji wa Mr Price Tanzania Paul Namuhisa alisema ‘Tunafurahi kushirikiana na Vodacom katika kampeni hii. Pamoja na punguzo la hadi asilima 10 ukinunua bidhaa kupitia M-Pesa, Tunatoa punguzo la asilimia 20 kwa manunizi ya bidhaa kwa siku hiyo, huu ni muendelezo wa utamaduni wetu wa kuleta kitu kipya kwa wateja wetu kila siku’


Kwa Upande mwingine, Vodacom kwa ushikiriano na Easybuy Africa itawarudishia wateja hadi asilimia 10 ya kiasi watakacholipa kwa M-PESA MASTERCARD kupitia tovuti ya www.easybuyAfrica.com. Wateja watarudishiwa hadi asilimia 10 wakifanya shopping kutoka mitandao kama Amazon.com, eBay, H&M, Walmart, GAP, Fashionova n.k kupitia EasyBuyAfrica.com na kulipa kwa M-PESA MASTERCARD. Pia watafurahia punguzo la hadi asilimia 10 ya oda zao kutoka EasyBuy pamoja na discount za hadi asilimia 85 kutoka tovuti husika siku ya BlackFriday.

Meneja wa Easybuy Africa, Juliana Siyame alisema, ‘Easybuyafrica inawezesha wateja kununua bidhaa yoyote wanayohitaji kutoka mitandao tofauti duniani na kuwaletea popote walipo Tanzania. Kipindi hiki cha Black Friday tunawawezesha kufurahia huduma zetu kukiwa na punguzo kubwa kwenye bidhaa tofauti pamoja na ofa maalum ya 10% discount wakiagiza nasi ijumaa hii tarehe 29. Ushikiriano wetu na M-Pesa Mastercard umeaongeza faida zaidi kwa wateja wetu kwa kuwapa njia salama ya kulipa mtandaoni’

Wateja ambao bado hawana M-Pesa Mastercard wanaweza kutengeneza kadi zao kwenye menyu ya M-Pesa kwa kupiga *150*00# >Chagua Lipa kwa M-Pesa > Chagua M-Pesa Mastercard kisha > Tengeneza Kadi. Baada ya hapo watapata namba ya kadi, code ya CVV na tarehe ya mwisho wa matumizi, taarifa zinazohitajika kwenye malipo mtandaoni.


AWESO AWATAKA WENYEVITI WAPYA WA VIJIJI,VITONGOJI WASIGEUKE KUWA WAUZA ARDHI BADALA YAKE WAWATUMIKIE WANANCHI

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso na Naibu Waziri wa Maji akizungumza na wananchi Kata ya Kipumbwi wilayani humo ambapo aliwataka wevyeviti wapya kuhakikisha wanachochea kasi ya maendeleo kwa wananchi wa
MWENYEKITI wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah akizungumza 
MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia akizungumza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah
KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akizungumza
MBUNGE wa Jimbo Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji katika akikata utepe kushiria ufunguzi wa tawi la kikoba la Jipe Moyo la Pangani kulia ni Mwenyekiti wa CCM Pangani Rajabu Abdallah
MBUNGE wa Jimbo Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji akicheza pamoja na wenyeviti wapya waliopita wilayani Pangani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa

Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Pangani(CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji
MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso amewataka wenyeviti wa Vijiji, vitongoji na mitaa waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita wasiwe chanzo cha migogoro kwa wananchi kwa kugeuka wauza ardhi bali wahakikishe wanashirikiana nao kutatua kero zinazowakabili.

Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji aliyasema wakati mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani ambapo alisema lazima watambue dhamana kubwa walioibeba ni kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuchochea maendeleo kwenye maeneo yao.

Alisema kwamba wananchi wanataka maendeleo ndio maana wamewachagua hivyo wanajukumu kubwa la kutekeleza hayo kwa vitendo ikiwemo kutetea maslahi yao pindi wanapokumbana na changamoto mbalimbali.

“Unapokuwa kiongozi lazima utetee maslahi ya wananchi wako pia utembue changamoto zinazowakabili hapa kipoumbwi asilimia kubwa wananchi shughuli zao na uvuvi hivyo Mwenyeviti mpya wa hapa kuwa imara kusimamia wavuvi waweze kuvua kwa usalama wapate ridhiki yao ya halali”Alisema Aweso.

Mbunge huyo pia aliwaambie wananchi kwamba hakuna demokrasia yoyote ya kutafuta viongozi kwenye Taifa hili zaidi ya uchaguzi hivyo vikiwemo kuwataka iongozi ambao wamepatikana watambue kwamba wana kipumbwi na wana Pangani wanahitaji maendeleo na sio jambo jingine.

Hata hivyo pia aliwataka pia hakikisha kila baada ya miezi mitatu wanasoma mapato na matumizi huku akiwaambia kwamba sio wakati ukiwa umefika hata simu zao hazipatikani kwa kuwaeleza huo utakuwa sio uoingozi.

“Wapo watu wamewaaminisha watu kwamba CCM ikiingia hapa Kipumbwi watateseka hawataleta maendeleo…lakini wapo watu wanasema baada ya CCM kuingia hapa eti boti zitafukuzwa hafukuzwi mtu hapa “Alisema Mbunge huyo.

Mbunge huyo aliwataka viongozi hao kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuwapa maendeleo wananchi hao maana hawana wenyeviuti wengine zaidi ya nyie.

“Eneo la Kipumbwi ni eneo lenye mapato makubwa watu wanataka kupata maendeleo leo sizije fedha zinakusanywa nyingi lakini hata choo cha kujisaidia hakuna hakikisheni mnabadika sasa”Alisema

DKT. CHAULA AFUMUA MFUMO WA UONGOZI WA VYUO VYA MAFUNZO VYA AFYA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akifungua Mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya 37 vilivyo chini ya wizara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtumba, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa vyuo vya Afya vilivyo chini ya wizara wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Katibu mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula (hayupo kwenye picha)wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya 37 vilivyo chini ya wizara ya Afya.
Prof. Andrea Pembe, wakwanza kushoto akiwa na baadhi ya Wakuu wa vyuo vya Afya na baadhi ya Viongozi katika Sekta ya Afya wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya 37 vilivyo chini ya Wizara ya Afya, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtumba, Jijini Dodoma.

Wakuu wa Vyuo vya Afya 37 pamoja na baadhi ya viongozi katika Sekta ya Afya, wakifuatilia taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, wakati wa mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtumba, Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu Dkt. Saitore Laizer (wakulia) akiwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Edward Mbanga katika mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya 37 vilivyo chini ya wizara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtumba, Jijini Dodoma.

**************************************

Na WAMJW-DOM

Katibu mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula amefumua mfumo wa uongozi katika vyuo vya Afya nchini na kuunganisha vyuo vyote vilivyokaribu na hivyo kufanya vyuo kupungua idadi kutoka vyuo 37 hadi kufikia vyuo 9, hali itayosaidia matumizi mazuri ya rasilimali chache zilizopo katika kuzalisha rasilimali watu.

Hayo yamejiri wakati wa mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya 37 vilivyo chini ya wizara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtumba, Jijini Dodoma.

“Wizara imeona ili kuboresha utoaji taaluma katika vyuo vyake ni vyema kubadilisha mfumo uliopo wa kuendesha vyuo vidogovidogo na kutengeneza mazingira ya kuwa na vyuo vikubwa vichache vyenye mfumo mzuri wa kiuongozi ili kuzalisha Wataalamu sahihi”, alisema.

Dkt. Chaula amesema kuwa, lengo la mkutano huo ni kupanga jinsi ya kuboresha taaluma ndani ya vyuo vya Afya nchini ili kutoa Watumishi bora zaidi jambo litakalosaidia kupunguza vifo visivyokuwa vya lazima kwa kiasi kikubwa.

Mbali na hayo Dkt. Chaula amesema kuwa, mfumo bora wa utawala vyuoni ni muhimili mkubwa na wa msingi katika kuhakikisha mafunzo bora yanatolewa katika vyuo vyetu na wahitimu wanaozalishwa kutoka vyuo hivyo wana umahiri unaokusudiwa katika kutoa huduma za Afya kwa wananchi.

Aliendelea kusema, Wizara imekiri kupokea changamoto za uendeshaji wa mafunzo vyuoni, ikiwemo uchache wa watumishi vyuoni, vifaa vya kufundishia, viwango vya ubora wa wahitimu kushuka, huku akisisitiza mabadiliko ya mfumo wa uongozi yatakuwa chachu ya utatuzi wa changamoto hizo.

Mbali na hayo, Dkt. Chaula amewaasa Viongozi wapya kushughulikia changamoto ya malalamiko kutoka kwa wazazi na wanafunzi wanaosoma vyuoni ikiwemo kukosa kwa baadhi ya haki zao, hali iliyopelekea kwa baadhi ya vyuo kupoteza uaminifu kwa wanafunzi na wazazi.

Nae, Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasiliamali Watu Dkt. Saitore Laizer ametoa wito kwa Wakuu wapya wa vyuo hivyo kufanya kazi kwa ushirikiano baina yao, jambo litalosaidia matumizi mazuri ya rasilimali chache zilizopo katika kuzalisha rasilimali watu.

TCRA YAKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA

$
0
0

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero (mwenye miwani) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaha Chrisdome Ambilikile hati ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) viliyotolewa na TCRA katika hafla kiliyofanyika shuleni hapo Kibaha mkoani Pwani.
Mwakilishi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani ,Katibu Tawala Msaidizi Abdulahman Mdimu akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) vilivyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa Shule ya Sekondari Kibaha iliyofanyika shuleni hapo Kibaha mkoani Pwani.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero akizungumza kuhusiana na vigezo vilivyotumika TCRA kutoa vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama)katika Shule ya Sekondari Kibaha.
Mkuu wa Shule ya Sekondari wa Kibaha Chrisdome Ambilikile akizungumza kuhusiana na msaada wa vifaa vya Tehama katika shule hiyo katika hafla ilyofanyika shuleni hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Fredrick Ntobi akitoa maelezo kuhusiana na utaratibu wa utoaji wa vifaa vya Tehama kwa Mamlaka hiyo katika shule ya Sekondari.
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Kibaha Samuel Makoye akitoa maelezo kuhusiana na msaada wa vifaa vya Tehama waliopewa katika shule hiyo.
Picha kati ya TCRA,Wanafunzi ,Walimu pamoja na viongozi wa serikali Mkoa wa Pwani 

************************************

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)imesema kuwa itaendelea kusaidia vifaa mbalimbali vya Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kwa shule za sekondari zinazofanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kitaifa ili kuweza kuwaanda vijana kuendana na mabadiliko ya sayanasi na teknolojia .

Akizungumza na mara baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya Tehama Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka, Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa vifaa vya Tehama wanavitoa kwa shule zinazofanya vizuri katika matokeo kidato cha Nne na Tano ambapo ni Kibaha sekondari ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri .

Amesema kuwa vifaa hivyo vitachochea shule hiyo kuendelea kufanya vizuri kwani vitabu mbalimbali vinapatikana katika mitandao ikiwemo na marejemeo mengineyo kwani dunia ndio inakwenda huko.

“Hatutarajii kuona vijana wetu mnatumia vifaa vya Tehama kinyume sheria kwani sheria mtandaoni imeanisha makosa hivyo wanafunzi mtakuwa watu wa kutumia Tehama katika maendeleo ya kufanya vizuri kwa kuendeleza rekodi ya shule ya sekondari Kibaha”amesema Odiero.

Nae Mgeni rasmi Mwakilishi wa Matibu Tawala wa Mkoa Abdulahman Mdimu amesema kuwa wanashukuru kwa msaada waliotoa TCRA na wanafunzi kutunza vifaa hivyo.

Amesema kuwa shule ya Sekondari Kibaha kutokana na kupata kigezo cha kupata vifaa vya Tehama kuongeza juhudi zaidi kwani kuna shule shindani nazo zinahitaji vifaa hivyo.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaha Chrisdome Ambilikile amesema kuwa kutokana na kukua kwa Tehama sasa tunatakiwa kuondokana mfumo wa ufundishaji wa vitabu na daftari ambapo nchi zingine zilishaanza ufundishaji huo.

Amesema kuwa shule inajenga jengo kubwa pamoja na kuweka vyumba vya Tehama ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi waliopo katika shule hiyo na kuongeza kuwa TCRA kuendelea kuingalia shule hiyo kwa jicho linguine kwa kuwaongeza vifaa vvya Tehama.

Mwanafunzi wa Kidoto cha Sita Samuel Makoye amesema kuwa dunia ya sasa imekwenda na mabadiliko mbalimbali ya ya Tehama ambapo wanafunzi lazima tufuate tekonolojia hiyo.

kwani kutumia tofauti na matarajio ni hasara kwani na mtakuwa

MADEREVA BAJAJI, BODABODA WAELEZA SABABU KASI MAAMBUKIZI VVU

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

KATIKA kuelekea maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yatakayofanyika Desemba Mosi mwaka huu jijini Mwanza na kubeba kauli ya, "Jamii ni Chachu ya Mabadiliko, Tuungane Kupunguza Maambukizi Mapya ya VVU." vijana mbalimbali wametoa maoni yao juu ya kasi ya maambukizi hayo hasa kwa vijana wa miaka 15 hadi 24 ambapo kwa mujibu wa tafiti asilimia 50.2 ya kundi hilo wameathirika na wanatambua hali zao huku wanawake wakiwa na maambukizi mara nne zaidi ya wanaume wa umri huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti madereva wa pikipiki maarufu Kama bodaboda katika kituo cha Tandamti Kariakoo jijini Dar es Salaam wamesema kuwa kasi ya maambukizi hayo inatokokana na ufinyu wa elimu kwa vijana ambapo wengi bado hawajatambua athari za kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

" Lazima vijana tutambue athari za kupata VVU lakini vijana wengi hatuna mawazo hayo, hatuna nafasi ya kupima afya kabla ya kukutana na wenza wetu hata wanawake wenyewe hawana ushawishi kuhusiana na matumizi ya Kinga, mwanaume asipokumbuka ndio basi tena na ni rahisi sana kumshawishi mwanamke kufanya mapenzi bila kutumia Kinga tunaamini kwa kuona jambo ambalo si salama kwa afya zetu" ameeleza mmoja wa dereva huyo ambaye hakutaka jina lake lichapwe.

Kuhusiana na kasi ya maambukizi kwa kundi la vijana walio na umri wa Mika 15 hadi 24 madereva hao wasema kuwa elimu zaidi kwa kundi hilo iendelee kutolewa ili kuwaokoa na hiyo ni kutokana changamoto na ushawishi wa hali ya juu wanaokutana nao.

"Bodaboda tumekuwa tukituhumiwa sana kwa kuharibu wanafunzi ila kwa hali ilivyo inaonekana wanafunzi hawapati elimu ya afya na UKIMWI na imekuwa rahisi kuwashawishi kwa vitu vidogo kama kuwapa lifti na vijisenti kidogo" ameeleza.

Vilevile Imani Charles dereva wa Bajaji Mbezi mwisho jijini humo amesema kuwa elimu pekee ndio itakayopunguza kasi ya maambukizi hayo hasa kwa watoto wa shule ambao wanatakiwa kufahamu madhara ya maambukizi hayo ili waweze kujikinga zaidi.

Imani amesema kuwa vijana wengi wa umri wa miaka 15 hadi 24 wameshaanza kushiriki ngono zisizo salama na wanaume tofauti hali inayochangia kasi ya maambukizi ya VVU, hivyo ni vyema Serikali na Mamlaka husika kutoa elimu ya nadharia na vitendo ili kuweza kupunguza kasi ya maambukizi hayo.

Tafiti zilizofanyika mwaka 2016/2017 zinaonesha kuwa watu 7200 hupata maambukizi mapya kwa mwaka ambapo kwa mwezi watu 6000 hupata maambukizi hayo kwa mwezi huku watu 8 hupata maambukizi hayo kwa siku huku kundi la vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 ambao hupata maambukizi hayo kwa mwaka yamefikia asilimia 40.

AKINA MAMA WAJASIRIAMALI WAMUOMBA RC MAKONDA KUINGILIA KATI BEI YA HUDUMA YA CHOO MBEZI MWISHO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

AKINA Mama wanaofanya biashara ndogondogo katika kituo cha magari cha Mbezi Mwisho  jijini Dar es Salaam wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuingilia kati bei ya huduma ya choo cha umma kwa kile wanachodai kuwa gharama ya huduma hiyo ipo juu sana ukilinganisha na maeneo mengine.

Wakizungumza na Globu ya jamii baadhi ya akina mama hao ambao wanafanya biashara ndogondogo ikiwemo kuuza karanga na matunda wameeleza kuwa gharama ya huduma ya choo kituoni hapo ni shilingi miatano tofauti na maeneo mengi ambayo hutoza shilingi mia mbili pekee.

"Tulitegemea hizo fedha wanazokusanya zingesaidia hata kuboresha maeneo yetu ya kufanyia biashara, tunahamishwa tuu, angalia tunakaa chini Serikali na Mkuu wa Mkoa Makonda watusaidie" ameeleza mmoja wa akina mama hao.

Vilevile baadhi ya madereva na makondakta wa daladala kituoni hapo wamesema wamekuwa wakitumia chupa za maji kwa kuhifadhi haja ndogo ili kuepuka gharama hiyo.

"Tunamwomba Mkuu wa Mkoa Paul Makonda asaidie hilo kwani mazingira yanachafuka kwa vitu ambavyo vinaweza kudhibitiwa" ameeleza mmoja wa dereva anayefanya safari za Mbezi mwisho kwenda Temeke.
Muonekano wa choo cha wanawake kilichopo kituo cha magari Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy Atoa Maagizo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akizungumza chimbuko wa siku 16 za Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia katika uzinduzi uliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Wanawake (UN-Women) Hodan Addou akieleza mchango wa shirika hilo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia wakati wa uzinduzi wa siku 16 za Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.
Mratibu wa Kitaifa wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) Anna Meela Kulaya akieleza jinsia Shirika lake linavyoshirikiana na Serikali katika kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili katika uzinduzi wa siku 16 za Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi kutoka Shule za Sekondari za Mkoa wa Dodoma wakiwa katika uzinduzi wa siku 16 za Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.
Msanii Barbabas Classic akitumbuiza katika uzinduzi Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja wanafunzi wa moja ya shule ya Sekondari ya Dodoma mara baada ya uzinduzi wa siku 16 za Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii kusimamia uanzishwaji na uendeshwaji wa Kamati za ulinzi wa wanawake na watoto katika mikoa na Halmashauri ambazo hazijaanzishwa ili kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia hadi ngazi ya Kata na Vijiji. 

Akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsi leo Jijini Dodoma, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli imetekeleza kwa vitendo azma ya kukomesha vitendo hivyo. 

Waziri Ummy ameongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na asasi za Kiraia katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa Kijinsia katika maeneo yote hapa nchini. 

Aidha, Mhe Ummy ameagiza kuanzishwa kwa Madawati ya Jinsia Katika Taasisi za Elimu ya Juu ili kukomesha vitendo vya rushwa ya ngono na ukatili mwingine kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu. 

Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa madawati ya Jinsia na Watoto katika Vituo vya Polisi yapatayo 420 yamewezesha wahanga 58,059 kuripoti aina mbalimbali za matukio ya ukatili wa kijinsia kwa rika mbalimbali wakiwemo watu wazima na watoto katika matukio ya ubakaji, ulawiti, vipigo na ukeketaji. 

Akizungumzia faida za madawti hayo Waziri amesema kuwa yameongeza mwamko wa wananchi katika kujiamini na kutoa taarifa za ukatilii unapotokea kwenye maeneo yao. 

Kuongeza vituo vya Mkono kwa Mkono vya Kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa Kijinsia (One Stop Centres) kutoka vituo 10 mwaka 2017 hadi 13 mwaka 2019 ili kiwezesha utoaji wa huduma rafiki na kwa haraka kwa wahanga. Hatua hiyo inapelekea Serikali ya Awamu ya Tano kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuendelea kutekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto 2017/2018- 2021/2022 ambao unalenga kupunguza kiwango cha ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Jamii yetu kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022. 

Kauli mbiu ya Kampeni ya siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa mwaka huu ni “Kizazi chenye Usawa: Simama Dhidi ya Ubakaji” kauli mbiu hii inawapa jukumu wananchi wote kutafakari wajibu wao kama kizazi kinachoamini na kuthamini usawa wa kijinsia. 

Kauli mbiu hii inatoa msukumo wa kuhakikisha kila mtu katika nafasi yake anapaza sauti na kuchukua hatua ya kuzuia na kutokomeza vitendo vyote vya ukatili wa kingono hasa ubakaji na matendo yote ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika nyumba na mahali pa kazi na katika taasisi mbalimbali ikiwemo shule na vyuo mbalimbali. 

Aidha, Serikali inapinga vikali mila, desturi na imani zote zenye madhara kwa jamii kama ukeketaji, kukatisha watoto wa kike shule kwa ajili ya kuolewa. 

Kwa upande wake Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake Bi Hodan Addou amesema kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia kwa makundi yote ili kujenga jamii yenye usawa. 

Pia alipongeza juhudi za Serikali katika kuhakikisha inakomesha vitendo hivyo kupitia mpango mkakati wake na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo. 

Aliongeza kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ni tatizo la kidunia linalohitaji jitihada za pamoja katika kulikomesha. 

Uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia umefanyika Jijini Dodoma na umefanywa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na kuhudhudhuriwa na Asasi zisizo za kiserikali, viongozi wa Serikali, Mashirika ya Umma pamoja na Viongozi wa Dini. 

MKUTANO WA 39 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC KUANZA KESHO JIJINI ARUSHA

$
0
0
Makatibu Wakuu Jumuiya ya Afrika Mashariki wakijadili jambo wakati wa Mkutano wao. Kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Afrika Mashariki – Uganda, Bibi. Edith Mwanje, akifuatiwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki – Tanzania, Dkt. Faraji Mnyepe. Wengine ni Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara, Viwanda na Masula ya EAC – Sudani Kusini, Bw. Mou Mou Athian Kuol, akifuatiwa na Meja Generali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa – Uganda, Balozi Charles Karamba. Wengine pichani ni Katibu Mwandamizi, Wizara ya Afrika Mashariki na – Kenya, Dkt. Margaret Mwakima na katibu Mkuu, Office ya Rais Inayohusu masula ya Afrika Mashariki – Burundi, Balozi Jean Rigi
Makatibu Wakuu Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano wao (Ngazi ya Makatibu Wakuu) uliomalizika leo jijini Arusha. 





Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano katika ngazi ya Makatibu Wakuu uliomalizika leo Jijini Arusha
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akiwasilisha mada kwa Makatibu wakuu (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa Makatibu wakuu wa EAC Jijini Arusha

………………..

Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unatarajiwa kwanza kesho tarehe 27 Novemba 2019 jijini Arusha.

Kuanza kwa mkutano huo kunafuatia kukamilika kwa Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ulioanza tarehe 25 na kumalizika tarehe 26 Novemba 2019.

Mkutano wa Makatibu Wakuu pamoja na mambo mengine, umejadili masuala mbalimbali ya utekelezaji ya jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa mapendekezo kwa mkutano wa ngazi ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta zinazohusiana na Jumuiya hiyo utakaoanza tarehe 27 Novemba 2019.

Mkutano huu wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umeandaliwa kwa lengo la kujadili na kukubabaliana na agenda zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Februari, 2020.

NYAMA YA NGURUWE TISHIO KWA WALAJI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi TV,Arusha


Minyoo ya Tegu ya Nguruwe (cysticercodis) imekuwa tishio kwa walaji Wa
nyama ya mnyama huyo na kupelekea kusababisha maradhi makubwa kwa binadamu kama ugonjwa Wa kifafa.

Hayo yamebainishwa na Naibu Wa afya Faustin Ndugulile wakati akifungua
mkutano Wa kwanza Wa kimataifa Wa kujadili minyoo ya Tegu Wa nguruwe
katika thana ya Afya ya pamoja unaofanyika katika ukumbi Wa Mounti Meru Arusha.

Mkutano huo umefanyika Leo November 26 ambapo alisema kuwa kwa wale
walaji Wa Nyama ya Nguruwe kunaminyoo ambayo iko katika nyama huyo
kupitia mayai yanayopatikana ndani ya inaweza kumuathiri binadamu
endapo atakula nyama ambayo ijapikwa vizuri pamoja na mbogamboga
ambazo azijaoshwa pamoja nakupikwa vizuri.

Alisema athari zinazoweza kupatikana katika mnyama huyu ni kubwa ikiwemo kupata ugonjwa Wa kifafa , na tatizo hili limeshaingia katika nchi yetu na limeanza kuathiri zaidi katika mikoa ya Manyara,Njombe, Mbeya ,Sogwe ,Mbeya pamoja na mkoa Wa Arusha na asilimia 16%ya wananchi wanaoishi mikoa hii wameshaathirika na ugonjwa huu.

"Lengo kubwa kuweka mkakati Wa pamoja Wa jinsi gani tunaweza kutokomeza ugonjwa huu Wa minyoo Wa Tegu Wa Nguruwe,nanianze kutoa rai kwa wafugaji Wa Nguruwe kufuga kisasa na kuacha wanyama wao kuzurura hovyohovyo kwani anavuozurura ovyo anaeza kuacha kinyesi chenye mdudu huyo katika mboga na pia wapate ushauri sahii wawataalamu Wa mifugo Wa namna ya kufuga mnyama
huyo ,pia wale wachinjaji Wasifanye uchinjaji Wa mnyama huyu bila
kizingatia utaalamu na msingi wawataalam wanaosimamia wanyama hao,aidha pia nitoe rai kwa wale wanaokula mnyama huyu kuhakikisha kwamba kimepikwa vizuri na sio mnakula nyama yenye damu damu yaani ile mbichimbichi kwani inaweza kukuletea mathara
 " alisema

Alibainisha kuwa hadi sasa serikali yetu haijapata chanjo kwa ajili ya
kumzuia mnyoo huyo wa nguruwe na ipo katika utafiti wakuangalia namna ya kumthibiti,lakini pia tunaweza kuzuia kwa kuakikisha kuwa tunafuga bila mifugo yetu kuzagaa,pia kwa wale tunaochinja tuhakikishe tumewapima mifugo yetu kwanza bila ya kuwachinja

Kwa upande wake mkuregenzi mkuu wa Taasisi ya magonjwa ya binadamu
(NIMR)Prof Yunus Mgaya wanatekeleza mradi huu kwa kusanya taarifa za
kutosha kuhusiana na minyoo huyu wa Tegu ambaye anapatikana kwa kula
mbogomboga ambazo zimebeba mayayi yaliotokana na vinyesi vya nguruwe au kinyesi cha binadamu

“mradi huu unatekelezwa na nchi zingine mbili afrika ambazo ni Mozambiq
pamoja Zambia na tunashirikiana na wadau wetu wa utafiti wa ujerumani
kutoka chuo kikuu cha Munchen ,mradi huu umetuwezesha kununuavifaa vya maabara kwa ajili ya kuweza kufanya utafiti wetu vizuri kwa kiwangoncha juu ,pia umetusaidia kuwapeleka vijana wetu kwenda kupata elimu katika shaghada zauthamini PHD, lakini mradi huu umetuleta pamoja nchi hizi za Afrika na lengo kubwa ikiwa ni kutokomeza au kuzuia watu wasipate ugonjwa huu unaotokana na minyoo hii ya Tegu ”

Naye Kaimu mkuu wa idara ya tiba ya mifugo na afya ya jamii ambaye pia ni
mkurugenzi wa mtandao wa utafiti wa kisayansi Prof,Helena Ngowi alisema
kuwa mnyoo ni hatari sana kwa sababu anaweza kuleta adhari kubwa katika
utumbo wa binadamu hadi katika ubongo wa binadamu ,anaamini bila ya kuwa na mfugo alie athirika binadamu hawezi kupata ugonjwa huu,pia tafiti hizi zilianza kufanyika tangu mwaka 199 na bado zinaendelea na kiwango cha tatizo kimeshajulikana ,tunashirikiana kwa lengo la kushirikiana katika
kupambana na tatizo hili kwa sababu hazina mipaka ,kwa ivyo
tunavyoshirikiana na nchi hizi zingine tunaweza kutokomeza kabisa tatizo
hili pia tutashirikisha jamii ili tuweze kutokomeza .

  Naibu Wa  afya Faustin Ndugulile wa kwanza kushoto katikati ni mkuregenzi mkuu wa Taasisi ya magonjwa ya binadamu (NIMR)Prof  Yunus Mgaya wakifatilia  mada zilizokuwa zikiendeshwa katika mkutano za namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Tegu la nguruwe
Prof kutoka nchi ya Canada Helene Carabin akitoa mada katika  mkutano huo





WATANZANIA WATAKIWA KUJIKITA KATIKA KILIMO HAI NA KUACHA KILE CHA KEMIKALI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii-Dodoma

WAZIRI wa Kilimo na Chakula Japhet Hasunga amesema umefika wakati kwa Watanzania kujikita katika kilimo hai kwani kuna ardhi ya kutosha na kilimo hicho kikifanikiwa nchi itakuwa imepunguza gharama kubwa ya uzalishaji unaotokana na kilimo kinachotumia kemikali huku akisisitiza Serikali itashirikiana na wadau kuhakikisha chakula kinacholiwa kunakuwa salama .

Pamoja na mambo mengine Waziri Hasunga amesema Serikali inatambua umuhimu wa kilimo hai nchini na kwamba katika mabadiliko makubwa ya sekta ya kilimo kuna mchakato wa kutungwa kwa sheria ya kilimo ambapo kilimo hai kitapewa kipaumbele na msukumo mkubwa.

Waziri Hasunga ameyasema hayo leo Novemba 26 mwaka 2019 wakati anafungua Kongamano la Kimataifa ambalo limewakutanisha wadau wa kilimo hai ndani na nje ya Afrika ambapo ametumia nafasi hiyo kutoa maelezo ya kina kuhusu kilimo hicho huku akiwataka Watanzania kujihusisha nacho.

Amesema kongamano hilo limekuja wakati muafaka kwasababu Wizara iko katika mabadiliko hayo makubwa yakiwemo ya mkachakato wa kutunga sheria inayohusu sekta ya kilimo.

"Watanzania kila siku wanaongezeka na hivyo lazima kuwe na uhakika wa kuzalisha kilimo cha uhakika, kabla ya miaka mitano hii kumalizika lazima tuwe na sheria ya kilimo ambayo mbali ya kujadili mambo mengine itajikita pia katika kukiendeleza kilimo Kilimo hai,"amesema.

Ameongeza katika mabadiliko makubwa ambayo yanafanyika ndani ya Wizara hiyo pia Wizara itakuwa na kanzi data ambayo itawatambua wakulima wote nchini na aina ya kilimo wanachofanya tofauti na sasa kila mtu anajiita mkulima na Serikali haijui analima nini.

Amesisitiza Serikali inatambua umuhimu wa kilimo hai nchini Tanzania. "Nawapongeza Taasisi ya Kuendeleza Kilimo Hai Tanzania (TOAM) kwa kazi mnayofanya katika kuendeleza kilimo hai. Nitumie nafasi hii kukushukuru Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) linavyowekeza katika kilimo hai ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti."

Hata hivyo amesema mazao ya kilimo hai yanasoko kubwa Duniani na Tanzania haiwezi kujiweka nyuma,hivyo nayo inakila sababu ya kujikita katika kilimo hicho kisichotumia kemikali. Amesema kuna faida nyingi za kilimohai likiwemo soko la uhakika kwani mahitaji ni makubwa na hiyo inatokana na ukweli uliopo vyakula vitokanavyo na kilimo hicho havina madhara ya kiafya tofauti na mazao ya kilimo kinachotumikia kemikali ambacho kimesababisha magonjwa mengi kiafya.

Hata hivyo amesema kwamba amemsikia Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge kutaka kuwepo na Idara maalumu ambayo itajihusisha kusimamia kilimo hai nchini ambapo katika hilo amesema hayo kwake ni maagizo na hivyo si kuanzisha Idara bali kuwa na Kurugenzi itakayokuwa na mamlaka kamili.

"Kwa kutambua umuhimu wa kilimo hai Serikali kupitia Wizara ya Kilimo tutaweka mikakati wa kukiendeleza kilimo hai ambacho mbali ya mazao yake kuwa na soko,kinafaida kubwa kiafya.Katika Dunia ya sasa eneo la chakula ni muhimu kuwa na uangalizi kwani watu wanaweza kutumia chakula kuwamaliza wananchi.Hivyo Serikali iwe makini kwa kuhakikisha chakula tunachozalisha kinakuwa cha uhakika na hili ni jukumu letu,"amesema Waziri Hasunga

Amesisitiza kwa mkakati ambao Serikali imeuweka katika kilimo hai wanaamini nchi ya Tanzania itakuwa kati ya nchi zitakazokuwa zinazalisha law wingi chakula kinachotokana na kilimo hai.

Amezungumzia umuhimu wa ubora na usalama wa mbegu nchini kwa kuhakikisha Hazina madhara kwa walaji huku ukitumia nafasi hiyo kueleza hakuna sababu ya wakulima kutumia mbolea ya kiwandani kama ardhi inajitosheleza law hotuba.

Kwa upande wake Rais wa Kilimo Hai Afrika ambaye pia ni Rais waTaasisi ya Kuendeleza Kilimo hai Tanzania (TOAM) Jordan Gama amesema pamoja na mambo mengine kongamano la wadau hao wa kilimo hai unalenga kujadili kwa kina changamoto na mafanikio yaliyopo.

"Dhumuni la kongamano hili litakalofanyika kwa siku mbili ni kuwaleta wadau mbalimbali wakiwamo watunga sera, wasimamia sheria,kanuni na miongozi, wanasiasa, watoa uamuzi, wazalishaji, wanunuzi pamoja na wadau wengine kutumia nafasi hiyo kwa kina kujadiliana, kupeana habari na kubadilisha maarifa kuhusu kuendeleza kilimo hai nchini,"amesema.

Pia katika mkutano huo mkuu wa wadau wataangalia kwa kina kuhusu kilimo hai kwa Tanzania , Afrika na Duniani kwa ujumla ili kuhakikisha kunakuwa na uzalishaji wa mazao kupitia kilimo hicho ambacho kimsingi kina mafanikio mengi makubwa na wakati huo huo kunachangamoto zake.

Amesema baada ya majadiliano, wadau hao watatoka na mapendekezo ambayo yatapelekwa kwa Serikali kwa ajili ya kupata mfumo mzuri wa kuendeleza kilimo hai nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mahmoud Mgimwa amesema kuwa kwa niaba ya wabunge wanashukuru kupata fursa ya kushiriki katika kongamano la kilimohai na kwamba wao ndio mara yao ya kwanza kushiriki.

Hata hivyo amesema sera ya kilimo hai ipo lakini hakijafanikiwa vya kutosha na ni amani yao Waziri wa Kilomo na Chakula atatoa muelekeo mzuri kuhusu kilimo hicho na kufafanua kuwa ndani ya Wizara ya kilimo hakuna Kitengo rasmi cha kilimohai.

Amesema kilimo hai kinafaida kubwa na kwamba ni matarajio yao Serikali itaangalia namna nzuri ya kuendeleza kilimo hai na kwamba wakulima zaidi ya 200,000 wanajihusisha na kilimo hicho kisicho na shaka,hivyo inahitajika mkakati madhubuti huku akifafanua pamoja na faida za kilimo hicho bado Serikali imekuwa kimya.

'Kupitia mkutano huo , wabunge tunatoa ombi kwako Waziri wa Kilimo na Chakula kuwekeza katika kilimo hai.

Amesema kna nchi kama India wameamua kujikita katika kilimo hai ambacho.mazao yake ni salama na Bora kiafya na hivyo tukiwekeza katika kilimo hicho hata magonjwa yatapungua,"amesema.

Mmoja wa Champion wa TOAM Dk.Mwatima Juma ambaye amejikita katika kilimo hai amefafanua kuwa Taasisi ya TOAM ilianzishwa mwaka 2005 kwa kushirkisha wadau mbalimbali katika kuangalia kilimo hicho katika mnyororo wa thamani wa mazao yatokanayo na kilimo hicho.
 Waziri wa Kilimo na Chakula, Mhe Japhet Hasunga akiwa kwenye mabanda ya maonesho katika kongamano la kilimo jijini Dodoma leo.
 Waziri wa Kilimo na Chakula, Mhe Japhet Hasunga akizungumza na washiriki wa kongamano la kilimo hai lililofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
 Wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi wakiwa wamejitokeza katika kongamano la kilimo hai lililofanyika jijini Dodoma leo na kuhudhuriwa na Waziri wa Kilimo na Chakula, Japhet Hasunga.
Champion wa TOAM, Dk Mwatima Juma akielezea umuhimu wa kilimo hai katkma kongamano la Kilimo lililofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mahmoud Mgimwa akitoa mchango wake kwenye kongamano hilo la Kilimo hai.
 Mbunge wa Jimbo la Chemba mkoani Dodoma, Juma Nkamia akichangia mada kwenye kongamano hilo

Chunya DC praises Petrobena for early delivery of fertilizers to tobacco growers

$
0
0


From a Correspondent in Chunya.

CHUNYA District looks forward to having increased tobacco harvests in the next season because relevant fertilizers and farm inputs have been delivered to growers well in time by Petrobena East Africa Company. 

The optimism was expressed here yesterday by Chunya District Commissioner, Engineer Mary Prisca Mahundi, when he received cargo of fertilisers and inputs from Petrobena Managing Director Peter
Kumalilwa. The company is a local distributor of Yara products. The company focuses on promotion of cash  and food crops, especially cereals.

The DC praised the company for timely delivery of cargo, saying that company does not only sell products but it also trains farmers on how to use the fertilizers and inputs. Tobacco is the district’s main cash crop, and the DC said an increase in tobacco production has huge impact on the district’s economy and the welfare of residents.

“We commend you for ensuring fertilizers and other inputs reach farmers in time.  Now we have cause to believe that harvests in the coming season will increase and life and livelihoods of growers will be equally enhanced,” she told listeners at the occasion.

Mr Kumalilwa said their company delivered the cargo in fulfilment of its pledged to ensure early delivery of tobacco fertilisers for planting and growth sustenance.  He said fertilisers have already been delivered to all tobacco growing districts on the Mainlandl.


“We have prepared ourselves to contribute steadily and positively to national agricultural reforms and to the agro-industry strategy championed by the fifth phase government by delivering inputs and helping farmers access markets,” he said. He said their company works closely with district and lower-levels leaders to increase agricultural production and remove farming hitches that often demoralise peasants.

DC Chunya aipa tano Petrobena kufikisha mbolea kwa mkulima kabla ya msimu

$
0
0


Na Mwandishi Wetu, Chunya

SERIKALI Wilayani Chunya imepongeza kampuni ya usambazaji mbolea za Yara na pembejeo nyinigne za kilimo ya Petrobena EastAfrica kwa kufanikisha kusambaza mbolea kwa wakati hali ambayo itasaidia kuongeza uzalishaji mazao msimu ujao wa kilimo.

Akizungumza mara baada ya kupokea shehena ya mbolea kupandia nakukuzia tumbaku kutoka kampuni hiyo, Mkuu wa Wilaya hiyo MhandisiMaryPrisca Mahundi alisema kuwasili kwa mbolea hiyo kabla ya msimu niishara njema kuwa wakulima kuweza kuzalisha kwa wingi na kuinua uchumiwa wilaya.

“Napenda kuishukuru kampuni ya Petrobena kwa kuonyesha dhamira ya dhati ya kuinua sekta ya kilimo kwa kusambaza mbolea kabla ya msimuhali inayompa mkulima msukumo wa kufanya uzalishaji,” alisema MhandisiMahundi.

Alisema jukumu lililobaki ni kwa wakulima kuchangamka kununua mboleahiyo ili msimu wa kilimo utakavyoanza wasipate tabu ya mbolea, haliitakayosaidia kuongeza uzalishaji ukilinganisha na misimu iliyopita yakilimo kutokana na uchelewesha wa mbolea.

“Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua katika kukuza uchumi nakuondokana na umaskini hiyo hatua zinazofanywa na wadau kama Petrobenani ishara kuwa azma Serikali inatekelezeka kwa vitendo kwa kuwapatiawananchi mahitaji muhimu katika shughuli zao ikiwemo kilimo,” alisemaDC Mahundi.

Alisema upatikanaji wa pembejeo za kilimo ilikuwa ni changamoto kubwakwa wakulima wa tumbaku katika Wilaya ya chunya,Petrobena imekuwamkombozi katika kuhakikisha mbolea inawafikia wakulima kwa wakati haliitakayochochea uzalishaji wa tumbaku kuongezeka.

“Kuongezeka kwa mavuno ya tumbaku yatapelekea soko la kukua nakufanya uchumi wa Wilaya yetu kuongezeka na kuwa sehemu ya kuchangiapato la taifa,” alisema Mhandisi Mahundi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PetrobenaEastAfrica, Bw.Peter Kumalilwa alisema kuwa kampuni yake imeweka nadhiri kuwa mikoa yote inayozalisha tumbaku itapata mbolea yakupandia na kukuzia kabla ya msimu kuanza ili kuwaondoa hofu wakulima
wa zao hilo.

“Sisi tumejipanga kuhakikisha tunafanikisha mageuzi katika sekta ya kilimo na kuunga mkono azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa kati naviwanda ifikapo mwaka 2025 inafakiwa kwa vitendo,” alisemaBw.Kumalilwa

Alisema mbali ya Chunya Kampuni yake tayari imeshasambaza mbolea yatumbaku kwa ajili ya kupandia na kukuzia katika mikoa mbalimbaliinayolima zao hilo hapa nchini kitu ambacho kitasaidia kuongezauzalishaji na kumsaidia mkulima kuondokana na hali ya umaskini.

“Petrobena itaendelea kufanya kazi kwa karibu na viongozi wa Serikalikuhakikisha kero mbalimbali za wakulima zinatatuliwa kikamilifu natutafanya kazi na wakulima bega kwa bega kuhakikisha wanazalisha kwatija na kuwaunganisha na masoko,” alisema Bw.Kumalilwa
Petrobena imekuwa ikipongezwa maeneo mengi kutokana na umahili na
uzoefu wake wa kusambaza mbolea kabla ya msimu hivyo kuwa mkombozi wakweli kwa mkulima hapa nchini.












Viongozi Wa Serikali Za mitaa Tabora Waapishwa Na Kuonywa Kutojihusisha Na Rushwa

$
0
0
Na, Editha Edward -Tabora

Jumla ya viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji 175 na wajumbe wa mitaa na vijiji wapatao 1520 wameapishwa Leo katika ofisi ya halmashauri ya Manispaa ya Tabora baada ya kuchaguliwa na wananchi huku wakisisitizwa kufanya kazi kwa uadilifu pamoja na kujiepusha na vitendo vya Rushwa ambavyo vimekuwa chanzo kikubwa cha migogoro

Akizungumza katika zoezi hilo la uapishaji Katibu tawala wilaya ya Tabora mjini Hammarkskjola Elisante Amesema viongozi waliyochaguliwa wanatakiwa kuangalia matarajio ya mpiga kura na kufanya kazi kwa haki na usawa

"Unapopata hii nafasi isiwe kigezo cha kumnyanyasa mtu mwingine kwa hiyo nafasi uliyoipata mtu akija na shida yake mtatulie ili aweze kupata haki yake kwa usawa na sii kumzungusha ndo maana halisi na kuchaguliwa na mwananchi"Amesema Elisante.

Kwa upande wake mjumbe kupitia chama cha CCM ambaye pia ni mlemavu wa macho Ahmad Bilayungu amesema nafasi aliyoipata ataitumia kwa kutenda haki bila ya kumuonea mtu yeyote katika utendaji kazi wake 

Aidha wenyeviti wa serikali za mitaa 134 na wajumbe 536 wenyeviti wa vijiji 41 nawajumbe wao ni 984 ambapo viongozi hao wa manispaa ya Tabora wameapishwa na hakimu mkazi wilaya ya Tabora mjini Saraphine Nsana.

Hata hivyo chama cha. Mapinduzi CCM kimeibuka kidedea kwa kushinda nafasi zote za wenyeviti wa mitaa vijiji pamoja na vitongoji kwa manispaa nzima ya Tabora mjini. 
baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa wakiapishwa Leo hii na hakimu mkazi wilaya ya Tabora mjini Saraphine Nsana
katibu Tawala wilaya ya Tabora mjini Hammarkskjola Elisante akizungumza kuhusiana na kuapishwa kwa viongozi hao wa serikali za mitaa.
Mjumbe kupitia chama cha CCM Ahmad Bilayungu ambae pia ni mlemavu wa macho akizungumza baada ya kuapishwa.

VIONGOZI WA MITAA HUDUMIENI WANANCHI BILA UBAGUZI-DAS TABORA

$
0
0
Hakimu wa Wilaya ya Tabora Seraphina Nsana (kulia) akiwaapisha leo Viongozi wa Serikali wa Manispaa ya Tabora waliochaguliwa katika Uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali za Mitaa wa Manispaa ya Tabora wakiwa ya ukumbi wa Manispaa ya Tabora leo wakisubiri kuapisha na Hakimu wa Wilaya ya Tabora.

****************************************

NA TIGANYA VINCENT, TABORA.

VIONGOZI wa Serikali za mitaa waliochaguliwa wametakiwa kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi na kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani ndiyo chanzo cha migogoro.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Tawala Wilaya ya Tabora Hammarskjold Yonaza wakati wa zoezi la kuwahapisha viongozi hao wa mita lilifanyika kwenye ofisi za Manispaa hiyo.

Yonaza alisema kuwa viongozi wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa wakitoa haki bila ubaguzi itasaidia kutimiza ndoto za wananchi waliowachagua za kuwaletea maendeleo na wao kuishi bila migogoro.

Alisema viongozi waliochaguliwa ni vema wakatanguliza maslahi ya waliowachagua na kutimiza matarajio yao ili wazidi kupata maendeleo.

Alisema kama wasipotenda haki ina maana watakuwa wameshindwa kuongoza na kutoa fursa ya kuwepo migogoro kwenye maeneo yao jambo ambalo halikubaliki.

Aidha Katibu Tawala huyo aliwaonya kujiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vinasababisha kuzalisha migogoro katika jamii na kuwatia aibu wao wenyewe pindi watakapobainika.

Kwa upande wa Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Manisapaa ya Tabora William Mpangala alisema kuwa Manispaa hiyo yenye Mitaa 134, wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) 126 walipita bila kupingwa na Mitaa nane ndio iliyofanya uchaguzi pia wagombea wa Chama hicho wameshinda.

Aliongeza kuwa Chama cha Mapinduzi pia kilinyakuwa Viti vyote vya wenyeviti wa vitongoji 41 na vijiji 156 baada ya wagombea wake kupita bila kupingwa.

Mpangala alisema alisema walitoa elimu hiyo kwa viongozi wa ngazi ya wilaya wa Vyama vyote juu ya ujazaji fomu lakini bahati mbaya inaelekea hawakuifikisha kwa wanachama wao ngazi za chini wakiwemo wagombea jambo lilipelekea majina yao kuengeliwa.

Alisema kuwa matokeo ya kutoipeleka elimu hiyo kwa wanachama wao,wengi walishindwa kujaza famu na hivyo kuonekana walishindwa kwa kukosea kuzijaza inavyotakiwa.

Mpangala alivitaka siku za baadaye ,vyama vya Siasa kuhakikisha vinatoa elimu ya uchaguzi kwa wanachama wao wa ngazi za chini ili jambo kama hilo lisitokee katika chaguzi zijazo.

Viongozi hao waliapishwa na Hakimu wa Wilaya ya Tabora,Seraphina Nsana,katika Ofisi za Manispaa ya Tabora.

Viongozi Wateule serikali za vijiji na vitongoji Tandahimba waapishwa

$
0
0
Wateule kwa nafasi mbalimbali za uongozi wa serikali  ngazi ya Kijiji ,vitongoji,Wajumbe mchanganyiko na viti maalum mwaka 2019  wa Wilaya ya Tandahimba wameapishwa leo

Akizungumza  na wateule hao baada ya kuapishwa mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya  Benaya Kapinga aliwaeleza kuwa habari ya siasa inaishia leo kinachofuata ni kufanya kazi 

"Mnatakiwa kwenda kufanya kazi katika maeneo yenu bila kujali itikadi yoyote ya vyama ,dini Wala rangi,kafanyeni kazi wananchi wanataka kuona maendeleo"alisema.

Naye mwezeshaji George Kashura aliwaeleza kuwa wananchi wanataka kujua mapato na matumizi hivyo muwashirikishe wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo

"Mfanye vikao na wananchi  na msome mapato na matumizi ya fedha zinazoletwa kwa ajili ya maendeleo mbalimbali katika ngazi za vijiji na vitongoji,ili wananchi wajue kinachoendelea,"alisema Kashura
 Wateule kwa nafasi mbalimbali za uongozi wa serikali  ngazi ya Kijiji ,vitongoji,Wajumbe mchanganyiko na viti maalum mwaka 2019  wa Wilaya ya Tandahimba wakiapishwa  leo

 Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Benaya Kapinga akitoa neno kwa wateule
 Mwezeshaji George Kashura akisistiza wateule Kusoma mapato na matumizi katika vijiji na vitongoji vyao
 Hakimu Mkazi wa Wilaya Joseph Waruku akiwaapisha wateule

Tumbi kutumia Sanamu kufanya mafunzo ya Afya kwa Vitendo

$
0
0
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afya cha Kibaha (Kibaha College of Health and Allied Science) wakishuhudia hafla ya makabidhiano ya sanamu. 
Mgeni Rasmi, Dkt. Damian (kushoto), Dkt. Msangi anayefuatia, Balozi Anisa na Dkt. Mwande (kulia) wakikata utepe kuashiria kuanza kutumika kwa sanamu kwa wataalamu wa afya katika kufundishia. 
Sanamu aliyebatizwa jin la Msafriri amezinduliwa rami ili watalamu wa afya wamtumie kufanya mafunzo kw vitendo. 
Dkt. Damian akipokea vitabu vya msaada vyenye thamani ya milioni 30 za Kitanzania kutoka taasisi ya TUHEDA. Vitabu hivyo vitasambazwa kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. 
Picha ya Pamoja 
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani (Tumbi, Kibaha), Dkt. Sylas Msangi akitoa neno la ukaribiho katika hafla ya makabidhiano ya Snamu kwa ajili ya mafunzo ya vitendo kwa wataalamu wa afya. Sanamu hilo limetolewa msaada na Umoja wa Wataalamu wa Afya wa Watanzania wanaoishi Uingereza (Tanzania-UK Healthcare Diaspora Asociation-TUHEDA) 
Mwakilishi wa TUHEDA ambaye ni Mtanzania anayeishi Uingereza na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Sukari, Bw. Nasibu Mwande akiongea machache kuhusu umuhimu wa Snamu kwa wataalamu wa afya katika mafunzo kwa vitendo. 
Mkurugenzi wa Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega akitoa maelezo namna Wizara ya Mambo ya Nje na Balozi za Tanzania zinavyofanya kazi ya kuhamasisha Diaspora waweze kuchangia maendeleo ya nchi yao. 
Meza Kuu ikipiga makofi kuunga mkono maelezo ya Balozi Anisa. 
Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Caroline Damian ambaye alikuwa Mgeni Rasmi aliyepokea Sanamu kwa niaba ya Serikali. 
Sanamu ambayo, Dkt. Damian alimpokea kwa niaba ya Serikali akiwa anapatiwa matibabu kwa madhumuni ya wataalamu wa afya kujifunza kwa vitendo. Anayetoa maelezo ni mtaalamu kutoka Uingereza ambaye ni rafiki wa Watanzania wanaoishi Uingereza. 
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa katika hafla ya makabidhiano ya Sanamu. 














IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 27,2019

$
0
0


   
       

   

LIVE: MBUNGE WA CHADEMA AMEJIBU KUGOMBEA NAFASI YA JUU CHADEMA”

 
 

DC CHONGOLO AKABIDHI MADARASA, OFISI ZA WALIMU KATIKA SHULE YA SEKONDARI TWIGA NA KIGOGO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amekabidhi madarasa sita na ofisi tatu za walimu katika Shule ya Sekondari Kigogo iliyopo kwenye Kata hiyo pamoja na Shule ya Sekondari Twiga iliyopo Kata ya Wazo ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wakuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi anakosa nafasi ya kusoma kwa changamoto ya madarasa.

Mhe. Chongolo amezindua madarasa hayo ikiwa ni katika mpango wake wa kujenga madarasa 100 kwakushirikiana na wadau mbalimbali wapenda maendeleo katika Halmshauri hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhe. Chongolo amefafanua kuwa anawapongeza wadau hao walioshirikiana naye katika ujenzi huo kwani madarasa hayo yatasaidia wanafunzi waliomaliza darasa la saba kuendelea na masomo ya Sekondari badala ya kukaa nyumba.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli iliamua kutoa elimu bure kwa kila mmoja ilikuhakikisha kwamba hakuna mtoto anayekaa nyumbani bila kusoma na kwamba atahakikisha madarasa hayo yanajengwa ilikutimiza adhma hiyo.

Amefafanua kuwa kutokana na mpango wa elimu bure uliotolewa na Rais Dk. Magufuli kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wanaosoma hivyo serikali itahakikisha kila mmoja anapata nafasi ya kusoma wakiwa kwenye vymba vya madarasa.

“ Awali tulikuwa na changamoto ya walimu lakini Mhe. Rais amehakikisha kuwa changamoto hiyo imekwisha ,hivi sasa tunachangamoto ya vyumba vya madarasa , hili nalo litakwisha, niwahakikishie serikali ya awamu ya tano ipo pamoja na wananchi wake” amesema Mhe. Chongolo.

Nakuongeza kuwa” leo hii nimekuja mwenyewe kuzindua madarasa haya ili kuona ufanisi uliopo, niseme tu kwamba nimeridhishwa na nimefurahi kuona madarasa haya yamekamilika, sasa imebaki viti na meza ili wanafunzi waweze kusoma nanimeambia tayari vimeshaagizwa.

Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao kwani viongozi wamekuwa wakifanya jitihada zakutosha zakuhakikisha kwamba wanapata madarasa yakusoma.

Mhe. Chongolo amemtolea mfano Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Aron Kagurumjuli kuwa ni kiongozi anayeonyesha katika kuhakikisha kuwa wanafunzi waliopo kwenye Halmashauri yake wanapata madarasa yakusomea ili wote waweze kupata elimu bora.

Mhe. Chongolo amesema kuwa “ kazi nzuri inayofanywa na rais wetu mpendwa ni kuona watu wenye hali ya chini na wale wenye hali ya juu wanapata elimu sawa, kwahiyo niwasihi sana wanafunzi msome kwa juhudi kubwa , wekeni juhudi kwenye masomo yenu, ili msingi tunaowajengea hivi sasa uweze kuimarika.
Muonekano wa madarasa ya shule ya Sekondari Kigogo yaliyojengwa kwa juhudi za Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo, waliokaa mbele ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM.

  Sehemu ya kukata utepe nje ya madarasa hayo  
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akizungumza na  wanafunzi, walimu washule ya Sekondari Twiga iliyopo Kata ya wazo hili leo, alikuwa akizindua na kukabidhi madarasa kwa walimu wa shule leo. 
 Kibao kinachoonyesha maelezo ya uzinduzi wa madarasa hayo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akimsikiliza mwananchi aliyekuwa akimueleza jambo mara baada ya kumaliza kuzindua na kukabidhi madarasa kwa walimu wa shule ya Sekondari Twiga.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akielekea kuzindua na kukabidhi majengo ya madarasa katika shule ya Sekondari Kigogo.
Picha ya pamoja

WAZIRI WA AFYA AZUNGUMZA NA WAANDISHI ZANZIBAR.

$
0
0
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na tukio la Daktari wa Hospitali ya Chake chake aliekamatwa kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Ngono hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Wizara ya Afya Ramadhan Khamis Juma akijibu maswali katika Mkutano wa Waziri wa afya kuzungumzia tukio la Daktari wa Hospitali ya Chake chake aliekamatwa kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Ngono hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.



Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Waziri wa afya kuzungumzia tukio la Daktari wa Hospitali ya Chake chake aliekamatwa kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Ngono hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

**************************************

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar 26/11/2019

Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed amewataka wagonjwa kutoa taaarifa wanapofikwa na jambo la udhalilishaji.

Ameyasema hayo huko Ofisini kwake Wizara ya afya, wakati akitoa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taarifa ya daktari wa Hospitali ya Chake kutaka rushwa ya ngono kwa mgonjwa.

Amesema kitendo hicho sio kizuri kwa taifa kwani kinawafanya wagonjwa kuwa na wasiwasi ambao wanapohitaji matibabu wakati wanapofika hospitali.

Aidha amesema Serikali haikufurahishwa na kitendo hicho hivyo kwa kushirikina na Wizara ya Afya wamechukua hatua ya kumtaka muhusika kutoa taarifa ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Pia Mhe. Hamad amesema katika kupambana na tatizo hilo Serikali imeamua kumsimamisha kazi daktari huyo ili kupitisha uchunguzi na kuchukua hatua za sheria ikiwa atathibitishwa kufanya udhalilishaji huo .

Hata hivyo Waziri huyo amewataka akina baba kushirikiana na wake zao wakati wanapokwenda Hospitali kimatibabu ili kuepuka vitendo vya udhalilishaji .

Akizungumzia suala la mshahara kuhusu daktari huyo Mkurugenzi Mtendaji Utumishi Wizara ya afya Ramadhan Khamis Juma amesema kwa sasa analipwa nusu mshahara hadi kukamilika uchunguzi na ikigundulika kufanya hivyo atasimamishiwa mshahara wake.

WAZIRI JENISTA MHAGAMA ATANGAZA PUNGUZO LA BEI UNUNUZI WA NYUMBA ZA PSSSF ZA BUYUNI-CHANIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb), ametangaza punguzo la bei kwa karibu asilimia 50 kwa atakayehitaji kununua nyumba zilizo katika mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazomilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) huko Buyuni-Chanika jijini Dar es Salaam.

Mheshmiwa Waziri ametangaza uamuzi huo wa Serikali wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili kutembelea vitegauchumi vinavyomilikiwa na Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Novemba 26, 2019 katika eneo la Mradi ambapo nyumba zilizoingia kwenye punguzo hilo ziko 480.

Akitoa mchanganua wa bei mpya Mhe. Waziri alisema, nyumba yenye vyumba viwili vya kawaida awali iliuzwa kwa shilingi milioni 66.80, sasa itauzwa kwa shilingi Milioni 36.58, nyumba ya vyumba vitatu vya kawaida awali iliuzwa kwa shilingi Milioni 67.260 na sasa itauzwa kwa shilingi Milioni 41.30.

Nyumba yanye vyumba viwili vya kawaida na Master Bedroom ilikuwa inauzwa shilingi Milioni 74.340 na sasa itauzwa Shilingi Milioni 46.20, aidha nyumba yenye vyumba vitatu na Master Bedroom iliyokuwa ikiuzwa shilingi Milioni 83.780 na sasa itauzwa kwa shilinhgi Milioni 61.360.

“Naielekeza Bodi na Menejimenti kuanzia leo (jana Novemba 26, 2019) ninapotoa tamko hili, nyumba hizo zote 204 ambazo hazijapata wanunuzi kabisa na zile 276 ambazo malipo yake yalikuwa bado hayajakamilika ambazo wafanyakazi walikuwa hawawezi kulipa hizo bei za mwanzo, nyumba hizo zote ziingie katika bei niliyotamka leo kwa niaba ya Serikali.” Alisisitiza na kuongeza……

“Baada ya kuona ununuzi wa nyumba hizo si wa kuridhisha, Menejimenti ya Mfuko imenifahamisha juu ya juhudi mbalimbali zilizofanywa kwa maelekezo ya Bodi ya Wadhamini wa Mfuko, na hatua hizi zililenga kupata njia bora ya kuuza nyumba hizi, kwani lengo kuu lilikuwa ni kujenga na kuuza nyumba kwa watumishi na watanzania kwa ujumla na sio kukaa nazo kama sehemu ya uwekezaji wa Mfuko.” Alifafanua Mhe. Waziri Jenista Mhagama.

Mheshimiwa Waziri alisema uamuzi huo wa serikali unatokana na ripoti ya Mthamini Mkuu wa Serikali baada ya kukamilisha tathmini na thamani halisi ya nyumba hizo kwa sasa.

"Nilipata taarifa kuwa katika mradi huu walikuwepo madalali kuanzia sasa hakuna haja ya kuwa na madalali kwani Mlango uko wazi kwa watu binafsi watakaohitaji kununua nyumba hizi kwani na wao ni watanzania wenzetu.
Moja ya nyumba zilizofanbyiwa punguzo kubwa la bei 
WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) (katikati) akitangaza punguzo hilo la bei Novemba 26, 2019., Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe na kulia na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF, Bw. Aggrey Mlimuka.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe, (aliyesimama), akizungumza kabla ya Mheshimiwa Waziri kutoa tamko hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF, Bw. Aggrey Mlimuka akitoa maelezo ya awali kabla Mhe. Waziri kutangaza punguzo hilo la bei.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kw aWatumishi wa Umma, (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba akitoa maelezo kuhusu mradi huo.
Rais wa Shirimkisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw., Tumaini Nyamhokya akizungumza.
Wakazi kwenye nyumba hizo wakimsikiliza Mhe. Waziri 
Waziri Mhagama na Katibu Mkuu, Bw. Massawe, wakitembelea moja ya nyumba hizo Novemba 25, 2019.
WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akisalimiana na mmoja wa wakazi kwenye nyumba hizo za mradi wakati alipofanya ziara ya kutembelea mradi huo Novemba 25, 2019.
Moja ya nyumba zilizofanbyiwa punguzo kubwa la bei
Maofisa wa PSSSF wakipitia taarifa mbalimbali kuhusiana na mradi huo.







WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb), (wapili kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe (wakwanza kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba walipotembelea mradi wa nyumba za bei nafuu za PSSSF huko Buyuni-Chanika jijini Dar es Salaam
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live




Latest Images