Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

AGIZO LA RAIS MAGUFULI LATEKELEZWA NDANI YA SAA 24

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Watendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Watendaji wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma wakionesha mfano wa hundi zao leo ambazo ni jumla ya shilingi bilioni 2.75, wakati wa hafla ya kuwasilisha gawio kwa Serikali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisisitiza kuhusu umuhimu wa Taasisi na Mashirika ya umma kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kuhakikisha kuwa zinawakilisha gawio lao ndani ya siku 60 zilizotolewa.

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Saa chache baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa siku 60 kwa Taasisi, Kampuni ambazo Serikali ina hisa chache na Mashirika ya Umma 187 ambayo hayajatoa gawio au mchango kwa Serikali tayari Taasisi nne zimetekeleza agizo hilo leo.

Akizungumza leo, jijini Dodoma, wakati akipokea gawio na michango kutoka Shirika la Posta, Shirika la Reli (TRC), Self Microfinance Fund, na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ambapo jumla ya fedha zilizowasilishwa ni shilingi bilioni 2.75, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema kuwa baada ya agizo la Rais alilolitoa jana, hakutakuwa na mzaha kwa Taasisi, Kampuni na Mashirika ambayo hayatekeleza agizo hilo ndani ya siku 59 zilizobaki.

“Nitasimamia kikamilifu agizo hili la Mheshimiwa Rais, itakapofika siku ya 60 nitatembeza panga bila uoga wala kupepesa macho kwa Taasisi, Kampuni na Mashirika ambayo hayatakuwa yametekeleza agizo hili, hatutanii katika hili” alisema Waziri Mipango.

Aidha, Waziri Mpango alizishukuru Taasisi hizo kwa kutekeleza agizo la Rais na kuongeza kuwa angependa kuona Mashirika yaliyobaki yakitekeleza agizo hilo kwa wakati, kwa kuwa fedha hizi si zake wala za Rais bali ni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa faida ya watanzania wote.

Naye, Msajili wa Hazina, Athumani Mbutuka alisema kuwa alitekeleza agizo la Rais Magufuli la kumtaka kuzijulisha Taasisi, Kampuni na Mashirika 187 ambayo hayakuwa yametoa gawio na michango kufanya hivyo ndani ya siku 60, ambapo Taasisi za TRC, TIC, Shirika la Posta na Self Microfinance Fund wamekuwa wa kwanza kutekeleza agizo hilo.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana alipokea gawio na michango kutoka kwa Taasisi, Kampuni na Mashirika 79 ambayo yalitoa jumla ya shilingi trilioni 1.05, ambapo Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro, Wakala wa Huduma za Misitu na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) yalikabidhiwa cheti kwa kufanya vizuri. Aidha, TPA iliyotoa gawio la shilingi bilioni 169 na TPC iliyotoa shilingi bilioni 14 yalipewa tuzo kwa kutoa gawio kubwa zaidi.

WAZIRI JENISTA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA VITEGAUCHUMI VYA PSSSF JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama(watatu kulia), akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Andrew Massawe (Wanne kulia), Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba (Wapili kulia) na maafisa wengine wa juu wa PSSSF, mwanzoni mwa ziara ya Waziri kutembelea vitegauchumi vya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Novemba 25, 2019.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama(katikati), akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Andrew Massawe (kushoto), Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba, (kulia), wakitoka kwenye moja ya majengo ya vitegauchumi vya Mfujo huo jijini Dar es Salaam Novemba 25, 2019. Mhe. Jenista ameanza ziara ya siku mbili kutembelea vitegauchumi vya Mfukjo huo hususan majengo.
Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo baada ya kutembekea jingo la PSSSF Twin Towers katikati ya jiji la Dar es Salaam, Novemba 25, 2019.

 Mhe. Waziri akifuatana na Katibu Mkuu pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF wakitembelea jingo la PSSSF Twin Towers katikati ya jiji la Dar es Salaam Novemba 25, 2019.
 Waziri Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa ziara hiyo huku Mkurugenzi wa Mipango na Uwelezaji PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo akimsikiliza.
 Waziri Mhagama akimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe, wakati akifafanua jambo wakati Mhe., Waziri na msafara wake walipotembelea jingo la Quality Plaza barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, ili kujionea hali ya sasa ya jingo hilo ambalo ni kitegauchumi cha PSSSF
 Waziri Mhagama akifuatana na Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Massawe wakati wakitembelkea jingo la PSSSF Twin Towers Novemba 25, 2019.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama(kushoto),  na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Andrew Massawe (kushoto), wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba wakati Mhe. Waziri alipotembelea jingo la uwekezaji la PSSSF la Jubilee Towers barabara ya Ohio katikati ya jiji la Dar es Salaam Novemba 25, 2019. 
 Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba akifafaua jambo







MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA IDARA YA MIPANGO MIJI NA ARDHI PAMOJA NA MCHUMI WA JIJI

$
0
0
Na Woinde Shizza michuzi Tv,Arusha

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt Maulid Madeni leo amemsimamisha kazi Mkuu wa Idara ya Mipango Miji na Ardhi, Dickley Nyato na Ofisa Mipango Takwimu na Ufuatiliaji (Mchumi Wa jiji ), Anna Mwambene ili kupisha uchunguzi wa eneo la ujenzi kituo cha mabasi lililopo eneo la Bondeni City mkoani hapa lenye ukubwa wa ekari 30.

Akizungumza na Waandishi wa habari Novemba 25, 2019, Dkt Madeni amesema baada ya halmashauri kubaini ubadhirifu wa Sh1.9 bilioni za ununuzi wa eneo la ekari 29.5 lililopo Mtaa wa Oloresho Kata ya Olasiti na kukataa kulipa fidia, wananchi waliamua kutafuta ekari 30 za bure zilizopo eneo la Bondeni City katika Kata hiyo.

“Eneo hili lilifanyiwa tathimini huko nyuma na muhtasari uliandikwa Februari 24 mwaka 2017 ukitutaka tulipe fidia Sh.bilioni 1.1 lakini mwaka huo huo Machi 6 ukaandikwa muhtasari mwingine ukitaka tulipe Sh.bilioni 1.9 sasa mimi nikakataa na nakataa hadi mwisho nanasema hamna ela ambayo itatoka kwa ajili ya kulipa fidia bora hiyo pesa tuendelee kujenga madarasa ya magorofa watotowetu wasome,” akibainisha Madeni 

Alifafanua kuwa kutokana na mvutano huo, alifanya uchunguzi na kuwataka wakuu hao wa idara kumuandikia barua za kujieleza juu ya mamlaka ya kubadilisha maamuzi ya Baraza walikopata na kuongeza kiasi hicho cha fedha.

Akibainisha kuwa uthamini wa pili uliofanywa haukuwa na vigezo vyovyote vya kisheria,ikiwemo kupitishwa au kukaa kwa kikao cha madiwani cha kuizinisha kufanya tathimini upya ya Julia fidia katika eneo hilo

Kwamujibu wa Dtk Madeni, waliandika barua zao na kumpelekea Novemba 19, mwaka huu, lakini baada ya kuzisoma hakuridhika na sababu zao hivyo ameamua kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi dhidi yao.

"Mkuu wa Idara ya Mipango Miji na Ardhi, Dickley Nyato amedanganya Ofisi Yangu kwakusema kuwa kiwanja hicho ambacho halmashauri imepewa kwa ajili ya kujenga standi hakina hati miliki lakini tumefatilia tukakuta ,kiwanja hicho kina hati tangu mwaka 1949 na itaisha mwaka 2048 kwaiyo hati hii itadumu kwa miaka 99 bado mbele ,kwaiyo ndugu huyu alipotosha mamlaka ya juu kwa kusema hamna hati ya kiwanja hicho na halmashauri ilitakiwa ikichukuwe na ijigawie wenyewe na sio kupewa" alibainisha Madeni

Alisema kwa upande WaOfisa Mipango Takwimu na Ufuatiliaji (Mchumi Wa jiji ), Anna Mwambene aliondolewa majukumu yake hadi pale uchunguzi utakamilika,huku akibainisha kwa kipindi chote cha kupisha uchunguzi ataruhusiwa kutoka nje ya mkoa bila kutoka taarifa kwa mwajiri wake pili anatakiwa kila baada ya wiki mbili katika Siku ya ijumaa anatakiwa aripoti katika OFISI ya mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi.
Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt Maulid Madeni  akiongea na waandishi Wa habari ofisini kwake

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 26,2019

SERIKALI YARIDHISHWA NA MAENDELEO MRADI MKUBWA WA MAJI JIJINI ARUSHA UNAOGHARIMU SHILINGI BILIONI 520

$
0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha


Serikali imesema kuwa imeridhishwa na utekelezaji Wa mradi mkubwa Wa Maji Wa shilingi bilioni 520 unaotekelezwa katika halmashauri ya jiji la Arusha utakao hudumia wananchi .

Akizungumza na Waandishi Wahabari Mara baada ya kukagua miundombinu ya mradi huo ,Mkurugenzi Wa Idara ya usambazaji Wa Maji na Usafi Wa mazingira kutoka Wizara ya Maji ,Nadhifa Kemikimba alisema kuwa amerithishwa na kasi ya ujenzi Wa mradi huo huku akibainisha kuwa nia ya serikali nikuona hadi ifikapo mwaka 2020 upatikanaji Wa huduma za Maji kwa Mjini umefikia asilimia 95% huku vijijini wananchi wanapata Maji kwa asilimia 85%.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi AUWSA Mhandisi Justine Mwangijomba alisema kuwa mradi huo umefikia hatua ya kusafisha mtandao Wa mabomba yanayopeleka Maji kwenye tanki pamoja na kuweka Maji dawa tayari kabisa kwa ajili ya wananchi kuanza kutumia.

"Kama ulivyoona tumepita katika matanki yetu ya Maji natumeona tanki moja la Lita milioni kumi tumeanza kuweka Maji kwani ujenzi Wa tanki hilo umekamilika hivyo muda sio mrefu wananchi watapata ongezeko la Maji na tutaanza kuwapa wale wenye matatizo ya Maji kama muriet na olasiti" alisema Mwangijomba.

Akiongelea mradi huo Mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa kuna ujenzi Wa makao makuu ya mamlaka ya Maji safi na Maji taka ambao ulikuwa unasuasua lakini baada ya OFISI yake kwakushirikiana na msimamizi Wa mkandarasi kufatilia kwa makini ujenzi huo umeanza kwenda vizuri

Akibainisha kuwa walipotembelea mradi huo ujenzi ulivyokuwa ukisuasua ulikuwa umefikia asilimia 7.5 lakini baada ya kuusimamia vizuri umeongezeka na kufikia asilimia 10 ambapo alibainisha mbali nakufuatilia mradi huo pia wamempa mkandarasi mashariti ya kufanya Kazi usiku na mchana ,kuwasilisha taarifa za mradi unavyoendelea kila wiki huku akimtaka ajenge kwa kufuata vipimo vinavyotakiwa na katika ubora unaotakiwa 

Kwa upande wake Mkuu Wa wilaya ya Arusha alisema kwamba kumalizika kwa mradi huo kutawasaidia wakazi Wa jiji la Arusha kuondokana na tatizo la Maji .
mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa maelekezo kwa mkandarasi mara baada ya kutembelea moja ya kisima cha maji ya mradi wa shilingi bilioni 520 kilichopo Ngaramtoni ndani ya wilaya ya Arumeru ambapo alimtaka mkandarasi kuhakikisha adi ifikapo November 30 wananchi wawe wameanza kupata maji




Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji AUWSA Mhandisi Justine Mwangijomba akimpa maelekezo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo jinsi maji yanavyoingia katika tanki kubwa la lita milioni 10 ambalo limekamilika na jana november 24 zoezi la usafishaji mabomba kwa ajili ya matumizi ya binadamu ,tanki hilo kubwa lipo mji mdogo wa ngaramtoni ndani ya wilaya ya Arumeru maji haya ni ya mradi wa kiasi cha shilingi bilioni 520 uliotolewa na serikali na yatahidumia jiji zima la Arusha (picha na Woinde Shizza,Arusha).
Mkurugenzi Wa Idara ya usambazaji Wa Maji na Usafi Wa mazingira kutoka Wizara ya Maji ,Nadhifa Kemikimba akiongea na wakandarasi na wafanyakazi Wa AUWSA Mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kutembelea mradi mkubwa Wa shilingi bilioni 520.(picha na Woinde Shizza Arusha) .
Moja ya bomba la Maji likiwa linatoa Maji mengi wakati Wa kusafisha mabomba.

TAASISI NNE ZATII AGIZO LA RAIS MAGUFULI LA KUZITAKA KAMPUNI, TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA KUTOA GAWIO

$
0
0
Watendaji wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma wakionesha mfano wa hundi zao leo ambazo ni jumla ya shilingi bilioni 2.75, wakati wa hafla ya kuwasilisha gawio kwa Serikali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jijini Dodoma.


Na Benny Mwaipaja, Dodoma


SIKU moja baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa muda wa siku 60 kwa wenyeviti wa bodi na watendaji wa Kampuni, Taasisi na Mashirika ya Umma yanayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 pamoja na yale ambayo Serikali ina hisa kutoa gawio na michango yao kwenye mfuko Mkuu wa Serikali lasivyo wangepoteza nyadhifa zao, taasisi 4 zimetoa gawio na michango kwa Waziri wa Fedha na Mipango Jijini Dodoma leo jioni

Taasisi zilizotoa gawio ni pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ambacho kimetoa shilingi bilioni 1 nukta 2, Shirika la Reli (TRC) Sh. bilioni 1, Shrika la Posta Tanzania (TPC) sh. milioni 350 na Mfuko wa SELF-Microfinance shilingi milioni 200 na kufanya jumla ya kiasi kilichopokelewa kuwa shilingi bilioni 2 nuta 75

Jana Mheshimiwa Rais Magufuli alipokea gawio na michango mbalimbali ya sh. trilioni 1.05 kutoka kwa Kampuni, taasisi na mashirika 79 kati ya 266 yaliyotakiwa kutoa gawio na michango hiyo huku taasisi 187 zikikwama kufanya hivyo.

Hatua ya taasisi hizo nne kutoa gawio na michango yao leo imefikisha gawio na michango iliyopokelewa na Serikali katika mwaka wa Fedha 2018/2019 kufikia sh. trilioni 1.325 huku kampuni 183 kukabiliwa na rungu la Waziri wa Fedha na Mipango kama hawatatekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais ya kuwataka watendaji na Bodi zao kutoa fedha za gawio na michango ndani ya siku 59 zilizobaki

BENKI YA BIASHARA NA MAENDELEO tdb YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KATIKA KUKUZA MAENDELEO

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Dodoma

RAIS wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Dkt. Admassu Tadesse ameahidi kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuipatia mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi yake ya kimkakati ya maendeleo kwa sababu uchumi wake uko imara na inakopesheka

Dkt. Tadesse ametoa ahadi hiyo Jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango ambapo wawili hao wamezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo hususan Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na ujenzi wa mradi wa kufua umeme kwa njia ya maporomoko ya maji ya mto Ruhudji mkoani Njombe

Amesema kuwa miezi michache iliyopita Benki yake imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola bilioni 1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kipaumbele inayotekelezwa na Serikali na kwamba wako mbioni kutoa kiasi kingine kikubwa cha fedha hivi karibuni.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa Benki hiyo ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika TDB imekuwa mdau muhimu katika maendeleo ya Taifa na kwamba pamoja na kiasi cha dola bilioni moja kilichopokelewa na Serikali mwezi Agosti Mwa huu 2019, Serikali inatarajia kupata kiasi kingine cha dola milioni 300.

Amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kitaelekezwa katika ujenzi wa miundombinu ya Reli ya Kati ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) pamoja na miradi ya kuzalisha nishati ya umeme ili nchi iweze kuimarisha sekta ya uzalishaji viwandani kwa kuwa na umeme wa uhakika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. Hamis Mwinyimvua akizunguza wakati wa kikao na Rais huyo wa TDB amesema kuwa amefurahi kwamba Benki hiyo imeonesha nia ya kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Ruhudji (MW 358) wenye thamani ya dola za Marekani milioni 460.2 ambapo kati ya hizo dola milioni 407 zitatumika kujenga mitambo ya kufua umeme na kiasi kingine cha dola milioni 53 kitatumika kujenga njia ya kusafirishia umeme urefu wa km 170.

Alisema kuwa lengo la Serikali ni kuzalisha megawati 10,000 za umeme ifikapo mwaka 2025 na kwamba kutekelezwa kwa mradi huo kutasaidia kufikia azma hiyo ili kuimarisha masuala ya uzalishaji viwandani na uendeshaji wa miundombinu mingine inayotumia nishati hiyo ya umeme.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amemweleza Rais huyo wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Admassu Tadesse kwamba ujenzi wa kipande cha Reli ya Kisasa kati ya Dar es Salaam na Morogoro umefikia asilimia 72 hivi sasa na kuishukuru Benki hiyo kwa utayari wake wa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Reli kipande cha Mwanza hadi Isaka.

Tanzania ni mongoni mwa wanahisa 31 wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini Mwa Afrika (TDB) ambapo hadi kufikia Disemba 31 mwaka 2018, Tanzania ilikuwa imeshika nafasi ya 4 ya uwekezaji katika Benki hiyo ikiwa na asilimia 8.33 ya hisa.

 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Dkt. Amassu Tadesse (kushoto), alipotua katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma akiwa katika ziara yake ya kikazi hapa nchini. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Doto James.
 Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt.  Hamis Mwinyimvua (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na Rais wa Benki ya Biashara na  Maendeleo  Mashariki na  Kusini mwa Afrika (TDB) Dkt. Admassu Tadesse (hayupo pichani) kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof.  Florens Luoga na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, jijini Dodoma. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akiteta jambo na Rais wa Benki ya Biashara na  Maendeleo  Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Dkt. Admassu Tadesse, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Rais huyo na Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli. 
Rais wa Benki ya Biashara na  Maendeleo  Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse (kulia) akimweleza jambo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) walipokutana na kufanya mazungumzo, Jijini Dodoma
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) na  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt.  Hamis Mwinyimvua wakisikiliza kwa makini mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse (hawapo pichani), Jijini Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Rais wa Benki ya Biashara na  Maendeleo  Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse (kulia), wakifurahia jambo baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya ujumbe wa Tanzania na Benki hiyo walipokutana Jijini Dodoma.
Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika ulioongozwa na Rais wa Benki hiyo Dkt. Admassu Tadesse (wa nne kulia) jijini Dodoma.Picha na Josephine Majura WFM – DODOMA).

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (wa pili kushoto) akiongoza ujumbe wa Tanzania kumpokea Rais wa Benki ya Biashara na  Maendeleo  ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse alipowasili Uwanja wa Ndege Jijini Dodoma.

TAARIFA YA UZINDUZI WA VIFURUSHI VYA BIMA YA AFYA


WATU ZAIDI YA MILIONI 100 WANAOTAFUTA HUDUMA ZA AFYA AFRIKA MASHARIKI KUNUFAIKA

$
0
0
App ya  ADA


Simu yako daktari wako....!

Na Mwandishi Wetu
TAKRIBANI watu zaidi ya milioni 100 wanaotafuta huduma za afya nchi za Afrika Mashariki wanatarajia kunufaika na Programu ya kwanza ya kishwahili yenye uwezo wa kutathmini dalili za magonjwa inayoendeshwa na akili bandia (“AI”).

Programu hiyo iliyozinduliwa kwa ushirikiano na Shirika la Fondation Botnar la Uswisi, Global Health Initiative - ADA pamoja na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) cha jijini Dar Es Salaam, Tanzania inatarajiwa kuwa mkombozi kwa jamii hasa za kipato cha chini na kati.

Taarifa zaidi za wadau wa program hiyo zinaeleza kuwa inawezesha upatikanaji wa taarifa za afya na ushauri App, iliyokuzwa na Ada Health, inachanganya hifadhidata ya maarifa bora zaidi ya kitiba duniani na teknolojia erevu ya fikra ili kuwasaidia watumiaji kuelewa nini kinaweza kuwa kinasababisha dalili zao, na pia kuwapa mwongozo maalum kuhusu wanachotakiwa kufanya baada ya hapo.

Programu hiyo ‘app’ inakusudia kuwawezesha wagonjwa kupata taarifa juu ya kinachowasumbua baada ya kuingiza dalili za ugonjwa kisha kufanya maamuzi kuhusu afya zao, huku ikisaidia kutoa huduma za afya zilizopo, madaktari, na kliniki. Ulimwenguni kote kuna watu bilioni 4 - zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani - hawawezi kufikia huduma za msingi za afya.

“Watu bilioni nne duniani kote hawawezi kufikia huduma za msingi za afya, na nchi nyingi zikiwemo Tanzania, Kenya, Somalia na Msumbiji zina daktari chini ya 1 kwa watu 1,000 ,” 2 alisema Hila Azadzoy, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Health Initiative ya Ada.

Bi Azadzoy anabainisha; “Kutokana na upokeaji mpana wa teknolojia ya kidijitali, kuna fursa kubwa kwa AI kusaidia kushughulikia hili suala [upungufu wa wahudumu wa afya] kwa kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa na kuwawezesha madaktari kuwa na athari kubwa zaidi kadri iwezekanavyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Magonjwa ya Watoto wa Chuo Kikuu cha Muhimbili Cha Afya na Sayansi Shirikishi anasema ili kuwa na ufanisi, teknolojia hizi lazima zirekebishwe kulingana na hali za kitiba, kitamaduni, na kilugha katika kila eneo.

Anasema Chuo Kikuu cha Muhimbili kimesaidia maboresho kwa app hiyo ya Kiswahili. “…Tutakuwa tunaendelea kushirikiana na wataalamu wa ndani ya Afrika Mashariki kugundua njia zaidi za kuweza kuboresha uwezekano wa kufikia huduma za afya.”

“Kuna upungufu mkubwa katika huduma za afya ndani ya Afrika Mashariki na itakuwa vigumu sana kushughulikia suala hili kwa kuongeza idadi ya wafanyakazi wa afya na madaktari tu. Tunaweza kutatua hili tatizo na kufanya kila familia iweze kufikia huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa,” alisema, Dk. Salim.

Naye Mkuu Mtendaji wa Fondation Botnar, Dk. Stefan Germann alisema wamefanikisha marekebisho kulingana na magonjwa na dalili zilizoenea zaidi eneo hili, tunapiga hatua muhimu katika kuwaongoza mamilioni ya watu kwenye kutafuta matibabu. AI ina uwezo mkubwa wa kusaidia kuboresha ufanisi na ubora wa mifumo yetu ya afya kupitia huduma ya kibinafsi na ya ubashiri zaidi; tunaamini ni muhimu kwamba faida hizi zinapatikana kwa kila mtu, ulimwenguni kote.

Kasoro za changamoto hii ya afya inawaathiri zaidi watu kwenye nchi zenye kipato cha chini na cha kati. Afrika Mashariki ni ukanda ambao umeathiriwa sana na suala hili. Kwa kutoa programu ya kitiba ya tathmini ya dalili inayoendeshwa na akili bandia kwa Kiswahili, lugha ambayo inatumiwa na zaidi ya watu milioni 100 kwenye nchi kama Tanzania, Kenya, Uganda, Msumbiji, mpaka Somalia, Ada inatumaini kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kufikia taarifa bora za afya na ushauri, haswa kwa vijana na familia. Toleo la Kiswahili la app ya Ada limekuzwa kama sehemu ya Mpango wa Afya Duniani, “Global Health Initiative (GHI)” wa Ada.

Huu ni mpango wa muda mrefu wenye lengo la kukabiliana na upungufu wa wafanyakazi katika sekta ya afya - ambao unatarajiwa kufikia zaidi ya milioni 12.9 ifikapo mwaka 2035. Ada inakabiliana na upungufu huu katika huduma za afya.

Dk. Germann, anaongeza kuwa App kama ya Ada inaweza kuwafanya wagonjwa, haswa vijana, kuwa wadau wenye ufahamu juu ya afya zao. Hivyo basi, kuunda vifaa vya afya vya kidijitali maalumu kwa matakwa na mahitaji ya eneo husika katika nchi za kipato cha chini na cha kati ni muhimu katika kufikia usawa kwenye upatikanaji wa huduma za afya.” aliongeza kusema, “Tunajivunia kuzindua toleo la Kiswahili la app ya Ada na tunatarajia kushirikiana zaidi ili kutekeleza maono yetu ya pamoja ya kutumia teknolojia kusaidia wagonjwa, bila kujali wanaishi wapi.”

Kuchanganya akili bandia, utaalamu wa matibabu ya kibinadamu na nguvu ya teknolojia ya kidijitali ili kufikisha huduma za afya na mwongozo kwa wengi. Washirika wa Ada katika kuikuza na kuifanya app iendane na mazingira ya Afrika Mashariki ni shirika la Fondation Botnar la Uswisi, ambalo ni shirika lililojikita kwenye kutumia teknolojia ili kuboresha afya na ustawi wa vijana katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

App inapatikana kupitia simu zote za iOS na Android. Kurekebisha AI za Ada kuendana na changamoto za kipekee za kiafya za Afrika Mashariki Ada imefanya kazi na washirika wenyeji, madaktari na mashirika ya afya ili kuhakikisha app inarekebishwa kuendeana na isimu ya lugha, utamaduni na maudhui ya kitiba ya kila eneo.

Wabunge kutoka Korea watembelea hospitali ya Mloganzila

$
0
0
WABUNGE kutoka Korea wametembelea Mloganzila Wabunge wa Serikali ya Korea ya Kusini wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya afya ya Bunge hilo, leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ili kufahamu huduma zinazotolewa hospitalini hapa.

Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wageni hao, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi amewaeleza kuwa hospitali ya Mloganzila ina vifaa tiba vya kisasa na inatoa huduma mbalimbali za afya ambapo kwa siku inahudumia wagonjwa wa nje 400 hadi 450.

“Hospitali yetu ina vifaa vya kisasa kama vile CT-Scan na MRI pamoja na kutoa huduma kwa wagonjwa ambapo kwa siku tunawahudumia wagonjwa 400 hadi 450,” Amesema Dkt. Magandi.

Aidha Dkt. Magandi amefafanua kuwa lengo la kuanzishwa kwa hospitali kama ya Mloganzila ni ili kupunguza gharama za kupeleka wagonjwa nje ya nchi na badala yake kuimarisha huduma za afya zinazotolewa na wataalam nchini ili kuweza kutibu magonjwa ambayo hapo mwanzo yalihitaji mgonjwa kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Bunge la Korea ya Kusini, Bw. Kim Se-Youn amesema kuwa wamefurahishwa na namna hospitali inavyohakikisha kuwa jamii inayowazunguka inapata huduma bora za afya.

“Tumefurahi sana kuitembelea hospitali hii na tunatumaini kuwa hospitali ya Mloganzila itaendelea kushirikiana na Serikali yetu ya Korea katika kuhakikisha huduma bora za afya zinatolewa kwa watanzania,” Amesema Bw. Kim.

Wageni hao wametembelea kitengo cha magonjwa ya dharura (EMD), radiolojia pamoja na maabara na kujionea namna wataalam wanavyofanya kazi.
 Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi (kushoto), kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Bunge la Korea ya Kusini, Bw. Kim Se-Youn wakisikiliza utambulisho wa wageni waliofika hospitalini hapa.
 Baadhi ya wabunge waliofika hospitali ya Mloganzila wakisikiliza mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa katika kikao hicho.
 Dkt. Frida Shao kutoka Kitengo cha Magonjwa ya Dharura katika hospitali ya Mloganzila (EMD) akiwaelezea wageni hao kazi zinazofanywa na kitengo hicho.
 Mtaalam wa Maabara katika Hospitali ya Mloganzila, Bw. Mbaruku Kisutu akiwaelezea wageni hao namna wataalam wa maabara wanavyofanya kazi.
Dkt Magandi katika picha ya pamoja na wabunge walioongozana na mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Bunge la Korea ya Kusini waliokuja kutembelea hospitalini hapa. 
Mtaalam wa mashine ya CT-Scan, Dkt. Charles Nchimbi akiwaelezea wageni jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.

Shule ya Sekondari Orkeeswa ya jijini Arusha yang'ara michezo ya shule za Kimataifa

$
0
0
 Ndajiri Lonyori kutoka shule ya secondari Orkeeswa akipokea kombe la ushindi wa mchezo wa mpira wa kikapu wa wasichana chini ya miaka 19 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka mkoani Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki. 

 Ndajiri Lonyori kutoka shule ya secondari Orkeeswa akionyesha kombe lao la ushindi wa mchezo wa netball chini ya miaka 15 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki.
 Amani Isaya kutoka shule ya sekondary Orkeeswa akionyesha kombe lao la ushindi wa  mchezo wa volleyball chini ya miaka 19 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki. 
Emmanuel Meibuko golikipa wa timu ya shule ya sekondari Orkeeswa akipokea kombe la ushindi wa mpira wa miguu wa wavulana chini ya miaka 19 baada ya kuibuka washindi kwa goli 3 - 2 katika mechi iliyokuwa ngumu sana kwa vijana hao wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki. 


Shule ya Secondari Orkeeswa iliyopo mkoani Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali ya Shule za Kimataifa. 
 
Shule hizo kutoka mikoa mbalimbali nchini zilikutana mkoani Kilimanjaro na kuchuana vikali katika michezo ikiwemo mpira wa kikapu, mpira wa miguu, tennis, swimmings, netball, volleyball, frisbie, rugby na michezo mingineyo. 
 
Timu za kikapu U19 wasichana na U19 wavulana pamoja na timu ya mpira wa miguu ya shule hiyo zilionekana kuwa imara zaidi baada ya kushinda kwa kishindo timu za shule mbalimbali zilizo pambana nao. 
 
Shule za kimataifa nchini zilikuwa na wikiendi ya michezo iliyoanza mwishoni mwa wiki,Ijumaa na kufikia tamati Jumapili. 

KANISA LA ABC TABATA LAANDAA KONGAMANO NA UIMBAJI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

KONGAMANO na Tamasha la Uimbaji wa nyimbo za injili linatarajia kufanyanyika kwa siku tatu mfululizo katika Kanisa la ABC lililopo Tabata Mandela Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mratibu wa Tamasha hilo Askofu Flaston Ndabila alisema maandalizi yote ya kongamano na tamasha hilo litakalo anza Desemba 6, 2019 yamekamilika.

" Maandalizi yote ya tamasha letu yamekwisha kamilika na wageni tulio waalika kutoka ndani na nje ya nchi wamethibitisha kuja kushiriki" alisema Ndabila. 

Alisema kwamba katika kongamano na tamasha hilo kutakuwa na mafundisho ya ndoa na familia ambayo yatafanyika Desemba 7, Ibada ya shukurani ambayoitafanyika Desemba 8 na kuhitimishwa na kilele cha furaha Desemba 9, 2019.

Askofu Ndabila aliwataja watumishi wa mungu watakaoshiriki katika kongamano hilo kuwa ni Bishop Mark Mugekenyi Kairuki (Kenya) Bishop Mussa Ngobese (Afrika Kusini) Apostle Moses Silwamba (Zambia) Pastor Harerimana Tharcise (Burundi) Pastor Fred Msungu (Tanzania) Bishop Robson Simkoko (Malawi) na Mimstori: Eliya Mwaitondo wa Tanzania.

Alisema Kongamano hilo litaanza kanisani hapo kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 12 jioni kila siku na kuwa watu wote wanakaribishwa na kwa maelezo zaidi ya kushiriki unaweza kupiga simu namba 0754 762301 na 0715684590.
Bishop Flaston Ndabila (kulia) na Mke wake Janeth Ndabila wa Kanisa la ABC Tabata waandaaji wa Kongamano na Tamasha la Uimbaji wakiwa katika picha ya pamoja. Tamasha hilo litakwenda sanjari na kuwapongeza wanandoa hao kwa kutimiza miaka 25 ya ndoa, miaka 25 ya huduma na miaka 50 ya kuzaliwa. 
Bishop Mark Mugekenyi Kairuki (Kenya)
Bishop Mussa Ngobese (Afrika Kusini)
Pastor Fred Msungu (Tanzania)
Pastor Harerimana Tharcise (Burundi)
Bishop Robson Simkoko (Malawi) 
Apostle Moses Silwamba (Zambia)

BRELA YASHIRIKI MKUTANO WA KIKANDA WA WATALAAMU WA MASUALA YA MILIKI BUNIFU AFRIKA KUSINI

$
0
0
KAIMU Mkuu wa Kitengo cha Leseni za Biashara- (wanne kutoka kushoto) Tawi Kilumile ndiye Mwenyekiti wa Mkutano huo unaohusisha nchi 15 wanachama wa SADC Mkutano huo Tanzania imewakilishwa na Bakari Mketo Mkurugenzi wa Huduma na Uwezeshaji wa BRELA (wa kwanza kulia mstari wa pili)

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara imeshiriki kwenye Mkutano wa wa Kikanda Wataalamu wa masuala ya Miliki Bunifu kwa nchi za jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC) Johannesburg- Afrika Kusini tarehe 25-26 Novemba, 2019.

Lengo la Mkutano huo ni Kuandaa Mpango kazi wa Utekelezaji wa Mkakati (Framework) na Taratibu za kusimamia na kutumia Miliki Bunifu katika Utekelezaji wa Mkakati wa Viwanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC.

Tanzania kwa Heshima iliyowekwa na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa SADC Bw. Mh Dr. John Pombe Joseph Magufuli Tanzania imepewa heshima ya kuwa Mwenyekiti pia wa Mkutano huo

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni -BRELA imewakilisha nchi katika Mkutano huo kwa kuwa ndiyo Ofisi ya Taifa ya Miliki Bunifu (National IP Office)

Serikali yanemeesha wachimba madini

$
0
0
 Pichani ni muonekano  wa nje wa jengo la Ofisi ya Madini na Kituo cha Umahiri,  mkoani Simiyu, Wilaya ya Bariadi ikiwa ni jitihada za Serikali za kuimarisha sekta ya madini nchini, kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini. 



Serikali kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), imeendelea kunufaisha wachimbaji wadogo wa madini kwa kuanzisha na kuboresha mifumo mbalimbali itakayosaidia kukuza sekta ya madini pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo.

Ujenzi wa Kituo cha Umahiri kilichopo katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kunatokana na Sera ya Madini ya Mwaka 2009 ambayo inasisitiza sana juu ya uendelezaji wa sekta ya madini na hasa wachimbaji wadogo, ni hatua itakayosaidia kutatua changamoto za wachimbaji wadogo wa madini.

Mnamo Septemba 05, 2018 Kituo cha Umahiri cha Bariadi kilianza kujengwa na Kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT  na kusimamiwa na Kampuni ya Sky Actate Consultants, kilikamilika Oktoba 16 mwaka huu  na kugharimu  shilingi  bilioni 1.308, kitasaidia  kutoa  mafunzo na maarifa kwa wachimbaji wadogo kuhusu sera ya madini, sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya kiutendaji katika shughuli za madini.


Aidha, kituo hicho kitasaidia kutoa elimu kuhusu ujasiriamali, utafutaji madini, uchimbaji madini, uchorongaji miamba, mazingira, afya na usalama migodini, pamoja na kutoa elimu juu ya mfumo wa kutathmini mashapo ya madini yaliyopo ili kufanya uchimbaji uwe na tija.


Akizungumza hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema ujenzi wa kituo hicho utajibu mahitaji ya mkoa katika kuwasaidia wachimbaji wadogo kuondokana na uchimbaji wa kienyeji na kwenda kwenye uchimbaji wa kisasa.


"Wachimbaji wetu wadogo wamekuwa wakifanya shughuli zao kienyeji lakini uwepo wa kituo hiki utajibu mahitaji yao kwa sababu kitakuwa ni sehemu sahihi ya wao kupata elimu juu ya uchimbaji bora, pamoja na uwepo wa wataalam wa madini karibu na maeneo yao”, alisema Mtaka.


 “ Sisi kama mkoa tuna faida ya uwepo wa rasilimali madini tuna nikeli, shaba, dhahabu, cobalt, tuna chumvi katika wilaya ya Meatu lakini pia tuna madini ya ujenzi kama kokoto, mchanga na mengine, hivyo uwepo wa kituo cha umahiri kutasaidia wachimbaji kufanya kazi zao katika utaalamu ili uchimbaji ufanyike kwa ufanisi na uwe na tija”, alisisitiza Mtaka.


Naye, mchimbaji mdogo wa madini kutoka mkoa wa Simiyu, James Bundala, anasema kituo hicho cha umahiri ni kituo cha msaada katika kazi zao, na wanatarajia kitasaidia kuongeza tija na kukuza kipato kwa vile watafanya kazi kisasa zaidi.


“Imani yetu ni kuwa kituo hiki kitatusaidia kutatua migogoro ya uchimbaji madini inayojitokeza, pamoja na kupata elimu kuhusu uongezaji thamani madini na upatikanaji wa masoko, na haya yote yatatusaidia kufanya biashara yetu vizuri zaidi na kukuza vipato vyetu”, alisema Bundala.


Vile vile, kituo hicho kitasaidia katika usimamizi na uratibu wa shughuli mbalimbali zinazohusu madini, pamoja na kuwezesha wachimbaji wadogo kupata taarifa sahihi za maeneo yaliyotengwa kwa ajili yao.


Katika kipindi cha miaka minne ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, sekta ya madini imetekeleza hatua mbalimbali zenye lengo la kuimarisha sekta ya madini nchini kwa kuboresha maisha ya wachimbaji wadogo, sambamba na kuongeza pato la taifa.


Aidha, Serikali imefanikiwa kuifanya sekta ya madini kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya mapato kwa kuwekeza utaalam wa rasilimali watu, majengo, upimaji na utaalam mbalimbali wa kusaidia wachimbaji wadogo. Waziri wa Madini, Dotto Biteko, wakati alipokuwa akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2019/20 alisema kuwa  mchango wa sekta ya madini kwenye pato la taifa kwa mwaka 2018/19 umeendelea kuimarika na kufikia asilimia 5.07 mwaka 2018.


Mchango huo ulitokana na kuongezeka kwa uelewa kwa wadau wa sekta ya madini na kuwepo kwa uwazi katika shughuli zao, ukuaji wa sekta, kuimarisha usimamizi wa shughuli za madini kwa kudhibiti utoroshwaji, kuimarisha ukaguzi katika sehemu za uzalishaji na biashara ya madini, kuongezeka kwa viwango vya mrabaha na kuanzishwa kwa ada ya ukaguzi wa madini kupitia Marekebisho ya Sheria ya Madini Sura ya 123 yaliyofanyika mwaka 2017.


Aidha, Biteko amesema kuwa kuhusu uendelezaji wa uchimbaji mdogo wa madini, Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa changamoto za sekta ya madini zinapatiwa ufumbuzi na hivyo kuwafanya wadau kufanya shughuli zao za uchimbaji na biashara ya madini katika mazingira ya kibiashara yanayovutia.


Mkakati mwingine  uliofanywa na Serikali  ili kuimarisha sekta ya madini  nchini ni pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kufanya mkutano na wachimbaji, wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini  Januari 22 na 23 mwaka huu, kwa lengo la kuondoa changamoto zilizokuwa zikiikabili sekta hiyo.


Katika mkutano huo, Serikali ilipokea kero na hoja mbalimbali zikiwemo, kupunguzwa kwa kodi na tozo zinazotozwa kwa wachimbaji wadogo wa madini, kufutwa kwa maeneo ya leseni za madini zisizoendelezwa na kuwekwa kwa maafisa madini kwenye maeneo ya machimbo ya madini.


Hoja nyingine katika mkutano huo zilikuwa, kudhibiti utoroshwaji wa madini, kuimarisha utunzaji wa mazingira katika maeneo ya uchimbaji madini, ukosefu wa miundombinu, tozo na ada kulipwa kwa fedha za kigeni,  pamoja na kuondoa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) asilimia 18 na kodi ya zuio (withholding tax) asilimia 5 kwa wachimbaji wadogo. Hii inafanya jumla ya kodi zote zilizofutwa kufikia asilimia 23.


Ni dhahiri kuwa, katika kipindi cha miaka minne, Serikali ya Awamu ya Tano inaimarisha sekta ya madini na kuneemesha wachimba madini kwa kuanzisha masoko ya madini na kujenga vituo vya mfano na umahiri ambavyo wachimbaji wadogo wanapata fursa ya kujifunza teknolojia na mbinu bora na za kisasa za uchimbaji na uchakataji madini, utunzaji wa mazingira, pamoja na kuanzisha mfumo wa masoko ya madini katika mikoa yote yenye madini ya metali na vito yaani metallic minerals and gemstones.


WAZIRI MHAGAMA KUTANGAZA UTARATIBU MPYA WA KUNUNUA NYUMBA ZA MRADI BUYUNI

$
0
0
Na. OWM, DAR ES SALAAM.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama leo tarehe 26 Novemba, 2019 anatarajia kutangaza utaratibu mpya wa kununua Nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.

Akiongea mara baada ya kumaliza kukagua mradi huo wa nyumba zinazomilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), tarehe 25 Novemba 2019, Mhe. Mhagama amebainisha kuwa atatoa utaratibu huo mpya wa namna ya kununua nyumba hizo zilizo wazi ili wananchi waweze kunufaika kwa kupata makazi bora na salama.

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), unaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, na umeanzishwa na Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2018, Jukumu kuu la mfuko huo ni kukusanya michango na kulipa mafao ya kustaafu kwa watumishi wa umma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi , Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu) Andrew Massawe (Kulia) na kushoto kwake Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hosea Kashimba, kukagua Nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi , Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu) Andrew Massawe wakati alipokagua Nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mkazi wa Buyuni, Benjamini Mvungi wakati alipokagua Nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.
Muonekanao wa mojawapo ya nyumba Nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam zinazonilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa wananchi waliofanikiwa kununua Nyumba za gharama nafuu za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa wananchi waliofanikiwa kununua Nyumba za gharama nafuu za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu) Andrew Massawe na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hosea Kashimba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa wananchi waliofanikiwa kununua Nyumba za gharama nafuu za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.

Nimeikumbuka Sanaa ya zamani, natamani kurudia utoto tena

$
0
0

Charles James

MALKIA wa Bongo Fleva na Dada mwenye nyota tano, Lady Jay Dee, Komando alipata kuimba 'natamani kuwa malaika, natamani nirudi kama mtoto.

Mimi naondoka na huo mstari wa ninatamani kurudi kuwa kama mtoto. 

Ndio. Kuna vitu sivioni hivi sasa kutokana na utandawazi wa Dunia basi natamani muda urudi nyuma nirudie utoto wangu nivione.

Vijana ambao wameikuta sanaa yetu katika nyakati hizi za Instagram ni ngumu kuelewa ninachozungumza.

Kuna mambo ya zamani kila nikiyakumbuka naona utamu wa muziki na maigizo yetu. Naona tasnia ya Burudani kuna vitu inamiss aisee.

Hebu tukumbuke namna ambavyo kwenye Taarab kulikua kunawaka moto siyo masihara? Hivi bado muziki huu wa mwambao upo maana hautambi tena.

Battle ya Bi Khadija Kopa na Chama lake la Tanzania One Theatre (TOT) dhidi ya mhasimu na mpinzani wake Marehemu Aunt Nasma Khamis Kidogo akiwa na Bendi yake ya Muungano Culture Group haikua na mfano wake.

Wapenzi wa Taarab waligawanyika. Watu waligawana upande. Hawa wangetamba na mipasho ya Bi Khadija, wengine wangewehuka na vijembe kutoka kwa Aunt Nasma. 

Upinzani na ushindani ulikuepo wa kutosha na bado haikuwahi kujulikana nani bora zaidi ya mwingine. Kila upande uliamini mtu wao ndiye bora.

Ushindani wa Nasma na Khadija ulikua ni wao peke yao haukuyahusu makundi. Ulikua ni upinzani binafsi ambao TOT wala Muungano haukuwahusu.

Ni kusema kwamba Nasma na Khadija walikua wakubwa kuliko Muungano Culture na TOT. Wakubwa kuzidi waajiri wao. Wanastahili nyota za kutosha hawa Mama zetu.

Baadaye kuliibuka ushindani wa makundi mawili ya Zanzibar Modern Taarab na East African Melody. Vita ilikua kubwa. 

Burudani ilitolewa. Siasa za Muziki zikayavunja makundi haya. Toka hapo Taarab imegeuka kuwa Bongo Fleva.

Vipi kuhusu Michezo ya kuigiza kila Jumamosi, Jumapili kwenye Runinga ya Mzee wetu Hayati Reginald Mengi? Ebwana Kaole walijua kututeka haswa.

Maisha, Jahazi enzi za kina Mr Bomba, Swebe Santana, Sinta na Mtunis katika ubora wao ilikua siyo masihara.

Kipindi hicho ikifika wikiendi unaoga mapema unasubiri taarifa ya habari iishe ngoma ianze. 

Hakukua na suala la kununua kifurushi cha King'amuzi ulikua ni mwendo wa kuzungusha Antenna kutegesha chaneli vizuri.

Maigizo yalikiki mjini. Hakukua na kusimuliana Tamthiliya za akina Sultana. 

Tungepeana stori za Maisha ya akina Mashaka au namna Joti na Mpoki walivyokua wakimdhulumu mlugaluga Masanja Mkandamizaji kwenye Maigizo ya Mambo Hayo.

Kipindi Fulani hata Maigizo ya Kenya yalitukamata kisawa-sawa. Ulikuepo mchezo wa Tausi. Uliojaa wakali akina Mzee Kasry, Kalumanzira, Sitti, Baraza na Mjuba. 

Walitisha kinoma noma. Siyo leo wamebaki na Komedi ya akina Omondi na Churchill Show. Hata wao wenyewe wanajua wamezingua.

Bado sijakushawish kumiss mambo ya zamani? Tusogee kwenye Bongo Fleva kidogo. Hivi ilishawahi kutokea battle kama ya wahuni wa TMK Wanaume Family na watoto wa kishua East Coast Team ya Upanga?

Ebwana hii ilikua ni zaidi ya vita. King Crazy Gk angepiga autro kwenye Leo Tena akisema, "TMK mwisho Rap kuwakilisha".

Kisha Juma Nature akajibu kwenye autro ya Kamua ngoma ya KR Mulla, " Najua umesikia TMK siyo mwisho Rap kuwakilisha". Ushindani ulikua mkubwa na ulisisimua.

Matamasha ya muziki yangejaa sana kutokana na battle za namna hii. ECT ya akina GK, AY na FA walikua watoto wa kishua kweli.

Video zao mavazi yao na mikogo yao ilijawa u-Marekani. TMK waliwateka watoto wa Kiswazi kwa Swaga zao. Staili ya Mapanga haijawahi kumuacha yeyote salama.

Hapo hapo Temeke wakati TMK wakipepetuana na ECT, Supastaa wa Bongo Fleva wakati huo na Kinara wa TMK, Juma Nature nae alikuwa na 'bifu' yake na Mkali wa Staili, Inspector Haroun Babu.

Kama kuna bifu ilichangamsha Bongo Fleva basi hii nayo ni mojawapo. Kosa kubwa lilifanywa walipokubali kurekodi remix ya Mzee wa Busara. 

Ghafla nimeukumbuka ubabe wa Kalapina na wajuba wake wa Kikosi Cha Mizinga. Hawa washikaji walikua watemi sana. 

Wangeweza kumkalisha yeyote ambaye wangemuona anaenda kinyume nao. Siwezi kusahau varangati lao na watoto wa Arusha Nako 2 Nako.

Memba wa N2N, Bou Nako aliingia kwenye rada za Kikosi, basi mkono ukapigwa siyo kitoto. Tokea hapo bifu likazidi. 

Washikaji wa Arusha wakaapa siku Kalapina na Kikosi wakienda Arusha hawatoki salama. Hivi Pina ushawahi kwenda Chuga tena?

Ila makundi ya muziki hayapo siku hizi, wako wapi Unique Sisters wale watoto wa Mzee Kipozi! HBC, Kwanza Unit na Mabaga Fresh? Hakika siwezi kusahau Banjo ya Mandojo na Domokaya.

Bado nakumbuka namna ambavyo Ray C alitumaliza na kiuno chake bila mfupa.Kama unadhani wakina Diamond ndio wasanii wa kwanza kurekodi video zao nje basi unajidanganya. 

Ray C mkwaju wake wa Uko wapi, alishuti video yake nchini Japan. Hiyo nazungumzia miaka 15 iliyopita. Rehema alikua mwanadada wa aina yake katika wakati wake.

Alituvuruga. Tulifurahia kusoma matukio na skendo zake kwenye magazeti kila wiki. Katika zama ambazo bado tuna ushamba wa ustaa, Ray C tayari alikua na Tattoo, vipini kwenye ulimi, kitovuni. 

Mavazi yake hayakumtofautisha na Beyonce wala Mary J Blige. Kweli nyakati hupita. Leo hatumzungumzi tena.

Stori za Wema na Diamond zimewahi kukuchanganya? Wazee wa Old School tulidatishwa na mahusiano ya mhuni Juma Nature na Sista Duu wa Maigizo Sista.

Shukrani kwa magazeti pendwa maana bila wao tusingejua namna Nature alivyokua amedatishwa na Sinta. Labda tungekuja kujua baada ya kupigana chini Kwa kuwa Juma alimtungia wimbo Sista.

Magazeti pendwa ndio yalikua Instagram kwetu. Ubuyu wote tungeupata kwenye Ijumaa au Amani. Hakukua na kununua bando. Ni mwendo wa Hard Copy tu.

Hivi unaona Miss Tanzania pako sawa pale? Nasikia Miss Mbeya wa mwaka huu alipewa Bodaboda kama mshindi.

Enzi ya Miss Tanzania ya Anko Lundega aisee msisimko ulikuepo. Kuanzia ngazi za chini mpaka Taifa.

Nani amesahau mchuano mkali wa mwaka 2001 kati ya Happiness Millen Magese na Miriam Odemba? Mzuka wa Miss Tanzania ulikua mkubwa sana. Lilikua ni shindano kubwa na maarufu zaidi Bongo. Leo ladha haipo tena.

Bado naendelea kukumbuka namna ambavyo shindano la Mkali wa Rhymes lilivyoiteka Nchi. Wapo watu mpaka kesho hawataki kukubali ushindi wa Afande Sale.

Sijui leo Braza Shigongo akiandaa tena nani atashinda. Wacha nimkumbuke mshikaji wetu Cool James Dandu ninapoona tuzo zake za Kilimanjaro Music Awards zikiwa zimefunikwa na hazipo tena. Mwamba hatumtendei haki.

0683 015145


KATIBU MKUU WA CCM DKT.BASHIRU ATUA ZANZIBAR.

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amewasili Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya kuimarisha Chama.  
Ziara hiyo itakayoanza Novemba 26 hadi Disemba 4 mwaka huu kwa upande wa Unguja na Pemba ambapo atashiriki shughuli mbali mbali za kichama kwa kuzungumza na Viongozi wa ngazi mbali mbali sambamba na kuzindua miradi ya maendeleo.
Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini hapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mzee Abeid Amani Karume, alishukru kwa mapokezi makubwa yaliyofanywa na Viongozi na Wanachama wa CCM.
 Katika maelezo yake Dkt.Bashiru mara baada ya kukutana na wenyeji wake, alisema ushindi wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopatikana kwa upande wa Tanzania bara ni kielelezo tosha cha ushindi wa mwaka 2020.
Alisema ushindi huo wa asilimia 99 umepatikana kutokana na kukubalika kwa Chama Cha Mapinduzi kwa wananchi wanaonufaika na utekelezaji wa Ilani ya CCM Mijini na Vijijini.
Aidha, Dkt.Bashiru akizungumzia ziara yake alifafanua kuwa lengo la ziara hiyo ni kushauriana na Wana CCM masuala mbali mbali yatakayosaidia kuendelea kuimarisha CCM.
“Nitaanza ziara yangu Unguja kasha kumalizia Pemba, nitakutana na Wanachama mbali mbali nizungumze nao kuhusu masuala ya kuendelea kukijenga Chama chetu kwani tupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.”,alisema Dkt.Bashiru.
Dr Bashiru ataanza ziara zake leo (jana) kwa kukutana na kuzungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar DK. Ali Mohamed Shein ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Naye Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao, aliwasihi Wanachama, Viongozi na makada wa Chama hicho kujitokeza kwa wingi katika maeneo mbali mbali ambayo Dkt.Bashiru atafanya ziara zake.
 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Bashiru Ally Kakurwa, akivishwa shada la maua na Vijana Maalum baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wa Zanzibar kwa ajili ya ziara ya kikazi na  kuimarisha Chama ya Siku Tisa Zanzibar.
 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Bashiru Ally Kakurwa, akizungumza na Viongozi na Watendaji mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi walioshiriki katika Mapokezi mara baada ya kuwasili Zanzibar kwa ajili ya ziara ya Siku Tisa, inayotajia kuanza Novemba 26 hadi Disemba 4 Mwaka huu.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Bashiru Ally Kakurwa,akisalimiana na Wanachama wa CCM pamoja na Vijana mbali mbali walioshiriki katika mapokezi yake mara baada ya kuwasili Zanzibar kwa ajili ya ziara ya Siku Tisa inayotajia kuanza Novemba 26 hadi Disemba 4 Mwaka huu.

VIFURUSHI BIMA YA AFYA YA NHIF HADHARANI, KUZINDULIWA NOVEMBA 28,2019

$
0
0

Na Avila Kakingo , Globu ya Jamii
VIFURUSHI vya Huduma ya afya kwa kutumia Bima ya afya ya mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) vyawekwa hadharani ili kila mtanzania aweze kutumia bima hiyo.

Hata hivyo katika taarifa iliyotolewa leo Novemba 26,2019 na mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) inaonyesha kuwa vifurushi hivyo vitazinduliwa Novemba 28 katika viwanja vya mnazi mmoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. 

Taarifa hiyo inaeleza kuwa uzinduzi huo wa vifurushi hivyo utafunguliwa na kampeni ya usajili wa wananchi watakaohitaji kujiunga na vifurushi hivyo ikiwa na upimaji afya bure kwa wananchi.

Vifurushi hivyo kwa mtu binafsi mwenye umri wa miaka 18 hadi 35 kwa kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 192,000, kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 384,000,  kifurushi cha timiza afya shilingi 516,000.

Kwa wenye umri wa miaka 36 hadi 59 kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 240,000, kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 444,000, na kifurushi cha timiza afya ni shilingi 612,000.

Na kwa wenye umri wa miaka 60 na kuendelea kwa kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 360,000 kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 660,000 na kifurushi cha timiza afya ni shilingi 984,000.

Kwa upande wa bima ya Mume na mke tuu kwa wenye umri wa miaka 18-35 Kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 384,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 732,000 ,  kifurushi cha timiza afya shilingi 996,000.

Kwa wenye umri wa miaka 36 hadi 59 kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 456,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 864,000 , na kifurushi cha timiza afya ni shilingi 684,000.

Na kwa wenye umri wa miaka 60 na kuendelea kwa kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 684,000 kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 1,284,000 na kifurushi cha timiza afya ni shilingi 1,906,000.

Hata hivyo kwa mke,mume na watoto mmoja wenye umri wa miaka 18 hadi 35 Kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 504,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 924,000 ,  kifurushi cha timiza afya shilingi 1,272,000.

Kwa wenye umri wa miaka 36 hadi 59 kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 576,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 1,068,000 , na kifurushi cha timiza afya ni shilingi1,464,000.

Hata hivyo kwa mke,mume na watoto wawili (2)wenye umri wa miaka 18 hadi 35 Kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 612,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 1,116,000 ,  kifurushi cha timiza afya shilingi 1536,000.

Kwa wenye umri wa miaka 36 hadi 59 wakiwa na watoto wao wawili kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 696,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 1,272,000 , na kifurushi cha timiza afya ni shilingi1,728,000.

Kuwa makini katika kufatilia hili na kwa mke,mume na watoto watatu (3)wenye umri wa miaka 18 hadi 35 na watoto wao Kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 720,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 1,284,000 ,  kifurushi cha timiza afya shilingi 1,788,000.

Kwa wenye umri wa miaka 36 hadi 59 wakiwa na watoto wao watatu kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 804,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 1,416,000 , na kifurushi cha timiza afya ni shilingi1,980,000.

Hapa ni kwa wale mume na mke na wenye watoto wanne (4) wenye umri wa miaka 18 hadi 35 pamoja na watoto wao Kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 8160,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 1,52,000 ,  kifurushi cha timiza afya shilingi 2,028,000.

Kwa wenye umri wa miaka 36 hadi 59 wakiwa na watoto wao wanne kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 900,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 1,584,000 , na kifurushi cha timiza afya ni shilingi 2,220,000.

Hata hivyo NHIF kwa upande wa mtu binafsi na mtoto mmoja (1) wameweka vifurushi vifuatavyo kwa wenye umri wa miaka 18 hadi 35 Kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 312,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 576,000 ,  kifurushi cha timiza afya shilingi 792,000.

Na Kwa wenye umri wa miaka 36 hadi 59 wakiwa na watoto wao wanne kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 360,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 648,000 , na kifurushi cha timiza afya ni shilingi 888,000.

Pamoja na hayo NHIF kwa Mtu binafsi na mwenye watoto wawili (2)vifurushi vifuatavyo kwa wenye umri wa miaka 18 hadi 35 Kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 312,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 576,000 ,  kifurushi cha timiza afya shilingi 792,000.

Na Kwa wenye umri wa miaka 36 hadi 59 wakiwa na watoto wao wanne kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 360,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 648,000 , na kifurushi cha timiza afya ni shilingi 888,000.

Pamoja na hayo NHIF kwa Mtu binafsi na mwenye watoto watatu (3)vifurushi vifuatavyo kwa wenye umri wa miaka 18 hadi 35 pamoja na watoto, Kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 540 ,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 924,000 ,  kifurushi cha timiza afya shilingi 1,308,000.

Na Kwaupande wa wenye umri wa miaka 36 hadi 59 wakiwa na watoto wa watatu kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 576,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 996,000 , na kifurushi cha timiza afya ni shilingi 1,404,000.

Hata hivyo NHIF kwa Mtu binafsi na mwenye watoto wanne (4)vifurushi vifuatavyo kwa wenye umri wa miaka 18 hadi 35 Kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 636,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 1,092,000 , na kifurushi cha timiza afya shilingi 1,548,000.

Na Kwa wenye umri wa miaka 36 hadi 59 akiwa na watoto wanne kifurushi cha Najali afya premium ni shilingi 672,000 , kifurushi cha wekeza afya premium ni shilingi 1,164,000 , na kifurushi cha timiza afya ni shilingi 1,644,000.

Hata hivyo taarifa hiyo inawakaribisha wananchi wote kwa ujumla kwaajili ya kujiunga katika mfuko huo kwaajili ya kujikinga na bima ya afya kabla ya kuugua kwa uhakika wa matibabu.

BENKI YA BIASHARA NA MAENDELEO MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA YAAHIDI KUTOA FEDHA UJENZI WA RELI YA KISASA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, akimpokea Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse wakikagua mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Dar es Salaam – Morogoro, wakiwa wameambatana na Ujumbe kutoka Benki hiyo, Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango na Watumishi wa TRC, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, akimuonesha Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse michoro ya Reli ya Kisasa itakavyokuwa baada ya ujenzi kukamilika, alipotembelea Ujenzi wa Mradi huo, sehemu ya kipande cha reli kutoka Dar es Salaam – Morogoro.

Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse akiangalia chuma kilichotumika kutengeneza njia ya treni alipotembelea Ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa alipotembelea Ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse akizungumza na vyombo vya habari ambapo ameipongeza Serikali kwa hatua nzuri ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), Jijini Dar es Salaam.

…………….

Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

Rais na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Dkt. Admassu Tadesse ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR) kwa kutumia fedha zake za ndani na kuahidi kuwa Benki yake itafanya kila linalowezekana kuhakikisha inatafuta fedha za kujenga reli hiyo

Dkt. Tadesse ametoa kauli hiyo alipotembelea sehemu ya ujenzi wa miundombinu ya reli hiyo, kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro na kujionea kazi kubwa iliyofanyika ambapo amesema mradi huo hautainufaisha Tanzania peke yake bali pia nchi za ukanda wa Afrika hususan ambazo hazipakani na Bahari.

Kiongozi huyo wa juu wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Dkt. Tadesse, ameeleza kuwa mwaka huu Benki yake imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani bilioni moja sawa na takribani sh. za Tanzania trilioni 2.3 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi yake mikubwa ya maendeleo.

Ameongeza kuwa Tanzania imenufaika pia na kiasi kingine cha zaidi ya dola za Marekani bilioni moja zilizotolewa na Benki yake miaka ya nyuma na ameelezea kufurahishwa kwake na namna nchi inavyokua kwa kasi kiuchumi na kwamba inakopesheka.

Aliahidi kuwa kwa kuwa fedha zinazohitajika kukamilisha ujenzi wa mradi huo wa reli ya kisasa ni nyingi, Benki yake itazishawishi taasisi nyingine za fedha ndani na nje ya Bara la Afrika kuchangia ujenzi huo ili mradi ukamilike kwa wakati ili kuchochea masuala ya Bashara na kuboresha shughuli za usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bw. Masanja Kadogosa, ameishukuru Benki hiyo kwa kuonesha nia ya kusaidia ujenzi wa Reli hiyo katika awamu zinazofuata.

Alisema kuwa mpaka sasa ujenzi wa Reli ya Kisasa ambao umetumia fedha za ndani kati ya Dar es Salaam hadi Morogoro umekamilika kwa asilimia 72 huku kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida kikiwa kimekamilika kwa asilimia 22.

Bw. Kadogosa amesema kuwa Serikali inatafuta fedha nyingine kwa ajili ya kujenga reli hiyo kuanzia Makutupora, Tabora, Isaka hadi Mwanza na kwamba watafanya mazungumzo na Benki hiyo kuona namna watakavyofadhili ujenzi huo.

WAZIRI WA KILIMO AWASILISHA TAKUKURU RIPOTI YA UKAGUZI WA VYAMA VYA USHIRIKA YENYE UBADHILIFU WA ZAIDI YA BIL 124

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Katikati) akimkabidhi Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbung’o muhtasari wa uchambuzi wa ukaguzi wa vyama vya Ushirika uliofanywa na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika COASCO katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kilimo katika mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kushoto), akisisitiza jambo wakati wa makabidhiano ya muhtasari wa uchambuzi wa ukaguzi wa vyama vya Ushirika uliofanywa na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika COASCO katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 kwa TAKUKURU hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kilimo katika mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma. Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Prof Siza Tumbo wakifatilia mkutano huo.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Katikati) akisisitiza jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya muhtasari wa uchambuzi wa ukaguzi wa vyama vya Ushirika uliofanywa na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika COASCO katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 kwa TAKUKURU hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kilimo katika mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya muhtasari wa uchambuzi wa ukaguzi wa vyama vya Ushirika uliofanywa na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika COASCO katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 kwa TAKUKURU hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kilimo katika mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma. Mwingine pichani ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbung’o.





Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Katika mwaka wa fedha wa 2018/19 Serikali ilitoa maagizo kwa Shirika la COASCO kukagua Vyama vya Ushirika vyote. Mpaka tarehe 30 Juni, 2019 Vyama vya Ushirika vilivyosajiliwa vilikuwa 11,410. Kati ya Vyama hivyo, Vyama hai ni 6,463; Vyama Sinzia ni 2,844 na Vyama ambavyo havipatikani 2,103.

Kutokana na maagizo hayo, hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2019 COASCO ilikagua Vyama vya Ushirika vipatavyo 4,413 sawa na asilimia 102.63 ya Lengo la Serikali la kukagua Vyama 4,300.

Katika vyama hivyo 4,413 vilivyokaguliwa, vyama 303 (6.87%) vilipata Hati inayoridhisha, vyama 2,378 (53.89%) vilipata Hati yenye shaka, vyama 879 (19.92%) vilipata Hati isiyoridhisha na vyama 853 (19.32%) vilipata Hati mbaya.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa takwimu hizo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kumkabidhi Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbung’o ya muhtasari wa uchambuzi wa ukaguzi wa vyama vya Ushirika uliofanywa na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika COASCO katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kilimo katika mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Waziri Hasunga alisema kuwa Kati ya Vyama Vikuu 38,Vyama 4 vilipata Hati Safi, vyama 22 vilipata Hati yenye shaka, 9 vilipata hati isiyoridhisha na 3 hati mbaya. Vyama hivyo Vikuu 3 vilivyopata HATI MBAYA inayohusisha hoja zenye viashiria vya ubadhirifu wenye Jumla ya shillingi 856,357,955 kwa RUNALI, SCCULT 4,878,662,431 na KYECU kwa kukosekana kwa hati za kuhesabu mali za kudumu mwisho wa mwaka. 

Alisema kuwa Chama Kilele (Shirikisho-TFC) kimepata Hati Isiyoridhisha ambayo inajumuisha fedha benki zisizofanyiwa malinganisho na pia kutooneshwa katika taarifa za fedha kiasi cha shilling 1,538,726,787

Kati ya Vyama vya Ushirika wa Mazao (AMCOS) 2,710 vilivyokaguliwa, vyama 15 vilipata Hati Safi, 1347 Hati yenye Shaka, 599 Hati Isiyoridhisha na vyama 749 vilipata Hati Mbaya. Matatizo makuu katika vyama hivyo vya AMCOS ni kushindwa kuandika vitabu vya hesabu, malipo mengi kutokuwa na vielelezo vya malipo, mifumo dhaifu ya udhibiti wa makusanyo na mauzo ya mazao, kukosekana kwa daftari la mali za vyama na watendaji wa vyama kutokuwa na weledi wa kuandika vitabu na taarifa za fedha za vyama. Kati ya SACCOS 1,448 SACCOS 261 zilipata Hati Safi, 887 yenye Shaka, 218 Isiyoridhisha na 82 Hati Mbaya.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyataja matatizo makuu ya SACCOS nyingi kuwa ni kushindwa kuandika vitabu ipasavyo, marejesho ya mikopo ya wanachama kutofanyika kwa wakati, baadhi ya waajiri kuchelewesha kuwasilisha makato ya wanachama kwa SACCOS, madeni makubwa yanayothiri utendaji wa SACCOS, miamala ya benki kutofanyiwa malinganisho na baadhi ya miamala kuwa na ubadhirifu.

Mhe Hasunga amesema kuwa katika ukaguzi wa kawaida kwa mwaka 2018/2019 Fedha zenye Mashaka (nia ovu) ni Tsh 87,694,976,970, Hasara iliyotengenzwa kwa uzembe ni Tsh 22,861,038,064 huku Wizi/Ubadhirifu ikiwa ni Tsh 2,840,752,866 ambapo jumla ya fedha hizo ni Tsh 113,396,767,900

Pia alisema kuwa katika ukaguzi maalumu kwa mwaka huo wa 2018/2019 Fedha zenye Mashaka (nia ovu) ni Tsh 6,266,796,345.63, Hasara iliyotengenzwa kwa uzembe ni Tsh 2,634,438,512.00 wakati Wizi/Ubadhirifu ni Tsh 1,755,248,116.00 ambapo jumla yake ni Tsh 10,656,482,973.63

Amesema kuwa jumla kuu ya fedha za ukaguzi wa kawaida na ukaguzi maalumu ni kwa mwaka wa fedha 2018/2019 mi Tsh 124,053,250,874.00
Alisema kuwa mbali na vyama hivyo vilivyokaguliwa, vipo vyama 682 vilikataa kuwasilisha vitabu kwa ajili ya ukaguzi na kuongeza kuwa Kati ya vyama 853 vyenye Hati Mbaya, vipo vyama vyenye viashiria vya ubadhirifu wa fedha na mali vipatavyo 130 na vyama vyenye matatizo mbalimbali ya uongozi na utendaji 723.

Pia, Amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa hiyo aliyoikabidhi TAKUKURU baadhi ya Waajiri wameonekana kuchelewesha michango ya Wanachama baada ya makato na kuathiri uhai wa vyama katika kutoa mikopo kwa Wanachama.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images