Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109977 articles
Browse latest View live

BILIONI 5 KUPELEKA MAJI YA ZIWA VICTORIA BUKENE WILAYANI NZEEGA

$
0
0
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa (kulia) akikagua jana chemba ya kutolea upepo kwenye eneo la Uchama wilayani Nzega wakati alipopita kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani Tabora.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa(katikati) akitoa maelekezo jana kwa Mkandarasi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Tabora wakati alipopita Wilayani Nzega kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo.
Meneja Mradi kutoka WAPCOS Mattewada Manohar(mwenye T shirt )akimuonyesha Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa(kushoto) sehemu ya maungio ya bomba la kupeleka maji Igunga na yale ya kwenda kwenye tenki la Ushirika Nzega wakati alipopita Wilayani Nzega kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani Tabora.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa (aliye mstari wa pili kushoto) akishuka kutoka kwenye Tenki kubwa la maji lilipo Ushirika Wilayani Nzega wakati alipopita jana kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani Tabora.PICHA NA TIGANYA VINCENT



NA TIGANYA VINCENT

SERIKALI inatarajia kutumia shilingi bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa bomba za maji ya ziwa Victoria kutoka katika tenki la Ushirika lilipo Nzega mjini kwenda Bukene .

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati alipopita Wilayani Nzega kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani Tabora.

Alisema kuwa tayari fedha za ujenzi wa mradi huo zipo na usanifu wa mradi huo umeshafanyika ambapo utakuwa umbali wa Kilometa 36 kutoka maji yatakapochukuliwa kwenye tenki la maji la Ushirika lilipo Nzega mjini hadi Bukene.

Profesa Mbarawa alisema katika mpango wa awali Bukene haikuwepo kwenye mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria ,lakini Serikali imetafuta pesa kwa ajili ya kujenga mradi huo.

Alisema kwa kuwa fedha zipo kazi hiyo itaanza mara moja ambapo kukamilika kwake utasaidia kutatua tatizo la maji katika Vijiji 19 vya Bukene kwa kuwahakikishia wakazi wa eneo hilo wanapata maji safi na salama mapema.Aidha Waziri huyo alisema utekelezaji wa mradi wa kuleta kutoka Ziwa Victoria kwa ujumla umefikia asilimia 85 na anatarajia kuanzia mwezi Desemba mwaka huu utakuwa umekamilika kwa kiwango kikubwa na wananchi wataanza kupata maji safi na salama.

Aliongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inapeleka maji safi na salama kwa wananchi wengi ili kuwaondolea tatizo la maji.
Awali Mhandisi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoani Tabora (TUWASA), Athuman Kilundumya alisema zaidi ya watu 240,000 wanatarajia kunufaika na ongezeko la eneo la utekelezaji wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria katika Wilaya za Igunga, Nzega na Uyui.

Alitaja maeneo ambayo yatanufaika kuwa ni Bukene wilayani Nzega ambapo Vijiji 19 vitapata maji hayo, Nkinga wilayani Igunga vijiji saba na Kigwa wilayani Uyui , vijiji 16 vya Kata za Igalula, Goweko na Kigwa navyo vinatarajia kupata maji hayo.

Kiludumya alisema kuwa utekelezaji wa mradi wa kuleta maji toka Ziwa Victoria huko katika hatua nzuri na ndani ya wiki tatu maji yatakuwa yamefika katika Manispaa ya Tabora.

NMB YAANDAA KONGAMANO LA SOKO LA HISA NA DHAMANA ZA SERIKALI KWA WEWEKEZAJI

$
0
0
 Meneja wa Masoko ya Fedha kutoka Benki Kuu (BoT), Bw. Lameck Kakulu (wakwanza kulia) akielezea kuhusu soko la hisa Tanzania kwa wawekezaji mbalimbali wakati wa kongamano lililoratibiwa na Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa utafiti, Sera na Mipango wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji (CMSA), Alfred Mkombo, Meneja Mwandamizi wa huduma za Dhamana kutoka NMB, Bw. Avith Massawe na Mkurugenzi Mtendaji wa FIMCO Bw Ivan Tarimo.  
 Mweka Hazina wa Benki ya NMB, Aziz Chacha akiongea na wawekezaji wa Soko la Hisa na Dhamana za Serikali kuhusu huduma mpya ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji katika masoko ya mitaji wakati wa kongamano lililoratibiwa na Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
Meneja Mwandamizi wa Huduma za Dhamana kutoka NMB, Bw. Avith Massawe akiwafunda wawekezaji wa soko la hisa na dhamana za serikali wakati wa kongamano hilo.

MTAZAMO/HOJA/NIONAVYO- MFUKO WA PAMOJA MKOMBOZI WA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI

$
0
0
Na Ismail Ngayonga,MAELEZO

DAR ES SALAAM

AFYA bora ni nguzo na raslimali muhimu katika kuchangia maendeleo ya mtu binafsi, familia na nchi hususan katika kuleta maisha bora na kupunguza umaskini.

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kutoa kipaumbele katika huduma za afya zenye ubora na zinazowafikia wananchi wote ili kuboresha afya zao kwa kuzingatia sera na miongozo iliyopo.

Sera ambayo imeendelea kutumika katika kuelekeza utoaji wa huduma za afya ilipitishwa mwaka 1990, ambapo tangu ilipopitishwa, yamekuwepo mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi na kijamii, mabadiliko ya sayansi na technolojia na kuongezeka kwa magonjwa.

Aidha mabadiliko na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Serikali yalitoa changamoto mpya katika utoaji wa huduma za afya na yamechangia kwa pamoja kuifanya sera iliyopitishwa mwaka 1990 kutokidhi mahitaji na matarajio ya sasa na ya miaka ijayo.

Mwaka 1996 marekebisho ya sera yalipitishwa kwa lengo la kuanzisha mfumo mpya wa utoaji na uendeshaji wa huduma za afya katika ngazi ya wilaya, na katika marekebisho hayo ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa afya ulitambuliwa na kupewa msukumo na kukasimu usimamizi wa utekelezaji katika mamlaka za Serikali za Mitaa.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaratibu Mfuko wa Pamoja wa Afya ulioanzishwa mwaka 1996 na kufadhiliwa na wadau 7, ambao ni Denmark, Uswisi (SDC), Ireland, Canada, Benki ya Dunia, UNICEF na Korea Kusini ili kuleta ufanisi na matokea makubwa katika utekelezaji wa miradi ya afya nchini.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2017/2018, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu anasema kupitia Sekretarieti ya Uratibu wa Mfukomajadiliano mbalimbali kati ya Serikali na Wadau vimekuwa vikifanywa ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya Serikali jinsi inavyotekeleza kazi zinazogharamiwa na fedha za Wadau.

Anaongeza kuwa wanufaika wa Mfuko huu ni OR -TAMISEMI, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto (Idara kuu ya Afya), Mikoa na Halmashauri zote nchini, ambapo Fedha hizo hugawiwa kwa fomula kwa kuzingatia makubaliano kati ya Serikali na Wadau wanaochangia Mfuko.

‘Serikali kupitia Wizara yake inaendelea na juhudi za kuwaleta pamoja wadau wengine zaidi ili wachangie katika Mfuko huo ili kuleta ufanisi na matokea makubwa katika utekelezaji wa miradi ya afya nchini’’ anasema Waziri Ummy.
Waziri Ummy anasema kuwa Asilimia 90 ya fedha zote hupelekwa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa, asilimia 6 ya fedha hizo hutumika katika Wizara ya Afya kwa ajili ya masuala ya uratibu, usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Kisera katika Sekta ya Afya.

Aidha Waziri Ummy anasema kuwa asilimia 3 ya fedha hizo hupelekekwa katika Mikoa kwa ajili ya kugharamia ufuatiliaji katika ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa na asilimia 1 ya fedha zote hupelekwa Makao Makuu ya OR– TAMISEMI kwa ajili ya kugharamia ufuatiliaji katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy, anasema hadi robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2016/17, kiasi cha Tsh. Bilioni 88.8 kimepokelewa kupitia Mfuko wa Pamoja wa Afya na kati ya fedha hizo, Tsh Bilioni 5.6 zilipokelewa na Wizara ya Afya, Tsh. milioni 865.1 zilipokelewa na OR-TAMISEMI, Tsh. Bilioni 2.6 zilipokelewa na Mikoa na kiasi cha Tsh. Bilioni 79.7 zilipokelewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

‘Fedha hizi hutumika kadiri ya Mkataba wa Makubaliano kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo, ambapo asilimia 33 ya fedha zinazopelekwa katika Halmashauri zinatakiwa kutumika kama nyongeza ya fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa na asilimia 67 ni kwa ajili ya utekelezaji wa afua mbalimbali ambazo zinalenga kuboresha huduma za afya nchini’’ alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy anaongeza kuwa pamoja na kuzingatia vigezo vya usawa katika kugawanya fedha za Mfuko, muelekeo wa Wadau kwa sasa ni kutoa umuhimu kwa ufanisi katika utekelezaji wa kazi zilizokubaliwa ili kuongeza ufanisi katika kazi zinazokubaliwa kuviwezesha vituo vya kutolea huduma za afya kupata fedha kwa wakati na kuweza kufanya maamuzi ya haraka ya kutumia fedha hizo kulingana na mahitaji ya kituo husika.

Akifafanua zaidi Waziri Ummy anasema Wizara imeandaa utaratibu wa kuwezesha fedha za Mfuko kutumwa moja kwa moja kwa vituo vya kutolea huduma za afya ili kuviwezesha vituo kununua dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi kulingana na mahitaji yao kwa haraka na Halmashauri zitabaki na jukumu la kusimamia na kufuatilia matumizi ya fedha hizo.

Mfuko wa Pamoja wa Afya ni Mpango mahsusi, ulioanzishwa na Serikali kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa fedha kupitia kamati za usimamizi za kutolea huduma za afya katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, hivyo ni wajibu wa Mamlaka hizo kuwajengea uwezo watoa huduma za afya utekelezaji wa afua mbalimbali ambazo zinalenga kuboresha huduma za afya nchini.

MAFUNZO YA AWALI JESHI LA AKIBA WILAYA YA CHEMBA YAMALIZIKA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga awapongeza wazazi wa wilaya ya Chemba kwa kuonyesha ushirikiano kwa kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika Mafunzo ya Jeshi la Akiba na ikumbukwe kuwa mzalendo ni pamoja na kutumikia nchi yako hata kwenye ulinzi na usalama wa Taifa. 

Mhe. Simon Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa anafunga rasmi Mafunzo ya Jeshi la Akiba kundi la kumi yaliyomalizika Tarehe , 23/11/2019 katika viwanja vya shule ya msingi Chemba. 

“Jamii inapaswa itambue kazi ya Mgambo mtu yoyote anaweza kuifanya awe mtu wa hali ya chini au juu anaweza kupata Mafunzo, kwani lengo hasa ni kujenga utimamu wa mwili,uzalendo ili kutumikia taifa lao”aliongeza kwa kusema hivyo Mhe.Simon Odunga. 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus H.Mashimba amefurahishwa kwa wito wa vijana kushiriki kwenye Mafunzo, inaonyesha dhahili kuwa wilaya ya Chemba inakuwa kimaendeleo na ameahidi wanafunzi waliohitimu mafunzo atafanya nao kazi kwa ushirikiano. 

Meja wa Wilaya ya Chemba Joseph Narsis amesema Mafunzo hayo yalianza Tarehe, 1/7/2019 na kumalizika 23/11/2019 ,walianza na wanafunzi 72 na kumalizika wanafunzi 52 ,wanawake 9 ,wanaume 43,changamoto zilikuwepo ikiwemo baadhi yao kutoona umuhimu wa mafunzo hayo na kukatishana tama lakini waliweza kukabiliana nazo paka kuweza kukamilisha Mafunzo hayo.

CHOMBO CHA MAJI CHA FADHILI MIRADI 119, BARA LA AFRIKA

$
0
0
Waziri wa maji na umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa mawaziri wa maji wa bara la Afrika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya mawaziri wa bara la Afrika wakimsikiliza moja ya watoa maada katika mkutano wa mawaziri wa bara la Afrika wanaoshughulikia maji.

MAWAZIRI wa maji wa bara la Afrika wakutana jijini Dar es Salaam kujadili mpango ya maendeleo ya maji safi na maji taka katika nchi za bara la Afrika.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa wa maji wa bara la Afrika jijini Dar es Salaam leo, Waziri wa maji na umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Chombo cha Maji cha Afrika kianzishwa kwa lengo la kuchangia maendeleo ya maji na usafi wa mazingila kwa nchi za Afrika.

Mbarawa amesema kuwa chombo hicho kilianzishwa 2006 hadi leo na kimemeshafadhili miradi 119 katika bara la Afrika na imegharimu zaidi ya uro milioni 156.

"Chombo cha Maji kwa upande wa Tanzania kimesaidia kuchimba bwawa lililosimamiwa na Tanesco, bwawa la kikongwe na takribani uro milioni moja nukta tisa sita (1.96) pia chombo hiki ndicho kilicho simamia mradi wa maji safi na salama cha Arusha uliogharimu shilingi bilion 520, ambapo mradi huo utakapomalizika utasaidia na kubadilisha maisha ya wakazi wa Arusha hasa kwenye eneo la maji safi na salama pia maji taka".Amesema Profesa Mbarawa

Profesa Mbarawa amesema kuwa kupitia chombo hicho wataweza kutoa fedha kwaajili upembuzi yakinifu kwenye mabwawa yanayotarajiwa kujengwa Songwe kwaajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wa Tanzania na Malawi.

Hata hivyo Profesa Mbalawa amesema kunajuhudi mbalimbali katika chombo hicho za kutafuta fedha kwaajili ya kuunganisha nchi zote kwa juhudi ya pamoja kwaajili ya kutafuta maji kwa nchi zote za Afrika ili huduma ya maji iwafikie watu wote.

Changamoto kubwa inayowakumba chombo hicho cha maji cha bara la Afrika ni kuwashirikisha sekta binafsi  katika huduma ya maji safi na salama pamoja na uongeza ubunifu katika miundombinu ya huduma ya maji na usafi wa mazingira.

Mhadhiri wa chuo aliyeomba rushwa ya ngono akiri shtaka, ahukumiwa, baada ya makubaliano na DPP

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii
MHADHILI wa Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samson Mahimbo (69), amehukumiwa kulipa faini ya Sh. Milioni tano au kwenda jela miaka mitatu baada kukiri mashtaka yaliyokuwa yakimkabili likiwemo la kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi wake.

Hukumu hiyo imesomwa leo Novemba 26,2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya mshtakiwa kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) ikiwamo kuomba msamaha na kukiri makosa yake.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema tabia ya rushwa ya ngono imekithili na ni gumzo katika vyuo hapa Nchini na kwamba inapaswa kukemewa.

Amesema, kitendo cha wanafunzi kuonyeshwa nyesha majibu kunapelekea kupata wataalamu wasiokuwa na viwango vinavyostahili hivyo njia sahihi ya watu kama mshtakiwa ni kukomesha vitendo Kama hivyo kwa kuwafikisha mahakamani na kuwapatia adhabu chungu. 
"Utalipa faini ya Sh.milioni tano au kwenda jela miaka mitatu" amesema Hakimu Shaidi.

Hakimu Shaidi ameongeza kuwa, kitendo alichofanya ni mshtakiwa huyo ni cha aibu kwa umri wake kwani mtu wa taaluma yake alipaswa kuwa mfano wa kuigwa lakini akaamua kujiingiza katika mapenzi na watoto wadogo ambao si hadhi yake.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo ameshailipa serikali fidia ya Sh.milioni mbili baada ya makubaliano hayo.

Mapema, Wakili wa Serikali Mkuu, Zakaria Ndasco amedai kuwa Jamhuri haina kumbukumbu ya makosa ya zamani ya mshtakiwa na kwamba tayari ameshalipa fidia ya Sh.milioni mbili.

Akitoa utetezi wake, kabla ya kusomwa  kwa hukumu hiyo, Wakili wa utetezi, Claudia Msando amedai mshtakiwa ana umri mkubwa na kwamba ameshaanza kupata maradhi yaa uzee ikiwamo kutokusikia na kuona vizuri na pia ni mstaafu na ana familia inayomtegemea.

Katika kesi ya msingi inadaiwa mshtakiwa  ambaye alikuwa akifundisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza 2015/16 aliomba rushwa hiyo kutoka kwa mwanafunzi Victoria Faustine.

Mwendesha Mashtaka wa taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukutu), Vera Ndeoya alidai kuwa Januari 12, mwaka 2017 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Camp David, iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam mshtakiwa aliomba rushwa ya ngono.

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa huyo akiwa mwajiriwa wa NIT katika kozi ya Usimamizi wa Barabara na Usafirishaji namba LTU 07101 kwakutumia mamlaka yake alimlazimisha mwanafunzi huyo kutoa rushwa ya ngono.

Ilidaiwa kuwa, aliomba rushwa hiyo ili aweze kumfaulisha katika mtihani  wake wa marudio katika kozi ya Usimamizi wa Barabara na Usafirishaji anayosomea ya Januari 5, mwaka 2017.

TRA YAKUSANYA TRILIONI 58.3 MIAKA MINNE

$
0
0
 Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Msafiri Mbibo akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani), kuhusu Mafanikio ya TRA katika Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Tano , Mkutano ulifanyika leo Jumatatu (Novemba 25, 2019) Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Msafiri Mbibo akizungumza na Waandishi wa Habari (Pichani), kuhusu Mafanikio ya TRA katika Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano ulifanyika leo Jumatatu (Novemba 25, 2019) Jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MAMLAKA ya Mapato Tanzania  (TRA) imefanikiwa kuongeza mapato ya serikali kipindi cha miaka minne toka 2016 hadi 2019 kwa jumla ya sh.trilioni 58.3 ikilinganishwa ni miaka minne iliyopita ambapo ilikuwa shilingi trilioni 34.97.

Kwa miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, TRA imekuwa ikikusanya wastani wa shilingi trilioni1.3 ikilinganishwa na wastani wa shilingi bilioni 850 kabla ya awamu ya tano haijaingia madarakani.

TRA imesema kuwa kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba mwaka huu, wastani wa makusanyo umeweza kupanda  na kufikia kiasi cha shilingi trilioni 1.45 kwa mwezi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo amesema kuwa, mafanikio hayo yametokana na msukumo wa serikali ya awamu ya tano  ya kuboresha mikakati ya kuimarisha ukusanyaji wa mapato.

"Mafanikio haya yanatokana na msukumo wa serikali kuendelea kuboresha mikakati ya ukusanyaji wa mapato, kuibua vyanzo vipya vya kodi pamoja na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tano wa TRA wa ukusanyaji wa kodi wenye dhamira ya kuongeza makusanyo  ya kodi za ndani ikiwemo kukuza ulipaji kodi wa hiari kutokana na Mazingira yaliyowekwa kwa wafanyabiashara" amesema Mbibo.

Mbibo amesema kuwa, sababu nyingine ya kuongezeka kwa makusanyo hayo ni pamoja na kuimarika kwa matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFD) baada ya kuondoka katika mfumo wa   stakabadhi zilizokuwa zikiandikwa kwa mkono.

"Mafanikio yametokana pia na uhamasishaji wa Mashine za EFD pamoja na kuboresha mifumo ya makusanyo yanayoendana na mazingira ya sasa ya ukuaji wa sayansi na teknolojia ili kuhakikisha walipa kodi wanalipa kwa urahisi kama ilivyo dhamira ya kurahisisha ulipaji kodi na kufanya mazingira kuwa bora na yanaokoa msongamano pamoja na muda," alibainisha Mbibo. 

Amewapongeza wafanyabiashara wote walioitikia wito wa Serikali kwa kutumia Mashine za Kielektroniki  za EFD bila kuwasahau wananchi ambao wamekuwa wakidai risiti kila wanaponunua bidhaa na huduma mbalimbali.

Naibu kamishna Mkuu huyo amezungumzia mafanikio mengine kuwa ni ongezeko la mizigo kutoka nje ya nchi kupitia bandari za Dar es Salaam na udhibiti wa  makusanyo ya bidhaa zinazopaswa kulipiwa kodi na ushuru ziendazo nje ya nchi mfano zao la korosho na mazao ya ngozi na kwato.

Pia, mwezi Juni mwaka 2018 TRA ilianzisha Mfumo wa Stempu za Kodi za Kielektroniki ulioanza kutumika rasmi  Januari 15 mwaka huu. 

Mbibo amesema kuwa, mfumo huo ni mbadala wa stempu za karatasi zakubandika ambazo zilikuwa zikitumika hapo awali.

Amefafanua kwamba,  lengo la kuanzisha mfumo huo mpya ni pamoja na kuongeza mapato ya serikali yanayotokana na ushuru wa bidhaa, Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Kodi ya Mapato pamoja na kuondoa malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara ya kutokutendewa haki ya makadirio ya kodi zinazosimamiwa na TRA.

"Kutoka na utekelezaji wa mfumo huo kwenye eneo la pombe kali na mvinyo tu, TRA imekusanya ushuru wa bidhaa sh. bilioni 77.8 kwa kipindi cha mwezi Februari hadi Oktoba, 2019 sawa na ongezeko la sh. bilioni 19.6," alisema Mbibo. 

Mbibo ameongeza kuwa, "Kwa upande wa bidhaa za vinywaji laini yaani soda na vinywaji vingine visivyo vya kilevi ambapo matumizi ya mfumo huo yalianza Agosti, 2019, kwa mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu, TRA ilifanikiwa kukusanya sh bilioni 10 ukilinganisha na sh bilioni 9.2 zilizokusanywa kipindi kama hicho mwaka uliopita". 

Msafiri Mbibo ameeleza kuwa ni matumaini ya TRA kuwa jinsi mfumo huo utakavyoimarika na jamii kutambua unavyofanya kazi na umuhimu wake ndivyo mapato yatakavyoongezeka. 

Zawadi zenye thamani ya zaidi ya 500m/- kutolewa kwa washindi

$
0
0


Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa-Tigo Pesa, James Sumari akizindua kampeni iitwayo kishindo cha funga mwaka, kwaajili ya wateja wanao tumia Tigo Pesa. kushoto ni Meneja wa Wateja Maalum-Tigo Pesa, Mary Rutta.
Meneja wa Wateja Maalum-Tigo Pesa, Mary Rutta akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kampeni iitwayo kishindo cha funga mwaka, kwaajili ya wateja wanao tumia Tigo Pesa Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa-Tigo Pesa, James Sumari


Kampuni ya Tigo, kupitia kitengo cha Tigo Pesa imezindua kampeni ijulikanayo kama ‘Kishindo cha Funga Mwaka’ kwa ajili ya kutoa zawadi zenye thamani ya zaidi ya 500m/- kwa wateja wa Tigo wanaoweka na kupokea pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa.

Wateja wa Tigo wanatakiwa kuweka pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa ili kuweza kushiriki kwenye kampeni hiyo ambayo ni maalumu kwa ajili ya msimu huu wa kufunga mwaka ambapo washindi wa zawadi watafunga mwaka kwa kishindo

Kampeni hiyo itakayodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja itashuhudia washindi watatu wakiibuka na fedha taslimu ikiwamo 20m/- kwa mshindi wa kwanza, 15m/- kwa mshindi wa pili na 10/- kwa mshindi wa tatu. Pia, kila wiki kutakua na washindi nane watakaopata 5m/- kila mmoja. Pamoja na washindi wa wiki na wa mwezi, kutakua na washindi nane kila siku ambao wataibuka na 1m/- kila mmoja.

“Wateja wanatakiwa kuweka pesa kwa Wakala au kupokea pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa kutoka benki, mitandao mingine au vyanzo vingine mbalimbali na moja kwa moja watakuwa kwenye nafasi ya kushinda. Hakuna gharama yoyote ya kuweka au kupokea pesa kwa Tigo Pesa,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa - Tigo Pesa, James Sumari, wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.

Kwenye kampeni hii hakuna masharti ya kushiriki kwa mteja wa Tigo Pesa isipokuwa; kadiri unavyoweka pesa nyingi ndivyo unajiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda.

“Tunategemea kupata washindi wapatao 331 ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na wiki moja wa kampeni yetu na lengo kubwa ni kuonesha na kurudisha shukrani kwa wateja wetu kwa kuwa pamoja na Tigo Pesa kwa kipindi cha mwaka mzima,” alisema Sumari.

Huduma ya Tigo Pesa imeendelea kuwa mstari wa mbele katika ubunifu, na kuongeza huduma na bidhaa bora zaidi ikiwamo kutoa mikopo, huduma za bima na huduma kwa makampuni na taasisi zinazowezesha kulipa na kukusanya pesa kwa ufanisi jambo linaloifanya Tigo Pesa kuwa huduma kamili ya kifedha ikiwa na mawakala zaidi ya 150,000 nchi nzima.

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA TDB

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse wakifurahia jambo mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dodoma 
Picha ya pamoja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema leo, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse ,Ikulu jijini Dodoma.

Bw. Tadesse akiwa ameambatana na ujumbe wake amewasili uwanja wa ndege wa jijini Dodoma leo, Novemba 25, 2019 na kulakiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango, na Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge. 

Akizungumza muda mfupi baada kumaliza mazungumzo na Mheshimiwa Rais Magufuli, Bw. Tadesse amesema TDB itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Tanzania na kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali maendeleo nchini.

Mhe. Dkt. Mpango amesema TDB imekuwa moja ya Benki kinara ambayo imekuwa ikitoa mikopo ya masharti nafuu kwa Tanzania hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye miradi ya maendeleo.

Aidha, Bw. Tadesse akiwa nchini atatembelea maeneo mbalimbali sambamba na kujionea miradi ya maendeleo inayotelezwa na Serikali ikiwemo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji, mradi wa kuzalisha umeme wa Kilwa na miradi mingine ambayo mkopo kutoka (TDB) utaelekezwa. 

Bw. Tadesse amesifu jitihada zinazofanywa na Serikali katika kufanya mageuzi ya kiuchumi nchini na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (katikati), Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge (mweji vazi la Jeshi) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (Watatu kushoto) wakijongea usawa wa ndege kumlaki Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse alipowasili jijini Dodoma Novemba 25, 2019. 
Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse wakati anawasili jijini Dodoma. 
Viongozi na Watendaji wa Serikali wakiwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse mara baada ya kumlaki katika uwanja wa ndege jijini Dodoma. 
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango.





JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA YAKAMATA MICHE YA BANGI, GONGO

$
0
0
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa 11 kwa tuhuma za kupatikana na Pombe Moshi na Bhangi katika misako na doria zilizofanyika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa wa Mbeya kama ifuatavyo:-

KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 13:30 mchana huko Mtaa wa Majengo mapya tazara, Kata ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, Askari Polisi walimkamata PASCHAL ULEDI [31] kondakta wa daladala na mkazi wa Iwambi akiwa amepanda miche nane [8] ya bhangi nyumbani anapoishi. Mtuhumiwa ni mtumiaji wa bhangi.

KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] 
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 13:30 mchana huko maeneo ya Mtaa wa Kagera, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata ROIDA IJANDE [60] mkazi wa Mama John akiwa na pombe haramu ya moshi lita ishirini [20]. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] NA BHANGI.
Mnamo tarehe 24.11.2019 saa 14:40 mchana huko Mtaa wa Mwatengule kwenye kilabu cha pombe za kienyeji kilichopo Kata ya Isyesye, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata JANEPHA COSMAS [28] mkazi wa Isyesye akiwa na pombe haramu ya moshi kiasi cha lita moja na nusu ikiwa kwenye chupa ndogo ndogo 15 pamoja na bhangi uzito wa gram 280. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe haramu @ gongo na bhangi.

KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI [GONGO]. 
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 15:00 alasiri huko maeneo ya Airport ya zamani, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata ENNY [65], mkazi wa Airport akiwa na pombe haramu ya moshi lita 5 kwenye kidumu cha lita tano. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]. 
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 15:05alasiri hadi saa 17:00 jioni umefanyika msako maeneo mbalimbali ya Kata za Iyela, Ruanda, Sinde, Maanga na Ilemi na katka msako huo wamekamatwa watuhumiwa wawili [02] kwa makosa ya kupatikana na gongo/bhangi ambao ni AMINA KABALE [42] mkazi wa Mtaa wa Ilembo akiwa na lita 02 za gongo na HASSAN NASSORO [25] mkazi wa Tunduma akiwa na bhangi gramu 10. 

KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 14:30 mchana huko Uyole kwenye klabu cha pombe za kienyeji kiitwacho America, Kata ya Nsalaga, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata MSAFIRI JACKSON [30] mkazi wa Nsalaga akiwa na bhangi gramu 10 kwenye mfuko wa suruali. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi.

KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 14:30 mchana huko Uyole kwenye klabu cha pombe za kienyeji kiitwacho America kilichopo Kata ya Nsalaga, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, Askari Polisi walimkamata AUGUSTINO MAHINYA [24] mkazi wa Nsalaga akiwa na bhangi gramu 10 kwenye mfuko wa suruali. Mtuhumiwa ni mtumiaji wa bhangi.

KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] 
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 13:30 mchana huko Uyole kwenye klabu cha pombe za kienyeji kiitwacho shimoni kilichopo Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata NAOMI SAID [43] mkazi wa Uyole ya kati akiwa na lita kumi [10] za gongo. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] 
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 13:40 mchana huko Uyole kwenye klabu cha pombe za kienyeji kiitwacho shimoni, kilichopo Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata LAZACK MWAKABUNGU [61] mkazi wa Uyole ya kati akiwa na lita kumi na tano [15] za gongo. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.

KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe 24.11.2019 majira ya saa 16:00 jioni huko mtaa wa Mwasote, Kata ya Itezi, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Askari Polisi walimkamata RAHIM MABLUKI, [18] mkazi wa Nsalaga akiwa na bhangi uzito wa gram 25 kwenye mfuko wa suruali yake. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumaji wa bhangi.

Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi wa mashauri yao kukamilika.
Imetolewa na:
[ULRICH OMATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA MWAKILISHI MKAAZI WA UNDP NCHINI TANZANI IKULU JIJINI ZANZIBAR LEO.

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapiunduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na mgeni wake Mwakilishi Mkaazi wa (UNDP) Nchini Tanzania.Bi.Christine Musisi, wakitabasamu wakati wakitoka katika ukumbi wa mkutano baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika leo 25-11-2019, katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mwakilishi Mkaazi wa (UNDP) Nchini Tanzania Bi. Christine Musisi (kulia kwa Rais) akiwa na Ujumbe wake walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais leo,25-11-2019.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikabidhiwa Ripoti ya Hiyari ya Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu,(SDG’s) na Mwakilishi Mkaazi wa (UNDP) Nchini Tanzania.Bi.Christine Musisi, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais leo 25-11-2019.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi Mkaazi wa (UNDP) Nchini Tanzania.Bi.Christine Musisi, alipowasili katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika leo, 25-11-2019.(Picha na Ikulu).

DKT.BASHIRU KUFANYA ZIARA YA SIKU 10 ZANZIBAR.

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Bashiru Ally anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku kumi (10) katika Mikoa Sita kichama visiwani Zanzibar kuanzia Novemba 26 hadi Disemba 4 mwaka 2019.

Dkt.Bashiru anafanya ziara hiyo kwa mara ya pili tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo. 

Akitoa taarifa ya ziara hiyo ya Katibu Mkuu huyo, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Catherine Peter Nao, alisema CCM Zanzibar tayari kimekamilisha maandalizi yote ya mapokezi ya kiongozi huyo.

Catherine alisema katika ziara yake hiyo pamoja na mambo mengine anatarajia kuzungumza na viongozi mbalimbali wa CCM na jumuiya zake na kuzindua miradi mbali mbali ya kijamii na Chama kwa ujumla.

Alisema ziara hiyo ya Dkt.Bashiru itakuwa ni ya kikazi hivyo atatembelea maeneo mbali mbali nchini na kutoa maelekezo mbali mbali ya kuimarisha Chama Cha Mapinduzi. 

“Natoa wito kwa Viongozi,Watendaji na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kujiandaa vizuri katika maeneo yao ambayo Katibu Mkuu wetu Dkt.Bashiru atatembelea”, alisema Catherine.

Katibu huyo wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar,Catherine alisema Novemba 25 Dkt.Bashiru atapokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar (AAKIA),Novemba 26 hadi Disemba 1 mwaka huu atatembelea na kufanya ziara katika Mikoa Minne ya CCM kwa upande wa Unguja.

Katika maelezo yake Catherine, alisema Katibu Mkuu huyo baada ya kukamilisha ziara yake Unguja, Disemba 2 hadi Disemba 4 ataendelea na ziara yake katika Mikoa Miwili ya Pemba na kuhitimisha ziara hiyo.

NMB Yashauriwa kutumia fursa za Kibiashara Sekta ya Madini

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akisisitiza jambo wakati wa kikao baina yake na Ujumbe kutoka Benki ya NMB pamoja na Wataalamkutoka Wizara ya Madini.
Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Serikali ya Benki ya NMB, Vicky Bishubo,
akieleza jambo wakati wa kikao baina ya Benki hiyo na Katibu Mkuu wa Wizaraya Madini. Wengine wanaofuatilia ni Watalaam kutoka Benki hiyo.
Wataalam kutoka Benki ya NMB wakifurahia jambo wakati wa kikao baina yaona Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msajil (hayupo pichani)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila katika picha ya pamojana Ujumbe kutoka Benki ya NMB pamoja na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Madini,Athony tarimo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini prof. Simon Msanjila akiongoza kikao baina yaUjumbe wa Benki ya NMB na Wizara ya Madini.
Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Madini Anthony Tarimo akifuatilia sambamba naMtaalam kutoka benki ya NMB Josephine Kulwa wakari wa kikao baina katibuMkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila na Ujumbe kutoka Benki ya NMB.

***************************************

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Benki ya NMB imeshauriwa kutumia fursa za Kibiashara zilizopo
katika Sekta ya Madini zikiwalenga Wachimbaji Wadogo na wa
Kati wanaofanya shughuli hizo katika sekta husika ikiwemo
kujifunza namna biashara ya Madini inavyofanyika.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof.
Simon Msanjila wakati wa kikao baina yake na Ujumbe wa
Wataalam kutoka Benki hiyo ulioongozwa na Mkuu wa Idara ya
Mahusiano ya Serikali ya Benki hiyo, Vicky Bishubo. Kikao hicho
kimefanyika Novemba 25, 2019, jijini Dodoma.

Aidha, kauli ya Katibu Mkuu kwa benki hiyo inafuatia juhudi za
Serikali kupitia Wizara ya Madini zinazolenga katika kuwapatia
elimu Wachimbaji ikiwemo za kutunza kumbukumbu za uzalishaji,
kufanya tafiti ili kujua kiasi cha mashapo kupitia Taasisi ya Jiolojia
na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), na Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO), hayo yote yakilenga katika kuwawezesha wachimbaji
hao kukopesheka na Taasisi za Fedha.

Pia, Prof. Msanjila ameitaka benki hiyo kutumia fursa zilizopo
katika masoko ya Madini yaliyoanzishwa katika mikoa mbalimbali
nchini ili kurahisisha biashara ya Madini na kutolea mfano wa
Soko la Madini Arusha kwamba benki hiyo haina huduma katika
soko hilo huku biashara ya Madini sokoni hapo ikifanyika kwa kiasi
kikubwa.

Aidha, Prof. Msanjila ameitoa wasiwasi benki hiyo kuwa, hivi sasa
biashara za Madini zinafanyika katika mfumo ulio wazi tofauti na
ilivyokuwa awali na kuongeza kwamba, “kuna biashara nyingi
kwenye sekta ya madini. Niwaambie hivi karibuni Serikali ya Qatar
itaanza kununua dhahabu moja kwa moja kutoka Geita.”

Katika hatua nyingine, kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 35(j) ya
Ilani ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2015-2020
kuhusu Kusimamia na kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za
uongezaji thamani madini ili kukuza mchango wa sekta hiyo katika
Pato la Taifa, Prof. Msanjila ameishauri benki hiyo kuangalia
namna ya kufanya biashara katika tasnia ya ukataji wa madini,
akieleza kwamba, ni miongoni mwa masuala yanayopewa kipaumbele na serikali ya kuhakikisha madini yanaongezwa
thamani kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.

“Sekta ya madini haijatumiwa vizuri na mabenki ninawakaribisha
kwenye sekta hii . Pale Arusha ndo mji pekee wa Ukataji Madini ya
Vito. Mwende mkaliangalie hili,” amesisitiza Prof. Msanjila.

Naye, Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Serikali ya Benki hiyo,
Vicky Bishubo amemshukuru Prof. Msanjila kwa kueleza fursa
zilizopo katika sekta husika na kueleza kwamba, benki hiyo
imeyachukua kwa uzito mkubwa yote yaliyoelezwa na iko tayari
kuyafanyia kazi.

“Tumejifunza namna sekta ya Madini inavyofanya kazi kuna
uwezekano wa sisi kuandaa mfumo wa kuwasaidia wachimbaji
wadogo,” ameeleza Bishubo.

ALIYEKUWA MEYA WA JIJI LA ARUSHA AKABIDHI OFISI

$
0
0
Meya Wa jiji la Arusha kwa tiketi ya chadema ambaye kwa sasa amejiuzuru na kuhamia chama cha mapinduzi (CCM),Kalisti Lazaro akimkabidhi Mkurugenzi Wa jiji la Arusha Dk. Maulidi Madeni baadhi ya tuzo alizozipata kipindi alipokuwa meya Wa jiji hilo ikiwemo Tuzo ya umeya bora Jana Oktoba 25 ndani ya ukumbi Wa halmashauri ya jiji la Arusha wakati akikabishi ofisi na kuwaaga wafanyakazi Wa halmashauri hiyo.

Na Woinde Shizza Globu ya jamii Arusha
ALIYEKUWA meya Wa jiji la Arusha kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA),Kalisti  Lazaro ambaye kwa sasa amejiuzuru nafasi yake  amewataka watumishi Wa jiji la Arusha waendelee kupiga Kazi bila kutetereka  wala kuyumbishwa na mtu yeyote ili kuiletea nchi yetu maendeleo

Ameyasema hayo Leo  wakati alipokua akikabithi ofisi pamoja na kuwaaga  wafanyakazi wa halmashauri wa jiji la Arusha pamoja na wakuu wa idara ambapo alubainisha kuwa ameiacha halmashauri hiyo ikiwa ya viwango vya juu, kwani inaongoza katika mambo mbalimbali ikiwemo uwepo Wa hati safi, shule, Barabara pamoja na kuongoza kitaifa katika matokeo ya darasa la saba.

Amebainisha kuwa alipokea halmashauri ikiwa na hati chafu ilikuwa na vurugu lakini alipoingia aliibadilisha na hadi anaondoka anaiacha halmashauri ikiwa na hati safi, ikiwa na amani na utulivu hivyo waendelee kudumisha na kuyaasisi yote aliyoyaanzisha

Amesema mara zote alipokuwa kiongozi alijitaidi kulinda maslahi ya watumishi, nchini, kwa ujumla  huku akitumia muda huo kuomba radhi kwa mtumishi yeyote ambaye walitofautiana kipindi  cha uongozi wake.

"Ninaiacha halmashauri ya jiji la Arusha  ikiwa ya viwango vya juu, kwanza tukiwa namba moja kitaifa kushika nafasi ya kwanza, naacha halmashauri ya jiji la Arusha katika ukaguzi wa miradi ya mwenge ikiwa bora tukiwa tumeongeza, naiacha halmashauri ya jiji la Arusha tukiwa na madara, vituo vya afya cha mwisho naiacha jiji la Arusha ikiwa na hospital ya jiji ambayo tunaijenga kwa mapato yetu" alisema Kalisti

Amefafanua kuwa ataendelea kuwa mwanasiasa hadi mwisho wa maisha yake na iwapo itatokea ataacha basis ataenda kufungua kanisa, huku akibainisha kuwa ameamua kuhamia chama cha mapinduzi bila kupewa mashariti yeyote aliopewa na kuhaidi ataitumikia chama cha mapinduzi kama mwanachama mwadilifu.

Alimpongeza mkurugenzi Wa jiji la Arusha kwa uashirikiano aliompa kwani ushirikiano huo ndio uliifikisha halmashauri hiyo ilipofika,alifafanua dkt Madeni amekuwa akishirikiana na watu kwa umoja na upendo na pale panapotokea tofauti amekuwa akiwaunganisha na hiki ndicho kitu kilichosababisha akaamua pia kuingia chama cha mapinduzi. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Maulid Madeni amesema kuwa  katika kipindi chake cha uongozi hajawai kupata au kufanya Kazi na meya mzuri na mwenyeushirikiano Na serikali  kama huyu huku akimsihi aendelee na moyo huo huo

Amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakiwasifia watu wakiwa wamekuwa ila yeye anamsifia akiwa hai huku akibainisha kuwa meya amekuwa  ni mtu mchapakazi  na kiongozi asiependa makuu  wala majungu huku akiwataka watumishi wengine Wa vyama vya Siasa kuiga mfano wake.

CLARIFICATION ON OFFICIAL EAC 20TH ANNIVERSARY LOGO

$
0
0
 The East African Community Secretariat wishes to clarify that there is only one official logo for the Community's 20th Anniversary celebrations which are currently underway.
f which are hereto attached, was developed by the Secretariat through a competitive bidding process and unveiled by the EAC Secretary General, Amb. Liberat Mfumukeko, during a media briefing at the EAC Headquarters on Wednesday, 20th November, 2019.
The Official Logo will act as a unifier/identifier for all sensitisation and other activities to be held at the national and regional level to commemorate the Community's 20th Anniversary.
The Secretariat further wishes to state that there is a separate logo for an online Citizens' Engagement Campaign with the youth in the region as the main target. This campaign will mainly be on the Social Media Channels such as Facebook, Twitter and Instagram.
The logo for the online campaign is meant to complement rather than contradict the Official 20th Anniversary Logo.

ALIEKUWA MEYA WA JIJI LA ARUSHA AKABIDHI OFISI RASMI LEO

$
0
0

Na Woinde Shizza Globu ya jamii Arusha

Aliyekuwa meya Wa jiji la Arusha kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Kalisti Lazaro ambaye kwa sasa amejiuzuru nafasi yake amewataka watumishi Wa jiji la Arusha waendelee kupiga Kazi bila kutetereka wala kuyumbishwa na MTU yeyote ili kuiletea nchi yetu maendeleo

Lazaro ameyasema hayo leo wakati alipokua akikabithi ofisi pamoja na kuwaaga wafanyakazi wa halmashauri ya jiji la Arusha pamoja na wakuu wa idara ambapo alubainisha kuwa ameiacha halmashauri hiyo ikiwa ya viwango vya juu ,kwani inaongoza katika mambo mbalimbali ikiwemo uwepo Wa hati safi,shule ,Barabara pamoja na kuongoza kitaifa katika matokeo ya darasa la saba.

Alibainisha kuwa alipokea halmashauri ikiwa na hati chafu ilikuwa na vurugu lakini alipoingia aliibadilisha na hadi anaondoka anaiacha halmashauri ikiwa na hati safi,ikiwa na amani na utulivu hivyo waendelee kudumisha na kuyaasisi yote aliyoyaanzisha

Alisema Mara zote alipokuwa kiongozi alijitaidi kulinda maslahi ya watumishi ,jiji,nchi ,,kwa ujumla huku akitumia muda huo kuomba radhi kwa mtumishi yeyote ambaye walitofautiana kipindi cha uongozi wake.

"Ninaiacha halmashauri ya jiji la Arusha ikiwa ya viwango vya juu ,kwanza tukiwa namba moja kitaifa kushika nafasi ya kwanza,naacha halmashauri ya jiji la Arusha katika ukaguzi Wa miradi ya mwenge ikiwa bora tukiwa tumeongeza,naiacha halmashauri ya jiji la Arusha tukiwa na madara ,vituo vya afya cha mwisho naiacha jiji la Arusha ikiwa na hospital ya jiji ambayo tunaijenga kwa mapato yetu" alisema Kalisti

Alifafanua kuwa ataendelea kuwa Mwanasiasa hadi mwisho Wa maisha yake na iwapo itatokea ataacha basis ataenda kufungua kanisa,huku akibainisha kuwa ameamua kuhamia chama cha mapinduzi bila kupewa mashariti yeyote aliopewa na kuhaidi ataitumikia chama cha mapinduzi kama mwanachama mwadilifu.

Alimpongeza Mkurugenzi Wa jiji la Arusha kwa uashirikiano aliompa kwani ushirikiano huo ndio uliifikisha halmashauri hiyo ilipofika,alifafanua dkt Madeni amekuwa akishirikiana na watu kwa umoja na upendo na pale panapotokea tofauti amekuwa akiwaunganisha na hiki ndicho kitu kilichosababisha akaamua pia kuingia chama cha mapinduzi. 

Kwa upande wake mkurugenzi Wa jiji la Arusha Maulid Madeni alisema kuwa katika kipindi chake cha uongozi hajawai kupata au kufanya Kazi na meya mzuri na mwenyeushirikiano Na serikali kama huyu huku akimsihi aendelee na moyo huo huo

Alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakiwasifia watu wakiwa wamekuwa ila yeye anamsifia akiwa hai huku akibainisha kuwa meya amekuwa ni MTU mchapakazi na kiongozi asiependa makuu wala majungu huku akiwataka watumishi wengine Wa vyama vya Siasa kuiga mfano wake.
 
 Aliyekuwa  Meya wa jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA ambaye kwa sasa amejiuzuru na kuhamia chama cha mapinduzi CCM,Kalisti Lazaro akimkabidhi mkurugenzi wa jiji la Arusha Dr Maulidi Madeni baadhi ya tuzo alizozipata kipindi alipokuwa meya Wa jiji hilo ikiwemo Tuzo ya umeya bora Jana October 25 ndani ya ukumbi Wa halmashauri ya jiji la Arusha wakati akikabishi ofisi na kuwaaga wafanyakazi Wa halmashauri hiyo.picha na Woinde Shizza,Arusha). 

RAIS DKT MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UWANJA WA MAADHIMISHO YA TAIFA, MAKAO MAKUU YA ULINZI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo na maafisa waandamizi wengine akifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa  jiwe la Msingi  la ujenzi wa Uwanja wa Maadhimisho ya Taifa eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Jumatatu Novemba 25, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akishuhudiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Luteni Jenerali Yakub Mohamed baada ya
kuweka  jiwe la Msingi  la ujenzi wa Uwanja wa Maadhimisho ya Taifa eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Jumatatu Novemba 25, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo na maafisa waandamizi wengine akikata utepe kuashiria mwanzo wa ujenzi wa Uwanja
wa Maadhimisho ya Taifa eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Jumatatu Novemba 25, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo na maafisa waandamizi wengine akiongea machache baada ya kuweka   jiwe la Msingi
la ujenzi wa Uwanja wa Maadhimisho ya Taifa eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Jumatatu Novemba 25, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi wa Kijiji cha Chimilolo alipotoka katika hafla ya uwekaji wa  jiwe la Msingi  la ujenzi wa Uwanja wa Maadhimisho ya Taifa eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Jumatatu Novemba 25, 2019


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wakimsikiliza  Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akitoa ufafanuzi kuhusu ujenzi wa Uwanja wa Maadhimisho ya Taifa eneo la
Chamwino jijini Dodoma leo Jumatatu Novemba 25, 2019
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo wakisikiliza maelezo toka kwa Mhandisi Kanali Zabron Mahenge akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa Uwanja wa Maadhimisho ya Taifa eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Jumatatu Novemba 25, 2019.


RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA BENKI YA BIASHARA NA MAENDELEO MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA DODOMA LEO

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika   baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Novemba 25, 2019. Kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango. PICHA NA IKULU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono kwa furaha na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Nchi za Mashariki na Kusini mwa Africa wakati wa mazungumzo yao Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Novemba 25, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya kinyago   Mkuu wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika  alipokutana naye kwa mazungumzo Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Novemba 25, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na   Mkuu wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika na ujumbe wake alipokutana naye Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Novemba 25, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika  baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Novemba 25, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na pamoja na Mkuu wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika na ujumbe wake na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Doto James na maafisa waandamizi wa wizara  alipokutana naye Ikulu Chamwino
jijini Dodoma leo Novemba 25, 2019

Rais Magufuli atoa shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa

$
0
0



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akishuhudiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Luteni Jenerali Yakub Mohamed baada ya
kuweka  jiwe la Msingi  la ujenzi wa Uwanja wa Maadhimisho ya Taifa eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Jumatatu Novemba 25, 2019


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa shilingi Bilioni 10 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa katika eneo la Kikombo Jijini Dodoma.


Mhe. Rais Magufuli ametoa fedha hizo leo tarehe 25 Novemba, 2019 baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo na ameagiza milima yote inayozunguka eneo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa lenye ukubwa wa ekari 5,567 imilikiwe na JWTZ kwa ajili ya shughuli za ulinzi.


Kuhusu madai ya fidia, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi kuwalipa fidia ya shilingi Bilioni 3 na Milioni 339 wananchi 1,500 wa Kata ya Kikombo ambao ardhi yao imechukuliwa na JWTZ kwa ajili ya Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, kuanzia tarehe 01 Desemba, 2019.


Pamoja na agizo hilo, Mhe. Rais Magufuli amewatahadharisha wananchi wa Kikombo kujiepusha na matapeli wanaowahamasisha kudai fidia wasiyostahili kwa mujibu wa sheria ama kudai ardhi isiyo yao.


Mhe. Rais Magufuli pia ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kujenga kwa kiwango cha lami kilometa 18 za barabara inayounganisha Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa na barabara kuu ya Dodoma – Morogoro.


Aidha, Mhe. Rais Magufuli amekubali ombi la Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Salvatory Mabeyo aliyeomba Serikali ibebeba jukumu la kulipa deni la takribani shilingi Trilioni 1 ambalo JWTZ inadaiwa baada ya kujengewa nyumba 6,064 za makazi ya Askari katika maeneo mbalimbali nchini, badala ya Askari kukatwa posho zao ili kupata fedha za kulipia deni hilo kama ilivyowekwa katika mkataba wa ujenzi.


“Nakuhakikishia hakuna kukatwa Askari yeyote, hilo deni litabebwa na Serikali, kabla sijaja hapa nimeshamwelekeza Waziri wa Fedha na Katibu Mkuu, na nafikiri kesho au keshokutwa wataanza kulipia hilo deni ambalo limeanza kuiva, tutaanza kulipa Dola za Marekani zaidi ya Milioni 25 (sawa na shilingi Bilioni 56 na Milioni 948). Mkataba ni kweli ulikosewa, nafikiri ilikuwa ni mwaka 2012/13 lakini siwezi kukubali makosa ya namna hiyo yakafanyika katika kipindi changu”amesema Mhe. Rais Magufuli.


Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Maafisa na Askari wa JWTZ kwa kazi nzuri ya kulinda mipaka ya nchi na kushiriki katika operesheni za kulinda amani katika Mataifa mbalimbali, majukumu ambayo yamelijengea heshima jeshi hilo na Tanzania.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Salvatory Mabeyo wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa maelekezo yake ya kujengwa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa katika eneo la Kikombo ambayo yanajengwa na jeshi lenyewe.


Mapema kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo, Mhe. Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa maadhimisho ya kitaifa katika eneo la Chamwino.

Ujenzi wa uwanja huo utakamilika Januari 2020 ukiwa na uwezo wa kuchukua watu 5,000 kwa gharama ya shilingi Bilioni 2, na awamu ya pili itahusisha ujenzi wa ukumbi wa mikutano, jengo la watu mashuhuri na jengo la kupumzikia watu.

 

 
Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chamwino

25 Novemba, 2019

TEKNOLOJIA YATAJWA KUWA SILAHA TOSHA YA USHINDANI KATIKA SOKO LA DUNIA

$
0
0
Balozi wa Korea Kusini nchini Tae Ick Cho akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliowakutanisha wadau na Wizara zinazoshughulikia masuala ya ardhi kutoka Korea na Tanzania ambapo Balozi Tae amesema kuwa ili kufanikiwa lazima teknolojia iwe silaha madhubuti, leo jijini Dar es Salaam.
1.viongozi mbalimbali wa kampuni kutoka Korea wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo ulilenga kupeana taarifa na uzoefu kuhusiana na teknolojia ya masuala ya ardhi, jijini Dar es Salaam.
Washiriki mbalimbali wakiwemo wanafunzi wakifuatilia mjadalo huo.


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

TEKNOLOJIA bora katika kukuza uchumi imeelezwa kuwa ndio silaha pekee ya kimaendeleo na yenye kuleta ushindani katika soko la dunia na hilo litafanikiwa kama taifa litajikita zaidi katika kuwekeza zaidi katika teknolojia ya sasa ambayo imeteka soko la dunia.

Akizungumza katika ufunguzi wa wa mkutano wa siku mbili wa wadau wa sekta ya Ardhi "Geospatial Information Road Show" uliowakutanisha wataalamu wa masuala ya ardhi kutoka nchini Korea na Tanzania; Balozi wa Korea nchini Tae Ick Cho amesema nchi hizo mbili zimekuwa na ushirikiano wa hali ya juu hasa katika masuala ya biashara zilizoruhusu kuvuka mipaka na hiyo yote ni kwa malengo ya kukuza uchumi baina ya nchi hizo mbili.

Balozi Tae Ick Cho amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa jukwaa la "Geospatial Information Road Show" malengo makuu ni pamoja na kuendesha semina za kiteknolojia katika usajili ardhi, mikutano ya biashara baina ya Serikali ya Tanzania Makampuni wakilishi ya Korea yaliyopo nchini pamoja na kupeana taarifa mbalimbali katika masuala ya ardhi.

Amesema kuwa ili kuendelea zaidi lazima teknolojia iwe silaha ya kwenda sambamba na maendeleo na bila teknolojia uwezo wa kushindana na mataifa mengine hautakuwepo.

"Matumizi ya teknolojia hasa ICT yana tija sana katika kuyafikia maendeleo na bila hiyo hatutaweza kushindana na mataifa mengine yenye teknolojia ya juu, tukumbuke msemo wa ukiona vyaelea ujue vimeundwa , hivyo hatuwezi kuendelea bila ya kuweka mbele teknolojia, kushirikiana na kuondoa vikwazo" amesema.

Vilevile amesema kuwa kama ilivyo Korea Kusini lazima watu wajue maeneo yao, ardhi yao na kuitumia katika shughuli za kimaendeleo na kueleza kuwa haba na haba hujaza kibaba hivyo ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili lazima udumishwe zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa upimaji na ramani kutoka Wizara ya Ardhi Hamdounny Masour amesema kupashana habari na kubadilishana uzoefu baina ya kampuni kutoka Korea na Tanzania ni moja katika ya hatua kubwa ambayo itasaidia nchi hizo mbili kufikia malengo.

Masour amesema kuwa kupitia mkutano huo wataendelea kudumisha ushirikiano huo pamoja na kupeana taarifa za kisekta katika masuala ya upimaji wa ardhi.

"Ushirikiano baina ya nchi hizo mbili umekuwa wa kindugu na kupitia Geospatial Information Road Show na Wizara ya Ardhi tutaendelea kupeana taarifa za kisekta ili kuweza kuyafikia maendeleo" ameeleza.

Mkutano huo uliodumu yangu 2013 umewakutanisha wadau kutoka Wizara ya Ardhi nchini pamoja na Wizara ya Ardhi, miundombinu na usafiri kutoka Korea pamoja na wataalamu mbalimbali yakiwemo makampuni makubwa 12 kutoka nchini Korea.

Viewing all 109977 articles
Browse latest View live




Latest Images