Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

msaada tutani tafazali: nahamia Lowell, marekani, je mambo niaje huko??

$
0
0

Habari zenu wadau wa blog ya jamii na Ankal kwa ujumla.
Mie ni mdau mkubwa wa blog hii, ni maswali mawili matatu naomba mnisaidie.
Nataka niende/nihamie USA ( kuhusu mambo ya makaratasi msijali yapo fresh), mji ninaotarajia kwenda ni Lowell, MA ila mwenyeji wangu sio mtz ndo nikaona niulize humu.
1:line gani nzuri ya simu kupiga Tz ukiwa USA?najua kuna sky pe, viber and co ila sio familia yangu yote ina huduma hiyo.
2: Je, nikikata insuarance USA itanicover incase nikipata na janga kama binadamu mfano kifo, itanirudisha kwetu nizikwe in time au ni bora kabla sijaenda nipite ofice za NSSF weledi( kama sijakosea) nikakate insurance ya hapo?.
Nimejaribu muuliza brother google kuhusu miji ambayo haina high criminal record, ila majibu yake yananichanganya.
Acha niwe mkweli natarajia kufanya kazi kama assistance nurse, kuja kuwa nurse. Je mji gani mnanishahuri ni mzuri ukiondoa Houston( huu story zake umenichosha tayari).
Najua mengine nitajifunza baada ya kufika huko ila si vibaya wadau mkianza kunipa hints kabla sijakwea pipa.
Asante na Mungu hawabariki na asante ankal kwa kijiwe hiki.


kanyaboya!

$
0
0
Dear All,
In case you receive an email from me saying something similar to "have uploaded the required documents on Google docs view - address www.asalamhomestayPLEASE DELETE IT WITHOUT OPENING IT...

Please do not follow the instructions saying "I have uploaded the required documents on Google docs View Here and sign on with your email respectively to preview the documents and do not hesitate to get back to me for further discussion"....

Thanks!
Sarah Chiduo

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA TFF Januari 14, 2014

KCC YA UGANDA YATWAA KOMBE LA MAPINDUZI KWA KUILAMBA SIMBA SC BAO 1-0

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akimkabidhi Kombe la Mapinduzi Nahodha wa Timu ya Kcc kutoka Kenya Kawoya Fahad,katika mchezo wa Fainali na Timu ya Simba,uliochezwa lao katika uwanja wa Amaan Mjni Zanzibar ikiwa sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi,katika mchezo huo Kcc ilifunga Simba kwa bao 1-0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akimkabidhi Kombe la Mapinduzi Nahodha wa Timu ya Kcc kutoka Kenya Kawoya Fahad,katika mchezo wa Fainali na Timu ya Simba,uliochezwa lao katika uwanja wa Amaan Mjni Zanzibar ikiwa sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi,katika mchezo huo Kcc ilifunga Simba kwa bao 1-0

INTRODUCING Niweje: Nas Tatu ft Izzo Bizzness & Dev D

Taarifa isiyo sahihi kuhusu Tsunami

$
0
0
Dear wadau, 
Kuna taarifa inayosambazwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS) kuhusiana na TMA kutoa tahadhari ya Tsunami. Taarifa hizo sio za kweli, uionapo ujumbe huu upuuzie kwa kuwa sio taarifa sahii, ni taarifa ya upotishaji.
Taarifa rasmi ni kama ilivyotumwa awali kuhusiana na upepo mkali kwa Ukanda wa Bahari ya Hindi na Mvua kubwa kama inavyoonesha hapa:
Ujumbe huo unasomeka kama hivi:
TAHADHARI ya Tsunami: Kuanzia saa moja usiku
Tsunami itafika Tanzania na mawimbi yatakuwa makubwa
kuanzia muda huo. Taarifa zaidi itatolewa na Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania wakati wowote kuanzia sasa, kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agness Kijazi.
Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa ili kutoa taarifa sahihi ni vizuri kuwasiliana na Ofisi zetu kwa maelezo ya kina zaidi kuepusha mkangamanyo kwa wananchi.
Asante tena kwa ushirikiano wako,
Nakutakia Sikukuu njema ya Maulid,

Monica Mutoni
Ofisi ya Uhusiano
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

KAMATI KUU YAMTEUA MAHMOUD THABITI KOMBO KUWA MGOMBEA WA NAFASI YA UWAKILISHI JIMBO LA KIEMBE SAMAKI

$
0
0
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM,  imefanya kikao cha siku, Januari 13, 2014 mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Kikwete na kujadili mambo kadhaa ikiwemo kumteua Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa kiti cha Uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki.

Taarifa iliyotolewa leo mjini Zanzibar na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, mgombea huyu wa CCM kesho, Jumanne, Januari 14, 2013, atachukua fomu za tume za kugombea.

Nape amesema uzinduzi wa kampeni za CCM utafanyika tarehe 22/01/2014 kwenye viwanja vya Kiembesamaki ambapo mgeni rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Gharib Bilal.

"Kampeni za CCM zitafungwa tarehe 01/02/2014 huko Chukwani na mgeni Rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Balozi Seif Ali Idi", alisema Nape na kuongeza;

Mahmoud Thabit Kombo
"Kampeni itaendeshwa na Kamati ya Siasa ya wilaya ya Dimani viongozi na wanachama wa wilaya husika, na ngazi zingine za Chama zitashirikiana na ngazi ya wilaya kuhakikisha CCM inashinda tena jimbo hili na Kamati Kuu inawatakia kila lakheri kwenye kampeni na hatimaye uchaguzi huo. Kampeni na hata upigaji kura uendeshwe kwa amani na utulivu kama ulivyo utamaduni wetu".

Nape alisema, pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu pia imeipongeza sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar na kufanikisha sherehe zake kwa ufanisi kutokana na maandalizi mazuri.

Kamati Kuu imetambua na kupongeza hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa tangu mapinduzi mwaka 1964 mpaka leo. Wito umetolewa kuyalinda na kuyaendeleza mema yote yatokanayo na mapinduzi hayo na mafanikio yaliyoletwa na serikali inayoongozwa na CCM.

HUYU NDIO KOCHA MPYA WA TIMU YA YANGA

$
0
0
Kocha Mpya wa timu ya Yanga, Hans Plujim akiwa kwenye uwanja wa Ndege wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam kabla ya kukwea pia kuwafuata wana Jangwani huko nchini Uturuki wanakoendelea na mazoezi yao ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara. Kocha huyo aliondoka jana alasiri kwenda nchini Uturuki kujiunga na Kocha Msaidizi wa timu hiyo,Charles Boniface Mkwasa na kikosi kizima cha Yanga.Kocha huyo ambaye amesaini mkataba wa miezi sita ya awali na klabu hiyo,amesema amejipanga vyema kukinoa kikosi hicho pamoja na mambo mengi mno kwa klabu hiyo,ambapo pia amesema anamjua vizuri kocha wa Simba Logarusic ambaye mwaka 2012 alimchapa kwa mabao 4-1 wakati huo Plujim akifundisha Berekum Chelsea ya Ghana na Loga akiwa Ashanti Goldb SC. 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA TFF LEO Januari 14, 2014

$
0
0
TAIFA STARS KUIKABILI NAMIBIA FIFA DATE
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco.

Stars na Brave Warriors zitacheza mechi hiyo Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Namibia. Mechi hiyo ipo katika kalenda ya mechi za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Makubaliano ya kucheza mechi hiyo yamefikiwa kutokana na mazungumzo kati ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Namibia (NFA), John Muinjo.

Benchi la Ufundi la Brave Warriors linaongozwa na kocha mzawa Ricardo Mannetti, na mechi hiyo itachezwa ama Uwanja wa Sam Nujoma au Uwanja wa Uhuru jijini Windhoek.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inafundishwa na kocha Kim Poulsen kutoka Denmark na inatarajia kuanza kucheza mechi za mchujo za AFCON Septemba mwaka huu.
  
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

WANANCHI UKONGA WAGOMEA FIDIA KIDUCHU BOMBA LA GESI

$
0
0

Mwenyekiti wa Kamati ya kufatilia malalamiko ya wananchi wa mji mpya relini Bw. Omari Msusa kushoto akihojiwa na vyombo vya habari kuhusu fidia wanayotakiwa kulipwa huku Mbunge wa Jimbo la Ukonga Dar es Salaam, Bi,Eugen Mwaiposa akimsikiliza kwa makini .

mbunge wa jimbo la Ukonga Dar es salaam, Bi,Eugen Mwaiposa (kulia) akisikiliza malalamiko ya wananchi wea eneo la Mji Mpya Relini jimboni kwake jana wakilalamika kutaka kulipwa fidia ndogo ambazo hazilingani na thamani ya nyumba zao.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mjipya Relini,Ilala Dar es Salaam Bw. Geofrey Chacha (aliyesimama) akitoa malalamiko ya wananchi mbele ya mbunge wa Jimbo la Ukonga, Bi. Eugen Mwaiposa wa pili kushoto wanaolalamikia kuhusu tahmini ya fidia ndogo inayopitishwa ili kupisha upanuzi wa bomba la gesi linalotoka Mtwara. 

Na Ripota wetu.

WANANCHI wa Mji mpya Relini wilaya ya Ilala waliopitiwa na mradi ya bomba la gesi ya Mtwara wamemuomba Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Bi. Eugen Mwaiposa awasilishe bungeni hoja ya kukataa mradi huo kutokana na kupunjwa fidia ya nyumba na mali zao wanayotakiwa kulipwa.

Wakizungumza na kutoa maazimio hayo katika mkutano wa dharura walioitisha na kuhudhuriwa na mbunge wao, wananchi hao walisema awali walikubali mradi huo kwa manufaa ya taifa lakini baada ya kuletewa dodoso la kutathmini mali na nyumba zao wamegundua kuna ujanja unatumika kuwanyima haki na kuwafanya kuwa masikini maisha yao yote.

Waliendelea kudai kuwa mpaka sasa hawajui serikali imemkabidhi nani jukumu la kuthamini nyumba zao kwani kampuni nyingi za ujanja ujanja zimejitokeza kutaka kuwathamini lakini kwa kiwango cha chini ambacho hakiwezi kumpatia makazi mengine.

Bw. Josephat Haule alisema waathirika wenzao katika Kata za Kivule, Pugu Kwalala na Mbande wao wamethaminiwa vizuri na wanatarajia kupata fedha za kujenga nyumba nyingine kutokana na gharama kuwa juu lakini wao nyumba iliyojengwa kwa sh. mil 57 anathaminiwa alipwe sh. mil. 11 na nyumba zenye thamani ya sh. mil. 10 wanataka alipwe sh, mil 3.

Bw. Robert Pius alisema kutoka taarifa ya Serikali itolewe ya  kutangaza kupitisha bomba la gesi eneo hilo waathirika wote walisimamisha uendelezaji wa makazi hayo na kusubiri kupewa haki zao lakini ni mwaka wa pili sasa hakuna taarifa zenye ukweli zinazowafikia hivyo kuwafanya waishi kama wanya aina ya digidigi porini,
Mbunge Mwaiposa akizungumza na wananchi hao aliahidi kushirikiana nao kujua ukweli wa kampuni gani iliyopewa jukumu la kuthamini nyumba na mali zao kwani anachofahamu ni kuwa Kampuni ya Kilwa Energy iliyopewa jukumu hilo awali hakiwa na uwezo wa kifedha kuwalipa wananchi kwa wakati.

Aliahidi kushirikiana na Kamati ya wananchi hao kushughulikia madai yao kwenda Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwenda kumuona Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwenda kumuona Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ikishindikana wanakwenda kumlalamikia Rais Jakaya Kikwete.

Alisema wananchi wanateseka kwa vile kuhamisha makazi kutoka sehemu moja kwenda nyingine kunarudisha maendeleo nyuma na kama anavyofahamu Serikali ya Rais Kikwete ni sikivu na yenye kufanya kazi kwa ufasaha hajui sababu za wananchi wake kushindwa kutimiziwa ahadi zao katika kiwango kinachostahili.

"Wananchi wangu wanadhiki, wanashida ya fedha lakini si kwa malipo kidogo kiasi hicho, tunapiga picha tuoneshe umma thamani ya nyumba na kiasi wanachotakiwa kulipwa ili wakaendelee na maisha yao sehemu nyingine" alisema Bi. Mwaiposa.

Bi. Mwaiposa alikiri kuona nyumba zilizothaminiwa kwa fedha kidogo ambazo haziwezi kununua kiwanja kingine ambavyo kwa sasa katika maeneo hayo vinauzwa kati ya sh. mil. 10 mpaka sh. mil. 15 kwa kiwanja cha nusu hekari.

KONGAMANO LA WASANII KUFANYIKA IJUMAA

$
0
0

 Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Twalib 'Teacher' 
(kushoto)
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa kongamano la umoja na mshikamano linalofanyika Januari 17 (Ijumaa) kwenye viwanja vya hoteli ya Lamada.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Caasim Taalib alisema madhumuni ya kongamano hilo ni kuhamasisha umoja kati ya wasanii ili kujenga uwezo na nguvu ya kumaliza matatizo yao ya kiuchumi.
Alisema wasanii, waandishi, wa habari na Vijana wanashindwa kumaliza matatizo yao ya kiuchumi bila kuombaomba au kusubiri misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali.  "Wasanii inatubidi tujifunze kujitegemea na tuache kusubiri wafadhili au serikali ituchangie hata kwa matibabu na katika mazishi yetu" alisema Taalib.
Katika kongamano hilo Shiwata itazingua mpango maalum ambao utawezesha wasanii kupata misaada ya fedha za kutengeneza filamu,kurekodi muziki,kuwezesha timu na vikundi mbalimbali kununua vifaa vya ichezona kuwapatia nauli ya usafiri ndani na nje ya nchi kwa shughuli za michezo na sanaa. 
Katika Mpango huo Shiwata pia itatoa fedha kwa mrithi wa msaniii kamaatakufa, akiugua au kulazwa kwa siku tatu katika hospitali zinazotambuliwa na Serikali.
Alisema Shiwata pia itatoia misada kwa wasanii wanaotaka kuoa au kuolewa ambako kila mwanachama atachangia sh. 1,000 kwa ajili ya kugharamikia mazishi ya msanii kununua sanduku n usafiri. 
Alisema Shiwata itakusanya zaidi ya sh. Mil.7 kutoka kwa wanachama 7,000 na wasanii watajiunga kwa sh. 20,000 ambazo zinaweza kulipwa kwa awamu tatu kutokana na uwezo wa msanii.
Sjiwata ina ekari 300 za makazi katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga ambapo hivi sasa kuna nyumba 40 zilizojengwa kwa nguvu ya wasanii wenyewe na ekari 500 za kilimo.

MKUU WA MKOA WA RUKWA AVAMIA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WIILAYA YA NKASI, AWATAKA KUBORESHA MAKUSANYO YA MAPATO YA HALMASHAURI YAO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia baraza kuu la madiwani wa Wilaya ya Nkasi (Full Council) lililokua kwenye kikao cha kujadili na kupitisha bajeti ya fedha ya mwaka 2014/2015 na kupitisha sheria ndogondogo za halmashauri. Katika hotuba yake aliwataka madiwani na viongozi wa halmashauri na wilaya ya Nkasi kushirikiana kwa pamoja na kuweka pembeni itikadi zao katika kuunda vyanzo vipya vya mapato na kuvisimamia kwa kuwekeana mikakati maalum ya makusanyo kwa kila kijiji, kata, tarafa, halmashauri na Wilaya kwa ujumla. Alisema halmshauri hiyo haitaweza kuendelea kwa kuendelea kuwa tegemezi kutoka Serikali kuu na badala yake waongeze makusanyo ya ushuru na mapato yasaididie katika mipango ya kujiendeleza. Kikao hicho kilipitisha bajeti ya Tsh Bilioni 25.4.Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akizungumza katika kikao hicho ambapo alisisitiza juu ya kuboresha na kusimamia upatikanaji wa mapato ya halmashauri ambayo pamoja na mambo mengine yatasaidia katika kuboresha miundombinu ya barabara katika Wilaya hiyo ambayo imekua ndio kilio kikubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Albinus Mugonya.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Kimulika Galikunga akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika kikao hicho. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Peter Mizinga.
Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi waliohudhuria kikao hicho.Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

Maulidi ya kuzaliwa Bwana Mtume (S.A.W.) Zanzibar

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi wengine (kutoka kushoto) Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohamed Gharib Bilali,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, na (kulia) makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi,wakiwa katika Maulidi ya kuzaliwa Bwana Mtume (S.A.W.) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Sheikh Sherali Champsi Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maulidi ya kuzaliwa Bwana Mtume (S.A.W.)  katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja  palipofanyika Maulid hayo. 
Picha na Ikulu Zanzibar. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Makatibu wa Bunge wa Jumuiya ya Madola (Afrika) wakutana Dar

$
0
0
Mweneyekiti wa Umoja wa Makatibu wa Bunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola barani Afrika na Katibu wa Bunge la Ghana Bwana Emmanuel Anyimadu (kushoto) akifungua rasmi Mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Umoja huo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola (Afrika), mwenyeji wa Mkutano huo na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah.
Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola (Afrika) wakiwa kwenye Mkutano wa kamati ya Utendaji Jijini Dar es Salaam. Washiriki katika Kamati ya Utendaji wanatoka katika nchi za Ghana, Uganda, Tanzania, Botswana, Kenya, Afrika Kusini na Zanzibar.
Picha ya pamoja ya Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola (Afrika) pamoja na maafisa waandamizi wakati wa Mkutano wa Kamati ya Utendaji Jijini Dar es Salaam. Lengo la Mkutano huu ni kuandaa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Makatibu wa Bunge wa Jumuiya ya Madola (Afrika) utakaofanyika nchini Kenya mwezi Juni, 2014. (Picha na Prosper Minja – Bunge)

hepi besdei ya kuzaliwa mtoto zainabu mhamila ikota super D leo

$
0
0
 LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA MTOTO ZAINABU MHAMILA 'IKOTA' SUPER D AMBAPO ANATIMIZA MIAKA  11 TANGIA AZALIWE PICHANI AKIWA NA BABA YAKE MZAZI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' AMBAYE NI KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI

TANZIA

$
0
0
KATIBU WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MFANYAKAZI WA OFISI YA BUNGE BI. CONSOLATA MAGERE KILICHOTOKEA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI DAR ES SALAAM USIKU WA TAREHE 10/01/2014.  MAZISHI YATAFANYIKA DODOMA TAREHE 14/01/2014. BWANA  ALITOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIDIWE. AMINA!

Ofisi ya Bunge


Dar es Salaam

DAMPO JIPYA NA LA KISASA LA KUTUPIA TAKATAKA LINALO JENGWA JIJINI MBEYA.

$
0
0
Huu ndio mwonekano wa Dampo hilo la kisasa kwa upande wa juu ambapo ujenzi upo katika hatua za mwishoni 
 Hili ni eneo ambapo magari yaliyobeba takataka yatakua yanaingia na kumwanga taka taka hizo 

 Mwonekano wa Karibu wa ndani wa Dampo hilo la kisasa Jijini Mbeya 
 Hii ni Chemba pekee ambayo ni maalum kwa ajili ya kupitishia takataka zenye kimiminika, pia kupitishia takataka ambazo zitakuwa zimesagwa na kupelekwa katika Bwawa maalum litakalo tumika kutengenezea umeme pamoja na mabaki mengine ya takataka yatatumika kutengenezea mbolea 
 Hapa Ndipo Takataka hizo zitakuwa zikitelemkia.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

KIKUNDI CHA TAARAB CHA TAIFA KIKIBURUDISHA WAKATI WA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI ZANZIBAR

TASWIRA MWANANA TOKA ZANZIBAR

MAALIM SEIF ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CUF

$
0
0
  Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad, akikabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, kutoka kwa Katibu wa tawi lake la Kidatu 'A' Mtoni, Bakar Hamad Ali. Aliijaza fomu hiyo na kuirejesha papo hapo. Picha na Salmin Said, OMKR
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wanachama wa chama hicho kufuata taratibu wakati wanapotaka kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama.
Amesema si halali kwa mwanachama yoyote kupelekewa fomu ya kugombea nyumbani au ofisini kwake, na badala yake anatakiwa kuchukua fomu hiyo katika tawi lake au kumtuma mwakilishi wake kufanya hivyo.
Mhe. Maalim Seif ametoa kauli hiyo katika tawi lake la Kidatu ‘A’ Mtoni, baada ya kuchukua fomu ya kugombea ujumbe wa mkutano mkuu Taifa.
Amesema ameamua kuchukua fomu hiyo katika tawi hilo, ili kudhihirisha ukomavu wa demokrasia ndani ya chama hicho, na kwamba hila mwanachama ana haki ya kuchukua fomu na kugombea nafasi yoyote anayoitaka ndani ya chama.
Amesema chama kitahakikisha kuwa chaguzi ndani ya chama zitakuwa za uwazi, huru na haki, na hakuna atakayependelewa wala kuonewa   katika chaguzi hizo.
Amefafanua kuwa katika kuhakikisha hilo linatendeka, chaguzi za Wilaya zitasimamiwa na wajumbe kutoka nje ya Wilaya husika, na ikiwezekana baadhi ya wasimamizi watatoka Tanzania Bara.
Jumla ya viongozi 20 kutoka Wilaya ya Magharibi wanatarajiwa kuchaguliwa kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, kupitia mkutano mkuu wa Wilaya unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, baada ya kukamilika kwa changuzi ngazi za majimbo.
Maalim Seif amechukua fomu hiyo ambayo aliijaza na kuirejesha papo hapo mnamo majira ya saa 6.00 mchana, ambapo alikabidhiwa na katibu wa tawi hilo nd. Bakar Hamad Ali.
Katika hatua nyengine, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amekemea tabia ya makundi na mitandao ndani ya chama, na kwamba makundi hayo hayakubaliki ndani ya chama hicho.
Amesema chama kinaweza kufuta uchaguzi wa ngazi yoyote ya chama iwapo kitabaini kuwepo kwa kampeni chafu, ikiwa ni pamoja na uwepo wa mitandao, makundi, pamoja kampeni chafu dhidi ya wagombea wengine.
Ameongeza kuwa mwanachama pia anayo haki ya kukata rufaa ikiwa hakuridhishwa na zoezi la uchaguzi, na kwamba rufaa yake itasikilizwa na kutolewa maamuzi yanayofaa kwa mujibu wa taratibu za chama.
Nae Mwenyekiti wa Tawi la Kidatu ‘A’ Mtoni bw. Ali Juma, amesema nafasi za uongozi ndani ya chama hicho ziko wazi, na kila mwanachama ana haki ya kuomba nafasi yoyote ya uongozi.
Amesema kitu cha msingi ni kufuata taratibu zilizowekwa, ambazo zinatoa fursa ya demokrasia ndani ya chama hicho.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images