Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA WIZI WA FEDHA KWENYE MASHINE ZA KUTOLEA FEDHA (ATM) NA ATM KADI 23

$
0
0

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Bi Halima Juma (23)Mkazi wa Chalinze kwa tuhuma za wizi wa fedha kwenye mashine za kutolea fedha (ATM).

Mnamo tarehe 19/11/2019 katika benki ya CRDB tawi la Mbagala akiwa katika ATM hizo, aidha alimtilia mashaka binti huyo aliyekuwa kwenye chumba cha ATM ya benki hiyo akijifanya kuwasaidia wazee na wastaafu wasiojua kutumia ATM mashine vizuri, lakini lengo lake ni kuchukua namba za siri za wastaafu na wazee hao na kisha kuwabadilishia ATM kadi zao na baadaye kuwaibia fedha kwenye akaunti zao kwa kutumia kadi halisi za wahusika baada ya kuwabadilishia kadi na kuchukua namba za siri.


Mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari wanaolinda Benki hiyo na alipopekuliwa alikutwa na ATM kadi 23 za watu mbalimbali za benki tofauti tofauti zikiwa katika pochi yake huku akiwa amezificha katika sehemu zake za siri ukeni.

Kadi hizo ni kama ifuatavyo;


1.CRDB kadi 07

2.NMB kadi 06

3.NBC kadi 02

4.AMANA kadi 02

5.POSTA BENKI kadi 02

6.ACB kadi 01

7.STANIBIC kadi 01

8.DTB kadi 01

9.EQUITY kadi 01.


Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani hivi karibuni.  



JESHI LA POLISI LATOA TAHADHARI YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam linapenda kutoa tahadhari kwa wakazi wa jiji la Dsm wote kuwa makini kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha ili kuepukana na majanga yanayoweza kuepukika. 

Hivyo wananchi wote wanatakiwa kuwa makini na watoto wadogo wanaohitaji uangalizi wa karibu, pia kujiepusha kupita kwenye maji ya mito midogomidogo au madimbwi ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wao.
Aidha hadi sasa zimepokelewa taarifa za watu wawili kufariki dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (SACP) Lazaro Mambosasa

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM KUIMARISHA ULINZI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika kwa amani na utulivu. 

Ndugu wana habari, tarehe 24/11/2019 ni siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji hivyo basi sisi kama Jeshi la Polisi tutaimarisha ulinzi maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam, 

katika vituo vya kupigia kura, ofisi zote za vyama vya siasa na ofisi zote za watendaji wa kata. 

Aidha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa onyo kali kwa mtu yeyote au kikundi chochote cha watu watakao jaribu kuvuruga amani jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

MEWATA WATAKIWA KUWEKA MSISITIZO KWENYE MASUALA YA CHANJO

$
0
0
Na. Catherine Sungura-Morogoro

MEWATA WATAKIWA KUWEKA MSISITIZO KWENYE MASUALA YA CHANJO

Na. Catherine Sungura-Morogoro

Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kimetakiwa kuweka msisitizo kwenye masuala ya utoaji elimu kuhusiana na chanjo nchini ili  idadi ya watoto wanaopatiwa chanjo kufikiwa.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa chama cha Madaktari Wanawake Tanzania  ambao unafanyika mkoani hapa.

Dkt. Magembe amesema kuwa elimu ya afya kwa wananchi inatakiwa kushushwa hadi chini ili taarifa kuweza kuwafikia walengwa wengi na hivyo kuweze kufika kwenye vituo vya afya kupata chanjo ili kuwakinga watoto katika  hatari ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. 

"Suala la chanjo ni la kuwekea msisitizo hivyo endapo tutashirikiana katika utoaji wa elimu hususan pale wizara inapokuwa na kampeni za chanjo ili watoto wetu wachanjwe na  kufikia adhima ya serikali ya kuwa na watoto waliokingwa kwa chanjo inatimia”.

Hata hivyo amekishukuru chama hicho kwa kutoa huduma za afya kwa upande wa wanawake hususani saratani ya mlango wa kizazi na ile ya matiti

“Wanawake ni taifa kubwa na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ni uchumi wa kati kupitia  viwanda hivyo hatuwezi kuwa na uchumi wa kati endapo wananchi wake ni wagonjwa hususani wanawake ambao ni wazalishaji” Alisisitiza Dkt. Magembe.

“Serikali inatambua mchango wengu MEWATA kwa upande wa saratani kwa miaka mingi hivyo imeweza kujenga vituo vya kutolea huduma zaidi ya mia nne na katika hivyo asilimia sabini ni vituo vya afya ambavyo vinatoa huduma ya upasuaji nchini yote inatokana na mchango wenu kwani mlipita nchi nzima kuwasaidia wanawake licha ya mazingira yaliyokuwepo”. 

Hata hivyo alisema hivi sasa magonjwa yasiyoambukiza  yanachangia asilimia arobaini ya vifo nchini hivyo serikali  kupitia wizara ya afya ilifanya tathimini ya sera ya afya na kuona magonjwa hayo yanaongezeka kwa kasi  na kuua watu wengi na kisababishi kikubwa  ni mtindo wa maisha pamoja na vyakula 

“kwa kuona hili kama wizara imekuja na mpango wa taifa wa magonjwa yasiyoambukizwa ili kila mdau aweze kuunganisha nguvu katika kupambana na magonjwa haya”.

Aidha, alibainisha kuwa  saratani ya mlango wa kizazi ni kati ya magonjwa  yanayoongoza kusababisha vifo kwa wanawake kwa takribani asilimia hamsini ya wanawake wote wanaoonwa na  saratani ya mlango wa kizazi inaongoza  ikifuatiwa na saratani ya matiti.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi huyo amewata MEWATA kutafuta namna  ya kushughulika na vitendo vya unyanyasaji  na ukatili wa kijinsia kwa watoto wadogo na wanawake kwani vitendo hivyo sasa hivi vimekua vikiongezeka kila siku,

 na hivyo kukitaka chama hicho kutoa elimu kwa jamii ili kuondoa vitendo hivyo kwa kuhakikisha inazungumza na jamii kuhusu suala la ukatili kwa watoto kwani hivi sasa watoto hawako salama na wanaathirika kisaikolojia na endapo jamii haitashiri katika malezi ya watoto jamii haitokuwa vizuri miaka ijayo.
 Mkurugenzi wa Tiba kutoka wizara ya afya Dkt. Grace Magembe akizungumza na wanachama wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa chama hicho
Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo Dkt. Dafrosa Lyimo akitoa mada  kuhusiana na saratani ya mlango wa kizazi kwenye mkutano huo
 Aliyekuwa Rais wa MEWATA miaka ya nyuma Dkt. Merina Njelekela akitoa neno la shukrani
 Rais wa MEWATA Dkt. Mary Charles akizungumza wakati wa mkutano huo
 Madaktari wanawake wa chama cha MEWATA wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 18 wa chama hicho
 Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi na wanachama wanaoshiriki mkutano huo wa  mwaka  wenye kauli mbiu "Umuhumu wa chanjo ya HPV  katika kukinga saratani ya mlango wa kizazi".

WAZIRI MKUU ASHIRIKI KATIKA SALA YA IJUMAA KATIKA MSIKITI WA GADDAFI, JIJINI DODOMA.

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Sala ya Ijumaa, kwenye Msikiti wa Gaddafi, Jijini Dodoma, Novemba 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waumini wa Dini ya Kiislamu, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, makati akizungumza baada ya Sala ya Ijumaa, kwenye Msikiti wa Gaddafi, Jijini Dodoma, Novemba 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Dodoma, Jafar Mwanyemba, mara baada ya Sala ya Ijumaa, kwenye Msikiti wa Gaddafi, Jijini Dodoma, Novemba 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UJUMBE KUTOKA HOSPITALI YA CHUO KIKUU YA HAUKELAND YA NCHINI NORWAY

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na (CEO,HUH) Mr.Eivind Hansen, alipowasili katika ukumbi wa Ikulu kwa mazungumza na Ujumbe kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland cha Nchini Norway, kulia Mr.Trond Mohn na Ms.Marit Mohn Westlake, wakiwa katika ukumbi Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na wageni wake kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland Nchini Norway baada ya kamaliza mazungumzo yao yaliofanyika leo 22-11-201 katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland cha Nchini Norway, ukiongozwa na (CEO HUH) Mr. Eivind Hansen (kulia kwa Rais) walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais leo 22-11-2019.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mr.Trond Mohn, alipowasili katika ukumbi wa Ikulu kwa mazungumzo na Ujumbe kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu ya Hakeland cha Nchini Norway.(Picha na Ikulu)

PICHA SPIKA AFUNGA BUNGE LA VIJANA MWAKA 2019

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Katibu wa Bunge la Vijana mwaka 2019, Ndugu Winfrida Gavana kabla ya kufunga Bunge hilo lilikuwa likiendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Katibu Mezani wa Bunge la Vijana, Ndugu Dolvin Olomi na Spika wa Bunge la Vijana Ndugu, Ramadhani Singa.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akitoa Hotuba ya Kufunga Bunge la Vijana mwaka 2019, lillilokuwa likiendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisalimiana wabunge wa Bunge la Vijana mwaka 2019 mara baada ya kulifunga Bunge hilo lililokuwa likiendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

TAASISI YA MOI YAOKOA TSH 38.4 ZA KUTIBIA WAGONJWA WAGONJWA NJE YA NCHI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI, Dkt.Respicious Boniface akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu mafanikio ya Taasisi hiyo kwa miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano,
Mkutano ulifanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar esSalaam.

TAASISI ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano imeokoa kiasi cha Tsh. Bilioni 38.4 zilizotakiwa kutumika kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa 43,200 nje ya nchi kwa ajili ya kupata huduma za matibabu ya upasuaji wa kibingwa.

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa (Novemba 22, 2019) Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Dkt Respicious Boniface na kuongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano, Taasisi hiyo imeendelea kuimarisha na kuboresha huduma mbalimbali za afya kwa wananchi.

Dkt. Respicious anasema kutokana na maboresho na kuimarika kwa huduma ya afya, Taasisi ya MOI ndani ya kipindi cha miaka minne imeweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa 43,200 waliofanyiwa upasuaji wa kibingwa na hivyo kuokoa maisha ya Watanzania wengi na pesa za Serikali ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.

‘Gharama za matibabu za wagonjwa hao kwa ndani ya nchi zilikuwa Tsh Bilioni 16.5 na kama wagonjwa hao wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu, jumla ya Tsh Bilioni 54.9 zingetumika, na hivyo kuifanya taasisi kuokoa kiasi cha Tsh Bilioni 38.4 ambazo zitatumika kwa shughuli nyingine za maendeleo’’.

Aliongeza kuwa Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne iliyopita imeweza kupokea kiasi cha Tsh. Bilioni 16.5 kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo jengo jipya la MOI pamoja na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa ambavyo vimeweza kuleta mageuzi na maboresho ya huduma za afya katika Taasisi hiyo.

Akitolea mfano, Dkt. Respicious anasema katika fedha hizo zilizotolewa na Serikali, taasisi hiyo iliweza kuongeza idadi ya vitanda kutoka 150 hadi 350 kwa wagonjwa wa kawaida, na kufanya kutowepo na mgongjwa anayelala chini kwa sasa, sambamba na kuongeza idadi ya vitanda kwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum kutoka vitanda 8 hadi 18.

Aidha Dkt. Respicious anasema kuwa pia katika fedha hizo, Taasisi hiyo imeweza kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka vyumba 6 hadi 9, kuongeza vyumba 32 vya wagonjwa binafsi vya daraja la juu pamoja na kuongeza chumba cha upasuaji kwa mgonjwa bila kulazimika kulala hospitali.

Kuhusu vifaa Dkt. Respicious anasema, katika fedha hizo, pia Taasisi ya MOI iliweza kununua mashine mpya za kutolea dawa za usingizi, mashine za kisasa za Radiolagia zikiwemo MRI, CT-Scan, Digital X-Ray, CR X-ray, Portable X-ray, Ultra Sound 2, ECHO na ECG, ununuzi wa mashine mbili mpya za kisasa za vipimo vya maabara.

Akifafanua zaidi, Dkt. Respicious anasema kutokana na maboresho hayo, Taasisi hiyo ndani ya kipindi cha miaka mine imeweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa 43,200 waliofanyiwa upasuaji wa kibingwa na hivyo kuokoa maisha ya Watanzania wengi na pesa za Serikali ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.

‘Mbinu hii imesaidia kuongeza idadi ya wagonjwa wa upasuaji kutoka 400-500 kwa mwezi hadi kufikia 700-900 kwa mwezi, na idadi ya wagonjwa hao waliofanyiwa upasuaji wa kibingwa ni pamoja na kubadilisha nyonga (900), kubadilisha magoti (870), upasuaji wa mfupa wa kiuno (618), watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi (2,070)’’ alisema Dkt. Respicious.

Aidha Dkt. Respicious anasema Taasisi ya MOI pia imeanzisha huduma mpya ikiwemo huduma ya upasuaji wa magoti/mabega kwa njia ya matundu ambapo hadi sasa wagonjwa 800 wamefanyiwa upasuaji pamoja na huduma ya upasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo ambapo wagonjwa watano pia wamefanyiwa upasuaji huo.

Anaitaja huduma nyingine kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa wodi maalum ya kulazwa na kufanyiwa upasuaji siku hiyo hiyo, ambapo wagonjwa 355 wamefanyiwa upasuaji na kufanya upasuaji wa uti wa mgongo kwa kupitia tundu dogo, ambapo hadi sasa wagonjwa 120 wamefanyiwa upasuaji.

‘Huduma hizi mpya, zimeiwezesha Taasisi kupunguza kwa kiasi kikubwa rufaa za wagonjwa nje ya nchi, ambapo kwa sasa kwa magonjwa ya Neurosurgies asilimia 95 tunafanya hapa na upasuaji wa mifupa asilimia 98 tunafanya hapa pia’’ alisema Dkt. Respicious

Kuhusu huduma ya tiba mtandao, Taasisi hiyo kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imejenga chumba maalum ambapo madaktari katika sehemu mbalimbali za nchi watatuma picha za X-ray/CT-Scan zitakazosomwa na madaktari bingwa wa radiolojia na majibu yatarudishwa kwa daktari aliyeomba kwa muda mfupi.

Aidha katika katika eneo la mafunzo, Dkt. Respicious anasema katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli, jumla ya madaktari bingwa 50 wa mifupa wamehitimu mafunzo, ukilinganisha na madaktari 7 waliohimtimu katika kipindi cha miaka mine iliyotangulia.

Ujumbe kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi kutoka Kenya wafanya ziara Sekretarieti ya Maadili nchini

$
0
0
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Ms na Ufisadiya Kenya iliyoongozwa na Kamishna wa Tume hiyo Bi Rose Mghoi Macharia (kulia kwa Mhe. Nsekela) baada ya kuhitimisha ziara yao ya siku tano katika Sekretarieti ya Maadili tarehe 22 Novemba, 2019 iliyokuwa na lengo la kubadilishana uzoefu wa kiutendaji baina ya taasisi hizo mbili. (Picha na Ally Mataula, Afisa Habari Sekretarieti ya Maadili)
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Harold Nsekela katikati na Watendaji
wengine wa Sekretarieti ya Maadili wakiwa katika picha pamoja na Ujumbe
kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi ya Kenya iliyoongozwa
na Kamishna wa Tume hiyo Bi Rose Mghoi Macharia (kulia kwa Mhe.
Nsekela) baada ya kuhitimisha ziara yao ya siku tano katika Sekretarieti ya
Maadili tarehe 22 Novemba, 2019 iliyokuwa na lengo la kubadilishana
uzoefu wa kiutendaji baina ya taasisi hizo mbili. ( Picha na Ally Mataula,
Afisa Habari Sekretarieti ya Maadili)
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Harold Nsekela katikati na Watendaji
wengine wa Sekretarieti ya Maadili wakiwa katika picha pamoja na Ujumbe
kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi ya Kenya iliyoongozwa
na Kamishna wa Tume hiyo Bi Rose Mghoi Macharia (kulia kwa Mhe.
Nsekela) baada ya kuhitimisha ziara yao ya siku tano katika Sekretarieti ya
Maadili tarehe 22 Novemba, 2019 iliyokuwa na lengo la kubadilishana
uzoefu wa kiutendaji baina ya taasisi hizo mbili. ( Picha na Ally Mataula,
Afisa Habari Sekretarieti ya Maadili).

*******************************************

Na. Ally Mataula,Afisa Habari Sekretarieti ya Maadili.

Viongozi Waandamizi wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi kutoka nchini Kenya wamefanya ziara katika Ofisi za Sekretearieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Makao Makuu Jijini Dodoma.

Ziara hiyo ya siku tano iliyoanza tarehe 18 – 22 Novemba, 2019 iliongozwa na Kamishna wa Tume hiyo Bi Rose Mghoi Macharia ambaye alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kubadilishana uzoefu wa kiutendaji baina ya Tume hiyo na Sekretarieti ya Maadili.

Bi Macharia alisema kuwa wameamua kuja Tanzania kupata uzoefu katika suala la usimamizi wa Maadili kutokana na misingi imara iliyowekwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuona kama kuna maeneo ambayo wanaweza kujifunza kutoka Tanzania.

Akielezea baadhi ya majukumu ya Taasisi yake, Bi Macharia aliyataja kuwa ni pamoja na kusimamia uzingatiaji wa Sura ya Sita na Ibara ya 151 ya Katiba ya Jamhuri ya Kenya, Kufanya uchunguzi na kutoa mapendekezo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka kushtaki kosa lolote linalohusu rushwa, uhujumu uchumi, vitendo vya ukiukaji wa misingi ya maadili na mambo mengine yaliyobainishwa na Sheria.

Shughuli nyingine ni Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Maadili kwa Maafisa na Viongozi wa Umma, kupokea malalamiko yanayohusu ukiukwa wa Sheria ya Maadili unaofanywa na Maafisa wa Umma, Kufanya uhakiki wa uadilifu kwa watu wanatafuta nafasi ya kuteuliwa au kuchaguliwa kushika ofisi za umma, pamoja na kutoa elimu na uelewa kuhusu mambo ya mapambano dhidi ya rushwa na maadili nchini Kenya.

Akizungumzia kuhusu utaratibu wa kisheria wa Tanzania unaowataka Viongozi wa Umma kusaini Hati ya Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma mara baada ya kuchaguliwa au kuteuliwa kushika nafasi katika Ofisi za Umma Bi Macharia alifurahishwa na utaratibu huo na kueleza kuwa unasaidia kuwakumbusha viongozi wakati wakitekeleza majukumu yao.

Naye Kamishna wa Maadili ambaye alikuwa ni mwenyeji wa ujumbe huo, alisema kuwa Sekretarieti ya Maadili ilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 132(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma yeyote kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yanazingatiwa ipasavyo.

Pia Mhe. Nsekela aliueleza ujumbe huo baadhi ya misingi ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inapaswa kuzingatiwa na Viongozi wa Umma wakati wakitekeleza majukumu yao. Aidha, kwa mujibu wa Mhe. Nsekela misingi hiyo inawataka watu wanaoshika nafasi fulani za madaraka kutoa mara kwa mara maelezo rasmi kuhusu mapato, rasilimali na madeni yao.

Pia, misingi ya maadili inapiga marufuku mienendo na tabia inayopelekea kiongozi kuonekana hana uaminifu, anapendelea au si muadilifu au inaelekea kukuza au kuchochea rushwa katika shughuli za umma au inahatarisha maslahi au ustawi wa jamii. Alifafanua Mhe. Nsekela.

Katika ziara hiyo ya siku tano, viongozi hao kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi ya nchini Kenya waliweza kujifunza mambo mbalimbali kutoka Sekretarieti ya Maadili hususani katika maeneo kadha wa kadha ambayo ni pamoja na Mfumo wa Sera na Sheria inayokuza na kusimamia Maadili nchini, Taratibu za Kuanzisha, Kufanya Uchunguzi kuhusu ukiukaji wa maadili, njia ya kuwasilisha malalamiko na namna ya kusimamia Matamko ya Rasilimali za Viongozi wa umma.

Mambo mengine ni Uendeshaji wa Baraza la Maadili, usikilizaji wa malalamiko pamoja na utekelezaji wa adhabu kwa viongozi ambao wamebainika kukiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Pia, Ujumbe huo ulipata fursa ya kujifunza Mifumo mbalimbali kama vile Mfumo wa Udhibiti wa Taarifa, Mfumo wa kielectroniki wa utoaji wa Matamko ambao upo katika hatua za mwisho kukamilika pamoja na Mfumo wa Ufuatiliaji wa Uzingatiaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Pamoja na kutembelea Sekretarieti ya Maadili, Ujumbe huo pia ulipata fursa ya kutembelea katika Taasisi nyingine za Umma ambazo ni Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, TAKUKURU, Chuo Kikuu cha Dodoma na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA).

DC CHONGOLO AMUAGIZA KAMANDA WA TAKUKURU KINONDONI KUMKAMATA NA KUMCHUNGUZA MKANDARASI ANAYEDAIWA KUIBA MILIONI 54 ZA WANANCHI.

$
0
0
Mkandarasi David Emanuel mwenyesuti nyeusi akiingia kwenye gari mara baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Mhe. Daniel Chongolo kumuagiza Kamanda wa Takukuru mkoa maalumu wa Kinondoni kumchunguza kulingana na tuhuma zinazomkabili.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo katikati mwenyesuti nyeus akizungumza na Kamati zilizoundwa na wananchi kwa ajili ya kuratibu na kusimamia zoezi la urasimishaji makazi. Kushoto wapili ni Katibu Tawala Stella Msofe.
********************************

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa Takukuru Mkoa maalumu wa Kinondoni kumchunguza Mkandarasi wa Savei anayesimamia urasimishaji makazi ya wananchi kanda ya Madale two , David Emanuel kutokana na tuhuma ya kudaiwa kuiba kiasi cha shilingi milioni 52 fedha zilizochangwa na wananchi.

Ameongeza kuwa milioni 52 zimelipwa pasipokufuata utaratibu kutokana na mkandarasi huyo kuwa sehemu ya waweka saini katika akaunti ya wananchi na kwamba alichokuwa anakifanya nikwenda mwenyewe benki na kuchukua fedha..

Mhe. Chongolo amefikia uamuzi huo leo (jana) katika kikao chake na Kamati zilizoundwa na wananchi kwa ajili ya kuratibu na kusimamia zoezi la urasimishaji pamoja na wakandarasi waliopewa jukumu la urasimishaji makazi ya wananchi katika Halmashauri hiyo.

Mhe. Chongolo ameeleza kuwa mkandarasi huyo alijilipa mwenyewe fedha hizo pasipokufuata utaratibu na kwamba kitendo hicho ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi na kuagiza Takukuru Kinondoni kumchukulia hatua pindi atakapobainika ukweli dhidi ya tuhuma hizo.

Amefafanua kuwa katika kanda hiyo, viwanja zaidi ya 1800 vimerasimishwa na hivyo wananchi wamechanga kiasi cha shilingi zaidi ya milioni 70 na kwamba hadi sasa mkandarasi huyo ameshalipwa shilingi milioni 62 ambapo kati ya hizo milioni 12 ndio zilizolipwa kwa kufuata utaratibu.

“ Sasa ukiona hivi unajua kabisa kunachangamoto ya matumizi yasio yasihi ya fedha za wananchi,nimechukua hatua nimemkabidhi Kamanda wa Takukuru mkoa maalumu wa Kinondoni, wamemchukua wanakwenda kushugulikia kufanya uchunguzi na pale watakapobaini kunaukiukwaji watamchukulia hatua” amesema Mhe. Chongolo.

Nakuongeza kuwa” kulingana na changamoto ambayo tumeibaini leo kwenye mtaa mmoja, nimeagiza kitengo cha ukaguzi wa ndani kwenda kukagua akaunti zote za urasimishaji ndani ya Halmashauri yetu ,ili kujiridhisha na yale watakayo yabaini sisi watuletee ripoti ilituweze kuchukua hatua stahiki kwa wakati muafaka”.

Awali Mhe. Chongolo amesema kuwa katika mkutano huo wanapokea taarifa ya kila mkandarasi juu ya mwenendo na matumizi ya fedha zinazochangwa kutoka kwa wananchi ilikukamilisha zoezi husika la urasimishaji.

Amebainisha kuwa , katika mkutano huo amejifunza kuwepo na changamoto ya usimamizi wafedha za wananchi katika maeneo mengi yanayoendesha zoezi hilo ipo haja ya haraka katika kutatua changamoto hizo.

Kitabu cha Mkapa, JPM Alikisoma Kabla Hakijaandikwa

$
0
0

Na: Lillian Shirima – Habari MAELEZO

Novemba 12, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Dkt. John Magufulializindua kitabu cha maisha binafsi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa cha (My Life My Purpose) (Maisha Yangu, Kusudi Langu) , hafla hiyo iliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa viongozi wengi wakiwemo na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete.

Kitabu hicho chenye kurasa 316, na sura 16 zilizogawanywa kwenye sehemu kuu tatu, kimesheheni wingi wa nasaha na ushauri lakini pia kinatoa mafundisho mengi kwa viongozi wa baadaye jambo ambalo Rais John Pombe Magufuli aliliona mapema pengine kabla ya kuandikwa kwenye kitabu hicho.

Katika sehemu ya mwisho ya kitabu inayoeleza kwa ufupi maisha ya Mzee Mkapa baada ya kumaliza miaka kumi ya kulitumikia taifa kwa ngazi ya urais, Mkapa anatoa ushauri kwa kutaja mambo sita ambayo kiongozi anawajibu kwa kuyazingatia.

Mambo hayo ni kuonyesha nia na bidii kwa majukumu unayopewa na wananchi, kuwa tayari kuwashirikisha wengine katika mawazo, mafanikio, matatizo na upimaji wa utekelezaji, kutofanya kazi kwa kukurupuka na kutotabirika.

Mengine ni kufuata na kutii sheria na taratibu, kuwa tayari kusikiliza na mwisho kutafuta mlezi (mentor) kama ambavyo yeye mwenyewe Mzee Mkapa anavyoeleza mlezi wake kuwa alikuwa Mwalimu Julius Nyerere.

Katika mahojiano yaliyofanyika na mtaalam wa masuala ya siasa Bwana Severine Kapinga kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salam, (UDSM), anasema, ushauri aliotoa Mzee Mkapa kuhusu wajibu wa kiongozi na mambo anayotakiwa kuzingatia hapana shaka Rais John Magufuli alianza kuyaishi na kuyazingatia kabla kitabu cha Mkapa hakijaandikwa 2016.

Anaongeza kuwa, nchi yoyote duniani toka ilipopata uhuru ikipita miaka 50 ni lazima nchi hiyo ifikie wakati wa kuweza kujipambanua na kujielewa ipo wapi, inataka kufika wapi na imekwama wapi; kazi ambayo sio ya sera pekee bali ni kazi itakayofanywa na kiongozi mwenye nia ya kuwatumikia wananchi kwa dhati.

“Hii sio kazi ya kisera tu, ni kazi ambayo itaongozwa na kiongozi ambaye
amechaguliwa na watu na yeye sasa ndiye anayetakiwa kubeba maono ya watu na dhamira ya walio wengi’. Anasema Bw. Kapinga.

Rais Magufuli amethubutu katika hili kuonesha nia na bidii ya kazi katika majukumu aliyopewa na wananchi na kwamba ameweza kuvaa taswira ya maono ya wananchi kwa namna anavyoisimamia na kuiongoza nchi, uwajibikaji wake umekuwa chachu kwa wananchi kufanya kazi kwa bidii.

Aidha, anasema mageuzi makubwa yanayoonekana sasa yanatokana na uwajibikaji wa Rais Magufuli katika kusimamia rasilimali za nchi, nidhamu kwenye matumizi ya fedha za umma na maarifa katika kushughulikia matatizo ya wananchi wanyonge.

Mara kadhaa tunashuhudia Rais Magufuli akifanya mikutano na watendaji wa Serikali kuanzia Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya na Makatibu Watendaji wa Tarafa. Mathalani, Septemba 2,mwaka huu, Rais Magufuli alikutana na Maofisa Watendaji wa Kata kutoka nchi nzima Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mbali na kuwashirikisha katika maamuzi kama ambavyo Mzee Mkapa ameshauri katika kitabu chake, Rais Magufuli ameenda mbali zaidi na kuwaasa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kata wanazozisimamia zinakuwa na ulinzi na usalama.

Rais Magufuli aliwaambia, “hakuna shughuli za maendeleo zinazoweza kufanyika bila kuwa na amani, ni lazima wananchi wafanye kazi bila hofu , bila bugudha…”.Ushauri wa Mzee Mkapa kwa viongozi wajao ni dhahiri ulianza kutekelezwa kitambo.

Kundi lingine lililokutana na Rais Magufuli Juni,mwaka huu ni wafanyabiashara kutoka katika wilaya zote nchini kwa nia ya kutaka kujadiliana kwa uwazi namna ya kutatua changamoto walizonazo na kubuni njia bora za kuboresha mazingira ya biashara nchini.

Wengine ni Mabalozi wetu wanaotuwakilisha katika nchi mbalimbali, wachimbajimadini na wadau wa sekta ya madini, na hata wachezaji wa timu ya Taifa, (Taifa Star) Hakika Rais hafanyi kazi kwa kukurupuka au kutotabirika isipokuwa kushirikisha kada tofauti katika mipango ya maendeleo, Ushauri aliotoa Mzee Mkapa katika kitabu chake.

Mara kadhaa Rais Magufuli amesikika akisema yeye si wa kundi lile, yeye ni wawanyonge na kwamba Watanzania wanyonge ndio watakajenga nchi hii.
Kwa kauli hii Bwana Kapinga anasema, Rais Magufuli angekuwa upande wa watuwachache miradi mikubwa tunayoiona sasa isingekuwepo lakini kwa kuwa ameamua kusimama upande wa Watanzania wanyonge mwamko wa watu kujituma kufanya kazi umekuwa mkubwa.

Wakati wa uzinduzi wa Kitabu hicho,Rais Magufuli ambaye alikuwa mgeni rasmialimshukuru Mzee Mkapa kwani katika uongozi wake wa Awamu ya Tatu mambo mengi yamefanyika ikiwa ni pamoja na kujenga barabara kwa fedha za ndani.

Alieleza namna alivyovutiwa na sura nyingi za Kitabu hicho ambazo zimeeleza jinsi ya kujitegemea, jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na kusisitizwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Akitoa mfano mdogo wa hatua ambazo Serikali ya Awamu ya Tano imeleta mwamko wa watu, Bwana Kapinga amesema, kuanzishwa kwa mpango wa utoaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo wenye biashara chini ya mzunguko wa shilingi milioni 3 kwa kiasi kikubwa umewaweka wajasiriamali katika mazingira huru yakujitegemea.

Mara baada ya zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara ndogondogo kukamilika, wengi wao wameanza kutambua kuwa nchi ipo katika mageuzi ya kiuchumi na wanashiriki kuchangia maendeleo ya nchi.

Anasema, ukifika Kariakoo, Tazara na maeneo ya wafanyabiashara ndogondogo,wamachinga,wanaweza kukueleza juu ya miradi mikubwa kama ujenzi wa reli yakisasa, madaraja na barabara za juu kwasababu wanatembea kwa amani wakifanya biashara pasipo chuki na Serikali.

“Siku hizi tumesahau mambo ya kukimbizana na wamachinga na mama ntilie mjini, kamatakamata ambayo haina mwelekeo haipo tena kwa sababu Rais aliamua kutafuta majibu ya kero za wafanyabiashara ndogondogo kwa kuwapa vitambulisho na ruhusa kufanya shughuli zao bila bughudha”, anasema Kapinga.

Tunamwona Rais akifanya ziara za ndani zaidi kuliko ziara za nje ya nchi kwa msingi wa kuwa tayari kusikiliza matatizo ya wananchi na kutafuta ufumbuzi wamatatizo hayo ikiwa ni pamoja na kuhakiki taarifa za maendeleo anazopewa na wasaidizi wake.

Hakuna ziara anayofanya bila kuwa na taarifa ya eneo husika hii ni kutokana nauzoefu wa muda mrefu katika kulitumikia taifa ndio unaopelekea kuwepo kwa ziara za kushtukiza.

Bwana Kapinga anasema, hatua hii ndio inayofanya wote waliokuwa wavivu wakwenda kwa wananchi kutambua kuwa kazi kubwa ipo kwa wananchi na sio nje ya nchi na kwamba Awamu ya Tano imerudisha mamlaka kwa wananchi kwasababu viongozi wakuu wa Serikali wanakwenda kwa wananchi mara kwa mara.

“Huwezi kuwa na mamlaka na Serikali kama huioni, tunasema hii ndio Serikali ya watu…. viongozi wanathamini watu, Rais amekaa nafasi ya waliokosa, nafasi ya mwananchi mwenye hali ngumu, kwa sababu amepewa dhamana na wao, anaumia kama anavyoumia yule mwananchi wa mwisho”, anasema Bwana Kapinga.

Ni katika kitabu hicho Mzee Mkapa ameshauri viongozi kutafuta mlezi (mentor) na kwamba kwake yeye Mwalimu Nyerere alikuwa mezi wake. Sio siri Mzee Mkapa ndiye aliyemuibua Rais Magufuli katika medani za siasa. Ndiye aliyetambua uwezo wake wa kazi katika kusimamia maamuzi sahihi na kuyatekeleza kwa ufasaha, na Mzee Mkapa ndiye aliyekuwa tayari kumtia nguvu pale alipokutana na vikwazo katika utekelezaji wa majukumu ya kazi kwa maslahi ya taifa.

Ushauri wa mambo sita yaliyotajwa katika kitabu cha Mzee Mkapa “Maisha Yangu Kusudi Langu” tunaona kuwa,Rais John Pombe Magufuli ameutekeleza mapema na ndiyo maana tunasema , alikisoma kitabu kabla hakijaandikwa, alianza kuzingatia mengi kwa vitendo na hata katika hotuba yake za uzinduzi wa kitabu hiki amekiri kuwa Mzee Mkapa ndio shujaa wake, ametoa wito kwa Watanzania kuwaenzi na kuwatunza wazee wote wakiwemo viongozi wastaafu ambao ama kwa hakika tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwao.

UTABIRI WA ASILI WALETA MANUFAA

$
0
0


SIMANJIRO-MANYARA

Katika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara asilimia 80 ni wafugaji na ufugaji ndiyo kazi kubwa inayowapatia kipato na chakula, kutokana na hali hiyo Wananchi wa vijiji 6;wamepatiwa elimu ya kukabiliana na matukio yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa katika sekta za mifugo, kilimo, uvuvi, na uchimbaji wa madini.

Akizungumza katika kijiji cha Korongo wilayani humo Afisa ufuatiliaji na Tathmini wa Mradi wa Ardhi Yetu kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Jumuiko la MaliAsili Tanzania (TNRF) Bwana Rogath Massay amesema kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wanaijengea jamii uwezo kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kuondoa changamoto mbalimbali ikiwemo ya taarifa kutofika kwa wakati kwa wananchi.

Wananchi walioshiriki mafunzo hayo ya siku mbili wamelishukuru Shirika la Jumuiko la MaliAsili Tanzania (TNRF) kuona umuhimu wa kuwapatia mafunzo juu ya kupata taarifa za tabiri za kiasili na Kisayansi; huku wakitoa wito kwa wadau kuendelea kushirikiana na serikali kuwajengea uwezo zaidi ili waweze kukabiliana na majanga katika maeneo yao.

Aidha wsahiriki hao wameelezea viashiria vya kiasili vinavyotumika kutoa taarifa za utabiri wa kiasili kwa wananchi huku wakieleza vikwazo vilivyowafanya wasifikie malengo msimu wa vuli uliopita baada ya kupatiwa mafunzo hayo.

Afisa Kilimo Wilaya ya Simanjiro Bi Jenifa Mbuya amesema taarifa za tabiri za hali ya hewa za kijadi na kisayansi ni msaada mkubwa kwa wakulima na wafugaji ingawa baadhi ya taarifa zinakosekana kutokana na wazee wa zamani waliokuwa wakitabiri wengi wao kufariki dunia, na kuwataka wazee wa sasa kuweka kumbukumbu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Daktari wa Mifugo Wilaya ya Simanjiro Yasini Mshana amesema taarifa za tabiri za kijadi na kisayansi ni muhimu kwa shughuli za kila siku za ufugaji kwani zinatoa mwanga kwa wafugaji kujua ni wapi wawekeze nguvu zao kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Mazingira Wilaya ya Simanjiro Bwana Jovin Rweyemamu amesema zamani utabiri wa kijadi ulikuwa na nguvu tofauti na sasa; wananchi wanategemea zaidi utabiri wa kisayansi kutokana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwaa na uharibifu wa mazingira.

Aidha Mtabiri wa Hali ya Hewa kitengo cha utafiti, mazingira, na Matumizi Ya Hali Ya Hewa Bibie Abdallah amesema lengo kubwa la mafunzo hayo ni kutoa uelewa kwa wakulima na wafugaji juu ya taarifa za hali ya hewa ili kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku za kilimo na ufugaji.

Vijiji vilivyonufaika kwa mafunzo hayo kupitia mradi wa Ardhi yetu unaosimamiwa na Shirika la Jumuiko la MaliAsili Tanzania (TNRF) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ni Korongo, Magadini, Kitwai A na B, Olchoronyori, pamoja na Loonderkes vilivyopo Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

TAA kujenga madarasa ya sekondari Wilaya ya Kibaha

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama (kushoto) akipokeamifuko 300 ya saruji kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara waMamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Josephine Kolola (kulia), katikahafla iliyofanyika leo nje ya jengo la Halmashauri ya Mji Kibaha. Kushoto niMkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jenifer Omolo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Leonard Mlowe (kushoto)leo akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara wa Mamlaka yaViwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Josephine Kolola, ambaye alimwakilishaMkurugenzi Mkuu, Mhandisi Julius Ndyamukama kutoa msaada wa mifuko 300ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari. Kulia ni Mkurugenzi wa Mji Kibaha, Jenifer Omolo na kushoto ni Afisa Habari wa MjiKibaha, Innocent Byarugaba.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama leo akizungumziamasuala mbalimbali ya wilaya hiyo, wakati wa hafla ya kuchangia mifuko 300 yasaruji, iliyotolewa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), ambapokulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara wa TAA, Josephine Kolola,aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Julius Ndyamukama.
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara wa Mamlaka ya Viwanjavya Ndege Tanzania (TAA), Josephine Kolola, leo akizungumza na waandishiwa habari na watendaji wa Halmashauri ya Mji Kibaha (hawapo pichani), wakatialipomuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi Julius Ndyamukama nakukabidhi mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya kujenga madarasa ya shule za sekondari za wilaya hiyo.

***********************************

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), leo imetoa mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari za Wilaya ya Kibaha, inayokabiliwa na upungufu wa madarasa 65.

Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara wa TAA, Josephine Kolola aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Julius Ndyamukama amesema Mamlaka hiyo inaunga mkono jitihada za serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kutoa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari, ambapo sasa kuongezeka kwa madarasa hayo kutachangia watoto wengi kupata elimu.

“Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, ipo bega kwa bega na jamii katikakuziunga mkono jitihada mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, iliyopo chini ya Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, ambapo inahakikisha vijana wengi wanapata elimu ya msingi na sekondari bure katika mazingira bora. Elimu wanayopata vijana wetu itawasaidia kukabiliana na changamoto za maisha kwa ajili ya ustawi wao na Taifa kwa ujumla,” amesema Kolola.

Amesema katika kufanikisha jitihada hizo kwa vitendo na pia ni sera ya Mamlaka kurudisha kwa jamii kiasi cha mapato wanayozalisha ili waweze kutatua changamoto zinazowakabili, hivyo wametoa mifuko hiyo wakiwa na imani itasaidia kujenga madarasa hayo.

Amesema TAA ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na.30 ya mwaka 1997 na kupewa dhamana na Serikali ya kusimamia na kuendesha jumla ya viwanja 58 vilivyopo Tanzania Bara, ambapo Serikali inafanya jitihada kubwa katika kuboresha miundombinu mbalimbali Viwanjani ili viweze kuendana na mahitaji ya soko na ushindani wa kibiashara.

“Hivyo kupitia juhudi hizi za serikali zimezalisha fursa mbalimbali viwanjani zikiwemo fursa za kibiashara, ajira rasmi na zisizo rasmi”, amesema.Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama pamoja na kuishukuru TAA kwa msaada huo mkubwa, amesema katika Kampeni yao ya “Elimisha Kibaha”,wamekusudia kujenga madarasa 65, na kununua viti 3250 na meza 3250 ili kuweka mazingira bora ya kusoma kwa wanafunzi.

“Tunaupungufu mkubwa wa madarasa ambapo wanafunzi 700 wa kidato cha Kwanza mwaka huu (2019) wamekumbwa na kadhia hii, nasi tukaamua waingie darasani kwa awamu mbili asubuhi na mchana, lakini bado ikawa shida kutokana na kuwa na watoto wengi, ndio maana tukaanzisha kampeni hii kwa lengo la kupunguza na ikiwezekana kuondoa kabisa tatizo na watoto wasome katika mazingira bora,” amesema Mkuu huyo.

Amesema hadi sasa tayari wamekusanya vifaa vya kutosheleza ujenzi wa madarasa 26, lakini bado hawajaanza ujenzi kutokana na fedha zilizowasilishwa Hazina kushindwa kutolewa hadi sasa kutokana na kuwa na utaratibu mrefu, ambapo amekuwa na hofu huenda hadi kufika Januari mwaka 2020 wakakumbwa na kadhia ya wanafunzi kushindwa kuendelea na kidato cha Kwanza kutokana na kukosekana na madarasa ya kutosha.

“Tunaomba huko tulipopeleka hizi fedha cash basi wazitoe ili ujenzi uanze mlolongo ni mrefu sana hatujui tatizo lipo wapi, na watui ndio kama hivi wanachangia vifaa tunashindwa kuanza ujenzi,” amesisitiza Mhe. Mkuu wa Wilaya.

Hatahivyo, amemshukuru Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kutoa elimu bure ambayo imesababisha mwamko mkubwa kwa wazazi wengikuwapeleka watoto wao shule. Hali kadhalika kawashukuru wananchi, walimu na wadau wote waliojitokeza kuchangia kwa kutoa fedha taslimu, vifaa na ahadi, ambapo tayari wameshakusanya Shilingi milioni 950.

MBUNGE WA GEITA MJINI, MHE.KANYASU AANZA KUWATAMBULISHA WENYEVITI WATEULE WA CCM

$
0
0
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi wa eneo la Mpomvu katika kata ya Mtakuja wakati akiwatambulisha Wenyeviti wateule wa CCM.
Katibu wa Mbunge wa Geita mjini, Mariamu Mkaka akitoa ufafanuzi wa jambo katika mkutano wa kuwatambulisha Wenyeviti wateule wa Serikali za mitaa wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Mpomvu kata ya Mtakuja mkiani Geita.
Msanii wa Vichekesho maarufu kwa jina la Kigwendu Kingwendulile akiwaburudisha wananchi waliofika ktika eneo la Mpomvu kwa ajili ya kuwatambulisha wakazi wa eneo la Mpomvu kabka ya Mbunge wa Geita mjini kuzungumza nao.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Benue, James Manakila akiwatambulisha Wajumbe wa mtaa wake kwa Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu.

*****************************


Mbunge wa Geita mjini na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameanza kuwatambulisha Wenyeviti wateule wa Chama cha Mapinduzi( CCM) kwa wananchi kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza na Wananchi wa eneo la Mpomvu katika Kata ya Mtakuja mkoani Geita, Mhe.Kanyasu ametumia fursa hiyo kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika katika kipindi chake cha Uongozi wa miaka minne.

Katika mkutano huo, Mhe.Kanyasu amewatambulisha Wenyeviti wateule wa mitaa saba kwa wananchi na kuwataka watoe ushirikiano ili kuleta maendeleo.Ametaja mafanikio hayo kuwa yamepatikana katika nyanja ya Elimu, Afya, Barabara, mikopo pamoja na Umeme.

Mbali ya kuelezea mafanikio hayo yaliyopatikana katika utekezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM (2015-2020) katika jimbo hilo, Mhe.Kanyasu ametaka wananchi kutoa ushirikiano kwa Wenyeviti wapya watakaopatikana katika uchaguzi huo ili kuharakisha miradi ya maendeleo.

Wanawake wenye ualibino, walio na watoto wenye ualibino wapewa mafunzo

$
0
0


Na George Binagi-GB Pazzo, Mwanza

Shirika la Under The Same Sun linaloshughulika na utetezi wa haki za watu wenye ualibino Tanzania limetoa mafunzo kwa akina wanawake wenye ualibino pamoja na wanawake wenye watoto walio na ualibino mkoani Mwanza ili kuwajengea uwezo kuhusu hali ya ualibino.

Mafunzo hayo ya siku tatu yameanza Novemba 22, 2019 jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Mfuko wa Kanada kwa ajili ya Mipango ya Kijamii (Canadian Fund for Local Initiative- CFLI) unaotekelezwa katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga.

Mratibu wa mradi huo, Grace Wabanhu amesema matarajio baada ya mradi huo wa miezi minne kufikia tamati ni wanawake hao kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu hali ya ualibino na hivyo kuwa na ujasiri wa kuielimisha jamii inayowazunguka ili kuondokana unyanyapaa na ukatili dhidi ya watu wenye ualibino na hatimaye kuleta usawa katika jamii.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualibino (TAS) Mkoa Mwanza, Alfred Kapole amesema akina mama ni jeshi kubwa hivyo baada ya kuelimishwa kupitia mradi huo watakuwa mabalozi wazuri wa kutoa elimu katika jamii kuanzia ngazi ya nyumbani na hatimaye kusambaa hadi vijijini.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo mama mwenye mtoto aliye na ualibino, Shika Madebe kutoka wilayani Misungwi wameahidi kuitumia vyema elimu watakayoipata kwa kuwaelimisha wanajamii wengine ambao bado hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na ualibino na hivyo kuondokana na unyanyapaa dhidi ya watu wenye ualibino ambao wamekuwa wakiitwa majina mabaya.
Mmoja wa akina mama mwenye mtoto aliye na ualibino akiwa kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Tazama Video hapa chini

Shibuda apigia chapuo upigaji kura Serikali za Mitaa

$
0
0
Na Ripota Wetu, Dodoma

MWENYEKITI wa Baraza la Vyama Vya Siasa nchini, John Shibuda, amewataka Watanzania wajitokeze kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika kesho.

Pamoja na hali hiyo amesema kuwa ni wajibu wa kila mtanzania kuchaguzi kiongozi anayemtaka kwani hatua hiyo itasaidia kujenga misingi ya utawala bora katika upatikaji wa viongozi hao.

Hayo aliyasema jana kupitia taarifa ailiyoitoa kwa vyombo vya habari ambapo aliwataka watanzania kujitokeza na kwenda kupiga kura kuchaga viongozi hao pamoja na wajumbe wao.

“Natoa wito kwa umma wote mjitokeze na kwenda kupiga kura. Wito unazingatia kwamba kamati ya uongozi ya Baraza la vyama vya siasa Tayari imechukua hatua ya kusimamia kutendeka kwa hatua za kutakatisha hitilafu zote, zinazoathiri sifa za uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019.

“Kwa hiyo sasa, nashauri kila mtu mwenye sifa za kupiga kura na alikuwa amekwazika na kero za watendaji waitwao waborongaji wa kanuni za uchaguzi huu. Sasa nawashauri watu wote  muwe na ufikiri mwema wa kuunda uamuzi mpya wa kushiriki katika uchaguzi huu wa kuchagua viongozi wa serikali za mitaa. Kwa hiyo jitokezeni mkapige kura siku ya Novemba 24, 2019 (kesho),” alisema Shibuda.

Aliwataka wananchi, wanasiasa na wakereketwa wa demokrasia na siasa za ushindani wa vyama vingi kutambua kwamba kususia upigaji kura sio ubani wa sadaka ya kafara la kuondoa matendo batili ya kuundika kwa mazalia ya hila za athari za kiini macho kwa haki na usawa za mfumo wa vyama vingi.

“Ukombozi dhidi ya tabia za matendo ya watekelezaji maovu ya hulka potofu, dawa yake ni vikao vya kukosoana Tupate masahihisho ya kujenga. Stahiki katika utungwaji wa kanuni mpya za uchaguzi.

“Kwa hiyo sasa, nawashauri wananchi, viongozi wa siasa na wakereketwa wa siasa kataeni kuwa mateka wa hasira za kuwapa ushindi waborongaji na waparaganishi wa kukwaza dhamiri zenu za kushiriki katika upigaji kura,” alisema

Shibuda ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa vyama vya CCM na Chadema kwa nyakati tofauti, alisema Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya siasa  ndiyo sauti kuu, hivyo vikao hivi vitawaarifu kuhusu matokeo ya kikao cha majadiliano na wasimamizi wa uchaguzi huu wa serikali za mitaa.
MWENYEKITI wa Baraza la Vyama Vya Siasa nchini, John Shibuda, 

Wahitimu wa VETA wasisitizwa kutumia TEHAMA kujiajiri

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mhandisi Samson Mwela amewataka wahitimu wa VETA kuitumia vyema taaluma ya Tehama kujiajiri.

Akizungumza katika Mahafali ya Chuo cha VETA Kipawa leo, Mhandisi Mwela amesema kuwa Serikali imewekeza sana katika miundombinu ya Tehama ambapo asilimia 94 ya maeneo yanayokaliwa na watu yamefikiwa na miundombinu ya mawasiliano.

Amesema kuwa vijana waliohitimu katika Chuo hicho ambacho kinaendesha kozi ya Tehama wana fursa za kujiajiri kutokana na Mazingira wezeshi ya Serikali katika miundombinu.

Amewataka vijana kuchangamkia fursa hizo hasa kwa kuzingatia kuwa fursa kwenye sekta hiyo hazihitaji mtaji mkubwa kuweza kujiajiri na kuwasisitiza kuwa waadilifu katika kazi zao ili kuepuka Uhalifu kwa kutumia Tehama.

Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa Dickson Mkasanga amesema kuwa Chuo hicho kinaendelea kufanya tafiti na bunifu mbalimbali zinazolenga kutatua changamoto zinazoikabili jamii pamoja na kuchangia katika uchumi wa viwanda.

Jumla ya vijana 122 wamehitimu mafunzo chuoni hapo katika fani za Tehama, Elektroniki na Kompyuta kwa ngazi za Ufundi Stadi Daraja la pili, Daraja la Tatu, Diploma pamoja na kozi za muda mfupi 

 Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mhandisi Samson Mwela akizungumza na wahitimu pamoja na wageni waalikwa kwenye Mahafali ya nane ya Chuo cha tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya vijana 122 wamehitimu mafunzo chuoni hapo katika fani za Tehama, Elektroniki na Kompyuta kwa ngazi za Ufundi Stadi Daraja la pili, Daraja la Tatu, Diploma pamoja na kozi za muda mfupi. 
 Mkuu wa Chuo Cha VETA Kipawa Dickson Mkasanga akizungumza na wahitimu pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye Mahafali ya nane ya Chuo cha tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mafunzo VETA Kanda ya Dar es Salaam  Florence Kapinga aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam akitoa salamu za mkurugenzi kwa wageni waalikwa na wahitimu waliofika kwenye Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Tanzania, Fortunatus Muslim akizungumza kwenye kwenye Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 
 Mhitimu wa  Level 2 Electronic Chuo cha Tehama VETA Kipawa Anzamen Frank akisoma risala kwa mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mhandisi Samson Mwela wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 

  Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mhandisi Samson Mwela  akiwakabidhi vyeti vya kuhitimu baadhi ya wahitimu katika fani za Tehama, Elektroniki na Kompyuta kwa ngazi za Ufundi Stadi Daraja la pili, Daraja la Tatu, Diploma pamoja na kozi za muda mfupi wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 
 Mwakilishi  wa waajili  kutoka BSS Ibsulators Company Limited, Joseph Nsoza akizungumzia namna wanavyowapokea waajiliwa wapya katika kampuni hiyo pamoja na changamoto wanazipata kwa wafanyakazi wapya wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 
 Mwakilishi wa wazazi wa wahitimu, Eliasi Yunusu akitoa neno kwa wahitimu wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 
 Picha za pamoja
Baadhi ya wahitimu wakiwa kwenye maandamano ya kitaaluma wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. 
Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mhandisi Samson Mwela  akiwa kwenye maandamano ya kitaaluma wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Chuo Cha VETA Kipawa Dickson Mkasanga .

DAWASA WATOA ELIMU KWA WATEJA WA MKOA WA KIHUDUMA KISARAWE

$
0
0
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wametembelea na kutoa elimu  kwa wateja wapya wa Mkoa wa Kihuduma Kisarawe.

Mradi wa maji wa Kisarawe umekamilika mwanzoni mwa mwezi huu na tayari wateja wameshaunganishiwa huduma ya maji safi.

Meneja wa Dawasa mkoa wa kihuduma Kisarawe Erasto Mbwambo ameambatana na Meneja mawasiliano Everlasting Lyaro na Meneja huduma kwa wateja Doreen Kiwango kuwatembelea na kutoa elimu ya maji kwa wateja wa mji wa kisarawe waliokwisha unganishiwa huduma ya Majisafi baada ya kukamilika kwa mradi wa Maji wa Kibamba-Kisarawe

 Akizungumzia ziara hiyo, Meneja huduma kwa wateja Doreen Kiwango amesema lengo la kuwatembelea wateja wapya ni kuwatambua, kutoa elimu ya mambo mbalimbali yahusuyo huduma ya maji ikiwa ni pamoja na bili za kila mwezi, jinsi ya kulipa, namna wanaweza kutoa taarifa pindi wanahitaji msaada wa Dawasa na mambo mengi yanayofanana na hayo

"Hawa wateja ni wapya na kama Mamlaka tumeona umuhimu wa kuja kuongea nao, kujua namna walivyopokea huduma ya Maji na changamoto za awali wanazokutana nao kwenye ugeni huu wa maji mabombani" amesema kiwango

Kwa upande wake Meneja wa Dawasa Kisarawe, Erasto Mbwambo amesema mpaka sasa zaidi ya wateja 300 wameshafungiwa huduma huku nguvu kubwa ikielekezwa kwa wateja wakubwa na taasisi za serikali kama vile Hospitali, shule za sekondari na msingi, mahakama na sehemu nyingine ambazo huduma ya maji ni muhimu sana.

"Tunaenda vizuri, maombi ya wateja ni mengi sana na kiwango tulichonacho kuwafungia maji ni kikubwa pia.  Mpaka sasa tumejitahidi kufunga Maji kwanza kwenye makazi ya mkuu  wa wilaya na watendaji wengine wa ngazi za wilaya.  Hivyo tunaendelea na wananchi wa kawaida na taasisi za umma na binafsi zilizoleta maombi ya huduma, "amesema Mbwambo

Nae meneja mawasiliano wa Dawasa, Everlasting Lyaro alimalizia kwa kuwataka wananchi waliopata huduma ya Maji kuwa wazalendo na mabalozi wazuri wa mradi huu kwa kulinda na kutunza miundombinu ya maji ili iwafae jamii yote kwa miaka mingi zaidi.

"Mradi huu umetekelezwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano kupitia Dawasa hivyo ni hela ya watanzania, tungependa sisi kama Mamlaka kuona mradi huu unatunzwa ili hata watoto wadogo wanakuja kuuona na kufurahi. Yoyote atakayekuwa chanzo cha uharibifu wa mradi huu tafadhali mtoe taarifa kwenye vyombo vya dola na DAWASA yenyewe "amesema Lyaro

Mradi wa Kisarawe  ulianza kutekelezwa mwezi Julai 2018, ukigharimu bilion 10.6 za kitanzania zikiwa ni fedha za ndani za DAWASA, mradi huo umehusisha ujenzi wa tanki la maji la Lita Milioni 6 na utahudumia wakazi wa Kisarawe na Vitongoji vyake pamoja na maeneo ya viwanda na hilo likiwa ni agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa anazindua mtambo wa Ruvu Juu.
Meneja huduma kwa wateja Doreen Kiwango DAWADA Doreen Kiwango( kulia)  akiwa na Meneja mawasiliano Everlasting Lyaro wakikagua mita ya maji sambamba na bomba la maji alilofungiwa mteja Mpya kwenye mradi wa maji Kisarawe.
Meneja wa Mawasiliano wa Dawasa Everlasting Lyaro akikabidhi kipeperushi kwa mteja aliyeunganishiwa maji akiwa ameambatana na Meneja wa Dawasa mkoa wa kihuduma Kisarawe Erasto Mbwambo (kulia) na Meneja huduma kwa wateja Doreen Kiwango baada ya  kuwatembelea na kutoa elimu ya maji kwa wateja wa mji wa kisarawe waliokwisha unganishiwa huduma ya Majisafi baada ya kukamilika kwa mradi wa Maji wa Kibamba-Kisarawe
Meneja wa Dawasa mkoa wa kihuduma Kisarawe Erasto Mbwambo (katikati) akiwa na Meneja mawasiliano Everlasting Lyaro (kulia) na Meneja huduma kwa wateja Doreen Kiwango baada ya  kuwatembelea na kutoa elimu ya maji kwa wateja wa mji wa kisarawe waliokwisha unganishiwa huduma ya Majisafi baada ya kukamilika kwa mradi wa Maji wa Kibamba-Kisarawe

MKURUGENZI MAZINGIRA NA AFYA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU JELA AU KULIPA FAINI SH.MILIONI SABA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Globu ya jamii 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Naibu Mkurugenzi Mazingira na Afya kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Elias Chinàmo kulipa faini ya Sh. milioni 7 au kutumikia kifungo cha miaka 3 gerezani baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka 14 ya kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Pia Hakimu Mkazi , Augustina Mmbando aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, amemuamuru mshtakiwa huyo kulipà jumla ya sh milioni 18 ambazo anadaiwa kuchukua wakati wa utendaji wa makosa hayo.

Katika kesi hiyo, Chinamo alikuwa akikabiliwa na jumla ya mashtaka 28,14 ya kujihusisha na vitendo vya rushwa na 14 ya wizi àkiwa mtumishi.

Alitiwa hatiani katika mashtaka 14 ya kujihusisha na vitendo vya rushwa ambapo mahakama ilimuhukumu kulipa fàini ya sh.500,000 kila kosa au kwenda jela miaka 3 kilakosa.Upande wa mashtaka uliokuwa ukiwakilishwa na wakili wa serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupàmbana na Rushwa Leonard Swai ,ulikuwa na jumla ya mashahidi wanane na vielelezo sita.

Hata hivyo, mshtàkiwa huyo amefànikiwa kulipà faini ya sh milioni 7 huku sh milioni 18 àmeamuliwa kuzilipa ndani ya mwaka mmoja.

Katika kesi hiyo ilidaiwa kuwa, katika nyakati tofauti kati ya mwaka 20011 na 2012 jijini Dar es Salaam,katika benki ya CRDB tawi la Holland na NBC tawi la Kichwele alijipatia jumla ya Sh milioni 18 kwa manufaa yake binafsi kupitia akanti zake zilizo katika matawi ya benki hizo.

Ilidaiwa alijipatia fedha hizo kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Anyitike Kitalima, Joseph Bilago, Emanuela Safari ,Fadhili Kinemile ,Suzana Mchala kiwango ambacho kama manufaa kwake ili aweze kuwapa nafasi nyingine ya kuratibu semina na warsha mbalimbali jambo ambalo lilikuwa chini ya mamlaka ya mwajiri wake.

PROF. KABUDI AKUTANA NA BALOZI WA CANADA JIJINI DODOMA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O’Donnell ofisini kwake jijini Dodoma

Prof. Kabudi na Mgeni wake wamezungumzia namna ya kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Canada kwa manufaa ya nchi zao.

Prof. Kabudi amempongeza Mhe. Balozi kwa Canada kuendelea kuwa rafiki mzuri wa Tanzania na kumtaka kuendeleza urafiki huo.

Amesema kazi kubwa na nzuri ya kupambana na rushwa na ubadhirifu wa fedha na mali za umma inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inalenga kuwapatia maisha bora watanzania na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa Kati na wa viwanda.

Naye Balozi O’Donell amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Tanzania ya kuimarisha ukuaji wa Uchumi, utoaji wa huduma bora za afya, elimu ya msingi bure kwa watoto wa kitanzania na uboreshaji wa miundimbinu kwa maendeleo ya Tanzania.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa na Balozi wa Canada nchini Mhe.Pamela O'Donnell walipokutana kwa mazungumzo Ofisi za Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma. 


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na Balozi wa Canada nchini Mhe.Pamela O'Donnell alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dodoma
Balozi wa Canada nchini Mhe.Pamela O'Donnell akizungumza alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi  patika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Viewing all 110150 articles
Browse latest View live




Latest Images