Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Teknolojia na ubunifu wa kampuni za simu unakuza biashara nchini

$
0
0
Ni jambo lililo wazi kuwa, teknolojia ni msingi wa maendeleo ya biashara nyingi. Kuanzia kwenye mifumo ya kupokea malipo, kulipa wafanyakazi, kuhifadhi taarifa muhimu hadi kutafanya utafiti wa masoko; kote huko teknolojia inahakikisha mambo yanakwenda sawia. Kwa maana hiyo, ili kuhakikisha biashara zinakwenda vyema katika zama hizi, teknolojia ni lazima iwe jambo la msingi. 

Kampuni nyingi hapa nchini hasa zile ndogo na za kati zinategemea huduma ya teknolojia toka kampuni za mawasiliano ya simu. Kampuni ya Tigo Tanzania ni moja ya kampuni za simu ambazo zinazipa kipaumbele biashara ndogo na za kati kuziwezesha kukua kupitia huduma za kiteknolojia. 

Tigo inatoa huduma kama Bulk SMS kwa kampuni mbalimbali kuziwezesha kuwasiliana na wateja wao kwa bei rahisi, huku pia ikitoa huduma bora ya mtandao wa intaneti kusaidia ukuaji wa biashara hizo. 

Hivi sasa Tigo imeanzisha huduma Customer Service Portal ambayo inasaidia kampuni na mashirika mbalimbali kukua katika ulimwengu huu wa teknolojia. Huduma hii inawezesha watumiaji kuona mwenendo wa biashara yao kila wakati kama malipo, matumizi na mapato na kuwawezesha kujua walipo na wanapoelekea muda wowote wanapotaka kufanya hivyo. 

Mbali na huduma hii, Tigo pia ndiyo kampuni pekee inayomiliki na kuendesha kituo cha kuhifadhi takwimu (data centre) chenye hadhi ya juu ya Tier II nchini. Katika zama hizi ambazo takwimu na taarifa ni jambo la muhimu sana,Tigo inahakikisha kuwa inawapa watumiaji wake uwezo wa kuhifadhi taarifa zao kwa ubora wa hali ya juu kabisa. 

Tunaweza kusema bila kupepesa macho kuwa kwa huduma kama hizi na nyingine lukuki, Tigo inaongoza njia katika teknolojia na ubunifu kusaidia kukua kwa biashara ndogo na za kati. 

Hii ni habari njema kwa wateja wa Tigo ambao kila mara wamekuwa wakinufaika na huduma bora za kampuni hii. 

Tigo inakusudia kuhakikisha kuwa huduma hizi zinapatikana kwa kila Mtanzania, kila kona ya nchi. 


Kama ilivyoripotiwa, Tigo sasa imejiunga na Zantel. Hatua hii inazifanya kampuni hizo mbili kuunganisha huduma zake Tanzania bara na visiwani. Habari njema sana hii kwa wateja kwani punde si punde wateja wa kampuni zote mbili wataanza kufurahia huduma na faida zote zipatikanazo katika kampuni hizo mbili.

UTAMBULISHO

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt . Pindi Chana akiwasilisha hati za utambulisho ofisi za Umoja wa Mataifa Nairobi, Kenya kuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi (UN Habitat) na Mazingira (UNEP).Kushoto ni Maimunah Mohd Sharing,Mkurugenzi Mtendaji, UN-Habitat.

KATORO ISLAMIC WATUMIA MAHAFALI YA 14 KUWAOMBEA DUA WENZAO WANAOSHIKILIWA.

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus - Michuzi TV.

Shule ya Sekondari ya Katoro Islamic Seminary wamefanya Mahafali ya 14 tangu kuanzishwa kwa Shule hiyo, huku kwikwi, simanzi na majonzi vikitawala juu ya Wenzao wanane wanaoshikiliwa Kwa tuhuma za Kifo cha  Mwanafunzi mwenzao kilichotokea Aprili Mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera.

Mahafali hayo yaliyohudhuliwa na Viongozi wa Dini na Siasa wakiwemo wazazi wa wahitimu, walezi pamoja na watu mbalimbali, yaliambatana na Dua ya kumuombea Muasisi wa Shule hiyo  Sheikh Mustapha Khalid Swidiq aliyefariki Machi Mwaka huu, huku Dua hiyo ikifuatiwa na Dua ya kuwaombea waliokuwa Wanafunzi wa kidato cha Nne pamoja na Wafanyakazi wawili wa Shule hiyo wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kifo cha mwanafunzi mwenzao.

Awali akizungumza na Michuzi TV ofisini kwake Mkuu wa Shule hiyo Sheikh Fakhrudin Mustapha ambae pia ni Miongoni mwa walioshikiliwa awali kwa tuhuma hizo, na kisha kuondolewa katika tuhuma hizo amesema kuwa, Yale yaliyosambazwa na Vyombo vya Habari kuhusu Tukio hilo siyo ya kweli na zaidi Kuna baadhi ya waandishi wamepandikizwa kwa nia ovu ya kutaka kuichafua Shule, na kusisitiza kuwa mwanafunzi yule marehemu Mudi Muswadiku alikuwa na majeraha kichwani ambayo aliyapata miezi mitatu kabla ya kifo chake baada ya kugombana na Mwenzake (jina limehifadhiwa)majeraha yaliyopelekea kufanyiwa upasuaji wa kichwa kwenye hospitali ya Bugando na tatizo hilo kama Mkuu wa shule ndo alilolidhania kuchangia kifo chake.

Mkuu wa Shule Katoro Islamic ameongeza kuwa Kufuatia ugomvi huo pamoja na mambo mengine Shule ilishiriki kiasi kikubwa kumuhudumia Marehemu ikiwa ni pamoja na kuishirikisha familia katika suala la matibabu, hadi mauti yanamfika Shule ilihusika kumpeleka Hospitali na hatimae umauti ukamkuta. Katika hali ya kushangaza miezi minne baada ya Kifo cha Marehemu Mudi, alijitokeza MTU (jina limehifadhiwa)  akilalamika na kutaka kukamatwa kwa Wafanyakazi na Wanafunzi ili uchunguzi ufanyike juu ya kifo hicho.

Tayari vyombo vya Dola vinaendelea na uchunguzi zaidi wa Tukio hilo, kwa kuendelea kuwashikilia wafanyakazi wawili na Wanafunzi sita Wa Kidato cha Nne ambao wamelazimika kufanya mtihani wao wa kuhitimu wakiwa jela.

Licha ya suala hilo pia kuibuka katika Risala ya Shule iliyosomwa na Mkuu wa Shule hiyo kwa Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Ndg. Murshidi Ngeze aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya Bukoba, kutokana na jamii kupokea taarifa  ya tukio kwa maelezo tata, Mkuu wa shule alisisiza na kuwashauri jamaa wa vijana wanaoshikiliwa kuwa na subira na kuwa kesi hiyo mahakamani na hawezi kuizungumzia kwa mapana na kuwa ana imani vyombo vya dola vitawatendea haki vijana wao.

Mhe. Ngeze alishauri kwakuwa kesi hiyo iko mahakamani ni vizuri kuwa na subira na kutolizungumzia sana kwani ana imani mamlaka husika zitalichunguza na kuhakikisha haki inatendeka mapema na kuishauri bodi ya shule izione mamlaka husika kwa malengo mazima ya uharaka wakujua hatima ya vijana wao.
 Pichani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Murshidi Ngeze akikabidhi cheti kwa mmoja kati ya wahitimu wa kidato NNE 2019 Katoro Islamic seminary, katika mahafali yaliyofanyika katikati ya wiki hii.

 Pichani Mkuu wa Shule Katoro Islamic Seminary Sheikh Fahrudin Mustapha akitoa salaam zake Kwa wageni, wazazi, walezi na wanafunzi wakati wa mahafali ya 14 ya kidato cha Nne Shuleni Katoro.
 Pichani baadhi ya Wahitimu wasichana wakionesha nyuso za furaha wakati Wa mahafali yao ya Kidato cha nne Shule ya Sekondari Katoro Islamic yaliyofanyika katika ukumbi Wa shule
 Pichani baadhi ya Wahitimu wavulana Shule ya Sekondari Katoro Islamic wakiwa katika katika mahafali yao yaliyofanyika katika ukumbi Wa shule.
 Pichani anaonekana Ustadh Nuru mshereheshaji wa mahafali akitoa utaratibu wa zawadi na vyeti
 Baadhi ya akina Mama wazazi Wa wahitimu wakiendelea kufuatailia matukio ukumbini wakati wa mahafali ya kidato cha NNE Katoro Islamic
Pichani Mhe. Murshid Ngeze akitoa hotuba yake kwa niaba ya Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, katika mahafali ya kidato cha Nne 2019 Shuleni Katoro

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 22,2019

BENKI YA KCB TANZANIA YANDAA SEMINA ‘BIASHARA CLUB’ KWA WAFANYA BIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME)

$
0
0
KCB Bank Tanzania imeendesha Kongamano la Biashara Club kwa mara ya pili jijini Mwanza ikiwa ni ni sehemu ya mikakati yao ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria za kodi kwa wafanyabiashara wadogo na wakati zaidi ya 200 wamepatiwa mafunzo hayo pamoja na kuwakutanisha na wafanyabisha wa ndani na nje ya nchi.
Kwa mujibu wa benki hiyo ni kwamba tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2017, KCB Biashara Club imeendelea kuonesha dhamira yake ya kukuza biashara katika seckta ya SME kwa kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati yaani (SME) pamoja na kuwaonesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli zao za kibiashara. Semina hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza ilikusanya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja mbali na kwa pamoja walipata kufahamu fursa zinazotolewa na benki hiyo kwa wanachama wa Biashara Club.
 Akizungumza katika warsha hiyo iliyofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Idara ya Masoko, Mahusiano na Mawasiliano Christine Manyeye amesema: ”Dhumuni kubwa la Biashara Club ni Pamoja na kuwajengea wachama wake mahusiano bora ya kibiashara na wajasiriamali wenzao.”
Kwa upande wake Meneja wa Tawi, KCB Bank Mwanza, Emmanuel Mzava amewashukuru wafanyabiashara na wajisiriamali kwa kujitokeza kwa wingi kuja kupata mbinu muhimu zitakazowasaidia katika kukabiliana na changamoto za kibiashara. “Mtegemee semina kama hizi kwa siku za mbeleni kwani Mwanza ni jiji linaloonyesha kushamiri kibiashara” aliongezea Nd. Mzava.
Wakati  Saada Sipemba kutoka Sadio Travel and Tourism ambaye ni mtaalamu wa safari za kibiashara amesema fursa za kibiashara walizozipata wafanyabiashara 10 ambao walisafiri kwenda nchini China hivi karubuni. Amebainisha kuwa bila juhudi za benki ya KCB kuhakikisha inawatengenezea wateja wake mianya ya kutumia fursa hizo kwa urahisi, safari ya China isingekuwa ya mafanikio.
Benki ya KCB Tanzania kupitia Biashara Club imekuwa ikiandalia wadau wake safari za kibiashara kwenda nchi kama China, Malaysia na Afrika Kusini kwa gharama nafuu kwa dhumuni la kuwafungulia masoko mapya na bidhaa nafuu za kuleta kwenye soko la Tanzania.
 Mmoja wa Wateja na Mwanachama wa KCB Biashara Club Jonex Kinyonyi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Texas Hardware Limited alikiri kwamba Benki ya KCB imefanya kazi kubwa sanakatika kumsaidi kukuza biashara yake hadi kufikia kufungua kamouni ya pili inayojihusisha na maswala ya bima.
Kuhusu Benki ya KCB Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki hiyo imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia.
Kwa sasa benki hiyo ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki. Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini.

Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba, Buguruni, Oysterbay, Mbagala jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro. Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300,inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi.

Timu ya Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Fuwai Hospital-China kuwasili nchini Novemba 28-30,2019.

$
0
0
Timu ya Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Fuwai Hospital  wa nchini China wanatarajiwa kuwasili nchini Tanzania Novemba 28-30,2019. 

Timu hiyo ya Madaktari Bingwa itaungana na Madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kufanya upasuaji kwa wagonjwa, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Ushirikiano uliosainiwa wakati wa ziara ya Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu nchini China iliyofanyika mwezi Agosti 2019. 

Hospitali ya Moyo ya Fuwai inaongoza ulimwenguni katika taasisi za matibabu ya Moyo ikiwa na vitanda 1200. Kupitia ushirikiano wa hospitali hiyo na JKCI- wataalam mabingwa wa Moyo kutoka JKCI wameanza kupata mafunzo katika hospitali ya FUWAI yanayojumuisha mafunzo ya teknolojia iliyovumbuliwa na Daktari Bingwa Prof PAN ijulikanayo kama (Percutaneous And Non-fluoroscopical procedure) ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za upasuaji wa moyo. Habari Picha kwa hisani ya Mdau Phelisters Wegesa-Beijing China.



TCRA yahimiza Wananchi kusajili laini za simu kwa alama za vidole mkoani Morogoro

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imesema kuwa kila kila mwananchi ajisajili laini yake ya simu  kwa alama za vidole kwani muda uliopangwa unatarajia kuisha hivyo wasiposajili laini zao kwa alama hizo laini itafungwa.

Hayo ameyasema Mwanasheria Mwandamizi wa masuala ya Mawasiliano Vaolet Eseko wakati usajili wa laini za simu kwa alama za vidole  katika Kata ya Mkundi mkoani Morogoro. amesema kuwa kwa sasa wananchi wakamilishe kupata vitambulisho vya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa au kuwa na namba za vitambulisho na kuweza kukidhi matakwa ya kisheria ya kusajili laini kwa alama za vidole.

Mwanasheria huyo amesema kuwa wale ambao walikamilisha awali usajili vitambulisho vya Taifa kufika sehemu yeyote ambako zoezi linaendelea na kwenda kuangalia namba ya utambulisho kwa wale Morogoro na akipata hiyo anasajili laini ya simu kwa alama za vidole.

Amesema kuwa Wananchi ambao hawajapata kufuata taratibu za usajili kwani Ofisi za NIDA kwa kila wilaya za Mkoa Morogoro wanasajili Wananchi.

Aidha amesema kwa  kipindi kilichopo kwa sasa watumie fursa ya kutafuta vitu vya Msingi katika kusajili kwani wasiofanya hivyo laini zao zitafungwa Desemba 31.

Nae wa Mwananchi wa Kata ya Mkundi Angelina Bwakila amesema kuwa kutoa elimu hiyo kumsaidia kupata namba na kuweza kusajili laini za simu.
Amesema Wananchi wafike katika vituo sahihi na kupata taarifa sahihi na sio kuchukua taarifa sehemu zisizohusika.
 Mwanasheria Mwandamizi wa masuala ya Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki  Vaolet Eseko akizungumza na Wananchi wa Kata ya Mkundi wakati usajili wa laini za simu kwa alama za vidole mkoani Morogoro.
 Wananchi wakiwa katika foleni kuangalia majina yao katika mfumo wa NIDA ili kupata namba na kuwa wamekidhi vigezo vya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
 Wananchi wakipata huduma ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika moja Kampuni ya simu za Mkononi
Mwanasheria Mwandamizi wa masuala ya Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Vaolet Eseko akitoa maelezo kwa mwananchi kuhusiana na taratibu za kupata kitambulisho Cha Taifa na kuweza kukidhi matakwa ya kisheria ya usajili kwa laini ya simu kwa alama za vidole.

SHIRIKA LA WOWAP LATOA WITO KWA JAMII KUUNGANA KUTOKOMEZA UKEKETAJI KWA MTOTO WA KIKE SINGIDA.

$
0
0
Mratibu Miradi wa Shirika lisilo la kiserikali la Wanawake Amkeni 'Women Wake Up' (WOWAP),Nasra Suleiman, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mangda kwenye mkutano wa hadhara kuhusu mila potofu na madhara ya ukeketaji kwa mtoto wa kike uliofanyika jana Kata ya Msange Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC.
Mzee Kinusa Muna akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri hiyo, Felix Maigo, akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida, Shukrani Mbago. akihamasisha jamii kuondokana na dhana ya ukeketaji kwenye mkutano huo.
Wanakwaya wa kikundi cha sanaa cha wanawake wa Kijiji cha Mangda wakitoa burudani.
Klabu ya Haki za Binadamu inayoundwa na kundi la wanafunzi wa Shule ya Sekondari Madasenga, wakiimba shairi maalumu lenye ujumbe wa kutokomeza ukeketaji kwenye mkutano huo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondary Madasenga wakiimba kwenye mkutano huo.
Wananchi wa Kijiji cha Mangda wakiwa kwenye mkutano huo.
Mtendaji wa Kata ya Msange, Samwel Nhango, akizungumza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la WOWAP wakifurahia moja ya igizo lenye ujumbe maalumu wa kupinga ukeketaji kwa mtoto wa kike.

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Wanawake Amkeni 'Women Wake Up' (WOWAP), limetoa wito kwa watanzania kuungana pamoja katika kukabiliana na vitendo vyote vya ukatili kwa mtoto wa kike, hususan masuala ya ukeketaji ambayo bado hufanyika kwa siri sana kwa baadhi ya maeneo, huku mtindo unaotumiwa kwa sasa ukigeukia zaidi watoto wachanga hali inayohatarisha mustakabali mzima wa ukuaji wa mtoto kiafya, kimwili na kiakili

Akizungumza mbele ya wakazi wa Kijiji cha Mangda, Kata ya Msange, Singida DC, mkoani hapa, kwenye mkutano wa hadhara ulioambatana na burudani za kwaya, mashairi na maigizo yenye ujumbe wa 'KATAA NA TOKOMEZA UKEKETAJI KWA MTOTO WA KIKE,' Mratibu Miradi kutoka WOWAP, Nasra Suleiman, alisema ukatili huo wa kutisha unachangiwa zaidi na mambo ya kiimani anayoaminishwa mtu, sambamba na mila na desturi potofu zilizopitwa na wakati 

"Nichukue nafasi hii kuwasihi sana viongozi wa dini, viongozi wa kimila, wazazi, Jeshi la Polisi na jamii kwa ujumla tushikamane ili kwa pamoja tuweze kutokomeza vitendo vya ukeketaji kwa watoto wetu hawa wa kike," alisema Suleiman.

Alisema kinachosikitisha zaidi ukatili huo kwa sasa unaelekezwa zaidi kwa watoto wachanga na hufanyika kwa siri sana kwa wahusika kuogopa mkondo wa sheria, hali inayopelekea ugumu wa kubaini vitendo hivyo mpaka labda pale madhara makubwa au hali ya ugonjwa inapojitokeza

Alibainisha kwamba pamoja na mambo mengine, madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike huweza kusababisha vifo kutokana na mwathirika wa tukio hilo kutokwa na damu nyingi, maambukizo ya magonjwa na hasa UKIMWI kutokana na vifaa vinavyotumika kwa ukeketaji kutokuwa safi na salama, maumivu makali wakati wa kujamiiana na kujifungua, na madhara ya kimwili na kisaikolojia

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Singida, Shukrani Mbago, alisema azma iliyopo kama mkoa ni kuhakikisha wanatokomeza kabisa vitendo vya ukeketaji ndani ya maeneo yote ya mkoa huo na wahusika watakaobainika kufanya vitendo hivyo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria

Mbago alisema haikubaliki hata kidogo kuona vitendo hivyo vikiendelea, huku akiwasihi wanasingida wote kushikamana na kuwa mabalozi wazuri wa kampeni hiyo- kwa kila mmoja kutamka neno 'acha' ili kwa pamoja kuweza kumaliza kabisa ukatili huo mkubwa anaofanyiwa mtoto wa kike

Alisema serikali mkoani hapa kwa kushirikiana na WOWAP wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu dhidi ya mila na desturi potofu zinazochochea vitendo hivyo vya ukeketaji... na kuwasihi wadau wengine kuunganisha nguvu katika kuhamasisha na kutoa elimu stahiki ambavyo vitaleta mageuzi chanya kwenye kampeni hiyo, na hasa kwenye eneo la kuwawezesha ndugu wa karibu na jamii kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufichua taarifa zenye viashiria vyovyote vya matendo ya ukeketaji kwa mtoto wa kike

Mbago alisema kwa mujibu wa takwimu za kitafiti, mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa mitano kitaifa ambayo masuala hayo ya ukeketaji yameonyesha kushamiri. Takwimu zinaonyesha asilimia 31 ya wanawake wa mkoa huo wamekumbwa na kadhia hiyo ya kufanyiwa ukeketaji, jambo ambalo alisisitiza sio la kujivunia hata kidogo, na kwamba jamii inapaswa kukataa hali hiyo na kubadilika.

Katika mkutano huo Klabu ya Haki za Binadamu inayoundwa na kundi la wanafunzi wa Shule ya Sekondari Madasenga, na kikundi cha sanaa cha wanawake cha Mangda ni miongoni mwa washiriki waliochagiza kampeni hiyo na kuibua hamasa ya aina yake na kupelekea wengi miongoni mwa waliohudhuria kampeni hiyo kuazimia kuwa mabalozi waaminifu dhidi ya mila kandamizi na matendo ya ukatili ikiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike.

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WAAPISHWA RASMI

$
0
0
Na Woinde Shizza globu ya jamii,Arusha 

Jumla ya wasimamizi 30 wa Vituo vya kupiga kura wameapishwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha mapema jana Novemba 21, 2019 na Hakimu Mkazi  Itikija Theoflo Nguvava .
Akizungumza na wasimamizi hao baada ya kuapishwa Msena Bina ambae ni msimamizi wa uchanguzi Wilaya ya Arusha amesema ni muhimu wasimamizi kuzingatia  kiapo hicho cha utii, uadilifu na uaminifu kwani  ndicho kitakacho waongoza katika kuwasimamia wapigakura ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wapiga kura ni Raia wa Tanzania, asiye na umri chini ya miaka 18, Mkazi wa Mtaa husika, aliye jiandikisha katika daftari la wapiga kura na awe anaakili timamu.
Hata hivyo Msena amesema mpiga kura awe na kitambulisho chochote kitakacho mtambulisha chenye picha yake mfano kitambulisho cha Utaifa, cha mpiga kura, Bima ya afya, Leseni ya udereva  na Pasi ya kusafiria .
Pamoja na hayo wasimamizi  wamehimizwa kuzingati muda wa kufungua na kufunga vituo ambapo ni saa 2:00 Asubuhi mpaka saa 10:00 Jioni na kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu, wazee, wamama wajawazito na wanaonyonyesha.
“Tume waamini ndio maana tumewateua  hivyo mzingatie viapo vyenu  mkafanye kazi kwa uadilifu, uaminifu na utii pia katika kipindi hiki epukeni kutumia vilevi”  alisema Msena Bina.
Alitumia muda huo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wao bora watakao watakao weza kuwaongoza na kuwaletea maendeleo katika vijiji vyao ,huku akiongeza kuwa kupiga kura ni haki yao ya msingi hivyo wasikubali ipotee bila kushiriki.
Mmoja wawasimamizi hao ambaye akutaka jina lake gazetini alisema kuwa wamepokea maelekezo yote na watafanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni zote zilizowekwa.
Wasimamizi 30 wa Vituo vya kupiga kura wakiapishwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha mapema jana Novemba 21, 2019 na Hakimu Mkazi Itikija Theoflo Nguvava .

DON WILLIAMS ALIYETAMBA NA MUZIKI WA COUNTRY

$
0
0
Na: Moshy Kiyungi,Tabora.
Wale waliokuwa vijana wa miaka ya 1950 hadi na 1990, wanakumbuka burudani za muziki tulivu wa Country toka kwa wanamuziki mbalimbali duniani.
Msomaji wa makala hii nikujuze muziki wa Country kuwa ni aina ya muziki ambao ilikuwa ikifurahiwa sana nchini Marekani kwa miaka mingi iliyopita.
Muziki huo pia una wasikilizaji huko nchini Canada, Uingereza, na sehemu zingine Ulimwenguni. Umaarufu wa muziki wa Country huja na kupotea mithiri ya maji ya bahari ambayo hujaa na kupwa.
“This World is not our home, we are just passing through…” ni kati ya mistari ya wimbo wa Country.
Miongoni mwa wanamuziki maarufu wa muziki huo wa Country ni pamoja na Johnny Cash, Patsy Cline, the Judds, Dolly Parton, Glen Campbell, George Jones na Tammy Wynette, Kenny Rogers, Loretta Lynn, Randy Travis, Don Williams, Tanya Tucker, Willie Nelson, Reba Mc Entire, Garth Brooks na Toby Keith.
Makala haya yanamzungumzia mwanamuziki Don Williams, ambaye alikuwa ni miongoni mwa wanamuziki hao.
Wasifu wa mwanamuziki huyo unaeleza kuwa alizaliwa Mei 27, 1939 katika kitongoji cha Floydada, huko Texas nchini Marekani.
Williams alianza kupiga gitaa kutoka kwa mama yake akiwa kijana. Baadaye aliweza kupiga muziki katika bendi ya Rock n 'roll na Folk ambazo ni za muziki wa Country.
Alikuwa na sauti ya chini, nyororo, tamu na laini, ilipachikwa majina bandia ya "Jitu Pole" la muziki wa Country.
Juhudi zake zilipelekea kuanzisha bendi yake ya kwanza na iitwayo "The Strangers Two".
Mwaka wa 1964 alimwajiri Susan Taylor ambapo walianzisha bendi ya Pozo-Seco Singers.
Bendi hiyo iliingia mkataba na kampuni ya Columbia Records, akaweza kuachia idadi kubwa ya nyimbo takriban hamsini.
Kundi hilo lilivunjika mwaka wa 1971, ambapo Williams akamua  kuimba kibinafsi.
Wimbo wake wa mwaka wa 1974, "We Should Be Together," ulichukua nafasi ya tano, na alitia saini na kampuni ya kurekodi ya ABC / Dot .
Wimbo wake wa kwanza akiwa na ABC / Dot, "I Wouldn't Want to Live If You Didn't Love Me," ulichukua nafasi ya kwanza, na ulikuwa wa kwanza wa msururu wa nyimbo zake zilizovuma za kwanza kumi kati ya mwaka wa 1974 na 1991.
Mwaka wa 1978, Don Williams alikuwa mwanaume muimbaji wa mwaka kwa mujibu wa Shirika la miziki wa Country na wimbo wake "Tulsa Time" ilikuwa wimbo wa mwaka.
Nyimbo zake zimerekodiwa na wasanii kama vile Johnny Cash, Eric Clapton, Lefty Frizzell, Josh Turner, Sonny James, Alison Krauss, Billy Dean, Charley Kiburi, Kenny Rogers, Alan Jackson, Waylon Jennings na Pete Townshend.
Mwanzoni wa mwaka wa 2006, Williams alitangaza "Matembezi yake ya buriani katika Ulimwengu" Aliimba nchini Marekani na nje ya nchi, kumalizia matembezi yake na "Buriani ya mwisho" alifanya huko Memphis, Tennessee katika kituo cha Cannon cha Waimbaji 21 Novemba 2006.
Tukio hilo la mwisho lilipokewa vizuri na kihisia kwa mashabiki waliohudhuria.
Kulingana na wafanyakazi wake, Williams sasa walitamka kuwa amestaafu na hakuna ziara tena, ingawa uwezekano wa kuwepo kwa rekodi mpya.
Don alifunga pingu za maisha na Joy Bucher Aprili 10, 1960, wakabarikiwa kupata watoto wawili, Gary na Tim.
Muziki wake pia ni maarufu kimataifa, ikiwa ni pamoja na Uingereza, Australia.
Mwanamuziki huyo aliiaga dunia Septemba 08, 2017, akiwa amefikisha umri wa miaka 78.
Mungu aipumzishe roho yake pahala pema peponi, Amina.

Mwisho
Mwandaaji wa makala haya anapatikana kwa namba
0767331200, 0736332200, 0784331200 na 0713331200.

WALIJUWA GWIJI LA TAARABU SITI BINTI SAAD?

$
0
0
Na Moshy Kiyungi,Tabora.

Histoiria ya muziki wa taarab haiwezi kukamilika iwapi hautalizungumzia jina la Siti binti Saad.

Mama huyo alibarikiwa kuwa na kipaji cha pekee cha kuimba, wakati alipokuwa akiimba, sauti yake iliweza kupaa na kusafiri kwa umbali maili nyingi.

Ilifikia kipindi cha sherehe yeyote ilishindwa kufana kama Siti binti Saadi hakuwepo jukwaani kutumbuiza.

Alikuwa Mzazibari aliyezaliwa katika kijiji cha Fumba huko Kisiwani Zanzibar mwaka 1880.

Siti mara baada ya kuzaliwa alipewa jina la 'Mtumwa'. Hiyo ilikuwa ni desturi ya kawaida kwa kuwa alizaliwa katika kipindi cha Utumwa wa Kiarabu, waliokuwa wakitala visiwa hivyo.

Siku zilivyokuwa zikiendelea, alitokea Kabaila mmoja wa Kiarabu wakati huo, akampa jina hilo la Siti.

Baba yake Bwana Saad, alikuwa ni wa kabila la Kinyamwezi kutoka mkoa wa Tabora, wakati mama yake alikuwa ni Mzigua toka mkoani Tanga.

Wazazi wote hao walizaliwa Zanzibar. Maisha ya familia yao ilikuwa ni duni sana, kwani walijishughulisha zaidi katika kilimo na ufinyanzi. Kazi hizo zote Siti aliweza kujifunza na kuzimudu vizuri mno.

Kama waswahili wasemavyo “kulala masikini, kuamka tajiri” Siti alibarikiwa kuwa na kipaji cha pekee cha uimbaji.

Kupitia kipaji hicho kilimsaidia sana tangu siku za awali za maisha yake. Alitumia uimbaji wake wakati akiuza vyungu vya mama yake alivyokuwa akimsaidia kuvitembeza mitaani huku akiimba.

Yaelezwa kwamba Siti alipokuwa akiimba, sauti yake iliweza kupaa na kusafiri kwa umbali maili nyingi. Hiyo ndio ilikuwa ishara ya watu kujua kwamba vyungu vya kina Mtumwa vinapita leo.

Alifananishwa kuwa ana mapafu yenye nguvu kama ya Simba, kutokana na awezo wa kupaza sauti yake mbali bila kuachia pumzi.

Wakati huo elimu kwa watoto wa kike haikutiliwa mkazo, Siti hakuwahi kwenda shule wala kuhudhuria mafunzo ya Koraani.

Mnamo mwaka 1911, aliona ni bora ahamie mjini Unguja akitokea kijiji cha Fumba, ili kubooresha maisha yake zaidi.

Siti mara baada ya kuingia mjini humo, ilikuwa ni neema kwani alikutana na Bwana mmoja aliyeitwa Muhsin Ali wa kundi la muziki wa taarabu la ‘Nadi Ikhwani Safaa’.

Katika kipindi hicho kundi hilo ndilo lilikuwa pekee la muziki wa taarab, lililoanzishwa na Sultani wa wakati huo Seyyid Barghash Said, aliyekuwa akipenda starehe na anasa.

‘Nadi Ikhwani Safaa’ lilikuwa ni la wanaume peke yake, wanawake hawakuruhusiwa kujiunga na vikundi vya muziki kwa vile ilikuwa ikichukuliwa kama ni uhuni.

Lakini Bwana Muhsin alikiona kipaji cha pekee cha Bi. Siti, akajitolea kumfundisha kuimba kwa kufuata mirindimo ya vyombo vya muziki, akaanza kuimba kwa lugha ya Kiarabu.

Baada ya hapo alikwenda kumtambulisha kwa wanamuziki wenzie wa ‘Nadi Ikhwani Safaa’, ambao bila kusita wakaanza kufanya naye maonesho mbalimbali katika jamii.

Kundi hilo lilipata mialiko mingi kwenda kutumbuiza hususan kutoka kwa Sultan Seyyid Barghash Said na matajiri wengine wa Kiarabu, katika harusi na sherehe zingine mbalimbali Kisiwani humo.

Siti alikuwa mithiri ya ‘moto’ wa kuotea mbali, jina lake likavuma kwa haraka sana hadi nje ya mipaka ya nchi na Bara la Afrika.

Punde Siti alianza kufananishwa na mwimbaji mahiri wa kike aliyetamba wakati huo kutoka nchi ya Misri, Umm Kulthum.

‘Moto’ wa Siti haukuwa wa kuusogelea karibu, kwani 1928 Kampuni ya kurekodi muziki ya Columbia and His Master's Voice, yenye makazi yake huko Mumbai nchini India, ilisikia umaarufu wa Siti binti Saadi.

Hivyo ikaliaki kundi la Nadi Ikhwani Safaa, akiwemo yeye kwenda kurekodi nyimbo kwa lugha adhimu ya Kiswahili, kujaribu kama muziki wake utauzika.

Kampuni hiyo haikuweza kuamini jinsi muziki ule ulivyo pata soko kwa kasi kubwa. Wastani wa santuri 900, ziliweza kuuzika katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo. Hadi kufikia mwaka 1931, santuri 72,000 zilikuwa tayari zimeuzwa.

Kutokana na kusambaa kwa santuri hizo, umaarufu wa Siti ulizidi kuongezeka mara dufu. Watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia walikuwa wakienda Zanzibar kumshuhudia.

Mambo yalizidi kuwa mazuri kwa Siti hadi ikafikia hatua Kampuni ya kurekodi ya Columbia, ikaamua kujenga studio maalum ya kurekodi muziki kwa ajili ya Siti binti Saadi hapo hapo mjini Zanzibar.

Hatua hiyo ya kujengewa studio watu wenye wivu, waliwaumizwa mno, wakaanza kumtungia nyimbo za kumkejeri, ili kumpunguzia kasi hasa walitumia kigezo kwamba hakuwa na uzuri wa sura!

Siti bint Saadi alitunga na kuimba nyimbo sana, lakini wimbo, huu ndio uliovuma sana. Msomaji mpendwa wa makala haya, nakusihi usome maneno ya kajeri na majibu yaliyomo kwenye wimbo wa nguli huyu:

Kejeri

“Siti binti Saadi kawa mtu lini,

Kaja mjini na Kaniki chini,

Kama si sauti angekula nini?

Siti bint Saadi kwa kujua hila za wabaya wake, akaona isiwe taabu akajibu mashambulizi kwa namna hii:

Majibu

“Si hoja uzuri,

Na sura jamali,

Kuwa mtukufu,

Na jadi kebeli,

Hasara ya mtu,

Kukosa akili”.

Kwa kujibu shambulio hilo kwa namna yake aliweza kuwafunga midomo wale wote waliokuwa wakimfuatafuata.

Uanaharakati

Siti alikuwa ni mwanamke wa kwanza kuwa mwanaharakati katika kipindi chake, aliweza kuwatetea wanawake na wanyonge kwa ujumla.

Kipindi hicho, watu waliokuwa matajiri walikuwa wakiwaonea masikini, walipofikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Waliweza kutoa hongo ili kuachiwa huru, halafu yule aliyeshitaki ndiye akafungwa!



Kijiti

Utunzi wake wa wimbo wa ‘Kijiti’ ulimpatia sifa kubwa kwani ulikuwa ukielezea kisa cha kweli kilichomkuta mwanamke mmoja mgeni kutoka Bara.

Mwanamke huyo alipofika Zanzibar, alikutana na tajiri mmoja ambaye alijifanya amempenda. Hivyo akamchukua na kulala naye halafu baadaye akakatisha maisha yake kwa kumuua!

Tajiri yule alishitakiwa kwa bahati nzuri walikuwepo mashahidi wawili walioshuhudia tukio lile.

Kupitis utajiri wake, alitoa hongo kesi ikawageukia wale mashahidi na wakafungwa.

Kwa Weledi aliokuwa nao Siti, akaachia kibao hiki:

“Tazameni tazameni,

Eti alofanya Kijiti,

Kumchukua mgeni,

Kumcheza foliti,

Kenda naye maguguni,

Kamrejesha maiti”.

Siti aliendelea kumwambia tajiri yule kupitia nyimbo zake kwamba asijethubutu kwenda Dar er Salaam, kwa maana watu wenye hasira wanamsubiri na wameapa kwa ajili yake.

Nguli huyo Aliendelea kufanya shughuli zake za muziki hadi uzee ulipompata.

Shaaban Robert.

Muda mfupi kabla ya kifo chake, Siti alikutana na mwandishi maarufu na mwanamashairi Shaaban Robert, ambaye alimhoji na kuweza kuandika Wasifu wake katika kitabu alichokiita ‘Wasifu wa Siti binti Saadi’

Wasifu huo unaonekana kuwa ndio bora zaidi uliowahi kuandikwa katika fasihi ya Tanzania. Kitabu hicho kinatumika kufundishia shule za sekondari za Tanzania.

Ilipotimu Julai 08, 1950 Siti binti Saadi alifariki dunia na kuacha pengo kubwa katika tasnia ya taarab.

Hata baada ya kifo chake jina lake bado linatumika sana kama kielelezo cha ushujaa wake.

Hadi leo hii Siti hutumika kama kipimo cha kufundishia uimbaji wa taarab. Anakumbukwa katika historia yake ya kuwa mwanamke wa kwanza Afrika mashariki kurekodi muziki katika santuri.


Bi. Kidude

Japo pengo hilo halikuweza kuzibika, lakini kuna watu wengine waliibuka wakawa na umaarufu wa kutunga na kuimba taarab kupitia kwake, mfano hai ni marehemu Fatuma Binti Baraka a.k.a Bi. Kidude.

Chama cha Waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA), kimetumia jina lake kulipa jina gazeti la chama chao ‘Sauti ya Siti.

Siku zinavyokwenda taarabu nayo imebadilika kwa kiasi kikubwa. Ala za muziki na mirindimo ya zamani huwezi kuzipata miaka ya hivi karibuni.

Wasanii wa miaka hii ya karibuni, wamedai kuuboresha muziki huo kwa kubadili mirindimo huku waimbaji kulishambulia jukwaa wakicheza pamoja na wanenguaji . Wameuita ‘Tara dansi’. Lakini wasanii hao wamekwenda mbali kwa kubuni mtindo wa ‘Tara Singeli’.

Swali la kujiuliuza muziki wa taarab wa siku za hivi karibuni uliojaa mipasho, utaishi?

Mungu ailaze roho yake pahala pema peponi, Amina.


Mwisho.

Mwandaaji wa makala haya anapatikana kwa namba: 0784331200, 0767331200, 0713331200 na 0736331200.

ALAT YAIPONGEZA MANISPAA YA KINONDONI KWA KUTEKELEZA MIRADI MIKUBWA KWA KUTUMIA FORCE ACCOUNT, YATAKA HALMASHAURI NYINGINE ZIIGE.

$
0
0
Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania ( ALAT) imeipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati kwakutumia Local Fundi (Force Account).

Akizungumza na watendaji wa Halmashauri hiyo mara baada ya kukamilisha ziara ya kukagua miradi ya Halmashauri hiyo, Makamu Mwenyekiti wa ALAT , Stephano Mhapa amesema kuwa Mkurugenzi Mtendaji Aron Kagurumjuli na timu yake wamefanikisha kujenga miradi mikubwa ya maendeleo kwa kutumia mafundi wa kawaida jambo ambalo limeonyesha nizamu ya matumizi mazuri ya fedha za serikali.

Amefafanua kuwa mradi wa Zahanati ya Mikoroshini iliyopo Kata ya Msasani imejengwa kwa shilingi milioni 400.8 kwa kutumia mafundi wa kawaida wakati kwa mkandarasi wakutangaza tenda ingetumia milioni 700 na kwamba Halmashauri hiyo imeokoa kiasi cha shilingi milioni 300.

Aidha Mhapa amesema kuwa“ ukiangalia Zahanati hii imekamilika vizuri na imara , tumejionea wenyewe, Mkurugenzi na timu yako tunakupongeza sana, na halmashauri nyingine ziige mfano huu kutoka kwako, kazi ni kubwa uliyoifanya lakini gharama yake ni ndogo, haya ni matumizi mazuri ya fedha za serikali.”

Akizungumzia mradi wa Soko la kisasa la Magomeni, linalojengwa kwa shilingi zaidi ya bilioni 8.9 na Kituo cha Afya kilichopo Kigogo kinachojengwa kwa shilingi milioni 700 , Mhapa amesisitiza kuwa Halmashauri ya Kinondoni inapaswa kuigwa na Halmashauri nyingine kwa kazi kubwa wanayoifanya sambamba na kuwa na matumizi mazuri ya serikali.

“ Halmashauri ya Kinondoni tangu mwaka 2015 imekuwa ikipata hati safi na hiyo ni kutokana na kuwa na nidhamu ya matumizi mazuri ya fedha za serikali, hati safi inamanisha kwamba mnapokea pesa za serikali lakini pia mnakusanya mapato ya ndani na kuyatumia vizuri” ameongeza.

Kuhusu asilimia 10 ya fedha kwa ajili ya mikopo ya vijana , wakina mama na walemavu,ambayo ni bilioni tatu, Katibu wa ALAT Elirehema Kaaya ameipongeza Halmashauri kwakufanya vizuri kwani kiasi hicho cha fedha ni sawa na bajeti nzima ya Halmashauri nyingine.

Kaaya amesisistiza kuwa kazi anayoifanya Mkurugenzi Kagurumjuli ndio inayotakiwa na Rais Dk. John Magufuli na hivyo kuagiza Halmashauri nyingine ziige mfano wake.

“ Umefanya matumizi mazuri na sahihi ya fedha ambazo ni kodi za wananchi wanyonge, kilichofanyika na Mkurugenzi mtedaji wa Kinondoni ni kwamba , Mhe. Rais Magufuli na Waziri wa Tamisemi Suleman Jafo wanasisitiza kutumia local fundi (Force Account) ninashauri wakurugenzi wengine wasikilize maagizo yanatotolewa na serikali.” Amesisitiza Kaaya.

Awali akizungumza na viongozi wa ALAT, Mkurugenzi Mtendaji Kagurumjuli amesema kuwa Halmashauri imefanikiwa kupata bilioni 32.8 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa miradi mitatu ya kimkakati ambayo itaongeza mapato kwa kiasi kikubwa.

Kagurumjuli alitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzo wa soko la kisasa la Magomeni, wenye thamani ya shilingi bilioni 8.9, ujenzi wa soko la kisasa la Tandale wenye thamani ya shilingi bilioni 8.7 na uboreshaji wa fukwe ya Osterbay (Coco Beach) wenye gharama ya shilingi bilioni 13.
Muonekano wa ndani wa soko la kisasa la Magomeni .
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Ndugu Aron Kagurumjuli, akiwa na wajumbe wa kamati ya ALAT Taifa , wakikagua Zahanati ya Mikoroshini iliyopo kata ya Msasani, katika ziara ya viongozi wa ALAT waliyokuwa wakikagua miradi ya Halmashauri hiyo jana.
Wajumbe wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania ( ALAT) wakiangalia jengo la soko la kisasa la Magomeni inalojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 8.9.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni , Ndugu Aron Kagurumjuli mwenye suti ya dakbluu, akiwaonyesha Makamu Mwenyekiti wa ALAT Stephano Mhapa mwenyeshati la madoa akiwaonyesha mazingira ya Zahanati ya Mikoroshini iliyopo Kata ya Msasani.

MRADI WA MIAKA MITANO UZALISHAJI BORA WA MAZIWA KUONGEZA SOKO LA BIDHAA WAZINDULIWA NCHINI

$
0
0
TANZANIA kwa kushirikiana na taasisi ya kimataifa ya uwezeshaji mifugo ya maziwa ya Land o'lakes imezindua mradi wa miaka mitano wa uzalishaji bora maziwa na kuongeza soko la bidhaa za maziwa nchini ifikapo mwaka 2025. 

Akizundua mradi huo jijini dar es salaam Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel amesema mradi huo unazingatia uwezeshasji kwa maafisa ugani mikoa 26 ya Tanzania bara na kwamba utaanza kutekelezwa katika mikoa minne ya Dar es salaam, Pwani, Tanga na Morogoro. Prof. Elisante Ole Gabriel amesema mradi huo utazingatia kuwezesha maafisa ugani, pembejeo na uzalishaji wenye tija hadi kufikia mahitaji ya soko la bidhaa za maziwa ndani na nje ya nchi.

Prof. Elisante Ole Gabriel amesema mradi huu ambao unaungwa mkono na ichi kadfha za wahjidsani ikiwemo marekani unalenga [pia luunga mkono juhudi za rais wa awamu ya tano mhe. Dk John Pombe Magufuli katika kuhakikisha nchi inakuwa katika uchumi wa viwanda na kujitegemea kiuchumi. Amesema kwa sasa Tanzania bado ina uzalishaji mdogo wa maziwa licha ya kuwa na idadi kubwa ya mifugo huku wafugaji na sekta ya kilimo ikiabiliwa na changamoto za ugani anautaja mradi huu kuja na ufumbuzi wa wa kuhakikisha uzalishaji maziwa unaongezeka mara dufu.

Hata hivyo prof. OLE GABRIEL anawataka watanzania kupokea mradi huu kwa mikono miliwi na kuondokana na ufugaji wa k,uchunga kuelekea ufugaji wa kibiashara na kuiwesha nchi kungezea thamani bidhaa za maziwa kwa mahitaji ya ndani na nje ya nchi

Kwa idha prof GABRIEL amesema kwa mujibu wa takwimu za mwaka huu Tanzania inao mifugo ngombe milioni 30 mbuzi milioni 20.5 kondoo million 5.5 lakini wanaotumika katika uzalishaji maziwa ni milioni mbili tuu

Kwa upande wa mratibu wa mradi huo nchini Tanzania kutoka taasis ya LAND O’LAKES bi. Neema mrema amesema mradio pia unatekelezwa katika nchi kadhaa baranmi afrika ambapo umeonyesha mafanikio makubwa kwa kuinua pato la wafugaji na nchi husika kwa ujumla.

Amesema taasisi hiyo ya kimataifa imekuwa ikitekeleza miradi hiyo kwa kuwaeeshesha maafisa ugani na pembejeo za kisasa kwa manufaa ya kuleta tija kwa ongezeko la maziwa kutoka ng”ombe mmoja kukamuliwa lita 5 hadi 15 kwa siku

NAIBU WAZIRI MGALU AKAGUA KAZI YA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI HANDENI

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria kuwashwa kwa umeme katika mtaa wa Konje shule.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akiongea na wananchi wa kijiji cha Kwedikabu baada kumaliza kukagua mgodi wa Kusini Gateaway. kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe.

Wananchi wa Kata ya Konje wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) kwenye hafla ya kuwasha umeme katika Kata hiyo

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akishuka ngazi mara baada ya kukagua moja ya majengo ya mgodi wa Kusini Gateaway.

**********************************

Na Hafsa Omar – Tanga

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Novemba 20 mwaka huu, ameendelea na ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme vijijini ili kuhakikisha kuwa lengo la Serikali kupeleka umeme katika vijiji vyote linafanikiwa.

Katika ziara hiyo, alikagua kazi husika katika Kata ya Konje, Kata ya Bwawani na mgodi wa dhahabu wa Kusini Gateway uliopo katika kijiji cha Kwedikabu, kitongoji cha Msenga, Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga na kuwasha umeme katika mtaa wa Konje Shule na mtaa wa Kwamneke.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwedikabu alisema, nia ya ziara yake kwenye mgodi ni kuhakikisha kwamba maeneo hayo ambayo yana faida nyingi kiuchumi nchini, yanapelekewa miundombinu ya umeme.

Aidha, alilitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuharakisha kupeleka umeme kwenye eneo hilo la mgodi, kwani shirika hilo litajiongezea mapato, ambayo yatasaidia kusambaza umeme kwenye maeneo mengine.

Aliongeza kuwa, wawekezaji wengi wa madini ambao bado huduma ya umeme haijawafikia katika maeneo yao, watashawishika kujiunga na huduma hiyo mara baada ya umeme kufika katika eneo hilo, na itakuwa faida kubwa kwa TANESCO, ambayo kwasasa inajiendesha yenyewe bila kutegemea ruzuku kutoka Serikalini.

“Mimi nataka niseme nimekuja kwenye eneo ambalo linaweza kuongeza mapato,na ukizingatia kuwa umeme ni huduma lakini pia ni biashara, kwa hiyo tupo kutafuta masoko na soko tumelikuta hapa.”

Naye Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe aliishukuru Serikali kwa kazi ya usambazaji wa umeme katika wilaya ya Handeni, ambapo alisema hapo awali walikuwa wanategemea umeme kutoka Hale na Korongwe lakini kwasasa, Serikali imewapelekea vituo viwili vya kupozea umeme.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo azishauri taasisi za kifedha kuwekeza katika teknolojia

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji (Tigo), Simon Karikari, akiwasilisha mada juu ya kukuza maendeleo ya sekta ya fedha kupitia mifumo ya kidigitali katika mkutano wa 19 wa taasisi za kifedha nchini unaoendelea jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye.

Mkurugenzi Mtendaji (Tigo), Simon Karikari, akiwasilisha mada juu ya kukuza maendeleo ya sekta ya fedha kupitia mifumo ya kidigitali katika mkutano wa 19 wa taasisi za kifedha nchini unaoendelea jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye.

TUNAZO FEDHA ZA KUKAMILISHA HOSPITALI YA UHURU - RAIS MAGUFULI

$
0
0
Na Englibert Kayombo, WAMJW – Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi kuwa Serikali inayo fedha za kutosha kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Uhuru. 

Rais Magufuli amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ospitali hiyo inayojengwa wilayani Chamwino, Dodoma.

“Fedha ya ujenzi wa hospitali ipo, tunayo Billioni 3.4” amesema Rais Magufuli ambaye ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa Hospitali hiyo.

Rais Magufuli amesema kuwa mwanzoni TBA ilipewa kazi ya ujenzi wa hospitali hiyo lakini hawakusimamia vizuri ujenzi kupelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo kuchukua maamuzi ya kukabidhi kazi kwa Jeshi la Kujenga Taifa ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati.

Naye Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenarali Charles Mbuge aliyepewa jukumu la kusimamia ujenzi wa Hospitali hiyo amesema kuwa Jeshi lake linauwezo wa kufanya kazi hiyo na kuikamilisha ndani ya muda uliopangwa.

“Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu, Jeshi letu lina nguvu ya kutosha na tutamaliza kwa muda kazi hii, sina mipango mingine ni kumaliza tuu” amesema Brigedia Jenerali Mbuge.

Mnamo tarehe 9 Desemba, 2018, Rais Magufuli alitoa maagizo ya fedha zilizotengwa kugharamia sherehe za uhuru kiasi cha Shilingi Milioni 995 kutumika kujenga hospitali katika Mkoa wa Dodoma. Kukamilika kwa hopitali hiyo kutatatua kero waliyokuwa wanaipata wananchi ya umbali wa kufuata huduma za afya.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa wilayani Chamwino, Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi (hawapo pichani) mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma.
 Viongozi mbalimbali wa Serikali waliojitokeza kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pichani juu akitizama ramani ya mchoro sanifu wa kengo la Hospitali ya Uhuru inayojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma.
Picha ya Mchoro sanifu wa jengo la Hospitali ya Uhuru inayojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma.
 Umati wa wananchi waliojitokeza kumlaki na kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma.
Mafundi ujenzi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino, Dodoma.

M-BET yamwaga vifaa Ruvuma Vijana Cup

$
0
0
Dar es Salaam. Kampuni ya michezo kubashiri ya M-BET Tanzania imedhamini mashindano ya soka ya Ruvuma Vijana Cup ambayo yanashirikisha timu za wilaya zote sita za Mkoa wa Ruvuma.

Msemaji wa M-BET Tanzania, David Malley alisema kuwa kampuni yao imetoa vifaa mbalimbali vya michezo ikiwa pamoja na Jezi na Mpira kwa timu mbalimbali zinazoshiriki katika mashindano hayo.

Malley alisema kuwa mbali ya jezi, soksi na mipira kwa timu , pia M-BET imedhamini vifaa vya mazoezi kama bips.

Alisema kuwa jezi hizo zitagawiwa kwa timu zitakazofuzu hatua ya 16 bora ya mashindano ambapo fainali yake itafanyika Desemba 15 kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Sokoine.

“Huu ni mwendelezo wa mchango wa kampuni yetu katika kuendeleza michezo, tulianza na KMC ambayo tumeidhamini kwa Sh 1 billioni kwa miaka mitano,” alisema Malley.

Kwa upande wake, mratibu wa mashindano hayo, Raymund Mhenga alisema kuwa mashindano hayo yalishirikisha jumla ya timu 32 ambapo sasa yapo katika hatua ya mtoani kuelekea hatua ya 16 bora.

“Tunawashukuru M-BET Tanzania kwa msaada huu ambao utahamasisha maendeleo ya soka mkoani Ruvuma ambapo mwaka jana, wachezaji 10 walisajiliwa na timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza ya Majimaji,” alisema Mhenga.

Mhenga alisema kuwa mashindano hayo yanazidi kushika kasi na mipango yao ni kuyafanya kuwa ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Alisema kuwa mipango yao ni kuziharika timu za Yanga na KMC kushuhudia mashindano hayo ili kusaka vipaji kama ilivyokuwa kwa Majimaji.
 
Msemaji wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-BET, David Malley (kulia) akimkabidhi mpira mratibu wa mashindano ya Ruvuma Vijana Cup, Raymund Mhenga baada ya kampuni hiyo kutangaza kudhamini mashindano hayo. 

RAIS DKT MAGUFULI AWEKA MAWE YA MSINGI KATIKA MIRADI YA HOSPOITALI YA UHURU, SOKO KUU, NYUMBA ZA POLISI NA STENDI KUU YA MABASI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo kuhusiana na Ujenzi wa Hospitali Kuu ya Uhuru inayojengwa maeneo ya Chamwino jijini Dodoma alikoiwekea jiwa la msingi leo. Ujenzi wa Hospitali hiyo umewezekana baada ya Rais Magufuli kuelekeza kiasi cha Shilingi Milioni 995.18 ambazo zilipangwa kutumika kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru mwaka jana zipelekwe
kwenmye ujenzi wa hospitali hiyo ya kisasa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai akifunua pazia kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali Kuu ya Uhuru inayojengwa maeneo ya Chamwino jijini Dodoma alikoiwekea jiwa la msingi leo Ujenzi wa Hospitali hiyo umewezekana baada ya Rais Magufuli kuelekeza kiasi cha Shilingi Milioni 995.18 ambazo zilipangwa kutumika kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru mwaka jana zipelekwe kwenmye ujenzi wa hospitali hiyo ya kisasa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugaio baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali Kuu ya Uhuru inayojengwa maeneo ya Chamwino jijini Dodoma alikoiwekea jiwa la
msingi leo. Ujenzi wa Hospitali hiyo umewezekana baada ya Rais Magufuli kuelekeza kiasi cha Shilingi Milioni 995.18 ambazo zilipangwa kutumika kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru mwaka jana zipelekwe kwenmye ujenzi wa hospitali hiyo ya kisasa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Ally Mwalimu  baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali Kuu ya Uhuru inayojengwa maeneo ya Chamwino jijini
Dodoma alikoiwekea jiwa la msingi leo. Ujenzi wa Hospitali hiyo umewezekana baada ya Rais Magufuli kuelekeza kiasi cha Shilingi Milioni 995.18 ambazo zilipangwa kutumika kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru mwaka jana zipelekwe kwenmye ujenzi wa hospitali hiyo ya kisasa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelekezo ya  maendeleo ya ujenzi kutoka kwa Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Charles Mbuge  baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali Kuu ya Uhuru inayojengwa maeneo ya Chamwino jijini
Dodoma alikoiwekea jiwa la msingi leo Ujenzi wa Hospitali hiyo umewezekana baada ya Rais Magufuli kuelekeza kiasi cha Shilingi Milioni 995.18 ambazo zilipangwa kutumika kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru mwaka jana zipelekwe kwenmye ujenzi wa hospitali hiyo ya
kisasa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Charles Mbuge  na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Daud Kondoro baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali Kuu ya Uhuru inayojengwa maeneo ya Chamwino jijini Dodoma alikoiwekea jiwa la msingi leo Ujenzi wa Hospitali hiyo umewezekana baada ya Rais Magufuli kuelekeza kiasi cha Shilingi Milioni 995.18 ambazo zilipangwa kutumika kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru mwaka jana zipelekwe kwenmye ujenzi wa hospitali hiyo ya kisasa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro akiwasili  eneo la Nzuguni jijini Dodoma Leo Tayari kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba za makazi ya Askari Polisi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akipata Maelezo  ya maendeleo ya Ujenzi wa Nyumba za makati ya Askari Polisi eneo la Nzuguni jijini Dodoma Leo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro akifunua pazia kuashiria uwekaji wa  jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba za makaki ya Askari Polisi eneo la Nzuguni jijin Dodoma Leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro baada ya kweka  jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba za makazi ya Askari Polisi eneo la Nzuguni jijin Dodoma Leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola baada ya kweka  jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba za makazi ya Askari Polisi eneo la Nzuguni jijin Dodoma Leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akikagua moja ya Nyumba za makazi ya askari baada ya kweka  jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba za makazi ya Askari Polisi eneo la Nzuguni jijin Dodoma Leo. Pamoja naye ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.
Kangi Lugola, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Meja Jenerali Jacob Kingu na IGP Simon Sirro.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kweka  jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba za makazi ya Askari Polisi eneo la Nzuguni jijin Dodoma lor ametoa jengo la Kwa adili ya Makao Makuu ya na kukabidhi nyaraka za jengo hilo kwa  Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola na IGP Simon Sirro.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Mhe. Godwin Kunambi akitoa Maelezo kuhusiana na maendeleo ya Ujenzi wa Soko kuu la jiji la Dodoma ambalo litaitwa Soko Kuu la (Spika wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Job
Ndugai eneo la Nzuguni
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifunua kitambaa kuweka jiwe la Msingi la  Ujenzi wa Soko kuu la jiji la Dodoma ambalo litaitwa Soko Kuu la (Spika wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai eneo la Nzuguni
 Muonekano wa  Soko Kuu la (Spika wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai eneo la Nzuguni jijini Dodoma
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiondoka baada ya kuweka jiwe la Msingi la  Ujenzi wa Soko kuu la jiji la Dodoma ambalo litaitwa Soko Kuu la (Spika wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo.PICHA NA IKULU

NAIBU WAZIRI SIMA AAGIZA BARAZA LA MAZINGIRA KUPITIA UPYA VIBALI VYA KUFANYA SHUGHULI YA UWEKEZAJI

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kushoto) akizungumza akiwa katika ziara eneo la ufukwe mjini Mtwara alipofanya ziara na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Katika ni Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC Prof. Esnat Chagu.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Esnat Chagu, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka na Meneja wa NEMC Kanda ya Kusini Jamal Baruti.
Viongozi wakiwa katika ziara katika ufukwe ambao mwekekezaji amekutwa akifanya shughuli eneo la feri mjini Mtwara.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Esnat Chagu wakimsikiliza mwekezaji Chandra Shekhar wa kiwanda cha Alpha Krust katika ufukwe mjini Mtwara walipofanya ziara eneo hilo.

…………………………………………….

Na Robert Hokororo, Mtwara

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amelielekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupitia upya vibali vya kufanya shughuli ya uwekezaji katika ufukwe wa bahari eneo la Feri mkoani Mtwara.

Sima ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake pamoja na NEMC kwenye mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara kuona namna shughuli za uhifadhi wa mazingira zinavyotekelezwa.

Akitoa maelekezo hayo kuhusu mwekezaji Chandra Shekhar wa kiwanda cha Alpha Krust alitaka NEMC ianze kupitia upya nyaraka ambazo aliombea vibali vya kufanya shughuli hizo katika eneo hilo.

Aidha, alisema baada ya kumsikiliza akidai alipewa vibali kuna haja sasa ya kumhakiki ili aweze kupewa cheti ya mazingira kama atakuwa amefuata sheria za mazingira.

Naibu waziri pia aliagiza uangaliwe upya mpango wa matumizi ya ardhi katika eneo hilo kuwa yamepangwa yatumikaje ili kama yako sahihi basi apate cheti cha kuendelea na shughuli zake.

“Watu wengu wamekuwa wakiwekeza katika maeneo ya fukwe bila utaratibu na kufanya uharibifu wa mazingira lakini sisi jukumu letu ni kulinda fukwe hizi na ambazo pia ni vyanzo vya sasa kama hatujalinda tutapoteza rasilimali hii ya bahari, hivyo nasitisha kwanza shughuli za mwekezaji huyu hadi pale NEMC watakapofanya review ya vibali vyake,” alisema.

Naibu waziri aliongeza kuwa Sheria ya Mazingira yam waka 2004 57 (2) inampa waziri dhamana ya kuamua ndani ya mita 60 pembezoni mwa bahari nini kifanyike kuendana na mazingira ya eneo hilo lakini si kila shughuli anaweza kuruhusu kufanyika.

RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI STENDI KUU YA MABASI YA MKOANI DODOMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine akivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi ujenzi wa Stendi Kuu ya Mabasi mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Dodoma akitoka kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo hicho Kikuu cha Mabasi mkoani Dodoma ambapo ujenzi wake upo mbioni kukamilika. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Stendi Kuu ya Mabasi mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Dodoma kabla ya kuwahutubia katika eneo la wa Stendi Kuu ya Mabasi mkoani Dodoma. 
Sehemu ya Stendi Kuu ya Dodoma kama inavyoonekana pichani. 

Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>