Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110017 articles
Browse latest View live

MATUKIO KATIKA PICHA MKUTANO WA SADC WA WATAALAMU WA UTATU SEKTA YA KAZI NA AJIRA

$
0
0
Mwakilishi wa sekretarieti ya SADC, Bw. Maxwell Parakokwa (kushuto) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo uliowakutanisha wataalamu wa utatu wa sekta ya kazi na ajira Novemba 20, 2019 Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe na Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu SADC, Bi. Duduzile Simelane (katikati).
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akizungumza na wataalamu wa sekta ya kazi na ajira wakati wa mkutano uliowakutanisha Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupitia na kujadili ajenda mbalimbali zinazohusu sekta hiyo.
Sehemu ya Wataalamu wa Sekta ya Kazi na Ajira kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilisha katika mkutano huo uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakisikiliza mada zilizokuwa zikiwasilisha kuhusu sekta ya Kazi na Ajira.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu SADC, Bi. Duduzile Simelane na Mwakilishi wa sekretarieti ya SADC, Bw. Maxwell Parakokwa wakati wa mkutano uliowakutanisha wataalamu wa sekta ya kazi na ajira.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wazee, Wanawake na Watoto Zanzibar Bi. Fatma Bilali wakati wa mkutano wa wataalamu wa sekta ya kazi na ajira.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Willington Chibebe akieleza jambo kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe wakati wa mkutano wa wataalamu wa sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Kazi kutoka Afrika Kusini Bw. Virgil Seafield akichangia mada wakati wa mkutano huo.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

Wataalam Usafiri wa Anga Jumuiya ya Afrika Mashariki wakutana Tanzania kujadili uboreshaji wa huduma na miundombinu kwa nchi wanachama

$
0
0
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (aliyesimama kushoto) akiwasilisha maelezo
yanayohusu majengo matatu ya abiria ya Kiwanja hicho kwa Wataalam wa
Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, leo wameanza mkutano wasiku tatu wa kujadili namna ya kuboresha huduma na miundombinu ya usafirihuo kwa nchi wanachama.
Meneja wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Mhandisi Burton Komba (mwenye koti la bluu kushoto), leo akiwaelezea mifumo mbalimbali ya jengo hilo Wataalam wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambao wanashiriki mkutano wa siku tatu wa kujadili namna bora ya kuboresha huduma na miundombinu ya usafiri huo kwa nchi wanachama.
Wataalam wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, leo
wakiwa eneo la kuwasili abiria maarufu kama “Ukuta wa Tanzania” (TanzaniaWall) la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere walipofanya ziaraya mafunzo, ambapo wapo kwenye mkutano wa siku tatu wa kujadili namna yakuboresha huduma na miundombinu ya usafiri huo kwa nchi wanachama.
Wataalam wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
ambao wapo nchini kushiriki mkutano wa siku tatu wa kujadili namna bora yakuboresha huduma na miundombinu ya usafiri huo, ambapo leo wametembeleamajengo ya mizigo yaliyopo kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha JuliusNyerere (JNIA).
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(aliyenyoosha kidole) akitoa maelezo mbalimbali kwenye ukumbi wa Watu
Mashuhuri (CIP) wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja hicho kwa Wataalam waUsafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, waliotembelea leo, ambapowapo kwenye mkutano wa siku tatu wa kujadili namna ya kuboresha huduma namiundombinu ya usafiri huo kwa nchi wanachama.

WASICHANA WATANO SINGIDA WACHAGULIWA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MBIO ZA WANAWAKE (LADIES FIRST) 2019 NGAZI YA TAIFA

$
0
0
Wasichana watano kutoka Mkoa wa Singida, waliochaguliwa kushiriki mashindano ya mbio za wanawake (Ladies First) 2019 wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa Kwenye eneo la viwanja vya michezo Shule ya Sekondari ya Mwenge mjini hapa leo. Kutoka kulia ni Emmy Hosea, Zakia Said, Faidha Ally, Tunu Andrea na Elvera Emmanuel.
Afisa Michezo na Utamaduni wa Mkoa wa Singida, Henry Kappela akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani), wakati akiwatangaza wanariadha wateule.
Washiriki wa mashindano hayo ngazi ya mkoa wakisikiliza hotuba za viongozi wao.
Afisa Michezo na Utamaduni wa Wilaya ya Ikungi, Abubakari Kisuda, akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ngazi ya mkoa.
Maofisa Michezo wa Mkoa wa Singida wakiwa kwenye shughuli hiyo. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Riadha, Said Swalehe, Katibu wa Chama cha Riadha, Juma Mataka na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Riadha, Juma Jambau.
Wanariadha hao wakionesha mshikamano.
Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Singida, Benno Msanga (wa tatu kutoka kuli), akiwa na Wanariadha hao.
Wanariadha hao wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi. 


Na Waandishi Wetu, Singida

Washiriki watano wa mchezo wa riadha kwa wasichana kutoka Shule mbalimbali za mkoa wa Singida wamechaguliwa kushiriki mashindano ya "Ladies First " 2019 kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao jijini Dar-es salaam. 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya 'Ladies First' ngazi ya mkoa, Afisa Utamaduni na Michezo Mkoa wa Singida, Henry Kapella alisema wanariadha 

wateule wanatarajia kuungana na wezao kote nchini mapema kuanzia Disemba 7-8 mwaka huu.Aliwataja washindi hao na maeneo wanayotoka kuwa ni Emmy Hosea (Itigi) ambaye atakuwa na kibarua cha kushiriki mbio za mita 100 na mita 200, Zakia Said (Manyoni)atakimbia mbio za mita 400 na 800,Faidha Ally (Ikungi) atakimbia mita 1500, Tunu Andrea (Ikungi) mita 500, pamoja na Elivila Emanuel (Ikungi) mita 1500.

"Lengo la mashindano haya ni kumwezesha mtoto wa kike kushiriki kikamilifu katika michezo hususani mchezo wa riadha," alisema Kapella. 
Kapella alisisitiza kuwa mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ngazi ya Taifa washindi watapata nafasi ya kushiriki mashindano hayo ngazi ya kimataifa yatakayofanyika Septemba 2020 nchini Japan.

Kapella alisema mashindano hayo ngazi ya mkoa yamewezeshwa na kuratibiwa na Katibu Tawala wa Mkoa huku ngazi ya kitaifa yakitarajiwa kudhaminiwa na Baraza la Michezo la Taifa na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA).

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 21,2019

MVUA ZAHARIBU NYUMBA ZAIDI YA 360 SONGWE

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen Nicodemus Mwangela akiangalia paa lililo ezuliwa na mvua ya upepo mkali katika makazi ya wananchi Wilayani Momba, zaidi ya nyumba 200 wilayani humo zimeharibiwa.
Nyumba ya mwananchi ikiwa imebomoka na kuezuliwa kutokana na mvua ya upepo Mkali iliyonyesha jana jioni na kusababisha uharibifu wa nyumba Zaidi ya 360 katika halmashauri za Momba na Mbozi Mkoani Songwe.


…………………………

Mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha jana jioni Mkoani Songwe imesababisha uharibifu wa nyumba Zaidi ya 360 Katika Wilaya za Mbozi na Momba pamoja na kujeruhi watoto wawili.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen Nicodemus Mwangela mapema leo ametoa taarifa hiyo mara baada ya kukagua hali ya uharibifu wa makazi ya watu na taasisi za serikali ambapo ameziagiza halmashauri husika kurejesha miundombinu ya serikali iliyoharibika.

“Kuna wananchi wamepata madhara lakini wametibiwa na kurejea nyumbani, nawapongeza sana viongozi na majirani ambao waliwahi kutoa msaada kwa wahanga aidha ninaagiza halmashauri za Momba na Mbozi warekebishe haraka nyumba za walimu na madarasa ili huduma ziendelee.”, amesema Brig. Jen. Mwangela.

Aidha ametoa pole kwa wahanga na amewapongeza majirani wa waliopata uharibifu wa nyumba kwa kuwahifadhi wenzao jana usiku huku akiwa hakikishia kuwa Kamati za Usalama za Wilaya na wataalamu wanafanya tathmini ya uharibifu na kupanga namna ya kutoa msaada.

Brig. Jen. Mwangela amewataka wananchi wote kuchukua tahadhari kwakuwa mvua za Mkoani Songwe ni nyingi hivyo waimarishe makazi yao pia watoe taarifa mapema endapo utatokea uharibifu wowote.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi Hanji Godigodi amesema wataalamu wa Halmashauri wanaendelea na tathmini ya hali ya uharibifu na kuwa nyumba za walimu na shule zitafanyiwa marekebisho haraka.

Afisa Mtendaji kata ya Msangano Halmashauri ya Wilaya ya Momba Focus Kadule amesema baada ya tathmini ya hali ya uharibifu katika kata yake ataitisha Mkutano wa hadhara ili wananchi waweze kujitolea kuwasaidia waliopata uharibifu kutokana na mvua hizo.

Fadeli Ng’aala mkazi wa Kijiji cha Hamwelo Halmashauri ya Mbozi amesema mvua iliyoambatana na upepo imeezua paa la nyumba yake huku yeye na watoto wakiwa ndani na kusababisha uharibifu wa vyakula na vifaa vingine kama vitanda, magodoro, televisheni, solar na masofa.

Naye Mwalimu Jacob Sambilila wa Shule ya Msingi Nkala Halmashauri ya Wilaya ya Momba amesema mvua zilianza saa tisa mchana na kusababisha mti kuangukia darasa hali iliyozua taharuki kwa wanafunzi lakini pia baada ya kurudi nyumbani kwake alikuta nyumba anayoishi imeezuliwa.

“Baada ya kutoka kazini nilikuta nyumba ya mwalimu mwenzangu imeezuliwa na nilipofika kwangu nimekuta nyumba imebomoka na kuezuliwa na kusababisha uharibifu hata kwenye chakula chote nilichotunza kimeharibika na vifaa vya ndani.”, amesema Mwalimu Sambilila.

RUSHWA NI ADUI WA HAKI,KATAA KIONGOZI ANAECHAGULIWA KWA RUSHWA

$
0
0
Uchaguzi wa serikalizamitaa unaelekea ukingoni, Wananchi mtakutana na viashiria mbalimbali vya rushwa, mkatae kiongozi anaechaguliwa kwa rushwa, chagua kiongozi asiyependa rushwa, Kanyaga rushwa chagua maendeleo, hata  kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa kataa rushwa tenda haki.

TAARIFA KWA UMMA YA KUSITISHA MATUMIZI YA DAWA ZENYE KIAMBATA HAI CHA RANITIDINE

ROSE MANUMBA AINGIA ORODHA YA WAJUMBE WA KUSHAURI TAASISI YA UMOJA WA MATAIFA WANAWAKE TANZANIA (UN WOMEN TANZANIA).

$
0
0
Msichana Rose Manumba Chini ya Umri wa Miaka 30,  ameingia Katika Orodha ya Wajumbe wa kushauri Taasisi ya Umoja wa Mataifa wa Wanawake Tanzania (UN Women Tanzania) 2019 - 2021 

 Rose Manumba ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania, amechaguliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wanaotokana na Asasi za Kiraia kuingia katika kikundi cha kushauri (Civil Society Advisory Group) Umoja wa Mataifa wa Wanawake Tanzania (UN Women Tanzania) namna gani tunaweza kufikia moja ya malengo ya maendeleo endelevu hususani lengo la 5 la Usawa wa Kijinsia (Gender Equality) katika maeneo mbalimbali.

Kikundi hicho cha washauri kina jumla ya Idadi ya Wajumbe wasiozidi 10 wanaotokea kwenye Taasisi mbalimbali.

Kikao cha kwanza kimefanyika  jana  Novemba 20/2019  na kufunguliwa rasmi na Naibu Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake Tanzania (Deputy Country Representative to UN Women Tanzania) Bi. Julie Taylor.

AFISA UTUMISHI MANYONI KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUBAKA WANAFUNZI WAWILI WA DARASA LA SITA

$
0
0
Na Jumbe Ismailly MANYONI 

AFISA utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida,Benjamen Mombeki (59) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Manyoni akikabiliwa na tuhuma za kubaka wanafunzi wawili wa shule ya msingi Manyoni.

Shauri hilo la jinai namba 167/2019 na namba 168/2019 lipo mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo,Stela Thomasi Kiama.

Mwendesha Mashtaka wa jeshi la polisi,Nasoro Saidi alidai kwamba katika shitaka la kwanza lenye usajili namba 167/2019 inadaiwa kuwa aug,15,mwaska huu saa nne asubuhi kwenye maeneo ya mjini Manyoni,mshitakiwa alimbaka mwanafunzi wa darasa la sita (jina limehifadhiwa) katika shule ya msingi Manayoni.

Mwendesha Mashtaka wa jeshi la polisi alidai kwamba katika shitaka la pili lenye namba za usajili 168/2019 linalomkabili afisa utumishi Mombeki ni kwamba aug,15,mwaka huu saa nne asubuhi kwenye maeneo ya Mjini Manyoni,mshitakiwa huyo alimbaka mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Manyoni(jina tunalo).

Hata hivyo Mombeki aliposomewa mashtata hayo yote mawili alikana na yupo nje kwa dhamana hadi disemba,05,mwaka huu kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUSIMAMIA MASLAHI YA WAFUGAJI NA KUWATAKA KUFUATA SHERIA ZA NCHI

$
0
0
Na. Edward Kondela

Serikali imewataka wafugaji katika Wilaya za Chunya na Mbarali Mkoani Mbeya kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na taratibu za nchi ikiwemo ya kutoingiza mifugo katika maeneo ya Hifadhi za Taifa ya Ruaha na Pori la Akiba la Ruangwa, hali ambayo imekuwa ikisababisha migogoro kati ya wafugaji na askari wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), wanaolinda hifadhi hizo ambapo baadhi ya migogoro hiyo imesababisha vifo vya wafugaji, askari na mifugo.

Akizungumza Jumanne hii (19.11.2019) wakati wa kuhitimisha ziara ya siku mbili ya makatibu wakuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Sheria na Katiba, waliozuru baadhi ya maeneo yenye migogoro katika wilaya hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka wafugaji kuacha tabia ya kuingiza mifugo katika maeneo ya hifadhi kwa ajili ya malisho kwa kuwa ni kinyume na taratibu za nchi.

“Serikali inawataka wafugaji wote kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na kutoingiza mifugo katika maeneo ya hifadhi za taifa kwa kuwa ni kinyume cha sheria pia serikali itaendelea kuhakikisha wafugaji wanafanya shughuli zao kwa amani bila kubughudhiwa ili mradi wanafuata sheria na taratibu za nchi ikiwemo ya kutoingiza mifugo katika mashamba ya wakulima.” Amesema Prof. Gabriel

Akizungumza kwa niaba ya makatibu wakuu wa wizara hizo, Prof. Gabriel amefafanua kuwa kutokana na Tangazo la Serikali (GN) Na. 28 la Tarehe 14 mwezi Machi mwaka 2008, ambalo liliongeza eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kutoka Kilometa za Mraba 5,878 hadi kufikia Kilometa za Mraba 20,226 hali hiyo imesababisha eneo la malisho kupungua kutoka hekta 259,000 za awali hadi 154,000 katika Wilaya za Chunya na Mbarali ambapo amewataka wafugaji katika wilaya hizo kuheshimu tangazo hilo wakati serikali ikifanyia kazi maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuainishwa kwa vijiji vilivyopo katika maeneo ya hifadhi ili maboresho yaweze kufanyika kwa maslahi ya vijiji hivyo.

Katika ziara hiyo ya makatibu wakuu kutoka wizara nne Mkoani Mbeya uongozi wa TANAPA umekubali kutengeneza barabara za kuainisha mipaka ya maeneo ya hifadhi na vijiji mara baada ya kuainishwa kwa mipaka mipya kufuatia agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutambuliwa kwa maeneo ya vijiji na hifadhi za taifa ambalo tayari linafanyiwa kazi.

Kufuatia matukio ya mauaji ya askari mmoja wa TANAPA na askari mgambo mmoja mwaka 2018 waliouawa na wafugaji wakati wakiswaga ng’ombe waliokamatwa katika Hifadhi ya Ruaha kuelekea Kambi ya Nyota ya TANAPA iliyopo Wilaya ya Mbarali na tukio la hivi karibuni la Tarehe 11 Mwezi Oktoba 2019 la kuvamiwa kwa kambi hiyo na baadhi ya wafugaji wakiwa na silaha za jadi kwa nia ya kukomboa mifugo iliyokamatwa katika Hifadhi ya Ruaha hali iliyosababisha kijana mmoja wa wafugaji (19) kupigwa risasi na askari wa TANAPA na ng’ombe 14 kuuawa, Katibu Mkuu Prof. Gabriel amewataka wafugaji kutumia njia zisizo halali kukomboa mifugo iliyokamatwa.

Akizungumza na baadhi ya wafugaji katika Kijiji cha Igunda, Kata ya Igava Wilayani Mbarali, katibu mkuu huyo amefafanua kwa wafugaji hao kuwa kutokana na sheria na haki za wanyama duniani ni makosa kuua mnyama bila kuwa na sababu za msingi hali iliyosababisha serikali kuchukua hatua kwa askari wa TANAPA waliohusika kupiga ng’ombe hao risasi na hivyo kuwataka wafugaji hao kuwa watulivu kwa kuwa suala hilo linashughulikiwa na vyombo vya dola.

Aidha ameeleza kuwa kuwa pindi mifugo inapokamatwa na askari wa TANAPA inapobainika kuingia kwenye maeneo ya hifadhi, wamiliki wa mifugo hiyo wanapaswa kufuata taratibu za kisheria za kulipa faini na kukabidhiwa mifugo yao na kusisitiza kuwa ni muhimu kwa wafugaji kujiepusha kuingiza mifugo maeneo wasiyoruhusiwa yakiwemo ya Hifadhi za Taifa.

“Sisi viongozi wa Wizara za Mifugo na Uvuvi, Maliasili na Utalii, Mambo ya Ndani ya Nchi na Sheria na Katiba tunasikitishwa sana na matukio haya ya mauaji kijana mdogo amefariki dunia kwa sababu ambazo zingeweza kuepukika kwa kutaka kumdhuru askari kwa kutumia silaha za jadi akiwa na wenzake takriban 20 ili kukomboa ng’ombe waliokamatwa hifadhini, tunawaomba mjiepushe na matukio ya namna hii fuateni sheria na taratibu za nchi ili mfuge bila bughudha.” Amefafanua Prof. Gabriel

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel akiwaongoza viongozi wenzake katika ziara hiyo akiwemo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Amon Mpanju na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda wamefika pia katika Kijiji cha Lualaje Kata ya Lualaje Wilayani Chunya na kuzungumza na baadhi ya wafugaji kufuatia matukio ya wafugaji hao kuingiza ng’ombe katika Hifadhi ya Ruaha.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima amewataka wafugaji hao kufuata sheria na taratibu za nchi na kwamba jeshi la polisi litazidi kutoa ushirikiano kwa wafugaji hao katika matukio mbalimbali yakiwemo ya kuwabaini baadhi ya wafugaji ambao wamekuwa wakiingiza mifugo katika maeneo ya hifadhi pamoja na kujihusisha na uhalifu.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Amon Mpanju amewataka wafugaji kuwa watulivu na walitambue Tangazo la Serikali Na. 20 la Tarehe 14 mwezi Machi mwaka 2008, ambalo liliongeza eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kupunguza eneo la malisho katika Wilaya za Chunya na Mbarali hali iliyosabisha baadhi ya maeneo waliyokuwa wakiyamiliki kubadilishwa matumizi na kuwa ya hifadhi, ambapo suala hilo tayari linafanyiwa kazi kwa maelekezo ya Rais Magufuli na kuwataka kutoingiza mifugo yao katika eneo la hifadhi hadi serikali itakapotangaza maamuzi mengine.

Kuhusu kuainishwa kwa mipaka kati ya vijiji na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha pamoja na Pori la Akiba la Ruangwa, akizungumza kwa niaba ya katibu mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kutoka katika wizara hiyo Dkt. Maurus Msuha amesema serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii itahakikisha inatuma timu ya wataamu katika maeneo hayo ili kuweka alama maeneo ambayo wananchi yanawatatiza kufahamu mipaka ya vijiji na maeneo ya hifadhi ili kuondoa migogoro kati ya maeneo ya wakulima na wafugaji na mipaka ya Hifadhi ya Ruaha na Pori la Akiba la Ruangwa.

Baadhi ya wananchi katika Wilaya za Chunya na Mbarali waliopata fursa ya kuzungumza wakati wa ziara ya makatibu wakuu kutoka Wizara za Mifugo na Uvuvi, Maliasili na Utalii, Mambo ya Ndani ya Nchi na Sheria na Katiba wamesema wamefurahishwa na ziara hiyo na kwamba watazingatia maelekezo waliyopatiwa ili kuhakikisha wanafuga kwa kufuata sheria na kwamba watashirikiana na serikali ili kuwabaini baadhi ya wafugaji wanaokiuka sheria na kuingiza mifugo katika maeneo ya Hifadhi ya Ruaha na Pori la Akiba la Ruangwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamefafanua kuwa wamefurahishwa kwa viongozi hao wa juu kutoka wizarani kufika hadi katika maeneo yao na kujionea changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya maji na malisho pamoja na kupata taarifa za matukio ambayo yamejitokeza katika wilaya hizo kutoka mamlaka mbalimbali za serikali wakiwemo viongozi wa serikali, wafugaji pamoja jeshi la polisi.

Awali kabla ya makatibu wakuu hao kutembelea wafugaji katika Wilaya za Chunya na Mbarali, wamefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mbeya na kuwa na mazungumzo na mkuu wa mkoa huo Mhe. Albert Chalamila pamoja Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya, ambapo Mhe. Chalamila amewaambia serikali ya mkoa huo itaendelea kufanya kazi kwa kusimamia sheria na kuwaasa viongozi wenzake wanapofika mkoani hapo kupata taarifa sahihi ya mkoa kabla ya kufika katika maeneo mbalimbali kuzungumza na wananchi.

Aidha Mhe. Chalamila amebainisha kuwa migogoro ya wafugaji katika Wilaya za Chunya na Mbarali ambao wamekuwa wakiingiza mifugo kwenye maeneo ya Hifadhi ya Ruaha na Pori la Akiba la Ruangwa katika Mkoa wa Mbeya unatokana na wafugaji kuwa na mifugo mingi tofauti na maeneo ya malisho, hali ambayo imekuwa ikiulazimu uongozi wa mkoa kutoa elimu kwa wafugaji juu ya ufugaji wa kisasa na wenye tija kwa wafugaji kuwa na ng’ombe wachache wanaoweza kuwapatia matokeo mazuri.

Ameongeza kuwa uongozi wa Mkoa wa Mbeya utazidi kusimamia na kutoruhusu mifugo kuingizwa katika maeneo ya hifadhi pamoja na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira ili kuhakikisha mkoa huo unakuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Katika ziara hiyo ya makatibu wakuu wanne Mkoani Mbeya, ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel akiambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Amon Mpanju na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda, ilikuwa na lengo la kupata taarifa sahihi ya hali ya wafugaji katika Wilaya za Chunya na Mbarali pamoja na kupata hadidu za rejea ambazo wataalam watatumia katika kufanya mapitio na maboresho ya Tangazo la Serikali (GN) Na. 28 la Mwaka 2008 ili iwe shirikishi na kupata suluhu ya migogoro ya wakulima na wafugaji.
 Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila akiwa na makatibu wakuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Maliasili na Utalii akiwakilishwa na mkurugenzi wa idara ya wanyamapori na Wizara ya Sheria na Katiba, mara baada ya mazungumzo kuhusu hali ya ufugaji katika Wilaya za Chunya na Mbarali mkoani humo, wakiwa tayari kutembelea maeneo ambayo yamekumbwa na migogoro ili kupata hadidu za rejea zitakazotumiwa na wataalam ili kutatua migogoro hiyo katika ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 18-19 mwezi Novemba 2019.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel akiangalia moja ya vielelezo pamoja na kuoneshwa ramani ya mipaka iliyowekwa kutenganisha maeneo ya vijiji na Hifadhi ya Ruaha na Pori la Akiba la Ruangwa, katika ziara ya siku mbili Mkoani Mbeya kuanzia tarehe 18-19 mwezi Novemba 2019 akiwa na viongozi wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Sheria na Katiba na Wizara ya Maliasili na Utalii.
 Kutoka kushoto picha ya kwanza: Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha akimwakilisha katibu mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii wakizungumza na wananchi katika Kijiji cha Igunda, wilayani Mbarali na kuwasisitiza serikali itaendelea kusimamia maslahi ya wafugaji na kuwataka wafuate sheria na kuheshimu mipaka ya hifadhi za taifa na maeneo ya vijiji, wakati viongozi hao walipokuwa wakihitimisha ziara ya siku mbili Mkoani Mbeya katika Wilaya za Chunya na Mbarali kuanzia tarehe 18-19 mwezi Novemba 2019.


BIASHARA YA MATUNDA SOKO LA BURUGURINI,ILALA JIJINI DAR

$
0
0
Na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv

Wafanyabiashara wa matunda katika Soko la Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wamesema kwa sasa matunda yanayopatikana kwa wingi ni Maembe na  Mananasi,

Wakizungumza na Michuzi Tv jijini Dar es Salaam wafanyabiashara hao wameeleeza kuwa hali iko shwari  kibiashara na matunda yanauzika,wateja wao wamekuwa wakipita sokoni hapo kujipatia matuda mbalimbali kuligana na mahitaji yao.
Bei ya tikitiki maji ni kati ya Sh 500 hadi Sh. 3000.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Bei ya machungwa katika soko la Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam yanauzwa kati ya sh. 50 hadi 100 kwa bei ya jumla.
Embe katika soko la Buguruni yanauzwa  kati ya Sh.300 hadi Sh 600/= lakini bei hiyo hiyo yanauzwa kwa rejareja.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv) 
Bei za matunda aina Parachichi ni shi 200,500 bei hiyo kwa wanaonunua kwa rejareja na jumla (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv) 

SERIKALI YAILEKEZA TPDC KUSHAWISHI VIWANDA NCHINI KUTUMIA GESI ASILIA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Esnat Chagu na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka wakitembelea mradi wa gesi uliopo Madimba mkoani Mtwara.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (wa pili kushoto) akiwasili katika kituo cha kuzalisha gesi asilia cha Mnazi Bay mkoani Mtwara kukagua namna wanavyotekeleza sheria ya mazingira ya mwaka 2004.
Meneja wa mradi wa kuchakata gesi wa kampuni ya Maurel and Prol Tanzania katika eneo la Mnazi Bay mkoani Mtwara akitoa maelezo kwa viongozi waliotembelea mradi huo.

******************************

Na Robert Hokororo, Mtwara

Serikali imeelekeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kushawishi viwanda mbalimbali nchini kutumia gesi asilia inayozalishwa hapa nchini hatua itakayosaidia kupunguza matumizi ya nishati zinazoharibu mazingira.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima ametoa maelekezo hayo alipotembelea miradi ya kuchakata gesi katika maeneo ya Mnazi Bay na Madimba mkoani Mtwara wakati wa ziara ya kukagua shughuli za mazingira zinavyofanyika katika miradi hiyo.

Sima pamoja na kupongeza miradi ya uzalishaji wa nishati hiyo alisema kuwa hakuna sababu ya viwanda kuharibu mazingira kwa kutumia nishati kama mafuta ambayo imezoeleweka na badala yake vianze kutumia gesi asilia ambayo ni rafiki wa mazingira.

“Katika ziara hii tumejifunza mambo mengi na hapa tunaona juhudi zinazofanyika kuhakikisha tunapata gesi asilia na tumeambiwa hapa kinazalishwa, kuchakatwa na kusafirishwa kiwango kikubwa cha gesi hivyo Serikali inaelekeza ninyi TPDC (Shirika la Petroli Tanzania) mkae na CTI (Shirikisho la Viwanda) muwashishi kuona sasa namna ya kutumia gesi asilia na kuachana na mafuta kwani yanaharibu mazingira,” alisema.

Aidha, Sima ambaye aliambatana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) alitoa maelekezo kwa kampuni zinazojihusisha na uchakataji wa gesi asilia kuomba kibali cha viwango cha uchafuzi wa hewa vinavyozalisha katika shughuli zao za kila siku.

Alifafanua kuwa viwanda hivi vina jukumu la kufuata Sheria ya Mazingara ya Mwaka 2004 hivyo pamoja na kuishirikisha jamii kujua madhara yanayoweza kutokea kutokana na nishati hiz lakini pia ni lazima NEMC watambue viwango vya uchafuzi wa mazingira hususan katika hewa zinazotokana na shughuli za uckakataji wa gesi.

“Hi sasa dunia inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi ambayo yana athari kubwa kwa mazingira yetu hivyo tunapoanzisha miradi kama hii lazima tuombe vibali ili tujue standards za pollution tunazozalisha na kama ikizidi utaratibu basi tuanze kulipa tozo kwa mujibu wa taratibu.

“Tunatambua juhudi kubwa zinazofanywa na viwanda hivi vya gesi na
hapa,tunaambiwa kuna visima takriban vitano na vinafanya vizuri ambapo
takriban futi za ujazo zaidi milioni 90 sawa na asilimia 90 ya pure gas
inasambazwa katika maeneo mengine ya nchi na hapa tayari tuna hazina kubwa ya nishati hii,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka alitaka viwanda vyote vinavyojishughulisha na shughuli kama hizo za uchakatiji wa gesi kuwa na mpango wa jinsi wanavyoratibu uchafuzi wa hewa ili kuweza kukabiliana na changamoto kama hizo katika mazingira.

Pamoja na mambo mengine pia Dkt. Gwamaka alitaka ziungwe mkono juhudi za uzalishaji wa gesi zinazofanyika katika miradi hii ili kuweza kuhifadhi mazingira kutokana na kuepukana na ukataji wa miti kwa ajili ya nishati.

Naibu Waziri Sima na NEMC wako katika ziara kwenyue mikoa ya Lindi na
Mtwara kukagua miradi ya visima vya gesi kuona kama inafuata Sheria ya
Mazingira ya mwaka 2004 na namna mabavyo wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kuchukua hatua pindi yanapotokea maafa yakiwemo kuvuja kwa nishati hiyo katika mabomba.

NAIBU WAZIRI MABULA AZITAKA HALMASHAURI NCHINI KUDHIBITI UJENZI HOLELA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mvomero Frolent Kyombo kuhusiana na utunzaji kumbukumbu za ardhi katika majalada ya ardhi wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani Morogoro jana. Wa pili kulia ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda maalum ya Morogoro Erick Makundi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Ujenzi wa Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wa pili kushoto Mhandisi Grace Musita wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za TFS zilizopo Mvomero Morogoro. Kushoto ni Kaimu Meneja wa NHC mkoa wa Morogoro Constantine Yuda.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipata maelekezo ya Ujenzi wa Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kutoka kwa Mhandisi Grace Musita wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za TFS zilizopo Mvomero Morogoro. Kulia ni Kaimu Meneja wa NHC mkoa wa Morogoro Constantine Yuda (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

**************************************

Na Munir Shemweta, WANMM MOROGORO

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka halamashauri nchini kuhakikisha zinadhibiti ujenzi holela kwa kuhakikisha utoaji vibali vya ujenzi ktika maeneo yao unazingatiwa na kusimamiwa ipasavyo.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti jana katika halmashauri za wilaya za Morogoro, Mvomero pamoja na Manispaa ya Morogoro wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro.

Alisema, halmashauri nchini zina wajibu wa kudhibiti ujenzi holela katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na Watendaji wa Mitaa na kuweka taratibu ambazo hazitamruhusu mtu kufanya ujenzi wowote bila kupata kibali cha ujenzi kutoka halmashauri husika.

‘’ ili kuondokana na ujenzi holela katika halmashauri zenu mwananchi asifanye ujenzi wowote bila kupata kibali cha ujenzi kutoka halmashauri ‘’ alisema Dkt Mabula

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, zoezi la urasimishaji linaloendelea sasa katika maeneo mbalimbali siyo zoezi la kudumu na kulegalega kudhibiti ujenzi holela kutasababisha zoezi hilo kutokuwa na maana kwa kuwa ujenzi holela utakuwa ukiendelea.

Akigeukia suala la utoaji hati za ardhi, Dkt Mabula aliagiza Hati zilizokamilika katika ofisi za Msajili wa Hati wamiliki wake watangaziwe kupitia njia mbalimbali zikiwemo radio za Kijamii (Local Radio) sambamba na hati hizo kutolewa kwa wamiliki wake katika eneo maalum litakaloandaliwa karibu na maeneo wanaoishi wamiliki wa hati hizo.

Alisema, njia ya kuwatafuta wananchi ambao hati zao zimekamilika itasaidia kupunguza mlundikano wa Hati za Ardhi zilizokamilika kwenye Ofisi za Msajili wa Hati tofauti na utaratibu wa sasa unaomtaka mwenye hati kuifuata ofisi za ardhi au ile ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi za Kanda kwenda kuchukua.

Awali Mkuu wa Idara ya Ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro Patrick Mwakilili alisema halmashauri yake imepanga kupima viwanja 1,000 kwenye makao makuu ya wilaya Mvuha na viwanja 3,900 katika mji mdogo wa Kisaki ambao ni lango la kuingilia Mradi wa Kufufua Umeme wa Stiglers George na Hifadhi ya Taifa ya Mwl Nyerere zamani Selous.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya wilaya ya Morogoro, tayari maeneo tisa ya kufanyiwa urasimishaji makazi yameanishwa aliyoyataja kuwa ni Pangawe, Mkambarani, Fulwe, Ngerengere, Mvuha, Kisaki , Mtamba, Mkuyuni na Dhutumi na kubainisha kuwa halmashauri yake imepokea na kuridhia maombi kutoka makampuni manne kwa ajili ya kazi hiyo.

Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) zilizopo katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, ujenzi unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Akiwa katika ukaguzi huo, Dkt Mabula mbali na kulipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kuisimamia vyema miradi yake ya ujenzi katika maeneo mbalimbali nchini ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Ofisi hizo za TFS hasa baada ya kuelezwa na Msimamizi wa ujenzi huo Mhandisi Grace Musita kuwa hatua iliyofikiwa sasa na Shirika lake katika kujenga ofisi hizo za TFS ilitakiwa kufikiwa tarehe 13 Desemba 2019.

Serikali yaridhia kupeleka vikosi vya ulinzi vijiji vya mipakani Tandahimba

$
0
0
Serikali imeridhia kupeleka vikosi maalumu vya ulinzi maeneo ya mipaka ya vijiji Wilayani Tandahimba

Akizungumza na wananchi wa kata ya Michenjele na Mihambwe Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba alisema kuwa vikosi hivyo vitakuja wakati wowote 

"Nimekuja kuzungumza nanyi kuwa serikali imeridhia ombi la kuleta Majeshi ya Ulinzi katika maeneo ya huku mipakani kwa kutambua kuwa Wilaya yetu imepakana na nchi ya Msumbiji na kwa Sasa Msumbiji hakuna amani "alisema Waryuba

Alisema kuwa tayari Jeshi la Polisi limeweka kambi katika kata ya Namikupa ambapo wameona ni katikati katika shughuli zao za ulinzi.

Waryuba  alisema ujio wao utakuwa ni kuangalia sehemu sahihi ya kuweka kambi ya kikosi maalum wakishajiridhisha ndipo watakuja rasmi

"Toeni ushirikiano ili vikosi vije tuishi kwa amani,usalama na utulivu katika maeneo yetu maana Hadi Sasa bado watu wanashindwa kwenda mashambani kwa hofu,"alisema Waryuba

Naye mkazi wa ng'ongo Dadi Tipila ameishukuru serikali kwa niaba ya wanamichenjele kwa hatua iliyochukuliwa na serikali kuhusu vijiji hivyo

" Tangu tukio la wenzetu kuuwawa bado tunayo hofu tunashindwa kwenda shambani kwa amani,tunaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa vikosi vya ulinzi pale watakapo hitaji msaada kutoka kwetu,"alisema Tipila 

Hatua ya kuimarisha ulinzi katika vijiji vya mipakani ndani ya Wilaya ya Tandahimba imekuja baada ya watu sita kuuawa na watu wasiojulikana .
 Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba akizungumza na wananchi wa kata ya Mihambwe
 Wananchi wa Mihambwe wakimsikiliza  DC wa Tandahimba 
Wananchi wa Michenjele wakimsikiliza Dc

MAFUNZO YA JESHI USU YAMELETA MAFANIKIO MAKUBWA KULINDA RASILIMALI ZA NCHI

$
0
0
Meja Jenarali Mstaafu Hamisi Semfuko akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya Jeshi Usu
Baadhi ya wahitimu wakionyesha mbinu mojawapo ya kukabiliana na adui bila silaha
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Katavi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katika mafunzo hayo Meja Jenerali Mstaafu Hamisi Semfuko.

**********************************

Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya Uhifadhi Wanyama Pori Nchini (TAWA) Meja Jenerali Mstaafu Hamisi Semfuko amesema mfumo wa mafunzo ya Jeshi Usu yanayobadili watumishi wa Wizara ya Mali asili kutoka katika hali ya uraia wa kawaida na kuwa askari yameleta mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka minne iliyopita

Amesema hayo wakati akifunga mafunzo hayo kwa wahitimu 535 katika Kituo cha Mafunzo Mlele mkoani Katavi

Aidha amewataka wahitimu hao kuishi yale waliyojifunza chuoni hapokwa kipindi cha miezi mitatu katika kuhakikisha Tanzania inatokomeza kabisa matukio ya ujangili yanayofanyika katika hifadhi na mapori mbalimbali hapa nchini

Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wameyasifu kwa kuwajengea ukakamau na kuwapa mbinumbalimbali za namna ya kukabiliana na adui

“Mbali na taaluma yangu ya uuguzi hapa nimeongezewa ujuzi ambapo sasa ninaweza kujumuika na askari katika doria na nikafanya nao kazi vizuri” alisema Ester Myaho ambaye ni mtumishi kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii

Pia wameiomba serikali kuboresha mazingira ya chuo hicho kwani kinakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa jiko la kupikia chakula cha wanafunzi na bwalo la chakula pamoja na ukosefu mitandao ya simu za mkononi 

Wahitimu hao wamepata mafunzo kadhaa ikiwemo namna ya kutumia silaha na kareti

Awali akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Katavi, Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lililan Matinga alisema mkoa wa Katavi unashirikiana na Wizara ya Mali Asili na Utalii katika kulinda mali asili


RC TABORA AWATAKA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KUCHUKUA TAHADHIRI YA MVUA KUEPUKA UCHAGUZI UJAO KUATHIRIWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye koti jeusi) akiwa ndani ya Kituo cha Kura cha Ilolangulu akitoa maelelekezo maalumu leo kwa Viongozi wa Wilaya ya Uyui wakati alipoongoza Kamati ya Usalama Mkoa wa Tabora kukagua Vituo vya Upigaji kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa siku ya Jumapili ijayo ili kujiridhisha maandalizi kama yanakwenda vizuri.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye tshirt yenye mistari ) na Wajumbe wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Tabora jinsi walivyojipanga kuhakikisha wapigaji kura maeneo ya wazi watakavyoshiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa wakati Kamati hiyo ilipokwenda kukagua Vituo vya Upigaji kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa siku ya Jumapili ijayo ili kujiridhisha maandalizi kama yanakwenda vizuri.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye koti jeusi) akiwa nje ya Kituo cha Kura cha Ilolangulu akitoa maelekezo maalumu kwa Viongozi wa Wilaya ya Uyui wakati alipoongoza Kamati ya Usalama Mkoa wa Tabora kukagua Vituo vya Upigaji kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa siku ya Jumapili ijayo ili kujiridhisha maandalizi kama yanakwenda vizuri.

********************************



WAKATI Mvua zimeanza kunyesha katika maeneo mbalimbali ,Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewaagiza Wasimamizi wa Uchaguzi wote mkoani humo kuhakikisha wanachukua tahadhari kwa kujenga na kuimarisha Vituo vya Kupigia Kura vilivyopo katika maeneo ya wazi kama vile kwenye miti kwa kuweka Maturubai mapema.

Hatua hiyo inalena kuhakikisha kuwa zoezi la upigaji kura la jumapili ijayo ariathiriwa na maji ya mvua.

Mwanri alitoa kauli hiyo jana wakati wa ziara yake na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uslama ya Mkoa na ile ya Wilaya ya Nzega , Uyui na Igunga wakati wa kukagua maandalizi ya maeneo ya kupigia kura Jumapili ijayo.

Alisema ni vema Vituo ambavyo vimepangwa katika maeneo ya wazi vikajengwa mapema kwa kutumia Maturubai katika eneo ambalo wananchi watakapotumia kupiga kura na eneo ambalo Mawakala wa Vyama vya Siasa watakapokaa.

Mwanri alisema pia lazima kuwepo eneo ambalo wananachi wanaosubiri kupiga kura wanaweza kujihifadhi endapo mvua itanyesha siku ya uchaguzi.

“Pamoja na kuwa Vituo vya wazi havipo katika majengo na kama mnapanga kujenga Mahema basi wekeni mazingira mazuri ya watu wanaokuja kupiga kura ili wawe na uhakika hata kama mvua ikinyesha ghafla , hatanyeshewa na vifaa vya kupiga kura havitaathirika na mvua” alisisitiza.

Alisema sanjari hilo amewataka Wasimamizi hao kuhakikisha kuwa vifaa vyote vya kuendesha zoezi la uchaguzi vinafika mapema katika eneo la tukio ili kuhakikisha zoezi linakwenda kwa kwa wakati uliopangwa na hakuna wananchi watakaokosa kupiga kura kwa sababu ya ukosefu wa vifaa hivyo.

Kwa upande wa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Rukia Manduta aliwataka Wasimamizi wa Uchaguzi kuhakikisha kuwa maeneo ambayo watajenga na kuweka Maturubai kuwa kwenye miununoko.

Alisema hatua hiyo itazuia kuharibika vifaa ikiwemo karatasi za kupigia kura kutokana na maji ya mvua

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Selemani Sikieti alisema tayari wameshanunua Maturubai kwa ajili ya kutekeleza zoezi hilo na watachukua tahadhari zote ili kufanya zoezi la upigaji kura kukamilika bila vikwazo

IGP Sirro Aagizwa kupeleka Timu ya Wataalamu Ujenzi Kituo cha Polisi Ikungi

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kutuma timu ya wataalamu kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kufika wilayani Ikungi Mkoani Singida, kutathmini maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi na Kituo kipya cha Polisi baada ya kituo cha awali kuchakaa hali inayopelekea askari na mahabusu kukaa sehemu isiyo salama.

Ameyasema hayo leo wakati wa ziara ya kutembelea Wilayani Ikungi ikiwa ni kuitikia wito wa Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, aliyetaka kauli ya Serikali juu ya uchakavu wa Ofisi, kituo cha polisi Ikungi na hali mbaya ya chumba cha mahabusu wakati wa kipindi cha maswali katika kikao cha Bunge kilichoisha hivi karibuni.

“Nimefika hapa nimeona mazingira wanayofanyia kazi hayaridhishi, serikali ilishaanza Ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Polisi ya Wilaya lakini ujenzi umesimama kwa miaka mitano sasa, namuagiza IGP Sirro alete wataalamu waje wafanye tathmini juu ya gharama za umalizwaji ujenzi huu na baada ya kujua basi hatua za haraka zifanyike ili ujenzi huu ukamilike” alisema Masauni

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu amesema hali ya kituo cha polisi hicho ni mbaya huku mahabusu wakikaa sehemu chafu ambayo si salama kwa afya ya binadamu.

“Mheshimiwa Naibu Waziri kama nilivyokueleza bungeni wakati nikiuliza swali la nyongeza nadhani sasa umejionea hali ilivyo mbaya, humo ndani umesikia harufu katika chumba cha mahabusu,wanajisaidia humo lakini pia umeona askari wanavyofanya kazi kwenye mazingira mabovu, naomba sasa serikali muangalie uwezekano wa kuharakisha kituo kile kipya hata mkianza na sehemu tu itasaidia adha hii wanayopata wananchi wa wilaya hii” alisema Mbunge Mtaturu

Nae Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogoro amesema uwepo wa kituo hicho kipya kikikamilika kitaimarisha Ulinzi na Usalama wilayani hapo ambapo kumekua na changamoto za kiusalama kwasababu ya upya wa wilaya hiyo ambayo imeanza.
Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu (kulia), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Edward Mpogolo wakiongozana kuingia katika kituo chakavu cha polisi , leo wilayani Ikungi mkoani Singida. Serikali iko mbioni kujenga kituo kipya ikiwa ni moja kati ya hatua ya kuhamisha kituo hicho pichani ambacho ni chakavu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu,akimuongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu)kutoka nje ya Kituo cha Polisi Ikungi , leo wilayani Ikungi mkoani Singida. Serikali iko mbioni kujenga kituo kipya ikiwa ni moja kati ya hatua ya kuhamisha kituo hicho pichani ambacho ni chakavu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu pamoja na viongozi wengine wilayani Ikungi, wakitoka kukagua Mradi wa Makao Makuu ya Polis wilayani hapo(pichani), leo ikiwa ni harakati za kujenga kituo kipya wilayani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo wakitoka kukagua Mradi wa Makao Makuu ya Polisi wilayani hapo, leo ikiwa ni harakati za kujenga kituo kipya wilayani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WAHITIMU CHUO CHA KODI WASHAURIWA KUWA WAZALENDO

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WAHITIMU 417 wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, astashahada na  shahada za kozi mbalimabali  zitakazotolewa na Chuo Cha Kodi nchini (ITA) katika mahafali ya 12 yatakayofanyika kesho Novemba 22, Chuoni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo hicho Profesa. Isaya Jairo amesema kuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philipo Mpango (Mb) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi atakayewatunuku  wahitimu hao vyeti na shahada mbalimbali.

Amesema kuwa licha ya kuwatunuku wahitimu hao vyeti na shahada mbalimbali Dkt. Mpango atatoa zawadi kwa wahitimu na wanafunzi waliofanya vizuri zaidi.

Prof. Jairo amesema kuwa wahadhiri waliofanya tafiti mbalimbali katika kipindi cha masomo cha 2018/2019 na tafiti zao kuchapishwa katika majarida mbalimbali ya kitaaluma na katika jarida la Chuo cha Kodi watatunukiwa tuzo katika mahafali hiyo.

Vilevile amesema kuwa katika miaka 12 ya Chuo hicho wanajivunia zaidi katika utoaji wa mafunzo ya forodha na Kodi wakiwa ni  Chuo pekee nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.

Vilevile amewashauri wahitimu kutumia mafunzo waliyoyapata kuleta tija kwa Jamii na kuwa wazalendo katika kulitumikia  taifa hasa kwa wakati huu ambao nchi imejikita katika kujenga uchumi wa kati na viwanda.
Mkuu wa Chuo cha Kodi Profesa. Isaya Jairo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mahafali ya kumi na mbili ya Chuo hicho yatakayofanyika kesho chuoni hapo ambapo amesema kuwa jumla ya wahitimu 417 watatunukiwa vyeti na shahada mbalimbali kulia ni Mkuu wa mawasiliano wa Chuo hicho Oliver Njunwa, leo jijini Dar es Salaam.

CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI KIBAHA (KFDC) CHAIOMBA SERIKALI KUWAKARABATIA MAJENGO

$
0
0
Mkuu wa chuo cha maendeleo ya wananchi Kibaha (KFDC) Joseph Nchimbi akizungumza na wazazi, wanafunzi na viongozi mbali mbali wa serikali ambao walihudhulia katika mahafali ya kuwaga wanafunzi wa chuo hicho yaliyofanyika mjini Kibaha.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Mjumbe wa bodi wa chuo hicho cha (KFDC) Elisante Ngure ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za mahafali hayo akisisitiza jambo kwa wanachu wa mwaka wa pili ambao wamehitimu katika fani mbali mbali (PICHA NA VICTOR MASANGU)

mjumbe wa bodi wa chuo hicho cha (KFDC) Elisante Ngure ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo wa kulia akiangalia moja ya kazi ya kufua umeme wa majumbani ambayo imefanywa na wanafunzi wa chuoni hapo, hawapo pichani.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

mmoja wa wanafunzi wa Chuo hicho akisoma risala kwa niaba ya wenzake Emmanuel Singambo mbele ya mgeni rasmi katika sherehe za mahafali hayo ya chuo cha maendeleo ya wananchi Kibaha Mkoani Pwani .(PICHA NA VICTOR MASANGU).

************************************

VICTOR MASANGU, KIBAHA.

CHUO cha maendeleo ya wananchi Kibaha (KFDC) kilichopo Mkoa wa Pwani tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1964 hakijafanyiwa ukarabati wowote katika baadhi ya majengo yake hivyo kupelekea miundombinu ya madarasa pamoja na majengo ya utawala kuwa katika hali ya uchakavu hivyo kuhatarisha usalama wa maisha ya watu hivyo wameiomba serikali ya awamu ya tano kuwasaidia kufanya ukarabati.

Hayo yalisema na Mkuu wa chuo hicho Joseph Nchimbi wakati wa mkutano wa wazazi ambao uliambatana na sherehe za mahafali pamoja na harambee ya kuchangia ujenzi amebainisha kuwa lengo lao kubwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli ya kuwa na uchumi wa viwanda hivyo wamejipanga kutoa mafunzo zaidi katika fani mbali mbali kwa vijana ili waweze kujiajiri na kuanzisha viwanda vyao wenyewe.

“Chuo chetu kwa sasa kinafundisha fani mbali mbali ikiwemo ufundi wa umeme wa majumbani, magari,uchomeleaji na uundaji wa vyumba,useremala,ushonaji, ufundi uashi, bomba, kilomo, mifugo, pamoja na fani ya upishi ambazo mafanikio yake ni makubwa kutokana na vijna wengine wamenufaika kupata ajira katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani na Taifa kwa ujumla.

Naye mmoja wa wanafunzi wa Chuo hicho akisoma risala kwa niaba ya wenzake Emmanuel Singambo alisbainisha kuwepo kwa changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili ikiwemo uchakavu wa vymba vya madarsa,ukosefu wa vitendea kazi,uckakavu mkubwa wa karakana wanazozitumia hivyo wameiomba serikali ya awamu tano kuwasaidia kwa hali na mali lengo ikiwa ni kusoma kwa vitendo katika mazingira ambayo ni rafiki.

Kwa upande wake mjumbe wa bodi wa chuo hicho cha (KFDC) Elisante Ngure ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo amewataka wanafunzi ambao wamehitimu mafunzo hayo kuachana na kuepukana kabisa na vitendo vya kujiingiza katika uvutaji wa madawa ya kulevya na kushinda vijweni na badala yake wahakikishe ujuzi walioupata wanautumia kwa maslahi ya nchi hasa katika kuanzisha viwanda vidogo na kujiajiri wao wenyewe.

“Kwa upande wangu mm napenda kuwahasa wanachuo ambao wamehitimu katika chuo hiki cha KFDC kwa sasa inabidi mbadilike achaneni kabisa na mambo ya kukaa vijiweni na kujihusisha na madawa ya kulevya kwani yanapoteza nguvu kazi ya Taifa, hivyo kitu kikubwa elimu ambayo mmeipata itumieni kwa kuleta maendeleo kwa nchi na sio kuitumia vinginevyo,alisema Ngure.

Pia Ngure alisistiza kuwa katika kuhakikisha kwamba vijana wanajikwamua kiuchumi ni lazima wahakikishe wanaachana na tabia ya kuitegemea serikali pekee katika suala zima la upatikanaji wa ajira na badala yake wanaweze kujiajiri wao wenyewe na kuanzisha vikundi mbali mbali kulingana na fani walizozozisome ili kuondokana na wimbi la umasikini

Kwa sasa Chuo cha maendeleo ya wananchi Kibaha ( KFDC) kilichopo Mkoa wa Pwani licha ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika utoaji wa fani mbali mbali na kuwapa fursa za ajira katika sekta binafsi na serikalini wanachuo wanaohitimu lakini bado wanahitaji sapoti kubwa ya rasilimali fedha kutoka serikalini ili kuweza kutimiza malengo waliyojiwekea.

THBUB kufuatilia uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019

$
0
0


Kama tunavyofahamu kuwa siku ya Jumapili Novemba 24, 2019 Watanzania kote nchini watafanya uchaguzi wa viongozi ngazi ya Serikali za Mitaa. Hatua hiyo ya uchaguzi imetanguliwa na uandikishaji wapiga kura, uteuzi wa wagombea na kampeni za wagombea, hatua ambazo zimetekelezwa kwa mafanikio makubwa. 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeridhishwa na idadi ya watu waliojitokeza kujiandikisha kupiga kura. Idadi hiyo imeongezeka ukilinganisha na idadi ya watu waliojiandikisha katika uchaguzi kama huo uliofanyika mwaka 2014. 

Katika kipindi kama hiki cha uchaguzi zipo taasisi za ndani na nje ya nchi ambazo zimeteuliwa kama waangalizi wa uchaguzi kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya 288. 

Napenda kuujulisha umma wa Watanzania kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni mojawapo ya taasisi ambayo itafanya ufuatiliaji wa uzingatiwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi huo kama Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Na. 7 ya 2001 inavyoelekeza. 

Tume inashiriki katika ufuatiliaji wa uchaguzi huu kama ilivyokuwa kwa chaguzi nyingine zilizopita ili kuhakikisha kuwa uchaguzi utakaofanyika unakuwa huru na wa haki. 

Hivyo basi, ili azma hiyo iweze kufikiwa ni muhimu kwa mamlaka na vyombo vinavyohusika katika zoezi hili kuhakikisha kuwa vinasimamia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyowekwa na kutenda haki. 

Aidha, wapiga kura na wagombea kwa upande wao, wahakikishe kuwa wanatumia haki yao na kutelekeleza wajibu wao wa kikatiba wa kupiga kura na kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyotolewa na mamlaka mbalimbali za nchi ili uchaguzi uweze kuwa huru na wa haki. 

Tume inatoa rai kwa wananchi wote nchini kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zote za upigaji kura na kuhakikisha kuwa zoezi la upigaji na uhesabu kura linafanyika kwa utulivu na amani. 

Mwisho, Tume inatoa wito kwa Wananchi wote waliojiandikisha kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili Novemba 24, 2019 na kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi watakaotuongoza kwa muhula mwingine wa miaka mitano. 

Tume inawatakia Watanzania wote uchaguzi huru na wa haki! 

Imetolewa na: 
Mhe. (Jaji Mstaafu) Mathew Pauwa Mhina Mwaimu 
Mwenyekiti 
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA 

Novemba 20, 2019 


Viewing all 110017 articles
Browse latest View live


Latest Images