Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

RC SHIGELLA: NCHI HAIWEZI KUJITEGEMEA KAMA WATANZANIA HAWATALIPA KODI

$
0
0

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa kikao cha kusikiliza kero za wafanyaabiashara wa Jiji la Tanga kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa kikao hicho
 Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza wakati wa kikao hicho
 MKUU wa Mkoa wa Tanga katikati akisisitiza jambo akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kulia na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kushoto wakati wa kikao hicho
 Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim kulia akiwa kwenye kikao hicho
 Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho kushoto akiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia wakifuatilia masuala mbalimbali kwenye kikao hicho
 MENEJA wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese (Aliyevaa suti ya darkblue) kulia akiwa na wadau wengine wakifuatilia kikao hicho

 KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Edward Bukombe kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakifuatilia kikao hicho
MENEJA wa Benki ya NMB Tawi la Mkwakwani Jijini Tanga akifuatilia kikao hicho 
 Wadau mbalimbali wakifuatilia kikao hicho wakiwemo wafanyabiashara  kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu 

Elirehema Kimambo ni Meneja Msaidizi Ukaguzi wa Kodi TRA Mkoa wa Tanga akati wa kikao hicho na kushoto ni Meneja Msaidizi Madeni ya Kodi TRA Mkoa wa tanga Lucas Kaigarula

 Wadau mbalimbali wakifuatilia kikao hicho wakiwemo wafanyabiashara  kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu 


MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella leo amekutana na wafanyabiashara wa Jiji la Tanga kusikiliza kero zao huku akiwaambia kwamba nchi haiwezi kujitegemea iwapo watanzania hawatalipa kodi ambayo wanapaswa kufanya hivyo.


RC Shigella aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha kusikiliza kero za wafanyaabiashara wa Jiji la Tanga kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huku akieleza pia kwamba serikali haiwezi kujitegemea iwapo watu hawataridhia kulipa kodi bila kushurutisha.


Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi,Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa,Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji,wafanyabiashara na viongozi mbalimbali.


Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba pia serikali haiwezi kujitegemea iwapo watu hawataridhia kulipa kodi bila kushurutishwa huku akisisitiza kwamba kazi kubwa anayoifanya Rais Dkt Magufuli ni kuhakikisha anasimamia mapato yanakusanywa.


Alisema kwamba serikali ina matarajio makubwa kwamba nchi katika misingi imara iliyoasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya dhana ya kujitegemea kwamba watanzania wanajitegemea wenyewe kwenye mipango yao, kuitekeleza na kuifanisi.


Aidha alisema watanzania wanajitegemea kwenye kutekeleza mipango yao na kufanikisha na moja ya chanzo cha cha mapato ni kuhakikisha kodi inalipwa na ndio maana serikali ya Rais Dkt John Magufuli imeweka jitihada zake kubwa katika kuhakikisha watanzania tunajitegemea.


“Lakini pia hatuna mjomba mwengine ambaye tunaweza kumuomba msaada na Serikali ya awamu ya tano sio ya kupiga magoti na rais wetu tunamfahamu matumaini yake macho yake yapo kwa watanzania kuhakikisha wana simamia miradi”Alisema.


Alisema miradi yote mkubwa inayoendelea inahitaji fedha ili iweze kujiendesha na hilo linatokana na watanzania kulipa kodi hivyo watambue kwamba kuna umuhimu wa kufanya hivyo.


Anasema kuioa ulipa kodi ndio wanaona ujenzi wa barabara ya poangani Tanga mkandarasi amekabidhiwa eneo na wiki ijayo ili barabara hiyo iweze kutengenezwa, bandari ya Tanga ilikuwa na tatizo la muda mrefu tayari ufumbuzi wake umanza kupatikana kuna mashine majini inachimba kina kutoka cha sasa mpaka kufikia mita 14 hadi 15 ili kuruhusu meli zinazokwenda Dar ziwezi kufika Tanga.


Awali akizungumza wakati wa kikao hicho Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure alisema kikao hicho kinakatokana na agizo la Naibu Kamisha wa TRA Msafiri Mbibo ambaye aliagiza kuandaa kikoa kingine ambacho kitajumuisha mamlaka hiyo na taasisi nyengine zinazohusika na wafanyabiashara.


Alisema kikao hicho ni kutiia agizo la Naibu Kamishna huyo ambapo Mkuu huyo wa mkoa alihaidi kwamba atakuwa mgeni rasmi kusimamia na kusikiliza kero za wafanyabiashara hao.

Indonesia kuwekeza Tanzania

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Indonesia kuwekeza Tanzania

Dodoma, 20 Novemba 2019


Mkutano wa Jukwaa la Viwanda kati ya Tanzania na Indonesia utafanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar Es Salaam tarehe 21 Novemba 2019. Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika mkutano huo ambapo kampuni kubwa 21 za Indonesia zinazojihusisha katika masuala ya ujenzi wa miundombinu na usafirishaji; kilimo; usindikaji vyakula; utengenezaji wa nguo, vifaa tiba na madawa ya binadamu; na uchimbaji wa madini na taasisi zinazosimamia masuala ya uwekezaji Tanzania (TIC, TPSF, CTI, TCCIA) zitashiriki katika mkutano huo.

Jukwaa hilo linatarajiwa kuwa fursa muhimu kwa jumuiya ya wafanyabiashara, wenye viwanda na wadau mbalimbali wa Tanzania na Indonesia kubadilishana mawazo, uzoefu na ujuzi pamoja na kuweka mikakati ya kushirikiana katika sekta ya viwanda kwa faida ya pande zote mbili.  

Kutoka na nchi ya Indonesia kuwa ni kubwa kiuchumi Kusini-Mashariki mwa Asia na ipo nafasi ya 16 katika kundi la nchi 20 tajiri zaidi duniani (G20), na uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji nchini, ni dhahiri kuwa kongamano hilo litakuwa na matokeo mazuri katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.            


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

RAIS DKT MAGUFULI AONGEA NA WANANCHI AKIWA NJIANI KUELEKEA DODOMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na kutoa maagizo kwa Simu kwa  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Dkt. Arnold M. Kihaule,mwananchi aliposimama kwa muda maeneo Dumilla Mkoani Morogoro akiwa njiani kuelekea Dlodoma leo Jumatano Novemba 20, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mwananchi aliposimama kwa muda maneo ya  Dumilla Mkoani Morogoro akida njiani kuelekea Dodoma leo Jumatano Novemba 20, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mtoto Hilal Salum (4)  aliposimama kwa muda maneo ya  Dumilla Mkoani Morogoro akida njiani kuelekea Dlodoma leo Jumatano Novemba 20, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiandika kero mbalimbali walizokuwa wakizitoa wananchi waliosimama pembezoni mwa Stendi ya Mabasi ya Msamvu mkoani Morogoro .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Msamvu mkoani Morogoro mara baada ya kusimama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA mara baada ya kupokea kero ya ucheleweshwaji wa vitambulisho vya Taifa katika eneo la Msamvu mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mmoja wa wafanya usafi wa Stendi ya Mabasi Msavu aliposimama na kuzungumza na wananchi waliosimama pembezoni mwa Stendi ya Mabasi ya Msamvu mkoani Morogoro
Sehemu ya Wananchi wa Msamvu mkoani Morogoro waliokuwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara aliposimama katika eneo hilo.

PICHA NA IKULU

KAIMU MKURUGENZI MKUU REA ATOA ANGALIZO KWA WAKANDARASI WA UMEME VIJIJINI

$
0
0
Kazi ya kufunga transfoma ikifanyika katika Kijiji cha Nyasato wilayani Mbogwe Mkoa wa Geita ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza (REA III)





Zahanati ya Mwamakiliga wilayani Nyang’hwale ni moja ya sehemu za huduma za kijamii zinazosambaziwa umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza (REA III)
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakili Julius Kalolo (kulia) akizungumza na watendaji kutoka kampuni ya Whitecity Guangdong JV na TANESCO wakati alipofanya ziara ya kukagua kazi ya kusambaza umeme kwenye Kijiji cha Mwamakiliga wilayani Nyang’hwale.
Wajumbe wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), watendaji kutoka kampuni ya Whitecity Guangdong JV na TANESCO na REA wakiangalia jinsi kazi ya kuvuta nyaya inavyofanyika katika Kijiji cha Mlange wilayani Mbogwe Mkoa wa Geita. Aliyenyoosha mkono ni Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Wakili Julius Kalolo
…………………..


Na Teresia Mhagama, Geita

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga ameeleza kuwa wakandarasi wa umeme vijijini wanaosuasua katika utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza (REA III) hawatapewa kazi katika miradi inayofuata.

Aliyasema hayo wilayani Mbogwe, Mkoa wa Geita mara baada ya ya Bodi ya REA ikiongozwa na Mwenyekiti wake Wakili Julius Kalolo kufanya ziara ya kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini wilayani Bukombe na Mbogwe.

” Tuko katika ziara hizi si kutoa maelekezo tu bali pia tunafanya tathmini za wakandarasi kwani tutakuwa na kanzidata itakayoonesha wakandarasi wanaotekeleza miradi kwa wakati na viwango vinavyotakiwa na wale wanaosumbua katika utekelezaji wa mradi unaoendelea.” Alisema Mhandisi Maganga.

Aliongeza kuwa, kanzidata hiyo itasaidia kuwatambua wakandarasi wote wasiofaa kupewa tena nafasi ya kutekeleza miradi ya umeme vijijini inayofuata hivyo aliwataka wakandarasi hao wajipange kufanya kazi vizuri.

Aidha, aliwataka wakandarasi wote kuzingatia agizo la Serikali la kuhakikisha kuwa ifikapo Disemba 31 mwaka huu, vijiji vyote vilivyo katika mradi wa REA III, mzunguko wa kwanza vinapelekewa umeme.

Kuhusu mkandarasi anayesambaza umeme mkoani Geita, kampuni ya Whitecity Guangdong JV, alimuagiza kuwa ifikapo tarehe 31 Disemba awe amepeleka umeme kwenye vijiji alivyopangiwa na kuwasilisha mpango kazi utakaoonesha pia kazi alizopanga kufanya katika kila Wiki.

Bodi ya REA kwa upande wake, ilimuagiza mkandarasi huyo kutekeleza ratiba za upelekaji umeme katika maeneo yote ambayo Bodi hiyo imetembelea mkoani Simiyu na Geita na kumweleza kuwa haitaacha kufuatilia utekelezaji wa ahadi hizo ili wananchi wapate nishati ya umeme.

Aidha, Bodi hiyo ilimuagiza mkandarasi kuhamasisha matumizi ya vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) ili kuwaondolea wananchi gharama kufanya wiring ndani ya nyumba na kwamba kipaumbele kiwe ni wajane, wazee na walemavu.

Pia Bodi hiyo iliwaasa viongozi wa vijiji katika maeneo mbalimbali nchini ambapo miradi ya umeme vijijini inaendelea kutekelezwa, kuwahamasisha wananchi ili waunganishiwe na huduma ya umeme hivyo miradi hiyo kuwa na tija.

Bodi hiyo pia ilikagua kazi ya usambazaji umeme wilayani Nyang’hwale mkoani Geita ambapo mkandarasi alieleza kuwa ndani ya Wiki hii atawasha umeme katika Vijiji Saba.

SERIKALI YASISITIZA UDHIBITI MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akifungua tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza Novemba 9, 2019 jijini Dodoma ambapo kilele chake ni Novemba 14, 2019.


Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma

Michezo ni nyenzo madhubuti katika kulinda afya za wanadamu kwa kuwajengea uimara na ustahimilivu, kukuza stadi za kijamii kiubunifu na kiuongozi ili kuwawezesha wanamichezo na watu wote kujifunza vitu vipya vinavyoweza kuchangia kutunza afya zao ili waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla. 

Sera ya Maendeleo ya Michezo ya mwaka 1995 inatambua umuhimu wa michezo ikiwemo kuhamasisha Umma wa Watanzania kushiriki katika michezo na mazoezi ya viungo. Kwa kutambua jambo hilo, Serikali imewezesha upatikanaji wa viwanja na vifaa vya michezo vilivyo bora na vya kutosha kwa ajili ya kuimarisha maendeleo ya michezo nchini. 

Kama taifa, kumekuwa na mtazamo chanya kwa viongozi kuthamini michezo kuanzia ngazi ya Serikali Kuu hadi Serikali za Mitaa kupitia mikoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji, mitaa na vitongoji. 

Kwa kulitambua na kulithamini suala la michezo kwa watu wa rika zote kuwa ni muhimu kwa afya, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mwaka 2016 alipokuwa akizindua kampeni ya kitaifa ya kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwenye viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam aliagiza watu katika maeneo yao nchini kushiriki kufanya mazoezi ambayo ni sehemu ya michezo.

Ili utaratibu wa kufanya mazoezi uwe endelevu, Makamu wa Rais alisisitiza “……….kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa siku ya mazoezi kwa afya, kwa sababu mazoezi ni afya na nawaasa wananchi kufanya mazoezi na kuanzisha na kujiunga na vikundi vya mazoezi na Serikali itatimiza wajibu wake wa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi kote nchini.” 

Wananchi wamekuwa na mwitikio mkubwa katika kulifanyia kazi agizo hilo kwa kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi ambao umeongeza idadi ya vikundi vya mazoezi ya pamoja katika maeneo mbalimbali ya nchini. 

Hamasa ya kufanya mazoezi sasa imekuwa nzuri ambapo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto zimeanzisha utaratibu wa kuwa na bonanza, matamasha ya michezo pamoja na vilabu vya kufanya mazoezi. Hatua hii imekuwa ni chachu mpya ya kutekeleza agizo la Makamu wa Rais Mama Samia la kufanya mazoezi kwa manufaa ya afya za Watanzania. 

Akiwasilisha Bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2019/2020 ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo Dkt. Harrison Mwakyembe aliliambia bunge na Watanzania wote kuwa, miongoni mwa majukumu ya sekta ya michezo ni kuratibu na kusimamia maendeleo ya michezo nchini ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushiriki wa wananchi katika michezo.

Mojawapo ya vitu vinavyoshirikisha watu wengi kujiunga na kufanya mazoezi ni kuwa na matamasha ya michezo mbalimbali ambayo yanalenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika michezo ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi ya viungo ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi hapa nchini. 

Magonjwa hayo hutokana na mitindo isiyofaa ya maisha kama matumizi ya tumbaku, lishe duni, matumizi ya pombe kupita kiasi, pamoja na kutoshughulisha mwili au kutofanya mazoezi ya viungo mara kwa mara. Magonjwa kama kisukari, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo na mishipa, saratani, pumu na magonjwa ya akilini miongoni mwa magonjwa hayo, ambapo yasipodhibitiwa huwa na sugu na yenye kuhitaji gharama kubwa kuyatibu.

Hapo awali, magonjwa hayo yalikuwa yakiwaathiri watu wenye umri mkubwa zaidi ya miaka 45, lakini kwa sasa yanazidi kuathiri watu watu wengi wakiwemo watoto wenye umri mdogo. 

Naibu Wiziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza hivi karibuni akiwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza lililofanyika Novemba 09, 2019 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma alihimiza watu kuchukua uamuzi wa kufanya mazoezi ili kujenga afya zao. 

“Mazoezi ni jambo lolote linalohusisha misuli na kusababisha kuongezeka kwa mapigo ya moyo na kasi ya kupumua. Wataalam wa afya wanasema kuwa kiwango cha mazoezi kinacholeta faida ni mazoezi yasiyopungua dakika 30 kwa siku angalau siku tatu kwa wiki na yanayomfanya mtu kutokwa na jasho” alisisitiza Naibu Waziri Shonza.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri Shonza watumishi wanaofanya kazi ofisini wametakiwa kuongeza bidii ya kufanya mazoezi kulingana na mtindo wa maisha ya mtumishi mmoja mmoja kuendana na hali yake ya maisha.

Kwa watumishi wa umma na sekta binafsi pamoja na watu wengine wanaotumia magari, wanapaswa kupanga shughuli ambazo zitawafanya kila siku watembee kwa miguu, wanaoishi au kufanya kazi ghorofani wajitahidi na wajizoeshe kutumia ngazi kila siku badala ya lifti, mtu anapokwenda mahali popote watumie njia ndefu kutembea badala ya njia ya mkato pamoja na kupunguza muda wa kutazama televisheni, badala yake muda huo utumike kufanya shughuli zinazotumia viungo vya mwili kama kufua, kuosha vyombo, kuosha gari, kusafisha nyumba, kazi za bustani na kufyeka majani ambazo zinasaidia kujenga utimamu wa mwili.

Naibu Waziri Shonza ametoa rai kwa waajiri kuboresha mazingira ya kazi kwa kuhakikisha watumishi wao wanashiriki katika michezo na kufanya mazoezi hata maeneo yao ya kazi na kutoa mfano wa kuanzisha timu mbalimbali za michezo na kutenga siku maalum katika mwezi kwa ajili ya mabonanza ya michezo. Mazingira rafiki ya kufanyia mazoezi kazini ni pamoja kutenga vyumba vya mazoezi na na kununua vifaa vya michezo. Hatua hiyo itaimarisha afya za watumishi na kupunguza gharama za matibabu katika taasisi husika. 

Aliongeza kuwa ili kufanya mazoezi kuwa endelevu, maafisa michezo na utamaduni wa mikoa na wilaya wana wajibu wa kuongeza uhamasishaji na uundaji wa vikundi vya mazoezi ya pamoja katika maeneo yao.

Wizara nyingine zenye uhusisano na mchango katika kufananikisha wananchi kufanya mazoezi ni Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Wizara hizo zina mamlaka ya kusimamia na kuweka mazingira bora ya watu kufanya mazoezi kwa kuendelea kutenga viwanja vya michezo na kuzuia uuzaji wa maeneo ya wazi hususani viwanja vya michezo na kuboresha barabara za waenda kwa miguu na baiskeli ili kuhamasisha watu kutembea na kuongeza usalama wa mazoezi.

Aidha, mamlaka za usafiri, zinawajibu wa kuboresha usafiri wa jumuiya ili kuongeza idadi ya watu wanaotumia usafiri wa jumuiya kwa sababu tafiti nyingi zinaonesha kuwa utumiaji wa usafiri wa jumuiya unaongeza uwezekano wa kutembea na kufanya mazoezi na hivyo kupunguza magonjwa yasiyoambukiza.

Matamasha ya michezo pamoja na matamasha mengine yakiwemo ya utamaduni yanatakiwa kuwa kichocheo cha kushirikisha vitu vingi ikiwemo michezo ya jadi na mashindano ya baiskeli katika maeneo mbalimbali ambayo yana mchango mkubwa katika kutunza afya za washiriki wa michezo hiyo.

Wakati wa matamasha hayo, ni vema wananchi wahamasishwe kupima afya zao hususani wa magonjwa yasiyoambukiza kwani tiba ya mapema ina manufaa kwa kuwa inapunguza uwezekano wa watu kupatwa na madhara zaidi. Hatua hiyo inaweza kuondoa magonjwa hayo moja kwa moja. Ili kuongeza hamasa ya wananchi na wanamichezo kupima afya zao, upimaji huo unapaswa kuwa ni wa bure ili watu wengi zaidi wapate fursa ya kupimwa.

Hivi karibuni Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa mwongozo wa kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambapo mataifa yameazimia kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, (SDGs) ili kupunguza kwa theluthi moja vifo vya mapema vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ifikapo mwaka 2030.

Akizungumzia mwongozo huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tedros Adhanon Ghebreyesus alisema, “Zaidi ya nusu ya watu duniani wanaishi mijini, na idadi yao inaongezeka. Viongozi wa miji wanapaswa kuchukua maamuzi ambayo yataboresha afya za wakazi wao, ili miji iweze kuchipua na kustawi. Kila mtu anapaswa kupata huduma ambazo zitaboresha afya, huduma za usafiri wa umma ziwe salama, makazi ya nje yawe safi na salama, mlo uwezo mzuri na huduma za afya ziwe bora.”

Naye Balozi wa WHO katika kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCDs) na majeraha, Michael Bloomberg alisema kuwa shirika hilo lipo mstari wa mbele katika kusambaza mikakati hiyo duniani kote ili kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.

“Tunafanya kazi kuhamasisha uelewa miongoni mwa viongozi wa miji na watunga sera kuhusu manufaa halisi yanayoweza kupatikana pindi programu hii ya kuboresha miji inapofanya kazi.” alisisitiza Balozi Bloomberg.

Ni kweli, wataalamu wa afya wanashauri kuwa ni vema kila mtu awajibike kuitunza afya yake kwa kufuata mtindo bora wa maisha kwani afya njema ni msingi wa maendeleo. Hatua hii inaunga mkono kauli mbiu tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza inayosema “Tutembee pamoja katika kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza.” 

EAC leo imezindua rasmi Maadhimisho ya Miaka 20 tangu Kuasisiwa mwaka 1999

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) jana imezindua rasmi maadhimisho ya miaka 20 tokea kuasisiwa upya kwa Jumuiya hiyo mwaka 1999 baada ya kuvunjika kw Jumuiya hiyo mwaka 1977

Uzinduzi huo umefanywa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Balozi Liberatus Mfumukeko na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mhandisi Steven Mlote Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Jijini Arusha

Wakati wa Uzinduzi huo balozi Mfumukeko alitaja mafanikio yaliyopatikana katika Jumuiya hiyo katika Kipindi cha miaka 20 tangu kuasisiwa upya

Alisema mafanikio hayo ni ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, reli, miradi ya nishati (Umeme), miradi ya kujenga uwezo na usimamizi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Pia miradi ya kukabili na kujenga uwezo ili kuhimili mabadiliko katika nchi za EAC na pia miradi ya kuziba pengo kati ya Sera na Utendaji.Alieleza Balozi Mfumukeko

Katibu Mkuu huyo wa EAC alisema mafanikio hayo yametokana na ufadhili aidha wa misaada kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) k wa mikopo nafuu ama kama misaada ya Jumuiya hiyo

Alitaja miradi mingine ya miundo mbinu ni mradi wa upembuzi yakinifu na ujenzi wa mradi wa barabara ya Nyakanazi-Kasulu-Rumange hadi Bujumbura

Pia EAC inatekeleza mradi kwa ufadhili wa AfDB kupitia nchi wanachama za EAC wa barabara ya Lusahunga-Rusumo-Kayonza,Masaka-Mutukula-Kyaka hadi Rugen

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo alisema Mkoa wa Arusha ni moja ya Mikoa iliyonufaika zaidi na miradi iliyotekelezwa na EAC kupitia ufadhili wa AfDB

Alitaja barabara hizo kuwa ni barabara ya Arusha hadi Namanga, Sakina hadi Tengeru, Barabara ya Bye Pass ya Kutoka Ngaramtoni hadi Usa River

Mafanikio mengine ya Jumuiya hiyo ni utekelezaji wa miradi ya Kilimo na Viwanda katika nchi wanachama za EAC miradi ambayo inatekelezwa kwa msada wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Alieleza Katibu Mkuu huyo wa EAC

Alisema Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo na Viwanda ni mambo ya muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Watu wan chi za Afrika ya Mashariki

‘Uchumi wa nchi hizi za EAC unategemea sekta ya Kilimo na Viwanda sekta ambazo ndizo mhimuli na nguzo kuu ya Uchumi wa Watu wake unaochangia asilimia 80 hadi 90 ya idadi ya watu waliomo katika nchi hizi’ Alisisitiza Balozi Mfumukeko

Alisema ‘Mafanikio katika kilimo ni muhimu kwa ajili ya kuwainua wananchi kuondokana na hali ya Umaskini .Pia Sekta hii inaajiri zaidi ya asilimia 80 ya wananchi kwani wengi wa wananchi hawa wanaishi maeneo ya Vijijini hivyo sekta hii inasaidia kuboresha Maisha ya wananchi wa mijini na Vijijini’

Hata hivyo Katibu Mkuu hali ya uchumi katika nchi hizi bado ulikuwa dhaifu hivyo ushirikiano wa mataifa haya utasaidia zaidi kujenga uchumi wa wananchi wa EAC

Alisisitiza kwamba’ watu mkiwa kitu kimoja utaimarisha zaidi nguvu katika kujenga uchumi imara na hivyo kuinua pato la nchi wanachama za EAC ambapo kwa sasa pato la nchi hii ni GDP 150’

Aidha alisema maendeleo ya mataifa yote duniani hata yale yaliyopiga hatua katika ukuaji wa uchumi wan chi hizo yanategemea zaidi ushiriki wa sekta binafsi

Katika kutekeleza programu mbalimbali mbali na sekta za miundo mbinu na nishati EAC imefanikiwa katika kutekeleza miradi ya elimu na afya kwa ufadhili wa benki hiyo

Pia ametaja mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 20 ya EAC ni kuanzishwa kwa mtangamano wa Soko la Pamoja, Ushuru wa Forodha pamoja na kuondoa Vikwazo mbalimbali vya kibiashara na Uingiaji wa watu kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine na pia kuondoa Vikwazo vya Visa

Kwa lengo la kuharakisha na kukuza biashara katika nchi wanachama za EAC pamoja na kupitisha sharia ya kuwa na sarafu moja EAC pia imeanzisha tume ya takwimu kwa nchi wanachama .Alisisitiza Katibu Mkuu

Aidha alifafanua kwmaba mafanikio mengine ni pamoja na kuwa na Shirikisho moja la Kisiasa na hadi sasa mchakato wa Katiba umezinduliwa mjini Kampala Uganda Novemba 18 na Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museven

Pia EAC imefanikiwa kushurikiana katika sekta ya afya kwa kuwa na maabara zinazotembea katika nchi wanachama ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko ukiwemo ugonjwa hatari wa EBOLA

Hata hivyo Katibu Mkuu Mfumukeko alisema Mkutano wa Wakuu wan chi wanachama za EAC ambao ulikuwa ufanyike Novemba 30 mwaka huu 2019 hautafanyika nabadala yake mkutano huo utafanyika kati ya Januari na February mwakani 2020

Alisema ili mkutano wa wakuu wan chi ufanyike ni lazima Wakuu wan chi zote wanachama wahudhurie.Hata hivyo hakuweza kuelezea kwa kina Sababu zilizofanya mkutano huo kuahirishwa

Heri ya Siku Ya Mtoto Duniani kutoka Benki ya NMB

$
0
0

Heri ya #SikuYaMtotoDuniani

Katika kuadhimisha #SikuYaMtotoDuniani, jengo letu la Benki ya NMB Makao Makuu liliwasha taa za bluu kuunga mkono Shirika la uniceftanzaniakatika maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 30 ya Mkataba juu ya Haki za Mtoto

Ni wakati wa kuwaunga mkono na kuwawezesha watoto na vijana ambao wanasimamia na kudai haki zao kote Ulimwenguni ni sasa.


#KwaKilaMtoto, Kil haki inatimizwa!


TANESCO ARUSHA YAWAONDOA WALIOJENGA MAKAZI YA KUDUMU CHINI YA MIUNDOMBINU YA NJIA YA KUPITISHA UMEME, YATOA ANGALIZO

$
0
0

Na Woinde Shizza Michuzi TV mArusha

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco)Mkoa wa Arusha limefanya operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara na wananchi waliojenga makazi ya kudumu katika miundombinu inayosafirisha umeme mkubwa wamsongo wa KV 66.

Umeme huo unaotoka Kituo cha kufua umeme cha Nyumba ya Mungu kuleta mkoani Kilimanjaro hadi mkoani Arusha.Katika operesheni hiyo shirika hilo limevunja zaidi ya maduka 32 na kuwaondoa wamachinga na wafanyabiashara wa vyuma chakavu zaidi ya 20.

Akizungumza wakati wa operesheni hiyo, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha ,Mhandisi Herin Mhina amesema wameamua kufanya hivyo baada ya wananch kukaidi kuondoka kwa hiyari katika maeneo hayo licha
ya uongozi wa shirika hilo kufanya mazungumzo nao na kuwapa
tangazo la notisi miezi miwili.

Amesema walitoa tangazo la kuwataka waliokaa chini ya miundombinu hiyo ya umeme iliopo Kata ya Ungalimited na Daraja mbili ndani ya Halmashauri ya Jiji la Arusha Arusha.

"Taarifa zilitolewa toka miezi miwili iliyopita ya kuanza kuwaondoa wafanyabiashara wachache walikubali na walioondoa biashara zao na wengine baadhi walikaidi na kuendelea kufanya biashara zao maeneo hayo na ndio maana wameamua kufanya operesheni ya kuwaondoa.

Amebainisha eneo hilo ni hatarishi maana linapitisha umeme ukubwa ambao ni wa msongo wa kv 66 ambapo laini hiyo iliyojengwa mwaka 1968 na likuwa inatoa umeme kituo cha kufua na kuzalisha umeme cha Nyumba ya Mungu kutoka mkoani Kilimanjaro hadi hapa Arusha pamoja

na laini ingine inayopitisha umeme wa msongo wa kv 34.
Amesema kwa mujibu wa sheria za Tanesco wananachi hawatakiwi kufanya biashara yeyote chini ya laini hizo kwani zinaweza kuleta madhara makubwa kwa maisha yao.

"Kama mnavyoona hii laini imevamiwa kwa maana ya watu kuweka shughuli chini ya laini, mkiangalia kwa mbele kunanyumba zimeingia chini ya laini kabisa ,hii laini inatakiwa iwe na korido ya mita 10 kila upande kutokana na ukubwa wake wa msongo wa kv 66.Ndio maana tumeamua kuja kuwatoa na hii sio kwa ajili ya Tanesco tu bali kwa ajili ya usalama wa maisha ya wananchi hawa,"amesema.

Ameongeza kuwa mbali na njia hiyo ya umeme kuna laini zingine mbili
zilizovamiwa ikiwemo ya Monduli ambako kuna watu wameisonga.Laini hiyo ni ya msongo wa Kv 33 na inaitaji korido ya nafasi ya mita tano kila upande ,hivyo ametoa mwito kwa wanachi waliojenga nyumba zao

chini ya miundombinu ya umeme waondoke ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.Amesema wakati wa operesheni hiyo, Mkuu wa kitengo cha usalama sehemu pa kazini Tanesco makao makuu Mhandisi Alexander Budigila amesema operesheni hiyo  halijaanzia katika maeneo hayo pekee bali ni muendelezo wa utekelezai wa sheria ya kutojenga chini ya miundo mbinu ya umeme.

"Sheria hii inatekelezwa nchi nzima, miundo mbinu ya umeme ya TANESCO inatakiwa ilindwe na wananchi wote na sio kuwategemea watumishi wa Tanesco peke yao kwani miundombinu hii ndio inayofanya hata uchumi wa wananchi ukue,"amesema.

Ametoa mwito kwa wananchi wote wazingatie matangazo yanayotolewa na TANESCO kwani ni kwa ajili ya usalama wao na mali zao.Kwa upande wake Ofisa Biashara Jiji la Arusha Godfrey Edward amewataka wafanyabiashara licha ya kufanya biashaa waangalie kwanza sehemu wanazofanyia biashara kama ni salama.

Kuhusu wafanyabiashara ambao mali zao zimechukuliwa wakati wa operesheni hiyo wazifuatilie yadi ya Halmashauri ya Jiji la Arusha ili walipe faini ya Sh.50000 na kisha kurejeshewa.
 Mafundi kutoka shirika la Umeme Tanesco mkoa wa Arusha wakiendelea kubomoa vibanda mbalimbali  nantumba vilivyojengwa chini ya njia za umeme mkubwa wa KV 66 unaopita katika kata ya Ungalimited pamoja na
Daraja mbili.(picha na Woinde Shizza,Arusha)
 wafanyakazi wa tanesco wakipakia baadhi ya vitu vilivyokuwa vimewekwa chini ya miundombinu ya umeme mkubwa tayari kanisa kupeleka Katika yadi ya jiji la Arusha

  wafanyakazi wa tanesco mkoa wa Arusha wakipakia kibanda katika gari ya shirika la umeme tayari kabisa kwa kupeleka katika yadi ya halimashauri ya jiji la Arusha ,vitu hivyo vitakaa hapo hadi wamiliki wao wakakomboe 
 Msimamizi wa njia ya kusimamisha umeme kilimanjaro ma Arusha Mhandisi  Pius Josephati akiendelea kuwapimia mita kutoka katika njia za umeme wananchi hao waliojenga kando ya njia hiyo ambapo alibaonisha
kutoka katika nguzo kubwa ya umeme mwamanchi anayakiwa ahache mita kumi(picha na Woinde Shizza,Arusha).

KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI ERICK KABENDERA MAZUNGUMZO YANAENDELEA KATI YA UPANDE WA UTETEZI NA DPP KUHUSU KUKIRI KOSA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Globu ya jamii

UPANDE wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wako katika mazungumzo na DPP kuhusu kukiri kosa lake lakini bado hawajafika muafaka.

Wakili Jebra Kambole anayemtetea Kabendera, ameeleza hayo leo Novemba 20,mwaka 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Mapema Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Janeth Mtega kuwa upepelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Wakili Kambole aliieleza Mahakama kuwa maombi waliyowasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuwa bado wako katika mazungumzo bado hawajafika muafaka, yakikamilika wataitaarifu Mahakama.

Akijibu hoja hiyo Wakili Simon alidai kuwa ni kweli kuna maombi hayo yaliyowasilishwa na upande utetezi ambayo wanayafanyia kazi yatakapokamilika watawataarifu. Hakimu Mtega amahirisha kesi hiyo mpaka Desemba 4, mwaka huu itakapotajwa tena.

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh.milioni 173.

Inadaiwa katika mashtaka ya kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Pia inadaiwa kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya Sh.173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Pia Kabendera inadaiwa alitakatisha Sh.173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji kodi.

AfDB YARIDHISHWA NA UJENZI WA MRADI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME CHA ZUZU MKOANI DODOMA

$
0
0
Muonekano wa mradi wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, Jijini Dodoma unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).
Kamishna Msaidizi wa masuala ya Nishati ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya AfDB, Bw. Amos Cheptoo (kushoto), katika chumba cha mitambo ya kupozea umeme katika mradi wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, Jijini Dodoma.
Mratibu wa mradi wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, Jijini Dodoma, Mhandisi Peter Kigandye (wa kwanza kushoto), akieleza utekelezaji wa mradi wa Kituo cha Umeme cha Zuzu ambapo unatarajia kukamilika Februari, 2020, wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bw. Amos Cheptoo (kushoto) ya kukagua mradi huo Jijini Dodoma.(Picha na Peter Haule, WFM, Dodoma)


Na Peter Haule, WFN, Dodoma

Benki ya Maendeleo ya Afrika – AfDB imeridhishwa na kasi ya maendeleo ya mradi wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kinachofadhiliwa na Benki hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan- JICA.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya AfDB, Bw. Amos Cheptoo, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Kituo hicho kilichopo katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma.

Bw. Cheptoo alisema kuwa amejionea kazi nzuri inayofanywa na Mkandarasi ya kuhakikisha mradi huo unakamilika Februari, 2020 na kutumika kikamilifu katika kupoza na kusambaza umeme kwa manufaa ya Tanzania na nchi jirani.

Alisema kuwa mradi huo utakua na tija zaidi baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere unaotarajia kuzalisha zaidi ya Megawati 2000, hivyo kuifanya miundombinu ya kupoza umeme kutumika kimailifu.

Mkurugenzi huyo wa AfDB alisema umeme ndio nyenzo muhimu katika ukuzaji wa uchumi na uendelezaji wa viwanda katika nchi za Afrika, kukamilika kwa miradi ya umeme kutasaidia uwepo wa umeme wa kutosha hasa katika nchi za Afrika mashariki na kusini mwa Afrika.

Serikali ya Tanzania imechukua hatua nzuri za kuboresha miundombinu wezeshi ya uzalishaji hasa Dodoma ambapo ndio Makao Makuu ya nchi.

Kwa upande wake mratibu wa mradi huo Mhandisi Peter Kigandye alisema kuwa, mradi huo utakuwa na uwezo wa kushusha umeme kwa Kilovoti 400 na kupoza umeme wenye uwezo wa takribani megawati 400 kisha kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali mkoani Dodoma.

Gharama ya mradi huo unajumuisha mradi mwingine uliopo Singida na gharama zake ni dola za Marekani milioni 53 ambazo zimetolewa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania, Benki ya AfDB na Shirika la JICA ambapo Kituo cha Kupozea Umeme cha Zuzu kinagharimu takribani dola za Marekani milioni 22.

Aidha Kamishna Msaidizi wa masuala ya Nishati ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati Mhandisi Innocent Luoga, ameishukuru Benki ya AfDB kwa kusaidia uboreshaji wa miundombinu hasa ya umeme kwa kuwa miradi hiyo itakapokamilika, utazinufaisha pia nchi za Zambia, Botswana na hata Afrika ya Kusini, kupitia mtandao wa umeme wa kusini

Amewataka wawekezaji walio na nia ya kuwekeza Dodoma kutumia fursa ya upatikanaji wa umeme wa uhakika kuwekeza hasa katika viwanda vikubwa na vidogo kwa kuwa mazingira ya uwekezaji yapo vizuri.

Mhandisi Luoga ameiomba Benki ya AfDB kusaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya usambazaji zaidi wa umeme katika Mkoa wa Dodoma na viunga vyake ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kulifanya jiji kuwa na hadhi stahiki.

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR DK.SHEIN AZUNGUMZA NA WAZEE WA CCM WA WILAYA YA KUSINI UNGUJA

$
0
0
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wazee wa CCM wa Wilaya ya Kusini Unguja wakati wa ziara yake, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo 20-11-2019.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.Dr. Abdalla Juma Mabodi akisisitiza jambo wakati wa mkutano na Wazee wa CCM wa Wilaya ya Kusini Unguja wakati wa ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman, alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi wakati wa hafla ya ziara yake kuzungumza na Wazee wa CCM wa Wilaya ya Kusini Unguja.
WAZEE wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kusini Unguja wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, (hayupo pichani) wakati akizungumza na Wazee hao katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo 20-11-2019.
KATIBU wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Ndg.Hafidh Hassan Mkadam akisoma risala ya Wazee wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo 20-11-2019
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.MheDk.Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa Risala ya Wazee wa CCM wa Wilaya ya Kusini Unguja na Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo.Ndg.Hafidh Hassan Mkadam, wakati wa ziara yake kuzungumza na Wazee wa CCM Zanzibar mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo.20-11-2019.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa zawadi ya kofia iliyotolewa na Wazee wa CCM wa Wilaya ya Kusini Unguja wakati wa ziara yake kuzungumza na Wazee wa CCM Zanzibar mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo.20-11-2019.


Picha na Ikulu)

KAMPENI YA LINDA ARDHI YA MWANAMKE KUZINDULIWA KESHO JIJINI DAR

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

KAMPENI ya "Linda Ardhi ya Mwanamke"  inayotekelezwa na asasi 26 za kiraia ambazo zinajihusisha na masuala ya ardhi kote nchini, kesho Novemba 21 zitazindua rasmi kampeni  hiyo huku mgeni rasmi wa hafla hiyo akitegemewa kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kampeni hiyo Tike Mwambipile amesema; Tanzania imekuwa nchi ya Kwanza kuendesha kampeni hiyo katika ngazi ya kimataifa na kuwezeshwa na mashirika ya LANDESA ulimwenguni, Habitat for Humanity, Huairou Commission, Benki ya dunia pamoja na asasi za kiraia ambazo zitafanya tafiti za kina zinazolenga kuleta mabadiliko ya umiliki wa Ardhi baina ya wanawake na wanaume.

Amesema kuwa kuchaguliwa kwa Tanzania kuendesha kampeni hiyo ni kutokana na sheria nzuri za masuala ya Sheria licha ya kuwa na changamoto chache za utekelezaji.

Time amesema kuwa malengo ya kampeni hiyo ni kufunga umbwe lililopo kati ya sera, sheria na taratibu za maisha ya kila siku ya wanajamii ikiwemo kubadilisha fikra za wanajamii kutoka katika mila kandamizi zinazozuia wanawake kumiliki ardhi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi (LANDESA) na mratibu wa kampeni hiyo Monica Mhoja amesema kuwa kampeni hiyo imejikita katika mambo makuu manne ikiwemo kuondoa mila na desturi potofu zinazowakwamisha wanawake kupata haki zao katika ardhi pamoja na kuwawezesha wanawake kutumia ardhi zao kwa manufaa ya kiuchumi.

Vilevile amesema kuwa kupitia kampeni hiyo wamejizatiti kuongeza ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi na hilo ni pamoja na haki za wanawake za umiliki wa ardhi.

Amesema kuwa kampeni hiyo imedhamiria kuwawezesha wanawake kumiliki na kufaidi mapato yatokanayo na ardhi.

"Kuna baadhi ya maeneo wanawake huona ni kawaida kutoshirikishwa katika suala zima za umiliki wa ardhi na hiyo hutokana na kutokuwa na uelewa kuhusiana na usawa wa jinsia katika umiliki wa ardhi" ameeleza.

Amesema kuwa kupitia kampeni hiyo wanaamini kuwa wanawake wengi watapata maarifa ya kuelewa haki zao katika umiliki wa ardhi na haki za upatikanaji wa ardhi.

Asasi 26 za kiraia zitakazoshiriki katika kampeni hizo ni pamoja na TAMWA, SHIVYAWATA, LANDESA, TGNP mtandao na TALA.
Mratibu wa Kampeni ya Linda Ardhi ya Mwanamke Monica Mhoja (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Kampeni hiyo ambayo imelenga kuwakomboa wanawake kuhusiana na suala zima la umiliki wa ardhi, kulia ni Mwenyekiti wa kampeni hiyo Time Mwambipile na anayefuatia ni Mkurugenzi wa TAMWA Rose Reuben.

SERIKALI KUCHIMBA VISIMA KUMI KUKABILIANA NA ADHA YA MAJI MEATU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu

Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali itachimba visima kumi vya maji mara moja katika eneo la Mto Semu Kijiji cha Magwila wilayani Meatu na kujenga mtandao wa bomba kutoka katika visima hivyo mpaka mjini Mwanhuzi wilayani humo Mkoani Simiyu, ili kukabiliana na adha ya maji kwa wananchi baada ya kukauka kwa bwawa la Mwanyahina.

Prof. Mbarawa amesema hayo jana Novemba 19, 2019 wakati akizungumza na wananchi wa Mwanhuzi mara baada ya kutembelea na kuona Bwawa la Mwanyahina lililokauka ambalo ndiyo chanzo kikuu cha maji katika Mji huo na eneo la Mto Semu kilipo kisima kinachotumiwa sasa, ambapo watu wanachota maji kwa magari na kuwauzia wananchi mjini Mwanhuzi.

“ Mhe.Rais amenielekeza kwamba tutachimba visima kumi haraka kutoka kule ambako maji yanachotwa sasa, tutajenga mtandao wa bomba kutoka kwenye visima mpaka hapa mjini, ili maji yale yatolewe visimani na kuletwa kwenye mfumo wa maji wa hapa mjini,” alisema Mbarawa.

Katika hatua nyingine Mbarawa ameelekeza Wataalam wa Bonde la Ziwa Victoria kufanya utafiti katika eneo hilo ili kujua wingi wa maji na kuwahakikishia wananchi kuwa kwa sasa Wizara ya maji imetoa maboza makubwa matatu kwa ajili ya kusaidia kubeba maji kutoka kisima na kusambaza kwa wananchi, huku akiagiza ukarabati wa Bwawa la Mwanyahina kufanyika kwa kutoa tope lililojaa kwenye bwawa hilo.

Awali akitoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa maji, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani amesema Bwawa la Mwanyahina limekauka kutokana na kujaa tope na ukame uliotokea wilayani humo katika msimu wa mvua wa mwaka 2018/2019.

Aidha, Dkt. Chilongani ameomba Wizara ya maji iweze kutoa kipaumbele kwa miradi yote ya maji iliyosanifiwa iweze kutekelezwa katika Wilaya ya Meatu, ili kuongeza hali ya upatikanaji wa maji vijijini na mjini.

Kwa upande wao wananchi wa Mji wa Mwanhuzi wameishukuru Serikali kwa kukubali kuwachimbia visima ambavyo vitawasaidia kuondokana na adha maji baada ya Bwawa la Mwanyahina kukauka na kusababisha wao kununua ndoo moja ya lita 20 kwa shilingi 100 hadi 200.

“Sasa hivi tunauziwa ndoo ya lita ishirini kwa shilingi 200, tunaishukuru Serikali kuona kilio chetu, pia tunamshukuru Waziri wetu wa Maji kwa mpango aliokuja nao wa kutuchimbia visima na kutuletea maji hapa mjini, tunaomba mpango huu ufanyike haraka, ili tuondakane na shida ya maji tuliyonayo sasa,” alisema Mariam Kashinje mkazi wa Mwanhuzi.

“Binafsi namshukuru Mbunge wetu kwa kutoa gari lake ambalo linatoa huduma ya maji bure, pia tunamshukuru Mhe. Diwani wetu Zakaria kuruhusu watu kuchota maji kwenye kisima chake na kubeba kwenye maboza na sisi wananchi tunanunua; lakini nimefurahishwa sana na mpango wa Waziri wa Maji aliyesema Mhe. Rais anataka tuchimbiwe visima naamini tatizo hili litaisha,” alisema Mboi Ngidinga.
 Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa(mwenye miwani katikati) akipata maelezo kuhusu kisima kilichopo eneo la Mto Semu kijiji cha Magwila wilayani Meatu, ambacho kinatumiwa kutoa huduma kwa sasa kwa wananchi wa Mji wa Mwanhuzi baada kukauka kwa Bwawa la Mwanyahina ambalo ndiyo chanzo kikuu cha Maji katika Mji wa Mwanhuzi.

 Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani  (kushoto) akimuongoza Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa(wa tatu kulia) kuelekea katika kisima kilichopo eneo la Mto Semu kijiji cha Magwila wilayani Meatu Novemba 19, 2019, ambacho kinatumiwa kutoa huduma kwa sasa kwa wananchi wa Mji wa Mwanhuzi baada kukauka kwa Bwawa la Mwanyahina ambalo ndiyo chanzo kikuu cha Maji katika Mji wa Mwanhuzi.

 Mbunge wa Jimbo la Meatu Mhe. Salum Khamis (mwenye kofia) akimuonesha jambo Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa(mwenye miwani kulia)alipotembelea kuona eneo la chujio la Maji katika Mji wa Mwanhuzi wilayani Meatu Novemba 19, 2019.

 Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani  (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa(wa pili kulia) kuhusu Bwawa la Mwanyahina chanzo kikuu cha Maji katika Mji wa Mwanhuzi ambalo limekauka kwa sasa, wakati wa ziara yake Novemba 19, 2019.

 Sehemu ya Bwawa la Mwanyahina chanzo kikuu cha Maji katika Mji wa Mwanhuzi ambalo limekauka kwa sasa ambalo Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa ameagiza lifanyiwe ukarabati kuondolewa tope.
 Baadhi ya wananchi wa Mjini Mwanhuzi wilayani Meatu wakipata huduma ya maji kutoka kwenye magari yanayosomba maji kutoka katika Kisima baada ya changamoto ya maji katika mji huo iliyosababishwa kukauka kwa Bwawa la Mwanyahina.
 aadhi ya wananchi wa Mji wa Mwanhuzi wakiwa katika foleni ya kupata huduma ya maji kutoka kwenye magari yanayosomba maji kutoka katika Kisima baada ya changamoto ya maji katika mji huo iliyosababishwa kukauka kwa Bwawa la Mwanyahina.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa(wa tatu kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya  Meatu, Mhe. Joseph Chilongani moja ya gari litakalotumika kwa dharura kusomba maji kutoka kisima kilichopo eneo la mto Semu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi kabla ya kuchimbwa kwa visima kumi , wakati wa ziara yake Novemba 19, 2019.

WAZAZI NA WALIMU WAJENGEENI WATOTO UWEZO WA KUZIISHI NDOTO ZAO

$
0
0
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Afrika Daniel Urioh.Picha na Vero Ignatus.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika mafunzo ya kubadili Tabia na Uongozi yaliyofanyika hivi karibuni katika Shule ya Sekondari ya Connerstone iliyopo Ngaramtoni mkoani Arusha.
Wanafunzi waliohudhuria katika mafunzo ya Kubadili tabia na uongozi yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Connerston wakishangilia baada ya mwenzao kuonyesha kipaji chake (hayupo pichani)

Wanafunzi waliohudhuria katika mafunzo ya Kubadili tabia na uongozi yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Connerston wakifuatilia kwa makini kile kilichokuwa kinaendelea katika Mafunzo hayo.


Na.Vero Ignatus,Arusha

Ikiwa leo ni siku ya watoto duniani, jamii imetakiwa kuwajengea uwezo Watoto ,kuziishi ndoto zao na kutambua kuwa Watoto huanza Maisha pale wanapozaliwa ,hivyo kila hatua iwe wezeshi kwa watoto kufikia ndoto zao.

Limekuwa ni jambo la kawaida katika jamii kubwa za kiafrika ,wazazi au walezi kuwalazimisha Watoto wao kufikia ndoto ambazo wao hawajazifikia, na haswa kwa kutumia mifumo rasmi kama ya Elimu ambayo inamuandaa mtoto kuwa kama jamii inavyotaka na siyo kama apendavyo yeye mwenyewe

'’Utamsikia mzazi akimlazimisha mtoto wake kwa kumwambia nataka usome uje kuwa daktari,askaripolisi,Mwanajeshi,mwanasheria,mwalimu,bila kumsikiliza mtoto anapenda kuja kuwa nani ili aweze kumtilia mkazo Zaidi katika jambo lile alipendalo’’

Daniel Urioh ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Afrika amewaambia waandishi wa habari kuwa wazazi wawe na muda wa kukaa na watoto wao, wapate kuwasoma, kujua vitu wanavyoelekea kuvipenda waanze kutilia mkazo ,ili waweze kuwakutanisha na watu ambao wamefanikiwa katika sekta hizo, ili kuwajengea hamasa za kufikia ndoto zao.

''Mazingira ya mtoto huanzia nyumbani pamoja na wale wanaomzunguka,mifumo sikivu kwa ndoto za watoto siyo kuwafanya waishi kwa matakwa ya kile wanachokipenda wazazi , jambo ambalo linapelekea mtoto kukwama kufikia malengo yake pindi anapokuwa mtu mzima na kuanza kujitegemea’’alisema Mkurugenzi 

Ametoa wito kwa walimu ambao wananafasi kubwa katika Maisha ya Watoto,kwa kuwa nao muda mwingi zaidi katika mazingira yao haswa shuleni kuliko mtu mwingine yeyote, watumie nafasi hiyo kulea ndoto, vipaji, ubunifu wawatoto hao kwa mbinu zisizodhalilisha,kuumiza au kuwakatisha tamaa (non-violence strategies)

‘’Baadhi ya walimu wamekuwa na tabia ya kuua ndoto, vipaji na ubunifu wa Watoto kwa lugha za kidhalilishaji,za kuumiza na kukatisha tamaa Watoto jambo ambalo siyo zuri kabisa’’alisema Daniel.

Aidha katika kuadhimisha siku ya Watoto duniani Elimu ya Afrika inachukua jukumu la kuleta suluhu kwa kutumia programu na makongamano ya kuwatia moyo, kuwatengenezea majukwaa ya kujifunza na kuonyesha vipaji na bunifu zao.

Amesema kuwa Vijana hupata nafasi kushirikiana kwa pamoja, kuhamasishana kuleta majibu ya changamoto zinazowazunguka na mwisho hutumia vipaji kuburudisha pia.

Siku ya watoto duniani huadhimishwa kila mwaka duniani ambapo ilianzishwa na mwaka 1954 na husheherekewa tarehe 20 mwezi wa novemba kila mwaka kwaajili ya kuhamasisha na kueneza uelewa miongoni mwa Watoto duniani.

KAMPENI YA LINDA ARDHI YA MWANAMKE KUZINDULIWA KESHO JIJINI DAR

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

KAMPENI ya "Linda Ardhi ya Mwanamke"  inayotekelezwa na asasi 26 za kiraia ambazo zinajihusisha na masuala ya ardhi kote nchini, kesho Novemba 21 itazindua rasmi kampeni  hiyo huku mgeni rasmi wa hafla hiyo akitegemewa kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa kampeni hiyo Tike Mwambipile amesema; Tanzania imekuwa nchi ya Kwanza kuendesha kampeni hiyo katika ngazi ya kimataifa na kuwezeshwa na mashirika ya LANDESA ulimwenguni, Habitat for Humanity, Huairou Commission, Benki ya dunia pamoja na asasi za kiraia ambazo zitafanya tafiti za kina zinazolenga kuleta mabadiliko ya umiliki wa Ardhi baina ya wanawake na wanaume.

Amesema kuwa kuchaguliwa kwa Tanzania kuendesha kampeni hiyo ni kutokana na sheria nzuri za masuala ya Sheria licha ya kuwa na changamoto chache za utekelezaji.

Time amesema kuwa malengo ya kampeni hiyo ni kufunga umbwe lililopo kati ya sera, sheria na taratibu za maisha ya kila siku ya wanajamii ikiwemo kubadilisha fikra za wanajamii kutoka katika mila kandamizi zinazozuia wanawake kumiliki ardhi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi (LANDESA) na mratibu wa kampeni hiyo Monica Mhoja amesema kuwa kampeni hiyo imejikita katika mambo makuu manne ikiwemo kuondoa mila na desturi potofu zinazowakwamisha wanawake kupata haki zao katika ardhi pamoja na kuwawezesha wanawake kutumia ardhi zao kwa manufaa ya kiuchumi.

Vilevile amesema kuwa kupitia kampeni hiyo wamejizatiti kuongeza ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi na hilo ni pamoja na haki za wanawake za umiliki wa ardhi.

Amesema kuwa kampeni hiyo imedhamiria kuwawezesha wanawake kumiliki na kufaidi mapato yatokanayo na ardhi.

"Kuna baadhi ya maeneo wanawake huona ni kawaida kutoshirikishwa katika suala zima za umiliki wa ardhi na hiyo hutokana na kutokuwa na uelewa kuhusiana na usawa wa jinsia katika umiliki wa ardhi" ameeleza.

Amesema kuwa kupitia kampeni hiyo wanaamini kuwa wanawake wengi watapata maarifa ya kuelewa haki zao katika umiliki wa ardhi na haki za upatikanaji wa ardhi.

Asasi 26 za kiraia zitakazoshiriki katika kampeni hizo ni pamoja na TAMWA, SHIVYAWATA, LANDESA, TGNP mtandao na TALA.
Mratibu wa Kampeni ya Linda Ardhi ya Mwanamke Monica Mhoja (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Kampeni hiyo ambayo imelenga kuwakomboa wanawake kuhusiana na suala zima la umiliki wa ardhi, kulia ni Mwenyekiti wa kampeni hiyo Time Mwambipile na anayefuatia ni Mkurugenzi wa TAMWA Rose Reuben.

MAADHIMISHO YA SIKU YA HAKI ZA WATOTO DUNIANI

$
0
0
Wanafunzi wakionyesha bango lenye ujumbe wa haki za watoto
mara baada ya kuzindua ajenda kuhusu haki za watoto uliofanyika kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Watoto kutoka Shule mbalimbali za Jijini Dar es Salaam, wakiwa katika
picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi, na viongozi wengine wa Serikali katika Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Watoto kutoka Kikundi cha Safi Theater cha Jijini Dar es Salaam,
wakionesha jinsi watoto wa shule wanavyofanyiwa ukatili wa kijinsia na
waendesha Bodaboda na Daladala na kukatishwa masomo, igizo lilitolewa katikaMaadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo chaMikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi (katikati),
akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Ally Possi, mara baada ya kuwasili katika Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi, baada ya kuwasili katika Sherehe za Kuadhimisha ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, leo Novemba 20, 2019, ambako alialikwa kuwa mgeni Rasmi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi, akipata maelezo
kutoka kwa mtalaam kutoka Shirika la Watoto Duniani (UNICEF), katika moja ya banda lililokuwepo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile, akizungumza na Washiriki wa Sherehe za
Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo chaMikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.
Ally Possi, akizungumza na Washiriki wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala mwaka wa
Tatu, Rose Mweleka, akiwasilisha mada kuhusu jinsi ya kutekeleza haki za watoto wa kike ikiwemo kuwafundisha hatua za makuzi ili kuwawezesha kukabiliana na hali wakifikia umri husika, Mada hiyo iliwasilishwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

Picha na Idara ya Habari-MAELEZO

PRESIDENT MUSEVENI LAUNCHES NATIONAL STAKEHOLDERS CONSULTATIONS TO DRAFT CONSTITUTION FOR EAC POLITICAL CONFEDERATION

$
0
0

Ugandan President Yoweri Kaguta Museveni on Monday, 18th November, 2019 at the launch of the National Stakeholders Consultations to Draft the Constitution for the East African Community Political Confederation at State House, Entebbe, Uganda.


Ugandan President Yoweri Kaguta Museveni on Monday, 18th November, 2019 launched the National Stakeholders Consultations to Draft the Constitution for the East African Community Political Confederation at State House, Entebbe, Uganda.

President Museveni underscored the importance of the EAC attaining a Political Federation, adding that the Political Confederation was a transitional model to the Political Federation as enshrined in the Treaty for the Establishment of the EAC.

President Museveni said that the Political Federation would re-energise efforts to promote the prosperity of all East Africans which can be attained through trade and economic growth.

The Head of State said that the Political Federation would also guarantee the strategic security of smaller member countries of the Community against external threats.He further cited fraternity of all East Africans noting that the peoples of the East African region share similar cultures, languages and origins with Kiswahili as a lingua franca. 

In his remarks, EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko said that the National Stakeholders Consultations would ensure participation of EAC citizens in the integration process and particularly the Political Federation pillar.

“The drafting of the EAC Political Confederation is being undertaken by a team of Constitutional Experts nominated by the Partner States. The 18-member team is chaired by Hon. Justice Dr. Benjamin Odoki, the Chief Justice Emeritus of the Uganda,” said Amb. Mfumukeko, adding that the Confederation Constitution development process was projected to be completed in 2022 with its adoption by the Summit.

Amb. Mfumukeko said that the development of the Constitution for the EAC Political Confederation was a political process that requires high levels of inclusion and participation of stakeholders.

“Consequently, it is an expensive project requiring substantial financial investment. So far, we have been behind the schedules in the process due to insufficienct financial allocation for this project. In our estimation, the process of drafting the Constitution will require resources to the tune of US$4.8 milion,” said the SG.

The SG urged the Summit of EAC Heads of State to consider a special funding arrangement to enable the completion of the project in good time.

Speaking at the event, the Chairperson of the Team of Constitutional Experts, Hon. Justice (retired) Dr. Benjamin Odoki, disclosed that the team had already completed a comprehensive study of various confederations around the world for purposes of appreciating the concept and practice of confederations.

Hon. Justice Odoki further said that the team had also finalised a study and analysing of the EAC establishment.   

The Political Federation is the fourth and ultimate pillar in the EAC integration process after the Customs Union, the Common Market and the East African Monetary Union. In May 2017, the Summit of EAC Heads of State agreed on the Political Confederation as a transitional model to the Political Federation.

In February 2018, the Summit through the Council of Ministers constituted a team of 18 Constitutional Experts and Legislative Draftspersons to draft a Constitution for the Political Confederation. The team was tasked with developing a Draft Constitution for consideration by the Summit. At its 20th Ordinary Meeting held in Arusha, Tanzania in February 2019, the Summit requested the team to provide it with a preliminary report by November 2019.

BILIONI 127 ZATOLEWA KUCHANGIA MFUKO WA AFYA WA PAMOJA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akizungumza na wananchi waliokwenda kupata huduma katika Kituo cha Afya Hombolo Jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza jambo na Wadau wa Maendeleo wanaochangia Mfuko wa Pamoja wa Afya-HBF (hawapo pichani) walipotembelea Kituo cha Afya Hombolo Jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili upande wa kulia) akiongea jambo na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bi Mette Norgaard Dissing Spandet mapema leo walipotembelea Kituo cha Afya Hombolo kujionea hali ya utoaji huduma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wa tatu lutona kushoto) akimuonyesha Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bi. Mette Spandet maboresho ya mioundombinu yaliyofanyika katika Kituo cha Afya Hombolo Jijini Dodoma.
“Ukiwa mkubwa unawake kuwa nani?; Nataka kuwa kama wewe” (Utani) Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisalimiana na mtoto Agatha Daniel alipotembelea Kituo cha Afya Hombolo leo Jijini Dodoma.
**************************************

Na Englibert Kayombo – WAMJW, Dodoma.

Wadau wa mfuko wa Afya wa pamoja (HBF) wanaofadhili upatikanaji wa huduma za afya ngazi ya jamii wachangia Shilingi Bilioni 127 ili kuboresha huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alipofaya ziara na wadau wa maendeleo wanaochangia mfuko wa afya wa pamoja walipotembelea Kituo cha Afya Hombolo Jijini Dodoma.

“Wenzetu hawa wanaochangia mfuko wa afya wa pamoja ambao ni wadau nane mwaka huu wa 2019/20 wametuopatia Bilioni 127 wka ajili ya kuboresha huduma za afya” Amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy amesema kuwa kiasi cha Shilingi BIlioni 104 zitapelekwa kwenye Halmashauri za Wilaya na Sekretarieti za Mikoa kwa ajili ya kuboresha huduma za afya ngazi ya Jamii huku kiasi cha Shilingi Bilioni 23 kikitarajiwa kutumika kwa ajili ya kusimamia uendeshaji wa mfuko wa afya ngazi ya juu.

“Kwa hiyo tunaona hapa fedha nyingi zitakuja huku chini kwenye Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitli za Wilaya, nawashukuru sana wadau wetu wa maendeleo kwa kutupatia Bilioni 127 kwa ajili kuboresha huduma za Afya Tanzania” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Kwa upande wake Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bi Mette Norgaard Dissing Spandet amesema kuwa mfuko huo umekuwa ukisaidia uboreshaji wa huduma za afya ngaza ya jamii kwa miaka 20 sasa na wanajivunia kuwa na uhusiano wa karibu na kusaidia katika upatikanaji wa bora huduma za afya nchini.

“Tunafuraha kufikia miaka 20 ya kusaidia katika kuboresha huduma za afya nchini Tanzania na tutaendelea kufanya hivyo zaidi kwa miaka mingi inayokuja” amesema Balozi Mette Spandet.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi ambaye Jiji lake ni mnufaika wa mfuko huo wa pamoja wa afya amesema kuwa walipokea fedha kiasi cha Shilingi Milioni 500 na walizitumia vizuri kwa kuboresha na kujenga miundombinu katika Kituo cha Afya hapa Hombolo.

“Kwa shilingi Milioni 500 tumeweza kujenga nyumba ya mganga, jengo la kuhifadhi maiti, jengo la upasuaji pamoja na jengo la wodi ya kina mama” anasema Mkurugenzi Kunambi.

Mkurugenzi Kunambi amesema kuwa kwa kutumia mapato ya ndani ya Jiji la Dodoma wamefanikiwa kujenga wodi ya wototo iliyogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 63.

Mfuko wa pamoja wa afya unaoratibiwa na Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI huku wadau wa maendeleo wakiwa ni Nchi ya Switzerland, Canada, Denmark na Korea ya Kusini, Shirika la UNFPA, UNICEF na Benki ya Dunia umekuwa ukichangia kuboresha huduma za afya nchini Tanzania kwa miaka 20 sasa toka mwaka 1999 ambapo huduma za afya ngazi ya jamii zimekuwa zikiimarika mwaka hadi mwaka.

TCRA Kanda ya Mashariki yaendelea kutoa elimu Mkoa wa Morogoro

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Morogoro

Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero  amesema kuwa Wananchi wote watasajili laini za simu kwa alama za vidole kutokana na jitihada walizoweka kwa kushirikiana na wadau katika kufanikisha usajili huo.

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro, Odiero amesema zoezi la elimu pamoja na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole linafanyika katika mkoa wote wa Morogoro kwa kupita kila Kata.

Amesema katika utoaji wa elimu wanashirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),Watoa Huduma wa Kampuni za Simu za Mkononi ,Wakala wa Usajili wa Vifo na Vizazi (RITA) kwa kupata Wananchi huduma kwa pamoja.

Amesema Wananchi watumie muda wao kutafuta viambatanisho vinavyohitajika kwa wadau wengine ili waweze kusajili laini zao kwa alama za vidole.Katika utoaji elimu hiyo wamepita katika vituo vya radio vya Mkoa wa Morogoro kutoa elimu hiyo watu kujitokeza kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Aidha amesema utoaji elimu unakwenda katika mikoa yote iliyopo katika kanda ya Mashariki ambapo zoezi hilo lilishamalizika katika Mkoa wa Pwani na kutaka Wananchi wa Mkoa huo ambao hawana vitambulisho vya Taifa kufanya utaratibu wa kupata katika Ofisi za NIDA ili waweze kusajiliwa.
Kwa upande mwananchi Amina Salumu wa Manispaa ya Morogoro amesema TCRA wamefanya vizuri kuhamasisha kwa kuungana na watoa huduma wote  katika usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Aidha amesema kuwa tatizo lingine ni wao Wananchi kushindwa kufuata taratibu za kuweza kupata vitambulisho kwa wakati kwa kizingizio cha majukumu yao.

Salumu ameshauri kuwa zoezi hilo lifanyike mara kwa mara ili wote waweze kujisajiliwa wasisubiri laini zifungwe ndipo waanze kuhangaika.
 Mwananchi akisubiri kupewa namba ya kitambulisho cha Taifa kwa kuangalia mfumo aliyessjiliwa na NIDA.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero aliyesimama akiangalia kazi data waliosajiliwa na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya Namba waweze kujisajili laini za simu kwa alama za vidole katika utoaji wa elimu katika Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.
 Wananchi wakisajili laini za simu kwa alama za vidole kwa watoa huduma wa Kampuni za Simu katika utoaji elimu  Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.
Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Vaoleth Esseko akimkabidhi kitabu Cha mkataba kwa Wateja Cha TCRA wakati utoaji elimu Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.
Wananchi wakipata huduma ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.

Man Mo: Msanii aliyeingia kanisani ili atoke kimuziki

$
0
0
*Familia yake ikamkalia kooni
*Sasa achomoka na 'Mapenzi Kazi'

HAKUNA jambo lolote linaloanza kwa utelezi hapa duniani. Kila kazi ina changamoto na msoto wake. Na katika kupitia changamoto hizo, baadhi yao wanafikia kukata tamaa kabisa, licha ya kuwa na kila kitu kinachoweza kuwapatia mwangaza katika mambo wanayopigania.

Hata katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya tunachoshuhudia vijana wengi wakichanua na kujimudu kiuchumi, pia una suluba na changamoto lukuki, msoto mzito unaowakumba wasanii wengi tangu siku walipoamua kujiingiza kwenye tasnia hiyo.

Katika kuangalia vijana hao wanaopitia katika msoto mzito ni Maneno Mohamed 'Man Mo'. Kijana huyu mwenye uwezo wa juu wa kuimba na kutunga nyimbo za muziki wa kizazi kipya, anapitia katika tanuri la moto, barabara yenye miba mikali kiasi cha kuwahi kukata tamaa ya kuendelea na sanaa yake.

Ndio, hii ni kwa sababu msanii huyo licha ya kuwa kwenye sanaa kwa muda mrefu sasa, lakini mlango wa mafanikio ulionekana kuchelewa kufunguka, licha ya kuwa na kipaji cha uimbaji na utunzi wa nyimbo kali, ukiwamo wimbo wa 'Nasimama' ulioimbwa na msanii nyota Judith Wambura 'Lady JayDee', ambao uliandikwa na Man Mo.

Katika mazungumzo na Gazeti hili, Man Mo anasema kwamba alianza kujihusisha na muziki tangu alipokuwa mdogo, akimfuatilia mama yake Bi Salama Mussa Kaduga, aliyekuwa anajihusisha na sanaa katika Matukio mbalimbali haswa ya kisiasa, huko kijijini kwao Kimange, mkoani Pwani.

"Muda mwingi nilikuwa namfuatilia mama yangu katika sanaa yake, jambo ambalo lilichochea kwa kiasi kikubwa mimi kupalilia kipaji changu cha kimuziki na kuweka nia kubwa ya kuja kuwa msanii nyota duniani kama wengine.

"Pamoja na mambo mengine, msanii mwingine ambaye kwa namna moja ama nyingine aliendelea kukuza kipaji changu ni Ali Kiba, ambaye muziki wake niliuelewa, haswa nilipofanikiwa kukutana naye katika studio za Sharobaro Records za jijini Dar es Salaam zilizokuja kuvuma kwa kutoa wasanii wengi mahiri, akiwamo Bob Junior, Diamond Platnumz, Shetta, Rich Mavoco na wengineo kibao ambao mara kwa mara walikuwa wakikutana kwenye studio hizo,"Alisema Man Mo.

Msanii huyo mwenye kiu kubwa kisanaa anasema rasmi kuingia kwenye sanaa ilikuwa ni mwaka 2010 ambapo kama vijana wengine, aliamua kuondoka kijijini kwao na kuvamia jiji la Dar es Salaam, akiwa na matarajio makubwa ya kuvuna kwa kupitia muziki wa kizazi kipya.

Kwa bahati mbaya jiji lilimlaki vibaya na kumchoma na jua tangu alipofika na kuamua kukimbilia kwenye kiwanda Cha nguo Cha Urafiki ili apunguze makali ya kimaisha kwa kufanya kibarua katika kitengo cha kuchambua nyuzi.
 
Mkali huyo wa kizazi kipya anasema licha ya kufanya kibarua Urafiki, lakini hamu ya kimuziki ilikuwa kubwa na kujikuta akienda Sharobaro kurekodi wimbo wake kwa pesa yake, hata hivyo baadae uongozi wa Studio hizo ulimpa ahueni kwa kumtaka awe chini ya Sharobaro Records ili akue kimuziki. 
 
Hata hivyo anakiri uamuzi huo pia ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na bidii yake pamoja na kujituma kwa kila aina ikiwamo kufanya usafi kwenye studio hizo, akitafuta upenyo wa kuchomoka kisanaa.

"Nikiwa Sharobaro Records nilifanikiwa kurekodi nyimbo nyingi na kupata marafiki wengi ambao naweza kusema nilikua kwa kiasi kikubwa mno kulinganisha na wakati ule natokea kwetu kijijini nikiwa sina mtandao wowote kisanaa na hata kula yangu ikawa ni mashaka matupu.

"Nyimbo ambazo nilitengeneza wakati ule ni Binti wa Kibara, Binti wa Kimasai na nyingine nyingi ambazo hazikuachiwa hewani bila kusahau zile nilizoandikia wasanii wengine ukiwamo ule wa dada yangu Lady JayDee uliojulikana kama Nasimama ambao ulifanya vizuri mno katika ulingo wa Bongo Fleva,"Alisema.

Wakati anaamini anaelekea pazuri, ghafla mambo yalibadilika na kurudi tena kwenye msoto ambapo kila alilopanga lilishindwa kutimia, ikiwamo kuwapata mameneja ambao bila wao ni ngumu msanii kutokea peupe. Anasema wakati anaelekea kuchoka, akapata meneja aliyempa sharti la kuimba muziki wa injili na sio muziki wa kidunia.

"Huyu ndugu yangu alikuwa anaitwa James Albert Katagira anayemiliki shule za Tusiime, ambaye alinionea huruma na msoto wangu na kunishawishi nihamie kwenye injili ili anisimamie jambo ambalo nililitekeleza haraka, kwa sababu lengo langu lilikuwa ni sanaa.

"Nilifanikiwa kurekodi nyimbo mbili na video zake ambazo ni Jicho Langu na Nimuimbie, ambazo zilifanya vizuri katika muziki wa injili na kuanza kupata shoo nyingi katika mikoa mbalimbali kwa kuunganishwa na wasanii wengi wa muziki huo bila kusahau kushiriki makongamano mengi ya kidini,"Alisema.

Man Mo anasema muziki huo ulikuwa unampa mwelekeo mzuri, licha ya kufikia kutengwa na familia yake kwa madai alitokea katika chimbuko la waumini wa dini ya Kiislamu, hivyo jamii ilishindwa kumuelewa, wakiwamo marafiki zake waliomkosoa kwa kitendo chake cha kuacha Bongo Fleva na kukimbilia injili.

Ili jamii imuelewe akiwamo mama yake mzazi, alitumia muda mwingi kuzungumza nao, huku akikiri kuwa aliingia kanisani na kuimba injili kama njia ya kumfikisha kileleni na sio nia ya kubadili dini, ingawa anasema katika kipindi chote hicho, jamii ya kikristo na wasanii hao wameishi kwa upendo na kushirikiana kwa kiasi kikubwa, akiwamo Madame Frola ambaye alishiriki naye katika matamasha kadhaa likiwamo la Tanga Mjini akiwa kama mwimbaji wa injili.

Man Mo anasema msoto haukumuacha, kwani msaada wake uligota, hivyo kuamua kuachana kabisa na muziki, akiingia katika biashara ya kilimo pamoja na kuuza kuku, biashara ambazo zilitokana na umri kuendelea kumtupa mkono huku akishindwa kutokea peupe.

Kijana huyo mwenye ndoto na maneno mengi mdomoni mwake anasema baada ya kukaa kwa miezi kadhaa bila kujihusisha na lolote linalohusu muziki, alishtushwa na simu kutoka kwa Belo Master, aliyekuwa anafanya wimbo kwenye Studio za classic Sound chini ya mtayarishaji wake Monagenster za Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
"Wakati ananipigia simu, sikuwa na ari, lakini kwakuwa jamaa anajua uwezo wangu na alitaka nikamuimbie kiitikio, hivyo nikaenda Studio kurekodi kama alivyotaka, jambo ambalo lilianza upya kunitekenya rohoni mwangu. 

"Kwakuwa niliimba vizuri kwenye wimbo ule, viongozi wa Monagenster walivutiwa na mimi na kunivuta karibu ili waendelee kuangalia uwezo wangu ambapo walinikubali zaidi haswa kwa uwezo wangu wa kuandika nyimbo kali, ukizingatia wengi nilikuwa nawatungia, hivyo kupata upenyo rasmi,"Alisema.

Kijana huyo anasema kwa Sasa anasimamiwa kazi zake chini ya Kampuni ya African Network Entertainment (ANE) kwa kushirikiana na Monagenster kwa kupitia classic Sound ambapo hadi sasa nimeachia nyimbo mbili kali pamoja na video matata ambazo ni 'Tike na Mapenzi Kazi zinazofanya vizuri katika ulimwengu wa muziki.

Msanii huyo anayetokea kwenye familia ya watoto wanne, huku yeye akiwa wa kwanza kuzaliwa mwaka 1994 huko Kimange, anawataja wadogo zake kuwa ni Mwahija, Sauda na Muhsin huku kiwango chake cha elimu kikiwa ni kidato cha nne, akiishia kiwango hicho kutokana na kuhangaikia muziki licha ya baba yake kutamani mtoto wake asome sana, aliishia njiani.

Man Mo alisoma elimu ya msingi katika shule mbili za Kimange na Bagamoyo, wakati elimu ya Sekondari aliipata katika shule ya Air wing ya Banana, jijini Dar es Salaam, huku akisema kuwa maisha ya muziki kabla ya kutoka ni magumu yanayoweza kukatisha tamaa wasanii wengi wenye vipaji.

"Kwa sasa sina ninachokifanya zaidi ya kusikiliza ushauri wa viongozi wangu wa ANE, nikiamini kuwa uwezekano wa kupasua anga ni mkubwa kutokana na Kampuni kuwa na watu wanaojua muziki na ndoto za sisi vijana kufika mbali.

"Lengo langu ni kufanya muziki mzuri wa kibiashara, nikitumia uzoefu wangu na kipaji changu cha kuimba na kuandika nyimbo kali ili nipate mafanikio ya kutimiza ndoto zangu, ukizingatia kuwa nimesota sana, nimekula ngarambe nyingi, hivyo hakuna kinachoweza kuniweka chini tena,"Alisema Man Mo.

Man Mo anasema kuwa licha ya muziki kuwa na ushindani mkubwa, lakini ukiweka bidii unafanikiwa, huku akisema kuwa anataka kuwa msanii 'simple' kama Ali Kiba lakini afanye muziki mzuri wa biashara kama Diamond Platnumz jambo linalompa utajiri mkubwa.

Msanii huyo anaendelea kusema kwa kuwataka wasanii kufanya juhudi kubwa kuutangaza muziki wao pamoja na chipukizi kukaza msuri ili nao wafikie malengo licha ya kwamba wasanii wachanga wengi huishia njiani kwa kushindwa kwenda na kasi ya msoto katika sanaa.

Man Mo anakumbuka jinsi alivyoshindwa kuwa na maelewano mazuri na baba yake kiasi cha kununiana, kisa kuwa kwenye muziki huku maisha yakiwa magumu kwa mtoto wao, ambapo juhudi za mama yake zilikuwa zinamlainisha mzee wake japo kwa uchache.

Mwimbaji huyo mwenye ndoto kubwa anasema muziki umezidi kupiga hatua kutokana na juhudi za wasanii wenyewe wanaokwenda na mabadiliko, ikiwamo mbinu ya kutumia vizuri mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, YouTube nk, ambapo kama ilivyokuwa kwa wasanii wengine, Man Mo pia anamiliki akaunti mbalimbali zinaoenda kwa jina la manmoofficial katika mitandao mbalimbali kwa ajili ya kutangaza muziki wake pamoja na kupata ulingo wa kujadiliana na mashabiki wake.

Anasema hali hiyo umeufanya muziki kuwa biashara nzuri licha ya msoto kabla ya kutoka kuwa pale pale, jambo linaloongeza hamasa ya kufanya vizuri kwa wasanii wote nchini Tanzania, ambapo nyimbo zake zinapatikana kwenye YouTube kwa akaunti ya Kampuni ya Africa Network Entertainment pamoja na kupatikana pia Audiomack, Boomplay, Spotify na kwingineko.

Kuhusu serikali, Man Mo anaitaka iendelee kushirikiana na wasanii wote sanjari na kuwatafutia upenyo katika muziki wa Dunia, bila kusahau kufanikisha wasanii wa ndani kutoka nje mara kwa mara ili wakaongeze wigo mkubwa katika sanaa yao, akisisitiza kuwa bila wasanii wa ndani kupata maonyesho ya Kimataifa muziki wao hautapiga hatua.

Huyo ndiye Man Mo, mmoja ya wasanii waliopokewa na msoto na mwenye ndoto lukuki za kisanaa.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images