Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 322 | 323 | (Page 324) | 325 | 326 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

  Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.

  Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.

  Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.

  Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.

  0 0

  Jumuiya ya Watanzania wa New York (ikijumuisha New Jersey, Connecticut na Pennsylvania) itafanya sherehe ya kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Jumapili tarehe 19 Januari 2014 kule Brooklyn. Anwani ya mahala sherehe itakapofanyika ni 3038 Atlantic Avenue, Brooklyn, NY 11208 kati ya Essex na Shepherd.

  Watanzania na rafiki wa Watanzania wote mnakaribishwa. Kiingilio kitakuwa dola 15 kwa wakubwa na dola 10 kwa watoto. Kutakuwa na Vinywaji, chakula, mziki na mambo mengi mengine.

  Vituo vya karibu vya treni J ni Norwood na Cleveland. Kumbuka Jumatatu ya tarehe 20 Januari 2014 ni Sikukuu ya Martin Luther King ambayo ni public holiday New York hivyo ni kusherehekea toka Jumapili hadi Jumatatu.

  Mungu ibariki Afrika. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Zanzibar.

  Kwa taarifa zaidi Wasiliana nasi kupitia:

  Email: info@nytanzaniancommunity.org
  Simu: 201-252-7220, 917-557-3195

  Wote mnakaribishwa.

  Jumuiya ya Watanzania New York.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu Serikali ameagiza kumalizwa kwa migogoro ya mipaka baina ya Hifadhi ya Tarangire, Pori la Akiba la Mkungunero na wananchi iliyodumu kwa muda wa takribani miaka kumi hadi sasa. Nyalandu amewataka wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi hizo kuacha kuvamia maeneo yaliyotengwa kisheria kwani kwa kufanya hivyo ni kuleta migogoro isiyo ya lazima.

  Mhe. Nyalandu alikuwa akiongea katika kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Manayara na Dodoma wilayani Babati mkoani Manyara zilizokutana kwa ajili ya kujadili suluhu ya migogoro hiyo.

  Aliongeza kusema kuwa serikali imedhamiria kumaliza mgogoro hiyo kwa kuishirikisha jamii kwa upana zaidi huku akisisitiza kwamba Serikali itaendelea kusimamia na kutekeleza Sheria ya Uhifadhi bila kumuonea mwananchi yoyote na kwa kuzingatia haki za binadamu.
  Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Manyara na Dodoma wakati wa kikao maalum cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Elaston Mbwilo akisitiza jambo wakati wa kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi.
  Sehemu wa wajumbe waliokutana katika kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
  Kutoka kulia: Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Profesa Alexander Songorwa na KatibuTawala wa Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge wakifuatilia mada zilizowasilishwa wakati wa kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara.
  Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Waheshimiwa Wabunge Zabein Mhita na Moza Abeid kutoka Dodoma wakati wa kikao hicho.
  Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na wanahabari mara baada ya kikao hicho.

  0 0
 • 01/12/14--13:27: Article 2
 • This is my new Mix..I did the mix live on air on Radio Mbao ( www.radiombao.com), The Mix is dedicated to all listeners of Radio Mbao in 103 countries.
  The mix has bongo flava bangers from year 2013 and some few Kenyans bangers too. You can find my mix on hulkshare ,soundcloud, & Mixcrate.. Justsearch #RadioMbaoEndOfTheYearMix#EndOfTheYearMix #RadioMbao #DjKvelli
  0 0
 • 01/12/14--13:36: MSAADA KWENYE TUTA
 • Hello mimi ni mtanzania niishie Kuwait City, Kuwait. Kampuni ninayofanyia kazi inataka kuniamishia Calgary, Alberta(Canada). 

  Bahati mbaya sijawahi kufika Canada. Naomba kama kuna mtanzania yuko huko au aliwahi kukaa huko tuwasiliane kupitia email: tzasheesh@gmail.com. Nitashukuru kupata msaada kutoka kwenu mlioko Calgary.


  Shukrani
  Mdau Asheesh


  0 0

  Ujumbe wa Algeria umepata nafasi ya kutembelea machimbo ya Tanzanite Mererani katika Kampuni ya TanzaniteOne ambapo walitembelea sehemu mbalimbali ikiwemo za uzalishaji, usafishaji, na uchongaji madini ya Tanzanite. 

  Vilevile, wakiwa Mkoani Kilimanjaro walipata fursa ya kutembelea Kiwanda cha kuzalisha mbolea ya kupandia cha Minjingu ambapo walijionea namna mbolea hiyo inavyozalishwa kwa kutumia masalia ya ndege aina ya Flamingo waliokuwepo eneo hilo miaka mingi iliyopita. 

  Aidha, ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea mbuga za wanyama katika bonde la ngorongoro ambapo wamehitimisha ziara yao nchini ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na nchi ya Tanzania katika sekta za gesi, mafuta,umeme na madini.
  Mkurugenzi Mkuu wa Migodi katika Wizara ya Nishati na Migodi ya Algeria Bw. Bourroudj Mohamed Tawar (aliyenyoosha mkono) akiangalia mwamba uliotokana na masalia ya ndege aina ya flamingo, yanayozalisha Mbolea ya kupanda ya Minjingu. Mwenye koti jeupe ni Mkuu wa uzalishaji wa kiwanda cha Minjingu Bw. Inyana Mwambete, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw. Tosky Hans na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Samaje.
  Mtaalamu wa madini katika machimbo ya Kampuni ya TanzaniteOne Mererani Bw. Damian Mansala akiueleza ujumbe wa Algeria namna mitambo ya kupeleka wachimbaji ardhini na namna mtambo huo unavyosafirisha mchanga wa madini uliochimbwa na kuusambaza katika hatua mbalimbali za uzalishaji wa madini ya Tanzanite.
  Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Sameja akiuongoza ujumbe wa Algeria kuondoka katika uwanja wa ndege wa Arusha , mara baada ya kumaliza ziara Mkoani humo.
  Meneja Mradi wa Kampuni ya TanzaniteOne Bw. Erenet Emmanuel Mtawali (mwenye kofia nyekundu) akiueleza ujumbe wa Algeria namna mitambo ya kusafisha na kuzalisha madini ya Tanzanite (haupo pichani) unavyofanya kazi.

  0 0

  Na Athumani Shariff

  WAZIRI wa Maji Profesa Jumanne Maghembe ametembelea mradi wa ulazaji wa bomba jipya la maji kwenye mradi mkubwa wa maji kutoka Ruvu chini, Mji mdogo wa Bagamoyo, utakao leta maji zaidi ya lita milioni 270 kwa siku.

  Mradi huo uliokamilika kwa zaidi ya asilimia 54 unakabiliwa na changamoto kubwa mbili zikiwemo za uhaba wa umeme katika kiwanda cha kutengeneza mabomba jambo ambalo linakwamisha upatikanaji wa mabomba yaliyyokadiriwa na kampuni hiyo ya Sinohydro inayotekeleza mradi huo.

  Changamoto nyingine iliyoelezwa katika mradi huo ni kesi zilizofunguliwa dhidi ya Mamlaka ya Maji Safi Dar es Salaam (DAWASA), kesi 12 zipo mahakani ambazo mamlaka hiyo imepanga kuzishughulikia haraka iwezekanavyo.

  Akijibu swali la waandishi wa habari juu ya hatua zinazochukuliwa na DAWASA katika kukabiliana na kesi hizo, Mwenyekiti wa bodi ya DAWASA Bi. Hawa Sinare alisema mpango uliopo ni kuonana na Jaji Mkuu kusaidia kesi hizo zisikilizwe kwa haraka na zitolewe hukumu mapema ili zisikwamishe mradi huo mkubwa wenye manufaa kwa watu walio wengi.

  Profesa Maghembe pia alitembelea upanuzi wa mtambo wa kusukuma maji uliokamilika kwa zaidi ya asilimia 98 wa Ruvu Chini Mji mdogo wa Bagamoyo uliojengwa ili kuongeza upatikanaji wa maji kwa jiji la Dar es Salaam, Kibaha na Bagamoyo.

  Awali Mtambo wa maji wa Ruvu chini kabla ya upanuzi ulikuwa ukizalisha lita za ujazo milioni 180 kwa siku, wakati huu wa sasa utaongeza lita za ujazo miliono 90 na kufanya lita za ujazo milioni 270 kwa siku kupelekwa jijini Dar es Salaam.

  Kuongezeka kwa lita hizo za ujazo katika uzalishaji kunatarajiwa kupunguza ukosefu wa maji kwa wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam na miji ya Kibaha na Bagamoyo ambao watapata maji kwa matumizi ya majumbani na viwandani.

  Waziri wa Maji pia aliongeza kuwa kazi ya upanuzi pia itaendelea katika mtambo wa Ruvu juu baada ya kukamilika mradi wa Ruvu chini na tayari pesa zake zipo zimeshatengwa zaidi ya bilioni 130. Aidha alisema, pia uchimbaji wa visima na mabwawa utaongeza upatikanaji wa maji na shida ya maji kuwa historia jijini Dar es Salaam.

  Akijibu swali juu ya kadhia ya maji jijini Dar es Salaam, Profesa Maghembe alisema, miradi ya maji haihitaji siasa, na wala huwezi ukaijenga kwa siku moja, nafikiri munaona ujenzi wake, huu mradi ni mkubwa na unahitaji utaalamu wa hali ya juu na hata kasi yake ya ujenzi munaiona.

  “Niwaambie wakazi wa Dar es Salaam nafahamu tabu wanayoipata kuhusu uhaba wa maji na kwakulijua hilo ndiyo maana natafuta suluhisho lakudumu, na maji haya kwa miradi hii yote itakuwa na uwezo wa kulihudumia jiji la Dar es Salaam mpaka mwaka 2034 bila shida ya maji na pia miundombinu ya kuongeza upatikanaji wa maji baada ya mwaka 2034 pia ilishawekwa” aliongeza Waziri Maghembe.
  Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wa mbele akiwa amesimama juu ya bomba jipya Boko nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Ulazaji wa bomba hilo umekamilika kwa asilimia 54. Nyuma yake ni maafisa wa Wizara ya Maji, Dawasa na wahandisi wa mradi.
  Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe wa kwanza kulia, akipewa maelezo juu ya pampu za kusukumia maji. Pampu moja inauwezo wa kusukuma lita milioni 90 kwa siku. Na huwa sinasukuma pampu tatu na moja hubaki akiba endapo moja itaharibika ili kufanya maji kusukumwa kwa ujazo uliokusudiwa.

  0 0

  DSC_0023
  CEO wa Kampuni ya MeTL Group na Mbunge wa Jimbo la Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji Balozi (kulia) akimsindikiza Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
  DSC_0024
  Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula, akifurahia jambo na Mh. Mohammed Dewji alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar.
  DSC_0029
  Mh. Mohammed Dewji akimtambulisha Mshauri wa miradi ya Kampuni ya MeTL Group, Bw. Sudi Mwanasala (kulia) kwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mh. Liberata Mulamula.
  DSC_0035
  Mh. Mohammed Dewji akibadilishana mawazo na Balozi Liberata Mulamula na Mshari wa Miradi ya Makampuni ya MeTL Group, Bw. Sudi Mwanasala.

  0 0

  746

  Zanzibar Second Vice President, Ambassador Seif Ali Iddi, presents a souvenir to the outgoing UN Resident Coordinator, Mr. Alberic Kacou when the latter paid him a visit in his office to bid him farewell.
  Kacou
  Zanzibar First Vice President, Mr Seif Sharif Hamad, in talks with the outgoing UN Resident Coordinator, Mr. Alberic Kacou when he paid him a visit in his office to bid farewell.

  and the people of Zanzibar when he met with H.E. First Vice President Seif Shariff Hamad and H.E. Second Vice President Seif Ali Iddi at the start of the year. He will be departing Tanzania mid-January to take on a new assignment as Chief of Staff and Director of the Executive Office at UNDP Headquarters, New York.

  After serving as the leader of the UN system in the United Republic of Tanzania for almost four and a half years, Mr. Kacou has nothing but good memories of the country and its people. He congratulated the Revolutionary Government of Zanzibar, especially in the operationalization of a Government of National Unity.

   He also conveyed his sincere appreciation for the trust, support and cooperation provided to the United Nations system, and assured the government of the continuing assistance from the United Nations in addressing Zanzibar’s development challenges.

  H.E. First Vice President congratulated Mr. Kacou for “his successful leadership in making the UN system grow stronger.” Similarly, H.E Second Vice President thanked Mr. Kacou for “leading the various UN agencies towards more coherent and effective assistance to Zanzibar.”

  Tanzania is one of seven pilot countries implementing the Delivering As One approach aimed at achieving greater impact on development challenges, through a more coordinated, coherent, and efficient manner. 

   The UN sub-office in Zanzibar, inaugurated in 2009 by the UN Secretary General, was established in order to make sure that UN agencies provide the most effective assistance to Zanzibar, in line with the principles of the Delivering As One initiative. It is one of a few joint offices in the world where UN agencies are under one roof and share in the management of the office.

  0 0


  0 0

   Hili lilikuwa igizo lililoendeshwa na askari polisi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman mjini Unguja jana Jumapili Januari 12, 2014.

  "Askari wa kikoloni", akipewa adhabu ya push up baada ya kuboronga wakati wa gwaride. Hili lilikuwa igizo lililoendeshwa na askari polisi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa michezo Aman mjini Unguja Jumapili Januari 12, 2014.


  Kamanda wa kikosi cha askari KAR, akiongoza wenzake kwenye onyesho la Maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi lililoendeshwa na askari polisi kuonyesha jinsi jeshi la kikoloni lilivyokuwa likifanya mambo yake,enzi hizo na ilikuwa ni burudani nzuri sana iliyomvutia kila aliekuwa akitazama.

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje,Mh. Edward Lowassa akifurahia jambo wakati akiwa katika maongezi na Mwenyekiti wa CCM tawi la Washington DC nchini Marekani,Bw. George Sebo aliyemtembelea ofisini kwake jijini dar es salaam leo.

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo mjini Zanzibar ,pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na wananchi wake kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar,Rais Dkt. Ali Mohamed Shein na upande wa kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mh. Phillip Mangula pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Mh. Abdulrahman Kinana.

  Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekuwa na kikao cha siku moja leo tarehe 13/01/2014 mjini Zanzibar chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Kikwete.

  Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wazanzibari na watanzania kwa ujumla kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Aidha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepongezwa kwa maandalizi mazuri na ya kufana ya sherehe hizo.

  Kamati Kuu imetambua na kupongeza hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa tangu mapinduzi mwaka 1964 mpaka leo. Wito umetolewa kuyalinda na kuyaendeleza mema yote yatokanayo na mapinduzi hayo na mafanikio yaliyoletwa na serikali inayoongozwa na CCM.

  Aidha Kamati Kuu imemteua Ndg. Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa uwakilishi jimbo la Kiembesamaki kupitia CCM.

  Kesho mgombea huyu wa CCM atachukua fomu za tume za kugombea. Uzinduzi wa kampeni za CCM utafanyika tarehe 22/01/2014 kwenye viwanja vya Kiembesamaki ambapo mgeni rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Mohamed Gharib Bilal.

  Kampeni za CCM zitafungwa tarehe 01/02/2014 huko Chukwani na mgeni Rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Balozi Seif Ali Idi.

  Kampeni itaendeshwa na Kamati ya Siasa ya wilaya ya Dimani viongozi na wanachama wa wilaya husika, na ngazi zingine za Chama zitashirikiana na ngazi ya wilaya kuhakikisha CCM inashinda tena jimbo hili.

  Kamati Kuu inawatakia kila lakheri kwenye kampeni na hatimaye uchaguzi huo. Kampeni na hata upigaji kura uendeshwe kwa amani na utulivu kama ulivyo utamaduni wetu.

  Imetolewa na;
  Nape Moses Nnauye
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
  13/01/2014

  0 0

  Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation points out the Mount Kilimanjaro on a gift given to the outgoing Resident Representative for the United Nations Development Programme and Resident Coordinator of the UN System in Tanzania, Dr. Alberic Kacou yesterday at the Serena Hotel in Dar es Salaam.  The Minister hosted the farewell dinner for Dr. Kacou, who had just completed his tenure of four years.    
  Minister Membe gives his remarks, praising Dr. Kacou for his superb work during his four-year tenure.
  Distinguished in attendance included Ambassador Vincent Kibwana (right), Acting Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs, Ambassador Simba Yahya (2nd right), Director of Middle East in the Ministry of Foreign Affairs, H.E. Filberto Cerian Sebregondi (3rd right), Head of the Delegation of the European Union in Tanzania.  Also in the photo here are Ambassador Juma Alfani Mpango (2nd left), Dean of the Diplomatic Corps and the Ambassador of the Democratic Republic of Congo in Tanzania and Ambassador Celestine Mushy (3rd left), Director of the Multilateral Cooperation in the Ministry of Foreign Affairs.   Other distinguished guests were Heads of the UN Agencies, Funds and Programmes and other officials from the Ministry of Foreign Affairs. 

  CLICK HERE FOR MORE PHOTOS

  0 0

  Zanzibar based photographer JAVED JAFFERJI presents a copy of the book Zanzibar Photographic Journey- 50 Years of the Revolution prior to the official launch o the book at the residence of H.E Malim Seif Sharif Hamad, First Vice President of Zanzibar. Hon Malim Seif Sharif did the introduction for the book along with Dr Abeid Amani Karume, former President of Zanzibar, who graced Forword for the same book. The Historical book will be launched with the exhibition at Peace Memorial Museum in Zanzibar before 12th JAN 2014 to celebrate the 50 years of revolution.


  0 0


  0 0

  GLOBU YA JAMII INAPENDA KUMPA HEPI BESDEI YA KUZALIWA MZEE YA CHRIS LUKOSI ( pichani, akiwa bado kinda) AMBAYE BAADA YA KUPAMBANA VYA KUTOSHA HIVI SASA NI MKURUGENZI WA KAMPUNI PENDWA YA SERENGETI FREIGHT FORWARDERS ILIYOKO UINGEREZA. HAKIKA UMETOKA MBALI NA HAPO ULIPO NI MBALI PIA. 
  TUNASHUKURU KWA KUWA MMOJA WA WADAU WANAOIPA TAFU GLOBU YA JAMII KWA HALI NA MALI. MOLA AKUZIDISHIE MAARIFA NA NGUVU ZA KUENDELEA KUWA NAMBARI WANI KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI MIZIGO MIKUBWA NA MIDOGO KUTOKA UINGEREZA HADI MAHALI POPOTE DUNIANI - ANKAL

  0 0


  0 0

  Na Mwandishi Maalum

  Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,  limeambiwa,   kuna taarifa za  uhakika na zisizo na  shaka  kuwa  kundi la waasi la M23 limeanza  kujiunda na kujipanga upya.

  Hayo yameelezwa leo na  Bw. Martin Kobler (pichani), Mwakilishi wa Katibu Mkuu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa Misheni ya Kulinda Amani  katika DRC, ( MONUSCO).

  Alikuwa  akiwasilisha   mbele ya Baraza Kuu la  Usalama la Umoja wa Mataifa, taarifa ya  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  kuhusu  Misheni ya  Kulinda  Amani  ya Umoja wa Mataifa  katika DRC ( MONUSCO).

   “Tunazo taarifa za uhakika kabisa kwamba kundi hili la M23 baada ya kusambaratishwa vibaya mwezi Novemba mwaka jana, sasa limeanza kujiunda na kujipanga upya” akasema Bw. Kobler

  Na kuongeza, “ Ninapenda kutumia nafasi hii, kuitaka Serikali ya DRC kuanza kutekeleza makubaliano  ya Nairobi. Na kwa nchi za Uganda na Rwanda kutoruhusu ardhi yao kutumiwa na kundi la M23 iwe ni  kujipanga upya au kwa mafunzo ya aina yoyote ”.

  Mbali ya  Mkuu wa MONUSCO kutoa taarifa yake kwa  Baraza  hilo, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu katika eneo la Maziwa Makuu, Bi. Mary Robinson naye aliwasilisha taarifa yake.

  Mkuu huyo wa Misheni ya  MONUSCO alieleza bayana kwamba  makundi ya waasi katika  Jamhuri ya  Kidemokrasi ya Kongo bado ni tishio kubwa katika mchakato mzima wa utafutaji wa Amani ya kudumu katika DRC na hususani katika eneo la Mashariki ya nchi hiyo.

  “Uwepo wa Brigedi Maalum ( FIB) na matumizi ya ndege zisizoendeshwa na  binadamu ( UAVs), makundi yote ya waasi yanajua wazi kwamba, sasa tuna nia na uwezo wa  kutumia  nguvu kubwa   wakati wowote”. Akasisitiza   Mkuu huyo wa MONUSCO.

  Katika  taarifa yake kwa Baraza  Kuu la Usalama, Bw. Kobler ,  alielezea  kwa kina hali ya usalama  ilivyo nchini DRC na  kazi kubwa inayofanywa na  MONUSCO katika kuyakabili makundi ya waasi na  vilevile kutoa ulinzi kwa raia.

   Bw. Kobler alibainisha zaidi kwa kusema kuwa,“ Katika wiki zijazo, tutakuwa tumekamilisha   mapitio ya mkao wa kijeshi  katika eneo lote la   Mashariki ya Kongo. Baada ya  kukamilisha kazi hiyo tutakuwa na  urahisi wa kwenda mahali popote  na  wakati wowote  tunapohitajika, kukabiliana na tishio la aina  yoyote na kutoa ulinzi  kwa raia “  

  Naye  Bi. Mary Robinson, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu katika eneo la Maziwa Makuu, akizungumza kwa njia ya  video tele-conferencing kutokea Kishansa DRC, ameliambia Baraza Kuu la  Usalama, kwamba wakati umefika sasa kwa nchi zile zilizotia saini Mpango Mpana wa Umoja wa Mataifa kuhusu Siasa,  Usalama na Maendeleo katika DRC na Maziwa Makuu  kuanza kutekeleza maamuzi  magumu.

  Akasema  juhudi za  kutafuta Amani na usalama katika  DRC zipo katika  kipindi  muhimu hivi sasa na kutoa wito kwa viongozi waliosaini mpango huo kuanza kutelekeza ahadi zao ili hatimaye Amani iweze kupatikana.

  Bi.  Robinson ambaye  kesho ( Jumanne) atahudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu ( ICGLR)utakaofanyika nchini  Rwanda alieleza pia  kwamba,  mazingira  ya utulivu yaliyokuwapo baada ya kusambaratishwa  kundi la M23 yamepotea na  kwamba eneo hilo sasa lipo katika  kipindi cha kurejea kwa machafuko.

   Akasema  utulivu huo umetoweka hasa  baada ya  kutokea kwa mashambulizi yaliyofanywa na kundi la waasi la  Alliend Democratic Forces ( ADF) katika eneo la Mashariki ya  DRC. 

  Aidha kuendelea kwa hali  ya machafuko katika  Jamhuri ya  Afrika ya Kati na  kuibuka kwa mapigano katika  Sudan ya Kusini,pia kumechangia kuwepo mdororo huo wa kiusalama mashariki ya DRC.


  Na kwa sababu hiyo anasema,   utekelezaji wa mpango mpana wa kisiasa bado unabaki kuwa  suluhu pekee ya  upatikanaji wa  Amani ya kudumu, usalama, ushirikiano na maendeleo katika   eneo la Maziwa Makuu.


older | 1 | .... | 322 | 323 | (Page 324) | 325 | 326 | .... | 3270 | newer