Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

Vijana nchini wamehimizwa kushiriki kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa

0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akiongea na wananchi wa na wanamichezo waliohudhuria kushuhudia fainali ya Kamsese jimbo Cup kati ya timu ya Kikilo dhidi ya Masange mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Kisese Disa wilayani Kondoa mkoa wa Dodoma.
Mbunge wa Kondoa, halmashauri ya wilaya ya Kondoa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akiwasalimia wananchi na kumkaribisha Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza kuhutubia hadhara na kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya Kamsese jimbo Cup yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Kisese Disa wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akipiga penati kuashiria kuanza kwa mchezo wa fainali ya Kamsese jimbo Cup iliyozikutanisha timu za Kikilo dhidi ya Masange mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Kisese Disa wilayani Kondoa mkoa wa Dodoma ambapo Kikilo iliibuka mshindi kwa kuifunga Masange 2:1.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akikaguatimu ya Masange kabla ya kuanza kwa mtanange wa fainali ya Kamsese jimbo Cup iliyozikutanisha timu za Kikilo dhidi ya Masange mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Kisese Disa wilayani Kondoa mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza (wa tatukushoto) akiwasili viwanja vya viwanja vya Kisese Disa wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki kufunga mashindano ya Kamsese jimbo kwa fainali iliyozikutanisha timu za Kikilo dhidi ya Masange. Na wa pili kushoto ni Mbunge wa Kondoa, halmashauri ya wilaya ya Kondoa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji.
Mashabiki wa timu ya Kikilo wakishangilia ushindi wa timu yao mara baada yamchezo uliyozikutanisha timu za Kikilo dhidi ya Masange kumalizika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Kisese Disa wilayani Kondoa mkoa wa Dodoma.

(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Kondoa)

********************************

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Kondoa

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza amewataka vijana kote nchini kushiriki kikamilifu katika kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa ifikapo Novemba 24, mwaka huu.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza wakati akifunga mashindano ya jimbo Cup yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Kisese Disa wilayani Kondoa mkoa wa Dodoma.

Lengo mashindano hayo ni kuhamasisha vijana na wananchi wote kote nchini kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kuwa chachu ya kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo nchini kwa vijana wa umri mbalimbali.

Naibu Waziri amewataka wadau wa michezo kuyatazama mashindano yanayofanyika nchini kuwa ni mkakati wa kuibua vipaji vya vijana katika michezo mbalimbali hatua inakayopelekea kuwa na timu bora za ligi na hatimaye timu za taifa.

“Wito wangu kwa vijana kote nchini, tumieni mashindano ya aina hii kujitokeza na kushiriki kikamilifu ili kuonesha vipaji vyenu, Serikali tumeendelea kuwekeza nguvu kubwa kwenye kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana.” amesema Naibu Waziri wa Shonza.

Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo, Naibu Waziri Shonza amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa timu za vijana kwa taifa ambapo alithibitisha kuwa sote tu mashahidi kwa namna ambavyo timu zetu za Taifa za vijana zinavyofanya vizuri katika mashindano mbalimbali na kutoa taifa kimasomaso na kusisitiza tuko vizuri.

Miongoni mwa mashindano ambayo Tanzania imefanya vizuri ni pamoja na mashindanoya timu kutoka kanda za Afrika Mashariki na Kati ambapo imekuwa washindi wamwaka 2019 kwa vijana chini ya miaka 20 (CECAFA U-20), Washindi wa kombe laBaraza la Vyama vya Mpira wa Miguu kusini mwa Afrika (COSAFA) kwa timu yawanawake ya Tanzanite kwa vijana chini ya miaka 20 (U20-2019), Novemba 15, 2019 timu ya Taifa Stars imewalaza timu ya Equatorial Guinea kwa kuifunga magoli 2-1 kwenye kinyang’anyiro cha kufuzu Afcon 2021, na October 18, 2019 Taifa Stars ilifuzu kucheza fainali za CHAN zinazotarajiwa kufanyika mwaka 2020 nchini Cameroon.

Mashindano hayo yalishirikisha kata zote 21 za wilaya ya Kondoa yakiongozwa na kauli mbiu ya “Uchaguzi wa Serikali za mitaa ndio msingi wa maendeleo yetu, twendeni tukashiriki pamoja” ambayo inawahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo ili kupata viongozi watakaowaongoza kwa miaka mitano kuanzia 2019 hadi 2024.

Aidha, Naibu Waziri Shonza amesema Mbunge na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji ameounga mkono Serikali ya Awamu ya Tano ambapo Sera ya Taifa ya Michezo ya mwaka 1995 inasema jukumu la kukuza na kuendeleza michezo nchini si la Serikali peke yake, bali ni jukumu la Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali akiwemo Mbunge wa Kondoa ambaye amewapa vijana wa jimbo hilo kounesha uwezo na vipaji vyao katika michezo.

Zaidi ya hayo, Naibu Waziri Shonza amesema kuwa mashindano hayo ya Kamsese wilaya ya Kondoa ni chachu ya kupata vijana wanaoweza kucheza timu ya mkoa wa Dodoma, Dodoma FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza na kuwaomba waandaaji wa mashindano hayo pamoja na wadau wengine kutanua na kuongeza wigo wa mashindano hayo yashirikishe pia michezo mingine ikiwemo mpira wa pete, riadhaa, mpira wa kikapu na michezo mingine ili kupata vipaji katika hiyo.

Mkoa wa Dodoma hususani wilaya ya Kondoa kwa historia ya michezo imekuwa ni eneo muhimu linalotoa wanamichezo bora akiwapo mwanariadha mkongwe Mzee wetu Juma Ikangaa ambao ni mfano wa kuiga na ni fursa kwa vijana nchini kuonesha vipaji vyao kwa maendeleo ya taifa lao.

Kwa upande wake Mbunge wa Kondoa, halmashauri ya wilaya ya Kondoa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amezipongeza timu zote za kata za wilaya ya Kondoa kushiriki mashindano hayo kwa amani, upendo na mshikamano na hatimaye kufikia kilele cha mashindano hayo kwa ufanisi na mafanikio makubwa.

Dkt. Ashatu ameeleza kuwa dhamira ya mashindano hayo ni kuileza Tanzania, dunia na kuimbia Kondoa kuwa kuna amani na usalama wa kutosha hatua inayotupelekea kwenda kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa amani na usalama.

“Michezo ni ushirikiano, mshirikamano na kudumisha michezo kwa sababu tunatambua kuwa michezo ni afya, michezo ni ajira na michezo ni furaha tumeungana kwa pamoja” Dkt. Ashatu.

Mashindano ya ligi ya Kamsese yalishirikisha timu kutoka kata 21 za wilaya ya Kondoa ambapo timu zilizofikia hatua ya fainali ni kata za Kikilo na Masange na hatimaye timu ya Kikilo kuifunga Masange 2:1 na kuzawadiwa kombe pamoja na fedha taslimu Sh. 500,000/= na kuandika historia ya kuwa mabingwa wa kwanza wa kihistoria wa mashindano hayo.

TADB YAKABIDHI PIKIPIKI MPYA KWA VYAMA VYA MSINGI KAGERA.

0
0
Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imekabidhi Pikipiki mpya mbili Kwa vyama viwili vya msingi vya Ruicho na Nyakatuntu vya Wilayani Karagwe na Kyerwa mwishoni mwa Wiki hii, katika Hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Chama cha Ushirika KDCU Wilayani Karagwe.

Awali katika salaam za Benki hiyo zilizotolewa na Meneja wa TADB Kanda ya Ziwa Ndg. Mike Granta kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Japhet Justine, amesema TADB kupitia mkopo inayotoa Kwa wakulima, imekuwa na mchango mkubwa wa maendeleo kwa Mkulima mmoja mmoja na pamoja na Vyama vya msingi, huku akiongeza kuwa mpaka sasa zaidi ya shilingi Bilioni 44 ambazo zimeingia katika mzunguko wa kiuchumi huku ikiwa shilingi Bilioni 34, kati ya pesa hizo zikiwa tayari zimelipwa kwa Wakulima wa Wilaya za Karagwe na Kyerwa.

Kupitia Hafla hiyo Meneja Granta amekabidhi Jumla ya Pikpiki mbili mpya zenye jumla ya thamani ya Shilingi Milioni Tano, Kwa Vyama vya Msingi vya Ruicho ( Karagwe) na Nyakantuntu (Kyerwa) ikiwa ni ahadi iliyotolewa hivi Karibuni na Mkurugenzi Mtendaji Japhet Justine alipofanya ziara yake Wilayani Karagwe. Sababu kubwa ikiwa Vyama hivyo kufanikisha zoezi la kuwashawishi na kuwaunganisha pamoja wanachama wao kwa asilimia kubwa kufungua akaunti katika Benki hiyo. 

Katika hatua nyingine Mgeni Rasmi katika hafla ya kukabidhi Pikipiki hizo Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza na Wakulima hao, alisema kwa Upande wa Serikali mpaka sasa hali ni shwari kwa msimu huu wa ukusanyaji wa kahawa, na Amani na Utulivu ni wa kutosha kulinganisha na msimu uliopita, hali iliyochangiwa na ulipaji wa malipo yote ya awali kwa wakulima wa zao hilo, na kwamba hakuna mkulima yeyote anayedai. 

Aidha Mhe. Gaguti ameongeza kuwa hakuna mnunuzi aliyezuiliwa kununua kahawa kutoka Kagera, Bali wanunuzi wa kahawa ya msimu huu kwa asilimia mia moja ni wanunuzi binafsi, na wale wachache wanaolalamika na kueneza uzushi ni wale ambao hawakukidhi vigezo vya kibiashara, na ndio sababu msimu huu umekuwa bora kuliko misimu iliyopita.
Pichani Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, akikabidhi Pikipiki Mbili Kwa Wakulima wa Vyama vya Msingi vya Ruicho na Nyakatuntu zenye thamani ya Shilingi Milioni tano
Pichani ni Ndg. Mike Granta, Meneja TADB kanda ya ziwa, akitoa salaamu kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Benki hiyo, katika hafla ya kukabidhi pikipiki Mbili mpya kwa wanachama wa vyama vya Msingi Ruicho na Nyakatuntu Wilayani Karagwe.
Pichani ni sehemu ya Wakulima na wanachama wakiendelea kufuatilia matukio mbalimbali kwenye Ukumbi wa Chama Kikuu cha Ushirika (KDCU), uliopo Kamahungu, Wilayani Karagwe.

WIZARA YA KILIMO YAKUTANA NA WADAU WA TUMBAKU KUJADILI CHANGAMOTO ZAO

0
0
Wizara ya Kilimo imekutana na wadau na wakulima wa kilimo cha Tumbaku hapa nchini ili kujadili changamoto zilizopo katika sekta hiyo nakuzitatua ili kuinua sekta ya kilimo cha Tumbaku hapa nchi.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika Jijini Dodoma na kuwakutanisha Wizara ya kilimo, fedha na wadau wa kilimo cha Tumbaku, wakulima na makampuni yanayonunua zao la Tumbaku na wenye viwanda vya Tumbaku, naibu Waziri wa Kilimo Husain Bashe amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kuhakikisha Wanakutana kwa pamoja na kujadili changamoto na vikwazo vyote vinavyopelekea kutoendelea kwa kilimo cha Tumbaku hapa nchini.

"Tumekutana hapa lengo likiwa ni kuangalia ni namna gani tunaweza kutoka hapa tulipo na kwenda mbele, ndio maana tumeshirikisha wadau wote sisi Wizara ya kilimo, fedha, wadau wa kilimo,wenye viwanda na wakulima ili kila mtu ajue nani ni kikwazo na kuanguka kwa sekta hii"

Ameongeza kuwa" zao la Tumbaku uzalishaji wake umekuwa ukishuka siku baada ya siku ukiangalia uzalishaji umeshuka kwa asilimia kubwa toka uzalishaji wa tani laki mojana ishirini (120,000) Hadi kufikia tani arobaini (40) kwa Sasa" Amesema Mhe. Bashe.

Amesema katika kikao hicho wameunda kamati ndogo ambayo itapitia sekta nzima ya kilimo cha Tumbaku na kukutana na wadau wote wa kilimo cha tumbaku na kuja na mapendekezo ya pamoja nini kitanyike na Kodi zipi zipunguzwe kwa Afya ya kilimo cha Tumbaku hapa nchini.

Amesema wameamua kuja na vikao hivyo vya kila kila zao peke yake ili kuona kila zao na tatizo lake kwa matatizo mengi yanatofautiana kwa kila zao na hivyo wameona ni vyema kukaa na wadau wa kila zao kuona namna ya kutatua changamoto za kila zao.

Amesema moja ya changamoto zilizoibuka ni baadhi ya makampuni ya ununuzi wa zao la Tumbaku kutaka kujitoa, na wamejadili na makampuni hayo likiwamo kampuni ya TLTC kutokana na kutorudi kwa VAT return lakini baada ya mazungumzo wamekubali kuendelea na ununuzi wa zao hilo.

Lengo kubwa la serikali ni kuona kilimo cha Tumbaku kinaanza kurudi katika uzalishaji wake wa kawaida na kuleta tija kwa serikali na wakulima kunufaika na kazi wanazozifanya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme, ambaye ni mdau wa kilimo cha Tumbaku amesema ni muhimu kwa taasisi za Serikali kujenga mazingira mazuri kwa wakulima na wafanya biashara wa zao la Tumbaku ili kuondoa migongano ambayo imekuwa ikitokea Mara kwa Mara.

Amesema kwa pamoja kama wakulima ni lazima lazima wasimamie ushirika katika zao hilo ili iwe rahisi katika hata katika kupanga bei, pia amesisitiza wale wanaopanga ubora wa tumbaku kuwa waaminifu na wazalendo kwa kupanga kwa usahihi.

Naye mmoja wa wakulima ambaye pia ni mwanachama wa chama Cha msingi Tabora, Uyui, Said Shabani, mbali na kumpongeza Naibu Waziri wa Kilimo kwa kuwakutanisha, amesema kwa kikao hicho ameanza kuona mwanga katika sekta ya kilimo na Sasa anaamini uzalishaji utaanza kupanda sasa.
 Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma, kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, na kushoto ni Naibu Waziri mwingine wa Wizara hiyo, Omary Mgumba
 Wandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga leo jijini Dodoma
 Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma, pengine yake ni manaibu Waziri wa Wizara hiyo, Hussein Bashe na Omary Mgumba
Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo.

WAZIRI HASUNGA AMUAGIZA CAG KUFANYA UCHUNGUZI MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KOROSHO

0
0

Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya uchunguzi kwenye mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao la Korosho baada ya kubaini kuwepo na udanganyifu.

Mhe Hasunga amemuagiza CAG kuchunguza kiasi cha Shilingi Bilioni 53.2 kilichobaki kwenye akaunti ya Mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao la Korosho ambazo zilikuwa kwa ajili ya kujenga viwanda vitatu vya kubangua korosho na maghala.

Aidha Mhe Waziri ameunda timu ya watu wasiozidi watano kwa ajili ya kuhakiki kiasi cha korosho kilichopokelewa na kilichouzwa katika msimu wa Korosho wa mwaka 2018/2019 baada ya kubaini uwepo wa udanganyifu.

Hayo ameyasema leo jijini Dodoma mbele ya wandishi wa habari ambapo amezitaka pia kamati za ulinzi na usalama kusimamia zoezi la uhakiki ambalo linaonekana kutawaliwa na udanganyifu ambapo timu iliyoundwa itashirikiana na timu iliyokuwepo chini ya wizara hiyo kuhakiki pia fedha zilizopatikana ili wahakikishe wanaolipwa ni wale wanaostahili.

Aidha amesema timu hiyo ihakikishe kuwa majina yaliyotoka kwenye vyama vya msingi kwenda kwenye vyama vikuu hadi fedha zilizoingia benki  kama kweli ziliingia kwenye akaunti za wakulima na kama kuna unyaufu uliojitokeza wabainishe ni kwa kiwango gani ili kusaidia serikali kutoa taarifa yenye uhalisia.

Waziri Hasunga amesema mwaka 2016 serikali iliamua kufuta mfuko wa Wakfu na kwenye akaunti kulikuwa na kiasi cha shilingi bilioni 53.2 lakini bodi ya Korosho iliamua kubadili matumizi na kutumia fedha hizo tofauti na maagizo yaliyotolewa na serikali.

" Kama Wizara hatupo tayari kuona ubadhilifu wowote wa fedha za umma unafanyika, Serikali ya awamu ya tano haiwezi kukubali kuona watu wachache wanafaidika na fedha za walipa kodi wa Tanzania.

Timu zote mbili naziagiza hadi kufikia Januari 15 mwaka 2020 wawe wameshatuletea ripoti wizarani. Niwahakikishie hatutomvumilie yeyote ambaye atajaribu kugusa fedha za wananchi, " Amesema Waziri Hasunga.

Amesema bodi hiyo ilitumia kiasi cha shilingi bilioni 28.1 kununua viuatilifu,walitumia kiasi cha shilingi bilioni 12.2 kulipia magunia ilhali katika msimu huo wanunuzi walikuwa wananunua magunia wao wenyewe.

Ametoa wito kwa wakulima kuwa kama kuna anayedai ushirika apelike madai yao kwenye kamati ya ulinzi na usalama na timu iliyoundwa ili waseme kama hawajalipwa.
 Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma, kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, na kushoto ni Naibu Waziri mwingine wa Wizara hiyo, Omary Mgumba
 Wandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga leo jijini Dodoma
 Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma, pengine yake ni manaibu Waziri wa Wizara hiyo, Hussein Bashe na Omary Mgumba
Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo.

Benki ya NIC yatoa mchango wa magodoro kwa shule ya sekondari ya wasichana Loyola

0
0
 Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited Margaret Karume, amewaasa wanafunzi wa shule ya sekondari Loyola kujifunza kwa kuzingatia mtizamo mpana wa kidunia ili kuendana na mfumo wa sasa wa kielimu wa kidunia unaohitaji wahitimu wenye uwezo mkubwa wa kuelewa mambo na matatizo mbali mbali na kisha kuyatafutia suluhisho.

Karume aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 21 ya shule hiyo alitoa wito huo, sambamba na kukabidhi mchango wa magodoro 100 kwa ajili ya kuboresha mazingira wanayoishi wanafunzi wa shule hiyo.

Mkurugenzi huyo pia aliwaambia wanafuzi wa Loyola kuwa ili kuendana na dunia ya sasa, wanatakiwa kufanya jitihada binafsi za kutafuta maarifa na ujuzi na siyo tu kutegemea kile wanachofundishwa na waalimu wao darasani na kusisitiza kuwa bado wana safari ndefu.

“Elimu mliyoipata bado ni ya hatua za mwanzo tu, hasa ukizingatia kukua kwa utandawazi. Kutokana na mabadiliko makubwa yanayoenda sambamba na ukuaji wa haraka wa Sayansi na Teknalojia yanayomgusa kila mtu na katika kila nyanja ya maisha, sote tutalazimika kuendelea form 6 kujifunza mambo mapya hadi mwisho wa maisha yetu,” alisema

Karume aliwaambia wahitimu hao watarajiwa kwamba ni wajibu wao kuendelea kujifunza mbinu mpya za kuyakabiliana na maisha na pia kujijengea uwezo wa kujiajiri pindi watakapomaliza elimu ya juu

Elimu mliyopata na ambayo mtaendelea kuipata itafungua maisha yenu na ya jamii nzima ikiwa ni pamoja na familia zenu na watoto wenu. Elimu hii pia itawapa uwezo wa kiuchumi, itawapa uwezo wa kuwa na sauti, mtaongea, mtasikika na kusikilizwa, pia itawajengea heshima katika jamii na kuwapa uwezo wa kuchangia mambo mbali mbali katika maisha. 

Aliwataka kuiga mifano ya wanafunzi waliosoma shuleni hapo na ambao wamefanikiwa kimaisha baadhi yao wakiwa ndani na wengine nje ya nchi

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Padri Obwanda Meyo, SJ alimuhakikishia mgeni rasmi kuwa wanafunzi wake wamejiandaa vizuri kwa ajiili ya mitihani ya mwisho na hivyo watafanya vizuri 

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume (kushoto) akiwa ni mgeni rasmi wa sherehe ya wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Loyola akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi  milioni 4.7/- kwa mkuu wa shule hiyo Father Ubwanda Meyo jana, ikiwa ni sehemu ya mchango wa benki ya NIC kwa ajili ya kununulia magodoro 100 yatakayotumika kwenye mabweni ya wasichana wa  shule hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited Margaret Karume akizungumza na wageni waalikwa , wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari Loyola waliohudhuria kwenye mahafali ya wanafunzi wa kidato cha nne shule hiyo jana jijini Dar es salaam

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa shule ya sekondari Loyola, Padri Obwanda Meyo (wa tatu kulia), mwakilishi wa wazazi watoto wa kidato cha nne, Joseph Tadayo (kulia), Brigitte Asenga na Annah Lupembe (kushoto) ambaye ni meneja wa tawi la NIC Kariakoo.

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited Margaret Karume akifurahi na wanafunzi wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Loyola.

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume (wa pili kulia mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Loyola, Mkuu wa Shule Padri Obwanda (aliyebeba mtoto), Mwakilishi wa wazazi, Joseph Tadayo , Mwenyekiti wa PTA Luyola, Brigitte Asenge na Meneja wa Tawi la NIC Kariakoo, Annah Lupembe (mwisho kushoto)

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Limited, Margaret Karume akiwa na kikombe alichopewa zawadi na uongozi wa shule ya sekondari Loyola.












SERIKALI YAAHIDI KUWA BEGA KWA BEGA NA MTOTO ALIYEFIWA NA WAZAZI WAKE WOTE NA WADOGO ZAKE WATATU

0
0

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

SERIKALI imesema itashirikiana na mtoto Anna Zambi bega kwa bega kuhakikisha anatimiza ndoto zake alizozipanga kabla hajafikwa na msiba mkubwa wa kuondokewa na wazazi wake wote wawili pamoja na wadogo zake watatu kwa mpigo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, nyumbani kwa kina Anna, Goba jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto, Dkt. John Jingu  amesema inafahamika kuwa mtoto Anna anamahitaji mengi yakiwemo ya kisaikolojia.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu tayari Serikali kupitia Maafisa Ustawi wa Jamii wameshaanza kumpatia tiba ya kisaikolojia tokea alipofika Dar es Salaam jana akitokea Shuleni mkoani Tanga.

Dkt. Jingu amesema wamepata taarifa kuwa mtoto Anna ataendelea kulelewa na Mama yake Mdogo huko Arusha lakini Serikali itaendelea kufuatilia hatua kwa hatua maisha yake ili kuhakikisha anapata stahiki zake ikiwemo Elimu.

"Mtoto Anna anahitaji kusoma, hatutamuacha peke yake tutabeba hilo jukumu, ingawa Mama Mdogo amekubali kuishi nae, hatutamuachia mwenyewe tutaendelea kuwa naye mpaka pale tutaona anauwezo wa kujitegemea, kuwa mtu mzima.

Aidha Mkoa wa Dar es Salaam unapanga kufanya kitu kwa ajili ya kumsaidia mtoto Anna ambapo mpaka sasa kuna Kamati za Ulinzi wa Mtoto kila mahali ambazo zimeelekezwa kuhakikisha haki za Anna hazipotei. Maendeleo na Ustawi wa Anna vitaendelea kuwa jukumu letu.

Naye Msemaji wa Familia, Ibrahim Zambi ameishukuru Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano katika kipindi chote cha Msiba, amesema wao kama Familia wamekaa tayari wamekubaliana Mtoto Anna ataishi na Mama yake Mdogo ambaye ni Isabella Raymond Lyimo.

Kwa upande wake Anna ameiomba serikali na jamii nzima kutomuacha peke yake. " Naombeni muwe na moyo wa kunisaidia mpaka pale ambapo nitatimiza ndoto zangu na ninawaahidi mkiniruhusu na mkinisaidia nitasoma kwa bidii ilo nije kiwasaidia wenzangu wengine ambao wako kwenye matatizo kama ya kwangu au wenye matatizo mengine," amesema Anna.

Naye Mama Mdogo wa Anna anayeenda kuishi na Mtoto huyo mkoani Arusha, Isabella Lyimo amesema, anamuomba mungu ampe nguvu za kumlea Anna, na amelipokea ombi hilo kwa moyo mmoja kwa kuwa Anna mwenyewe pia amemchagua yeye kuishi naye.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. John Jingu akizungumza walipomtembelea Mtoto aliyepoteza Wazazi wake wote kwa mpigo na Wadogo zake watatu, Anna Zambi nyumbani kwao Goba jijini Dar es Salaam 
 Mtoto  Anna Zambi akizungumza na vyombo vya habari leo nyumbani kwao Goba jijini Dar es Salaam

Mtoto  Anna Zambi akifarijiwa na Watu mbalimbali waliomtembelea nyumbani kwao Goba jijini Dar es Salaam
Mama Mdogo, Isabella Raymond Lyimo akizungumza na Waandishi wa Habari, Goba jijini Dar es Salaam. 
Msemaji wa Familia, Ibrahim Zambi akizungumza na Waandishi wa Habari, Goba jijini Dar es Salaam wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya alipofika nyumbani hapo.

TFF YAFANYA MAZUNGUMZO NA CHAMA CHA SOKA CHA UMOJA WA NCHI ZA FALME ZA KIARABU (UAE FA)

0
0
Rais wa TFF Wallace Karia leo amefanya Mazungumzo na Rais wa Chama cha Soka cha Umoja wa Nchi za Falme ya Kiarabu Eng.Marwan Bin Ghalita(Watatu kutoka kushoto) mazungumzo yaliyohudhuriwa na Katibu Mkuu TFF Kidao Wilfred na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka UAE Mohamed Abdulla Hazzam Al Dhahari,mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Chama cha Soka UAE,pande hizo mbili zimekubaliana kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali.

WADAU WA ELIMU TIMIZENI WAJIBU SIMIYU IENDELEE KUNG’ARA KIELIMU: RAS SIMIYU

0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na viongozi na wataalam wa elimu kuanzia ngazi ya shule, kata, wilaya na Mkoa pamoja na wadau wengine mkoani Simiyu katika kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha Taaluma mwaka 2020 Mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Novemba 16, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wataalam wa elimu kuanzia ngazi ya shule, kata, wilaya na Mkoa pamoja na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu, wakimsikiliza Karibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini wakati akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha Taaluma mwaka 2020 Mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Novemba 16, 2019 Mjini Bariadi.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akiwasilisha taarifa ya Maendeleo ya Elimu mkoani humo, katika kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha Taaluma mwaka 2020 Mkoa wa Simiyu , kilichofanyika Novemba 16, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na viongozi na wataalam wa elimu kuanzia ngazi ya shule, kata, wilaya na Mkoa pamoja na wadau wengine mkoani Simiyu katika kikao cha kutangaza mkakati wa Mkoa wa kuboresha Taaluma mwaka 2020, kilichofanyika Novemba 16, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wataalam wa elimu kuanzia ngazi ya shule, kata, wilaya na Mkoa pamoja na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu, wakimsikiliza Karibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini wakati akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha Taaluma mwaka 2020, kilichofanyika Novemba 16, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wataalam wa elimu kuanzia ngazi ya shule, kata, wilaya na Mkoa pamoja na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu, wakimsikiliza Karibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini wakati akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha Taaluma mwaka 2020, kilichofanyika Novemba 16, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wataalam wa elimu kuanzia ngazi ya shule, kata, wilaya na Mkoa pamoja na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu, wakimsikiliza Karibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini wakati akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha Taaluma mwaka 2020, kilichofanyika Novemba 16, 2019 Mjini Bariadi.

……………..

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ametoa wito kwa viongozi, wataalam wa Elimu, jamii na wadau wote wa elimu kila mmoja kutimiza wajibu wake, ili mkoa wa Simiyu uendelee kufanya ya vizuri kielimu na uwe miongoni mwa mikoa mitatu bora inayofanya vizuri katika ufaulu wa mitihani yote ya Taifa.

Sagini ameyasema hayo Novemba 16, 2019 wakati akizungumza na viongozi, wataalam na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu katika kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mwaka 2020 kilichofanyika Mjini Bariadi.

“Tukitoka hapa kila mtu akitimiza wajibu wake nina uhakika tutautekeleza mkakati huu wa kuboresha taaluma, matarajio yetu ni kusonga mbele si kurudi nyuma, dhamira yetu iwe kuwa namba moja, mbili na tatu,” alisema Sagini.

Aidha, Sagini amesema ni vema walimu wakaboresha mfumo wa ufundishaji kwa wanafunzi wao ambao utawaandaa kwa umahiri katika mitihani yao ikiwa ni pamoja na kuwapa majaribio na mitihani ya mara kwa mara.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema azma ya viongozi, wataalam na wadau wa elimu mkoa wa Simiyu ni kuufanya mkoa kuwa miongoni mwa mikoa yenye mafanikio kielimu, ambapo azma hii imeonekana kutimizwa kupitia matokeo ya mitihani ya Kitaifa ya mwaka 2017, 2018 na 2019 ambayo ufaulu wake ulikuwa mzuri.

“Kidato cha nne 2017 mkoa ulikuwa wa 11 kati ya mikoa 31 mwaka 2018 ukawa wa 9 kati ya mikoa 31; kidato cha sita mwaka 2018 mkoa ulikuwa wa 10 na mwaka 2019 umeshika nafasi hiyo hiyo ya 10 kati ya mikoa 31, darasa la saba mwaka 2018 mkoa ulikuwa wa 22 na mwaka 2019 mkoa umeshika nafasi ya 8 kati ya mikoa 31 na ufaulu umekuwa ukipanda pia kila mwaka,” alisema Hinju.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo amewapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayofanya ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ufaulu na kuuweka mkoa katika nafasi nzuri kielimu.

Mwl. Milembe Mange kutoka Shule ya Msingi Sangida Bariadi amesema, Mkakati wa taaluma umetoa dira katika maeneo mengi ya kuboresha elimu ikiwemo ushirikishaji wadau hususani wazazi, ambapo kupitia ushirikishwaji huo, wazazi wataendelea kushirikishwa katika kuchangia ujenzi wa madarasa yatakayosaidia kupunguza idadi ya wanafunzi darasani na kuboresha mazingira ya kujifunzia.

Kwa upande wake, Mdhibiti Ubora wa Shule katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mwl. John Magwila amesema wadhibiti ubora wote wa Mkoa wa Simiyu watahakikisha wanakagua katika shule zote kujiridhisha utekelezaji wa masuala yote muhimu yaliyoainishwa katika mkakati wa kuboresha taaluma, ili kufikia lengo la kuongeza ufaulu na kuufikisha mkoa katika nafasi tatu bora kitaifa kwenye mitihani yote ya Kitaifa.

Mkakati huu Simiyu umezingatia vipaumbele kadhaa baadhi ya hivyo ni uwajibikaji wa maafisa elimu kata na mfumo mzima wa utawala, huduma bora na mawasiliano kubalika kwa walimu na wadau wa elimu, utoaji wa motisha na zawadi kwa wadau wanaofanya vizuri, ufuatiliaji kambambe wa ufundishaji na ujifunzaji, upimaji, mafunzo kazini na kambi za kitaaluma.

KAMPUNI YA VISA YAZINDUA KAMPENI YA KUFANYA MALIPO KWA NJIA YA VISA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA SIKUKUU YA KRISMASI, WATEJA KUPATIWA ZAWADI 

0
0
Na Said Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

KAMPUNI ya Teknolojia ya malipo ulimwenguni(VISA) imezindua kampeni katika msimu huu wa sikukuu Watanzania wenye kadi ya  VISA wataweza kufanya malipo yao ya manunuzi bila kutumia fedha taslimu ambapo pia watakaofanya manunuzi watapata zawadi mbalimbali .

Kampeni hiyo imezinduliwa jijini Dar es Salaam na Kampuni ya VISA imewahimiza wanunuaji bidhaa katika Jiji hilo kwenda katika maduka makubwa kwa ajili ya kufanya manunuzi katika msimu huu wa sikukuu.

Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Meneja wa VISA nchini Tanzania Olever Njoroge amesema itaendelea hadi Desemba 22 mwaka huu ambapo wateja ambao watafanya malipo kwa kutumia kadi ya VISA na VISA kwenye simu ya mkononi  watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali.

Amesema kampeni hiyo ambayo wameizundua kwa ajili ya wateja wenye Kadi za VISA ina malengo  ya kuhamasisha utumiaji wa kadi ya VISA au VISA kwenye simu wakati wa manunuzi katika maduka ya Mliman City Mall, Shoppers Masaki na Shopers Mikochoni.

"Kampeni hii ina malengo ya kukuza utumiaji wa kadi ya VISA na VISA kwenye simu ya mkononi, Tunawahamiza wateja wetu wa Tanzania kufanya malipo kwa njia ya Visa ambapo itawapa urahisi na usalama kipindi cha manunuzi wakati huu wa Krismasi,"amesema Njoroge.

Ameongeza kuwa wanaileta VISA kwa Watanzania wakizingatia faida katika kufanya manunuzi yao kwa kutumia kadi ya VISA au VISA kwenye simu ya mkononi ma kwamba wanajivua kwamba sasa Watanzania wapo huru kutumia njia mpya za malipo bila kuwa na fedha mkononi.

Amefafanua kuwa kampeni hiyo ya Krismasi na VISA itawapa wanunuzi  fursa ya kuchagua Zawadi za aina gani kumpatia mteja wao kwa njia rahisi na salama wanaponunua bidhaa kwenye Mall.

Amesema mapema mwaka huu VISA kwa kushirikiana na benki 15 za Tanzania wazilizindua VISA kwa njia ya simu ya mkononi ."VISA kwa kushirikiana kwa njia ya simu ya mkononi ni suluhisho la malipo ya dijiti ambayo inaruhusu watumiaji kutumia fedha kwa kila mmoja bila kulipa ada ya ununuzi. 

"Kutumia huduma hiyo ,mtu anapaswa kupakua app ya benki yake, atafute VISA kwenye app na alipe  bidhaa na huduma kwa kuiscan code ya QR au kwa kutumia nambari ya USSD,"amesema huku akielezea wazi Watanzania wengi wamekuwa na muamko mkubwa wa kutumia VISA kufanya malipo katika manunuzi mbalimbali.
 Mfanyakazi wa Kampuni ya VISA Mary Njau (kushoto) akiwa na moja ya wateja wanatumia VISA kufanya malipo wakati wa uzinduzi wa kampeni inayoitwa  'Sherekea na Visa' ambayo imezinduliwa jijini Dar es Salaam

KAMBI YA MAGEREZA KATESH YAPEWA LENGO LA KULISHA MAGEREZA YOTE YA MKOA WA MANYARA

0
0


Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Phaustine Kasike(kushoto) akikagua maandalizi ya awali ya shamba la mahindi alipofanya ziara ya kikazi leo Novemba 17, 2019 katika Kambi ya Magereza – Katesh iliyopo wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Manyara, ACP. Lipina Lyimo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) akikagua moja ya trekta linalotumika kwa shughuli za Kilimo katika Kambi ya Magereza – Katesh iliyopo wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara, leo Novemba 17, 2019 alipotembelea Kambi hiyo.
Moja ya maghala ya kuhifadhia mazao mbalimbali yanayozalishwa katika Kambi ya Magereza – Katesh iliyopo wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua mradi wa tofali za saruji ambazo zinafyatuliwa katika Gereza la Babati tayari kwa ujenzi wa nyumba za Maafisa na askari wa kituo hicho.(Picha zote na Jeshi la Magereza).




Na ASP. Lucas Mboje, Hanang;

KAMBI ya Magereza Katesh imepewa malengo mahususi ya kuzalisha mahindi ili kutosheleza mahitaji ya chakula cha wafungwa na mahabusu katika magereza yote ya Mkoa wa Manyara.

Hayo yamebainishwa leo na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike alipotembelea kambi hiyo kwa lengo la kujionea hatua mbalimbali za awali za maandalizi ya kilimo katika msimu 2019/2020.

Kamishna Jenerali Kasike amesema kuwa kambi ya Katesh ni moja ya eneo la kimkakati katika kutimiza lengo la uzalishaji wa chakula cha wafungwa na Mahabusu katika Mkoa wa Manyara.

“Kambi ya Magereza Katesh ni eneo ambalo lina fursa kubwa ya ardhi yenye rutuba na inayofaa kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali ya chakula na ya kibiashara hivyo lazima tuhakikishe kuwa tunafanikisha malengo tuliyopewa na Serikali kuhusu uzalishaji wa chakula cha wafungwa,” amesisitiza Jenerali Kasike.

Kwa upande wake Mkuu wa Kambi hiyo, Mkaguzi wa Magereza Nasoro Juma amesema kuwa katika msimu wa kilimo 2019/2020 tayari wameanza maandalizi ya awali na wanatarajia kulima ekari 150 za mahindi na ekari 50 za zao la arizeti ili kufanikisha lengo la mahitaji ya chakula cha wafungwa katika Magereza ya Mkoa wa manyara.

Kambi ya Magereza Katesh ilianzishwa rasmi mwaka 2009. Kambi hii ina ukubwa ekari 300 ambapo ekari 200 ndizo zinazofaa kwa shughuli za kilimo cha mahindi, Arizeti na mazao mengineyo ya kibiashara ikiwemo zao la dengu.

WANAHARAKATI WAMTAKA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUHOJI MAAMUZI YA VYAMA VILIVYOJITOA

0
0
Aliyewahi kuwa mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Mkuranga Kunje Ngombale Mwiru akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuomba msajiri kuchukua hatua ya kuchunguza maamuzi ya vyama vya saisa vilivyojitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, Kulia ni Mwanaharakati Felix Makuwa anayeiwakilisha Taasisi ya Society Awareness.
Mwanaharakati Felix Makuwa anayeiwakilisha Taasisi ya Society Awareness akifafanua jambo katika mkutano huo, kulia ni Aliyewahi kuwa mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Mkuranga Kunje Ngombale Mwiru.

.....................................................

Wanaharakati wa masuala ya kisiasa aliyewahi kuwa mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Mkuranga Kunje Ngombale Mwiru pamoja na mwanaharakati mwenzie anayeiwakilisha Taasisi ya Society Awareness Felix Makuwa,wamemtaka Msajili wa vyama vya siasa kuvihoji vyama vilivyotangaza kujitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa ili aweze kubaini kama kweli maamuzi yao yalitokana na makubaliano ya halmashauri kuu za vyama hivyo lkama siyo ubinafsi wa viongozi wachache katika vyama hivyo.

Viongozi hao wamesema wanachoaamini wao viongozi wa ngazi za juu wa vyama hivyo wametoa maamuzi hayo bila maamuzi ya vikao halali ndani ya vyama hivyo wakidai kuwa mara nyingi viongozi hao wamekuwa wakurupukaji wanaofanya mambo yao kinyemela suala walilosema limekuwa likiua demokrasia ndani ya vyama hivyo.

Wamewataka watanzania kuachana na siasa ‘uchwara’ wanazodai kufanywa na vyama vilivyotangaza kujitoa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 Mwaka huu.

“Wanayoyasababisha haya yote yanayoendelea ni viongozi wa juu wa vyama vya upinzani, tena baadhi yao wameenda mbali na kukejeli kuwa vyama vingine katika uchaguzi huu havina hata wabunge bungeni hata vikiamua kushiriki, hiyo ni kejeli zaidi msajili anapaswa kuvifuatilia ili kuona kama vilijitoa kutokana na maamuzi ya halmashauri kuu za vyama hivyo” amesema Kunje.

Wamesema wanachoamini vyama hivyo vyenye wabunge ndiyo hasa vinavyoua suala la upinzani kwa kuwa mara nyingi wabunge wao hutoa ahadi hewa kwa wananchi kwa kuwatajia mambo mengi ambayo endapo watapewa ridhaa watawafanyia lakini mwisho wa siku huishia kuvimbisha matumbo yao bila kutekeleza jambo walilosema huwapa hasira wananchi hao na kukataa kuwapa kura zao kipindi kingine.

“Tena itapendeza kama msajili wa vyama vya siasa atawashughulikia wabunge hao ambao baadhi yao wamekuwa wakichukua posho za bure bungeni bila hata kuingia katika vikao vya bunge zaidi wamekuwa wakipiga kelele zisizo na tija na kusababisha maneno ya hovyo katika jamii".Ameongeza Mwiru 

Akitoa mfano Mwanaharakati Kunje Ngombale Mwiru amesema "Nilipotangaza kumuunga mkono Rais John Magufuli wakati Nikigombea Ubunge Mwaka 2015 katika jimbo la Mkuranga , niliona hakuna sababu ya kupoteza kura yake kumchagua rais asiye faa zaidi ya kiongozi huyo ambaye hadi sasa ameweza kuipa thamani kura yake kwa kufanya mambo mengi ya kimaendeleo nchini.

Ameongeza kuwa kama ingewezekana uchaguzi ujao asisimame mgombea yoyote katika nafasi ya kiti cha urais na kumuacha Rais Magufuli aendelee na nafasi yake ili kuokoa fedha ambazo zingetumika katika kampeni yake ziweze kwenda katika kuhudumia maendeleo.

“Rais aachwe katika nafasi yake, tukachague wabunge tu, anafanya mambo mazuri katika taifa hili ambayo kila mtanzania anayaona” Amesema Mwiru.

Naye Mwanahrakati Felix Makuwa amesema hii tabia ya kususasusa kutoka katika vyama vya upinzani siyo jambo la kushangaza kuona vikisusia tena uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa sababu ni mazoea yao na hii tabia inaua Demokrasia kwa sababu maamuzi ya kususia uchaguzi yanafanywa na vipongozi wa juu kwa kuwashurutisha wagombea wao ilihali wagombea bado wanataka kuendelea na uchaguzi .

TANZANIA YAKABIDHI SHEHENA YA KWANZA YA MBEGU ZA KOROSHO NCHINI ZAMBIA

0
0
Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia, na Mhe. Mukela Manyindo Waziri Mkuu wa Jimbo la Mongu (katika ngazi ya kimila) wakikata utepe kuashiria mapokezi ya mbegu za korosho katika hafla iliyofanyika Mongu, Zambia 
Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia akihutubia adhira iliyojitokeza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mbegu za korosho jimbo la Mongu, Zambia tarehe 16 Novemba, 2019 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi shehena ya mbegu za korosho kwa Serikali ya Jamhuri ya Zambia katika hafla iliyofanyika mjini Mongu nchini humo. 

Korosho hizo zimekabidhiwa kufuatia ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. 

Edgar Lungu kwenye uzinduzi wa Kituo cha Pamoja cha Huduma Mpakani (OSBP) Tunduma tarehe 5 Oktoba, 2019.Katika tukio hilo Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia, nakwa upande wa Zambia, Serikali aliwakilishwa na Waziri wa 
Jimbo la Mongu Mhe. Richard Kapita, Watendaji kutoka Serikalini na viongozi wa Kimila.

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Kapita kwa naiba yaSerikali ya Jamhuri ya Zambia ametoa shukurani za pekeekwa Mhe. Rais Magufuli kwa upendo aliouoneshakwa Zambia na kwa upekee kabisa kwa wananchi wa jimbola Mongu.

Aliongezea kusema wananchi wa Mongu wanamatumaini makubwa kuwa, mbegu hizo zitawapa 
chachu ya kuzalisha korosho kwa wingi na kunufaika kiuchumi kama ambavyo imekuwa kwa wananchi waTanzania
Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia (kushoto) na Waziri wa Jimbo la Mongu Mhe. Richard Kapita (kulia) wakijadili jambo muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhi na kupokea korosho iliyofanyika Mongu, Zambia 
Waziri wa Jimbo la Mongu, Zambia Mhe. Richard Kapita akihutubia hadhira iliyojitokeza kwenye hafla ya mapokezi ya mbegu za korosho 
Picha ya pamoja baada ya hafla ya kukabidhi mbegu za korosho 
Mhe. Hassan Simba Yahaya Balozi wa Tanzania nchini Zambia (kushoto) na Afisa kutoka Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia wakifuatilia tukio lililokuwa likiendelea wakati wa hafla ya kukabidhi mbegu za korosho 
Shemu ya wananchi wa Mongu, Zambia waliojitokeza kwenye hafla ya mapokezi ya mbegu za korosho 

MILIONI 254 ZAKAMILISHA MAKAZI YA FAMILIA SITA ZA ASKARI MKOANI TABORA

0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora (RPC) Barnabas Mwakalukwa akitoa salama Jeshi hilo jana wakati wa uzinduzi wa nyumba mpya za makazi mapya ya Askari mjini Tabora.


Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tabora (Serikali za Mitaa) Nathalis Linuma akitoa salamu za Mkoa jana wakati wa sherehe fupi ya uzinduzi wa nyumba mpya Askari mjini Tabora.

Baadhi ya Maaskati na Wageni waalikwa walioshiriki uzinduzi wa nyumba mpya za makazi ya askari jana mjini Tabora.Picha na Tiganya Vincent

………………..

NA TIGANYA VINCENT

MAJENGO matatu ya makazi mapya ya Polisi yamegharimu jumla ya shilingi milioni 254 kukamilika zikiwemo zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na wadau Mkoani Tabora.

Akisoma risala wakati wa uzinduzi wa majengo hayo Marakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Msabila Kulwa Bundala alisema kila jengo lina nyumba mbili za makazi ambalo kila moja limegharimu shilingi milioni 84.6.

Alisema katika kiasi cha fedha cha shilingi bilioni 10 , Mkoa wa Tabora ulipata shilingi milioni 150 ambapo wadau wa Jeshi hilo walichangia zaidi ya milioni 100.
Bundala alisema michango ya wadau ilijumuisha fedha tasimu , saruji , vifaa vya umeme na maji.

Naye Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tabora (Serikali za Mitaa) Nathalis Linuma alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuboresha makazi ili wawe na mazingira mazuri ya kuishi na kutoa huduma nzuri kwa jamii.

Alisema maendeleo hayana mwisho ni vema utaratibu wa jamii kushirikiana na Polisi kuboresha mazingira ya kuishi na kufanyia kazi yakaendelea ili kuwawezesha kuishi sehemu moja ambayo itakuwa rahisi kuisaidia jamii pindi wanapohitajika.
Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Barnabas Mwakalukwa alitoa wito kwa wadau mbalimbali Mkoani Tabora kusaidia kukamilisha majengo ya Ofisi likiwemo la Asakari wa Usalama barabarani ambayo yalianza kujengwa mwaka 2015 ambayo yamesimama.

Alisema uwepo wa Ofisi ya za kutosha utaongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa kuwa na mazingira mazuri ya kutoa huduma kwa wananchi mbalimbali.

ONGEZEKO LA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA TISHIO LA MAISHA

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala(katikati) akipima uzito jana wakati wa uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza kwa Mkoa wa Tabora.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala (aliyekaa) akipima Shinikizo la Damu jana ikiwa ni sehemu ya kushiriki uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukizwa kwa Mkoa wa Tabora.
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Tabora wakishiriki mazoezi ya viuongo jana ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha uzinduzi wa wiki ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukizwa.
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Tabora wakisikiliza mada mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha uzinduzi wa wiki ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukizwa kwa Mkoa wa Tabora jana.
Katibu Tawala Msaidizi (Afya) Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha utatinisibwa akitoa taarifa kuhusu ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa Mkoa wa Tabora jana ikiwa ni sehemu ya wiki ya maadhimisho ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa hayo.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Hamis Mkunga akitoa salamu za Mkoa jana wakati wa wiki ya maadhimisho ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala akizundua jana wiki ya maadhimisho ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza kwa Mkoa wa Tabora.Picha na Tiganya Vincent

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Tabora wakishiriki mazoezi ya kukimbia jana ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha uzinduzi wa wiki ya Kampeni ya kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukizwa.


NA TIGANYA VINCENT

IDARA ya Afya Mkoani Tabora imesema kuwa jitihada za makusudi zinahitajika kuzuia na kudhibiti ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza mkaoni humo.

Baadhi ya magonjwa yasiyoambukizwa ni kisukari, shinikizo la damu, seli mundu, saratani , magonjwa ya akili na pumu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni wa kuzuia na kudhibiti magonjwa hayo Katibu Tawala Msaidizi (Afya) Dkt. Honoratha Rutatinisibwa alisema toka mwaka 2017 hadi 2019 kumekuwepo na ongezeko la magonjwa hayo Mkoani humo.

Alitaja baadhi ya wagonjwa wa magonjwa yasioambukizwa waliongeza kuwa ni kisukari ambapo mwaka 2017 walikuwa 4,345 na kuongezaka hadi kufikia 6,732 mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la wagonjwa 2,387 sawa na asilimia 35.

Dkt. Rutatinisibwa alisema kwa upande ugonjwa wa Shikizo la Damu, wagonjwa wameongezeka katika kipindi hicho hicho kutoka 13,940 hadi kufikia 19,460 ikiwa ni ongezeko wagonjwa 5,520 sawa na asilimia 28.

Aliongeza kuwa upande wa ugonjwa wa pumu umeongezeka kutoka wagonjwa 5,338 hadi kufikia wagonjwa 8,434 ikiwa kuna ongezeko la wagonjwa 3,096 sawa na asilimia 37 ndani ya kipindi hicho hicho.

Akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya maadhimisho ya Kapambana na magonjwa hayo ,Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala aliwataka wakazi wa Mkoa wa Tabora kujenga tabia ya kuchunguza afya zao mapema walau mara mbili kwa mwaka.

Alisema hatua hiyo itasaidia kugundua matatizo mapema na kuwahi kukabiliana nalo likiwa bado katika hatua za awali kwa kutumia gharama kidogo.
Kitwala aliongeza kuwa suluhisho jingine ambalo halihitaji gharama kubwa kukabiliana na tatizo hilo ni pamoja na wakazi wa Tabora kubadili mfumo wa maisha juu ya ulaji wa vyakula na kushiriki mazoezi.

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 18,2019

0
0

             
 

NMB YAFUNGUA TAWI JIPYA MBEZI LOUIS

0
0
MKUU wa Wilaya ya Ubungo – Kisare Makori, akikata Utepe kuzindua rasmi Tawi jipya la Benki ya NMB Mbezi Louis wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika juzi Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam – Badru Idd, Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa NMB – Omari Mtiga, Katibu Tawala Wilaya ya Ilala – James Mkumbo na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Fortunata Shija.
MKUU wa Wilaya ya Ubungo – Kisare Makori (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB – Omari Mtiga (wa pili kulia) wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi jipya la NMB Mbezi Louis. Kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam – Badru Idd.


Benki ya NMB imefungua tawi lake jipya jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa mpango wake wa kufikisha huduma za kibenki kwa Watanzania wengi ili kuchochea ukuaji wa uchumi.

Ufunguzi wa tawi hilo la NMB Mbezi Louis unaifanya benki hiyo kuwa na jumla ya matawi matano ndani ya wilaya ya Ubungo pekee. 

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa tawi hilo mwishoni mwa wiki, mkuu wa kitengo cha wateja binafsi wa NMB, Omari Mtiga, alisema uamuzi wa kufungua tawi hilo umetokana na tafiti mbalimbali zilizoonyesha kuwa Mbezi Louis ni eneo linalokuwa kwa kasi katika biashara.

“Tumeona eneo hili linakuwa kwa kasi sana kibiashara lakini wateja wetu bado wamekuwa wakilazimika kusafiri kilometa 15 wakifuata huduma zetu katika matawi ya Ubungo, Sinza, Mlimani City na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Sambamba na kauli mbiyo yetu ya: Karibu Yako, tumeona tufungue tawi hapa hapa,” alisema.

Akifungua tawi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, alisema upatikanaji wa huduma za kibenki ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

“Ufunguzi wa tawi hili la NMB utasaidia kukuza idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki ambao kwa hivi sasa wapo chini ya asilimia 20,” alisema.

Aliipongeza NMB kwa kuja na njia za kidijiti za kufikisha huduma zake kwa Watanzania, akitolea mfano wa huduma inayowezesha watu kufungua akaunti ya benki hiyo moja kwa moja kwa kutumia simu za mkononi bila kulazimika kwenda katika tawi lolote la benki.

“Hivi karibuni, NMB imekuja na huduma inayolenga kuwahudumia waendesha bodaboda. Hii ni hatua inayostahili pongezi,” alisema Makori.

Tawi la Mbezi Louis linaifanya NMB kuwa na jumla ya matawi 224 nchi nzima

RC SONGWE ATEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII ILEJE,AFURAHISHWA NA MRADI WA SHAMBA LA IYONDO-MSWIMA.

0
0






RC wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemas Mwangela aliye mbele na DC wa Ileje Ndg.Joseph Mkude wakiwa kwenye Maporomoko ya Lusalala yaliyopo kwenye Mto Sange Wilayani Ileje
Mkuu wa Mkoa wa Songwe akiongozana na DC wa Ileje kutembelea kitalu cha miti cha Shamba la Iyondo Mswima.
Barabara ya Isoko hadi Katengele na Sange ikikatisha katikati ya msitu wa asili wa Iyondo Mswima wanamoishi nyani jamii ya mbega wenye rangi nyeupe na nyeusi moja ya vivutio vya utalii.
Mzee Yangison Mtawa aliye kushoto akitoa maelezo kwa RC Mwangela wa Songwe ambapo alielezea ugumu wa soko kwa bidhaa za mianzi anazozalisha.
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Songwe na Wilaya ya Ileje wakigongeana glasi kusherekea Siku ya Kuzaliwa ya Mkuu wa Mkoa wao Nicodemas Mwangela aliyetimiza miaka 62.



Na Daniel Mwambene Ileje Utalii

RC wa Songwe atembelea vivutio vya utalii wilayani Ileje afurahishwa na Mradi wa Shamba la Iyondo-Mswima akihimiza kulindwa kwa misitu ya asili iliyopo wilayani humo asherehekea siku yake ya kuzaliwa katika vilele vya milima ya shamba hilo.

Ukiwa ni mwisho wa juma siku ya Jumamosi Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemas Mwangela alitembelea vivutio vya utalii vilivyopo wilayani Ileje ikiwa ni sehemu ya utalii wa ndani kwa timu nzima aliyokuwa amefuatana nayo.

Ziara hiyo ya siku moja ilimwezesha kufika hadi Kijiji cha Ndembo mahali panapozalishwa nyungo zitokanazo na mianzi ambapo aliweza kukutana na wasukaji akiwahimiza kuungana kkatika vikundi ili kuweza kutambuliwa na serikali na kuongeza uzalishaji wenye tija.

Kiongozi huyo,aliweza kufika nyumbani kwa Mzee Mtawa akiagiza uongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanamsaidia kutafuta soko la bidhaa anazozalisha mzee huyo baada ya kuambiwa kuwa amekuwa akisubiri tu matukio kama vile nane nane na kimondo baada ya hapo bidhaa alizozalisha kwa gharama zikihifadhiwa.

Safari hiyo ikiendelea kwa kuupanda mlima Kashima ambao kwa madereva wengine huwa ni kipimo tosha cha fani hiyo kutokana na kona kali zilizofunikwa na misitu ya asili inayoongeza radhaa a utalii.

Alipofika katika Mradi wa Shamba la Miti wa Iyondo Mswima aliweza kupokea taarifa ya mradi huo toka kwa Meneja wa hamaba Ndg.Deograsian Kavishe akiridhishwa na taarifa hiyo jinsi inavyoakisi uhalisia wa mazingira ya eneo hilo na kuwa kiutio tosha cha kitalii.

Msafara ulielekea shamani ilikopandwa miti,huku macho yakiendelea kufaidi mandhari nzuri ya vilele vya milima vilivyofunikwa nyasi fupi ambazo baadeya zaweza potea kutokana na kufunikwa na miti inayoendelea kupandwa.

Mara baada ya kufika sehemu maalum iliyokuwa imeandaliwa likafanyika tukio la kukumbuka tarehe ya kuzaliwa kiongozi huyo yaani ikifurahiwa na kila mmoja kutokana na mahali ilipoandaliwa huku ikinyunyiziwa na manyunyu yaliyoshuka polepole yakiashiria neema na utukufu wa Mwenyezi Mungu.

Mwisho wa safari yake ilikuwa ni katika Maporomoko ya Lusalala yaliyopo kwenye Mto Sange ambapo kuliweza kuwatoa jasho watalii hao wa ndani kutokana na mteremko mkali ambao haukuonesha kumteteresha Brigedia Jenerali huyo mstaafu.

MISS TANZANIA 2019 AKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA DUNIA

MKUTANO WA WAFADHILI WA TAFITI KUFANYIKA MEI, 2020 NCHINI AFRIKA KUSINI, MKUTANO WA DAR WAFUNGWA

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolijia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa ufunga mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu uliokuwa ukifanyika kuanzia Novemba 11-15 katika Hoteli ya Serena. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya utafiti ya taifa nchini Afrika Kusini, Dkt. Molapo Qhobela.

Na Avila Kakingo, Globu ya jamii.
MKUTANO wa sayansi, teknolojia na ubunifu wa fungwa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa Mkutano wa mkubwa utakaofanyika nchini Afrika ya Kusini Mei 2020 kwa nchi zote duniani zinazofadhili utafiti katika nchi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolijia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu, amesema kuwa sasa wako kwenye maandalizi ya mkutano wa kimataifa wa nchi zinazofadhili utafiti dunianikote.

"Leo tulikutunajadili kuhusiana na maandalizi ya mkutano mkuu utakaofanyika Afrika Kusini hapo 2020" utakaohusisha mataifa yanayofadhili utafiti duniani kote".

Pia Dkt. Nungu amewaasa wanaofanya utafiti wa kisayasni waaswa kufanya tafiti zinazotatua matatizo ya jamii na sio matatizo ya leo tuu.

Amesema kuwa katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam wamejadili mambo mbalimbali ili kuboresha tafiti kwa kila nchi ya kusini mwa Jangwa la Sahara.

"Tulikuwa tunaangalia mifumo ya maendeleo na ubunifu, uwekezaji kwenye utafiti kwaajili ya maendeleo ya nchi zetu tumejadili kwa mapana kubadilishana uzoefu, lakini Pia tuliangalia kwa hawa wafadhili kuwa na mashirikiano yenye usawa wakati wa kufanya utafiti".

Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya utafiti ya taifa nchini Afrika Kusini, Dkt. Molapo Qhobela amesema kuwa Mkutano huu umefanikiwa sana nchi 15 za kusini mwa jangwa la Sahara za utafiti kwa Dar es Salaam tumefanikiwa kujadili mada mbalimbali na kubadilishana uzoefu wa kitafiti.

Dkt Molapo Amesema kuwa kwa Tanzania Tumemaliza kwa mafanikio makubwa na kwa mwakani 2020 utafanyika nchini Afrika Kusini.

MBUNGE MUSA SIMA ATOA PHOTOKOPI MASHINE MASHULENI MKOANI SINGIDA

0
0
Mbunge wa Singida mjini ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano Mazingira), Musa Sima. 


Na Dotto Mwaibale, Singida.

MBUNGE wa Singida mjini ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano Mazingira), Musa Sima ametoa photokopi mashine sita kwa ajili ya kurahisisha kazi katika shule za msingi na sekondari mkoani Singida.

Akizungumza juzi katika hafla ya kukabidhi photokopi mashine moja kwa Shule ya Sekondari ya Mufumbu iliyopo Kata ya Kisaki mkoani hapa alisema lengo lake ni kuhakikisha walau kila shule zilizopo katika jimbo lake la uchaguzi zinapata mashine hizo.

"Changamoto kubwa iliyopo katika shule zetu ni kupata huduma ya photokopi mashine kwani wanalazimika kwenda mjini au kwa watu binafsi jambo ambalo linawapotezea muda na ndio maana nimeguswa kusaidia katika eneo hilo" alisema Sima.

Alisema mpaka sasa amekwisha toa photokopi nne katika shule za sekondari na moja katika shule ya msingi na nyingine kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Singida.

Katika hatua nyingine Sima amemshukuru Rais Dkt.John Magufuli kwa kuwapatia vifaa vya maabara ambapo Shule ya Sekondari ya Mufumbu imekuwa ya kwanza kupata vifaa hivyo.

Alisema katika kumuunga mkono Rais Dkt.John Magufuli katika sekta ya afya na elimu ametoa mifuko ya saruji 300 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Kisaki.

Sima aliongeza kuwa katika sekta ya elimu amemsaidia kumsomesha mwanafunzi aliyefanya vizuri mwaka 2018 katika mtihani wake kwa Kanda ya Kati aliyetoka Shule ya Sekondari ya Mufumbu aliyepata Divisheni 1.8 ambaye kwa sasa anaendelea na masomo shule ya Ilboru.

Mbunge Sima alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kujenga tabia ya kusaidia shughuli za maendeleo badala ya kuiachia serikali pekee.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images