Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

Wanafunzi wafaidika na elimu ya kuweka akiba kupitia Benki ya NMB

$
0
0
Katika kutambua umuhimu wa vijana ambao ni Taifa la kesho, Wanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya Wasichana ya Barbro Johansson Model iliyopo jijini Dar es Salaam, wamepata elimu ya fedha na umuhimu wa matumizi makini ya fedha ikiwemo kuweka akiba benki, walipotembelea Makao Makuu ya benki hiyo kujionea shughuli mbalimbali za kibenki kwa vitendo.
Kaimu Mkurugenzi wa NMB – Ruth Zaipuna akikata keki pamoja na wanafunzi.
Mmoja wa Wanaafunzi akimlisha kipande cha keki Kaimu Mkurugenzi wa NMB – Ruth Zaipuna akikata keki pamoja na wanafunzi.Pamoja na hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna amewaasa wanafunzi hao kuwekeza nguvu zaidi katika elimu, kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanatimiza malengo yao.

Wanafunzi wakifurahi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa NMB- Ruth Zaipuna na Mwalimu wao- Jennifer Dominick.
Wanafunzi wakipata elimu kutoka kwa Ofisa wa benki ya NMB- Monica Job. Wanafunzi hao walipata nafasi ya kujifunza na kutembelea idara na vitengo tofauti ili kufahamu shughuli zao lakini pia walitembelea Tawi la NMB Ohio. 

Baada ya mafunzo hayo, wanafunzi wote walipata nafasi ya kufungua akaunti zitakazowawezesha kutunza fedha na kujijengea tabia ya kuweka akiba na kunufaika na huduma na bidhaa za benki ya NMB hususan Chipukizi na Mwanachuo Akaunti.

BODI YA REA YAMPA SIKU 14 MKANDARASI WA UMEME MKOANI SIMIYU KUJIREKEBISHA

$
0
0
Kazi ya usimikaji nguzo ikifanyika katika Kijiji cha Mwasubuya wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu, mzunguko wa kwanza (REA III).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakili Julius Kalolo (wa tatu kushoto) akipata maelezo kuhusu kazi ya usambazaji umeme vijijini mkoani Simiyu. Anayetoa maelezo ni Mkurugenzi wa kampuni inayosambaza umeme mkoani Simiyu, Whitecity Guangdong JV, Nuhu Mringo (wa kwanza kulia). Wa Pili kulia ni Mjumbe wa Bodi ya REA, Dkt. Andrew Komba.
Kazi ya usambazaji umeme ikifanyika katika Kijiji cha Sesele wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu, mzunguko wa kwanza (REA III).





Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakili Julius Kalolo akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kabla ya kukagua kazi ya usambazaji umeme mkoani humo. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini na kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya REA, Dkt. Andrew Komba
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakili Julius Kalolo (wa tatu kulia) akikagua kazi ya usambazaji umeme katika Kijiji cha Sesele wilayani Bariadi. Wa Pili kulia ni Mjumbe wa Bodi ya REA, Dkt. Andrew Komba na wa Pili kushoto ni Meneja wa TANESCO, Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Rehema Mashinji.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakili Julius Kalolo (wa tatu kulia) akizungumza na vibarua wanaofanya kazi ya kusambaza umeme katika Kijiji cha Mwasubuya wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu. Wa Pili kulia ni Mjumbe wa Bodi ya REA, Dkt. Andrew Komba na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga.
……………….


Na Teresia Mhagama, Simiyu

Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imempa siku 14 mkandarasi wa umeme vijijini mkoani Simiyu kuongeza kasi ya usambazaji umeme katika vijiji alivyopangiwa la sivyo Bodi hiyo haitasita kuchukua hatua mbalimbali za kimkataba ikiwemo ya kusitisha mkataba.

Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Wakili Julius Kalolo alisema hayo tarehe 16 Novemba, 2019 wilayani Busega mkoani Simiyu mara baada ya kukagua kazi ya usambazaji umeme katika Vijiji mbalimbali vya wilaya ya Bariadi na Busega akiwa amembatana na Mjumbe wa Bodi hiyo, Dkt Andrew Komba na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga.

” Bodi haijaridhishwa na kasi ya mkandarasi huyu kwani amepewa kazi ya kupeleka umeme katika vijiji 152 vya Mkoa wa Simiyu lakini mpaka sasa amesambaza katika vijiji 54 ambayo ni takribani asilimia 30 tu ya kazi anayopaswa kufanya hivyo tumempa siku 14 aonyeshe mabadiliko la sivyo tutachukua hatua.” Alisema

Wakili Kalolo alieleza kuwa, Serikali imetimiza jukumu la kutoa malipo kwa mkandarasi huyo ili kazi ya usambazaji umeme ifanyike kwa kasi hivyo visingizio vya ucheleweshaji wa kazi havikubaliki kwani kwa mujibu wa mkataba wa mkandarasi huyo anapaswa kumaliza kazi mwezi Aprili mwaka 2020.

Aidha, alimwagiza mkandarasi huyo kampuni ya Whitecity Guangdong JV, kuwasilisha mpango kazi wake kwa Bodi hiyo, Mameneja wa TANESCO mkoani Simiyu pamoja Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu ili kuweza kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa kazi anazofanya.

Awali Bodi hiyo ilikutana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini ambapo, Mjumbe wa Bodi ya REA, Dkt. Andrew Komba alitoa shukrani kwa viongozi wa mkoa wa Simiyu kwa kufuatilia utekelezaji wa kazi ya usambazaji umeme vijijini.

Aidha, aliomba kasi hiyo iongezeke ili Mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA III) ukamilike kwa wakati.

Alisema kuwa, msukumo wa kuwafuatilia wakandarasi unahitajika ili kutimiza lengo la Serikali la kupeleka umeme katika vijiji vyote vilivyopo katika mpango wa REA III mzunguko wa kwanza ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.

Aidha alitoa wito kwa viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali za mkoa, kuhamasisha wananchi kujiunga na huduma ya umeme kwani Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika kuwasambazia umeme wananchi hivyo wanapaswa kuunganisha umeme kwa wingi na kuutumia katika shughuli za kiuchumi na kijamii

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 17,2019

RAIS MAGUFULI NA MKEWE JANETH MAGUFULI WASHIRIKI MISA TAKATIFU DOMINIKA YA 33 MWAKA “C” KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA OYSTERBAY JIJINI DAR

$
0
0
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli, Mama Marry Majaliwa (Mke wa Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa) pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 33 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko wa parokia hiyo Padre Dkt. Alister Makubi, Novemba 17, 2019. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli, Mama Marry Majaliwa (Mke wa Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa) wakipeana mikono ya Amani na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakati wa ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 33 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko wa parokia hiyo Padre Dkt. Alister Makubi, Novemba 17, 2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mtoto Cephas Kinunda mara baada ya ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 33 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko wa parokia hiyo Padre Dkt. Alister Makubi, Novemba 17, 2019.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Paroko wa parokia hiyo Padre Dkt. Alister Makubi na Mzee wa Kanisa Dkt. Adelhelm Meru mara baada ya ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 33 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Novemba 17, 2019.

TCRA WATOA ELIMU KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM- KILIMANJARO

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akisalimiana na Katibu wa chama cha Viziwi mkoa wa Kilimanjaro Christina Shirima .Picha zote na Vero Ignatus.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akipeana Mkono na Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akiendelea kusalimia na watu wenye mahitaji maalum leo katika Semina ya Siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Kanda ya Kaskazini (TCRA )
Baadhi ya Watumishi wa Malaka ya Mawasiliano Nchini Kanda ya Kaskazini kutoka katikati ni Mhandisi Mwandamizi Jan Kaaya,Wa kwanza kulia ni Lucy Mbogoro Afisa Masoko ,pamoja na Oswarld Octavian wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano Mkoani Kilimanjaro ilipofanyika Semina hiyo ya siku moja ya watu wenye mahitaji malum.
Watu wenye mahitaji maalumu wasioona na Viziwi wakiwa ukumbini tayari kwa kupatiwa elimu juu ya Umuhimu wa kusajili laini za simu kwa njia ya alama za vidole.
Mafunzo yakiendelea katika ukumbi wa ofisi ya mkoa wa Kilimanjaro leo.
Mkalimani akiendelea kuwatafsiria watu wenye mahitaji maalumu wasiosikia kile kinachoendelea katika mafunzo hayo ya siku moja yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya Kaskazini TCRA.
Watu wenye mahitaji maalumu wasisikia wakiwa makini katika mafunzo kama wanavyoonekana katika picha.
Baadhi ya watu wenye ulemavu wa kutokuona (vipofu)wakiwa katika semina ya siku moja iliyoandaliwa ma Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kanda ya Kaskazini yaliyofanyika leo Mkoani Kilimanjaro.
Makundi mawili ya watu wenye ulemavu Viziwi na Wasioona Vipofu wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira.


Na.Vero Ignatus,Kilimanjaro.

Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA Kanda ya Kaskazini imefanya mkutano wa siku moja na wadau wa mawasiliano wenye mahitaji maalum ,wakiwa katika makundi mawili viziwi na walemavu wa kutokuona .

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mwandamizi kutoka TCRA kanda ya kaskazini Jan Kaaya amesema lengo kuu ni kutoa elimu hususani usajili wa kutumia alama za vidole.

Kaaya amesekuwa walemavu wasioona na kusikia kutokana na mahitaji waliyonayo kwamba ni kundi ambalo linaweza kusahaulika kirahisi kutokana na hali zao,hivyo Mamlaka hiyo ikaamua kuwapa elimu ili watambue majukumu na wajibu wa kusajili laini zao simu.

Akifungua Semina hiyo siku moja Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amesema matumizi ya simu yasiwe mzigo kwa wananchi haswa kwenye eneo la mihamala ya fedha.

"Tunajua makampuni ya simu yatahitaji fedha kwaajili ya uendeshaji lakini isiumize wananchi bali iwe gharama nafuu." Alisema mkuu wa mkoa.

Ameyataka makampuni yote ya simu kuangalia uwezekano wa kupeleka mawasiliano vijijini kwani maeneo mengi wananchi wanateseka kutoka kata kwenda nyingine kwenda kingine kufuata mawasiliano.

Amesisitiza kuwa ni ukweli usiopingika kwamba asilimia kubwa ya mazao tunayotumia mijini yanatoka kijijini,hivyo vijijini wanahitaji huduma ya mawasikiano kwa asilimia ya juu zaidi kuliko mijini

"Jana nilikuwa kijiji cha Vudee wilaya ya Same watu wanatoka kata moja hadi nyingine sehemu yenye mnara ili wapate mawasiliano jambo ambalo ni usumbufu mkubwa kwa wananchi,nyie makampuni ya simu litazaneni jambo hili.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha wasiosikia mkoa wa Kilimanjaro Christina Shirima ameishukuru TCRA kwa kuwapatia elimu hiyo,pia amesema changamoto kubea waliyonayo ni kushindwa kupata vitambulisho vya NIDA kwa hivyo kukwamisha zoezi la kusajili laini zao za simu kwa wakati.

"Nashindwa kuelewa kwanini hivi vitambulisho vya NIDA vinachekewa kwetu sisi au kwa vile sisi ni walemavu !aliuza mlemavu asiyesikia Ahadiel Sowene Mphuru.

WAASWA KUZINGATIA SHERI, KANUNI NA TARATIBU

$
0
0
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe, Dkt. Atuganile Ngwala(kushoto) akitoa Mafunzo kwa Wasaidizi wa Kumbukumbu, Makatibu Mahsusi na Wasaidizi wa ofisi wa Mahakama hiyo, ambapo aliwataka kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao ya kazi. Aidha Dkt. Ngwala aliwataka watumishi hao kuzingaatia maadili ya kazi zao kuwa mstari wa mbele katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA). Kulia ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Dare Salaam, Mhe.Ruth Massam.
Msaidizi wa Kumbukumbu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Bi. Tupokigwe Mwaipopo akichangia jamboMsaidizi wa Kumbukumbu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Bi. Neema Lucasi akichangia jambo.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakiwa katika mafunzo hayo
(Picha na Magreth Kinabo- Mahakama)

NAIBU WAZIRI SHONZA AZINDUA MCHEZO FAINALI YA KIMSESE CUP KONDOA

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akipiga penati kuashiria kuanza kwa mchezo wa Fainali ya Kamsese Cup 2019 kati ya timu ya Kikilo na Masange iliyofanyika jana Wilayani Kondoa.

Mashindano hayo yaliyomalizika kwa timu ya Kikilo kuibuka mshindi yalishirikisha timu 21 kutoka katika kila kata ya Jimbo la Kondoa Vijijini yaliandaliwa na kuratibiwa na mbunge wa jimbo hilo Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambapo lengo kuu lilikuwa kuwaamasisha vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo pamoja na uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

WAZIRI MPINA AZINDUA AGENDA ZA UTAFITI NA KUIBUA TAFITI ZILIZOFICHWA MAKABATINI

$
0
0
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Agenda ya Kitaifa za Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA mjini Morogoro wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu SUA, Profesa Raphael Chibunda. Picha na Mpiga Picha Wetu
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Dar es Salaam, Feisal Mohamed Ally Agenda ya Kitaifa za Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 baada ya kuizindua katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA mjini Morogoro. Wengine Katikati ni Katibu Mkuu Mifugo, Prof. Elisante Ole Gabriel na Katibu Mkuu Uvuvi, Dk. Rashid Tamatamah Picha na Mpiga Picha Wetu
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akionesha kitabu cha Agenda ya Kitaifa ya Utafiti wa Mifugo muda mfupi baada ya uzinduzi wa Agenda ya Kitaifa za Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA mjini Morogoro wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu SUA, Profesa Raphael Chibunda. Picha na Mpiga Picha Wetu.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akimkabidhi Mdau wa Ufugaji Samaki kwenye Vizimba –Ziwa Victoria, Said Mecky Sadiq Agenda ya Kitaifa za Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 baada kuizindua katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Mjini Morogoro. Katikati ni Katibu Mkuu Mifugo, Prof. Elisante Ole Gabriel. Picha na Mpiga Picha
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare Agenda ya Kitaifa za Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 baada kuizindua katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Mjini Morogoro. Wengine ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu SUA, Profesa Raphael Chibunda. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na Wafugaji na Wadau wa Ufugaji wa Samaki kwenye Mabwawa kutoka Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu huku wakionesha kitabu cha Agenda ya Kitaifa za Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 baada kuzinduliwa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Mjini Morogoro

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua Agenda ya Kitaifa ya Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 na kutangaza kuzifumua na kuziibua tafiti zote  zilizofanywa na wasomi na kutelekezwa kwenye makabati miaka ya nyuma na kuziingiza kwenye mfumo rasmi wa matumizi ili kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na maendeleo.

Pia agenda hizo zitaleta msisimko mpya wa kufanya utafiti nchini na kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na maendeleo tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo tafiti nyingi zilifanywa na kutelekezwa kwenye makabati na watafiti mbalimbali wakiwemo Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili (Masters Degree)  na Shahada ya Uzamivu (PHD) katika vyuo vikuu mbalimbali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa agenda hizo kitaifa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),  Kampasi ya Mazimbu mjini Morogoro, Waziri Mpina aliziagiza Taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TALIRI) na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi(TAFIRI) kubadilika ili kufanya tafiti kwa vigezo vilivyowekwa na kuleta mabadiliko chanya katika sekta za mifugo na uvuvi nchini.

Waziri Mpina alisema chimbuko la kuandaliwa kwa ajenda hizo za utafiti ni baada ya kubaini kuwa ajenda zilizokuwepo awali za Mifugo na Uvuvi zilishindwa kuibua na kuzitumia tafiti zilizofanywa kuchochea mabadiliko kwenye sekta hiyo muhimu ya uzalishaji.

Pia ajenda za utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi hazikuwa na utaratibu wa kuzitambua, kuziorodhesha na kuzitumia tafiti zinazofanywa na Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili (Masters Degree) na Uzamivu (PHD) lakini sasa ajenda za utafiti zilizozinduliwa zimeweka utaratibu wa namna ya kuzitambua, kuziorodhesha na kuzitumia tafiti za wasomi hao.

“Haiwezekani tafiti za wasomi wa kiwango cha juu kiasi hicho wanazozifanya wakati wa kukamilisha masomo yao ziishie kupata alama za ufaulu na kutupwa kwenye makabati, Leo kila mhitimu atalazimika kuandaa policy brief ambayo itawezesha watumiaji na Serikali kurekebisha au kuandaa Sera na Sheria” alisema Waziri Mpina.

Aliongeza kuwa Ajenda za Utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi hazikuwa na utaratibu wa kuweka Kanuni ambazo zitahakikisha kuwa utekelezaji  wa ajenda za utafiti unafanyika, lakini ajenda za utafiti iliyotangazwa inaweka Kanuni zitakazotoa mwongozo na usimamizi wa utekelezaji na wajibu wa kila mhusika.

Aidha Waziri Mpina alibainisha kuwa ajenda za utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi hazikuwa na utaratibu wa kuwaunganisha Watafiti wa Mifugo na Uvuvi nchini, na hivyo kupelekea kila mmoja kufanya utafiti kivyake hali iliyosababisha jambo moja kufanyiwa utafiti na mtafiti zaidi ya mmoja na kukosa jukwaa la kuratibu na kuchambua tafiti zinazofanywa nchini.

“Agenda ninayoizindua leo inakwenda kujumuisha watafiti na wataalam mbalimbali waliobobea katika fani za mifugo, uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji ili kuyapitia matokeo ya utafiti, teknolojia zilizoibuliwa na utafiti na kuzisambaza kwa watumiaji kwa manufaa ya Taifa” alisema Waziri Mpina

Pia Waziri Mpina alibainisha mapungufu mengine yaliyomo kwenye ajenda za utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi ni pamoja na kutoweka msingi mzuri wa kusimamia Watafiti na kufanya tafiti kulingana na mahitaji ya soko badala yake  Taasisi za Utafiti na Watafiti kufanya tafiti nyingi za nje na mambo muhimu ya wananchi yanayohitaji kufanyiwa utafiti kutelekezwa.

“Leo hii agenda ninazozizindua zimeweka utaratibu wa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa, kupanua mtandao wa utafiti  na kufanya tafiti zote kulingana na mahitaji ya wananchi.  Mfano katika maeneo ya nyama, maziwa, samaki, ngozi, chakula cha samaki na mifugo, magonjwa, malisho na migogoro” alisema Mpina.

Aidha dosari nyingine zilizokuwepo kwenye ajenda za utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi ni kutojumuisha katika vipaumbele masuala mengi muhimu yenye changamoto nyingi ikiwemo  Mitaala na hali ya ajira.

Mpina alisema mitaala inapoanzishwa haifanyiwi utafiti wa mara kwa mara matokeo yake mafunzo yanayotolewa sio yale yanayohitajika katika soko la ajira huku Wanafunzi wanaohitimu mafunzo hawajulikani wanakwenda wapi baada ya kuhitimu na hakuna mfumo wowote wa uratibu.

“Ukienda kwa wafugaji wanaofuga na kuchunga sio hao waliosomea mifugo, ukienda kwa Wavuvi na Ukuzaji viumbe maji wanaovua na kufuga si hao waliosomea taaluma hizo, ukienda viwandani vilevile”alisema Mpina.

Pia Masoko na Biashara, Uongezaji wa mnyororo wa thamani wa mazao ya mifugo na uvuvi (Livestock & Fisheries value chain & value addition), agenda iliyopita ilizingatia uzalishaji pekee bila kuangalia upande wa soko wakati vitu hivi vinakwenda kwa pamoja kwani hakuna uzalishaji bila soko.

Waziri Mpina pia alisema licha ya kushamiri kwa migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi na eneo hilo kugubikwa na changamoto nyingi  ikiwemo  mifugo kutaifishwa, kupigwa risasi, kufilisiwa, kuuwawa kwa watu na mifugo  na kupigwa faini kubwa kiasi cha kutishia uendelevu wa sekta lakini eneo hili halikujumuishwa katika Agenda ya utafiti iliyopita.

Pia masuala mtambuka, afya ya wanyama na magonjwa ya afya ya jamii (Zoonotic Diseases) ambapo hivi sasa asilimia 60 ya magonjwa yasiyoambukiza yanatokana na mazao ya mifugo, malisho, nyanda za malisho na vyakula vya mifugo na samaki, uvuvi endelevu katika maji ya asili (Uvuvi Haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi)  ambayo nayo hayakuzingatiwa katika agenda za utafiti zilizopita .

Hivyo Waziri Mpina aliwahakikishia watanzania kuwa Wizara yake itaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha kuwa matokeo ya tafiti zinazofanywa zinawafikia walengwa kwa wakati ili tafiti hizo ziongeze tija na kipato kwa watuamiaji na Taifa kwa ujumla. 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Profesa Raphael Chibunda alimhakikishia Waziri Mpina kuwa kwa niaba ya watafiti wa Chuo kikuu hicho watatakwenda kuwa sehemu ya utekelezaji wa agenda hizo.

Tigo yazindua duka jipya Kigoma mjini

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Tigo ‘Tigo Shop’ mkoani Kigoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati. 
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akihakiki utendaji kazi wa mfumo wa kusajili namba za simu kwa alama za vidole katika duka jipya la Tigo lililopo eneo la Lubengela Mkoani Kigoma jana mara baada ya kuzindua duka hilo.Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati. 
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga wakati wa uzinduzi wa Duka la Tigo ‘Tigo Shop’ mkoani Kigoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akizungumza na wakazi wa Kigoma pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo wakati wa uzinduzi wa duka la Tigo Mkoani Kigoma, Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati. 



Wateja wa Tigo Mkoani Kigoma wataweza kupata huduma zilizoboreshwa zaidi katika duka jipya ‘Tigo Shop’ lililozinduliwa leo mkoani humo.

Duka hilo jipya litakuwa sehemu maalumu kwaajili ya wateja kujionea na kufanya majaribio ya bidhaa na huduma mbalimbali mpya na za kidigitali kama Tigo Pesa zitolewazo na kampuni hiyo.

Wateja pia wataweza kupata huduma ya kusajili upya namba za simu kwa mfumo wa alama za vidole.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati alisema “Ufunguzi wa duka hili ni utekelezaji wa mkakati wa Tigo wa kufikisha huduma karibu na wateja na tunaamini kuwa duka hili litatoa fursa za biashara kwa wateja na kuchochea ukuaji wa uchumi mkoani hapa,” alisema Karembo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga aliipongeza Tigo kwa Kwa jitihada zake za kuhakikisha wateja wanapata huduma zenye viwango vya kimataifa maeneo yote ya nchi.

“Duka hili jipya litakuwa chachu katika uboreshaji wa huduma za mawasiliano hapa mkoani Kigoma.Mkoa huu una wakazi wachapa kazi na wafanyabiashara ambao wanatamani kujikwamua kiuchumi hivyo hii ni fursa muhimu kwao,” alisema.

Aliongeza “Hii ni faraja kuona kwamba sasa huduma za Tigo zitapatikana kwa urahisi zaidi na hii itasaidia kufungua fursa nyingi za kiuchumi.”
Duka hilo linalopatikana katika mtaa wa Lubengela Kigoma Mjini, ni la kwanza mkoani humo na litakuwa likitoa huduma sambamba na dawati la wateja lililopo Wilayani Kasulu.

“Duka hili limewekwa katika eneo hili kimkakati ili kufikika kwa urahisi kwa wakazi wa Kigoma na maeneo jirani na mipakani,” alisema Madati.
Duka hilo linaifanya Tigo kuongeza kasi ya usambazaji wa huduma zake maeneo mbalimbali ya nchi ili kufikia wateja wake zaidi ya 11.6 milioni jambo linalofungua milango kwa wateja kufurahia huduma za kidigitali zinazotolewa na kampuni hiyo.

BITEKO ANG’AKA KUHUSU MISHAHARA YA WATANZANIA MIGODINI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa GGM Richard Jordonson wa tatu kulia
akimuonyesha kitu Waziri wa Madini Doto Biteko wa pili kushoto.
Kulia ni Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel na kushoto Makamu
Mkurugenzi Mtendaji wa GGM Simon Shayo wakati wa ziara ya
Waziri wa Madini mgodini hapo.

Waziri wa Madini Doto Biteko katikati akiwa kwenye kikao na uongozi
wa mgodi wa dhahabu wa Geita “GGM” wakati wa ziara yake mgodini
hapo. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu
wa Wilaya Joseph Maganga na kushoto kwa waziri ni Mkurugenzi
Mtendaji wa GGM Richard Jordonson.

**************************************

Na Issa Mtuwa – Geita

Waziri wa Madini Doto Biteko pamoja na kuupongeza uongozi wa mgodi
wa dhahabu wa Geita “GGM” katika mambo mengi leo tarehe 16/11/2019
alikuwa “mbogo” kwa uongozi huo kuhusu suala la mishahara wanayolipwa
Watanzania ambapo amebaini kutokuwepo kwa usawa.

Biteko amesema anaumizwa sana na jambo la malipo ya mishahara kati ya
Watanzania na wageni licha ya kulingana kwa sifa, ujuzi na elimu na wakati
mwingine mtazania anasifa zaidi kuliko mgeni lakini bado mtanzania
analipwa chini kuliko yule mgeni.

Kutokana na hali hiyo, Biteko ameuagiza uongozi wa GGM kuwasilisha
orodha ya malipo ya mishahara ya wafanyakazi wote (Payroll) kwa
Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa wiki ijayo. Biteko alianza
kuhoji idadi ya idara zilizopo na zinaongozwa na akina nani huku akiuliza
kuna watu wangapi wa kigeni katika idara hizo na majukumu yako.

“Sheria ya madini hasa sheria ya Local content inatoa muongozo ni namna
gani na wakati gani mgodi unaweza kumuajiri mtaalamu wa fani fulani
kutoka nje endapo hakuna mtanzania wa kuweza kushika wadhifa huo”
amesema Biteko.

Ameongea hayo wakati akiongea na uongozi wa mgodi wa GGM mkoani
geita alipotembelea mgodini hapo kwa ziara maalum ya kikazi kwa lengo la
kufuatilia na kukagua uendeshaji wa shughuli za mgodi huo, ufuatilia na
kuangalia utekelezaji wa malalamiko ya wananchi na malipo ya ushuru wa
Halmashauri (Service Levy) ambapo mgodi huo unawajibika katika malipo
hayo.

Aidha, Biteko amekwenda kujiridhishi katika masuala mbalimbali ambayo
kamati maalumu aliyoiunda kwenda mgodini hapo kwa ajili ya kuangalia na
kukagua ili ajiridhishe kabla ya kutoa idhini ya kuruhusu mgodi huo kuanza
uchimbaji wa chini kwa chini (Underground) kufuatia maombi ya mgodi huo
kwa waziri.

Kwa mujibu wa kifungu cha 40 cha marekebisho ya sheria ya madini ya
mwaka 2017 hairuhusu uchimbaji wa chini kwa chini kwa mwekezaji au
mgodi mpaka apate idhini (Kibali) ya waziri mwenye dhamana ya Madini
ambapo Waziri alianisha mambo mengi ya kuzingatiwa na mgodi kabla
hawajaruhusiwa.

Biteko ameendelea kusisitiza kauli yake ya mara kwa mara kuwa raslimali
hizi ziwe neema kwa wananchi na sio mateso. Kauli hiyo ameitoa kufuatia
malalamiko ya wananchi wapatao 350 ambao makazi yao yalipitiwa na
tetemeko wakati wa milipuko mbalimbali mgodini hapo wakati wa ulipuaji
wa miamba.

Ameongeza kuwa hadi kufikia mwisho mwaka huu ukurasa wa suala la
malipo ya fidia ya suala hili liwe limefungwa na kwamba wenye malalamiko
wote wapeleke kwa Mkuu wa Wilaya Geita kuanzia tarehe 18-23/11/2019.

Kwa upande wa uongozi wa mgodi ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji
wa Mgodi Richard Jordanson na Makamu Mkurugenzi Mtendaji Simon
Shayo kwa nyakati tofauti wametoa shukrani kwa ujio wa Waziri kwenye
mgodi wao ikiwa ni mara yake ya kwanza kutembelea tangu alipoteuliwa
kuwa Waziri wa Madini.

Wameongeza kuwa mgodi wao upo mstari wa mbele kutekeleza maagizo
ya serikali na kwamba wanapenda kuwa msistari mbele na wawe wa
kwanza katika kuchangia sehemu kubwa itakayo changia pato (GDP) la
taifa kwa upande wa madini.

Shayo amemwambia waziri kuwa mambo mengi aliyoyasema Waziri kama
vile; mpango wa ufukiaji mashimo baada ya mgodi kufungwa, ulipaji wa
ushuru wa Halmashauri za wilaya (Service levy), mchakato wa ulipaji wa
fidia ya wananchi na utekelezaji wa sheria ya local content vinatekelezwa
baadhi vimeshakamilishwa na baadhi vipo kwenye taratibu za kukamishwa.

Akiwa kwenye mgodi wa RZ unaomilikiwa na mwekezaji kutoka china anae
fahamika kwa jina la “Lyuu” amemtaka mwekezaji huyo kwa kufanya kazi
zake kwa kuzingatia sheria zote zikiwemo za madini, kazi na utoaji wa
mikataba ya ajira na makato ya NSSF kwa wafanyakazi wake na
kuiwasilisha kwa mamlaka husika.

“Lyuu” amesema ameshukuru waziri kutembelea mgodi kwake na
amepokea maelekezo ambayo ameyakubali na kuahidi kuyatekeleza.
Wakati wakati huo huo wafanayakazi walipo mgodini hapo amewataka
kuwa waaminifu na kuepuka vitendo vihovu kwa mwekezaji.

WALIOPANGA KULETA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI WASHUGHULIKIWE BILA HURUMA-WAZIRI WA MAMBO YA NDANI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto) na ndugu zake wakati wa maadhimisha miaka 15 ya Kumbukizi ya kifo cha Baba yake mzazi, Waziri huyo, tukio lililofanyika Kijiji cha Nyamitwebili, Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Lugola amewataka makamanda wa polisi nchini kulinda amani na kuwashughulikia watu waliopanga kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe, alipokua anazungumza katika maadhimisho miaka 15 ya Kumbukizi ya kifo cha Baba yake mzazi, Waziri huyo, tukio lililofanyika Kijiji cha Nyamitwebili, Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Kamanda huyo alimpongeza Waziri huyo kwa kuwa na ushirikiano mzuri wa utendaji kazi ndani ya mkoa huo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza katika maadhimisha miaka 15 ya Kumbukizi ya kifo cha Baba yake mzazi, Waziri huyo, tukio lililofanyika Kijiji cha Nyamitwebili, Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Lugola amewataka makamanda wa polisi nchini kulinda amani na kuwashughulikia watu waliopanga kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Daniel Sillah, alipokua anazungumza katika maadhimisho miaka 15 ya Kumbukizi ya kifo cha Baba yake mzazi, Waziri huyo, tukio lililofanyika Kijiji cha Nyamitwebili, Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Kamanda huyo alimuahidi Waziri huyo linda amani kipindi hiki cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

**********************************************************

Na Mwandishi Wetu, Bunda.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka makamanda wa polisi nchini kusimamia kampeni zilizoanza za uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwalinda wagombea wa vyama vya siasa ambavyo vilitangaza kujitoa, pamoja na kuwashughulikiwa bila huruma watu waliopanga kufanya vurugu.

Waziri Lugola amesema ana taarifa za kutosha kuhusu baadhi ya watu waliopanga kufanya vurugu wakati wa kampeni kwa lengo la kuvuruga uchaguzi huo, aliwataka makamanda hao kuwasaka kila kona, kuwakamata watu hao ambao wana nia mbaya ya kuvuruga uchaguzi huo.

Lugola ameyazungumza hayo wakati wa maadhimisha miaka 15 ya Kumbukizi ya kifo cha Baba yake mzazi, James Ndege Lugola, tukio lililofanyika Kijijini kwa Waziri huyo, Nyamitwebili, Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo, na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi wakiwemo viongozi wa Serikali, vyama vya siasa kutoka Mkoani humo na nje ya Mkoa.

“Nawataka mtende haki katika usimamizi wa uchaguzi huu, lakini wapo baadhi ya watu ambao wamepanga kufanya vurugu, watu hao msicheke nao, watu hao washughulikieni bila huruma, na badala ya kuwamwagia maji ya kuwasha, sasa watumbukizeni ndani ya tenki la maji hayo ili waweze kuwashwa zaidi, hatutaki vurugu, tunataka amani na utulivu ndani ya nchi yetu,” alisema Lugola.

Kwa upande wa vyama vya siasa vilivyojitoa kushiriki uchaguzi huo, Lugola alisema wagombea wapo ambao wamekataa agizo hilo la vyama vyao, hivyo wameamua kushiriki uchaguzi huo wakigombea nafasi walizoziomba, hivyo wanapaswa kulindwa kwa nguvu zote kwani ni haki yao kugombea.

“Wameweka mpira kwapuni, lakini wachezaji wapo uwanjani bado wanataka kucheza,bado wanaenda uwanjani kuwapiga wachezaji hao wasiweze kucheze, bado wanataka kuwapiga waamuzi wasiweze kutoa pointi tatu muhimu kwa timu ambayo imeendelea kucheza, hao muwashughulikie kiisawasawa,” alisema Lugola.

Aliongeza kuwa, agizo alilolitoa Waziri Mkuu la kuwataka Watanzania kushirikia uchaguzi huo kwa amani wakati alitoa hotuba yake Bungeni, hivyo Wizara yake inamhakikishia italinda amani hiyo katika kila mikutano ya hadhara, pamoja na kuwathibiti watakaofanya vurugu.

Hivyo, Waziri Lugola aliwataka wananchi kwenda kusikiliza sera za wagombea wao kuanzia mwanzo wa kampeni mpaka utakapokamilika, na pia wapige kura kwa amani bila ya kuwa na wasiwasi wowote, kwasababu Jeshi la Polisi limeapa kuwanga kuwalinda wananchi hao pamoja na mali zao.

Maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa na Makamanda wa Polisi Mikoa ya Mara na Kanda Maalum Tarime/Rorya ambapo waliahidi kuyafanyia kazi maagizo ya Waziri Lugola kwa kuimarisha amani katika Mikoa yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Daniel Sillah, alisema ameyapokea maelezo ya Waziri huyo, na askari wake wamejpanga vizuri kulinda amani mkoani humo, na aliwataka wananchi kuacha kuvuruga aamani.

“Tumepokea maelekezo na tutayafanyia kazi, sisi Jeshi la Polisi tumejipanga vizuri kulinda amani katika kampeni zitakazoanza kesho, wakati wa kupiga kura na kipindi cha kuhesabu kura, tunawataka wananchi kutokuvuruga amani, na watakaofanya vurugu tutawashughulikia,” alisema Sillah.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe alimshukuru Waziri huyo kwa ushirikiano wake wa kumpigia sim umara kwa mara akitaka kujua hali ya amani ndani ya kanda hiyo, ushirikiano huo umemsaidia kufanya kazi kwa kasi zaidi.

“Waziri Lugola wewe ni mtendaji Mkuu wa Wizara yetu, lakini umetutumia kadi ya mwaliko mpaka tumefika hapa, ulikua na haki ya kutuambia waambie hao waje, umetupa heshima kubwa sana, mheshimiwa waziri mara nyingi sana umenipigia simu kunionya na kunielekeza, mara nyingi unaponipa kazi nikikuambia unaniamini, haiwezekani mkoa wa mara ambao wewe ni mzaliwa wa mkoa huu ni mlezi kiusalama, itakua aibu sana kutokee uhalifu mkubwa katika mkoa unaotoka wewe, ni aibu sana,” alisema Mwaibambe.

Kwa upande wake, Mkazi wa Kijiji hicho, Lucas Magesa Masinde, akimshukuru Waziri Lugola kwa kuwaalika wananchi hao, na pia kuwahakikishia usalama kipindi hiki cha uchaguzi, hivyo ameahidi kujitokeza bila woga kusikiliza kampeni za wagombea, kupiga kura na atakapotangazwa mshindi.

Ohoooo.....pasi ya mkaa!

JAJI MKUU – TANGAZENI MABORESHO YA MAHAKAMA

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikao cha wamiliki wa maeneo ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania,akizungumza jambo wakati wa kikao hicho kilichofanyika Novemba 16, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), uliopo jijini Dar es Salaam.
Balozi Mteule, ambaye alikuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akitoa mada ya makabidhiano ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania.
Picha ya pamoja kati ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na viongozi wakuu wa Mahakama ya Tanzania wa sasa na waliopita, wakiwemo wamiliki wa maeneo ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania.

Wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia makabidhiano hayo. 
Balozi Mteule, ambaye alikuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (kulia) akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru(kushoto) nyaraka muhimu za Mahakama ya Tanzania.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabundunguru akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.
(Picha na Mary Gwera-Mahakama)



Na Magreth Kinabo-Mahakama

17.11.2019

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof.Ibrahim Hamis Juma amewataka watumishi na viongozi wa Mahakama ya Tanzania kutangaza maboresho na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mahakama hiyo ili ziweze kufahamika kwa jamii.

Akizungumza wakati wa uahirishaji kikao cha wamiliki wa maeneo ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania wa Miaka Mitano kuanzia 2015/16 hadi 2019/20 , kilichofanyika Novemba 16, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), uliopo jijini Dar es Salaam.

Jaji Mkuu alisema kuna haja ya kutafuta namna ya kujitangaza katika maboresho yanayofanyika, ikiwemo shughuli mbalimbali ili ziweze kufahamika kwa umma.

‘ Tuna tatizo la kujitangaza kuwa tunafanya nini, tutafuta namna ya kujitangaza, kama inavyofanya Serikali Kuu, mfano yapo mambo mazuri yamefanyika Kigoma na Sumbawanga , Mahakama ziko vizuri. Tunaona Serikali Kuu inavyojitangaza, hivyo kuna umuhimu wa kufanya jambo hili,’ alisema Jaji Mkuu.

Aliongeza kwamba katika kuboresha taasisi hiyo, mambo ya urasimu yanatakiwa kuvunjwa na kuweka pembeni tofauti ya vyeo au hadhi, kwani jambo linalopaswa kuzingatiwa ni utaalamu wa mtu.

Huku akisisitiza kwamba mkubwa akikosea kuna namna ya kumsaidia , hivyo watumishi wanapaswa kutoa hoja na michango yao ili kuweza kuendeleza maboresho yanayofanyika.

‘Naona mambo mengi yanayofanyika yanatokana na hoja zenu, kazi zetu sisi ni kukubali na kupendekeza mabadiliko, nguvu ya taasisi iko kwa watumishi,’ alisema.

Aidha Jaji Mkuu aliwataka watumishi hao, kuwa huru kuzungumza wakiwa kwenye mikutano ili changamoto mbalimbali ziweze kufahamika na kutatuliwa, hivyo kama kuna hoja zipitishwe kwenye ngazi zinazohusika. 

Alifafanua kuwa lazima watumishi hao wawe na matamanio ya hali ya juu ya kuweza kukabiliana na changamoto zinazoikabili Mhimili huo.

Akizungumzia kuhusu ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2020 (Uwezeshaji na Ukuzaji wa Biashara), alisema imeeleza namna ya kupunguza muda na gharama za kutatua migogoro ya biashara. Ripoti hiyo imeeleza urahisi wa kufanya biashara, hivyo Mhimili huo iitumie kwa sababu imeeleza vigezo vya mwaka 2020 ili kutayarisha ya kwake.

‘Sisi tutayarishe ya kwetu tuoneshe namna tumeweza kusaidia kurahisisha uwekezaji na namna ya kufanya biashara na kujitangaza kuwa tumeweza zaidi ya vigezo vya Benki ya Dunia,’ alisisitiza.

Kwa mujibu wa Mjumbe wa kikao hicho, Bw. William Machumu, ambaye ni Mtendaji wa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, alisema katika ripoti hiyo,Tanzania imekuwa ni nchi ya 71 duniani kati ya nchi 190 zinazopimwa kwa kutumia kigezo cha uvutiaji wa biashara, ambapo Mahakama inapimwa kwa kufanyiwa tathimini hiyo.

Machumu alisema katika ripoti ya mwaka 2019 ya benki hiyo, Tanzania ilikuwa ya 64. Hivyo eneo hilo ninatakiwa lipewe kipaumbele.

Kwa upande wake Balozi Mteule, Mhe. Hussein Kattanga, akizungumzia mpango huo alizungumzia kuhusu maeneo ambayo yamefanyiwa kazi na mengine yanayohitaji mkazo wa kufanyiwa kazi.

Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru aliwataka watumishi hao, kuendeleza tabia ya kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kuwa wannapofanya kazi vizuri Mahakama ndipo inaposifiwa.

KAMPENI YA ELIMU KWA MLIPAKODI YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA ZAIDI YA 700 MOROGORO

$
0
0
Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Chama Siriwa (kulia) akimuelimisha mfanyabiashara wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro kuhusu umuhimu wa kutunza kumbukumbu za mauzo wakati wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Wilayani hapo.
Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Morgan Njama (kulia) akiwaelimisha Wafanyabiashara wa Wilaya ya Kilosa katika Mji wa Mikumi mkoani Morogoro wakati wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Wilayani hapo.

Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Dinah Lwaga (kulia) akichukua maoni ya Mfanyabiashara wa Wilaya ya Kilosa katika Mji wa Mikumi mkoani Morogoro wakati wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Wilayani hapo.


********************************************


Na Veronica Kazimoto

Morogoro

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewafikia na kuwaelimisha wafanyabiashara zaidi ya 700 kupitia kampeni ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi iliyofanyika mkoani Morogoro.

Lengo la kampeni hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki, Afisa Msimamizi wa Kodi Mkuu wa TRA, Julius Mjenga amesema kuwa, mamlaka hiyo ililenga kuwafikia wafanyabiasha 500 lakini kutokana na mwitikio mkubwa, TRA imefanikiwa kuvuka lengo hilo na kuwafikia zaidi ya 700.

“Wiki hii moja ya elimu kwa mlipakodi, tuliwalenga wafanyabiashara wa wilayani ambapo kumekuwa na changamoto ya kutokupata elimu ya kodi kwa wakati. Nashukuru tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu tumeweza kuwaelimisha wafanyabiashara 774 katika kampeni hii”, alisema Mjenga.

Mjenga ameongeza kuwa “Tumefika karibu wilaya zote za mkoa huu wa Morogoro ambazo ni Malinyi, Ulanga, Kilosa, Mvomero, Kilombero na Gairo na kila mahali tulipopita tumepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wafanyabiashara na wananchi mbalimbali.”

Kwa upande wa wafanyabiashara waliotembelewa na TRA, wameishukuru mamlaka hiyo kwa kuwaelimisha masuala mbalimbali yanayohusu kodi na kuomba elimu hiyo iwe endelevu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema kuwa, TRA ya sasa sio ile ya zamani kwa sababu sasa hivi maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wamekuwa karibu na walipakodi na siku hizi hawana tabia ya kufunga biashara zao.

“Zamani mtu alikuwa akisikia watu wa TRA wanakuja, anafunga duka anaondoka lakini siku hizi, TRA wamekuwa marafiki, wanatuelimisha na wala hawafungi biashara zetu, kwakweli tunashukuru sana,” alisema Eleonora Kisimba, mfanyabiashara wa duka la nguo wa wilayani Mvomero.

Naye Stanphord Mjumbe ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi wilayani Gairo mkoani hapa alisema kuwa, kampeni ya elimu kwa mlipakodi ifanyike mara kwa mara kwa sababu wafanyabiashara walio wengi hususani wadogo hawajasoma hivyo wanahitaji kuelimishwa zaidi juu ya haki na wajibu wao katika ulipaji kodi.

“Sisi wafanyabiashara wadogo, tulio wengi hatujasoma hivyo tunahitaji elimu hii angalau kwa mwaka mara tatu ili tuweze kuelewa kwa kina haya mambo ya ulipaji kodi maana wakati mwingine tunakuwa hatujui haki zetu,” alisisitiza Mjumbe.

Aidha, wafanyabiashara hao wameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania kurejesha Kodi ya Zuio kwa wamiliki wa majengo kwa kuwa baadhi yao hawataki wapangaji kuzuia asimilia kumi na kuiwasilisha TRA.

Vilevile, wameomba kuelimishwa jinsi ya kulipa kodi ya mapato kwa awamu mara tu wanapokadiriwa kodi hususani kwa wafanyabiashara wapya kwani wengi wao wanapitiliza tarehe za kulipa kodi hiyo kwa kukosa uelewa. 

Kampeni ya huduma na elimu kwa mlipakodi imemalizika tarehe 17 Novemba, 2019 na ilifanyika katika Mikoa ya Morogoro na Pwani ambapo wafanyabiashara wamepata fursa ya kutembelewa katika maduka yao na wengine walihudhuria semina kwa ajili ya kuelimishwa masuala mbalimbali yanayohusu kodi.

RC SINGIDA AONGOZA KUFUNGA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA KWA KUFANYA MAZOEZI

$
0
0
Mkufunzi Mkuu wa Karate Mkoa wa Singida, Salum Musa (kushoto), akifanya mazoezi na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa kilele cha kufunga wiki ya Maadhimisho ya Magonjwa Yasio ya Kuambukiza yaliyofanyika viwanja vya Bombadia mjini hapa jana. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi (katikati) akifanya mazoezi.
Wanafunzi wakifanya mazoezi.
Mwalimu Juma Mataka kutoka Manispaa ya Singida, akiongoza mazoezi hayo.
Afisa Utamaduni Mkoa wa Singida, Henry Kapella, akiongoza kufanya mazoezi.
Mazoezi yakiendelea.
Mazoezi yakiendelea.
Mazoezi yakiendelea. Kulia ni msaidizi wa mkuu wa mkoa wa Singida, Mbwana Mkingule.
Mazoezi yakiendelea.
Sister Maria Corola kutoka Mtiko, akipima uzito na urefu katika maadhimisho hayo. Katika maadhimisho hayo kulikuwepo na huduma za upimaji wa afya kama, macho, kisukari, shinikizo la damu, urefu, na Ukimwi kwa usimamizi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Sightsaver.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi (kushoto) akifanya mazoezi na Afisa wa Uhamiaji Mkuu wa Mkoa wa Singida, Safina Muhindi.
Mazoezi yakiendelea.
Wauguzi kutoka Kituo cha Afya cha Sokoine wakiwajibika kwa kupima afya za wananchi katika maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Consitancia Muua, Innocencia Paul na Lenicu Kilasi.
Vijana wa Skati wakionesha ukakamavu.
Muuguzi Catherine Msukuma kutoka Kituo cha Afya cha Sokoine, akimpima urefu Mwanafunzi Buruani Bashiri wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi, Al-Furuquni.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida,Victolina Ludovick akisoma hutuba katika maadhimisho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akihutubia. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Singida, Anwar Mlulu. 
Wanafunzi wakipima urefu na uzito.

Mtaalamu wa macho kutoka Kituo cha Afya cha Sokoine, Onesmo Magile, akimpima macho mtoto Spriani Issaya. Kushoto ni mama wa mtoto huyo, Elinaja Lissu.
Mtaalamu wa macho kutoka Kituo cha Afya cha Sokoine, Julieth Tesha, akimuongoza kusoma herufi mgonjwa wa macho (hayupo pichani)
Viongozi wa mkoa huo wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akimkabidhi cheti Dkt. George Mwakahesya cha kushiriki mafunzo ya upimaji wa viashiria vya awali vya saratani ya kizazi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akifurahi na wanafunzi walokuwa wakimpongeza kwa siku yake ya kuzaliwa.

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR NA RAIS WA ZANZIBAR.DK.SHEIN AZUNGUMZA NA WAZEE WA WILAYA YA DIMANI KICHAMA LEO

$
0
0

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wazee wa CCM wa Wilaya ya Dimani Kichama katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar,(kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dimani Kichama Ndg.Hussein Ali Mgema.(Picha na Ikulu)
KATIBU wa CCM Wilaya ya Dimani Ndg.Yussuf Ramadhani Abdalla akiwasilisha Taarifa fupi ya Wazee wa CCM, wakati wa mkutano wao na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjiniu Amani, leo 17-11-2019
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa Taarifa ya Wazee wa Wilaya ya Dimani Kichana na Katibu wa CCM Wilaya ya Dimani Ndg. Yussuf Ramadhani Abdalla na (kushoto kwa Rais) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.Dr, Abdalla Juma Sadala Mabodi wakati wa hafla ya mkutano wake na Wazee uliofanyika leo 17-11-2019 katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr, Abdalla Juma Sadala Mabodi akizungumza wakati wa hafla ya mkutano na Wazee wa CCM Wilaya ya Dimani Kichama uliofanyika katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar.(Picha na Ikulu).
BAADHI ya Washauri wa Rais wa Zanzibar na Viongozi wa CCM na Wazee wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani ).
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dimani Kichama Ndg.Hussein Ali Mgema (Kimti) kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar. Dr, Abdalla Juma Sadala, wakati akiwasili katika viwanja vya Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani kwa ajili ya mkutano wake na Wazee wa CCM wa Wilaya ya Dimani leo 17-11-2019.(Picha na Ikulu)

CCM KIMEJIPANGA UCHAGUZI SERIAKLI ZA MITAA-POLE POLE

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud,Arusha

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM),kimesema kuwa kimejipanga kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika novemba 24 mwaka huu na kimewaonya wale wote ambao wamepanga kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kuacha mara moja kuchochea wananchi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa,Humphrey Polepole alitoa kauli hiyo Novemba 17 jijini Arusha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha na kueleza kuwa ushindi wa kishindo wanaotarajia kuupata ni kutokana na wananchi kuridhishwa na utendaji wa serikali ya awamu ya tano.

Amevitaka vyama vyama vya upinzani kuheshimu kanuni,sheria na taratibu za uchaguzi na kwamba wasipange au wasiwashawishi wafuasi wao kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani wakati wote kuanzia kipindi cha kampeni,upigaji kura,kuhesabu matokeo pamoja na kutangazwa kwa mshindi kwa kuwa chama hicho kimejipanga kikamilifu.

“Wananchi wameridhishwa na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwani katika kipindi cha miaka mine ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano miradi mingi ya maendeleo inayogusa moja kwa moja maisha ya mwananchi wa kawaida imetekelezwa kwa kiwango kikubwa sana”alisema.

Polepole aliitaja baadhi ya miradi ambayo imetekelezwa kwa kiwango kikubwa katika kipindi kifupi cha miaka mine kuwa ni ujenzi wa vituo vya afya na hosipitali za Wilaya,upatikanaji wa maji safi na salama,ujenzi wa barabara na madaraja,usambazaji wa umeme katika maeneo mengi ya mijini na vijijini,ujenzi wa vyumba wa madarasa,nyumba za walimu pamoja na maabara.

Alisema kuwa mkutano huo na wanahabari ni matokeo ya kikao kazi cha kufanya tathmini ya kimaendeleo ya miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli na kueleza kuwa Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa hapa nchini ambayo miradi mingi ya kimaendeleo imetekelezwa.

Alisema kuwa wimbi la wananchama waliotoka kwenda vyama vya upinzani mara baada ya mzee na Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kuhamia huko ndio lililopelekea chama hicho kuanza kujitathmini na kuandaa mikakati ya ushindi ikiwemo kurudi nyumbani kwa kiongozi huyo kumekisaidia chama hicho kuvuna wanachama wengi zaidi kwa kipindi kifupi.

Alisema kuwa mkutano huo na wanahabari ni matokeo ya kikao kazi cha kufanya tathmini ya kimaendeleo ya miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli na kueleza kuwa Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa hapa nchini ambayo miradi mingi ya kimaendeleo imetekelezwa.

Kadhalika katibu huyo wa Itikadi na uenezi alieleza kushangazwa kwake na baadhi ya vyama vya upinzani ambavyo vimetangaza kujitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kueleza kuwa baadhi ya vyama vilivyotangaza kujitoa havikuwahi kusimamisha mgombea hata mmoja na kuhoji wanajitoa wapi.

Awali akimkaribisha Katibu huyo wa Itikadi na uenezi Taifa,Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha,Mussa Matoroka alisema kuwa kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa CCM Mkoa wa Arusha imejipanga kikamilifu, kimkakati na kisayansi kwa kuhakikisha kuwa wanashinda kwa kishido katika uchaguzi huo.

Aliwataka wananchi wa mkoani hapa kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kutimiza haki yao ya msingi kikatiba ya kuchagua katika maeneo mbalimbali yaliyotengwa kwa ajili ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambapo pia amewasishi kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani kabla na baada ya uchaguzi.

Katika mkutano huo katibu huo wa Itikadi na uenezi taifa aliambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya Mkoa na Wilaya ambapo kila mmoja alipata fursa ya kuzunguza juu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika eneo lake.

WANAFUNZI 62 WA MASOMO YA SAYANSI WAHITIMU KIDATO CHA NNE FEO SEKONDARI

$
0
0
Na Muhidin Amri,Songea

JUMLA ya wanafunzi 62 wamehitimu masomo ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Wasichana FEO iliyopo Halmashauri ya Madaba wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Hii ni mara ya kwanza kwa shule hiyo kutoa wanafunzi wa kidato cha nne tangu ilipoanzishwa mwaka 2016 shule inayotajwa kuwa na mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia kuliko shule zote katika mkoa wa Ruvuma.

Wanafunzi wa shule hiyo katika risala yao iliyosomwa na Jackline Mgina walisema, walianza safari ya masomo ya sekondari mwaka 2016 wakiwa 78, hata hivyo wanafunzi wengine walishindwa kuendelea kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa na wengine kuhama shule.

Aidha walisema, wahitimu wote 62 wamechukua mchepuo wa sayansi kwa kuzingatia sera ya nchi ya viwanda, na kumpongeza Rais Dkt John Magufuri kwa kazi kubwa anayofanya kuanzisha viwanda ambavyo vitakuwa mkombozi mkubwa wa kiuchumi hapa Nchini.

Walisema, tangu kuanzishwa kwake shule imeweza kufanikisha kuwa na matokeo mazuri kitaaluma kwa kidato cha pili kwa miaka miwili mfululizo 2017 ilishika nafasi ya kwanza kiwilaya na mkoa na mwaka 2018 ilishika nafasi ya kwanza kiwilaya na mkoa ilishika nafasi ya tatu.

Walisema, matokeo hayo mazuri kitaaluma yametokana na walimu kutoa mitihani ya kutosha kila wiki,mwezi,robo muhula na ya mwaka ya ndani na nje na kuwa na mazoezi ya kutosha madarasani.

Hata hivyo, wameuomba uongozi wa shule hiyo chini ya mmiliki na meneja wake Omari Msigwa kuanzisha kidato cha tano na sita ili wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne waweze kupata maarifa zaidi katika mchepuo wa sayansi na ndoto zao ziweze kutimia hata kwa wahitimu wengine wa kidato cha nne kwa manufaa ya Tanzania ya viwanda.

Mgeni rasmi katika mahafali hao Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi amepongeza uwekezaji mkubwa uliofanyika katika shule hiyo hasa kwa kuwa na majengo ya kutosha na yenye ubora wa hali ya juu ambayo yanatoa fursa kwa wanafunzi kujisomea na walimu kufundisha vizuri.

Alisema,kuwepo kwa maabara za kisasa na zenye vifaa vya kutosha katika masomo ya sayansi vinawezesha wanafunzi kufanya mazoezi kwa vitendo ambapo Benki ya TPB imetoa msaada wa kompyuta 10 kwa shule hiyo ambazo zitawasaidia wanafunzi kuongeza maarifa na walimu kuandaa masomo.

Moshingi alisema, wazazi hawakufanya makosa kupeleka watoto wao katika shule hiyo ambayo ina mazingira rafiki inayowezesha wanafunzi kupenda na kufurahia masoma ikilinganisha na shule nyingine hapa nchini.

Moshingi,amewapongeza wanafunzi hao kwa matokeo mazuri waliyopata katika mitihani mbalimbali ya majaribio kwani yanatia matumaini ya kufanya vizuri zaidi kwenye mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne.

Amewataka wahitimu hao, kuwa mfano mzuri kwa wazazi na jamii inayowazunguka, na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kukatisha ndoto zao wakati huu wanaposubiri matokeo ya mitihani yao.

Moshingi ambaye ni mlezi wa shule hiyo,amewaasa wazazi kwenda kuwalea vijana hao kwa maadili mema na nidhamu ya hali ya juu ili wale watakao chaguliwa kuingia kidato cha tano wakawe mabalozi wazuri wa shule ya FEO Girls kwa kufanya vizuri katika masomo yao.

Moshingi,amewataka wanafunzi na wazazi kuona umuhimu wa kutumia huduma ya benki ya TPB Tanzania ambayo imekuwa kimbilio la wananchi wengi kutokana na ubora wa huduma zake kama ,mikopo ambayo imewasaidia watu wengi kuanzisha na kukuza shughuli zao za kiuchumi na wanafunzi kuweka akiba kwa ajili ya kutimiza malengo yao katika masomo.

Kwa upande wake meneja wa shule hiyo Omari Msigwa, amewashukuru wazazi kwa kuiamini shule hiyo na kupeleka watoto wao bila kujali muda tangu ilipoanzishwa ambapo amehaidi kuendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili wanafunzi na walimu wa shule hiyo kila upande uweze kutekeleza majukumu yake vizuri.

Msigwa alisema, malengo yaliyopo ni shule kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani mbalimbali kuanzia ngazi ya wilaya,mkoa na Taifa ili iwe miongoni mwa shule kumi bora hapa nchini.

Alisema, ni matumaini yake kuwa wazazi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wataendelea kupeleka watoto katika shule hiyo kwa ajili ya kupata elimu bora na sio bora elimu hasa kwa kuzingatia uwekezaji mkubwa uliofanyika kama walimu wa kutosha na wenye uwezo,vifaa na miundombinu ya shule.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA RAIS WA KAMATI YA OLIMPIKI ZA AFRIKA.

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Rais wa Umoja wa Kamati za Olimpiki za Afrika.Bw.Mustapha Berraf, alipofika Ikulu Zanzibar na Ujumbe wake kuonana na Rais wa Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Kocha Gulam Abdalla, wakati wa hafla ya mazungumzo na Ujumbe wa Umoja wa Kamati za Olimpiki za Afrika walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais leo,17-11-2019, kulia Katibu wa TOC Ndg. Filbert Bayi.(Picha na Ikulu).





RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Rais wa Kamati za Umoja wa Olimpiki za Afrika Bw.Mustapha Berraf kulia akiwa na Ujumbe wake walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 17-11-2019.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimia na kuagana na Rais wa Umoja wa Kamati za Olimpiki za Afrika Bw.Mustapha Berraf, baada ya kumaliza nmazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo,17-11-2019.(Picha na Ikulu)

WANAWAKE KISARAWE WACHANGAMKIA NAMBA YA UTAMBULISHO WA MLIPAKODI

$
0
0
NA RIPOTA WETU, KISARAWE

KATIKA hali isiyo ya kawaida, idadi kubwa ya wanawake wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani wamejitokeza kujisajili Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) hatimaye watambulike kama walipakodi na waweze kufanya biashara zao kwa uhuru na halali.

Hali hiyo ilijitokeza wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma, elimu ya kodi na usajili wa walipakodi inayoendelea katika mkoa wa Pwani ambapo katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji idadi kubwa ya wanaume ndiyo iliyokuwa inajitokeza kupata TIN lakini hali imekuwa tofauti katika Wilaya ya Kisarawe ambapo idadi kubwa ya wanawake ndiyo iliyojitokeza.

Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi kutoka TRA, Honesta Ndunguru amesema ni kweli kwamba idadi kubwa ya wanawake wamejitokeza kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi katika Wilaya ya Kisarawe ukilinganisa na wilaya zingine za mkoa wa Pwani walikopita.

Ndunguru amesema, TRA imevutiwa na mwamko wa wananchi wa wilaya zote katika mkoa wa Pwani na kuwapongeza wale wote waliojitokeza kupata huduma, elimu pamoja na kujisajili kuwa walipakodi.

“Kwa mwitikio huu, inadhihirisha kwamba elimu ya kodi tunayoitoa inawafikia walengwa na wanafuata sheria ya kodi inayomtaka kila mfanyabiashara kujisajili na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi inayotolewa bure na TRA”, amesema Ndunguru.

Kwa mujibu wa Ndunguru kati ya wananchi 10 waliojitokeza kupata TIN 8 kati yao walikuwa wanawake, tofauti na wilaya nyingine ambapo idadi kubwa walikuwa wanaume.

Baadhi ya wanawake waliojitokeza katika viwanja vya stendi ya zamani ili kusajiliwa na kupata TIN hawakusita kueleza hisia zao ya kwamba wanawake wa wilaya ya Kisarawe wamepata mwamko wa kufuata sheria za nchi zikiwemo za kulipa kodi ili waweze kutumia fursa mbalimbali ambazo zionatokana na kutambulika na serikali kama vile kupata mikopo ya wajasiliamali na huduma zingine muhimu.

“Binafsi nimehamasika na kuja kupata Tin kwa sababu nimeelimishwa na maofisa wa TRA na nimeelewa umuhimu wa kujisajili kama mlipakodi na kulipa kodi kwa nchi yangu”, amesema Fatma Omari

Naye Sophia Ndume mkazi wa Kisarawe ameongeza kuwa wanawake wa Kisarawe ni wahangaikaji katika biashara ndiyo maana wamehamasika kwa wingi kuja kuchukua TIN ili wakafanya biashara zao kwa uhuru bila kubughudhiwa.Zainess Madeng’ha ambaye ni mmiliki wa saluni ya kike, amesema amehamasika kuchukua TIN baada ya kupata elimu kutoka kwa maofisa wa TRA na kwamba huduma hiyo imesogezwa karibu na inapatikana bure.

“Kwa kweli nimeona nitumie fursa hii kwa kuwa huduma imenifuata dukani kwangu na vile vile Napata huduma hii bure bila kulipia chochote”, alisema.
TRA inafanya wiki ya elimu kwa mlipakodi katika mikoa ya Pwani na Morogoro kwa lengo la kusogeza huduma za ulipaji kodi karibu na wananchi lakini pia kusajili walipakodi ili kuongeza idada ya walipakodi nchini.
Zainess Madeng'ha (kulia), mkazi wa Kisarawe mkoani Pwani akifurahia kupokea Cheti cha Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kutoka kwa maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika wiki ya mlipakodi inayoendelea mkoa wa Pwani.
Afisa wa TRA akiwahudumia akina mama hawa kupata Vyeti vya Utambulisho wa Mlipa kodi yaani TIN, huko Kisarawe mkoani Pwani.
Wanawake wa wilaya ya Kisarawe wakichangamkia fursa ya kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN)
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images