Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 321 | 322 | (Page 323) | 324 | 325 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Mabalozi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa wakati wa Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya (Sherry Party) aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam leo January 10, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakisikiliza hotuba toka kwa Balozi wa DRC nchini Mhe Asumani Mpango ambaye pia ndiye Kiongozi wa Mabalozi nchini akihutubia wakati wa Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya(Sherry Party) Ikulu jijini Dar es salaam leo January 10, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja Mabalozi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa wanawake wakati wa Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya (Sherry Party) aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam leo January 10, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja Mabalozi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa wakati wa Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya (Sherry Party) aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam leo January 10, 2014. PICHA NA IKULU

  0 0

  Naibu Katibu wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Hamis , akipokea sehemu ya Tisheti maalum kwa niaba ya Makamu, kutoka kwa Meneja wa NMB Tawi la Zanzibar Town, Bakari Hamis Mohamed, kwa ajili ya Vijana wa Mkoa wa Kusini Pemba zitakazotumika katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, zinazofanyika kesho kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar. Katikati ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Abuu Msagula. Picha na OMR

  0 0

   Jeneza lenye mwili wa Marehemu Sultan Sikilo,aliekuwa Mweka Hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na mchezaji wa timu ya Waandishi wa Habari za Michezo TASWA Fc ambaye pia alikuwa Mtangazaji wa Radio Aboud ya Mjini Morogoro,ukitolewa ndani ya Nyumba yao,eneo la Mbagala Maji Matitu kwa ajili ya kusaliwa na kuanza kwa safari ya kwenda mashikoni.
  Waumini wa Kiislam wakiswalia Mwili wa Marehemu Sultan Sikilo.
  Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sultan Sikilo likiwa limebebwa tayari kwa safari ya kwenda kwenye nyumba ya Milele.
  Wadau mbali mbali wakishirikiana kubeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sultan Sikilo.


  0 0
 • 01/11/14--09:32: Article 22
 • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  MFUKO WA PENSHENI WA PSPF  Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanaungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein pamoja na wananchi wote wa Tanzania katika kuadhimisha miaka hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar, 12 Januari 2014.

  Kwa Mahitaji yako ya Hifadhi ya Jamii PSPF ni chaguo lako, Jiunge sasa

  “PSPF TULIZO LA WASTAAFU”

  Mkurugenzi Mkuu,
  PSPF

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtunuku nishani ya Mapinduzi Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Salmin Amour Juma,katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,katika shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduziya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtunuku nishani ya Mapinduzi Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Amani Abeid Karume,katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,katika shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduziya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtunuku Nishani ya Mapinduzi Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Ali Hassan Mwinyi,katika hafla kutunuku Nishani iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduziya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtunuku Nishani ya Mapinduzi Viongozi wenye sifa Maalum kwa Dk. Salim Ahmed Salim,katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduziya Zanzibar.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 01/11/14--10:39: SALAAM ZA RAMBIRAMBI
 • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
   JESHI LA MAGEREZA TANZANIA BARA

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja na Maafisa, Askari na Watumishi raia wote wa Jeshi la Magereza wanatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Wizara ya Fedha na Familia ya aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. William A. Mgimwa.

  Jeshi la Magereza  litamkumbuka kwa ushauri wake na ushirikiano aliouonyesha akiwa Waziri wa Fedha katika kufanikisha maendeleo na ustawi wa Jeshi la Magereza.

  Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

  AMIN

  0 0

  Former Israeli Prime Minister Ariel Sharon, the trailblazing warrior-statesman who transformed the region and was reviled by Arab foes, died on Saturday aged 85, after eight years in a coma caused by a stroke.

  Sharon left historic footprints on the Middle East through military invasion and Jewish settlement-building on occupied land the Palestinians seek for a state but also with a shock decision to withdraw from the Gaza Strip.

  The United States and other foreign powers mourned Sharon as a peacemaker, noting his late pursuit of dialogue with the Palestinians. Those talks continue under Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu, though differences remain wide.

  Sharon died at Sheba Medical Center, near Tel Aviv, where he had been in a coma since being hit by a stroke at the pinnacle of his power as prime minister in January 2006. His condition had declined precipitously since the middle of last week.

  "Arik was a valorous soldier and a bold statesman who contributed much to the security and building up of the State of Israel," said President Shimon Peres, a former political ally of Sharon and, with the ex-premier's death, the last of the Jewish state's founders still in public life.


  0 0

  Mhandiri Msaidizi wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Missanya Bingi, (kulia) akiwa na Mkuu wa kituo cha polisi Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, SP Ally Mohamed Mkalipa , wakiwa wamemaliza warsha ya wadau wa madini kuhusiana na ugatuzi na ugatuaji wa madini yaaani kunufaika kupitia rasilimali hiyo.
  Mhandiri Msaidizi wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Missanya Bingi, (kulia) akiwaelekeza wadau wa madini wa wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, jana mji mdogo wa Mirerani katika warsha ya ugatuzi (kunufaika) na madini.

  0 0

  Javed Jafferji , Tanzania top photogarpher and film maker had a pleasure to present a copy of his new book, Zanzibar Photographic Journey - 50 years of the Revolution to former Prime Minister of United Republic of Tanzania, Edward Lowassa in Zanzibar prior to Revolution day in Zanzibar today. The book consistd of 328 pages and it took almost one year to publish .

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa 8 wa kanisa la kiinjili na kilutheri Tanzania KKKT la mjini Sumbawanga ambapo utafanyika uchaguzi Mkuu wa Kanisa hilo na kuzaa Dayosisi mpya ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika. Katika hotuba yake hiyo aliwaasaviongozi na waumini wa kanisa hilo kuepukana na vitendo vya rushwa katika kuweka uongozi kanisani hapo pamoja na kuepukana na mambo maovu na machafu ikiwemo kudumisha amani ya nchi.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiimba moja ya wimbo wa maubiri na Baba Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga Askofu Damian Kiaruzi wakiwa miongoni mwa wageni waalikwa katika Mkutano huo.
  Kwaya ya Kanisa hilo.
  Sehemu ya waumini na waalikwa katika Mkutano huo.
  Picha ya pamoja.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiagana na viongozi wa kanisa hilo na baadhi ya wageni waalikwa.(Picha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

  0 0

  Picha na Urban Pulse
  Imeandikwa na Freddy Macha

  Mradi wa majaribio ya mwezi mmoja ulioandaliwa na Waingereza kuendeleza shule sita wilaya za Arusha na Moshi unatazamiwa kuanza wiki hii, ilitangazwa London, mwishoni mwa juma.

  Mradi huu unaosimamiwa na kampuni ya kitalii, Safari Hub na Chuo cha Eton wakisaidiana na Ubalozi wa Tanzania, Uingereza, unatuma Mkuu wa Mafunzo ya Michezo Eton, Bwana Glen Pierce na wanafunzi watatu waliomaliza kidato cha sita wanaotarajia kuingia vyuo vikuu baadaye mwakani.

  Nchini shughuli hii itasaidiwa na ushirikiano wa chuo cha michezo Arusha (Future Stars Academy) na shirika la ufadhili linalopigana kuondoa umaskini, (ACE Africa).

  Akiongea katika tafrija ndogo iliyofanywa Ubalozini, London kuuaga msafara , Mkurugenzi Mkuu wa Safari Hub, bwana Dilip Navapurkar alisema iko haja ya kujenga ujuzi toka utotoni ili “kuhakikisha timu ya taifa ya Tanzania inafanya vizuri katika michuano ya Kombe la Afrika na Dunia na kufikia kiwango cha mafanikio tunayoyaona nchi nyingine mathalan Nigeria, Ghana, Afrika Kusini na Ivort Coast.”

  Mwalimu Pierce mwenye uzoefu wa Miaka 27 chuo cha Eton aliwafundisha pia wajukuu wa Malkia Uingereza, William na Harry. Wanafunzi atakaoongozana nao ni Tom Pearson, 18 ( ulinzi) Nicholas Zafiriou, 18 (kiungo) na Ali Lyon, 19 (mshambuliaji ). Wamechaguliwa kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ukiwemo mpira waliocheza timu ya shule ya Eton.

  Eton ilianzishwa karne ya 15 na Mfalme Henry wa 6 na ni moja ya shule bora sana duniani. Mawaziri Wakuu 19 wa Uingereza (akiwemo Winston Churchill, Tony Blair, David Cameron na Meya wa Jiji la London, Boris Johnson) walisoma hapa. Wabunge, mawaziri, waandishi maarufu (George Orwell na Ian Fleming mtunzi wa visa vya James Bond) na watoto wa wafalme mbalimbali duniani vile vile wamesoma Eton.

  Tafrija ya kuwaaga ilifanywa na Balozi Peter Kallaghe na Afisa Balozi, Amos Msanjila aliyewakaribisha Tanzania. Mbali na kutoa mafunzo ya michezo wageni wanatazamiwa kukutana na wanahabari Jumanne, kutembelea mbuga za wanyama, Zanzibar na kupanda mlima Meru, Arusha.

  Lengo la mradi huu ni safari au mradi mfupi na hatimaye kuendeleza mahusiano kati ya wanafunzi wa Tanzania na Eton. Iko siku “timu ya mpira ya Eton itafanya ziara Tanzania na hatimaye Watanzania pia kuitembelea Eton,” Bwana Navapurkar alisema.

  Akihimiza umuhimu wa safari hii, Balozi Kallaghe aliwaambia wageni kwamba Watanzania wanapenda sana soka na kuwaahidi wageni kuwa watafaidi uzuri wa nchi watakapofika kama sehemu ya mafanikio ya kibiashara siku za mbeleni na kufurahia michezo Tanzania.

  Akijibu maswali ya wanahabari, Bwana Navapurkar alisema gharama za safari na vifaa vimetokana na michango ya watu binafsi na shule zinazopakana na Eton ambazo zimefikia shilingi milioni 61 na nusu.

  Mbali na mafunzo ya mpira wanafunzi Arusha na Moshi watapewa vifaa na kufundishwa maana ya nidhamu, elimu na michezo, aliongeza kocha Glen Pierce. “Watoto watakaopewa fursa hiyo ni wale tu watakaohudhuria shule,” alisisitiza.

  Akisifia tabia ya Watanzania, Mkurugenzi wa Safari Hub, yenye makao Tanzania, Bwana Navapurkar, alisema Tanzania imechaguliwa shauri ni nchi yenye amani, demokrasia na utulivu wa kisiasa, ukilinganisha na nchi nyingine za Kiafrika. “Tanzania ni kito cha maendeleo ya Afrika.” Alisema.
  Balozi Peter Kallaghe
  Bw John Collenette wa ACE Africa
  Afisa Balozi -Minister Counsellor- Amos Msanjila akizungumza na Freddy Macha na Urban Pulse.
  Amos Msanjila, Tom Pearson, Dilip Navapurkar, Balozi Kallaghe, Ali Lyon, Nicolas Zafiriou, Glen Pierce, Yusuf Kashangwa.
  Balozi Kallaghe na msafara. Kulia kwake ni Bw Dilip Navapurkar na mwanzo Kocha Glen Pierce-picha na Urban Pulse.
  Balozi na wageni wote. Kwanza kabisa kulia ni Mkurugenzi wa Biashara Ubalozini, Yusuf Kashangwa- pic by Urban Pulse.

  0 0

  Excel Management and Outsourcing company (T) Limited is a professional organization offering a comprehensive range of HR and Investment advisory as well as corporate branding services. Excel commences its operations in Tanzania in January 2014 with the goal of offering quality advisory services to Tanzanian and African corporate and SMEs.

  Excel has positioned itself to provide HR and investment advisory services with the specific goal of helping client organizations address their human resource and investment planning challenges, which have been identified as major encumbrances to business growth and competitiveness.


  According to the HR Landscape Report 2013, there has been a simultaneous challenge to traditional HR practices with the rapid rise of mobile technology and social media. Such developments have helped to drive changes in the past three years, both in terms of the acceptance of technology in assessment and in its perceived value.


  0 0

  Ibra's Birthday. 034Ibra akiwa na mama yake Mariam waliposheherekea mwaka mmoja wa kuzaliwa kwake huko Vienna Virginia Jumamosi January 11,2014. Ibra's Birthday. 088Mama Ibra na Mindy wakimpongeza Ibra. Ibra's Birthday. 092Wadau waliojitokeza kumpongeza motto Ibra. Kwa picha zaidi ungana na sundayshomari.com

  0 0

  Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadiq ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo (wa pili kulia) akisisitiza jambo wakati uzinduzi wa baraza hilo mwishoni mwa wiki Dar es Salaam. kulia ni Kamishina wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova; Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi (kushoto) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Theresia Mbando.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa baraza la biashara la mkoa wa Dar es Salaam mwishini mwa wiki jijini humo. Wengine ni Mwenyekiti wa baraza hilo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadiq (wa pili kulia), Kamishina wa Polisi, Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova (kulia) na Katibu Tawala, Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Theresia Mmbando (wa pili kushoto).

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

  Wajumbe wa Baraza la Biashara Mkoa wa Dar es Salaam wamehimizwa kuunganisha nguvu zao pamoja ili baraza hilo liwe na nguvu kubwa ya kutekeleza majukumu yake kwa ajili ya kukuza biashara na uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla.

  Mwenyekiti wa baraza hilo Said Meck Sadiq ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo aliwambia waandishi wa habari wakati wa kikao cha uzinduzi wa  baraza hilo kuwa nguvu ya pamoja itasaidia mkoa kufikia malengo yake zaidi ya biashara na uchumi.

  “Ili baraza liweze kuwa na nguvu na maamuzi sahihi wajumbe wote wanahitaji kushiriki kwa uzito wao,” alisema na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo watasaidia mkoa wao kuzidi kupiga hatua kibiashara.

  Alisema uchumi wa nchi unategemea ushiriki wa sekta ya umma na sekta ya binafsi na baraza hilo liliundwa ili kuwa chombo kinacho wakutanisha kwa ajili ya maswala hayo.

  Alisema pamoja na kwamba baraza la mkoa tangu kuzinduliwa mwaka 2007 halikuweza kufanya mikutano, kwa sasa litakuwa linakutana kila baada ya miezi mitatu kutokana na umuhimu wake.

  Alifafanua kwamba baraza hilo ni semu muhimu kwa wafanyabiashara wa mkoa wake kuzungumza kero zote za kibiashara ili wote kwa pamoja waweze kuja na majibu ya uboreshaji shughuli za biashara.

  “Hakuna sememu nyingine muhimu kwa sekta binafsi kusemea maswala yao kama hii,” alisema na kufafanua kuwa maswala kama ya msongamano wa magari na changamoto za mashine za risiti zinaweza kutatuliwa na baraza hilo.

  Pia aliyasisitiza mabaraza ya wilaya zote tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni kufanya mikutano haraka ili ajenda zao zifikishwe kwenye baraza la mkoa na kujadiliwa kwa maamuzi zaidi.

  Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi alisema kikao hicho kilikuwa cha maandalizi ya mkutano wa baraza unaotarajia kufanyika mwezi ujao baada ya baraza la mkoa kupata wajumbe wake wapya mwezi Novemba mwaka jana.
  “Mabaraza kama haya yameonyesha mafanikio makubwa sana katika mikoa mingine hapa nchini,” alisema.

  Alisema baraza la mkoa wa Dar es Salaam ni muhimu sana kwa vile thamani ya biashara inayofanyika katika mkoa huo inachangia kwa kiwango kikubwa uchumi wa Tanzania.

  “Kikao hiki tumekifanya ili wajumbe waweze kufahamishwa kuhusu majukumu yao na tutaendelea kufanya hivyo ili kuwasaidia kutimiza majukumu ya baraza,” alisema.

  Alisistiza kuwa sekta binafsi ni wabia wa maendeleo na kuwa TNBC itahakikisha inafanya kazi kwa karibu na baraza hilo ili kufikia malengo ya kibiashara yanayokusudiwa.


  Baraza hilo la mkoa linaundwa na wajumbe 40, nusu kutoka sekta ya umma na wengine kutoka sekta binafsi.

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akizungumza wakati wa kuzindua programu ya kutoa elimu ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana iitwayo Ishi Huru.

  0 0

  Nawashukuru sana ndg,jamaa na marafiki popote mlipo kwa Dua zenu katika Kumuombea mtoto Mpendwa Sheikha Abdulaziz ambaye ametimiza Umri wa Miaka 3 toka azaliwe tarehe 11 jan 2011 Hakika dua zenu ni msingi mwema wa Maisha yake..Sote kwa pamoja tuzidi kumjazia heri ili asaidie Maendeleo ya Nchi yetu Natanguliza shukrani 

   Mdau wenu-ABDULAZIZ VIDEO-LINDI

  0 0

  MWENYEKITI Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maulid kwa wanawake wa    mkoa wa Dar es Salaam, kuadhimishwa kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W),  Aisha Sururu (wa kwanza kulia), akiwaongoza wanawake wengine kuomba    dua, baada ya kumaliza kikao cha maandalizi ya sherehe hizo
  zitakazofanyika kesho, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
  =======  =====  =======
  WANAWAKE viongozi wa kitaifa na mkoa wa Dar es salaam, wameombwa
  kujitokeza ili kuungana na wanawake wengine wa kiislam, katika
  sherehe ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W).

  Wito huo ulitolewa na Kamati ya Maandalizi ya sherehe hizo kwa upande
  wa wanawake, na kubainisha kuwa hawataalika mgeni rasmi, badala yake ,
  viongozi na wanawake wengine wawe kitu kimoja kuadhimisha siku hiyo.

  Mwenyekiti wa kamati hiyo, Aisha Sururu, alisema, sherehe itafanyika
  Januari 14, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, na kwamba
  itawakutanisha wanawake waislam wa mkoa wa Dar es Salaam na mkoa
  jirani wa Pwani.

  "Wanawake wa hali ya chini, wamefikiria kwanini sherehe za kidini
  ambazo hazina harambee, michango wala kitu chochote, tualike mgeni
  rasmi? Wakaona ni vyema kutangaza ili nao kama wananchi wajumuike na
  wanawake wa hali ya chini, ambao watafarijika zaidi, kuona wamekaa
  mkekani pamoja na viongozi wakubwa,"alisema
  Aisha.

  Mwenyekiti huyo, ambaye pia ni diwani viti maalum Ilala, alisema, kwa
  wale ambao hawatafikiwa kwa mualiko wa mmoja mmoja, wanaruhusiwa
  kujumuika na wenzao siku hiyo ya maadhimisho.

  Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), huadhimishwa duniani  kote kila ifikapo mfungo wa sita kwa kalenda ya kiislam. ikiwa ni
  kumbukumbu tangu kuzaliwa kwa kiongozi huyo wa wafuasi wa dini ya
  kiislam.

  Maandalizi ya sherehe hiyo kitaifa, mwaka huu yatafanyika mkoani
  Kigoma, ambapo Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), limesema
  mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.

  0 0

  Baadhi ya watoto yatima wa kituo cha Sifa Group Children Foundation Center kilichopo Bunju, Dar es Salaam wakiwapokea kwa furaha wafanyakazi wa Idara ya mauzo na Usambazaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania wakati walipoenda kutoa msaada kwenye kituo hicho. Msaada huo wa chakula na vitu mbali mbali kupitia kampeni ya pamoja na Vodacom.
  Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kutoka kushoto ni Happiness Macha na Elihuruma Ngoi wakisaidia kushusha msaada wa chakula iliyotolewa na wafanyakazi wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo kwa kituo cha kulea watoto yatima cha Sifa Group Children Foundation Center kilichopo Bunju, Dar es Salaam kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom.
  Mkurugenzi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Sifa Group Children Foundation Center Bi. Sifa John kutoka kulia akipokea kiroba cha chakula kama sehemu ya msaada kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom, anaekabidhi (Katikati) ni Mkuu wa idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Julius Kastabu, (kushoto) ni Meneja wa Mipango na Uuzaji Baraka Bitebu.

  BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI

  0 0

  By Jestina George,
  “Tanzania has taken the first step towards producing their first Premier League player – thanks to Eton College, England’s premier public school.
  Eton Coach, Glen Pierce speaking at the press conference on Friday 10 Jan 2014 at Tanzania House London. 
  Together with Safarihub and charity organisation ACE Africa, Eton are sending Glen Pierce, head of sports, plus Ali Lyon, 19, Nicholas Zafirios, 18,  and Tom Pearson,18, who are on a gap year before starting university, to Tanzania to teach local children the finer arts of football.
  Ali has already passed his  Level 1 Football Association coaching badge and the quartet cannot wait for the challenge ahead of them.
  Coach Glen Pierce with Eton students who will be travelling to Tanzania, Nicolas Zafiriou, Ali Lyon and Tom Pearson
  Pierce said: “We are about to embark on a wonderful trip. I have taught at Eton for 27 years and was offered the opportunity to take a sabbatical. This is an chance to see a new country with boys I tutored. We shall be going into schools to coach and to encourage kids to attend school through football. If they do not go to school they will not have this opportunity. We want to attract them to go to school and football is the icing on the cake. I hope the boys will be an encouragement to local kids.”Eton was founded in 1440 and among the college’s more recent famous old boys are Prime Minister David Cameron, Mayor of London Boris Johnson, the Archbishop of Canterbury plus Prince Harry and Prince William, who Pierce taught.
  Minister Counsellor  Amos Msanjila speaking Freddy Macha & Urban Pulse
  Amos Msanjila, Minister Counselor of the High Commission, did not hide his pride about the venture. He said: “We are honoured to have the boys going because Eton is not a normal school. In Tanzania we do not have a culture of different schools, but I have been in England long enough to know which school you attend matters. Eton has produced 19 Prime Ministers so, as I said, it is not a normal school. The boys could have gone to any country in Africa, indeed in the world, and we have so much pleasure that they chose Tanzania.” 
  Director of  Safari Hub, Dilip Navapurkar  speaking at the press conference on Friday 10 Jan 2014 at Tanzania House London.
  Dilip Navapurkar from Safarihub said: “I recently formed the company and one aim is to set up a pilot scheme to play football. We hope to see Tanzania qualify for the World Cup for the first time and produce some top-class Premier League footballers, but it will not happen overnight.

  "Tanzania has the raw talent, it is our belief that we will one day produce players who will perform on the world's biggest stage."

  John Collenette, chairman of ACE Africa and Future Stars Academy, said: “I have been in Tanzania for five years and I am particularly excited about this venture. Children have different problems to confront in their daily lives and we are committed to help them.”
  High Commissioner Peter Kallaghe speaking at the press conference on Friday 10 Jan 2014 at Tanzania House London.
  Peter Kallaghe, the High Commissioner, hosted a reception in London on Friday to announce the collaboration with Eton College and sent the football party away with his best wishes. He said:“We are greatly honoured by this initiative. We are fully behind a wonderful plan. Eton has produced 19 British Prime Ministers, maybe we have the 20th travelling to Tanzania this weekend."
  High Commissioner Pete Kallaghe poses with guests after the press conference.
  Images by Urban Pulse

  0 0

  Sehemu ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama vilivyoshiriki kwenye Sherehe za Maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yanayoendelelea kufanyika hivi sasa kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la heshima wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014.
  Vijana wakiachia njiwa kama alama ya amani wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein wakimpongeza Rais Yoweri Kaguta Museveni aliyeongea machache wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein kwa hotuba nzuri aliyotoa wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiongea wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014. PICHA NA IKULU.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 321 | 322 | (Page 323) | 324 | 325 | .... | 3284 | newer