Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki kusheherekea miaka 20,kufanya mkutano jijini Arusha

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPST), Godfrey Sembeye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha mkutano wa wafanyabiashara wa nchi za Juimuiya ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPST), Godfrey Sembeye katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha mkutano wa wafanyabiashara wa nchi za Juimuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Novemba 28,29, mwaka huu jijini Arusha. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Afrika mashariki Emma Oriyo na kushoto ni Mwakilishi wa EABC, Rafael Maganga.
 Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPST), Godfrey Sembeye jijini Dar es Salaam leo.

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
BARAZA la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) linatarajia kusheherekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwake pamoja na kufanya mkutano wa kujitadhimini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPST), Godfrey Sembeye, amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika Novemba 28-29, 2019 jijini Arusha kwa kuwakutanisha wafanyabiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema kuwa mada kuu katika mkutano huo itakuwa ni kuangalia masuala ya kodi kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuangalia minyonyoro ya thamani, kuangalia viwango vya bidhaa, gharama za usafirishaji, muda wa usafirishaji pamoja na mawasiliano katika biashara.

Aidha Sembeye amesema kuwa wanatarajia marais wa nchi hizi za Afrika Mashariki kuhudhuria ingawa kuna baadhi ya viongozi hawajathibitisha kama watahudhuria katika mkutano huo.

"Tunategemea marais wote wa Afrika Mashariki watahudhuria kwenye Mkutano wa Biashara na uwekezaji kabla hawajajumuika kwenye mkutano wa Viongozi ambao unatarajiwa kufanyika Novemba 30, 2019", amesema Sembeye.

Kwa Upande wake Mwakilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rafael Maganga amesema zaidi ya wafanyabishara zaidi mia tano wanatarajia kuhudhulia mkutano huo. 

Amesema ni nafasi nzuri kwa watanzania kuangalia fursa za kuanza kuwauzia majirani bidhaa mbalimbali kwa hiyo kongamano hilo walitumie vizuri.

Washiriki ni wafanyabiashara wa Nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda na Sudani Kusini. 

Muungano wa Tigo na Zantel utakuza uchumi kupitia soko la mawasiliano ya simu

$
0
0
ILITANGAZWA siku za karibuni kuwa Tanzania imepanda toka nafasi ya 144 hadi ya 141 katika taarifa ya Benki ya Dunia kuhusu ubora wa mazingira ya kufanya biashara. Hii inaifanya Tanzania kuwa nafasi ya nne katika eneo la Afrika ya Mashariki ukitazama nchi 190 duniani ambazo ripoti hiyo imeziainisha.

Zipo sababu mbalimbali ambazo zimechangia maendeleo haya kutoka katika sekta binafsi na juhudi za serikali katika kusaidia ukuaji wa sekta hiyo. Juhudi hizo zimesaidia si tu kukua kwa biashara lakini pia zimefanya mazingira ya kufanya biashara nchini kuwa na unafuu.

Tukichukulia kwa mfano sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi ambayo kwa muda mrefu imekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi nchini. Unafahamu kwamba mpaka kufikia mwaka 2016 sekta hiyo imechangia karibu dola za Kimarekani bilioni 2.5 katika uchumi wa Tanzania? Hii ni sawa na shilingi za Kitanzania trilioni 5.75 au asilimia 5.2 ya pato la taifa.

Tafiti nyingi za kiuchumi zimeendelea kuweka bayana ushahidi wa wazi kuhusu umuhimu wa sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi na ni kwa sababu hii kama taifa hatuna budi kuendelea kuhakikisha kwamba sekta hii inalindwa na kusaidiwa kukua vizuri.

Wabobezi wa uchumi wanasema kuwa mojawapo ya njia za kuboresha sekta hii ni kuunganisha makampuni ambayo yako sokoni. Hivi sasa kuna kampuni sita za mawasiliano ya simu za mkononi nchini ikiwa yamepungua kutoka saba ya awali baada ya kampuni ya Smart kuondoka.

Namba hii japo imepungua moja lakini inaelezwa kuwa ni kubwa kwa aina ya soko lililopo nchini. Jambo hili lina athari hasi kwa maendeleo ya sekta hii na hata uwekezaji wenye tija ambao ungeweza kuboresha sana huduma.

Licha ya tatizo hilo, mwanga umeanza kuonekana. Kampuni ya Tigo Tanzania imeungana na kampuni ya Zantel. Hii inaonyesha makampuni yameanza kuelewa umuhimu wa kuungana na kuwekeza vyema zaidi kupanua huduma. Mbali na kuwa ni jambo la afya kwa sekta na uchumi lakini pia ni muhimu zaidi kwa wateja. Mapema mwaka huu wa 2019 Wakurugenzi wa Tigo na Zantel walipokuwa wakizungumza na jarida maarufu duniani la Forbes walikaririwa wakieleza ni kwa namna gani muungano wa kampuni hizo mbili utaboresha huduma na ubunifu katika soko na kuongeza wateja wengi zaidi.

Ama kwa hakika ni jambo jema kuona sekta ya mawasiliano inavyouinua uchumi wetu. Sekta ya mawasiliano yenye muungano wenye tija kama ule wa Tigo na Zantel itakuwa na mchango mkubwa zaidi kwa ukuaji wa uchumi wetu sambamba na kuwapa watumiaji wa simu za mkononi nchini kile kilicho bora.

VODACOM YABORESHA MFUMO WAKE WA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0

Yatambulisha menyu mpya ya USSD kwa huduma binafsi 

‘Customer Service’ sasa kuitwa ‘VODACARE’ 

Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania PLC, hivi karibuni iliadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, kwa kutangaza mabadiliko katika mfumo wake wa huduma kwa wateja. Lengo la mabadiliko hayo ni kutoa uhuru kwa wateja wake kupata huduma kwa urahisi pale inapotakiwa.

“Tuna zaidi ya njia nane ambazo mteja anaweza kuzitumia kutufikia na leo tunaiongeza nyingine ambayo itampa mteja fursa ya kujihudumia; hii ni menyu ya USSD, ambayo inapatikana katika simu,” alisema Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom, Harriet Lwakatare

Kwa kupiga *149*01# mteja anaweza kufanya miamala ya M-Pesa, kuangalia taarifa za matumizi, kupata huduma muhimu kama vile kununua Luku, kuangalia salio, kifurushi cha intaneti na taarifa kuhusu bidhaa mbalimbali za Vodacom. 

“Kwa idadi ya zaidi ya wateja milioni 14, kitengo cha huduma kwa wateja ni kati ya vitengo vyenye kazi muda wote. Vodacom inaendelea kukua kiteknolojia na kuwapa huduma ya kidigitali wateja wake ili kutoa huduma endelevu kupitia njia kadha wa kadha 

“Tunajali mahitaji ya wateja kwa huduma ya haraka na nyepesi. Ndio maana hatujachoka kufanya kazi na kuendelea kuwapa wateja wetu kilicho chaguo kwao na hasa linapokuja suala la kuhitaji msaada. Tuna huduma kwa wateja kwa njia ya kidigitali kupitia WhatsApp, Mitandao ya kijamii, majibizano kwa njia ya sauti (IVR) na mawasiliano ya moja kwa moja. Na sasa tunawaletea menyu ya USSD kwaajili ya huduma binafsi kwa mteja,” alisema Harriet.

Katika hatua nyingine, Harriet alisema kuwa, kuanzia sasa njia zote za huduma kwa mteja zitakuwa zikifahamika kama VODACARE; hii ni ishara kwa Vodacom kuwa imeamua huduma binafsi na za kipekee kwa wateja 

“Tumebadilisha jina la ‘Customer Care’ kwenda ‘VODACARE’ sambamba na maboresho ya kipekee tuliyoyafanya katika kitengo cha huduma kwa wateja ya kwa kiwango cha hali ya juu,” alisema Harriet

Huduma za VODACARE zinapatikana kwa mteja kupiga 100/01 kwenda kituo cha huduma au kwa kutumia mitandao ya kijamii; WhatsApp, mawasiliano ya moja kwa moja au My Vodacom App, menu ya msaada binafsi na katika maduka yote ya Vodashops na kupitia dawati la huduma.

“Aliongezea kusema “Wiki hii Vodacom si kwamba inasherehekea nguvu ya huduma bora kwa wateja kama sehemu ya maudhui yake, ila tunasema kwamba ukiwa na Vodacom matumizi na upatikanaji wa msaada wa huduma kwa mteja ni rahisi wakati wote kupitia katika njia zetu zote za mawasiliano,” alimalizia kusema Harriet

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU PSSSF, BALOZI WA ANGOLA NCHINI JIJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Ndg. Hosea Kashimba alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Kwa ziara ya kikazi ya kusikiliza kero za Wabunge
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Ndg. Hosea Kashimba alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Kwa ziara ya kikazi ya kusikiliza kero za Wabunge
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akikabidhiwa kipeperushi na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Ndg. Hosea Kashimba alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Kwa ziara ya kikazi ya kusikiliza kero za Wabunge, Kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Ndg. Abdul Njaidi
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Mhe. Sandro De Oliveira alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Mhe. Sandro De Oliveira (katikati) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na ugeni kutoka Ubalozi wa Angola, ulioongozwa na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Mhe. Sandro De Oliveira (kushoto kwake), wageni wengine ni Wabunge wa Tanzania ambao ni Wawakilishi kwenye Jukwaa la Kibunge la SADC walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja wakati akikabidhiwa zawadi ya kitabu na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Mhe. Sandro De Oliveira (wa pili kulia), Wageni wengine ni Wabunge wa Tanzania ambao ni Wawakilishi kwenye Jukwaa la Kibunge la SADC walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AKAGUA UJENZI WA MAKAZI YA MAOFISA MAGEREZA UKONGA, APONGEZA HATUA KUBWA ILIYOFIKIWA

$
0
0
Moja ya majengo ya ghorofa yaliyojengwa kwa ajili ya makazi ya Maafisa na askari wa Magereza katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, jijini Dar es Salaam yakiwa tayari yamekamilika kama inavyoonekana katika picha (Picha na Jeshi la Magereza).
Ofisa wa SUMAJKT, Meja Ashrafu Hassan akitoa taarifa fupi kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike alipotembelea leo Novemba 13, 2019 kwa lengo la kukagua ujenzi huo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua ujenzi wa majengo mbalimbali ya makazi ya Maafisa na Askari wa Magereza katika eneo la Gereza Kuu Ukonga. Kulia kwake ni Ofisa wa SUMAJKT, Meja Ashrafu Hassan akimuonesha baadhi ya maeneo ambayo bado yanafanyia maboresho ya miundombinu.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua miundombinu ya mitaro ya kupitishia maji ya mvua katika ujenzi wa majengo mbalimbali za makazi ya Maafisa na Askari wa Magereza katika eneo la Gereza Kuu Ukonga.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akisalimiana na Maafisa wa SUMAJKT pamoja na Maafisa wa Jeshi la Magereza alipowasili katika eneo la ujenzi Gereza Kuu Ukonga leo Novemba 13, 2019 katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua ujenzi unaoendelea wa makazi ya Maafisa na askari wa Magereza katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, jijini Dar es Salaam.

MKUTANO WA TAASISI ZA FEDHA NCHINI KUFANYIKA ARUSHA NOVEMBA 21 & 22, 2019

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kushirikiana na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) imeandaa mkutano wa taasisi za fedha nchini utakaofanyika jijini Arusha kujadili namna ya kuchochea maendeleo ya sekta ya fedha nchini.

Mkutano huo wa 19 wa taasisi za fedha unatarajiwa kufunguliwa na kiongozi wa ngazi ya kitaifa. Utahudhuriwa na washiriki wapatao 300 wakiwemo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, mawaziri, wakuu wa taasisi za fedha, wachumi wabobezi, wanataaluma na washirika mbalimbali wa maendeleo.

Mada zingine zitakazotolewa na kujadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na, ‘Matumizi ya teknolojia katika kukuza sekta ya fedha ili kuleta mapinduzi ya viwanda’; ‘Maeneo yenye fursa za uwekezaji katika sekta ya fedha’ na ‘Vigezo vinavyochangia kujenga tabia za ukopaji’.

Pia, washiriki wa mkutano huo watajadili kuhusu ‘Jinsi ya kukinga vihatarishi katika sekta ya fedha’; ‘Namna ya kuoanisha sekta ya fedha na maendeleo ya viwanda’; na ‘Tathmini ya mchango wa sekta ya benki katika huduma jumuishi za kifedha nchini’.

Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikiandaa mikutano ya taasisi za fedha kila baada ya miaka miwili tangu miaka ya 1980. Katika mikutano hii, viongozi wakuu wa taasisi za fedha, yakiwemo mabenki, mashirika ya bima, mifuko ya hifadhi za jamii na taasisi zingine za fedha wamekuwa wakikutana na kujadili masuala mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya fedha na uchumi wa nchi kwa ujumla. 

Mkutano wa 18 wa taasisi za fedha ulifanyika mwaka 2016 jijini Arusha na mada kuu katika mkutano huo ilikuwa ni ‘Jinsi sekta ya fedha inavyoweza kuifanya Tanzania inufaike kiuchumi kutokana na uwepo wake kijiografia’ (Harnessing Tanzania’s Geographical Advantage: The role of financial sector).

RC SINGIDA DKT. REHEMA NCHIMBI AKAGUA SHAMBA LA KOROSHO MASIGATI MANYONI

$
0
0

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akionesha mabibo aliyoyaokota kwenye shamba la mfano la korosho lenye ukubwa wa ekari 12,000 lililopo Kijiji cha Masigati, wilayani Manyoni wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kukagua shamba hilo jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akiweka mabibo hayo kwenye mfuko akisaidiwa na Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Aderaide Rweikiza.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi na  Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Aderaide Rweikiza wakiokota  mabibo katika shamba hilo. 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akiokota mabibo kwenye shamba hilo.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi  amekagua shamba la mfano la korosho lenye ukubwa wa ekari 12,000 lililopo Kijiji cha Masigati, wilayani Manyoni na kueleza kuwa  linaendelea vizuri.

Akizunguza na waandishi wa habari jana wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya kukagua shamba hilo Dkt. Nchimbi alisema linaendelea vizuri na kuwa linaleta matumaini makubwa.

"Hivi sasa mabibo yameanza kuanguka na watu wanayaokota ni dalili nzuri ya maendeleo ya shamba letu na kazi inayoendelea katika shamba hili ni kufanya usafi tayari kwa msimu huu" alisema Nchimbi.

Dkt. Nchimbi aliongeza kuwa katika msimu huu wanatarajia kupanda ekari zote 12,000 kwani mbegu zipo tayari na zipo za kutosha.Akizungumza na wananchi na baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo waliokuwepo katika shamba hilo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Singida Oktoba 4, 2019, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimpongeza  Dkt. Nchimbi kwa kulibeba wazo la kuanzisha shamba hilo na kuhakikisha linatimia.

“Nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa kulibeba jambo hili, lakini nikuombe wewe na viongozi wenzako mhamasishe wengine walime zaidi zao hili kwa sababu korosho ni zao kubwa duniani na tena zao hili lina bei nzuri kimataifa,” alisema.

Alisema anatambua kwamba timu ya wataalamu kutoka kituo cha utafiti wa kilimo cha Naliendele, Mtwara imeshawasili Manyoni ili kufanya utafiti za zao hilo na jinsi linavyoweza kuzaa mara mbili kwa mwaka.

“Kwa kawaida, mkorosho mmoja hutoa kilo 40 za korosho kwa msimu mmoja, kwa hiyo kwa misimu miwili mtapata kilo 80. Ninawasii limeni korosho kwa ajili ya watoto wenu ambao wako darasa la pili au la tatu. Mkulima ukianza kuvuna, utaendelea kuvuna kwa miaka 20 mfululizo na kwa hiyo hao watoto hawatahitaji kulipiwa ada wakiwa chuo kikuu sababu korosho itakuwa inawalipia,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka wakulima wanaolima zao hilo wilayani Manyoni, waunde Ushirika wao ambao utawasaidia kuagiza dawa kwa pamoja ama kuuza kwa pamoja.Hivyo, alimwagiza Afisa Ushirika wa Wilaya hiyo,  Yusta Philipo ahakikishe anasimamia jambo hilo kuanzia sasa.
Akitoa taarifa juu ya mradi huo mbele ya Waziri Mkuu, Meneja wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Kanda ya Kati, Ray Mtangi alimweleza Waziri Mkuu kwamba mradi wa kilimo cha korosho unajumuisha mashamba makubwa mawili ambapo shamba la Misigati lina ukubwa wa ekari 7,000  na lile la Mikwese lenye ukubwa wa ekari 5,000.

Alisema watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kitaifa wamekuwa wakifika shambani hapo ili  wajifunze mbinu mpya za kuzalisha korosho kwenye maeneo yao. “Wiki mbili zilizopita, Mheshimiwa Spika na madiwani wa Kongwa walipita hapa ili kujifunza zao hili,” alisema.Pia alisema Halmashuri yao imetenga eneo la ujenzi wa viwanda na kwamba hadi sasa wanazo ekari 50 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kubangua korosho.

Mapema, Waziri Mkuu alikagua shamba hilo na kujionea hali halisi ya shambani ikoje. Pia alioneshwa mabibo na korosho ambazo zimevunwa kutoka kwenye shamba hilo la mfano, kutoka  kwenye mashamba ya wakulima ambao walipanda miche tangu januari mwaka jana.

Mawaziri wa mambo ya Nje, Mawaziri wa Ulinzi wa SADC wakutana kujadili hali ya amani DRC

$
0
0
Mawaziri wa Mambo ya nchi za Nje pamoja na Mawaziri wa Ulinzi na vyombo vya ulinzi  vya Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC) ijulikanao kama DOUBLE TROIKA wamekutana kwa dharura kujadili hali ya kisasa na amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kuweka mikakati ya kuendelea kuimarisha amani katika nchi hiyo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa dharura wa DOUBLE TROIKA inayojumuisha Troika ya siasa na Troika ya Ulinzi na Usalama, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi amesema kuwa lengo la mkutano huo wa dharura ni kuweka mikakati itakayosaidia kuimarisha amani nchini Congo DRC na kumaliza migogoro inayotishia ustawi wa nchi hiyo iliyodumu kwa miongo mingi.
  
Aidha, Waziri Kabudi amebainisha kuwa mkutano huo utasaidia nchi za SADC zenye vikosi vya ulinzi na usalama nchini DRC yaani Tanzania, malawai na Afrika Kusini kuimarisha amani na DRC kwa kufanya tathmini na kukubaliana hatua za kuchukua ili vita na migogoro ya mara kwa mara inayoibuka Nchini Congo DRC ifikie tamati na amani ya kudumu ipatikane.

“Mkutano huu wa leo ni wa Troika ya Siasa na Troika ya ulinzi na usalama ambapo kupitia mkutano huu tunaamini kuwa tutafanya tathimini ya hali ya amani DRC na kukubaliana ni hatua gani za kuchukua,” amesema Prof. Kabudi

Katika hatua nyingine Prof. kabudi ameongeza kuwa ndani ya mwaka huu amani na demokrasia vimezidi kuimarika katika nchi wanachama wa SADC, kutokana na baadhi ya nchi wanachama kuendesha chaguzi za kidemokrasia zilizomalizika kwa amani katika nchi za Msumbiji na Botswana. 

Aidha Prof. Kabudi amesema Tanzania na Nchi 16 wanachama wa SADC bado zinaendelea kupaza sauti kwa jumuiya za kimataifa na nchi ambazo zimeiwekea vikwazo Zimbabwe kuviondoa mara moja kutokana na vikwazo hivyo kutokuwa na uhalali jambo linalosababisha mateso kwa raia wan chi hiyo hususani akina mama na watoto .

"Katika hili la Zimbabwe lazima sisi kama SADC tushikamane na kusafiri pamoja ili tufike kwa umoja wetu" Amesema Prof. kabudi.

Awali akitoa hutuba katika mkutano huo, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADC), Stegomena Taxi amesema kuwa ana matumaini makubwa na mkutano huo unaofanyika jijini Dar es salaam utatathimini na kutoa mapendekezo ya muda mfupi na mrefu kuhusu hali ya usalama, amani na siasa katika nchi ya Congo DRC  na ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ili kuhakikisha ukanda huo unakuwa salama na amani

Ameongeza kuwa amani na usalama ni nyenzo mojawapo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na hivyo kupata maendeleo yanayohitajika kwa ajili ya mataifa ya Afrika.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi akifungua mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje pamoja na Mawaziri wa Ulinzi na vyombo vya ulinzi na usalama vya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi akihutubia mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya nchi za Nje pamoja na Mawaziri wa Ulinzi wa vyombo vya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa SADC, Stegomena Taxi paamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe.

 Katibu Mtendaji wa SADC, Stegomena Taxi akihutubia mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya nchi za Nje pamoja na Mawaziri wa Ulinzi wa vyombo vya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Dar es Salaam 
 Baadhi ya mawaziri pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa vyombo vya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mkutano wa Troika 
Baadhi ya mawaziri pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa vyombo vya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mkutano wa Troika

MATUKIO YA MHESHIMIWA WAZIRI MKUU BUNGENI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiakisalimiana na Mbunge wa Mbunge wa Manyoni Magharibi, Yahaya Masare, kwenye Jengo la Utawala Bungeni jijini Dodoma, Novemba 13, 2019. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani kikwete. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa,Bungeni jijini Dodoma, Novemba 13, 2019
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Arusha, Joyce Mukya, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 13, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na Mbunge wa Ndada, Sesil Mwambe (chini kushoto) na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 13, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Edalardus Kilangi, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 13, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama(chini kushoto) akijadili jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angellah Kairuki (juu kushoto) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa(kulia),Bungeni jijini Dodoma, Novemba 13, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Novemba 13, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiakisalimiana na Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Novemba 13, 2019. Katikati ni Mbunge wa Viti Maalum, Hamida Abdallah.

BENKI YA BIASHARA NA MAENDELEO MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA KUSAIDIA UTEKELEZAJI MIRADI YA KIMKAKATI YA TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akijadiliana mambo mbalimbali na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) walipokutana katika Mji wa Sandton, Johannersburg, Afrika Kusini, Kando ya Kongamano kubwa la Pili la Jukwaa la Uwekezaji lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ambapo Benki hiyo imeahidi kuipatia mikopo zaidi Tanzania.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akijadiliana mambo mbalimbali na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) walipokutana katika Mji wa Sandton, Johannesburg, Afrika Kusini, Kando ya Kongamano kubwa la Pili la Jukwaa la Uwekezaji lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ambapo Benki hiyo imeahidi kuipatia mikopo zaidi Tanzania.
Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) akimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), walipokutana na kufanya mazungumzo katika Mji wa Sandton, Johannersburg, Afrika Kusini, Kando ya Kongamano kubwa la Pili la Jukwaa la Uwekezaji lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ambapo Benki hiyo imeahidi kuipatia mikopo zaidi Tanzania.(Picha na Wizara ya Fedha na Mipango-Johannesburg)





Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akisalimiana na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) walipokutana na kufanya mazungumzo katika Mji wa Sandton, Johannesburg, Afrika Kusini, Kando ya Kongamano kubwa la Pili la Jukwaa la Uwekezaji lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akiagana na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Mji wa Sandton, Johannesburg, Afrika Kusini, Kando ya Kongamano kubwa la Pili la Jukwaa la Uwekezaji lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ambapo Benki hiyo imeahidi kuipatia mikopo nafuu zaidi Tanzania kuanzia mwakani
…………………….

Na Benny Mwaipaja, Johannesburg

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini wa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse, ambapo Benki hiyo imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 200 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mazungumzo ya viongozi hao yamefanyika katika Mji wa Sandton, Johannesburg nchini Afrika Kusini, kando ya Kongamano la Pili la Jukwaa la Uwekezaji Afrika lililoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB.

Dkt Mpango amesema kuwa Benki hiyo imekuwa mbia mzuri wa Tanzania ambapo mwaka huu pekee imetoa mkopo wa dola bilioni 1 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na imeahidi kutoa kiasi kingine cha dola milioni 200 baada ya Bodi ya Benki hiyo kukutana mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu kwa ajili kuidhinisha mkopo huo

Alisema kuwa amemwalika Rais huyo wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Bw. Tadesse, kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania hivi karibuni ili kujionea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme wa Kilwa pamoja na miradi mingine ambayo Benki hiyo inaweza kutoa mkopo

Kwa upande wake, Rais wa TDB Bw. Admassu Tadesse amesifu uhusiano imara uliopo kati ya Benki yake na Serikali ya Tanzania na kuahidi kuwa Benki hiyo itahakikisha inashirikiana nayo kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya wananchi wake.

“Tumekuwa na mjadala mzuri na Mhesimiwa Dkt. Mpango na Benki yetu imekuwa mshirika mzuri wa maendeleo ya Tanzania katika kipindi cha miaka michache iliyopita kwenye yyanja za nishati ya umeme na miundombinu ya usafirishaji” alisema Bw. Tadesse

Alisema kuwa mwaka huu Benki yake kwa kushirikiana na washirika wake wengine ambao ni taasisi za kibenki imeongeza mtaji wa dola milioni 500 hatua iliyoijengea Benki yake uwezo wa kutoa mikopo zaidi ambapo mwakani itaipatia mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya kimkakati ya miundombinu itakayokuwa na umuhimu mkubwa si tu kwa Tanzania, bali pia kikanda.

Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) ilianzishwa mwaka 1985 ikiwa na mali zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5.6 ambapo lengo lake kubwa ni kutoa mikopo inayochochea miradi inayochochea ukuaji wa biashara, ikiwemo miundombinu, utangamano wa kiuchumi na ushauri wa kibiashara kwa nchi wanachama.

Mikoa ya pembezoni ya Kigoma, Arusha na Kilimanjaro kinara wa uingizaji wa dawa bandia

$
0
0

NA ANDREW  CHALE,

MIKOA ya pembezoni mwa Nchi ikiwemo ya Kanda ya Magharibi, Kanda ya Ziwa na ile ya Kaskazini imeripotiwa kuwa  kinara wa dawa duni za binadamu na mifugo, vifaa tiba na vitendanishi ambavyo havikusajiliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA).

Akitangaza matokeo ya operesheni maalum  ya dawa, vifaa tiba, vitendanishi, dawa asili na tiba mbadala, mbele ya waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar e Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Akida Khea   alisema katika zoezi hilo Wilaya zaidi ya 33 katika mikoa 20 wameweza kukamata dawa bandia aina saba zenye thamani ya fedha za kitanzania Tsh. 12,495,500.

Dawa hizo bandia ni pamoja na  Sonaderm Cream toleo namba A1912 na A1758, Gentrisome cream (namba GNTRO X030), Sulphadoxine Pyrimethamine (ilikuwa na namba ya kughushi TAN)

Pia dawa zingine ni  ALPRIM (Sulfamethoxazole 400mg + Trimethoprim 80mg tablets (namba  6L74) ambapo kiwanda cha Elys Pharmaceutical cha nchini Kenya kinachozalisha dawa yenye jina kama hilo kimethibitisha kuwa dawa hizo ni bandia.

Bw. Khea alizitaja dawa zingine kuwa ni pamoja na Homidium Chloride,  Cold cap ambapo dawa halisi yake ilitambuliwa  kama COLDCAP, na dawa nyingine bandia ni dawa ya mifugo aina ya TEMEVAC NDV strain 1&2  ambayo ni chanjo ya kuku  kwa ajili ya ugonjwa wa mdondo.

“katika dawa hizo, uchunguzi wetu baada ya kuzibaini tuliweza kuwasiliana nawamiliki wa dawa husika ambapo waliweza kututhibitishia kuwa ni bandia na zingine zimegushiwa maandishi” alisema Khea.

 “Tumebaini mikoa  iliyo pembezoni ikiwemo Kigoma kubainika kuwa na dawa nyingi bandia pamoja na Mwanza. Lakini pia mikoa ya Kaskazini ikiwemo Arusha na Kilimanjaro nayo imebainika kuwa na wingi wa dawa hizo” alisema  Kaimu Mkurugenzi huyo wa TMDA, Akida Khea. 

 Katika tukio hilo TMDA waliwashirikisha mamlaka mbalimbali wakiwemo Jeshi la Polisi, Msajili wa Baraza la dawa asili na tiba mbadala pamoja na TAMISEMI.

Nae Mrakibu wa jeshi la Polisi kutoka Makao makuu ya upelelezi kitengo cha Interpool,  Alekunda Urio  amesema jeshi hilo linafuatilia kwa karibu na wahusika wote ambao wamebainika katika kuingiza ama kusambaza watachukuliwa hatua.

"Wajibu wa jeshi la Polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao. Usalama wa raia ni pamoja na afya za wananchi sisi kama jeshi la polisi kwa pamoja tunahakikisha usalama wa raia unalindwa na wahusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria uchunguzi ukikamilika" alisema Bi Alekunda Urio.

 Aina saba ya dawa duni na bandia zilizokamatwa katika ukaguzi maalum wa dawa ulioendeshwa na TMDA.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), Akida Khea akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mapema wakati wa kutangaza matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa  vifaa tiba, vitendanishi, dawa asili na tiba mbadala, tukio lililofanyika makao makuu ya TMDA, Mabibo Jijini Dar e Salaam.
 Mrakibu wa Polisi kutoka makao makuu ya upelelezi Kitengo cha Interpoool, Alekunda Urio akizungumza katika tukio hilo. 
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), Akida Khea akionesha moja ya dawa zilizokanatwa katika tukio hilo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema wakati wa kutangaza matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa  vifaa tiba, vitendanishi, dawa asili na tiba mbadala, tukio lililofanyika makao makuu ya TMDA, Mabibo Jijini Dar e Salaam.

IFM yaanzisha bonanza la michezo kabla ya mahafali ya kila mwaka

$
0
0
Na Chalila Kibuda,MIchuzi TV

CHUO cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeanzisha bonaza la michezo a bonanza kwa ajili ya wanafunzi na Wahadhiri pamoja na wafanyakazi i katika kuelekea mahafali ya Chuo hicho yatakayofanyika Novemba 29 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Michezo kwa wanafunzi na wakufunzi wa chuo kuanzia sasa kufanyika kabla ya kongamano la kitaaluma kabla ya mahafali ikiwa ni maalumu katika kujenga umoja baina ya wanajumuiya wa chuo hicho.

Akizungumza wakati wa kufungua bonanza hilo Mkuu wa hicho Profesa Tadeo Satta, amesema pamoja na malengo mengine bonanza hilo limelenga kuimarisha afya za wanafunzi na wahadhiri na wafanyakazi wa chuoni hapo na hivyo kuimarisha afya pamoja na kufanya kitu tofauti kwa kujumuika pamoja.

Amesema bonanza hilo mahususi kwa ajili ya kukaribisha kongamano la kila mwaka la Chuo hicho siku chache kabla ya kufanyika kwa mahafali, lilianzishwa rasmi mwaka 2011 na baadae kusitishwa kutokana na sababu mbalimbali hadi hapo jana lilipozinduliwa rasmi kwa wanafunzi na wakufunzi hao kushiriki katika michezo na kila mmoja kuonyesha kipaji chake.

“Kuanzia sasa huu ndiyo utaratibu utakaoweza kutuleta wanamichezo wote pamoja, imani yangu mtaweza kushiriki vyema wakati wote ili kujenga afya zenu, malengo kadri miaka inavyokuja tutazidi kuliboresha bonanza hili” alisema Profesa Satta.
 Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa bonanza la michezo la chuo hicho ililofanyika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

 Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta akizungumza na wanamichezo wa chuo wakati akifungua bonanza la michezo wa chuo lililofanyika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dkt. Imanuel Mnzava akitoa maelezo kuhusiana na maandalizi ya bonanza hilo na mikakati waliojiwekea katika uboreshaji wa michezo mbalimbali katika chuo hicho, Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. 
 Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta akikagua timu ambazo zinashiriki bananza la michezo la chuo hicho lililofanyika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi, wahadhili na wanafanyakazi wa chuo hico wakiwa katika bonanza.Kibuda,MIchuzi TV


LESENI NA HUDUMA ZOTE ZA BRELA KUTOLEWA KWA NJIA YA MTANDAO

$
0
0

Na Robertha Makinda, BRELA 

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Emmanuel Kakwezi amesema kwamba, moja kati ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ni utoaji wa huduma zake zote kwa njia ya mtandao.

Bw. Kakwezi ameyasema hayo akiwa katika mkutano na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam ulioandaliwa na Idara ya Habari Maelezo.
Ameeleza kwamba Wananchi wanaweza kuwasilisha maombi ya huduma zote zinazotolewa na BRELA popote pale walipo nchini kwa Mfumo wa Usaili kwa njia ya mtandao, (Online Registration System / ORS).

Hivi sasa maombi yote ya Usajili yanatumwa kwa njia ya Mtandao,  iwe ni Usajili wa Kampuni, Usajili wa Jina la  Biashara, usajili wa Alama ya Biashara au Huduma, utoaji wa Leseni za Viwanda, utoaji wa Leseni za Biashara kundi A na utoaji wa Hataza amesema Bw. Kakwezi.

Bw. Kakwezi ameongeza kwamba Mabadiliko haya yanaambatana na faida nyingi, ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa kufanya usajili, mathalani usajili wa Kampuni hivi sasa unaweza kukamilika ndani ya siku moja. Mfumo huu uwasaidia watumiaji kutuma maombi yao popote pale walipo nchini nan je ya nchi vilevile. 

Zaidi ya hilo mfumo huu unamsaidia mtumiaji kufuatilia maendeleo ya maombi yake na kupata mrejesho kwa ajili ya kufanya marekebisho pale maombi yanapoonekana kuwa na kasoro.

Aidha katika kipindi cha miaka minne, BRELA pia imefanikisha uanzishwaji wa Shahada ya Uzamivu ya Miliki Ubunifu kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Shirika la Miliki Ubunifu la Kanda (ARIPO) na Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO).

Mpango huu una lengo la kuongeza elimu kwa Umma na wataalam katika eneo la Miliki Ubunifu. Shahada hiyo ya Uzamivu imeanza kutolewa mwezi Agosti 2019.

BRELA kwa kushirikiana na COSTECH pamoja na Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) imetekeleza mradi wa Upatikanaji wa taarifa za teknolojia zilizopo kwenye kanzidata za Hataza (TISCs) kwa ajili ya kutumiwa na watafiti na watumiaji wengine ambapo jumla ya Hataza milioni sabini na sita (76,000,000) zinaweza kupatikana kwenye kanzidata husika.

Katika kipindi cha Miaka minne, BRELA imefanikisha kuanzisha Utoaji wa Leseni za Biashara kundi A na kundi B kwa njia ya mtandao. Mfumo huu umeunganishwa na Mifumo ya Malipo ya Serikali yani Government Electronic Payment Gateway (GEPG) na Mfumo wa Taarifa za Makusanyo ya Mapato wa Mamlaka za Serikali za mitaa yaani Local Government Revenue Collection Information System (LGRCIS).

Majaribio ya Mfumo huu yalianza tarehe 1 Oktoba 2019 na mpaka sasa Leseni za Biashara Kundi A zinazotolewa na BRELA na Leseni za Biashara kundi B katika Manispaa za Bukoba, Chalinze, Wilaya ya Karagwe,Mji wa Mafinga, Manispaa za Ilala na Halmashauri za Jiji la Mwanza zinatolewa kwa njia ya Mtandao.

Katika utoaji wa Leseni kwa mfumo huu takwimu zinaonesha jumla ya Leseni za Biashara 1206 zimetolewa kupitia mfumo huo ambapo kati ya hizo BRELA imetoa Leseni 470, Jiji la Mwanza Leseni 199 na Manispaa ya Ilala Leseni 537.

Bw. Kakwezi ameeleza zaidi kwamba ndani ya miaka minne BRELA imefanikiwa kuanzisha dirisha la Mfumo wa utoaji wa taarifa za Kibiashara za Kimataifa. Dirisha hili linamuwezesha mtuamiaji au mwombaji kufahamu taarifa mbalimbali za upatikanaji wa Leseni na vibali kwa bidhaa zinazouzwa nje na zinazoingizwa ndani ya nchi.

Dirisha hili linatoa fursa kwa mwombaji kutembelea tovuti ya www.trade.business.go.tz na kupata taarifa zote za Biashara zinazohusiana na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi (Export) na uaigizaji ndani ya nchi (Import).

Vilevile mtumiaji atafahamu Sheria, Kanuni, taratibu muda utakaotumika pamoja na gharama za kila aina ya huduma (Administrative procedures) atakayohitaji na wapi apite ili kufanikisha upatiakanaji wa huduma anayohitaji.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ilianzishwa chini ya sheria ya wakala wa serikali namba 30 ya Mwaka 1997 na hatimae kuzinduliwa rasmi tarehe 3 mwezi Disemba 1999. 

BRELA ipo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara na ilianzishwa kwa ajili ya kuratibu shughuli za biashara na kudhibiti sheria pamoja na utoaji wa huduma za Usajili wa Kampuni, usajili wa majina ya biashara, usajili wa alama za biashara na huduma, utoaji wa leseni za viwanda, utoaji wa leseni za biashara kundi, utoaji wa Hataza na Miliki bunifu.
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw.Emmanuel Kakwezi (mbele) akizungumza na waandishi wa Habari leo katika Mkutano wa BRELA na vyombo mbalimbali vya Habari kuzungumzia mafanikio ya BRELA ndani ya Miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano. Mkutano huo umeandaliwa na Idara ya Habari maelezo na umefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo uliofanyika leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),Jijini Dar es Salaam.


STAILI YA TRA YA KUTOA ELIMU YA MLIPA KODI “DUKA KEA DUKA” YAMKOSHA DC WA RUFIJI JUMA NJWAYO

$
0
0
Afisa wa TRA akimuelimisha mfanyabiashara huhu (kulia) katika stendi ya mabasi Ikwiriri, Wilayani Rufiji Mkoani Pwani leo Novemba 13, 2019 kuhusu elimu ya kodi katika maduka yao mtindo unaotumiwa na TRA kutoa elimu ya kodi unajulikana kama "Duka kwa Duka"


Na Mwandishi wetu, Rufiji

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani Juma Njwayo amepongeza juhudi zinazofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) za kutoa elimu ya Kodi kwa kuwafuata wafanyabiashara katika maeneo yao "duka kwa duka".

Mkuu huyo wa Wilaya amebainisha kuwa aina hii ya utoaji elimu ya kodi kwa kuwafuata wafanyabiashara utaongeza ari ya ulipaji kodi miongoni mwa wafanyabiasha na walipakodi wengine siyo tu katika Wilaya ya Rufiji bali hata kwa watanzania wote.

"Niwapongeze sana TRA kwa kuamua kufanya wiki ya elimu na huduma kwa walipakodi katika Wilaya yetu, naamini wana Rufiji tutafaidika na elimu hii na mapato yataongezeka", amesema DC Njwayo.

Aidha, Mkuu wa Wilaya amewataka wafanyabiasha na wananchi wa Wilaya ya Rufiji kutumia fursa hii kufahamu mambo yanayohusu ulipaji kodi ili walipe kodi kwa hiari na kwa wakati na kuiwezesha serikali kutekeleza miradi mikubwa yenye tija kwa Taifa.

"Sote tunashuhudia jinsi Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli anavyotekeleza miradi mikubwa kama huu wa kufua umeme wa Nyerere Hydro power tena upo wilayani kwetu, kwa hiyo tutumie fursa ya elimu ya kodi na kila mmoja aone ana wajibu wa kulipa Kodi kwa hiari ili tupate maendeleo zaidi", amesisitiza Mkuu wa Wilaya Njwayo.

DC Njwayo ameongeza kuwa Kodi zinazokusanywa na TRA ndizo zinazoleta maendeleo ukiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kitaifa kwa kutumia Kodi mradi wa umeme ambao utainua wilaya kiuchumi na kijamii pamoja na kuinua hali za wananchi.

Ameongeza kuwa ni vyema wananchi kushirikiana na TRA katika kuhakikisha kuwa elimu watakayoipata wanaifanyia kazi na kuchangia maendeleo ya taifa letu.

Naye Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi kutoka TRA Honesta Ndunguru ameushukuru uongozi wa Wilaya ya Rufiji kwa ushirikiano waliouonesha na kuwa TRA itahakikisha inafika katika sehemu zote muhimu zenye wafanyabiasha na kuwasajili kuwa walipakodi na kuwapatia cheti Cha utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

"Tutatoa TIN kwa kila anayestahili kupata kwa ajili kufanya biashara au kupata huduma zingine kama vile leseni ya udereva", amesema Ndunguru.

TRA inafanya wiki ya huduma, elimu na usajili wa walipakodi katika mikoa ya Morogoro na Pwani kuanzia tarehe 11 hadi 16 ili kuongeza uelewa wa masuala ya ulipaji kodi miongoni mwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani, Mhe. Juma Njwayo (mwenye fulana nyeupe) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliofika ofisini kwake kutoa taarifa ya wiki ya huduma, elimu na usajili wa walipakodi inayoendelea katika wilaya hiyo iliyopo Mkoa wa Pwani
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mhe. Juma Njwayo (kushoto) akiagana na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania waliofika ofisini kwake kutoa taarifa ya wiki ya huduma, elimu na usajili wa walipakodi inayoendelea katika wilaya hiyo.

Watoa huduma waaswa kujiepusha na Rushwa

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu na Utawala Bi. Njoikiki
Mapunda wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi kwa wataalam tarajali 80 ambapo amewataka kufanyia kazi yote waliyofundishwa ili kuwa watumishi bora.
Muuguzi kutoka Hospitali ya Mloganzila, Bw. Mosama John akiwaelekeza
wataalam namna ya kuwahudumia wateja wanaokuja hospitalini hapa.
Mtaalam elekezi wa masuala ya Ukimwi kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti
Ukimwi (TACAIDS), Bw. Patrick Kanyamwege akiwaelimisha wataalam tarajali kuhusu maambukizi ya Ukimwi na jinsi ya kujikinga.
Waaalam Tarajali wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa katika
mafunzo elekezi katika Hospitali ya MNH-Mloganzila.
Afisa Mwandamizi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) Bi. Heavenlight Majule akiwasilisha mada kuhusu udhibiti wa
rushwa mahala pa kazi.

****************************

Watoa huduma wa afya wameaswa kuzingatia uadilifu na uaminifu mahala pa kazi kwa kutokuomba wala kupokea rushwa wakati wa kutoa huduma.

Hayo yamezungumzwa na Afisa Mwandamizi kutoka Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa kufunga mafunzo elekezi kwa wataalam tarajali 80 walioko kwenye mafunzo ya mwaka mmoja katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa njia ya vitendo yanayolenga kuwawezesha kutoa huduma bora za afya kwa jamii.

“Kupokea zawadi au pesa kabla na baada ya kutoa huduma ni kosa kisheria na pindi utakapogundulika umefanya hivyo basi utachukuliwa hatua kulingana na vifungu 24 vya makosa ya rushwa vilivyoainishwa katika sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kuzuia na kupambana na rushwa,” Amesema Bi. Majule.

Amesisitiza kila mmoja ana wajibu wakushiriki katika mapambano dhidi ya
rushwa kwa kutoa huduma bora za afya bila malipo yoyote kwani rushwa
humnyima haki anayepatiwa huduma na kupunguza ufanisi katika kazi.

Kwa upande wake Muuguzi katika Hospitali ya Mloganzila, Bw. Mosama John ametoa wito kwa wataalam hao kuwa na kauli nzuri wakati wa kuwahudumia  wateja wanaokuja hospitalini hapa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Mada ziliwasilishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na elimu elekezi juu ya
udhibiti wa rushwa mahala pa kazi, elimu ya maambukizi ya ukimwi na jinsi ya kujikinga, kanuni za maadili ya utendaji kwa watumishi wa Umma, matumizi bora ya vifaa tiba na dawa, huduma za kliniki, mahusiano kwa Umma na huduma kwa wateja.

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAJIDHATITI KUSIMAMIA HAKI NCHINI – PROF. MCHOME

$
0
0
Mtaalam wa ulinzi na usalama wa mtoto kutoka UNICEF Bi. Victoria Mgonela akiongea na washiriki wa mkutano wa Jukwaa la Haki Mtoto.
Washiriki wa Mkutano wa Jukwaa la Haki Mtoto wakisikiliza mada kutoka kwa mwezeshaji
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa Mkutano wa Jukwaa la Haki Mtoto.
Mkurugenzi wa Katiba na Ufuatiliaji Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina akifungua mkutano wa siku mbili wa Jukwaa la Haki Mtoto unaopitia na kuboresha rasimu ya mkakati wa pili wa miaka mitano wa Haki mtoto unaoendelea Jijini Dodoma.

***************************

“Wizara ya Katiba na Sheria imejidhatiti katika kuhakikisha masuala ya Hakiyanasimamiwa kwa umakini ili kila mmoja wetu aweze kufurahia uhuru, amani na utulivu pasipo kuvunja sheria za nchi.”

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Bw. Patience Ntwina wakati akifungua mkutano wa Jukwaa la Haki Mtoto kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria. Mkutano huo wa siku mbili unaoendelea Jijini Dodoma umekutanisha wadau mbalimbali ukiwa na lengo la kupitia na kuboresha rasimu ya Mkakati wa Pili wa Miaka Mitano wa Haki Mtoto.

Bw. Ntwina alisema Katika kutimiza hayo, Wizara ya Katiba na Sheria imekuwaikisimamia mifumo ya haki na kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati na bilaupendeleo wala uonevu wa aina yoyote.

Alisema “ mifumo ya haki inawaangalia watu wote bila kujali hali ya mtu. Na hii ndio ilipelekea Wizara ya Katiba na Sheria kuja na mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya Msaada wa Kisheria na sheria zingine kama Sheria ya kuwalinda watoa taarifa na sheria ya upashaji wa habari. Hii yote ni kuhakikisha Haki inapatikana kwa wakati na kwa watu wote”.

Aliongeza, masuala ya watoto ni mtambuka katika Wizara na sekta mbalimbali na hivyo utekelezaji wake unahitaji mpango mkakati mahususi ili kuwezesha kila mdau kutekeleza majukumu yake katika maeneo yaliyobainishwa ili kupata ufanisi na tija katika kumhudumia mtoto.

Mpango Mkakati wa Pili wa Haki Mtoto unategemea kuangalia kwa kina na kukidhi matakwa yaliyopo kwenye mazingira ya sasa na kukamilisha yale ambayo hayakutekelezwa kwenye mkakati wa kwanza ambao uliisha mwaka 2017.

Aidha alitoa shukrani kwa washirika wa maendeleo ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuendesha Mpango Mkakati wa Haki za Watoto na shughuli za Jukwaa la Haki Mtoto.

AG KILANGI ATETA NA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

$
0
0
 Sehemu ya Ujumbe wa  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakiwamo Makamisha  wakati walipomtembelea ( Courtesy Call) Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi (AG) akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mhe. Methew Mwaimu  wakati  yeye na Makamisha wanaounda Tume hiyo walipomtembelea Mwanasheria  Mkuu wa Serikali na kufanya naye mazungumzo.
Sehemu ya Ujumbe wa  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakiwamo Makamisha  wakati walipomtembelea ( Courtesy Call) Mwanasheria Mkuu wa Serikali.


DODOMA , Nov 13,2019 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi ( AG)leo ( jumatano) amekutana na kisha kuwa na mazungumzo na Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. 

Mazungumzo baina ya AG na Tume hiyo ambayo iliongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Mhe. Methew Mwaimu yamefanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyopo katika Mji wa Kiserikali Mtumba Jijini Dodoma. 

Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe. Jaji Mstaafu Methew Mwaimu alimueleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwamba, Madhumuni ya ziara hiyo pamoja na masuala mengine, yalikuwa ni kujitambulisha kwake lakini pia kujadiliana na kubadilishana mawazo ya namna Ofisi hizo mbili zinaweza kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao. 

Kwa upande wake Profesa Kilangi, aliishukuru Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora wa kuona umuhimu wa kumtembelea na kubadilishana naye mawazo ikiwa ni muda mfupi tangu kuteuliwa kwao na kuapishwa kwao. 

AG ameihahidi tume hiyo ushirikiano madhubuti kutoka katika Ofisi yake. 
Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu na Huduma za Kisheria, Dkt. Gift Kweka. 

Itakumbukwa kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Jaji Mstaafu Methew Mwaimu na Makamisha wake waliteuliwa Mwezi Septemba mwaka huu na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

WATATU MBARONI KWA TUHUMA ZA WIZI WA KOMPYUTA

$
0
0
NA FARIDA SAIDY MOROGORO 

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Morogoro Linawashikilia Watuhumiwa Watatu Kwa Kosa La Kuvunja Moja Ya Ofisi Za Shule ya msingi msamvu B iliyoko kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro Majira Ya Usiku Na Kuiba Computer 23. 

Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Mororgoro Willibroard Mutafungwa Amesema Tukio Hilo Limetokea Manamo Tar 11 Mwezi Novemba Mwaka Huu Katika Shule Hiyo ndani ya Chumba Kilicho Na Computer Hizo Kisha Kuzibeba Kwenye Viroba Na Kuzipakia Kwenye Gari Isiyofahamika Na Kutoweka Nazo Kusiko Julikana. 

Kamanda Mutafungwa Amesema Watuhumiwa Wote Watatu Wamehojiwa Na Kukiri Kutenda Kosa Hilo Na Uchunguzi Zaidi Unaendelea Kuwabaini Watuhumiwa Wote Walioshirikiana Nao Akiwemo Mlinzi Wa Shule Hiyo Ambaye Amekimbia Baada Ya Tukio Hilo. 

Kwa Upande Wa Mwalimu Mkuu Wa Shule Hiyo Bwa Elidalimetusi Selemani Likomba Amelishukuru Jeshi La Polisi Kwa Jitihada Walizofanya Mpaka Kufanikiwa Kuzipata Computer Hizo huku Mwanafunzi Wa shule hiyo Bi Mwajuma Ramadhani amesema amesikitishwa Na kitendo cha kuiibiwa kwa Kompyuter Hizo, kwani zilikuwa zinawasaidia katika masoma yao. 

Katika Hatua Nyingine Jeshi La Polisi Kwa Kushirikiana Na Askari Wanyamapori Wamefanikiwa Kumkamata Mtu Mmoja Akiwa Na Pembe Ya Ndovu Yenye Urefu Wa Sentimeter 90 Na Uzito Wa Kilogram 3.85 Aliyokuwa Ameliweka Kwenye Mfuko Na Kusafirisha Kwa Kutumia Pikipiki Aina Ya Haojue Yenye No.818btu Rangi Nyeusi .

WIZARA YA KILIMO YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA WANAJESHI WASTAAFU KUIMARISHA SEKTA YA KILIMO

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi ya mkutano wa semina ya mafunzo kwa muungano wa wanajeshi wastaafu Tanzania (MUWAWATA) uliofanyika tarehe 13 na 14 Novemba 2019 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi Jijini Dodoma (Dodoma Convention Center) tarehe 13 Novemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza mipango ya wizara ya kilimo katika kuimarisha sekta ya kilimo nchini wakati wa ufunguzi ya mkutano wa semina ya mafunzo kwa muungano wa wanajeshi wastaafu Tanzania (MUWAWATA) uliofanyika tarehe 13 na 14 Novemba 2019 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi Jijini Dodoma (Dodoma Convention Center) tarehe 13 Novemba 2019. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa sera na Mipango wa Wizara ya Kilimo Ndg Obey Assery (Kulia) na Mwenyekiti wa muungano wa wanajeshi wastaafu Tanzania (MUWAWATA) Ndg Assedy Mayuggi (Kushoto).
Sehemu ya wanajeshi wastaafu Tanzania (MUWAWATA) wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi ya mkutano wa semina ya mafunzo kwa muungano wa wanajeshi wastaafu Tanzania (MUWAWATA) uliofanyika tarehe 13 na 14 Novemba 2019 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi Jijini Dodoma (Dodoma Convention Center) tarehe 13 Novemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi ya mkutano wa semina ya mafunzo kwa muungano wa wanajeshi wastaafu Tanzania (MUWAWATA) uliofanyika tarehe 13 na 14 Novemba 2019 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi Jijini Dodoma (Dodoma Convention Center) tarehe 13 Novemba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo_Dodoma
Serikali imewahakikishia Wanajeshi wastaafu kupitia muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania (MUWAWATA) kuwa imekusudia kuwashirikisha kwa karibu katika sekta ya kilimo kwani shughuli za kilimo zitaimarisha usalama wa chakula kwa kaya zao na Taifa kwa ujumla.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 13 Novemba 2019 wakati wa ufunguzi ya mkutano wa semina ya mafunzo kwa muungano wa wanajeshi wastaafu Tanzania (MUWAWATA) uliofanyika tarehe 13 na 14 Novemba 2019 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi Jijini Dodoma (Dodoma Convention Center).
Aliongeza kuwa shughuli hizo zitaongeza kipato na kuboresha maisha ya wanajeshi hao kwa ujumla; Kuimarisha afya zao kwa kupunguza utegemezi wa ndugu, jamaa na marafiki kwa ajili ya kujikimu na maisha baada ya kustaafu.
Alisema kuwa Wizara ya Kilimo ipo tayari katika lengo la kufanya shughuli za kilimo kwa kutoa ushauri wa kitaalamu ikiwa ni pamoja na; kuwahakikishia upatikanaji wa mbegu bora, mbolea, zana za kisasa za kilimo na viuatilifu.
Mhe Hasunga amesema kwa kupitia Taasisi za Serikali na Mamlaka zilizopo, Wizara imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa pembejeo kwa ujumla kwani ndio muhimili mkubwa katika sekta ya kilimo.
Kadhalika, amewahimiza wanajeshi hao na wakulima wote nchini kuzingatia matumizi bora ya pembejeo na kufuata ushauri wa kitaalamu; kwa kufanya hivyo ni Dhahiri kuwawataongeza tija na faida katika uzalishaji wa mazao ya kilimo.
Mhe Hasunga amesema kuwa sekta yakilimoinachangia takribani asilimia 28.7yaPatolaTaifa, asilimia 65.5yaajira, asilimia 65yamalighafi yaviwandana asilimia 30yamapatoyanje.ProgramuyaKuendelezaSekta yaKilimo AwamuyaPili(ASDPII)inatambua umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau mbalimbali ili kuwezesha sekta na kilimo kuchangia kwa ufanisi katika ukuaji wauchumiwa nchina kuwezeshautekelezajiwavipaumbelevya Taifa kwa ujumla.
Jitihada za Serikali zinalenga kuondoavikwazona changamotoza ukuajiwa sektanakuimarishaMapatoya Kilimo,kuboreshaukuaji wa mapatoyawakulimawadogo,kujitoshelezakwa chakula, uongezaji thamani ya mazao, ajira na hatimaye kufikia Nchi ya kipato cha katiifikapo mwaka 2025.
Waziri Hasunga amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni;  Kuwashirikisha wadau fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya kilimo ili kuongeza mchango wa sekta ya kilimo katika Pato la Taifa ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha ya wakulima wadogo.
Amesema kuwa katika mkutano huo MUWAWATA wanapaswa kufanya wasilisho la shughuli za kilimo wanazozifanya na zile wanazotarajia kufanya kubainisha changamoto walizonazo na mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto hizo.
Alisema kuwa matarajio ya mkutano huo ni pamoja na Kuongeza ufahamu (awareness creation) wa fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya kilimo, kupata fursa ya kuunganishwa na Wadau mbalimbali yakiwemo mabenki n.k.
Matarajio mengine ni Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini na sekta binafsi kupata fursa ya kutoa maoni, ufafanuzi na kuwashauri MUWAWATA namna ya kushiriki katika kilimo; Kusikiliza changamoto zinazowakabili MUWAWATA na kuwashauri namna ya kuzitatua; na Kujenga uelewa kwa washiriki wa mkutano kuhusu Mikakati na Mipango ya Serikali katika kuiendeleza Sekta ya Kilimo;
Vilevile Waziri Hasunga ameitaja Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) kuwa ni muhimu kwa wakulima nchini kwani inahimiza uongezaji thamani mazao ya kilimo kabla ya kuyauza ambapo pia itakuwa imeongeza nafasi za ajira kwa Watanzania.
Alisema hatua hiyo itaongeza ushindani wa bidhaa za ndani na nje ya nchi na itaiwezesha nchi kufikia malengo ya kuwa kwenye uchumi wa kati ifikapo 2025. “Ninawasihi MUWAWATA kujihusisha na kilimo kwa kuzingatia mnyororo wa thamani hasa kwa mazao ya vipaumbele ambayo yamebainishwa kwa kila eneo la kiikolojia” Alikaririwa Mhe Hasunga

CCM YAITAKA SERIKALI KUTOYUMBA KATIKA MCHAKATO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, WAELEZA WALIVYOJIPANGA KUHAKIKISHA WANASHINDA ILI KUWATUMIKIA WATANZANIA

$
0
0
*Yasema upinzani wamechungulia mapema wameona hawana nafasi ya kushinda, ndio maana wamejitoa 

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii.

WAKATI Vyama vya siasa upande wa upinzani nchini vikiwa vimetangaza kujitoa kwa kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu wa 2019 unaotarajia kufanyika Novemba 24, Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimesema kinatambua umuhimu na thamani ya uchaguzi huo, hivyo kitashiriki kikamilifu huku kikitoa rai kwa Serikali kutoyumbishwa na yoyote.

Pia CCM imeeleza kwa kina hatua mbalimbali za mchakato za uchaguzi huo ambazo zimefanyika na katika hatua kadhaa muhimu vyama vya upinzani vimeshiriki hatua kwa hatua na cha kushangaza baada ya kuchukua fomu na kuzirejesha wametangaza kutoshiriki kwa kutoa sababu ambazo imedai sio za msingi wowote.

Akizungumza leo Novemba 13 mwaka 2019, mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Haumphrey Polepole ameeleza pamoja na mambo mengine uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa unaendeshwa kwa sheria, kanuni na miongozo na hatua mbalimbali za uandaaji wa kanuni na miongozo vyama vya upinzani walipata nafasi ya kushiriki.

"Tunazo kanuni ambazo sote tumeshiriki kwa kuweka maoni yetu tangu mwanzo , ipo kanuni imeeleza kwa kina mchakato wa uchaguzi lakini kama haitoshi kanuni hiyo imewekewa muongozo wa vijiji na mitaa kuhusu uchaguzi utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.Kama haitoshi kanuni na muongozo umeweka kalenda ikiwemo ya kutoa tarehe ya siku ya kufanyika uchaguzi na sote tumeshiriki, ukaja mchakato wa kufuatilia uchaguzi wwote tukashiriki, ikaja hatua ya majina na mipaka ya vijiji na kisha yakafanyika mambo mengine.

"Ukaja mchakato wa uandikishaji wa upigaji kura lakini zoezi hilo, pia lipo katika uchaguzi wa serikali ya mtaa lakini misingi ni mmoja tu kuandikisha kwenye daftari la mpiga kura na wakati huo huo kuhamasisha wapiga kura kujiandikisha.Sheria inazuia wanasiasa kutoa elimu ya mpiga kura na sisi CCM tumejizuia katika hilo.Hivyo tulitumia mikutano ya ndani na CCM kuandaa wanachama wetu kwa kutumia taasisi za kimuundo ambazo tunazo ndani ya Chama.

"Wenzetu(vyama vya upinzani) wakavunja utaratibu kwa kwenda hadharani pamoja na kutumia mitandao ya kijamii na maeneo mengine. Hata hivyo tuliamua kukaa kimya maana ni kawaida yao.Hilo likapita na kisha ikaja hatua ya kukagua orodha ya wapiga kura, sote pamoja na wapinzani tukamaliza hilo.Nataka kueleza kitu hapa mwaka 2014 wenzetu walitufanyia uhuni walihamisha wapiga kura kutoka kitongoji kimoja kwenda kingine na wakifika huko wanapiga kura,"amesema.

Polepole ameongeza kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu wa Serikali za mitaa tumekuwa makini kwa kuhakikisha wanaopiga kura ni watu wa eneo husika.Baada ya kupita hatua zote hizo, CCM waliamua kuingia katika mchakato wa ndani wa kupata wagombea wao kwa kufuata tararibu za Chama, ambapo wamehakikisha demokrasia inatumika kwa kila mtu kupata haki inayostahili.

"Hapo tuliangalia nani anaweza kusimama kwa niaba ya CCM.Mchakato huo umefanyika katika ngazi mbalimbali na kwa umakini mkubwa, CCM tunatambua umuhimu wa uchaguzi huu na hivyo tumejiandaa vya kutosha ikiwa pamoja na kutoa elimu kuandaa watu wetu kuhakikisha sheria, kanuni na muongozo wa uchaguzi unafuatwa,"amesema Polepole.

Amesema kwa bahati mbaya wenzao wa upinzani hawakuwa na mchakato wa kupata wagombea wao , hivyo CCM na upinzani wakaja kukutana tena tarehe 29 wakati wa kuchukua fomu za kugombea."Tuliwauliza wenzetu vipi mchakato wa ndani wao hakuwa na majibu zaidi ya kuchukua fomu tu.Mchakato wa ndani kwa CCM ilikuwa nafasi tosha ya watu kujinoa, hivyo haikuwa tatizo kujaza fomu.Huenda wenzetu walikuwa wanataka kuchukua wale ambao wataondoka CCM baada ya kumalizika kwa mchakato wetu wa ndani, lakini safari hii hilo hakuna wote waliopata nafasi na waliokosa tumebaki wamoja".

Amefafanua kwamba, baada ya CCM kubaki wamoja, upinzani ndipo ulipoanza mizengwe na wakawa wa kwanza kwenda kulalamika ili kuonesha wanaonewa wakati kabla ya hapo hatua zote walishiriki kikamlifu na kuongeza sheria iko wazi kwa wale ambao watakuwa na matatizo ya fomu zao na wanahisi wameonewa wanayo nafasi ya kukata rufaa, lakini wapinzani waliamua kujitoa badala ya kufuata taratibu za kisheria.

"Wakati hawa wenzetu wanabwaga manyanga wapo waliokuwa wamechukua fomu, wengine majina yao yamepitishwa na wengine wamekata rufaa na sheria iko wazi ukihisi umeonewa kata rufaa lakini wenzetu kabla ya hatua ya kukata rufaa wakawekwa mpira kwapani.Kumekuwa na matamko kadhaa yametokea.Chadema ,ACT Wazalendo, NCCR-Mageuzi wametangaza kujitoa na hata Chama cha Hashim Rungwe nacho kimetangaza kujitoa.Huyu Rungwe sijawahi kuona uongozi wake wa taifa, sijawahi kuona kikao chao cha halmashauri kimekaa, hata takwimu zao za uchaguzi uliopita chama cha Rungwe hakikuambulia kitu.

"Hatukumuona akienda kuchukua fomu, kurejesha fomu, hakukwenda kukata rufaa, lakini baada ya vyama vya upinzani kuanza kujitoa naye Rungwe akaita waandishi wa habari kujitoa, niliuliza kajitoa katika nini?Maana hakuwepo.Baada ya hapo wameanza kutoa matamko mbalimbali na hapa nasisitiza katika hilo tulitoa msisitizo kwa Serikali isiyumbe kwenye jambo hilo maana hilo ni jambo la kisheria na katika sheria sote tulikubaliana na ndio maana tulishiriki mpaka kuchukua fomu.

"Mtu akikosea masuala ya sheria, sheria ni msumeno, na ukikosea katika sheria haina huruma , sisi tunawashukuru sana wana CCM na Watanzania kwa kutuunga mkono.Tuliamua kupeleka jeshi la wanasheria na mawakili nchi nzima kwa ajili ya kutoa elimu pamoja na kusaidia mchakato wa kujaza fomu ambalo ni hatua ya kisheria, wenzetu walishindwa kujaza majina, wadhamini, namna ya kuandika majina sawasawa kwa mujibu wa tangazo la serikali kijiji kinaitwajwe, na hayo yote wenzetu hawakuwa nayo maana hawakujiandaa na mchakato wa uchaguzi,"amesema Polepole.

Hata hivyo amesema kwa takwimu zilizopo vyama vya upinzani ambao wamechukua fomu ni ndogo ukilinganisha na ya CCM na hata ya waliorudisha fomu nao ni ndogo, kwa maana hiyo CCM kabla hata yauchaguzi kufanyika tayari imeshapata asilimia za ushindi na katika maeneo mengine hakuna hata mpinzani mmoja aliyechukua fomu kwa ajili ya uchaguzi huo."Hadi sasa tunavyoongea kuna mitaa tumaeshachukua maana wenzetu hawapo kabisa huko.Na hii ndio imewatisha na kuamua kuweka mpira kwapani maana ushindi wetu hautakuwa wa sunami bali ni ushindi kama wa upepo wa kisulisuli maana ndio habari ya mjini".

Ameeleza katika uchaguzi wa Serikali za Mtaa CCM wanakwenda wakiwa na ushahidi ambao unaonekana kwa macho na kwa vitendo kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dk.John Magufuli ya kuboresha maisha ya watu kwa kujenga miundombinu ya huduma muhimu za Watanzania na wanatambua kuwa kupitia uchaguzi huo wanataka kupata Wana CCM makini ambao watapata nafasi ya kushinda na kisha kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ya wananchi.

"Kutokana na mambo makubwa yamefanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetu Dk.Magufuli wale watu wa upinzani wamefanya uungwana na hivyo wameona mwaka huu ushindi utakuwa ni wa kisuli suli, na hivyo wameamua kuweka mpira kwapani.Tunaishukuru Serikali katika hili kutoyumba, imebaki na msimamo wake , hawa wenzetu ukitoa mwanya ndipo wanakuja na mambo mengine mengi yakiwemo ya kutaka kuongozewa muda,"amesema.

Hata hivyo ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa TAMISEMI kuhakikisha wanaandaa taarifa za mchakato wa uchaguzi huo na kwa lugha ya Kingereza kwani kinachofanywa na upinzani wanaandika taarifa za uongo na kupeleka kwa mataifa ya Ulaya kuonesha wanaonewa, hivyo TAMISEMI nayo ikiandika kwa lugha ya Kingereza hakutakuwa na sehemu ya kuongopa kuhusu uchaguzi na kila kitu kitakuwa wazi.

"Katika kipindi hiki cha uchaguzi tunafahamu kuna mambo mengi yanayofanyika kuna watu wachache wasioitakia mema nchi yetu, hivyo watataka kutumia nafasi hii kutuvuruga.Tunatambua ushirikiano wetu na mataifa mengine lakini katika mambo ya ndani ni vema wakaheshimu mikataba iliyopo ya nchi mmoja kutoingilia nchi nyingine kwa mambo yake ya ndani,"amesisitiza.

Hata hivyo amesema sio vizuri kutoa siri ya uchaguzi, lakini ameeleza ambavyo CCM wamejipanda katika uchaguzi kwa kila idadi ya wanachama ambao wamewekwa kusimamia uchaguzi huo na kufanya kampeni ambapo kwa idadi yao inatosha kabisa CCM kuifanya ishinde na hilo hawana shaka nalo na kuongeza kinachoonekana upinzani wanataka kucheza mchezo wa kombolela lakini wao wamejipanga imara na uchaguzi huo ni muhimu, hivyo hawatakuwa na mchezo wa aina yoyote.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images