Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 11,2019

$
0
0

                 
 


SERIKALI KUTOA MILIONI 13 KUKARABATI SEKONDARI YA MISUNGWI

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kutoa shilingi milioni 31 kwa shule ya Sekondari Misungwi ili kukamisha ujenzi wa bweni la wasichana.

Waziri Ndalichako ametoa ahadi hiyo mwishoni mwa wiki alioofika shuleni hapo kukagua miundombinu ya shule hiyo ambapo amesema amefurahishwa kuona uongozi wa shule jiyo  umekuwa ukitumia fedha visiting na kuweka akiba ya fedha kidogokidogo ambazo zimewawezesha kuanza ujenzi wa bweni hilo

"Nimefurahishwa  na mpango wa shule wa kuhifadhi fedha kidogo kidogo mpaka wamepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa bweni la watoto wa kike jitihada hizi ni kazima ziungwe mkono nami nikiwa waziri wa elimu natoa mchango wangu wa kuhakikisha naleta fedha za kumalizia " Amesema Waziri ndalichako.

Profesa Ndalichako amesema pamoja na kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi pia atahakikisha samani za bweni zinanuliwa  ili bweni hilo likamilike na kutumika.Aidha, Waziri Ndalichako amewata wanafunxi wa kike katika shule hiyo kuzingatia masomo yao wawapo shikeni hapo na kutojiingiza katika mambo ambayo yatawakatisha masomo yao na mwisho kupoteza ndoto zao.

Mkuu wa Shule ya sekondari Misungwi Mwanani Asembandwa amemshukuru Waziri wa Elimu kwa kutambua jitihada za shule za kuweka fedha kidogokidogo kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana 

Asembandwa amesema shule hiyo imefanikiwa kuwekeza fedha kidogo kidogo mpaka ikafanikiwa kupata  miliini 44  ambazo zimetumiwa kuanza ujenzi wa bweni la wasichana ambalo likikamilika itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kwa wakati mmoja.

"Kukamilika kwa bweni hili kutasaidia kutatua changamoto ya sehemu ya kulala kwa wanafunzi wa kike wa shule  pamoja na kuongeza wigo wa kutoa elimu kwa watoto wa kike wengi zaidi" Amesema Mkuu huyo wa Shule.

Naye Mwanafunzi wa shule hiyo Zemda Robert amemshukuru Waziri kwa kutoa ahadi hiyo ambayo inakwenda kupunguza changamoto ya malizi shukeni hapo.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikagua eneo linalojengwa bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Misungwi
 Moja ya jengo la bweni la wasichana katika shule ya sekondari Misungwi lililojengwa na serikali kupitia mradi wa EP4R.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari  Misungwi alipofika shuleni hapo kukagua mindombinu ya shule hiyo.

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YARIDHISHWA NA TASAF KATIKA KUONDOA KERO YA UMASKINI NCHINI.

$
0
0

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii {TASAF} Awamu ya 3 kipindi cha Pili umejikita zaidi kufanya kazi na walengwa katika masuala ya uimarishaji wa Elimu, Afya, pamoja na mafao kwa Walemavu waliomo ndani ya Kaya Maskini kupitia Shehia mbali mbali Unguja na Pemba. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo Nd. Ladislaus Mwamanga alisema hayo wakati akitoa Taarifa ya matayarisho ya kuanza kwa Awamu hiyo katika Kikao cha Wakurugenzi na Maafisa wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar mkutano uliofanyika Vuga Mjini Zanzibar. 

Ndugu Ladislaus Mwamanga alisema Awamu ya Tatu kipindi cha Pili ambayo Fedha za Mfuko huo jumla ya shilingi Trilioni 2.1 sawa na Dola za Kimarekani Milioni 883 zimeshatiwa saini inategemewa kuwafikia Wananchi wote katika Vijiji mbali mbali hadi vile visivyopata huduma ya TASAF na Awamu zilizopita. 

Alisema Uongozi wa TASAF utasimamia vyema miradi yote iliyopendekezwa na Wananchi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Mabwawa ya kufugia Samaki pamoja na Miundombinu ya Umwagiliaji Maji kwenye Mashamba ya Wana TASAF kwa lengo la kuongeza uzalishaji. 

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii {TASAF} aliwahakikishia Wakurugenzi na Waratibu hao wa TASAF wa Zanzibar kwamba mafao yote yanayolalamikiwa katika kipindi cha nyuma yatalipwa mapema kabla ya muendelezo wa kipindi cha Pili kuanza rasmi. 

Nd. Mwamanga alifahamisha kwamba yapo mabadiliko ya muundo mzima wa TASAF kipindi cha pili yatakayozingatia zaidi maboresho ya shughuli za mfuko huo ili miradi yake iweze kufanya kazi kwa ufanisi kupitia mfumo wa kisasa wa Mtandao wa mawasiliano katika kutanua wigo wa maendeleo ya Kiuchumi. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii {TASAF} alielezea faraja yake kutokana na mafanikio makubwa ya Awamu zilizopita za Mfuko huo zilizowezesha Wanafunzi 277 wa Kaya Maskini Tanzania wamepata mikopo ya elimu ya juu kutoka taasisi ya HELB ili waweze kuendelea na masomo yao ya Vyuo Vikuu mwaka 2019. 

Wakitoa michango yao katika Kikao hicho cha matayarisho ya kuanza kwa Awamu ya Tatu sehemu ya Pili ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Wajumbe wa Kikao hicho walisema TASAF Awamu ya Tatu Kipindi cha Pili inapaswa kutoa upendeleo zaidi kwa Wananchi wenye mahitaji maalum ili kuwapunguzia utegemezi. 

Wajumbe hao pia wakaelezea changamoto zinazowakumba Watendaji wa Mfuko huo ambazo zinapaswa kutafutiwa ufumbuzi wakizitaja kuwa ni pamoja na ucheleweshaji wa Taarifa, udanganyifu kwa baadhi ya Watendaji pamoja na ufinyu wa Elimu kwa Walengwa. 

Akitoa nasaha zake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed aliushukuru Uongozi Mzima wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii {TASAF} kwa jitihada zake za kuunga mkono Miradi ya Wananchi katika maeneo mbali mbali Nchini. 

Waziri Aboud aliwakumbusha Viongozi na Watendaji wanaosimamia Mfuko huo kuangalia zaidi uimarishaji wa Miradi ya maendeleo hasa katika Sekta ya Elimu, na Kilimo ambayo inasaidia kukwamua Kaya Maskini katika kujiletea maendeleo yao. 

Katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud alimkabidhi rasmi Uenyekiti wa Kamati ya Mfuko wa TASAF Unguja Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Hassan Khatib Hassan. Mapema asubuhi Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii {TASAF} Nd. Ladislaus Mwamanga alikutana kwa mazungumzo ya kubadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar. 

Katika mazungumzo yao Balozi Seif aliwapongeza Viongozi wa Mfuko wa TASAF kutokana na kazi nzuri wanayoifanya hususan kwa upande wa Visiwa vya Unguja na Pemba kwa kuendeleza kuwatumikia Wananchi ili waweze kujikomboa Kiuchumi. 

Aliwataka na kuwashauri Watumishi hao wa TASAF waendelee kutoa Elimu kwa Wananchi kutokana na faida zinazopatikana kupitia miradi na mafao ya TASAF katika kusukuma gurudumu la Maendeleo.Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza ufuatiliaji wa Taarifa sahihi za Wananchi ili kuhakikisha kila mstahiki anapatiwa fursa hiyo na kuitumia ipasavyo. Nao Wananchi kwa upande wao wanapaswa kutoa taarifa zilizo sahihi kupitia Sheha wa Shehia zao ili ziweze kusaidia katika ugawaji wa mafao ndani ya Kaya zao. 
Makamu wa pili wa SMZ Balozi Seif Ali Idd akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (wa pili kushoto juu ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga  aliyevaa miwani) akisisitiza jambo kwenye mkutano wa viongozi wa SMZ juu ya utekelezaji  wa shughuli za TASAF .

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ, Mhe. Mohamed Abood akizungumza kwenye kikao cha kuwajengea uelewa viongozi wa SMZ juu ya utekelezaji wa shughuli za TASAF.

 Baadhi ya maafisa wa SMZ (picha ya juu na chini) wakiwa katika kikao cha kuwajemgea uelewa juu ya masuala mbalimbali ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF 

Serikali yaipongea Taasisi ya CCBRT kutoa huduma kwa jamii kwa miaka 25

$
0
0
Taasisi ya CCBRT Tanzania imetimiza miaka 25 ya kutoa huduma za tiba kwa watoto wenye matatizo ya macho, miguu pinde, mgongo wazi na afya ya uzazi ikiwemo fistula.


Akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa, Rais wa bodi ya CCBRT Tanzania, Dkt. Wilbrod Slaa alisema tulianzisha hospitali ya CCBRT mwaka 1994 mwezi wa Nne tukiwa na malengo ya kusaidia watoto wenye ulemavu, lakini wazo lilikuja nikiwa na Dan Wood tukiwa Zanzibar baada ya ajali ya ndege iliyotokea Rwanda 

" Nakumbuka mwanzo tulikuwa tunapita mitaani kwenye nyumba na kukuta watoto wenye matatizo ya miguu na macho, kuna nyumba tulikuta mtoto ambaye alikuwa hana uwezo wa kuona mchana lakini usiku anaona vizuri wataalamu wanakumbuka , huyu ndio alikuwa mgonjwa wetu wa kwanza". alisema Slaa. Kina mama wengi ilikuwa tukipita mitaani walikuwa wanalia kuomba msaada wa watoto wao wenye matatizo mbalimbali na tuliweza kuwasiadia 

Tulipata changamoto ya kupata sehemu ya kufanyia operesheni, ikabidi tuende hospitali ya Mwananyamala na kuomba kupewa ruhusa ya kuwafanyia operesheni wagonjwa wetu wakaturuhusu na changamoto nyingine ilikuwa mahali pa kulaza wagonjwa wetu, na ilibidi tukiuke taratibu na kwenda kuwapangishia kwenye nyumba ya kulala wageni ambazo tulikodi kwa wagonjwa tu, na kwa bahati waziri wa afya kipindi hicho, mhe. Anna Abdallah alitoa baraka zake wagonjwa waweze kuwekwa kwenye nyumba hiyo. Aliendelea kusema Dkt. Slaa

Tunashukuru serikali ya Tanzania kuwa mdau mkubwa sana wa CCBRT kwa kutoa ardhi kubwa bure  kuwezesha kujenga hospitali na kupandisha hadhi hospitali yetu kuwa ya rufaa (zonal referral) alisema Dkt. Slaa

Pia tunatoa huduma zetu kulingana na wagonjwa tunaowapokea, hii inategemea mgongwa private au sio private na gharama tunazowachaji wagonjwa wa private zinaenda kutibia wagongwa wasio na uwezo gharama za matibabu alimaliza kusema Dkt. Slaa

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, alisema, Naomba kuchukua nafasi hii kuwapongeza Taasisi ya CCBRT kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake nchini. Najua mmepitia changamoto nyingi sana pindi mlipoanza kama alivyokwisha kusema Rais wa bodi ya Taasisi ya CCBRT Dkt. Wilbrod Slaa.

Pia niwapongeze kwa kuwa na huduma za mkoba (mobile outreach) ambazo zimekuwa na ubia na hospitali mbalimbali nchini kama vile Bombo mkoani Tanga, Seko Toure Mwanza, Mnazi Mmoja Zanzibar, Kabanga Kigoma, Bagamoyo na Ikwiriri hii inaonyesha jinsi gani mmeweza kuwa bega kwa bega nasi serikali alisema Mhe. Mwalimu.
Nachukua fursa hii pia kuwapongeza, kituo cha CCBRT Moshi ambacho kinafanya kazi nzuri sana, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996 kimeweza kuhudumia watoto wenye ulemavu na familia zao zaidi ya 10,000 na kuwarejeshea matumaini aliendelea Mhe. Mwalimu

Nimepewa taarifa CCBRT ndani ya miaka 9 mnashirikiana na timu ya usimamizi na uendeshaji wa huduma za afya mkoa wa Dar es salaam kutoa mafunzo kwa watoa huduma zaidi ya 900 kila mwaka hasa kwa madaktari na wauguzi. Na mradi wa kuwajengea uwezo watumishi kwenye vituo vya afya na zahanati 22 katika manispaa zote tano za mkoa wa Dar es salaam na Pia mradi huu umewekeza kiasi kikubwa cha miundombinu, ukarabati wa wodi za wazazi, ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 1,895,615,400 na uwekezaji wa vyumba maalum vya watoto njiti, vyoo maalum kwa wenye ulemavu, utambuzi wa mapema wa watoto wenye ulemavu na kina mama wenye fistula ya uzazi aliendelea kusema Mwalimu.

Kwenye fistula wastani ya akina mama 800 kwa mwaka walipata huduma ya upasuaji, takwimu zinaonyesha akima mama takribani 2000 hadi 3000 hupata fistula ya uzazi nchini , CCBRT kushirikiana na MUHAS, Chuo kikuu Dodoma, KCMC kumewezesha kutoa mafunzo na Taasisi ya kimataifa ya madaktari bingwa magonjwa ya kinamama na wajawazito,(figo) kuwa miongoni mwa vituo vya mafunzo ya upasuaji fistula duniani, na mpaka kufikia mwezi 10 mwaka 2019 watakuwa wamefanya upasuaji fistula kina mama wapatao 10,000 alimaliza kusema.
Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB kwa kununua picha iliyouzwa kwenye mnada kwa thamani ya shilingi millioni 4.5 huku Dkt. Wilbrod Slaa akimpongeza mmoja kati ya wafanyakazi wa benki hiyo.Taasisi ya CCBRT Tanzania imetimiza miaka 25 ya kutoa huduma za tiba kwa watoto wenye matatizo ya macho, miguu pinde, mgongo wazi na afya ya uzazi ikiwemo fistula.
Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wageni waalikwa kwenye tafrija ya maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi ya  hospitali ya CCBRT jana jijini Dar es Salaam 
 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda Msangi akizungumza na wageni waalikwa
 Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa PWC kwa kununua picha iliyouzwa kwenye mnada kwa thamani ya shilingi millioni 2 ili kuchangia gharama za matibabu kwa wasiojiweza

 Rais wa bodi ya Taasisi ya hospitali ya  CCBRT, Wilbrod Slaa akibadilishana mawazo na  Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda Msangi

 Rais wa bodi ya Taasisi ya hospitali ya  CCBRT, Wilbrod Slaa (kulia) akimkabidhi picha ya zawadi kwa mchango alioutoa kwa taasisi hiyo Makamu wa zamani wa Rais bodi ya CCBRT, Biharilal Tanna , kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda Msangi

 
 Baadhi ya wakina mama waliopokea vyeti vya kutambua mchango wao kwa CCBRT wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda Msangina Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda Msangi

 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye tafrija ya CCBRT usiku wa jana

 Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wapili kushoto waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa bodi ya Taasisi ya hospitali ya CCBRT, Wilbrod Slaa (wapili kulia waliokaa) Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda Msangi na Makamu wa Rais wa zamani wa bodi hiyo, Biharilal Tanna na wadau mbalimbali kwenye tafrija ya maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi ya  hospitali ya CCBRT  jijini Dar es Salaam jana.

Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na  wafanyakazi wa Taasisi ya hospitali ya CCBRT jana kwenye tafrija ya maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi hiyo.

UBALOZI WA CHINA,TAASISI YA SUKOS KOVA FOAUNDATION WACHANGIA MRADI WA KUZUIA UJANGILI KANDO YA HIFADHI ZA TAIFA NCHINI

$
0
0
Picha mbalimbali za Awamu ya Pili ya muendelezo wa mradi wa kuzuia ujangili katika vijiji vilivyopo kando kando ya hifadhi za Taifa nchini Tanzania. 

Mradi huu umefadhiliwa na Ubalozi wa China nchini Tanzania na kuratibiwa na Taasisi ya Sukos Kova Foundation. 

Awamu ya Pili ya mradi huu umehusisha msaada kwa wakazi wa kijiji cha Mhenda wilayani Kilosa mkoani Morogoro, kijiji kilichopo kando kando ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi. Baadhi ya wanakijiji wa Mhenda hasa vijana hujihusisha na Ujangili kama njia ya kujiingizia kipato. 

Ubalozi wa China nchini Tanzania pamoja na Sukos Kova Foundation umewasilisha msaada  wa:

a) Mbegu za Mahindi - 2,500kgs
b) Mbegu za Alizeti - 1,500kgs
c) Mbegu za korosho- 800kgs 
Msaada huu unalenga kuwasaidia wanakijiji wa mhenda wapatao 3,000 kujishughulisha na kilimo badala ya ujangili kama njia ya kujiingizia kipato.

Aidha misaada mingine iliyotolewa ni:

d) Uniform - 13
e) Boots - 13 
Kama njia ya kuunga mkono juhudi za kikundi cha ulinzi shirikishi wilayani kisaki ambao ni wananchi wanaoshiriki kulinda hifadhi ya Taifa ya Mikumi. 

Pia Ubalozi wa China na Sukos Kova Foundation wamekabidhi Kompyuta pakata (Laptop) 4 pamoja na runinga 1 (TV set) kwa ajili ya kusaidia maafisa wa mikumi kuelimisha zaidi wakazi wa vijiji vilivyopo kando kando ya hifadhi hiyo kupinga ujangili na kuungana na Serikali katika kulinda na kutunza hifadhi hizo. 



 




WAGENI 250 KUANZA MKUTANO WA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU LEO JIJINI DAR

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Amos Nungu katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na mkutano wa kubadilishana uzoefu wa  Masuala ya Sayansi Techinolojia  na Uzoefu unaoanza leo hapa nchini kulia ni Ofisa Mtafiti wa Costech, Neema Tindamanyire na kushoto ni Meneja Sayansi Hai kutoka Costech, Hulda Gideon.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimzikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Amos Nungu.

WAGENI 250 kutoka nchi mbalimbali duniani wamewasili hapa nchini kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Baraza la Sayansi Kanda ya Afrika kwa lengo la kubadilishana uzoefu pamoja kujifunza kuhusu masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu mkutano huo ambao unaoanza leo.

Alisema mada inayotawala mkutano huo ni sayansi wazi na shirikishi katika utafiti na ubunifu wa maendeleo, hivyo Costech kama mratibu wa masuala hayo ya utafiti, teknolojia na ubunifu imepewa dhamana ya kuandaa mkutano huo.

“Kupitia mkutano huu tutabadilishana uzoefu pamoja na kujifunza kutoka kwa kila mmoja, pia kujenga mahusiano pale inapowezekana,” alisema Dk. Nungu.

Dk. Nungu alisema, Tanzania ipo kwenye sera ya uchumi wa viwanda hivyo katika mkutano huo watajifunza mambo mengi kutoka kwa wengine kwa kuwa nchi 16 za Afrika zinashiriki pamoja na mataifa makubwa karibu kila bara.

Katika mkutano huo, Dk. Nungu alisema Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Dk. Joyce Ndalichako atafungua.

Kwa upande wa Meneja Sayansi Hai kutoka Costech, Hulda Gideon alisema mkutano huo utazungumzia sayansi wazi kwa maana kuwa mawazo yote yanayotolewa yawe shirikishi, andiko pamoja na utafiti unaofanyika kuwa wazi na mwishoni taarifa ziwe wazi kwa ajili yaw engine kuzitumia.

Alisema sayansi wazi haiangali maandiko tu ya utafiti bali hata vifaa vinavyotumika ambavyo vinaweza kusaidia wengine ambao hawana vifaa hivyo.

Alisema Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazokuza sayansi nayo imeshiriki kwenye utafiti na data katika sekta ya afya na maliasili ambavyo kwa Tanzania inaongelewa kuwa ina viumbe hai wengi.

“Inabidi sayansi ilivyofanyika ikatumika kuwaambia watu kuwa kuna utafiti huo umefanyika. Hata kwa upande wa dawa unakuta mimea mingi ipo kwa nchi za Afrika ambazo ni maskini utafiti ukifanyika huku kama hakuna uwazi, yale maandiko yatabakia nchi zilizoendelea wataingia kwenye viwanda vyao na kuzalisha dawa halafu sisi tunasubiri kununua dawa kutoka kwao.

“Lakini kama tukiwa ile sayansi wazi watajua kuwa dawa zile pamoja na kuwa zimetengenezwa kwenye viwanda vya nje lakini zilitokea Afrika ni rahisi kushare ile keki iliyotokana na dawa hizo,” alisema.

Alisema hiyo ndiyo maana halisi ya kuhamasisha Tanzania kuingia kwenye michakato yote ya kuwa na sayansi hai inayokuwa na uwazi zaidi.

“Lengo kubwa la kuwa na sayansi hai ni kukuza sayansi yenyewe, kama Afrika au nchi zinazoendelea hatujafika kule lakini tukiifanya ile sayansi ikawa wazi ina maana wale wenzetu kule nje wanachokifanya na sisi tutakijua, tukikijua hatuna haja ya kuanza kitu upya tutatumia vile ambavyo wamevifanya na kuvileta huku kwetu kwa ajili ya kuviendeleza,” alisema.

 Sayansi wazi pia inasaidia kupunguza gharama hivyo mtu anayefanya utafiti wa aina hiyo nchini hatakuwa na haja ya kununua kifaa kinachohitajika ikiwa ni pamoja na kukuza ushirikiano baada ya kujua mwingine ana nini au anafanya nini.

Hata hivyo Ofisa Mtafiti wa Costech, Neema Tindamanyire alisema hadi kufikia jana nusu ya wageni walioalikwa walikuwa wameshafika.

Katika mkutano huo takribani sh. milioni 500 zitatumiwa na wageni hao kama gharama za kwenye hoteli, vyakula na huduma mbalimbali watakazozipata nchini ikiwa ni pamoja na kutembelea vivutio mbalimbali

NDUGU WAOMBWA KUJITOKEZA

MAADHIMISHO YA MIAKA 105 YA VITA YA KWANZA NA MIAKA 75 YA VITA VYA PILI VYA DUNIA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini Mhe. Joerg Herrera wakipokea heshima wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa anasoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa amesimama pamoja na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke (kushoto) na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini (kulia) Mhe. Joerg Herrera wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Meja Jenerali Sherrif  Sheikh Othman (wa pili kutoka kulia) akiwa na baadhi ya Makamanda kutoka Ujerumani na Uingereza wakiwa wamesimama kutoa heshima katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Baadhi ya askari wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini kama ishara ya heshima wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa ameongozana Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke (kulia) na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini (kushoto) Mhe. Joerg Herrera kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) pamoja na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini Mhe. Joerg Herrera wakiweka mashada ya maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
 Mmoja wa wapiganaji wa vita ya pili ya dunia Mzee Malagila Shimba mwenye umri wa miaka 98 akipiga saluti mara baada ya kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini Mhe. Joerg Herrera wakiwaongoza  baadhi ya makamanda kutoka nchi za Tanzania,Ujerumani na Uingereza kuweka shada la maua katika mnara wa askari ulioko Posta Jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia.






WPP Scangroup yazindua mkutano, kuzungumzia mabadiliko ya kidigitali

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Nala, Benji Fernandez, Mkurugenzi Mkuu wa Unilever, David Minja, na Mkurugenzi Mkuu wa Mwananchi Communications, Francis Majige katika mkutano wa Reboot Tanzania iliyoandaliwa na WPP Scangroup hivi karibuni.
Mkuu wa idara ya mikakati,Squad Digital, Parusha Partab akisikiliza katika Mkutano wa Reboot Tanzania iliandaliwa na WPP Scangroup.
Idriss Sultan, Omary Tambwe ( Lil Ommy) na Webiro Wassira (Wakazi) katika mkutano wa Reboot Tanzania iliyoandaliwa na WPP Scangroup hivi karibuni.

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya WPP Scangroup imezindua mkutano ya kwanza kuhusiana na mabadiliko ya kidigitali kwa lengo la kujadili mipango ya kuendeleza mazugumzo kuchochea mabadiliko ya kibiashara katika ulimwengu wa kidigitali.

Mkutano huo umezinduliwa leo na ni wa kwanza kufanyika nchini Tanzania, kwani kwa mara kwanza mkutano wa aina hiyo ulifanyika nchini Kenya mwaka 2018 na katika mkutano huo kampuni kubwa zinazojihusisha na ulimwengu wa kidigitali walipata nafasi ya kushiriki kikamilifu.

Wakati wa mkutano huo wadau wametazama mazingira ya kibiashara na wameona kunamabadiliko makubwa na hasa kuongeza kwa watumiaji wa mtandao na mawasiliano.Kupitia mkutano huo imeelezwa kwamba kampuni ya WPP Scangroup mkakati wao ni kuwa kiongozi katika eneo la teknolojia na ubunifu.

Pia WPP Scangroup wamesema wanataka kuingiza toleo rahisi na bora ambalo lililobuniwa kwa lengo la kukamata fursa za soko zinazobadilika, na muundo ulioratibiwa uliojengwa na mahitaji ya wateja wao.

"Katika kuhakikisha tunafanikiwa katika ulimwengu wa kidigitali, tulifanya mkutano mdogo uliowakutanisha Mkurugenzi Mkuu wa Standard Chartered Bank Aljamair Riaz, Mkurugenzi Mkuu wa Nala Benji Fernandez, Mkurugenzi Mkuu wa Unilever David Minja na Mkurugenzi Mkuu wa Mwananchi Communications Francis Majige Nanai,"imesema taarifa ya WPP Scagroup.

Katika mazugumzo yao Aljamair Riaz amesema kwamba kwasababu ya hali ya kidigitali kwa sasa, benki ya Standard Chartered wamebadilisha mkakati yao na kufuata upepo wa kidigitali. "Hapo mwanzo gharama ya ununuzi ilikuwa juu. Lakini tulivyo badilisha na kwenda kidigitali, tumeweza kuokoa fedha na kuwaongezea wateja katika bidhaa mbalimbali,"amesema.

Ameongeza kuwa huko Hong Kong wamezindua benki ya kidigitali tu ikiitwa ‘Virtual bank’. Pamoja na mambo mengine Kampuni ya WPP Scangroup katika kuhakikisha eneo hilo la digitali linapewa kipaumbele waliamua kuwaalika pia watu mashuhuri nchini ambao wako katika mabadiliko ya kidigitali.

Akizungumza katika mkutano huo Webiro Wassira ambaye anajulikana kama Wakazi amesema kama mtu mashuhuri ametoa maoni yake kuhusu nini kifanyike katika kuhakikisha digital inatumika kubadili maisha ya watu.

Wakati Omary Tambwe 'Lil Ommy' ambaye ni Mtangazaji wa Times FM aliyeshinda tuzo ya mtangazaji bora amesema kuna utofauti ya kuwa na followers wengi nak ujijengea brand.

Kwa upande wake Manish Sardana ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Squad Digital amesema kuwa ujio wa dijitali kumewafanya wao kama wafanyabiashara wanafikiria mikakati yao hasa linapokuja suala la matangazo wakati walengwa wengine wanafikiria tofauti kwa sababu ya uwepo wa hii ya media za kijamii."Hapa ndipo tunapoingia na kuamini kuwa ni muhimu kuwajulisha na kuelimisha washirika wetu wa biashara njia hii kupitia wakati huu wa ajabu."

WANAHARAKATI WAWAASA WAGOMBEA WA UCHAGUZI SERIKALI ZA MTAA KUJITAFAKARI UPYA

$
0
0
 Mwanaharakati wa Mambo ya kijamii, Mackdeo Shilinde akizungumza jijini Dar es Salaam leo na kuviasa vyama vya siasa kutunza afya ya demokrasia hapa nchini.
Mwanaharakati wa Mambo ya kijamii, Mackdeo Shilinde akizungumza jijini Dar es Salaam leo na kuviasa vyama vya siasa kutunza afya ya demokrasia hapa nchini. Kulia ni Mwanaharakati kutoka ADO, Ally Mwinyi.
Baadhi ya Waandishi wa habari.

Na Avila Kakingo,Glou ya Jamii
WANAHARAKATI wa mambo ya kijamii wamewasa viongozi wa vyama vya upinzani nchini kujitafakari upyaa jinsi wagombea wao wa uchaguzi wa serikali za mtaa wanavyojitoa katika nafasi walizochaguliwa kugombea   uchaguzi wa serikali za mtaa unaotarajia kufanyika Novemba 24,2019 nchini kote.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwanaharakati wa Mambo ya kijamii, Mackdeo Shilinde, amesema kuwa mambo yanayotakiwa yafanyike na chama pamoja na wagombea yafanyike kwa haki na kwa amani kwani wananchi wapo tayari kuchagua kiongozi wanae mtaka.

"Viongozi wa vyama vya upinzani warudi tena wakatafakari na wagombea wao wakawashirikishe waseme je ni kweli wagombea wao hawataki kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa? lakini vilevile vyama vya upinzani wakafate taratibu wa katiba yao kwenye mambo yanayotakiwayafanyike yafanyike." Amesema Shilinde

Hata hivyo Mwanaharakati wa mambo ya kijamii kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya  Alliance for Development (ADO), Ally Mwinyi amesema kuwa wagombea wa vyama vya upinzani wanaojiondoa kugombea katika uchaguzi wa serikali za mtaa wanadhoofisha afya ya demokrasia nchini na kuwanyima wananchi demokrasia ya kuchagua kiongozi wanaye mtaka.

"Jambo hili la kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa si jambo zuri kwa afya ya Demokrasia na ni kuwanyima wananchi demokrasia ndani ya demokrasia"

Mwinyi amesema kuwa demokrasia ni kuwa tayari kufata zile hatua zote za uchaguzi kwa sababu zisipofatwa ni kuharibu kanuni na taratibu zilizowekwa kwaajili ya afya ya Demokrasia.

Hata hivyo Mwinyi amesema kuwa kitendo cha baadhi ya vyama vya siasa kutoa tamko kabla  ya majibu ya rufaa zao hayajatoka hii si picha nzuri kwani vyama hivyo kwani vinasigina demokrasia.

"Sisi kama wanaharakati tunachopenda kutoa rai yetu kwa vyama viheshimu demokrasia, vionyeshe kuwa wao ndio wa kwanza wa kuonyesha afya ya demokrasia".

Mwinyi amesema kuwa watanzania wanahitaji watu kwaajili ya kuwatetea pamoja na kuwaongoza na hakuna njia nyingine isipokuwa ni kufanya uchaguzi kwa kufata taratiu zilizowekwa.

Corporate Unwind ya Smartlab yalenga vijana kujifunza mbinu za kibiashara

$
0
0
Baadhi ya Wavumbuzi na wageni mbali mbali wakiuliza maswali katika warsha ya pili ya Corporate Unwind iliofanyika ofisi za Smartcodes, Mikocheni Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Smartcodes,Edwin Bruno akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani na wavumbuzi na  wageni mbali mbali katika picha ya pamoja wakati wa warsha ya pili ya Corporate Unwind iliofanyika pale ofisi za Smartcodes, Mikocheni Dar es Salaam

Mwandishi wetu
KUTOKANA na uhitaji viongozi shupavu wenye uelewa kuhusu teknolojia nchini, kampuni ya masuala ya kiteknolojia Smart Lab imetoa wito kwa wamiliki wa makampuni na mashirika mbalimbali kuwekeza kwa vijana na wajasiriamali wabunifu ili kuisaidia serikali kupunguza tatizo la uhaba wa ajira nchini.

Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Smart Codes, Edwin Bruno wakati akizungumza katika warsha iliyopewa jina la ‘Corporate Unwind’.

Warsha hiyo ambayo imefanyika kwa mara ya pili, hufanyika kila baada ya miezi mitatu kwa kuwakutanisha vijana wajasiriamali wabunifu wa masuala ya kitenlojia na wawekezaji au wamiliki wa makampuni waliofanikiwa ili kuwajenga kibiashara na kuwapatia mbinu za kukua zaidi kulingana na mawazo waliyobuni.

Bruno alisema Corporate unwind pia hulenga kujenga daraja kati ya wavumbuzi wakubwa na wachanga kwa kuwakutanisha pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kukua kibiashara.

“SmartLab inafanya kazi hii kuhakikisha kuwa tunapata viongozi bora katika mifumo yetu ya uvumbuzi watakojenga kampuni zenye nguvu na mwishowe biashara imara, na hii ndiyo sababu tunatumia ujuzi na rasilimali zetu kwa kuwajenga uwezo wa vijana ili kupunguza tatizo la ajira.

“Hivyo ni muhimu makampuni na mashirika kutekeleza mikakati yenye kuwasaidia vijana wenye shida mbalimbali  kutoka kaya maskini hasa wasichana na kuelekeza nguvu katika utoaji elimu, ujuzi wa ajira na kujifunza ujasiriamali. Hili litaongeza mpango wa ushiriki sawa wa kijisni kimaendeleo na kukuza upatikanaji wa ajira,” alisema.

Alisema Corporate Unwind msimu huu imekuja na kauli mbiu inayosema “Uongozi bora unaochochea ukuaji kwenye sekta ya kibenki” inalenga kuwaandaa vijana kuwa viongozi bora katika sekta ya benki nchini.

Aidha, akizungumza katika jukwaa hilo, Mzungumzaji mkuu wa misimu wa pili wa Corporate Unwind ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani alisema, benki yake imelenga kutoa kipaumbele kwa vijana kujifunza maarifa mbalimbali katika sekta hiyo ili kukua kiuchumi.

“Tuna programu mbalimbali zinazowawezesha vijana kukua kibiashara, pia tunawafundisha namna kufanya kazi kutimiza ndoto zao.

“Nina furaha kuwa sehemu ya Corporate Unwind toleo la pili na pia ninafurahi kwa kupewa nafasi ya kujuana na hadhira ya watu ambao naamini wanapigania mabadiliko katika uchumi wa Tanzania na mfumo wa ubunifu kwa jumla" alisema.

TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA YAFUNGIA VITUO VITATU VYA AFYA KUTOA HUDUMA MKOANI MWANZA

$
0
0
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk Thomas Rutachuuzibwa wa tatu kutoka kushoto mstari wa kwanza akiwa na kamati ya Usimamizi wa Afya ya Mkoa wa MWanza na Mkuu wa ofisi ya Kanda ya Ziwa ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania,Bwana Miguta Ngulimi wakiwa katika picha ya pamoja mara baaada ya kupata matokeo ya ukaguzi uliofanyika katika mkoa wa Mwanza.


Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) katika ukaguzi wake wa kawaida wa kila mwaka umevifungia vituo vitatu vya afya kutoa huduma ya mionzi (X-ray) kutokana na kutokidhi matakwa ya Sheria Na. 7 ya Nguvu za Atomiki ya Mwaka 2003 na kwamba vitarejeshewa huduma hiyo mara vituo hivi vitakaporekebisha mapungufu yaliyoonekana. 

Vituo vilivyofungiwa ni vya Wilaya ya Sumve, Hospitali ya Wilaya ya Ngudu na Hospitali ya Wilaya ya Misungwi.

Vituo hivyo vimefungwa kufuatia ukaguzi unaoendelea mkoani Mwanza ikiwa ni zoezi linalofanyika kila mwaka katika kuhakikisha usalama wa utoaji wa huduma ya mionzi unafuatwa kama ambavyo ilivyoelekezwa katika Sheria Na. 7 ya Nguvu za Atomiki Tanzania ya Mwaka 2003 ili kulinda wafanyakazi, wagonjwa, wananchi na mazingira dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi. Katika vituo vya Sumve na Ngudu imegundulika kuwa watumishi wake hawana sifa za upigaji wa picha za mionzi huku katika kituo cha Misungwi imegundulika kuwa vifaa vyao vya mionzi havina ubora unaostahili.

TAEC inavitaka vituo vyote vinavyotumia mionzi katika utoaji wao wa huduma mbalimbali kuhakikisha vinafuata Sheria na taratibu za kiusalama kama ilivyoelekzwa katika sheria ikiwemo kuishirikisha TAEC katika hatua zote za ujenzi wa vituo hivyo kwa lengo la kulinda afya za Watanzania.

Katika ukaguzi huu unaoendelea jumla ya Vituo 32 vimekaguliwa ambapo vituo 28 ni vya sekta ya afya na vituo 4 ni katika sekta ya viwanda.

ELIMU YA KODI YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA NA WANANCHI WA MALINYI

$
0
0
Afisa Kodi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Julius Mjenga akiwaelimisha baadhi ya Wafanyabiashara wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro wakati wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa Mikoa ya Morogoro na Pwani.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro wakisikiliza elimu ya kodi kutoka kwa Afisa Kodi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Julius Mjenga (hayupo pichani) wakati wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa Mikoa ya Morogoro na Pwani.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro wakijisomea kitabu cha Kodi na Ushuru Mbalimbali wakati wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa Mikoa ya Morogoro na Pwani.(PICHA ZOTE NA TRA)

………………………………………………..

Na Veronica Kazimoto-Malinyi

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekutana na wafanyabiashara pamoja na wananchi wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro kwa ajili ya kutoa elimu ya kodi ikiwa ni pamoja na kuwasajili wafanyabiashara wasiokuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi.

Akizungumza na wafanyabiashara hao wakati wa utoaji wa elimu hiyo, Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Julius Mjenga, amewahimiza kutunza kumbukumbu za biashara zao ili kukadiriwa kodi stahiki.

“Mara nyingi wafanyabiashara wamekuwa wakilalamika kuwa TRA inawakadiria kodi kubwa lakini mlio wengi hamtunzi kumbukumbu kwenye daftari linaloonyesha manunuzi na mauzo ya kila siku ili mwisho wa mwaka Afisa wa Kodi atumie daftari hilo kukukadiria kodi ambayo inaendana na uhalisia wa biashara yako,” alisema Mjenga.

Mjenga ameongeza kuwa, mfanyabiashara anaetunza kumbukumbu analipa kodi kidogo ukilinganisha na mfanyabiashara ambaye hatunzi kabisa kumbukumbu za biashara yake.

Naye mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi, Samson Nyanda wa wilayani hapa, ameiomba TRA kutoa elimu ya kodi mara kwa mara kwa kuwa wafanyabiashara huongezeka kila wakati.

“Elimu hii tuliyoipata ni nzuri mno ila tunaomba iwe endelevu na ifanyike hata kwa mwaka mara tatu kwa sababu kila wakati wafanyabiashara wanaongezeka na wengi wao hawana hii elimu ya utunzaji wa kumbukumbu”, alieleza Nyanda.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inafanya Kampeni ya Elimu, Usajili na Huduma kwa Mlipakodi katika Mikoa ya Morogoro na Pwani ambapo kwa Mkoa wa Morogoro, timu ya maafisa wa TRA inatarajia kuwafikia wafanyabiashara na wananchi wa Kilosa, Ulanga, Kilombero, Mvomero, Gairo na Morogoro vijijini.

Wakati katika Mkoa wa Pwani, timu ya maafisa wa TRA imelenga kuwafikia wafanyabiashara wote wa maeneo ya Kibaha, Kibiti, Kisarawe, Mkuranga, Chalinze na Bagamoyo ambapo kampeni hiyo imeanza tarehe 11 na itamalizika tarehe 17 Novemba, 2019.

POLISI ARUSHA WAKAMATA BUNDUKI MBILI ZA KIVITA NA NYARA ZA SERIKALI

$
0
0
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Jonathan Shana akiwaonyesha waandishi wa Habari Meno ya Tembo yaliokamatwa na kikosi kazi cha polisi KDU Tanapa Hifadhi ya Ngorongoro kwenye kijiji cha NAAN Tarafa ya Loliondo mpakani mwa Tanzania na Kenya kama zinavyoonekana pichani picha na Ahmed Mahmoud Arusha
Nyara za serikali zilizokamatwa na jeshi la Polisi mkoani hapa huko wilayani Ngorongoro Tarafa ya Loliondo kwenye Kijiji cha NAAN ikiwemo nyama ya Twiga waya za kutegea bunduki mbili simu sita mashine mbili za kuwekea alama za videlo zinazotumia na mawakala wa makampuni ya simu Picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
…………………………………………..

Na Ahmed Mahmoud Arusha
JESHI la polisi mkoani hapa limefanikiwa kukamata bunduki mbili za kivita pamoja na nyara za serikali ambazo ni nyama ya twiga pamoja na vipande viwili vya meno ya tembo sanjari na silaha za jadi yakiwemo mapanga,sime na visu.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa,Jonathan Shana alizitaja silaha hizo kuwa ni AK 47 yenye namba 174364 ikiwa na risasi 6 kwenye magazine na G3 yenye namba A36011858 ikiwa na risasi 9ndani ya magazine na kwamba zilikamatwa katika eneo la Naani lililopo katika
mpaka wa Tanzania na Kenya tarafa ya Loliondo Mkoani hapa.

Alisema kukamatwa kwa silaha hizo kunatokana na ushirikiano kati ya jeshi la polisi,Tanapa,Hifadhi ya Ngorongoro,kikosi dhidio ya ujangili(KDU)Kanda ya kaskazini na kikosi kazi cha taifa kinachopambana na ujangili kanda ya ziwa katika operesheni inayorndelea huko Loliondo.

“Bunduki hizo zilipatikana baada ya majibizano ya risasi baina ya kikosi kazi hicho kabambe na majangili mara baada ya kuona mashambulizi yamezidi majangili hao walitelekeza silaha hizo na kukimbilia nchi jirani,hata hivyo kikosi kikosi hicho kilifanikiwa kumjeruhi kwa risasi jangili mmoja ambaye pia alifanikiwa kukimbia huku akivuja damu”alisema Shana.

Kamanda huyo wa polisi aliongeza kuwa mnamo tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka huu katika eneo la Oleng’usa kijiji na kata ya oloipiri ndani ya eneo la pori tengefu la Loliondo walifanikiwa kukamata watu wawili wanaojihusisha na ujangili ambao ni Yamhanga Mwita(19)na Chacha
Marwa(20) wakazi wa Serengeti Mkoani Mara wakiwa wameuwa Twiga.

Alisema kuwa watuhumiwa hao walikutwa wakiwa wanaendelea kuanika nyama hizo porini kwa ajili ya kusafirisha baada ya kuwa wamezikata vipande vipande ambapo ndio waliokutwa na panga,sime mbili,kisu tochi pamoja na nyaya za kutegea wanyama zikiwa katika mafungu saba.

Kuhusu meno ya tembo alisema kuwa tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka huu majira ya 17:40,maeneo ya mbuyuni wilayani Arumeru waliwakamata watu watano wakiwa na meno hayo pamoja na pikipiki mbili aina za Kinglion namba T917 BUA na Sunlag namba MC 819 ACD ambapo walitokea wilayani Simanjiro mkoani Manyara walipokuwa wameyahifadhi na kwamba walikuja Mkoani hapa kwa ajili ya kuyauza.

Kadhalika Kamanda Shana alisema kuwa polisi inawashikilia Juma Yahaya(33)na Amani Mbise(32) wanaojishughulisha na kusajili laini za simu,wakazi wa jijini hapa kwa tuhuma za kutumia jina la Gavana wa benki kuu ya Tanzania(BOT)Profesa Frorence Luoga katika mitandao ya kijamii na kuwatapeli watu mbalimbali kwa kutumia jina hilo ambapo baada ya upelelezi wamekiri kosa hilo.

“Baada ya kuwapekuwa watuhumiwa tuliwakuta na simu 6,mashine mbili ya kusajili kwa alama za vidole,laini mbalimbali,vitambulisho 9 ya wateja ambao walishawasajilia laini zao za simu na kwamba tumebabaini mtuhumiwa huyu anamiliki jumba la kifahari eneo la Sombetini jijini hapa hali ambayo aiendani na kipato chake”alisema

Aliongeza kuwa pia jeshi la polisi kwa kushirikiana na Idara ya ya ustawi wa jamii jiji la Arusha imefanya operesheni ya kuwaondoa watoto wadogo wanaofanya biashara mbalimbali ikiwemo kubebeshwa mizigo kati masoko mbalimbali ya jijini hapa ambapo waliwakamata watoto 105 ambapo kati yao 46 wana umri chini ya miaka 18 na 59 wana umri wa zaidi ya
miaka 18.

MLELA, HEMED PHD NDANI YA TAMTHILIA YA KAULI

$
0
0
 Msanii wa Bongomuvie, Yusuf Mlela akizungumza na waandishi wahabari wakati akitambulisha kazi yake mpya ya tamthilia ya Kauli aliyomshirikisha Hemed Suleiman maarufu kama Hemed PHD na wengine wengi itakayorushwa kwenye mtandao wa kuuza na kununua kazi za sanaa wa Swahiliflix
Msanii wa Bongomovie Hemed Suleiman maarufu kama hemed PHD  akizungumza na waandishi wahabari wakati wa kitambulisha kazi mpya ya tamthilia ya Kauli ya Yusuf Mlela itakayorushwa kwenye mtandao wa kuuza na kununua kazi za sanaa wa Swahiliflix.

        Na Khadija seif, Michuzi TV
MSANII wa Bongomovie Yusuf Mlela awahimiza wasanii kubadilisha soko la filamu kwa kutengeneza filamu zenye maudhui yanayogusa jamii zaidi.

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa utambulisho wa tamthilia yake mpya "Kauli" ambayo wasanii kama hemed phd na wengine wengi wameshiriki katika tamthilia hiyo.

Hata hivyo amesema tamthilia hiyo itakua ikipatikana kwenye mtandao wa kuuza na kununua kazi za filamu wa Swahiliflix.

"Kutokana na teknolojia kukua kwa kasi zaidi kwa sasa hata wadau wa sekta hii ya filamu wameamua kuleta vitu vya tofauti zaidi ili kufanya kazi za sanaa kuendelea kuishi na kupatikana kwa urahisi zaidi na ndio maana Swahiliflix wameleta uhondo kwenye viganja vyetu unapakua filamu kupitia simu ya mkononi,kompyuta au hata vifaa vingine vyenye uwezo wa kupata mtandao,"

Huku msanii mwenzie Hemed phd ameeleza jinsi ya tamthilia ya Kauli ilivyobeba maudhui ya kitanzania zaidi na kufanya utofauti na tamthilia zingine zinazotumia tamaduni za nje ya nchi.

"Ifike wakati Sanaa yetu wenyewe iwe ndo chanzo kikuu Cha kutangaza utalii,tamaduni na hata lugha yetu kwani mara nyingi tumekua tukitumia vitu ambavyo ni vya wenzetu ila kupitia tamthilia ya Kauli tutaona jinsi ya mipangalio ilivyopangwa kuanzia kwa mtunzi mwenyewe,waandaaji pamoja na waongozaji kwa ujumla.

Hata hivyo hemed amesema zamani wasanii walikua hawawezi kufanya vitu kwa upana zaidi kutokana na kukosa baadhi ya vifaa ili kuboresha kazi zao.

'' Kuongeza kwa Tuzo mbalimbali mfano tuzo za sinema zetu,ziff na nyingine nyingi Ni kipimo tosha kuwa soko la filamu kwa sasa limeimarika na ndio maana wadau wanaleta vitu kama hivo kwa wingi ili kuleta ushindani wa kibiashara kwa wasanii na waandaaji wa filamu".

DC CHONGOLO ASIMAMA KIDETE NA WANAOZURUMU NYUMBA , ATOA ONYO KALI KWA WAHUSIKA, BI SHARIFA ARUDISHIWA NYUMBA YAKE

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akiwasikiliza mashuhuda wanaofahamu kuzurumiwa kwa nyumba ya Bi Sharifa Mbaruku mara baada ya kufika katika eneo hilo mapema leo asubuhi.
Muonekano wa nyumba aliyozurumiwa Bi Sharifa Mbaruku mkazi wa Magomeni mzimuni miaka mitatu iliyopita.
Bi Sharifa Mbaruku ,aliyezurumiwa nyumba yake akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurudishiwa nyumba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo mapema leo asubuhi
Baadhi ya wananchi waliofika katika eneo la nyumba ya Bi Sharifa Mbaruku aliyezurumiwa kwa kipindi cha miaka mitatu wakishuhudia akirudishiwa nyumba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo.

…………………….

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amesimamia haki na hivyo kuwezesha kurudishwa kwa Nyumba ya mkazi wa Magomeni Mzimuni,Bi Sharifa Mbaruku aliyenyang’anywa kwa muda wa miaka mitatu iliyopita.

Mhe. Chongolo alichukua maamuzi hayo leo alipofika kwenye nyumba ya Bi Sharifa ikiwa ni baada ya bibi huyo kupeleka malalamiko ya kudai kuzurumiwa na Bi Magrethi ambaye kwa sasa inadaiwa kuwa anaishi nje ya Nchi.

Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kufika katika nyumba hiyo ,Mhe. Chongolo amesema kuwa aliyemuondoa kwenye nyumba hiyo mwaka 2016 alifanya makosa na kwamba hakuwa na haki ya kumiliki nyumba hiyo.

Amefafanua kuwa kazi ya serikali ya awamu ya tano ni kutetea wanyonge wanaozurumiwa haki zao na kwamba akiwa Mkuu wa Wilaya hiyo amerudisha umiliki wa nyumba hiyo kwa mhusika ambaye ni Bi Sharifa.

Amesema “kuanzia hivi ninavyozungumza unarudi kwenye nyumba yako rasmi, wewe ndio mmiliki wa nyumba hii, kwahiyo nendeni mkaondoe mabati yote ambayo yamezungushiwa na sisi kama serikali tutawachukulia hatua wote waliohusika na mchezo huu.

Amefafanua kuwa kilichotendeka ni uonevu wa hali ya juu na kwamba serikali itamchukulia hatua kazi za kisheria kwani aliyemtoa alikuwa ameuziwa nyumba namba 159 kama ambavyo alikuwa ameuziwa mwenye namba 154.

“ Baada ya Magreth kuuziwa iwe ilikuwepo au haikuwepo, hakuwa na mamlaka ya kuja kuchukua ulichouziwa wewe, alitakiwa atafute alichouziwa yeye na hata kama angekikosa alipaswa kurudi kwa aliyemuuzia nasio kukufuata wewe, kwahiyo utaendelea kuishi kwenye nyumba yako kwa sababu ulifuata sheria na taratibu zote” amefafanua Mhe. Chongolo.

Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo ametoa agizo na kuwataka wote wenye tabia ya kupora nyumba za watu hasa masikini na wanyonge kuacha mara moja kwani hatamuonea haya mtu yeyote aliyekuwa kwenye manispaa yake.

Kwaupande wake Bi Sharifa aliyezurumiwa nyumba hiyo, amesema kuwa Disemba 27 mwaka 2016 akiwa amelala ilikuja gari ya polisi wakiwa na diwani wa Kata ya Magomeni wakati huo Ally Kondo pamoja na Kuruthumu Ramadhani walimtolea vitu nje na kumtaka kuondoka katika nyumba hiyo bila kutoa maelezo yoyote.

Ameeleza kuwa hakujua sababu za yeye kuondolewa katika nyumba hiyo kwakuwa aliyemtoa alikuwa na nyumba yenye namba 159 Bolock X nakusema kuwa kilichofanyika ni uonevu na hivyo kumshukuru Mhe. Chongolo kwakuwasaidia masikini kurudishiwa haki zao.

“ Mhe. Mkuu wa Wilaya nakupongeza sana baba kwakutujali masikini, mungu akubariki na akupe maisha marefu , hata Mahakama pia inachangia kwakuwa awali ilikuja toleo la kwanza lilionyesha 159 Block four, toleo la pili 159 Block eigth, toleo la tatu halikuwa na namba ya nyumba kwakweli huu ni uonevu” amesisitiza Bi Sharifa.

WADAU KANDA YA ZIWA WATOA MAONI SERA YA MAENDELEO YA WANAWAKE NA JINSIA

$
0
0
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Emil Kasagara akifungua kikao kazi cha wadau wa maendeleo ya Wanawake na Jinsia waliokutana na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Grace Mwangwa akitoa maneno ya awali kabla ya ufunguzi wa kikao kazi cha wadau wa maendeleo ya Wanawake na Jinsia waliokutana na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.
Mshauri Elekezi Prof. Linah Mhando akifafanua jambo kwa Wadau wa maendeleo ya Wanawake na Jinsia katika kikao kilichowakutanisha na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.
Wadau wa Maendeleo ya Wanawake na Jinsia wakifuatilia majadiliano katika kikao kilichowakutanisha na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.
Wadau wa Maendeleo ya Wanawake na Jinsia wakifanya majadiliano katika kikao kilichowakutanisha na Wizara kujadili na kutoa maoni katika kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

………….

Na Mwandishi Wetu Mwanza

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekutana na wadau wa maendeleo ya wanawake na Jinsia kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa katika kufanya tathimini ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 na Mkakati wa utekelezaji wa mwaka 2005 ili tathimini hiyo isaidie kufanya mapitio na maboresho ya Sera itakayozingatia makubaliano ya mikataba mbalimbali, Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Mpango wa pili wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano.

Haya yameelezwa leo mkoani Mwanza na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Grace Mwangwa wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kilichowakutanisha wadau wa maendeleo ya wanawake na Jinsia kutoka mikoa ya Mwanza. Mara, Kagera, Geita, Simiyu, Shinyanga na Kagera na Wizara.

Bi. Grace amesema Wizara ndio yenye jukumu ya utekelzaji wa Msualaya jinsi nchini yanazingatiwa na hivyo ili yaweze kutekelzwa yanahitaji kuwa na Sera na Mikakati ni muhimu katika kuleta maendeleo ya wanawake na jinsia.Amesisitiza kuwa madhumuni ya Sera iliyopo yalikuwa ni kutoa mwelekeo ambao ungehakikisha kuwa mipango, Mikakati na shughuli mbalimbali za uongozi na maendeleo katika kila Sekta na Taasisi inazingatia usawa wa kijinsia.

Ameongeza kuwa lengo kuu la kupitia Sera hiyo ni kuifanya iendane na wakati na iwezi kubeba mabadiliko yaliyojitokeza katika miaka kumi na tisa tangu kuandaliwa kwake mwaka 2000 ikiwemo changamoto katika utekelezaji wa Sera hii ikiwemo mapungufu yake na nini kifanyike ili kuiboresha Sera ili kueandana na wakati husika.

“Tunahitaji kupata maoni yenu tunahitaji maelekezo yenu nini hakikuzingatiwa tunaomba maoni yenu ili tuwe na Sera itakayosaidia maendelo ya Waanwake na Jinsia nchini ”Alisema Bi. Grace

Bi Grace ameongeza kuwa bali na kukutana na wadau na kupata maoni pia watakutana na vikundi vya kijamii na mwananchi mmoja mmjoja kwa kupita katika baadhi ya vijiji vya mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kuwafuata walipo ili kuweza kupata maoni yao ili kuweza kiboresha Sera hiyo.

Akifungua kikao kazi hicho kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Bw. Emil Kasagara amesema kuwa Kikao hicho kinatarajia kufikia malengo ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake katika kufikia maendeleo jumuishi hususan katika Sekta ya Afya, Elimu, Kilimo na Masuala ya kifedha, uwezeshaji wa wanawake katika nafasi za uongozi na siasa, mazingira na Uzazi na Afya ya Mtoto na kukusanya Taarifa na Takwimu zitakazowezesha kuandaa Rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia.

Ameongeza kuwa kikao kazi hicho kitawezesha kukusanya maoni yatayowezesha kuwa na Sera Shirikishi inayozingatia masuala yote muhimu na kupata uelewa wa pamoja kuhusu wajibu wa Serikali na wadau katika uwepo wa Sera ya maendeleo ya Wanawake na Jinsia .

“Natumai mtatumia muda huu vizrui kujadiliana na kupata maoni yatakayowezesha kupata Sera mbayo itakuwa imekidhi mahitaji ya wakati tulionao na hata kuhakisi yatakayojitokeza hapo mbele” Alizema Bw. Kasagara

Mshauri Elekezi Prof. Linah Mhando ameeleza maeneo yanayopewa kipaumbelekatika Sera mpya ni Jinsia na maendeleo ya Mji/Vijiji, Jinsai na haki za umiliki ardhi, Jinsia, maji na usafi wa mazingira, Haki za mtoto wa kike, Jinsia na ulemavu, Ukatili wa Kijinsia,jinsia, sayansi ,teknolojia na ufumbuzi , Jinsia, afya uzazi na Ukimwi, Jinsia, uongozi na maamuzi, Jinsia, ajira na kazi, Jinsia, Sheraia na haki za binadamu na Jinsia na hifadhi ya jamii.

Ameyataja maeneo mengine kuwa ni Jinsia na kuwawezesha wanawake kiuchumi, Jinsia na ujumuishwaji wa kifedha, Jinsia na mabadiliko ya tabianchi,Jinsia na Nishati, Jinsia na Miundombinu, Jinsia na Takwimu, Jinsia na Madini, Jinsia na vyombo vya habari na Mawasiliano, Jinsia na Mila na Desturi, Jinsia na Jmii za ufugaji, Ufadhili na Jinsia na Jinsia na uvuvi.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ipo katika machakato wa kukusanya maoni kwa wadau kutoka Kanda saba za Tanzania Bara ili kuwezesha maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya Mwaka 2000.

KANYASU ATEMBELEA SHAMBA LA MITI LA SAO HILL KUJIONEA HEKTA 1000 ZA MITI ZILIZOUNGUA KWA MOTO NA KUSABABISHA HASARA YA ZAIDI SH.BILIONI 5

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine John Kanyasu jana akikagua gari aina ya Isuzu lori lililoteketea kwa moto ulitokea mwishoni mwa wiki kwa muda wa siku 6 katika Shamba la misitu la Sao Hill ambapo jumla ya hekta za miti 1000 aina ya misindano na mikaratusi zimeathiriwa na moto na kusababisha jumla ya hasara ya kiasi cha shilingi bilioni tano. ( Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii) Miti aina ya mikaratusi iliyoathiriwa na moto uliotokea mwishoni mwa wiki uliosababishwa na wananchi wanaoandaa mashamba kwa ajili ya kilimo ambapo jumla y ya hekta za miti 1000 aina ya misindano na mikaratusi zimeathiriwa na moto na kusababisha jumla ya hasara ya kiasi cha shilingi bilioni tano.


Gari aina ya ISUZU lori lililotekea kwa moto ulitokea mwishoni mwa wiki kwa muda wa siku 6 katika Shamba la misitu la Sao Hill ambapo jumla ya hekta za miti 1000 aina ya misindano na mikaratusi zimeathiriwa na moto na kusababisha jumla ya hasara ya kiasi cha shilingi bilioni tano



Miti aina ya misindano yenye miaka miwili iliyoathiriwa na moto uliotokea mwishoni mwa wiki uliosababishwa na wananchi wanaoandaa mashamba kwa ajili ya kilimo ambapo jumla y ya hekta za miti 1000 aina ya misindano na mikaratusi zimeathiriwa na moto na kusababisha jumla ya hasara ya kiasi cha shilingi bilioni tano.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kutembelea sehemu ya shamba la miti la Sao Hill baada ya kujionea hasara kubwa iliyosabishwa na moto.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akisalimiana na baadhi ya watuishi wa shamba la miti la Sao Hill mara baada ya kuwasili kwa ajilli ya kutembelea shamab hilo lililoungua kwa muda wa siku sita na kusababisha hekta 1000 kuungua kwa moto na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 5.



…………

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu jana amefanya ziara ya kutembelea sehemu ya Shamba la miti Sao Hill lilipo wilayani Mufindi mkoani Iringa ambalo limeathiriwa na moto.

Moto huo uliotokea mwishoni mwa wiki katika kipindi cha siku sita na umeathiri zaidi ya hekta 1000 za miti likiwemo shamba hilo la Serikali pamoja na mashamba mengine ya Taasisi zingine na watu binafsi.

Katika shamba hilo pekee jumla ya hekta 600 za miti aina ya misindano na mikaratusi imeathirika na moto huku vyanzo vya moto huo vikidaiwa kuwa ni wananchi kuandaa mashamba kwa ajili ya kilimo, urinaji wa asali pamoja na shughuli za uvunaji miti.

Mbali ya hasara hiyo, Moto huo pia umeleta madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kumuunguza mtumishi wa kiwanda cha Sao Hill alipokuwa katika jitihada za kuzima moto huo,

Aidha, moto huo umeteketeza gari aina Isuzu Lori. mizinga ya nyuki 24 kati ya 83 , mbao, magogo pamoja na mashine za kuchania mbao zilizokuwemo katika shamba hilo.Akizungumzia kuhusu hasara hiyo, Naibu Waziri Kanyasu amesema moto huo umesababisha hasara ya zaidi ya jumla ya kiasi cha shilingi bilioni tano huku ukiwaacha wananchi waliokuwa na mashamba ya miti kwenye wakati mgumu.

Amesema kwa mwaka jana pekee Shamba hilo la miti la Sao Hill, moto huo uliunguza hekta 400 za miti na hivyo kusababisha hasara ya zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 1.Kufuatia hali hiyo Waziri Kanyasu ameuagiza Uongozi wa Shamba hilo kuiuza haraka miti iliyokuwa imefikia umri wa kuanzia miaka 10 hadi miaka 27.

Amesema taratibu hizo zifanyike haraka kwa vile miti iliyoungua kwa moto ikiendelea kubaki kama ilivyo huharibika kwa haraka na hivyo kupelekea kutokufaa kwa mbao.

Hata hivyo, Mhe. Kanyasu amesema licha ya kuwa miti hiyo itauzwa , Shamba hilo limepata hasara kubwa kwa vile sehemu kubwa ya miti iliyoathiriwa na moto ni yenye umri wa miaka mitatu ambayo haiwezi kutumika kwa matumizi yoyote.

Kufuatia hali hiyo Naibu Waziri Kanyasu ameutaka Uongozi wa wilaya ya Mufindi kuandaa sera itakayowazuia wananchi kuandaa mashamba yao katika kipindi cha msimu wa kilimo kwa kutumia moto ili kuzuia hasara kubwa inayotokea kila mwaka.

Aidha, Ameuagiza Uongozi wa shamba hilo kuja na mkakati mpya wa namna ya kukabiliana na janga hilo la moto ikiwa ni pamoja na kuandaa kingo zenye ukubwa wa kutosha kati ya shamba moja na jingine ili kuzuia moto endapo utaweza kutokea usiweze kuathiri sehemu kubwa ya miti.

”Matukio haya ya moto yanayotokea kila mwaka inabidi yatufundishe namna ya kuweza kukabiliana nayo, tusipotaka kujifunza mwakani tutapoteza hekta nyingi zaidi” alisisitiza Kanyasu.

Amesema licha ya kuwa inaonekana kulikuwa na maandalizi ya kutosha kutoka kwenye vikosi vya kuzuia moto lakini hata hivyo kuna haja ya kutumia teknolojia mpya ya namna ya kupambana na moto huo uliounguza hekta 1000 kwa muda wa masaa mawili.

Akizungumzia kuhusu hatua zilizochukuliwa hadi hivi sasa za kukabiliana na majanga ya moto katika shamba hilo, Mhe. Kanyasu amesema licha ya kuwa shamba hilo limeagiza gari la zima moto lenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 800 lakini hata hivyo kutokana na jiografia la eneo hilo halitaweza kuleta ufanisi.

kwa upande wake Kaimu Meneja wa Shamba hilo, Sillima Kombe amesema ili kukabiliana na majanga hayo ya moto katika shamba hilo la Sao Hill lenye ukubwa hekta 135,903 linahitaji ndege zisizo na rubani tatu, Helikopta 3 pamoja Darubini za kisasa

SERIKALI YAPIGA HATUA KUBWA UREJESHWAJI WA KODI YA ONGEZEKOLA THAMANI

$
0
0
Poleni na Majukumu, naomba msaada wenu wa Story hii kutoka Dodoma

……………………………………..

Na. Peter Haule, WFM, Dodoma

Serikali imefanikiwa kuwarejeshea wafanyabiashara na wawekezaji Kodi ya Ongezeko la Thamani-VAT baada ya uhakiki wa madai yao kwa lengo la kuimarisha kipato cha mtu mmoja mmoja na uwekezaji nchini.

Hayo yamesemwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Khadija Nassir Ali, aliyetaka kujua namna Serikali ilivyojipanga kurejesha Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa wawekezaji ili kuimarisha uwekezaji.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, Serikali imelipa zaidi ya asilimia 90 ya VAT kwa watu waliokuwa wakidai Serikali baada ya kufanyika kwa uhakiki wa madai hayo, uhakiki unaendelea kwa asilimia kumi iliyobaki ili kujiridhisha kabla ya kufanya malipo.

“Tulikua na changamoto kubwa ya udanganyifu kwenye eneo la urejeshwaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani, hivyo Serikali ilianza mkakati wa kujiridhisha na kila muamala unaoletwa ili kuweza kuirejesha kwa wazalishaji, wanunuzi pamoja na viwanda vilivyopo nchini”, alieleza Dkt. Kijaji.

Aidha, akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Busega, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni, aliyetaka kujua maana ya dhana ya ukuaji wa uchumi kwa kuoanisha na Maisha ya wananchi, Dkt. Kijaji alisema kuwa dhana hiyo inatafsiriwa kwa kuangalia upatikanaji, ubora na gharama ya huduma za jamii zinazotolewa na Serikali.

Alisema baadhi ya huduma hizo ni pamoja na elimu, afya, maji, umeme na miundombinu ya usafiri na usafirishaji inayosaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa na na matengenezo ya vyombo vya usafiri.

Dhana nyingine ya kutafsiri ukuaji wa uchumi na maisha ya wananchi ni ushiriki wa wananchi wenyewe katika shughuli za kiuchumi hivyo ukuaji wa uchumi ni matokeo ya ushiriki wa wananchi katika uzalishaji mali na huduma.

Alisema kuwa wananchi wanaoshiriki katika shughuli za uchumi wananufaika kwa tafsiri ya dhana ya ukuaji wa uchumi kupitia huduma za kijamii zinazotolewa na Serikali pamoja na matokeo ya shughuli zinazofanywa na mwananchi.

Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kufanya jitihada za kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara ili kila mtanzania aweze kutumia kikamilifu fursa zilizopo katika uzalishaji na huduma.

Naibu Waziri Dkt. Kijaji alisema kuwa uwekezaji katika viwanda utaongeza ajira na uzalishaji katika Sekta ya kilimo kwa kuwa Sekta hiyo inaajiri idadi kubwa ya watu nchini.

DC SAME ATANGAZA VITA NA MAJANGILI WANAOUA WANYAMA KWENYE HIFADHI

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki ametangaza vita mpya na majangili wanaoingia kwenye hifadhi na kuua wanyama kwamba hawatapata nafasi kutokana namna serikali ilivyojipanga kukabiliana nao huku akieleza watakaokamatwa watashughulikiwa kwa hatua kali za kisheria.

Pia amewataka wabadilishe biashara hiyo na sasa waanza kujikita kwenye kufanya ujenzi wa hoteli za kitalii ili waweze kujiingizia kipato badala ya kufikiria kuendelea kufanya vitendo vya ujangili kwenye hifadhi.

DC Staki aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna kama serikali walivyojipanga kuhakikisha wanapambana na vitendo vya ujangili vilivyopo kwenye maeneo yao ambapo alisema watu hao hawana nafasi kwenye wilaya hiyo.

“Labda tu niwaambie kwamba hifadhi zote zina askari nikihesabu majeshi yote niliyokuwa nayo hatutawapa nafasi kwani serikali wamejipanga na ukienda kwenye hifadhi zote ni askari kwa maana ya kuzuia watu wasiingie na kuuwa wanyama na kuharibu mazingira hivyo na ambao watasubutu kufanya hivyo tutawachukua hatua kali kama tukikuta mvua anadhamira mbaya na hifadhi zetu tumesimama imara tunataka vivutio hivyo vizazi vya sasa na na vijavyo vivikute”Alisema DC Staki.

Alisema kwamba kasi ya serikali ni kuhakikisha inafanya utalii unakuwa sehemu ya kiuungia mapato kwenye nchi hivyo wo hawawezi kufanya uzembe ambao utafanya vivutio hivyo kupunguza hadhi yake au kupunguza sifa yake ikiwemo wanyama na kuharibu mazingira.

Hata hivyo alisema kwamba hivi sasa wanafuatilia maeneo ambayo wanyama walikuwa wanapita waone kama maeneo hayo yameendeleza kiasi gani au hayaendelezwa kama hayajaendelezwa yaachwe wazi kusiwe na muingiliano kati ya shughuli za binadamu na wanyama ili kuona namna ya kufanya ili kuondoa hali hiyo.

Akizungumzia suala la wafugaji kuingia mifugo kwenye hifadhi hiyo Mkuu huyo wa wilaya anasema kwamba changamoto hiyo ilikuwa ni kubwa ilikuwa inawasumbua sana lakini miaka ya hivi karibuni kutokana na juhudi kubwa za kusimamia sheria na kutoa elimu kwa wafugaji mifugo idadi ya mifugo inayoingia ngombe na mbuzi wanaoingia kwenye hifadhi hiyo.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images