Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

HEKTA 357.3 ZA ITOA ZAKABIDHIWA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE

0
0
Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu Bi Emmy Hudson kutoka RITA akitoa Taarifa ya Uchunguzi wa Mgogoro wa Bodi ya Wadhamini Wakulima wa Chai Igominyi -Igominyi Tea Out grawers Association(ITOA)
Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu Bi Emmy Hudson (aliyesimama) kutoka RITA akizungumza na Waandishi wa Habari akitoa maelekezo ya mgogoro wa ITOA.Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi Sheria RITA Lina Msanga
Mkuu wa Wilaya ya Njombe (wa pili kulia)akiwa pamoja na Ujumbe kutoka Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu RITA na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe.



HYASINTA KISSIMA,AFISA HABARI-HALMASHAURI YA MJI NJOMBE

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) umetoa hatma ya Mgogoro uliokuwa ukihusisha Bodi ya Wadhamini wa Chai Igominyi –Igominyi Tea Out grawers Association (ITOA) mara baada ya Ofisi ya Kabidhi Wasihi Mkuu inayosimamia bodi za wadhamini kufanya uchunguzi na kubaini uwepo wa migogoro katika suala la udhamini na utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuhakikisha kuwa mazao ya Kimkakati yanakuwa chini ya ushirika na sio bodi za wadhamini, na kusabisha hekta 357.3 zilizokuwa zinamilikiwa na ITOA kukabidhiwa Halmashauri ya Mji Njombe.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson amesema kuwa Uchunguzi uliofanywa na timu ya Wataalamu kutoka Ofisi ya Msajili Vyama vya Hiari, Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu Ofisi ya Mrajisi na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri imebaini kukiukwa kwa taratibu kwa mujibu wa sheria zilizowamilikisha maeneo hayo.

“Lengo la mashamba waliyokabidhiwa ITOA ilikuwa ni kwa lengo la kuyaendeleza kupitia kilimo mkakati. Timu ya uchunguzi imebaini kuwa mashamba hayo hayakutumika kama yalivyokusudiwa. Yapo pia maelekezo ya Serikali yaliyotoewa kuwa Taasisi zote zinazojishughulisha na mazao ya kimkakati ikiwemo chai ziweze kujisajili kwenye vyama vya ushirika. 

Ofisi yangu imeelekeza kwamba mashamba hayo yarejeshwe kwenye Halmashauri ili iweze kupanga matumizi ambayo yatajielekeza katika kuendeleza zao la chai ambalo ni zao la Kimkakati.”Alisema Emmy

Aidha Bi Emmy amesema kuwa yapo mambo ambayo kwa kushirikiana na taasisi yake yanatakiwa kutekelezwa ndani ya siku thelathini ili kufanikisha maelekezo yaliyotolewa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri alisema kuwa mgogoro wa ITOA ni miongoni mwa changamoto zilizokuwa zinakabili wakulima wa chai kwa muda mrefu na amepongeza kwa jitihada zilizochukuliwa kwani kwa sasa Mashamba hayo yatakuwa chini ya Mkurugenzi na wakulima wa chai kuendelea kunufaika na kuishukuru RITA kwa maamuzi yaliyofikiwa.

WAKONGWE WA BONGO FLEVA WANOGESHA WASAFI FESTIVAL 2019

WANAMUZIKI NYOTA WAKONGWE WALIPOUNGANA KUFANYAN KAZI PAMOJA

0
0


Wanamuziki wakongwe kutoka bendi mbalimbali mwaka 2011 waliungana na kufanya mazoezi kwa asili ya onesho maalumu la sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika. Waimbaji ni pamoja na King Kikii, Hassan Rehani Bitchuka, John Kitime na Waziri Ally, Hamza "Komandoo" Kalala alipiga gitan la solo huku Juma Ubao akipiga Rythim huku tumba likipigwa na Ally Jamwaka wakaty Mafumu Bilali Bombenga, Joseph na Shaaban Lendi wakipuliza Sax.

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKESHA WA SHERERE ZA MAULID YA MTUME MUHAMMAD

0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, wakati akiwasili kwenye viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza, kumwakilisha Rais Magufuli, katika sherehe za Maulid, zitazofanyika Kitaifa mkoani humo. Novemba 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu, waliyohudhuria, katika sherehe za Maulid ya Mtume Muhammad, zilizofanyika Kitaifa mkoani Mwanza, Novemba 10, 2019
 Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu, waliyohudhuria, katika sherehe za Maulid ya Mtume Muhammad, zilizofanyika Kitaifa mkoani Mwanza, Novemba 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  
 Mjumbe wa Baraza la Ulamaa na Sheikh wa Mkoa wa Arusha, Sheikh Shaaban Juma, akizungumza kwenye sherehe za Maulid ya Mtume Muhammad, zilizofanyika Kitaifa mkoani Mwanza, Novemba 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, katika sherehe za Maulid, zitazofanyika Kitaifa mkoani Mwanza, kwenye viwanja vya Furahisha. Waziri Mkuu, amemwakilisha Rais Magufuli, katika sherehe hiyo. Novemba 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, katika sherehe za Maulid, zitazofanyika Kitaifa mkoani Mwanza, kwenye viwanja vya Furahisha. Waziri Mkuu, amemwakilisha Rais Magufuli, katika sherehe hiyo. Novemba 10, 2019
 Mwananchi mkazi wa Dar es Salaam, Mohammed Yusuf, akifurahia sherehe za Maulid, zilizofanyika Kitaifa mkoani Mwanza, kwenye viwanja vya Furahisha. Novemba 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 


  Baadhi ya viongozi wa dini, wakiwa katika sherehe za Maulid, zilizofanyika Kitaifa mkoani Mwanza, kwenye viwanja vya Furahisha, Novemba 10, 2019. Kutoka kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Hauzat, Sheikh Mohammed Abdi na  Mkurugenzi wa Hauzat, Jaafar Aswad.
 Baadhi ya viongozi wa dini, wakiwa katika sherehe za Maulid, zilizofanyika Kitaifa mkoani Mwanza, kwenye viwanja vya Furahisha, Novemba 10, 2019. Kutoka kushoto ni Sheikh wa Mkoa Mara na Sheikh wa Mkoa wa Kagera, Haruna Kichwa Buta. 
 Waumini wa Kiislamu wakiwa katika sherehe za Maulid, zilizofanyika Kitaifa mkoani Mwanza, kwenye viwanja vya Furahisha. Novemba 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 



MAGUFULI ABATILISHA UFUTAJI SHAMBA LA EKARI 1000 MVOMERO

0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia moja ya Majalada katika ofisi ya Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero jana. Kulia kwa Lukuvi ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mwl Mohamed Utaly na kulia ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda maalum ya Morogoro Erick Makundi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia moja ya Majalada katika ofisi ya Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero jana.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na viongozi wa wilaya ya Mvomero pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi mkoa wa Morogoro. Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mwl Mohamed Utaly.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

………………….

Na Munir Shemweta, WANMM MVOMERO

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amebatilisha pendekezo la kufutwa shamba lenye ukubwa wa ekari 1000 lililopo Kidunda wilayani Mvomero mkoani Morogoro linalomilikiwa na Cecilia George Rusimbi.

Uamuzi wa Dkt Mafuli kubatilisha ufutaji shamba hilo unatokana na kubainika kuwa pendekezo lililowasilishwa la kufutwa shamba hilo kwa madai ya kutoendelezwa kutokuwa za kweli na ulilenga kumdhulumu mmiliki wake.

Akitangaza uamuzi huo wa Raisi jana wilayani Mvomero, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema, baada ya kufuatilia mashamba yaliyopendekezwa kufutwa Dkt Magufuli alibaini taarifa alizopelekewa za kufuta shamba Cecilia hazikuwa sahihi na hivyo kuamua kubatilisha pendekezo lililowasilishwa kwake na kumpatia haki yake mmiliki.

Kufuatia hali hiyo Waziri Lukuvi aliwaonya Aaafisa ardhi nchini kuhakikisha wakati wa kufanya zoezi la ukaguzi/Upekuzi wa mashamba yasiyoendelezwa wanazingatia haki pamoja na kufuata sheria badala ya kufanya kazi hiyo kwa upendeleo au kumuonea mtu.

Hata hivyo, Waziri wa Ardhi alisema, utendaji kazi katika wilaya ya Mvomero umekuwa wa hovyo na usiozingatia maadili jambo linalopelekea wilaya hiyo kuongoza katika mkoa wa Morogoro kuwa na migogoro mingi ya ardhi sambamba na malalamiko mengi ya wananchi dhidi ya ofisi ya ardhi.

‘’Baadhi ya watumishi katika ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Mvomero mnajifanya ni Maafisa ardhi au Wapima wakati hamkuajiriwa kwa nafasi hiyo, mnasaini nyaraka za ardhi na kuwaumiza wananchi’’ alisema Lukuvi

Kwa upande wake Cecilia George Rusimbi alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kubatilisha ufutaji sahamba lake na kuuelezea uamuzi huo kuwa umezingatia haki na kusikia kilio chake ambapo alisema umempa faraja baada ya kuhangaika sana kuhusiana na shamba hilo.

‘’ Nimemiliki shamba tangu mwaka 1987 na kuhangaikia hati kwa muda mrefu na nimeshangazwa kuelezwa kuwa shamba langu liko katika mpango wa kufutwa kutokana na kutoendelezwa, hii imenifanya kuishi kwa wasiwasi’’ alisema Cecilia.

Waziri Lukuvi ameagiza shamba hilo la kilimo cha Michikichi, Mitiki na Bamboo kupangwa upya na mmiliki wake kupatiwa hati kulingana na upimaji utakaofanywa na kumtaka kuliendeleza kwa mujibu wa sheria.

Sambamba na sakata la shamba la Cecilia, Lukuvi aliagiza kupunguzwa ukubwa wa Shamba Sangasanga na Lubango lililodaiwa kuwa na ukubwa wa ekari 1,103 wakati uhalisia wa shamba hilo ni ekari 500 na kuagiza mmiliki wake kurudisha hati ili apatiwe hati ilinayolingana na uhalisia wake na ekari 603.5 zilizoongezwa zitabaki kuwa ardhi ya akiba.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mwl Mohamed Utaly alieleza kuwa wilaya yake ina tatizo kubwa la migogoro ya ardhi pamoja na jitihada kubwa inayofanywa na ofisi yake kukabiliana na tatizo hilo na kuongeza kuwa mingine inachochewa na uhamasishaji unaowafanya wananchi kukata tamaa.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alitembelea ofisi ya Ardhi katika halmashauri ya Mvomero na kubaini ‘madudu’ katika ofisi hiyo ambapo alibaini baadhi ya majalada ya wananchi waliomba kumilikishwa ardhi tangu mwaka 2012 katika halmashauri hiyo kushindwa kupatiwa hati huku.

Hali hiyo ilimfanya Waziri Lukuvi kumuagiza Kaimu Kamishana Msaidizi wa Ardhi Kanda Maalum ya Morogoro Erick Makundi kuhakikisha wale wote walioomba hati na kutumiza vigezo vya kupatiwa hati wanapatiwa kufikia mwezi ujao Desemba 2019. Pia ameagiza kufuatiliwa majalada 300 ambayo wamiliki wake wamekamilisha taratibu za kupatiwa hati lakini hawajapatiwa.

Sambamba na hilo Lukuvi aliagiza wafanyakazi wa ofisi ya ardhi katika halmashauri hiyo wanaojitolea kutosaini nyaraka zozote za ardhi kwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakishiriki kutoza tozo kwa gharama za juu za shilingi 50,000 wakati gharama halisi ni 20,000.

CCM YAPITA BILA KUPINGWA KWENYE VIJIJI 6,248 NA MITAA 1,169, WALIOENGULIWA SASA KUSHIRIKI UCHAGUZI HUO

0
0

Charles James, Michuzi TV

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kupita bila kupingwa kwenye maeneo mbalimbali nchini katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kutokana na kukosekana kwa wagombea wa upinzani kwenye maeneo hayo.

CCM imepita bila kupingwa katika vijiji 6,248 kati ya vijiji 12,319 sawa na asilimia 51 ambapo kwa upande wa mitaa wamepita bila kupingwa katika mitaa 1,169  kati ya mitaa 4,262 sawa na asilimia 27 huku kwenye vitongoji wakipita kwa asilimia 58.

Akizungumza jijini Dodoma leo wakati akitoa taarifa ya zoezi la uchukuaji fomu, urudishaji, uteuzi, pingamizi na rufaa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo amewataka pia wagombea ambao walichukua fomu na kuzirejesha basi washiriki uchaguzi huo ifikapo Novemba 24 ambapo pia amefuta  maamuzi ya kuwaengua wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.

Waziri Jafo amesema licha ya vyama vya Chadema na ACT-Wazalendo kutangaza kujiondoa kwenye uchaguzi huo bado wagombea wao waliendelea kurudisha fomu ba kufuatilia rufaa zao jambo ambalo linaonesha jinsi gani wanavyohitaji kushiriki uchaguzi huo lakini wananyimwa haki yao na vyama vyao.

" Hata kabla ya zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu halijafungwa bado kuna wanachama walikua wanarudisha fomu na kuendelea na mchakato, hii inaonesha jinsi gani ambavyo watu wanahitaji kushiriki uchaguzi huu wa kidemokrasia lakini wananyimwa fursa hiyo na vyama vyao.

Sasa safari hii hakuna kurudisha Mpira kwa kipa, hivyo kupitia kanuni no 52 ninatoa muongozo kwamba wagombea wote ambao waliteuliwa na kudhaminiwa na vyama vyao na kufanikiwa kurejesha fomu zao za uteuzi kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi wana sifa ya kupigiwa kura na wananchi katika uchaguzi huu kulingana na maeneo wanayogombea," Amesema Mhe Jafo.

Amesema kwa kuwa imeonekana wazi wananchi kutoka vyama mbalimbali wamekua na nia kubwa ya kushiriki uchaguzi huo licha ya vyama vyao kutokueka umuhimu katika kuwaelekeza wanachama wao mambo muhimi, Mamlaka ya uchaguzi imeona ni vema kutoa nafasi kwao kushiriki kwani imejiridhisha licha ya vyama hivyo kujitoa bado wanachama wao waliendelea na mchakato wa zoezi la urejeshaji wa fomu.

Waziri Jafo amesema mambo pekee ambayo yanaweza kumuengua mtu kwenye uchaguzi huo ni kutokua Raia wa Tanzania, Kutojiandikisha katika Kijiji, Mtaa au Kitongoji husika, Kujiandikisha mara mbili, Kutodhaminiwa na Chama chake cha Siasa, Wagombea zaidi ya mmoja kutoka Chama kimoja kurejesha fomu katika nafasi moja.

Amesema katika zoezi hilo la uchukuaji na urejeshaji wa fomu kulikua na changamoto kubwa kwa wagombea wengi kufanya makosa ya kikanuni yaliyopelekea kutoteuliwa.

" Ndugu zangu kulikua na makosa mengi katika zoezi hili la urejeshaji fomu, baadhi ya makosa hayo ni pamoja na kujidhamini wenyewe, kutojaza fomu namba IV, kutofautiana kwa majina, kutojaza fomu kwa ukamilifu, kukosea umri ambapo makosa hayo yalitokana na vyama kushindwa kuwajibika katika kuwaelekeza wanachama wao jambo ambalo limesababisha zaidi ya mapingamizi 15, 380 kuwasilishwa," Amesema Jafo.

Amesema msimamizi wa uchaguzi ataanza kupokea ratiba za kampeni kutoka vyama vyao Siasa kuanzia Novemba 10 hadi 11 kwa ajili ya kuziunganisha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Dodoma leo kuhusiana na zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mitaa litakalofanyika Novemba 24 mwaka huu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akitoa taarifa ya zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu, uteuzi, pingamizi na rufaa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa. 

SERIKALI WILAYANI IKUNGI MKOANI SINGIDA YATAIFISHA MAGUNIA 121 YA MKAA

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo (katikati) akionesha magunia ya mkaa yaliyokamatwa baada ya kukiuka sheria ya misitu na nyuki katika msitu wa Sambalu mkoani Singida wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) eneo la tukio juzi. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ikungi (OCD), Fortunatus Biyacca na kulia ni Mshauri wa Jeshi la Akiba la wilaya hiyo, Kapteni Chabimia na kushoto ni Afisa wa Wakala wa Huduma ya Misitu (TFS) 
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akiwa aamini anachokiona kufuatia uharibifu mkubwa wa mazingira wa ukataji wa miti na kuchoma mkaa. Kushoto huyo mama ni Mfanyabiashara wa mkaa Rose Nari, kutoka mkoani Arusha ambaye amekamatwa kuhusiana na tukio hilo. 
Shehena ya magunia ya mkaa yaliyo kamatwa.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akisisitiza jambo eneo la tukio.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akiwaongoza wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya kukagua maeneo yaliyo haribiwa kwa kukatwa miti.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akisalimiana na mwananchi Baraka Musa ambaye anafanyashughuli za kilimo na ufugaji katika hifadhi hiyo ya Taifa ya Sambalu.
Hivi ndivyo hali ilivyo baada ya kukatwa miti katika hifadhi hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akizungumza na moja ya familia inayoishi ndani ya familia hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akizungumza na na Balozi wa Mtaa wa Makulunde, Hamis Juma kuhusu uharibifu huo wa mazingira ambaye alisema wanakata miti hiyo na kuchoma mkaa ambao wanauza gunia sh.5000 kwa ajili ya kupata fedha za kununulia mahitaji yao mengine ya kila siku.
Miti ikiwa imekatwa.
Maofisa wa TFS wanaohusishwa na tukio hilo wakiwa eneo la tukio. Kutoka kushoto ni Selemani Elifuraha na Isack Maluma aliyekutwa akimkabidhi stakabadhi ya malipo mfanyabiashara huyo.

Mfanyabiashara wa mkaa, Rose Nari, akizungumza na waandishi wa habari alisema wakati katazo hilo lilipokuwa linatoka mkaa huo ulikuwa umechomwa tayari.




Na Dotto Mwaibale, Singida

SERIKALI Wilaya ya Ikungi mkoani Singida imetaifisha magunia ya mkaa 121 yaliyokamatwa wakati yakitaka kusafirishwa kwa njia za ujanja baada ya kukiuka taratibu za sheria ya misitu na nyuki.

Na katika hatua nyingine serikali wilayani hapa imeomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kulichunguza tukio hilo ilikuweje vitolewe vibali vya kusafirisha mkaa huo wakati kulikuwepo na katazo na wamevitaka vyombo vya dola kumchukulia sheria mfanyabiashara aliyekamatwa na mkaa huo pamoja na maofisa wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) wilayani hapo waliohusika kutoa vibali hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo eneo la tukio katika Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Sambalu uliopo Kata ya Mang’onyi ambapo magunia hayo ya mkaa yalikamatwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo alisema kitendo hicho ni kibaya sana na kimekiuka sheria ya misitu namba 14 na namba 15 ya nyuki ni kitendo ambacho kinaathiri mazingira.

Alisema kwa mujibu wa sheria za misitu na uanzishwaji wa TFS ya mwaka 2010 kitendo walichokifanya hao maofisa wa TFS ni kinyume na taratibu kwani wao wametoa vibali vya kusafirisha mkaa huo wakidai ni kwa ruhusa yangu wakati sio kweli.

“TFS walikwenda polisi kuomba kibali cha kutaka wapewe askari kwa ajili ya kusindikiza mkaa huo kwenda mjini Singida kwa mauzo wakidai nimetoa kibali hicho wakati sio kweli nimempongeza mkuu wa polisi wa wilaya kwa kunishirikisha kwa kuniuliza” alisema Mpogolo.

Alisema baada ya kufika kituoni hapo aliwakuta maofisa hao wa TFS wakiwa tayari wamemuandikia risti mfanyabiashara huyo na ndipo walipowakamata na siku iliyofuata kamati nzima ya ulinzi na usalama wilayani hapo ilikwenda katika msitu huo na kujionea uharibifu mkubwa wa mazingira wa ukataji miti na uchomaji mkaa.

Mpogolo alisema baada ya kukamata magunia hayo serikali imeyataisha na baada ya kuyauza fedha hizo zitatumika kujengea maabara ya Shule ya Sekondari ya Ikungi.

Alisema kufuatia hatua hiyo mfanyabiashara aliyekamatwa na mkaa huo aliyetajwa kwa jina la Rose Nari kutoka mkoani Arusha kuwa atachukuliwa hatua za kisheria na wale maofisa wa TFS waliohusika katika tukio hilo watawasiliana na TFS makao makuu na mkoa kuona ni hatua gani watawachukulia na kwamba watalifuatilia suala hilo kwa karibu kuona mwisho wake.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AHUDHURIA MAULI YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD S.A.W VIWANJA VYA MAISARA SULEIMAN ZANZIBAR

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzin Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akijumuika katika Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W.yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja kushoto kwa Rais (Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khamis Haji Khamis na (kulia kwa Rais) Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Wadi akipiga fatha kabla ya kuaza kwa hafla hiyo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiitikia dua ikisoma na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar.Sheikh.Mahmoud Wadi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na (kushoto kwa Rais) Kadhi Mkuu wa Zanzibare Sheikh Khamis Haji Khamis na Waziri swa Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe Mohammed Ramia Abdulwawa, wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ua Maulidi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyiuka katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja 9-11-2019

MKE wa Rais wa Zanzibaer Mama Mwanamwema Shein akiidikia dua baada ya kumalizika kwa hafla ya Maulidi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad(S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja kulia kwa Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma na kushoto Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe. Marine Thomas Joe. Wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo

SHEIKH Abubakar Said Abubakar kutoka Mji Mkongwe Wilaya ya Mjini Unguja akisoma Dua ya Barzanji wakati wa hafla ya Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja yaliofanytika jana usiku 9-11-2019.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa `akikabidhiwa Qasweeda ya Mwaka na Mshauri wa Jumuiya ya Malade Nabii Zanzibar Sheikh. Sherali Champsi, wakati wa hafla ya kuadhimisha Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad(S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu

TAASISI YA UONGOZI YATAKIWA KUTOA MAFUNZO KWA VIONGOZI KATIKA MAENEO YAO YA KAZI ILI KUIMARISHA UTAWALA BORA

0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akihimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Taasisi ya Uongozi (UONGOZI Institute) ( hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Uongozi (UONGOZI Institute) wakisikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha watumishi hao na Naibu waziri huyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika katika ukumbi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Uongozi (UONGOZI Institute) mara baada ya kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) mara baada ya Naibu Waziri huyo kuwasili katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kikao kazi cha kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo.

………………………..

Na. Aaron Mrikaria – Dar es Salaam

Serikali imeitaka Taasisi ya UONGOZI (UONGOZI Institute) kutoa mafunzo ya ungozi kwa viongozi mbalimbali wa Serikali katika maeneo yao kazi ili kuiwezesha Serikali kufikia lengo la kuimarisha utawala bora, badala ya kusubiri viongozi hao kufuata huduma mafunzo katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo jijini Dar es Salaam.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watendaji wa taasisi hiyo, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, kuwapelekea mafunzo viongozi wa Serikali katika maeneo yao ya kazi kutapunguza gharama kubwa zinazotumika kuwasafirisha viongozi hao kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata semina elekezi na mafunzo mbalimbali ya uongozi yanayotolewa na taasisi hiyo.

Dkt. Mwanjelwa amefafanua kuwa, mafunzo ya viongozi yakitolewa mahala pa kazi yatasaidia kuharakisha utoaji wa elimu ya maadili kwa viongozi wa umma, hivyo taasisi hiyo itakuwa na mchango mkubwa katika kuwezesha kuifikia azma ya Serikali ya kuwa na viongozi waadilifu. 

Sanjali na hilo, Dkt. Mwanjelwa ameitaka Taasisi ya UONGOZI kuhakikisha inatoa elimu ya umuhimu wa viongozi katika Taasisi zote Umma nchini kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi. 

Aidha, Dkt. Mwanjelwa ameishauri taasisi hiyo kuhakikisha inawasilisha Serikalini wazo lao la kuanzisha Kituo cha Tathmini ya Viongozi kwani kituo hicho kitakuwa ni msaada mkubwa kwa viongozi kutambua maeneo ambayo hawafanyi vizuri kiutendaji na kuyaboresha na kwa yale wanayofanya vizuri kiutendaji kuyaendeleza.

Naye, Mkuu wa Idara ya Mafunzo kwa Viongozi wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo amesema, Taasisi hiyo imeshatoa mafunzo elekezi kwa viongozi mbalimbali nchini kwa vipindi tofauti licha ya kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya viongozi kutomaliza mafunzo yao na wengine wanapomaliza hatua ya mwanzo hawaendelei na hatua inayofuata kwa mujibu wa taratibu ya mafunzo husika.

Pamoja na kuwepo kwa changamoto hiyo, Bw. Singo hakusita kuishauri Serikali kuendelea kuweka msisitizo wa kutoa mafunzo kwa viongozi wanaoteuliwa ili kuwajengea uwezo kiutendaji utakaowawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu. 

“Taasisi ya UONGOZI inaishauri Serikali kuwa na utaratibu endelevu wa kutoa mafunzo kwa viongozi kabla ya kupandishwa vyeo, na iendelee kusisitiza utoaji wa mafunzo elekezi kwa viongozi wanaoteuliwa ili kuwajengea uelewa wa namna Serikali inavyofanya kazi, ikiwa ni pamoja na kuwapatia fursa ya kufahamu vipaumbele vya Serikali na miiko ya Utumishi wa Umma’’, Bw. Singo amesisitiza.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Prof. Joseph Semboja amemshukuru Dkt. Mwanjelwa kwa kufanya ziara ya kikazi kuhimiza uwajibikaji katika Taasisi yake na kumhakikishia kuwa, taasisi yake itafanyia kazi maelekezo na ushauri alioutoa kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika Taasisi hiyo. 

Ziara hiyo ya kikazi ya Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika Taasisi ya UONGOZI ni mwendelezo wa utekelezaji wa majukumu yake ya kusimamia na kuhimiza uwajibikaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO YA JESHI LA POLISI, CP LIBERATUS SABAS AFANYA MKUTANO WA KUWASHUKURU WANANCHI

0
0
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas,
akifurahia jambo na wanafunzi wa shule za msingi waliokuja kumsalimia baada ya kumalizika kwa mkutano wake na wananchi zaidi amewapongeza kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kupunguza uhalifu kwenye makazi yao. (Picha na Jeshi la Polisi).

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas,
akisalimiana na wakazi wa Pasua Boma Mbuzi wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya kumalizika kwa kikao chake na wananchi hao aliowapongeza kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kupunguza uhalifu katika makazi yao. (Picha na Jeshi la Polisi).
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas
akizungumza na wakazi wa Pasua Boma Mbuzi wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro katika mkutano wake na wananchi juu ya kutatua matatizo madogo madogo huku akiwapongeza kwa kuhakikisha wamepunguza uhalifu kwenye makazi yao. (Picha na Jeshi la Polisi).

MAADHIMISHO YA MIAKA 105 VITA YA KWANZA YA DUNIA NA MIAKA 75 VITA YA PILI YA DUN

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa ameongozana Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke (kulia) na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini (kushoto) Mhe. Joerg Herrera kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa anasoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini Mhe. Joerg Herrera wakiwaongoza baadhi ya makamanda kutoka nchi za Tanzania,Ujerumani na Uingereza kuweka shada la maua katika mnara wa askari ulioko Posta Jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia.

Baadhi ya askari wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini kama ishara ya heshima wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini Mhe. Joerg Herrera wakipokea heshima wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
Mmoja wa wapiganaji wa vita ya pili ya dunia Mzee Malagila Shimba mwenye umri wa miaka 98 akipiga saluti mara baada ya kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa amesimama pamoja na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke (kushoto) na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini (kulia) Mhe. Joerg Herrera wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
Meja Jenerali Sherrif Sheikh Othman (wa pili kutoka kulia) akiwa na baadhi ya Makamanda kutoka Ujerumani na Uingereza wakiwa wamesimama kutoa heshima katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Serikali yasitisha shughuli ya uokoaji wachimbaji wadogo,Vilio na huzuni vyatawala tena mgodi wa Imalanguza,

0
0
Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika maeneo
hayo wakiwa kwenye eneo la tukio siku ya tarehe 1/10/2019
walipofukiwa.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakiongozwa na Naibu Waziri wa
Madini Stanslaus Nyongo wa katikati meza kuu, kushoto kwake ni
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, kulia ni Katibu
mkuu wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila na Yuma yake ni
Kamishna wa Madini Mhandisi David Mlabwa.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akitoa tamko la serikali la
kusitishwa kwa zoezi la uokoaji.

********************************

Na Issa Mtuwa “WM” – Geita

Majonzi na huzuni vimetawala kwenye mgodi wa wachimbaji wadogo wa
Imalanguza wilaya ya Geita kata ya Lwamgasa katika Kijiji cha Imalanguzu,
mara baada ya kuwasili Naibu Waziri wa Madini Stanslausi Nyongo
mgodini hapo akiwa na viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya
Madini, uongozi wa mkoa na viongozi wa dini kwa ajili ya kwenda kusitisha
shughuli za uokoaji wa wachimbaji wadogo wawili Karos Msukuma Paulo
mwenyeji wa Chato na Kulwa Joseph Mahungija mwenyeji wa Busolwa
Nyang’wale waliofukiwa kifusi siku ya tarehe 1/10/2019.

Usitishaji wa zoezi hilo umefanyika tarehe 9/11/2019 ikiwa ni siku 39 tangu
wachimbaji hao wafukiwe na kifusi kutokana na uwepo wa changamoto
mbalimbali zilizo jitokeza katika kipindi chote cha uokoaji. Ripoti maalam ya
timu ya wataalam wa uokoji imeeleza kuwa kumekuwa na changamoto
nyingi wakati wote wa ukoji zilizopelekea kuwa na ugumu wa kuwaokoa
wachimbaji hao.

Akiwasilisha taarifa ya wataalam wa uokoaji iliyoishauri serikali kusitisha
kwa zoezi hilo la uokoaji kwa Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo,
mkuu wa wilaya ya Geita Josephat Maganga amemwambia Naibu Waziri
wa Madini kuwa miongoni mwa changamoto zilizojitokeza wakati wa
uokoaji ni pamoja na uwepo wa maji chini ya mgodi, mwingiano wa
magogo mbalimbali chini ya shimo la mgodi, na kutokuwa na usalama
katika eneo hilo hata kwa vyombo vya uokoaji.

Maganga aliongeza kuwa, kulikuwa na wataalam wa makundi mbalimbali
ya uokoaji na vifaa vya kutosha kutoka kwa jeshi na uokoaji, mgodi wa
dhahabu wa Geita (GGM), na makampuni mengine kutoka kwenye migodi
mbalimbali, lakini pamoja na juhudi zote hizo imeshindikana kupatikana
kwao.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa siku ya tukio hilo, kwenye shimo hilo
kulikuwa na wachimbaji 5 ambapo 3 kati yao waliokolewa siku hiyo hiyo na
wawili hawakuweza kupatikana hadi zoezi hilo la uokoaji linasitishwa.

Kwa upande wake Naibu Waziri Nyongo, akiongea kwa masikitiko na
majozi kwenye hadhara hiyo, Nyongo amesema kwanza lililotokea ni bahati
mbaya na kwamba serikali imesikitishwa na tukio hilo na kwamba iko
pamoja wafiwa na wachimbaji wote.

Ameongeza kuwa, serikali inathamini sana hata uhai wa mtu mmoja kuliko
dhahabu au madini yote yaliko chini na ndio maana inasisitiza wachimbaji
kuchimba kwa kufuata utaratibu na sharia ili wachimbe kwa kuzingaatia
usalama ili kuepukana na majanga kama hayo.

Nyongo ametowa kauli ya serikali ya kuhitimisha shughuli za uokoaji na
kutoa maelekezo kuhusu eneo hilo ambalo wachimbaji hao wamefukiwa na
kifusi.

“Na sasa tunakwenda kufanya ibada ya kwenda kuwazika wenzetu, viongi
wetu wa dini wako hapa watatuongoza katika ibada hiyo kwa ajili ya
maombi. Natamka kuwa, shughuli zote za uchimbaji katika eneo ambalo
tunaamini kuwa ndipo wezentu hawa wapo, basi eneo hilo litambuliwe
rasmi kuwa ndio kabuli lao na kama kuna undelezaji wa shughuli ya
uchimbaji utaendelea katika eneo lingine na kwa utaratibu mwingine.”
alisema Nyongo.

Nyongo pia alitoa maagizo kwa afisa madini mkazi mkoa wa Geita na timu
yake kusimamia usitishwaji wa shughuli za uchimbaji katika eneo hilo
mpaka pale hatua za uzingatiaji usalama ziwe zimefuatwa ili kuepusha ajali
nyingine.

Kwa upannde wake Mchungaji Nuhu Suleman alie ongoza ibada hiyo ya
kuwaombea marehemu alisema, hapana budi kumshukuru mungu kwa kila
jambo na kila jambo hukusudiwa na mungu. Amewakumbusha waumini
wote kumuelekea mungu kwani yeye ndie mwenye upekee na ufalme na
kwamba maisha ya binaadamu yana ukomo ni vyema kila mmoja
akajiandaa na safari hiyo.

WAZIRI MPINA AMTUMBUA MENEJA MKUU RANCHI ZA TAIFA ALIYEKUMBWA NA KASHFA YA RUSHWA MILIONI 12

0
0
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa(NARCO), Profesa Philemon Wambura ambaye uteuzi wake umetenguliwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina

Na Mwandishi Wetu


WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametengua uteuzi wa Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Profesa Philemon Nyagi Wambura aliyefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa makosa ya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka, uhujumu uchumi na ubadhirifu wa mali za umma.

Kwa Mujibu wa Taarifa kwa Umma iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Edward Kondela imesema Waziri Mpina amefikia uamuzi huo kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni Sura 212 na Sheria ya Mashirika ya Umma Na. 2 ya mwaka 1992.

Pia taarifa hiyo imebainisha kuwa uteuzi huo umetenguliwa kuanzia 08, Novemba 2019 na kwamba kuwa taratibu za kumpata Meneja Mkuu mpya wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) zinaendelea.

Wiki iliyopita Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera, John Joseph aliwaambia waandishi wa habari mjini Bukoba kuwa Prof. Wambura aliomba na kupokea rushwa kiasi cha shilingi milioni 12 kutoka kwa mtu ambaye aliomba kupatiwa kitalu kwenye moja ya Ranchi za Taifa zilizopo Missenyi Mkoani Kagera.

Alisema mnamo tarehe 23.09.2019 Takukuru ilipokea taarifa kwamba Profesa Wambura ambaye ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni za Ranchi za Taifa anajihusisha na vitendo dhidi ya rushwa ambapo walianzisha uchunguzi mara moja.

Mkuu huyo wa Takukuru alisema kwenye uchunguzi huo walibaini kwamba mnamo Tarehe 3.1.2018, Profesa Wambura aliomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni 12 kwa mtu ambaye aliomba kupewa kitalu lakini hakukubali kumpatia hadi apatiwe milioni 12 na mtu huyo ambaye kwa mujibu wa TAKUKURU jina lake limehifadhiwa aliweza kumpatia kiasi hicho cha fedha na ndipo alipofanikiwa kumpatia kitalu hicho.

Joseph alisema ni makosa kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa mtu yoyote kujihusisha na vitendo vya rushwa ambapo tayari TAKUKURU imetoa onyo kali kwa watu wote kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwani TAKUKURU iko macho wakati wote na itanawasa na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.

KIKUNDI CHA WAKE WA VIONGOZI CHAKABIDHI MADARASA MANNE NA VYOO KUMI KWA KITUO CHA WATOTO WENYE MAHITAHJI MAALUM CHA BUHANGIJA

0
0
Mlezi wa Kikundi cha Wake wa Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu , Mama Tunu Pinda (wa tatu kulia) wakiwapa chakula watoto wa kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga baada ya kukabidhi majengo ya vyumba vinne vya madarasa na vyoo kumi, Novemba 10, 2019.
Mlezi wa Kikundi cha Wake wa Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisoma hotuba yake wakati kikundi hicho kilipokabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa Kituo cha waotot wenye ulemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga Novemba 10, 2019. Kushoto ni Mgeni rasmi katika makabidhino hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizindua madarasa manne ya Kituo cha watoto walemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga yaliyojengwa kwa ufadhili wa kikundi cha wake wa viongozi cha New Melleanium Women Group. Wa nne kulia ni Mlezi wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Wapili kulia ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Tunu Pinda, kulia ni Mama Hasina Kawawa, wa tano kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko.
Mlezi wa kikundi cha Wake wa Vingozi cha Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimiana na watoto wa kituo cha walemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga baada ya kikundi hicho kukabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa shule hiyo, Novemba 10, 2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack
Mlezi wa kikundi cha wake wa Vingozi cha New Millennium Group, Mke wa Waziri mkuu, Mama Mary Majaliwa akikumbatiana na Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Mama Tunu Pinda, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu katika hafla ya kukabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa Kituo cha Watoto Walemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga yaliyojengwa kwa ufadhili wa kikundi hicho, Novemba 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WASITENGWE-MAMA MAJALIWA

0
0
Mlezi wa Kikundi cha Wake wa Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisoma hotuba yake wakati kikundi hicho kilipokabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa Kituo cha waotot wenye ulemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga Novemba 10, 2019. Kushoto ni Mgeni rasmi katika makabidhino hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

…………….

MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa ametoa wito kwa wazazi na walezi watoto wenye mahitaji maalumu kutowaficha na kuwatelekeza na badala yake wawape nafasi ya kupata elimu kwa sababu ni haki yao ya msingi.

Mama Majaliwa ambaye pia ni Mlezi wa Umoja wa Wake wa Viongozi (New Mellenium Women Group), ametoa wito huo leo (Jumapili, Novemba 10, 2019), wakati alipokabidhi majengo ya madarasa manne na matundu ya vyoo kumi kwa Kituo cha Watoto Wenye Ulemavu cha Buhangija mkoani Shinyanga yaliyojengwa na umoja huo.

Mama Majaliwa amesema si vyema kuwatenga au kuwakatia tamaa watoto wenye ulemavu kwani wao pia ni watoto sawa na watoto wengine, hivyo wanastahili kupewa haki zote bila kubaguliwa.

Amesema hatua waliyochukuwa akinamama wa umoja huo inaunga mkono jitihada za serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuwapatia watoto wa kitanzanai elimu bure na katika mzingira mazuri.

Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako ameupongeza umoja huo kwa shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuwajali watoto wenye mahitaji maalumu.

Profesa Ndalichako amesema katika kipindi cha mwaka 2019/2020 Serikali imetenga jumla ya sh 3,809,758,460.00 kwa ajili ya kununua na kusambaza vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na vifaa visaidizi kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum (wakiwemo Albino), katika shule na vitengo vya elimu maalum. 

Waziri huyo ameongeza kuwa pamoja na juhudi hizo za Serikali, bado wanafurahi wanapopata michango kama huo uliotolewa leo. “Wito wangu kwenu tusichoke kuwasaidia hawa watoto wetu. Napenda kuwakumbusha na kusisitiza kwamba Watu wenye Ulemavu wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwenu.”

“Tuwasaidie na tushirikiane kuwapatia mahitaji yao muhimu ikiwa ni pamoja na elimu, huduma za afya na mazingira mazuri ya kuwawezesha kuishi bila ya matatizo. Serikali kwa upande wake itaendelea kujitahidi kwa uwezo kutoa fursa zinazojali mahitaji yao.”

Amesema madarasa pamoja na vyoo alivyokabidhiwa leo kwa niaba ya uongozi wa kituo cha Buhangija na Kikundi cha New Millenium ni tunu kwao na wananchi wa Shinyanga na ni sadaka kwa watoto wa Buhangija, hivyo, ameutaka uongozi wa Mkoa na Uongozi wa Kituo kwa pamoja washirikiane kuyatunza vizuri ili yaweze kutumika kwa muda mrefu.

Akitoa taarifa ya ujenzi huo kwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela amesema fedha zilizotumika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne ni sh. 65m,884,523/= ambapo kila chumba cha darasa kimejengwa kwa wastani wa sh. 16,471,130.

Amesema ujenzi wa vyumba kumi vya vyoo unaendelea na ukikamilika utagharimu sh.26, 271,922.44 na kwamba vyoo hivyo vitakuwa vya kisasa vikiwa na maji ndani pamoja na masinki ya kunawia ili kukidhi mahitaji ya watoto wenye ulemavu.

SEKTAYA AFYA NCHINI YACHANGIA UKATILI WA KIJINSIA

0
0
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea wakati wa kutoa majumuisho yake katika semina ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA) iliyomalizika leo Jijijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bw. Peter Serukamba wakati wa kutoa majumuisho yake katika semina ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA) iliyomalizika leo Jijijini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia jambo kuhusu Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA) iliyomalizika leo Jijijini Dodoma.

……………….

Anthony Ishengoma -Dodoma

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema Sekta ya Afya Nchini inachangia vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa Nchini kwa baadhi ya watoa huduma ya Afya kushiriki kuficha ushaidi kwa njia ya rushwa.

Dkt. Ndugulile amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa kutoa majumuisho yake katika semina ya wabunge kuhusu Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA) iliyomalizika leo Jijijini Dodoma ili kujenga uelewa kwa kamati ya Bunge kuhusu mpango huo.

Dkt. Ndugulile amesema watoa huduma ya Afya wanawajibu wanapopata zile kesi zinazohusiana na ukatili wa Kijinsia kuhakikisha wanazingatia miiko na misingi ya taaluma zao kuhakikisha hawawi sehemu ya kuvuruga ushaidi.

“Sisi kama Wizara tutakapobaini kwamba mtoa huduma wa Afya yoyote atakayeshiriki katika katika kosa la kuvuruga ushaidi kwa waanga wa ukatili wa kijinsia hapa Nchini tutamfutia lesseni ya kufanya kazi ya kutoa huduma za Afya katika Nchi yetu’’. Aliongeza Dkt. Ndugulile.

Pamoja na masuala ya ukatili wa Kijinsia Dkt. Ndugulile amesema pia vijana wengi wanaanza kujamiina wakiwa katika umri mdogo na kwa mjibu wa takwimu za masula ya ukimwi za mwaka 2017 zinaonesha asilimia 40 ya Watanzania ni vijana na kati hao mabinti peke yake ni 80%.

Kufuatia hali hiyo ya vijana kujihusisha na masuala ya kujiimiana Dkt. Ndugulile amesema serikali inakusudia kupeleka Sheria Bungeni ili kupunguza umri wa vijana kuanzia miaka 15 kupima umri kwa hiari lakini pia kujipima wenyewe na kuweza kujilinda lakini pia kulinda wenzi wao.

Aidha Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa sheria iliyopo inasema mtoto chini ya umri wa miaka 18 harusiwi kupima virusi kwa hiari labda kwa ruhusa ya mzazi wake lakini wiki ijayo Wizara inapeleka bungeni mabadiliko ya sheria ili suala la kupima virusi kwa hiari lianze kufanyika mpaka umri wa miaka 15 kwa kuwa watoto sasa wanaanza kujiamiina katika umri huo na bila idhini ya wazazi.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Takwimu za Viashiria vya Hali ya Afya Nchini zinaonesha kwamba kati ya 27% ya mabinti walio katika umri wa miaka 15-19 mmoja kati ya watatu ama ni mjazito au ana mtoto hii inatoa picha kwamba watoto hawa wanaanza ngono katika umri mdogo ndio maana serikali inatoa chanjo ya kansa ya mlango kizazi kwa watoto wa kike wenye umri huo lakini pia sula limepelekea kufanyika kwa marekebisho ya sheria ili wapime virusi kwa hiari.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bw. Peter Serukamba amewataka Wajumbe wa Kamati yake kuwa mabarozi wa masuala ya ukatili wa Kijinsia Nchini ili masuala hayo yaweze kupewa kipaumbele katika Bajeti za Wizara mbalimbali Serikalini.

Pamoja na maoni yake hayo Bw. Serukamba ameyataja matendo ya ukatili kuwa yamekuwepo kwa mingi lakini Jamii kama zilivyo mila na desturi zetu imukuwa ikifanya vitendo hivyo kwa usiri tofauti na wenzetu wa Nchi za Magharibi ambapo watu wanajitangaza hadharani kuwa ni wao ni mashoga na wanaweza kujitokeza hata kugombea nafasi za juu katika uongozi.

Aidha kiongozi huyo wa Bunge ameongeza kuwa pamoja na uwepo wa sheria mbalimbali lakini haitoshi tu kutokomeza matendo haya hivyo kuitaka Wizara pamoja na wadau kutoa elimu ya kutosha kwa umma ikiwemo adhabu kwa wote wanaohusika na makosa haya kupewa adhabu kali.

Bw. Serukamba ameutaja umasikini kuwa sababu mojawapo ya kuchochochea ukatili wa kijinsia kwa wanawake kwa kuwa baadhi ya wanawake wanakubali kunyanyaswa kwasababu ya umasikini wa kipato na utegemezi hivyo kukubali kupigwa au kuonewa kwa namna mbalimbali.

Semina ya wabunge kuhusu Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA) imemalizika leo Jijijini Dodoma na imelenga kujenga uelewa kwa kamati ya Bunge kuhusu masuala ya ukatili na mpanga mkakati huo wa miaka mitano unaotegemea kukamilika mwaka 2022.

NBC yazindua Klabu ya Biashara (NBC-B-Club) Mkoani Morogoro

0
0
  Ofisa Uvuvi na Mifugo wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim (kushoto),  aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro katika uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya Benki ya NBC mkoani Morogoro,  akishikana mikono na Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassimu Hussein wakati akizindua rasmi klabu hiyo mkoani humo jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru.

 Ofisa Uvuvi na Mifugo wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim (wa tatu kushoto),  aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro katika uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya Benki ya NBC mkoani humo jana, akishikana mikono na Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassimu Hussein katika uzinduzi wa klabu hiyo Mkoani Morogoro jana. Klabu hiyo imeanzishwa kusaidia mahitaji ya wafanyabiashara wadogo na wa mkoa huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara NBC, Elvis Ndunguru, Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashra wa kati na Wadogo, Evance Luhimbo na Meneja wa Tawi la NBC Morogoro, Sophia Mwombelo.
  Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashra wa Kati na Wadogo wa Benki ya NBC, Evance Luhimbo akizungumza katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake wafanyabiashara  wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.

 Ofisa Uvuvi na Mifugo wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim (kushoto),  aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro katika uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya Benki ya NBC mkoani humo akikaribishwa na Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassimu Hussein wakati akiwasili kuzindua rasmi klabu hiyo mkoani humo jana. Katikati ni Meneja wa Tawi la NBC Morogoro, Sophia Mwombelo. Uzinduzi huo  ulitanguliwa na semina ya siku moja   juu ya kuwajengea uwezo wafanyabiasha wadogo na wa kati.
 Ofisa Biashara Mwandamizi Taarifa za Biashara na Takwimu kutoka Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade), Magdalena Shirima akitoa elimu kuhusu fursa za masoko ya nje ya nchi katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
 Ofisa Biashara wa Asasi ya Kusaidia Uwekezaji kwenye Kilimo (PASS), Irene Benedicto akizungumza katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.

  Ofisa Mkuu Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Julius Mjenga akitoa elimu kuhusu kodi katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia mada katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyuabiashara wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.

HIVI NDIVYO MAADHIMISHO YA MIAKA 105 YA VITA YA KWANZA YA DUNIA NA MIAKA 75 YA VITA YA PILI YA DUNIA YALIVYOFANYIKA JIJINI DAR

Washindi wa 'Paka na Ushinde' wajinyakulia zawadi

0
0






KAMPUNI ya Rangi ya Plascon Tanzania, imewazawadia washindi mbalimbali wa promosheni ya 'Paka Rangi na Ushinde'.Promosheni hiyo sasa imefikia wiki ya tano, ambayo hadi sasa washindi 21 wamepatikana na kujishinda sh. milioni 1 kila mmoja.

Promosheni hiyo ilikuwa imepokea zaidi ya washindi 1,000 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Rangi ya Plascon Tanzania, Hussein Jamal, alisema:“Tukiwa kama kampuni tulianza rasmi shindano hili Oktoba, kiukweli tumepata mwitikio mzuri. Promosheni ya Paka Rangi na Ushinde imethibitisha kuwa kampuni yetu hurudisha kwa uaminifu au fadhila kwa wateja wetu”.

Jamal pia alisema promosheni hiyo inaonesha jinsi gani Plascon inavyotimiza wajibu wake kwa Watanzania pamoja na dhumuni lao la kuongeza thamani ya soko la rangi kupitia bidhaa yao, katika ubora, uvumbuzi na kuwa suluhisho la rangi kwa watanzania.

Promosheni hiyo iliyopewa jina la 'Paka Rangi na Ushinde', ilianza Oktoba na itafikia ukomo Desemba 14 na kuwavutia mamia na maelfu kwa kila mshiriki kuwa na uhakika wa kujipatia muda wa maongezi wa sh.500 na bado anakuwa na nafasi ya kushinda sh. milioni moja.

Plascon hutoa zawadi ya sh. milioni 5 kila wiki kwa washindi mbalimbali.

Jamal aliongeza washiriki wanatakiwa kununua lita 20 ya rangi ya Plascon, na utapata utapewa kadi utakayoikwangua na kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15054, ili kuwa katika nafasi ya kushinda.

Watengenezaji wa vifaa vya jikoni wazindua duka la kwanza Afrika mjini Dar

0
0
 
Meneja wa Biashara za Nje wa Sachsenküchen, Dominik Shulze Doring akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka jipya la kisasa la vyombo vya jikoni la Sachsenküchen, Mikocheni jijini Dar es salaam jana. Pembeni ni Meneja wa Sachsenküchen –Tanzania, Ronald Harold
Meneja wa Biashara za Nje wa Sachsenküchen, Dominik Shulze Doring akielezea kuhusu ubora wa bidhaa walizonazo kwa wateja waliojitokeza kwenye duka jipya lakisasa la vyombo vya jikoni la Sachsenküchen lililoko Mikocheni jijini Dar es salaam 

Meneja wa Biashara za Nje wa Sachsenküchen, Dominik Shulze Doring akielezea kuhusu ubora wa bidhaa walizonazo kwa wateja waliojitokeza kwenye duka jipya lakisasa la vyombo vya jikoni la Sachsenküchen lililoko Mikocheni jijini Dar es salaam


Meneja wa Biashara za Nje wa Sachsenküchen, Dominik Shulze Doring akielezea kuhusu ubora wa bidhaa walizonazo kwa wateja waliojitokeza kwenye duka jipya lakisasa la vyombo vya jikoni la Sachsenküchen lililoko Mikocheni jijini Dar es salaam
Meneja wa Biashara za Nje wa Sachsenküchen, Dominik Shulze Doring akielezea kuhusu ubora wa bidhaa walizonazo kwa wateja waliojitokeza kwenye duka jipya lakisasa la vyombo vya jikoni la Sachsenküchen lililoko Mikocheni jijini Dar es salaam
Meneja wa Sachsenküchen –Tanzania, Ronald Harold akielezea kuhusu ubora wa bidhaa walizonazo kwa wateja waliojitokeza kwenye duka jipya lakisasa la vyombo vya jikoni la Sachsenküchen lililoko Mikocheni jijini Dar es salaam


Meneja wa Sachsenküchen –Tanzania, Ronald Harold akielezea kuhusu ubora wa bidhaa walizonazo kwa wateja waliojitokeza kwenye duka jipya lakisasa la vyombo vya jikoni la Sachsenküchen lililoko Mikocheni jijini Dar es salaam
Meneja wa Biashara za Nje wa Sachsenküchen, Dominik Shulze Doring akizungumza na wageni na waandishi wa habari waliohudhuria kwenye uzinduzi wa duka jipya la kisasa la vyombo vya jikoni

Novemba 9, 2019, Dar es Salaam:

Kampuni ya Kitanzania, Power Systems (T) Ltd, imeshirikiana na wasanifu na watengenezaji wanaotambulika kimataifa wa vifaa vya jikoni, Sachsenküchen, kusambaza bidhaa zenye viwango kwenye soko la Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa moja ya maduka yake Mikocheni, jijini Dar es Salaam, Meneja wa Biashara za Nje wa Sachsenküchen, Dominik Shulze Doring, amesema kwamba ukaribu na wateja utarahisisha kufikisha huduma zao kwa wateja wa Tanzania.

“Kwa kuzindua duka la Sachsenküchen, ikiwa ni la kwanza barani Afrika, tunawaletea Watanzania bidhaa mbalimbali ambazo tunazizalisha. Pia tunaleta huduma za usanifu wa majiko kutokana na mahitaji ya mteja,” Doring ameelezea.

Meneja wa Sachsenküchen –Tanzania, Ronald Harold nae amesema: “Tunafuraha kwa kuweza kushirikiana na watengenezaji wa vyombo vya jikoni wanaotambulika duniani ili kuweza kuleta bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwenye soko. Tanzania pia itafaidika kwa kupata uzoefu na ujuzi watakaoleta washirika wetu kutoka Ujerumani ambao wana uzoefu wa zaidi ya miaka 100”

Harold pia ametoa wito kwa Watanzania kutembelea duka hilo jipya la Sachsenküchen kujionea wenyewe bidhaa bora na kufurahia huduma hiyo mpya.“Jikoni ni mahali ambapo mtu anatakiwa kufanya shughuli zake kwa furaha. Bidhaa zetu zimetengenezwa kuhakikisha matumizi mazuri ya nafasi huku pia zikiwa ni za kisasa, zenye kuvutia na kuridhisha wateja,” ameongeza Harold.

“Hapa Sachsenküchen kila kitu kinapewa kipaumbele, hususan ubora wa bidhaa ambazo zinabadilisha na kulifanya liwe ni sehemu halisi ya kuishi,” amesema.Sachsenküchen ni kiwanda kipo Dippoldiswalde, karibu na Dresden, Ujerumani, na wamekuwa wakisanifu majiko na kutengeneza vifaa vya jikoni kwa zaidi ya miaka 100.

Tokea miaka ya 1990, Sachsenküchen imekuwa ikikua huku ikiwa na wafanyakazi 220 na inasavifirisha zaidi ya asilimia 50 ya bidhaa zake nje ya nchi, mapato ya Euro milioni 40 kwa mwaka huu faida ikiwa ni asilimia 12.
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images